124 Maana ya Kazi ya Mungu Katika Nchi ya Joka Kubwa Jekundu

1 China ni nchi iliyo nyuma zaidi kimaendeleo kuliko zote; ni nchi ambapo joka kuu jekundu hulala likiwa limejiviringisha, ina watu wengi zaidi wanaoabudu sanamu na kushiriki katika uchawi, ina hekalu nyingi zaidi, na ni mahali ambapo pepo wachafu huishi. Ulizaliwa kutoka kwayo, umeelimishwa nayo na ukaloweshwa katika ushawishi wake; umepotoshwa na kuteswa nayo, lakini baada ya kugutushwa unaachana nayo na unapatwa kabisa na Mungu. Huu ni utukufu wa Mungu, na hii ndiyo maana hatua hii ya kazi ina umuhimu mkubwa. Mungu amefanya kazi ya kiwango kikubwa hivi, amenena maneno mengi sana, na hatimaye Atawapata ninyi kabisa—hii ni sehemu moja ya kazi ya usimamizi ya Mungu, na ninyi ndio “mateka wa ushindi” wa vita vya Mungu na Shetani.

2 Kadiri mnavyozidi kuelewa ukweli na kadiri maisha yenu ya kanisa yalivyo bora zaidi, ndivyo joka kuu jekundu linavyotishwa zaidi. Haya yote ni mambo ya ulimwengu wa kiroho—ni vita vya ulimwengu wa kiroho, na Mungu anapokuwa mshindi, Shetani ataaibishwa na kuanguka chini. Hatua hii ya kazi ya Mungu ina umuhimu wa ajabu. Mungu anafanya kazi kwa kiwango kikubwa sana na kukiokoa kabisa kikundi hiki cha watu ili uweze kuponyoka kutoka kwa ushawishi wa Shetani, uishi katika nchi takatifu, uishi katika nuru ya Mungu, na uwe na uongozi na mwongozo wa nuru. Kisha kuna maana katika maisha yako.

Umetoholewa kutoka katika “Utendaji (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 123 Mungu Amekamilisha Kundi la Washindi Uchina

Inayofuata: 125 Mungu Ametukuzwa Kikamilifu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp