364 Wewe ni Mwasi Sana

1 Nyinyi ni waasi sana, upinzani wenu ni mkubwa sana, mnaniangalia kwa dharau sana, hamnithamini hata kidogo Kwangu, mnanipenda kidogo sana, na mnanichukia sana. Mnadharau kazi Yangu, na kutweza vitendo Vyangu sana. Utiifu wenu uko wapi? Tabia zenu ziko wapi? Upendo wenu uko wapi? Ni lini mmeonyesha wazi dalili ya upendo ndani yenu? Ni lini mmechukua kazi Yangu kwa uzito kabisa?

2 Je, mliwahi kutambua kile mfanyacho leo: kufanya ghasia ulimwenguni, kupanga njama dhidi ya nyinyi kwa nyinyi, kudanganyana, kutenda kwa uongo, wasiri na kwa ukavu wa macho, kutojua ukweli, kuwa wasio waaminifu na wadanganyifu, kutenda ubembelezaji, nyinyi kujiona daima kuwa waadilifu na bora zaidi kuliko wengine, kuwa wenye kiburi, na kutenda kikatili kama wanyama wa mwitu milimani na kwa fujo kama mfalme wa wanyama—huu ndio mfano wa mwanadamu? Nyinyi ni fidhuli na wasio na busara. Hamjawahi kuliona neno Langu kuwa hazina, lakini badala yake mmechukua mtazamo wa dharau.

3 Kwa njia hii, mafanikio, maisha ya kweli ya binadamu, na matumaini mazuri yangetoka wapi? Je, wazo lako badhirifu litakuokoa kwa kweli kutoka kwa kinywa cha chui? Kweli litakuokoa kutoka kwa moto unaowaka? Je, ungekuwa umeanguka hadi hapa iwapo kwa kweli ungeiona kazi Yangu kuwa kitu cha thamani kubwa mno? Inaweza kuwa kwamba majaliwa yako kweli hayawezi kubadilishwa? Je, uko tayari kufa na majuto kama haya?

Umetoholewa kutoka katika “Asili na Utambulisho wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 363 Watu Hawajui Jinsi Walivyo Duni

Inayofuata: 365 Asili Yako ni Potovu Sana

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp