676 Kwa Sababu ya Usafishaji Imani Inakuja

1 Ni kutoka ndani ya imani yako tu ndipo utaweza kumwona Mungu, na wakati una imani Mungu atakukamilisha. Bila imani, Hawezi kufanya hivyo. Wakati una imani kwamba utaona matendo Yake katika uzoefu wako wa utendaji, basi Mungu atakuonekania, na Atakupa nuru na kuongoza kutoka ndani. Bila hiyo imani, Mungu hataweza kufanya hivyo. Kama umepoteza matumaini katika Mungu, utawezaje kupata uzoefu wa kazi Yake? Kwa hiyo, ni wakati tu una imani na huweki mashaka kumhusu Mungu, ni wakati una imani ya kweli Kwake tu bila kujali Anachokifanya ndipo Atakuangazia na kukupa nuru kupitia katika mapito yako, na ni hapo tu ndipo utaweza kuona matendo Yake. Mambo haya yote yanafanikishwa kupitia kwa imani. Imani huja kupitia tu usafishaji, na wakati hakuna usafishaji, imani haiwezi kukua.

2 Je, neno hili “imani”, linarejelea nini? Imani ni kusadiki kwa kweli na moyo wa dhati ambao wanadamu wanapaswa kumiliki wakati wao hawawezi kuona au kugusa kitu, wakati kazi ya Mungu haiambatani na za binadamu, wakati inazidi uwezo wa binadamu. Hii ndiyo imani Ninayozungumzia. Watu wanahitaji imani katika nyakati za shida na usafishaji, na imani ni kitu kinachofuatwa na usafishaji; usafishaji na imani haviwezi kutenganishwa. Haijalishi jinsi Mungu anavyofanya kazi, na haijalishi mazingira uliyomo, unaweza kufuatilia maisha na kutafuta ukweli, na kutafuta maarifa ya kazi ya Mungu, na kuwa na ufahamu wa matendo Yake, na unaweza kutenda kulingana na ukweli. Kufanya hivi ndiko kuwa na imani ya kweli, na kufanya hivyo kunaonyesha kwamba hujapoteza imani katika Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Wale Wanaopaswa Kukamilishwa Lazima Wapitie Usafishaji” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 675 Kusudi la Kazi ya Mungu ya Usafishaji

Inayofuata: 677 Jinsi ya Kumpenda Mungu Katika Usafishaji

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp