128 Kazi ya Mungu Inaendelea Kuboreshwa

1 Kazi ya Mungu inaendelea kusonga mbele, na ingawa madhumuni ya kazi Yake bado hayajabadilika, njia anazozitumia kufanya kazi zinabadilika mara kwa mara, na hivyo pia wale wanaomfuata Mungu. Zaidi iwapo kazi ya Mungu, zaidi mwanadamu anakuja kumjua kwa kina Mungu, na tabia ya mwanadamu inabadilika ipasavyo pamoja na kazi Yake. Hata hivyo, ni kwa sababu kazi ya Mungu milele inabadilika ndio wale wasiojua kazi ya Roho Mtakatifu na wale wanadamu wajinga wasiojua ukweli wanakuwa wapinzani wa Mungu. Kazi ya Mungu kamwe haifuati dhana za mwanadamu, kwani kazi Yake daima ni mpya na siyo nzee. Kamwe Hairudii kazi ya zamani lakini badala Anasonga mbele na kazi ambayo haijafanywa hapo awali.

2 Mungu haendelezi kazi sawa, na kazi Yake daima inabadilika na daima ni mpya, jinsi kila siku Nazungumza nanyi maneno mapya na kufanya kazi mpya. Hii ndiyo kazi Ninayofanya, umuhimu wake ukiwa kwa maneno “mpya” na “ajabu.” “Mungu habadiliki, na Mungu daima Atakuwa Mungu”; usemi huu hakika ni ukweli. Kiini cha Mungu hakibadiliki, Mungu daima ni Mungu, na Hawezi kamwe kuwa Shetani, lakini haya hayathibitishi kwamba kazi Yake ni ya daima na kabambe kama kiini Chake. Unatangaza kwamba Mungu yuko hivyo, lakini ni jinsi gani basi unaweza kueleza kwamba Mungu daima ni mpya na kamwe si mzee? Kazi ya Mungu inaendelea kuenea, na mapenzi ya Mungu yanaendelea kujitokeza na kufanywa kujulikana na mwanadamu.

Umetoholewa kutoka katika “Ni Jinsi Gani Ambavyo Mwanadamu Ambaye Amemwekea Mungu Mipaka katika Fikira Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 127 Mungu Amefichua Tabia Yake Yote kwa Mwanadamu

Inayofuata: 129 Kazi ya Mungu Haijirudii

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp