990 Ni Wale tu walio na Ukweli Wanaweza Kuishi kwa Kudhihirisha Maisha Halisi

1 Katika dunia hii ya sasa iliyo chini ya miliki ya Shetani, kupitia miaka elfu ya historia ya mwanadamu, ni nani aliyepata uzima? Hamna. Je, mbona hivi? Wote ni watu ambao wamempinga Mungu. Kila kitu ambacho wameishi maisha yao kwacho na kudumu kinatoka kwa Shetani na kilikubalika kutoka kwa Shetani na hasa ni upinzani kwa neno la Mungu na kilikubaliwa kutoka kwa Shetani na hasa ni upinzani kwa neno la Mungu. Hivyo, ni viumbe wanaompinga Mungu, wanaopitia laana Yake, na hawana uzima wa kuzungumzia.

2 Ikiwa watu wana ufahamu wa kweli wa tabia ya Mungu, na wanaweza kutoa sifa ya kweli kwa utakatifu Wake na haki Yake, basi wanajua Mungu kwa kweli na kumiliki ukweli; ni hapo tu ndipo wanaishi nuruni. Ni wakati tu ambapo maoni ya watu kuhusu dunia na maisha yanabadilika ndipo wanabadilika kimsingi. Mtu anapokuwa na lengo la maisha na kujiheshimu kulingana na ukweli, mtu anapomtii Mungu kabisa na kuishi kulingana na neno la Mungu, mtu anapohisi kuwa na amani na kuchangamshwa ndani ya roho yake, moyo wa mtu unapokuwa huru bila giza, na mtu anapoishi kwa huru kabisa na bila kuzuiwa kwa uwepo wa Mungu—hapo tu ndipo atakapoishi maisha ya mwanadamu ya kweli na kuwa mtu anayemiliki ukweli.

3 Ukweli wote unaomiliki unatoka kwa neno la Mungu na kwa Mungu Mwenyewe. Mtawala wa ulimwengu mzima na kila kitu—Mungu Mkuu Zaidi—Anakupenda wewe, kama mtu halisi anayeishi maisha ya kweli ya mwanadamu. Je, nini linaweza kuwa la maana zaidi kuliko kibali cha Mungu? Mtu wa aina hii ni yule aliye na ukweli. Mungu tu ndiye ukweli. Mungu hudhibiti mbingu na dunia na vyote vilivyomo na ana mamlaka juu ya vyote. Kutoamini Mungu, kutomtii Mungu ni kutokuwa na uwezo wa kupata ukweli. Ukiishi kulingana na neno la Mungu, utahisi uwazi, udhabiti, na utamu usioweza kulinganishwa ndani kabisa ya moyo wako; utakuwa umepata uzima kwa kweli.

Umetoholewa kutoka katika “Ni Kwa Kufuatilia Ukweli Tu Ndiyo Unaweza Kupata Mabadiliko Katika Tabia Yako” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Iliyotangulia: 989 Azimio Linalohitajika ili Kufuatilia Ukweli

Inayofuata: 991 Jinsi ya Kuchunguza Asili Yako

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

83 Upendo wa Kweli

1 Namrudia Mungu na kuuona uso Wake upendezao, nikiwa huru kutokana na udhibiti wa kaida za dini. Neno Lake linanijaza na raha na furaha...

269 Nitampenda Mungu Milele

1 Ee Mungu! Maneno Yako yananiita nirudi Kwako. Nakubali kufundishwa katika ufalme Wako mchana na usiku. Mara nyingi sana nilikuwa dhaifu...

84 Umuhumi wa Maombi

1 Maombi ni njia moja ya mwanadamu kishirikiana na Mungu, kuita Roho Wake na kuguswa na Mungu. Kadiri unavyoomba zaidi, ndivyo...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki