Kazi na Kuingia (3)

Mungu amewaaminia wanadamu vitu vingi sana na Amezungumza bila kikomo juu ya kuingia kwao. Lakini kwa sababu ubora wa tabia ya watu ni duni mno, maneno mengi ya Mungu yameshindwa kuanza kustawi. Kuna sababu mbalimbali za huu ubora duni wa tabia, kama vile uharibifu wa mawazo na maadili ya binadamu, na kutokuwa na malezi mazuri; imani za usihiri zilizojaa moyoni mwa mwanadamu; mitindo ya maisha iliyopotoka ambayo imeweka maovu mengi katika sehemu ya ndani kabisa ya moyo wa mwanadamu; ufahamu wa juujuu wa utamaduni, na takribani asilimia tisini na nane ya watu ambao hawana elimu ya utamaduni na, aidha, watu wachache sana wanaopata viwango vya juu vya elimu ya utamaduni. Kwa hivyo, kimsingi watu hawajui ni nini maana ya Mungu au Roho, bali wana taswira hafifu ya Mungu na isiyoeleweka vizuri kama iliyopatikana kutoka kwa imani ya usihiri. Ushawishi wenye madhara ambao maelfu ya miaka ya “roho wa juu sana wa utaifa” umeacha ndani kabisa ya moyo wa mwanadamu pamoja na fikira za kikabaila ambazo watu wamefungwa nazo na kutiwa minyororo, bila uhuru wowote, na kusababisha watu kutokuwa na hamasa au ustahimilivu, hawana shauku ya kusonga mbele, lakini badala yake wanakuwa baridi na kurudi nyuma, wakiwa na akili ya utumwa ambayo ina nguvu sana, na kadhalika—sababu hizi zimetengeneza taswira chafu na mbaya kwa mitazamo ya njozi, mawazo, maadili, na tabia ya binadamu. Inaonekana, wanadamu wanaishi katika dunia ya giza la kutisha, na hakuna anayetafuta kusonga mbele miongoni mwao, hakuna anayefikiria kwenda katika ulimwengu ulio bora, badala yake, wanaridhika na waliyo nayo maishani, kutumia siku zao kuzaa na kuwalea watoto, wakikazana, wakitoka jasho, wakifanya kazi zao, wakiwa na njozi ya kuwa na familia ya raha na yenye furaha, ya upendo wa ndoa, ya watoto wenye upendo, ya maisha yenye furaha katika miaka yao ya uzeeni wanapoishi kwa kudhihirisha maisha yao kwa amani. … Kwa makumi, maelfu, makumi ya maelfu ya miaka hadi sasa, watu wamekuwa wakipoteza muda wao kwa njia hii, hakuna anayetengeneza maisha makamilifu, wanapigana tu wenyewe kwa wenyewe katika ulimwengu huu wa giza, wakipambana kupata umaarufu na utajiri, na kufanyiana njama wao kwa wao. Nani amewahi kutafuta mapenzi ya Mungu? Kuna mtu yeyote aliyewahi kutilia maanani kazi ya Mungu? Sehemu hizi zote za binadamu zinazomilikiwa na ushawishi wa giza zimekuwa asili ya mwanadamu tangu zamani, kwa hiyo ni vigumu sana kutekeleza kazi ya Mungu na hata watu hawana moyo wa kuzingatia kile ambacho Mungu amewaaminia leo. Vyovyote vile, Ninaamini kwamba watu hawatajali Ninapotamka maneno haya kwa vile kile Ninachokisema ni historia ya maelfu ya miaka. Kuzungumza juu ya historia kuna maana ya ukweli na, zaidi ya hayo, kashfa zinazojulikana kwa wote, sasa kuna maana gani kuzungumza kitu ambacho ni kinyume na ukweli? Lakini pia Naamini kwamba watu wenye akili, wanapoona maneno haya, wataamka na kujitahidi kwa ajili ya kuendelea mbele. Mungu hutumaini kwamba wanadamu wanaweza kuishi na kufanya kazi kwa amani na kuridhika huku wakati ule ule wakiweza kumpenda Mungu. Ni mapenzi ya Mungu kwamba binadamu wote waweze kuingia katika raha; zaidi ya hili, kuijaza nchi yote na utukufu wa Mungu ni shauku kubwa ya Mungu. Ni aibu tu kwamba wanadamu husalia katika hali ya kusahauliwa kabisa na wasiotambua mambo, waliopotoshwa vibaya sana na Shetani hivi kwamba leo hawafanani tena na binadamu. Kwa hiyo mawazo ya binadamu, uadilifu na elimu huunda kiungo muhimu, pamoja na mafunzo katika kujua kusoma na kuandika utamaduni yakiunda kiungo cha pili, bora zaidi ya kuinua ubora wa tabia wa utamaduni wa binadamu na kubadilisha mtazamo wao wa kiroho.

Kwa kweli, mahitaji ya Mungu kwa binadamu si mengi, lakini kwa sababu pengo kati ya uhodari wa watu na kiwango anachohitaji Mungu ni kikubwa sana, watu wengi sana hutazama tu upande wa matakwa ya Mungu lakini hukosa uwezo wa kuyatimiza. Kipaji cha watu cha asili, pamoja na kile wanachojiandaa nacho baada ya kuzaliwa, kiko mbali sana na kutimiza matakwa ya Mungu. Bali kutambua tu wazo hili si suluhisho la hakika kufanikiwa. Maji ya mbali hayawezi kukata kiu ya sasa hivi. Hata watu wakijifahamu kuwa duni kuliko vumbi, kama hawana azimio la kuuridhisha moyo wa Mungu, sembuse kuifuata njia iliyoko mbele ili kutimiza matakwa ya Mungu, basi maarifa ya aina hiyo yana thamani gani? Je, si kama kuchota maji na chungio—juhudi isiyo na maana? Kiini cha kile Nisemacho kinahusu kuingia; hiyo ndiyo mada kuu.

Wakati wa kuingia kwa mwanadamu, maisha huwa ya kuchosha daima, yaliyojaa sifa za lazima zisizobadilika za maisha ya kiroho, kama vile kufanya maombi, kula na kunywa maneno ya Mungu kiasi, au kufanya mikusanyiko, ili watu wahisi daima kwamba kumwamini Mungu hakuleti raha kuu. Shughuli za kiroho kama hizo kila mara hutekelezwa kwa msingi wa tabia ya asili ya binadamu, ambao wamepotoshwa na Shetani. Ingawa wakati mwingine watu wanaweza kupokea nuru ya Roho Mtakatifu, kufikiri kwao kwa asili, tabia, mitindo ya maisha na mienendo bado imekita mizizi, na kwa hiyo asili yao husalia isiyobadilika. Shughuli za kishirikina ambazo watu wanashughulika nazo ndizo Mungu anazichukia sana, lakini watu wengi bado hawawezi kuachana nazo, wakifikiri kwamba shughuli hizi za kishirikina zimeamriwa na Mungu, na hata leo bado hawajaziacha kabisa. Mambo kama mipango ambayo vijana hufanya kwa ajili ya sherehe za arusi au mahari, zawadi za pesa, dhifa, na maneno mengine na virai vinavyohusiana na matukio ya sherehe; maneno ya zamani ambayo yamerithishwa; shughuli zote za kishirikina zisizokuwa na maana zinazofanywa kwa niaba ya wafu na taratibu za mazishi; yote haya yanachukiwa sana na Mungu. Hata siku ya ibada (ikiwemo Sabato, kama inavyoadhimishwa na ulimwengu wa dini) inachukiwa naye; mahusiano ya kijamii na mawasiliano ya kidunia kati ya mwanamme na mwanamme pia yanachukiwa na kukataliwa zaidi na Mungu. Hata Sikukuu ya Machipuko na Siku ya Krismasi, ambazo zinajulikana kwa kila mtu, haziamriwi na Mungu, sembuse wanasesere na mapambo ya sherehe za siku kuu hizi kama vile mashairi, mafataki, kandili, Komunyo, zawadi za Krismasi na sherehe za Krismasi—je, sio sanamu katika akili za wanadamu? Kumega mkate siku ya Sabato, mvinyo, na kitani nyembamba navyo ni sanamu zaidi. Siku zote za sherehe za kijadi ambazo ni maarufu sana nchini China, kama vile Siku ya kuinua Vichwa vya Joka, Sikukuu ya Mashua ya Joka, Sikukuu ya Majira ya Kati ya Kupukutika, Sikukuu ya Laba, na Siku ya Mwaka Mpya, na sikukuu zisizothibitika katika ulimwengu wa kidini, kama vile Pasaka, Siku ya Ubatizo, na Siku ya Krismasi, zote hizi zimepangwa na kurithishwa kwa watu wengi tangu zama za kale hadi leo. Ni uwezo mkubwa wa fikra za binadamu na dhana bunifu ambazo zimewaruhusu kurithishwa hadi leo. Zinaonekana kuwa hazina kasoro, lakini kwa kweli ni hila ambazo Shetani alifanya kwa binadamu. Kadri Shetani wanavyoishi katika eneo fulani, na kadri eneo hilo lilivyo nyuma kimaendeleo na kutofaa, ndivyo desturi zake za kikabaila zinakuwa nyingi zaidi. Vitu hivi vinawafunga watu kwa nguvu, bila kutoa nafasi kwa ajili ya maendeleo. Sikukuu nyingi katika ulimwengu wa kidini zinaonekana kuonyesha ubunifu mkubwa na zinaonekana kujenga daraja kwa kazi ya Mungu, lakini kweli ni vifungo visivyoshikika ambavyo Shetani hutumia kuwafunga watu ili wasije kumjua Mungu—hizi zote ni hila za ujanja za Shetani. Kwa kweli, hatua ya kazi ya Mungu inapomalizika, tayari Amekwishaharibu zana na mtindo wa wakati huo, bila kuacha alama yoyote. Hata hivyo, “waumini wasalihina” bado wanaabudu vitu hivyo vya kushikika; wakati huo huo wanaacha kile Alicho nacho Mungu, bila hata kukichunguza zaidi, wakionekana wamejawa na upendo wa Mungu lakini kwa uhalisi walimtoa ndani ya nyumba zamani sana na kumweka Shetani mezani kwa ajili ya kumwabudu. Sanamu ya Yesu, Msalaba, Maria, Ubatizo wa Yesu na Karamu ya Mwisho—watu wanavichukulia hivi kama Bwana wa Mbinguni, wanaviabudu wakati wote wakilia kwa sauti kwa kurudiarudia “Bwana, Baba wa Mbinguni.” Je, huu wote sio utani? Hadi leo, misemo mingi ya kimapokeo kama hiyo iliyorithishwa miongoni mwa wanadamu ni chukizo kwa Mungu; inazuia kabisa njia ya kuendelea mbele kwa Mungu na, zaidi ya hayo, inasababisha vipingamizi vikubwa kwa kuingia kwa mwanadamu. Mbali na kiwango ambacho Shetani amemharibu mwanadamu, sheria ya Witness Lee, uzoefu wa Lawrence, uchunguzi wa Watchman Nee, na kazi ya Paulo, haya yote yameuteka moyo wa mwanadamu. Mungu hana namna ya kufanya kazi kwa wanadamu, kwa sababu ndani yao kuna ubinafsi mwingi, sheria, kanuni, taratibu na mifumo, na vitu kama hivi; vitu hivi, ukiongezea vitendo vya watu vya imani za kishirikina, vimewakamata na kuwaharibu wanadamu. Ni kana kwamba mawazo ya watu ni filamu ya ajabu ya kichimbakazi katika rangi kamili, ikiwa na watu wa ajabu wakiendesha mawingu, ya kubuni sana kiasi cha kuwastaajabisha watu, ikiwaacha watu wametunduwazwa na kupigwa butwaa. Kusema kweli, kazi ambayo Mungu huja kufanya leo ni hasa kushughulikia na kuondoa sifa za ushirikina za binadamu na kugeuza kabisa mtazamo wao wa akili. Kazi ya Mungu haijadumu hadi leo kwa sababu ya urithi ambao umepitishwa kwa vizazi na binadamu; ni kazi kama ilivyoanzishwa na Yeye binafsi na kukamilishwa na Yeye, bila haja yoyote ya kuurithi urithi wa mwanadamu fulani mkuu wa kiroho, au kurithi kazi yoyote ya asili ya uwakilishi iliyofanywa na Mungu katika enzi nyingine fulani. Binadamu hawahitaji kujishughulisha na jambo lolote kati ya haya. Mungu ana mtindo mwingine leo wa kuzungumza na wa kufanya kazi, kwa hiyo mbona binadamu wajisumbue? Kama wanadamu watatembea njia ya leo katika mkondo wa sasa huku wakiendeleza urithi wa “babu” zao, hawatafikia hatima yao. Mungu huhisi kinyaa sana kwa hali hii hasa ya tabia ya mwanadamu, jinsi Anavyoichukia mno miaka, miezi na siku za ulimwengu wa binadamu.

Njia bora zaidi ya kubadilisha tabia ya mwanadamu ni kuondoa vitu hivi vyenye sumu kubwa katika mioyo ya wanadamu, kuwaruhusu watu kuanza kubadilisha fikira na maadili yao. Kwanza kabisa, watu wanatakiwa kuona waziwazi kwamba kaida zote hizi za kidini, shughuli za kidini, miaka na miezi, na sikukuu zote ni za kumchukiza Mungu. Wanatakiwa kuwa huru kutoka kwa vifungo hivi vya fikira za kishirikina na kuondoa kila alama ya kishirikina iliyozama kabisa ndani. Mambo haya yote ni sehemu ya kuingia kwa mwanadamu. Mnatakiwa kuelewa kwa nini Mungu huwatoa watu katika ulimwengu usiokuwa na dini, na pia kwa nini Huwatoa katika desturi na kanuni. Hili ndilo lango la kuingia kwenu, na ingawa mambo haya hayahusiani na uzoefu wenu wa kiroho, hivi ndivyo vizuizi vikubwa vinavyozuia kuingia kwenu, vinavyowazuia kumjua Mungu. Vinatengeza wavu unaowakamata watu. Watu wengi husoma Biblia sana na wanaweza hata kukariri mafungu mengi kutoka katika Biblia. Katika kuingia kwao leo, watu bila kujua wanaitumia Biblia kupima kazi ya Mungu, kana kwamba msingi wa hatua hii katika kazi ya Mungu ni Biblia na chanzo chake ni Biblia. Kazi ya Mungu inapokuwa sambamba na Biblia, watu huiunga mkono kazi ya Mungu kwa nguvu zote na kumwangalia Mungu kwa taadhima mpya; kazi ya Mungu inapokuwa haifanani na Biblia, watu huwa na dukuduku sana kiasi cha kuanza kutokwa jasho, wakitafuta ndani yake msingi wa kazi ya Mungu; kama kazi ya Mungu haikutajwa katika Biblia, watu watampuuza Mungu. Inaweza kusemwa kwamba, watu wengi wanaikubali kwa hadhari sana, wanatii kwa kusita, na hawajali kuhusu kuijua kazi ya Mungu; na kuhusu mambo yaliyopita, wanashikilia nusu moja na kuacha nusu nyingine. Je, huku kunaweza kuitwa kuingia? Kushikilia vitabu vya wengine kama hazina, na kuvichukulia kama ufunguo wa dhahabu wa kufungua lango la ufalme, watu hawaonyeshi kuvutiwa na matakwa ya Mungu ya leo. Aidha, “wataalamu wengi wenye akili” katika mkono wao wa kushoto wanashikilia maneno ya Mungu, huku katika mkono wa kulia wanashikilia “kazi kuu” za wengine, kana kwamba wanataka kupata msingi wa maneno ya Mungu ya leo ndani ya kazi hizi kuu ili kuthibitisha kwa ukamilifu kwamba maneno ya Mungu ni sahihi, na hata wanatoa ufafanuzi kwa wengine kwa kuunganisha na kazi kuu, kana kwamba walikuwa wanafanya kazi. Kusema kweli, kuna “watafiti wa kisayansi” wengi miongoni mwa wanadamu ambao hawajawahi heshimu mafanikio makubwa ya kisayansi ya leo, mafanikio ya kisayansi ambayo hayana kigezo (yaani, kazi ya Mungu, maneno ya Mungu, na njia ya kuingia uzimani), hivyo watu wote “wanajitegemea,” “wakihubiri” mbali sana wakitegemea sana ufasaha wao, wakiringia “jina zuri la Mungu.” Wakati huo huo, kuingia kwao kuko hatarini na umbali wa matakwa ya Mungu unaonekana kuwa mbali sana jinsi uumbaji ulivyo mbali na wakati huu. Ni rahisi kiasi gani kufanya kazi ya Mungu? Inaonekana kwamba watu wamekwishaamua kuacha nusu yao kwa mambo ya zamani na kuleta nusu yao kwa wakati wa leo, kuwasilisha nusu kwa Shetani na kukabidhi nusu kwa Mungu, kana kwamba hii ndiyo njia ya kutuliza dhamiri yao na kuweza kuwa na hisia ya utulivu fulani. Mioyo ya watu inadhuru sana kwa siri, wanaogopa sio tu kupoteza kesho bali pia wanahofia kupoteza jana, wanaogopa sana kumkosea Shetani na kumkosea Mungu wa leo, Anayeonekana kuwa na bado kutokuwa. Kwa sababu watu wameshindwa kukuza vizuri fikira na maadili yao, wanakosa utambuzi kabisa, na kimsingi hawajui kama kazi ya leo ni ile ya Mungu au siyo. Pengine ni kwa sababu fikra za kishirikina za watu zimekita mizizi sana kiasi kwamba ushirikina na ukweli, Mungu na sanamu, vimewekwa katika kundi moja; wala hawajali kuvibainisha vitu hivi, na inaonekana kama wametesa bongo zao lakini bado mambo hayo hayajawa wazi. Na hiyo ndio maana wanadamu wamesimama katika njia zao na hawasongi mbele tena. Haya yote yanatokea kwa sababu watu hawana elimu ya itikadi ambayo ni sahihi, kitu ambacho husababisha ugumu katika kuingia kwao. Na matokeo yake, watu wanapoteza mvuto kabisa katika kazi ya Mungu wa kweli, bali wanashikilia kwa kung’ang’ania[1] kazi ya mwanadamu (kama vile watu wanaotazamwa kuwa ni watu wakubwa) kana kwamba wamepigwa chapa nayo. Je, hizi si mada mpya kabisa ambazo wanadamu wanapaswa kuingia ndani?

Tanbihi:

1. “Wanashikilia kwa kung’ang’ania” inatumiwa kwa dhihaka. Kirai hiki kinaonyesha kwamba watu ni wakaidi na wasiodhibitiwa kwa urahisi, wakishikilia vitu vilivyopitwa na wakati na wasiopenda kuviachilia.

Iliyotangulia: Kazi na Kuingia (2)

Inayofuata: Kazi na Kuingia (4)

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp