Kujua Kazi ya Mungu (II)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 188)

Kama mtu anayemwamini Mungu, inakupasa kuelewa kuwa, leo, katika kupokea kazi ya Mungu nyakati za mwisho na kazi yote ya mpango wa Mungu ndani yako, umepokea utukufu mkuu na wokovu wa Mungu kabisa. Kazi yote ya Mungu ulimwengu mzima imelenga watu wa kikundi hiki. Amejitolea kwa nguvu Zake zote na kutoa vyote kwa ajili yako; Amekurejesha na kukupa kazi yote ya Roho ulimwenguni kote. Ndiyo sababu Nasema kuwa wewe una bahati. Zaidi ya hayo, Amehamisha utukufu wake kutoka kwa Israeli, watu wake wateule, hadi kwako, ili kufanya kusudio lake lijidhihirishe kwenu kama kundi. Kwa hiyo, ninyi ndio mtakaopokea urithi wa Mungu, na hata zaidi warithi wa utukufu wa Mungu. Pengine utayakumbuka maneno haya: “Kwa kuwa huzuni yetu nyepesi, ambayo ni ya muda mdogo pekee, inatufanyia utukufu mkubwa na wa daima ambao unazidi kuwa mkuu kabisa.” Zamani, mlisikia msemo huu, lakini hakuna aliyeelewa maana kamili ya maneno yale. Leo, unajua vyema umuhimu wa maneno yale. Maneno haya ndiyo yatakayotimizwa na Mungu katika enzi za mwisho. Yatatimia kwa wale walioteswa na joka kuu jekundu katika sehemu linakoishi. Joka kuu jekundu humtesa Mungu na ni adui wa Mungu, kwa hiyo katika nchi hii, wanaomwamini Mungu wanateswa na kudhihakiwa. Ndiyo sababu maneno haya yatakuja kuwa kweli kwenu nyie kundi la watu. Kazi inapotekelezwa katika nchi inayompinga Mungu, kazi Yake yote inakabiliwa na vizuizi vya kupita kiasi, na mengi ya maneno Yake hayawezi kutimizwa katika wakati ufaao: ndiyo maana, watu husafishwa kwa ajili ya neno la Mungu. Hiki pia ni kipengele cha mateso. Ni vigumu kabisa kwa Mungu kutekeleza kazi yake katika nchi yenye joka kuu jekundu, lakini ni kupitia ugumu huu ndipo Mungu Hupiga hatua katika kazi Yake ili kudhihirisha hekima Yake na matendo Yake ya ajabu. Mungu Huchukua fursa hii kuwakamilisha watu hawa wa kikundi hiki. Kwa ajili ya mateso ya watu, tabia yao na hulka ya kishetani ya watu katika nchi hii najisi, Mungu Anafanya kazi Yake ya kutakasa na ushindi, ili, kutokana na hili, apokee utukufu na kuwapata wale wote wanaoshuhudia matendo Yake. Huu ndio umuhimu wa kujitoa kwa Mungu kwa ajili ya kikundi hiki cha watu. Ina maana kuwa Mungu hufanya kazi ya ushindi kupitia wale wanaompinga. Kufanya vile tu ndiko kunaweza kudhihirisha nguvu kuu za Mungu. Kwa maneno mengine, ni wale tu walio katika nchi najisi ndiyo wanaostahili kuurithi utukufu wa Mungu na ni hili tu ambalo litafanya nguvu kuu za Mungu kuwa maarufu. Ndiyo maana Nasema kuwa utukufu wa Mungu unapatikana katika nchi najisi na kwa wale wanaoishi humo. Haya ndiyo mapenzi ya Mungu. Hii ni kama tu ilivyokuwa katika kazi ya Yesu; Angetukuzwa tu kati ya Mafarisayo waliomdhihaki. Isingelikuwa mateso na usaliti wa Yuda, Yesu asingelidhihakiwa na kudharauliwa, na hata zaidi kusulubiwa, na hivyo asingelipokea utukufu. Kila mara Mungu Anapofanya kazi katika wakati fulani na kila mara anapofanya kazi Yake kwa kupitia mwili, huwa Anapokea utukufu na papo hapo huwapata Anaotaka kuwapata. Huu ndio mpango wa kazi ya Mungu na hivi ndivyo anavyosimamia kazi Yake.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Kazi ya Mungu Ni Rahisi Kama Vile Mwanadamu Anavyodhania?

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 189)

Katika mpango wa Mungu wa miaka elfu kadhaa, kazi inayofanywa ndani ya mwili ni katika sehemu mbili: Kwanza ni kazi ya kusulubiwa, ambayo kwayo anatukuzwa; nyingine ni kazi ya ushindi na ukamilifu katika nyakati za mwisho, ambayo kwayo pia Atapokea utukufu. Huu ni usimamizi wa Mungu. Hivyo basi, usichukulie kazi ya Mungu au agizo Lake kwako kuwa rahisi sana. Ninyi ndio warithi wa uzito wa milele wa utukufu wa Mungu, hili liliteuliwa na Mungu. Katika sehemu hizo mbili za utukufu wa Mungu, moja inafichuliwa ndani yako; ukamilifu wa sehemu moja ya utukufu Wake umepewa ili uwe urithi wako. Huku ndiko kutukuzwa kutoka kwa Mungu na mpango wake uliopangwa kitambo. Kutokana na ukuu wa kazi aliyoifanya Mungu katika nchi ambako joka kuu jekundu linaishi, kazi kama hii, ikipelekwa katika sehemu nyingine, ingezaa tunda zuri kitambo na ingekubaliwa na mwanadamu kwa urahisi. Na kazi kama hii ingekuwa rahisi sana kukubaliwa na viongozi wa dini wa Magharibi wanaomwamini Mungu, kwani kazi ya Yesu ni kama kielelezo. Ndio maana Hawezi kutekeleza hatua hii ya kazi ya utukufu mahali pengine; yaani, kwa kuwa kuna uungaji mkono kwa watu wote na utambulisho wa mataifa yote, hamna mahali ambapo utukufu wa Mungu unaweza “kupumzikia.” Na huu ndio umuhimu wa kipekee wa hatua hii ya kazi katika nchi hii. Kati yenu, hamna mtu mmoja anayepokea ulinzi wa sheria; badala yake, unaadhibiwa na sheria, na ugumu mkubwa zaidi ni kuwa hapana mtu anayekuelewa, awe ni jamaa yako, wazazi wako, marafiki wako, ama watendakazi wenzako. Hakuna anayekuelewa. Mungu “Anapokukataa,” hapana uwezekano wako kuendelea kuishi duniani. Hata hivyo, watu hawawezi kumwacha Mungu; huu ndio umuhimu wa ushindi wa Mungu kwa watu, na huu ni utukufu wa Mungu. Kile ambacho umerithi wakati huu, kimepiku walichorithi mitume na manabii na ni kikuu zaidi kuliko alichopokea Musa na Petro. Baraka haziwezi zikapokewa kwa siku moja au mbili; sharti zipatikane kwa kujitolea kwingi. Yaani, lazima uwe na upendo uliosafishwa, imani kuu, na ukweli mwingi ambao Mungu Anakuagiza uufikie; zaidi ya hayo, sharti uelekeze uso wako kwa haki wala usikubali kushindwa, na lazima uwe na upendo usiofikia kikomo kwa ajili ya Mungu. Azimio linahitajika kutoka kwako, na vilevile mabadiliko katika tabia ya maisha yako. Upotovu wako lazima utibiwe, na lazima ukubali mipango ya Mungu pasipo kulalamika, na hata uwe mtiifu hadi kifo. Hicho ndicho unachopaswa kutimiza. Hili ndilo lengo la mwisho la kazi ya Mungu, na matakwa ya Mungu kwa watu wa kundi hili. Anapokukarimia mengi, anakutaka wewe badala yake na kukufanyia matakwa yanayokufaa. Kwa hiyo, kazi yote ya Mungu haipo bila sababu, na kutokana na hili inaonekana ni kwa nini Mungu kila mara hufanya kazi ya hali ya juu na yenye mahitaji makali. Ndiyo maana unafaa kujawa na imani katika Mungu. Kwa ufupi, kazi yote ya Mungu hufanywa kwa ajili yako, ili kwamba uweze kupokea urithi Wake. Hii sio kwa ajili ya utukufu wa Mungu bali ni kwa ajili ya wokovu wako na kufanya kundi hili la watu walioteswa na nchi najisi kuwa wakamilifu. Sharti uelewe mapenzi ya Mungu. Kwa hiyo Nawahimiza wale wote wasiojua, wasio na hisia na ufahamu: Usimjaribu Mungu wala kumpinga tena. Mungu Ameshavumilia mateso yote ambayo mwanadamu hajaweza kupitia, na hapo awali Ameteseka na kudhihakiwa kwa niaba ya mwanadamu. Je, nini kingine ambacho huwezi kukiachilia? Je, ni nini muhimu zaidi kuliko mapenzi ya Mungu? Ni nini zaidi kuliko upendo wa Mungu? Ni kazi ambayo ina ugumu mara mbili zaidi kwa Mungu kufanya katika nchi najisi. Ikiwa mtu atatenda dhambi kimakusudi na akifahamu, kazi ya Mungu itaendelezwa kwa muda mrefu zaidi. Katika tukio lolote, hili silo pendeleo la yeyote wala si la maana kwa yeyote. Mungu Hafungwi na wakati; kazi Yake na utukufu Wake huchukua mstari wa mbele. Kwa hiyo, hata ikichukua muda mrefu, Hataacha kutoa dhabihu yoyote ikiwa ni kazi Yake. Hii ndiyo silika ya Mungu: Hatapumzika hadi pale kazi Yake itakapokamilika. Ni pale tu ambapo wakati unapowadia na anapokea sehemu ya pili ya utukufu wake ndipo kazi Yake itakapokwisha. Mungu Asipokamilisha sehemu ya pili ya utukufu wake ulimwenguni, Siku Yake haitawadia, mkono wake hauwezi kuwaachilia wateule wake, utukufu wake hautashuka juu ya Israeli na mpango wake kamwe hauwezi kukamilishwa. Mnapaswa kuona mapenzi ya Mungu na kuona kwamba kazi ya Mungu si rahisi kama ilivyokuwa katika kuumba mbingu na nchi na vyote vilivyomo. Hiyo ni kwa sababu kazi ya leo ni mabadiliko ya wale waliopotoshwa, wale walio baridi kwa kiasi kikubwa zaidi, ni ili kuwatakasa wale walioumbwa lakini wakashughulikiwa na Shetani. Si uumbaji wa Adamu na Hawa, sembuse kuumba mwanga, ama aina yote ya mimea na wanyama. Kazi Yake sasa ni kutakasa wote waliopotoshwa na Shetani ili kwamba wamrejelee, wawe miliki Yake na wawe utukufu wake. Kazi kama ile si rahisi jinsi mwanadamu anavyofikiria kuhusu kuumbwa kwa mbingu na nchi na vilivyomo, wala si sawa na kumkemea Shetani aende katika shimo lisilo na mwisho, kama anayodhania mwanadamu. Bali, ni kumbadilisha mtu, kubadili kilicho hasi kuwa chanya na kufanya kuwa miliki Yake ambacho si chake. Huu ndio undani wa hadithi ya hatua hii ya kazi ya Mungu. Lazima ufahamu wala usirahisishe mambo. Kazi ya Mungu ni tofauti na kazi nyingine. Uzuri wake hauwezi kutambuliwa na akili za mwanadamu wala hekima Yake kupatikana vile. Wakati wa hatua hii ya kazi Yake, Mungu Haumbi kila kitu wala kuharibu kila kitu. Bali, Anabadilisha viumbe vyote na kutakasa vyote vilivyonajisiwa na Shetani. Kwa hiyo, Mungu Ataanzisha kazi kuu, na huu ndio umuhimu wa kazi ya Mungu. Baada ya kusoma maandishi haya, je, unaamini kuwa kazi ya Mungu ni rahisi vile?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Kazi ya Mungu Ni Rahisi Kama Vile Mwanadamu Anavyodhania?

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 190)

Miaka 6,000 ya kazi ya Mungu ya usimamizi imegawanywa katika hatua tatu: Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Hatua hizi zote tatu za kazi ni kwa ajili ya wokovu wa wanadamu, yaani, ni kwa ajili ya wokovu wa wanadamu ambao wamepotoshwa na Shetani kwa kiasi kikubwa. Wakati uo huo, hata hivyo, pia ni ili kwamba Mungu afanye vita na Shetani. Hivyo, kama kazi ya wokovu ilivyogawanywa katika hatua tatu, kwa hivyo pia vita dhidi ya Shetani vimegawanywa katika hatua tatu, na vipengele hivi viwili vya kazi ya Mungu vinafanywa sawia. Vita dhidi ya Shetani kwa kweli ni kwa ajili ya wokovu wa wanadamu, na kwa kuwa kazi ya wokovu wa wanadamu silo jambo linaloweza kukamilishwa kwa mafanikio katika hatua moja, vita dhidi ya Shetani pia vimegawanywa katika hatua na vipindi, na vita vinapiganwa dhidi ya Shetani kulingana na mahitaji ya mwanadamu na kiwango cha kupotoshwa kwa mwanadamu na Shetani. Pengine, katika mawazo ya mwanadamu, anaamini kuwa katika vita hivi Mungu atajiandaa kupigana na Shetani, katika njia sawa na vile ambavyo majeshi mawili yangepigana. Hili tu ni jambo ambalo akili ya mwanadamu ina uwezo wa kukisia, na ni wazo lisilo dhahiri kupita kiasi na lisiloweza kutendeka, na bado ndilo mwanadamu analiamini. Na kwa sababu Nasema hapa kuwa njia ya wokovu wa mwanadamu ni kupitia vita na Shetani, mwanadamu anawaza ya kwamba hivi ndivyo vita vinavyoendeshwa. Katika kazi ya wokovu wa mwanadamu, hatua tatu zimefanywa, ambayo ni kusema kuwa vita na Shetani vimegawanyika katika hatua tatu kabla ya kushindwa kabisa kwa Shetani. Na bado ukweli wa ndani wa kazi yote ya vita dhidi ya Shetani ni kwamba matokeo yake yanatimizwa kupitia kwa hatua kadhaa za kazi: kumpa mwanadamu neema, na kuwa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, kuzisamehe dhambi za mwanadamu, kumshinda mwanadamu, na kumfanya mwanadamu akamilishwe. Kusema ukweli, vita na Shetani hajiandai kupigana na Shetani, bali ni wokovu wa mwanadamu, kuyashughulikia maisha ya mwanadamu, na kubadilishwa kwa tabia ya mwanadamu ili kwamba aweze kumshuhudia Mungu. Hivi ndivyo Shetani anashindwa. Shetani anashindwa kwa kubadilisha tabia potovu ya mwanadamu. Wakati Shetani ameshindwa, yaani, wakati mwanadamu ameokolewa kabisa, basi Shetani aliyeaibika atafungwa kabisa, na kwa njia hii, mwanadamu atakuwa ameokolewa kabisa. Na kwa hivyo, kiini cha wokovu wa mwanadamu ni vita dhidi ya Shetani, na vita na Shetani vitajitokeza kimsingi katika wokovu wa mwanadamu. Hatua ya siku za mwisho, ambapo mwanadamu atashindwa, ni hatua ya mwisho katika vita dhidi ya Shetani, na pia kazi ya wokovu kamili wa mwanadamu kutoka kwa miliki ya Shetani. Maana ya ndani ya ushindi wa mwanadamu ni kurudi kwa mfano halisi wa Shetani, mtu ambaye amepotoshwa na Shetani, kwa Muumba baada ya ushindi wake, kwa njia ambayo atamwacha Shetani na kurejea kabisa kwa Mungu. Kwa njia hii, mwanadamu atakuwa ameokolewa kabisa. Na kwa hivyo, kazi ya ushindi ni kazi ya mwisho katika vita dhidi ya Shetani, na hatua ya mwisho katika kazi ya Mungu ya usimamizi kwa ajili ya kushindwa kwa Shetani. Bila kazi hii, wokovu kamili wa mwanadamu hatimaye haungewezekana, kushindwa kikamilifu kwa Shetani kusingewezekana, na wanadamu kamwe hawangekuwa na uwezo wa kuingia kwenye hatima ya ajabu, ama kuwa huru kutoka kwa ushawishi wa Shetani. Kwa hivyo, kazi ya wokovu wa mwanadamu haiwezi kukamilishwa kabla vita dhidi ya Shetani havijahitimishwa, kwa kuwa msingi wa kazi ya Mungu ya usimamizi ni kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu. Mwanadamu wa kwanza kabisa alikuwa kwa mikono ya Mungu, lakini kwa sababu ya majaribu ya Shetani na upotovu wake, mwanadamu alifungwa na Shetani na kuanguka katika mikono ya yule mwovu. Kwa hivyo, Shetani akakuwa mlengwa wa kushindwa katika kazi ya Mungu ya usimamizi. Kwa sababu Shetani alichukua umiliki wa mwanadamu, na kwa sababu mwanadamu ndiye kiini cha usimamizi wote wa Mungu, kama mwanadamu ni wa kuokolewa, basi ni lazima anyakuliwe kutoka mikononi mwa Shetani, yaani mwanadamu ni lazima achukuliwe baada ya kutekwa nyara na Shetani. Hivyo, Shetani lazima ashindwe kupitia mabadiliko ya tabia ya mwanadamu ya zamani, mabadiliko ambayo hurejesha hisia zake za awali, na kwa njia hii, mwanadamu, ambaye ametekwa nyara, anaweza kunyakuliwa kutoka mikononi mwa Shetani. Kama mwanadamu anawekwa huru kutokana na ushawishi wa Shetani na utumwa wake, Shetani ataaibika, mwanadamu hatimaye atarejeshwa, na Shetani atakuwa ameshindwa. Na kwa sababu mwanadamu amewekwa huru kutoka kwa ushawishi wa giza wa Shetani, mwanadamu atakuwa mabaki ya vita hivi vyote, na Shetani atakuwa ndiye mlengwa ambaye ataadhibiwa punde tu vita hivi vitakapokamilika, na baada ya hapo kazi nzima ya wokovu wa mwanadamu itakuwa imekamilika.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 191)

Mungu Amekuwa mwili katika nchi ya China, ambayo wenyeji wa Hong Kong na Taiwan wanaiita bara. Mungu Alipokuja kutoka juu na kuja duniani, hakuna mtu mbinguni wala duniani aliyejua, maana hii ndiyo maana ya kweli ya Mungu kurudi kwa namna ya siri. Amekuwa katika mwili Akifanya kazi na kuishi kwa muda mrefu, bado hakuna mtu yeyote aliyejua. Hata leo hii, hakuna mtu anayetambua. Pengine hiki kitabakia kuwa kitendawili cha milele. Mungu kuja katika mwili wakati huu sio kitu ambacho mtu yeyote anaweza kujua. Haijalishi ni kwa kiwango kikubwa kiasi gani Roho Mtakatifu Anafanya kazi, siku zote Mungu yupo katika hali ya utulivu, kamwe Hajiachilii mbali. Mtu anaweza kusema kwamba inaonekana kama hatua hii ya kazi Yake inafanyika mbinguni. Ingawa ipo wazi kabisa kwa kila mtu, hakuna anayeitambua. Mungu Atakapomaliza hatua hii ya kazi Yake, binadamu wote wataachana na mtazamo wao wa kawaida,[1] na kuamka kutoka katika ndoto yao ndefu. Nakumbuka Mungu Alishawahi kusema, “Kuja katika mwili wakati huu ni sawa na kuanguka katika tundu la duma.” Hii ina maana kwamba kwa sababu awamu hii ya kazi ya Mungu imemfanya Mungu kuja katika Mwili na kuzaliwa katika makazi ya joka kuu jekundu, hata kuliko awali, Anakumbwa na hatari kubwa kwa kuja duniani wakati huu. Anachokabiliana nacho ni visu na bunduki na kumbi za starehe; Anavyokabiliana navyo ni vishawishi; Anaokutana nao ni umati wa watu wenye sura za wauaji. Ana hatari ya kuuawa wakati wowote. Mungu Alikuja na ghadhabu. Hata hivyo, Alikuja ili Aweze kufanya kazi ya utakasaji, ikiwa na maana kwamba kufanya sehemu ya pili ya kazi Yake inayoendelea baada ya kazi ya wokovu. Kwa ajili ya hatua hii ya kazi Yake, Mungu Amejitolea mawazo na uangalizi wa hali ya juu kabisa na Anatumia njia yoyote inayoweza kufikiriwa ili kuepuka mashambulio ya majaribu, Anajificha katika unyenyekevu Wake na kamwe haringii utambulisho Wake. Katika kumwokoa mwanadamu msalabani, Yesu Alikuwa Anakamilisha tu kazi ya wokovu; Alikuwa hafanyi kazi ya utakasaji. Hivyo ni nusu tu ya kazi ya Mungu ndiyo ilikuwa inafanywa, na kukamilisha kazi ya ukombozi ilikuwa ni nusu ya mpango Wake mzima. Kwa kuwa enzi mpya ilikuwa inakaribia kuanza na ile ya zamani kukaribia kutoweka, Mungu Baba Alianza kukusudia sehemu ya pili ya kazi Yake na Akaanza kujiandaa kwa ajili yake. Wakati uliopita, kupata mwili huku katika siku za mwisho huenda hakukutolewa unabii, na hivyo kuweka msingi wa usiri mkubwa unaozunguka ujio wa Mungu katika mwili kipindi hiki. Wakati wa mapambazuko, bila kujulikana kwa mtu yeyote, Mungu Alikuja duniani na Akaanza maisha Yake katika mwili. Watu hawakujua kipindi hiki. Pengine wote walikuwa wamelala, pengine wengi waliokuwa wanakesha walikuwa wanasubiri, na pengine wengi walikuwa wanamwomba Mungu wa mbinguni kimyakimya. Lakini miongoni mwa watu hawa wote, hakuna hata mmoja aliyejua kuwa Mungu tayari Amekwishawasili duniani. Mungu Alifanya hivi ili Aifanye kazi Yake kwa urahisi na kupata matokeo bora zaidi, na pia ilikuwa ni kwa sababu ya kuepuka majaribu zaidi. Mwanadamu anapoamka kutoka usingizini, kazi ya Mungu itakuwa imekwishakamilika zamani sana na Ataondoka, na kufunga maisha Yake ya kutembeatembea na kusafiri duniani. Kwa kuwa kazi ya Mungu inamtaka Mungu kutenda na kuzungumza kwa nafsi Yake mwenyewe, na kwa kuwa hakuna namna ambayo mwanadamu anaweza kuingilia kati, Mungu Ameyavumilia maumivu makali ya kuja duniani kufanya kazi Yeye Mwenyewe. Mwanadamu hawezi kushikilia nafasi ya kazi ya Mungu. Kwa hiyo Mungu Alijihatarisha mara elfu kadhaa kuliko ilivyokuwa katika wakati wa Enzi ya Neema na kuja chini mahali ambapo joka kuu jekundu linaishi ili kufanya kazi Yake, kuweka mawazo Yake yote na uangalizi katika kuokoa kundi hili la watu maskini, kulikomboa kundi hili la watu lililogeuka na kuwa rundo la samadi. Ingawa hakuna anayejua uwepo wa Mungu, Mungu Hahangaiki kwa sababu ni faida kubwa kwa kazi ya Mungu. Kila mtu ni mwovu sana, sasa inawezekanaje kila mtu avumilie uwepo wa Mungu? Ndiyo maana duniani, Mungu Anakuwa kimya siku zote. Haijalishi mwanadamu ni katili kiasi gani, Mungu wala Hazingatii hayo moyoni Mwake hata kidogo, bali Anaendelea kufanya kazi Anayotaka kufanya ili kutimiza agizo kuu ambalo Baba wa mbinguni Alimpatia. Ni nani miongoni mwenu aliyetambua upendo wa Mungu? Ni nani anayejali sana mzigo Alionao Mungu Baba kuliko Mwana Wake Anavyofanya? Ni nani awezaye kuelewa mapenzi ya Mungu Baba? Roho wa Mungu Baba Aliyeko mbinguni Anasumbuka kila mara, na Mwana Wake duniani Anaomba mara kwa mara juu ya mapenzi ya Mungu Baba, Akihofia moyo Wake kuumia. Kuna mtu yeyote anayejua kuhusu upendo wa Mungu Baba kwa Mwana Wake? Kuna mtu yeyote anayejua jinsi ambavyo Mwana mpendwa Anavyomkumbuka Mungu Baba? Wakipata shida ya kuchagua kati ya mbingu na nchi, utaona wawili Hawa wanatazamana wakati wote kutoka kwa mbali, sambamba na Roho. Ee binadamu! Ni lini mtaufikiria moyo wa Mungu? Ni lini mtaielewa nia ya Mungu? Baba na Mwana siku zote Wamekuwa Wakitegemeana. Kwa nini tena Watengane, mmoja juu mbinguni na mmoja chini duniani? Baba Anampenda Mwana Wake kama vile Mwana Anavyompenda Baba Yake. Kwa nini sasa asubiri kwa muda mrefu huku Akiwa na shauku hiyo? Ingawa Hawajatengana kwa muda mrefu, je, mtu yeyote anajua kwamba Baba tayari Amekuwa Akitaka sana kwa shauku kwa siku nyingi na Amekuwa Akitarajia kwa muda mrefu kurudi haraka kwa Mwana Wake mpendwa? Anatazama, Anakaa kwa utulivu, Anasubiri. Hii yote ni kwa ajili ya kutaka Mwana Wake mpendwa Arudi haraka. Ni lini Atakuwa tena na Mwana ambaye Anazungukazunguka duniani? Ingawa watakapokuwa pamoja tena, Watakuwa pamoja milele, Anawezaje kustahimili maelfu ya siku za utengano, mmoja juu mbinguni na mwingine chini duniani. Makumi ya miaka duniani ni kama maelfu ya miaka mbinguni. Mungu Baba Anawezaje kutokuwa na wasiwasi? Mungu Anapokuja duniani, Anakabiliana na mabadiliko mengi ya ulimwengu wa kibinadamu kama mwanadamu. Mungu Mwenyewe hana hatia, sasa kwa nini Mungu Ateseke kwa maumivu kama mwanadamu? Pengine ndiyo maana Mungu Baba Anatamani sana Mwana Wake Arudi haraka; nani awezaye kuujua moyo wa Mungu? Mungu Anampatia mwanadamu vitu vingi sana; mwanadamu anawezaje kuulipa moyo wa Mungu kikamilifu? Lakini mwanadamu anampatia Mungu kidogo sana; sasa Mungu Atawezaje kutokuwa na wasiwasi?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (4)

Tanbihi:

1. “Kubadilika kutokana na mtazamo wao wa kawaida” inahusu jinsi fikira za watu na maoni kumhusu Mungu hubadilika mara tu wanapokuja kumjua Mungu.

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 192)

Ni wachache sana miongoni mwa wanadamu wanaouelewa moyo wa Mungu kwa sababu tabia za watu ni duni sana na hisia zao za kiroho zimepoa sana, na kwa sababu hawaoni wala kutilia maanani kile ambacho Mungu anafanya. Hivyo Mungu Anaendelea kuwa na hofu juu ya mwanadamu, kana kwamba asili ya tabia ya wanyama ndani ya mwanadamu inaweza kuonekana muda wowote. Hii inaonyesha zaidi kwamba kuja kwa Mungu duniani kunaambatana na majaribu makubwa. Lakini kwa ajili ya kukamilisha kundi la watu, Mungu, Akiwa na utukufu, Alimwambia mwanadamu juu ya kila kusudi lake, bila kuficha kitu. Ameamua kwa dhati kukamilisha kundi hili la watu. Kwa hiyo, ije shida yoyote au jaribu, Anatazama mbali na kuyapuuzia yote. Anafanya kazi yake kimyakimya tu, Akiamini kwamba siku moja ambapo Mungu Atapata utukufu, mwanadamu atamjua Mungu, na kuamini kwamba mwanadamu atakapokuwa amekamilishwa na Mungu, atakuwa ameuelewa moyo wa Mungu kikamilifu. Sasa hivi kunaweza kuwepo watu wanaomjaribu Mungu au kumwelewa vibaya Mungu au kumlaumu Mungu; Mungu wala hayazingatii haya moyoni. Mungu atakapoingia katika utukufu, watu wote wataelewa kwamba kila kitu ambacho Mungu Anafanya ni kwa ajili ya mema ya binadamu, na watu wote wataelewa kwamba kila kitu ambacho Mungu Anafanya ni kwa sababu binadamu aweze kuishi vizuri. Ujio wa Mungu umeambatana na majaribu, na Mungu pia Anakuja katika adhama na ghadhabu Yangu. Muda ambapo Mungu Anamwacha mwanadamu, Atakuwa tayari Amepata utukufu, na Ataondoka Akiwa Amejawa na utukufu mwingi na furaha ya kurudi. Mungu Anayefanya kazi duniani Hazingatii mambo moyoni Mwake haijalishi watu wamemkataa kiasi gani. Yeye Anafanya tu kazi Yake. Uumbaji wa Mungu wa ulimwengu unaanzia mbali maelfu ya miaka huko nyuma, Amekuja duniani kufanya kazi isiyoweza kupimika, na Amepitia uzoefu mkubwa wa kukataliwa na kashfa. Hakuna anayekaribisha ujio wa Mungu; kila mtu anamwangalia tu kwa jicho kavu. Katika kipindi hiki cha maelfu ya miaka ya taabu, matendo ya mwanadamu yamevunjavunja moyo wa Mungu tangu zamani sana. Wala Hazingatii tena uasi wa watu, lakini badala yake Anatengeneza mpango tofauti ili kumbadilisha na kumsafisha mwanadamu. Dhihaka na kashfa, mateso, dhiki, mateso ya msalaba, kutengwa na wanadamu, na kadhalika ambayo Mungu Alipitia Akiwa katika mwili, Mungu Amepitia ya kutosha. Dhihaka na kashfa, mateso, dhiki, mateso ya msalaba, kutengwa na wanadamu, na kadhalika ambayo Mungu Alipitia Akiwa katika mwili, Mungu Amepitia ya kutosha. Mungu katika mwili Ameteseka kikamilifu na shida za ulimwengu wa wanadamu. Roho wa Mungu Baba wa mbinguni Aliona mambo hayo hayavumiliki na Akarudisha kichwa Chake nyuma na kufumba macho Yake, Akisubiri Mwana Wake mpendwa kurudi. Yote Anayoyatamani ni kwamba watu wote wasikie na kutii, waweze kuhisi aibu kubwa mbele ya mwili Wake, na wasiasi dhidi Yake. Anachokitamani ni kwamba watu wote waamini kwamba Mungu yupo. Aliacha zamani sana kutaka mambo makubwa kutoka kwa mwanadamu kwa sababu Mungu Amelipa gharama kubwa sana, lakini mwanadamu bado anajistarehesha,[1] na kamwe haiweki kabisa kazi ya Mungu moyoni mwake hata kidogo.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (4)

Tanbihi:

1. “Anajistarehesha” inamaanisha kwamba watu hawapendezwi kuhusu kazi ya Mungu na hawaizingatii kama muhimu.

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 193)

Wakati ambapo, katika Enzi ya Neema, Mungu alirudi kwa mbingu ya tatu, kazi ya Mungu ya kuwakomboa wanadamu wote ilikuwa kwa kweli tayari imeendelea katika tendo lake la kumaliza. Vyote vilivyobaki duniani vilikuwa msalaba ambao Yesu aliubeba, sanda ya kitani ambayo Yesu alifungiwa ndani, na taji ya miiba na joho la rangi nyekundu ambavyo Yesu alivaa (hivi vilikuwa vitu ambavyo Wayahudi walitumia kumdhihaki Yeye). Yaani, baada ya kazi ya kusulubiwa kwa Yesu isababishe mhemko mkubwa, mambo yalitulia tena. Tangu wakati huo na kuendelea, wanafunzi wa Yesu wakaanza kuendeleza kazi Yake, wakiyachunga na kunyunyizia katika makanisa kila mahali. Maudhui ya kazi yao yalikuwa haya: kuwafanya watu wote watubu, waungame dhambi zao, na wabatizwe; mitume wote wakieneza hadithi ya ndani ya kusulubiwa kwa Yesu na kile kilifanyika kwa kweli, kila mtu asiweze kujizuia kuanguka chini mbele za Yesu kuungama dhambi zake, na zaidi ya hayo mitume wakieneza kila mahali maneno yaliyonenwa na Yesu na sheria na amri Alizozianzisha. Kuanzia wakati huo ujenzi wa makanisa ulianza katika Enzi ya Neema. Kile ambacho Yesu alizungumzia wakati wa enzi hiyo pia kililenga maisha ya mwanadamu na mapenzi ya Baba wa mbinguni. Ni kwa sababu tu enzi hizo ni tofauti ndiyo nyingi za semi na matendo hayo yanatofautiana sana na ya leo. Lakini kiini cha vyote viwili ni sawa. Yote mawili kwa uhakika na usahihi ni takriban kazi ya Roho wa Mungu katika mwili kabisa. Aina hii ya kazi na matamko yameendelea wakati wote mpaka siku hii, na kwa hivyo kitu cha aina hii bado kinashirikiwa kati ya mashirika ya dini leo na hakijabadilika hata kidogo. Wakati ambapo kazi ya Yesu ilikamilishwa, na makanisa tayari yalikuwa yameingia kwenye njia sahihi ya Yesu Kristo, Mungu bado alianzisha mpango Wake wa hatua nyingine ya kazi Yake, jambo la kupata mwili katika siku za mwisho. Kwa mwanadamu, Mungu kusulubiwa kulihitimisha kazi ya Mungu kupata mwili, Aliwakomboa binadamu wote, na Akamruhusu kuteka ufunguo wa Kuzimu. Kila mtu anadhani kwamba kazi ya Mungu imekamilika kikamilifu. Kwa uhalisia, kwa Mungu, ni sehemu ndogo tu ya kazi Yake ndiyo imekamilika. Amemkomboa tu binadamu; Hajamshinda mwanadamu, wala kubadilisha ubaya wa Shetani kwa binadamu. Hiyo ndiyo maana Mungu Anasema, “Ingawa mwili Wangu ulipitia maumivu ya kifo, hilo sio lengo lote la Mimi kupata mwili. Yesu ni Mwana Wangu mpendwa na Alisulubishwa msalabani kwa ajili Yangu, lakini hakukamilisha kikamilifu kazi Yangu. Alifanya tu sehemu.” Hivyo Mungu Akaanza mpango wa mzunguko wa pili ili kuendeleza kazi ya Mungu kupata mwili. Lengo kuu la Mungu ni kumkamilisha na kumpata kila mmoja aokolewe kutoka katika mikono ya Shetani, hiyo ndiyo sababu Mungu Alijiandaa tena kujihatarisha kuja katika mwili. Maana ya “kupata mwili” ni Yule ambaye haleti utukufu (kwa sababu kazi ya Mungu bado haijamalizika), lakini yule anayeonekana katika utambulisho wa Mwana mpendwa, na Yeye ndiye Kristo, ambaye Mungu amependezwa naye. Ndiyo maana hili linasemekana kuwa “kujitayarisha kwa ajili ya hatari”. Mwili ni wenye nguvu kidogo sana na lazima utahadhari sana,[1] na nguvu Yake ni tofauti sana na mamlaka ya Baba wa mbinguni; Yeye hutimiza tu huduma ya mwili, Akifanikisha kazi na agizo la Mungu Baba bila kujihusisha katika kazi nyingine. Yeye hufanikisha tu sehemu moja ya kazi. Hii ndiyo maana Mungu anaitwa “Kristo” alipokuja duniani. Hii ndiyo maana ya ndani. Sababu ya kusema kwamba kuja huko kunaandamana na majaribu ni kwa kuwa mradi wa kazi mmoja pekee ndio unafanikishwa. Zaidi ya hayo, sababu Mungu Baba humwita tu “Kristo” na “Mwana mpendwa” na Hajampa utukufu wote ni hasa kwa vile mwili uliokuwa mwili huja kufanya mradi wa kazi moja, sio kumwakilisha Baba aliye mbinguni, bali kutimiza huduma ya Mwana mpendwa. Mwana mpendwa atakapomaliza agizo lote Alilokubali kubeba juu ya mabega Yake, Baba atampa Yeye utukufu kamili pamoja na utambulisho wa Baba. Mtu anaweza kusema kwamba hii ni kanuni ya mbinguni. Kwa sababu Yule ambaye amekuja katika mwili na Baba aliye mbinguni wako katika hali mbili tofauti, hao wawili huonana tu katika Roho, Baba akimtazama kwa makini Mwana mpendwa lakini Mwana asiweze kumwona Baba kutoka mbali. Ni kwa sababu kazi ya mwili ni ndogo sana na Ana uwezo wa kuuawa wakati wowote, kwamba kuja huku kunasemekana kuambatana na hatari kuu. Hii ni sawa na Mungu mara tena kumwachilia Mwana Wake mpendwa na kumweka ndani ya mdomo wa chui mkubwa mwenye milia. Ni hatari kwa maisha kwamba Mungu alimweka Yeye mahali ambapo Shetani amekolea sana. Hata kwa kupata mashaka kama hayo, Mungu bado alimkabidhi Mwana Wake mpendwa kwa watu wa mahali pachafu, fisadi ili wao “wamlee.” Hii ni kwa sababu ni njia pekee ya kazi ya Mungu kuleta maana kabisa na njia pekee ya kutimiza mapenzi yote ya Mungu Baba na kufanikisha sehemu ya mwisho ya kazi Yake miongoni mwa wanadamu. Yesu alifanikisha tu hatua moja ya kazi ya Mungu Baba. Kwa sababu ya kizuizi cha mwili uliopata mwili na tofauti katika kazi iliyofanikishwa, Yesu Mwenyewe hakujua kwamba kungekuwa na kurudi kwa pili kwa mwili. Kwa hivyo hakuna mfafanuaji au nabii wa Biblia aliyethubutu kutabiri wazi kwamba Mungu angepata mwili katika siku za mwisho, yaani, angekuja katika mwili tena ili kufanya sehemu ya pili ya kazi Yake katika mwili. Kwa hivyo, hakuna aliyetambua kwamba Mungu tayari Alikuwa amejificha kwa muda mrefu katika mwili. Si ajabu, kwani ilikuwa tu baada ya Yesu kufufuka na kupaa mbinguni ndipo Akakubali agizo hili, kwa hiyo hakuna unabii ulio wazi kuhusu kupata mwili kwa Mungu mara pili, na ni jambo lisilofikirika na akili ya binadamu. Katika vitabu vyote vingi vya unabii ndani ya Biblia, hakuna maneno yanayotaja hili kwa dhahiri. Lakini Yesu alipokuja kufanya kazi, tayari kulikuwa na unabii wa wazi uliosema kwamba bikira atashika uja uzito, naye atamzaa mwana, kumaanisha kwamba mimba Yake ilipatikana kwa njia ya Roho Mtakatifu. Hata hivyo, Mungu bado alisema hili lilifanyika kwa hatari ya kifo, hivyo hali ingekuwaje ya hatari katika hali ya leo? Si ajabu Mungu asema kwamba kupata mwili wakati huu kuna hatari mara elfu zaidi kuliko zile za wakati wa Enzi ya Neema. Katika maeneo mengi, Mungu Alitabiri kupata kundi la washindi katika nchi ya Sinimu. Ni katika Mashariki mwa ulimwengu ambapo washindi watapatwa, hivyo nchi ambapo Mungu anashukia katika kupata mwili Kwake mara ya pili bila shaka ni nchi ya Sinimu, mahali ambapo joka jekundu linaishi. Hapo Mungu Atawapata warithi wa joka kuu jekundu na litashindwa na kuaibishwa. Mungu Anataka kuwaamsha watu hawa walioteseka sana, kuwaamsha kabisa, na kuwafanya waondoke katika ukungu na kulikataa joka kuu jekundu. Mungu Anataka Awaamshe kutoka katika ndoto zao, kuwafanya waelewe tabia ya joka kuu jekundu, kuutoa moyo wao wote kwa Mungu, kuinuka kutoka katika nguvu kandamizi za giza, kusimama Mashariki mwa dunia, na kuwa uthibitisho wa ushindi wa Mungu. Baada ya hapo Mungu Atakuwa Amepata utukufu. Kwa sababu hii tu, kazi ambayo ilisitishwa Israeli Mungu Aliipeleka katika nchi ambapo linakaa joka kuu jekundu na, takribani miaka elfu mbili baada ya kuondoka, Amekuja tena katika mwili ili kuendeleza kazi ya Enzi ya Neema. Mwanadamu anashuhudia kwa macho yake, Mungu Akizindua kazi mpya katika mwili. Lakini kwa Mungu, Anaendeleza kazi ya Enzi ya Neema, kwa mwachano wa miaka elfu kadhaa, na badiliko tu la eneo la kufanyia kazi na mradi wa kazi. Ingawa taswira ya mwili ambayo Mungu Ameichukua katika kazi ya leo ni mtu mwingine tofauti na Yesu, Wanashiriki hulka na mzizi mmoja, na wanatoka katika chanzo kimoja. Pengine wana tofauti za umbo la nje, lakini kweli za ndani za kazi Zao zinafanana kabisa. Hata hivyo, enzi zenyewe, ni tofauti kama ilivyo usiku na mchana. Inawezekanaje kazi ya Mungu isibadilike? Au inawezekanaje kazi ziingiliane?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (6)

Tanbihi:

1. “Ni wenye nguvu kidogo sana na lazima utahadhari sana” inaashiria kwamba ugumu wa mwili ni mwingi sana, na kazi iliyofanywa ni ndogo sana.

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 194)

Imemchukua mwanadamu mpaka siku hii kutambua kwamba kile mtu anachokosa si tu kuruzukiwa maisha ya kiroho na uzoefu wa kumjua Mungu, lakini, muhimu zaidi, mabadiliko katika tabia yake. Kutokana na ujinga kamili wa mwanadamu wa historia na utamaduni wa kale wa wanadamu, hana ujuzi wa kazi ya Mungu hata kidogo. Mwanadamu hutumaini kuwa ndani kabisa ya moyo, mwanadamu anaweza kumpenda Mungu kwa kina moyoni mwake, lakini kwa kuwa mwili wa mwanadamu umepotoshwa kwa kina sana, kwa kufa ganzi pamoja na kuwa usiohisi, hii imemsababisha kutojua chochote hata kidogo kumhusu Mungu. Mungu Anakuja miongoni mwa wanadamu siku ya leo kwa kusudi la kubadilisha mawazo na roho zao, na taswira ya Mungu katika mioyo yao ambayo wamekuwa nayo kwa mamilioni ya miaka. Kupitia fursa hii, Atamfanya mwanadamu kuwa mkamilifu. Yaani, kupitia maarifa ya mwanadamu, Atabadilisha namna wanavyomfahamu na mitazamo yao Kwake, ili kwamba maarifa yao juu ya Mungu, yaweze kuanza katika rekodi safi, na mioyo yao itakuwa imesafishwa upya na kubadilishwa. Kushughulika na nidhamu ni njia, na ushindi na kufanya upya ni malengo. Kuondoa mawazo ya kishirikina aliyonayo mwanadamu kuhusu Mungu asiye dhahiri ndilo limekuwa kusudi la Mungu milele, na hivi karibuni limekuwa suala la haraka kwake. Ingekuwa kwamba watu wote wangetafakari kwa kina kwa kuzingatia hali hii. Wabadilishe jinsi kila mtu anavyopitia uzoefu ili kwamba kusudi hili la haraka la Mungu liweze kufanyika hivi karibuni na hatua ya mwisho ya kazi ya Mungu duniani iweze kuhitimishwa kwa matokeo mazuri. Onyesheni uaminifu wenu kama mnavyopaswa, na ufariji moyo wa Mungu kwa mara ya mwisho. Ni matumaini Yangu kwamba hakuna mtu yeyote miongoni mwa kaka na dada atakayekwepa jukumu hili au kuzungukazunguka tu. Mungu Anakuja katika mwili wakati huu kwa mwaliko, na kutokana na hali ya mwanadamu. Yaani, Anakuja kumpatia mwanadamu kile alichokuwa anahitaji. Atakuja kumwezesha kila mwanadamu, wa tabia yoyote au jamii, kuona neno la Mungu na, kutoka katika neno Lake, kuona uwepo na udhihirishaji wa Mungu na kukubali ukamilishaji wa Mungu. Neno lake litabadilisha mawazo na mitazamo ya mwanadamu ili kwamba sura ya kweli ya Mungu ikite mizizi kabisa katika moyo wa mwanadamu. Hili ndilo tamanio pekee la Mungu duniani. Haijalishi jinsi gani asili ya mwanadamu ilivyo, jinsi gani asili yake ilivyo duni, au matendo yake yalivyokuwa huko nyuma, Mungu Hajali haya. Anatumainia tu mwanadamu kuisafisha kabisa taswira ya Mungu aliyonayo moyoni mwake na kuijua asili ya binadamu, na hapo Atakuwa Amebadilisha mtazamo wa kiitikadi wa mwanadamu. Anatarajia mwanadamu kuwa na shauku ya kina kwa Mungu na kuwa na mahusiano ya milele na Yeye. Hiki ndicho Mungu Anachomwomba mwanadamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (7)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 195)

Nimezungumza mara nyingi sana kwamba kazi ya Mungu ya siku za mwisho ni kwa ajili ya kubadilisha roho ya kila mtu, kubadilisha nafsi ya kila mtu, ili kwamba moyo wake, ambao umeteseka sana na kiwewe, uwe umebadilishwa, hivyo kuokoa nafsi yake, ambayo imeumizwa kwa kina zaidi na uovu; ni kwa sababu ya kuamsha roho za watu, kuyeyusha mioyo yao baridi, na kuwaruhusu kurudisha nguvu za ujana. Haya ndiyo mapenzi makubwa ya Mungu. Weka pembeni mazungumzo ya ni namna gani maisha na uzoefu wa mwanadamu ni ya kiburi au ya kina; mioyo ya watu itakapokuwa imeamshwa, wanapokuwa wameamshwa kutoka kwa ndoto zao na kujua kikamilifu madhara yaliyoletwa na joka kuu jekundu, kazi ya huduma ya Mungu itakuwa imekamilika. Siku ambayo kazi ya Mungu itakuwa imekamilika pia ni siku ambapo mwanadamu ataanza rasmi kwenye njia sahihi ya kumwamini Mungu. Wakati huu, huduma ya Mungu itakuwa imekamilika: Kazi ya Mungu katika mwili itakuwa imekamilika kabisa, na mwanadamu atakuwa ameanza rasmi kufanya kazi ambayo anapaswa kufanya—atatekeleza huduma yake. Hizi ni hatua za kazi ya Mungu. Hivyo mnapaswa kutafuta kwa kupapasa kuingia kwenu katika misingi ya kujua mambo haya. Haya yote ndiyo mnayopaswa kuyajua. Kuingia kwa mwanadamu kutaboreka tu pale ambapo mabadiliko yatatokea ndani kabisa ya moyo wake, maana kazi ya Mungu ni wokovu kamili wa mwanadamu—mwanadamu aliyekombolewa, ambaye bado anaishi chini ya nguvu za giza, na ambaye hajawahi kuzinduka kutoka katika eneo hili la kusanyiko la pepo; ili kwamba mwanadamu aweze kuwekwa huru dhidi ya milenia ya dhambi, na kuwa wapendwa wa Mungu, kumkanyaga kabisa joka kuu jekundu, kuanzisha ufalme wa Mungu, na kuupumzisha moyo wa Mungu mapema, ni kutoa mawazo bila woga, bila kubania, kwa chuki inayovimbisha kifua chenu, kuondoa kabisa vijidudu hivyo, kuwafanya muache maisha haya ambayo hayana tofauti na maisha ya ng’ombe au farasi, ili msiwe watumwa tena, ili msiweze kukanyagwa tena au kuamrishwa na joka kuu jekundu; hamtakuwa tena wa taifa hili lililoanguka, hamtakuwa tena wa joka kuu jekundu lenye chuki, hamtafungwa nalo tena. Kiota cha pepo hakika kitachanwachanwa na Mungu, na mtasimama kando ya Mungu—nyinyi ni wa Mungu, na sio wa milki hii ya watumwa. Mungu ameichukia sana jamii hii ya giza toka zamani. Anasaga meno Yake, Akitamani kumkanyaga mwovu huyu, joka wa zamani mwenye chuki, ili kwamba asiinuke tena, na hatamnyanyasa tena mwanadamu; Hatasamehe matendo yake ya zamani, Hatavumilia udanganyifu wake kwa mwanadamu, atalipiza kisasi kwa kila kosa alilofanya katika enzi zote. Mungu hatamsamehe hata kidogo huyu kiongozi wa uovu wote,[1] Atamwangamiza kabisa.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (8)

Tanbihi:

1. “Kiongozi wa uovu wote” inahusu ibilisi mkongwe. Kirai hiki kinaonyesha kutopenda kabisa.

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 196)

Mungu amevumilia sana kulala bila kupata usingizi kwa ajili ya kazi ya binadamu. Kutoka vina vya juu hadi vya chini, Amepanda kwenda katika kuzimu ambapo mwanadamu anaishi kupitisha siku Zake na mwanadamu, hajawahi kulalamikia uchakavu walionao wanadamu, hajawahi kumlaumu kwa ukaidi wake, lakini Anavumilia mateso makuu kadri Anavyofanya kazi Yake. Inawezekanaje Mungu awe wa kuzimu? Inawezekanaje Aishi maisha Yake kuzimu? Lakini kwa ajili ya binadamu wote, ili binadamu wote waweze kupata pumziko mapema zaidi, Amestahimili fedheha na kupitia udhalimu kuja duniani, na Aliingia mwenyewe “jahanamu” na “kuzimu,” katika tundu la duma, kumwokoa mwanadamu. Mwanadamu amestahili vipi kumpinga Mungu? Ana sababu gani tena ya kumlaumu Mungu? Anawezaje kuwa na ujasiri wa kumwangalia Mungu tena? Mungu wa mbinguni Amekuja katika nchi hii chafu zaidi ya uovu, na Hajawahi kutangaza manung’uniko au malalamiko Yake kuhusu mwanadamu, lakini badala yake Anakubali kimyakimya maangamizi[1] na ukandamizaji wa mwanadamu. Kamwe Hajawahi kujibu matakwa ya mwanadamu yasiyokuwa na msingi, hajawahi kutaka mambo mengi yanayomuelemea mwanadamu, na hajawahi kumwekea mwanadamu matakwa yasiyokuwa na msingi; Anafanya tu kazi ambazo mwanadamu alitakiwa kufanya bila malalamiko: kufundisha, kutia mwanga, kukaripia, usafishaji wa maneno, kukumbusha, kusihi, kufariji, kuhukumu na kufunua. Ni hatua gani Alizozichukua ambazo si kwa ajili ya maisha ya mwanadamu? Ingawa Ameondoa matarajio na majaliwa ya mwanadamu, ni hatua zipi zilizochukuliwa na Mungu ambazo hazikuwa kwa ajili ya majaliwa ya mwanadamu? Ni ipi kati ya hatua hizo ambayo haijawahi kuwa kwa ajili ya mwanadamu kuendelea kuishi? Ni ipi kati ya hatua hizo haijakuwepo kwa ajili ya kumweka mwanadamu huru dhidi ya mateso haya na kunyanyaswa na nguvu za giza ambazo ni nyeusi kama usiku? Ni ipi kati ya hatua hizo si kwa ajili ya mwanadamu? Ni nani awezaye kuujua moyo wa Mungu, ambao ni sawa na mama mwenye mapenzi? Ni nani awezaye kuujua moyo wa Mungu wenye shauku? Moyo wa upendo na matarajio ya shauku ya Mungu vimelipwa kwa mioyo ya baridi, na usugu, na macho yanayoonyesha kutojali, kwa makaripio ya kujirudia na matusi ya mwanadamu, kwa maneno ya mkato na dhihaka na udhalilishaji, vimelipwa kwa dhihaka ya mwanadamu, kwa kukanyagwa na kukataliwa, kwa kutokuwa na ufahamu, na kupiga kite, na farakano, na uepukaji, kwa uongo, mashambulizi na ukali. Maneno ya wema ya Mungu yamekutana na nyuso kali na ufidhuli wa vidole elfu moja vinavyotikisika. Mungu anaweza tu kustahimili, Akiwa Ameinamisha kichwa, Akiwahudumia watu kama ng’ombe aliye radhi kufungwa.[2] Miezi na jua nyingi sana, Amekabiliana na nyota mara nyingi sana, Ameondoka alfajiri na kurudi jioni mara nyingi sana, na kurushwarushwa na kugeuzwa, Akivumilia maumivu makubwa mara elfu moja kuliko maumivu Aliyoyapata Alipokuwa Anaondoka kwa Baba Yake, Akivumilia mashambulizi na “kuvunja” kwa mwanadamu, na “kumshughulikia” na “kumpogoa” mwanadamu. Unyenyekevu na kufichika kwa Mungu vimelipwa kwa upendeleo[3] wa mwanadamu, kwa mitazamo na vitendo vya mwanadamu visivyokuwa vya haki, na kutojulikana Kwake, ustahimilivu, na uvumilivu vimelipizwa kwa jicho la tamaa la mwanadamu, mwanadamu hujaribu kumkanyaga Mungu hadi afe, bila majuto, na anajaribu kumkanyagia Mungu ardhini. Mtazamo wa mwanadamu kwa namna anavyomtendea Mungu ni wa “ujanja adimu,” na Mungu ambaye Anachokozwa na kutwezwa na mwanadamu, Anakanyagwa na kuwa bapa kwa miguu ya makumi elfu ya watu wakati mwanadamu mwenyewe anasimama juu kabisa, kana kwamba angeweza kuwa “mfalme wa kasri,” kana kwamba anataka kuchukua mamlaka kamili,[4] “kuendesha mahakama akiwa nyuma ya skrini,” kumfanya Mungu kuwa makini na mwenye kanuni “mwongozaji nyuma ya matukio,” ambaye haruhusiwi kupigana au kusababisha shida; lazima Mungu achukue nafasi ya “Mtawala wa Mwisho,” ni lazima Awe “kibaraka,”[5] bila uhuru wote. Matendo ya mwanadamu hayasemeki, sasa ana sifa gani ya kutaka hili au lile kuhusu Mungu? Ana sifa gani ya kutoa mapendekezo kwa Mungu? Anafaa kwa kiasi gani kumtaka Mungu amhurumie juu ya udhaifu wake? Anafaa kwa kiasi gani kupokea huruma ya Mungu? Anafaa kwa kiasi gani kupokea ukarimu wa Mungu kila mara? Anafaa kwa kiasi gani kupokea msamaha wa Mungu kila mara? Dhamiri yake ipo wapi? Alivunja moyo wa Mungu muda mrefu uliopita, ni muda mrefu toka ameuacha moyo wa Mungu katika vipande. Mungu alikuja miongoni mwa wanadamu Akiwa na nguvu nyingi na mwenye shauku kubwa, Akitegemea kwamba mwanadamu atakuwa mkarimu Kwake, hata kama ni kwa wema kiasi kidogo tu. Bado moyo wa Mungu haujafarijiwa na mwanadamu, yote Aliyoyapokea ni mashambulizi na mateso ya kuongezeka haraka;[6] moyo wa mwanadamu ni wenye tamaa sana, tamaa yake ni kubwa sana, hawezi akatosheka, siku zote ni mwenye fitina na jasiri pasi busara, hawezi kamwe kumpatia Mungu uhuru au haki ya kuzungumza, na anamwacha Mungu bila budi ila kukubali unyanyasaji, na kumruhusu mwanadamu kumtawala vyovyote apendavyo.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (9)

Tanbihi:

1. “Maangamizi” inatumiwa kuweka wazi kutotii kwa wanadamu.

2. “Anaweza tu kustahimili, Akiwa Ameinamisha kichwa, Akiwahudumia watu kama ng’ombe aliye radhi kufungwa” ni kwa asili sentensi moja, lakini hapa imegawanywa mara mbili ili kuyafanya mambo wazi zaidi. Sentensi ya kwanza inahusu matendo ya mwanadamu, huku ya pili inaonyesha mateso aliyoyapitia Mungu, na kwamba Mungu ni mnyenyekevu na Aliyefichika.

3. “Upendeleo” unahusu tabia ya watu ya ukaidi.

4. “Kuchukua mamlaka kamili” inahusu tabia ya watu ya ukaidi. Wanajitukuza, huwafunga wengine, wakiwafanya wawafuate na kuteseka kwa ajili yao. Wao ni majeshi ambayo ni ya uadui kwa Mungu.

5. “Kibaraka” inatumiwa kuwadhihaki wale ambao hawamjui Mungu.

6. “Kuongezeka haraka” inatumiwa kuonyesha tabia duni ya watu.

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 197)

Hali ya Mungu kupata mwili imesababisha mawimbi mazito katika dini na madhehebu yote, “imeparaganya” mpangilio wa awali wa jamii ya kidini, na imetikisa mioyo ya wale wanaotamani sana kujitokeza kwa Mungu. Ni nani asiyeabudu? Nani hatamani kumwona Mungu? Mungu amekuwa miongoni mwa wanadamu kwa miaka mingi sana, lakini mwanadamu kamwe hajawahi kutambua. Leo, Mungu Mwenyewe amejitokeza, na Ameonyesha utambulisho Wake kwa watu—inawezekanaje hii isiupatie moyo wa mwanadamu furaha? Mungu aliwahi kushiriki furaha na huzuni pamoja na mwanadamu, na leo Ameunganika tena na mwanadamu, na kushiriki visa vya muda uliopita pamoja naye. Baada ya kutoka Uyahudi, watu hawakuweza kupata alama Yake yoyote. Wanatamani kukutana tena na Mungu, bila kujua kwamba leo wamekutana Naye tena, na kuungana Naye tena. Inawezekanaje hii isiamshe mawazo ya jana? Siku kama ya leo miaka elfu mbili iliyopita, Simoni mwana wa Yona, uzao wa Wayahudi, alimtazama Yesu Mwokozi, alikula meza moja pamoja Naye, na baada ya kumfuata kwa miaka mingi alihisi kumpenda sana: Alimpenda sana kwa dhati, alimpenda sana Bwana Yesu. Watu wa Uyahudi hawakujua chochote kuhusu vile mtoto huyu mwenye nywele za dhahabu, Aliyezaliwa katika hori la ng’ombe, Alikuwa ni sura ya kwanza ya Mungu kupata mwili. Wote walidhani kwamba Alikuwa ni mmoja wao, hakuna aliyedhani kwamba Yupo tofauti nao—watu wangewezaje kumtambua Yesu wa desturi na wa kawaida kabisa? Watu wa Uyahudi walidhani kwamba alikuwa ni mtoto wa Kiyahudi wa wakati huo. Hakuna aliyemtazama kama Mungu mwenye upendo, na watu hawakufanya chochote isipokuwa kufanya maombi bila kutambua, wakiomba Awape neema nyingi na maradufu, na amani, na furaha. Walijua tu kwamba, kama milionea, Alikuwa na kila kitu ambacho mtu angetamani kuwa nacho. Lakini watu hawakumchukulia kama mtu ambaye Alikuwa mpendwa; watu wa wakati huo hawakumpenda, na walimpinga tu, na walifanya maombi Kwake yasiyokuwa na mantiki, na Hakuwahi kupinga, Aliendelea kutoa neema kwa mwanadamu, ingawa mwanadamu hakumjua. Hakufanya chochote isipokuwa kwa kimya kumpatia mwanadamu wema, upendo, na huruma, na zaidi, Alimpatia mwanadamu njia mpya ya kutenda, kumwongoza mwanadamu kutoka katika vifungo vya sheria. Mwanadamu hakumpenda, alimhusudu tu na kutambua “talanta Zake za kipekee.” Inawezekanaje mwanadamu kipofu kujua jinsi Yesu Mwokozi alipitia mateso makubwa Alipokuja miongoni mwa wanadamu? Hakuna aliyejali shida Zake, hakuna mtu aliyejua upendo Wake kwa Mungu Baba, na hakuna ambaye angejua upweke Wake; ingawa Maria alikuwa mama Yake wa kumzaa, angewezaje kujua mawazo yaliyopo moyoni mwa Bwana Yesu mwenye huruma? Nani alijua mateso yasiyoweza kutamkika Aliyoyapitia Mwana wa Adamu? Baada ya kumwomba watu wa kipindi hicho walimweka nyuma ya akili zao, na kumtupa nje Akizungukazunguka mitaani, siku baada ya siku, mwaka baada ya mwaka, na kwenda bila mwelekeo kwa miaka mingi hadi Alipofikisha miaka thelathini na mitatu, miaka ambayo ilikuwa mirefu pia mifupi. Watu walipomhitaji, walimwalika nyumbani mwao wakiwa na nyuso za tabasamu, wakijaribu kumwomba kitu—na baada ya kuwa Ametoa mchango wake kwao, walimsukuma mara moja nje ya mlango. Watu walikula kile Alichokitoa mdomoni Mwake, walikunywa damu Yake, walifurahia neema Aliyowapatia, lakini bado walimpinga, maana hawakujua nani aliwapa uhai walionao. Hatimaye, walimsulubisha msalabani, lakini bado Hakutoa hata sauti. Hata leo, bado Anabakia kimya. Watu wanakula mwili Wake, wanakunywa damu Yake, wanakula chakula Anachowatengenezea, na wanapita njia Aliyofungua kwa ajili yao, lakini bado wanakusudia kumkataa, kimsingi wanamchukulia Mungu ambaye Amewapatia maisha yao kama adui, na badala yake wanawachukulia wale ambao ni watumwa kama wao kama Anavyofanya Baba wa mbinguni. Katika hili, je, hawampingi kwa makusudi? Yesu aliwezaje kufa msalabani? Je, mnajua? Je, Hakusalitiwa na Yuda, ambaye alikuwa karibu kabisa Naye, na akamla, akamnywa, na akamfurahia? Je, Yuda hakumsaliti Yesu kwa sababu Alikuwa tu mwalimu wa kawaida Asiye na umuhimu? Ikiwa watu walikuwa wameona kwamba Yesu alikuwa si wa kawaida kabisa, na Ambaye Alitoka mbinguni, wangewezaje kumsulubisha msalabani Akiwa hai kwa masaa ishirini na nne, hadi Alipoishiwa na pumzi yote katika mwili wake? Nani awezaye kumjua Mungu? Watu hawafanyi chochote isipokuwa kumfurahia Mungu kwa tamaa isiyotosheka, lakini hawajawahi kumjua. Walipewa inchi na wamechukua maili, na wanamfanya “Yesu” kutii kabisa amri zao, na maelekezo yao. Ni nani ambaye ameonyesha huruma kwa huyu Mwana wa Adamu, Ambaye hana mahali pa kuweka kichwa Chake? Ni nani ambaye amewahi kufikiria kushikana mikono Naye kukamilisha agizo la Mungu Baba? Ni nani amewahi kumuwaza? Ni nani mbaye amewahi kuyajali matatizo Yake? Bila upendo hata kidogo, mwanadamu anamvuta nyuma na mbele; mwanadamu hajui nuru na uhai wake unatoka wapi na hafanyi chochote isipokuwa kupanga kwa siri jinsi ya kumsulubisha tena “Yesu” wa miaka elfu mbili iliyopita, ambaye amepitia maumivu miongoni mwa wanadamu. Je, “Yesu” anawatia watu moyo kuwa na chuki ya namna hiyo? Je, yote Aliyoyafanya yamesahaulika zamani? Chuki ambayo ilichanganyika kwa maelfu ya miaka itaibuka tena juu. Nyinyi mfano wa Wayahudi! Ni lini “Yesu” amekuwa adui yenu, hadi mmchukie kiasi hicho? Amefanya mengi na kuzungumza mengi—je hakuna chochote chenye manufaa kwenu? Ameyatoa maisha Yake kwenu bila kuomba kurudishiwa kitu chochote, Amejitoa mzima kwenu—kweli bado mnataka kumla Akiwa mzima? Amejitoa kwenu kikamilifu bila kuacha kitu chochote, bila kufurahia utukufu wa kidunia, wema miongoni mwa wanadamu, na upendo miongoni mwa wanadamu, au baraka zote miongoni mwa wanadamu. Watu ni wabinafsi sana Kwake, hajawahi kufurahia utajiri wote wa duniani, Amejitoa kikamilifu, moyo wa upendo wa dhati kwa mwanadamu, Amejirithisha mzima kwa mwanadamu—ni nani ambaye amemfanyia wema? Ni nani aliyewahi kumpatia faraja? Mwanadamu amemjazia mashinikizo yote, balaa yote amempatia Yeye, shida zote mbaya Alizozipitia ni mwanadamu amempatia Yeye, anamtupia lawama kwa uonevu wote, na Amezikubali kimyakimya. Je, Amewahi kumpinga mtu yeyote? Je, Amewahi kuomba fidia hata kidogo kutoka kwa mtu yeyote yule? Ni nani amewahi kumwonyesha huruma yoyote? Kama watu wa kawaida, ni nani miongoni mwenu ambaye hajawahi kuwa na kipindi cha utotoni chenye mapenzi ya dhati? Ni nani ambaye hajawahi kuwa na ujana wa kupendeza? Ni nani ambaye hana joto la wapendwa? Ni nani ambaye hana upendo wa rafiki wa karibu? Ni nani ambaye haheshimiwi na wengine? Ni nani ambaye hana familia yenye upendo? Ni nani ambaye hana faraja ya wandani wao? Je, Amekwishawahi kufurahia moja ya haya? Ni nani ambaye amewahi kumtendea wema hata kidogo? Ni nani ambaye amekwishawahi kumpatia faraja hata kidogo? Ni nani ambaye amekwishawahi kumwonyesha angalau maadili hata kidogo ya kibinadamu? Ni nani ambaye amewahi kuwa mvumilivu Kwake? Ni nani ambaye amewahi kuwa pamoja naye katika nyakati za shida? Ni nani ambaye amewahi kupitia maisha ya shida pamoja Naye? Mwanadamu bado hajaacha kumwomba Yeye; anapeleka tu maombi Kwake bila hata haya, kana kwamba kuja katika ulimwengu wa mwanadamu, Alipaswa kuwa ng’ombe au farasi wake, na Alipaswa kumpatia mwanadamu kila kitu chake; Asipofanya hivyo, mwanadamu hatamsamehe, hatamtendea vizuri, hatamwita Mungu, na hatamheshimu kwa kiwango cha juu. Mwanadamu ni katili sana katika mtazamo wake kwa Mungu, kana kwamba yupo ili kumtesa Mungu hadi kifo, ni baada ya hapo tu ndipo anapunguza maombi yake kwa Mungu; kama sivyo, mwanadamu hatapunguza kiwango cha matakwa yake kwa Mungu. Inawezekanaje mwanadamu kama huyu asidharauliwe na Mungu? Je, hili si janga la siku hizi? Dhamiri ya mwanadamu haionekani popote. Anasema tu atalipa upendo wa Mungu, lakini anamchanachana Mungu na kumtesa hadi kifo. Je, hii sio “mbinu ya siri” kwa imani yake kwa Mungu, iliyorithishwa kutoka kwa mababu zake? Hakuna mahali ambapo huwezi kuwakuta “Wayahudi,” na leo bado wanafanya kazi ile ile, bado wanafanya kazi ile ile ya kumpinga Mungu, na bado wanaamini kwamba wanamwinua Mungu juu? Inawezekanaje macho ya mwanadamu yamjue Mungu? Inawezekanaje mwanadamu, anayeishi katika mwili, kumchukulia Mungu kama Mungu mwenye mwili ambaye Amekuja kutoka katika Roho? Ni nani miongoni mwa wanadamu anaweza kumjua? Ukweli upo wapi miongoni mwa wanadamu? Haki ya kweli ipo wapi? Ni nani anayeweza kuijua tabia ya Mungu? Ni nani anayeweza kushindana na Mungu mbinguni? Haishangazi kwamba, Alipokuwa miongoni mwa wanadamu, hakuna aliyemjua Mungu, na amekataliwa. Inawezekanaje mwanadamu kuvumilia uwepo wa Mungu? Anawezaje kuvumilia kuruhusu mwanga kuondosha giza la ulimwengu? Je, hii yote si kujitoa kwa heshima kwa mwanadamu? Je, huku sio kuingia adilifu kwa mwanadamu? Je, kazi ya Mungu haijajikita katika kuingia kwa mwanadamu? Ningependa muunganishe kazi ya Mungu na kuingia kwa mwanadamu, na kurekebisha uhusiano kati ya mwanadamu na Mungu, na kufanya majukumu ambayo yanapaswa kufanywa na mwanadamu kwa uwezo wako wote. Kwa njia hii, kazi ya Mungu hatimaye itafikia mwisho, ikiwa ni pamoja na utukufu Wake!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (10)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 198)

Leo, Ninafanya kazi miongoni mwa watu wateule wa Mungu walio Uchina kufichua tabia zao zote za uasi na kuufunua ubaya wao wote, na hili linatia muktadha wa kusema kila Ninachotaka kusema. Baadaye Nitafanya hatua nyingine ya kazi ya kuushinda ulimwengu wote. Nitatumia hukumu Yangu kwenu kuhukumu udhalimu wa kila mtu duniani kote kwa sababu ninyi watu ndio wawakilishi wa waasi miongoni mwa wanadamu. Wasiojikakamua watakuwa foili[a] na vyombo vya kuhudumu tu, ila watakaojikakamua watatumika vizuri. Ni kwa nini Ninasema watakuwa foili? Ni kwa sababu maneno na kazi Yangu ya sasa vinalenga usuli wenu na kwa sababu mmekuwa wawakilishi na vielelezo vya uasi miongoni mwa wanadamu. Baadaye Nitapeleka maneno haya yanayowashinda kwa nchi za kigeni na kuyatumia kuwashinda watu wa huko, ila hutakuwa umeyafaidi. Je, hilo halitakufanya foili? Tabia potovu za wanadamu wote, matendo ya uasi wa mwanadamu, maumbile na sura mbaya za mwanadamu, zimeratibiwa zote katika maneno yanayotumiwa kuwashinda nyinyi. Baadaye Nitayatumia maneno haya kuwashinda watu wa kila taifa na kila dhehebu kwa sababu nyinyi ni mfano, kigezo. Hata hivyo, Sikupanga kuwaacha kwa makusudi; ukikosa kufanya vizuri katika utafutaji wako na kwa hivyo unathibitisha kuwa asiyeponyeka, hautakuwa tu chombo cha huduma na foili? Wakati mmoja Nilisema kwamba hekima Yangu hutumiwa kutegemea njama za Shetani. Kwa nini Nilisema hilo? Je, huo si ukweli unaounga mkono Ninachosema na kufanya wakati huu? Kama huwezi kuchukua hatua, kama hujakamilishwa lakini badala yake unaadhibiwa, je, hutakuwa foili? Labda umeteseka sana katika wakati wako, lakini sasa bado huelewi chochote; hujui kila kitu kuhusu uzima. Ingawa umeadhibiwa na kuhukumiwa, hujabadilika kamwe na ndani yako kabisa hujapata uzima. Wakati wa kutathmini kazi yako utakapofika, utapitia majaribio makali kama moto na hata majonzi makuu zaidi. Moto huu utageuza nafsi yako yote kuwa majivu. Kama mtu asiyekuwa na uzima, mtu asiye na aunsi ya dhahabu safi ndani yake, mtu ambaye bado amekatalia tabia potovu ya kale, na mtu asiyeweza hata kufanya kazi nzuri ya kuwa foili, ni jinsi gani hutaweza kuondoshwa? Kazi ya kushinda ina faida gani kwa mtu aliye na thamani ya chini kuliko peni na asiyekuwa na uzima? Wakati huo ufikapo, siku zenu zitakuwa ngumu zaidi kuliko za Nuhu na Sodoma! Maombi yenu hayatawasaidia wakati huo. Mara tu kazi ya wokovu ikiisha, utaanzaje tena kutubu? Mara tu kazi ya wokovu itakuwa imefanywa, hakutakuwa tena na kazi ya wokovu. Kitakachokuwepo ni mwanzo wa kazi ya kuadhibu uovu. Wewe hupinga, huasi, na hufanya mambo unayojua ni maovu. Je, wewe sio shabaha ya adhabu kali? Ninakuelezea hili wazi leo. Ukichagua kutosikia, wakati maafa yakufike baadaye, je, hautakuwa umechelewa kama utaanza wakati huo tu kuhisi majuto na kuanza kuamini? Nakupa nafasi ya kutubu leo, lakini wewe hauko radhi kufanya hivyo. Unataka kungoja kwa muda gani? Mpaka siku ya kuadibu? Sikumbuki dhambi zako za zamani leo; Nakusamehe tena na tena, kugeuka kutoka upande wako mbaya kutazama tu upande wako mzuri, kwa sababu maneno na kazi Yangu yote ya sasa yanatakiwa kukuokoa wewe na sina nia mbaya kwako. Lakini unakataa kuingia; huwezi kutambua mema kutoka kwa mabaya na hujui namna ya kufurahia wema. Je, mtu wa aina hii hanuii tu kungoja ile adhabu na malipo yenye haki?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (1)

Tanbihi:

a. “Foili” Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 199)

Musa alipougonga mwamba, na maji yaliyokuwa yametolewa na Yehova yakaruka, ilikuwa ni kwa sababu ya imani yake. Daudi alipocheza kinubi kwa kunisifu Mimi, Yehova—moyo wake ukiwa umejaa furaha—ilikuwa ni kwa sababu ya imani yake. Ayubu alipowapoteza wanyama wake waliojaa kote milimani na mali nyingi sana, na mwili wake kujawa na majipu mabaya, ilikuwa ni kwa sababu ya imani yake. Alipoweza kusikia sauti Yangu, Yehova, na kuuona utukufu Wangu, Yehova, ilikuwa ni kwa sababu ya imani yake. Kwamba Petro aliweza kumfuata Yesu Kristo, ilikuwa ni kwa imani yake. Kwamba Alitundikwa misumari msalabani kwa ajili Yangu na kutoa ushahidi mtukufu, pia ilikuwa kwa imani yake. Yohana alipoona mfano wa utukufu wa Mwana wa Adamu, ilikuwa kwa imani yake. Alipoona maono ya siku za mwisho, yote yalikuwa zaidi kwa sababu ya imani yake. Sababu ya yanayodaiwa kuwa mataifa mengi yasiyo ya Kiyahudi kupata ufunuo Wangu, na yakajua kwamba Nimerudi katika mwili kufanya kazi Yangu miongoni mwa wanadamu, pia ni kwa sababu ya imani yao. Wale wote wanaogongwa na maneno Yangu makali na bado wanatulizwa nayo na wanaookolewa—hawajafanya hivyo kwa sababu ya imani yao? Watu wamepokea vitu vingi sana kupitia imani. Kile ambacho wao hupokea sio baraka kila mara—kuhisi aina ya furaha na shangwe ambayo Daudi alihisi, au kuwa na maji yaliyotolewa na Yehova kama alivyofanya Musa. Kwa mfano, Ayubu alibarikiwa na Yehova kwa sababu ya imani yake, lakini pia alipitia maafa. Kama utapokea baraka au kupatwa na baa, yote ni matukio yaliyobarikiwa. Bila imani, hungeweza kupokea hii kazi ya kushinda, sembuse kuyaona matendo ya Yehova yanayoonyeshwa mbele ya macho yako leo. Hungeweza kuona, sembuse kuweza kupokea. Mabaa haya, maafa haya, na hukumu yote—kama haya hayangekufika, je, ungeweza kuona matendo ya Yehova leo? Leo hii ni imani inayokuruhusu kushindwa, na kushindwa ndiko kunakufanya uamini kila tendo la Yehova. Ni kwa sababu tu ya imani unapokea kuadibu na hukumu ya aina hii. Kupitia kuadibu na hukumu hizi, umeshindwa na kukamilishwa. Bila aina hii ya kuadibu na hukumu upokeayo leo hii, imani yako ingekuwa bure, kwa sababu humtambui Mungu; haijalishi unamwamini kiasi gani, imani yako bado itakuwa maonyesho matupu yasiyokuwa na misingi katika uhalisi. Ni baada tu ya kupokea aina hii ya kazi ya kushinda inayokufanya mtiifu kabisa ndipo imani yako inakuwa kweli na inayotegemewa na roho yako kumrudia Mungu. Japo umehukumiwa na kulaaniwa sana kwa sababu ya hili neno “imani,” una imani ya kweli, na unapokea kitu cha kweli zaidi, halisi zaidi, na chenye thamani zaidi. Hii ni kwa sababu ni katika harakati ya hukumu tu ndipo unaona hatima ya viumbe wa Mungu; ni katika hukumu hii ndio unapata kuona kuwa Muumba anapaswa kupendwa; ni katika kazi kama hiyo ya kushinda ndio unapata kuona mkono wa Mungu; ni katika kushinda huku unapata kutambua kwa ukamilifu maisha ya mwanadamu; ni katika kushinda huku unapata kujua njia ya haki ya maisha ya mwanadamu na kufahamu maana ya kweli ya “mwanadamu”; ni kupitia tu huku kushinda ndiko unaweza kuona tabia ya haki ya mwenye Uweza na uso Wake mzuri na mtukufu. Ni katika kazi hii ya kushinda ndiko unaweza kujifunza kuhusu asili ya mwanadamu na kufahamu “historia isiyokufa” ya mwanadamu; ni katika kushinda huku ndiko unapata kufahamu mababu za wanadamu na asili ya upotovu wa mwanadamu; ni katika kushinda huku ndio unapokea furaha na starehe pamoja na kuadibu, nidhamu, na maneno ya kuonya kutoka kwa Muumba kwa wanadamu ambao Aliwaumba; katika kazi hii ya kushinda, ndipo unapokea baraka na majanga ambayo mwanadamu anapaswa kupokea…. Je, haya yote si kwa ajili ya hiyo imani yako ndogo? Je, baada ya kuvipata vitu hivi vyote imani yako haijakua? Hujapata kiwango kikubwa ajabu? Hujasikia tu maneno ya Mungu na kuona hekima ya Mungu, lakini wewe binafsi umepitia pia kila hatua ya kazi. Labda utasema kuwa usingekuwa na imani, basi usingepata aina hii ya kuadibu au aina hii ya hukumu. Ila unapaswa kufahamu kuwa bila imani, usingeweza tu kupokea aina hii ya kuadibu na ulinzi kutoka kwa mwenye Uweza, bali pia daima ungepoteza fursa ya kumwona Muumba. Usingejua asili ya wanadamu na kufahamu umuhimu wa maisha ya mwanadamu. Japo mwili wako utakufa na roho yako kuondoka, bado hutayafahamu matendo yote ya Muumba. Aidha hutafahamu kuwa Muumba alifanya kazi kubwa kiasi hicho duniani baada ya kuwaumba wanadamu. Kama mmojawapo wa hawa wanadamu Aliowaumba, je, uko tayari kutumbukia gizani kiasi hiki bila fahamu na kukumbana na adhabu ya milele? Ukijitenga na kuadibu na hukumu ya sasa, utapatana na kitu gani? Je, unafikiri ukishajitenga na hukumu ya sasa, utaweza kuepukana na haya maisha magumu? Je, si kweli kwamba ukiondoka “mahala hapa,” utakachokipata ni mateso machungu au majeraha kutoka kwa ibilisi? Je, waweza kukumbana na mchana na usiku zisizostahimilika? Je, unafikiri kwamba kwa kuepuka hukumu leo, unaweza kukwepa milele yale mateso ya siku zijazo? Ni kitu gani kitakukumba? Inaweza kuwa paradiso ya duniani unayoitarajia? Unafikiri unaweza kuepuka kuadibu kwa milele kwa baadaye kwa kuukimbia uhalisi kama ufanyavyo? Baada ya leo, je, utawahi kuweza kuipata fursa na baraka kama hii tena? Je, utapata fursa na baraka utakapokuwa umekumbwa na misukosuko? Je, utapata fursa na baraka wanadamu wote waingiapo katika pumziko? Maisha yako ya furaha ya sasa na hiyo familia yako ndogo yenye amani—vyaweza kuwa kibadala cha hatima yako? Iwapo una imani ya kweli, na iwapo unafaidi pakubwa kwa sababu ya imani yako, basi hayo yote ndiyo—wewe kiumbe—unapaswa kufaidi na vilevile kile ambacho ulipaswa kuwa nacho. Aina hii ya kushinda ndiyo ya faida zaidi kwa imani na maisha yako.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (1)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 200)

Leo, unapaswa kuelewa namna ya kushindwa, na jinsi watu wanavyofanya baada ya kushindwa. Unaweza kusema umeshashindwa, lakini unaweza kutii hata kufa? Unapaswa uwe na uwezo wa kufuata hadi mwisho kabisa bila kujali kama kuna matumaini yoyote, na hupaswi kupoteza imani kwa Mungu bila kujali mazingira. Mwishowe, unapaswa kutimiza hali mbili za ushuhuda: ushuhuda wa Ayubu—utii hata kifo—na ushuhuda wa Petro—upendo mkuu wa Mungu. Kwa upande mmoja, unapaswa kuwa kama Ayubu: Hakuwa na mali hata kidogo, na alisumbuliwa na maumivu ya mwili, lakini hakulikana jina la Yehova. Huu ulikuwa ushuhuda wa Ayubu. Petro aliweza kumpenda Mungu hadi kifo. Alipokufa—alipoangikwa msalabani—bado alimpenda Mungu; hakufikiria juu ya matarajio yake mwenyewe au kufuatilia mambo yaliyo makuu au fikra za anasa, na alitafuta tu kumpenda Mungu, na kutii mipango yote ya Mungu. Hicho ndicho kiwango unachopaswa kutimiza kabla hujahesabiwa kuwa na ushuhuda, kabla hujawa mtu ambaye amefanywa mkamilifu baada ya kushindwa. Leo, ikiwa watu wangekuwa wanajua kabisa hulka na hadhi yao, je, bado wangetafuta matarajio yao na matumaini yao? Unachopaswa kujua ni hiki: Bila kujali kama Mungu atanifanya mkamilifu, ni lazima nimfuate Mungu; kila kitu anachofanya sasa ni chema na kinafanywa kwa ajili yangu, na ili tabia yetu iweze kubadilika na tuweze kuepukana na ushawishi wa Shetani, kuturuhusu kuzaliwa katika nchi ya uchafu na hata hivyo kuepukana na uchafu, kuondoa uchafu na ushawishi wa Shetani, kutuwezesha kuacha nyuma ushawishi wa Shetani. Bila shaka, hiki ndicho unachotakiwa kuwa nacho, lakini kwa Mungu ni ushindi tu, ili watu wawe na azimio la kutii, na waweze kutii mipango yote ya Mungu. Kwa njia hii, mambo yatakamilishwa. Leo, watu wengi tayari wamekwishashindwa, lakini ndani yao bado kuna mengi ambayo ni ya uasi na ukaidi. Kimo cha kweli cha watu bado ni kidogo sana, na wao huwa na nguvu kamili ikiwa kuna matumaini na matarajio, kama hayapo, wanakuwa na mitazamo hasi, na hata wanafikiria kuhusu kumwacha Mungu. Na watu hawana shauku kuu ya kutafuta kuishi kulingana na maisha ya ubinadamu wa kawaida. Hilo halitafaulu. Hivyo, bado lazima Nizungumze juu ya ushindi. Kwa kweli, ukamilifu hutokea wakati mmoja na ushindi: Unaposhindwa, matokeo ya kwanza ya kufanywa mkamilifu pia yanatimizwa. Panapokuwa na tofauti kati ya kushindwa na kufanywa mkamilifu, ni kulingana na kiwango cha mabadiliko kwa watu. Kushindwa ni hatua ya kwanza ya kufanywa mkamilifu, na haimaanishi kwamba wamefanywa wakamilifu kabisa, wala kuthibitisha kwamba wamepatwa na Mungu kabisa. Baada ya watu kushindwa, kunakuwa na mabadiliko fulani katika tabia yao, lakini mabadiliko hayo ni pungufu sana yakilinganishwa na mabadiliko ya watu ambao wamepatwa kabisa na Mungu. Leo, kile kinachofanywa ni kazi ya mwanzo ya kuwafanya watu kuwa wakamilifu—kuwashinda—na kama huwezi kutimiza kushindwa, basi hutaweza kuwa na uwezo wa kufanywa mkamilifu na kupatwa kabisa na Mungu. Utapata tu maneno machache ya kuadibu na hukumu, lakini hayatakuwa na uwezo wa kuubadilisha kabisa moyo wako. Hivyo utakuwa mmoja wa wale ambao wameondolewa; haitakuwa tofauti na kutazama tu karamu ya gharama mezani lakini huli. Je, hilo si la huzuni? Na hivyo, ni lazima utafute mabadiliko: Kama ni kushindwa au kufanywa mkamilifu, yote yanahusiana na kama kuna mabadiliko ndani yako, na kama wewe ni mtii au la, na hili linaamua kama unaweza kupatwa na Mungu au la. Jua kwamba “kushindwa” na “kufanywa mkamilifu” yamejikita katika kiwango cha mabadiliko na utii, vilevile katika jinsi upendo wako kwa Mungu ulivyo. Kinachotakiwa leo ni kwamba uweze kufanywa mkamilifu kabisa, lakini mwanzoni ni lazima ushindwe—ni lazima uwe na ufahamu wa kutosha juu ya kuadibu na hukumu ya Mungu, lazima uwe na imani ya kufuata, na kuwa mtu ambaye anatafuta mabadiliko na matokeo kuweko. Wakati huo tu ndipo utakuwa mtu ambaye anatafuta kufanywa mkamilifu. Unapaswa kuelewa kwamba wakati wa kufanywa kuwa mkamilifu, mtashindwa, na wakati wa kushindwa mtafanywa kuwa wakamilifu. Leo, unaweza kutafuta kufanywa kuwa mkamilifu au kutafuta mabadiliko katika ubinadamu wako wa nje na maendeleo katika ubora wa tabia yako, lakini muhimu kabisa ni kwamba unaweza kuelewa kwamba kila kitu ambacho Mungu anafanya leo kina maana na ni cha manufaa: Kinakuwezesha wewe ambaye unazaliwa katika nchi ya uchafu kuepuka uchafu na kuuondoa wote, kinakuwezesha kushinda ushawishi wa Shetani na kuacha nyuma ushawishi wa giza wa Shetani—na kwa kulenga vitu hivi, unakuwa umelindwa katika nchi hii ya uchafu. Mwishowe, utaambiwa utoe ushuhuda gani? Unazaliwa katika nchi ya uchafu lakini unaweza kuwa mtakatifu, usichafuliwe na najisi tena, unamilikiwa na Shetani, lakini unaachana na ushawishi wa Shetani, na humilikiwi au kunyanyaswa na Shetani, na unaishi mikononi mwa Mwenyezi. Huu ndio ushuhuda, na thibitisho la ushindi katika vita na Shetani. Unaweza kumwacha Shetani, hufichui tabia za kishetani tena katika kile unachoishi kwa kudhihirisha, lakini badala yake unaishi kwa kudhihirisha kile ambacho Mungu alitaka mwanadamu afikie Alipomuumba mwanadamu: ubinadamu wa kawaida, urazini wa kawaida, umaizi wa kawaida, azimio la kawaida la kumpenda Mungu, na utii kwa Mungu. Huo ndio ushuhuda ambao kiumbe wa Mungu huwa nao. Unasema, “Tunazaliwa katika nchi ya uchafu, lakini kwa sababu ya ulinzi wa Mungu, kwa sababu ya uongozi Wake, na kwa sababu Ametushinda, tumejiondoa katika ushawishi wa Shetani. Kwamba tunaweza kutii leo pia ni matokeo ya kushindwa na Mungu, na sio kwa sababu sisi ni wema, au kwa sababu tunampenda Mungu kwa asili. Ni kwa sababu Mungu alituchagua, na kutujaalia, ndio tumeshindwa leo, tunaweza kuwa na ushuhuda Kwake, na tunaweza kumhudumia, kwa hiyo, pia, ni kwa sababu Alituchagua, na kutulinda, ndio tumechaguliwa na kutolewa katika miliki ya Shetani, na tunaweza kuachana na uchafu na kutakaswa katika nchi ya joka kuu jekundu.”

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (2)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 201)

Kazi ya siku za mwisho inavunja kanuni zote, bila kujali kama umelaaniwa au kuadhibiwa, maadamu tu uisaidie kazi Yangu, na una manufaa kwa kazi ya ushindi ya leo, na bila kujali kama wewe ni uzao wa Moabu au kizazi cha joka kuu jekundu, maadamu tu unatekeleza wajibu wa kiumbe wa Mungu katika hatua hii ya kazi, na kufanya kadri unavyoweza, basi matokeo yanayotarajiwa yatatimizwa. Wewe ni kizazi cha joka kuu jekundu, na ni uzao wa Moabu; kwa ujumla, wale wote walio wa mwili na damu ni viumbe wa Mungu, na waliumbwa na Muumba. Wewe ni kiumbe wa Mungu, hupaswi kuwa na chaguo lolote, na huu ndio wajibu wako. Bila shaka, leo kazi ya Muumba imeelekezwa kwa ulimwengu mzima. Bila kujali wewe ni uzao wa nani, zaidi ya yote, nyinyi ni mojawapo wa viumbe wa Mungu, ninyi—uzao wa Moabu—ni sehemu ya viumbe wa Mungu, ni vile tu nyinyi mna thamani ya chini. Kwa kuwa, leo, kazi ya Mungu inatekelezwa miongoni mwa viumbe wote, na imelenga ulimwengu mzima, Muumba yuko huru kuchagua watu, masuala, au vitu vyovyote ili viweze kufanya kazi Yake. Hajali wewe ni uzao wa nani; maadamu tu wewe ni mmoja wa viumbe wake, na maadamu una manufaa katika kazi Yake—kazi ya ushindi na ushuhuda—Ataifanya kazi Yake ndani yako bila haya yoyote. Hili linaharibu kabisa dhana za watu za kitamaduni, ambayo ni kwamba Mungu hatawahi kamwe kufanya kazi miongoni mwa Mataifa, hususan wale ambao wamelaaniwa na ambao ni duni; kwa maana wale ambao wamelaaniwa, uzao wao wa baadaye nao utaendelea kulaaniwa milele, hawatakuwa na nafasi ya wokovu; Mungu hatawahi kamwe kushuka na kufanya kazi katika nchi ya Mataifa, na Hatakanyaga mguu Wake katika nchi yenye uchafu, maana Yeye ni mtakatifu. Dhana hizi zote zimevunjwa na kazi ya Mungu katika siku za mwisho. Jua kwamba Mungu ni Mungu wa viumbe vyote, ni mtawala wa mbingu na nchi na vitu vyote, na si Mungu wa watu wa Israeli pekee. Hivyo, kazi hii katika nchi ya Uchina ni ya umuhimu mkubwa, na unadhani haitaenea miongoni mwa mataifa yote? Ushuhuda mkubwa wa siku za usoni hautakomea Uchina tu; ikiwa Mungu angewashinda nyinyi tu, je, mapepo wangeshawishika? Hawaelewi maana ya kushindwa, au nguvu kubwa ya Mungu, na ni pale tu ambapo wateuliwa wa Mungu katika nchi yote watakapoona matokeo ya mwisho ya kazi hii ndipo viumbe wote watakuwa wameshindwa. Hakuna ambao wapo nyuma sana au waovu sana kuliko uzao wa Moabu. Iwapo tu watu hawa wataweza kushindwa—wale ambao ni waovu sana, ambao hawakumtambua Mungu au kuamini kwamba kuna Mungu wameshindwa, na kumtambua Mungu katika vinywa vyao, wakimtukuza, na wanaweza kumpenda—ndipo huu utakuwa ushuhuda wa ushindi. Ingawa wewe si Petro, mnaishi kwa kudhihirisha mfano wa Petro, mnaweza kuwa na ushuhuda wa Petro, na ushuhuda wa Ayubu, na huu ni ushuhuda mkubwa sana. Hatimaye utasema: “Sisi sio Waisraeli, bali ni uzao wa Moabu uliotelekezwa, sisi sio Petro, ambaye hatuwezi kuwa na ubora wa tabia yake, wala sisi sio Ayubu, na hata hatuwezi kujilinganisha na azimio la Paulo la kuteseka kwa ajili ya Mungu na kujitoa kikamilifu kwa Mungu, na sisi tupo nyuma sana, na hivyo, hatustahili kufurahia baraka za Mungu. Mungu bado Ametuinua leo; kwa hiyo tunapaswa kumridhisha Mungu, na ingawa tuna ubora wa tabia au sifa haba, tupo radhi kumridhisha Mungu—tuna azimio hili. Sisi ni uzao wa Moabu, na tulilaaniwa. Hili lilitangazwa na Mungu, na wala hatuwezi kuibadilisha, lakini kuishi kwetu kwa kudhihirisha na maarifa yetu yanaweza kubadilika, na tumeazimia kumridhisha Mungu.” Utakapokuwa na azimio hili, itathibitisha kwamba umeshuhudia kuwa umeshindwa.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (2)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 202)

Matokeo ya kutimizwa kutoka kwa kazi ya kushinda kimsingi ni kwa ajili ya mwili wa mwanadamu kuacha kuasi, yaani, ili fikira za mwanadamu zipate ufahamu mpya wa Mungu, moyo wake umtii Mungu kabisa, na aamue kuwa wa Mungu. Watu hawahesabiwi kuwa walioshindwa wakati ambapo ambapo mwenendo ama mwili wao unapobadilika; wakati ambapo fikira, ufahamu, na utambuzi wa mwanadamu unabadilika, ambayo ni kusema, wakati ambapo mwelekeo wako wote wa akili unabadilika—huo utakuwa wakati ambapo umeshindwa na Mungu. Ukiamua kutii na kupata fikira mpya, pale ambapo huingizi mawazo na nia zako katika maneno na kazi ya Mungu, na wakati ubongo wako unaweza kufikiri kwa njia ya kawaida, yaani, unapoweza kujitolea kwa Mungu kwa moyo wako wote—huyu ni mtu aliyeshindwa kabisa. Katika ulimwengu wa dini, watu wengi huteseka pakubwa maishani mwao mwote, kwa kuihini miili yao au kuubeba msalaba wao, au hata kuteseka na kustahimili hadi pumzi zao za mwisho! Wengine huwa wanafunga hadi siku ya kifo chao. Katika maisha yao yote wanajinyima chakula kizuri na mavazi mazuri, wakisisitiza mateso tu. Wanaweza kuihini miili yao na kuinyima miili yao. Uwezo wao wa kustahimili mateso unastahili sifa. Ila fikira zao, mawazo yao, mielekeo yao ya kiakili, na kwa hakika asili yao ya kale, havijashughulikiwa hata kidogo. Hawana ufahamu wowote wa kweli kujihusu. Picha ya Mungu akilini mwao ni ile ya kijadi na ya kidhahania, Mungu asiye yakini. Uamuzi wao wa kuteseka kwa ajili ya Mungu unaletwa na azma na asili yao chanya. Hata ikiwa wanamwamini Mungu, hawamfahamu Mungu wala kuyafahamu mapenzi Yake. Wanamfanyia Mungu kazi na kumtesekea Mungu kama vipofu. Hawawekei utambuzi thamani yoyote na hawajishughulishi na jinsi ambayo huduma yao inatimiza mapenzi ya Mungu kwa kweli. Aidha hawajui jinsi ya kutimiza ufahamu kuhusu Mungu. Mungu wanayemhudumia si Mungu katika sura Yake ya asili, ila ni Mungu waliyejifikiria, Mungu waliyemsikia, au Mungu wa kihadithi wanayemsoma katika maandiko. Kisha wanatumia mawazo yao dhahiri na mioyo yao ya kiungu kumtesekea Mungu na kuifanya kazi ambayo Mungu anapaswa kufanya. Huduma yao haiko sahihi, kiasi kwamba hakuna yeyote kati yao anayeweza kuhudumu kulingana na mapenzi ya Mungu. Haijalishi wako radhi kiasi gani kuteseka, mitazamo yao asilia ya huduma na picha ya Mungu akilini mwao havibadiliki kwani hawajapitia hukumu ya Mungu na kuadibu na usafishaji Wake na ukamilifu, na kwa sababu hakuna yeyote aliyewaongoza na ukweli. Japo wanasadiki kwa Yesu Mwokozi, hamna kati yao aliyewahi kumwona Mwokozi. Wamemsikia tu kwa hadithi na uvumi. Hivyo huduma yao ni sawa na kuhudumu mara mojamoja macho yao yakiwa yamefungwa kama kipofu anayemhudumia baba yake. Ni nini kinaweza kupatikana kutokana na huduma kama hiyo? Na ni nani anaweza kuikubali? Huduma yao haibadiliki kamwe toka mwanzo hadi mwisho. Wanapokea mafunzo ya kibinadamu na kukita huduma yao katika uasili wao na kile wanachokipenda wao. Hili laweza kuzalisha faida gani? Hata Petro, aliyemwona Yesu, hakujua jinsi ya kumhudumia Mungu kwa njia inayotimiza mapenzi ya Mungu. Ni katika uzee wake ndipo alipopata ufahamu. Hili linaonyesha nini kuhusu wanadamu vipofu ambao hawajapitia ushughulikiaji na hawana upogoaji na ambao hawajawahi kupata yeyote wa kuwaongoza? Je, si huduma ya wengi miongoni mwenu leo ni kama ile ya vipofu? Wale wote ambao hawajapokea hukumu, hawajapokea upogoaji na ushughulikiaji, na hawana mabadiliko—je, wao si waliokosa kushindwa kabisa? Wana manufaa gani watu kama hao? Ikiwa fikira zako, ufahamu wako wa maisha, na ufahamu wako wa Mungu hauonyeshi mabadiliko mapya na hautoi faida hata kidogo, hutatimiza chochote kizuri katika huduma yako. Bila maono na bila ufahamu mpya wa kazi ya Mungu, huwezi kuwa mtu aliyeshindwa. Njia yako ya kumfuata Mungu itakuwa kama ile ya wale wanaoteseka na kufunga—itakuwa ya thamani ndogo! Hii ni kwa sababu kuna ushuhuda kidogo katika yale wayafanyayo ndipo Nasema huduma yao ni bure! Wanashinda maisha yao wakiteseka na kukaa gerezani; ni wastahimilivu, wenye upendo daima na wao daima hubeba msalaba, wao hukejeliwa na kukataliwa na dunia, wao hupitia kila aina ya ugumu, na ingawa wao ni watiifu hadi mwisho kabisa, bado hawajashindwa, na hawawezi kutoa ushuhuda kuhusu kushindwa.. Wameteseka si haba, ila kwa ndani hawamfahamu Mungu kabisa. Hakuna fikira zao za zamani, mawazo ya zamani, vitendo vyao, uelewa wa wanadamu, na mawazo ya wanadamu yaliyoshughulikiwa. Kamwe hakuna uelewa mpya ndani yao. Hakuna hata chembe ya ufahamu wao wa Mungu ambao ni wa kweli au ni sahihi. Wamekosa kuyaelewa mapenzi ya Mungu. Je, huku kwaweza kuwa kumhudumia Mungu? Japo ulimfahamu Mungu zamani, tuseme umeudumisha ufahamu huo hadi leo na kuendelea kukita ufahamu wako kuhusu Mungu kwenye fikira na mawazo yako bila kujali Mungu anafanya nini. Yaani, ikiwa huna ufahamu mpya na wa kweli kuhusu Mungu na ukose kutambua sura na tabia ya kweli ya Mungu. Ikiwa ufahamu wako wa Mungu bado unaongozwa na fikira za uhasama na ushirikina na bado una mawazo na fikira za mwanadamu. Ikiwa hii ndiyo hali, basi hujashindwa. Lengo langu la kukwambia maneno haya yote sasa ni kukupa fursa ya kufahamu na kutumia utambuzi huu kukuongoza katika ufahamu sahihi na mpya. Aidha yanalengwa kukuondolea mawazo ya zamani na utambuzi wa zamani ulio nao ili uweze kuwa na ufahamu mpya. Ikiwa unakula na kunywa matamshi Yangu kweli, basi ufahamu wako utabadilika kwa kiwango kikubwa. Bora tu udumishe moyo mtiifu kwa kula na kunywa matamshi ya Mungu, mtazamo wako utabadilika. Bora tu unaweza kukubali kuadibu kwa kila mara, fikira zako za zamani zitabadilika taratibu. Bora tu fikira zako za zamani zimebadilishwa kabisa na kuwa mpya, vitendo vyako vitabadilika ipasavyo. Kwa njia hii, huduma yako itaendelea kuwa yenye malengo zaidi, na itaweza kutimiza mapenzi ya Mungu. Kama unaweza kubadilisha maisha yako, ufahamu wako wa maisha ya binadamu, na mawazo yako mengi kuhusu Mungu, basi uasili wako utadidimia taratibu. Hili, na hakuna jingine ila hili, ndilo tokeo baada ya Mungu kumshinda mwanadamu; haya ndiyo mabadiliko yatakayoonekana ndani ya mwanadamu. Ikiwa katika kumwamini Mungu, yote ujuayo ni kuutiisha na kuuhini mwili wako na kustahimili na kuteseka, na hujui wazi ikiwa unachokifanya ni sawa au la, bila kujali unamfanyia nani kazi, basi vitendo kama hivi vitaletaje mabadiliko?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (3)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 203)

Kukamilishwa kuna maana gani? kushindwa kuna maana gani? Ni vigezo vipi mtu anapaswa kuwa navyo ili apate kushindwa? Na ni vigezo vipi mtu anapaswa kuwa navyo ili afanywe mkamilifu? Kushinda na kukamilisha yote yanakusudiwa kumkamilisha mwanadamu ili kwamba aweze kurejeshwa katika asili yake, na awe huru na tabia zake potovu za shetani na ushawishi wa Shetani. Huu ushindi huja mapema katika mchakato wa kumfinyanga mwanadamu, ikiwa na maana kwamba ni hatua ya kwanza ya kazi. Kukamilisha ni hatua ya pili, au hitimisho la kazi. Kila mwanadamu ni lazima apitie hali ya kushindwa; la sivyo hataweza kumfahamu Mungu na hawezi kujua kuwa kuna Mungu, yaani, hawezi kumtambua Mungu. Na iwapo mtu hamtambui Mungu, hataweza kufanywa mkamilifu na Mungu kwa sababu hatakuwa na vigezo vya kufanywa mkamilifu. Ikiwa humtambui Mungu, utawezaje kumfahamu? Utawezaje kumtafuta? Aidha, hutaweza kumshuhudia, wala kumtosheleza. Kwa hivyo, kila anayetaka kukamilishwa, hatua ya kwanza lazima iwe kupitia kazi ya kushinda. Hili ndilo sharti la kwanza. Ila, iwe ni kushinda au ukamilifu, kila moja ni lengo la mwanadamu afanyaye kazi na kubadilishwa na kazi hiyo, na kila moja ni kipengele katika kazi ya kusimamia mwanadamu. Hizi hatua mbili ndizo zinahitajika kumgeuza yeyote kuwa mtu mkamilifu; hakuna moja kati ya hizo inaweza kurukwa. Ni kweli kuwa “kushindwa” hakuonekani kuwa ni jambo zuri, ila ni kweli kuwa mchakato wa kumshinda mtu ni mchakato wa kumbadilisha. Baada ya wewe kushindwa, tabia yako potovu huenda ikawa haijafutwa kabisa, lakini utakuwa umeijua. Kupitia kazi ya kushinda, utapata kujua uduni wa ubinadamu wako, na vilevile kufahamu utovu wako wa nidhamu. Japo hutaweza kuyaacha haya au kuyabadilisha ndani ya muda mfupi wa kazi ya kushinda, utayajua baadaye. Haya yanaujenga msingi wa ukamilifu wako. Kwa hivyo kushinda na kukamilisha yote yanafanywa kumbadilisha mwanadamu, kumtoa mwanadamu tabia zake mbovu za Kishetani ili ajitolee kikamilifu kwa Mungu. Ni kwamba tu kushindwa ni hatua ya kwanza katika kubadilisha tabia ya mwanadamu na pia hatua ya kwanza ya mwanadamu kujitoa kikamilifu kwa Mungu, hatua iliyo chini ya ukamilifu. Tabia za maisha ya mtu aliyeshindwa hubadilika kiasi kidogo kuliko ya mtu ambaye amepata ukamilifu. Kushindwa na kufanywa mkamilifu ni tofauti kabisa kwa kuwa ni hatua tofauti za kazi na kwa kuwa huhitaji vigezo tofauti kutoka kwa wanadamu, huku ushindi ukiwa na vigezo vya chini na ukamilifu ukiwa na vigezo vya juu. Walio wakamilifu ni wenye haki, watu watakatifu na safi; wao ni udhihirisho wa kazi ya kusimamia wanadamu, au matokeo ya mwisho. Japo si wanadamu wasio na doa, ni watu wanaotaka kuishi maisha ya thamani. Lakini walioshindwa hukiri tu kwa vinywa vyao kuwa Mungu Yupo; wanakiri kuwa Mungu amepata mwili, kwamba neno linaonekana katika mwili, na kwamba Mungu amekuja duniani kufanya kazi ya hukumu na kuadibu watu. Aidha wanakiri kuwa hukumu na kuadibu kwa Mungu na mapigo Yake na usafishaji Wake ni faida kwa mwanadamu. Yaani, wameanza kuwa na sifa za ubinadamu, na wana ufahamu mdogo kuhusu maisha ila si bayana. Kwa maneno mengine, wameanza tu kuwa na ubinadamu. Haya ni matokeo ya kushindwa. Watu waingiapo katika njia ya ukamilifu, tabia zao za zamani zaweza kubadilishwa. Aidha, maisha yao huendelea kukua na taratibu hujitosa zaidi katika ukweli. Wanaweza kuchukia dunia na kuwachukia wale wote ambao hawafuati ukweli. Hususan hujichukia wao wenyewe, na hata zaidi ya hayo, wanajitambua vyema. Wana hiari kuishi kulingana na ukweli na hulenga kufuata ukweli. Hawako radhi kuishi katika mawazo ya bongo zao, na huchukia kujitukuza, kujisifu, na kujiinua kwa mwanadamu. Wananena kwa adabu ya hali ya juu, wanafanya mambo kwa utambuzi na hekima, ni waaminifu na watiifu kwa Mungu. Wakipitia kuadibu na hukumu, wao hawakuwi wanyonge au wasioonyesha hisia tu, bali hutoa shukrani kwa ajili ya kuadibu na hukumu zitokazo kwa Mungu. Wanaamini hawawezi kuishi bila kuadibu na hukumu ya Mungu; wanaweza kupata ulinzi Wake kupitia haya. Hawafuati imani ya amani na furaha na ya kutafuta mkate wa kuwashibisha. Wala hawafuati raha za muda za kimwili. Hili ndilo wakamilifu huwa nalo. Baada ya watu kushindwa, wao hukubali kwamba kuna Mungu. Lakini matendo yo yote ambayo huja na kukubali kuweko kwa Mungu, matendo haya ni machache ndani yao. Neno kuonekana katika mwili lina maana gani kwa kweli? Kupata mwili kuna maana gani? Ni nini ambacho Mungu mwenye mwili amefanya? Ni nini lengo na umuhimu wa kazi Yake? Baada ya kupitia kazi Yake nyingi sana, kupitia matendo Yake katika mwili, umepata nini? Ni baada tu ya kufahamu mambo haya yote ndiyo utakuwa mtu aliyeshindwa. Kama wewe utasema tu kwamba unakubali kuwa kuna Mungu, lakini huwachi kile unachopaswa kuwacha na kukosa kuacha raha za mwili ambazo unapaswa kuacha, lakini badala yake uendelee kutamani maliwazo ya mwili kama ulivyofanya daima, na ikiwa huwezi kuachilia ubaguzi wowote dhidi ya ndugu, na kuhusu utendaji mwingi rahisi huwezi kulipa stahili yako kutimiza matendo hayo, basi hilo linathibitisha wewe bado hujashindwa. Kwa hiyo, hata kama unaelewa mengi, yote itakuwa bure. Walioshindwa ni watu ambao wametimiza mabadiliko fulani ya mwanzo na kuingia kwa mwanzo. Kupitia hukumu na kuadibu kwa Mungu huwasababisha kuwa na maarifa ya mwanzo ya Mungu na ufahamu wa mwanzo wa ukweli. Hata kama kuhusu ukweli mwingi wa kina, na wa chembechembe zaidi huwezi kuingia kabisa katika uhalisi wake, unaweza kutia katika vitendo ukweli mwingi wa mwanzo katika maisha yako halisi, kama vile unaohusu raha zako za mwili au hali yako binafsi. Yote haya, bila shaka, ni kile kinachotimizwa ndani ya wale wanaopitia kushinda. Mabadiliko fulani katika tabia yanaweza pia kuonekana ndani ya walioshindwa. Kwa mfano, mavazi na unadhifu wao na maisha yao—haya yanaweza kubadilika. Mtazamo wao kuhusu kumwamini Mungu hubadilika, wao hupata uwazi kuhusu chombo cha ukimbizaji wao, na matamanio yao huongezeka. Wakati wa kushindwa, tabia yao ya maisha inaweza pia kubadilika kwa kukubaliana. Sio kwamba wao hawabadiliki kabisa. Ni vile tu mabadiliko yao ni ya juujuu, ya mwanzo, na madogo zaidi kuliko mabadiliko katika tabia na chombo cha ukimbizaji ambayo yangeonekana baada ya mtu kukamilishwa. Kama wakati wa kushindwa, tabia ya mtu haibadiliki kabisa na hapati hata ukweli kidogo, basi mtu wa aina hii huwa tu kipande cha takataka na ni bure kabisa! Watu ambao hawajashindwa hawawezi kukamilishwa! Na kama mtu hutafuta tu kushindwa, hawezi kufanywa kuwa kamili kwa ukamilifu, hata kama tabia yake ilionyesha mabadiliko fulani ya kukubaliana wakati wa kazi ya kushinda. Yeye pia atapoteza ukweli wa mwanzo aliopata. Kuna tofauti kubwa mno kati ya kiasi cha mabadiliko ya tabia ndani ya walioshindwa na waliokamilishwa. Lakini kushindwa ni hatua ya kwanza katika mabadiliko; ni msingi. Kukosa mabadiliko haya ya mwanzo ni thibitisho kwamba mtu kwa kweli hamjui Mungu kabisa kwa sababu ufahamu huu hutoka kwa hukumu, na hukumu hii ni kipengee kikuu katika kazi ya kushinda. Kwa hiyo, kila mtu aliyekamilishwa amepitia kushindwa. Ama sivyo, hangeweza labda kukamilishwa.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (4)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 204)

Leo, Nawaonya hivi kwa ajili ya kupona kwenu wenyewe, ili kazi Yangu iendelee vizuri, na ili kazi Yangu ya uzinduzi kote ulimwenguni iweze kufanyika kwa njia inayofaa na kikamilifu, ikifichua maneno Yangu, mamlaka, adhama na hukumu kwa watu wa nchi zote na mataifa. Kazi Ninayoifanya miongoni mwenu ni mwanzo wa kazi Yangu katika ulimwengu wote. Ingawa sasa ni siku za mwisho tayari, jua kwamba “siku za mwisho” ni jina tu la enzi: Kama tu vile Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema, linaashiria enzi, na linaashiria enzi nzima, badala ya mwisho wa miaka au miezi michache. Hata hivyo siku za mwisho ni tofauti kabisa na Enzi ya Neema na Enzi ya Sheria. Kazi ya siku za mwisho haifanyiki katika taifa la Israeli, lakini kati ya mataifa; ni ushindi mbele ya kiti Changu cha enzi cha watu kutoka mataifa yote na makabila yote nje ya Israeli, ili utukufu Wangu katika ulimwengu wote uweze kujaza ulimwengu na anga. Iko hivyo ili Niweze kupata utukufu mkuu, ili viumbe vyote duniani viweze kupitisha utukufu Wangu kwa mataifa yote, milele katika vizazi vyote, na viumbe vyote mbinguni na duniani viweze kuuona utukufu wote ambao Nimepata duniani. Kazi inayofanyika katika siku za mwisho ni kazi ya ushindi. Sio uongozi wa maisha ya watu wote duniani, lakini hitimisho la maisha ya milenia ya mwanadamu yasiyoangamia, ya mateso katika dunia. Matokeo yake ni kwamba kazi ya siku za mwisho haiwezi kuwa kama miaka elfu kadhaa ya kazi katika Israeli, wala haiwezi kuwa kama ile miaka kadhaa tu ya kazi katika Yuda ambayo iliendelea kwa milenia mbili mpaka kupata mwili kwa mara ya pili kwa Mungu katika mwili. Watu wa siku za mwisho hukutana tu na kuonekana tena kwa Mkombozi katika mwili, na kupokea kazi binafsi na maneno ya Mungu. Haitakuwa miaka elfu mbili kabla ya siku za mwisho hazijafika ukingoni; zi fupi, kama wakati ambao Yesu alifanya kazi ya Enzi ya Neema katika Yuda. Hii ni kwa sababu siku za mwisho ni hitimisho la nyakati nzima. Ni ukamilisho na tamatisho la mpango wa miaka elfu sita wa usimamizi wa Mungu, na kuhitimisha safari ya maisha ya mateso ya mwanadamu. Hazichukui binadamu wote hadi katika enzi mpya au kuruhusu maisha ya mwanadamu kuendelea. Hiyo haitakuwa na umuhimu wowote kwa ajili ya mpango Wangu wa usimamizi au kuwepo kwa mwanadamu. Kama mwanadamu angeendelea kwa namna hii, basi hivi karibuni wao wangeangamizwa kabisa na ibilisi, na zile nafsi za wale walio Wangu hatimaye zingeangamizwa na mikono yake. Kazi Yangu inadumu kwa miaka elfu sita tu, na Mimi niliahidi kwamba udhibiti wa yule mwovu juu ya wanadamu wote utakuwa pia si zaidi ya miaka elfu sita. Na kwa hivyo, wakati umeisha. Nami wala Sitaendelea wala kuchelewa tena: Katika siku za mwisho Nitamshinda Shetani, nami Nitaumiliki tena utukufu Wangu wote, na kurudisha nafsi zile zote zilizo Zangu duniani ili nyoyo hizi za dhiki ziweze kutoroka kutoka bahari ya mateso, na hivyo Nitakuwa nimetimiza kazi Yangu nzima duniani. Kutoka siku hii na kuendelea, kamwe Sitawahi kuwa mwili duniani, na kamwe Roho Wangu wa kudhibiti yote Hatafanya kazi tena duniani. Lakini Nitafanya jambo moja duniani: Nitamfanya tena mwanadamu, mwanadamu aliye mtakatifu, na aliye mji Wangu mwaminifu duniani. Lakini ujue kwamba Sitaiangamiza dunia nzima, wala kuangamiza ubinadamu mzima. Nitahifadhi theluthi moja iliyobaki—theluthi moja inayonipenda na imeshindwa kabisa na Mimi, na Nitaifanya theluthi hii iwe yenye kuzaa matunda na kuongezeka duniani kama Israeli walivyofanya chini ya sheria, kuwalisha kwa kondoo wengi mno na mifugo, na utajiri wote wa dunia. Mwanadamu huyu atabaki na Mimi milele, hata hivyo si mwanadamu mchafu wa kusikitisha wa leo, lakini mwanadamu ambaye ni mkusanyiko wa wale wote ambao wamepatwa na Mimi. Mwanadamu wa aina hii hataharibiwa, kusumbuliwa, au kuzungukwa na Shetani, na atakuwa mwanadamu wa pekee anayepatikana duniani baada ya ushindi Wangu juu ya Shetani. Ni wanadamu ambao leo wameshindwa na Mimi na wamepata ahadi Yangu. Na hivyo, wanadamu ambao wameshindwa katika siku za mwisho pia ndio watakaosamehewa na kupata baraka Zangu za milele. Huu utakuwa ushahidi wa pekee wa ushindi Wangu dhidi ya Shetani, na nyara za pekee za vita Vyangu na Shetani. Hizi nyara za vita zimeokolewa nami kutoka utawala wa Shetani, na ni thibitisho la pekee na matunda ya mpango Wangu wa usimamizi wa miaka elfu sita. Wao huja kutoka kila taifa na dhehebu, na kila mahali na nchi ulimwenguni mwote. Ni wa jamii tofauti, na wana lugha mbalimbali, mila na rangi ya ngozi, na huenea katika kila taifa na dhehebu la duniani, na hata kila pembe ya dunia. Hatimaye, watakuja pamoja na kuunda ubinadamu kamili, mkusanyiko wa binadamu usiofikiwa na majeshi ya Shetani. Wale miongoni mwa wanadamu ambao hawajaokolewa na kushindwa na Mimi watazama kwa kimya mpaka chini ya bahari, na watachomwa kwa moto wa kuteketeza milele. Nitamwangamiza mwanadamu huyu mzee aliye mchafu sana, kama tu vile Nilivyoangamiza wazaliwa wa kwanza na ng’ombe wa Misri, na kuacha tu Waisraeli, waliokula nyama ya mwanakondoo, kunywa damu ya mwanakondoo, na kutia alama vizingitini mwa milango yao kwa damu ya mwanakondoo. Si watu ambao wameshindwa na Mimi na ni wa jamii Yangu ndio wale pia wanaokula nyama Yangu, Mwanakondoo na kunywa damu Yangu, Mwanakondoo, na wamekombolewa na Mimi na kuniabudu Mimi? Si watu wa namna hiyo kila mara huandamwa na utukufu Wangu? Si hao wasio na nyama Yangu, Mwanakondoo tayari wamezama kimya kwa kina cha bahari? Leo mnanipinga, na leo maneno Yangu ni kama tu yale yaliyosemwa na Yehova kwa wana na wajukuu wa Israeli. Lakini ugumu katika kina cha nyoyo zenu unafanya ghadhabu Yangu kukusanya, na kuleta mateso zaidi juu ya miili yenu, hukumu zaidi juu ya dhambi zenu, na ghadhabu zaidi juu ya udhalimu wenu. Ni nani atakayeweza kusamehewa katika siku Yangu ya ghadhabu, mnaponitendea kwa namna hii leo? Udhalimu wa nani utaweza kuepuka macho Yangu ya kuadibu? Dhambi za nani zinaweza kuepuka mikono Yangu, Mwenyezi? Uasi wa nani unaweza kuhepa hukumu Yangu, Mwenyezi? Mimi, Yehova, Nasema hivyo kwenu, kizazi cha jamii ya Mataifa, na maneno Ninayosema nanyi yanashinda matamko yoyote yale ya Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema, ilhali bado nyinyi ni wagumu kuliko watu wote wa Misri. Je, si mnahifadhi ghadhabu Yangu Ninapofanya kazi kwa utulivu? Jinsi gani mnaweza kuepuka salama bila ya madhara kutoka siku Yangu, Mwenyezi?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Hakuna Aliye wa Mwili Anayeweza Kuepuka Siku ya Ghadhabu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 205)

Mnafaa kutoa kila kitu chenu kwa ajili ya kazi Yangu. Mnapaswa kufanya kazi inayonifaidi Mimi. Nataka Niwaambie kuhusu yale yote ambayo hamna ufahamu kamili kuyahusu ili muweze kupata yale yote mnayokosa kutoka Kwangu. Hata ingawa kasoro zenu ni nyingi kiasi kwamba haziwezi kuhesabika, Nina nia ya kuendelea kufanya kazi Ninayopaswa kuwa Nikifanya kwenu, kuwapa huruma Zangu za mwisho ili mpate kufaidika kutoka Kwangu, na mpate utukufu ambao hauko ndani yenu na ambao dunia haijawahi kuuona. Nimefanya kazi kwa miaka mingi sana, ilhali hakuna yeyote miongoni mwa binadamu ambaye amewahi kunijua. Nataka kuwaambia siri ambazo sijawahi kumwambia mtu yeyote yule.

Miongoni mwa binadamu, Nilikuwa roho ambaye hawakuweza kuona, Roho ambayo hawangeweza kuigusa. Kwa sababu ya hatua Zangu tatu za kazi duniani (kuumba ulimwengu, ukombozi, na kuiharibu), Naonekana miongoni mwao katika nyakati tofauti (kamwe sio hadharani) ili kutenda kazi Yangu miongoni mwa binadamu. Mara ya kwanza Nilipokuja miongoni mwa binadamu ilikuwa katika Enzi ya Ukombozi. Bila shaka Nilikuja miongoni mwa jamii ya Wayahudi; kwa hivyo watu wa kwanza kumwona Mungu Akija ulimwenguni walikuwa Wayahudi. Sababu Yangu ya kufanya kazi hii mwenyewe ilikuwa kwa sababu Nilitaka kutumia kupata mwili Kwangu kama sadaka ya dhambi katika kazi Yangu ya ukombozi. Kwa hivyo watu wa kwanza kuniona Mimi walikuwa Wayahudi wa Enzi ya Neema. Huo ndio ulikuwa wakati wa kwanza Mimi kufanya kazi Nikiwa katika mwili. Katika Enzi ya Ufalme, kazi Yangu ni kushinda na kutakasa, kwa hivyo kwa mara nyingine Nafanya kazi ya uchungaji katika mwili. Hii ni mara Yangu ya pili kufanya kazi katika mwili. Katika hatua mbili za mwisho za kazi, wanachokutana nacho watu si tena Roho asiyeonekana, asiyeshikika, bali ni mwanadamu ambaye ni Roho Aliyefanyika mwili. Hivyo machoni pa binadamu, Nilikuwa tena mtu asiye na sura wala hisia za Mungu. Zaidi ya hayo, Mungu ambaye watu huona, si wa kiume pekee, bali pia ni wa kike, kitu ambacho ni cha kushtua na kushangaza kwao. Muda baada ya muda, kazi Yangu ya ajabu huziondoa imani za kale ambazo zimekuwa kwa miaka mingi sana. Watu hushangazwa! Huyu Aitwaye Mungu si Roho Mtakatifu pekee, huyo Roho, Roho aliyeongezeka mara saba, Roho anayehusisha yote, bali pia mtu, mtu wa kawaida, mtu wa kipekee wa kawaida. Si wa kiume pekee, bali pia kike. Wako sawa kwamba wote wanazaliwa na binadamu, na tofauti kwamba mmoja alizaliwa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu na mwingine Anazaliwa kwa mwanadamu lakini Anatoka kwa Roho moja kwa moja. Wako sawa kwa namna kwamba wote kupata miili kwa Mungu hutenda kazi ya Baba yao, na kutofautiana kwa namna kwamba mmoja Anafanya kazi ya ukombozi na mwingine anafanya kazi ya ushindi. Wote wanamwakilisha Mungu Baba, lakini mmoja ni Bwana wa Ukombozi aliyejaa upendo, ukarimu na huruma, na yule mwingine ni Mungu wa uhaki Aliyejaa hasira na hukumu. Mmoja ni Jemadari Mkuu Anayeanzisha kazi ya ukombozi na mwingine ni Mungu wa uhaki wa kukamilisha kazi ya kutamalaki. Mmoja ni Mwanzo na mwingine Mwisho. Mmoja ni mwili usio na dhambi na mwingine ni mwili unaokamilisha ukombozi, Anaendelea na kazi hiyo na kamwe hana dhambi hata. Wote ni Roho mmoja lakini wanaishi katika miili tofauti na walizaliwa katika sehemu tofauti. Na wametenganishwa na maelfu kadhaa ya miaka. Ilhali kazi Zao ni kijalizo kwa nyingine, hazina mgongano kamwe na zinaweza kuzungumziwa kwa wakati mmoja. Wote ni watu, lakini mmoja ni mtoto wa kiume na mwingine mtoto mchanga wa kike. Katika hii miaka yote, ambayo watu wamekiona si Roho pekee na mwanamume, bali pia vitu vingi visivyoambatana na fikira za binadamu, na kwa hivyo hawawezi kunielewa kikamilifu kamwe. Wanashinda wakiniamini mara nyingine na mara nyingine wakiwa na shaka kunihusu, na iwapo Nipo kwa uhakika na ilhali Mimi ni ndoto ya mawazo. Ndio maana mpaka siku ya leo, watu hawatambui Mungu ni nini. Unaweza kweli kunieleza kwa sentensi moja? Unaweza kweli kusema kwa uhakika kwamba “Yesu si mwingine ila ni Mungu, na Mungu si mwingine ila Yesu”? Una ujasiri wa kusema kwamba “Mungu si mwingine bali Roho na Roho si mwingine bali ni Mungu”? Una ujasiri wa kusema kwamba “Mungu ni binadamu tu aliyevalia mwili?” Kwa kweli una ujasiri wa kusema kuwa “Taswira ya Yesu ni taswira kubwa ya Mungu?” Unaweza kuelezea kwa umakinifu tabia ya Mungu na umbo kwa uwezo wa kipawa chako cha maneno? Unaweza hakika kuthubutu kusema kuwa Mungu Aliumba kiume pekee, sio kike, kwa mfano Wake mwenyewe? Ukisema hivi, basi kusingekuwepo na mwanamke miongoni mwa wateule Wangu na hata zaidi wanawake wasingekuwa aina miongoni mwa wanadamu. Sasa, unajua hakika Mungu ni nini? Je, Mungu ni binadamu? Je, Mungu ni Roho? Je, Mungu kwa uhakika ni wa kiume? Je, ni Yesu pekee Anayeweza kukamilisha kazi ambayo Ninataka kufanya? Ukichagua moja tu kati ya haya kujumuisha kiini Changu, basi utakuwa muumini mjinga kabisa. Nikifanya kazi kama mwili uliopatikana mara moja tu, je, unaweza kuniwekea mipaka? Je, unaweza hakika kuniangalia mara moja na ukajua yaliyo ndani Yangu? Je, unaweza hakika kunieleza kikamilifu kwa mujibu tu wa yale ambayo umeyafahamu wakati wa maisha yako? Na iwapo katika kuingia Kwangu kwa mwili mara mbili Nafanya kazi inayofanana, utanichukulia vipi? Unaweza kuniacha milele msalabani nikiwa na misumari? Je, Mungu anaweza kuwa wa kawaida jinsi unavyosema?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufahamu Wako Kumhusu Mungu Ni Upi?

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 206)

Hatua moja ya kazi ya enzi mbili za awali ilifanyika Israeli; nyingine ilifanyika Yudea. Kuzungumza kwa jumla, hakuna hatua ya kazi hii iliyoondoka Israeli; zilikuwa ni hatua za kazi zilizofanywa miongoni mwa wateule wa mwanzo. Hivyo, kwa mtazamo wa Waisraeli, Yehova Mungu ni Mungu wa Waisraeli pekee. Kwa sababu ya kazi ya Yesu huko Yudea, na kwa sababu ya kukamilisha Kwake kazi ya kusulubiwa, kwa mtazamo wa Wayahudi, Yesu ni Mkombozi wa watu wa Kiyahudi. Yeye ni Mfalme wa Wayahudi pekee, sio wa watu wengine wowote; Yeye si Bwana anayewakomboa Waingereza, wala Bwana anayewakomboa Wamarekani, lakini Yeye ni Bwana anayewakomboa Waisraeli, na katika Israeli ni Wayahudi ndio Anaowakomboa. Kwa kweli, Mungu ni Bwana wa mambo yote. Yeye ndiye Mungu wa viumbe vyote. Yeye si Mungu wa Waisraeli pekee, na Yeye si Mungu wa Wayahudi pekee; Yeye ni Mungu wa viumbe vyote. Hatua mbili za awali za kazi Yake zilifanyika Israeli, na kwa njia hii, dhana zingine zimejitokeza ndani ya watu. Watu wanafikiri kuwa Yehova alikuwa akifanya kazi Israeli na Yesu Mwenyewe alitekeleza kazi Yake Yudea—zaidi ya hayo, ilikuwa kupitia kupata mwili ambapo Alikuwa akifanya kazi Yudea—na kwa vyovyote, kazi hii haikuenea zaidi ya Israeli. Hakuwa akifanya kazi na Wamisri; Hakuwa akifanya kazi na Wahindi; Alikuwa tu akifanya kazi na Waisraeli. Watu basi wanaunda dhana mbalimbali; aidha, wanapanga kazi ya Mungu ndani ya eneo fulani. Wanasema kwamba wakati Mungu anafanya kazi, ni lazima ifanywe miongoni mwa wateule na ndani ya Israeli; mbali na Waisraeli, Mungu hana mpokeaji mwingine wa kazi Yake, wala Hana eneo lingine la kazi Yake; ni wakali hasa katika “kumfundisha nidhamu” Mungu mwenye mwili, kutomruhusu kuenda zaidi ya eneo la Israeli. Je, hizi zote si dhana za binadamu? Mungu aliunda mbingu na dunia yote na vitu vyote, na kuumba viumbe vyote; Angewezaje kuzuia kazi Yake ndani ya Israeli peke yake? Katika hali hiyo, kungekuwa na haja gani ya Yeye kuumba viumbe Vyake vyote? Aliiumba dunia nzima; Ametekeleza mpango Wake wa usimamizi wa miaka elfu sita sio tu ndani ya Israeli lakini pia na kila mtu ulimwenguni. Bila kujali kama anaishi Uchina, Amerika, Uingereza ama Urusi, kila mtu ni wa ukoo wa Adamu; wote wameumbwa na Mungu. Hakuna mtu hata mmoja anayeweza kuondoka katika mawanda ya viumbe wa Mungu, na hakuna mtu hata mmoja anayeweza kuepuka utambulisho wa “ukoo wa Adamu.” Wote ni viumbe wa Mungu, na wote ni wa ukoo wa Adamu; pia ni wazawa wapotovu wa Adamu na Hawa. Sio tu Waisraeli ambao ni viumbe wa Mungu, lakini ni watu wote; hata hivyo, wengine miongoni mwa viumbe wamelaaniwa, na wengine wamebarikiwa. Kuna mambo mengi ya kupendeza kuwahusu Waisraeli; Mungu awali alikuwa akifanya kazi nao kwa sababu walikuwa watu wapotovu kwa kiasi kidogo zaidi. Wachina ni dhaifu wakilinganishwa nao, na hawawezi hata kutumaini kulingana nao; hivyo, Mungu awali alifanya kazi miongoni mwa watu wa Israeli, na hatua ya pili ya kazi Yake ilifanywa tu Yudea. Kwa sababu hii, watu huunda dhana nyingi na kanuni nyingi. Kwa kweli, iwapo Angetenda kulingana na dhana za binadamu, Mungu angekuwa tu Mungu wa Waisraeli; kwa njia hii Asingeweza kupanua kazi Yake katika mataifa yasiyo ya Kiyahudi, kwa sababu Angekuwa tu Mungu wa Waisraeli badala ya Mungu wa viumbe vyote. Unabii ulisema kuwa jina la Yehova lingekuwa kubwa katika mataifa yasiyo ya Kiyahudi na kuwa jina la Yehova lingeenezwa kwa mataifa yasiyo ya Kiyahudi—mbona ulisema hivi? Iwapo Mungu angekuwa Mungu wa Waisraeli tu, basi Angefanya kazi tu Israeli. Zaidi ya hayo, Asingepanua kazi hii, na Asingefanya huu unabii. Kwa sababu Alifanya huu unabii, Angehitaji kuipanua kazi Yake hadi mataifa yasiyo ya Kiyahudi na hadi kila taifa na mahali. Kwa sababu Alisema hili, basi Angefanya hivyo. Huu ndio mpango Wake, kwani Yeye ndiye Bwana aliyeumba mbingu na dunia na vitu vyote, na Mungu wa viumbe vyote. Bila kujali iwapo Anafanya kazi na Waisraeli ama katika Yudea nzima, kazi Anayoifanya ni kazi ya ulimwengu mzima na kazi ya binadamu wote. Kazi Anayoifanya leo katika taifa la joka kubwa jekundu—katika taifa lisilo la Kiyahudi—bado ni kazi ya binadamu wote. Israeli inaweza kuwa kituo cha kazi Yake duniani; vivyo hivyo, Uchina pia inaweza kuwa kituo cha kazi Yake miongoni mwa mataifa yasiyo ya Kiyahudi. Je, sasa Hajatimiza unabii kwamba “jina la Yehova litakuwa kubwa katika mataifa yasiyo ya Kiyahudi”? Hatua ya kwanza ya kazi Yake miongoni mwa mataifa yasiyo ya Kiyahudi inahusu kazi hii Anayoifanya katika taifa la joka kuu jekundu. Kwa Mungu mwenye mwili kufanya kazi katika nchi hii na kufanya kazi miongoni mwa hawa watu waliolaaniwa hasa inaenda kinyume na dhana za binadamu; hawa watu ni wa chini zaidi na wasio na thamani yoyote. Hawa wote ni watu ambao Yehova alikuwa amewaacha mwanzoni. Watu wanaweza kuachwa na watu wengine, lakini wakiachwa na Mungu, hawa watu hawatakuwa na hadhi, na watakuwa na thamani ya kiwango cha chini zaidi. Kama sehemu ya viumbe, kumilikiwa na Shetani ama kuachwa na watu wengine yote mawili ni mambo machungu, lakini sehemu ya viumbe ikiachwa na Bwana wa viumbe, hii inaashiria kwamba hadhi yake iko katika kiwango cha chini kabisa. Wazawa wa Moabu walilaaniwa, na walizaliwa ndani ya nchi hii isiyo na maendeleo; bila shaka, wazawa wa Moabu ni watu walio na hadhi ya chini zaidi chini ya ushawishi wa giza. Kwa sababu hawa watu walimiliki hadhi ya chini zaidi zamani, kazi inayofanywa miongoni mwao inaweza kabisa kuzivunja dhana za binadamu, na pia ni kazi yenye faida kubwa zaidi kwa mpango Wake mzima wa usimamizi wa miaka elfu sita. Ili Afanye kazi miongoni mwa watu hawa ni kitendo kinachoweza zaidi kuzivunja dhana za binadamu; Akiwa na hili Anazindua enzi; na hili Anavunja dhana zote za binadamu; Akiwa na hili Anatamatisha kazi ya Enzi nzima ya Neema. Kazi Yake ya awali ilifanywa Yudea, ndani ya eneo la Israeli; katika mataifa yasiyo ya Kiyahudi Hakufanya kazi yoyote ya uzinduzi wa enzi hata kidogo. Hatua ya mwisho ya kazi Yake haifanywi tu miongoni mwa watu wa mataifa yasiyo ya Kiyahudi; hata zaidi ya hayo, inafanywa miongoni mwa watu waliolaaniwa. Jambo hili moja ndio ushahidi unaoweza zaidi kumwaibisha Shetani; hivyo, Mungu “anakuwa” Mungu wa viumbe vyote ulimwenguni na kuwa Bwana wa vitu vyote, Anayeabudiwa na kila kiumbe mwenye uhai.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu Ndiye Bwana wa Viumbe Vyote

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 207)

Kwa sasa bado kuna watu wengine wasioelewa ni aina gani ya kazi mpya ambayo Mungu amezindua. Mungu amefanya mwanzo mpya katika mataifa yasiyo ya Kiyahudi na Ameanza enzi nyingine na kuzindua kazi nyingine, na Anafanya kazi miongoni mwa ukoo wa Moabu. Je, hii si kazi Yake mpya kabisa? Hakuna yeyote katika enzi zote aliyeipitia kazi hii, wala hakuna aliyeisikia, sembuse kuithamini. Hekima ya Mungu, ajabu ya Mungu, kutoeleweka kwa Mungu, ukubwa wa Mungu, utakatifu wa Mungu vinategemea hatua hii ya kazi katika siku za mwisho, ili kuibuka wazi. Je, hii si kazi mpya inayovunja dhana za binadamu? Bado kuna wale wanaofikiria hivi: “Kwa sababu Mungu alimlaani Moabu na kusema kuwa Angewaacha wazawa wa Moabu, Angeweza kuwaokoaje sasa?” Hao ni wale watu kutoka mataifa yasiyo ya Kiyahudi waliolaaniwa na kulazimishwa nje ya Israeli; Waisraeli waliwaita “mbwa wasio wa Kiyahudi.” Kwa mtazamo wa kila mtu, wao sio mbwa wasio wa Kiyahudi pekee, lakini mbaya hata zaidi, ni wana wa maangamizi; kwa maneno mengine, wao si wateule wa Mungu. Ingawa awali walikuwa wamezaliwa ndani ya eneo la Israeli, wao siyo sehemu ya watu wa Israeli; wao pia walifukuzwa kwenda kwa mataifa yasiyo ya Kiyahudi. Wao ndio watu wa chini zaidi. Ni kwa sababu hasa wao ni watu wa chini zaidi miongoni mwa binadamu ndio Mungu anatekeleza kazi Yake ya kuzindua enzi mpya miongoni mwao, kwani wao ni wawakilishi wa binadamu wapotovu. Kazi ya Mungu haikosi uchaguzi ama madhumuni, kazi Anayoifanya miongoni mwa watu hawa leo pia ni kazi inayofanywa miongoni mwa viumbe. Nuhu alikuwa sehemu ya viumbe, kama walivyo wazawa wake. Yeyote duniani aliye na mwili na damu ni sehemu ya viumbe. Kazi ya Mungu imeelekezwa kwa viumbe wote; haitekelezwi kulingana na kama mtu amelaaniwa baada ya kuumbwa. Kazi Yake ya usimamizi imeelekezwa kwa viumbe wote, sio wale wateule wasiolaaniwa. Kwa sababu Mungu anataka kutekeleza kazi Yake miongoni mwa viumbe Vyake, kwa hakika Ataifanya hadi kukamilika kwa mafanikio; Atafanya kazi miongoni mwa hao watu walio na manufaa kwa kazi Yake. Kwa hivyo, Anavunja mikataba yote ya kufanya kazi miongoni mwa watu; Kwake, maneno “kulaaniwa,” “kuadibu” na “kubarikiwa” hayana maana! Wayahudi ni wazuri hasa, na wateule wa Israeli sio wabaya pia; ni watu wenye ubora mzuri wa tabia na ubinadamu mzuri. Awali Yehova alizindua kazi Yake miongoni mwao na Akafanya kazi Yake ya awali, lakini ingekuwa bila maana kama Angewatumia kama wapokeaji wa kazi Yake ya ushindi sasa. Ingawa wao pia ni sehemu ya viumbe na wana vipengele vingi vyema, ingekuwa bila maana kutekeleza hatua hii ya kazi miongoni mwao. Asingeweza kumshinda yeyote, wala Asingeweza kushawishi viumbe wote. Huu ndio umuhimu wa uhamisho wa kazi Yake kwa watu hawa wa taifa la joka kubwa jekundu. Maana ya ndani zaidi hapa ni ya uzinduzi Wake wa enzi, ya kuvunja Kwake kwa kanuni zote na dhana zote za mwanadamu na pia kwa kumaliza Kwake kazi ya Enzi nzima ya Neema. Kama kazi Yake ya sasa ingefanywa miongoni mwa Waisraeli, ikifika wakati ambao mpango Wake wa usimamizi wa miaka elfu sita kukamilika, kila mtu angeamini kuwa Mungu ni Mungu tu wa Waisraeli, kuwa Waisraeli tu ndio wateule wa Mungu, kuwa Waisraeli tu ndio wanaostahili kurithi baraka na ahadi za Mungu. Katika siku za mwisho, Mungu anapata mwili katika taifa lisilo la Kiyahudi la joka kubwa jekundu; Ametimiza kazi ya Mungu kama Mungu wa viumbe wote; Amekamilisha kazi Yake yote ya usimamizi, na Atamaliza sehemu kuu ya kazi Yake kwa taifa la joka kubwa jekundu. Kiini cha hatua hizi tatu za kazi ni wokovu wa mwanadamu—ambao ni, kufanya viumbe wote vimwabudu Bwana wa viumbe. Hivyo basi, kila hatua ya kazi hii ni muhimu sana; Mungu hatafanya chochote kisicho na maana ama thamani. Kwa upande mmoja, hatua hii ya kazi inajumuisha kuzindua enzi na kukamilisha enzi mbili za awali; kwa upande mwingine inajumuisha kuvunja dhana zote za mwanadamu na njia ya zamani ya imani ya mwanadamu na maarifa. Kazi ya enzi mbili za awali ilifanywa kulingana na dhana tofauti za binadamu; hatua hii, hata hivyo, inafuta kabisa dhana za binadamu, na hivyo kuwashinda binadamu kikamilifu. Kwa kutumia ushindi wa ukoo wa Moabu na kutumia kazi iliyotekelezwa miongoni mwa ukoo wa Moabu, Mungu atawashinda binadamu wote katika ulimwengu mzima. Huu ndio umuhimu wa kina zaidi wa hatua hii ya kazi Yake, na ndicho kipengele cha thamani ya hatua hii ya kazi Yake. Hata kama sasa unajua kuwa hadhi yako ni ya chini na kuwa una thamani ya chini, bado utahisi kwamba umekutana na jambo linalofurahisha sana: Umerithi baraka kubwa, ukapata ahadi kubwa, na unaweza kamilisha hii kazi kubwa ya Mungu, na unaweza kuuona uso wa kweli wa Mungu, kujua tabia Yake ya asili, na kufanya mapenzi ya Mungu. Hatua mbili za awali za kazi ya Mungu zilifanywa Israeli. Iwapo hatua hii ya kazi Yake katika siku za mwisho bado ingefanywa miongoni mwa Waisraeli, viumbe wote havingeamini kwamba Waisraeli tu ndio waliokuwa wateule, lakini pia mpango wa usimamizi wa Mungu wote haungefikia athari iliyotaka. Wakati ambapo hatua hizi mbili za kazi Yake zilifanywa Israeli, hakuna kazi yoyote mpya iliyokuwa imefanywa na hakuna kazi yoyote ya Mungu ya kuzindua enzi ilikuwa imewahi kufanywa katika mataifa yasiyo ya Kiyahudi. Hatua hii ya kazi ya kuzindua enzi inafanywa kwanza katika mataifa yasiyo ya Kiyahudi, na zaidi ya hayo, inafanywa kwanza miongoni mwa ukoo wa Moabu; hii imezindua enzi mpya. Mungu amevunja maarifa yoyote yaliyo ndani ya dhana za binadamu na hajaruhusu yoyote yaendelee kuwa hai. Katika kazi Yake ya kushinda Amevunja dhana za binadamu, hiyo njia ya zamani, ya maarifa ya binadamu, Anaruhusu watu waone kuwa kwa Mungu hakuna kanuni, kwamba hakuna kitu kizee kumhusu Mungu, kwamba kazi Anayoifanya ni ya uhuru kabisa, ni huru kabisa, kwamba Yeye yuko sahihi katika chochote Anachofanya. Ni lazima utii kikamilifu kazi yoyote Anayoifanya miongoni mwa viumbe. Kazi yoyote Anayoifanya ni ya maana na inafanywa kulingana na mtazamo Wake na maarifa Yake na sio kulingana na chaguo za watu na dhana za watu. Anafanya yale mambo yaliyo na manufaa kwa kazi Yake; kama kitu hakina manufaa kwa kazi Yake, Hatakifanya, hata kiwe kizuri vipi! Anafanya kazi na kuchagua mpokeaji na eneo la kazi Yake kulingana na maana na madhumuni ya kazi Yake. Hafuati kanuni za zamani, wala Hafuati fomula nzee; badala yake, Anapanga kazi Yake kulingana na umuhimu wa kazi; mwishowe, Anataka kufikia matokeo yake ya kweli na madhumuni yanayotarajiwa. Iwapo huelewi mambo haya sasa, kazi hii haitatimiza matokeo yoyote kwako.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu Ndiye Bwana wa Viumbe Vyote

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 208)

Je, vikwazo kwa kazi ya Mungu ni vikubwa vipi? Je, kuna yeyote aliyewahi kujua? Watu wakiwa wamefungwa tunduni na rangi za ushirikina zenye nguvu, ni nani anayeweza kuujua uso wa kweli wa Mungu? Kwa ujuzi huu wa kitamaduni wenye maendeleo ya nyuma mno ulio wa juujuu na wa upuuzi, wangewezaje kuelewa kwa ukamilifu maneno yaliyosemwa na Mungu? Hata wakati wanapozungumziwa ana kwa ana, na kulishwa, mdomo kwa mdomo, wangewezaje kuelewa? Wakati mwingine ni kana kwamba maneno ya Mungu yamepuuzwa kabisa: Watu hawana mjibizo hata kidogo, wao hutikisa vichwa vyao na hawaelewi chochote. Je, hili lingekosaje kuwa lenye kutia wasiwasi? Hii “historia ya kitamaduni ya kale na maarifa ya kitamaduni ya mbali[1]” imekuza kikundi cha watu wasio na thamani hasa. Utamaduni huu wa kale—urithi wa thamani—ni rundo la takataka! Uligeuka kuwa aibu ya milele kitambo, na haustahili kutajwa! Umewafundisha watu hila na mbinu za kumpinga Mungu, na “mwongozo wa utaratibu, wa upole”[2] wa elimu ya kitaifa umewafanya watu kuwa wakaidi hata zaidi kwa Mungu. Kila sehemu ya kazi ya Mungu ni ngumu sana, na kila hatua ya kazi Yake duniani imekuwa ya kumhuzunisha Mungu. Jinsi kazi Yake duniani ilivyo ngumu! Hatua za kazi ya Mungu duniani zinahusisha shida kubwa: Kwa ajili ya udhaifu wa mwanadamu, upungufu, utoto, ujinga na kila kitu cha mwanadamu, Mungu hufanya mipango yenye uangalifu na hufikiria kwa makini. Mwanadamu ni kama duma wa kutisha ambaye mtu hathubutu kumtega au kumchokoza; anapoguswa tu anauma, au vinginevyo anaanguka chini na kupoteza mwelekeo wake, na ni kana kwamba, akipoteza umakini kidogo tu, anarudia uovu tena, au anampuuza Mungu, au anakimbia kwa wazazi wake walio kama nguruwe na mbwa kuendeleza mambo machafu ya miili yao. Ni kizuizi kikubwa kiasi gani! Katika kila hatua ya kazi Yake, Mungu anakabiliwa na ushawishi, na takribani katika kila hatua Mungu anakumbana na hatari kubwa. Maneno yake ni ya kweli na ya uaminifu, na bila uovu, lakini nani yupo tayari kuyakubali? Nani yupo tayari kutii kikamilifu? Inavunja moyo wa Mungu. Anafanya kazi usiku na mchana kwa ajili ya mwanadamu, Anasongwa na wasiwasi kuhusu maisha ya mwanadamu na Anauonea huruma udhaifu wa mwanadamu. Amevumilia shida nyingi katika kila hatua ya kazi Yake, kwa kila neno Analozungumza; Yupo katikati ya mwamba na sehemu ngumu, na kufikiria juu ya udhaifu wa mwanadamu, ukaidi, utoto, na vile alivyo hatarini wakati wote … tena na tena. Nani amewahi kulijua hili? Nani anaweza kuwa na imani? Nani anaweza kufahamu? Anachukia dhambi za wanadamu daima, na ukosefu wa uti wa mgongo, mwanadamu kutokuwa na uti wa mgongo, ndiko kunamfanya kuwa na hofu juu ya hatari aliyonayo mwanadamu, na kutafakari njia zilizopo mbele ya mwanadamu; siku zote, anapoangalia maneno na matendo ya mwanadamu, je, yanamjaza huruma, hasira, na siku zote vitu hivi vinamletea maumivu moyoni Mwake. Hata hivyo, wasio na hatia wamekuwa wenye ganzi; kwa nini ni lazima Mungu siku zote afanye vitu kuwa vigumu kwao? Mwanadamu dhaifu, ameondolewa kabisa uvumilivu; kwa nini Mungu awe na hasira isiyopungua kwa mwanadamu? Mwanadamu aliye dhaifu na asiye na nguvu hana tena uzima hata kidogo; kwa nini Mungu anamkaripia siku zote kwa ukaidi wake? Nani anayeweza kuhimili matishio ya Mungu mbinguni? Hata hivyo, mwanadamu ni dhaifu, na yupo katika dhiki sana, Mungu ameisukuma hasira Yake ndani kabisa moyoni Mwake, ili kwamba mwanadamu ajiakisi mwenyewe taratibu. Ilhali mwanadamu, aliyepo katika matatizo makubwa, hazingatii hata kidogo mapenzi ya Mungu; amedondoshwa miguuni na mfalme mzee wa pepo, na bado haelewi kabisa, siku zote anajiweka dhidi ya Mungu, au si moto wala baridi kwa Mungu. Mungu amezungumza maneno mengi sana, lakini nani ambaye ameyazingatia? Mwanadamu haelewi maneno ya Mungu, lakini bado hashtuki, bila kuwa na shauku, na hajawahi kuelewa kabisa hulka ya ibilisi wa kale. Watu wanaishi Kuzimu, lakini wanaamini wanaishi katika kasri la chini ya bahari; wanateswa na joka kuu jekundu, lakini bado wanadhani “wamependelewa”[3] na nchi; wanadhihakiwa na ibilisi lakini wanadhani wanafurahia ustadi wa hali ya juu wa mwili. Ni wachafu kiasi gani, ni mafidhuli kiasi gani! Mwanadamu amekutana na bahati mbaya, lakini haijui, na katika jamii hii ya giza anapatwa na ajali baada ya ajali,[4] lakini hajawahi kufahamu hili. Ni lini atakapoachana na wema wake wa kibinafsi na tabia ya mawazo ya kiutumwa? Kwa nini hajali moyo wa Mungu kiasi hicho? Je, anajifanya haoni ukandamizaji na shida hii? Je, hatamani kuwe na siku ambayo atabadilisha giza kuwa nuru? Je, hatamani zaidi kuponya uonevu dhidi ya haki na ukweli? Je, yupo tayari kutazama tu bila kufanya chochote watu wakitupilia mbali ukweli na kupindua ukweli? Je, anafurahia kuendelea kuvumilia matendo haya mabaya? Je, yupo radhi kuwa mtumwa? Je, yupo tayari kuangamia mkononi mwa Mungu pamoja na watumwa wa taifa hili lililoanguka? Azma yako ipo wapi? Malengo yako yapo wapi? Heshima yako ipo wapi? Maadili yako yapo wapi? Uhuru wako upo wapi? Je, uko tayari kutoa maisha yako yote[5] kwa ajili ya joka kuu jekundu, mfalme wa pepo? Je, unafurahi kumwacha akutese hadi kufa? Kina chake ni vurugu na giza, ilhali mtu wa kawaida, anayeteseka na mateso kama hayo, analalamika bila kupumzika. Ni lini mwanadamu ataweza kunyanyua kichwa chake juu? Mwanadamu amekuwa kimbaumbau na amekonda, anawezaje kuridhika na ibilisi huyu katili na dikteta? Kwa nini asiyatoe maisha yake kwa Mungu mapema awezavyo? Kwa nini bado anayumbayumba? Anaweza kumaliza kazi ya Mungu lini? Hivyo anaonewa na kunyanyaswa bila sababu yoyote, maisha yake yote hatimaye yatakuwa bure; kwa nini ana haraka hivyo ya kufika, na haraka hiyo ya kuondoka? Kwa nini hahifadhi kitu kizuri cha kumpa Mungu? Je, amesahau milenia ya chuki?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (8)

Tanbihi:

1. “Ya mbali” inatumiwa kwa dhihaka.

2. “Mwongozo wa utaratibu, wa upole” imetumika kimzaha.

3. “Wamependelewa” inatumiwa kuwadhihaki watu wanaoonekana wagumu na hawajitambui.

4. “Anapatwa na ajali baada ya ajali” inaonyesha kuwa watu walizaliwa katika nchi ya joka kubwa jekundu, na hawawezi kuwa na ujasiri.

5. “Kutoa maisha yako yote” imetumika kwa namna ya kimatusi.

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 209)

Njia ya leo si rahisi kuitembea. Inaweza kusemekana kwamba ni vigumu kuipata, na katika enzi zote imekuwa adimu sana. Hata hivyo, nani angeweza kufikiria kuwa mwili wa mwanadamu pekee ungetosha kumwangamiza? Kazi ya leo hakika ni ya thamani kama vile mvua ya majira ya kuchipua na ni ya thamani kama wema wa Mungu kwa mwanadamu. Hata hivyo, ikiwa mwanadamu hajui kusudi la kazi Yake ya sasa au kuelewa kiini cha mwanadamu, basi inawezekanaje tunu na thamani yake vizungumziwe? Mwili si wa wanadamu wenyewe, hivyo kwa kweli hakuna mtu anayeweza kuona waziwazi hatima yake itakuwa wapi. Hata hivyo, unapaswa kujua vizuri kwamba Mungu wa uumbaji Atawarudisha binadamu, ambao waliumbwa, katika nafasi yao ya asili, na kurejesha sura yao ya asili kutoka wakati wa kuumbwa kwao. Atachukua tena kikamilifu pumzi Aliyoipuliza ndani ya binadamu, na kuchukua tena mifupa na mwili wake na kurudisha vyote kwa Bwana wa viumbe. Atabadilisha na kufanya upya binadamu kikamilifu, na kuchukua tena kutoka kwa binadamu urithi wote wa Mungu ambao si wa binadamu, bali ni wa Mungu, na kamwe hatampa tena binadamu urithi huo. Hii ni kwa sababu kiasili, hakuna hata kitu kimoja kati ya hivyo kilichokuwa cha binadamu. Atavichukua vyote tena—huu si uporaji usio wa haki; lakini badala yake, unakusudiwa kuirejesha mbingu na dunia katika hali zake za asili, na vile vile kubadilisha na kumfanya upya binadamu. Hii ndiyo hatima inayofaa kwa mwanadamu, ingawa pengine haitakuwa kutwaa tena kwa mwili baada ya kuadibiwa, kama watu wanavyoweza kufikiri. Mungu hataki mifupa ya mwili baada ya maangamizi yake; Anataka vitu vya asili katika mwanadamu ambavyo mwanzo vilikuwa vya Mungu. Hivyo, Hatawaangamiza binadamu au kuuondoa kabisa mwili wa mwanadamu, kwa kuwa mwili wa mwanadamu si mali yake binafsi. Badala yake, ni kiungo cha Mungu, ambaye anasimamia binadamu. Angewezaje kuuangamiza mwili wa mwanadamu kwa ajili ya “furaha” Yake? Kufikia sasa, je, umeachana kwa kweli na ukamilifu wa huo mwili wako ambao hauna thamani hata ya senti moja? Kama ungeweza kuelewa asilimia thelathini ya kazi ya siku za mwisho (hii asilimia ndogo thelathini inamaanisha kuifahamu kazi ya Roho Mtakatifu leo na vile vile kazi ya Mungu ya neno katika siku za mwisho), basi usingeweza kuendelea “kuutumikia” au “kuwa” na upendo kwa mwili wako—mwili ambao umepotoka kwa miaka mingi—kama ilivyo leo. Unapaswa kuona wazi wazi kwamba binadamu sasa wameendelea hadi kufikia hali ambayo haijawahi kufikiwa na hawataendelea tena kusonga mbele kama magurudumu ya historia. Mwili wako ulioota kuvu umeshafunikwa na nzi tangu zamani, hivyo unawezaje kuwa na nguvu ya kurudisha nyuma magurudumu ya historia ambayo Mungu ameyawezesha kuendelea hadi siku hii ya leo? Unawezaje kufanya saa ipigayo kimya kimya ya siku za mwisho ipige tena, na iendelee kusogeza mikono yake kwa upande wa kulia? Unawezaje kuubadilisha upya ulimwengu ambao unaonekana kama umefunikwa na ukungu mzito? Je, mwili wako unaweza kuifufua milima na mito? Je, mwili wako, ambao una kazi kidogo tu, unaweza kweli kurejesha aina ya ulimwengu wa binadamu ambao umekuwa ukiutamani sana? Unaweza kweli kuwaelimisha wazawa wako wawe “binadamu”? Je, unaelewa sasa? Mwili wako unamilikiwa na nini hasa? Makusudi asili ya Mungu ya kumwokoa mwanadamu, ya kumkamilisha mwanadamu, na ya kumbadilisha mwanadamu hayakuwa kukupatia nchi nzuri ya asili au kuleta pumziko la amani kwa mwili wa mwanadamu; ilikuwa ni kwa ajili ya utukufu Wake na ushuhuda Wake, kwa furaha bora ya binadamu hapo baadaye, na ili kwamba hivi karibuni waweze kupumzika. Bado, ilikuwa kwa ajili ya mwili wako, maana mwanadamu ni mtaji wa usimamizi wa Mungu, na mwili wa mwanadamu ni kiungo tu. (Mwanadamu ni kitu chenye roho na mwili, ilhali mwili ni chombo kiozacho tu. Hii humaanisha kwamba mwili ni chombo cha kutumiwa katika mpango wa usimamizi.) Unapaswa kujua kwamba Mungu kuwakamilisha, kuwatimiza, na kuwapata wanadamu hakuleti kitu chochote ila panga na maangamizi juu ya miili wao, na na vile vile mateso yasiyokoma, moto mkali, hukumu zisizokuwa na huruma, kuadibu, laana, na majaribu yasiyokuwa na mipaka. Hicho ni kisa cha ndani na ukweli wa kazi ya kumsimamia binadamu. Hata hivyo, vitu hivi vyote vinalengwa kwa mwili wa mwanadamu, na mishale yote ya uhasama bila huruma inaelekezwa kwenye mwili wa mwanadamu (kwa maana mwanadamu hana hatia). Haya yote ni kwa ajili ya utukufu na ushuhuda Wake, na kwa ajili ya usimamizi Wake. Hii ni kwa sababu kazi Yake si kwa ajili ya binadamu tu, bali pia kwa ajili ya mpango wote, na vile vile kutimiza mapenzi Yake ya asili Alipomuumba binadamu. Kwa hiyo, pengine asilimia tisini ya kile ambacho mwanadamu hupitia kinajumuisha mateso na majaribu ya moto, na kuna siku chache sana ambazo ni tamu na zenye furaha au hata hakuna kabisa, ambazo mwili wa mwanadamu umekuwa ukitamani sana. Sembuse mwanadamu kuweza kufurahia nyakati za furaha katika mwili, akishinda nyakati nzuri pamoja na Mungu. Mwili ni mchafu, hivyo kile ambacho mwili wa mwanadamu unakiona au unakifurahia ni kuadibu kwa Mungu tu ambako mwanadamu huona kukiwa kusiko kuzuri, na ni kana kwamba hakuna mantiki ya kawaida. Hii ni kwa sababu Mungu atadhihirisha tabia Yake ya haki, ambayo haipendwi na mwanadamu, haivumilii makosa ya mwanadamu, na huchukia kabisa maadui. Mungu hufichua waziwazi tabia Yake yote kwa njia yoyote inayolazimu, na hivyo Akihitimisha kazi ya vita Vyake na Shetani vya miaka elfu sita—kazi ya wokovu wa binadamu wote na maangamizo ya Shetani wa zamani!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kusudi la Kuwasimamia Binadamu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 210)

Siku za mwisho zimefika na nchi nyingi ulimwenguni ziko katika machafuko. Vurugu ya kisiasa, njaa, ndwele, mafuriko, na ukame unaonekana kila mahali. Kuna maangamizi katika ulimwengu wa mwanadamu; Mbingu pia imetuma msiba hapa chini. Hizi ni ishara za siku za mwisho. Lakini kwa watu, unaonekana kama ulimwengu wa uchangamfu na fahari, ambao unaendelea kuwa hivyo zaidi na zaidi. Mioyo ya watu yote inavutiwa nao, na watu wengi wananaswa na hawawezi kujinasua kutoka kwa ulimwengu; idadi kubwa itadanganywa na wale wanaoshiriki katika hila na uchawi. Usipojitahidi kuendelea mbele, huna maadili, na hujajikita mizizi katika njia ya kweli, utapeperushwa na mawimbi yavumayo ya dhambi. China ni nchi iliyo nyuma zaidi kimaendeleo kuliko zote; ni nchi ambapo joka kuu jekundu hulala likiwa limejiviringisha, ina watu wengi zaidi wanaoabudu sanamu na kushiriki katika uchawi, ina hekalu nyingi zaidi, na ni mahali ambapo pepo wachafu huishi. Ulizaliwa kutoka kwayo, umeelimishwa nayo na ukaloweshwa katika ushawishi wake; umepotoshwa na kuteswa nayo, lakini baada ya kugutushwa unaachana nayo na unapatwa kabisa na Mungu. Huu ni utukufu wa Mungu, na hii ndiyo maana hatua hii ya kazi ina umuhimu mkubwa. Mungu amefanya kazi ya kiwango kikubwa hivi, amenena maneno mengi sana, na hatimaye Atawapata ninyi kabisa—hii ni sehemu moja ya kazi ya usimamizi ya Mungu, na ninyi ndio “mateka wa ushindi” wa vita vya Mungu na Shetani. Kadiri mnavyozidi kuelewa ukweli na kadiri maisha yenu ya kanisa yalivyo bora zaidi, ndivyo joka kuu jekundu linavyotishwa zaidi. Haya yote ni mambo ya ulimwengu wa kiroho—ni vita vya ulimwengu wa kiroho, na Mungu anapokuwa mshindi, Shetani ataaibishwa na kuanguka chini. Hatua hii ya kazi ya Mungu ina umuhimu wa ajabu. Mungu anafanya kazi kwa kiwango kikubwa sana na kukiokoa kabisa kikundi hiki cha watu ili uweze kuponyoka kutoka kwa ushawishi wa Shetani, uishi katika nchi takatifu, uishi katika nuru ya Mungu, na uwe na uongozi na mwongozo wa nuru. Kisha kuna maana katika maisha yako. Mnachokula na kuvaa ni tofauti na wasioamini; mnafurahia maneno ya Mungu na kuishi maisha yenye maana—na wao hufurahia nini? Wao hufurahia tu “urithi wa babu” zao na “fahari yao ya kitaifa.” Hawana hata chembe ndogo kabisa ya ubinadamu! Mavazi, maneno, na matendo yenu yote ni tofauti na yao. Hatimaye, mtatoroka kabisa kutoka katika uchafu, msitegwe tena katika majaribu ya Shetani, na mpate riziki ya Mungu ya kila siku. Mnapaswa kila mara kuwa waangalifu. Ingawa mnaishi mahali pachafu hamjawekwa mawaa na uchafu na mnaweza kuishi ubavuni mwa Mungu, mkipokea ulinzi Wake mkuu. Mungu amewachagua kutoka miongoni mwa wote walio katika nchi hii ya manjano. Je, ninyi sio watu waliobarikiwa zaidi? Wewe ni kiumbe aliyeumbwa—unapaswa bila shaka kumwabudu Mungu na kufuatilia maisha yenye maana. Usipomwabudu Mungu lakini unaishi ndani ya mwili wako mchafu, basi wewe si mnyama tu aliye ndani ya vazi la mwanadamu? Kwa kuwa wewe ni binadamu, unapaswa kujitumia kwa ajili ya Mungu na kuvumilia kila mateso! Unapaswa kukubali kwa furaha na kwa hakika mateso kidogo unayopitia leo na kuishi maisha yenye maana, kama Ayubu na Petro. Katika ulimwengu huu, mwanadamu huvaa mavazi ya ibilisi, hula chakula kutoka kwa ibilisi, na hufanya kazi na kutumika chini ya uelekezi wa Shetani, na kukanyagiwa kabisa ndani ya uchafu wake. Usipoelewa maana ya maisha au kupata njia ya kweli, basi kuna umuhimu gani katika kuishi kwa namna hii? Ninyi ni watu mnaofuatilia njia sahihi, wale mnaotafuta maendeleo. Ninyi ni watu ambao huinuka katika nchi ya joka kuu jekundu, wale ambao Mungu huwaita wenye haki. Je, hayo si maisha yenye maana zaidi?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Utendaji (2)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 211)

Leo, kazi Nifanyayo ndani yenu inakusudiwa kuwaongoza hadi katika maisha ya ubinadamu wa kawaida; ni kazi ya kukaribisha enzi mpya na ya kuwaongoza wanadamu katika maisha ya enzi mpya. Kazi hii inatekelezwa na kukuzwa miongoni mwenu hatua kwa hatua na moja kwa moja: Nawafunza ana kwa ana; Nawaongoza moja kwa moja; Nawaambia chochote msichokielewa, Nawapa chochote msicho nacho. Inaweza kusemekana kwamba, kwenu, hii kazi yote ni kwa ajili ya ruzuku yenu ya maisha, kuwaongoza pia katika maisha ya ubinadamu wa kawaida; inakusudiwa hasa kuruzuku maisha ya kundi hili la watu wakati wa siku za mwisho. Kwangu Mimi, hii kazi yote inakusudiwa kukamilisha enzi ya kale na kukaribisha enzi mpya; kumhusu Shetani, Nilipata mwili hasa ili nimshinde. Kazi Nifanyayo miongoni mwenu sasa ni ruzuku yenu ya leo na wokovu wenu wa wakati mzuri, lakini katika miaka hii michache mifupi, Nitawaambia ukweli wote, njia nzima ya maisha, na hata kazi ya siku zijazo; hili litatosha kuwawezesha mpitie mambo kwa njia ya kawaida katika siku zijazo. Nimewaaminia maneno Yangu yote pekee. Sitoi ushawishi mwingine wowote; leo, maneno yote Ninayowazungumzia ni ushawishi Wangu kwenu, kwa sababu leo hamjapitia maneno mengi Ninenayo, na hamwelewi maana yake ya ndani. Siku moja, uzoefu wenu utatimika jinsi tu Nilivyosema leo. Maneno haya ni maono yenu ya leo, na ndiyo mtakayotegemea katika siku zijazo; ni ruzuku ya maisha leo na ushawishi wa siku zijazo, na hakuna ushawishi unaoweza kuwa bora zaidi. Hii ni kwa sababu muda Nilio nao kufanya kazi duniani si mrefu kama muda mlio nao kupitia maneno Yangu; Namaliza kazi Yangu tu, wakati ninyi mnafuatilia maisha, mchakato unaohusisha safari ndefu katika maisha. Ni baada tu ya kupitia mambo mengi ndipo mtaweza kupata njia ya maisha kikamilifu; ni hapo tu ndipo mtaweza kubaini maana ya ndani ya maneno Nizungumzayo leo. Mtakapokuwa na maneno Yangu mikononi mwenu, wakati kila mmoja wenu amepokea maagizo Yangu yote, punde Nitakapowaagizia yote Nipasayo, na wakati kazi ya maneno Yangu imemalizika, basi utekelezaji wa mapenzi ya Mungu pia utakuwa umetimizwa, bila kujali jinsi matokeo makubwa yamefanikishwa. Siyo jinsi unavyodhani, kwamba ni lazima ubadilishwe hadi kiwango fulani; Mungu hatendi kulingana na fikira zako.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Utendaji (7)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 212)

Katika siku za mwisho, Mungu alipata mwili ili kufanya kazi Aliyopaswa kufanya na kutekeleza huduma Yake ya maneno. Alikuja yeye mwenyewe ili kufanya kazi kati ya wanadamu kwa lengo la kuwakamilisha wale watu ambao wanaipendeza nafsi Yake. Kutoka wakati wa uumbaji hadi leo Yeye hufanya tu hiyo kazi wakati wa siku za mwisho. Ni wakati wa siku za mwisho tu ambapo Mungu alipata mwili ili kufanya kazi kwa kiwango kikubwa. Ingawa Yeye huvumilia shida ambazo watu wanaweza kupata ugumu kuvumilia, ingawa Yeye kama Mungu mkuu ana unyenyekevu wa kuwa mtu wa kawaida, hakuna kipengele cha kazi Yake kimecheleweshwa, na mpango Wake haujatupwa katika mchafuko hata kidogo. Anafanya kazi kulingana na mpango Wake wa awali. Mojawapo ya madhumuni ya kupata mwili huku ni kuwashinda watu. Mengine ni kuwakamilisha watu Anaowapenda. Yeye hutamani kuwaona kwa macho Yake mwenyewe watu Anaowakamilisha, na Yeye hutaka kujionea Mwenyewe jinsi watu Anaowakamilisha humshuhudia. Sio mtu mmoja ambaye hukamilishwa, na sio wawili. Hata hivyo, ni kikundi cha watu wachache sana. Kikundi hiki cha watu huja kutoka nchi mbalimbali za dunia, na kutoka kwa makabila mbalimbali ya ulimwengu. Kusudi la kufanya kazi hii nyingi ni kukipata kikundi hiki cha watu, kupata ushuhuda ambao kikundi hiki cha watu humtolea, na kupata utukufu ambao Yeye hupata kupitia kwa kikundi hiki cha watu. Yeye hafanyi kazi ambayo haina umuhimu, wala hafanyi kazi ambayo haina thamani. Inaweza kusemwa kuwa, kwa kufanya kazi nyingi sana, lengo la Mungu ni kuwakamilisha watu wote ambao Yeye anataka kuwakamilisha. Katika wakati wowote wa ziada Alio nao nje ya hili, Atawaondosha wale walio waovu. Jua kwamba Haifanyi kazi hii kubwa kwa sababu ya wale walio waovu; kwa kinyume, Yeye hufanya kadri Awezavyo kwa sababu ya idadi hiyo ndogo ya watu ambao hawana budi kukamilishwa na Yeye. Kazi ambayo Yeye hufanya, maneno ambayo Yeye hunena, siri ambayo Yeye hufichua, na hukumu Yake na adhabu zote ni kwa ajili ya idadi hiyo ndogo ya watu. Yeye hakupata mwili kwa sababu ya wale walio waovu, sembuse wao kuchochea ghadhabu kubwa ndani Yake. Yeye husema ukweli, na huzungumzia kuingia, kwa sababu ya wale watakaokamilishwa, Alipata mwili kwa sababu yao, na ni kwa sababu yao Yeye hutoa ahadi na baraka Zake. Ukweli, kuingia, na maisha katika ubinadamu ambayo Yeye huzungumzia si kwa ajili ya wale walio waovu. Yeye hutaka kuepuka kuzungumza na wale walio waovu, na hutaka kuwapa wale ambao watakamilishwa ukweli wote. Lakini kazi Yake inahitaji kwamba, kwa sasa, wale walio waovu waruhusiwe kufurahia baadhi ya utajiri Wake. Wale ambao hawatekelezi ukweli, ambao hawamridhishi Mungu, na ambao hukatiza kazi Yake wote ni waovu. Hawawezi kukamilishwa, na wanachukiwa kabisa na kukataliwa na Mungu. Kwa kinyume, watu ambao hutia ukweli katika vitendo na wanaweza kumridhisha Mungu na ambao hujitolea wenyewe kabisa katika kazi ya Mungu ndio watu ambao watakamilishwa na Mungu. Wale ambao Mungu hutaka kuwakamilisha sio wengine bali ni kikundi hiki cha watu, na kazi ambayo Mungu hufanya ni kwa ajili ya watu hawa. Ukweli ambao Yeye huzungumzia unaelekezwa kwa watu ambao wako tayari kuutia katika vitendo. Yeye huwa hazungumzi na watu ambao hawatii ukweli katika vitendo. Ongezeko la umaizi na ukuaji wa utambuzi ambao Yeye huzungumzia umelengwa kwa watu ambao wanaweza kutekeleza ukweli. Anapozungumza juu ya wale ambao watakamilishwa, ni watu hawa Anaozungumza kuwahusu. Kazi ya Roho Mtakatifu inaelekezwa kwa watu ambao wako tayari kutenda ukweli. Mambo kama kuwa na hekima na binadamu yanaelekezwa kwa watu ambao wako tayari kutia ukweli katika vitendo. Wale ambao hawatekelezi ukweli wanaweza kusikia maneno mengi, lakini kwa sababu wao ni waovu sana kiasili na hawavutiwi na ukweli, kile wanachoelewa is mafundisho ya dini na maneno tu, na nadharia tupu, bila kujali hata kidogo kuingia kwao katika maisha. Hakuna hata mmoja wao aliye mwaminifu kwa Mungu; wao wote ni watu wanaomwona Mungu lakini hawawezi kumpata; wote wamehukumiwa na Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Wale Wanaolenga Kutenda tu Ndio Wanaoweza Kukamilishwa

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 213)

Shabaha kuu ya kazi ya kushinda ni kuwatakasa binadamu ili mwanadamu aweze kuwa na ukweli, kwa sababu mwanadamu sasa anauelewa ukweli kidogo sana! Kufanya kazi ya kushinda kwa watu hawa ni jambo la umuhimu mkubwa mno. Nyote mmeanguka katika ushawishi wa giza na mmeumizwa mno. Shabaha ya kazi hii, basi, ni kuwawezesha kujua asili ya binadamu na hivyo basi kuishi kwa ukweli. Kukamilishwa ni kitu ambacho viumbe wote wanafaa kukubali. Kama kazi ya awamu hii inahusu tu kufanya watu kuwa wakamilifu, basi inaweza kufanywa Uingereza, au Amerika, au Israeli; inaweza kufanywa kwa watu wa taifa lolote. Lakini kazi ya kushinda ni kuwa inachagua. Hatua ya kwanza ya kazi ya kushinda ni ya muda mfupi; aidha, itatumika kumdhalilisha Shetani na kuushinda ulimwengu mzima. Hii ndiyo kazi ya mwanzo ya kushinda. Mtu anaweza kusema kwamba kiumbe yeyote anayemwamini Mungu anaweza kufanywa kuwa kamili kwa sababu kukamilishwa ni kitu ambacho mtu anaweza kufikia tu baada ya mabadiliko ya muda mrefu. Lakini kushindwa ni tofauti. Kielelezo na mlengwa wa kushinda lazima awe yule anayebaki nyuma zaidi, akiishi kwenye giza totoro kabisa, na vilevile mwenye hadhi kidogo kabisa, na asiyekuwa radhi kumkubali Mungu zaidi, na asiyetii Mungu zaidi. Huyu ndiye aina ya mtu anayeweza kutoa ushuhuda wa kushindwa. Shabaha kuu ya kazi ya kushinda ni kumshinda Shetani. Shabaha kuu ya kufanya watu kuwa wakamilifu, kwa upande mwingine, ni kuwapata watu wale. Ni kwa ajili ya kuwawezesha watu kuwa na ushuhuda baada ya kushindwa ndio kazi ya kushinda imewekwa hapa, kwa watu kama ninyi. Lengo ni kuwafanya watu kutoa ushuhuda baada ya kushindwa. Watu hawa walioshindwa watatumika kufikia shabaha ya kumdhalilisha Shetani. Kwa hivyo, mbinu kuu ya ushindi ni gani? Kuadibu, hukumu, kutupilia mbali laana, na kufichua—kutumia tabia ya haki katika kuwashinda watu ili waweze kushawishika kabisa kwa sababu ya tabia ya haki ya Mungu. Ili kutumia uhalisi wa neno na kutumia mamlaka ya neno ili kuwashinda watu na kuwashawishi kabisa—hii ndiyo maana ya kushindwa. Wale waliofanywa kuwa wakamilifu hawawezi tu kuwa watiifu baada ya kushindwa, lakini wanaweza pia kuwa na maarifa ya kazi ya hukumu, kubadilisha tabia yao na kumjua Mungu. Wanapitia njia ya kumpenda Mungu na wamejazwa na ukweli. Wanajua namna ya kupitia kazi ya Mungu, wanaweza kuteseka kwa ajili ya Mungu, na wanayo hiari zao wenyewe. Wale waliokamilishwa ni wale walio na ufahamu halisi wa ukweli kutokana na kupitia neno la Mungu. Wale walioshindwa ni wale wanaojua kuhusu ukweli lakini hawajakubali maana halisi ya ukweli. Baada ya kushindwa, wanatii, lakini utiifu wao wote unatokana na hukumu waliyopokea. Hawana uelewa kabisa wa hali halisi ya ukweli mwingi. Wanautambua ukweli kwa matamshi, lakini bado hawajapitia ukweli; wanauelewa ukweli, lakini hawajapitia ule ukweli. Kazi inayofanywa kwa wale wanaokamilishwa inajumuisha kuadibiwa na kuhukumiwa, pamoja na kupokea uzima. Mtu anayethamini kuingia katika ukweli ni mtu anayefaa kukamilishwa. Tofauti kati ya wale watakaofanywa kuwa wakamilifu na wale walioshindwa ni iwapo wanaingia ukweli. Wale wanaouelewa ukweli, wameingia katika ukweli, na wanauishi ukweli huo ndio wale waliokamilishwa; wale wasioelewa ukweli, hawauingii ukweli, yaani, wale wasioishi ukweli, ni watu wasioweza kukamilishwa. Ikiwa watu kama hao wanaweza sasa kutii kabisa, basi wameshindwa. Kama wale walioshindwa hawatafuti ukweli—kama wanafuata lakini hawaishi kwa njia ya ukweli, kama wanaona na kuusikia ukweli lakini hawathamini kuthamini kuishi kwa njia ya ukweli—basi hawawezi kukamilishwa. Watu ambao ni wa kufanywa kuwa wakamilifu wanatenda ukweli kulingana na mahitaji ya Mungu kwao katika njia ya ya kuelekea kukamilishwa. Kupitia haya, wanatimiza mapenzi ya Mungu, na wanapata kufanywa kuwa wakamilifu. Yeyote anayefuata hadi mwisho kabla ya kazi hiyo ya ushindi kuhitimishwa ni aliyeshindwa, lakini hawezi kusemekana kuwa ndiye aliyekamilishwa. Waliokamilishwa kunarejelea wale ambao, baada ya kumalizika kwa kazi ya ushindi, wanaweza kufuatilia ukweli na kumilikiwa na Mungu. Kunaashiria wale ambao, baada ya kukamilika kwa kazi ya ushindi, wanasimama imara katika majaribio na wanaishi kwa kudhihirisha ukweli. Kile kinachotofautisha kushindwa na kukamilishwa ni zile tofauti katika hatua za kufanya kazi na tofauti katika kiwango ambacho watu huelewa na kuingia katika ukweli. Wale wote ambao hawajaingia katika njia ya kukamilishwa, kumaanisha wale wasio na ukweli, mwishowe bado wataondolewa. Ni wale tu walio na ukweli na wanaoishi ukweli wanaoweza kumilikiwa kabisa na Mungu. Yaani, wale wanaoishi kwa kudhihirisha mfano wa Petro ndio wanaofanywa kuwa wakamilifu, huku wengine wote ndio ambao wameshindwa. Kazi inayofanywa kwa wale wote wanaoshindwa inajumuisha tu kuweka laana, kuadibu, na kuonyesha hasira, na yale yanayowajia ni haki na laana tu. Kushughulikia mtu kama huyo ni kufichua waziwazi—kufichua tabia potovu iliyo ndani yake ili aweze kuitambua mwenyewe na kushawishika kabisa. Punde binadamu anapokuwa mtiifu kabisa, kazi ya ushindi inakamilika. Hata kama watu wengi wangali hawatafuti kuelewa ukweli, kazi ya ushindi itakuwa imekamilika.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Waliokamilishwa Pekee Ndio Wanaoweza Kuishi Maisha Yenye Maana

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 214)

Mungu Anamfanyaje mwanadamu kuwa kamili? Tabia ya Mungu ni gani? Na ni nini kilicho ndani ya tabia Yake? Ili kuyabainisha mambo haya yote: mtu huliita kusambaza jina la Mungu, mtu huliita kuwa na ushuhuda kwa Mungu, na mtu huliita kumtukuza na kumsifu Mungu, na bila shaka mwanadamu atafikia mabadiliko katika tabia ya maisha yake kwa msingi wa kumjua Mungu. Kadri mwanadamu anavyopitia kushughulikiwa na kusafishwa, ndivyo nguvu yake inavyoongezeka zaidi, na hatua za Mungu zinavyozidi kuwa nyingi, ndivyo mwanadamu anavyofanywa kamili. Leo, katika uzoefu wa mwanadamu, kila hatua ya kazi ya Mungu inayagonga mawazo ya mwanadamu, na kila hatua haiwezi kuwazwa na akili ya mwanadamu, na kuzidi matarajio ya mwanadamu. Mungu Anakimu mahitaji yote ya mwanadamu, na kwa kila njia yote huwa yanakinzana na mawazo ya mwanadamu, na ukiwa mdhaifu, Mungu Ananena maneno Yake. Ni kwa njia hii tu ndio Anaweza kukupa uhai wako. Kwa kuzigonga fikira zako, unakuja kukubali kazi ya Mungu, na kwa njia hii pekee ndio unaweza kuondoa upotovu wako. Leo hii, kwa upande mmoja Mungu mwenye mwili Anafanya kazi katika uungu, na kwa upande mwingine Anafanya kazi katika ubinadamu wa kawaida. Unapoacha kuweza kukana kazi yoyote ya Mungu, unapoweza kutii bila kujali lolote Analosema Mungu au kufanya katika hali ya ubinadamu wa kawaida, unapoweza kutii na kuelewa bila kujali ni ukawaida wa aina gani Anadhihirisha: ni wakati huo tu ndio unaweza kuwa na uhakika kwamba Yeye ni Mungu, na ni hapo tu utakoma kuwa na dhana, na ni hapo tu ndio utaweza kumfuata mpaka mwisho. Kuna hekima katika kazi ya Mungu, na Anajua jinsi mwanadamu Anaweza kuwa na ushuhuda Kwake. Anajua pale ambapo udhaifu wa uhai wa mwanadamu upo, na maneno Anayozungumza yanaweza kukugonga pale penye udhaifu wako upo, lakini pia Anatumia maneno Yake makuu na yenye busara kukufanya uwe na ushuhuda Kwake. Hayo ndiyo matendo ya kimiujiza ya Mungu. Kazi inayofanywa na Mungu haiwezi kufikiriwa na akili ya mwanadamu. Hukumu ya Mungu inafunua aina za upotovu ambazo mwanadamu, kwa kuwa ni mwili, amejawa nao, na vitu vipi ndivyo umuhimu wa mwanadamu, na humwacha mwanadamu bila mahali pa kujificha aibu yake.

Mungu anafanya kazi ya hukumu na kuadibu ili kwamba mwanadamu amjue, na kwa ajili ya ushuhuda Wake. Bila hukumu Yake ya tabia potovu ya mwanadamu, basi mwanadamu hangeweza kujua tabia Yake ya haki isiyoruhusu kosa lolote, na hangeweza kubadili ufahamu Wake wa Mungu kuwa mpya. Kwa ajili ya ushuhuda Wake, na kwa ajili ya usimamizi Wake, Anafanya ukamilifu Wake kuwa wazi kwa kila mtu, hivyo kumwezesha mwanadamu kupata ufahamu wa Mungu, na kubadili tabia yake, na kuwa na ushuhuda mkuu kwa Mungu kupitia kuonekana kwa Mungu wa hadharani. Mabadiliko yanafanikishwa kwa tabia ya mwanadamu kupitia njia tofauti ya kazi ya Mungu; bila mabadiliko ya aina hii katika tabia ya mwanadamu, mwanadamu hangeweza kuwa na ushuhuda kwa Mungu, na hangekuwa wa kuupendeza moyo wa Mungu. Mabadiliko katika tabia ya mwanadamu yanaashiria kwamba mwanadamu amejiweka huru kutokana na minyororo ya Shetani, amejiweka huru kutokana na ushawishi wa giza, na kwa kweli amekuwa mfano na kifaa cha kujaribiwa cha kazi ya Mungu, amekuwa shahidi wa kweli wa Mungu na mtu aliye wa kuupendeza moyo wa Mungu. Leo hii, Mungu mwenye mwili Amekuja kufanya kazi Yake duniani, na Anahitaji kwamba mwanadamu apate ufahamu kumhusu, aweze kumtii, awe na ushuhuda Kwake—aweze kujua kazi Yake ya matendo na ya kawaida, atii maneno Yake yote na kazi ambayo haiambatani na mawazo ya mwanadamu, na kuwa na ushuhuda kwa kazi Yake yote ya kumwokoa mwanadamu, na matendo yote Anayofanya ya kumshinda mwanadamu. Wale walio na ushuhuda kwa Mungu lazima wawe na ufahamu wa Mungu; ni aina hii tu ya ushuhuda ndio ulio sahihi, na wa kweli, na ni aina hii tu ya ushuhuda ndio unaoweza kumpa Shetani aibu. Mungu Anawatumia wale waliomjua baada ya kupitia hukumu Yake na kuadibu, ushughulikiaji na upogoaji, kuwa na ushuhuda Kwake. Anawatumia wale waliopotoshwa na Shetani kumtolea Yeye ushuhuda, na vilevile Anawatumia wale ambao tabia yao imebadilika, na wale basi ambao wamepokea baraka Zake, kumtolea ushuhuda. Yeye hana haja na mwanadamu kumsifu kwa maneno tu, wala hana hitaji lolote la sifa na ushuhuda kutoka kwa namna ya Shetani, ambao hawajaokolewa na Yeye. Ni wale tu wanaomjua Mungu ndio wanaohitimu kumtolea Mungu ushuhuda, na ni wale tu ambao tabia zao zimebadilika ndio wanaofaa kumshuhudia Mungu, na Mungu hatamruhusu mwanadamu kwa makusudi aliletee jina Lake aibu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 215)

Kumbuka tukio katika Biblia ambapo Mungu aliangamiza Sodoma, na fikiria pia jinsi mke wa Lutu alivyokuwa nguzo ya chumvi. Fikiria nyuma jinsi watu wa Ninawi walitubu dhambi zao kwa gunia na majivu, na kumbuka kilichofuata baada ya Wayahudi kumsulubisha Yesu miaka 2,000 iliyopita. Wayahudi walitolewa Israeli na kukimbilia nchi duniani kote. Wengi waliuwawa, na taifa lote la Kiyahudi lilikabiliwa na uharibifu wa kipekee. Walimsulubisha Mungu—wakafanya uhalifu wa kuchukiza—na kuchochea tabia ya Mungu. Walifanywa kulipa kwa ajili ya walichofanya, walifanywa kukubali matokeo ya vitendo vyao. Walimlaani Mungu, walimkataa Mungu, na hivyo walikuwa na majaliwa moja pekee: kuadhibiwa na Mungu. Haya ndiyo matokeo machungu na maafa ambayo viongozi wao waliletea nchi na taifa lao.

Leo, Mungu amerudi duniani kufanya kazi Yake. Atasimama kwanza kwa mkutano mkubwa wa viongozi madikteta: Uchina, ngome kali ya ukanaji Mungu. Mungu amepata kundi la watu kwa hekima na nguvu Zake. Wakati huu, Anawindwa na chama tawala cha Uchina kwa kila namna na kukabiliwa na mateso makubwa, bila mahala pa kupumzisha kichwa Chake na kutoweza kupata makazi. Licha ya haya, Mungu bado anaendelea kufanya kazi Aliyonuia kufanya: Anatamka sauti Yake na kueneza injili. Hakuna anayeweza kuelewa uweza wa Mungu. Uchina, nchi inayomchukulia Mungu kama adui, Mungu hajawahi kukoma kazi Yake. Badala yake, watu zaidi wamekubali kazi na neno Lake, kwani Mungu anafanya yote Awezayo kuokoa kila mshiriki wa ubinadamu. Tunaamini hakuna nchi ama nguvu inayoweza kuzuia yale anayotaka kutimiza Mungu. Wale wanaozuia kazi ya Mungu, wanaopinga neno la Mungu, kuvuruga na kudhoofisha mpango wa Mungu hatimaye wataadhibiwa na Mungu. Anayeasi kazi ya Mungu atatumwa kuzimu; nchi yoyote inayoasi kazi ya Mungu itaangamizwa; taifa lolote linaloinuka kupinga kazi ya Mungu litafutwa kutoka dunia hii, na litakoma kuwepo. Nahimiza watu wa mataifa, nchi na hata viwanda vyote kusikiza sauti ya Mungu, kutazama kazi ya Mungu, kuzingatia majaliwa ya mwanadamu, hivyo kumfanya Mungu kuwa mtakatifu zaidi, wa heshima zaidi, wa juu zaidi na chombo cha pekee cha kuabudu miongoni mwa wanadamu, na kuruhusu wanadamu wote kuishi chini ya baraka za Mungu, kama tu ukoo wa Ibrahimu ulivyoishi chini ya ahadi ya Yehova, na kama tu Adamu na Hawa, walioumbwa awali na Mungu, walivyoishi kwa Bustani ya Edeni.

Kazi ya Mungu ni kama mawimbi yanayotapakaa kwa nguvu. Hakuna anayeweza kumweka kizuizini, na hakuna anayeweza kusimamisha nyayo Zake. Wale tu wanaosikiza maneno Yake kwa makini, na wanaomtafuta na kuwa na kiu naye, wanaweza kufuata nyayo Zake na kupokea ahadi Zake. Wasiofanya hivyo watakabiliwa na maafa makuu na adhabu inayostahili.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 2: Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 216)

Kazi ya usimamizi wa Mungu ilianza Alipoumba ulimwengu, na mwanadamu ni kiini cha kazi Yake. Uumbaji wa Mungu wa kila kitu, unaweza kusemwa, ni kwa ajili ya mwanadamu. Kwa sababu Kazi ya usimamizi Wake imesambaa katika maelfu ya miaka, na haijatekelezwa katika dakika na sekunde tu, ama kufumba na kufumbua, ama katika mwaka mmoja au miwili, ilimbidi Aumbe vitu vingine zaidi kwa ajili ya maisha ya mwanadamu, kama vile jua, mwezi, na aina zote za viumbe walio hai, na chakula na mazingira kwa ajili ya wanadamu. Huu ndio ulikuwa mwanzo wa usimamizi wa Mungu.

Baada ya hapo, Mungu Alimkabidhi mwanadamu kwa Shetani, mwanadamu aliishi chini ya miliki ya Shetani, na hili taratibu lilisababisha kazi ya Mungu ya enzi ya kwanza: hadithi ya Enzi ya Sheria…. Kipindi cha miaka elfu kadhaa za Enzi ya Sheria, wanadamu walikuwa wazoefu wa maelekezo ya Enzi ya Sheria, na wakaanza kupuuza, na taratibu wakaacha ulinzi wa Mungu. Na hivyo, pamoja na kushikilia sheria, walimwabudu Mungu na kutenda matendo maovu. Walikuwa bila ulinzi wa Yehova, na waliishi tu mbele ya madhabahu ndani ya hekalu. Kwa kweli, Kazi ya Mungu ilikuwa imejitenga nao kitambo sana, na hata kama Waisraeli walijikita katika sheria, na kulitaja jina la Yehova, na kwa majivuno kuamini kuwa wao pekee ndio walikuwa watu wa Yehova na walikuwa wamechaguliwa na Yehova, utukufu wa Mungu uliwaacha kimyakimya …

Mungu Anapofanya kazi Yake, huacha sehemu moja na taratibu hutekeleza kazi Yake katika sehemu nyingine mpya. Hii huonekana ya kiajabu sana kwa watu ambao wamepooza. Watu wameishi kuvithamini vya zamani na kuvirejelea vipya, vitu visivyofahamika kwa uhasama, au hata kuonekana kama bughudha. Aidha, kazi yoyote mpya Aifanyayo Mungu, kutoka mwanzo hadi mwisho, mwanadamu ndiye huwa wa mwisho kufahamu kuihusu miongoni mwa kila kitu.

Kama ilivyokuwa kawaida, baada ya kazi ya Yehova katika Enzi ya Sheria, Mungu Alianza kazi yake ya hatua ya pili: kwa kuutwaa mwili—kuwa na mwili kama binadamu kwa miaka kumi, ishirini—na kuongea na kufanya kazi Yake Kati ya waumini. Na bado bila mapendeleo, hakuna aliyejua, na ni idadi ndogo tu ya watu walitambua kuwa Alikuwa Mungu Aliyepata mwili baada ya Yesu Kristo kupigiliwa misumari msalabani na kufufuka. … Baada tu ya kazi ya Mungu katika hatua ya pili kukamilika—baada ya kusulubishwa—kazi ya Mungu ya kutoa mwanadamu kwenye dhambi (ambayo ni kusema, kumtoa mwanadamu mikononi mwa Shetani) ilitimilika. Na hivyo, kutoka wakati huo kuendelea mbele, wanadamu walipaswa tu kumpokea Yesu Kristo kama Mwokozi ili dhambi zao ziweze kusamehewa. Yaani, dhambi za wanadamu hazikuwa tena kizuizi cha kuufikia wokovu wake na kuja mbele za Mungu na hazikuwa tena nguvu za kushawishi ambazo Shetani alitumia kumlaumu mwanadamu. Hii ni kwa sababu Mungu Mwenyewe Alikuwa Amefanya kazi halisi, na kuwa katika mfano na limbuko la mwili wenye dhambi, na Mungu mwenyewe Alikuwa sadaka ya dhambi. Kwa njia hii, mwanadamu alishuka kutoka msalabani, akiwa amekombolewa na mwili wa Mungu, mfano wa huu mwili wa dhambi. Na hivyo, baada ya kushikwa mateka na Shetani, mwanadamu alikuja hatua moja mbele karibu na kukubali wokovu mbele za Mungu. Kwa hakika, huu ulingo wa kazi ndio ulikuwa usimamizi wa Mungu ambao ulikuwa hatua moja mbali na Enzi ya sheria, na wa kiwango cha ndani kuliko Enzi ya Sheria.

Huu ni mfano wa usimamizi wa Mungu: kuwakabidhi wanadamu kwa Shetani—wanadamu ambao hawajui kile Mungu Alicho, Muumba ni nini, jinsi ya kumwabudu Mungu, na ni kwa nini inafaa kujitoa kwa Mungu—na kutoa utawala huru kwa uovu wa Shetani. Hatua baada ya hatua, Mungu Anamtoa mwanadamu mikononi mwa Shetani, hadi mwanadamu amwabudu Mungu kikamilifu na kumkataa Shetani. Huu ndio usimamizi wa Mungu. Hili linasikika kama hadithi ya visasili; na inaonekana inatatanisha. Watu wanahisi kwamba ni kama hadithi ya visasili, na hii ni kwa sababu hawana fununu kuhusu yaliyomtokea mwanadamu katika maelfu ya miaka iliyopita, sembuse kujua hadithi ngapi ambazo zimetokea katika ulimwengu na anga. Na zaidi ya hayo, hii ni kwa sababu hawawezi kufahamu kinachostaajabisha sana, dunia inayoibua hofu zaidi ambayo iko zaidi ya dunia yakinifu, lakini ambayo macho yao ya mwili yanawazuia kuiona. Inasikika ya kutofahamika kwa mwanadamu. Na hii ni kwa sababu mwanadamu hana ufahamu wa umuhimu wa Mungu kumwokoa na umuhimu wa kazi ya usimamizi wa Mungu, na hafahamu jinsi Mungu Anavyotamani zaidi wanadamu wawe. Je, ni wanadamu mfano wa Adamu na Hawa, wasiopotoshwa na Shetani? Hapana! Usimamizi wa Mungu ni kwa ajili ya kupata kikundi cha watu ambao humwabudu Mungu na kujitoa kwake. Hawa wanadamu wamepotoshwa na Shetani, lakini hawamwoni Shetani kama baba yao: hutambua uso usiopendeza wa Shetani, na kuukataa, na kuja mbele Zake Mungu na kukubali hukumu na kuadibu Kwake. Hujua kisichopendeza na jinsi kinavyotofautiana na kile kilicho kitakatifu, na hutambua ukubwa wa Mungu na uovu wa Shetani. Wanadamu kama hawa hawatamfanyia Shetani kazi tena, au kumwabudu Shetani, au kumsetiri Shetani. Hii ni kwa sababu wao ni kikundi cha watu ambao wamemilikiwa na Mungu. Huu ndio umuhimu wa Mungu kuwasimamia wanadamu. Katika kazi ya usimamizi wa Mungu wa wakati huu, wanadamu ndio chombo cha maovu ya Shetani, na kwa wakati uo huo ni chombo cha ukombozi wa Mungu, aidha ni sababu ya vita dhidi ya Mungu na Shetani. Wakati sawia na wakati wa kutekeleza kazi Yake, Mungu taratibu Humtoa mwanadamu kutoka mikononi mwa Shetani, na hivyo mwanadamu anakuja karibu zaidi na Mungu …

Baadaye kukaja Enzi ya Ufalme, ambayo ni hatua ya utendaji zaidi na bado ni ngumu zaidi kukubalika na mwanadamu. Hii ni kwa sababu jinsi mwanadamu ajavyo karibu na Mungu, ndivyo afikapo karibu na kiboko cha Mungu, na ndivyo uso wa Mungu unavyokuwa wazi mbele ya mwanadamu. Kwa kufuatia kukombolewa kwa wanadamu, mwanadamu kirasmi anarejelea familia ya Mungu. Mwanadamu alifikiria kuwa huu ndio wakati wa kufurahia, bado ameegemezwa kwa shambulizi la Mungu na mifano ya yale ambayo bado hayajaonekana na yeyote: Inavyokuwa, huu ni ubatizo ambao watu wa Mungu wanapaswa “kuufurahia.” Katika muktadha huo, watu hawana lingine ila kuacha na kujifikiria wao wenyewe, Mimi ndimi mwanakondoo, aliyepotea kwa miaka mingi, ambaye Mungu Amegharamika kumnunua, sasa kwa nini Mungu Ananitendea hivi? Ama ni njia ya Mungu kunicheka, na kunifichua? … Baada ya miaka mingi kupita, mwanadamu amedhoofika, kwa kuupitia ugumu wa usafishaji na kuadibu. Ijapokuwa mwanadamu amepoteza “utukufu” na “mapenzi” ya wakati uliopita, bila ya kufahamu amekuja kuelewa kanuni za tabia ya mwanadamu, na amekuja kutambua kazi ya Mungu ya kujitolea kuokoa wanadamu. Taratibu mwanadamu anaanza kuchukia ushenzi wake mwenyewe. Anaanza kuchukia jinsi alivyo mkali, na lawama kuelekea kwa Mungu, na mahitaji yote yasiyokuwa na mwelekeo aliyodai kutoka Kwake. Wakati hauwezi ukarudishwa nyuma, matendo ya zamani huwa ya kujuta katika kumbukumbu za mwanadamu, na maneno na upendo wa Mungu vinakuwa ndivyo vinavyomwendesha mwanadamu katika maisha Yake mapya. Majeraha ya mwanadamu hupona siku baada ya siku, nguvu humrudia, na akasimama na kutazamia uso Wake mwenye Uweza … ndipo anagundua kuwa daima Ameishi kando yangu, na kwamba tabasamu Lake na sura Yake ya kupendeza bado zinasisimua. Moyo Wake bado unawajali wanadamu Aliowaumba, na mikono Yake bado ina joto na nguvu kama ilivyokuwa hapo mwanzoni. Ni kama mwanadamu alirudi kwenye bustani ya Edeni, lakini wakati huu mwanadamu hasikizi ushawishi wa nyoka, na hatazami kando na uso wa Yehova. Mwanadamu anapiga magoti mbele ya Mungu, na kutazama uso Wake wenye tabasamu, na kumtolea Mungu kafara yenye thamani—Ee! Bwana wangu, Mungu wangu!

Upendo na huruma za Mungu hupenyeza katika kila sehemu ya kazi ya usimamizi Wake, na bila kujali kama watu wanaweza kuelewa nia njema za Mungu, bado Anafanya Kazi bila kuchoka na Anapania kuikamilisha. Haijalishi ni kwa kiasi gani watu wanaelewa usimamizi wa Mungu, manufaa na usaidizi wa Kazi inayofanywa na Mungu unaweza kukubalika na kila mtu. Labda, leo, hujahisi upendo wowote au maisha yaliyowezeshwa na Mungu, lakini bora tu humwachi Mungu, na hupotezi matumaini yako ya kutafuta ukweli, basi kutakuwa na siku ambapo tabasamu la Mungu litafichuliwa kwako. Kwa kuwa dhumuni la kazi ya usimamizi wa Mungu ni kuwatoa wanadamu wanaomilikiwa na Shetani, sio kuwaacha wanadamu waliopotoshwa na Shetani na kumpinga Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 3: Mwanadamu Anaweza tu Kuokolewa Katikati ya Usimamizi wa Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 217)

Watu wote wanahitaji kuelewa kusudio la kazi Yangu ulimwenguni, yaani, lengo la mwisho la kazi Yangu na ni kiwango kipi ambacho lazima Nitimize katika kazi hii kabla inaweza kukamilika. Kama, baada ya kutembea na Mimi hadi leo, watu hawaelewi kazi Yangu inahusu nini, basi hawajakuwa wakitembea na Mimi bure? Watu wanaonifuata Mimi wanafaa kujua mapenzi Yangu. Nimekuwa nikifanya kazi ulimwenguni kwa maelfu ya miaka, na hadi leo ningali nafanya kazi Yangu vivyo hivyo sasa. Ingawa kunavyo vipengele vingi hasa vilivyojumuishwa katika kazi Yangu, kusudio la kazi hii linabakia lilelile. Kwa mfano, ingawa Nimejazwa na hukumu na adabu kwa binadamu, kila ninachofanya bado ni kwa ajili ya kumwokoa binadamu, kwa ajili ya kueneza injili Yangu kwa njia bora zaidi na kupanua zaidi kazi Yangu miongoni mwa Mataifa baada ya binadamu kufanywa kuwa kamili. Kwa hiyo leo, katika wakati ambapo watu wengi tayari wametamauka pakubwa, Naendelea na kazi Yangu, Nikiendeleza kazi ambayo lazima Nifanye ili kuhukumu na kuadibu binadamu. Licha ya ukweli kwamba binadamu amechoshwa na kile Ninachosema na licha ya ukweli kwamba hana tamanio la kujali kuhusu kazi Yangu, Ningali natekeleza wajibu Wangu kwa sababu kusudio la kazi Yangu halijabadilika na mpango Wangu asilia hautabadilika. Kazi ya hukumu Yangu ni kumfanya binadamu anitii Mimi kwa njia bora zaidi, na kazi ya kuadibu Kwangu ni kuruhusu binadamu awe na mabadiliko bora zaidi. Ingawa kile Ninachofanya ni kwa minajili ya usimamizi Wangu, Sijawahi kufanya chochote ambacho hakikufaidi binadamu. Hiyo ndiyo maana Nataka kufanya mataifa yote nje ya Israeli kuwa matiifu tu kama Waisraeli na kuwabadilisha kuwa binadamu halisi, ili Niwe na mahali pa usalama katika nchi zilizo nje ya Israeli. Huu ndio usimamizi Wangu; ndiyo kazi Ninayotimiza katika nchi za Mataifa. Hata sasa, watu wengi bado hawauelewi usimamizi Wangu kwa sababu hawajautilia maanani, badala yake wanafikiria tu kuhusu mustakabali na hatima zao. Haijalishi ni nini Ninachosema, watu hawajali kazi Yangu, badala yake wanalenga tu hatima zao za baadaye. Mambo yakiendelea kwa namna hii, kazi Yangu itapanuliwa vipi? Injili Yangu itaenezwa vipi kotekote ulimwenguni? Lazima mjue kwamba wakati kazi Yangu inapanuka, Nitawatawanya, Nitawaadhibu kama vile tu Yehova alivyoyaadhibu makabila ya Israeli. Haya yote yatafanywa ili injili Yangu iweze kuenea kotekote kwenye ulimwengu mzima, ili kazi Yangu iweze kuenezwa kwa Mataifa, ili kwamba jina Langu litukuzwe na watu wazima na watoto kwa pamoja na jina Langu takatifu litatukuzwa katika vinywa vya watu kutoka makabila na mataifa yote. Ili kwamba katika enzi hii ya mwisho jina Langu litatukuzwa miongoni mwa Mataifa, kwamba matendo Yangu yataonekana na mataifa mengine na wataniita Mwenyezi kwa sababu ya matendo Yangu, na kwamba maneno Yangu yatatimika karibuni. Nitawafanya watu wote wajue kwamba Mimi siye tu Mungu wa Waisraeli, lakini Mimi ni Mungu wa Mataifa yote, hata mataifa yale Niliyoyalaani. Nitawafanya watu wote waone kwamba Mimi ndimi Mungu wa viumbe vyote. Hii ndiyo kazi Yangu kubwa zaidi, kusudio la mpango wa kazi Yangu katika siku za mwisho, na kazi ya pekee kutimizwa katika siku za mwisho.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 218)

Kazi ambayo Nimekuwa nikisimamia kwa maelfu ya miaka inafichuliwa kabisa tu kwa binadamu katika siku za mwisho. Ni sasa tu ndipo Nimelifumbua fumbo kamili la usimamizi Wangu kwa mwanadamu. Binadamu anajua kusudio la kazi Yangu na zaidi ya yote anapata uelewa wa mafumbo Yangu yote. Na Nimemwambia binadamu kila kitu kuhusu hatima ambayo amekuwa akijali kuhusu. Tayari Nimemfichulia binadamu mafumbo yote yaliyofichwa kwa zaidi ya miaka 5,900. Yehova ni nani? Masiha ni nani? Yesu ni nani? Mnafaa kuyajua haya yote. Mabadiliko makubwa ya kazi Yangu yamo katika majina haya. Je, mmeelewa haya? Jina Langu takatifu linafaa kutangazwa vipi? Jina Langu linafaa kuenezwaje katika taifa lolote ambalo limeniita kwa jina Langu lolote? Kazi Yangu tayari imeanza kupanuka, na Nitaeneza ukamilifu wake katika mataifa yote. Kwa sababu kazi Yangu imetekelezwa ndani yenu, Nitawapiga kama vile Yehova alivyowapiga wale wachungaji wa nyumba ya Daudi kule Israeli, na kuwasababisha kutawanyika miongoni mwa mataifa yote. Kwani katika siku za mwisho, Nitapondaponda mataifa yote kuwa vipande vidogo vidogo na kusababisha watu wao kuenezwa upya. Nitakaporudi tena, mataifa yatakuwa tayari yamegawanywa kwa mipaka iliyowekwa na mwako wa moto Wangu utakaokuwa ukichoma. Katika wakati huo, Nitajionyesha upya kwa binadamu kama jua linalochoma, Nikijionyesha kwao hadharani kwa taswira ya yule Aliye Mtakatifu ambaye hawajawahi kumwona, Nikitembea miongoni mwa mataifa yote, kama vile tu Mimi, Yehova, Nilivyotembea miongoni mwa makabila ya Wayahudi. Kuanzia hapo kuendelea, Nitawaongoza watu huku wakiishi ulimwenguni. Hakika watauona utukufu Wangu hapo na hakika wataona pia nguzo ya wingu hewani ili uwaongoze, kwani Nitaonekana katika sehemu takatifu. Binadamu ataiona siku Yangu ya haki na pia maonyesho Yangu ya utukufu. Hilo litafanyika Nitakapoutawala ulimwengu mzima na kuwaleta wana wengi katika utukufu. Kila pahali duniani, watu watainama, nalo hema Langu takatifu litaundwa miongoni mwao juu ya mwamba wa kazi ambayo Natekeleza sasa. Watu watanihudumia pia hekaluni. Madhabahu, yaliyojaa mambo machafu na ya kuchukiza, Nitayavunjavunja vipandevipande na Nitajenga upya mengine. Madhabahu matakatifu yatarundikwa wanakondoo na ndama waliozaliwa karibuni. Nitaangusha hekalu lililopo leo na kujenga jingine upya. Hekalu lililopo sasa na lililojaa watu wenye chuki litaporomoka na lile Nitakalojenga litajaa watumishi watiifu Kwangu. Kwa mara nyingine watasimama na kunihudumia Mimi kwa utukufu wa hekalu Langu. Kwa hakika mtaiona siku ambayo Nitapokea utukufu mkuu na hakika mtaiona siku ambayo Nitaliangusha hekalu na kujenga lingine upya. Pia, hakika mtaona siku ya kuletwa kwa hema Langu takatifu hapa ulimwenguni mwa binadamu. Huku Nikilibomoa hekalu, ndivyo Nitakavyoleta hema Langu takatifu hapa ulimwenguni mwa binadamu; itakuwa kama vile tu ambavyo watu wanavyoniona Nikishuka. Baada ya kuangamiza mataifa yote, Nitayakusanya pamoja upya, Nikilijenga hekalu Langu na kuandaa madhabahu Yangu, ili wote waweze kutoa kafara zao Kwangu, kunihudumia Mimi hapo, na kujitolea kwa uaminifu katika kazi Yangu kwenye mataifa mengineyo. Itafanywa namna tu ambavyo wana wa Israeli wanavyofanya sasa, na joho la kuhani na taji la mfalme, utukufu Wangu, Yehova, ukiwa miongoni mwao na uadhama Wangu ukivinjari juu yao na ukiwa nao. Kazi Yangu katika Mataifa itatekelezwa pia katika njia hiyo. Kama vile kazi Yangu kule Israeli ilivyokuwa, ndivyo kazi Yangu katika Mataifa itakavyokuwa kwa sababu Nitaongeza kazi Yangu kule Israeli na kuieneza katika mataifa yale mengine.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 219)

Sasa ndio wakati ambao Roho Wangu anafanya kazi pakubwa, na wakati Ninapofanya kazi miongoni mwa Mataifa. Hata zaidi, ndio wakati ambapo Naainisha viumbe wote na kuweka kila kiumbe katika kundi lenye uhusiano, ili kazi Yangu iweze kuendelea haraka zaidi na kwa njia ya kufaa zaidi. Kwa hiyo, bado Nahitaji kwamba mjitoe mzimamzima kwa minajili ya kazi Yangu yote; aidha, mnafaa kutambua waziwazi na kuwa na hakika ya kazi ile yote ambayo Nimefanya ndani yako, na kuweka nguvu zako zote katika kazi Yangu ili iweze kuwa ya matokeo bora zaidi. Hilo ndilo ambalo lazima uelewe. Msipigane tena wenyewe kwa wenyewe, kutafuta mbinu za usuluhishi, au kutafuta raha za mwili, mambo ambayo yanaweza kuchelewesha kazi Yangu na kuharibu mustakabali wako mzuri. Kufanya hivyo, mbali na kuweza kukupa ulinzi, litakuletea maangamizo. Je, si huu utakuwa ujinga kwa upande wako? Kile ambacho unafurahia leo kwa tamaa ndicho kile kile ambacho kinaharibu mustakabali wako, huku yale maumivu unayopitia leo ndiyo yaleyale ambayo yanakulinda. Lazima ufahamu waziwazi kuhusu jambo hilo, ili uepuke majaribio ambayo yatakuwa magumu kujinasua kutoka na kuepuka kuingia kwenye ukungu mzito unaozuia jua katika maisha yako. Wakati ukungu huu mzito utakapotoweka, utajipata katika hukumu ya siku kuu. Kufikia wakati huo, siku Yangu itakuwa imekaribia binadamu. Utatorokaje hukumu Yangu? Utawezaje kuvumilia joto kali la jua? Ninapompa binadamu wingi Wangu, haufurahii kwa dhati, lakini badala yake anautupa nje kwenye sehemu zisizotambulika. Wakati siku Yangu itawadia, binadamu hataweza tena kugundua wingi Wangu au kupata ukweli mkali Niliompa zamani sana. Ataomboleza na kulia, kwa sababu amepoteza mwangaza anaofuata na kuingia katika giza totoro. Kile mnachoona leo ni upanga tu mkali wa kinywa Changu. Bado hamjakiona kiboko kilicho katika mkono Wangu au moto Ninaotumia kumchoma binadamu, na ndiyo maana bado mna kiburi na msio na kadiri mbele Yangu. Ndiyo maana bado mnapigana na Mimi katika nyumba Yangu, huku mkipinga kwa ulimi wa mwanadamu kile ambacho Nimenena na kinywa Changu. Binadamu haniogopi Mimi. Akiwa bado katika uhasama na Mimi hadi leo, bado haniogopi kamwe. Mnao ulimi na meno ya wale wasio na haki vinywani mwenu. Maneno na matendo yenu ni kama yale ya yule nyoka aliyemshawishi Hawa na kumfanya kutenda dhambi. Mnadai nyinyi kwa nyinyi kulipiza kisasi, na mnashindana mbele Yangu kwa ajili ya nafasi, umaarufu, na faida kwa ajili yenu wenyewe, ilhali hamjui kwamba Natazama maneno na matendo yenu kwa siri. Kabla hata ya nyinyi kuja mbele Yangu, Nimejua vina vya nyoyo zenu kabisa. Siku zote binadamu hutamani kutoroka kutoka mfumbato Wangu na kuepuka uangalizi wa macho Yangu, lakini Sijawahi kuepuka maneno au matamshi yake. Badala yake, kwa kusudio kuu huwa Nayaruhusu maneno na matendo hayo yaingie katika macho Yangu, ili Niweze kuadibu udhalimu wake na kuhukumu uasi wake. Kwa hiyo, maneno na matendo fiche ya binadamu siku zote yanawekwa mbele ya kiti Changu cha hukumu, na hukumu Yangu haijawahi kumtoka binadamu, kwa sababu uasi wake ni mwingi mno. Kazi Yangu ni kuteketeza na kusafisha maneno na matendo yote ya binadamu yaliyotamkwa na kufanywa mbele ya Roho Wangu. Kwa njia hiyo, baada ya Mimi kuondoka ulimwenguni, binadamu wataweza bado kuendeleza utiifu Kwangu, na bado watanihudumia kama vile watumishi Wangu watakatifu wanavyofanya katika kazi Yangu, wakiruhusu kazi Yangu hapa ulimwenguni iendelee mpaka siku itakapokamilika.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 220)

Je, mmeona kazi ambayo Mungu ataikamilisha katika kundi hili la watu? Mungu alisema, hata katika Ufalme wa Milenia watu ni lazima waendelee kufuata matamshi Yake, na katika maisha ya baadaye, matamshi ya Mungu bado yatakuwa yanaongoza maisha ya mwanadamu moja kwa moja kwenda katika nchi ya Kanaani. Musa alipokuwa jangwani, Mungu alimwelekeza na kuzungumza naye moja kwa moja. Kutoka mbinguni Mungu alituma chakula, maji, na mana ili watu waweze kuvifurahia, na leo bado ni hivyo: Mungu mwenyewe ametuma vitu chini kwa ajili ya kula na kunywa ili watu wafurahi, na yeye mwenyewe ametuma laana ili kuwaadibu watu. Na hivyo kila hatua ya kazi Yake inafanywa na Mungu Mwenyewe. Leo, watu wanatamani utokeaji wa kweli, wanajaribu kuona ishara na maajabu, na kuna uwezekano mkubwa watu wa namna hiyo kutelekezwa, maana kazi ya Mungu inazidi kuwa halisi. Hakuna anayejua kwamba Mungu ameshuka kutoka mbinguni, bado hawajui kwamba Mungu ametuma chini chakula na maji ya kutia nguvu kutoka mbinguni, lakini Mungu kimsingi yupo, na mazingira mazuri ya Ufalme wa Milenia ambao watu wanaufikiria pia ni matamshi ya Mungu Mwenyewe. Huu ni ukweli, ni huu tu ndio unaotawala pamoja na Mungu duniani. Kutawala na Mungu duniani kunarejelea mwili. Kile ambacho si cha mwili hakipo duniani, na hivyo wale wote wanaojikita katika kusonga mbele katika mbingu ya tatu wanafanya hivyo bure. Siku moja, ambapo ulimwengu mzima utarudi kwa Mungu, kitovu cha kazi Yake katika ulimwengu wote kitafuata matamko ya Mungu; kwingineko watu watapiga simu, wengine watapanda ndege, wengine watapanda boti na kupita baharini, na wengine watatumia leza kupokea matamshi ya Mungu. Kila mmoja atakuwa anatamani na mwenye shauku, wote watakuja karibu na Mungu, na kukusanyika kwa Mungu, na wote watamwabudu Mungu—na yote haya yatakuwa matendo ya Mungu. Kumbuka hili! Mungu hawezi kuanza tena kwingineko. Mungu atatimiza ukweli huu: Atawafanya watu wote ulimwengu mzima kuja mbele Yake, na kumwabudu Mungu duniani, na kazi Yake katika maeneo mengine itakoma, na watu watalazimishwa kutafuta njia ya kweli. Itakuwa kama Yusufu: Kila mtu alimwendea kwa ajili ya chakula, na kumsujudia, kwa sababu alikuwa na vyakula. Ili kuweza kuepuka njaa watu watalazimishwa kutafuta njia ya kweli. Jumuiya yote ya kidini itapitia njaa kubwa, na ni Mungu tu wa leo ndiye chemchemi ya maji ya uzima, akiwa na kisima chenye maji yasiyokauka kilichotolewa kwa ajili ya furaha ya mwanadamu, na watu watakuja na kumtegemea. Huo ndio utakuwa muda ambapo matendo ya Mungu yatafichuliwa, na Mungu atatukuzwa; watu wote katika ulimwengu wote watakuja na kumwabudu “mtu” asiyekuwa wa kawaida. Je, hii haitakuwa siku ya utukufu wa Mungu? Siku moja, wachungaji wa zamani watatuma ujumbe wakitafuta maji kutoka katika chemchemi za maji ya uzima. Watakuwa wazee, lakini watakuja kumwabudu mtu huyu ambaye walimdharau. Katika vinywa vyao watakiri na katika mioyo yao wataamini—je, hii si ishara na maajabu? Siku ambapo ufalme wote utafurahia ni siku ya utukufu wa Mungu, na mtu yeyote atakayewajia, na kupokea habari njema za Mungu atabarikiwa na Mungu, na nchi hizi na watu hawa watabarikiwa na kulindwa na Mungu. Mwelekeo wa maisha yajayo utakuwa hivi: Wale ambao watapata matamshi kutoka katika kinywa cha Mungu watakuwa na njia ya kutembea duniani, na wawe wafanya biashara au wanasayansi, au waelimishaji au wataalamu wa viwandani, wale ambao hawana maneno ya Mungu watakuwa na wakati mgumu wa kuchukua hata hatua moja, na watalazimishwa kutafuta njia ya kweli. Hiki ndicho kinamaanishwa na, “Ukiwa na ukweli utatembea ulimwengu mzima; bila ukweli, hutafika popote.” Ukweli ni huu: Mungu atatumia Njia (ikiwa na maana kwamba maneno Yake yote) kuuamuru ulimwengu wote na kumwongoza na kumshinda mwanadamu. Watu siku zote wanatarajia kuwa na mageuko makubwa katika namna ambayo Mungu anafanya kazi. Kuzungumza kwa wazi, ni kupitia maneno ndipo Mungu anawadhibiti watu, na unapaswa kufanya kile Anachokisema haijalishi kama unataka au hutaki; huu ni ukweli halisi, na unapaswa kutiiwa na watu wote, na hivyo haubadiliki, na kujulikana kwa wote.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufalme wa Milenia Umewasili

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 221)

Maneno ya Mungu yataenea katika nyumba zisizohesabika, yatafahamika kwa wote, na wakati huo tu ndipo kazi yake itaenea ulimwenguni kote. Ambapo ni sawa na kusema, ikiwa kazi ya Mungu itaenea ulimwenguni kote, basi maneno Yake ni lazima yaenee. Katika siku ya utukufu wa Mungu, maneno ya Mungu yataonesha nguvu yake na mamlaka. Kila neno Lake kuanzia wakati huo hadi leo litatimizwa na kuwa la kweli. Kwa njia hii, utukufu utakuwa wa Mungu duniani—ambavyo ni sawa na kusema, kazi yake itatawala duniani. Wote ambao ni waovu wataadibiwa na maneno katika kinywa cha Mungu, wale wote ambao ni wa haki watabarikiwa na maneno katika kinywa Chake, na wote watathibitishwa na kukamilishwa na maneno katika kinywa Chake. Wala hataonyesha ishara zozote na maajabu; yote yatakamilishwa na maneno Yake, na maneno Yake yatazalisha ukweli. Kila mtu duniani atasherehekea maneno ya Mungu, ama ni watu wazima au watoto, wanaume, wanawake, wazee, au vijana, watu wote watajinyenyekeza katika maneno ya Mungu. Maneno ya Mungu yaonekana katika mwili, yakiwaruhusu watu kuyaona duniani, waziwazi na kufanana na kiumbe chenye uhai. Hii ndiyo maana ya Neno kufanyika mwili. Mungu amekuja duniani kwa lengo la kukamilisha ukweli wa “Neno kufanyika mwili,” ni sawa na kusema, Amekuja ili kwamba maneno Yake yaweze kutolewa kutoka katika mwili (sio kama wakati wa Musa katika Agano la Kale, ambapo Mungu alizungumza moja kwa moja kutoka mbinguni). Baada ya hapo, kila neno Lake litatimizwa wakati wa Enzi ya Ufalme wa Milenia, zitakuwa ni kweli ambazo zitaonekana katika macho ya watu, na watu watazitazama kwa kutumia macho bila tofauti hata kidogo. Hii ndiyo maana kuu ya Mungu kupata mwili. Ni sawa na kusema, kazi ya Roho imetimizwa kupitia mwili, na kupitia maneno. Hii ndiyo maana ya kweli ya “Neno kufanyika mwili” na “Neno Laonekana katika mwili.” Ni Mungu pekee ndiye anayeweza kuzungumza mapenzi ya Roho, na ni Mungu pekee katika mwili ndiye anayeweza kuzungumza kwa niaba ya Roho; maneno ya Mungu yamewekwa wazi katika Mungu kupata mwili, na kila mtu anaongozwa nayo. Hakuna aliyeachwa, wote wanakuwa ndani ya mawanda haya. Ni kutoka tu katika matamshi haya ndipo watu wanaweza kujua; wale ambao hawatapata njia hii wanaota ndoto za mchana ikiwa wanadhani wanaweza kupata matamshi kutoka mbinguni. Hayo ndiyo mamlaka yaliyooneshwa katika mwili wa Mungu uliopata mwili: kuwafanya wote kuamini. Hata wataalamu wa kuheshimiwa sana na wachungaji hawawezi kuzungumza maneno haya. Wote ni lazima wajinyenyekeze chini yao, na hakuna anayeweza kuanza mwanzo mpya. Mungu atatumia maneno kuushinda ulimwengu. Atafanya hivi si kwa kupata kwake mwili, lakini kwa kutumia matamshi kutoka kwa Mungu katika mwili kushinda watu wote duniani; Namna hii tu ndiye Mungu katika mwili, na huu tu ndio kuonekana kwa Mungu katika mwili. Labda kwa watu, inaonekana kana kwamba Mungu hajafanya kazi kubwa—lakini Mungu analazimika kutamka maneno Yake ili watu washawishike kabisa, na wao kutishika kabisa. Bila kweli, watu wanapiga makelele na kupiga mayowe; kwa maneno ya Mungu, wote wananyamaza kimya. Mungu hakika atakamilisha ukweli huu, maana huu ni mpango ulioanzishwa na Mungu: kukamilisha ukweli wa Neno kuwasili duniani. Kimsingi, sina haja ya kuelezea—kuwasili kwa Ufalme wa Milenia duniani ni kuwasili kwa neno la Mungu duniani. Kushuka kwa Yerusalemu mpya kutoka mbinguni ni kuwasili kwa maneno ya Mungu kuishi miongoni mwa mwanadamu, kuenenda na kila tendo la mwanadamu, na mawazo yake yote ya ndani. Huu pia ni ukweli kwamba Mungu atatimiza, na mandhari mazuri kabisa ya Ufalme wa Milenia. Huu ndio mpango uliowekwa na Mungu: Maneno Yake yataonekana duniani kwa miaka elfu moja, na yatashuhudia matendo yake yote, na kukamilisha kazi Yake yote duniani, ambapo baada ya hatua hii mwanadamu atakuwa amefikia kikomo.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufalme wa Milenia Umewasili

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 222)

Wakati Sinim inapofanikishwa duniani—wakati ufalme unapofanikishwa—hakutakuwa na vita tena duniani, hakutakuwa tena na njaa, tauni, na matetemeko ya ardhi; watu wataacha kutengeneza silaha za uharibifu, wote wataishi kwa amani na utulivu; na kutakuwa na shughuli za kawaida kati ya watu, na shughuli za kawaida kati ya mataifa. Hata hivyo wakati uliopo haulinganishwi na hili. Yote chini ya mbingu yako katika machafuko, mapinduzi yanaanza hatua kwa hatua katika kila nchi. Mungu anapotamka sauti Yake watu wanabadilika hatua kwa hatua, na, kwa ndani, kila nchi inaharibika polepole. Misingi imara ya Babiloni inaanza kutetemeka, kama kasri kwenye mchanga, na makusudi ya Mungu yanavyobadilika, mabadiliko makubwa yanatokea ulimwenguni bila kutambuliwa, na kila aina ya ishara zinaonekana wakati wowote, zikiwaonyesha watu kuwa siku ya mwisho ya dunia imewadia! Huu ni mpango wa Mungu, hizi ni hatua ambazo kwazo Yeye anafanya kazi, na hakika kila nchi itapasuka vipande vipande, Sodoma ya kale itaangamizwa mara ya pili, na hivyo Mungu anasema “Dunia inaanguka! Babeli imelemaa!” Hakuna mtu ila Mungu Mwenyewe anayeweza kufahamu jambo hili kabisa; kuna, hata hivyo, kikomo kwa ufahamu wa watu. Kwa mfano, mawaziri wa masuala ya ndani wanaweza kujua kwamba hali za sasa si imara na kuna machafuko, lakini hawawezi kuzishughulikia. Wanaweza tu kuvumilia, wakitaraji mioyoni mwao siku ambayo wanaweza kuwa na ujasiri, wakitamani kwamba siku itakuja wakati jua litachomoza tena upande wa mashariki, likiangaza kutoka upande mmoja hadi upande mwingine wa nchi na kugeuza hali hii ya kusikitisha ya mambo. Hawajui hata kidogo, hata hivyo, kwamba wakati jua linapochomoza kwa mara ya pili, kutoka kwa jua sio kwa ajili ya kurejesha utaratibu wa kale—huu ni ufufuo, mabadiliko. Huo ndio mpango wa Mungu kwa ulimwengu wote. Yeye atasababisha ulimwengu mpya, lakini zaidi ya yote, Atamfanya mwanadamu upya kwanza.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufafanuzi wa Mafumbo ya “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima”, Sura ya 22 na 23

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 223)

Duniani, mitetemeko ya ardhi ni mwanzo wa maafa. Kwanza, Ninaufanya ulimwengu, yaani dunia, ubadilike. Hiyo inafuatwa na mapigo na njaa. Huu ni mpango Wangu, hizi ni hatua Zangu, nami Nitakihamasisha kila kitu kunitumikia, ili kuukamilisha mpango Wangu wa usimamizi. Kwa hiyo ulimwengu dunia wote utaangamizwa, hata bila Mimi kuingilia moja kwa moja. Nilipopata mwili mara ya kwanza na kusulubishwa msalabani, dunia ilitetemeka kwa nguvu sana; itakuwa vivyo hivyo mwishowe. Mitetemeko ya ardhi itaanza wakati huo huo Nitakapoingia katika ulimwengu wa kiroho kutoka katika mwili. Kwa hiyo Nasema, bila shaka wazaliwa wa kwanza hawatapitia maafa. Watu ambao si wazaliwa wa kwanza wataachwa katika maafa na kuteseka. Kwa hiyo, kwa wanadamu, kila mtu yuko tayari kuwa mzaliwa wa kwanza. Katika jakamoyo za watu si kwa ajili ya kufurahia baraka, bali kwa ajili ya kuepuka kupitia maafa. Hii ni hila ya joka kuu jekundu. Lakini Sitaliruhusu litoroke kamwe. Nitalisababisha lipitie adhabu Yangu kali na bado lisimame na kunitolea huduma (hii inamaanisha kuwafanya wana Wangu na watu Wangu kuwa kamili), Niliache lilaghaiwe daima na njama zake lenyewe, likubali hukumu Yangu milele, na likubali uunguzaji Wangu milele. Hii ndiyo maana ya kweli ya kuwafanya watendaji huduma wanisifu (kuwatumia kufichua uwezo Wangu mkubwa). Sitaliruhusu joka kuu jekundu liingie kisirisiri ndani ya ufalme Wangu, na Sitalipa joka kuu jekundu haki ya kunisifu! (Kwa sababu halistahili, halistahili kamwe!) Nitalisababisha tu kutoa huduma Kwangu hadi milele! Nitalisababisha tu linisujudie. (Wale wanaoangamizwa ni bora zaidi kuliko wale walio katika hali ya kuteseka milele. Maangamizi ni adhabu kali ya muda mfupi tu, lakini wale walio katika hali ya kuteseka milele watapitia adhabu kali milele, kwa hiyo Mimi hutumia “kusujudu.” Kwa sababu watu hawa huingia nyumbani Mwangu kisirisiri na kufurahia neema Yangu nyingi nao wana ufahamu fulani kunihusu, Mimi hutumia adhabu kali. Kwa wale walio nje ya nyumba Yangu, unaweza kusema kuwa wasiojua hawatateseka.) Katika fikira za watu, wanadhani kuwa wale ambao wanaangamizwa ni wabaya zaidi kuliko wale ambao wako katika mateso ya milele, lakini badala yake, wale walio katika hali ya kuteseka milele wanapaswa kuhukumiwa kwa ukali milele, na wale wanaoangamizwa watarudia hali ya kutokuwepo milele.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 108

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 224)

Wakati saluti kwa ufalme inapolia—ambao pia ni wakati sauti saba za radi zinanguruma—sauti hii inatetemesha mbingu na dunia, inatetemesha mbingu na kusababisha mishipa ya moyo wa kila binadamu kutetemeka. Wimbo wa taifa kwa ufalme unainuka kwa shangwe katika taifa la joka kuu jekundu, kuthibitisha kwamba Nimeliangamiza taifa la joka kuu jekundu na kisha kuanzisha ufalme Wangu. Hata la muhimu zaidi, ufalme Wangu unaanzishwa duniani. Wakati huu, Naanza kutuma malaika Wangu kwa kila mtu wa mataifa ya dunia ili waweze kuwachunga wanangu, watu Wangu; hili pia ni kukidhi mahitaji ya hatua ya pili ya kazi Yangu. Lakini Mimi binafsi Naenda mahali ambapo joka kuu jekundu limelala likiwa limejizongomeza, Nipigane nalo. Na wakati binadamu wote wanapata kunijua Mimi kutoka ndani ya mwili, na kuweza kuyaona matendo Yangu kutoka ndani ya mwili, wakati huo makazi ya joka kuu jekundu yatageuzwa kuwa jivu na kutoweka yasipatikane tena. Kama watu wa ufalme Wangu, kwa kuwa unalichukia joka kuu jekundu katika mifupa yako, ni lazima uuridhishe moyo Wangu na matendo yako na kwa njia hii uweze kuleta aibu juu ya joka. Je, unahisi kwamba joka kuu jekundu ni lenye chuki? Je, unahisi kweli kwamba yeye ndiye adui wa Mfalme wa ufalme? Je, una imani kwa kweli kwamba unaweza kuwa na ushuhuda wa ajabu Kwangu? Je, una imani kwa kweli ya kumshinda joka kuu jekundu? Haya ndiyo Ninayotaka kutoka kwako. Yote Ninayohitaji kutoka kwako ni kwamba uweze kufika mpaka hatua hii; je, utaweza kufanya hili? Je, una imani kwamba unaweza kufikia hili? Binadamu ana uwezo wa kufanya nini? Si ni afadhali Nifanye hivyo Mwenyewe? Mbona Ninasema kwamba Mimi binafsi Nateremka mahali ambapo vita hujiunga? Ninachotaka ni imani yako, sio matendo yako. Wanadamu hawana uwezo wa kupokea maneno Yangu kwa halisi, lakini wanachungulia tu kutoka kando. Na wewe umefikia malengo haya kwa njia hii? Umekuja kunijua kwa njia hii? Kwa kusema ukweli, kati ya wanadamu walio duniani, hakuna hata mmoja aliye na uwezo wa kuniangalia Mimi moja kwa moja usoni, hakuna hata mmoja aliye na uwezo wa kupokea maana safi na nadhifu ya maneno Yangu. Na kwa hiyo Nimeweka mwendo wa kufaa usiokuwa wa kawaida wa kupanga mambo juu ya dunia, ili kufikia lengo Langu na kuanzisha mfano halisi Wangu mwenyewe katika mioyo ya watu, na kwa njia hii kutamatisha kipindi ambapo fikira huwa na mamlaka juu ya wanadamu.

Leo hii, Sishuki tu juu ya taifa la joka kuu jekundu, Mimi pia Nageuza uso Wangu kuelekea ulimwengu mzima, mpaka kila kitu cha mbingu kinatetemeka. Kunayo sehemu hata moja isiyopitia hukumu Yangu? Kunayo sehemu isiyo chini ya mateso Ninayovurumisha kuelekea chini? Kila Ninapoenda Nimesambaza “mbegu za maafa” ya kila aina. Hii ni mojawapo ya njia ambazo Nafanya kazi, na bila shaka ni kitendo cha ukombozi kwa ajili ya mwanadamu, na kile Ninachompa bado ni aina ya upendo. Nataka kufanya hata watu zaidi wapate kunijua Mimi, waweze kuniona Mimi, na kwa njia hii wapate kumcha Mungu ambaye wao hawajamwona kwa miaka mingi sana lakini ambaye, leo hii, ni halisi. Ni kwa sababu gani Niliumba dunia? Kwa sababu gani, wakati mwanadamu alipogeuka na kuwa mpotovu, Sikumwangamiza kabisa? Kwa sababu gani jamii ya wanadamu inaishi chini ya mateso? Ni kwa sababu gani Mimi Mwenyewe Niliuvaa mwili? Wakati Mimi Natekeleza kazi Yangu, binadamu haujui tu ladha ya uchungu pekee bali pia ya utamu. Kati ya watu wa dunia, ni nani asiyeishi ndani ya neema Yangu? Je, kama Sikuwapa wanadamu baraka yakinifu, nani angeweza kufurahia utoshelevu katika ulimwengu? Hakika, kuwaruhusu kuchukua nafasi kama watu Wangu si baraka pekee Niliyowapa, sivyo? Na kama msingekuwa watu Wangu na badala yake muwe watendaji-huduma, hamngekuwa mnaishi ndani ya baraka Zangu? Hapana mmoja kati yenu anayeweza kuelewa asili ya maneno Yangu. Binadamu—mbali na kuthamini vyeo ambavyo Nimeweka juu yao, wengi wao, kwa sababu ya jina “watendaji-huduma,” wanaweka chuki katika nyoyo zao, na wengi sana, kwa sababu ya jina “watu Wangu,” huzalisha upendo Kwangu katika nyoyo zao. Hakuna anayepaswa kujaribu kunidanganya; macho Yangu huona kila kitu! Ni nani kati yenu hupokea kwa hiari, ni nani kati yenu hunipa utiifu kamilifu? Kama saluti kwa ufalme haingelia, je ungeweza kutii mpaka mwisho? Kile ambacho mwanadamu ana uwezo wa kufanya, kufikiria, anaweza kwenda umbali gani—haya yote Nimeyaamua kabla tangu kitambo.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 10

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 225)

Licha ya ukweli kwamba ujenzi wa ufalme umeanza rasmi, maamkuzi kwa ufalme bado hayajatangazwa rasmi—sasa ni unabii tu wa kile kitakachokuja. Wakati ambapo watu wote watakuwa wamefanywa kamili na mataifa yote ya dunia kugeuka kuwa ufalme wa Kristo, basi huo utakuwa wakati ambapo radi saba zitanguruma. Siku ya sasa ni hatua ndefu ya kwenda mbele katika mwelekeo wa hatua hiyo, shambulio limeachiliwa huru kwa muda ujao. Huu ni mpango wa Mungu—hivi karibuni utafanikishwa. Hata hivyo, Mungu tayari amefanikisha yote ambayo Amesema. Hivyo, ni dhahiri kwamba mataifa ya dunia ni makasri tu yaliyo mchangani yanayotetemeka bamvua linapokaribia: Siku ya mwisho iko karibu sana na joka kubwa jekundu litaanguka chini ya neno la Mungu. Ili kuhakikisha kwamba mpango wa Mungu unatekelezwa kwa ufanisi, malaika wa mbinguni wameshuka juu ya dunia, wakifanya kila wanaloweza kumridhisha Mungu. Mungu Mwenyewe mwenye mwili Amejipanga katika uwanja wa vita kupigana na adui. Po pote ambapo Aliyepata mwili huonekana, adui anaangamiziwa mahali hapo. Uchina ni ya kwanza kuangamizwa, kuharibiwa kabisa kwa mkono wa Mungu. Mungu haipi Uchina upande wowote kabisa. Thibitisho la kuendelea kuanguka kwa joka kubwa jekundu linaweza kuonekana katika ukomavu wa watu unaoendelea. Hili linaweza kuonekana wazi na mtu yeyote. Ukomavu wa watu ni ishara ya kifo cha adui. Huu ni ufafanuzi kidogo wa kile kinachomaanishwa na “kufanya vita.” Hivyo, Mungu aliwakumbusha watu wakati mwingi watoe ushuhuda mzuri kwa Mungu kutangua hali ya fikira, ubaya wa joka kubwa jekundu ndani ya mioyo ya wanadamu. Mungu hutumia kumbusho kama hizo kuchangamsha imani ya mwanadamu na, kwa kufanya hivyo, Hutimiza ujuzi katika kazi Yake. Hili ni kwa sababu Mungu amesema, “Binadamu ana uwezo wa kufanya nini? Si ni afadhali Nifanye hivyo Mwenyewe?” Wanadamu wote wako hivyo. Si kwamba wao hawawezi tu, bali pia huvunjika moyo na husikitishwa kwa urahisi. Kwa sababu hii, hawawezi kumjua Mungu. Mungu hafufui tu imani ya mwanadamu, kwa siri Yeye humjaza mwanadamu nguvu siku zote.

Linalofuata, Mungu alianza kunena kwa ulimwengu wote. Mungu hakuanzisha tu kazi Yake mpya Uchina, Kotekote ulimwenguni Alianza kufanya kazi mpya ya leo. Katika hatua hii ya kazi, kwa vile Mungu anataka kufichua matendo Yake yote kotekote katika dunia ili wanadamu wote ambao wamemsaliti watakuja tena kuinama kwa utiifu mbele ya kiti Chake cha enzi, hivi ndani ya hukumu ya Mungu bado kuna huruma na upendo wa Mungu. Mungu hutumia matukio ya sasa kotekote ulimwenguni kutetemesha mioyo ya wanadamu, Akiiamsha kumtafuta Mungu ili waweze kumiminika kwenda Kwake. Hivyo Mungu asema, “Hii ni mojawapo ya njia ambazo Nafanya kazi, na bila shaka ni kitendo cha ukombozi kwa ajili ya mwanadamu, na kile Ninachompa bado ni aina ya upendo.”

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufafanuzi wa Mafumbo ya “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima”, Sura ya 10

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 226)

Natumia mamlaka Yangu duniani, Nikidhihirisha kazi Yangu yote. Yote yaliyo katika kazi Yangu yanajitokeza duniani; mwanadamu hajawahi, duniani, kuweza kuufahamu mwendo Wangu mbinguni, wala kutafakari kabisa mizunguko na njia za Roho Wangu. Wanadamu wengi wanaelewa tu maelezo madogo yaliyo nje ya roho, bila kuweza kuelewa hali halisi ya roho. Matakwa Yangu kwa binadamu hayatoki kwa Mimi wa mbinguni Nisiye dhahiri, ama kwa Mimi wa dunia Nisiyekadiriwa: Natoa matakwa ya kufaa kulingana na kimo cha mwanadamu. Sijawahi kumweka yeyote kwa matatizo, wala Sijawahi “kukamua damu ya mtu yeyote” ili kujiridhisha—inawezakana kwamba matakwa Yangu kuzuiliwa na masharti haya pekee? Kwa viumbe lukuki duniani, ni yupi asiyetii tabia za maneno yaliyo mdomoni Mwangu? Ni yupi kati ya viumbe hawa, wanaokuja mbele Yangu, hajachomwa kabisa kupitia maneno Yangu na moto Wangu unaochoma? Ni yupi kati ya viumbe hawa anayethubutu kujigamba mbele Yangu? Ni yupi kati ya viumbe hawa hainami mbele Yangu? Mimi ni Mungu anayelazimisha tu ukimya kwa viumbe? Kwa mambo lukuki katika uumbaji, Nachagua yale yanaoridhisha nia Yangu; kwa wanadamu lukuki, Nawachagua wale wanaotunza roho Yangu. Nachagua bora zaidi kwa nyota zote, hivyo Naongeza mwangaza hafifu kwa ufalme Wangu. Natembea duniani, Nikitawanya harufu Yangu nzuri kila mahali, nami Naacha umbo Langu kila mahali. Kila pahali panatingika kwa mvumo wa sauti Yangu. Watu kila mahali wanadumu kwa hamu ya mambo waliyozea ya urembo wa mandhari ya jana, kwani binadamu wote wanakumbuka siku za nyuma …

Binadamu wote wanatamani kuona uso Wangu, lakini Nishukapo Mwenyewe duniani, wote wanakirihishwa na ujio Wangu, wote wanaufukuza mwangaza usije, kana kwamba Mimi ni adui ya mwanadamu mbinguni. Mwanadamu ananisalimu na mwangaza wa kujikinga machoni mwake, na daima anabaki katika tahadhari, akihofia sana kwamba Naweza kuwa na mipango mingine kwake. Kwa sababu binadamu wananiona kama rafiki asiyejulikana, wanahisi kwamba Nina nia ya kuwaua bila kujali. Katika macho ya mwanadamu, Mimi ni adui wa mauti. Baada ya kuonja joto Langu katikati ya msiba, mwanadamu hata hivyo bado hafahamu pendo Langu, na bado ameamua kunifukuza na kunikaidi. Mbali na kujinufaisha na yeye kuwa katika hali hii ili kuchukua hatua dhidi yake, Namfunika mwanadamu na joto la kumbatio, Najaza mdomo wake na utamu, na kuweka chakula anachohitaji tumboni mwake. Lakini, wakati hasira Yangu ya ghadhabu inapotingiza milima na mito, Sitamtawaza mwanadamu aina mbalimbali za msaada, kwa sababu ya woga wake. Wakati huu, Nitakuwa na ghadhabu, Nikiwanyima viumbe hai fursa ya kutubu na, kuachana na matumaini Yangu yote kwa mwanadamu, Nitatoa adhabu anayostahili sana. Wakati huu, radi na umeme vinang’aa ghafla na kunguruma, kama mawimbi ya bahari yakisonga kwa hasira, kama milima makumi ya maelfu ikigonga chini. Kwa ajili ya uasi wake, mwanadamu anaangushwa na radi na umeme, viumbe wengine wanafutwa katika milipuko ya radi na umeme, ulimwengu mzima unazorota ghafla katika machafuko, na uumbaji huwezi kupata pumzi muhimu ya uhai. Majeshi lukuki ya binadamu hayawezi kutoroka kishindo cha radi, katikati ya nuru ya ghafla ya umeme, wanadamu, makundi mengi sana, wanaanguka ndani ya mto unaobubujika haraka, kutokomezwa na mafuriko yanayotiririka chini kutoka milima. Ghafla, panakutana dunia ya “wanadamu” badala ya hatima ya binadamu. Maiti wanasongasonga juu ya bahari. Binadamu wote wanaenda mbali nami kwa sababu ya ghadhabu Yangu, kwani mwanadamu ametenda dhambi dhidi ya kiini cha Roho Wangu, uasi wake umenikosea Mimi. Lakini, mahali ambapo hakuna maji, wanadamu wengine bado wanafurahia, wakicheka na kuimba, ahadi ambazo Nimewapa.

Binadamu wote wanapotulia, Natoa kimulimuli cha mwangaza mbele ya macho yao. Hapo, wanadamu wanakuwa na uwazi wa akili na uangavu wa jicho, na wanakoma kuwa na nia ya kukimya; hivyo, hisia ya kiroho inakusanywa ndani ya mioyo yao mara moja. Wakati huu, binadamu wote wanafufuka. Wakiweka kando malalamiko yao, wanadamu wote wanakuja mbele Yangu, baada ya kushinda nafasi nyingine ya kusalimika kupitia maneno Ninayotangaza. Hii ni kwa sababu wanadamu wote wanataka kuishi duniani. Lakini nani miongoni mwao amewahi kuwa na nia ya kuishi kwa ajili Yangu? Nani miongoni mwao amewahi kufichua mambo mazuri ndani yake kunipa furaha? Nani miongoni mwao amewahi kugundua harufu ya kuvutia Kwangu? Wanadamu wote ni vitu hafifu na visivyotakaswa: Nje, wanaonekana kuangaza macho, lakini kwa nafsi zao muhimu hawanipendi kwa dhati, kwa sababu ndani ya nafasi ya kina cha moyo wa binadamu hakujawahi kuwa hata na kiasi kidogo cha Mimi. Mwanadamu anakosa sana: Kumlinganisha nami Mwenyewe, ingeonekana kwamba tuko mbali sana kama dunia kutoka kwa mbingu. Lakini, hata hivyo, Simshambulii mwanadamu katika sehemu zake dhaifu na zenye kasoro, wala Simcheki kudharau upungufu wake. Mikono Yangu imekuwa kazini duniani kwa maelfu ya miaka, na muda huo wote, macho Yangu yamelinda binadamu wote. Bado, Sijawahi kuchukulia mzaha maisha ya binadamu hata mmoja kana kwamba ni kitu cha kuchezea. Nachunguza machungu mwanadamu amechukua na kuelewa bei ambayo amelipa. Anaposimama mbele Yangu, Sitamani kumpata mwanadamu kwa kumshtua kwa nia ya kumwadibu, wala kumtakia na kutawaza kwake vitu visivyohitajika. Badala yake, wakati huu wote nimemchunga mwanadamu, na kumpa mwanadamu, wakati huu wote. Hivyo basi, yote anayofurahia mwanadamu ni neema Yangu, yote ni fadhila inayotoka kwa mkono Wangu. Kwa sababu Niko duniani, mwanadamu hajawahi lazimika kuteseka mateso ya njaa. Badala yake, Namruhusu mwanadamu kupokea kutoka mikono Yangu mambo ambayo anaweza kufurahia, na kumruhusu mwanadamu kuishi ndani ya baraka Zangu. Je, wanadamu wote hawaishi chini ya kuadibu Kwangu? Kama tu jinsi kuna mengi ndani ya vina vya milima, na vitu vingi vya kufurahia ndani ya maji, je, watu wanaoishi ndani ya maneno Yangu leo wanavyo, hata zaidi, chakula wanachopenda na kuonja? Niko duniani, na mwanadamu anafurahia baraka Zangu duniani. Niachapo dunia nyuma, ambapo ndipo pia kazi Yangu itafika ukamilishaji wake, wakati huo, wanadamu hawatapata tena hisani yoyote kutoka Kwangu kwa sababu ya udhaifu wao.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 17

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 227)

Je, mnalichukia kwa kweli lile joka kuu jekundu? Mnalichukia kwa kweli? Mbona Nimewauliza mara nyingi? Mbona Nimewauliza swali hili, mara tena na tena? Kuna picha gani ya joka kuu jekundu katika mioyo yenu? Picha hiyo kwa kweli imeondolewa? Hamchukulii kwa kweli kama baba yenu? Watu wote wanafaa kuona nia Yangu katika maswali Yangu. Sio kuwafanya watu wawe na hasira, au kuchochea uasi kati ya mwanadamu, au ili mwanadamu agundue njia yake mwenyewe, bali ni kuwawezesha watu wote wajifungue kutoka kwa minyororo ya lile joka kuu jekundu. Ila mtu yeyote asiwe na wasiwasi. Yote yatakamilika na maneno Yangu; hakuna mwanadamu atakayekula, na hakuna mwanadamu anayeweza kufanya kazi ambayo Nitaifanya. Nitaifanya hewa ya nchi yote iwe safi na Nitatoa madoadoa yote ya mapepo duniani. Tayari Nimeanza, na Nitaanza hatua ya kwanza ya kazi Yangu ya kuadibu katika makazi ya joka kuu jekundu. Hivyo inaweza kuonekana kuwa kuadibu Kwangu kumeifikia dunia nzima, na lile joka kuu jekundu na mapepo yote machafu yatashindwa kuepuka kuadibu Kwangu, kwa kuwa Ninaziangalia nchi zote. Kazi Yangu duniani itakapokamilika, hapo ndipo, kipindi cha hukumu Yangu kitakamilika, Nitamuadibu kirasmi lile joka kuu jekundu. Watu Wangu wataona kuadibu Kwangu kwa haki kwa lile joka kuu jekundu, watamwaga sifa mbele kwa sababu ya haki Yangu, na milele watalisifu jina Langu takatifu kwa sababu ya haki Yangu. Hivyo basi, mtatenda wajibu wenu kirasmi, na mtanisifu kirasmi kotekote katika nchi, milele na milele!

Kipindi cha hukumu kitakapofika kilele, Sitaharakisha kumaliza kazi Yangu, bali Nitajumuisha ndani ushahidi wa enzi ya kuadibu na kuruhusu ushahidi huo kuonekana na watu Wangu wote; na katika haya kutazaliwa matunda mengi zaidi. Ushahidi huu ndio njia ambayo kwayo Naliadibu lile joka kuu jekundu, na Nitafanya watu Wangu kuliona kwa macho yao ili wajue zaidi kuhusu tabia Yangu. Wakati watu Wangu wananifurahia ni wakati joka kuu jekundu linaadibiwa. Kuwafanya watu wa joka kubwa jekundu kusimama na kuliasi joka ndiyo nia Yangu, na ndiyo njia ambayo Ninawakamilisha watu Wangu, na ni nafasi nzuri ya watu Wangu wote kukua maishani.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 28

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 228)

Mwezi unaong’aa unapochomoza, usiku mtulivu unaangamizwa mara moja. Ingawa mwezi umepasuka, mwanadamu yumo katika hali ya uchangamfu, na anakaa kwa utulivu chini ya mwangaza wa mwezi, akifurahia eneo la kupendeza chini ya mwangaza. Mwanadamu hawezi elezea hisia zake; ni kama ana matamanio ya kuelekeza mawazo yake kwa wakati wa kale, ni kama anataka kuangalia mbele kwa mambo ya baadaye, ni kama anafurahia yanayojiri. Tabasamu linaonekana usoni mwake, na katika hali ya hewa ya kupendeza kunatokea harufu kavu; wakati upepo mwanana unapopuliza, mwanadamu anagundua harufu hiyo nzuri na anaonekana kuleweshwa nayo, akishindwa kujisimamisha. Huu ndio wakati haswa ambapo Mimi Mwenyewe Nimekuja miongoni mwa mwanadamu, na mwanadamu anahisi kwa hali ya juu harufu yenye uzuri tele, na kwa hivyo wanadamu wote wanaishi kati ya harufu hii. Niko na amani na mwanadamu, na mwanadamu anaishi kwa amani Nami, na hana uasi tena katika jinsi anavyonichukulia, Sipogoi tena upungufu wa mwanadamu, hakuna tena huzuni katika uso wa mwanadamu. Kifo hakitishii tena wanadamu wote. Leo, Naenda pamoja na mwanadamu katika enzi ya kuadibu, kuenda mbele pamoja na yeye upande kwa upande. Nafanya kazi Yangu, ambayo ni kusema, Naipiga fimbo Yangu chini miongoni mwa mwanadamu na inaanguka juu ya kile kilicho na uasi ndani ya mwanadamu. Katika macho ya mwanadamu, fimbo Yangu huonekana kuwa na nguvu spesheli: inaangukia wale wote ambao ni maadui Wangu na haiwasamehei kwa urahisi: miongoni mwa wale wote wanaonipinga, fimbo hiyo inafanya kazi yake ya kiasili; wale wote walioko mikononi Mwangu wanafanya wajibu wao kulingana na nia Yangu, na wala hawajawahi enda kinyume na matakwa Yangu au kubadilisha nia yao. Kutokana na hayo, maji yatanguruma, milima itaanguka, mito mikuu itatawanyika, mwanadamu atabadilika, jua litakua na mwangaza mdogo, mwezi utakuwa na giza zaidi, mwanadamu hatakuwa tena na siku za kuishi kwa amani, hakutakuwa tena na wakati wa amani katika nchi, mbingu haitawahi tena kuwa shwari, na kimya na haitawahi tena kuendelea. Vitu vyote vitafanywa vipya na kurudia hali vilivyoonekana mwanzoni. Nyumba zote duniani zitasambaratishwa, na mataifa yote duniani yatagawanywa; siku za marudiano kati ya mke na mume zitapita, mama na mwanawe hawatakutana tena, hakutakuwa tena na kuja pamoja kwa baba na bintiye. Nitayaharibu yote yaliyokuwa duniani. Siwapi watu fursa ya kutoa hisia zao, kwani Mimi sina hisia, na Nimekua katika kuchukia hisia za watu kwa kiasi kikubwa. Ni kwa sababu ya hisia baina ya watu ndiposa Nimewekwa kando, na hivyo Nimekuwa “mwingine” machoni mwao; ni kwa sababu ya hisia kati ya binadamu ndiposa Nimesahaulika; ni kwa sababu ya hisia za mwanadamu ndipo anapochukua fursa ya kuchukua “dhamira” yake; ni kwa sababu ya hisia za mwanadamu ndiposa kila mara amekuwa mwoga wa kuadibu Kwangu; ni kwa sababu ya hisia za mwanadamu ndiposa ananiita mkosa haki na mdhulumu, na kusema kuwa Sisikizi hisia za mwanadamu Ninapofanya mambo Yangu. Je Nina mrithi duniani? Ni nani kamwe, kama Mimi, amewahi kufanya kazi usiku na mchana, bila kufikiria chakula au usingizi, kwa ajili ya mipangilio yangu yote ya usimamizi? Mwanadamu anawezaje kulinganishwa na Mungu? Anawezaje kuwa sambamba na Mungu? Inawezekanaje, Mungu, anayeumba, Awe sawa na mwanadamu, anayeumbwa? Ninawezaje kuishi na kufanya mambo pamoja na mwanadamu duniani? Nani anahofia moyo Wangu? Ni maombi ya mwanadamu? Wakati mmoja Nilikubali kujumuika na mwanadamu na kutembea pamoja na yeye—na ndio, hadi sasa mwanadamu anaishi chini ya ulinzi Wangu, lakini kutakuwa na siku ambapo mwanadamu atajitenga kutoka kwa ulinzi Wangu? Hata ingawa mwanadamu hajawahi kujibebesha nzigi kwa ajili ya moyo Wangu, nani anaweza kuendelea kuishi katika nchi isiyo na mwangaza? Ni kwa sababu tu ya baraka Zangu ndiposa mwanadamu ameishi mpaka leo.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 28

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 229)

Nchi ziko katika machafuko makubwa, kwa sababu fimbo ya Mungu imeanza kutimiza wajibu wake duniani. Kazi ya Mungu inaweza kuonekana katika hali ya dunia. Mungu anaposema “maji yatanguruma, milima itaanguka, mito mikuu itatawanyika,” hii ni kazi ya kwanza ya fimbo duniani, na matokeo yake ni kwamba “Nyumba zote duniani zitasambaratishwa, na mataifa yote duniani yatagawanywa; siku za marudiano kati ya mke na mume zitapita, mama na mwanawe hawatakutana tena, hakutakuwa tena na kuja pamoja kwa baba na bintiye. Nitayaharibu yote yaliyokuwa duniani.” Hiyo ndiyo itakuwa hali ya jumla ya familia duniani. Kwa kawaida, haingeweza kuwa hasa hali ya wote, lakini ni hali ya wengi wao. Kwa upande mwingine, inahusu hali ambazo watu wa mkondo huu wamepitia katika siku za baadaye. Inatabiri kwamba, mara wakishapitia kuadibu kwa maneno na wasioamini wamepatwa na msiba, hakutakuwa tena na mahusiano ya familia miongoni mwa watu duniani; wote watakuwa watu wa Sinim, na wote watakuwa waaminifu katika ufalme wa Mungu. Hivyo, siku za marudiano kati ya mke na mume zitapita, mama na mwanawe hawatakutana tena, hakutakuwa tena na kuja pamoja kwa baba na bintiye. Na kwa hiyo, familia za watu duniani zitatenganishwa, zitapasuliwa vipande vipande, na hii itakuwa kazi ya mwisho ambayo Mungu anafanya katika mwanadamu. Na kwa sababu Mungu ataeneza kazi hii kotekote ulimwenguni, Anachukua fursa ya kuwafafanulia watu neno “hisia,” hivyo Akiwawezesha kuona kwamba mapenzi ya Mungu ni kuzitenganisha familia zote za watu, na kuonyesha kwamba Mungu hutumia kuadibu ili kutatua migogoro yote ya familia miongoni mwa wanadamu. La sivyo, hapangekuwa na njia ya kuimaliza sehemu ya mwisho ya kazi ya Mungu duniani. Sehemu ya mwisho ya maneno ya Mungu huonyesha udhaifu mkubwa kabisa wa wanadamu—wote huishi katika hisia—na hivyo Mungu haepuki hata mmoja wao, na Hufunua siri zilizofichwa mioyoni mwa wanadamu wote. Kwa nini ni vigumu sana kwa watu kujitenga na hisia? Je, ni muhimu zaidi kuliko viwango vya dhamiri? Je, dhamiri inaweza kufanikisha mapenzi ya Mungu? Je, hisia inaweza kuwasaidia watu kupitia shida? Machoni pa Mungu, hisia ni adui Yake—hili halijanenwa wazi katika maneno ya Mungu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufafanuzi wa Mafumbo ya “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima”, Sura ya 28

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 230)

Maneno yote ya Mungu yana sehemu ya tabia Yake; tabia Yake haiwezi kuonyeshwa kwa ukamilifu kwa maneno, kwa hiyo hii inaonyesha kiasi gani cha utajiri kiko ndani Yake. Kile ambacho watu wanaweza kukiona na kukigusa ni, hata hivyo, finyu, kama ulivyo uwezo wa watu. Ingawa maneno ya Mungu ni dhahiri, watu hawawezi kuyaelewa kwa ukamilifu. Kama maneno haya tu: “Katika mwako wa umeme, kila mnyama hufichuliwa katika hali yake halisi. Hivyo pia, kama wameangaziwa na mwanga Wangu, wanadamu wamepata tena utakatifu waliokuwa nao wakati mmoja. Oh, ya kwamba dunia potovu ya zamani mwishowe imeanguka na kutumbukia ndani ya maji ya taka na, kuzama chini ya maji, na kuyeyuka na kuwa tope!” Maneno yote ya Mungu yana nafsi Yake, na ingawa watu wote wanajua maneno haya, hawajawahi kuelewa maana yake. Machoni pa Mungu, wote wanaompinga ni adui Zake, yaani, wale ambao ni wa pepo wabaya ni wanyama. Kutokana na hili hali halisi ya kanisa inaweza kuchunguzwa. Bila kupitia hotuba ya watu au kuadibu, bila kupitia kufukuzwa kwa watu moja kwa moja au sehemu ya mbinu za kibinadamu au kutajwa na watu, wanadamu wote wanajichunguza chini ya mwangaza wa maneno ya Mungu, na kuona kwa dhahiri kwa mtazamo wa “hadubini” kiasi gani cha maradhi kiko ndani yao kweli. Katika maneno ya Mungu, kila aina ya roho imeainishwa na umbo la asili la kila roho linafichuliwa. Roho za malaika huangazwa zaidi na kupata nuru zaidi, kwa hiyo kile Mungu alisema, kwamba “wamepata tena utakatifu waliokuwa nao wakati mmoja” inategemea matokeo ya mwisho yaliyotimizwa na Mungu. Bila shaka sasa bado hayawezi kutimizwa kwa ukamilifu—hili ni limbuko tu. Mapenzi ya Mungu yanaonekana kupitia kwa hili na inaonyesha kuwa idadi kubwa ya watu wataanguka katika maneno ya Mungu na watashindwa katika mchakato wa watu wote kuwa watakatifu hatua kwa hatua. “Kuyeyuka na kuwa tope” kulikotajwa hapa hakupingani na Mungu kuuangamiza ulimwengu kwa moto, na “umeme” unahusu ghadhabu ya Mungu. Wakati Mungu atatoa ghadhabu Yake kubwa, ulimwengu wote utapata maafa ya kila aina kama matokeo, kama kufoka kwa volkano. Ninaposimama juu ya anga, inaweza kuonekana kuwa juu ya dunia kila aina ya maafa yanawakaribia wanadamu wote, siku baada ya siku. Nikiangalia chini kutoka juu, dunia inafanana na mandhari mbalimbali kabla ya tetemeko la ardhi. Maji ya moto yanatiririka kila mahali, lava inatiririka kila mahali, milima inahama, na mwanga wa baridi unametameta kila mahali. Dunia nzima imezama katika moto. Hii ndiyo mandhari ya Mungu akitoa ghadhabu Yake, nao ni wakati wa hukumu Yake. Wale wote ambao ni wa mwili hawataweza kutoroka. Kwa hiyo vita kati ya nchi na migogoro kati ya watu havitahitajika kuharibu ulimwengu mzima, lakini “itafurahia kwa kufahamu” chanzo cha kuadibu kwa Mungu. Hakuna mtu atakayeweza kuiepuka na wataipitia mmoja mmoja. Baada ya hapo ulimwengu wote utaanza tena kuangaza kwa miale takatifu na wanadamu wote wataanza tena maisha mapya. Na Mungu atakuwa Amepumzika juu ya ulimwengu na Atawabariki wanadamu wote kila siku. Mbingu haitakuwa na ukiwa usiovumilika, lakini itarudia nguvu ambayo haijawahi kuwa nayo tangu kuumbwa kwa ulimwengu, na “siku ya sita” itakuwa wakati Mungu ataanza maisha mapya. Mungu na mwanadamu wote wataingia katika pumziko na ulimwengu hautakuwa tena mchafu au wenye najisi, lakini utapata upya tena. Ndio maana Mungu alisema: “Dunia si kimya na nyamavu tena, mbingu si ya ukiwa na yenye huzuni tena.” Katika ufalme wa mbinguni hakujakuwa na udhalimu au hisia za kibinadamu, au tabia zozote za wanadamu za upotovu kwa sababu usumbufu wa Shetani haupo. Watu wote wanaweza kuelewa maneno ya Mungu, na maisha mbinguni ni maisha yaliyojaa furaha. Wote walio mbinguni wana hekima na heshima ya Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufafanuzi wa Mafumbo ya “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima”, Sura ya 18

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 231)

Inaweza kusemwa kwamba matamko yote ya leo yanatabiri masuala ya siku za baadaye, yanahusu Mungu kufanya mpango kwa ajili ya hatua inayofuata ya kazi Yake. Mungu karibu amemaliza kazi Yake ndani ya watu wa kanisa, baadaye Atatumia ghadhabu kuonekana mbele ya watu wote. Kama asemavyo Mungu, “Nitawafanya watu walio duniani wakubali mambo Yangu, na mbele ya ‘kiti cha hukumu,’ matendo Yangu yatathibitishwa, ili yakubalike miongoni mwa watu walio kote duniani, ambao watasalimu amri.” Je, uliona chochote ndani ya maneno haya? Humu mna muhtasari wa sehemu inayofuata ya kazi ya Mungu. Kwanza, Mungu atawafanya walinzi wote wanaotawala kwa nguvu za kisiasa waridhike kabisa na wajiondoe katika jukwaa la historia, kutowahi kupigania hadhi tena au kufanya hila na kula njama. Kazi hii lazima itekelezwe kwa njia ya Mungu kusababisha mabaa mbalimbali duniani. Lakini Mungu hataonekana; kwa sababu, wakati huu, nchi ya joka kubwa jekundu bado itakuwa ni nchi ya uchafu, Mungu hataonekana, lakini ataibuka tu kwa njia ya kuadibu. Hiyo ndiyo tabia ya Mungu yenye haki, na hakuna anayeweza kuiepuka. Katika wakati huu, vyote vinavyoishi katika taifa la joka kubwa jekundu vitapitia maafa, ambavyo kwa kawaida ni pamoja na ufalme ulio duniani (kanisa). Huu ndio hasa wakati ambao ukweli hujitokeza, na kwa hiyo unapitiwa na watu wote, na hakuna anayeweza kuepuka. Hili limejaaliwa na Mungu. Ni kwa sababu ya hatua hii ya kazi hasa ndio Mungu asema, “Huu ndio wakati wa kutekeleza mipango mikuu.” Kwa sababu, katika siku za baadaye, hakutakuwa na kanisa duniani, na kwa ajili ya majilio ya machafuko, watu wataweza tu kufikiria kuhusu kile kilicho mbele yao na watapuuza kila kitu kingine, na ni vigumu kwao kumfurahia Mungu katikati ya machafuko, hivyo, watu wanatakiwa kumpenda Mungu kwa moyo wao wote katika wakati huu wa ajabu, ili wasikose nafasi. Ukweli huu unapopita, Mungu amelishinda kabisa joka kubwa jekundu, na hivyo kazi ya ushuhuda wa watu wa Mungu imefika mwisho; baadaye Mungu ataanza hatua inayofuata ya kazi, Akifanya uharibifu kwa nchi ya joka kubwa jekundu, na hatimaye kuwagongomelea watu juu chini msalabani kotekote katika ulimwengu, baadaye Atawaangamiza wanadamu wote—hizi ni hatua za siku za baadaye za kazi ya Mungu. Hivyo, mnapaswa kutaka kufanya lote muwezalo kumpenda Mungu katika mazingira haya ya amani. Katika siku za baadaye hamtakuwa na nafasi zaidi za kumpenda Mungu, kwani watu huwa tu na nafasi ya kumpenda Mungu katika mwili; wanapoishi katika ulimwengu mwingine, hakuna atakayenena kuhusu kumpenda Mungu. Je, hili si jukumu la kiumbe aliyeumbwa? Kwa hiyo unapaswa kumpenda Mungu vipi katika siku zako za uhai? Umeshawahi kufikiri juu ya hili? Je, unangoja mpaka ufe ili umpende Mungu? Je, haya si maneno matupu? Leo, kwa nini hufuatilii kumpenda Mungu? Je, kumpenda Mungu huku ukiwa na shughuli nyingi kunaweza kuwa upendo halisi wa Mungu? Madhumuni ya kusema kwamba hatua hii ya kazi ya Mungu itafika mwisho hivi punde ni kwa sababu Mungu tayari ana ushuhuda mbele ya Shetani; hivyo, hakuna haja ya mwanadamu kufanya lolote, mwanadamu anatakiwa tu kufuatilia kumpenda Mungu katika miaka ambayo yuko hai—hili ndilo jambo muhimu. Kwa sababu masharti ya Mungu si mengi, na, zaidi ya hayo, kwa kuwa kuna hamu kuu ndani ya moyo Wake, Amefichua muhtasari wa hatua inayofuata ya kazi kabla ya hatua hii ya kazi kumalizika, ambalo linaonyesha kwa dhahiri kuna kiasi gani cha muda: kama Mungu hangekuwa na hamu ndani ya moyo Wake, je, Angeyanena maneno haya mapema hivyo? Ni kwa sababu muda ni mfupi ndio maana Mungu anafanya kazi kwa njia hii. Inatarajiwa kwamba mnaweza kumpenda Mungu kwa mioyo yenu yote, kwa akili zenu zote, na kwa nguvu zenu zote, jinsi tu mnavyotunza maisha yenu wenyewe. Je, haya siyo maisha yenye maana kuu zaidi? Ni wapi pengine ambapo mngeweza kupata maana ya maisha? Je, ninyi si vipofu kabisa? Uko radhi kumpenda Mungu? Je, Mungu anastahili upendo wa mwanadamu? Je, watu wanastahili ibada ya mwanadamu? Kwa hiyo, unapaswa kufanya nini? Mpende Mungu kwa ujasiri, bila kusita, na uone kila ambacho Mungu atakufanya. Uone kama Atakuchinja. Kwa muhtasari, kazi ya kumpenda Mungu ni muhimu zaidi kuliko kunukuu na kuandika mambo kwa ajili ya Mungu. Unapaswa kukipa kipaumbele kilicho muhimu zaidi, ili maisha yako yaweze kuwa ya thamani zaidi na yajae furaha, na kisha unapaswa kusubiri “hukumu” ya Mungu kwako. Nashangaa iwapo mpango wako utahusisha kumpenda—Ningependa kwamba mipango ya watu wote iwe ile inayokamilishwa na Mungu, na iwe ya uhalisi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufafanuzi wa Mafumbo ya “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima”, Sura ya 42

Iliyotangulia: Kujua Kazi ya Mungu (I)

Inayofuata: Tabia ya Mungu na Kile Anacho na Alicho

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp