Nyongeza: Sura ya 2

Watu wanapomwona Mungu wa vitendo, wanapoishi maisha yao binafsi na, wanapotembea sako kwa bako na, na wanapoishi na Mungu Mwenyewe, wao huweka kando udadisi ambao umekuwa ndani ya mioyo yao kwa miaka mingi sana. Ufahamu wa Mungu uliozungumziwa awali ni hatua ya kwanza tu; ingawa watu wana ufahamu wa Mungu, bado kuna mashaka mengi ya kuchagiza ndani ya mioyo yao: Mungu alitoka wapi? Je, Mungu hula? Mungu yuko tofauti sana na watu wa kawaida? Kwa Mungu, kushughulikia watu wote ni jambo la uhakika, kazi rahisi tu? Je, yote yanayonenwa kutoka kwa kinywa cha Mungu ni siri za mbinguni? Je, yote Asemayo ni makubwa zaidi kuliko yale ya viumbe vyote vilivyoumbwa? Je, nuru hung’aa kutoka kwa macho ya Mungu? Na kadhalika—dhana za watu zinaweza kufanya hili. Mambo haya ndiyo mnayopaswa kuelewa na kuingia ndani kabla ya mengine yote. Katika dhana za watu, Mungu aliyepata mwili bado ni Mungu asiye dhahiri. Isingekuwa kupitia kwa ufahamu wa vitendo, watu wasingeweza kamwe kunielewa, na wasingeona kamwe matendo Yangu katika uzoefu wao. Ni kwa sababu tu Nilipata mwili ndiyo maana watu “hawawezi kuelewa” mapenzi Yangu. Kama Singekuwa Nimepata mwili, na Ningekuwa bado mbinguni, bado katika ulimwengu wa kiroho, basi watu “wangenijua,” wangeinama na kuniabudu, na wangezungumza kuhusu wao “kunifahamu” kupitia kwa uzoefu wao—lakini ufahamu kama huo ungekuwa na maana gani? Thamani yake kama kumbukumbu ingekuwa gani? Je, ufahamu unaotokana na dhana za watu ungekuwa halisi? Sitaki ufahamu wa akili za watu—Nataka ufahamu wa vitendo.

Mapenzi Yangu hufichuliwa miongoni mwenu nyakati zote, na nyakati zote huwa kuna mwangaza Wangu na kupata nuru. Na Ninapotenda moja kwa moja katika uungu, halichujwi kupitia kwa akili, hakuna haja ya kuongeza “viungo”—hili ni tendo nyoofu la uungu. Watu wanaweza kufanya nini? Je, yote tangu wakati wa uumbaji mpaka leo hayajatekelezwa binafsi na Mimi? Wakati uliopita, Nilizungumza kuhusu Roho aliyeongezwa nguvu mara saba, lakini hakuna mtu aliyeweza kufahamu kiini Chake—hata walipokijua, hawakuweza kufahamu kabisa. Wakati ambapo Nafanya kazi katika ubinadamu kwa kuongozwa na uungu, kwa kuwa kazi hii inatekelezwa katika hali ambazo watu wanaamini si za mwujiza bali za kawaida, inatajwa kuwa kazi ya Roho Mtakatifu. Ninapofanya kazi moja kwa moja katika uungu, kwa vile Sizuiwi na dhana za watu, na Sipaswi kutii mipaka ya “mwujiza” katika dhana zao, kazi hii ina matokeo ya mara moja, inaelekea kwa kiini cha jambo, inagonga ndipo. Kutokana na hilo, hatua hii ya kazi ni takatifu zaidi, ni ya haraka mara mbili, ufahamu wa watu umechapuka, na maneno Yangu yanaongezeka, kusababisha watu wote kuharakisha kuyafikia. Kwa kuwa matokeo ni tofauti, kwa kuwa njia, asili, na maudhui ya kazi Yangu si sawa—na, zaidi ya hayo, kwa kuwa Nimeanza kufanya kazi rasmi katika mwili, kwa kuzingatia yaliyotangulia, hatua hii ya kazi inatajwa kama kazi ya Roho aliyeongezwa nguvu mara saba. Si kitu dhahania. Kufuatia maendeleo katika njia ambayo kwayo Nafanya kazi ndani yenu, na kufuatia majilio ya ufalme, Roho aliyeongezwa nguvu mara saba anaanza kufanya kazi, na kazi hii daima hupanuka zaidi na kuwa na nguvu zaidi. Watu wote wanapomwona Mungu na wote waone kwamba Roho wa Mungu yuko miongoni mwa wanadamu, umuhimu kamili wa kupata mwili Kwangu huwa dhahiri. Hakuna haja ya kufupisha—watu wanalijua hili kwa kawaida.

Kuzingatia hali nyingi—mbinu ambazo kwazo Nafanya kazi, hatua za kazi Yangu, sauti ya maneno Yangu leo, na kadhalika—yanayotoka kinywani Mwangu sasa pekee ndiyo “matamko ya Roho saba” Katika hali ya kweli. Ingawa Nilizungumza pia wakati uliopita, huo ulikuwa wakati wa hatua ya ujenzi wa kanisa. Lilikuwa kama dibaji na faharasa katika riwaya—halikuwa na kiini; ni matamko ya leo pekee ndiyo yanaweza kuitwa kiini cha matamko ya Roho saba. “Matamko ya Roho saba” yanahusu matamko yanayotoka kwa kiti cha enzi, ambalo ni kusema, yanatamkwa moja kwa moja katika uungu. Wakati ambapo matamko Yangu yaligeuka kufichua siri za mbinguni ulikuwa wakati ambapo Nilizungumza moja kwa moja katika uungu. Kwa maneno mengine, bila kuzuiwa na ubinadamu, Nilifichua moja kwa moja siri na hali zote za ulimwengu wa kiroho. Kwa nini Nasema kwamba hapo awali Nilipaswa kutii mipaka ya ubinadamu? Hili linahitaji ufafanuzi. Machoni pa watu, hakuna mtu anayeweza kufichua siri za mbinguni; isingekuwa Mungu Mwenyewe, hakuna mtu mwingine duniani angeweza kujua siri hizi. Hivyo, Nazungumzia dhana za watu na Nasema kwamba zamani Sikufichua siri zozote kwa sababu Nilipaswa kutii mipaka ya ubinadamu. Kwa ubayana zaidi, hata hivyo, huu si ukweli: Maudhui ya maneno Yangu hutofautiana kama vile kazi Yangu hutofautiana, na hivyo, wakati ambapo Nilianza kutekeleza huduma Yangu katika uungu, Nilifichua siri; zamani, ilinibidi Nifanye kazi katika hali ambazo watu wote waliziona kuwa kawaida, na maneno Niliyonena yalikuwa na uwezo wa kutimizwa katika dhana za watu. Nilipoanza kufichua siri, hakuna hata moja ya hizi iliyofikiwa na dhana za watu—hazikuwa kama fikira za binadamu. Kwa hiyo, Nilianza rasmi kugeukia unenaji katika uungu, na haya yalikuwa matamko ya Roho saba katika hali ya kweli. Ingawa maneno ya zamani yalikuwa matamko kutoka kwa kiti cha enzi, yalinenwa kwa msingi wa kile kilichoweza kufikiwa na watu, na hivyo hayakutamkwa moja kwa moja katika uungu—kwa sababu hiyo hayakuwa matamko ya Roho saba katika hali ya kweli.

Iliyotangulia: Sura ya 11

Inayofuata: Sura ya 12

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp