2. Utofautishaji Kati ya Kazi ya Roho Mtakatifu na Ile ya Pepo Wabaya

Maneno Husika ya Mungu:

Mungu harudii kazi Yake, Hafanyi kazi ambayo si halisi, Hamtaki mwanadamu afanye mambo zaidi ya uwezo wake, na Hafanyi kazi ambayo inazidi akili ya mwanadamu. Kazi yote Anayofanya ipo ndani ya mawanda ya akili ya kawaida ya mwanadamu, na haizidi ufahamu wa ubinadamu wa kawaida, na kazi Yake ni kulingana na mahitaji ya kawaida ya mwanadamu. Ikiwa ni kazi ya Roho Mtakatifu, mwanadamu anakuwa wa kawaida zaidi, na ubinadamu wake unakuwa wa kawaida kabisa. Mwanadamu ana maarifa mengi ya tabia yake ya kishetani na iliyopotoka, na asili ya mwanadamu, na ana shauku kubwa ya kuuelewa ukweli. Hiyo ni kusema, maisha ya mwanadamu yanakua zaidi na zaidi, na tabia upotovu ya mwanadamu inakuwa na uwezo wa mabadiliko zaidi na zaidi—yote hiyo ni maana ya Mungu kuwa maisha ya mwanadamu. Kama njia haiwezi kufunua vitu hivyo ambavyo ni asili ya mwanadamu, haiwezi kubadilisha tabia ya mwanadamu, na, zaidi ya hayo, hauwezi kumleta mbele ya Mungu au kumpa ufahamu wa kweli juu ya Mungu, na hata kufanya ubinadamu wake kuwa duni zaidi na hisia zake kuwa si za kawaida zaidi, basi njia hii itakuwa si njia ya kweli, na inaweza kuwa ni kazi ya roho mchafu, au njia ya zamani. Kwa ufupi, haiwezi kuwa kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake Ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu

Lazima uelewe ni mambo yapi yanatokana na Mungu ni mambo yapi yanatokana na Shetani. Mambo yanayotokana na Mungu hukusababisha kuwa wazi zaidi kuhusu maono, na hukusababisha kusogea karibu na karibu zaidi na Mungu, ukishiriki upendo na ndugu kwa bidii; unakuwa na uwezo wa kutilia maanani mzigo wa Mungu, na moyo wako umpendao Mungu haupungui; kuna njia mbele yako kuitembea. Mambo ambayo hutokana na Shetani hukusababisha kupoteza maono na vyote ulivyokuwa navyo awali vimetoweka; unajitenga na Mungu, huna upendo kwa ndugu nawe una moyo wa chuki. Unakuwa mwenye kukata tamaa, hutaki tena kuishi maisha ya kanisa, na moyo wako umpendao Mungu hauko tena. Hii ni kazi ya Shetani na pia ni matokeo ambayo yameletwa na kazi ya roho mbaya.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 22

Kazi ya Roho Mtakatifu ni aina ya mwongozo wa kimatendo na kupata nuru kwa hali nzuri. Haiwaruhusu watu kuwa baridi. Huwaletea faraja, huwapa imani na uamuzi na kuwawezesha kufuatilia kufanywa kamili na Mungu. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi, watu wanaweza kuingia kwa vitendo; wao si baridi wala hawalazimishwi, lakini ni wa kimatendo. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi, watu wana faraja na wenye radhi, na wako tayari kutii, na wana furaha kujinyenyekeza, na hata ingawa wana maumivu na ni dhaifu ndani, wana uamuzi wa kushirikiana, wanateseka kwa furaha, wanaweza kutii, na hawajatiwa doa na mapenzi ya mwanadamu, hawajatiwa doa na fikira ya mwanadamu, na hakika hawajatiwa doa na tamaa na motisha za mwanadamu. Wakati watu wanapitia kazi ya Roho Mtakatifu, ndani yao ni watakatifu hasa. Wale ambao wanamiliki kazi ya Roho Mtakatifu huishi kwa kudhihirisha upendo wa Mungu, upendo wa kaka na dada zao, na kufurahia vitu ambavyo Mungu hufurahia na kuchukia vitu ambavyo Mungu huchukia. Watu ambao wanaguswa na kazi ya Roho Mtakatifu wana ubinadamu wa kawaida, na wao daima hufuatilia ukweli na wanamiliki ubinadamu. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi ndani ya watu, hali zao huwa nzuri zaidi na zaidi, na ubinadamu wao unakuwa wa kawaida zaidi na zaidi, na ingawa ushirikiano wao mwingine unaweza kuwa mpumbavu, motisha zao ziko sahihi, kuingia kwao ni kwa hali nzuri, hawajaribu kukatiza, na hakuna nia mbaya ndani yao. Kazi ya Roho Mtakatifu ni ya kawaida na ya kweli, Roho Mtakatifu hufanya kazi kwa mwanadamu kulingana na amri za maisha ya kawaida ya mwanadamu, na Yeye huwapa nuru na kuongoza watu kulingana na ufuatiliaji halisi wa watu wa kawaida. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi kwa watu, Yeye huwaongoza na kuwapa nuru kulingana na mahitaji ya watu wa kawaida, Anawakimu kwa msingi wa mahitaji yao, na Yeye huwaongoza na kuwapa nuru kwa hali nzuri kwa msingi wa kile ambacho wanakosa, na kwa upungufu wao. Kazi ya Roho Mtakatifu ni kuwapa watu nuru na kuwaongoza katika maisha halisi; wakipitia maneno ya Mungu katika maisha yao tu ndipo wanaweza kuona kazi ya Roho Mtakatifu. Iwapo, katika maisha yao ya kila siku, watu wako katika hali nzuri na wana maisha ya kawaida ya kiroho, basi wanamiliki kazi ya Roho Mtakatifu. Katika hali kama hiyo, wakati wanakula na kunywa maneno ya Mungu wana imani, wakati wanaomba wanatiwa moyo, wakati kitu kinawafanyikia wao si baridi, na wakati kinawafanyikia wanaweza kuona masomo ambayo Mungu anawahitaji kujifunza, na hawako baridi, ama dhaifu, na ingawa wana ugumu wa kweli, wako tayari kukubali mipango yote ya Mungu.

Ni matokeo yapi yanayotimizwa na kazi ya Roho Mtakatifu? Unaweza kuwa mpumbavu, na kunaweza kuwa hakuna utofautishaji wowote ndani yako, lakini Roho Mtakatifu anapaswa tu kufanya kazi ili kuwe na imani ndani yako, ili wewe daima uhisi kwamba huwezi kumpenda Mungu vya kutosha, ili uwe tayari kushiriki, uwe tayari kushiriki bila kujali ugumu mkuu ulio mbele. Mambo yatakufanyikia na haitakuwa wazi kwako iwapo yanatoka kwa Mungu ama kwa Shetani, lakini utaweza kungoja, na hutakuwa baridi wala mzembe. Hii ndiyo kazi ya kawaida ya Roho Mtakatifu. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi ndani yao, watu bado hukabiliwa na ugumu wa kweli, wakati mwingine wanalia, na wakati mwingine kuna mambo ambayo hawawezi kuyashinda, lakini hii yote ni hatua ya kazi ya kawaida ya Roho Mtakatifu. Ingawa hawashindi mambo hayo, na ingawa, wakati huo, wao ni dhaifu na hulalamika, baadaye bado wanaweza kumpenda Mungu na imani dhabiti. Ubaridi wao hauwezi kuwazuia kuwa na uzoefu wa kawaida, na bila kujali kile watu wengine husema, na jinsi wanavyowashambulia, bado wanaweza kumpenda Mungu. Wakati wa maombi, daima wanahisi kwamba walikuwa wadeni wa Mungu sana, na wanaamua kumridhisha Mungu na kuukataa mwili wakati wanakabiliwa na mambo kama hayo tena. Nguvu hii inaonyesha kuna kazi ya Roho Mtakatifu ndani yao, na hii ndiyo hali ya kawaida ya kazi ya Roho Mtakatifu.

Ni kazi ipi hutoka kwa Shetani? Katika kazi inayotoka kwa Shetani, maono ndani ya watu si yakini na ni dhahania, na hawana ubinadamu wa kawaida, motisha za vitendo vyao si sahihi, na ingawa wanataka kumpenda Mungu, daima kuna lawama ndani yao, na lawama hizi na fikira daima zinaingilia ndani yao, zikizuia kukua kwa maisha yao, na kuwasitisha kuja mbele ya Mungu katika hali ya kawaida. Hii ni kusema, punde tu kazi ya Shetani inapokuwa ndani ya watu, mioyo yao haiwezi kuwa kwa amani mbele ya Mungu, na hawajui cha kufanya, kuona mkutano kunawafanya kutaka kuhepa, na hawawezi kufumba macho yao wakati wengine wanaomba. Kazi ya roho waovu huharibu uhusiano wa kawaida kati ya mwanadamu na Mungu, na huvuruga maono ya awali ya watu au njia yao ya awali ya kuingia katika maisha, katika mioyo yao hawawezi kamwe kumkaribia Mungu, daima mambo hufanyika ambayo huwasababishia vurugu na kuwatia pingu, na mioyo yao haiwezi kupata amani, kuacha upendo wao wa Mungu bila nguvu, na kuwafanya kusononeka. Hayo ndiyo maonyesho ya kazi ya Shetani. Kazi ya Shetani inadhihirishwa katika yafuatayo: kutoweza kushikilia msimamo na kuwa na ushuhuda, kukusababisha kuwa mtu ambaye ana makosa mbele ya Mungu, na ambaye hana uaminifu kwa Mungu. Kwa kuingilia kwa Shetani, unapoteza upendo na uaminifu kwa Mungu ndani yako, unaondolewa uhusiano wa kawaida na Mungu, hufuatilii ukweli, ama kujiendeleza, unarudi nyuma, na kuwa baridi, unajipendeza, unaachia uenezaji wa dhambi, na huchukii dhambi; zaidi ya hayo, kuingilia kwa Shetani kunakufanya mpotovu, kunasababisha mguso wa Mungu kutoweka ndani yako, na kunakufanya kulalamika kuhusu Mungu na kumpinga Yeye, kukufanya uwe na shaka na Mungu, na hata kuna hatari ya wewe kumwacha Mungu. Hii yote ni kazi ya Shetani.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Roho Mtakatifu na Kazi ya Shetani

Mungu anafanya kazi kwa njia ya upole, laini, yenye upendo na ya kujali, kwa njia iliyopimwa kwa namna ya ajabu na sahihi. Njia Yake haikufanyi uhisi hisia kali ya mhemuko kama vile; “Mungu lazima aniache nifanye hivi” ama “Lazima Mungu aniache nifanye vile.” Mungu kamwe hakupi mawazo makali ya aina hiyo ama hisia kali zinazofanya mambo kutovumilika. Sivyo? Hata unapoyakubali maneno ya Mungu ya hukumu na kuadibu, unahisi vipi basi? Unapohisi mamlaka ya Mungu na nguvu ya Mungu, unahisi vipi basi? Unahisi kwamba Mungu ni mtakatifu na asiyekosewa? (Ndiyo.) Unahisi ukiwa mbali na Mungu nyakati hizi? Unahisi unamwogopa Mungu? La, badala yake, unahisi heshima inayomcha Mungu. Je, watu hawahisi haya mambo yote kwa sababu ya kazi ya Mungu? …

… Mungu anafanya kazi kwa mwanadamu na mwanadamu anathaminiwa katika mtazamo wa Mungu na moyo Wake. Kinyume na hayo, je, Shetani anamthamini mwanadamu? Hamthamini mwanadamu. Anachofikiria tu ni kumdhuru mwanadamu. Hii si sahihi? Wakati anafikiria kumdhuru mwanadamu, anafanya hivyo katika hali ya dharura ya akili? (Ndiyo.) Kwa hivyo inapokuja kwa kazi ya Shetani kwa mwanadamu, hapa Nina virai viwili vinayoweza kuelezea vizuri asili yenye nia mbaya na ovu ya Shetani, vinavyoweza kuwaruhusu kujua chuki ya Shetani: Katika mtazamo wa Shetani kwa mwanadamu, daima anataka kumiliki na kumtawala kwa nguvu, kila mmoja wao, ili aweze kufika mahali ambapo anaweza kumdhibiti mwanadamu kabisa, kumdhuru mwanadamu, ili aweze kutimiza lengo hili na tamaa isiyowezekana. “Umiliki wa nguvu” unamaanisha nini? Unafanyika na kibali chako, ama bila kibali chako? Unafanyika na kujua kwako, ama bila kujua kwako? Ni bila kujua kwako kabisa! Katika hali ambazo huna ufahamu, pengine wakati hajasema chochote ama pengine wakati hajafanya chochote, wakati hakuna kauli kigezo, hakuna muktadha, yuko hapo karibu nawe, akikuzunguka. Anatafuta fursa ya kukunyonya, kisha anakumiliki kwa nguvu, anakutawala, akitimiza lengo lake la kukudhibiti kikamilifu na kukudhuru. Hii ni nia na tabia ya kawaida zaidi katika mapambano ya Shetani dhidi ya Mungu kwa ajili ya mwanadamu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV

Watu wengine husema kwamba Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yao nyakati zote. Hili haliwezekani. Ikiwa wangesema kwamba Roho Mtakatifu yuko nao kila mara, hilo lingekuwa la kweli. Ikiwa wangesema kwamba fikira na hisia zao ni za kawaida nyakati zote, hilo pia lingekuwa la kweli, na lingeonyesha kwamba Roho Mtakatifu yuko nao. Ikiwa wanasema kwamba Roho Mtakatifu hufanya kazi ndani yao kila mara, kwamba wamepata nuru kutoka kwa Mungu na kuguswa na Roho Mtakatifu kila wakati, na wanapata ufahamu mpya kila wakati, basi hili si la kawaida hata kidogo! Ni la kupita uwezo wa binadamu kabisa! Bila tashwishi yoyote, watu kama hao ni pepo wabaya! Hata wakati ambapo Roho wa Mungu huja ndani ya mwili, kuna nyakati ambapo lazima Ale, na lazima apumzike—sembuse mwanadamu. Wale ambao wamemilikiwa na pepo wabaya huonekana kutokuwa na hisia na udhaifu wa mwili. Wanaweza kutelekeza na kuacha kila kitu, ni wasio na hisia, ni wenye uwezo wa kustahimili mateso na hawahisi uchovu hata kidogo sana, kana kwamba wamevuka mipaka ya mwili. Je, hili silo la kupita uwezo wa binadamu kabisa? Kazi ya pepo waovu ni ya kupita uwezo wa binadamu—hakuna mwanadamu anayeweza kutimiza mambo kama haya. Wale wasio na utambuzi huwa na wivu wanapowaona watu kama hao; Wao husema kwamba wana nguvu mno katika imani yao katika Mungu, wana imani kubwa na kamwe hawaonyeshi ishara yoyote ya udhaifu!. Kwa kweli, hili lote ni dhihirisho la kazi ya pepo mwovu. Kwa sababu watu wa kawaida bila kuzuilika huwa na udhaifu wa binadamu; hii ni hali ya kawaida ya wale walio na uwepo wa Roho Mtakatifu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Utendaji (4)

Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:

Kazi kuu ya Roho Mtakatifu ni kutoa nuru na mwangaza, kumfanya mtu aelewe maneno ya Mungu, na kuingia katika maneno ya Mungu; yaani, ni kuwaongoza watu katika kuelewa ukweli na kuingia katika ukweli, kuwapatia watu nuru na mwangaza katikati ya majaribu yote, na kuwafanya waelewe mapenzi ya Mungu. Bila shaka, kupitia watu mbalimbali, vitu na zana Roho Mtakatifu pia hufichua watu, huwapogoa, huwafundisha nidhamu, na huwaadhibu, yote kwa lengo la kuwaleta katika wokovu. Roho Mtakatifu hutawala vyote, hupanga aina zote za hali kuwabadilisha watu, kuwakamilisha. Katika kazi ya wokovu wa Mungu, ingawa kazi ya roho Mtakatifu ina sehemu nyingi, inahusika kikamilifu kwa njia fulani na wokovu. Ingawa kazi ya Roho Mtakatifu imejificha, na haionekani kabisa isiyo ya dunia hii kwa kuitazama kwa juu juu, wale wenye uzoefu wanaelewa vizuri ndani ya mioyo yao. Kinyume chake, kazi ya roho waovu ni ya rohoni ajabu, inaonekana, inaweza kuhisiwa, na si ya kawaida kabisa. Kutokana na kazi za roho waovu, inaweza kuonekana kwamba roho waovu hasa wanapenda kujifichua, ni waovu kupindukia, bila hata chembe ya ukweli. Haijalishi ni miaka mingi kiasi gani roho waovu wanafanya kazi ndani ya mtu, tabia yake iliyopotoshwa haibadiliki hata kidogo kabisa. Badala yake anazidi kupungua kuwa kawaida zaidi na zaidi, hata kupoteza urazini wa binadamu wa kawaida. Haya ni matokeo ya kazi ya roho mtakatifu. Hivi ndivyo Shetani na roho waovu wa aina zote huwapotosha watu, huwatega watu, na kuwadanganya watu. Mwishoni watu wanakuwa mapepo, na wale ambao wamedanganywa na roho waovu wanatwaliwa na Shetani na kumezwa. Kazi ya Roho Mtakatifu inahusu wokovu wa binadamu, na kadri ambavyo mtu anakuwa na kazi zaidi ya Roho Mtakatifu, ndivyo zaidi anakuwa na uwezo wa kuelewa ukweli; ubinadamu wake unakuwa wa kawaida zaidi na zaidi, na anakuwa binadamu zaidi na zaidi. Mwishoni atapata wokovu wa Mungu, kuwa mtu mwenye ukweli na ubinadamu. Tofauti kubwa baina ya kazi ya Roho Mtakatifu na ya roho waovu ni: Roho waovu wanaweza tu kuwapotosha watu, kuwatega watu, na hatimaye kuwabadilisha kuwa mapepo; kazi ya Roho Mtakatifu hutakasa waliopotoshwa katika wokovu, kuwapatia ukweli na ubinadamu. Kazi ya Roho Mtakatifu inaweza kufanya watu watakatifu kweli kutoka kwa wale waliopotoshwa na Shetani na kuhesabiwa miongoni kwa mashetani, na mtu anaweza kusema tu, inawachukua wale ambao wamepotoshwa na Shetani na kuwa mapepo na kuwageuza kurejea kuwa watu. Hii ndiyo tofauti baina ya kazi ya Roho Mtakatifu na ile ya roho waovu.

Kimetoholewa kutoka katika Ushirika kutoka kwa Aliye Juu

Hapa chini, hebu tuangalie baadhi ya utofauti mwingine waziwazi kati ya kazi mbalimbali za pepo wabaya na kazi ya Roho Mtakatifu, na namna ambavyo zinaonyeshwa kwa njia mahususi. Roho Mtakatifu huwachagua watu wanaofuatilia ukweli, na walio na dhamiri na mwelekeo, na wanaomiliki uadilifu. Hawa ndio aina ya watu ambao Roho Mtakatifu hufanya kazi ndani yao. Pepo wabaya huchagua watu ambao ni wajanja na wa kipuuzi, wasiopenda ukweli, na wasio na dhamiri wala mwelekeo. Watu kama hao ndio pepo wabaya hufanya kazi ndani yao. Ni nini tunachoona tunapolinganisha wale waliochaguliwa kwa kazi ya Roho Mtakatifu, na wale waliochaguliwa kwa kazi ile ya pepo wabaya? Tunaweza kuona kwamba Mungu ni mtakatifu, na mwenye haki, kwamba wale wanaochaguliwa na Mungu huutafuta ukweli, na wanayo dhamiri na mwelekeo, kwamba wanao uadilifu na wanapenda kile ambacho ni haki. Wale wanaochaguliwa na pepo wabaya ni wajanja, ni wachoyo na wenye dharau, hawaupendi ukweli, hawana dhamiri na mwelekeo, na hawautafuti ukweli. Pepo wabaya huchagua tu mambo mabaya na wale watu ambao si wa kweli, ambapo tunaona ya kwamba pepo wabaya wanapenda uovu na giza, kwamba wanawakimbia wale wanaoutafuta ukweli, na ni wepesi wa kuwamiliki wale ambao wako kombo na ni wajanja, wale ambao wanavutiwa na udhalimu, na wanaorogwa kwa urahisi. Wale ambao pepo wabaya huchagua kufanyia kazi ndani yao hawawezi kuokolewa, na wanaondolewa na Mungu. Ni lini, na ni katika mazingira gani, ndipo pepo wabaya hufanya kazi? Wao hufanya kazi wakati watu wamesonga mbali na Mungu na kuasi dhidi ya Mungu. Kazi ya pepo wabaya huwaroga watu, na hufanya hivyo kwa kuchukua fursa ile wanapotenda dhambi. Wakati watu wako katika hali yao dhaifu zaidi, hasa wanapokuwa katika maumivu makuu ndani ya mioyo yao, wakati wanapohisi vibaya na wakiwa wamechanganyikiwa, pepo mbaya huchukua fursa hii kujiingiza ndani polepole ili kuwaroga na kuwapotosha, kuleta kutoelewana kati yao na Mungu. Kunao wakati wa kazi ya Roho Mtakatifu: Wakati watu wanapomwita Mungu, wakati mioyo yao inapomgeukia Mungu, wanapomhitaji Mungu, wanapotubu kwa Mungu, na wanapoutafuta ukweli, basi ndipo Roho Mtakatifu huanza kufanya kazi ndani yao. Tazama namna ambavyo kila dhana ya kazi ya Roho Mtakatifu ilivyo ili kumwokoa mwanadamu, namna Anavyotafuta fursa za kumwokoa mwanadamu, ilhali pepo wabaya hutafuta fursa za kuwapotosha na kuwalaghai watu. Pepo wabaya wanayo dharau na ni waovu, ni wenye kudhuru kwa siri na wabaya, kila kitu wanachofanya kinalenga katika kumpotosha mwanadamu, na kumdhuru mwanadamu, na kumteketeza yeye. Wakati watu wanapohitaji msaada, wanapomtafuta Mungu kwa dharura, wanapohitaji wokovu wa Mungu, na wanapotaka kusonga karibu na Mungu ndani ya mioyo yao, Roho Mtakatifu hujitokeza kwao na kufanya kazi ya wokovu. Mungu ni upendo, na pepo wabaya ni chuki—hili liko wazi kwako, sivyo? Kile tu ambacho pepo wabaya hufanya ni ili kuwezesha kumteketeza na kumpotosha mwanadamu, na kile tu ambacho Roho Mtakatifu hufanya ni kwa upendo na wokovu wa mwanadamu. Athari ya kazi ya Roho Mtakatifu ni kuwatakasa watu, kuwaokoa dhidi ya kupotoka kwao, kuwaruhusu kujijua na kumjua Shetani, kuweza kuasi dhidi ya Shetani, kuweza kuufuatilia ukweli, na hatimaye kuishi kwa kudhihirisha mfanano wa mwanadamu. Pepo wabaya hupotosha, hutia najisi, na kuwafunga watu, huwaweka ndani zaidi ya dhambi, na kuwasababishia maumivu makubwa zaidi katika maisha yao, na hivyo wakati pepo wabaya wanapofanya kazi ndani ya watu, watu hao wamo hatarini; hatimaye, wanateketezwa na Shetani, jambo ambalo ni matokeo ya kazi ya pepo wabaya. Athari ya kazi ya Roho Mtakatifu ni kuweza hatimaye kuwaokoa watu, kuwafanya kuishi kwa kudhihirisha maisha halisi, kuwa huru na kukombolewa kabisa, na kupokea baraka za Mungu. Tazama: Pepo wabaya humweka mwanadamu katika giza, humpeleka kwenye shimo la kuzimu; Roho Mtakatifu humchukua mwanadamu kutoka kwenye giza, na kumpeleka kwenye mwangaza, na hadi kwenye uhuru. Kazi ya Roho Mtakatifu huwapa watu nuru na kuwaongoza watu, Huwapa fursa mbalimbali, na wanapokuwa wanyonge na dhambi Yeye huwapa faraja. Huwaruhusu watu kujijua, huwaruhusu kuufuatilia ukweli, na Halazimishi watu kufanya mambo, lakini Huwaacha kujichagulia njia yao wao wenyewe, na hatimaye Huwapeleka kwenye mwangaza. Pepo wabaya huwalazimisha watu kufanya mambo na kuwaamrisha hapa na pale. Kila kitu wanachosema ni uongo na kinawaroga watu, kuwadanganya na kuwafunga; pepo wabaya hawawapatii watu uhuru, hawawaruhusu kuchagua, huwalazimisha kufuata barabara ya maangamio, na hatimaye kuwaingiza ndani ya dhambi zaidi na zaidi, nakuwasababishia kifo.

Kimetoholewa kutoka katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha

Sifa ya wazi zaidi ya kazi ya pepo wabaya ni kwamba ni ya mwujiza, kwamba maneno ambayo pepo wabaya huyanena au huwauliza watu kufanya siyo ya kawaida, siyo ya mantiki, na hata huyasaliti maadili ya msingi ya ubinadamu wa kawaida na uhusiano wa kibinadamu, na kwamba yanakusudiwa kutofanya chochote ila kuwadanganya watu, kuwavuruga watu, na kuwapotosha watu. Pepo wabaya wanapowapagawa watu, baadhi yao huhisi hofu kubwa, wengine huingia katika hali isiyo ya kawaida, huku wengine wakichanganyikiwa, na wengine bado hujikuta wakiwa na wasiwasi wa ajabu na hawawezi kutulia tuli. Kwa vyovyote vile, pepo wabaya wanapowapagawa watu, watu hubadilika, kuwa kitu ambacho si binadamu wala pepo mbaya, na wao hupoteza ubinadamu wao wa kawaida. Hili linatosha kuthibitisha kuwa asili ya pepo wabaya ni mbaya na mbovu, ambayo kwa usahihi ndiyo asili ya Shetani. Pepo wabaya huwafanya watu kuwachukia kabisa na kuwadharau, na bila shaka hawana faida yoyote au msaada kwa watu. Mambo ya pekee ambayo Shetani na kila aina ya pepo wabaya wana uwezo wa kufanya ni kuwapotosha, kuwadhuru, na kuwameza watu.

Maonyesho makuu ya wale ambao wana kazi ya pepo wabaya (wale waliopagawa na pepo wabaya) ni:

Aina ya kwanza ni kwamba pepo wabaya huwaambia watu kufanya hili na lile, au kumwambia mtu kitu fulani, au kuwaelekeza watu kunena unabii wa uongo.

Aina ya pili ni kwamba watu mara nyingi hunena kile kinachodaiwa kuwa “lugha” katika sala ambazo hakuna anayezielewa, na hata wasemaji wenyewe hawaelewi. Baadhi ya wanenaji wanaweza hata “kuifasiri lugha” wenyewe.

Aina ya tatu ni kwamba mtu mara nyingi hupokea ufunuo, kwa marudio mengi, wakati huu akielekezwa kwa njia hii na pepo wabaya, wakati ufuatao akielekezwa kwenye njia ile, katika hali ya daima ya wasiwasi.

Aina ya nne ni kwamba watu ambao wana kazi ya pepo wabaya wanataka kufanya hili ama lile kwa haraka, wakikosa subira mno kiasi cha kutongoja, huwa hawafikirii kama hali zinaruhusu, hata hukimbia nje usiku wa manane na tabia yao hasa si ya kawaida.

Aina ya tano ni kwamba watu wenye kazi ya pepo wabaya huwa na kiburi ovyo ovyo, hawana mantiki, na usemi wao wote ni wa kujionyesha kuwa bora na huwa unakuja kutoka kwa nafasi ya kuamuru. Wao huwakanganya watu, na kama pepo wabaya, huwalazimisha watu kufanya mambo.

Aina ya sita ni kwamba watu ambao wana kazi ya pepo wabaya hawawezi kushiriki kuhusu ukweli, sembuse kuzingatia kazi ya Mungu, na wao ni waasi kwa Mungu na hutenda kiholela, wakifanya vitendo viovu vya ukatili vya kila aina ili kuharibu utaratibu wa kawaida wa kanisa.

Aina ya saba ni kwamba mtu ambaye ana kazi ya pepo wabaya hujifanya kuwa mtu mwingine bila sababu yoyote, au hudai kwamba alitumwa na mtu fulani na kwamba watu wanafaa kumsikiliza. Hakuna mtu anayeweza kuelewa alikotoka.

Aina ya nane ni kwamba watu ambao wana kazi ya pepo wabaya aghalabu hawana hisi ya kawaida, wala hawaelewi ukweli wowote; hawana uwezo wowote wa kupokea na pia hawajapatiwa nuru na Roho Mtakatifu, na kile ambacho watu huona ni kwamba katika kupokea mambo hawa watu ni wapuuzi visivyo kawaida na si sahihi hata kidogo.

Aina ya tisa ni kwamba watu ambao wana kazi ya pepo wabaya huzingatia hasa kuwakemea wengine wakati wa kazi, daima wao hutenda ovyo ovyo na daima husababisha vurugu na usumbufu; kila kitu wanachokifanya na kusema huwashambulia, kuwafunga na kuwapotosha watu wengine, na wao hufikia kiwango cha kuwavunjia watu azma zao na kuwafanya kuwa hasi ili wasiweze kufanikiwa upya baada ya hali ngumu. Wao ni mashetani, kwa kweli kabisa, ambao huwadhuru wengine, hucheza na wengine na kuwala, nao hufurahi kwa siri wanapofanya wapendavyo. Hili ndilo lengo kuu la kazi ya pepo wabaya.

Aina ya kumi ni kwamba watu ambao wana kazi ya pepo wabaya huishi maisha yasiyo ya kawaida kabisa. Macho yao hutoa kimulimuli cha kiuaji, na maneno wanyozungumza ni ya kuogofya kabisa, kana kwamba pepo mbaya alikuwa ameshuka ulimwenguni. Hakuna utaratibu wa maisha kwa mtu wa aina hii, ni vigeugeu sana, na ni watu wasiobashirika kama mnyama wa mwitu ambaye hajafunzwa. Wao ni wa kuwakirihi na kuwachukiza wengine sana. Hivyo ndivyo hasa mtu ambaye pepo wabaya wamemfunga anavyoonekana.

Aina kumi zilizo hapo juu ndizo maonyesho makuu ya kazi ya pepo wabaya. Mtu yeyote ambaye huonyesha mojawapo ya maonyesho haya bila shaka atakuwa na kazi ya pepo wabaya. Ili kuwa dhahiri, wote ambao huonyesha maonyesho yaliyo hapo juu ya kazi ya pepo wabaya, bila kujali ni aina gani wanamiliki, ni watu ambao wana kazi ya pepo wabaya. Watu ambao wamepagawa na pepo wabaya mara nyingi hasa wanakuwa wenye chuki na kujitenga na wale ambao Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yao na wanaoweza kuuongea ukweli. Ndivyo inavyokuwa mara nyingi kwamba watu wanapokuwa bora zaidi, ndipo wanapotaka kuwashambulia na kuwashutumu, ilhali watu wanapokosa mwelekeo na kuchanganyikiwa zaidi, ndipo wanapofanya kadri wanachoweza kuwalaghai na kuwavisha kilemba cha ukoka, na hasa wao kuwa radhi kujihusisha nao. Kazi ya pepo wabaya hugeuza nyeusi ikawa nyeupe, na kuyafanya mazuri kuwa mabaya na mabaya kuwa mazuri. Hayo ndiyo matendo ya pepo wabaya.

Kimetoholewa kutoka katika Mipango ya Kazi

Roho yoyote ambayo kazi yake inajionyesha katika hali isiyo ya ulimwenguni humu ni pepo mbaya, na kazi na matamko ya roho yoyote inayotekeleza kazi isiyo ya ulimwenguni humu ndani ya watu ni kazi ya pepo mbaya; mbinu hizi zote ndizo ambazo pepo wabaya hufanya kazi na si za kawaida na za humu ulimwenguni, na zinaonyeshwa kimsingi kwa njia sita zifuatazo:

1. Udhibiti wa moja kwa moja wa uneni wa watu, jambo ambalo linaonyesha waziwazi kwamba pepo mbaya anazungumza, na wala si watu wenyewe wanaozungumza kwa kawaida;

2. Hisia kwamba pepo mbaya anawaelekeza watu na kuwaamuru kufanya hiki na kile;

3. Watu ambao, wakati wakiwa kwenye chumba, wanaweza kujua wakati mtu yuko karibu kuingia ndani;

4. Watu ambao mara nyingi wanazisikia sauti zikiwazungumzia na ambazo wengine hawawezi kuzisikia;

5. Watu ambao wanaweza kuona na kusikia mambo ambayo wengine hawawezi;

6. Watu ambao siku zote wanafadhaishwa, na wanajizungumzia wenyewe, na hawawezi kuwa katika mazungumzo ya kawaida au utangamano na watu.

Wale wote ambao pepo mbaya anafanya kazi ndani yao bila kuepukika wanayo maonyesho haya sita. Wao hawana urazini, siku zote wako katika hali ya taharuki, hawawezi kutangamana na watu kwa njia ya kawaida, ni kana kwamba wao hawashawishiki kwa lolote lile, na kuna jambo lililojitenga na lisilo lao. Watu kama hao wamepagawa na pepo mbaya au wanaye pepo mbaya anayefanya kazi ndani yao, na kazi yote ya pepo wabaya inajionyesha na si ya ulimwenguni humu. Hii ndiyo kazi inayotambulika kwa haraka zaidi kuhusu pepo wabaya. Wakati pepo mbaya anapompagaa mtu, anacheza nao kiasi cha kwamba wanaathirika kabisa. Wanakosa urazini, kama zuzu, hali ambayo inathibitisha kwamba kiini cha mambo ni kuwa, pepo wabaya ni pepo waovu wanaopotosha na kuteketeza watu. Matamko ya pepo wabaya ni rahisi kuyatambua: Matamko yao yanaonyesha kikamilifu kiini chao cha uovu, yapo palepale, yamevurugika, na yananuka, yanarishai harufu ya kifo. Kwa watu walio na uhodari mzuri, maneno ya pepo wabaya huwafanya kuhisi utupu na kutovutiwa, yasiyorekebisha maadili, yasiyo na chochote ila uongo na maneno yasiyo na maana, wanahisi wakiwa wamevurugika na wanaona ugumu kuelewa yote haya, kama zigo la upuuzi. Huu ni baadhi ya upuuzi unaotambulika kwa haraka zaidi kuhusu pepo wabaya. Kuwaroga watu, baadhi ya wale pepo wabaya wa “kiwango cha juu” hujifanya kuwa Mungu au Kristo wanapoongea, huku wengine wakijifanya kuwa malaika au watu maarufu. Wanapoongea, pepo hawa wabaya ni stadi katika kuiga maneno au kauli fulani za Mungu, au sauti ya Mungu, na watu wasiouelewa ukweli wanadanganywa kwa urahisi na pepo kama hawa wabaya wa “kiwango cha juu.” Watu wa Mungu waliochaguliwa lazima wawe wazi kwamba, kiini cha mambo ni kwamba, pepo wabaya ni waovu na wasio na aibu, na hata kama wao ni pepo wabaya wa “kiwango cha juu,” wao hawana ukweli kabisa. Pepo wabaya, zaidi ya yote, ni pepo wabaya, kiini cha pepo wabaya ni uovu, na wenye sampuli moja na Shetani.

Kimetoholewa kutoka katika Mipango ya Kazi

Iliyotangulia: 1. Utofautishaji Kati ya Kazi ya Mungu na Ile ya Mwanadamu

Inayofuata: 3. Utofautishaji Kati ya Kristo wa Kweli na Makristo wa Uongo

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp