410 Bado Una Imani Iliyokanganywa

1 Wengi wamenifuata bila kusita hadi leo, na katika miaka hii michache, nyote mmepitia uchovu mwingi. Nimefahamu vizuri tabia ya asili na mazoea ya kila mmoja wenu, na imekuwa vigumu sana kuingiliana nanyi. Cha kusikitisha ni kwamba ingawa nina maarifa nyingi kuwahusu, hamna ufahamu hata kidogo kunihusu. Hamwelewi chochote kuhusu tabia Yangu, na hata zaidi hamwezi kufahamu yaliyo akilini Mwangu. Sasa ninyi kunielewa visivyo kunaongezeka haraka, na imani yenu Kwangu inabaki ile imani iliyokanganyika.

2 Badala ya kusema kwamba mna imani na Mimi, ingekuwa bora kusema kwamba nyote mnajaribu kujipendekeza Kwangu na kunibembeleza. Nia zenu ni rahisi sana—yeyote anayeweza kunituza, nitamfuata, na yeyote anayeweza kuniwezesha kutoroka majanga makubwa, nitaamini kwake, awe Mungu ama Mungu fulani yeyote. Hakuna kati ya haya yanayonihusu. Kuna wanadamu wengi kama hao kati yenu, na hali hii ni nzito sana. Ikiwa siku moja, majaribio yatafanywa kuona ni wangapi kati yenu wanamwamini Kristo kwa sababu mna umaizi kuhusu kiini Chake, basi Nahofia kwamba hakuna mmoja wenu atakuwa na uwezo kufanya Ninavyotaka.

3 Hivyo haitakuwa hoja kwa kila mmoja wenu kuzingatia swali hili: Mungu mliye na imani na Yeye ni tofauti sana na Mimi, na kwa hivyo, nini basi ni kiini cha imani yenu kwa Mungu? Kadri mnavyozidi kuamini katika mnayedai kuwa Mungu wenu, ndivyo mnavyozidi kupotea mbali sana nami. Basi, ni nini msingi wa suala hili? Nina uhakika hakuna mmoja wenu amewahi kufikiria suala hili, lakini mmefikiria uzito wake? Mmewaza kuhusu matokeo ya kuendelea na imani ya namna hii?

Umetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 409 Watu Hawamwamini Mungu kwa Kweli

Inayofuata: 411 Kumwamini Mungu Lakini Kutokubali Ukweli ni Kuwa Asiyeamini

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp