340 Kazi Afanyayo Mungu Kwako ni ya Thamani Sana

1 Wengi wa wale kati yenu waliitwa, lakini kama mazingira hayangewalazimisha au kama hamngeitwa, hamngekuwa tayari kabisa kutokea wazi. Nani yuko tayari kutelekeza mambo kwa namna hii? Ni nani yuko tayari kuacha anasa za mwili? Ninyi nyote ni watu ambao husherehekea kwa ulafi katika faraja na kutafuta maisha ya anasa! Mmepata baraka nyingi mno—nini kingine mnacho cha kusema? Mna malalamiko yapi? Mmefurahia baraka nyingi mno na neema kuu mno mbinguni, na kazi sasa imefichuliwa kwenu ambayo haikuwahi kufanywa duniani awali. Je, si hii ni baraka?

2 Kwa sababu mmempinga na kuasi dhidi ya Mungu, sasa mmepitia kuadibu kiasi hiki. Kwa sababu ya kuadibu huku mmeziona rehema na upendo wa Mungu, na hata zaidi mmeziona haki na utakatifu Wake. Kwa sababu ya kuadibu huku na kwa sababu ya uchafu wa wanadamu, mmeiona nguvu kuu ya Mungu, na mmeuona utakatifu na ukuu Wake. Je, si huu ni ukweli adimu mno? Je! Si haya ni maisha yenye maana? Kazi ambayo Mungu hufanya ina maana tele! Hivyo nafasi yenu ilivyo chini zaidi, ndivyo inavyoonyesha zaidi kuinuliwa na Mungu, na ndivyo inavyothibitisha zaidi jinsi kazi Yake ilivyo na thamani kwenu leo. Ni hazina yenye thamani mno hasa!

Kwa muda mrefu hakuna mtu aliyefurahia wokovu mkubwa hivi. Ukweli kwamba nafasi yenu ni ya chini inaonyesha jinsi wokovu wa Mungu ulivyo mkuu, na inaonyesha kwamba Mungu ni mwaminifu kwa wanadamu—Yeye huokoa, sio kuangamiza.

Umetoholewa kutoka katika “Umuhimu wa Kuukoa Uzao wa Moabu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 339 Wewe ni Mwaminifu kwa Nani?

Inayofuata: 342 Mungu Huchukia Hisia Kati ya Watu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp