453 Kazi ya Roho Mtakatifu ina Kanuni Zake

1 Kazi ya Roho Mtakatifu ina kanuni zake, na ni yenye masharti. Roho Mtakatifu hufanya kazi katika mtu wa aina gani? Mtu anapaswa kuwa na nini ili apate kazi ya Roho Mtakatifu? Katika imani ya mtu, mtu lazima aelewe wazi kuwa angalau lazima awe na dhamiri na moyo mwaminifu. Mara unapokuwa na moyo mwaminifu—na vile vile dhamiri na mantiki ambayo ubinadamu lazima umiliki—ndipo Roho Mtakatifu anaweza kufanya kazi kwako.

2 Umeweza kuelewa mfumo wa jinsi Roho Mtakatifu anafanya kazi? Roho Mtakatifu kawaida hufanya kazi kwa wale ambao mioyo yao ni miaminifu, na Yeye hufanya kazi wakati watu wanaingia katika shida na wanatafuta ukweli. Mungu hatajali kuhusu wale wasio na chembe ya mantiki ya au dhamiri ya binadamu. basi watu hawa wanapaswa kufanya nini? Lazima watubu kweli. Kwanza, moyo wako lazima uwe wazi kwa Mungu, na lazima utafute ukweli kutoka kwa Mungu; ukishaelewa ukweli, unaweza kuutenda. Kisha unaweza kutii mpangilio wa Mungu na kumruhusu Mungu achukue usukani kwako. Ni kwa njia hii tu ndiyo utasifiwa na Mungu.

3 Lazima kwanza uweke kando kiburi na majivuno yako, na uachilie masilahi yako mwenyewe. Baada ya hapo, weka mwili wako wote na roho yako katika wajibu wako na katika kazi ya kushuhudia kwa ajili ya Mungu. Lazima kwanza ujisalimishe, na uufungue moyo wako kwa Mungu, na uweke kando vitu unavyopenda na kuthamini. Ukiendelea kushikilia vitu hivyo huku ukiomba kwa Mungu, je, utaweza kupata kazi ya Roho Mtakatifu? Kazi ya Roho Mtakatifu ni yenye masharti, na Mungu ni Mungu anayechukia uovu na aliye mtakatifu. Watu wakishikilia mambo haya kila wakati, wakijifungia nje kila wakati kwa Mungu na kukataa kazi na mwongozo wa Mungu, basi Mungu ataacha kufanya kazi juu yao. Kwa hivyo, wale wasio na mantiki au dhamiri ya binadamu lazima watubu kweli, la sivyo Roho Mtakatifu hatafanya kazi juu yao.

Umetoholewa kutoka kwa “Unaweza Kupata Ukweli Baada ya Kumkabidhi Mungu Moyo Wako Halisi” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Iliyotangulia: 452 Kanuni ya Kazi Ya Roho Mtakatifu

Inayofuata: 454 Roho Mtakatifu Afanya Kazi Zaidi kwa Wale Wanaotamani Kukamilishwa

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

85 Njia Yote Pamoja na Wewe

1Naelea na kuzurura katika dunia, nikihisi kupotea na mnyonge ndani.Ninapoamshwa na maneno Yako ya upole, naona kuonekana kwa mwanga.Maneno...

64 Upendo wa Kweli

1Namrudia Mungu na kuuona uso Wake upendezao,nikiwa huru kutokana na udhibiti wa kaida za dini.Neno Lake linanijaza na raha na furaha...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki