625 Bila Kumjua Mungu, Utamkosea Mungu kwa Urahisi

1 Wale ambao huhudumu kama viongozi daima hutaka kuwa na ubunifu mkubwa, kuwa wazuri kuliko wengine, kupata hila mpya ili Mungu aweze kuona jinsi kweli walivyo na uwezo. Hata hivyo, hawazingatii kufahamu ukweli na kuingia katika uhalisi wa neno la Mungu. Wao daima hutaka kuringa; si huu ni ufunuo kwa usahihi wa asili ya kiburi? Usifanye tu chochote kijacho akilini mwako bila kufikiri. Je, inawezaje kuwa sawa ikiwa huzingatii matokeo ya matendo yako? Wakati wale kati yenu ambao huudhi tabia ya Mungu na kuziudhi amri Zake za utawala wataondolewa wakati huo, hakutakuwa na maneno mnayoweza kusema. Kama wewe huelewi tabia ya Mungu au huyaelewi mapenzi ya Mungu, kwa urahisi utamkosea Mungu na kwa urahisi utaziudhi amri Zake za utawala, hiki ni kitu ambacho kila mtu ni lazima ajichunge dhidi yake.

2 Mara unapoziudhi amri za utawala za Mungu au kuiudhi tabia ya Mungu, Mungu hataangalia kama ulifanya hivyo makusudi au bila kukusudia; hiki ni kitu ambacho ni lazima uone kwa dhahiri. Ikiwa huwezi kuona ukweli halisi wa suala hili, basi unahakikishiwa kuwa na tatizo. Katika kumhudumia Mungu, watu wanataka kupiga hatua kubwa, kufanya mambo makubwa, kusema maneno makubwa, kufanya kazi kubwa, kufanya mikutano mikubwa na kuwa viongozi wakuu. Kama siku zote una matarajio makuu, basi utaziudhi amri kuu za utawala za Mungu. Kama wewe si mwenye tabia njema, mwenye kumcha Mungu au mwenye busara katika kumhudumia Mungu, ipo siku utaziudhi amri za utawala za Mungu. Wewe huzingatii zaidi kitu chochote na humwogopi Mungu, kwa hiyo ni lazima upate adhabu!

Umetoholewa kutoka katika “Bila Ukweli Ni Rahisi Kumkosea Mungu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 624 Mungu Hawasifu Wale Wanaohudumu Kama Paulo

Inayofuata: 626 Wale Wasio na Ubinadamu Hawastahili Kumhudumia Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp