470 Maneno ya Mungu: Kanuni Pekee ya Kuwepo kwa Mwanadamu
1 Katika kuonyesha Kwake ukweli, Mungu huonyesha tabia na kiini Chake; havionyeshwi kulingana na mihutasari ya wanadamu ya mambo mbalimbali chanya na njia za kuzungumza ambazo wanadamu wanatambua. Maneno ya Mungu ni maneno ya Mungu; maneno ya Mungu ni ukweli. Hayo ndiyo msingi na sheria ambayo kwayo wanadamu wanapaswa kuishi, na hizo zinazodaiwa kuwa kanuni zinazotokana na binadamu zimelaaniwa na Mungu. Hazikubaliwi na Yeye, sembuse kuwa asili au msingi wa matamshi Yake. Maneno yote yaliyotolewa na maonyesho ya Mungu ni ukweli, kwa maana Yeye anacho kiini cha Mungu, na Yeye ndiye uhalisi wa mambo yote chanya.
2 Tamaduni za jadi za wanadamu na njia za kuishi hazitakuwa ukweli kwa sababu ya mabadiliko au kupita kwa wakati, na wala maneno ya Mungu hayatakuwa maneno ya mwanadamu kwa sababu ya shutuma na kusahau kwa wanadamu. Kiini hiki hakitabadilika kamwe; ukweli ni ukweli kila wakati. Kuna ukweli ndani ya hili: Hiyo misemo yote inayofupishwa na wanadamu inatoka kwa Shetani—ni fikira na mawazo ya wanadamu, hata inatokana na hamaki ya binadamu, na haihusiani hata kidogo na mambo chanya. Maneno ya Mungu, kwa upande mwingine, ni maonyesho ya kiini na hadhi ya Mungu.
3 Yeye huyaonyesha maneno haya kwa sababu gani? Kwa nini Ninasema maneno hayo ni ukweli? Sababu ni kwamba Mungu anatawala juu ya sheria, kanuni, vyanzo, viini, uhalisi na siri zote za vitu vyote, na vimefumbatwa mkononi Mwake, na ni Mungu pekee Anayejua kanuni, uhalisi, ukweli, na siri zote za vitu vyote; Anajua asili ya vitu hivyo na vyanzo vyao ni nini hasa. Kwa hivyo, ni ufafanuzi wa vitu vyote uliotajwa katika maneno ya Mungu pekee ndio sahihi kabisa, na mahitaji kwa wanadamu yaliyo ndani ya maneno ya Mungu ndicho kiwango pekee kwa wanadamu—kigezo pekee ambacho mwanadamu anapaswa kuishi kwa kufuata.
Umetoholewa kutoka katika “Kuhusu Ukweli ni Nini” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo