15 Mungu Amerejea Na Ushindi

1 Sayuni! Salamu! Sayuni! Ita kwa sauti! Nimerudi kwa ushindi, Nimerudi nikiwa mshindi! Watu wote! Harakisheni mpange foleni kwa utaratibu! Vitu vyote! Mtakuja kusimama kabisa, kwa sababu nafsi Yangu inaukabili ulimwengu mzima na nafsi Yangu inaonekana katika Mashariki ya dunia! Nani anayethubutu kutopiga magoti katika ibada? Nani anayethubutu kutoniita Mungu wa kweli? Nani anayethubutu kutoangalia juu kwa kumcha? Nani anayethubutu kutotoa sifa? Nani anayethubutu kutangaza kwa shangwe? Watu wangu wataisikia sauti Yangu!

2 Milima, mito, na vitu vyote vitashangilia bila kukoma, na kurukaruka bila kupumzika. Wakati huu, hakuna atakayethubutu kurudi nyuma, hakuna atakayethubutu kusimama katika upinzani. Hili ni tendo Langu la ajabu, na hata zaidi ni nguvu Yangu kuu! Nitafanya kila kitu kiniche Mimi katika moyo wake na hata zaidi Nitafanya kila kinisifu Mimi. Hili ni lengo la msingi la mpango Wangu wa usimamizi wa miaka elfu sita, nami Nimeamua hili. Hakuna hata mtu mmoja, hakuna hata kitu kimoja wala jambo moja, linathubutu kusimama kunipinga Mimi, au linathubutu kusimama kushindana na Mimi.

3 Watu wangu wote wataelekea mlimani Kwangu nao watatii mbele Zangu kwa sababu Ninao uadhama na hukumu, nami Nina mamlaka. Hakuna kitu kitakuwa kigumu Kwangu. Kila kitu kitaharibiwa kwa maneno kutoka kinywani Mwangu, na ni kwa sababu ya maneno kutoka kinywani Mwangu ndipo yatatukia na kufanyika kamili, hiyo ni nguvu Yangu kuu na hayo ni mamlaka Yangu. Kwa sababu Nina nguvu tele na nimejawa na mamlaka, hakuna mtu anayeweza kuthubutu kunizuia Mimi. Tayari Nimepata ushindi juu ya kila kitu na Nimewashinda wana wote wa uasi.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 120” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 14 Mungu Ameonekana Mashariki mwa Dunia na Utukufu

Inayofuata: 16 Hema ya Mungu Yamekuja Duniani

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp