592 Kufanya Kazi kwa Uzembe Si Kutekeleza Wajibu
1 Kwa kufanya kazi kwa namna isiyo ya dhati ni kitu kichukiwacho sana kwa wajibu. Ukiendelea tu kutenda kwa namna isiyo ya dhati, hutaweza kutekeleza wajibu wako kiasi cha kutosha. Lazima uwe na shauku ya kuutekeleza! Fursa ya mtu kufanya wajibu wake ni jambo adimu, na asipochukua fursa hiyo ambayo Mungu amempa, basi itapotea. Siku moja akijaribu tena kutafuta nafasi ya kutekeleza wajibu wake, haitakuwa rahisi; kwa kweli, yawezekana fursa kama hiyo haitatokea hata kidogo. Kazi ya Mungu haimsubiri mtu yeyote, vilevile nafasi ya kutekeleza wajibu wa mtu. Si fursa nyingi ambazo huja, kwa hivyo lazima uzichukue.
2 Watasema kwamba wewe hufanya kila kitu kwa namna ya shaghalabaghala, ukipuuza chochote unachofanya; wewe si mwangalifu hata kidogo katika kazi yako. Ukilazimishwa kufanya jambo, basi wakati huo tu ndipo unapotia bidii kidogo; kama kuna mtu anayeangalia iwapo kazi yako imefikia kiwango kinachotakiwa, wakati huo unafanya kazi nzuri zaidi—lakini iwapo hapana mtu wa kuangalia, unazembea kidogo. Ukishughulikiwa, basi unajitahidi; vinginevyo, unasinzia kila wakati kazini na kujaribu kukwepa lawama kadiri uwezavyo, ukidhani kuwa hakuna atakayegundua. Muda unapita, na watu wanagundua. Watu watambaini kabisa, na atakuwa amepoteza kabisa heshima na uadilifu. Iwapo hakuna mtu anayeweza kumwamini, basi Mungu anawezaje kumwamini? Mtu kama huyo haaminiki.
3 Kwa upana, iwapo mtu kama huyo hufanya tu wajibu wake kwa namna isiyo ya dhati kila mara, na akiendelea kuwa mzembe kwa Mungu, basi yeye yuko katika hatari kubwa! Je, matokeo ya kuwa mdanganyifu kwa makusudi ni yapi? Kwa muda mfupi, utakuwa na tabia potovu, utafanya dhambi za mara kwa mara bila kutubu na hutajifunza jinsi ya kutenda ukweli wala hutautia katika vitendo. Kwa muda mrefu, unapofanya mambo hayo siku zote, matokeo yako yatatoweka; jambo hili litakuingiza matatani. Hali hii inajulikana kama kutofanya makosa makubwa bali kufanya makosa madogo siku zote. Mwishowe jambo hili litakusababishia athari zisizorekebishika. Hilo litakuwa jambo baya sana!
Umetoholewa kutoka katika “Uingiaji Katika Uzima Lazima Uanze na Uzoefu wa Kutenda Wajibu wa Mtu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo