103 Kazi ya Kumsimamia Mwanadamu ni Kazi ya Kumshinda Shetani

1 Mungu hana nia mbaya kwa viumbe na anataka tu kumshinda Shetani. Kazi yote Yake—iwe ni kuadibu ama hukumu—inaelekezwa kwa Shetani; inafanyika kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu, yote ni kwa ajili ya kumshinda Shetani, na ina lengo moja: kufanya vita na Shetani mpaka mwisho kabisa! Na Mungu kamwe hatapumzika kabla ya kuwa mshindi dhidi ya Shetani! Atapumzika tu punde atakapomshinda Shetani. Kwa sababu kazi yote ambayo inafanywa na Mungu inaelekezwa kwa Shetani, na kwa sababu wale waliopotoshwa na Shetani wote wanadhibitiwa na milki ya Shetani na wote wanamilikiwa na Shetani, bila kupigana dhidi ya Shetani na kuwa huru dhidi yake, Shetani hangepumzisha kushika kwake kwa watu hawa, na hawangeweza kupatwa. Kama hawangepatwa, ingethibitisha kwamba Shetani hajashindwa, ya kwamba hajatiishwa.

2 Na kwa hivyo, katika miaka 6,000 ya mpango wa usimamizi wa Mungu, katika hatua ya kwanza Yeye alifanya kazi ya sheria, wakati wa hatua ya pili Yeye alifanya kazi ya Enzi ya Neema, yaani, kazi ya kusulubiwa, na wakati wa hatua ya tatu Yeye alifanya kazi ya kumshinda mwanadamu. Kazi hizi zote zinaelekezwa kwa kiwango ambacho Shetani alikuwa amewapotosha wanadamu, yote ni kwa ajili ya kumshinda Shetani, na hakuna hatua hata moja ambayo si kwa ajili ya kumshinda Shetani. Kiini cha miaka 6,000 ya kazi ya Mungu ya usimamizi ni vita dhidi ya joka kubwa jekundu, na kazi ya kusimamia watu pia ni kazi ya kumshinda Shetani, na kazi ya kufanya vita na Shetani. Mungu amepigana vita kwa miaka 6,000, na hivyo kufanya kazi kwa miaka 6,000, ili hatimaye kuleta mwanadamu katika ulimwengu mpya. Wakati Shetani atashindwa, mwanadamu atakuwa amewekwa huru kabisa. Kila hatua ya kazi ni kwa mujibu wa mahitaji halisi na matakwa ya mwanadamu, na ni kwa ajili ya kumshinda Shetani.

Umetoholewa kutoka katika “Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 102 Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Zimemwokoa Mwanadamu Kabisa

Inayofuata: 104 Watu Ambao Wamepatwa na Mungu Watafurahia Baraka za Milele

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp