5. Hukumu tu na Kuadibu kwa Mungu katika Siku za Mwisho ndiyo Kazi Yake Muhimu, Inayoweza Kuamua ya Kumuokoa Mwanadamu

Aya za Biblia za Kurejelea:

“Akisema kwa sauti kuu, Mwogopeni Mungu, na kumpa utukufu; kwa kuwa saa ya hukumu yake imekuja” (Ufunuo 14:7).

“Kwa maana muda umekuja ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu” (1 Petro 4:17).

“Naye atafanya hukumu miongoni mwa mataifa, na atawakemea watu wengi” (Isaya 2:4).

“Na mtu yeyote akiyasikia maneno Yangu, na asiyaamini, Mimi sitamhukumu: kwa kuwa mimi sikuja ili niihukumu dunia, bali kuiokoa dunia. Yeye ambaye ananikataa Mimi, na hayakubali maneno Yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho” (Yohana 12:47-48).

“Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati Yeye, Roho wa ukweli, Atakapokuja, Atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana Hatazungumza yaliyo Yake Mwenyewe; bali chochote Atakachosikia, Atakinena: na Atawaonyesha mambo yajayo” (Yohana 16:12-13).

Maneno Husika ya Mungu:

Yesu Alipokuja katika ulimwengu wa mwanadamu, Aliikaribisha Enzi ya Neema na Akatamatisha Enzi ya Sheria. Wakati wa siku za mwisho, Mungu kwa mara nyingine Alipata mwili, na kwa mwili huu, Alitamatisha Enzi ya Neema na Akaikaribisha Enzi ya Ufalme. Wale wote wanaoweza kukubali kupata mwili kwa Mungu mara ya pili wataongozwa kuingia katika Enzi ya Ufalme, na zaidi ya hayo watakuwa na uwezo wa kukubali kibinafsi uongozi wa Mungu. Hata ingawa Yesu Alikuja miongoni mwa wanadamu na akafanya kazi nyingi, Alimaliza tu kazi ya kuwakomboa wanadamu wote na Akawa kama sadaka ya dhambi ya mwanadamu; Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuwa kama sadaka ya dhambi tu na kuchukua dhambi za mwanadamu, lakini pia kulimlazimu Mungu afanye hata kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake iliyopotoshwa na Shetani kikamilifu. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Alirudi katika mwili kumwongoza mwanadamu kuingia katika enzi mpya, na Akaanza kazi ya kuadibu na hukumu. Kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wale wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na wao watapata ukweli, njia na uzima.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji

Nilijulikana kama Yehova wakati mmoja. Pia niliitwa Masihi, na wakati mmoja watu waliniita Yesu Mwokozi kwa sababu walinipenda na kuniheshimu. Lakini leo Mimi si yule Yehova au Yesu ambaye watu walimfahamu nyakati zilizopita—Mimi ni Mungu ambaye Amerejea katika siku za mwisho, Mungu ambaye Ataikamilisha enzi. Mimi ni Mungu Mwenyewe ambaye Anainuka kutoka mwisho wa dunia, Nimejawa na tabia Yangu nzima, na Nimejawa na mamlaka, heshima na utukufu. Watu hawajawahi kushirikiana na Mimi, hawajawahi kunifahamu, na daima hawaijui tabia Yangu. Tangu uumbaji wa dunia hadi leo, hakuna mtu yeyote ambaye ameniona. Huyu ni Mungu anayemtokea mwanadamu katika siku za mwisho lakini Amejificha kati ya wanadamu. Anaishi kati ya wanadamu, ni wa kweli na halisi, kama jua liwakalo na moto unaochoma, Aliyejaa nguvu na kujawa mamlaka. Hakuna mtu au kitu chochote ambacho hakitahukumiwa kwa maneno Yangu, na mtu au kitu chochote ambacho hakitatakaswa kupitia moto unaowaka. Hatimaye, mataifa yote yatabarikiwa kwa ajili ya maneno Yangu, na pia kupondwa na kuwa vipande vipande kwa sababu ya maneno Yangu. Kwa njia hii, watu wote katika siku za mwisho wataona kuwa Mimi ndiye Mwokozi aliyerejea, Mimi ndiye Mungu Mwenyezi ambaye Anawashinda binadamu wote, nami Nilikuwa sadaka ya dhambi kwa mwanadamu wakati mmoja, lakini katika siku za mwisho Ninakuwa pia miale ya Jua linalochoma vitu vyote, na pia Jua la haki Linalofichua vitu vyote. Hivyo ndivyo ilivyo kazi Yangu ya siku za mwisho. Nilichukua jina hili nami Ninamiliki tabia hii ili watu wote wapate kuona kuwa Mimi ni Mungu mwenye haki, na Mimi ni jua linalochoma, na moto unaowaka. Ni hivyo ili watu wote waweze kuniabudu, Mungu pekee wa kweli, na ili waweze kuuona uso Wangu wa kweli: Mimi si Mungu wa Wayahudi tu, na Mimi si Mkombozi tu—Mimi ni Mungu wa viumbe vyote katika mbingu na dunia na bahari.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe”

Kazi katika siku za mwisho ni kunena maneno. Mabadiliko makuu yanaweza kusababishwa kwa watu kupitia katika maneno hayo. Mabadiliko yanayosababishwa sasa kwa watu hawa kwa sababu ya kukubali maneno haya ni makubwa kuliko yale ya watu katika Enzi ya Neema kwa kukubali ishara na maajabu hayo. Kwa maana, katika Enzi ya Neema, mapepo yalitolewa kutoka kwa mwanadamu kwa kuwekewa mikono na maombi, lakini tabia potovu ndani ya mwanadamu bado zilibaki. Mwanadamu aliponywa ugonjwa wake na kusamehewa dhambi zake, lakini kuhusu jinsi tu mwanadamu angesafishwa na tabia potovu za kishetani ndani yake, kazi hii ilikuwa bado kufanywa. Mwanadamu aliokolewa na kusamehewa dhambi zake kwa imani yake, lakini asili ya dhambi ya mwanadamu haikuchukuliwa na ikabaki naye. Dhambi za mwanadamu zilisamehewa kupitia mwili wa Mungu mwenye mwili, lakini hili halikumaanisha kuwa mwanadamu hakuwa na dhambi ndani yake. Dhambi za mwanadamu zingesamehewa kupitia sadaka ya dhambi, lakini mwanadamu hajaweza kutatua suala la vipi hangeweza kutenda dhambi na vile asili Yake ya dhambi ingetupiliwa mbali kabisa na kubadilishwa. Dhambi za mwanadamu zilisamehewa kwa sababu ya kazi ya Mungu ya kusulubiwa, lakini mwanadamu akaendelea kuishi katika tabia yake potovu ya zamani ya kishetani. Hali hii ikiwa hivyo, mwanadamu lazima aokolewe kabisa kutoka kwa tabia yake potovu ya kishetani, ili asili yake ya dhambi iweze kung’olewa kabisa, isiweze kukua tena, hivyo kuwezesha tabia ya mwanadamu kubadilishwa. Hii inampasa mwanadamu kuelewa njia ya kukua katika maisha, njia ya maisha, na jinsi ya kubadilisha tabia yake. Inamhitaji pia mwanadamu kutenda kulingana na njia hii ili tabia ya mwanadamu iweze kubadilika hatua kwa hatua na aishi chini ya nuru inayong’aa, na aweze kufanya mambo yote kulingana na mapenzi ya Mungu, atupilie mbali tabia potovu za kishetani, na kutoka kwa ushawishi wa Shetani wa giza, hivyo kutoka kabisa katika dhambi. Ni hapo tu ndipo mwanadamu atapokea wokovu kamili. Yesu Alipokuwa Akifanya kazi Yake, maarifa ya mwanadamu juu Yake yalikuwa bado hayakuwa bayana na hayakuwa wazi. Mwanadamu aliamini kila wakati kuwa Alikuwa Mwana wa Daudi na kumtangaza kuwa nabii mkuu na Bwana mwema Aliyezikomboa dhambi za mwanadamu. Wengine, wakiwa na msingi wa imani, wakaponywa tu kwa kugusa vazi Lake; vipofu wakaona na hata wafu kurejeshwa katika uhai. Hata hivyo, mwanadamu hangeweza kutambua tabia potovu za kishetani zilizokita mizizi ndani yake na pia mwanadamu hakujua jinsi ya kuitoa. Mwanadamu alipokea neema nyingi, kama amani na furaha ya mwili, baraka ya familia nzima juu ya imani ya mmoja, na kuponywa magonjwa, na mengine mengi. Yaliyobaki ni matendo mema ya mwanadamu na kuonekana kwa kiungu; kama mtu angeishi katika huo msingi, angechukuliwa kama muumini mzuri. Waumini hao tu ndio wangeingia mbinguni baada ya kifo, ambayo ilimaanisha kuwa walikuwa wameokolewa. Lakini katika maisha yao, hawakuelewa kamwe njia ya maisha. Walitenda tu dhambi, na kisha kukiri kila wakati bila njia yoyote ya kubadili tabia yao; hii ndiyo ilikuwa hali ya mwanadamu katika Enzi ya Neema. Je mwanadamu amepokea wokovu kamili? La! Kwa hivyo, hatua ilipokamilika, bado kuna kazi ya hukumu na kuadibu. Hatua hii ni ya kumfanya mwanadamu awea safi kupitia neno, na hivyo kumpa njia ya kufuata. Hatua hii haingekuwa na matunda ama ya maana kama ingeendelea na kukemea mapepo, kwani msingi wa dhambi wa mwanadamu haungetupwa mbali na mwanadamu angekoma tu baada ya msamaha wa dhambi. Kupitia kwa sadaka ya dhambi, mwanadamu amesamehewa dhambi zake, kwani kazi ya kusulubisha imefika mwisho na Mungu Ametawala juu ya Shetani. Lakini tabia potovu ya wanadamu bado imebaki ndani yao na mwanadamu anaweza kutenda dhambi na kumpinga Mungu; Mungu hajampata mwanadamu. Hiyo ndio sababu katika hatua hii ya kazi Mungu Anatumia neno kufichua tabia potovu ya mwanadamu na kumuomba mwanadamu kutenda kulingana na njia sahihi. Hatua hii ni ya maana zaidi kuliko zile za awali na pia yenye mafanikio zaidi, kwani wakati huu ni neno ambalo linatoa maisha moja kwa moja kwa mwanadamu na linawezesha tabia ya mwanadamu kubadilishwa kabisa; ni hatua ya kazi ya uhakika kabisa. Kwa hivyo, Mungu kupata mwili katika siku za mwisho imekamilisha umuhimu wa Mungu kupata mwili wa Mungu na kukamilisha usimamizi wa Mungu katika mpango wa kuokoa mwanadamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)

Kabla ya mwanadamu kukombolewa, sumu nyingi za Shetani zilikuwa tayari zimepandwa ndani yake na, baada ya maelfu ya miaka ya kupotoshwa na Shetani, ndani yake ana asili inayompinga Mungu. Kwa hiyo, mwanadamu alipokombolewa, haikuwa chochote zaidi ya kisa cha ukombozi. Yaani, mwanadamu ananunuliwa tena kwa gharama ya juu, lakini asili ya sumu ndani yake haikuwa imeondolewa. Mwanadamu ambaye ni mchafu sana lazima apitie mabadiliko kabla ya kuwa mwenye kustahili kumtumikia Mungu. Kupitia kazi hii ya kuadibu na hukumu, mwanadamu atakuja kujua kikamlifu kiini cha uchafu na upotovu kilicho ndani yake, na ataweza kubadilika kabisa na kutakasika. Ni kwa namna hii tu ndivyo mwanadamu ataweza kustahili kurudi mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Kazi yote ifanywayo siku hii ya leo ni ili mwanadamu afanywe msafi na kubadilika; kupitia hukumu na kuadibiwa na neno, na pia kutakaswa, mwanadamu anaweza kuacha nje upotovu wake na kufanywa safi. Badala ya kuichukua hatua hii ya kazi kuwa ile ya wokovu, itafaa zaidi kusema kuwa ni kazi ya utakaso. Kwa kweli hatua hii ni ile ya ushindi na pia hatua ya pili ya wokovu. Mwanadamu anatwaliwa na Mungu kupitia hukumu na kuadibu na neno; kwa kutumia neno kusafisha, hukumu na kufichua, uchafu wote, fikira, nia, na matumaini ya mtu mwenyewe katika moyo wa mwanadamu zinafuliwa.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Fumbo la Kupata Mwili (4)

Mungu Anapopata mwili mara hii, kazi Yake ni kuonyesha tabia Yake, kimsingi kupitia kuadibu na hukumu. Akitumia haya kama msingi, Analeta ukweli zaidi kwa mwanadamu, kuonyesha njia zaidi za matendo, na hivyo Hufikia lengo Lake la kumshinda mwanadamu na kumwokoa mwanadamu kutokana na tabia yake potovu. Hili ndilo liko katika kazi ya Mungu katika Enzi ya Ufalme.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji

Kristo wa siku za mwisho hutumia aina mbalimbali za ukweli kumfundisha mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchanganua maneno na matendo ya mwanadamu. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na vilevile hekima na tabia ya Mungu. Maneno haya yote yanaelekezwa kwa kiini cha mwanadamu na tabia zake potovu. Hasa, maneno yanayofichua jinsi mwanadamu humkataa Mungu yanaelekezwa hata zaidi kwa jinsi mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani, na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. Katika kufanya kazi Yake ya hukumu, Mungu haelezi kwa ukamilifu asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anafichua na kupogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi zote tofauti za kufichua, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida; badala yake, ukweli ambao mwanadamu hana kabisa hutumiwa kutekeleza kazi hii ya ufichuzi na upogoaji. Ni mbinu kama hizi pekee ndizo zinaweza kuitwa hukumu; ni kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndiyo mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kuhusu Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu halisi wa Mungu. Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu imemwezesha mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa nia za Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia imemwezesha mwanadamu kuelewa na kujua kiini chake potovu na asili ya upotovu wake, na vilevile kugundua sura yake mbaya. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa kweli kiini cha kazi hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli wa Mungu, njia, na uzima wa Mungu kwa wale wote walio na imani Kwake. Kazi hii ndiyo kazi ya hukumu inayofanywa na Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli

Katika Enzi ya Ufalme, Mungu hutumia maneno kuikaribisha enzi mpya, kubadilisha njia ambayo kwayo Yeye hufanya kazi, na kufanya kazi ya enzi nzima. Hii ndiyo kanuni ambayo kwayo Mungu hufanya kazi katika Enzi ya Neno. Alikuwa mwili ili Anene kutoka katika mitazamo tofauti, ili mwanadamu aweze kumwona Mungu kweli, ambaye ni Neno kuonekana katika mwili, na angeweza kuona hekima na ajabu Yake. Kazi kama hiyo inafanywa ili kufikia malengo ya kumshinda mwanadamu, kumkamilisha mwanadamu na kumuondoa mwanadamu. Hii ndiyo maana halisi ya kutumia Neno kufanya kazi katika Enzi ya Neno. Kupitia kwa Neno, mwanadamu anakuja kuijua kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, kiini cha mwanadamu, na kile ambacho mwanadamu anafaa kuingia ndani. Kupitia kwa Neno, kazi ambayo Mungu anataka kufanya katika Enzi ya Neno inatimizwa kwa ukamilifu. Kupitia kwa Neno, mwanadamu anafichuliwa, anaondolewa, na kujaribiwa. Mwanadamu ameliona Neno, amelisikia Neno, na kuwa na ufahamu wa kuwepo kwa Neno. Kwa sababu hiyo, anaamini katika kuwepo kwa Mungu, katika uweza na hekima ya Mungu, na vilevile katika upendo wa Mungu kwa mwanadamu na hamu Yake ya kumwokoa mwanadamu. Ingawa neno “Neno” ni rahisi na la kawaida, Neno kutoka katika kinywa cha Mungu mwenye mwili hutikisa ulimwengu mzima; linabadilisha moyo wa mwanadamu, mawazo, na tabia ya zamani, na jinsi ulimwengu wote ulivyokuwa ukionekana. Katika enzi zote, ni Mungu wa leo tu ndiye Anayefanya kazi kwa njia hii, na ni Yeye Anayezungumza kwa namna hii na kuja kumwokoa mwanadamu hivi. Kuanzia wakati huu na kuendelea, mwanadamu anaishi chini ya mwongozo wa maneno ya Mungu, akichungwa na kuruzukiwa na maneno Yake. Watu wanaishi katika ulimwengu wa maneno ya Mungu, kati ya laana na baraka za maneno ya Mungu, na kuna hata watu wengi zaidi ambao wamekuja kuishi chini ya hukumu na kuadibu kwa maneno Yake. Maneno haya na kazi hii vyote ni kwa sababu ya wokovu wa mwanadamu, kwa sababu ya kutimiza mapenzi ya Mungu, na kwa sababu ya kubadilisha kuonekana kwa asili kwa ulimwengu wa uumbaji wa zamani. Mungu aliuumba ulimwengu kwa kutumia maneno, Anawaongoza watu ulimwenguni kote kutumia maneno, na Anawashinda na kuwaokoa kutumia maneno. Hatimaye, Atatumia maneno kuutamatisha ulimwengu mzima wa zamani, hivyo kuukamilisha mpango Wake mzima wa usimamizi. Katika Enzi nzima ya Ufalme, Mungu hutumia Neno kufanya kazi Yake na kufikia matokeo ya kazi Yake; Yeye hafanyi maajabu au kufanya miujiza; Yeye hufanya tu kazi Yake kupitia Neno. Kwa sababu ya maneno haya, mwanadamu hulishwa na kuruzukiwa, na hupata maarifa na uzoefu wa kweli.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Enzi ya Ufalme Ni Enzi ya Neno

Kwa kweli, kazi inayofanywa sasa ni kuwafanya watu kumtoroka Shetani, kutoroka babu zao wa kale. Hukumu zote kwa neno zinalenga kufichua tabia potovu ya binadamu na kuwawezesha watu kuelewa kiini cha maisha. Hukumu hizi zinazorudiwa mara kwa mara zote huchoma mioyo ya watu. Kila hukumu inaathiri moja kwa moja hatima yao na inakusudiwa kuumiza mioyo yao ili waweze kuachana na mambo hayo yote na hivyo basi kuja kujua maisha, kuujua ulimwengu huu mchafu, na pia kujua hekima ya Mungu na uweza Wake na kujua mwanadamu huyu aliyepotoshwa na Shetani. Kadiri aina hii ya kuadibu na hukumu inavyozidi, ndivyo moyo wa mwanadamu unavyoweza kujeruhiwa na ndivyo roho yake inavyoweza kuamshwa. Kuziamsha roho za watu hawa waliopotoshwa sana na waliodanganyika sana ndilo lengo la aina hii ya hukumu. Mwanadamu hana roho, yaani, roho yake ilikufa zamani na hajui kwamba kuna Mbingu, hajui kwamba kuna Mungu, na kwa hakika hajui kwamba anahangaika katika shimo la kifo; anaweza kujuaje kwamba anaishi katika kuzimu hii yenye maovu hapa ulimwenguni? Angewezaje kujua kwamba maiti hii yake ambayo imeoza, kwa kupotoshwa na shetani, imeanguka Kuzimuni kwenye kifo? Angewezaje kujua kwamba kila kitu hapa ulimwenguni kimeharibiwa kitambo kiasi cha kutokarabatika na mwanadamu? Na angewezaje kujua kwamba Muumba amekuja duniani leo na anatafuta kikundi cha watu wapotovu ambao Anaweza kuwaokoa? Hata baada ya mwanadamu kupitia kila usafishaji na hukumu inayowezekana, ufahamu wake wa chini unashtuka kwa shida na kwa kweli hauitikii chochote. Binadamu wamezoroteka kweli! Ingawa aina hii ya hukumu ni kama mvua katili ya mawe inyeshayo kutoka mbinguni, ni yenye manufaa makubwa zaidi kwa binadamu. Lau si kwa kuwahukumu watu namna hii, kusingekuwa na matokeo na isingewezekana kabisa kuwaokoa watu kutoka kwenye dimbwi la taabu. Kama isingekuwa kwa kazi hii, ingekuwa vigumu sana kwa watu kutoka Kuzimuni kwa sababu mioyo yao imekufa kitambo na roho zao kukanyagiwa kitambo na Shetani. Kuwaokoa nyinyi ambao mmeanguka kwenye kina kirefu cha uozo kunahitaji kuwaita kwa bidii sana, kuwahukumu kwa bidii sana, na kwa kufanya hivi tu ndipo mioyo hiyo yenu migumu itakapozinduka.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Waliokamilishwa Pekee Ndio Wanaoweza Kuishi Maisha Yenye Maana

Katika kazi Yake ya mwisho ya kuhitimisha enzi, tabia ya Mungu ni ya kuadibu na hukumu, ambapo Anafichua yote yasiyo ya haki, ili kuhukumu hadharani watu wote, na kuwakamilisha wale wanaompenda kwa moyo wa kweli. Ni tabia tu kama hii ndiyo ambayo inaweza kufikisha enzi hii mwisho. Siku za mwisho tayari zimewadia. Vitu vyote katika uumbaji vitatenganishwa kulingana na aina yao, na kugawanywa katika makundi tofauti kulingana na asili yao. Huu ni wakati ambapo Mungu Atafichua matokeo na hatima ya binadamu. Ikiwa watu hawatapitia kuadibu na hukumu, basi hakutakuwa na njia ya kufichua uasi wao na udhalimu wao. Ni kwa njia ya kuadibu na hukumu ndipo mwisho wa mambo yote yatafunuliwa. Mwanadamu huonyesha tu ukweli ulio ndani yake anapoadibiwa na kuhukumiwa. Mabaya yataekwa na mabaya, mema na mema, na wanadamu watatenganishwa kulingana na aina. Kupitia kuadibu na hukumu, mwisho wa mambo yote utafichuliwa, ili mabaya yaadhibiwe na mazuri yatunukiwe thawabu, na watu wote watakuwa wakunyenyekea chini ya utawala wa Mungu. Kazi hii yote lazima itimizwe kupitia kuadibu kwa haki na hukumu. Kwa sababu upotovu wa mwanadamu umefikia kilele chake na kutotii kwake kuwa kubaya kupita kiasi, ni tabia ya Mungu tu ya haki, ambayo kimsingi imechangiwa na kuadibu na hukumu na kufichuliwa wakati wa siku za mwisho, inayoweza kumbadilisha na kukamilisha mwanadamu kikamilifu. Ni tabia hii pekee ambayo itafichua maovu na hivyo kuwaadhibu watu wote dhalimu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maono ya Kazi ya Mungu (3)

Mungu anafanya kazi ya hukumu na kuadibu ili kwamba mwanadamu amjue, na kwa ajili ya ushuhuda Wake. Bila hukumu Yake juu jya tabia potovu ya mwanadamu, basi mwanadamu hangeweza kujua tabia Yake ya haki isiyoruhusu kosa lolote, na hangeweza kubadili ufahamu Wake wa Mungu kuwa mpya. Kwa ajili ya ushuhuda Wake, na kwa ajili ya usimamizi Wake, Anafanya ukamilifu Wake kuwa wazi kwa kila mtu, hivyo kumwezesha mwanadamu kupata ufahamu wa Mungu, na kubadili tabia yake, na kuwa na ushuhuda mkuu kwa Mungu kupitia kuonekana kwa Mungu hadharani. Mabadiliko ya tabia ya mwanadamu yanafanikishwa kupitia kazi nyingi tofauti za Mungu; bila mabadiliko ya aina hii katika tabia ya mwanadamu, mwanadamu hangeweza kuwa na ushuhuda kwa Mungu, na hangeweza kuambatana na nia za Mungu. Mabadiliko ya tabia ya mwanadamu yanaashiria kwamba mwanadamu amewekwa huru kutoka kwa utumwa wa Shetani na kutoka kwa ushawishi wa giza, na kwa kweli amekuwa mfano na kielelezo cha kazi ya Mungu, shahidi wa Mungu, na mtu ambaye anaambatana na nia za Mungu. Leo hii, Mungu mwenye mwili Amekuja duniani kufanya kazi Yake, na Anahitaji kwamba mwanadamu apate ufahamu kumhusu, apate kumtii Yeye, na awe na ushuhuda Kwake—mwanadamu anapaswa kujua kazi Yake ya vitendo na ya kawaida, anapaswa kutii maneno Yake yote na kazi ambayo haiambatani na mawazo ya mwanadamu, na anapaswa kuwa na ushuhuda kwa kazi Yake yote anayofanya kumwokoa mwanadamu, na vilevile matendo Yake yote ya kumshinda mwanadamu. Wale walio na ushuhuda kwa Mungu lazima wawe na ufahamu wa Mungu; ni ushuhuda wa aina hii tu ndio ulio sahihi, na wa vitendo, na ni ushuhuda wa aina hii tu ndio unaoweza kumwaibisha Shetani. Mungu anawatumia wale ambao wamepata kumjua kupitia hukumu Yake, kuadibu, na upogoaji, kuwa na ushuhuda Kwake. Yeye huwatumia wale waliopotoshwa na Shetani kumtolea Yeye ushuhuda. Yeye huwatumia wale ambao tabia yao imebadilika, na wale ambao wamepokea baraka Zake, kumtolea ushuhuda. Yeye hamhitaji mwanadamu amsifu kwa kinywa chake, wala hana hitaji lolote la sifa na ushuhuda kutoka kwa aina ya Shetani, ambao hawajaokolewa na Yeye. Ni wale tu wanaomjua Mungu ndio wanaostahili kumtolea Mungu ushuhuda, na ni wale tu ambao tabia zao zimebadilika ndio wanastahili kumshuhudia Mungu, na Mungu hatamruhusu mwanadamu aliletee jina Lake aibu kwa makusudi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu

Je, sasa unaelewa hukumu ni nini na ukweli ni nini? Ikiwa umeelewa, basi Nakusihi ujisalimishe kwa hukumu kwa utii, la sivyo hutapata kamwe fursa ya kusifiwa na Mungu au kupelekwa na Mungu katika ufalme Wake. Wale wanaokubali hukumu pekee yake lakini hawawezi kamwe kutakaswa, yaani, wale wanaotoroka wakati kazi ya hukumu inapoendelea, watachukiwa na kukataliwa na Mungu milele. Dhambi zao ni nyingi zaidi, na za kusikitisha zaidi, kuliko zile za Mafarisayo, kwa maana wamemsaliti Mungu na ni waasi dhidi ya Mungu. Wanadamu wa aina hii wasiostahili hata kufanya huduma watapokea adhabu kali zaidi, aidha adhabu inayodumu milele. Mungu hatamsamehe msaliti yeyote ambaye kwa wakati mmoja alidhihirisha uaminifu kwa Mungu kwa maneno tu ilhali alimsaliti Mungu. Wanadamu kama hao watapata adhabu ya malipo kupitia adhabu ya roho, nafsi, na mwili. Je, huu si ufichuzi wa tabia yenye haki ya Mungu? Je, hili silo kusudi la Mungu katika kumhukumu mwanadamu na kumfichua mwanadamu? Wakati wa hukumu, Mungu huwapeleka wote wanaofanya aina zote za uovu mahali palipojaa roho waovu, Akiacha miili yao ya nyama iharibiwe vile wapendavyo roho hao waovu. Miili yao inatoa harufu mbaya ya maiti, na adhabu kama hiyo ndiyo inayowafaa. Mungu huandika kwenye vitabu vyao vya kumbukumbu kila mojawapo ya dhambi za waumini hawa wanafiki wasio waaminifu, mitume wanafiki, na wafanyakazi bandia; kisha, wakati unapowadia, Anawatupa katikati ya roho wachafu, Akiacha miili yao ichafuliwe na roho hao wachafu wanavyopenda, na matokeo yake ni kwamba hawatawahi kamwe kuzaliwa upya katika miili mipya na hawatauona mwanga kamwe. Wale wanafiki waliotoa huduma wakati mmoja lakini hawawezi kuwa waaminifu mpaka mwisho wanahesabiwa na Mungu miongoni mwa waovu, ili watembee katika baraza la waovu, na kuungana na halaiki ya wasio na mpangilio; mwishowe, Mungu atawaangamiza. Mungu huwatenga na Hawatambui wote ambao hawajawahi kuwa waaminifu kwa Kristo au kuweka juhudi yoyote, na Atawaangamiza wote wakati wa mabadiliko ya enzi. Hawatakuwepo tena duniani, sembuse kupata njia ya kuingia katika ufalme wa Mungu. Wale ambao hawajawahi kuwa wa kweli kwa Mungu lakini wamelazimishwa na hali kumshughulikia Mungu kwa uzembe wanahesabiwa miongoni mwa wale wanaotoa huduma kwa watu wa Mungu. Ni idadi ndogo tu ya wanadamu wa aina hii ndio wanaweza kuendelea kuishi, huku wengi wao wataangamia pamoja na wasiohitimu hata kufanya huduma. Hatimaye, Mungu ataleta kwenye ufalme Wake wale wote walio na mawazo kama Yake, watu na wana wa Mungu na vilevile waliojaaliwa na Mungu kuwa makuhani. Hili ndilo tone Analopata Mungu kutokana na kazi Yake. Na kwa wale wasio katika sehemu zozote zilizotengwa na Mungu, watahesabiwa miongoni mwa wasioamini. Na kwa hakika mnaweza kuwaza jinsi hatima yao itakavyokuwa. Tayari Nimewaambia yote Ninayopaswa kusema; njia mnayochagua itakuwa uamuzi wenu kufanya. Mnachopaswa kuelewa ni hiki: Kazi ya Mungu kamwe haimsubiri mtu yeyote asiyeweza kwenda sambamba na hatua za Mungu, na tabia ya Mungu ya haki haimwonyeshi mwanadamu yeyote huruma.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli

Wakati mataifa na watu wa dunia watakaporudi mbele ya kiti Changu cha enzi, basi Nitachukua fadhila ya mbinguni na kuiweka kwa sababu ya ulimwengu wa binadamu, ili, kwa mujibu Wangu, itajazwa na fadhila isiyo ya kufananisha. Lakini ulimwengu wa kitambo ukiendelea kuwepo, Nitavurumisha hasira Yangu kwa mataifa yake, Nikieneza amri Zangu za utawala katika ulimwengu mzima, na kuleta kuadibu kwa yeyote anayezikiuka:

Ninapozungumza na ulimwengu mzima, watu wote huisikia sauti Yangu, yaani, watu wote huona matendo yote ambayo Nimetekeleza katika ulimwengu mzima. Wale wanaokwenda kinyume na nia Zangu, yaani, wanaonipinga kwa matendo ya mwanadamu, wataanguka chini katikati ya kuadibu Kwangu. Nitazifanya upya halaiki ya nyota mbinguni; kwa nguvu Yangu, jua na mwezi vitafanywa upya, mbingu hazitakuwa kama zilivyokuwa; na vitu vyote duniani vitafanywa upya—haya yote yatatimia kwa sababu ya maneno Yangu. Nchi zote ulimwenguni zitagawanywa upya na nafasi yake kuchukuliwa na ufalme Wangu, ili kwamba nchi zilizo duniani zitatoweka milele, na kutakuwepo na ufalme unaoniabudu Mimi tu; nchi zote za dunia zitaangamizwa na zitatoweka. Kati ya wanadamu walio ulimwenguni, wale wote ambao ni wa mashetani wataangamizwa. Wote wanaomwabudu Shetani wataanguka chini katikati ya moto Wangu unaochoma—yaani, kando na wale walio ndani ya mkondo, wote watageuka kuwa majivu. Ninapowaadibu kila watu, jamii za kidini, kwa viwango tofauti, zitarudi katika ufalme Wangu, na kushindwa kupitia kwa matendo Yangu, kwa sababu watakuwa wameona kwamba “Mtakatifu aliye juu ya wingu jeupe” tayari Amewasili. Watu wote wataainishwa kulingana na aina zao, na watapata kuadibu mbalimbali kulingana na matendo yao; wale wote walionipinga Mimi wataangamia, na kwa wale ambao matendo yao duniani hayajanihusisha Mimi, kwa sababu ya jinsi walivyotenda, wataendelea kuwepo duniani chini ya utawala wa wana Wangu na watu Wangu. Nitazionekania nchi zisizohesabika na watu wasiohesabika, na Nitaionyesha sauti Yangu mwenyewe duniani, Nikitangaza kukamilika kwa kazi Yangu kuu, nikiwaruhusu watu wote waone hili kwa macho yao wenyewe.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 26

Wanaoweza kusimama imara wakati wa kazi ya Mungu ya hukumu na kuadibu siku za mwisho—yaani, wakati wa kazi ya mwisho ya utakaso—watakuwa wale watakaoingia katika raha ya mwisho na Mungu; kwa hivyo, wanaoingia rahani wote watakuwa wametoka katika ushawishi wa shetani na kupokewa na Mungu baada tu ya kupitia kazi Yake ya mwisho ya utakaso. Hawa watu ambao hatimaye wamepokewa na Mungu wataingia katika raha ya mwisho. Sababu ya kazi ya Mungu ya kuadibu na hukumu katika kiini ni ili kuwatakasa binadamu kwa ajili ya pumziko la mwisho; bila utakaso wa aina hii, hakuna binadamu yeyote angeainishwa katika makundi tofauti kulingana na aina yake ama kuingia katika pumziko. Hii kazi ni njia ya pekee ya binadamu kuingia rahani.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja

Iliyotangulia: 4. Kusudi na Umuhimu wa Kazi ya Mungu katika Enzi ya Neema

Inayofuata: 6. Uhusiano Kati ya Kila Mojawapo ya Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp