Utangulizi

Katika Enzi ya Ufalme, Mungu hutumia maneno kuikaribisha enzi mpya, kubadilisha njia ambayo kwayo Yeye hufanya kazi, na kufanya kazi ya enzi nzima. Hii ndiyo kanuni ambayo kwayo Mungu hufanya kazi katika Enzi ya Neno. Alikuwa mwili ili Anene kutoka katika mitazamo tofauti, ili mwanadamu aweze kumwona Mungu kweli, ambaye ni Neno kuonekana katika mwili, na angeweza kuona hekima na ajabu Yake. Kazi kama hiyo inafanywa ili kufikia malengo ya kumshinda mwanadamu, kumkamilisha mwanadamu, na kumwondoa mwanadamu vyema zaidi, ambayo ndiyo maana ya kweli ya matumizi ya maneno kufanya kazi katika Enzi ya Neno. Kupitia katika maneno haya, watu huja kuijua kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, kiini cha mwanadamu, na kile ambacho mwanadamu anapaswa kuingia katika. Kupitia katika maneno, kazi ambayo Mungu anataka kufanya katika Enzi ya Neno inafanikiwa kwa ukamilifu. Kupitia katika maneno haya, watu wanafunuliwa, kuondolewa, na kujaribiwa. Watu wameyaona maneno ya Mungu, kuyasikia maneno haya, na kutambua uwepo wa maneno haya. Kama matokeo, wameamini katika uwepo wa Mungu, katika kudura na hekima ya Mungu, na pia katika upendo wa Mungu kwa mwanadamu na tamanio Lake la kumwokoa mwanadamu. Neno "maneno" linaweza kuwa rahisi na la kawaida, lakini maneno yanayonenwa kutoka katika kinywa cha Mungu mwenye mwili yanautikisa ulimwengu, kuibadilisha mioyo ya watu, kubadilisha fikira zao na tabia zao za zamani, na kubadilisha jinsi ambavyo ulimwengu wote ulikuwa ukionekana. Katika enzi zote, ni Mungu wa leo tu ndiye Aliyefanya kazi kwa njia hii, na ni Yeye Anayezungumza kwa namna hii na kuja kumwokoa mwanadamu hivi. Kuanzia wakati huu na kuendelea, mwanadamu anaishi chini ya mwongozo wa maneno ya Mungu, akichungwa na kuruzukiwa na maneno Yake. Watu wanaishi katika ulimwengu wa maneno ya Mungu, kati ya laana na baraka za maneno ya Mungu, na kuna hata watu wengi zaidi ambao wamekuja kuishi chini ya hukumu na kuadibu kwa maneno Yake. Maneno haya na kazi hii vyote ni kwa sababu ya wokovu wa mwanadamu, kwa sababu ya kutimiza mapenzi ya Mungu, na kwa sababu ya kubadilisha kuonekana kwa asili kwa ulimwengu wa uumbaji wa zamani. Mungu aliuumba ulimwengu kwa kutumia maneno, Anawaongoza watu ulimwenguni kote kutumia maneno, na Anawashinda na kuwaokoa kutumia maneno. Hatimaye, Atatumia maneno kuutamatisha ulimwengu mzima wa zamani, hivyo kuukamilisha mpango Wake mzima wa usimamizi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Enzi ya Ufalme Ni Enzi ya Neno

Katika enzi hii, na miongoni mwenu, Mungu atatimiza ukweli ufuatao: kwamba kila mtu ataishi kwa kuyadhihirisha maneno ya Mungu, ataweza kuuweka ukweli katika vitendo, na atampenda Mungu kwa dhati; kwamba watu wote watatumia maneno ya Mungu kama msingi na kama uhalisi wao, na watakuwa na mioyo inayomcha Mungu; na kwamba, kupitia kutenda maneno ya Mungu, mwanadamu kisha atashikilia mamlaka ya kifalme pamoja na Mungu. Hii ndiyo kazi inayopaswa kufanikishwa na Mungu. Je, unaweza kuishi bila kusoma maneno ya Mungu? Leo, kuna wengi ambao wanahisi kuwa hawawezi kuishi hata siku moja au mbili bila kusoma maneno Yake. Lazima wayasome maneno Yake kila siku, na ikiwa muda hauruhusu, kuyasikiza kutatosha. Hii ndiyo hisia ambayo Roho Mtakatifu huwapa watu, na ndiyo njia ambayo Anaanza kuwagusa. Yaani, Yeye huwatawala watu kupitia maneno, ili kwamba waweze kuingia katika uhalisi wa maneno ya Mungu. Ikiwa, baada ya siku moja tu bila kula na kunywa maneno ya Mungu, unahisi giza na kiu, na huwezi kustahimili hali hiyo, hili linaonyesha kwamba umeguswa na Roho Mtakatifu, na kwamba Hajakukuacha. Wewe basi, ni mtu aliye kwenye mkondo huu. Hata hivyo, ikiwa baada ya siku moja au mbili bila kula na kunywa maneno ya Mungu, huhisi kitu, ikiwa huna kiu, na hujaguswa hata kidogo, hili linaonyesha kwamba Roho Mtakatifu amekuacha. Hili linamaanisha, basi, kwamba kuna kitu kibaya na hali yako; hujaingia katika Enzi ya Neno, na wewe ni mmoja wa wale ambao wamebaki nyuma. Mungu hutumia maneno kuwatawala watu; unahisi vizuri ukila na kunywa maneno ya Mungu, na usipokula na kunywa maneno ya Mungu, huna njia ya kufuata. Maneno ya Mungu huwa chakula cha watu, na nguvu inayowaendesha. Biblia inasema “Mwanadamu hataishi kwa mkate pekee, lakini kwa kila neno linalotoka kinywani mwa Mungu”. Leo, Mungu ataikamilisha kazi hii, naye Ataukamilisha ukweli huu ndani yenu. Ni vipi kwamba hapo zamani, watu wangeweza kwenda siku nyingi bila kusoma maneno ya Mungu na bado waweze kula na kufanya kazi kama kawaida, lakini hivi sivyo ilivyo leo? Katika enzi hii, Mungu haswa hutumia maneno kutawala vyote. Kupitia katika maneno ya Mungu, mwanadamu anahukumiwa na kukamilishwa, kisha hatimaye kupelekwa katika ufalme. Maneno ya Mungu tu ndiyo yanayoweza kuyaruzuku maisha ya mwanadamu, na ni maneno ya Mungu tu yanayoweza kumpa mwanadamu mwangaza na njia ya kutenda, hasa katika Enzi ya Ufalme. Alimradi hupotei kutoka katika ukweli wa maneno ya Mungu, kula na kunywa maneno Yake kila siku, Mungu ataweza kukufanya mkamilifu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Enzi ya Ufalme Ni Enzi ya Neno

Kotekote katika ulimwengu Ninafanya kazi Yangu, na katika Mashariki, mashambulio ya radi yanapiga bila kukoma, yakiyatingisha mataifa yote na madhehebu. Ni sauti Yangu ndiyo imewaleta watu katika wakati wa sasa. Nitawasababisha watu wote kushindwa na sauti Yangu, kuingia katika mkondo huu, na kunyenyekea mbele Yangu, kwa maana Nilijirudishia utukufu Wangu kutoka duniani kote zamani na Nikautoa upya Mashariki. Ni nani asiyetamani kuuona utukufu Wangu? Ni nani asiyesubiri kwa hamu kurudi Kwangu? Ni nani asiye na kiu cha kuonekana Kwangu tena? Ni nani asiyetamani kuona kupendeza Kwangu? Ni nani hangetaka kuja kwenye nuru? Ni nani hangeuona utajiri wa Kanaani? Ni nani hangoji kwa hamu kurudi kwa Mkombozi? Ni nani asiyempenda kwa dhati Mwenyezi Mkuu? Sauti Yangu itaenea kotekote duniani; Ningependa, kuwazungumzia maneno mengi zaidi wateule wangu, Nikiwatazama. Kama radi yenye nguvu inayotingisha milima na mito, Nanena maneno Yangu kwa ulimwengu wote na kwa wanadamu. Hivyo maneno yaliyo kinywani Mwangu yamekuwa hazina ya mwanadamu, na watu wote wanayahifadhi maneno Yangu kwa upendo mkubwa. Umeme wa radi unaangaza kutoka Mashariki mpaka Magharibi. Maneno Yangu ni kiasi kwamba mwanadamu huchukia kuyaacha na pia huyaona kama yasiyoeleweka, lakini zaidi ya yote mwanadamu huyafurahia. Wanadamu wote wana uchangamfu na furaha, wakisherehekea kuja Kwangu, kana kwamba mtoto mchanga amezaliwa hivi karibuni. Kwa sauti Yangu, nitawaleta wanadamu wote mbele Yangu. Tangu hapo, Nitaingia rasmi katika jamii ya wanadamu ili waje kuniabudu. Kwa utukufu Ninaoutoa na maneno yaliyo kinywani Mwangu, Nitawafanya watu wote kuja mbele Yangu na kuona kwamba umeme unaangaza kutoka Mashariki na kwamba Mimi pia Nimeshuka kwenye “Mlima wa Mizeituni” wa Mashariki. Wataona kwamba Mimi tayari Nimekuwa duniani kwa muda mrefu, sio kama Mwana wa Wayahudi tena lakini kama Umeme wa Mashariki. Kwani Nimeshafufuka kitambo, na Nimeondoka miongoni mwa wanadamu, na kisha Nimeonekana tena miongoni mwa wanadamu Nikiwa na utukufu. Mimi ndiye Niliyeabudiwa enzi nyingi kabla ya wakati huu, na pia Mimi ni “mtoto mchanga” Aliyeachwa na Israeli enzi nyingi kabla ya wakati huu. Zaidi ya hayo, Mimi ndiye Mwenyezi Mungu mwenye utukufu wote wa enzi hii! Hebu wote waje mbele ya kiti Changu cha enzi ili waone uso Wangu mtukufu, wasikie sauti Yangu, na kuangalia matendo Yangu. Huu ndio ukamilifu wa mapenzi Yangu; ni mwisho na kilele cha mpango Wangu, na vilevile madhumuni ya usimamizi Wangu. Hebu kila taifa liniabudu Mimi, kila ulimi unikiri Mimi, kila mtu aniamini Mimi, na watu wote wawe chini Yangu!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ngurumo Saba Zatoa Sauti—Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni

Mungu alisema, hata katika Ufalme wa Milenia watu ni lazima waendelee kufuata matamshi Yake, na katika maisha ya baadaye, matamshi ya Mungu bado yatakuwa yanaongoza maisha ya mwanadamu moja kwa moja kwenda katika nchi ya Kanaani. Musa alipokuwa jangwani, Mungu alimwelekeza na kuzungumza naye moja kwa moja. Kutoka mbinguni Mungu alituma chakula, maji, na mana ili watu waweze kuvifurahia, na leo bado ni hivyo: Mungu mwenyewe ametuma vitu chini kwa ajili ya kula na kunywa ili watu wafurahi, na yeye mwenyewe ametuma laana ili kuwaadibu watu. Na hivyo kila hatua ya kazi Yake inafanywa na Mungu Mwenyewe. Leo, watu wanatamani utokeaji wa kweli, wanajaribu kuona ishara na maajabu, na kuna uwezekano mkubwa watu wa namna hiyo kutelekezwa, maana kazi ya Mungu inazidi kuwa halisi. Hakuna anayejua kwamba Mungu ameshuka kutoka mbinguni, bado hawajui kwamba Mungu ametuma chini chakula na maji ya kutia nguvu kutoka mbinguni, lakini Mungu kimsingi yupo, na mazingira mazuri ya Ufalme wa Milenia ambao watu wanaufikiria pia ni matamshi ya Mungu Mwenyewe. Huu ni ukweli, ni huu tu ndio unaotawala pamoja na Mungu duniani. Kutawala na Mungu duniani kunarejelea mwili. Kile ambacho si cha mwili hakipo duniani, na hivyo wale wote wanaojikita katika kusonga mbele katika mbingu ya tatu wanafanya hivyo bure. Siku moja, ambapo ulimwengu mzima utarudi kwa Mungu, kitovu cha kazi Yake katika ulimwengu wote kitafuata matamko ya Mungu; kwingineko watu watapiga simu, wengine watapanda ndege, wengine watapanda boti na kupita baharini, na wengine watatumia leza kupokea matamshi ya Mungu. Kila mmoja atakuwa anatamani na mwenye shauku, wote watakuja karibu na Mungu, na kukusanyika kwa Mungu, na wote watamwabudu Mungu—na yote haya yatakuwa matendo ya Mungu. Kumbuka hili! Mungu hawezi kuanza tena kwingineko. Mungu atatimiza ukweli huu: Atawafanya watu wote ulimwengu mzima kuja mbele Yake, na kumwabudu Mungu duniani, na kazi Yake katika maeneo mengine itakoma, na watu watalazimishwa kutafuta njia ya kweli. Itakuwa kama Yusufu: Kila mtu alimwendea kwa ajili ya chakula, na kumsujudia, kwa sababu alikuwa na vyakula. Ili kuweza kuepuka njaa watu watalazimishwa kutafuta njia ya kweli. Jumuiya yote ya kidini itapitia njaa kubwa, na ni Mungu tu wa leo ndiye chemchemi ya maji ya uzima, akiwa na kisima chenye maji yasiyokauka kilichotolewa kwa ajili ya furaha ya mwanadamu, na watu watakuja na kumtegemea. Huo ndio utakuwa muda ambapo matendo ya Mungu yatafichuliwa, na Mungu atatukuzwa; watu wote katika ulimwengu wote watakuja na kumwabudu “mtu” asiyekuwa wa kawaida. Je, hii haitakuwa siku ya utukufu wa Mungu? Siku moja, wachungaji wa zamani watatuma ujumbe wakitafuta maji kutoka katika chemchemi za maji ya uzima. Watakuwa wazee, lakini watakuja kumwabudu mtu huyu ambaye walimdharau. Katika vinywa vyao watakiri na katika mioyo yao wataamini—je, hii si ishara na maajabu? Siku ambapo ufalme wote utafurahia ni siku ya utukufu wa Mungu, na mtu yeyote atakayewajia, na kupokea habari njema za Mungu atabarikiwa na Mungu, na nchi hizi na watu hawa watabarikiwa na kulindwa na Mungu. Mwelekeo wa maisha yajayo utakuwa hivi: Wale ambao watapata matamshi kutoka katika kinywa cha Mungu watakuwa na njia ya kutembea duniani, na wawe wafanya biashara au wanasayansi, au waelimishaji au wataalamu wa viwandani, wale ambao hawana maneno ya Mungu watakuwa na wakati mgumu wa kuchukua hata hatua moja, na watalazimishwa kutafuta njia ya kweli. Hiki ndicho kinamaanishwa na, “Ukiwa na ukweli utatembea ulimwengu mzima; bila ukweli, hutafika popote.” Ukweli ni huu: Mungu atatumia Njia (ikiwa na maana kwamba maneno Yake yote) kuuamuru ulimwengu wote na kumwongoza na kumshinda mwanadamu. Watu siku zote wanatarajia kuwa na mageuko makubwa katika namna ambayo Mungu anafanya kazi. Kuzungumza kwa wazi, ni kupitia maneno ndipo Mungu anawadhibiti watu, na unapaswa kufanya kile Anachokisema haijalishi kama unataka au hutaki; huu ni ukweli halisi, na unapaswa kutiiwa na watu wote, na hivyo haubadiliki, na kujulikana kwa wote.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufalme wa Milenia Umewasili

Maneno ya Mungu yataenea katika nyumba zisizohesabika, yatafahamika kwa wote, na wakati huo tu ndipo kazi yake itaenea ulimwenguni kote. Ambapo ni sawa na kusema, ikiwa kazi ya Mungu itaenea ulimwenguni kote, basi maneno Yake ni lazima yaenee. Katika siku ya utukufu wa Mungu, maneno ya Mungu yataonesha nguvu yake na mamlaka. Kila neno Lake kuanzia wakati huo hadi leo litatimizwa na kuwa la kweli. Kwa njia hii, utukufu utakuwa wa Mungu duniani—ambavyo ni sawa na kusema, kazi yake itatawala duniani. Wote ambao ni waovu wataadibiwa na maneno katika kinywa cha Mungu, wale wote ambao ni wa haki watabarikiwa na maneno katika kinywa Chake, na wote watathibitishwa na kukamilishwa na maneno katika kinywa Chake. Wala hataonyesha ishara zozote na maajabu; yote yatakamilishwa na maneno Yake, na maneno Yake yatazalisha ukweli. Kila mtu duniani atasherehekea maneno ya Mungu, ama ni watu wazima au watoto, wanaume, wanawake, wazee, au vijana, watu wote watajinyenyekeza katika maneno ya Mungu. Maneno ya Mungu yaonekana katika mwili, yakiwaruhusu watu kuyaona duniani, waziwazi na kufanana na kiumbe chenye uhai. Hii ndiyo maana ya Neno kufanyika mwili. Mungu amekuja duniani kwa lengo la kukamilisha ukweli wa “Neno kufanyika mwili,” ni sawa na kusema, Amekuja ili kwamba maneno Yake yaweze kutolewa kutoka katika mwili (sio kama wakati wa Musa katika Agano la Kale, ambapo Mungu alizungumza moja kwa moja kutoka mbinguni). Baada ya hapo, kila neno Lake litatimizwa wakati wa Enzi ya Ufalme wa Milenia, zitakuwa ni kweli ambazo zitaonekana katika macho ya watu, na watu watazitazama kwa kutumia macho bila tofauti hata kidogo. Hii ndiyo maana kuu ya Mungu kupata mwili. Ni sawa na kusema, kazi ya Roho imetimizwa kupitia mwili, na kupitia maneno. Hii ndiyo maana ya kweli ya “Neno kufanyika mwili” na “Neno Laonekana katika mwili.” Ni Mungu pekee ndiye anayeweza kuzungumza mapenzi ya Roho, na ni Mungu pekee katika mwili ndiye anayeweza kuzungumza kwa niaba ya Roho; maneno ya Mungu yamewekwa wazi katika Mungu kupata mwili, na kila mtu anaongozwa nayo. Hakuna aliyeachwa, wote wanakuwa ndani ya mawanda haya. Ni kutoka tu katika matamshi haya ndipo watu wanaweza kujua; wale ambao hawatapata njia hii wanaota ndoto za mchana ikiwa wanadhani wanaweza kupata matamshi kutoka mbinguni. Hayo ndiyo mamlaka yaliyooneshwa katika mwili wa Mungu uliopata mwili: kuwafanya wote kuamini. Hata wataalamu wa kuheshimiwa sana na wachungaji hawawezi kuzungumza maneno haya. Wote ni lazima wajinyenyekeze chini yao, na hakuna anayeweza kuanza mwanzo mpya. Mungu atatumia maneno kuushinda ulimwengu. Atafanya hivi si kwa kupata kwake mwili, lakini kwa kutumia matamshi kutoka kwa Mungu katika mwili kushinda watu wote duniani; Namna hii tu ndiye Mungu katika mwili, na huu tu ndio kuonekana kwa Mungu katika mwili. Labda kwa watu, inaonekana kana kwamba Mungu hajafanya kazi kubwa—lakini Mungu analazimika kutamka maneno Yake ili watu washawishike kabisa, na wao kutishika kabisa. Bila kweli, watu wanapiga makelele na kupiga mayowe; kwa maneno ya Mungu, wote wananyamaza kimya. Mungu hakika atakamilisha ukweli huu, maana huu ni mpango ulioanzishwa na Mungu: kukamilisha ukweli wa Neno kuwasili duniani. Kimsingi, sina haja ya kuelezea—kuwasili kwa Ufalme wa Milenia duniani ni kuwasili kwa neno la Mungu duniani. Kushuka kwa Yerusalemu mpya kutoka mbinguni ni kuwasili kwa maneno ya Mungu kuishi miongoni mwa mwanadamu, kuenenda na kila tendo la mwanadamu, na mawazo yake yote ya ndani. Huu pia ni ukweli kwamba Mungu atatimiza, na mandhari mazuri kabisa ya Ufalme wa Milenia. Huu ndio mpango uliowekwa na Mungu: Maneno Yake yataonekana duniani kwa miaka elfu moja, na yatashuhudia matendo yake yote, na kukamilisha kazi Yake yote duniani, ambapo baada ya hatua hii mwanadamu atakuwa amefikia kikomo.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufalme wa Milenia Umewasili

Inayofuata: Hatua Tatu za Kazi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp