903 Mamlaka ya Mungu ni ya Pekee

1 Mamlaka ya Mungu ni ya kipekee. Ndiyo maonyesho ya sifa ya, na hali halisi maalum ya, utambulisho wa Mungu Mwenyewe. Hakuna kiumbe ambacho kiliumbwa wala kile ambacho hakikuumbwa kinachomiliki maonyesho ya sifa kama hizi na hali halisi maalum; Muumba tu ndiye anayemiliki aina hii ya mamlaka. Hivyo ni kusema kwamba, ni Muumba tu—Mungu Yule wa Kipekee—ambaye anaonyeshwa kwa njia hii na ndiye aliye na hali halisi hii.

2 Ingawaje kauli hii “Mamlaka ya Mungu” inaweza kuonekana kama isiyoeleweka, mamlaka ya Mungu kwa kweli si ya dhahania kamwe. Yeye yupo na binadamu kila dakika ya maisha yake, akimwongoza kila siku. Kwa hivyo, katika maisha ya kila siku ya kila mtu ataweza haswa kuona na kupitia dhana halisi ya mamlaka ya Mungu. Uhalisi huu ni ithibati tosha kwamba mamlaka ya Mungu kwa kweli yapo, na unakuruhusu kabisa kutambua na kuelewa hoja hii kwamba Mungu anamiliki mamlaka haya. Mungu aliumba kila kitu, na baada ya kukiumba, Anao utawala juu ya kila kitu. Kuongezea kuwa na utawala juu ya kila kitu, pia anadhibiti kila kitu.

3 Kutoka kwenye kauli ile ile “Mungu anadhibiti kila kitu” tunafaa kuona kwamba kile ambacho Mungu anadhibiti si sehemu ya sayari, sehemu ya uumbaji, wala sehemu ya mwanadamu, lakini kila kitu: kuanzia kwa viumbe vile vikubwa hadi vile vidogovidogo, kuanzia kwa vile vinavyoonekana hadi visivyoonekana, kuanzia kwa nyota ulimwenguni hadi kwenye vitu vilivyo na uhai ulimwenguni, pamoja na viumbe vidogovidogo visivyoweza kuonekana kwa macho ya kawaida au viumbe vilivyo katika maumbo mengine. Huu ndio ufafanuzi hakika wa “kila kitu” ambacho Mungu “anadhibiti,” na ndio upana ambao Mungu anaonyesha ukuu Wake, urefu wa utawala na kanuni Yake.

Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 902 Hadhi na Utambulisho wa Mungu Mwenyewe

Inayofuata: 904 Mamlaka ya Mungu ni Ishara ya Utambulisho Wake

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp