365 Asili Yako ni Potovu Sana

1 Wale wasioelewa mapenzi ya Mungu ni wapinzani wa Mungu; wale wanaoelewa mapenzi ya Mungu lakini bado hawauweki ukweli katika vitendo ni wapinzani wa Mungu; wale wanaokula na kunywa maneno ya Mungu lakini bado wanaenda dhidi ya kiini cha maneno ya Mungu ni wapinzani wa Mungu; wale walio na dhana za Mungu mwenye mwili na wanaasi makusudi ni wapinzani wa Mungu; wale wanaomhukumu Mungu ni wapinzani wa Mungu; na yeyote asiyeweza kumjua Mungu na kumshuhudia ni mpinzani wa Mungu. Kwa hivyo sikiliza ushawishi Wangu: Kama kweli una imani ya kutembea njia hii, basi zidi kuifuata. Iwapo huwezi kuepuka upinzani kwa Mungu, basi ni bora kwenda zako kabla hujachelewa. Vinginevyo, inaashiria mabaya badala ya mazuri, kwani asili yenu ni potovu sana.

2 Kama kweli una imani ya kutembea njia hii, basi zidi kuifuata. Iwapo huwezi kuepuka upinzani kwa Mungu, basi ni bora kwenda zako kabla hujachelewa. Vinginevyo, inaashiria mabaya badala ya mazuri, kwani asili yenu ni potovu sana. Huna uaminifu ama utii hata kidogo, ama moyo ulio na kiu ya haki na ukweli. Na wala huna upendo hata kidogo kwa Mungu. Inaweza kusemwa kuwa hali yako mbele ya Mungu imesambaratika kabisa. Huwezi kushika unachopaswa wala kusema unachopaswa. Huwezi kuweka katika vitendo kile ambacho unapaswa, na huwezi kutekeleza kazi unayopaswa. Huna uaminifu, dhamiri, utii ama azimio unalopasa. Hujavumilia mateso unayopaswa kuwa umevumilia, na huna imani unayopaswa kuwa nayo. Huna sifa yoyote kabisa; una heshima binafsi ya kuendelea kuishi?

3 Unaamini katika Mungu lakini bado hujui mapenzi Yake; unakula na kunywa maneno ya Mungu lakini bado huwezi kukidhi mahitaji Yake. Unaamini katika Mungu lakini bado humjui, na kuishi ingawa huna lengo la kujaribu kufikia. Huna maadili na huna madhumuni. Unaishi kama mwanadamu lakini huna dhamiri, uadilifu wowote wala hata uaminifu kidogo. Unafikiriwaje kuwa wanadamu? Unaamini katika Mungu lakini unamdanganya. Zaidi ya hayo, unachukua pesa za Mungu na kula sadaka Yake, na bado, mwishowe, huonyeshi fikira kwa hisia za Mungu ama dhamiri kwa Mungu. Huwezi hata kukidhi mahitaji ya Mungu ya chini zaidi. Kwa hivyo unawezaje kufikiriwa kuwa mwanadamu? Chakula unachokula na hewa unayopumua vimetoka kwa Mungu, unafurahia neema Yake, na bado mwishowe, huna hata ufahamu mdogo wa Mungu. Kinyume na hayo, umekuwa mtu asiye na maana anayempinga Mungu. Si basi wewe ni mnyama asiye bora kuliko mbwa? Kuna mnyama yeyote aliye mkatili kukuliko wewe?

Umetoholewa kutoka katika “Watu Wote Wasiomjua Mungu Ni Watu Wanaompinga Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 364 Wewe ni Mwasi Sana

Inayofuata: 366 Wale Wasioweza Kufuata Kazi ya Mungu Wataondolewa

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp