A. Kuhusu Mamlaka ya Mungu

529. Katika upana wa ulimwengu na anga, viumbe wasiohesabika wanaishi na kuzaana, hufuata sheria ya mzunguko wa maisha na kufuata sheria isiyobadilika. Wanaokufa huenda na hadithi za walio hai, na walio hai hurudia historia hii yenye huzuni ya wale waliokufa. Na kwa hivyo wanadamu hawawezi kujizuia ila kujiuliza wenyewe; Kwa nini tunaishi? Na kwa nini inatulazimu kufa? Nani anayeitawala dunia hii? Na ni nani muumbaji wa mwanadamu? Je, kweli wanadamu waliumbwa na mazingira asilia? Je, kweli wanadamu wana uamuzi juu ya hatima yao? … Kwa maelfu ya miaka wanadamu wameyauliza haya maswali, tena na tena. Kwa bahati mbaya, jinsi wanadamu wanavyopagawa na haya maswali, ndivyo kiu yao ya sayansi huendelea kukua. Sayansi hupatiana kutosheleza kwa muda na raha ya muda ya mwili, ila haitoshi kumpa mwanadamu uhuru kutokana na upweke, ukiwa, na hofu isiyodhihirika na kutosaidika ndani ya moyo wake. Wanadamu hutumia ujuzi wa kisayansi ambao wanaweza kuona kwa macho na kuelewa kwa akili yake ili kuutuliza moyo wao. Ilhali maarifa kama hayo ya kisayansi hayatoshi kuwazuia wanadamu kutafiti siri. Wanadamu hawajui kabisa Mkuu wa ulimwengu na vitu vyote ni nani, sembuse kujua mwanzo na mustakabali wa wanadamu. Wanadamu wanaishi tu, bila budi, katikati ya hii sheria. Hakuna anayeweza kuiepuka wala kuibadilisha kwani katika vitu vyote na katika mbingu kuna Mmoja kutoka milele hadi milele ambaye ni Mkuu wa kila kitu. Ni Yeye ambaye Hajawahi kuonekana na mwanadamu, ambaye wanadamu hawajawahi kumjua, ambaye wanadamu hawajawahi kuamini kuwepo Kwake, na bado ni Yeye Aliyewapulizia pumzi mababu wa wanadamu na kuwapa wanadamu uhai. Ni Yeye ndiye Huruzuku na kustawisha wanadamu kwa kuishi kwao, na huwaongoza wanadamu hadi siku ya leo. Aidha, Yeye na Yeye pekee ni wa kutegemewa na wanadamu ili kuendelea kuishi. Ni Mkuu wa kila kitu na Hutawala viumbe vyote vyenye uhai chini ya dunia. Huamrisha misimu yote minne, na ni Yeye huita upepo, jalidi, theluji na mvua. Huwapa wanadamu mwangaza wa jua na huleta machweo ya jioni. Ni Yeye Aliyeumba mbingu na ardhi, Akampa mwanadamu milima, maziwa na mito na kila kitu kilicho na uhai ndani yake. Matendo Yake yamo kila mahali, nguvu Zake ziko kila mahali, busara Zake ziko kila mahali na mamlaka Yake yako kila mahali. Kila mojawapo ya hizi sheria na kanuni ni mfano mzuri wa matendo Yake, na kila mojawapo inafichua hekima na mamlaka Yake. Nani anayeweza kujiondoa kutoka kwa ukuu Wake? Na ni nani anayeweza kujitoa mwenyewe katika njia Zake? Kila kitu kinaishi chini ya uangalizi Wake, zaidi ya hayo, kila kitu huishi chini ya ukuu Wake. Matendo na nguvu Zake huwaacha wanadamu bila chaguo ila kutambua ukweli kwamba ni Yeye pekee Anayeishi na Ana ukuu juu ya kila kitu. Hakuna kitu chochote ila Yeye kinachoweza kuamuru dunia, wala kuwajibikia wanadamu bila kukoma. Bila kujali kama unaweza kutambua vitendo vya Mungu, bila kujali kama unaamini katika kuwepo kwa Mungu, hakuna shaka kuwa hatima yako inaegemea katika mipango ya Mungu, na hakuna shaka kuwa Mungu atakuwa na ukuu juu ya kila kitu. Uwepo na utawala Wake haviwezi kutabiriwa ikiwa vinatambulika na kufahamika na binadamu au la. Ni Yeye pekee Anayejua kuhusu yaliyopita ya mwanadamu, yaliyomo na yanayojiri, na Yeye pekee ndiye mwamuzi wa hatima ya wanadamu. Haijalishi kama unaukubali huu ukweli, haitachukua muda mrefu kabla mwanadamu kushuhudia haya yote kwa macho yake mwenyewe, na huu ni ukweli ambao hivi karibu Mungu Ataudhihirisha. Wanadamu huishi na hufa chini ya macho yake Mungu. Wanadamu huishi kwa usimamizi wa Mungu, na wakati macho Yake yatafumbika kwa mara ya mwisho, hio pia ni kwa usimamizi Wake. Tena na tena, mwanadamu huja na kwenda, nyuma na mbele. Bila mapendeleo, yote ni sehemu ya ukuu na michoro ya Mungu. Usimamizi wa Mungu ungali unaendelea mbele na haujawahi kusimama. Atawafanya wanadamu wafahamu uwepo Wake, waamini katika ukuu Wake, watazame matendo Yake, na warudi katika ufalme Wake. Huu ni mpango Wake, na kazi ambayo Amekuwa Akiitekeleza kwa maelfu ya miaka.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 3: Mwanadamu Anaweza tu Kuokolewa Katikati ya Usimamizi wa Mungu

530. Tangu Alipoanza uumbaji wa viumbe vyote, nguvu za Mungu zilianza kuonyeshwa na zikaanza kufichuliwa, kwani Mungu alitumia maneno kuumba vitu vyote. Haijalishi ni njia gani Alitumia, haijalishi ni kwa nini Aliviumba, viumbe vyote viliumbwa na kusimama imara na kuwepo kwa sababu ya matamshi ya Mungu, na haya ndiyo mamlaka ya kipekee ya Muumba. Kwenye muda kabla ya mwanadamu kuumbwa ulimwenguni, Muumba alitumia nguvu na mamlaka Yake kuumba viumbe vyote kwa minajili ya mwanadamu, na Akatumia mbinu za kipekee kutayarisha mazingira yanayofaa kuishi mwanadamu. Kwa yote Aliyoyafanya, ilikuwa ni kwa kumtayarishia mwanadamu ambaye hivi karibuni angepokea pumzi Zake. Hivi ni kusema kwamba, kwenye muda ule kabla ya mwanadamu kuumbwa, mamlaka ya Mungu yalionyeshwa kupitia kwenye viumbe vyote tofauti na mwanadamu, na vitu vikubwa kama vile mbingu, nuru, bahari, na ardhi, na vile vilivyo vidogo kama vile wanyama na ndege, pamoja na wadudu na vijiumbe vyote vya kila aina, zikiwemo vimelea mbalimbali visivyoonekana kwa macho ya kawaida. Kila mojawapo kilipewa maisha kwa matamshi ya Muumba, na kila kiumbe mojawapo kilizaana kwa sababu ya matamshi ya Muumba na kila kimojawapo kiliishi chini ya ukuu wa Muumba kwa sababu ya matamshi ya Muumba. Ingawa hawakupokea pumzi za Muumba, bado walionyesha maisha na nguvu walizopewa na Muumba kupitia kwa mifumo na miundo yao mbalimbali; Ingawa hawakupokea uwezo wa kuongea aliopewa mwanadamu na Muumba, kila kimojawapo kilipokea njia ya kuelezea maisha yao ambayo walipewa na Muumba, na ambayo ilitofautiana na ile lugha ya Mwanadamu. Mamlaka ya Muumba hayatoi tu nguvu za maisha kwenye vifaa vinavyoonekana kuwa tuli, ili visiwahi kutoweka, lakini, vilevile, hupatia silika ya kuzaana na kuongezeka kwa kila kiumbe hai, ili visiwahi kutoweka, na ili kizazi baada ya kizazi, vitaweza kupitisha sheria na kanuni za kuishi walizopewa na Muumba. Namna ambavyo Muumba anatilia mkazo mamlaka Yake haikubaliani kwa lazima na mtazamo wa mambo makubwa makubwa au madogomadogo, na haiwekewi mipaka ya umbo lolote; Anaweza kuamuru utendaji mambo katika ulimwengu na kushikilia ukuu juu ya maisha na kifo cha viumbe vyote, na, vilevile, Anaweza kushughulikia viumbe vyote ili viweze kumhudumia Yeye; Anaweza kusimamia kazi zote za milima, mito, na maziwa, na kutawala viumbe vyote ndani yake, na, zaidi ya hayo, Anaweza kutoa kile ambacho kinahitajika na viumbe vyote. Haya ndiyo maonyesho ya mamlaka ya pekee ya Muumba miongoni mwa viumbe vyote mbali na mwanadamu. Maonyesho kama hayo si tu ya maisha tunayoishi, na hayatawahi kusita, au kupumzika, na hayawezi kubadilishwa au kuharibiwa na mtu yeyote au kitu chochote, wala hayawezi kuongezwa au kupunguzwa na mtu yeyote au kitu chochote—kwani hamna kile kinachoweza kubadilisha utambulisho wa Muumba, na, hivyo basi, mamlaka ya Muumba hayawezi kubadilishwa na kiumbe chochote kilichoumbwa, na hayawezi kufikiwa na kiumbe chochote ambacho hakikuumbwa. Chukulia wajumbe na malaika wa Mungu kwa mfano. Hawamiliki nguvu za Mungu, isitoshe hawamiliki mamlaka ya Muumba, na sababu ambayo hawana nguvu na mamlaka ya Mungu ni kwa sababu hawamiliki ile hali halisi ya Muumba. Vile viumbe ambavyo havikuumbwa, kama vile wajumbe na malaika wa Mungu, Ingawa vinaweza kufanya baadhi ya mambo kwa niaba ya Mungu, haviwezi kuwakilisha Mungu. Ingawa wanamiliki nguvu fulani zisizomilikiwa na binadamu, hawamiliki mamlaka ya Mungu, hawamiliki mamlaka ya Mungu ya kuumba viumbe vyote, na kuamuru viumbe vyote, na kushikilia kuwa na ukuu juu ya viumbe vyote. Na kwa hivyo upekee wa Mungu hauwezi kubadilishwa na kiumbe chochote ambacho hakikuumbwa, na vilevile, mamlaka na nguvu za Mungu haviwezi kusawazishwa na kiumbe chochote ambacho hakikuumbwa. Kwenye Biblia, je, umewahi kusoma kuhusu mjumbe yeyote wa Mungu aliyeumba viumbe vyote? Na kwa nini Mungu hakuwahi kutuma mmojawapo wa wajumbe Wake au malaika kuumba viumbe vyote? Kwa sababu hawakumiliki mamlaka ya Mungu, na kwa hivyo hawakumiliki uwezo wa kutekeleza mamlaka ya Mungu. Sawa tu na viumbe vyote, viumbe vyote visivyoumbwa viko chini ya ukuu wa Muumba, na chini ya mamlaka ya Muumba, na kwa hivyo, kwa njia ile ile, Muumba pia ni Mungu wao na pia ndiye Mtawala wao. Miongoni mwa kila mmoja wao—haijalishi kama wao ni sharifu au kina yahe, wenye nguvu nyingi au kidogo—hakuna hata mmoja anayeweza kuzidi mamlaka ya Muumba, na kwa hivyo miongoni mwao, hakuna hata mmoja wao anayeweza kubadilisha utambulisho wa Muumba. Hawatawahi kuitwa Mungu, na hawatawahi kuweza kuwa Muumba. Huu ni ukweli na hoja zisizobadilika!

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

531. Mungu alitazama viumbe vyote Alivyokuwa ameumba vikiumbika na kusimama wima kwa sababu ya matamshi Yake, na kwa utaratibu vikianza kubadilika. Wakati huu, Mungu alikuwa ametosheka na mambo mbalimbali Aliyoyaumba kwa matamshi Yake, na vitendo mbalimbali Alivyokuwa ametimiza? Jibu ni kwamba “Mungu akaona kwamba ni vizuri.” Wewe unaona nini hapa? Kinawakilisha nini kwamba “Mungu akaona kwamba ni vizuri”? Kusema hivi kunaashiria nini? Kunamaanisha kwamba Mungu alikuwa na nguvu na hekima ya kukamilisha kile Alichokuwa amepangilia na kushauri, kukamilisha shabaha Alizokuwa ameweka wazi ili kuzikamilisha. Baada ya Mungu kukamilisha kila kazi, je, Alijutia chochote? Jibu lingali kwamba “Mungu akaona kwamba ni vizuri.” Kwa maneno mengine, Hakujutia chochote, lakini Alitosheka. Ni nini maana ya Yeye kutojutia chochote? Tunaelezewa kwamba Mpango wa Mungu ni mtimilifu, kwamba nguvu na hekima Zake ni timilifu, na hiyo ni kutokana tu na mamlaka Yake kwamba utimilifu kama huo unaweza kukamilishwa. Wakati binadamu anapotekeleza kazi, je, anaweza, kama Mungu, kuona kwamba kazi hiyo ni nzuri? Je, kila kitu anachofanya binadamu kinaweza kukamilika na kuwa timilifu? Je, binadamu anaweza kukamilisha kitu mara moja na kikawa hivyo daima dawamu? Kama vile tu binadamu anavyosema, “hakuna kitu kilicho timilifu, kinaweza tu kuwa bora zaidi,” hakuna kitu ambacho binadamu hufanya kinaweza kufikia utimilifu. Wakati Mungu alipoona kwamba kile Alichokuwa amefanya na kutimiza kilikuwa kizuri, kila kitu kilichoumbwa na Mungu kiliwekwa kwa matamshi Yake, hivi ni kusema kwamba, wakati “Mungu akaona kwamba ni vizuri,” kila kitu Alichoumba kikachukua mfumo wa kudumu, kikaainishwa kulingana na aina, na kikapewa mahali maalum, kusudio, na kazi, kwa mara ya kwanza na kwa daima dawamu. Vilevile, wajibu wao miongoni mwa viumbe vyote na safari ambayo lazima waabiri kwenye usimamizi wa Mungu wa viumbe vyote, ulikuwa tayari umeamriwa na Mungu, na usingebadilishwa. Hii ilikuwa sheria ya mbinguni iliyotolewa na Muumba kwa viumbe vyote.

“Mungu akaona kwamba ni vizuri,” matamshi haya mepesi, yasiyopongezwa, yanayopuuzwa mara nyingi, ndiyo matamshi ya sheria ya mbinguni na maelekezo ya mbinguni kwa viumbe vyote kutoka kwa Mungu. Ni mfano mwingine halisi wa mamlaka ya Muumba, mfano ambao ni wa kimatendo zaidi na unaojitokeza zaidi. Kupitia kwa matamshi Yake, Muumba hakuweza tu kufaidi kila kitu Alichoweka wazi ili kufaidi, na kutimiza kila kitu Alichoweka wazi ili kutimiza, lakini pia Aliweza kudhibiti mikononi Mwake, kila kitu Alichokuwa ameumba, na kutawala kila kitu Alichokuwa ameumba kulingana na mamlaka Yake, na, vilevile, kila kitu kilikuwa cha mfumo na cha kawaida. Viumbe vyote pia vilizaa, vikawepo na vikaangamia kwa matamshi Yake na, vilevile, kwa mamlaka Yake, vilikuwepo katikati ya sheria Aliyokuwa ameiweka wazi, na hakuna kiumbe kilichoachwa! Sheria hii ilianza punde tu “Mungu alipoona kuwa ni vyema,” na itakuwepo, itaendelea, na kufanya kazi kwa minajili ya mpango wa Mungu wa usimamizi mpaka siku ile itabatilishwa na Muumba! Upekee wa mamlaka ya Muumba ulionyeshwa si tu katika uwezo Wake wa kuumba viumbe vyote na kuamuru viumbe vyote kuwepo, lakini pia katika uwezo Wake wa kutawala na kushikilia ukuu juu ya viumbe vyote, na kupatia maisha na nguvu kwa viumbe vyote, na, vilevile, katika uwezo Wake kusababisha, kwa mara ya kwanza na kwa daima dawamu, viumbe vyote ambavyo Angeumba katika mpango Wake ili kuonekana na kuwepo katika ulimwengu ulioumbwa na Yeye kwa umbo timilifu, na kwa muundo wa maisha timilifu, na wajibu timilifu. Na ndivyo pia ilivyoonyeshwa kwa njia ambayo fikira za Muumba hazikutegemea vizuizi vyovyote, hazikuwekewa mipaka ya muda, nafasi, au jiografia. Kama mamlaka Yake, utambulisho wa kipekee wa Muumba utabakia vilevile milele hata milele. Mamlaka yake siku zote yatakuwa uwakilishi na ishara ya utambulisho Wake wa kipekee, na mamlaka Yake yatakuwepo milele sambamba na utambulisho Wake!

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

532. Mungu aliumba kila kitu, na hivyo yeye hufanya viumbe wote kuwa chini ya utawala wake, na kujiwasilisha kwenye utawala wake; Yeye ataamuru kila kitu, ili kila kitu kiwe mikononi mwake. Vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu, pamoja na wanyama, mimea, mwanadamu, milima na mito, na maziwa—vyote ni lazima vije chini ya utawala Wake. Vitu vyote mbinguni na ardhini lazima zije chini ya utawala Wake. Haviwezi kuwa na hiari yoyote na vyote ni lazima vitii mipango Yake. Hii iliagizwa na Mungu, na ni mamlaka ya Mungu. Mungu huamuru kila kitu, na huagiza na kuainisha kila kitu, ambapo kila kimoja huainishwa kulingana na aina, na kutengewa nafasi zao zenyewe, kulingana na mapenzi ya Mungu. Bila kujali kitu ni kikubwa namna gani, hakuna kitu kinachoweza kumpita Mungu, na vitu vyote ambavyo vinamtumikia mwanadamu aliyeumbwa na Mungu, na hakuna kitu kinachothubutu kumuasi Mungu ama kumdai Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea

533. Kabla ya binadamu hawa kujitokeza, viumbe vyote—sayari zote, nyota zote kule mbinguni—tayari vilikuwepo. Kwenye kiwango cha vitu vikubwa, vyombo hivi vya mbinguni vimekuwa vikizunguka mara kwa mara chini ya udhibiti wa Mungu, kwa uwepo wavyo wote, hata hivyo miaka mingi imepita. Ni sayari gani inaenda wapi na wakati gani haswa; ni sayari gani inafanya kazi gani, na lini; ni sayari gani inazunguka katika mzingo gani, na ni lini inatoweka au inabadilishwa—vitu hivi vyote vinasonga mbele bila ya kosa lolote dogo. Nafasi za sayari na umbali kati yazo ni masuala yanayofuata ruwaza maalum, ni masuala ambayo yanaweza kufafanuliwa kwa data yenye uhakika; njia ambazo zinasafiria, kasi na ruwaza ya mizingo yao, nyakati ambapo zinapatikana kwenye nafasi mbalimbali zinaweza kufafanuliwa kwa hakika na kufafanuliwa kwa sheria maalum. Kwa miaka na mikaka sayari zimefuata sheria hizi na hazijawahi kupotoka hata chembe. Hakuna nguvu inaweza kubadilisha au kutatiza mizingo yazo au ruwaza zao ambazo zinafuata. Kwa sababu sheria maalum zinazotawala mzunguko wazo na data yenye uhakika inayozifafanua iliamuliwa kabla na mamlaka ya Muumba, zinatii sheria hizi zenyewe, kulingana na ukuu na udhibiti wa Muumba. Kwenye kiwango cha mambo makubwamakubwa, si vigumu kwa binadamu kujua zaidi kuhusu ruwaza fulani, data fulani, pamoja na sheria au matukio fulani yasiyoeleweka au yasiyoelezeka. Ingawaje binadamu hawakubali kwamba Mungu yupo, haukubali hoja kwamba Muumba aliumba na anatawala kila kitu na zaidi ya yote hautambui uwepo wa mamlaka ya Muumba, wanasayansi wa kibinadamu, wanafalaki, nao wanafizikia wanachunguza na kugundua zaidi na zaidi kwamba uwepo wa kila kitu kwenye ulimwengu, na kanuni na ruwaza zinazoonyesha mzunguko wavyo, vinatawaliwa na kudhibitiwa na nishati nyeusi kubwa na isiyoonekana. Hoja hii inampa binadamu mshawasha wa kukubaliana na kutambua kwamba kunaye Mwenyezi aliye miongoni mwa ruwaza hizi za mzunguko, anayepangilia kila kitu. Nguvu zake si za kawaida, na ingawaje hakuna anayeweza kuona uso Wake wa kweli, Yeye hutawala na kudhibiti kila kitu kila dakika. Hakuna binadamu au nguvu zozote zile zinazoweza kuuzidi ukuu Wake. Huku binadamu akiwa amekabiliwa na hoja hii, lazima atambue kwamba sheria zinazotawala uwepo wa kila kitu haziwezi kudhibitiwa na binadamu, haziwezi kubadilishwa na yeyote; na wakati uo huo binadamu lazima akubali kwamba, binadamu hawezi kuelewa kikamilifu sheria hizi. Na hizi sheria hazitokei kiasili lakini zinaamrishwa na Bwana na Mungu. Haya yote ni maonyesho na mamlaka ya Mungu yanayoonyesha kwamba mwanadamu anaweza kuelewa katika kiwango cha mambo makubwa.

Kwenye kiwango cha mambo madogomadogo, milima, mito, maziwa, bahari, na maeneo ya ardhi yote ambayo binadamu anatazama nchini, misimu yote ambayo yeye anapitia, mambo yote yanayopatikana kwenye ulimwengu, kukiwemo mimea, wanyama, vijiumbe na binadamu, vyote viko chini ya ukuu wa Mungu na vinadhibitiwa na Mungu Mwenyewe. Katika ukuu na udhibiti wa Mungu, vitu vyote vinakuwepo au vinatoweka kulingana na fikira Zake, maisha ya vitu hivi yanatawaliwa na sheria fulani, na vinakua na kuzaana kulingana nazo. Hakuna binadamu au kiumbe chochote kilicho juu ya sheria hizi. Kwa nini hali iko hivi? Jibu la pekee tu ni, kwa sababu ya mamlaka ya Mungu. Au, nikijibu kwa njia nyingine, kwa sababu ya fikira za Mungu na matamshi ya Mungu; kwa sababu Mungu Mwenyewe hufanya haya yote. Hivi ni kusema, ni mamlaka ya Mungu na ni akili ya Mungu ambayo iliunda sheria hizi; zitasonga na kubadilika kulingana na fikira Zake, na kusonga huku na mabadiliko haya yote yanafanyika au kutoweka kwa minajili ya mpango Wake.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III

534. Punde tu matamshi ya Mungu yanapotamkwa, mamlaka ya Mungu yanachukua usukani wa kazi hii, na hoja iliyoahidiwa kwa kinywa cha Mungu kwa utaratibu huanza kugeuka na kuwa uhalisi. Miongoni mwa viumbe vyote, mabadiliko huanza kufanyika katika kila kitu kutokana na hayo, sawa na vile, kwenye mwanzo wa msimu wa mchipuko, nyasi hugeuka kuwa kijani, maua huchanua, macho ya maua yanachanua kutoka mitini, ndege wanaanza kuimba, nao batabukini wanaanza kurejea, nayo mashamba yanaanza kujaa watu…. Wakati wa msimu wa machipuko unapowadia viumbe vyote hupata nguvu, na hiki ndicho kitendo cha miujiza cha Muumba. Wakati Mungu anapokamilisha ahadi zake, viumbe vyote mbinguni na ardhini vinapata nguvu mpya na kubadilika kulingana na fikira za Mungu—na hakuna kiumbe ambacho kinaachwa. Wakati kujitolea au kuahidi kunapotamkwa kutoka kwa Mungu, viumbe vyote vinatimiza wajibu wake, na vinashughulikiwa kwa minajili ya kutimizwa kwake, na viumbe vyote vinaundwa na kupangiliwa chini ya utawala wa Mungu, na vinaendeleza wajibu wao maalum, na kuhudumu kazi zao husika. Haya ndiyo maonyesho ya mamlaka ya Muumba. Unaona nini katika mambo haya? Unajuaje mamlaka ya Mungu? Kunao upana wa mamlaka ya Mungu? Kuna kipimo cha muda? Je, inaweza kusemekana kuwa na kimo fulani, au urefu fulani? Je, inaweza kusemekana kuwa na ukubwa au nguvu fulani? Je, inaweza kupimwa kwa vipimo vya binadamu? Mamlaka ya Mungu hayawakiwaki yakizima, hayaji yakienda, na hakuna mtu anayeweza kupima namna ambavyo mamlaka Yake yalivyo makubwa. Haijalishi ni muda gani utakaopita, wakati Mungu anabariki mtu, baraka hizi zitaendelea kuwepo, na kuendelea kwake kutadhihirisha agano la mamlaka ya Mungu yasiyokadirika, na kutaruhusu mwanadamu kutazama kule kujitokeza upya kwa nguvu za maisha zisizozimika za Muumba, mara kwa mara. Kila onyesho la mamlaka Yake ni onyesho timilifu la maneno kutoka kwenye kinywa Chake, na linaonyeshwa kwa vitu vyote, na kwa mwanadamu. Zaidi ya hayo, kila kitu kinachokamilishwa na mamlaka Yake ni bora zaidi ya kulinganishwa, na hakina dosari kamwe. Yaweza kusemekana kwamba fikira Zake, matamshi Yake, mamlaka Yake, na kazi zote Anazozikamilisha, zote ni picha nzuri isiyolinganishwa, na kwa viumbe, lugha ya binadamu haiwezi kuelezea umuhimu na thamani yake. Mungu anapotoa ahadi kwa mtu, haijalishi kama ni kuhusiana na pale wanakoishi, au kile wanachofanya, asili yao kabla na baada ya kupata ahadi, au hata ni vipi ambavyo mageuzi makubwa yamekuwa makubwa katika harakati zao za kuishi kwenye mazingira yao—haya yote yanajulikana kwa Mungu kama sehemu ya nyuma ya mkono Wake. Haijalishi ni muda upi umepita baada ya matamshi ya Mungu kutamkwa, kwake Yeye, ni kama vile ndio mwanzo yametamkwa. Hivi ni kusema kwamba Mungu anazo nguvu, na Anayo mamlaka kama hayo, kiasi cha kwamba Anaweza kufuatilia, kudhibiti, na kutambua kila ahadi Anayotoa kwa mwanadamu, haijalishi ahadi hiyo ni nini, haijalishi ni muda gani itachukua kutimizwa kikamilifu, na, zaidi, haijalishi upana wa sehemu ambazo kukamilika huko kunagusia—kwa mfano, muda, jiografia, kabila, na kadhalika—ahadi hii itakamilishwa, na kutambuliwa, na, zaidi, kukamilishwa kwake na kutambuliwa kwake hakutahitaji jitihada Zake hata kidogo. Na haya yanathibitisha nini? Kwamba upana wa mamlaka ya Mungu na nguvu vinatosha kudhibiti ulimwengu mzima, na wanadamu wote.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

535. Katika maendeleo ya mwanadamu leo, sayansi ya mwanadamu inaweza kusemekana kwamba inanawiri, na mafanikio ya uchunguzi wa kisayansi wa binadamu unaweza kufafanuliwa kama wa kuvutia. Uwezo wa kibinadamu, lazima isemwe, unazidi kukua mkubwa zaidi, lakini kunao ushindi mmoja wa kisayansi ambao mwanadamu hajaweza kufanya: Mwanadamu ameunda ndege, vibebaji vya ndege, na hata bomu la atomiki, mwanadamu ameenda angani, ametembea mwezini, amevumbua Intaneti, na ameishi maisha ya kiwango cha juu ya teknolojia, ilhali mwanadamu hawezi kuumba kiumbe hai kinachopumua. Silika za kila kiumbe kilicho hai na sheria ambazo zinatawala kuishi kwake na mzunguko wa maisha na kifo wa kila kiumbe kilicho hai—vyote hivi haviwezekani na havidhibitiki na sayansi ya mwanadamu. Wakati huu, lazima isemekane kwamba haijalishi ni viwango gani vya juu zaidi vitakavyofikiwa na sayansi ya binadamu, haviwezi kulinganishwa na fikira zozote za Muumba na haiwezekani kutambua miujiza ya uumbaji wa Muumba na uwezo wa mamlaka Yake. Kunazo bahari nyingi sana juu ya nchi, ilhali hazijawahi kukiuka mipaka yao na kuja kwenye ardhi kwa nguvu, na hiyo ni kwa sababu Mungu aliwekea mipaka kila mojawapo ya bahari hizo; zilikaa popote pale Aliziamuru kukaa; na bila ya ruhusa ya Mungu haziwezi kusongasonga ovyo. Bila ya ruhusa ya Mungu, haziwezi kuingiliana, na zinaweza kusonga tu pale ambapo Mungu anasema hivyo, na pale ambapo zinaenda na kubakia ni suala na uamuzi wa mamlaka ya Mungu.

Ili kuweka wazi zaidi, “mamlaka ya Mungu” yanamaanisha kwamba ni wajibu wa Mungu. Mungu anayo haki ya kuamua namna ya kufanya kitu na kinafanywa kwa vyovyote vile Anavyopenda. Sheria ya vitu vyote ni wajibu wa Mungu, na wala si wajibu wa binadamu; na wala haiwezi kubadilishwa na binadamu. Haiwezi kusongeshwa kwa mapenzi ya binadamu, lakini inaweza badala yake kubadilishwa kwa fikira za Mungu, na hekima ya Mungu, na amri za Mungu, na hii ni kweli ambayo haiwezi kukataliwa na binadamu yeyote. Mbingu na nchi na viumbe vyote, ulimwengu, mbingu yenye nyota, misimu minne ya mwaka, ile inayoonekana na isiyoonekana kwa binadamu—yote haya yapo, yanafanya kazi, na kubadilika bila ya kosa hata dogo, chini ya mamlaka ya Mungu, kulingana na shurutisho za Mungu, kulingana na amri za Mungu, na kulingana na sheria za mwanzo wa uumbaji. Si hata mtu mmoja au kifaa kimoja kinaweza kubadilisha sheria zao, au kubadilisha mkondo wa asili ambao sheria hizi zinafanya kazi; zilianza kutumika kwa sababu ya mamlaka ya Mungu, na zitaangamia kwa sababu ya mamlaka ya Mungu. Haya ndiyo mamlaka yenyewe ya Mungu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

536. Kwanza, inaweza kusemekana kwa uhakika kwamba mamlaka na nguvu vyote ni vizuri. Havina uunganisho wowote na kitu chochote kibaya, na havina uhusiano wowote na viumbe vyovyote vilivyoumbwa au vile ambavyo havikuumbwa. Nguvu za Mungu zinaweza kuumba viumbe vya mfumo wowote ulio na uzima na nguvu, na haya yote yanaamuliwa na uzima wa Mungu. Mungu ni uzima, kwa hivyo Yeye ndiye chanzo cha viumbe hai vyote. Vilevile, mamlaka ya Mungu yanaweza kufanya viumbe vyote kutii kila neno la Mungu, yaani kuumbika kulingana na matamshi yanayotoka kwenye kinywa cha Mungu, na kuishi na kuzaana kwa amri ya Mungu, ambapo baadaye Mungu anatawala na kuamuru viumbe vyote hai, na hakutakuwa na kupotoka kokote, daima dawamu. Hakuna mtu au kifaa kilicho na mambo haya; Muumba tu ndiye anayemiliki na aliye na nguvu kama hizo, na hivyo basi yanaitwa mamlaka. Huu ndio upekee wa Muumba. Kwa hivyo, haijalishi kama ni neno lenyewe “mamlaka” au hali halisi ya mamlaka haya, kila mojawapo linaweza tu kuhusishwa na Muumba kwa sababu ni ishara ya utambulisho na hali halisi ya kipekee ya Muumba; na inawakilisha utambulisho na hadhi ya Muumba, mbali na Muumba, hakuna mtu au kifaa kinachoweza kuhusishwa na neno “mamlaka” Huu ni ufasiri wa mamlaka ya kipekee ya Muumba.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

537. Naweka upinde wangu mawinguni, na utakuwa alama ya agano kati ya Mimi na dunia.” Haya ni matamshi ya asili yaliyotamkwa na Muumba kwa mwanadamu. Aliposema matamshi haya, upinde wa mvua ulionekana mbele ya macho ya binadamu, ambapo ulibakia mpaka leo. Kila mmoja ameuona upinde wa mvua kama huo, na unapouona, je, unajua namna unavyojitokeza? Sayansi haiwezi kuthibitisha haya, au kutafuta chanzo chake, au kutambua mambo yanayosababisha upinde huu wa mvua. Hiyo ni kwa sababu, upinde wa mvua ni ishara ya agano lilioanzishwa kati ya Muumba na binadamu; hauhitaji msingi wowote wa kisayansi, haukuumbwa na binadamu, wala binadamu hawezi kuubadilisha. Ni maendelezo ya mamlaka ya Muumba baada ya Yeye kuongea matamshi Yake. Muumba alitumia mbinu fulani Yake mwenyewe kutii agano lake na binadamu na ahadi Yake, na hivyo basi matumizi Yake ya upinde wa mvua kama ishara ya agano ambalo Alianzisha ni maelekezo na sheria ya mbinguni yatakayobakia milele hivyo, haijalishi kama ni kuhusiana na Muumba au mwanadamu aliyeumbwa. Ilhali sheria hii isiyobadilika ni, lazima isemwe, maonyesho mengine ya kweli ya mamlaka ya Muumba kufuatia uumbaji Wake wa viumbe vyote, na lazima isemwe kwamba mamlaka na nguvu za Muumba havina mipaka; matumizi Yake ya upinde wa mvua ni ishara ya maendelezo na upanuzi wa mamlaka ya Muumba. Hiki kilikuwa kitendo kingine kilichotekelezwa na Mungu kwa kutumia matamshi Yake, na kilikuwa ni ishara ya agano ambalo Mungu alikuwa ameanzisha na mwanadamu kwa kutumia matamshi. Alimwambia binadamu kuhusu kile ambacho Aliamua kuleta, na kwa njia gani kingekamilishwa na kutimizwa, na kwa njia hii suala liliweza kutimizwa kulingana na matamshi kutoka kwenye kinywa cha Mungu. Mungu pekee ndiye anayemiliki nguvu kama hizo, na leo, miaka elfu kadhaa baada ya Yeye kuongea matamshi haya, binadamu angali bado anaweza kuangalia upinde wa mvua uliozungumziwa kutoka kwenye kinywa cha Mungu. Kwa sababu ya matamshi hayo yaliyotamkwa na Mungu, kitu hiki kimebakia bila ya kusongezwa na kubadilishwa mpaka hadi leo. Hakuna anayeweza kuuondoa upinde huu wa mvua, hakuna anayeweza kubadilisha sheria zake, na upo kimsingi kutokana na matamshi ya Mungu. Haya kwa hakika ni mamlaka ya Mungu. “Mungu ni mzuri tu kama matamshi Yake, na matamshi Yake yataweza kukamilishwa, na kile ambacho kimekamilishwa kinadumu milele.” Matamshi kama haya kwa kweli yanaonyeshwa waziwazi hapa, na ni ishara na sifa wazi kuhusu mamlaka na nguvu za Mungu. Ishara au sifa kama hiyo haimilikiwi na au kuonekana katika viumbe vyovyote vile vilivyoumbwa, wala kuonekana kwenye viumbe vyovyote vile ambavyo havikuumbwa. Inamilikiwa tu na Mungu wa kipekee, na inapambanua utambulisho na hali halisi inayomilikiwa tu na Muumba kutoka ile ya viumbe. Wakati uo huo, ni ishara na sifa pia ambayo mbali na Mungu Mwenyewe, haitawahi kupitwa na kiumbe chochote kilichoumbwa au kile ambacho hakikuumbwa.

Uanzishaji wa agano Lake Mungu na binadamu kilikuwa ni kitendo chenye umuhimu mkubwa, na ambao Alinuia kutumia ili kuwasilisha hoja kwa binadamu na kumwambia binadamu mapenzi Yake, na hadi hapa, Alitumia mbinu ya kipekee, kwa kutumia ishara maalum ya kuanzisha agano na binadamu, ishara ambayo ilikuwa ahadi ya agano ambalo Alikuwa ameanzisha na binadamu. Kwa hivyo, je, uanzishaji wa agano hili ulikuwa ni tukio kubwa? Na tukio hili lilikuwa kubwa vipi? Hii haswa ndiyo inayoonyesha namna ambavyo agano hili lilivyo maalum: si agano lililoanzishwa kati ya binadamu mmoja na mwingine, au kundi moja na jingine, au nchi moja na nyingine, lakini agano lililoanzishwa kati ya Muumba na wanadamu kwa ujumla, na litabakia halali mpaka siku ambayo Muumba atakomesha mambo yote. Mtekelezaji wa agano hili ni Muumba, na mwendelezaji pia ni Muumba. Kwa ufupi, uzima wa agano la upinde wa mvua ulioanzishwa pamoja na mwanadamu ulikamilishwa na kutimizwa kulingana na mazungumzo kati ya Muumba na mwanadamu, na umebakia vivyo hivyo mpaka leo. Ni nini kingine ambacho viumbe vinaweza kufanya mbali na kujinyenyekeza, na kutii, na kusadiki, na kushukuru, na kutolea ushuhuda, na kusifu mamlaka ya Muumba? Kwani hamna yeyote yule isipokuwa Mungu wa pekee anayemiliki nguvu za kuanzisha agano kama hilo. Kujitokeza kwa upinde wa mvua mara kwa mara, kunatangaza kwa mwanadamu na kumtaka azingatie agano lile kati ya Muumba na mwanadamu. Katika kujitokeza kwingine kwa agano kati ya Muumba na binadamu, kile kinachoonyeshwa kwa mwanadamu si upinde wa mvua au agano lenyewe, lakini ni mamlaka yenyewe yasiyobadilika ya Muumba. Kujitokeza kwa upinde wa mvua, mara kwa mara, kunaonyesha yale matendo ya kipekee na ya kimiujiza ya Muumba yanayopatikana kwenye sehemu zilizofichwa, na, wakati uo huo ni onyesho muhimu la mamlaka ya Muumba ambayo hayatawahi kufifia, na wala kubadilika. Je, hili si onyesho la dhana nyingine ya mamlaka ya kipekee ya Muumba?

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

538. Baada ya kusoma “Ibrahimu hakika atakuwa taifa kubwa na lenye nguvu, na mataifa yote ya dunia yatabarikiwa kupitia yeye” kwenye Mwanzo 18:18, je, unaweza kuhisi mamlaka ya Mungu hapo? Unaweza kuhisi hali isiyokuwa ya kawaida ya Muumba? Unaweza kuhisi hali ya mamlaka ya juu ya Muumba? Maneno ya Mungu yana uhakika. Mungu hasemi maneno kama hayo kwa sababu ya, au kwa kuwakilisha, ujasiri Wake katika ufanisi; hayo ni, badala yake, ithibati ya mamlaka ya matamshi, na ni amri inayotimiza maneno ya Mungu. Kunazo semi mbili ambazo unafaa kutilia maanani hapa. Wakati Mungu anaposema “Ibrahimu hakika atakuwa taifa kubwa na lenye nguvu, na mataifa yote ya dunia yatabarikiwa kupitia yeye,” kunayo dalili ya kutoeleweka kwenye maneno haya? Kunayo dalili yoyote ya wasiwasi? Kunayo dalili yoyote ya woga? Kwa sababu ya matamshi “ataweza kwa hakika” na “atakuwa” kwenye matamshi ya Mungu, dalili hizi, ambazo zinapatikana tu kwa binadamu na mara nyingi zinajionyesha ndani yake, hazijawahi kupata uhusiano wowote na Muumba. Hakuna mtu angethubutu kutumia maneno kama haya wakati akiwatakia wengine mema, hakuna yule angethubutu kubariki mwingine apate taifa kubwa na lenye nguvu kwa uhakika kama huo, au kutoa ahadi kwamba mataifa yote ya dunia yatabarikiwa kupitia kwake. Maneno ya Mungu yanapokuwa na uhakika zaidi, ndipo yanathibitisha kitu fulani—na kitu hicho ni nini? Yanathibitisha kuwa Mungu anayo mamlaka kama hayo, kuwa mamlaka Yake yanaweza kutimiza mambo haya, na kwamba ufanisi wake ni lazima. Mungu alikuwa na uhakika katika moyo Wake, bila kusita kokote, kwa kila kitu Alichombariki Ibrahimu. Aidha, uzima wa haya utakamilishwa kulingana na maneno Yake, na hakuna nguvu ingeweza kubadilisha, kuzuia, kuharibu, au kutatiza kukamilika kwake. Licha ya kilichotendeka, hakuna kitu ambacho kingebatilisha au kuathiri kutimia na kukamilika kwa matamshi ya Mungu. Huu ndio uzito wenyewe wa maneno yaliyotamkwa kutoka kinywa cha Muumba, na mamlaka ya Muumba ambayo hayavumilii kanusho la binadamu! Baada ya kuyasoma maneno haya, ungali unahisi shaka? Maneno haya yalitamkwa kutoka kinywa cha Mungu, na kunazo nguvu, adhama na mamlaka katika maneno ya Mungu. Uwezo na mamlaka kama haya, na kutozuilika kwa kukamilika kwa hoja, haviwezi kufikiwa na kiumbe chochote kilichoumbwa au kile ambacho hakikuumbwa na haviwezi kupitwa na kiumbe chochote kilichoumbwa au kile ambacho hakikuumbwa. Muumba pekee ndiye anaweza kuongea na binadamu kwa sauti na mkazo kama huo, na hoja zimethibitisha kuwa ahadi Zake si maneno matupu, au majigambo ya kupitisha wakati, lakini ni maonyesho ya mamlaka ya kipekee yasiyoweza kupitwa na mtu, kitu, au kifaa chochote.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

539. Wakati Mungu alisema “uzao wako nitazidisha mithili,” hili lilikuwa agano ambalo Mungu alianzisha na Ibrahimu, sawa na agano la upinde wa mvua, lingeweza kutimizwa milele hadi milele, na pia ilikuwa ahadi iliyotolewa na Mungu kwa Ibrahimu. Mungu pekee ndiye anayefuzu na kuweza kufanya ahadi hii kutimia. Bila kujali kama binadamu anaisadiki au la, bila kujali kama binadamu aikubali au la, na bila kujali namna binadamu anavyoitazama, na namna anavyoichukulia, haya yote yataweza kutimizwa, hadi mwisho wa maelezo ya agano hili, kulingana na matamshi yaliyotamkwa na Mungu. Matamshi ya Mungu hayatabadilishwa kwa sababu ya mabadiliko katika mapenzi au dhana za binadamu, na hayatabadilishwa kwa sababu ya mabadiliko ndani ya mtu yeyote, kitu au kifaa. Viumbe vyote vitaweza kutoweka lakini matamshi ya Mungu yatabaki milele hadi milele. Kinyume cha mambo ni, siku ambapo viumbe vyote vitatoweka ndiyo siku ile ile ambayo matamshi ya Mungu yataweza kutimizwa kabisa, kwani Yeye ndiye Muumba, na Anamiliki mamlaka ya Muumba, na nguvu za Muumba, na Anadhibiti vitu na viumbe vyote na nguvu zote za maisha; na Anaweza kusababisha kitu kutoka kule kusikokuwa na kitu, au kitu kuwa kile kisichokuwepo, na Anadhibiti mabadiliko ya viumbe vyote vilivyo na uhai na vile vilivyokufa, na kwa hivyo kwake Mungu, hakuna kinachokuwa rahisi kuliko kuzidisha uzao wa mtu. Haya yote yanaonekana ya kufikiria tu akilini mwa binadamu, sawa na hadithi za uwongo, lakini kwa Mungu, kile Anachoamua kufanya, na kuahidi kufanya, si cha kufikiria tu akilini wala si hadithi za uwongo. Badala yake ni hoja ambayo Mungu tayari ameiona, na ambayo kwa kweli itaweza kutimizwa. Je, unashukuru kuyasikia haya? Je, hoja hizi zinathibitisha kwamba uzao wa Ibrahimu ulikuwa mwingi? Na ulikuwa mwingi kiasi kipi? Mwingi kiasi cha “nyota za mbinguni, na mithili ya mchanga uliopo kwenye ukanda wa pwani” kama ilivyosemwa na Mungu? Je, uliweza kuenea kotekote katika mataifa na maeneo, kwenye kila sehemu ya ulimwengu? Na ni nini kilichotimiza hoja hii? Iliweza kutimizwa kutokana na mamlaka ya matamshi ya Mungu? Kwa miaka kadhaa ifikayo mamia au elfu baada ya matamshi ya Mungu kutamkwa, matamshi ya Mungu yaliendelea kutimizwa, na bila kusita yakaendelea kuwa hoja; huu ndio uwezo wa matamshi ya Mungu, na ithibati ya mamlaka ya Mungu. Wakati Mungu alipoumba viumbe vyote hapo mwanzo, Mungu alisema na hebu kuwe na nuru, na kukawa na nuru. Tokeo hili lilifanyika haraka sana, lilitimizwa kwa muda mfupi sana, na hakukuwa na kuchelewa kokote kuhusu kukamilika na kutimizwa kwake; athari za matamshi ya Mungu zilitokea papo hapo. Vyote vilikuwa onyesho la mamlaka ya Mungu, lakini wakati Mungu alipombariki Ibrahimu, Aliruhusu binadamu kuuona upande mwingine wa mamlaka ya Mungu, na Akaruhusu binadamu kuona mamlaka ya Muumba yasiyokadirika, na zaidi, Akaruhusu binadamu kuona upande halisi, bora zaidi wa mamlaka ya Muumba.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

540. Baada ya Mungu kuwabariki Ibrahimu na Ayubu, Mungu hakubakia mahali Alipokuwa, wala Yeye kuwaweka wajumbe Wake kazini huku Akisubiri kuona matokeo yake yatakuwa yapi. Kinyume cha mambo ni kuwa, pindi Mungu alipotamka maneno Yake, akiongozwa na mamlaka ya Mungu, mambo yote yalianza kukubaliana na kazi ambayo Mungu alinuia kufanya, na kulikuwepo na watu waliokuwa wamejitayarisha, vitu, na vifaa ambavyo Mungu alihitaji. Hivi ni kusema kwamba, punde tu maneno hayo yalipotamkwa kutoka kwenye kinywa cha Mungu, mamlaka ya Mungu yalianza kutumika kotekote kwenye ardhi nzima, na Akaweka wazi mkondo ili kuweza kukamilisha na kutimiza ahadi Alizotoa kwa Ibrahimu na Ayubu, huku Akifanya pia mipango na matayarisho yote kuhusiana na kila kitu kilichohitajika kwa kila awamu Aliyopanga kutekeleza. Kwa wakati huu, hakuwashawishi tu wafanyakazi Wake, lakini pia na viumbe vyote vilivyokuwa vimeumbwa na Yeye. Hivyo ni kusema kwamba upana ambao mamlaka ya Mungu yalitiliwa maanani haukujumuisha tu wajumbe, lakini, vilevile, vitu vyote, vilivyoshawishiwa ili kutii ile kazi ambayo Alinuia kukamilisha; hizi ndizo zilizokuwa tabia mahususi ambazo mamlaka ya Mungu yalitumiwa. Katika kufikiria kwako, baadhi ya watu wanaweza kuwa na ufahamu ufuatao kuhusiana na mamlaka ya Mungu: Mungu anayo mamlaka, na Mungu anao uwezo, na hivyo basi Mungu anahitaji kubaki katika mbingu ya tatu, au Anahitajika tu kubakia mahali maalum, na hahitajiki kufanya kazi yoyote fulani, na uzima wa kazi ya Mungu unakamilishwa katika fikira Zake. Baadhi wanaweza kusadiki kuwa, Ingawa Mungu alibariki Ibrahimu, Mungu hakuhitajika kufanya kitu chochote, na ilitosha kwake Yeye kutamka tu matamshi Yake. Je, hivi ndivyo ilivyofanyika kweli? Bila shaka la! Ingawa Mungu anamiliki mamlaka na nguvu, mamlaka Yake ni ya kweli na halisia, si matupu. Uhalisi na ukweli wa mamlaka ya Mungu na nguvu hufichuliwa kwa utaratibu, kuwekwa ndani ya uumbaji Wake wa vitu vyote, na udhibiti wa vitu vyote, na katika mchakato ambao Anaongoza na kusimamia wanadamu. Kila mbinu, kila mtazamo na kila maelezo ya ukuu wa Mungu juu ya wanadamu na vitu vyote, na kazi yote ambayo Amekamilisha, vilevile ufahamu Wake kuhusu vitu vyovyote—vinathibitisha kwa kweli kwamba mamlaka na nguvu za Mungu si maneno matupu. Mamlaka na nguvu Zake vyote vinaonyeshwa na kufichuliwa kila mara, na katika mambo yote. Maonyesho haya na ufunuo vyote vinazungumzia uwepo wa halisi wa mamlaka ya Mungu, kwani Yeye ndiye anayetumia mamlaka na nguvu Zake kuendeleza kazi Yake, na kuamuru vitu vyote, na kutawala vitu vyote kila wakati, na nguvu na mamlaka Yake, vyote haviwezi kubadilishwa na malaika, au wajumbe wa Mungu. Mungu aliamua ni baraka gani Angempa Ibrahimu na Ayubu—uamuzi ulikuwa wa Mungu. Hata Ingawa wajumbe wa Mungu waliweza kumtembelea Ibrahimu na Ayubu wao binafsi, vitendo vyao vilikuwa kulingana na amri za Mungu, na kulingana na mamlaka ya Mungu, na pia walikuwa wakifuata ukuu wa Mungu. Ingawa binadamu anawaona wajumbe wa Mungu wakimtembelea Ibrahimu, na hashuhudii Yehova Mungu binafsi akifanya chochote kwenye rekodi za Biblia, kwa hakika Yule Mmoja tu ambaye anatilia mkazo nguvu na mamlaka ni Mungu Mwenyewe, na hali hii haivumilii shaka yoyote kutoka kwa binadamu yeyote! Ingawa umewaona malaika na wajumbe wakimiliki nguvu nyingi, na wametenda miujiza, au wamefanya baadhi ya mambo yaliyoagizwa na Mungu, vitendo vyao ni kwa minajili tu ya kukamilisha agizo la Mungu, na wala si tu kuonyesha mamlaka ya Mungu—kwani hakuna binadamu au kifaa kilicho na, au kinachomiliki, mamlaka ya Muumba ya kuumba vitu vyote na kutawala vitu vyote. Na kwa hivyo hakuna binadamu au kifaa chochote kinaweza kutumia au kuonyesha mamlaka ya Muumba.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

541. Je, Mungu angeweza kufanya kitu ili kuthibitisha utambulisho Wake Mwenyewe? Kwa Mungu, huu ulikuwa upepo mwanana—lilikuwa jambo rahisi sana. Angefanya kitu popote, wakati wowote ili kuthibitisha utambulisho na kiini Chake, lakini Mungu alikuwa na njia Yake ya kufanya mambo—kwa mpango, na kwa hatua. Hakufanya vitu bila mpangilio; Alitafuta muda unaofaa, na fursa inayofaa kufanya kitu chenye maana zaidi kwa wanadamu kuweza kuona. Hili lilithibitisha mamlaka Yake na utambulisho Wake. Hivyo basi, kufufuka kwa Lazaro kungeweza kuthibitisha utambulisho wa Bwana Yesu? Hebu tuangalie kifungu hiki cha maandiko: “Na baada ya yeye kuzungumza, akasema kwa sauti kuu, Lazaro, kuja nje. Na yeye ambaye alikuwa amefariki akatoka nje….” Wakati Bwana Yesu alipofanya haya, Alisema tu jambo moja: “Lazaro, kuja nje.” Kisha Lazaro akatoka nje ya kaburi—hii ilikamilika kwa sababu ya mstari mmoja uliotamkwa na Bwana. Katika wakati huu, Bwana Yesu hakuweza kuandaa madhabahu, na Hakutekeleza hatua zote nyingine. Alisema tu jambo moja. Hili linaweza kutaitwa muujiza au amri? Au lilikuwa aina fulani wa uchawi? Kwa juujuu, yaonekana ingeweza kuitwa muujiza, na ukiangalia hali hiyo kutoka mtazamo wa kisasa, bila shaka mnaweza bado kuliita muujiza. Hata hivyo, bila shaka hali hiyo isingeweza kuitwa apizo la kuiita nafsi kurudi kutoka kwa wafu, na bila shaka si uchawi. Ni sahihi kusema kwamba muujiza huu ulikuwa ni onyesho la kawaida zaidi, dogo ajabu la mamlaka ya Muumba. Haya ndiyo mamlaka, na uwezo wa Mungu. Mungu ana mamlaka ya kumwacha mtu afe, kuruhusu nafsi yake iondoke mwilini mwake na kurudi kuzimu au popote pale itakapoenda. Mtu anapokufa, na anakokwenda baada ya kifo—haya yanaamuliwa na Mungu. Yeye anaweza kufanya haya wakati wowote na mahali popote. Yeye hazuiliwi na binadamu, matukio, vifaa, nafasi au mahali. Akitaka kulifanya Anaweza kulifanya, kwa sababu vitu vyote na viumbe vyenye uhai vinatawaliwa na Yeye, na vitu vyote vinaongezeka, vinaishi na kuangamia kwa neno Lake na mamlaka Yake. Anaweza kumfufua binadamu aliyekufa, na pia hiki ni kitu Anachoweza kufanya wakati wowote mahali popote. Haya ndiyo mamlaka ambayo Muumbaji pekee humiliki.

Bwana Yesu alipofanya kitu kama vile kumleta Lazaro kutoka kwa wafu, lengo Lake lilikuwa ni kutoa ithibati kwa wanadamu na Shetani aweze kuona, na kuacha wanadamu na Shetani kujua kwamba kila kitu cha wanadamu, maisha na kifo cha wanadamu vyote vinaamuliwa na Mungu, na kwamba ingawa Alikuwa amekuwa mwili ilivyo kama siku zote, Alibaki katika mamlaka juu ya ulimwengu wa kimwili unaoweza kuonekana pamoja na ulimwengu wa kiroho ambao wanadamu hawawezi kuuona. Huku kulikuwa kuwaruhusu wanadamu na Shetani kujua kwamba kila kitu cha wanadamu hakiko katika amri ya Shetani. Huu ulikuwa ni ufunuo na onyesho la mamlaka ya Mungu, na ilikuwa pia njia ya Mungu kuutuma ujumbe wake kwa viumbe vyote kwamba maisha na kifo cha wanadamu kimo mikononi mwa Mungu. Bwana Yesu kumfufua Lazaro—kutenda kwa aina hii ni mojawapo ya njia za Muumba za kumfunza na kumwelekeza wanadamu. Ilikuwa ni hatua thabiti ambapo Aliutumia uwezo Wake na mamlaka Yake kuwaelekeza wanadamu, na kuwatolea wanadamu. Ilikuwa njia bila matumizi ya maneno kwa Muumba ya kuwaruhusu wanadamu kuweza kuuona ukweli wa Yeye kuwa na mamlaka juu ya viumbe vyote. Ilikuwa njia Yake ya kuwaambia binadamu kupitia kwa hatua za kimatendo kwamba hamna wokovu mbali na kupitia Yeye. Mbinu za aina hii za kimya za Yeye kuwaelekeza wanadamu zinadumu milele—hazifutiki, na iliweza kuleta katika mioyo ya wanadamu mshtuko na kupatikana kwa nuru ambayo haiwezi kufifia. Kufufuliwa kwa Lazaro kulimtukuza Mungu—hali hii inayo athari ya kina katika kila mojawapo wa wafuasi wa Mungu. Inakita mizizi kwa kila mmoja anayeelewa kwa kina tukio hili, ufahamu, maono kwamba ni Mungu tu anayeweza kuamuru maisha na kifo cha wanadamu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III

542. Tangu unapoingia katika dunia hii ukilia, unaanza kutekeleza wajibu wako. Kwa kuchukua jukumu lako katika mpango wa Mungu na katika utaratibu Wake, unaanza safari yako katika maisha. Licha ya asili yako na licha ya safari iliyoko mbele yako, hakuna kitakachoepuka mpango na utaratibu ambao mbingu imeunda, na hakuna aliye na udhibiti wa hatima yake mwenyewe, kwa maana yule Anayetawala kila kitu ndiye tu Aliye na uwezo wa kazi hiyo. Tangu siku aliyoumbwa binadamu, Mungu amekuwa akitenda kazi Yake kwa njia hii, kusimamia ulimwengu huu na kuelekeza mifuatano ya mabadiliko katika mambo yote na njia ambazo yanasongea. Pamoja na vitu vyote vingine, mwanadamu polepole na bila kujua anastawishwa na utamu na mvua na umande kutoka kwa Mungu. Kama vitu vyote vingine, mwanadamu bila kujua, anaishi chini ya mpango wa mkono wa Mungu. Moyo na roho ya mwanadamu vimeshikwa katika mkono wa Mungu, na maisha yake yote yanatazamwa machoni mwa Mungu. Haijalishi kama unayaamini mambo haya au la, vitu vyote, viwe hai au vilivyokufa, vitahamishwa, vitabadilika, kufanywa vipya, na kutoweka kulingana na mawazo ya Mungu. Hii ndiyo njia ambayo Mungu huongoza vitu vyote.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu

543. Kama kuzaliwa kwa mtu kulipangiwa na maisha ya awali ya mtu, basi kifo cha mtu kinaadhimisha mwisho wa hatima hiyo. Kama kuzaliwa kwa mtu ndiyo mwanzo wa kazi maalum ya mtu ya maisha, basi kifo cha mtu kinaadhimisha mwisho wa kazi hiyo maalum. Kwa sababu Muumba amepangilia mseto maalum wa hali mbalimbali za kuzaliwa kwa mtu, ni wazi na dhahiri shahiri kwamba amepangilia pia mseto wa hali zisizobadilika kwa minajili ya kifo cha mtu. Kwa maneno mengine, hakuna anayezaliwa kwa bahati na hakuna kifo cha mtu ambacho hakitarajiwi, na si kuzaliwa, si kufa vyote vina uhusiano na maisha ya mtu ya awali na ya sasa. Hali za kuzaliwa na kifo cha mtu, vyote viliamuliwa kabla na Muumba; hii ni kudura ya mtu, hatima ya mtu. Kama vile tu mengi yanaweza kuzungumzwa kuhusu kuzaliwa kwa mtu, hata kifo cha kila mtu kitafanyika katika mseto tofauti katika hali maalum, hivyo basi urefu wa maisha tofauti miongoni mwa watu na njia tofauti pamoja na nyakati tofauti zinaandama vifo vyao. Baadhi ya watu wana nguvu na afya na ilhali wanakufa mapema; wengine ni wanyonge na wanauguaugua ilhali wanaishi hadi umri wa uzee, na wanaaga dunia kwa amani. Baadhi wanafarakana na dunia kutokana na sababu zisizokuwa za kawaida, wengine kutokana na sababu za kawaida. Baadhi wanakata roho wakiwa mbali na nyumbani, wengine wanayafumba macho yao kwa mara ya mwisho wakiwa na wapendwa wao kando yao. Baadhi ya watu hufia hewani, wengine hufia chini ya nchi. Wengine huzama chini ya maji, wengine nao kwenye majanga. Baadhi hufa asubuhi, wengine hufa usiku. … Kila mtu hutaka kuzaliwa kwa heshima, maisha mazuri, na kifo kitukufu, hakuna mtu anayeweza kufika zaidi ya hatima yake mwenyewe, hakuna mtu anayeweza kukwepa ukuu wa Muumba. Hii ni hatima ya binadamu. Binadamu anaweza kufanya aina zote za mipango ya siku zote za usoni, lakini hakuna mtu anayeweza kupanga njia na muda wa kuzaliwa kwake na kuondoka kwake ulimwenguni. Ingawaje watu hufanya kila wawezalo kuepuka na kuzuia kuja kwa kifo chao, ilhali, bila wao kujua, kifo huwa kinakaribia polepole. Hakuna anayejua ni lini atakapofarakana na dunia au ni vipi, isitoshe hata pale hayo yote yatakapofanyikia. Bila shaka, si binadamu wanaoshikilia nguvu za maisha na kifo, wala si kiumbe fulani kwenye ulimwengu wa kimaumbile, lakini ni Muumba, ambaye mamlaka yake ni ya kipekee. Maisha na kifo cha binadamu si zao la sheria fulani ya ulimwengu wa kimaumbile, lakini athari ya ukuu wa mamlaka ya Muumba.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III

544. Katika mamlaka ya Mungu kila mtu anakubali waziwazi au kimyakimya ukuu Wake na mipangilio Yake, na haijalishi ni vipi ambavyo mtu anashughulika katika mkondo wa maisha yake, haijalishi ni njia ngapi mbovu ambazo mtu ametembelea, mwishowe atarudi tu kwenye mzingo wa hatima ambayo Muumba amempangia yeye. Hii ndiyo hali isiyoshindika ya mamlaka ya Muumba, namna ambavyo mamlaka Yake yanavyodhibiti na kutawala ulimwengu. Ni hii hali ya kutoshindika, mfumo huu wa kudhibiti na kutawala, ambao unawajibikia sheria zinazoamuru maisha ya mambo yote, zinazoruhusu binadamu kuweza kuhama hadi kwenye mwili tofauti baada ya kifo tena na tena bila uingiliaji kati, zinazofanya ulimwengu kugeuka mara kwa mara na kusonga mbele, siku baada ya siku, mwaka baada ya mwaka. Mmeshuhudia hoja hizi zote na unazielewa, haijalishi kama ni za juujuu ama ni za kina; kina cha ufahamu wako kinategemea kile unachopitia na maarifa ya ukweli, na maarifa yako kuhusu Mungu. Kujua kwako vyema uhalisia wa ukweli, ni kiwango kipi ambacho umepitia matamshi ya Mungu, ni vipi unajua vyema hali halisi ya Mungu na tabia yake—hii inawakilisha kina cha ufahamu wako wa ukuu na mipangilio ya Mungu. Je, uwepo wa ukuu wa Mungu na mipangilio unategemea kama binadamu wanainyenyekea? Je, hoja kwamba Mungu anamiliki mamlaka haya inaamuliwa na kama binadamu watayanyenyekea? Mamlaka ya Mungu yapo licha ya hali mbalimbali; katika hali zote, Mungu anaamuru na kupangilia hatima ya kila binadamu na mambo yote kulingana na fikira Zake, mapenzi Yake. Hali hii haitabadilika kwa sababu binadamu hubadilika, na iko huru wala haitegemei mapenzi ya binadamu, haiwezi kubadilishwa na mabadiliko yoyote ya muda, anga, na jiografia, kwani mamlaka ya Mungu ndiyo hali yake halisi kabisa. Kama binadamu anaweza kujua na kuukubali ukuu wa Mungu, na kama binadamu anaweza kuunyenyekea, haiwezi kwa vyovyote vile kubadilisha hoja kwamba ukuu wa Mungu upo juu ya hatima ya binadamu. Hivi ni kusema kwamba, haijalishi ni mtazamo gani ambao binadamu atachukua kwa ukuu wa Mungu, hauwezi tu kubadilisha hoja kwamba Mungu anashikilia ukuu juu ya hatima ya binadamu na juu ya mambo yote. Hata kama hutanyenyekea katika ukuu wa Mungu, angali Anaamuru hatima yako; hata kama huwezi kujua ukuu Wake, mamlaka Yake yangali yapo. Mamlaka ya Mungu na hoja ya ukuu wa Mungu dhidi ya hatima ya binadamu viko huru dhidi ya mapenzi ya binadamu, havibadiliki kulingana na mapendeleo na machaguo yako ya binadamu. Mamlaka ya Mungu yapo kila mahali, kila saa, kila muda. Kama mbingu na nchi zingepita, mamlaka Yake yasingewahi kupita, kwani Yeye ni Mungu Mwenyewe, Anamiliki mamlaka ya kipekee, na mamlaka Yake hayazuiliwi au kuwekewa mipaka na watu, matukio, au vitu, na anga au na jiografia. Siku zote Mungu hushikilia mamlaka Yake, huonyesha uwezo Wake, huendeleza usimamizi Wake wa kazi kama kawaida; kila wakati Anatawala viumbe wote, hutosheleza viumbe wote, huunda na kupangilia viumbe wote, kama Alivyofanya siku zote. Hakuna anayeweza kubadilisha hili. Hii ni hoja; huu umekuwa ukweli usiobadilika tangu zama za kale!

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III

545. Ukweli kuhusiana na mamlaka ya Mungu ni ukweli ambao kila mmoja lazima atilie maanani kwa umakinifu, lazima apitie na aelewe katika moyo wake; kwani ukweli huu unao mwelekeo katika maisha ya kila mmoja, kwenye maisha ya kale, ya sasa, na ya siku za usoni ya kila mmoja, kwenye awamu muhimu ambazo kila mtu lazima apitie maishani, katika maarifa ya binadamu kuhusu ukuu wa Mungu na mtazamo ambao anafaa kuwa nao katika mamlaka ya Mungu, na kawaida, kwa kila hatima ya mwisho ya kila mmoja. Kwa hivyo inachukua nguvu za maisha yako yote kujua na kuyaelewa. Unapochukua mamlaka ya Mungu kwa umakinifu, unapoukubali ukuu wa Mungu, kwa utaratibu utaanza kutambua na kuelewa kwamba mamlaka ya Mungu kwa kweli yapo. Lakini kama hutawahi kutambua mamlaka ya Mungu, hutawahi kukubali ukuu Wake, basi haijalishi ni miaka mingapi utakayoishi, hutafaidi hata chembe maarifa ya ukuu wa Mungu. Kama hutajua na kuelewa kwa kweli mamlaka ya Mungu, basi utakapofika mwisho wa barabara, hata kama utakuwa umesadiki katika Mungu kwa miongo mingi, hutakuwa na chochote cha kuonyesha katika maisha yako, maarifa yako ya ukuu wa Mungu juu ya hatima ya binadamu yatakuwa kwa hakika sufuri bin sufuri. Huoni kuwa jambo hili ni la huzuni mno? Kwa hivyo haijalishi umetembea kwa umbali gani maishani, haijalishi unao umri wa miaka mingapi sasa, haijalishi safari inayosalia itakuwa ya umbali gani, kwanza lazima utambue mamlaka ya Mungu na kuyamakinikia, ukubali hoja kwamba Mungu ni Bwana wako wa kipekee. Kutimiza maarifa yaliyo wazi, sahihi na kuelewa ukweli huu kuhusiana na ukuu wa Mungu juu ya hatima ya binadamu ni funzo la lazima kwa kila mmoja, ndio msingi wa kuyajua maisha ya binadamu na kutimiza ukweli, ndiyo maisha ya kila siku na mafunzo ya kimsingi ya kumjua Mungu ambayo kila mmoja anakabiliana nayo, na ambayo hakuna yeyote anayeweza kuyakwepa. Kama mmoja wenu angependa kuchukua njia za mkato ili kufikia shabaha hii, basi Ninakuambia, hilo haliwezekani! Kama mmoja wenu anataka kukwepa ukuu wa Mungu, basi hilo nalo ndilo haliwezekani zaidi! Mungu ndiye Bwana wa pekee wa binadamu, Mungu ndiye Bwana wa pekee wa hatima ya binadamu, na kwa hivyo haiwezekani kwa binadamu kuamuru hatima yake mwenyewe, haiwezekani kwake kuishinda. Haijalishi uwezo wa mtu ni mkubwa kiasi kipi, mtu hawezi kuathiri, sikwambii kuunda, kupangilia, kudhibiti, au kubadilisha hatima za wengine. Yule Mungu Mwenyewe wa kipekee ndiye Anayeweza kuamuru tu mambo yote kwa binadamu, kwani Yeye tu ndiye anayemiliki mamlaka ya kipekee yanayoshikilia ukuu juu ya hatima ya binadamu; na kwa hivyo Muumba pekee ndiye Bwana wa kipekee wa binadamu. Mamlaka ya Mungu yanashikilia ukuu sio tu juu ya binadamu walioumbwa, lakini juu ya hata viumbe ambavyo havikuumbwa visivyoweza kuonekana na binadamu, juu ya nyota, juu ya ulimwengu mzima. Hii ni hoja isiyopingika, hoja ambayo kweli ipo, ambayo hakuna binadamu au kiumbe chochote kinaweza kubadilisha. Kama mmoja wenu angali hajatosheka na mambo kama yalivyo, akiamini kwamba una ujuzi fulani maalum au uwezo, na bado anafikiria unaweza kubahatika na kubadilisha hali zako za sasa au vinginevyo kuzitoroka; kama utajaribu kubadilisha hatima yako kupitia kwa jitihada za binadamu, na hivyo basi kujitokeza kati ya wengine na kupata umaarufu na utajiri; basi Ninakwambia, unayafanya mambo kuwa magumu kwako, unajitakia taabu tu, unajichimbia kaburi lako mwenyewe! Siku moja, hivi karibuni au baadaye, utagundua kwamba ulifanya chaguo baya, kwamba jitihada zako ziliambulia patupu. Malengo yako, tamanio lako la kupambana dhidi ya hatima, na mwenendo wako binafsi wa kupita kiasi, utakuongoza kwenye barabara isiyoweza kukurudisha kule ulikotoka, na kwa hili utaweza kujutia baadaye. Ingawaje sasa huoni ubaya wa athari hiyo, unapopitia na kushukuru zaidi na zaidi ukweli kwamba Mungu ndiye Bwana wa hatima ya maisha, utaanza kwa utaratibu kutambua kile Ninachozungumzia leo na athari zake za kweli. Haijalishi kama kwa kweli unao moyo na, haijalishi kama wewe ni mtu anayependa ukweli, inategemea tu ni mtazamo aina gani ambao utachukua kuhusiana na ukuu wa Mungu na ule ukweli. Na kwa kawaida, hili linaamua kama kweli unaweza kujua na kuelewa mamlaka ya Mungu. Kama hujawahi katika maisha yako kuhisi ukuu wa Mungu na mipangilio yake, na isitoshe hujawahi kutambua na kukubali mamlaka ya Mungu, basi utakosa thamani kabisa, bila shaka utakuwa athari ya chukizo na zao la kukataliwa na Mungu, hayo yote ni kutokana na njia uliyochukua na chaguo ulilofanya. Lakini wale ambao, katika kazi ya Mungu, wanaweza kukubali jaribio Lake, kukubali ukuu Wake, kujinyenyekeza katika mamlaka Yake, na kufaidi kwa utaratibu hali halisi waliyopitia na matamshi Yake, watakuwa wametimiza maarifa halisi ya mamlaka ya Mungu, ufahamu halisi wa ukuu Wake, na watakuwa kwa kweli watakuwa wanatii Muumba. Watu kama hao tu ndio watakaokuwa wameokolewa kwa kweli.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III

546. Mungu aliumba dunia hii, Aliumba mwanadamu huyu, na zaidi ya hayo Alikuwa muasisi wa utamaduni wa zamani wa Giriki na ustaarabu wa binadamu. Ni Mungu tu anayemfariji huyu mwanadamu, na ni Mungu tu anayemtunza mwanadamu huyu usiku na mchana. Ukuaji na maendeleo ya binadamu hayatengani na ukuu wa Mungu, na historia na mustakabali wa mwanadamu ni zisizochangulika kutoka kwa miundo ya Mungu. Kama wewe ni Mkristo wa kweli, basi hakika utaamini kwamba kupanda na kushuka kwa nchi ama taifa lolote hufanyika kulingana na miundo ya Mungu. Mungu pekee hujua majaliwa ya nchi ama taifa, na Mungu pekee hudhibiti mwendo wa huyu mwanadamu. Iwapo mwanadamu anataka kuwa na majaliwa mazuri, iwapo nchi inataka kuwa na majaliwa mazuri, basi lazima mwanadamu ampigie Mungu magoti kwa ibada, atubu na kukiri mbele ya Mungu, la sivyo majaliwa na hatima ya mwanadamu hayataepuka kumalizika kwa janga.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 2: Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote

547. Hatima za binadamu na zile za ulimwengu zimeingiliana kwa ndani na ukuu wa Muumba, zimefungamanishwa na haziwezi kutenganishwa na mipango ya Muumba; na hatimaye, haziwezi kutenganishwa na mamlaka ya Muumba. Kupitia kwenye sheria za mambo yote binadamu huja kuelewa mipango ya Muumba na ukuu Wake; kupitia kwenye sheria za namna ya kuishi ambazo anaona katika utawala wa Muumba; kutoka kwenye hatima za mambo yote anapata hitimisho kuhusu njia ambazo Muumba huonyesha ukuu Wake na kuvidhibiti; na kwenye mzunguko wa maisha ya binadamu na mambo yote ambayo binadamu kwa kweli hupitia ile mipango na mipangilio ya Muumba kwa mambo yote na kwa viumbe vyote vilivyo hai na anashuhudia kwa kweli namna ambavyo mipango na mipangilio hiyo inavyozidi sheria zote za nchi, kanuni, na taasisi, mamlaka na nguvu zote nyingine. Kwa mujibu wa haya, binadamu wanashawishiwa kutambua kwamba, ukuu wa Muumba hauwezi kukiukwa na kiumbe chochote kilichoumbwa, kwamba hakuna nguvu zinazoweza kuharibu au kubadilisha matukio na mambo yaliyoamuliwa kabla na Muumba. Ni kupitia kwenye sheria na kanuni hizi takatifu ambapo binadamu na viumbe vyote wanaweza kuishi na kuzalisha, kizazi baada ya kizazi. Je, huu si mfano halisi wa mamlaka ya Muumba?

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III

548. Ingawa Mungu anayamiliki mamlaka na nguvu, Anayo bidii sana na Anafuata kanuni katika vitendo Vyake, na Anashikilia maneno Yake. Bidii Yake na kanuni za vitendo Vyake, vinaonyesha namna Muumba asivyoweza kukosewa na namna ambavyo mamlaka ya Muumba yalivyo magumu kushindwa. Ingawa Anamiliki mamlaka ya juu, na kila kitu kinatawaliwa na Yeye, na japokuwa Anazo nguvu za kutawala vitu vyote, Mungu hajawahi kuharibu mpango Wake au kutatiza mpangilio Wake mwenyewe, na kila wakati Anapotumia mamlaka Yake, ni kulingana na umakinifu unaohitajika kwenye kanuni Zake mwenyewe na hasa kwa kufuata kile kilichotamkwa kutoka kwenye kinywa Chake, na kufuata hatua na majukumu ya mpango Wake. Sina haja ya kusema kwamba kila kitu kinachotawaliwa na Mungu pia kinatii kanuni ambazo mamlaka ya Mungu yanatumika, na hakuna mwanadamu au kitu kisichojumuishwa kwenye mipangilio ya mamlaka Yake, wala hakuna anayeweza kubadilisha kanuni ambazo mamlaka Yake yanatumika. Kwenye macho ya Mungu, wale wanaobarikiwa hupokea utajiri mzuri unaoletwa na mamlaka Yake, na wale wanaolaaniwa hupokea adhabu yao kwa sababu ya mamlaka ya Mungu. Chini ya ukuu wa mamlaka ya Mungu, hakuna binadamu au kitu ambacho hakijumuishwi, kwenye utumiaji wa mamlaka Yake, wala hakuna kinachoweza kubadilisha kanuni hizi ambazo mamlaka Yake yanatumiwa. Mamlaka ya Muumba hayabadilishwi kwa mabadiliko ya aina yoyote ile, na, vilevile, kanuni ambazo mamlaka Yake yanatumiwa hazibadiliki kwa sababu yoyote ile. Mbingu na ardhi vyote vinaweza kupitia misukosuko mingi, lakini mamlaka ya Muumba hayatabadilika; vitu vyote vitatoweka, lakini mamlaka ya Muumba hayatawahi kutoweka. Hiki ndicho kiini cha mamlaka ya Muumba ambayo hayabadiliki na ni yasiyokosewa, na huu ndio upekee wenyewe wa Muumba!

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

549. Shetani hajawahi kuthubutu kukiuka mamlaka ya Mungu, na, vilevile, amesikiliza kwa umakinifu siku zote na kutii shurutisho na amri mahususi za Mungu, asiwahi thubutu kuzivunja, na, bila shaka asithubutu kubadilisha kwa hiari shurutisho zozote za Mungu. Hiyo ndiyo mipaka ambayo Mungu amemwekea wazi Shetani, na hivyo Shetani hajawahi thubutu kuvuka mipaka hiyo. Huu si uwezo wa mamlaka ya Mungu? Je, huu si ushuhuda wa mamlaka ya Mungu? Wa namna ya kuwa mbele ya Mungu, na namna ya kumtazama Mungu, Shetani anao ung’amuzi bora zaidi kuliko mwanadamu, hivyo, katika ulimwengu wa kiroho, Shetani anaona hadhi na mamlaka ya Mungu vizuri sana, na anatambua sana ule uwezo wa mamlaka ya Mungu na kanuni zinazotilia mkazo kwenye mamlaka Yeye. Hathubutu, kamwe, kutozitilia maanani kanuni hizo, wala hathubutu kukiuka kanuni hizo kwa vyovyote vile, au kufanya chochote ambacho kinakiuka mamlaka ya Mungu, na hathubutu kukabiliana na hasira ya Mungu kwa njia yoyote. Ingawa ni mwovu na mwenye kiburi kiasili, Shetani hajawahi kuthubutu kuvuka mipaka na viwango alivyowekewa na Mungu. Kwa miaka milioni, ametii kwa umakinifu mipaka hii, ametii kila amri na shurutisho lililotolewa na Mungu na hajawahi kuthubutu kukanyaga juu ya alama. Ingawa ni mwenye kijicho, Shetani ni “mwerevu” zaidi kuliko mwanadamu aliyepotoka; anajua utambulisho wa Muumba, na anajua mipaka yake. Kutokana na vitendo vya Shetani vya kunyenyekea tunaweza kuona kwamba mamlaka na nguvu za Mungu ni maelekezo ya mbinguni ambayo hayawezi kukiukwa na Shetani, na kwamba yanatokana na upekee na mamlaka ya Mungu ndiposa viumbe vyote vinabadilika na kuzalisha katika njia ya mpangilio, kwamba mwanadamu anaweza kuishi na kuongezeka kupitia ndani ya mkondo ulioanzishwa na Mungu, huku hakuna mtu au kifaa kinachoweza kuuharibu mpango huu, na hakuna mtu au kifaa kinachoweza kubadilisha sheria hii—kwani vyote vinatoka kwenye mikono ya Muumba na kwenye mpangilio na mamlaka ya Muumba.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

550. Ule utambulisho wa pekee wa Shetani umesababisha watu wengi kuonyesha shauku thabiti kwenye maonyesho yake ya dhana mbalimbali. Kunao hata watu wengi wajinga wanaosadiki kwamba, kama vile Mungu, Shetani anamiliki mamlaka, kwani Shetani anaweza kuonyesha miujiza, na anaweza kufanya mambo ambayo mwanadamu hawezi kufanya. Kwa hivyo, mbali na kumwabudu Mungu, mwanadamu pia anahifadhi nafasi kwenye moyo wake, na hata humwabudu Shetani kama Mungu. Watu hawa wote ni wa kusikitikiwa na kuchukiwa. Ni wa kusikitikiwa kwa sababu ya kutojua kwao, na wa kuchukiwa kwa sababu ya hali yao ya uasi wa kidini na hali halisi ya maovu ya ndani kwa ndani. Wakati huu Nahisi kwamba ni muhimu niwafahamishe kuhusu maana ya mamlaka, yanaashiria nini, na yanawakilisha nini. Kwa mazungumzo ya jumla, Mungu Mwenyewe ni mamlaka, mamlaka Yake yanaashiria mamlaka ya juu na hali halisi ya Mungu, na mamlaka ya Mungu Mwenyewe yanawakilisha hadhi na utambulisho wa Mungu. Kwa hiyo, je, Shetani huthubutu kusema kwamba yeye ni Mungu? Je, Shetani huthubutu kusema kwamba aliumba viumbe vyote, na anashikilia ukuu juu ya viumbe vyote? Bila shaka la! Kwani hawezi kuumba viumbe vyote; mpaka leo, hajawahi kuumba chochote kilichoumbwa na Mungu, na hajawahi kuumba chochote kilicho na maisha. Kwa sababu hana mamlaka ya Mungu, hatawahi endapo itawezekana kumiliki hadhi na utambulisho wa Mungu, na hili linaamuliwa na hali yake halisi. Je, anazo nguvu sawa na Mungu? Bila shaka hana! Tunaita nini vitendo vya Shetani, na miujiza inayoonyeshwa na Shetani? Je, ni nguvu? Vitendo hivi vinaweza kuitwa mamlaka? Bila shaka la! Shetani huelekeza wimbi la maovu, na misukosuko, uharibifu, na kuchachawiza kila dhana ya kazi ya Mungu. Kwa miaka elfu kadhaa iliyopita, mbali na kupotosha na kunyanyasa mwanadamu, na kumjaribu na kumdanganya binadamu hadi kufikia kiwango cha uovu, na ukataaji wa Mungu, ili binadamu aweze kutembea kwenye bonde la kivuli cha mauti, je, Shetani amefanya chochote ambacho kinastahili hata kumbukumbu ndogo zaidi, pongezi au sherehe ndogo zaidi kutoka kwa binadamu? Kama Shetani angemiliki mamlaka na nguvu, je, binadamu angepotoshwa naye? Kama Shetani angemiliki mamlaka na nguvu, je, mwanadamu angepata madhara kutokana nayo? Kama Shetani angemiliki mamlaka na nguvu, je, mwanadamu angemwacha Mungu na kugeukia mauti? Kwa sababu Shetani hana mamlaka au nguvu, ni nini ambacho tunafaa kuhitimisha kuhusu hali halisi ya kila kitu anachofanya? Kunao wale wanaofafanua kila kitu ambacho Shetani hufanya kama ujanja mtupu, ilhali Nasadiki kwamba ufafanuzi kama huo haufai sana. Je, Matendo maovu ya kupotosha mwanadamu ni ujanja mtupu tu? Nguvu za maovu ambazo Shetani alimnyanyasia Ayubu, na tamanio lake kali la kumnyanyasa na kumpotosha, lisingewezekana kutimizwa kupitia kwa ujanja mtupu tu. Tukiangalia nyuma, tunaona kwamba, mara moja, kondoo na ng’ombe wa Ayubu walitawanyishwa kila pahali kotekote kwenye milima na vilima, walikuwa hawapo tena; kwa muda mfupi tu, utajiri mwingi wa Ayubu ukatoweka. Je, yawezekana kwamba haya yote yalitimizwa kupitia kwa ujanja mtupu tu? Asili ya yale yote ambayo Shetani hufanya yanalingana na kuingiliana na istilahi mbaya kama vile kudhoofisha, kukatiza, kuharibu, kudhuru, maovu, hali ya kuwa na kijicho, na giza, na kwa hivyo matukio haya yote ambayo si ya haki na ni maovu yanahusiana na kuunganika kwenye vitendo vya Shetani, na hayawezi kutenganishwa na ile hali halisi ya uovu wa Shetani. Haijalishi ni vipi ambavyo Shetani “alivyo na nguvu”, haijalishi ni vipi Shetani alivyo mwenye kuthubutu na haijalishi ni vipi uwezo wake ulivyo mwingi katika kusababisha madhara, haijalishi ni vipi anavyotumia mbinu zenye mseto mpana ambazo zinapotosha na kudanganya binadamu, haijalishi ni vipi alivyo mwerevu kupitia kwenye ujanja na njama zake ambazo anadhalilisha binadamu, haijalishi ni vipi anavyoweza kujibadilisha katika mfumo ule aliomo, hajawahi kuweza kuumba kiumbe chochote kimoja, hajawahi kuweza kuweka wazi sheria au kanuni za uwepo wa viumbe vyote, na hajawahi kutawala na kudhibiti kifaa chochote, kiwe ni chenye uhai au kisichokuwa na uhai. Ndani ya ulimwengu na mbingu, hakuna hata mtu au kifaa kimoja kilichotokana na Shetani, au kilichopo kwa sababu ya Shetani; hakuna hata mtu au kifaa kimoja ambacho kimetawaliwa na Shetani, au kudhibitiwa na Shetani. Kinyume cha mambo ni kwamba, hana budi kuishi katika utawala wa Mungu lakini, vilevile, lazima atii shurutisho na amri zote za Mungu. Bila ruhusa ya Mungu, ni vigumu sana kwa Shetani kugusa hata tone la maji au chembechembe ya mchanga kwenye ardhi; bila ruhusa ya Mungu, Shetani hana hata hiari ya kusongea mchwa wanaojiendea zao kwenye ardhi, sikwambii hata mwanadamu, aliyeumbwa na Mungu. Kwenye macho ya Mungu, Shetani ni duni zaidi ya yungiyungi kwenye mlima, hadi kwenye ndege wanaopaa hewani, hadi kwenye samaki walio baharini, hadi kwenye funza kwenye juu ya nchi. Wajibu wake miongoni mwa viumbe vyote ni kuhudumia viumbe vyote, na kufanyia kazi mwanadamu, na kuhudumia kazi ya Mungu na mpango Wake wa usimamizi. Licha ya vile anavyoonea wenzake kijicho katika asili yake, na vile ambavyo hali yake halisi ya maovu ilivyo, kitu ambacho Shetani anaweza kufanya tu ni kuweza kukubaliana kwa wajibu kuhusiana na kazi yake: kuwa mwenye huduma kwa Mungu, na kuwa mjalizo kwa Mungu. Hiki ndicho kiini na nafasi ya Shetani. Hali yake halisi haijaungana na maisha, haijaungana na nguvu, haijaungana na mamlaka; ni kitu cha kuchezea tu kwenye mikono ya Mungu, mtambo tu kwenye huduma ya Mungu!

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

551. Ingawa Shetani alimwangalia Ayubu kwa macho ya kutamani mali yake, bila ya ruhusa ya Mungu hakuthubutu kugusa hata unywele mmoja wa mwili wa Ayubu. Ingawa ni mwenye uovu na unyama wa ndani, baada ya Mungu kutoa shurutisho Lake kwake, Shetani hakuwa na chaguo lakini kutii shurutisho la Mungu. Na kwa hivyo, hata Ingawa Shetani alionekana kana kwamba ameshikwa na kichaa sawa na mbwa-mwitu miongoni mwa kondoo alipomjia Ayubu, hakuthubutu kusahau mipaka aliyowekewa wazi na Mungu, hakuthubutu kukiuka shurutisho za Mungu, na kwa hayo yote, Shetani hakuthubutu kutoka kwenye kanuni ya maneno ya Mungu—je, hii si kweli? Kutokana na mtazamo huu wa maisha, tunaona kwamba Shetani hathubutu kuvunja matamshi yoyote yale ya Yehova Mungu. Kwake Shetani, kila neno kutoka kwenye kinywa cha Mungu ni shurutisho, na sheria ya mbinguni, na maonyesho ya mamlaka ya Mungu—kwani nyuma ya kila neno la Mungu kunadokezwa adhabu ya Mungu kwa wale wanaokiuka maagizo ya Mungu, na wale wasiotii na wanaopinga sheria za mbinguni. Shetani anajua wazi kwamba kama atakiuka shurutisho za Mungu, basi lazima akubali athari za kukiuka mamlaka ya Mungu na kupinga sheria za mbinguni. Na sasa athari hizi ni zipi? Sina haja ya kusema kwamba, athari hizi bila shaka, ni adhabu kutoka kwa Mungu. Vitendo vya Shetani kwake Ayubu vilikuwa tu mfano mdogo wa yeye kumpotosha binadamu, na wakati ambapo Shetani alipokuwa akitekeleza vitendo hivi, ile mipaka ambayo Mungu Aliweka na amri Alizotoa kwake Shetani vilikuwa tu mfano mdogo wa kanuni zinazotokana na kila kitu anachofanya. Aidha, wajibu na nafasi ya Shetani katika suala hili ulikuwa tu mfano mdogo wa wajibu na nafasi yake katika kazi ya usimamizi wa Mungu, na utiifu kamili wa Shetani kwa Mungu wakati alipomjaribu Ayubu, ulikuwa tu mfano mdogo wa namna ambavyo Shetani hakuthubutu kuweka hata upinzani mdogo kwa Mungu katika kazi ya usimamizi wa Mungu. Ni onyo gani ambalo mifano hii midogo inakupa? Miongoni mwa mambo yote, akiwemo Shetani, hakuna mtu au kitu kinachoweza kukiuka sheria na kanuni za mbinguni zilizowekwa wazi na Muumba, na hakuna mtu au kitu kinachothubutu kukiuka sheria na kanuni hizi za mbinguni, kwani hakuna mtu au kifaa kinaweza kubadilisha au kuepuka adhabu ambayo Mungu anawawekea wale wanaokosa kumtii. Ni Muumba tu anayeweza kuanzisha sheria na kanuni za mbinguni, ni Muumba tu aliye na nguvu za kuanza kuzitekeleza na nguvu za Muumba ndizo haziwezi kukiukwa na mtu au kitu chochote. Haya ndiyo mamlaka ya kipekee ya Muumba, mamlaka haya yako juu zaidi miongoni mwa mambo yote, na kwa hivyo haiwezekani kusema kwamba “Mungu ndiye mkubwa zaidi naye Shetani ni nambari mbili.” Isipokuwa Muumba anayemiliki mamlaka ya kipekee, hakuna Mungu mwingine.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

552. Shetani amekuwa akipotosha mwanadamu kwa maelfu ya miaka. Ameleta kiwango kisichosemezeka cha maovu, amedanganya vizazi baada ya vizazi, na ametenda uhalifu wa kuchukiza ulimwenguni. Amedhulumu binadamu, amedanganya binadamu, ameshawishi binadamu ili ampinge Mungu, na ametenda vitendo vya maovu ambavyo vimetatiza na kuharibu mpango wa Mungu mara kwa mara. Ilhali, chini ya mamlaka ya Mungu, viumbe vyote na viumbe vyenye uhai vinaendelea kutii kanuni na sheria zilizowekwa wazi na Mungu. Yakilinganishwa na mamlaka ya Mungu, asili ovu ya Shetani na kuenea kwake ni vitu vibaya mno, vinakera mno na ni vya kuleta aibu na ni vidogo mno na vinyonge. Hata Ingawa Shetani anatembea miongoni mwa viumbe vyote vilivyoumbwa na Mungu, hawezi kutekeleza mabadiliko madogo zaidi kwa watu, vitu, na vifaa vilivyoamriwa na Mungu. Miaka elfu kadhaa imepita, na mwanadamu angali anafurahia nuru na hewa aliyopewa na Mungu, angali anapumua pumzi iliyotolewa na Mungu Mwenyewe, angali anafurahia maua, ndege, samaki na wadudu walioumbwa na Mungu, na kufurahia viumbe vyote vilivyotolewa na Mungu; mchana na usiku zingali zinabadilishana nafasi zao bila kusita; hiyo misimu minne inabadilishana kama kawaida; nao batabukini wanaopaa wanaondoka msimu huu wa kipupwe, lakini bado watarudi kwenye msimu ujao wa machipuko; samaki ndani ya maji hawajawahi kuondoka kwenye mito, maziwa—maskani yao; wadudu aina ya nyenje kwenye mchanga wanaimba kwelikweli kwenye siku za kiangazi; nyenje kwenye nyasi wanaimba kwa sauti ya polepole huku wakikaribisha msimu wa mapukutiko, wale batabukini wanaanza kutembea kwa makundi, huku nao tai wanabakia pweke; fahari za simba wakijitosheleza wenyewe kwa kuwinda; nao kunguni wa kaskazini wa Ulaya hawatoki kwenye nyasi na maua…. Kila aina ya kiumbe kilicho hai miongoni mwa viumbe vyote kinaondoka na kurudi, kisha kinaondoka tena, mabadiliko milioni yanafanyika kwa muda wa kufumba na kufumbua—lakini kile kisichobadilika ni silika zao na sheria za kusalia. Wanaishi katika ruzuku na kustawishwa na Mungu, na hakuna mtu anayeweza kubadilisha silika zao, na vilevile hakuna mtu yeyote anayeweza kukiuka sheria hizi za kuishi. Ingawa mwanadamu, anayeishi miongoni mwa viumbe vyote amepotoka na kudanganywa na Shetani, angali hawezi kupuuza maji yaliyoumbwa na Mungu, hewa iliyoumbwa na Mungu, na vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu, na binadamu angali bado anaishi na kuzaana kwenye anga hii iliyoumbwa na Mungu. Silika za mwanadamu zingali hazijabadilika. Binadamu angali anategemea macho yake kuona, masikio yake kusikia, ubongo wake kufikiria, moyo wake kuelewa, miguu na viganja vyake kutembea, mikono yake kufanya kazi, na kadhalika; silika zote ambazo Mungu alimpa binadamu ili aweze kukubali toleo la Mungu limebakia hivyo bila kubadilishwa, welekevu ambao binadamu alitumia kushirikiana na Mungu bado haujabadilika, welekevu wa mwanadamu wa kutenda wajibu wa kiumbe kilichoumbwa haujabadilishwa, mahitaji ya kiroho ya mwanadamu hayajabadilika, tamanio la mwanadamu kuweza kujua asili zake halijabadilika, hamu ya mwanadamu kuweza kuokolewa na Muumba haijabadilika. Hizi ndizo hali za sasa za mwanadamu, anayeishi katika mamlaka ya Mungu, na ambaye amevumilia maangamizo mabaya yaliyoletwa na Shetani. Ingawa mwanadamu amepitia unyanyasaji wa Shetani, na yeye si Adamu na Hawa tena kutoka mwanzo wa uumbaji, badala yake amejaa mambo ambayo yana uadui na Mungu kama vile maarifa, fikira na kadhalika, na amejaa tabia ya kishetani iliyopotoka, kwenye macho ya Mungu, mwanadamu yungali bado mwanadamu yule yule Aliyemuumba. Mwanadamu angali anatawaliwa na kupangiwa na Mungu, na angali anaishi ndani ya mkondo uliowekwa wazi na Mungu, na kwa hivyo kwenye macho ya Mungu, mwanadamu ambaye amepotoshwa na Shetani amefunikwa tu na uchafu na tumbo linalonguruma, na miitikio ambayo ni ya kujikokota kidogo, kumbukumbu ambayo si nzuri kama ilivyokuwa, na ni mzee kidogo—lakini kazi na silika zote za binadamu bado hazijapata madhara kamwe. Huyu ndiye mwanadamu ambaye Mungu ananuia kuokoa. Mwanadamu huyu anahitaji tu kusikia mwito wa Muumba na kusikia sauti ya Muumba, naye atasimama wima na kukimbia kutafuta ni wapi sauti imetokea. Mwanadamu huyu lazima tu aweze kuona umbo la Muumba naye hatakuwa msikivu wa kila kitu kingine, ataacha kila kitu, ili kuweza kujitolea mwenyewe kwa Mungu, na hata atayatenga maisha yake kwa ajili Yake. Wakati moyo wa mwanadamu unapoelewa maneno hayo ya moyoni kutoka kwa Muumba, mwanadamu atakataa Shetani na atakuja upande wake Muumba; wakati mwanadamu atakuwa ametakasa kabisa uchafu kutoka kwenye mwili wake, na amepokea kwa mara nyingine toleo na ukuzaji kutoka kwa Muumba, basi kumbukumbu la mwanadamu litarejeshwa, na kwa wakati huu mwanadamu atakuwa amerejea kwa kweli katika utawala wa Muumba.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

553. Mamlaka ya Mungu hayawezi kuigwa na binadamu, na utambulisho na hadhi ya Mungu haiwezi kuigizwa na binadamu. Ingawa unaweza kuiga sauti ambayo Mungu huongea nayo, huwezi kuiga hali halisi ya Mungu. Ingawa unaweza kusimama mahali pa Mungu na kujifanya kuwa Mungu, hutawahi kuweza kufanya kile ambacho Mungu ananuia kukifanya, na hutawahi kutawala na kuamuru viumbe vyote. Katika macho ya Mungu, utabakia kuwa kiumbe kidogo, na haijalishi ni vipi ambavyo mbinu na uwezo wako ulivyo mkubwa, haijalishi ni vipaji vingapi unavyo, uzima wako wewe umetawaliwa na Muumba. Ingawa unaweza kusema maneno fulani ya kijeuri, hilo haliwezi kuonyesha kuwa unayo hali halisi ya Muumba, wala kuwakilisha ya kwamba unamiliki mamlaka ya Muumba. Mamlaka na nguvu za Mungu ni hali halisi ya Mungu Mwenyewe. Hayakufunzwa wala kusomwa, au kuongezewa kutoka nje, lakini ni hali ya asili ya Mungu Mwenyewe. Na kwa hivyo uhusiano kati ya Muumba na viumbe hauwezi katu kubadilishwa. Kama mojawapo ya viumbe, lazima mwanadamu achukue nafasi yake mwenyewe, na ajiendeleze kwa uangalifu, na kulinda kwa wajibu kile ambacho ameaminiwa na Muumba. Naye binadamu lazima asitende mambo nje ya mipaka yake au kufanya mambo zaidi ya uwezo wake au kufanya mambo ambayo ni ya kuchukiza Mungu. Binadamu ni lazima asijaribu kuwa mkubwa, au wa kipekee, au zaidi ya wengine, wala asitafute kuwa Mungu. Hivi ndivyo watu hawafai kutamani kuwa. Kutamani kuwa mkubwa au wa kipekee ni jambo la upuuzi. Kutafuta kuwa Mungu ndilo hata jambo la aibu zaidi; linaudhi na linastahili kudharauliwa. Kile cha kupongezwa, na ambacho viumbe vinastahili kushikilia kuliko chochote kile ni kuwa viumbe vya kweli; hii ndiyo shabaha pekee ambayo watu wote wanafaa kufuatilia.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Iliyotangulia: XI. Maneno Juu ya Kumjua Mungu

Inayofuata: B. Kuhusu Tabia ya Haki ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp