Kiambatisho 2: Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote

Kama washiriki wa jamii ya binadamu na Wakristo wamchao Mungu, ni jukumu na wajibu wa sisi wote kutoa akili na mwili wetu kwa kutimiza agizo la Mungu, kwani uhai wetu wote ulitoka kwa Mungu, na upo kwa sababu ya ukuu wa Mungu. Kama akili zetu na miili yetu si kwa ajili ya agizo la Mungu na si kwa sababu ya kusudi la haki la mwanadamu, basi nafsi zetu hazina thamani kwa wale waliokufa kishahidi kwa ajili ya agizo la Mungu, na thamani ndogo zaidi kwa Mungu, aliyetupa kila kitu.

Mungu aliumba dunia hii, Aliumba mwanadamu huyu, na zaidi ya hayo Alikuwa muasisi wa utamaduni wa zamani wa Giriki na ustaarabu wa binadamu. Ni Mungu tu anayemfariji huyu mwanadamu, na ni Mungu tu anayemtunza mwanadamu huyu usiku na mchana. Ukuaji na maendeleo ya binadamu hayatengani na ukuu wa Mungu, na historia na mustakabali wa mwanadamu ni zisizochangulika kutoka kwa miundo ya Mungu. Kama wewe ni Mkristo wa kweli, basi hakika utaamini kwamba kupanda na kushuka kwa nchi ama taifa lolote hufanyika kulingana na miundo ya Mungu. Mungu pekee hujua majaliwa ya nchi ama taifa, na Mungu pekee hudhibiti mwendo wa huyu mwanadamu. Iwapo mwanadamu anataka kuwa na majaliwa mazuri, iwapo nchi inataka kuwa na majaliwa mazuri, basi lazima mwanadamu ampigie Mungu magoti kwa ibada, atubu na kukiri mbele ya Mungu, la sivyo majaliwa na hatima ya mwanadamu hayataepuka kumalizika kwa janga.

Angalia nyuma wakati wa safina ya Nuhu: Wanadamu walikuwa wapotovu sana, walikuwa wamepotea kutoka katika baraka za Mungu, hawakuwa wanatunzwa na Mungu tena, na walikuwa wamepoteza ahadi za Mungu. Waliishi gizani, bila mwangaza wa Mungu. Hivyo wakawa waasherati kwa asili, wakajiachilia katika mkengeuko wa kutisha. Watu kama hao hawangeweza tena kupokea ahadi za Mungu; hawakufaa kushuhudia uso wa Mungu, wala kusikia sauti ya Mungu, kwani walikuwa wamemwacha Mungu, kuweka kando yote Aliyowapa, na kusahau mafunzo ya Mungu. Mioyo yao ilipotea mbali zaidi na zaidi na Mungu, na ilivyofanya hivyo, wakawa wapotovu zaidi ya mantiki na ubinadamu wote na wakazidi kuwa waovu. Hivyo walikaribia kifo zaidi, na kukabiliwa na ghadhabu na adhabu ya Mungu. Ni Nuhu tu aliyemwabudu Mungu na kuepukana na uovu, na hivyo aliweza kusikia sauti ya Mungu, na kusikia maelekezo ya Mungu. Alijenga safina kulingana na maelekezo ya neno la Mungu, na kukusanya aina yote ya viumbe hai. Na kwa njia hii, wakati kila kitu kilikuwa kimetayarishwa, Mungu aliangamiza dunia. Nuhu tu na wanachama saba wa familia yake walinusurika maangamizi, kwani Nuhu alimwabudu Yehova na kuepukana na uovu.

Kisha angalia enzi ya sasa: Hawa watu wenye haki kama Nuhu, ambao wangeweza kumwabudu Mungu na kuepuka uovu, wamekoma kuwepo. Lakini bado Mungu ana fadhili kwa mwanadamu huyu, na Anamsamehe mwanadamu wakati huu wa enzi ya mwisho. Mungu anawatafuta wanaomtaka Yeye ajitokeze. Anawatafuta wale wanaoweza kuyasikia maneno Yake, wale ambao hawajasahau agizo Lake na wanatoa mioyo na miili yao Kwake. Anawatafuta wale walio watiifu kama watoto wachanga mbele Yake, na hawampingi. Kama hujazuiliwa na nguvu zozote katika ibada yako Kwake, basi Mungu atakutazama na neema, na kukupea baraka Zake. Kama wewe ni wa daraja la juu, wa sifa ya heshima, aliyemiliki maarifa mengi, mmiliki wa mali nyingi, na kuungwa mkono na watu wengi, lakini mambo haya hayakuzuii kuja mbele za Mungu kuukubali wito Wake na agizo Lake, kufanya kile Mungu anachokuambia ufanye, basi yote unayoyafanya yatakuwa yenye umuhimu zaidi duniani na yenye haki zaidi ya binadamu. Ukiukataa wito wa Mungu kwa sababu ya hadhi yako na malengo yako mwenyewe, yote utakayoyafanya yatalaaniwa na hata kudharauliwa na Mungu. Labda wewe ni rais, ama mwanasayansi, ama mchungaji, ama mzee, lakini bila kujali ukuu wa ofisi yako, ukitegemea maarifa yako na uwezo katika shughuli zako, basi daima utakuwa wa kushindwa na kamwe utanyimwa baraka za Mungu, kwa sababu Mungu hakubali chochote unachofanya, na Hakubali kwamba kazi yako ni yenye haki, wala kukubali kwamba unafanya kazi kwa msaada wa mwanadamu. Atasema yote unayofanya, ni ya kutumia maarifa na nguvu za mwanadamu kumvulia mwanadamu ulinzi wa Mungu na kumnyima baraka za Mungu. Atasema kuwa unamwongoza mwanadamu kuelekea gizani, kuelekea kifo, na kuelekea mwanzo wa kuwepo bila mipaka ambapo mwanadamu amempoteza Mungu na baraka Zake.

Kutoka wakati mwanadamu kwanza alikuwa na sayansi ya jamii, akili yake ilishughulishwa na sayansi na maarifa. Kisha sayansi na maarifa vikawa vyombo vya kutawala mwanadamu, na hapakuwa tena na nafasi ya kutosha kumwabudu Mungu, na hapakuwa tena na mazingira mazuri ya kumwabudu Mungu. Nafasi ya Mungu ikashuka hata chini zaidi moyoni mwa mwanadamu. Dunia moyoni mwa mwanadamu bila nafasi ya Mungu ni giza, tupu bila matumaini. Na hivyo kukatokea wanasayansi wa jamii, wataalamu wa historia na wanasiasa wengi kueleza nadharia ya sayansi ya jamii, nadharia ya mageuko ya binadamu, na nadharia nyingine zinazopinga ukweli kwamba Mungu alimuumba mwanadamu, kujaza moyo na akili ya mwanadamu. Na kwa njia hii, wanaoamini kwamba Mungu aliumba kila kitu wanakuwa wachache zaidi, na wale wanaoamini nadharia ya mageuko wanakuwa hata wengi kwa nambari. Watu zaidi wanachukulia rekodi za kazi ya Mungu na maneno Yake wakati wa enzi ya Agano la Kale kuwa hadithi na hekaya. Kwa mioyo yao, watu wanakuwa wasiojali heshima na ukubwa wa Mungu, kwa imani kwamba Mungu yupo na anatawala kila kitu. Kusalia kwa mwanadamu na majaliwa ya nchi na mataifa si muhimu kwao tena. Mwanadamu anaishi katika dunia tupu akijishughulisha tu na kula, kunywa, na ufuatiliaji wa furaha. … Watu wachache wanashughulika kutafuta Afanyapo Mungu kazi Yake leo, ama kutafuta jinsi Anavyoongoza na kupanga majaliwa ya mwanadamu. Na kwa njia hii, ustaarabu wa ubinadamu bila fahamu ukawa huwezi kukutana na matakwa ya mwanadamu hata zaidi, na hata kuna watu zaidi wanaohisi kwamba, kuishi kwa dunia kama hii, wanayo furaha ya chini kuliko watu walioenda. Hata watu wa nchi zilizokuwa na ustaarabu wa juu wanaeleza malalamiko haya. Kwani bila mwongozo wa Mungu, bila kujali jinsi viongozi na wanasosiolojia wanatafakari kuhifadhi ustaarabu wa binadamu, haina mafanikio. Hakuna anayeweza kujaza utupu kwa moyo wa mwanadamu, kwani hakuna anayeweza kuwa uhai wa mwanadamu, na hakuna nadharia ya kijamii inayoweza kumwokoa kutokana na utupu unaomtesa. Sayansi, maarifa, uhuru, demokrasia, wasaa wa mapumziko, faraja, haya yote ni mapumziko ya muda, Hata na mambo haya, mwanadamu hataepuka kufanya dhambi na kuomboleza udhalimu wa jamii. Mambo haya hayawezi kupunguza tamaa ya mwanadamu na hamu ya kuchunguza. Kwa sababu mwanadamu aliumbwa na Mungu na kafara na uchunguzi usio na sababu wa mwanadamu vitamwongoza tu kwa dhiki zaidi. Mwanadamu daima atakuwa katika hali ya hofu isiyoisha, hatajua jinsi ya kuukabili mustakabali wa wanadamu, ama jinsi ya kuikabili njia iliyo mbele. Mwanadamu atakuja hata kuogopa sayansi na elimu, na kuhofia hata zaidi utupu ulio ndani yake sana. Duniani humu, bila kujali kama unaishi katika nchi huru ama isiyo na haki za binadamu, huwezi kabisa kuponyoka majaliwa ya mwanadamu. Kama wewe ni kiongozi ama anayeongozwa, huwezi kabisa kuponyoka hamu ya kuchunguza majaliwa, siri na majaliwa ya mwanadamu. Chini ya hayo, huna uwezo wa kutoroka hisia ya utupu inayotatiza. Matukio kama haya, yaliyo kawaida kwa wanadamu wote, yanaitwa matukio ya kijamii na wanasosiolojia, lakini hakuna mtu mkubwa anayeweza kuja mbele kutatua shida kama hizi. Mwanadamu, hata hivyo, ni mwanadamu. Nafasi na maisha ya Mungu hayawezi kubadilishwa na mwanadamu yeyote. Mwanadamu hahitaji tu jamii iliyo na haki, ambapo kila mtu analishwa vyema na ana uhuru na usawa, lakini wokovu wa Mungu na Yeye kuwapa uhai. Wakati tu mwanadamu atapokea wokovu wa Mungu na kupatiwa uhai na Yeye ndipo mahitaji, hamu ya kuchunguza, na utupu wa kiroho wa mwanadamu utaweza kutatuliwa. Iwapo watu wa nchi ama taifa hawawezi kupokea wokovu na utunzaji wa Mungu, basi nchi ama taifa kama hilo litatembelea njia inayoelekea uharibifuni, inayoelekea gizani, na litaangamizwa na Mungu.

Labda nchi yako inafanikiwa sasa, lakini ukiruhusu watu wako kupotea kutoka kwa Mungu, basi nchi yako itazidi kujipata bila baraka za Mungu. Ustaarabu wa nchi yako utazidi kukanyagiwa chini, na kabla ya muda mrefu watu watamwasi Mungu na kulaani Mbingu. Na hivyo, bila kujulikana kwa mwanadamu, majaliwa ya nchi yataletwa kwa uharibifu. Mungu ataziinua nchi zenye nguvu ili kukabiliana na nchi hizo zilizolaaniwa na Mungu, na anaweza hata kuzifuta kutoka uso wa dunia. Kupanda na kushuka kwa nchi ama taifa kunategemea kama viongozi wao wanamwabudu Mungu, na kama wanawaongoza watu wao karibu na Mungu na kumwabudu. Lakini, kwa hii enzi ya mwisho, kwa sababu wale wanaomtafuta Mungu kwa kweli na kumwabudu wanazidi kuwa wachache, Mungu anaweka fadhili ya pekee juu ya nchi ambapo Ukristo ni dini ya serikali. Anazikusanya pamoja kuunda kambi ya haki kiasi ya dunia, wakati nchi zikanazo Mungu ama zile zisizomwabudu Mungu wa kweli zinakuwa wapinzani wa kambi ya haki. Kwa njia hii, Mungu hana tu mahali miongoni mwa wanadamu pa kufanyia kazi Yake, lakini pia Anapata nchi zinazoweza kutumia mamlaka ya haki, ili kulazimisha mipaka na vikwazo kwa nchi hizo zinazompinga Mungu. Lakini licha ya hayo, bado hakuna watu zaidi wanaokuja mbele kumwabudu Mungu, kwa sababu mwanadamu amepotea mbali sana kutoka Kwake, na Mungu hajakuwa kwa mawazo ya mwanadamu kwa muda mrefu. Kunabakia tu duniani nchi zinazotumia haki na kupinga udhalimu. Lakini hii ni mbali na matakwa ya Mungu, kwani hakuna kiongozi wa nchi yoyote atamruhusu Mungu kuongoza watu wake, na hakuna chama cha kisiasa kitakachokusanya pamoja watu wake kumwabudu Mungu; Mungu amepoteza mahala Pake halali kwa mioyo ya nchi zote, taifa, chama tawala, na hata kwa moyo wa kila mtu. Ingawa nguvu za haki ziko kwa dunia hii, utawala ambapo Mungu hana mahali kwa moyo wa mwanadamu ni dhaifu. Bila baraka ya Mungu, uwanja wa kisiasa utaanguka katika vurugu na wenye kuweza kudhuriwa na mashambulizi. Kwa mwanadamu, kuwa bila baraka ya Mungu ni kama kuwa bila jua. Bila kujali jinsi viongozi wanafanya mchango kwa watu wao kwa uangalifu, bila kujali idadi ya mikutano ya haki wanadamu wanafanya pamoja, hakuna kati ya hii itakayorejesha mambo ama kubadilisha majaliwa ya mwanadamu. Mwanadamu anaamini kuwa nchi ambapo watu wanalishwa na kuvalishwa nguo, ambapo watu wanaishi kwa amani, ni nchi nzuri, na iliyo na uongozi mzuri. Lakini Mungu hafikirii hivyo. Anaamini kuwa nchi ambapo hakuna mtu anayemwabudu ndiyo Atakayoiangamiza. Njia ya mwanadamu ya kufikiria ni tofauti kabisa na ya Mungu. Kwa hiyvo, kama mkuu wa nchi hamwabudu Mungu, basi majaliwa ya nchi hii itakuwa ya kutisha, na nchi haitakuwa na majaliwa.

Mungu hashiriki katika siasa za mwanadamu, lakini majaliwa ya nchi ama taifa inadhibitiwa na Mungu, Mungu anadhibiti dunia hii na ulimwengu mzima. Majaliwa ya mwanadamu na mpango wa Mungu yanashikamana kwa undani, na hakuna mwanadamu, nchi ama taifa limetolewa kwa mamlaka ya Mungu. Iwapo mwanadamu anatamani kujua majaliwa yake, basi lazima aje mbele ya Mungu. Mungu atawafanya wanaomfuata na kumwabudu kufanikiwa, na Atashusha na kuwaangamiza wale wanaompinga na kumkataa.

Kumbuka tukio katika Biblia ambapo Mungu aliangamiza Sodoma, na fikiria pia jinsi mke wa Lutu alivyokuwa nguzo ya chumvi. Fikiria nyuma jinsi watu wa Ninawi walitubu dhambi zao kwa gunia na majivu, na kumbuka kilichofuata baada ya Wayahudi kumsulubisha Yesu miaka 2,000 iliyopita. Wayahudi walitolewa Israeli na kukimbilia nchi duniani kote. Wengi waliuwawa, na taifa lote la Kiyahudi lilikabiliwa na uharibifu wa kipekee. Walimsulubisha Mungu—wakafanya uhalifu wa kuchukiza—na kuchochea tabia ya Mungu. Walifanywa kulipa kwa ajili ya walichofanya, walifanywa kukubali matokeo ya vitendo vyao. Walimlaani Mungu, walimkataa Mungu, na hivyo walikuwa na majaliwa moja pekee: kuadhibiwa na Mungu. Haya ndiyo matokeo machungu na maafa ambayo viongozi wao waliletea nchi na taifa lao.

Leo, Mungu amerudi duniani kufanya kazi Yake. Atasimama kwanza kwa mkutano mkubwa wa viongozi madikteta: Uchina, ngome kali ya ukanaji Mungu. Mungu amepata kundi la watu kwa hekima na nguvu Zake. Wakati huu, Anawindwa na chama tawala cha Uchina kwa kila namna na kukabiliwa na mateso makubwa, bila mahala pa kupumzisha kichwa Chake na kutoweza kupata makazi. Licha ya haya, Mungu bado anaendelea kufanya kazi Aliyonuia kufanya: Anatamka sauti Yake na kueneza injili. Hakuna anayeweza kuelewa uweza wa Mungu. Uchina, nchi inayomchukulia Mungu kama adui, Mungu hajawahi kukoma kazi Yake. Badala yake, watu zaidi wamekubali kazi na neno Lake, kwani Mungu anafanya yote Awezayo kuokoa kila mshiriki wa ubinadamu. Tunaamini hakuna nchi ama nguvu inayoweza kuzuia yale anayotaka kutimiza Mungu. Wale wanaozuia kazi ya Mungu, wanaopinga neno la Mungu, kuvuruga na kudhoofisha mpango wa Mungu hatimaye wataadhibiwa na Mungu. Anayeasi kazi ya Mungu atatumwa kuzimu; nchi yoyote inayoasi kazi ya Mungu itaangamizwa; taifa lolote linaloinuka kupinga kazi ya Mungu litafutwa kutoka dunia hii, na litakoma kuwepo. Nahimiza watu wa mataifa, nchi na hata viwanda vyote kusikiza sauti ya Mungu, kutazama kazi ya Mungu, kuzingatia majaliwa ya mwanadamu, hivyo kumfanya Mungu kuwa mtakatifu zaidi, wa heshima zaidi, wa juu zaidi na chombo cha pekee cha kuabudu miongoni mwa wanadamu, na kuruhusu wanadamu wote kuishi chini ya baraka za Mungu, kama tu ukoo wa Ibrahimu ulivyoishi chini ya ahadi ya Yehova, na kama tu Adamu na Hawa, walioumbwa awali na Mungu, walivyoishi kwa Bustani ya Edeni.

Kazi ya Mungu ni kama mawimbi yanayotapakaa kwa nguvu. Hakuna anayeweza kumweka kizuizini, na hakuna anayeweza kusimamisha nyayo Zake. Wale tu wanaosikiza maneno Yake kwa makini, na wanaomtafuta na kuwa na kiu naye, wanaweza kufuata nyayo Zake na kupokea ahadi Zake. Wasiofanya hivyo watakabiliwa na maafa makuu na adhabu inayostahili.

Iliyotangulia: Kiambatisho 1: Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya

Inayofuata: Kiambatisho 3: Mwanadamu Anaweza tu Kuokolewa Katikati ya Usimamizi wa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp