23. Kusudi la Kazi ya Usimamizi wa Mungu Ni Kumwokoa Binadamu
Ⅰ
Upendo na huruma ya Mungu
vinapenyeza kazi Yake ya usimamizi
kutoka kipengele cha kwanza hadi cha mwisho.
Ⅱ
Kama mwanadamu anahisi mapenzi Yake ya ukarimu au la,
Yeye hachoki katika kufuatilia kazi anayohitaji kufanya.
Kama mwanadamu anaelewa usimamizi Wake ama haelewi,
kazi ya Mungu inaleta usaidizi na utoaji ambao unaweza kuhisiwa na wote.
Upendo na huruma ya Mungu
vinapenyeza kazi Yake ya usimamizi
kutoka kipengele cha kwanza hadi cha mwisho.
Ⅲ
Pengine leo huhisi upendo na uzima ambavyo Mungu anatoa,
lakini bora tu usitoke upande Wake,
wala kutoacha ridhaa yako ya kutafuta ukweli,
siku moja, hakika, utaona tabasamu la Mungu.
Kwani kusudi la Mungu katika kazi Yake ya usimamizi
ni kumtoa binadamu kutoka kwa utawala wa Shetani,
na kutowaacha wale ambao wamepotoshwa na Shetani,
na kupinga mapenzi Yake.
Upendo na huruma ya Mungu
vinapenyeza kazi Yake ya usimamizi
kutoka kipengele cha kwanza hadi cha mwisho.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili