717 Washahidi wa Mungu Lazima Wawe na Badiliko katika Tabia

1 Mabadiliko yanafanikishwa kwa tabia ya mwanadamu kupitia njia tofauti ya kazi ya Mungu; bila mabadiliko ya aina hii katika tabia ya mwanadamu, mwanadamu hangeweza kuwa na ushuhuda kwa Mungu, na hangekuwa wa kuupendeza moyo wa Mungu. Mabadiliko katika tabia ya mwanadamu yanaashiria kwamba mwanadamu amejiweka huru kutokana na minyororo ya Shetani, amejiweka huru kutokana na ushawishi wa giza, na kwa kweli amekuwa mfano na kifaa cha kujaribiwa cha kazi ya Mungu, amekuwa shahidi wa kweli wa Mungu na mtu aliye wa kuupendeza moyo wa Mungu.

2 Leo hii, Mungu mwenye mwili Amekuja kufanya kazi Yake duniani, na Anahitaji kwamba mwanadamu apate ufahamu kumhusu, aweze kumtii, awe na ushuhuda Kwake—aweze kujua kazi Yake ya matendo na ya kawaida, atii maneno Yake yote na kazi ambayo haiambatani na mawazo ya mwanadamu, na kuwa na ushuhuda kwa kazi Yake yote ya kumwokoa mwanadamu, na matendo yote Anayofanya ya kumshinda mwanadamu. Wale walio na ushuhuda kwa Mungu lazima wawe na ufahamu wa Mungu; ni aina hii tu ya ushuhuda ndio ulio sahihi, na wa kweli, na ni aina hii tu ya ushuhuda ndio unaoweza kumpa Shetani aibu.

3 Mungu Anawatumia wale waliomjua baada ya kupitia hukumu Yake na kuadibu, ushughulikiaji na upogoaji, kuwa na ushuhuda Kwake. Anawatumia wale waliopotoshwa na Shetani kumtolea Yeye ushuhuda, na vilevile Anawatumia wale ambao tabia yao imebadilika, na wale basi ambao wamepokea baraka Zake, kumtolea ushuhuda. Yeye hana haja na mwanadamu kumsifu kwa maneno tu, wala hana hitaji lolote la sifa na ushuhuda kutoka kwa namna ya Shetani, ambao hawajaokolewa na Yeye. Ni wale tu wanaomjua Mungu ndio wanaohitimu kumtolea Mungu ushuhuda, na ni wale tu ambao tabia zao zimebadilika ndio wanaofaa kumshuhudia Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 716 Ni Wale tu walio na Ukweli Wanaweza Kuishi kwa Kudhihirisha Maisha Halisi

Inayofuata: 718 Kuwa na Imani Katika Mabadiliko ya Tabia

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Tafadhali weka neno unalotafuta katika kisanduku cha kutafuta

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp
Yaliyomo
Mipangilio
Vitabu
Tafuta
Video