Tabia ya Mungu na Kile Anacho na Alicho

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 232)

Mimi ni mwenye haki, Mimi ni mwaminifu, Mimi ndimi Mungu anayechunguza moyo wa ndani zaidi wa mwanadamu! Nitafichua mara moja aliye wa kweli na aliye wa uongo. Hakuna haja ya kuwa na hofu, vitu vyote hufanya kazi kwa wakati Wangu. Ni nani asiyenitaka Mimi kwa dhati, ni nani asiyenitaka Mimi kwa dhati—Nitawaambia. Kuleni tu vizuri, kunyweni vizuri, njoo mbele Yangu na Nikaribieni nami Nitafanya kazi Yangu Mwenyewe. Msiwe na hamu sana ya matokeo ya haraka, kazi Yangu si kitu ambacho kinaweza kufanywa mara moja. Ndani yake kuna hatua Zangu na hekima Yangu, hivyo hekima Yangu inaweza kufichuliwa. Nitawawezesha kuona ni nini kinachofanywa kwa mikono Yangu—kuadhibu uovu na kuzawadia mema. Mimi hakika Simpendelei mtu yeyote. Ninakupenda kwa dhati wewe unayenipenda kwa dhati, na ghadhabu Yangu daima itakuwa pamoja na wale wasionipenda kwa dhati, ili kwamba waweze kukumbuka daima kwamba Mimi ni Mungu wa kweli, Mungu anayechunguza moyo wa ndani zaidi wa mwanadamu. Usitende kwa njia moja mbele ya wengine na utende kwa namna nyingine bila wao kufahamu; Ninaona wazi kila kitu unachofanya na ingawa unaweza kuwadanganya wengine huwezi kunidanganya Mimi. Ninaona yote waziwazi. Haiwezekani kwako kuficha chochote; vyote vimo mikononi Mwangu. Usifikiri kuwa wewe ni mjanja sana, kwa kufanya hesabu zako ndogondogo zikufaidi. Nakwambia: Haijalishi mwanadamu anaweza kubuni mipango kiasi kipi, iwe elfu kadhaa ama elfu nyingi, mwishowe hawezi kuepuka kutoka kwenye kiganja cha mkono Wangu. Vitu na matukio yote huendeshwa katika mikono Yangu, sembuse mtu mmoja! Usijaribu kuepuka au kujificha, usijidanganye au kuficha. Je, huwezi kuona kwamba uso Wangu mtukufu, hasira Yangu na hukumu Yangu imefichuliwa hadharani? Nitahukumu mara moja na bila huruma wale wote ambao hawanitaki Mimi kwa dhati. Huruma Yangu imefika mwisho na hakuna tena iliyobaki. Usiwe mnafiki tena na acha njia zako za kishenzi.

Mwanangu, tahadhari; tumia muda zaidi mbele Zangu nami Nitakuwa msaada wako. Usiogope, toa upanga Wangu mkali ukatao kuwili, na—kulingana na mapenzi Yangu nami—pigana na Shetani mpaka mwishoni, Nitakulinda; usiwe na wasiwasi. Mambo yote yaliyofichwa yatafunguliwa na kufichuliwa. Mimi ni Jua ambalo linatoa nuru, likimulika giza lote bila huruma. Hukumu Yangu imeshuka kabisa na kanisa ni uwanja wa vita. Nyote mnapaswa kuwa tayari na mnapaswa kutoa nafsi zenu zote kwa vita vya mwisho vya uamuzi; Mimi hakika Nitakulinda ili uweze kunipigania vita vizuri, vya ushindi.

Kuwa makini, mioyo ya watu leo ni yenye udanganyifu na haitabiriki na hawapaswi kuaminiwa. Ni Mimi tu Niliye upande wako kabisa. Hakuna udanganyifu ndani Yangu; Niegemee Mimi tu! Hakika wana Wangu watashinda katika vita vya mwisho vya uamuzi na bila shaka Shetani atajitokeza na kushambulia katika uchungu wake wa kifo. Usiogope! Mimi ni nguvu yako, Mimi ni kila kitu chako. Usifikiri juu ya mambo mara kwa mara, huwezi kushughulikia mawazo mengi sana. Nimesema hapo awali, Sitawavuta tena katika njia kwa kuwa hakuna muda wa kupoteza hata kidogo. Sina wakati wa kuwahitaji msikilize kwa makini tena na kuwakumbusha—haiwezekani! Malizeni tu maandalizi yenu kwa ajili ya vita. Mimi nakuwajibikia kikamilifu; vitu vyote viko mikononi Mwangu. Hivi ni vita vya kufa na kupona na yatakuwa mapambano ya kufa na kupona. Lakini unapaswa kutambua kwamba Mimi ni mshindi milele na Asiyeshindwa, na kwamba Shetani bila shaka ataangamia. Hii ni mbinu Yangu, kazi Yangu, mapenzi Yangu na mpango Wangu!

Imekamilika! Yote yamekamilika! Usiwe mwoga au mwenye hofu. Mimi pamoja na wewe na wewe pamoja na Mimi tutakuwa wafalme milele na milele! Maneno ambayo Nimesema hayatabadilika milele na matukio yatawafika hivi karibuni. Kesheni! Mnapaswa kutafakari vizuri kila neno; msiwe na mashaka kuyahusu tena. Lazima muwe wazi kuyahusu! Kumbuka—tumia muda zaidi mbele Zangu!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 44

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 233)

Nimeanza kuchukua hatua kuadhibu wale ambao hufanya uovu, wale ambao hushika madaraka, na wale ambao hutesa wana wa Mungu. Kuanzia sasa kuendelea, mkono wa amri Zangu za utawala utakuwa daima juu ya wale wanaonipinga mioyoni mwao. Fahamu hili! Huu ndio mwanzo wa hukumu Yangu, na hakuna huruma itakayoonyeshwa kwa yeyote wala hakuna atakayesamehewa, kwani Mimi ni Mungu asiyependelea ambaye hutenda haki, na ingekuwa vyema kwenu nyote kutambua hili.

Si kwamba Nataka kuadhibu wale ambao hufanya uovu, badala yake ni adhabu inayoletwa kwao na uovu wao wenyewe. Mimi siwi na haraka ya kumwadhibu yeyote, wala Simtendei yeyote bila haki—Natenda haki kwa wote. Kwa hakika Napenda wana Wangu na hakika Nachukia wale waovu wasionitii; hii ndiyo kanuni ya matendo Yangu. Kila mmoja wenu anapaswa kuwa na umaizi wa amri Zangu za utawala. Iwapo sivyo, hamtakuwa na hofu hata kidogo na mtakuwa wazembe mbele Yangu, na hamtajua kile Ninachotaka kutimilisha, kile Ninachotaka kufanya kuwa kamili, kile Ninachotaka kupata ama ufalme Wangu unahitaji mtu wa aina gani.

Amri Zangu za utawala ni:

1. Haijalishi wewe ni nani, ukinipinga Mimi katika moyo wako, utahukumiwa.

2. Kwa wale ambao Nimechagua, watafundishwa nidhamu mara moja kwa sababu ya wazo lolote lisilo sahihi.

3. Nitawaweka wale wasioniamini kwa upande mmoja. Nitawaruhusu wazungumze na kutenda kwa uzembe hadi mwisho kabisa ambapo Nitawaadhibu kabisa na kupambana nao.

4. Kwa wale ambao wananiamini, Nitawatunza na kuwalinda nyakati zote. Nyakati zote Nitawapa uzima kwa kutumia njia ya wokovu. Watu hawa watakuwa na upendo Wangu na hakika hawataanguka ama kupoteza njia yao. Udhaifu wowote ambao wako nao utakuwa wa muda, na kwa hakika Sitaukumbuka.

5. Kwa wale ambao wanaonekana kuamini lakini ambao kwa kweli hawaamini—kumaanisha wale ambao wanaamini kuna Mungu lakini hawamtafuti Kristo, lakini ambao pia hawapingi—watu wa aina hizi ni wa kusikitisha zaidi, na kupitia vitendo Vyangu Nitawafanya waone kwa dhahiri. Kupitia matendo Yangu, Nitawaokoa watu wa aina hizi na kuwarudisha.

6. Wazaliwa wa kwanza ambao walikuwa wa kwanza kukubali jina Langu watabarikiwa! Hakika Nitawapa baraka bora zaidi na mtakuwa na furaha hadi kuridhika kwa mioyo yenu; hakuna atakayethubutu kuizuia. Kila kitu kimetayarishwa kabisa kwa ajili yenu, kwani hii ni amri Yangu ya utawala.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 56

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 234)

Wamebarikiwa wale ambao wamelisoma neno Langu na kuamini kwamba litatimizwa—Sitakutendea vibaya, lakini Nitafanya yale unayoamini yatimizwe kwako. Hii ni baraka Yangu ikija kwako. Neno Langu linapiga siri zilizofichwa ndani ya kila mtu. Kila mtu ana majeraha ya mauti, na Mimi ni tabibu mzuri ambaye anayaponya—njoo tu katika uwepo Wangu. Kwa nini Nilisema kuwa katika siku zijazo hakutakuwa na huzuni tena na hakutakuwa na machozi tena? Ni kwa sababu ya hili. Ndani Yangu, kila kitu kinatimizwa, lakini ndani ya wanadamu, vitu vyote ni vipotovu na bure, na vyote ni vidanganyifu kwa wanadamu. Katika uwepo Wangu utapokea vitu vyote, na utaona na pia kufurahia baraka zote ambazo hungewahi kufikiria. Wale wasiokuja mbele Yangu bila shaka ni waasi, na hakika ndio wanaonipinga Mimi. Hakika Sitawaacha kwa urahisi; Nitamwadibu vikali mtu wa aina hii. Kumbuka hili! Wale wanaokuja mbele Yangu zaidi watapata zaidi, lakini haitakuwa zaidi ya neema. Baadaye, watapata baraka nyingi hata zaidi.

Tangu uumbaji wa ulimwengu Nimeanza kuamulia kabla na kuchagua kundi hili la watu, yaani, ninyi leo. Tabia yako, ubora wa tabia, sura, kimo, familia ambayo ulizaliwa kwayo, kazi yako na ndoa yako, nafsi yako yote, hata rangi ya nywele yako na ngozi yako, na wakati wa kuzaliwa kwako vyote vilipangwa na mikono Yangu. Hata mambo unayofanya na watu unaokutana nao kila siku hupangwa na mikono Yangu, sembuse ukweli kwamba kukuleta katika uwepo Wangu leo kwa kweli ni mpango Wangu. Usijitupe katika vurugu; unapaswa kuendelea kwa utulivu. Kile Ninachokuruhusu kufurahia leo ni mgawo ambao wewe unastahili, na Nilikipangia kabla katika uumbaji wa dunia. Wanadamu wote ni waliozidi sana—wao huwa vichwa ngumu sana au wasio na aibu kabisa. Hawawezi kufanya mambo kulingana na mpango Wangu na mpangilio. Usifanye hilo tena. Ndani Yangu vyote vinakombolewa; usijifunge mwenyewe, kwani utayapoteza maisha yako. Kumbuka hili!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 74

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 235)

Mimi ni Mungu Mwenyewe wa pekee, hata zaidi Mimi pekee ndimi nafsi ya Mungu, na Mimi, ukamilifu wa mwili, ni hata zaidi dhihirisho kamili la Mungu. Yeyote anayethubutu kutonicha, yeyote anayethubutu kunionyesha uasi katika macho yake, yeyote anayethubutu kuyasema maneno ya uasi dhidi Yangu hakika atakufa kutokana na laana Yangu na ghadhabu (kutakuwa na kulaani kwa sababu ya ghadhabu Yangu). Na yeyote anayethubutu kutokuwa mwaminifu au na upendo Kwangu, yeyote anayethubutu kujaribu kunifanyia hila hakika atakufa katika chuki Yangu. Haki Yangu, uadhama na hukumu vitadumu milele na milele. Mwanzoni, Nilikuwa mwenye upendo na rehema, lakini hii si tabia ya uungu Wangu kamili; haki, uadhama na hukumu ni tabia Yangu tu—Mungu Mwenyewe mkamilifu. Wakati wa Enzi ya Neema Nilikuwa mwenye upendo na rehema. Kwa sababu ya kazi Niliyopaswa kumaliza Nilikuwa na fadhila na rehema, lakini baadaye hakukuwa na haja ya fadhila yoyote au rehema (hakujakuwepo na yoyote tangu wakati huo). Yote ni haki, uadhama na hukumu na hii ni tabia kamili ya ubinadamu Wangu wa kawaida pamoja na uungu Wangu kamili.

Wale ambao hawanijui wataangamia katika kuzimu na wale ambao wana uhakika kunihusu wataishi milele, ili watunzwe na kulindwa ndani ya upendo Wangu. Punde Ninenapo neno moja, ulimwengu mzima na miisho ya dunia hutetemeka. Ni nani anayeweza kusikia maneno Yangu na asitetemeke kwa hofu? Nani hawezi kukuza moyo ambao unanicha? Nani hawezi kujua haki Yangu na uadhama kutokana na matendo Yangu? Na nani hawezi kuona uweza Wangu na hekima ndani ya matendo Yangu? Yeyote asiyezingatia kwa hakika atakufa. Hii ni kwa sababu wale wasiozingatia ni wale wanaonipinga na wasionijua; wao ni malaika wakuu na ndio watukutu zaidi. Jichunguzeni: Yeyote aliye mtukutu, anayejidai na mwenye majivuno hakika ni mlengwa wa chuki Yangu na ataangamia!

Sasa Natamka amri za utawala wa ufalme Wangu: Vitu vyote vimo ndani ya hukumu Yangu, vitu vyote vimo ndani ya haki Yangu, vitu vyote vimo ndani ya uadhama Wangu, na haki inatendwa kwa wote. Wale ambao husema wananiamini Mimi ilhali wananipinga mioyoni mwao, au ambao mioyo yao imeniacha watafukuzwa, lakini yote ni kwa wakati Wangu mzuri. Wale ambao huzungumza kwa kejeli kunihusu, lakini kwa njia ambayo watu hawatambui, watakufa mara moja (watafariki katika roho, mwili na nafsi). Kwa wale ambao huwadhulumu ama kuwadharau wale Ninaowapenda, ghadhabu Yangu itawahukumu mara moja. Hii ni kusema kwamba wale ambao wana mioyo ya wivu kwa wale Ninaowapenda na kufikiri kuwa Mimi si mwenye haki watakabidhiwa kwa wale ambao Ninawapenda ili kuwahukumu. Wale wote wenye tabia nzuri, wanyenyekevu (pamoja na wale ambao hawana hekima) na ambao ni watiifu kwa dhati Kwangu watabaki wote katika ufalme Wangu. Wale ambao hawajapitia katika mafunzo, kumaanisha watu ambao ni waaminifu wanaokosa hekima na ufahamu, watakuwa na uwezo katika ufalme Wangu. Hata hivyo wao pia wamepitia ushughulikiwaji na kuvunjwa. Kwamba hawajapitia mafunzo si hakika, lakini badala yake kupitia mambo hayo Nitaonyesha kila mtu uweza Wangu na hekima Yangu. Nitawafukuza wale ambao bado wananishuku sasa, Sitaki hata mmoja wao (Ninawachukia sana wale ambao bado hunituhumu wakati kama huu). Kwa matendo ambayo Mimi hufanya katika ulimwengu wote, Nitawaonyesha watu waaminifu matendo Yangu ya kustaajabisha, papo kukuza busara zao, ufahamu na utambuzi, na Mimi mara moja Nitasababisha watu wadanganyifu kuharibiwa kwa ajili ya matendo Yangu ya kustaajabisha. Wazaliwa wote wa kwanza waliokuwa wa kwanza kulikubali jina Langu (kumaanisha wale watakatifu wasio na dosari, watu waaminifu) watakuwa wa kwanza kuingia katika ufalme na kutawala mataifa yote na watu wote pamoja na Mimi, kutawala kama wafalme katika ufalme na pamoja kuhukumu mataifa yote na watu wote (kumaanisha wazaliwa wote wa kwanza katika ufalme, na sio wengine). Wale walio katika mataifa yote na watu wote ambao wamekwisha kuhukumiwa na wametubu wataingia katika ufalme Wangu na kuwa watu Wangu, na wale ambao ni wakaidi na wasiotubu watatupwa katika shimo la kuzimu (ili waangamie milele). Hukumu katika ufalme itakuwa mara ya mwisho na itakuwa utakaso Wangu kwa kina duniani. Hakutakuwa tena na udhalimu wowote, huzuni yoyote, machozi yoyote na hata zaidi hakutakuwa na dunia. Kila kitu kitakuwa dhihirisho la Kristo, kila kitu kitakuwa ufalme wa Kristo. Utukufu ulioje! Utukufu ulioje!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 79

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 236)

Sasa Nawatangazia rasmi amri Zangu za utawala (zinaanza kazi kuanzia siku zilipotangazwa rasmi, kutoa kuadibu tofauti kwa watu tofauti):

Natimiza ahadi Zangu, na kila kitu kiko mikononi Mwangu: Yeyote aliye na shaka hakika atauwawa. Hakuna nafasi ya huruma yoyote; wataangamizwa mara moja, hivyo kuondoa chuki kutoka moyoni Mwangu. (Kuanzia sasa inathibitika kwamba yeyote anayeuwawa lazima asiwe mshiriki wa ufalme Wangu, na lazima awe wa ukoo wa Shetani.)

Kama wazaliwa wa kwanza wa kiume, ni sharti mtunze nafasi zenu na mtimize wajibu wenu vema, na msiwe wadadisi. Ni sharti mjitolee kwa mpango Wangu wa usimamizi, na popote muendapo, ni sharti muwe na ushuhuda mzuri Kwangu na mlitukuze jina Langu. Msitende vitu vya aibu; kuweni mfano kwa wana Wangu wote na watu Wangu. Msiwe waasherati hata kwa muda kidogo: Lazima muonekane kila mara mbele ya kila mtu mkiwa na utambulisho wa wazaliwa wa kwanza wa kiume, na msiwe watumwa; badala yake, mnapaswa kutembea kwenda mbele kwa kujiamini. Nawaomba mlitukuze jina Langu, sio kulitia aibu jina Langu. Wale ambao ni wazaliwa wa kwanza wa kiume kila mmoja wao ana kazi yake binafsi, na hawawezi kufanya kila kitu. Hili ndilo jukumu Nililowapa, na halipaswi kuepukwa. Lazima mjitolee kwa mioyo yenu yote, kwa akili zenu zote na nguvu zenu zote, kwa kutimiza kile ambacho Nimewaaminia.

Kuanzia leo kuendelea, katika Ulimwengu wote, jukumu la kuongoza wana Wangu wote na watu Wangu wote litakabidhiwa wazaliwa Wangu wa kwanza wa kiume walitimize, na Nitamwadibu yeyote asiyeweza kuutoa moyo wake wote na akili katika kulitimiza. Hii ni haki Yangu. Sitawasamehe au kuwabembeleza hata wazaliwa Wangu wa kiume wa kwanza.

Ikiwa kuna yeyote kati ya wana Wangu wote au kati ya watu Wangu wote anayemdhihaki na kumtusi mmoja wa wazaliwa Wangu wa kwanza wa kiume, Nitamwadhibu vikali, kwa sababu wana Wangu wazaliwa wa kwanza wananiwakilisha Mimi Mwenyewe; kile ambacho mtu anawafanyia, ananifanyia Mimi pia. Hii ndiyo kali zaidi kati ya amri Zangu za utawala. Nitawaruhusu wazaliwa Wangu wa kwanza, kulingana na matamanio yao, watoe haki Yangu dhidi ya yeyote kati ya wana Wangu wote na watu Wangu anayeikiuka amri hii.

Taratibu Nitamtenga yeyote anayenitazama kipuuzi na anayelenga tu chakula Changu, mavazi na usingizi anayeshughulikia tu mambo Yangu ya nje na haudhukuru mzigo Wangu, na hatilii maanani kutimiza kazi zake inavyostahili. Hili linaelekezwa kwa wote walio na masikio.

Yeyote amalizaye kunifanyia huduma lazima aondoke kwa utiifu bila vurugu yoyote. Kuwa makini, la sivyo Nitakushughulikia. (Hii ni amri ya ziada).

Wazaliwa Wangu wa kwanza wa kiume watachukua fimbo ya chuma kuanzia sasa na kuendelea na kuanza kutekeleza mamlaka Yangu kutawala mataifa na watu wote, kutembea kati ya mataifa na watu wote na kuzitekeleza hukumu Zangu, haki, na uadhama kati ya mataifa yote na watu. Wana Wangu wote na watu Wangu wote wataniogopa, watanipa sifa, watanishangilia, na kunitukuza bila kukoma kwa sababu mpango wangu wa usimamizi umekamilika na wazaliwa Wangu wa kwanza wa kiume wanaweza kutawala nami.

Hii ni sehemu ya amri Zangu za utawala; baada ya hili, Nitawaambia kuyahusu kazi inapoendelea. Kutokana na amri za utawala zilizoko hapo juu, mtaona kasi ambayo kwayo Nafanya kazi Yangu, na vile vile ni hatua ipi ambayo kazi Yangu imefika. Hili litakuwa thibitisho.

Nimeshamhukumu Shetani. Kwa sababu mapenzi Yangu hayapingwi na kwa sababu wazaliwa Wangu wa kwanza wa kiume wametukuzwa pamoja na Mimi, tayari Nimetumia haki Yangu na uadhama juu ya dunia na vitu vyote ambavyo ni mali ya Shetani. Sikiinui kidole wala kumsikiliza Shetani kabisa (kwa sababu hastahili hata kuzungumza na Mimi). Nazidi tu kufanya kile Ninachotaka kufanya. Kazi Yangu inaendelea kwa ulaini, hatua kwa hatua, na mapenzi Yangu hayapingwi duniani kote. Hili limemwaibisha Shetani kwa kiwango na ameangamizwa kabisa, lakini hili peke yake halijatimiza mapenzi Yangu. Naruhusu pia wazaliwa Wangu wa kwanza wa kiume kutekeleza amri Zangu za utawala juu ya mambo yote yaliyo ya Shetani. Kwa upande mmoja, kile Ninachomruhusu Shetani aone ni hasira Yangu kuelekea kwake; kwa upande, mwingine Namruhusu auone utukufu Wangu (kuona kwamba wazaliwa Wangu wa kwanza wa kiume ndio mashahidi wakubwa sana kwa udhalilishaji wa shetani). Simwadhibu Mimi mwenyewe; badala yake, bali Naruhusu wazaliwa wangu wa kwanza wa kiume kutekeleza haki Yangu na uadhama. Kwa sababu Shetani alikuwa anawanyanyasa wana Wangu, kuwatesa wana Wangu na kuwaonea wana Wangu, leo, baada ya huduma yake kuisha, Nitawaruhusu wazaliwa Wangu wa kwanza wa kiume waliokomaa washughulike nalo. Shetani amekuwa hana nguvu dhidi ya maangamizi. Kiharusi cha mataifa yote duniani ndio ushuhuda mzuri zaidi; watu kupigana na nchi zikiwa vitani ni onyesho la wazi kabisa la kuanguka kwa ufalme wa Shetani. Sababu iliyofanya Sikuonyesha ishara na maajabu yoyote hapo zamani ilikuwa ili kumletea Shetani fedheha na kulitukuza jina Langu hatua kwa hatua. Wakati shetani ameangamizwa kabisa Naanza kuonyesha nguvu Zangu: kile Ninachosema kinatokea, na vitu vya kuvuka mipaka ambavyo havina usawa na fikira za kibinadamu vitatimia (hivi vinarejelea baraka zinazokuja karibuni). Kwa sababu Mimi ndimi Mungu Mwenyewe wa vitendo na Sina amri, na kwa sababu Nazungumza kulingana na mabadiliko katika mpango Wangu wa usimamizi, kwa hivyo kile Nilichosema zamani si lazima kiwe cha kutumika sasa. Msishikilie mawazo yenu wenyewe! Mimi siye Mungu anayezingatia amri; Kwangu, kila kitu ni huru, cha kuvuka mipaka, na kimeachiliwa kabisa. Labda kilichosemwa jana kimepitwa na wakati leo, au huenda kikawekwa kando leo (hata hivyo, amri Zangu za utawala, kwa sababu zimetangazwa rasmi hazitabadilika kamwe). Hizi ndizo hatua katika mpango Wangu wa usimamizi. Msishikilie kanuni. Kila siku kuna mwanga mpya na kuna ufunuo mpya, na huo ndio mpango Wangu. Kila siku mwanga wangu utafichuliwa kwako na sauti Yangu itaachiliwa kwa ulimwengu dunia. Je, unaelewa? Huu ni wajibu wako, jukumu ambalo Nimekuaminia. Ni lazima usilipuuze hata kidogo. Nitawatumia mpaka mwisho watu Ninaowaidhinisha, na hili halitabadilika kamwe. Kwa sababu Mimi ni mwenyezi Mungu, Najua ni mtu wa aina gani anayepaswa kufanya kitu kipi, na vile vile ni mtu wa aina gani anaweza kufanya kitu kipi. Huu ndio uweza Wangu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 88

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 237)

Kila sentensi Ninayotamka huwa na mamlaka na hukumu na hakuna mtu anayeweza kuzibadilisha. Mara tu maneno Yangu yanapotoka, mambo yatafanyika kwa mujibu wa maneno Yangu, na hii ndiyo tabia Yangu. Maneno Yangu ni mamlaka na yeyote anayeyarekebisha hukosea kuadibu Kwangu na ni lazima Nimwangamize. Hali ikiwa mbaya hayo husababisha uharibifu katika maisha yao wenyewe nao huenda kuzimu, au huenda jahanamu. Hii ndiyo njia ya pekee ambayo kwayo Ninawashughulikia wanadamu na mwanadamu hawezi kuibadilisha—hii ni amri Yangu ya utawala. Kumbuka hili! Hakuna mtu anayeruhusiwa kuikosea amri Yangu; lazima hili lifanyike kulingana na mapenzi Yangu! Zamani Nilikuwa mpole sana kwenu nanyi mlikabiliwa na maneno Yangu tu. Maneno Niliyonena kuhusu kuwaangamiza watu hayajatokea bado. Lakini kuanzia leo, majanga yote (haya yanayohusiana na amri Zangu za utawala) yatatokea moja baada ya lingine ili yawaadhibu wale wote wasiotii mapenzi Yangu. Lazima kuwe na ujio wa ukweli, vinginevyo watu hawataweza kuona ghadhabu Yangu lakini watapotoshwa tena na tena. Hii ni hatua ya mpango Wangu wa usimamizi nayo ni njia ambayo kwayo Mimi kushughulikia hatua inayofuata ya kazi Yangu. Nawaambieni hivi mapema ili muweze kuepuka kufanya makosa na kupitia mateso milele. Hiyo ni kusema, kuanzia leo Nitawafanya watu wote ila wazaliwa Wangu wa kwanza kuchukua nafasi zao halisi kwa mujibu wa mapenzi Yangu, nami Nitawaadibu mmoja baada ya mwingine. Sitamsamehe hata mmoja wao. Hebu thubutu tu kuwa wapotovu tena! Hebu thubutu tu kuwa mwasi tena! Nimesema mbeleni kuwa Mimi ni mwenye haki kwa wote bila hisia yoyote, na huu ni mfano kwamba tabia Yangu haipaswi kukosewa. Hii ni nafsi Yangu. Hakuna mtu anayeweza kubadilisha jambo hili. Watu wote husikia maneno Yangu na watu wote huuona uso Wangu mtukufu. Watu wote wanapaswa kunitii kabisa na kwa ukamilifu—hii ni amri Yangu ya utawala. Watu wote katika ulimwengu mzima na katika miisho ya dunia wanapaswa kunisifu na kunitukuza, kwa maana Mimi ni Mungu Mwenyewe wa pekee, kwa maana Mimi ni nafsi ya Mungu. Hakuna mtu anayeweza kubadili maneno na matamshi Yangu, usemi na mwenendo Wangu, kwa kuwa haya ni mambo Yangu peke Yangu, na kile ambacho Nimemiliki tangu milele na kile ambacho kitakuwepo milele.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 100

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 238)

Kazi Niliyopanga inaendelea kusonga mbele bila kukoma hata kwa muda kidogo. Baada ya kuingia katika Enzi ya Ufalme, na baada ya kukuingiza katika ufalme Wangu kama watu Wangu, Nitakuwa na madai mengine ya kuweka dhidi yenu; hiyo ni kusema, Nitaanza kutangaza rasmi mbele yenu katiba ambayo Nitatumia kuongoza enzi hii:

Kwa sababu mnaitwa watu Wangu, mnapaswa kuwa na uwezo wa kulitukuza jina Langu, yaani, kushuhudia wakati wa majaribio. Mtu yeyote akijaribu kunirairai na kunificha ukweli, au kushiriki katika shughuli zisizo za heshima nyuma Yangu, bila ubaguzi Nitamfukuza nje, aondolewe kutoka katika nyumba Yangu akisubiri Mimi nimshughulikie. Wale ambao hawajakuwa waaminifu na wasio na upendo wa mtoto kwa mzazi Kwangu zamani, na leo hii wanainuka tena kunihukumu hadharani, wao pia watafukuzwa kutoka kwa nyumba Yangu. Wale ambao ni watu Wangu lazima wajali kuhusu mizigo Yangu kila mara na vile vile kutafuta kujua maneno Yangu. Ni watu kama hawa tu ndio Nitakaowapa nuru, na wao kwa hakika wataishi chini ya uongozi Wangu na nuru, na kamwe hawatakutana na kuadibu. Wale ambao, kwa kutojali mizigo Yangu, wanamakinika na kupanga mustakabali yao wenyewe, yaani, wale ambao hawalengi kwa matendo yao kukidhi Moyo Wangu bali wanataka kuomba omba vya bure, viumbe hawa walio kama waombaji, Ninakataa kata kata kuwatumia, kwa sababu tangu walipozaliwa hawajui chochote kuhusu maana ya kujali mizigo Yangu. Wao ni watu wasiokuwa na akili ya kawaida; watu kama hawa wanaugua kutokana na “utapiamlo” wa ubongo, na wanahitaji kwenda nyumbani wapate “lishe.” Siwahitaji watu wa aina hii. Miongoni mwa watu Wangu, kila mtu atatakiwa kuzingatia kunijua kama wajibu wa lazima unaotakiwa kutekelezwa mpaka mwisho, kama kula, kuvaa, na kulala, mambo ambayo mtu kamwe hawezi kusahau hata kwa muda mfupi, ili kwamba mwishowe kunijua litakuwa jambo la kawaida kama vile kula, jambo ambalo wewe hufanya bila jitihada yoyote, kwa mkono uliozoea. Kuhusu maneno Ninayoyanena, kila neno lazima lichukuliwe kwa uhakika mkubwa na lichukuliwe kikamilifu; hakuwezi kuwa na hatua nusu za uzembe. Yeyote asiyekuwa makini na maneno Yangu ataonekana kama ananipinga Mimi moja kwa moja; mtu yeyote asiyeyala maneno Yangu, au hatafuti kuyajua, ataonekana kama ambaye hanizingatii, na moja kwa moja atafagiliwa nje ya mlango wa nyumba Yangu. Kwa maana, kama Nilivyosema zamani, Ninachotaka sio watu wengi ila wateule wachache. Kati ya watu mia, kama mmoja tu anaweza kunijua kupitia maneno Yangu, basi bila kusita Ningewatupilia mbali wengine wote ili Nizingatie kumpa nuru na mwangaza mmoja huyu. Kutokana na hili unaweza kuona kuwa, si lazima iwe ukweli kwamba idadi kubwa pekee ndio inaweza kunidhihirisha, kuishi kulingana na Mimi. Ninachotaka ni ngano (hata ingawa viini vya mbegu huenda havijajaa) na sio magugu (hata wakati viini vya mbegu vimejaa vya kutosha kutamanika). Na kuhusu wale wasiojali kuhusu kutafuta lakini badala yake kuwa na tabia za kuzembea, wanapaswa kuondoka kwa hiari yao wenyewe; Mimi sitaki kuwaona tena, wasije wakaleta aibu kwa jina Langu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 5

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 239)

Kwa sababu kwamba wewe ni mmoja wa watu nyumbani Mwangu, na kwa sababu wewe ni mwaminifu katika Ufalme wangu, kila unachofanya lazima kifikie viwango Ninavyohitaji Mimi. Sisemi kwamba uwe tu kama wingu linalofuata upepo, bali uwe kama theluji inayong’aa, na uwe na hali kama yake na hata zaidi uwe na thamani yake. Kwa sababu Nilitoka katika nchi takatifu, si kama yungiyungi, ambalo lina jina tu na halina dutu kwa sababu lilikuja kutoka katika matope na si kutoka nchi takatifu. Wakati ambapo mbingu mpya inashuka duniani na nchi mpya kuenea juu ya anga ndio pia wakati hasa ambao Ninafanya kazi kirasmi miongoni mwa binadamu. Ni nani kati ya wanadamu anayenijua Mimi? Ni nani aliyeona wakati wa kuwasili Kwangu? Ni nani ameona kwamba Mimi sina jina tu, bali zaidi ya jina Nina dutu? Mimi huyasongeza mawingu meupe kwa mkono wangu na kwa karibu Naichunguza anga; katika anga, hakuna kitu kisichopangwa kwa mkono wangu, na chini ya anga, hakuna mwanadamu asiyechangia juhudi yake ndogo kwa ukamilishaji wa shughuli Yangu kuu. Mimi Simwekei mwanadamu madai mazito duniani, kwa maana Mimi daima Nimekuwa Mungu wa vitendo, na kwa sababu Mimi ni Mwenyezi Aliyeumba mwanadamu na Anayejua mwanadamu vizuri. Watu wote wako machoni pa Mwenyezi. Hata wale walio katika pembe zote mwisho wa dunia watawezaje kuepuka uchunguzi wa Roho Yangu? Ingawa mwanadamu “anajua” Roho Wangu, yeye pia huikosea Roho Wangu. Maneno Yangu yanaweka wazi uso mbaya wa wanadamu wote, na kuweka wazi mawazo ya ndani kabisa ya watu wote, na kusababisha wote duniani kufanywa wazi na mwanga Wangu na kuanguka chini ndani ya uchunguzi Wangu. Ijapokuwa mwanadamu anaanguka chini, moyo wake hauthubutu kwenda mbali Nami. Miongoni mwa viumbe, ni nani asiyekuja kunipenda kwa sababu ya matendo Yangu? Ni nani asiyekuwa na hamu kwa ajili ya kuyasikia maneno Yangu? Ni nani asiyezaliwa ndani mwake na hisia za ibada kwa sababu ya upendo Wangu? Ni kwa sababu tu ya ufisadi wa Shetani ndio maana mwanadamu anashindwa kuufikia ulimwengu kama Ninavyomhitaji kufika. Hata viwango vya chini kabisa ambavyo Mimi Namhitaji kufika huzalisha mashaka ndani yake, bila kutaja chochote cha leo, enzi ambayo Shetani anaendesha ghasia na ni mdhalimu mkuu, au wakati ambapo mwanadamu amekanyagwa sana na Shetani mpaka mwili wake mzima umejaa uchafu. Ni lini ambapo kutojali kwa mwanadamu kuhusu moyo Wangu kwa sababu ya upotovu wake hakujanisababishia Mimi huzuni? Je, inawezekana kwamba Mimi namwonea Shetani huruma? Je, inawezekana kwamba Mimi Nimekosea katika upendo wangu? Wakati mwanadamu ananikaidi, Moyo wangu unaomboleza kwa siri; wakati mwanadamu ananipinga, Ninamwadibu; wakati Ninamwokoa mwanadamu na kumfufua kutoka wafu, Mimi Huwalisha kwa uangalifu wanaponyenyekea mbele zangu, Moyo Wangu unatulia tuli na mara moja Ninahisi mabadiliko makubwa katika mbinguni na duniani na vitu vyote. Wanadamu wanaponisifu Mimi, itawezekanaje Nisiwe na furaha? Wakati mwanadamu ananishuhudia na kupatwa na Mimi, itawezekanaje Nisitukuzwe? Inawezekana kwamba kila anachofanya mwanadamu hakiongozwi na kutolewa na Mimi? Wakati ambapo Sitoi mwelekeo, wanadamu wanazembea na kuwa wanyamavu, na, nyuma Yangu, wao wanashiriki katika zile shughuli chafu “zenye kusifika.” Je, unafikiri kwamba mwili Ninaouvaa, haufahamu chochote kuhusu matendo yako, tabia zako, na maneno yako? Nimestahimili mvua na upepo kwa miaka mingi, na vile vile Nimepitia machungu ya ulimwengu wa binadamu, lakini ukitafakari kwa karibu, hakuna kiasi cha mateso kinachoweza kumfanya mwanadamu aliye katika nyama za mwili kupoteza matumaini ndani Yangu, kama vile hakuna utamu wowote unaoweza kumfanya mwanadamu wa mwili awe bila hisia, mwenye kuvunjika moyo au mwenye kunipuuza Mimi. Je, upendo wa mwanadamu Kwangu una mipaka kwa hali ya kutokuwa na maumivu au kutokuwa na utamu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 9

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 240)

Leo, sababu Nimewaongoza hadi hapa, Nimefanya mipango ya kufaa, na Nina malengo Yangu Mwenyewe. Ningewaeleza kuyahusu leo, mngeweza kweli kuyajua? Nayajua vizuri mawazo ya akili ya mwanadamu na matakwa ya moyo wa mwanadamu: Nani hajawahi kutafuta njia ya kujitoa mwenyewe? Nani hajawahi fikiria matarajio yake mwenyewe? Lakini hata kama mwanadamu ana akili tajiri na wa mche nani aliweza kutabiri kwamba, kufuatia enzi, sasa kungekuwa kulivyo? Hili kweli ni tunda la juhudi zako binafsi? Haya ni malipo ya kazi yako ya bidii? Hii ndiyo picha nzuri iliyoonwa na akili yako? Nisingewaongoza wanadamu wote, nani angeweza kujitenga na mipango Yangu na kupata njia nyingine ya kutoka? Ni fikira akilini mwa mwanadamu na tamaa yake ambayo yamemleta hadi leo? Watu wengi wanaishi maisha yao yote bila kutimiziwa kwa matakwa yao. Kweli hili ni kwa sababu ya kosa katika fikira zao? Maisha ya watu wengi yamejawa na furaha na ridhaa isiyotarajiwa. Kweli ni kwa sababu wanatarajia kidogo sana? Je, nani kati ya wanadamu wote hatunzwi mbele ya macho ya Mwenyezi? Nani haishi maisha kati ya majaaliwa ya Mwenyezi? Je, kuishi kwa mwanadamu kifo chake kinatokana na uchaguzi wake mwenyewe? Je, mwanadamu anadhibiti hatima yake? Wanadamu wengi wanalilia kifo, lakini kiko mbali nao; watu wengi wanataka kuwa watu wenye nguvu maishani na wanahofia kifo, lakini bila kujua kwao, siku ya kufa kwao inasongea karibu, ikiwatumbukiza ndani ya dimbwi la kifo; watu wengi wanatazama angani na kutoa pumzi kwa undani; watu wengi wanalia sana, wakiomboleza; watu wengi wanaanguka kuwapo majaribu; na watu wengi wanakuwa wafungwa wa majaribu. Ingawa Sijitokezi binafsi kumruhusu mwanadamu kunitazama vizuri, watu wengi wanaogopa kuona uso Wangu, wanaogopa sana Nitawapiga chini, kwamba Nitawaangamiza. Mwanadamu kweli ananijua Mimi ama hanijui? Hakuna anayeweza kusema kwa hakika. Sivyo? Mnaniogopa na pia kuadibu Kwangu, lakini bado mnasimama na kunipinga wazi na kunihukumu hadharani. Sivyo? Kwamba mwanadamu hajawahi kunijua ni kwa sababu hajawahi kuuona uso Wangu ama kuisikia sauti Yangu. Hivyo, hata kama Niko ndani ya moyo wa mwanadamu, je, kuna wale ambao Sionekani mwenye ukungu na asiye dhahiri katika mioyo yao? Kuna wale Ninaoonekana vizuri ndani ya mioyo yao? Sitamani wale walio watu Wangu pia kutoniona vizuri, na hivyo Naanza kazi hii kubwa.

Nakuja polepole miongoni mwa wanadamu, na Naondoka taratibu. Kuna aliyewahi kuniona? Jua linaweza kuniona kwa sababu ya moto wake unaochoma? Mwezi unaweza kuniona kwa sababu ya uwazi wake unaong’aa? Kundinyota zinaweza kuniona kwa sababu ya mahali zipo angani? Nikujapo, mwanadamu hajui, na mambo yote yanabakia gizani, na Niondokapo, bado mwanadamu hafahamu. Nani anaweza kuwa na ushuhuda Kwangu? Inaweza kuwa sifa ya watu wa dunia? Inaweza kuwa mayungiyungi yanayochanua porini? Inaweza kuwa ndege wanaoruka angani? Inaweza kuwa simba wanaonguruma milimani? Hakuna anayeweza kunishuhudia kikamilifu. Hakuna anayeweza kufanya kazi Nitakayoifanya! Hata kama wangefanya kazi hii, ingekuwa na athari gani? Kila siku Naona vitendo vyote vya watu wengi, na kila siku Nachunguza mioyo na akili za watu wengi; hakuna aliyewahi kutoroka hukumu Yangu, na hakuna aliyewahi kuachana na uhalisi wa hukumu Yangu. Nasimama juu ya mawingu na kuangalia kwa umbali: Nimewaangamiza watu wengi, lakini pia watu wengi wanaishi katika huruma, na wema Wangu. Nyinyi pia hamuishi chini ya hali kama hizi?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 11

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 241)

Duniani, Mimi ni Mungu wa vitendo Mwenyewe katika mioyo ya watu; mbinguni, Mimi Ndiye Mkuu wa viumbe vyote. Nimepanda milima na kuvuka mito, na Nimeingia na kutoka katikati ya binadamu. Nani anathubutu kwa uwazi kumpinga Mungu wa vitendo Mwenyewe? Nani anathubutu kutoka kati ya ukuu wa Mwenyezi? Nani anayethubutu kudai kuwa Mimi, bila shaka, Niko mbinguni? Tena, nani ambaye anathubutu kudai kuwa Mimi, bila kukosea, Niko duniani? Hakuna binadamu kati ya wote anayeweza kujieleza kwa ufasaha na undani mahali ambapo Mimi Naishi. Inawezekana kuwa kwamba, wakati Mimi niko mbinguni, Mimi ni Mungu Mwenyewe asiye wa kawaida? Inawezekana kuwa kwamba, wakati Mimi niko hapa duniani, Ninakuwa Mungu wa vitendo Mwenyewe? Kwamba Mimi ni Mtawala wa viumbe vyote, au kwamba Mimi ninapitia mateso ya ulimwengu wa mwanadamu—hakika hivi haviwezi kuamua iwapo Mimi ni Mungu wa vitendo Mwenyewe? Kama mwanadamu anadhani hivyo[a], si yeye ni mpumbavu asiye na matumaini ya kubadilika? Mimi niko mbinguni; Mimi pia Niko duniani; Niko miongoni mwa mambo idadi kubwa ya viumbe, na pia katikati ya idadi kubwa ya watu. Mwanadamu anaweza kunigusa kila siku; zaidi ya hayo, anaweza kuniona kila siku. Kulingana na binadamu, Mimi huonekana kuwa wakati mwingine Nimejificha na wakati mwingine Naonekana; Mimi kwa kweli nipo, lakini pia naonekana kutokuwepo. Ndani Mwangu kuna siri kubwa sana zisizoweza kufahamika na binadamu. Ni kana kwamba watu wote wananitazama kwa njia ya hadubini ili kugundua siri hata zaidi ndani Mwangu, wakiwa na matumaini ya kuondoa hisia za wasiwasi katika nyoyo zao. Lakini hata watumie darubini ya nguvu kivipi, binadamu watawezaje kuziweka wazi siri zilizo ndani Mwangu?

Wakati watu Wangu, kupitia kwa kazi Yangu, wanatukuzwa pamoja na Mimi, wakati huo maficho ya joka kubwa jekundu yatafichuliwa, matope yote na uchafu kufagiliwa mbali, na maji machafu, yaliyokusanyika kwa miaka mingi, kukaushwa na moto Wangu unaochoma, yasikuwepo tena. Hapo joka kubwa jekundu litaangamia katika ziwa la moto wa jehanamu. Je, kweli unayo nia ya kusalia chini ya ulinzi Wangu ili usinyakuliwe na joka? Je, kweli unachukia mbinu yake ya udanganyifu? Nani ambaye anaweza kuwa shahidi Wangu wa dhati? Kwa ajili ya jina Langu, kwa ajili ya Roho Wangu, na kwa sababu ya mpango Wangu mzima wa usimamizi, ni nani anayeweza kutoa nguvu zake zote? Leo, wakati ambao ufalme upo katika ulimwengu wa wanadamu, ni wakati ambao Nimekuja binafsi miongoni mwa binadamu. Kama haingekuwa hivyo, je, kuna yeyote ambaye anaweza kujitokeza aende kwenye uwanja wa vita kwa niaba Yangu bila hofu yoyote? Ndipo ufalme uweze kuchukua mkondo, ili moyo Wangu uweze kuridhika, na tena, ili siku Yangu iweze kuja, ili wakati uweze kuja ambapo mambo mengiya uumbaji yamezaliwa upya na kukua kwa wingi, ili kwamba mwanadamu aweze kuokolewa kutoka kwenye bahari ya mateso, ili siku inayofuata iweze kuja, na ili iwe ni ya ajabu, yenye kutoa maua na kushamiri, na tena, ili starehe ya siku za usoni itimizwe, binadamu wote wanajitahidi kwa nguvu zao zote, bila kuwacha chochote katika kujitoa sadaka wenyewe kwa ajili Yangu. Je, hii si ishara kwamba ushindi tayari ni Wangu, na alama ya kukamilika kwa mpango Wangu?

Wanadamu wanavyozidi kukaa katika siku za mwisho, ndivyo watakavyozidi kuhisi utupu wa dunia na ndivyo watakavyopungukiwa na ujasiri wa jinsi ya kuishi. Kwa sababu hii, watu wasiohesabika wamekufa katika hali ya kuvunja matumaini, wengine wengi wamevunjwa matumaini katika jitihada zao, na wengine wengi kuteseka wenyewe kuwa kunyanyaswa katika mikono ya shetani. Mimi Nimewaokoa watu wengi, Nimewapa wengi msaada, na mara nyingi, wakati binadamu wamepoteza mwanga, Mimi Nimewaongoza kurudi katika nafasi ya mwanga, ili wapate kunijua wakiwa kwenye mwanga, na kunifurahia katika furaha. Kwa sababu ya ujio wa mwanga Wangu, kuabudu hukuzwa katika mioyo ya watu wanaokaa katika ufalme Wangu, kwa maana Mimi ni Mungu wa kupendwa na binadamu, Mungu ambaye binadamu unajishika katika hali ya upendo, na mwanadamu anajazwa na maono ya kudumu ya umbo Langu. Hata hivyo, baada ya yote, hakuna mtu anayeelewa ikiwa hii ni kazi ya Roho au ni kazi ya mwili. Itawachukua watu maisha yote kupitia jambo hili moja. Wanadamu hawajawahi kunichukia ndani ya vina vya mioyo yao; badala yake, wananishikilia katika vina vya roho zao. Hekima yangu inaibua upendezewaji wake, maajabu Ninayotenda ni ukuu machoni pake, maneno Yangu yanastaajabisha akili yake, na bado yeye ana mapenzi tele kwayo. Uhalisi Wangu unawaacha wanadamu wasijue la kufanya, wakipigwa na butwaa na kukanganyikiwa, na bado wako tayari kuukubali. Je, hiki si kipimo cha mwanadamu jinsi alivyo hasa?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 15

Tanbihi:

a. Maandiko ya asilia yanasema “Katika hali hii.”

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 242)

1. Mwanadamu hapaswi kujitukuza wala kujipa sifa. Anapaswa kumwabudu na kumsifu Mungu.

2. Unapaswa kufanya lolote ambalo lina manufaa kwa kazi ya Mungu, na hupaswi kufanya chochote ambacho kitaleta madhara kwa manufaa ya kazi ya Mungu. Unapaswa kutetea jina la Mungu, ushahidi Wake, na kazi ya Mungu.

3. Pesa, vitu vya dunia, na mali yote ambayo yako katika kaya ya Mungu ni sadaka ambazo zinapasa kutolewa na binadamu. Sadaka hizi hazifai kufurahiwa na binadamu yeyote ila kasisi na Mungu Mwenyewe, kwani sadaka zinazotolewa na binadamu ni za kufurahiwa na Mungu, Mungu pekee ndiye Anayeweza kumgawia kasisi sadaka hizi, na hakuna mwingine yeyote aliyehitimu wala kuwa na haki ya kufurahia sehemu yoyote ya sadaka hizi. Sadaka zote zinazotolewa na mwanadamu (ikiwemo pesa na vitu vinavyoweza kufurahiwa) vinapewa Mungu, na sio kwa mwanadamu. Na hivyo, vitu hivi havipaswi kufurahiwa na mwanadamu; iwapo mwanadamu angevifurahia vitu hivi, basi angekuwa anaiba sadaka. Yeyote yule atakayefanya hili ni msaliti kama Yuda, kwa kuwa, zaidi ya Yuda kuwa msaliti. Yuda alijitwalia vilivyokuwa katika mfuko wa hela.

4. Mwanadamu anayo tabia ya upotovu na, zaidi ya hayo, amejawa na hisia. Kwa hivyo, ni marufuku kabisa kwa watu wa jinsia mbili tofauti kufanya pamoja kazi wakati wa kumtumikia Mungu bila kuwepo na mtu mwingine. Yeyote yule atakayepatikana na kosa hili atatupiliwa mbali, bila ubaguzi—na hakuna atakayeepuka hili.

5. Hupaswi kumhukumu Mungu, au kujadili kwa kawaida mambo yanayomuhusu Mungu. Unapaswa kutenda vile mwanadamu anavyopaswa kutenda, na kuzungumza jinsi mwanadamu anapasa kuzungumza, na hupaswi kuvuka upeo wako wala kuvuka mipaka yako. Uchunge ulimi wako na uwe mwangalifu na hatua zako. Yote haya yatakuzuia kufanya jambo lolote linaloweza kukosea tabia ya Mungu.

6. Unapaswa kufanya yale yanayopaswa kufanywa na mwanadamu, na kutenda wajibu wako, na kutimiza majukumu yako, na kushikilia jukumu lako. Kwa sababu unaamini katika Mungu, unapasa kutoa mchango wako kwa kazi ya Mungu; kama huwezi, basi wewe hufai kula na kunywa maneno ya Mungu, na hufai kuishi katika nyumba ya Mungu.

7. Katika kazi na mambo yanayohusiana na kanisa, kando na kumtii Mungu, katika kila kitu unapaswa kufuata maagizo ya mwanadamu anayetumiwa na Roho Mtakatifu. Hata kosa lolote hata liwe dogo kivipi halikubaliwi. Lazima uwe mkamilifu katika kutii kwako, na hupaswi kuchunguza kati ya mazuri na mabaya; yaliyo mazuri au mabaya hayakuhusu. Unapaswa kujishughulisha tu na utiifu kamili.

8. Watu wanaoamini katika Mungu wanapaswa kumtii na kumwabudu. Hupaswi kusifu au kumwabudu mtu yeyote; hupaswi kumpa Mungu nafasi ya kwanza, binadamu unayemheshimu nafasi ya pili, kisha wewe mwenyewe nafasi ya tatu. Mtu yeyote asishikilie nafasi yoyote moyoni mwako, na hufai kuzingatia watu—hasa wale unaowaenzi—kuwa katika kiwango sawa na Mungu, kuwa sawa na Yeye. Mungu hawezi kustahimili hili.

9. Mawazo yako yanapasa kuwa ya kazi ya kanisa. Unapaswa kuweka kando matarajio ya mwili wako, uwe na msimamo thabiti kuhusu mambo ya kifamilia, na ujitoe kwa moyo wako wote kwa kazi ya Mungu, na uiweke kazi ya Mungu kwanza kisha maisha yako katika nafasi ya pili. Huu ndio mwenendo mwema wa utakatifu.

10. Jamaa zako (watoto, mke au mume, dada zako au wazazi wako na kadhalika) wasio wa imani yako hawapaswi kulazimishwa kuja kanisani. Nyumba ya Mungu haina ukosefu wa washirika, na hakuna haja ya kuijaza na watu wasiokuwa na maana katika nyumba Yake. Wale wote wasioamini kwa moyo mchangamfu, hawapaswi kuongozwa kuingia kanisani. Amri hii inaelekezwa kwa kila mwanadamu. Kuhusu hili jambo mnapaswa kuchunguza, mfuatilie na mkumbushane, na hakuna anayepasa kukiuka amri hii. Hata jamaa wako wasio wa imani yako wanapoingia kanisani shingo upande, hawapaswi kupatiwa jina jipya wala kupewa vitabu vya kanisa; watu kama hao si wa kaya ya Mungu, na kuingia kwao kanisani kunapaswa kukomeshwa kwa udi na uvumba. Iwapo matatizo yataletwa kanisani kwa sababu ya uvamizi wa mapepo, basi wewe mwenyewe utafukuzwa au kuwekewa vikwazo. Kwa ufupi, kila mmoja analo jukumu katika hili jambo, lakini pia hupasi kuwa asiyejali, wala kutumia jambo hili kulipiza kisasi cha kibinafsi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Amri Kumi za Utawala Ambazo Lazima Wateule wa Mungu Katika Enzi ya Ufalme Wazitii

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 243)

Watu lazima wafuate majukumu mengi wanayostahili kuyatekeleza. Hili ndilo watu wanalopaswa kufuata, na wanalostahili kufanya. Mruhusu Roho Mtakatifu afanye linalostahili kufanywa na Roho Mtakatifu; mwanadamu hawezi kulichangia lolote. Mwanadamu sharti ashike yale ambayo lazima yatendwe na mwanadamu, ambayo hayana uhusiano na Roho Mtakatifu. Si lolote bali lile ambalo lazima litendwe na mwanadamu, na lazima lifuatwe kama amri, kama ufuasi wa sheria za Agano la Kale. Ingawa sasa si Enzi ya Sheria, bado kuna maneno mengi yanayolingana na Enzi ya Sheria ambayo yanahitaji kufuatwa, na hayatendwi tu kwa kutegemea kuguswa na Roho Mtakatifu, lakini ni yale yanayostahili kufuatwa na wanadamu. Kwa mfano: Hupaswi kuihukumu kazi ya Mungu wa vitendo. Hupaswi kumpinga mtu anayeshuhudiwa na Mungu. Mbele za Mungu, utahifadhi nafasi yako, na hutakuwa mwovu. Matamshi yako yanapaswa yawe wastani, na maneno yako na matendo yako yanapaswa kufuata mpangilio wa mwanadamu aliyeshuhudiwa na Mungu. Unapaswa kuheshimu ushuhuda wa Mungu. Usipuuze kazi ya Mungu wala maneno kutoka kinywa chake. Usiige sauti na malengo ya matamshi ya Mungu. Kwa nje, usifanye lolote linalodhihirisha kumpinga mtu anayeshuhudiwa na Mungu. Na mengineyo. Haya ndiyo yanayopaswa kufuatwa na kila mmoja. Katika kila enzi, Mungu hutaja amri nyingi zinazoambatana na amri na zinazopaswa kufuatwa na mwanadamu. Kupitia hili, anazuia tabia ya mwanadamu, na kugundua ukweli wake. Tazama maneno “Onyesha heshima kwa baba na mama yako” kutoka kwa nyakati za Agano la Kale, kwa mfano. Maneno haya hayatumiki hivi leo; wakati huo, yalizuia tabia zingine za mwanadamu tu, yalitumika kuonyesha uaminifu wa imani ya mwanadamu kwa Mungu, na yalikuwa alama ya wale waliomwamini Mungu. Ingawa sasa ni Enzi ya Ufalme, bado kuna amri nyingi ambazo mwanadamu lazima azifuate. Amri za kale hazitumiki; leo, kuna mazoea mengi, mwafaka kwa mwanaadamu kutekeleza, na ambayo ni muhimu. Hayahusiani na kazi ya Roho Mtakatifu na lazima yatendwe na mwanadamu.

Katika Enzi ya Neema, mazoea mengi ya Enzi ya Sheria yaliondolewa kwa sababu sheria hizi hazikufaa hasa kazi ya wakati huo. Baada ya kuondolewa, mazoea mengi yaliwekwa ambayo yalifaa enzi hiyo, na ambayo yamekuwa amri nyingi za sasa. Mungu wa leo alipokuja, kanuni hizi zilitupiliwa mbali, na hazikuhitajika kufuatwa tena, na mazoea mengi ambayo yalifaa kazi ya wakati huu yakawekwa. Leo, mazoea haya si kanuni, lakini ili kuwa na athari; ni mazuri kwa ajili ya leo—na kesho, pengine, yatakuwa kanuni. Kwa ujumla, unafaa kufuata yale ambayo yatafanikisha kazi ya leo. Usizingatie kesho: Yanayofanywa leo ni kwa ajili ya leo. Pengine kesho kutakuwa na mazoea mazuri ambayo utahitajika kutekeleza—lakini usizingatie hayo sana, yafuate yanayofaa kufuatwa leo ili uepuke kumpinga Mungu. Leo, hakuna lolote muhimu analopaswa kufuata mwanadamu zaidi ya yafuatayo: Usijaribu kumbembeleza Mungu anayesimama mbele ya macho yako, au kumficha jambo lolote. Usizungumze uchafu ama matamshi ya kiburi mbele ya Mungu aliye mbele yako. Usimdanganye Mungu mbele ya macho yako kwa maneno mazuri wala kwa maneno ya kuridhisha ili uweze kujipatia uaminifu Wake. Usitende bila heshima mbele za Mungu. Tii yote yatokayo kinywani mwa Mungu, wala usikatae, usipinge, ama kusaili maneno Yake. Usitafsiri unavyoona kuwa sawa, maneno yanayonenwa kutoka kinywani mwa Mungu. Chunga ulimi wako ili usikutie katika mtego wa hila danganyifu za yule mwovu. Unapaswa kulinda nyayo zako ili kuepuka kupita mipaka uliyowekewa na Mungu. Kufanya hivyo kutakufanya uzungumze maneno ya majivuno na yenye fahari kuu kulingana na mtazamo wa Mungu, na hivyo kufanya uchukiwe na Mungu. Usieneze maneno kutoka kinywa cha Mungu ovyo ovyo, usije ukadhihakiwa na wengine na kufanywa kuwa mjinga na mapepo. Tii kazi yote ya Mungu wa leo. Hata ikiwa hauifahamu, usiihukumu; unachoweza kufanya ni kutafuta na kushiriki. Hakuna mtu atapatendea dhambi mahali pa Mungu pa asili. Huwezi kufanya lolote ila kumhudumia Mungu wa leo kwa mtazamo wa mwanadamu. Huwezi kumfunza Mungu wa leo kwa mtazamo wa mwanadamu—kufanya hivyo ni kupotoka. Hakuna anayeweza kusimama kwa niaba ya mtu aliyeshuhudiwa na Mungu; katika maneno yako, matendo, na mawazo yako ya ndani, unasimama katika nafasi ya mwanadamu. Hili ni la kufuatwa, ni wajibu wa mwanadamu, hakuna anayeweza kulibadilisha, na kufanya hivyo ni ukiukaji wa amri za utawala. Inapaswa kukumbukwa na kila mtu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Amri za Enzi Mpya

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 244)

Kunayo mambo mengi ambayo Ninatumai mtaweza kufikia. Hata hivyo, matendo yenu na maisha yenu yote hayawezi kuridhisha matakwa Yangu kikamilifu, kwa hiyo lazima Niseme kile hasa ninachotaka kusema na kuwafafanulia mapenzi Yangu. Kwa kuwa utambuzi wenu ni ndogo na shukrani yenu pia ni ndogo, karibu mmekosa kabisa kujua tabia Yangu na dutu Yangu pia, na hivyo ni suala la dharura kwangu Mimi kuwafahamisha kuyahusu. Haijalishi hapo awali ulielewa kiwango kipi au kama uko radhi kujaribu kuelewa masuala haya, lazima bado Niyaelezee kwenu kwa undani. Masuala haya si mageni kabisa kwenu, lakini inaonekana kwamba hamwelewi au hamjazoea maana iliyomo ndani yao. Wengi wenu mnao ufahamu dhaifu tu na aidha ufahamu kiasi na usiokamilika. Ili kuwasaidia kutenda ukweli kwa njia bora zaidi, yaani, kuweka maneno Yangu katika matendo kwa njia bora zaidi, Nafikiri kwamba ni masuala haya ambayo lazima kwanza myajue. Vinginevyo, imani yenu itabakia isiyo wazi, ya unafiki, na iliyopambwa sana na dini. Kama huelewi tabia ya Mungu, basi haitawezekana kwako kufanya kazi unayofaa kumfanyia. Kama hujui dutu ya Mungu, haitawezekana wewe kumwonyesha heshima na uchaji, lakini badala yake utakuwa tu mzembe asiyejali na kuepuka kusema ukweli wote, na zaidi, kukufuru kusikorekebishika. Ingawa kuelewa tabia ya Mungu kwa kweli ni muhimu sana, na maarifa ya dutu ya Mungu hayawezi kupuuzwa, hakuna yeyote amewahi kuchunguza kwa umakini au kudadisi masuala haya. Ni wazi kuona kwamba nyote mmepuzilia mbali amri za utawala Nilizozitoa. Kama hamuelewi tabia ya Mungu, basi mtaweza kukosea kwa urahisi sana tabia Yake. Kosa kama hilo ni sawa na kumkasirisha Mungu Mwenyewe, na tunda la msingi la tendo lako linakuwa ni kosa dhidi ya amri ya utawala. Sasa unafaa kutambua kwamba kuelewa tabia ya Mungu huja na kujua dutu Yake, nakwamba pamoja na kuelewa tabia ya Mungu huja kuelewa amri za utawala. Bila shaka, amri nyingi za utawala zinahusisha tabia ya Mungu, lakini tabia Yake haijaonyeshwa ndani yao kikamilifu. Kwa hivyo mnawahitaji kuongeza hatua nyingine katika kukuza ufahamu wenu wa tabia ya Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 245)

Tabia ya Mungu ni mada ambayo inaonekana kuwa ya dhahania sana kwa kila mtu na aidha ambayo haikubaliwi kwa urahisi, kwani tabia Yake ni tofauti na hulka ya binadamu. Mungu, vilevile, anazo hisia za raha, hasira, huzuni, na furaha, lakini hisia hizo zinatofautiana na zile za binadamu. Mungu ndicho kile Alicho na Anacho kile anacho. Kila kitu Anachokidhihirisha na kukifichua ni viwakilishi vya dutu Yake na utambulisho Wake. Kila alicho na anacho, pamoja na dutu na utambulisho Wake vyote ni vitu ambavyo haviwezi kubadilishwa na binadamu yeyote. Tabia Yake inajumuisha upendo Wake kwa binadamu, tulizo kwa binadamu, chuki kwa binadamu, na hata zaidi, uelewa wa kina wa binadamu. Hulka ya binadamu, hata hivyo, inaweza kuwa yenye matumaini mema, changamfu, au ngumu. Tabia ya Mungu ni ile ambayo inamilikiwa na Mtawala wa vitu vyote na viumbe vyote vyenye uhai, kwa Bwana wa viumbe vyote. Tabia Yake inawakilisha heshima, nguvu, uadilifu, ukubwa, na zaidi kuliko vyote, mamlaka ya juu kabisa. Tabia Yake ni ishara ya mamlaka, ishara ya kila kitu kilicho cha haki, cha kuvutia, ishara ya kila kitu kilicho chema na kizuri. Aidha, ni ishara ya Yeye ambaye hawezi[a] kushindwa au kushambuliwa na giza na nguvu yoyote ya adui, pamoja na ishara ya Yeye ambaye hawezi kukosewa(wala Hatavumilia kukosewa)[b] na kiumbe yeyote aliyeumbwa. Tabia Yake ni ishara ya nguvu za kiwango cha juu zaidi. Hakuna mtu au watu wanao uwezo au wanaoweza kutatiza kazi Yake au tabia Yake. Lakini hulka ya binadamu ni ishara tu ya mamlaka kidogo ya binadamu juu ya wanyama. Binadamu mwenyewe hana mamlaka, hana uhuru, na hana uwezo wa kuzidi nafsi, bali katika dutu yake ni yule ambaye kwa woga yuko chini ya watu, matukio na mambo ya kila aina. Raha ya Mungu inatokana na uwepo na kuibuka kwa haki na mwangaza; kwa sababu ya kuangamizwa kwa giza na maovu. Anafurahia kwa sababu Ameuleta mwangaza na maisha mazuri kwa wanadamu; raha Yake ni raha ya haki, ishara ya uwepo wa kila kitu kilicho kizuri, na zaidi, ishara ya fadhili. Hasira ya Mungu inatokana na uharibifu ambao kuwepo na kuingilia kwa dhuluma kunaleta kwa wanadamu Wake, kwa sababu ya uwepo wa maovu na giza, kwa sababu ya uwepo wa vitu vinavyoondoa ukweli, na hata zaidi kwa sababu ya uwepo wa vitu vinavyopinga kile ambacho ni kizuri na chema. Hasira Yake ni ishara ya kwamba vitu vyote vibaya havipo tena, na fauka ya hayo, ni ishara ya utakatifu Wake. Huzuni Yake ni kwa sababu ya wanadamu, ambao Amekuwa na matumaini nao lakini ambao wameanguka katika giza, kwa sababu kazi Afanyayo kwa mwanadamu haifikii matarajio Yake, na kwa sababu binadamu Awapendao hawawezi wote kuishi katika mwanga. Anahisi huzuni kwa sababu ya wanadamu wasio na hatia, kwa yule binadamu mwaminifu lakini asiyejua, na kwa yule mwanadamu mzuri lakini mwenye upungufu katika maoni yake mwenyewe. Huzuni Yake ni ishara ya wema Wake na huruma Yake, ishara ya uzuri na ukarimu. Furaha yake, bila shaka, inatokana na kuwashinda adui Zake na kupata imani nzuri ya binadamu. Aidha, inatokana na kuondolewa na kuangamizwa kwa nguvu zote za adui na kwa sababu wanadamu hupokea maisha mazuri na yenye amani. Furaha ya Mungu ni tofauti na raha ya binadamu; badala yake, ni ile hisia ya kupokea matunda mazuri, hisia ambayo ni kubwa zaidi kuliko raha. Furaha Yake ni ishara ya wanadamu kuwa huru dhidi ya mateso kutoka wakati huu kuendelea, na ishara ya wanadamu kuingia katika ulimwengu wa mwangaza. Hisia za mwanadamu, kwa upande mwingine, zote huibuka kwa ajili ya masilahi yake mwenyewe, na wala si kwa ajili ya haki, mwangaza, au kile ambacho ni cha kupendeza, sembuse neema inayotolewa na Mbinguni. Hisia za wanadamu ni za ubinafsi na zinamilikiwa na ulimwengu wa giza. Hisia hizo hazipo kwa ajili ya mapenzi, sembuse mpango wa Mungu, na kwa hiyo mwanadamu na Mungu hawawezi kamwe kuzungumziwa hapohapo. Mungu siku zote anayo mamlaka ya juu zaidi na ni mwenye heshima kila wakati, ilhali mwanadamu siku zote ni wa chini, siku zote asiye na thamani. Hii ni kwa sababu Mungu siku zote anajitolea mhanga na kujitoa Mwenyewe kwa wanadamu; mwanadamu, hata hivyo, siku zote huchukua na kujitahidi kwa ajili yake pekee. Siku zote Mungu anashughulikia kwa dhati kuendelea kuishi kwa wanadamu, ilhali mwanadamu kamwe hachangii kitu kwa ajili ya mwangaza au haki. Hata kama mwanadamu anajitahidi sana kwa muda, ni dhaifu sana kiasi cha kutoweza kustahimili dhoruba hata kidogo, kwani jitihada za mwanadamu siku zote ni kwa ajili yake mwenyewe na wala si kwa ajili ya wengine. Mwanadamu siku zote ni mbinafsi, huku naye Mungu siku zote si mwenye ubinafsi. Mungu ndiye chanzo cha vyote vilivyo vya haki, vyema, na vya uzuri, huku naye mwanadamu ni yule anayerithi na kudhihirisha vyote vyenye sura mbaya na vyenye maovu. Mungu hatawahi kubadilisha dutu Yake ya haki na uzuri, ilhali mwanadamu anaweza kabisa, wakati wowote, kusaliti haki na kupotoka kutoka kwa Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu

Tanbihi:

a. Maandishi asilia yanasema “ni ishara ya kutoweza.”

b. Maandishi asilia yanasema “na vilevile ishara ya kutoweza kukosewa kuwa (na kutovumilia kukosewa).”

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 246)

Kila sentensi Niliyoizungumza ina tabia ya Mungu ndani yake. Mngefanya vizuri endapo mngetafakari kuhusu maneno Yangu kwa umakini, na kwa kweli mtafaidi pakubwa kutoka kwa maneno hayo. Dutu ya Mungu ni ngumu sana kuelewa, lakini Ninaamini kwamba nyinyi nyote mnayo angalau mawazo fulani kuhusu tabia ya Mungu. Ninatumai, basi, kwamba mtanionyesha Mimi na kufanya mengi zaidi ya yale ambayo hayakosei tabia ya Mungu. Kisha Nitatulizwa moyo. Kwa mfano, mweke Mungu katika moyo wako siku zote. Unapochukua hatua, fanya hivyo kulingana na maneno Yake. Tafuta nia Zake katika kila kitu, na usifanye kile ambacho kitavunjia heshima na kumdhalilisha Mungu. Hata zaidi usimweke Mungu nyuma ya akili zako ili ukajaze uwazi wa baadaye katika moyo wako. Ukifanya hivyo, basi utakuwa umekosea tabia ya Mungu. Tena, tuchukulie kwamba kamwe hutamki matamshi ya kukufuru au kulalamika dhidi ya Mungu maisha yako yote, na tena, tuchukulie kwamba unaweza kufanya kikamilifu kila kitu ambacho amekuaminia wewe na pia kutii maneno Yake yote katika maisha yako yote, basi utakuwa umeweza kuepuka kwa kukosea amri za utawala. Kwa mfano, kama umewahi kusema “Kwa nini sifikirii kwamba Yeye ni Mungu?” “Nafikiri kwamba maneno haya ni nuru kiasi ya Roho Mtakatifu tu,” “Katika maoni yangu, si kila kitu ambacho Mungu anakifanya lazima ni sahihi,” “Ubinadamu wa Mungu hauna ukubwa zaidi kuliko wangu,” “Maneno ya Mungu hayaiaminiki kabisa,” au matamshi mengine kama hayo ya kuhukumu, basi Nakusihi wewe kukiri na kutubu dhambi zako mara nyingi zaidi. Vinginevyo, hutawahi kuwa na fursa ya msamaha, kwani hukosei mwanadamu, ila Mungu Mwenyewe. Unaweza kuamini kwamba wewe unamhukumu mtu tu, lakini Roho wa Mungu haichukulii hivyo. Wewe kutoheshimu mwili Wake ni sawa na kumvunjia Yeye heshima. Kama hali ni hivi, basi si ni kweli kwamba umekosea tabia ya Mungu? Lazima ukumbuke kwamba kila kitu kinachofanywa na Roho wa Mungu kinafanywa ili kukinga kazi Yake katika mwili na ili kazi hii ifanywe vizuri. Ukiyapuuza haya, basi Nasema kwamba wewe ni mtu ambaye kamwe hataweza kufaulu katika kumwamini Mungu. Kwani umechochea hasira ya Mungu, kwa hivyo Atatumia adhabu inayofaa ili kukufunza adabu.

Kupata kujua dutu ya Mungu si jambo dogo. Lazima uelewe tabia Yake. Katika njia hii, polepole na bila kujua, utaanza kujua dutu ya Mungu. Wakati umeingia katika maarifa haya, utajipata ukisonga mbele hadi kwa hali iliyo ya juu na ya kupendeza zaidi. Hatimaye, utaaibika kutokana na nafsi yako ya kuchukiza, kiasi kwamba unahisi hakuna mahali pa kujificha. Wakati huo, kutakuwa na machache zaidi na zaidi katika mwenendo wako ya kukosea tabia ya Mungu, moyo wako utakuwa karibu zaidi na zaidi na ule wa Mungu, na polepole upendo wako Kwake utakua ndani ya moyo wako. Hii ni ishara ya wanadamu kuingia katika hali nzuri. Lakini kufikia sasa bado hamjapata hili. Mnaposhughulika huku na kule kwa ajili ya majaaliwa yenu, ni nani angefikiria kujaribu kujua dutu ya Mungu? Kama hali hii itaendelea, nyinyi mtazikosea amri za utawala bila kujua, kwani mnafahamu kidogo sana kuhusu tabia ya Mungu. Kwa hivyo, kile mfanyacho sasa hakiweki msingi wa makosa yenu dhidi ya tabia ya Mungu? Kwamba Ninawaomba muelewe tabia ya Mungu haipingani na kazi Yangu. Kwani mkikosea amri za utawala mara nyingi, basi ni nani kati yenu anayeweza kutoroka adhabu? Je, basi kazi Yangu haingekuwa bure kabisa? Kwa hivyo, Ningali Naomba kwamba, pamoja na kuchunguza mienendo yenu binafsi, muwe waangalifu zaidi na hatua mnazochukua. Haya ndiyo yatakuwa mahitaji ya juu zaidi nitakayowaomba, na Ninatumai kwamba nyote mtayafikiria kwa umakini na kuyaona kuwa muhimu kabisa. Endapo siku ifike ambapo matendo yenu yatanichochea Mimi hadi kuwa katika hali iliyojaa hasira, basi matokeo yatakuwa yenu pekee kufikiria, na hakutakuwa na mwingine yeyote atakayevumilia adhabu hiyo kwa niaba yenu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 247)

Watu husema Mungu ni Mungu wa haki, na kwamba mradi tu mwanadamu atamfuata mpaka mwisho, basi Hatakuwa na upendeleo kwa mwanadamu, kwani Yeye ni mwenye haki. Je, mwanadamu akimfuata mpaka mwisho kabisa, Mungu anaweza kumtupa mwanadamu nje? Sina upendeleo kwa mwanadamu yeyote, na Huwahukumu wanadamu wote kwa tabia Yangu ya haki, ilhali kuna mahitaji yanayofaa Ninayohitaji kutoka kwa mwanadamu, na Ninahitaji yakamilishwe na wanadamu wote, bila kujali ni nani. Sijali kiwango cha kufuzu kwako au kuheshimiwa kwako; najali tu kama utatembea kwa njia Yangu, na kama unapenda na una kiu ya ukweli. Kama huna ukweli, na unaleta aibu katika jina Langu, na matendo yako ni kinyume cha njia Yangu, kufuata tu bila kujali, basi wakati huo nitakupiga na kukuadhibu kwa uovu wako, na utakuwa na nini la kusema? Utaweza kusema Mungu si mwenye haki? Leo kama umezingatia maneno ambayo nimenena, basi wewe ni mtu ambaye Namkubali. Unasema umeumia ukifuata Mungu, kwamba umemfuata kwa marefu na mapana, na umeshiriki na yeye katika wakati mzuri na mbaya, lakini hujaishi kulingana na maneno yaliyosemwa na Mungu; unataka tu kukimbia huku na kule kwa ajili ya Mungu na kujitumia kwa ajili ya Mungu kila siku, na hujafikiria kuishi kwa kudhihirisha maisha yenye maana. Unasema pia, “Kwa vyovyote, naamini Mungu ni mwenye haki. Nimeteseka kwa ajili Yake, nikashughulika kwa ajili Yake, kujitoa kikamilifu Kwake, na nimefanya bidii ingawa sijapata kutambuliwa; Yeye hakika atanikumbuka.” Ni ukweli kwamba Mungu ni mwenye haki, na haki hii haijatiwa doa na uchafu wowote: Haina mapenzi ya binadamu, na haijatiwa doa na mwili, ama kitendo chochote cha binadamu. Wale wote ambao ni waasi na wako kwa upinzani, na hawazingatii njia Zake wataadhibiwa; hakuna atakayesamehewa, na hakuna atakayeepuka! Watu wengine husema, “Leo nakimbia juu yako; mwisho ukifika, utanipa baraka kidogo?” Sasa Nakuuliza, “Umezingatia maneno Yangu?” Haki unayoongelea inategemea matendo. Unafikiria kwamba Mimi ni mwenye haki, na asiye na mapendeleo kwa binadamu wote, na kwamba wale wanifuatao hadi mwisho wataokolewa na kupata baraka Yangu. Kuna maana ya ndani kwa maneno Yangu kwamba “wale wote wanifuatao hadi mwisho wataokolewa”: Wale wanifuatao mpaka mwisho ndio Nitakaowapata, ni wale, baada ya kushindwa Nami, watautafuta ukweli na kufanywa wakamilifu. Ni hali gani umepata? Umepata kunifuata hadi mwisho, lakini nini kingine? Je, umezingatia maneno Yangu? Umekamilisha moja kati ya tano ya mahitaji Yangu, ilhali huna mpango wa kumaliza manne yaliyobaki. Umepata ile njia rahisi, na ukafuata ukifikiria umebahatika. Kwa mtu kama wewe, haki Yangu ni adabu na hukumu, ni adhabu ya haki, na ni adhabu ya haki kwa watenda maovu wote; wale wote wasiotembea kwa njia Yangu wataadhibiwa, hata kama watafuata mpaka mwisho. Hii ndio haki ya Mungu. Wakati tabia hii ya haki inapodhihirishwa katika adhabu ya mwanadamu, mwanadamu atakosa la kusema, na kujuta kwamba, alipokuwa akimfuata Mungu hakutembea katika njia Yake. “Wakati huo niliteseka kidogo tu nikimfuata Mungu, lakini sikutembea katika njia ya Mungu. Kuna udhuru gani? Hakuna namna ila kuadibiwa!” Ila kwa akili yake anafikiria, “Nimefuata hadi mwisho, hata Ukiniadibu haitakuwa adabu kali, na baada ya kuadibu kwa kuchosha, bado Utanihitaji. Najua Wewe ni mwenye haki, na Hutanifanyia hivyo milele. Mimi si kama wale watakaofagiliwa nje; wale watakaofagiliwa watapokea adabu kuu, na adabu Yangu itakuwa kidogo.” Adabu ya Mungu ya tabia ya haki si unavyosema. Sio kwamba wale ambao wanatubu dhambi zao kila wakati wataadibiwa kwa huruma. Haki ni utakatifu, na ni tabia ambayo haivumilii makosa ya mwanadamu, na yale yote ambayo ni machafu na hayajabadilika ndiyo shabaha ya chukizo kwa Mungu. Haki ya Mungu si sheria, lakini amri ya utawala: Ni amri ya utawala katika ufalme, na hii amri ya utawala ni adhabu ya haki kwa yeyote asiye na ukweli na hajabadilika, na hakuna kiwango cha wokovu. Mwanadamu akiwekwa kulingana na aina, wazuri watazawadiwa na wabaya kuadhibiwa. Ndio wakati hatima ya mwanadamu itawekwa wazi, na ndio ni wakati ambao kazi ya wokovu itafika mwisho, baada ya hapo, kazi ya kuokoa binadamu haitafanyika tena, na adabu italetwa kwa wale waliotenda maovu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 248)

Mimi ni moto uteketezao na Sivumilii kosa. Kwa sababu wanadamu wote waliumbwa na Mimi, chochote Nisemacho na kufanya, watu lazima watii na hawawezi kukiasi. Watu hawana haki ya kuingilia kazi Yangu, na wao hasa siyo wenye sifa zinazostahili kuchambua kilicho cha kweli au chenye makosa katika kazi Yangu na maneno Yangu. Mimi ni Bwana wa uumbaji, na viumbe wanapaswa kutimiza kila kitu Ninachohitaji kwa moyo wa kunicha Mimi; hawapaswi kutoa sababu ili kunishawishi Mimi na wao hasa hawapaswi kunipinga. Ninatumia mamlaka Yangu kuwatawala watu Wangu, na wale wote ambao ni sehemu ya uumbaji Wangu wanapaswa kuyatii mamlaka Yangu. Ingawa leo ninyi ni, jasiri na wenye kiburi mbele Yangu, ninyi hukaidi maneno ambayo Nawafunzia, na hamwogopi, Mimi hukumbana tu na uasi wenu na uvumilivu. Singekasirika na kuathiri kazi Yangu kwa sababu mabuu wadogo sana walipindua uchafu katika rundo la samadi. Mimi huvumilia kuendelea kuwepo kwa kila kitu ambacho Mimi huchukia kabisa na mambo ambayo Mimi huchukia kabisa kwa ajili ya mapenzi ya Baba Yangu, mpaka matamshi Yangu yawe kamili, mpaka dakika Yangu ya mwisho kabisa. Usijali! Siwezi kuzama katika kiwango sawa na buu asiyefaa kutajwa, na Sitafananisha kiwango cha ujuzi na wewe. Nakuchukia kabisa, ilhali Naweza kuvumilia. Wewe hunikaidi Mimi, ilhali huwezi kuepuka siku ya Mimi kukuadibu ambayo Baba Yangu ameniahidi Mimi. Je, buu aliyeumbwa anaweza kufananishwa na Bwana wa uumbaji wote? Katika majira ya kupukutika kwa majani, majani yaangukayo hurudi kwa mizizi yake, wewe hurudi kwa nyumba ya “baba” yako, na Mimi hurudi ubavuni pa Baba Yangu. Mimi huandamana na upendo mwema wa Baba Yangu, na wewe hufuatwa na kuvyogwa kwa baba Yako. Nina utukufu wa Baba Yangu, na wewe una aibu ya baba yako. Mimi hutumia kuadibu ambako Nimeshikilia kwa muda mrefu kuandamana na wewe, na wewe hukutana na kuadibu Kwangu na mwili wako uliooza ambao tayari umekuwa mpotovu kwa makumi ya maelfu ya miaka. Nimehitimisha kazi Yangu ya maneno ndani yako, ikiandamana na uvumilivu, na umeanza kutimiza wajibu wa kupitia msiba kutoka kwa maneno Yangu. Mimi hufurahia sana na kufanya kazi katika Israeli; wewe hulia na kusaga meno yako na huishi na kufa matopeni. Nimepata tena umbo Langu la asili na Sibaki tena ndani ya uchafu na wewe, huku umepata tena ubaya wako wa asili na bado unafukua kila mahali katika lundo la samadi. Wakati ambapo kazi na maneno Yangu yatakamilika, itakuwa siku ya furaha Kwangu. Wakati ambapo upinzani na uasi wako utakwisha, itakuwa siku ya kulia kwako machozi. Sitakuonea huruma, na hutaniona Mimi tena. Sitakuwa tena na mazungumzo na wewe, na hutakutana na Mimi tena. Nitachukia uasi wako, na utakosa kupendeza Kwangu. Nitakupiga wewe, na utanikosa Mimi. Nitaondoka kwako kwa furaha, na utafahamu deni lako Kwangu. Sitakuona wewe tena, lakini wewe kila mara utanitarajia Mimi. Nitakuchukia kwa sababu unanipinga Mimi sasa, na utanikosa Mimi; kwa sababu Nakuadibu sasa. Siko radhi kuishi ubavuni pako, lakini utalitamani sana kwa uchungu na kulia machozi katika milele, kwa sababu utajuta kila kitu ambacho umenifanyia Mimi. Utajuta uasi wako na upinzani wako, na hata utaulaza uso wako juu ya ardhi kutokana na kujuta, na utaanguka chini mbele Yangu na kuapa kutonikaidi Mimi tena. Lakini ndani ya moyo wako wewe hunipenda Mimi tu na hutaweza kamwe kuisikia sauti Yangu, lazima Nikufanye ujionee haya.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Majani Yaangukayo Yatakaporudi kwa Mizizi Yake, Utajuta Maovu Yote Ambayo Umefanya

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 249)

Huruma Yangu inaonyeshwa kwa wale wanaonipenda Mimi na kujinyima. Kwa sasa, adhabu itakayowapata waovu, ni thibitisho hasa la tabia Yangu ya haki na, hata zaidi, ushuhuda wa hasira Yangu. Msiba utakapofika, wote wanaonipinga watalia watakapokumbwa na njaa na baa. Wale ambao wametenda aina zote za uovu, lakini ambao wamenifuata kwa miaka mingi, hawataepuka kulipia dhambi zao; wao pia, watatumbukia katika maafa, ambayo yameonekana kwa nadra kotekote katika mamilioni ya miaka, na wataishi katika hali ya taharuki na woga daima. Na wale kati ya wafuasi Wangu ambao wamekuwa waaminifu Kwangu watafurahi na kushangilia ukuu Wangu. Watakuwa na ridhaa isiyo na kifani na kuishi kwa raha ambayo Sijawahi kuwapa wanadamu. Kwa sababu Ninathamini matendo mema ya mwanadamu na kuchukia matendo yake maovu. Tangu Nilipoanza kuwaongoza wanadamu, Nimekuwa Nikitamani kwa hamu kupata kikundi cha watu ambao wanafikiria kama Mimi. Wale ambao hawana fikira sawa na Zangu, wakati ule ule, Siwasahau kamwe; Ninawachukia kabisa moyoni Mwangu daima, Nikisubiri nafasi ya kutoa adhabu kwao, jambo ambalo Nitafurahia kuona. Sasa siku Yangu imefika hatimaye, na Sihitaji kusubiri zaidi!

Kazi Yangu ya mwisho si kwa ajili ya kumwadhibu mwanadamu tu bali pia kwa ajili ya kupanga hatima ya mwanadamu. Aidha, ni kwa ajili ya kupokea shukrani kutoka kwa kila mtu kwa yale yote ambayo Nimefanya. Ninataka kila mtu aone kwamba yale yote ambayo Nimefanya ni sahihi na kwamba yote ambayo Nimefanya ni dhihirisho la tabia Yangu; si kwa uwezo wa mwanadamu, sembuse ulimwengu, ambao uliwaleta wanadamu. Kinyume na hili, mimi Ndiye Ninalisha kila kiumbe miongoni mwa vitu vyote. Bila uwepo Wangu, wanadamu wataangamia tu na kusumbuka kutokana na mashambulizi ya misiba. Hamna mwanadamu atakayeona uzuri wa jua na mwezi au dunia ya kijani kibichi; wanadamu watakumbana tu na usiku wenye baridi na bonde kali la uvuli wa mauti. Mimi tu Ndiye wokovu wa wanadamu. Mimi tu ndiye tumaini la wanadamu na zaidi ya hayo; Mimi tu Ndiye mwamba wa uwepo wa wanadamu wote. Bila Mimi, wanadamu watasimama kabisa mara moja. Bila mimi, wanadamu watakumbana na msiba mkuu na kukanyagwa na mapepo wa aina yote, hata kama hamna anayenisikiliza. Nimefanya kazi ambayo haiwezi kufanywa na yeyote yule ila mimi. tumaini Langu la pekee ni kwamba mwanadamu anaweza kunilipa kwa kutenda matendo kiasi mema. Ingawa wanaoweza kunilipa ni wachache, bado Nitahitimisha safari Yangu duniani na Nianze hatua ifuatayo ya kazi Yangu inayotokea, kwa sababu kukimbia kimbia Kwangu miongoni mwa wanadamu kwa miaka hii mingi imekuwa na matokeo mazuri, na Nimefurahishwa sana. Sijali kuhusu idadi ya watu ila kuhusu matendo yao mazuri. Kwa hali yoyote ile, Ninatumaini kwamba mtatayarisha matendo mema ya kutosha kwa ajili ya hatima yenu wenyewe. Huo ndio wakati Nitakaporidhika; la sivyo, hakuna yeyote miongoni mwenu atakayepuka maafa yatakayowafikia. Maafa haya hutoka Kwangu na bila shaka Mimi ndiye Niliyeyapanga. Ikiwa hamwezi kuonekana kuwa wema mbele Yangu, basi hamtaweza kuyaepuka maafa. Wakati wa majonzi, vitendo vyenu havikuchukuliwa kama vinavyofaa kabisa, kwa sababu imani na upendo wenu vilikuwa tupu, na mlijionyesha tu kuwa wenye woga au sugu. Kuhusu hili, Nitafanya hukumu ya mazuri au mabaya tu. Shaka Yangu inaendelea kuwa jinsi kila mmoja wenu hutenda na kujionyesha, kwa msingi ambao Nitatumia kufanya uamuzi kuhusu hatima yenu. Hata hivyo, ni sharti Niseme wazi kwamba: Sitawahurumia tena wale ambao hawakuwa waaminifu Kwangu kabisa wakati wa majonzi, kwa sababu huruma Yangu ina mipaka. Zaidi ya hayo, Simpendi yeyote yule ambaye amewahi kunisaliti Mimi, wala Sipendi kujihusisha na wale ambao hawawajali wenzao. Bila kujali huyo mtu ni nani, hii ndiyo tabia Yangu. Ni lazima Niwaambie hili: Yeyote atakayeuhuzunisha moyo Wangu hatapokea huruma kutoka Kwangu mara ya pili, na yeyote ambaye amekuwa mwaminifu Kwangu atadumu moyoni Mwangu milele.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 250)

Mungu alipokuja duniani Yeye hakuwa wa ulimwengu na Yeye hakuwa mwili ili apate kuufurahia ulimwengu. Mahali ambapo kufanya kazi kungefichua tabia Yake vizuri sana na pawe mahali pa maana zaidi ni mahali Alipozaliwa. Kama ni nchi takatifu au yenye uchafu, na bila kujali Anapofanya kazi, Yeye ni mtakatifu. Kila kitu duniani kiliumbwa na Yeye; Ni kwamba tu kila kitu kimepotoshwa na Shetani. Hata hivyo, vitu vyote bado ni Vyake; vyote viko mikononi Mwake. Kuja Kwake katika nchi yenye uchafu kufanya kazi ni kufichua utakatifu Wake; Yeye hufanya hivi kwa ajili ya kazi Yake, yaani, Yeye huvumilia aibu kubwa kufanya kazi kwa njia hii ili kuwaokoa watu wa nchi hii yenye uchafu. Hii ni kwa ajili ya ushuhuda na ni kwa ajili ya wanadamu wote. Kile aina hii ya kazi inawaruhusu watu kuona ni haki ya Mungu, na ina uwezo zaidi wa kuonyesha mamlaka ya juu kabisa ya Mungu. Ukuu na uadilifu Wake vinaonyeshwa kupitia wokovu wa kundi la watu wa hali ya chini ambao hakuna mtu anayewapenda. Kuzaliwa katika nchi yenye uchafu haimaanishi kabisa kuwa Yeye ni duni; inawaruhusu tu viumbe vyote kuuona utuu Wake na upendo wake wa kweli kwa wanadamu. Zaidi Anavyofanya kwa njia hii, zaidi inavyofichua upendo Wake safi zaidi kwa mwanadamu, upendo wake usio na dosari. Mungu ni mtakatifu na mwenye haki. Hata ingawa Alizaliwa katika nchi yenye uchafu, na ingawa Anaishi na watu hao ambao wamejawa uchafu, kama vile Yesu alivyoishi na wenye dhambi katika Enzi ya Neema, si kazi Yake yote kwa ajili ya kuishi kwa wanadamu wote? Je, si yote ni ili mwanadamu aweze kuupata wokovu mkuu? Miaka elfu mbili iliyopita Aliishi na wenye dhambi kwa miaka kadhaa. Hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya ukombozi. Leo, Anaishi na kikundi cha watu wachafu, wa hali ya chini. Hii ni kwa ajili ya wokovu. Je, si kazi Yake yote ni kwa ajili yenu, wanadamu hawa? Kama haingekuwa ili kuwaokoa wanadamu, kwa nini Angeishi na kuteswa pamoja na wenye dhambi kwa miaka mingi sana baada ya kuzaliwa horini? Na kama haingekuwa ili kuwaokoa wanadamu, kwa nini Angeurudia mwili kwa mara ya pili, kuzaliwa katika nchi hii ambako mapepo hukusanyika, na kuishi na watu hawa ambao wamepotoshwa kwa kina na Shetani? Je, si Mungu ni mwaminifu? Ni aina gani ya kazi Yake ambayo haijakuwa kwa ajili ya wanadamu? Ni aina gani ambayo haijakuwa kwa ajili ya kudura yako? Mungu ni mtakatifu. Hili haliwezi kubadilika! Yeye hanajisiwi na uchafu, ingawa Amekuja katika nchi yenye uchafu; yote haya yanamaanisha tu kwamba upendo wa Mungu kwa wanadamu ni wenye kuwajali wengine sana, mateso na aibu Anayoyavumilia ni makubwa sana! Hamjui kwamba Yeye hupitia aibu kubwa sana kwa ajili yenu wote na kwa ajili ya kudura yenu? Je, hamjui hivyo? Yeye hawaokoi watu wakuu au wana wa familia tajiri na zenye uwezo, lakini Yeye huwaokoa hasa wale ambao ni wa hali za chini na wanaodharauliwa na wengine. Je, si haya yote ni utakatifu Wake? Je, si haya yote ni haki Yake? Afadhali Azaliwe katika nchi yenye uchafu na kuteseka aibu yote kwa ajili ya kuishi kwa wanadamu wote. Mungu ni halisi sana—Hafanyi kazi ya uwongo. Je, si kila hatua ya kazi Yake imefanyika kwa utendaji hivi? Ingawa watu wote wanamkashifu na kusema kuwa Anakaa mezani pamoja na wenye dhambi, ingawa watu wote wanamdhihaki na kusema kuwa Anaishi na wana wa uchafu, na watu wa hali ya chini sana, bado Anajitolea bila ubinafsi, na bado Anakataliwa kwa njia hii kati ya wanadamu. Je, si mateso Anayoyahimili ni makubwa zaidi kuliko yenu? Je, si kazi Yake ni zaidi ya gharama ambayo mmelipa?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Umuhimu wa Kuukoa Uzao wa Moabu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 251)

Mungu amejinyenyekeza Mwenyewe kwa kiwango fulani, kufanya kazi Yake katika watu hawa wachafu na wapotovu, na kukikamilisha kikundi hiki cha watu. Mungu hakupata mwili tu ili kuishi na kula kati ya watu, kuwalisha watu, kutoa wanachohitaji watu. Jambo muhimu zaidi ni kwamba Yeye hufanya kazi Yake kubwa ya wokovu na ushindi kwa watu hawa walio na upotovu usiovumilika. Alikuja katika kiini cha joka kubwa jekundu ili kuwaokoa watu hawa wapotovu mno, ili watu wote waweze kubadilishwa na kufanywa wapya. Tatizo kubwa ambalo Mungu huvumilia siyo tu shida ambayo Mungu mwenye mwili huvumilia, lakini hasa ni kwamba Roho wa Mungu hupitia udhalilishaji uliokithiri—Yeye hujinyenyekeza na kujificha Mwenyewe sana kiasi kwamba Yeye huwa mtu wa kawaida. Mungu alipata mwili na kuchukua mfano wa mwili ili watu waone kwamba Ana maisha ya kawaida ya binadamu, na kwamba ana mahitaji ya kawaida ya binadamu. Hili linatosha kuthibitisha kwamba Mungu amejinyenyekeza Mwenyewe kwa kiwango fulani. Roho wa Mungu hufanyika katika mwili. Roho Wake ni wa juu sana na mkuu, lakini Yeye huchukua mfano wa mwanadamu wa kawaida, wa mwanadamu asiye muhimu ili kufanya kazi ya Roho Wake. Ubora wa tabia, umaizi, hisi, ubinadamu, na maisha ya kila mmoja wenu vinaonyesha kwamba hamfai kweli kupokea kazi ya Mungu ya aina hii. Hakika hamfai kumruhusu Mungu kuvumilia shida kama hiyo kwa ajili yenu. Mungu ni mkubwa sana. Yeye ni mkuu sana, na watu ni duni sana na wa hali ya chini, lakini Yeye bado huwafanyia kazi. Yeye hakupata mwili tu ili kuwaruzuku watu, kuzungumza na watu, Yeye hata huishi pamoja na watu. Mungu ni mnyenyekevu sana, wa hupendeka sana.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Wale Wanaolenga Kutenda tu Ndio Wanaoweza Kukamilishwa

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 252)

Mungu amevumilia sana kulala bila kupata usingizi kwa ajili ya kazi ya binadamu. Kutoka vina vya juu hadi vya chini, Amepanda kwenda katika kuzimu ambapo mwanadamu anaishi kupitisha siku Zake na mwanadamu, hajawahi kulalamikia uchakavu walionao wanadamu, hajawahi kumlaumu kwa ukaidi wake, lakini Anavumilia mateso makuu kadri Anavyofanya kazi Yake. Inawezekanaje Mungu awe wa kuzimu? Inawezekanaje Aishi maisha Yake kuzimu? Lakini kwa ajili ya binadamu wote, ili binadamu wote waweze kupata pumziko mapema zaidi, Amestahimili fedheha na kupitia udhalimu kuja duniani, na Aliingia mwenyewe “jahanamu” na “kuzimu,” katika tundu la duma, kumwokoa mwanadamu. Mwanadamu amestahili vipi kumpinga Mungu? Ana sababu gani tena ya kumlaumu Mungu? Anawezaje kuwa na ujasiri wa kumwangalia Mungu tena? Mungu wa mbinguni Amekuja katika nchi hii chafu zaidi ya uovu, na Hajawahi kutangaza manung’uniko au malalamiko Yake kuhusu mwanadamu, lakini badala yake Anakubali kimyakimya maangamizi[1] na ukandamizaji wa mwanadamu. Kamwe Hajawahi kujibu matakwa ya mwanadamu yasiyokuwa na msingi, hajawahi kutaka mambo mengi yanayomuelemea mwanadamu, na hajawahi kumwekea mwanadamu matakwa yasiyokuwa na msingi; Anafanya tu kazi ambazo mwanadamu alitakiwa kufanya bila malalamiko: kufundisha, kutia mwanga, kukaripia, usafishaji wa maneno, kukumbusha, kusihi, kufariji, kuhukumu na kufunua. Ni hatua gani Alizozichukua ambazo si kwa ajili ya maisha ya mwanadamu? Ingawa Ameondoa matarajio na majaliwa ya mwanadamu, ni hatua zipi zilizochukuliwa na Mungu ambazo hazikuwa kwa ajili ya majaliwa ya mwanadamu? Ni ipi kati ya hatua hizo ambayo haijawahi kuwa kwa ajili ya mwanadamu kuendelea kuishi? Ni ipi kati ya hatua hizo haijakuwepo kwa ajili ya kumweka mwanadamu huru dhidi ya mateso haya na kunyanyaswa na nguvu za giza ambazo ni nyeusi kama usiku? Ni ipi kati ya hatua hizo si kwa ajili ya mwanadamu? Ni nani awezaye kuujua moyo wa Mungu, ambao ni sawa na mama mwenye mapenzi? Ni nani awezaye kuujua moyo wa Mungu wenye shauku? Moyo wa upendo na matarajio ya shauku ya Mungu vimelipwa kwa mioyo ya baridi, na usugu, na macho yanayoonyesha kutojali, kwa makaripio ya kujirudia na matusi ya mwanadamu, kwa maneno ya mkato na dhihaka na udhalilishaji, vimelipwa kwa dhihaka ya mwanadamu, kwa kukanyagwa na kukataliwa, kwa kutokuwa na ufahamu, na kupiga kite, na farakano, na uepukaji, kwa uongo, mashambulizi na ukali. Maneno ya wema ya Mungu yamekutana na nyuso kali na ufidhuli wa vidole elfu moja vinavyotikisika. Mungu anaweza tu kustahimili, Akiwa Ameinamisha kichwa, Akiwahudumia watu kama ng’ombe aliye radhi kufungwa.[2] Miezi na jua nyingi sana, Amekabiliana na nyota mara nyingi sana, Ameondoka alfajiri na kurudi jioni mara nyingi sana, na kurushwarushwa na kugeuzwa, Akivumilia maumivu makubwa mara elfu moja kuliko maumivu Aliyoyapata Alipokuwa Anaondoka kwa Baba Yake, Akivumilia mashambulizi na “kuvunja” kwa mwanadamu, na “kumshughulikia” na “kumpogoa” mwanadamu. Unyenyekevu na kufichika kwa Mungu vimelipwa kwa upendeleo[3] wa mwanadamu, kwa mitazamo na vitendo vya mwanadamu visivyokuwa vya haki, na kutojulikana Kwake, ustahimilivu, na uvumilivu vimelipizwa kwa jicho la tamaa la mwanadamu, mwanadamu hujaribu kumkanyaga Mungu hadi afe, bila majuto, na anajaribu kumkanyagia Mungu ardhini. Mtazamo wa mwanadamu kwa namna anavyomtendea Mungu ni wa “ujanja adimu,” na Mungu ambaye Anachokozwa na kutwezwa na mwanadamu, Anakanyagwa na kuwa bapa kwa miguu ya makumi elfu ya watu wakati mwanadamu mwenyewe anasimama juu kabisa, kana kwamba angeweza kuwa “mfalme wa kasri,” kana kwamba anataka kuchukua mamlaka kamili,[4] “kuendesha mahakama akiwa nyuma ya skrini,” kumfanya Mungu kuwa makini na mwenye kanuni “mwongozaji nyuma ya matukio,” ambaye haruhusiwi kupigana au kusababisha shida; lazima Mungu achukue nafasi ya “Mtawala wa Mwisho,” ni lazima Awe “kibaraka,”[5] bila uhuru wote. Matendo ya mwanadamu hayasemeki, sasa ana sifa gani ya kutaka hili au lile kuhusu Mungu? Ana sifa gani ya kutoa mapendekezo kwa Mungu? Anafaa kwa kiasi gani kumtaka Mungu amhurumie juu ya udhaifu wake? Anafaa kwa kiasi gani kupokea huruma ya Mungu? Anafaa kwa kiasi gani kupokea ukarimu wa Mungu kila mara? Anafaa kwa kiasi gani kupokea msamaha wa Mungu kila mara? Dhamiri yake ipo wapi? Alivunja moyo wa Mungu muda mrefu uliopita, ni muda mrefu toka ameuacha moyo wa Mungu katika vipande. Mungu alikuja miongoni mwa wanadamu Akiwa na nguvu nyingi na mwenye shauku kubwa, Akitegemea kwamba mwanadamu atakuwa mkarimu Kwake, hata kama ni kwa wema kiasi kidogo tu. Bado moyo wa Mungu haujafarijiwa na mwanadamu, yote Aliyoyapokea ni mashambulizi na mateso ya kuongezeka haraka;[6] moyo wa mwanadamu ni wenye tamaa sana, tamaa yake ni kubwa sana, hawezi akatosheka, siku zote ni mwenye fitina na jasiri pasi busara, hawezi kamwe kumpatia Mungu uhuru au haki ya kuzungumza, na anamwacha Mungu bila budi ila kukubali unyanyasaji, na kumruhusu mwanadamu kumtawala vyovyote apendavyo.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (9)

Tanbihi:

1. “Maangamizi” inatumiwa kuweka wazi kutotii kwa wanadamu.

2. “Anaweza tu kustahimili, Akiwa Ameinamisha kichwa, Akiwahudumia watu kama ng’ombe aliye radhi kufungwa” ni kwa asili sentensi moja, lakini hapa imegawanywa mara mbili ili kuyafanya mambo wazi zaidi. Sentensi ya kwanza inahusu matendo ya mwanadamu, huku ya pili inaonyesha mateso aliyoyapitia Mungu, na kwamba Mungu ni mnyenyekevu na Aliyefichika.

3. “Upendeleo” unahusu tabia ya watu ya ukaidi.

4. “Kuchukua mamlaka kamili” inahusu tabia ya watu ya ukaidi. Wanajitukuza, huwafunga wengine, wakiwafanya wawafuate na kuteseka kwa ajili yao. Wao ni majeshi ambayo ni ya uadui kwa Mungu.

5. “Kibaraka” inatumiwa kuwadhihaki wale ambao hawamjui Mungu.

6. “Kuongezeka haraka” inatumiwa kuonyesha tabia duni ya watu.

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 253)

Kila kitu ambacho Mungu hufanya ni cha vitendo, na hakuna Anachofanya ambacho ni kitupu. Mungu huja kati ya wanadamu, Akijinyenyekeza kuwa mtu wa kawaida. Haondoki baada ya kufanya tu kazi kidogo na kunena maneno machache; badala yake, kwa kweli Yeye huja kati ya wanadamu ili kupitia mateso ya ulimwengu. Analipa gharama ya uzoefu Wake mwenyewe wa kuteseka ili kulipia hatima ya wanadamu. Je, si hii ni kazi ya vitendo? Wazazi wanaweza kulipa gharama ya dhati kwa ajili ya watoto wao, na hii inawakilisha uaminifu wao. Kwa kufanya hivi, Mungu mwenye mwili bila shaka anakuwa mnyoofu na mwaminifu kabisa kwa wanadamu. Kiini cha Mungu ni uaminifu; Yeye hufanya Anachosema, na chochote Afanyacho hutimizwa. Kila kitu Anachowafanyia wanadamu ni cha kweli. Yeye haneni tu maneno; Anaposema kuwa atalipa gharama, Yeye kwa kweli hulipa gharama. Anaposema kwamba Atapitia mateso ya wanadamu na kuteseka badala yao, kwa kweli Yeye huja kuishi kati yao, Akihisi na kupitia mateso haya Yeye binafsi. Baada ya hapo, vitu vyote ulimwenguni vitakiri kuwa kila kitu ambacho Mungu hufanya ni sahihi na chenye haki, kwamba vyote ambavyo Mungu hufanya ni halisi: Hiki ni kipande cha ushahidi chenye nguvu. Wanadamu watakuwa na hatima nzuri katika siku zijazo, na wale wote watakaobaki watamsifu Mungu; watasifu sana kwamba matendo ya Mungu kweli yalifanywa kutokana na upendo Wake kwa wanadamu.

Asili ya Mungu ya uzuri na wema inaweza kuonekana katika umuhimu wa kupata mwili Kwake. Lolote Afanyalo ni la kweli; lolote Asemalo ni la dhati na halisi. Vitu vyote Anavyokusudia kuvifanya hufanywa kwa vitendo, na Yeye huvilipia gharama halisi; Yeye haneni tu maneno. Kwa hiyo, Mungu ni Mungu mwenye haki; Mungu ni Mungu mwaminifu.

Kimetoholewa kutoka katika “Kipengele cha Pili cha Umuhimu wa Kupata Mwili” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 254)

Njia ya maisha si kitu ambacho mtu yeyote anaweza kumiliki, wala si kitu ambacho mtu yeyote anaweza kufikia kwa urahisi. Hii ni kwa sababu maisha yanaweza kuja tu kutoka kwa Mungu, ambayo ni kusema, Mungu Mwenyewe tu ndiye Anamiliki mali ya maisha, hakuna njia ya maisha bila Mungu Mwenyewe, na hivyo Mungu tu ndiye chanzo cha uzima, na kijito cha maji ya uzima kinachotiririka nyakati zote. Kutoka Alipoumba dunia, Mungu amefanya kazi kubwa inayoshirikisha uhai wa maisha, Amefanya kazi kubwa ambayo huletea mwanadamu maisha, na Amelipa gharama kubwa ili mtu aweze kupata uzima, kwa kuwa Mungu Mwenyewe ni uzima wa milele, na Mungu Mwenyewe ni njia ambayo kwayo mtu hufufuliwa. Mungu kamwe hajawahi kosa kwa moyo wa mwanadamu, na Anaishi miongoni mwa binadamu wakati wote. Amekuwa nguvu ya kuendesha maisha ya mwanadamu, chanzo cha kuwepo kwa binadamu, na amana ya fahari ya kuwepo kwa binadamu baada ya kuzaliwa. Husababisha binadamu kuzaliwa upya, na kumwezesha kwa ushupavu kuishi kwa kila jukumu lake. Kwa sababu ya uwezo Wake, na nguvu ya maisha Yake yasiyopungua, binadamu ameishi kwa kizazi baada ya kizazi, ambapo nguvu ya uhai wa Mungu umekuwa uti wa mgongo wa kuwepo kwa binadamu, na ambayo Mungu amelipia gharama ambayo hakuna mtu wa kawaida amewahi kulipa. Nguvu za Mungu za maisha zinaweza kutawala juu ya nguvu zozote; zaidi ya hayo, inazidi mamlaka yoyote. Maisha Yake ni ya milele, nguvu zake za ajabu, na nguvu Zake za maisha haziwezi kuzidiwa na kiumbe yeyote au nguvu za adui. Nguvu za maisha ya Mungu zipo, na hung’aa mwangaza wake ulio mzuri sana, bila ya kujali muda au mahali. Mbingu na dunia zinaweza kupitia mabadiliko makubwa, lakini uzima wa Mungu ni ule ule daima. Mambo yote hupita, lakini maisha ya Mungu hubaki, kwa maana Mungu ni chanzo cha kuwepo kwa mambo yote, na mizizi ya kuwepo kwao. Asili ya maisha ya mwanadamu hutoka kwa Mungu, kuwepo kwa mbingu ni kwa sababu ya Mungu, na kuwepo kwa ardhi kunatokana na nguvu ya uhai wa Mungu. Hakuna kitu kinachomiliki nguvu kinachoweza kuzidi ukuu wa Mungu, na hakuna kitu chenye nguvu kinachoweza kuvunja mipaka ya mamlaka ya Mungu. Kwa njia hii, bila kujali wao ni nani, kila mtu lazima ajiwasilishe kwa utawala wa Mungu, kila mtu lazima aishi chini ya amri za Mungu, na hakuna mtu anayeweza kutoroka kutoka katika utawala Wake.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 255)

Kama kweli unataka kupata njia ya uzima wa milele, na kama wewe unayo tamaa katika utafutaji wako kwa ajili yake, basi kwanza ulijibu swali hili: Mungu yuko wapi leo? Labda utajibu kwamba Mungu anaishi mbinguni, bila shaka—Hangeishi katika nyumba yako? Labda unaweza kusema, kawaida Mungu anaishi kati ya mambo yote. Au unaweza kusema kwamba Mungu anaishi katika moyo wa kila mtu, au kwamba Mungu yuko katika ulimwengu wa kiroho. Mimi sipingi lolote kati ya haya, lakini lazima nifafanue suala hilo. Sio sahihi kabisa kusema kwamba Mungu anaishi katika moyo wa mwanadamu, wala si makosa kabisa. Hiyo ni kwa sababu, miongoni mwa waumini katika Mungu, kuna wale ambao imani yao ni ya kweli na wale ambao imani yao ni uongo, kuna wale ambao Mungu anawakubali na wale ambao hawakubali, kuna wale ambao humfurahisha na wale ambao ni chukizo, na kuna wale ambao Yeye huwafanya kamili na wale ambao hupunguza. Na hivyo Mimi Nasema kwamba Mungu Anaishi tu katika nyoyo za watu wachache, na watu hawa bila shaka ni wale ambao kweli wanaamini katika Mungu, wale ambao Mungu anawakubali, wale ambao humpendeza, na wale ambao Yeye huwafanya kamili. Wao ni wale wanaoongozwa na Mungu. Kwa kuwa wanaongozwa na Mungu, kwa hivyo ni watu ambao tayari wamesikia na kuona njia ya Mungu ya uzima wa milele. Wale ambao imani yao kwa Mungu ni ya uongo, wale ambao hawajaidhinishwa na Mungu, wale ambao wanadharauliwa na Mungu, wale ambao wamechujwa na Mungu—wamefungwa katika kukataliwa na Mungu, wamefungwa kubaki bila njia ya maisha, na wamefungwa kubaki wajinga wa kujua aliko Mungu. Kwa upande mwingine, wale ambao Mungu anaishi katika nyoyo zao wanajua aliko Mungu. Wao ni watu wale ambao Mungu huwapa njia ya uzima wa milele, na ni wale wanaomfuata Mungu. Je, unajua, sasa, aliko Mungu? Mungu yupo katika moyo wa mtu na upande wa mtu. Hayupo tu katika ulimwengu wa kiroho, na juu ya mambo yote, lakini hata zaidi Yupo duniani ambapo mwanadamu huishi. Na hivyo kufika kwa siku za mwisho kumechukua hatua ya kazi ya Mungu katika sehemu mpya. Mungu ana ukuu juu ya mambo yote katika ulimwengu, na Yeye ni uti wa mgongo wa mwanadamu katika moyo wake, na zaidi ya hayo, Yeye yuko miongoni mwa wanadamu. Ni kwa njia hii pekee Anaweza kuleta njia ya maisha kwa binadamu, na kumleta mwanadamu katika njia ya maisha. Mungu amekuja duniani, na Anaishi kati ya wanadamu, ili wanadamu wanaweza kupata njia ya maisha, na hivyo binadamu anaweza kuwepo. Wakati huo huo, Mungu pia huamuru mambo yote katika ulimwengu, ili wapate kushirikiana na usimamizi Wake miongoni mwa wanadamu. Na hivyo, kama wewe unakiri tu kwamba Mungu yuko mbinguni na katika moyo wa mwanadamu, lakini usikiri ukweli wa kuwepo kwa Mungu miongoni mwa watu, basi kamwe hutapata uzima, na kamwe hutapata njia ya kweli.

Mungu Mwenyewe ni maisha, na kweli, na uzima Wake na ukweli hutawala. Wale ambao hawana uwezo wa kupata ukweli kamwe hawatapata uzima. Bila mwongozo, msaada, na utoaji wa kweli, nanyi tu mtapata barua, mafundisho, na zaidi sana, kifo. Maisha ya Mungu ni ya milele, na ukweli wake na maisha hupatana. Kama huwezi kupata chanzo cha ukweli, basi huwezi kupata lishe ya maisha; kama huwezi kupata starehe ya maisha, basi utakuwa hakika huna ukweli, na hivyo mbali na mawazo na dhana, ukamilifu wa mwili wako hautakuwa chochote ila mwili, mwili wako unaonuka. Ujue kwamba maneno ya vitabu hayahesabiki kama maisha, kumbukumbu za historia haziwezi kupokelewa kama ukweli, na mafundisho ya siku za nyuma hayawezi kutumika kama sababu ya maneno ya sasa anayosema Mungu. Kinachoonyeshwa tu na Mungu anapokuja duniani na kuishi miongoni mwa binadamu ni ukweli, maisha, mapenzi ya Mungu, na njia Yake ya sasa ya kufanya kazi. Kama wewe utatumia rekodi ya maneno yaliyosemwa na Mungu wakati wa enzi zilizopita leo, basi wewe ni mtafutaji wa mambo ya kale, na njia bora ya kukueleza wewe ni mtaalamu wa urithi wa kihistoria. Kwa sababu wewe daima unaamini katika athari ya kazi ambayo Mungu alifanya katika nyakati zilizopita, amini tu katika kivuli cha Mungu alichowacha awali Alipokuwa Akifanya kazi miongoni mwa wanadamu, na kuamini tu kwa njia ambayo Mungu aliwapa wafuasi wake katika nyakati za zamani. Huamini katika mwelekeo wa kazi ya Mungu leo, huamini katika uso wa utukufu wa Mungu leo, na huamini katika njia ya sasa ya kweli iliyotolewa na Mungu. Na hivyo wewe ni mwotaji wa mchana ambaye hana ufahamu kamwe na hali ya mambo ya sasa. Kama sasa bado wewe unafuata maneno yasiyokuwa na uwezo wa kuleta maisha kwa binadamu, basi wewe ni kipande cha ukuni uliokauka kisicho na matumaini[a], kwa maana wewe ni mwenye kushikilia ukale mno, asiyeweza kutiishwa kwa urahisi, huwezi kusikiza wosia!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele

Tanbihi:

a. Kipande cha gogo lililokufa: Nahau ya Kichina yenye maana “-siyoweza kusaidiwa.”

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 256)

Mungu Mwenyewe ni ukweli, Mwenyewe anao ukweli, na Yeye ndiye chanzo cha ukweli. Kila kitu chanya na kila ukweli unatoka Kwake. Anaweza kutoa hukumu juu ya wema na ubaya wa mambo yote na matukio yote; Anaweza kutoa hukumu juu ya mambo ambayo yametukia, mambo ambayo yanatukia sasa, na mambo ya baadaye ambayo bado hayajajulikana kwa mwanadamu. Yeye ndiye hakimu wa pekee Anayeweza kutoa hukumu juu ya wema na ubaya wa mambo yote, na hii inamaanisha kuwa wema na ubaya wa mambo yote unaweza kuhukumiwa na Yeye tu. Anajua sheria za mambo yote. Huu ndio mfano halisi wa ukweli, jambo ambalo linamaanisha kwamba Yeye Mwenyewe anacho kiini cha ukweli. Ikiwa mwanadamu angeuelewa ukweli na kupata ukamilifu, basi angekuwa na uhusiano wowote na mfano halisi wa ukweli? Mwanadamu anapokamilishwa, yeye huwa na ufahamu sahihi wa yote ambayo Mungu hufanya sasa na mambo Anayohitaji, naye huwa na njia sahihi ya kutenda; mwanadamu pia huyaelewa mapenzi ya Mungu na hujua tofauti kati ya mema na mabaya. Lakini kuna mambo kadhaa ambayo mwanadamu hawezi kuyafikia, mambo ambayo anaweza kuyajua tu baada ya Mungu kumwambia kuyahusu—je, mwanadamu anaweza kujua mambo ambayo bado hayajajulikana, mambo ambayo bado Mungu hajamwambia? (Hawezi.) Mwanadamu hawezi kufanya utabiri. Aidha, hata kama mwanadamu angeupata ukweli kutoka kwa Mungu, na awe na uhalisi wa ukweli, na ajue kiini cha ukweli mwingi, na awe na uwezo wa kutofautisha mema na mabaya, basi angekuwa na uwezo wa kudhibiti na kutawala vitu vyote? (La.) Hiyo ndiyo tofauti. Viumbe walioumbwa wanaweza tu kuupata ukweli kutoka kwa chanzo cha ukweli. Je, wanaweza kuupata ukweli kutoka kwa mwanadamu? Mwanadamu anaweza kuwapa ukweli? Mwanadamu anaweza kumtunza mwanadamu? Hawezi, na hiyo ndiyo tofauti. Unaweza kupokea tu, siyo kutoa–je, unaweza kuitwa mfano halisi wa ukweli? Kiini cha mfano halisi wa ukweli ni kipi hasa? Ni chanzo kinachoutoa ukweli, chanzo cha utawala na mamlaka juu ya vitu vyote, na pia ni viwango na sheria ambazo kwazo vitu vyote na matukio yote yanahukumiwa. Huu ndio mfano halisi wa ukweli.

Kimetoholewa kutoka katika “Kwa Viongozi na Wafanyakazi, Kuchagua Njia Ni Muhimu Sana X” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 257)

Katika kuonyesha Kwake ukweli, Mungu huonyesha tabia na kiini Chake; havionyeshwi kulingana na mihutasari ya wanadamu ya mambo mbalimbali chanya na njia za kuzungumza ambazo wanadamu wanatambua. Maneno ya Mungu ni maneno ya Mungu; maneno ya Mungu ni ukweli. Hayo ndiyo msingi na sheria ambayo kwayo wanadamu wanapaswa kuishi, na hizo zinazodaiwa kuwa kanuni zinazotokana na binadamu zimelaaniwa na Mungu. Hazikubaliwi na Yeye, sembuse kuwa asili au msingi wa matamshi Yake. Mungu huonyesha tabia Yake na kiini Chake kupitia maneno Yake. Maneno yote yaliyotolewa na maonyesho ya Mungu ni ukweli, kwa maana Yeye anacho kiini cha Mungu, na Yeye ndiye uhalisi wa mambo yote chanya. Ukweli kwamba maneno ya Mungu ni ukweli haubadiliki kamwe, bila kujali jinsi wanadamu hawa wapotovu wanavyoyachukulia au kuyafafanua, wala jinsi wanavyoyaona au kuyaelewa. Haijalishi ni maneno mangapi ya Mungu ambayo yamezungumzwa, na bila kujali jinsi binadamu hawa wapotovu na wenye dhambi wanavyoyashutumu kwa kiasi kipi, hata kiasi kwamba hawayasambazi, na hata kufikia kiwango ambacho yanadharauliwa na wanadamu wapotovu—hata katika hali hizi, bado kuna ukweli ambao hauwezi kubadilishwa: Hizi zinazodaiwa kuwa mila na desturi ambazo wanadamu huthamini haziwezi kuwa vitu chanya na haziwezi kuwa ukweli, hata sababu zilizopo hapo juu zikizingatiwa. Hili haliwezi kubadilika.

Tamaduni za jadi za wanadamu na njia za kuishi hazitakuwa ukweli kwa sababu ya mabadiliko au kupita kwa wakati, na wala maneno ya Mungu hayatakuwa maneno ya mwanadamu kwa sababu ya shutuma na kusahau kwa wanadamu. Kiini hiki hakitabadilika kamwe; ukweli ni ukweli kila wakati. Kuna ukweli ndani ya hili: Hiyo misemo yote inayofupishwa na wanadamu inatoka kwa Shetani—ni fikira na mawazo ya wanadamu, hata inatokana na hamaki ya binadamu, na haihusiani hata kidogo na mambo chanya. Maneno ya Mungu, kwa upande mwingine, ni maonyesho ya kiini na hadhi ya Mungu. Yeye huyaonyesha maneno haya kwa sababu gani? Kwa nini Ninasema maneno hayo ni ukweli? Sababu ni kwamba Mungu anatawala juu ya sheria, kanuni, vyanzo, viini, uhalisi na siri zote za vitu vyote, na vimefumbatwa mkononi Mwake, na ni Mungu pekee Anayejua kanuni, uhalisi, ukweli, na siri zote za vitu vyote; Anajua asili ya vitu hivyo na vyanzo vyao ni nini hasa. Kwa hivyo, ni ufafanuzi wa vitu vyote uliotajwa katika maneno ya Mungu pekee ndio sahihi kabisa, na mahitaji kwa wanadamu yaliyo ndani ya maneno ya Mungu ndicho kiwango pekee kwa wanadamu—kigezo pekee ambacho mwanadamu anapaswa kuishi kwa kufuata.

Kimetoholewa kutoka katika “Kuhusu Ukweli ni Nini” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 258)

Tangu unapoingia katika dunia hii ukilia, unaanza kutekeleza wajibu wako. Kwa kuchukua jukumu lako katika mpango wa Mungu na katika utaratibu Wake, unaanza safari yako katika maisha. Licha ya asili yako na licha ya safari iliyoko mbele yako, hakuna kitakachoepuka mpango na utaratibu ambao mbingu imeunda, na hakuna aliye na udhibiti wa hatima yake mwenyewe, kwa maana yule Anayetawala kila kitu ndiye tu Aliye na uwezo wa kazi hiyo. Tangu siku aliyoumbwa binadamu, Mungu amekuwa akitenda kazi Yake kwa njia hii, kusimamia ulimwengu huu na kuelekeza mifuatano ya mabadiliko katika mambo yote na njia ambazo yanasongea. Pamoja na vitu vyote vingine, mwanadamu polepole na bila kujua anastawishwa na utamu na mvua na umande kutoka kwa Mungu. Kama vitu vyote vingine, mwanadamu bila kujua, anaishi chini ya mpango wa mkono wa Mungu. Moyo na roho ya mwanadamu vimeshikwa katika mkono wa Mungu, na maisha yake yote yanatazamwa machoni mwa Mungu. Haijalishi kama unayaamini mambo haya au la, vitu vyote, viwe hai au vilivyokufa, vitahamishwa, vitabadilika, kufanywa vipya, na kutoweka kulingana na mawazo ya Mungu. Hii ndiyo njia ambayo Mungu huongoza vitu vyote.

Usiku uingiapo polepole, mwanadamu huwa hafahamu, kwani moyo wa mwanadamu hauwezi kujua jinsi giza linapokaribia au wapi linakotoka. Usiku unapotoweka polepole, mwanadamu hukaribisha mwanga wa mchana, lakini ikija kwa kulikotoka nuru na jinsi imeliondoa giza la usiku, mwanadamu anajua hata machache na hata ana ufahamu mchache zaidi Mabadiliko haya ya kawaida ya mchana na usiku humpitisha mwanadamu kutoka kipindi kimoja hadi kingine, kutoka kipindi kimoja cha kihistoria hadi kingine, wakati huu wote yakihakikisha kwamba kazi ya Mungu katika kila kipindi na mpango Wake wa kila enzi unatekelezwa. Mwanadamu ametembea katika enzi hizi tofauti pamoja na Mungu, lakini bado hafahamu kwamba Mungu huongoza hatima ya mambo yote na viumbe hai au jinsi Mungu hupanga na kuelekeza mambo yote. Hili ni jambo ambalo limekwepa ufahamu wa binadamu tangu enzi za kale mpaka leo. Kuhusu sababu, siyo kwa sababu matendo ya Mungu hayafahamiki, au kwa sababu mpango wa Mungu bado haujakamilika, lakini ni kwa sababu moyo na roho ya mwanadamu viko mbali sana na Mungu, kiasi ya kwamba, mwanadamu anabaki katika huduma ya Shetani wakati ule ule anapomfuata Mungu—na hata halitambui hili. Hakuna anayetafuta nyayo za Mungu kwa vitendo au kuonekana Anakoonyesha, na hakuna aliye na hiari ya kuwepo katika huduma na utunzaji wa Mungu. Badala yake, wao wako tayari kutegemea upotoshaji wa Shetani, yule mwovu, ili kurekebishwa kufuatana na dunia hii na kanuni za kuwepo ambazo watu waovu hufuata. Wakati huu, moyo na roho za mwanadamu hutolewa ushuru kwa shetani na kuwa riziki ya Shetani. Hata zaidi, moyo wa binadamu na roho yake zimekuwa mahali ambapo Shetani anaweza kuishi na uwanja wake wa kuchezea unaofaa. Kwa njia hii, mwanadamu kwa kutojua hupoteza ufahamu wake wa kanuni za kuwa binadamu, na wa thamani na maana ya kuwepo kwa binadamu. Sheria za Mungu na agano kati ya Mungu na mwanadamu huangamia hatua kwa hatua kutoka katika moyo wa mwanadamu, na yeye huacha kumtafuta na kumsikiza Mungu. Wakati upitavyo, mwanadamu haelewi tena kwa nini Mungu alimuumba, wala haelewi maneno yanayotoka katika kinywa cha Mungu na yote yanayotoka kwa Mungu. Mwanadamu kisha huanza kupinga sheria na amri za Mungu na moyo na roho zake hufishwa…. Mungu humpoteza mwanadamu ambaye Alimuumba mwanzoni, na mwanadamu hupoteza mzizi wa mwanzo wake: Hii ndiyo huzuni ya hii jamii ya wanadamu. Kusema ukweli, tangu mwanzo mpaka sasa, Mungu amepanga janga kwa wanadamu, ambapo mwanadamu ni mhusika mkuu na mwathiriwa; kuhusu nani ndiye mwelekezi wa hadithi hii ya janga, hakuna anayeweza kujibu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 259)

Mungu aliumba dunia hii na kuleta mwanadamu, kiumbe hai ambaye alitia uhai ndani yake. Kisha, mwanadamu akaja kuwa na wazazi na jamaa na hakuwa mpweke tena. Tangu mwanadamu alipotua macho kwa mara ya kwanza katika dunia hii ya mali, ilibainika kuwa angeishi ndani ya utaratibu wa Mungu. Ni pumzi ya uhai kutoka kwa Mungu ndiyo hustawisha kila kiumbe hai katika ukuaji wake hadi kinapokomaa. Wakati wa mchakato huu, hakuna anayehisi kwamba mwanadamu anakua chini ya uangalizi wa Mungu, bali badala yake anaamini kwamba mwanadamu anafanya hivyo chini ya utunzaji wa upendo wa wazazi wake, na kwamba ni silika yake mwenyewe ya maisha ambayo inaongoza mchakato huu wa kukua kwake. Hii ni kwa sababu mwanadamu hajui aliyeleta maisha au yalikotoka maisha hayo, sembuse jinsi silika ya maisha husababisha miujiza. Anajua tu kwamba chakula ndicho msingi wa kuendelea kwa maisha yake, kwamba uvumilivu ndio chanzo cha kuwepo kwake, na kwamba imani zilizomo akilini mwake ndizo raslimali ambazo kwazo kuendelea kuishi kwake kunategemea. Mwanadamu hajui kabisa kuhusu neema na riziki zitokazo kwa Mungu, na kwa njia hii yeye hupoteza. uzima aliopewa na Mungu bila azma…. Hakuna hata mmoja wa wanadamu hawa ambaye Mungu anamwangazia usiku na mchana huchukua jukumu la kumwabudu. Mungu anaendelea tu kufanya kazi juu ya mwanadamu, akiwa hana matarajio yoyote kutoka kwake, kama jinsi ambavyo Amepanga. Anafanya hivyo kwa matumaini kwamba siku moja, mwanadamu ataamka kutoka katika ndoto yake na ghafla kuelewa thamani na maana ya maisha, gharama aliyolipa Mungu kwa yote ambayo Amempa, na wasiwasi wa hamu ambao kwao Mungu anangoja mwanadamu amgeukie. Hakuna yeyote amewahi kuchunguza siri zinazoongoza asili na kuendelea kwa maisha ya mwanadamu. Ni Mungu tu, ambaye Anaelewa yote haya, kwa kimya huvumilia mapigo na maumivu ambayo binadamu, ambaye amepokea kila kitu kutoka kwa Mungu lakini bila shukurani, humpa. Binadamu huchukulia kila kitu kinacholetwa na maisha kimzaha, na, vilevile, nini “jambo lisilo na shaka,” kwamba Mungu anasalitiwa na mwanadamu, anasahaulika na mwanadamu, na kutozwa kwa nguvu na mwanadamu. Je, inaweza kuwa kwamba mpango wa Mungu ni wa maana namna hii kweli? Je inaweza kuwa kwamba mwanadamu, kiumbe huyu hai ambaye alitoka katika mkono wa Mungu, ni wa maana namna hiyo kweli? Mpango wa Mungu hakika ni wa umuhimu kabisa; hata hivyo, kiumbe chenye uhai kilichoumbwa na mkono wa Mungu kipo kwa ajili ya mpango Wake. Kwa hivyo, Mungu hawezi kuuharibu mpango Wake kwa sababu ya chuki kwa jamii hii ya wanadamu. Ni kwa ajili ya mpango Wake na kwa ajili ya pumzi aliyotoa ndiyo maana Mungu hustahimili mateso yote, sio kwa ajili ya mwili wa mwanadamu ila ni kwa sababu ya uhai wa mwanadamu. Yeye hufanya hivyo ili kurudisha pumzi Aliyopuliza ndani mwa mwanadamu, wala sio nyama za mwili. Huu ndio mpango wake.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 260)

Wote wanaokuja duniani humu lazima wapitie maisha na kifo, na wengi wao walipitia mzunguko wa kifo na kuzaliwa upya. Wale wanaoishi watakufa hivi karibuni na wafu watarejea karibuni. Yote haya ni mwendo wa maisha uliopangwa na Mungu kwa kila kiumbe hai. Hata hivyo, njia hii na mzunguko huu hasa ni ukweli ambao Mungu anataka binadamu aone: kwamba uzima aliopewa mwanadamu na Mungu hauna mipaka, na hauzuiliwi na maumbile ya nje, wakati, au nafasi. Hili ndilo fumbo la uzima aliopewa binadamu na Mungu, na dhihirisho kwamba maisha yalikuja kutoka Kwake. Ingawa watu wengi wanaweza kukosa kuamini kwamba maisha yalitoka kwa Mungu, binadamu bila ya kufahamu hufurahia yote yatokayo kwa Mungu, iwe wanaamini au wanakana uwepo Wake. Iwapo siku moja Mungu kwa ghafla Atabadili moyo na Atake kurudisha yote yaliyomo duniani na kuchukua maisha Aliyotoa, basi yote duniani yataisha. Mungu hutumia maisha Yake kukimu vitu vyote vilivyo hai na visivyo na uhai, na kuleta yote kwa utaratibu mzuri kwa mujibu wa uwezo na mamlaka Yake. Huu ni ukweli ambao hauwezi kuwazika au kueleweka na yeyote, na kweli hizi zisizoeleweka kwa fikira zetu ni dhihirisho halisi na ushahidi wa nguvu za Mungu katika maisha. Sasa hebu nikupe siri: Ukuu wa uzima wa Mungu na nguvu ya uzima Wake haziwezi kueleweka na kiumbe yeyote. Hivi ndivyo hali ilivyo sasa, kama ilivyokuwa awali, na itakuwa hivyo wakati ujao. Siri ya pili Nitakayotoa ni hii: Chanzo cha uhai hutoka kwa Mungu, kwa viumbe wote, bila kujali jinsi wanavyoweza kuwa tofauti katika maumbile au muundo. Hata uwe kiumbe hai wa aina gani, huwezi kwenda kinyume na njia ya maisha ambayo Mungu ameweka. Katika hali yoyote, kile Napenda ni kuwa mwanadamu kuelewa hili: Bila ulinzi, utunzaji, na utoaji wa Mungu, mwanadamu hawezi kupokea yote aliyokusudiwa kupokea, haijalishi anajaribu kwa juhudi au kupambana kwa bidii namna gani. Bila ruzuku ya uhai kutoka kwa Mungu, mwanadamu hupoteza maana ya thamani ya kuishi na madhumuni ya maana katika maisha. Mungu angewezaje kumruhusu mwanadamu, ambaye bila umakini hupoteza thamani ya uhai wake, kuishi hivyo bila ya kujali? Kama vile nimesema awali: Usisahau kwamba Mungu Ndiye chanzo cha maisha yako. Iwapo mwanadamu atashindwa kuthamini yote ambayo Mungu Amemfanyia, Mungu Hatachukua tu kile Alichotoa mbeleni pekee, lakini Atatoza, kutoka kwa binadamu kama fidia, thamani ya yote ambayo Ametoa mara mbili.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 261)

Yote yaliyo duniani humu yanabadilika haraka sawasawa na mawazo ya Mwenye uweza, na chini ya macho Yake. Mambo ambayo wanadamu hawajawahi kuyasikia yanaweza kuja kwa ghafla, ilhali vitu ambavyo wanadamu wamemiliki kwa muda mrefu vinaweza kutoweka bila wao kujua. Hakuna anayeweza kutambua mahali alipo Mwenye uweza sembuse yeyote kuweza kuhisi kuzidi uwezo wa mwanadamu na ukuu wa nguvu za uzima za Mwenye uweza. Anazidi uwezo wa mwanadamu kwa vile Anavyoweza kufahamu yale ambayo wanadamu hawawezi. Yeye ni mkuu kwa vile ni Yeye anayekataliwa na wanadamu na bado Anawaokoa wanadamu. Yeye anajua maana ya maisha na mauti na, isitoshe, Anajua ni kanuni gani zinazofaa katika kuongoza uwepo wa wanadamu Aliowaumba. Yeye ndiye msingi ambao kwao uwepo wa wanadamu hutegemea, na ndiye Mkombozi ambaye hufufua wanadamu tena. Yeye huilemea mioyo yenye furaha kwa huzuni na kuiinua mioyo yenye huzuni kwa furaha, yote kwa ajili ya kazi Yake, na kwa ajili ya mpango Wake.

Wanadamu, baada ya kuuwacha utoaji wa uzima kutoka kwa Mwenye uweza, hawajui azma ya kuishi, lakini hata hivyo wanaogopa kifo. Hawana usaidizi wala msaada, lakini bado wanasita kufumba macho yao, na wanajitayarisha kuendeleza uwepo wa aibu ulimwenguni humu, magunia ya miili wasio na hisia za roho zao wenyewe. Unaishi hivi, bila matumaini, kama vile wafanyavyo wengine, bila lengo. Kuna aliye Mtakatifu tu katika hekaya atakayekuja kuwaokoa watu ambao, wakiwa wanapiga kite katika mateso yao, wanatamani sana kufika Kwake. Hadi sasa, imani hii haijafikiwa kwa wale ambao hawana fahamu. Hata hivyo, watu bado wanaitaka sana. Mwenye uweza ana rehema kwa watu hawa ambao wameteseka sana. Wakati uo huo, Amechoshwa na watu hawa wasio na fahamu, maana imembidi Asubiri sana kupata jibu kutoka kwa wanadamu. Anatamani kutafuta, kuutafuta moyo wako na roho yako, kukuletea chakula na maji na kukuzindua, ili usione kiu na kuhisi njaa tena. Unapokuwa umechoka na unapoanza kuhisi huzuni kubwa ya ulimwengu huu, usipotoke, usilie. Mwenyezi Mungu, Mlinzi, atakaribisha kuwasili kwako wakati wowote. Yuko kandokando yako akiangalia, akikusubiri urudi. Anasubiri siku ambayo utarudisha ghafla kumbukumbu yako: ukitambua ukweli kwamba ulitoka kwa Mungu, lakini wakati fulani usiojulikana ukapoteza mwelekeo wako, wakati fulani usiojulikana ukaanguka barabarani ukiwa hujitambui na tena wakati fulani usiojulikana ukampata “baba.” Isitoshe, unagundua kuwa Mwenye uweza amekuwa hapo muda huo wote, akiangalia, akisubiri kurejea kwako, kwa muda mrefu sana. Amekuwa akitazama na tamanio kubwa, Akingoja itiko pasipo jibu. Kusubiri Kwake kunazidi thamani, na ni kwa ajili ya moyo na roho ya wanadamu. Pengine kusubiri huku hakuna mwisho, na pengine kumefikia mwisho. Lakini unapaswa kujua moyo wako na roho yako hasa viko wapi sasa hivi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kutanafusi kwa Mwenye Uweza

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 262)

Kama washiriki wa jamii ya binadamu na Wakristo wamchao Mungu, ni jukumu na wajibu wa sisi wote kutoa akili na mwili wetu kwa kutimiza agizo la Mungu, kwani uhai wetu wote ulitoka kwa Mungu, na upo kwa sababu ya ukuu wa Mungu. Kama akili zetu na miili yetu si kwa ajili ya agizo la Mungu na si kwa sababu ya kusudi la haki la mwanadamu, basi nafsi zetu hazina thamani kwa wale waliokufa kishahidi kwa ajili ya agizo la Mungu, na thamani ndogo zaidi kwa Mungu, aliyetupa kila kitu.

Mungu aliumba dunia hii, Aliumba mwanadamu huyu, na zaidi ya hayo Alikuwa muasisi wa utamaduni wa zamani wa Giriki na ustaarabu wa binadamu. Ni Mungu tu anayemfariji huyu mwanadamu, na ni Mungu tu anayemtunza mwanadamu huyu usiku na mchana. Ukuaji na maendeleo ya binadamu hayatengani na ukuu wa Mungu, na historia na mustakabali wa mwanadamu ni zisizochangulika kutoka kwa miundo ya Mungu. Kama wewe ni Mkristo wa kweli, basi hakika utaamini kwamba kupanda na kushuka kwa nchi ama taifa lolote hufanyika kulingana na miundo ya Mungu. Mungu pekee hujua majaliwa ya nchi ama taifa, na Mungu pekee hudhibiti mwendo wa huyu mwanadamu. Iwapo mwanadamu anataka kuwa na majaliwa mazuri, iwapo nchi inataka kuwa na majaliwa mazuri, basi lazima mwanadamu ampigie Mungu magoti kwa ibada, atubu na kukiri mbele ya Mungu, la sivyo majaliwa na hatima ya mwanadamu hayataepuka kumalizika kwa janga.

Angalia nyuma wakati wa safina ya Nuhu: Wanadamu walikuwa wapotovu sana, walikuwa wamepotea kutoka katika baraka za Mungu, hawakuwa wanatunzwa na Mungu tena, na walikuwa wamepoteza ahadi za Mungu. Waliishi gizani, bila mwangaza wa Mungu. Hivyo wakawa waasherati kwa asili, wakajiachilia katika mkengeuko wa kutisha. Watu kama hao hawangeweza tena kupokea ahadi za Mungu; hawakufaa kushuhudia uso wa Mungu, wala kusikia sauti ya Mungu, kwani walikuwa wamemwacha Mungu, kuweka kando yote Aliyowapa, na kusahau mafunzo ya Mungu. Mioyo yao ilipotea mbali zaidi na zaidi na Mungu, na ilivyofanya hivyo, wakawa wapotovu zaidi ya mantiki na ubinadamu wote na wakazidi kuwa waovu. Hivyo walikaribia kifo zaidi, na kukabiliwa na ghadhabu na adhabu ya Mungu. Ni Nuhu tu aliyemwabudu Mungu na kuepukana na uovu, na hivyo aliweza kusikia sauti ya Mungu, na kusikia maelekezo ya Mungu. Alijenga safina kulingana na maelekezo ya neno la Mungu, na kukusanya aina yote ya viumbe hai. Na kwa njia hii, wakati kila kitu kilikuwa kimetayarishwa, Mungu aliangamiza dunia. Nuhu tu na wanachama saba wa familia yake walinusurika maangamizi, kwani Nuhu alimwabudu Yehova na kuepukana na uovu.

Kisha angalia enzi ya sasa: Hawa watu wenye haki kama Nuhu, ambao wangeweza kumwabudu Mungu na kuepuka uovu, wamekoma kuwepo. Lakini bado Mungu ana fadhili kwa mwanadamu huyu, na Anamsamehe mwanadamu wakati huu wa enzi ya mwisho. Mungu anawatafuta wanaomtaka Yeye ajitokeze. Anawatafuta wale wanaoweza kuyasikia maneno Yake, wale ambao hawajasahau agizo Lake na wanatoa mioyo na miili yao Kwake. Anawatafuta wale walio watiifu kama watoto wachanga mbele Yake, na hawampingi. Kama hujazuiliwa na nguvu zozote katika ibada yako Kwake, basi Mungu atakutazama na neema, na kukupea baraka Zake. Kama wewe ni wa daraja la juu, wa sifa ya heshima, aliyemiliki maarifa mengi, mmiliki wa mali nyingi, na kuungwa mkono na watu wengi, lakini mambo haya hayakuzuii kuja mbele za Mungu kuukubali wito Wake na agizo Lake, kufanya kile Mungu anachokuambia ufanye, basi yote unayoyafanya yatakuwa yenye umuhimu zaidi duniani na yenye haki zaidi ya binadamu. Ukiukataa wito wa Mungu kwa sababu ya hadhi yako na malengo yako mwenyewe, yote utakayoyafanya yatalaaniwa na hata kudharauliwa na Mungu. Labda wewe ni rais, ama mwanasayansi, ama mchungaji, ama mzee, lakini bila kujali ukuu wa ofisi yako, ukitegemea maarifa yako na uwezo katika shughuli zako, basi daima utakuwa wa kushindwa na kamwe utanyimwa baraka za Mungu, kwa sababu Mungu hakubali chochote unachofanya, na Hakubali kwamba kazi yako ni yenye haki, wala kukubali kwamba unafanya kazi kwa msaada wa mwanadamu. Atasema yote unayofanya, ni ya kutumia maarifa na nguvu za mwanadamu kumvulia mwanadamu ulinzi wa Mungu na kumnyima baraka za Mungu. Atasema kuwa unamwongoza mwanadamu kuelekea gizani, kuelekea kifo, na kuelekea mwanzo wa kuwepo bila mipaka ambapo mwanadamu amempoteza Mungu na baraka Zake.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 2: Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 263)

Kutoka wakati mwanadamu kwanza alikuwa na sayansi ya jamii, akili yake ilishughulishwa na sayansi na maarifa. Kisha sayansi na maarifa vikawa vyombo vya kutawala mwanadamu, na hapakuwa tena na nafasi ya kutosha kumwabudu Mungu, na hapakuwa tena na mazingira mazuri ya kumwabudu Mungu. Nafasi ya Mungu ikashuka hata chini zaidi moyoni mwa mwanadamu. Dunia moyoni mwa mwanadamu bila nafasi ya Mungu ni giza, tupu bila matumaini. Na hivyo kukatokea wanasayansi wa jamii, wataalamu wa historia na wanasiasa wengi kueleza nadharia ya sayansi ya jamii, nadharia ya mageuko ya binadamu, na nadharia nyingine zinazopinga ukweli kwamba Mungu alimuumba mwanadamu, kujaza moyo na akili ya mwanadamu. Na kwa njia hii, wanaoamini kwamba Mungu aliumba kila kitu wanakuwa wachache zaidi, na wale wanaoamini nadharia ya mageuko wanakuwa hata wengi kwa nambari. Watu zaidi wanachukulia rekodi za kazi ya Mungu na maneno Yake wakati wa enzi ya Agano la Kale kuwa hadithi na hekaya. Kwa mioyo yao, watu wanakuwa wasiojali heshima na ukubwa wa Mungu, kwa imani kwamba Mungu yupo na anatawala kila kitu. Kusalia kwa mwanadamu na majaliwa ya nchi na mataifa si muhimu kwao tena. Mwanadamu anaishi katika dunia tupu akijishughulisha tu na kula, kunywa, na ufuatiliaji wa furaha. … Watu wachache wanashughulika kutafuta Afanyapo Mungu kazi Yake leo, ama kutafuta jinsi Anavyoongoza na kupanga majaliwa ya mwanadamu. Na kwa njia hii, ustaarabu wa ubinadamu bila fahamu ukawa huwezi kukutana na matakwa ya mwanadamu hata zaidi, na hata kuna watu zaidi wanaohisi kwamba, kuishi kwa dunia kama hii, wanayo furaha ya chini kuliko watu walioenda. Hata watu wa nchi zilizokuwa na ustaarabu wa juu wanaeleza malalamiko haya. Kwani bila mwongozo wa Mungu, bila kujali jinsi viongozi na wanasosiolojia wanatafakari kuhifadhi ustaarabu wa binadamu, haina mafanikio. Hakuna anayeweza kujaza utupu kwa moyo wa mwanadamu, kwani hakuna anayeweza kuwa uhai wa mwanadamu, na hakuna nadharia ya kijamii inayoweza kumwokoa kutokana na utupu unaomtesa. Sayansi, maarifa, uhuru, demokrasia, wasaa wa mapumziko, faraja, haya yote ni mapumziko ya muda, Hata na mambo haya, mwanadamu hataepuka kufanya dhambi na kuomboleza udhalimu wa jamii. Mambo haya hayawezi kupunguza tamaa ya mwanadamu na hamu ya kuchunguza. Kwa sababu mwanadamu aliumbwa na Mungu na kafara na uchunguzi usio na sababu wa mwanadamu vitamwongoza tu kwa dhiki zaidi. Mwanadamu daima atakuwa katika hali ya hofu isiyoisha, hatajua jinsi ya kuukabili mustakabali wa wanadamu, ama jinsi ya kuikabili njia iliyo mbele. Mwanadamu atakuja hata kuogopa sayansi na elimu, na kuhofia hata zaidi utupu ulio ndani yake sana. Duniani humu, bila kujali kama unaishi katika nchi huru ama isiyo na haki za binadamu, huwezi kabisa kuponyoka majaliwa ya mwanadamu. Kama wewe ni kiongozi ama anayeongozwa, huwezi kabisa kuponyoka hamu ya kuchunguza majaliwa, siri na majaliwa ya mwanadamu. Chini ya hayo, huna uwezo wa kutoroka hisia ya utupu inayotatiza. Matukio kama haya, yaliyo kawaida kwa wanadamu wote, yanaitwa matukio ya kijamii na wanasosiolojia, lakini hakuna mtu mkubwa anayeweza kuja mbele kutatua shida kama hizi. Mwanadamu, hata hivyo, ni mwanadamu. Nafasi na maisha ya Mungu hayawezi kubadilishwa na mwanadamu yeyote. Mwanadamu hahitaji tu jamii iliyo na haki, ambapo kila mtu analishwa vyema na ana uhuru na usawa, lakini wokovu wa Mungu na Yeye kuwapa uhai. Wakati tu mwanadamu atapokea wokovu wa Mungu na kupatiwa uhai na Yeye ndipo mahitaji, hamu ya kuchunguza, na utupu wa kiroho wa mwanadamu utaweza kutatuliwa. Iwapo watu wa nchi ama taifa hawawezi kupokea wokovu na utunzaji wa Mungu, basi nchi ama taifa kama hilo litatembelea njia inayoelekea uharibifuni, inayoelekea gizani, na litaangamizwa na Mungu.

Labda nchi yako inafanikiwa sasa, lakini ukiruhusu watu wako kupotea kutoka kwa Mungu, basi nchi yako itazidi kujipata bila baraka za Mungu. Ustaarabu wa nchi yako utazidi kukanyagiwa chini, na kabla ya muda mrefu watu watamwasi Mungu na kulaani Mbingu. Na hivyo, bila kujulikana kwa mwanadamu, majaliwa ya nchi yataletwa kwa uharibifu. Mungu ataziinua nchi zenye nguvu ili kukabiliana na nchi hizo zilizolaaniwa na Mungu, na anaweza hata kuzifuta kutoka uso wa dunia. Kupanda na kushuka kwa nchi ama taifa kunategemea kama viongozi wao wanamwabudu Mungu, na kama wanawaongoza watu wao karibu na Mungu na kumwabudu. Lakini, kwa hii enzi ya mwisho, kwa sababu wale wanaomtafuta Mungu kwa kweli na kumwabudu wanazidi kuwa wachache, Mungu anaweka fadhili ya pekee juu ya nchi ambapo Ukristo ni dini ya serikali. Anazikusanya pamoja kuunda kambi ya haki kiasi ya dunia, wakati nchi zikanazo Mungu ama zile zisizomwabudu Mungu wa kweli zinakuwa wapinzani wa kambi ya haki. Kwa njia hii, Mungu hana tu mahali miongoni mwa wanadamu pa kufanyia kazi Yake, lakini pia Anapata nchi zinazoweza kutumia mamlaka ya haki, ili kulazimisha mipaka na vikwazo kwa nchi hizo zinazompinga Mungu. Lakini licha ya hayo, bado hakuna watu zaidi wanaokuja mbele kumwabudu Mungu, kwa sababu mwanadamu amepotea mbali sana kutoka Kwake, na Mungu hajakuwa kwa mawazo ya mwanadamu kwa muda mrefu. Kunabakia tu duniani nchi zinazotumia haki na kupinga udhalimu. Lakini hii ni mbali na matakwa ya Mungu, kwani hakuna kiongozi wa nchi yoyote atamruhusu Mungu kuongoza watu wake, na hakuna chama cha kisiasa kitakachokusanya pamoja watu wake kumwabudu Mungu; Mungu amepoteza mahala Pake halali kwa mioyo ya nchi zote, taifa, chama tawala, na hata kwa moyo wa kila mtu. Ingawa nguvu za haki ziko kwa dunia hii, utawala ambapo Mungu hana mahali kwa moyo wa mwanadamu ni dhaifu. Bila baraka ya Mungu, uwanja wa kisiasa utaanguka katika vurugu na wenye kuweza kudhuriwa na mashambulizi. Kwa mwanadamu, kuwa bila baraka ya Mungu ni kama kuwa bila jua. Bila kujali jinsi viongozi wanafanya mchango kwa watu wao kwa uangalifu, bila kujali idadi ya mikutano ya haki wanadamu wanafanya pamoja, hakuna kati ya hii itakayorejesha mambo ama kubadilisha majaliwa ya mwanadamu. Mwanadamu anaamini kuwa nchi ambapo watu wanalishwa na kuvalishwa nguo, ambapo watu wanaishi kwa amani, ni nchi nzuri, na iliyo na uongozi mzuri. Lakini Mungu hafikirii hivyo. Anaamini kuwa nchi ambapo hakuna mtu anayemwabudu ndiyo Atakayoiangamiza. Njia ya mwanadamu ya kufikiria ni tofauti kabisa na ya Mungu. Kwa hiyvo, kama mkuu wa nchi hamwabudu Mungu, basi majaliwa ya nchi hii itakuwa ya kutisha, na nchi haitakuwa na majaliwa.

Mungu hashiriki katika siasa za mwanadamu, lakini majaliwa ya nchi ama taifa inadhibitiwa na Mungu, Mungu anadhibiti dunia hii na ulimwengu mzima. Majaliwa ya mwanadamu na mpango wa Mungu yanashikamana kwa undani, na hakuna mwanadamu, nchi ama taifa limetolewa kwa mamlaka ya Mungu. Iwapo mwanadamu anatamani kujua majaliwa yake, basi lazima aje mbele ya Mungu. Mungu atawafanya wanaomfuata na kumwabudu kufanikiwa, na Atashusha na kuwaangamiza wale wanaompinga na kumkataa.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 2: Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 264)

Katika upana wa ulimwengu na anga, viumbe wasiohesabika wanaishi na kuzaana, hufuata sheria ya mzunguko wa maisha na kufuata sheria isiyobadilika. Wanaokufa huenda na hadithi za walio hai, na walio hai hurudia historia hii yenye huzuni ya wale waliokufa. Na kwa hivyo wanadamu hawawezi kujizuia ila kujiuliza wenyewe; Kwa nini tunaishi? Na kwa nini inatulazimu kufa? Nani anayeitawala dunia hii? Na ni nani muumbaji wa mwanadamu? Je, kweli wanadamu waliumbwa na mazingira asilia? Je, kweli wanadamu wana uamuzi juu ya hatima yao? … Kwa maelfu ya miaka wanadamu wameyauliza haya maswali, tena na tena. Kwa bahati mbaya, jinsi wanadamu wanavyopagawa na haya maswali, ndivyo kiu yao ya sayansi huendelea kukua. Sayansi hupatiana kutosheleza kwa muda na raha ya muda ya mwili, ila haitoshi kumpa mwanadamu uhuru kutokana na upweke, ukiwa, na hofu isiyodhihirika na kutosaidika ndani ya moyo wake. Wanadamu hutumia ujuzi wa kisayansi ambao wanaweza kuona kwa macho na kuelewa kwa akili yake ili kuutuliza moyo wao. Ilhali maarifa kama hayo ya kisayansi hayatoshi kuwazuia wanadamu kutafiti siri. Wanadamu hawajui kabisa Mkuu wa ulimwengu na vitu vyote ni nani, sembuse kujua mwanzo na mustakabali wa wanadamu. Wanadamu wanaishi tu, bila budi, katikati ya hii sheria. Hakuna anayeweza kuiepuka wala kuibadilisha kwani katika vitu vyote na katika mbingu kuna Mmoja kutoka milele hadi milele ambaye ni Mkuu wa kila kitu. Ni Yeye ambaye Hajawahi kuonekana na mwanadamu, ambaye wanadamu hawajawahi kumjua, ambaye wanadamu hawajawahi kuamini kuwepo Kwake, na bado ni Yeye Aliyewapulizia pumzi mababu wa wanadamu na kuwapa wanadamu uhai. Ni Yeye ndiye Huruzuku na kustawisha wanadamu kwa kuishi kwao, na huwaongoza wanadamu hadi siku ya leo. Aidha, Yeye na Yeye pekee ni wa kutegemewa na wanadamu ili kuendelea kuishi. Ni Mkuu wa kila kitu na Hutawala viumbe vyote vyenye uhai chini ya dunia. Huamrisha misimu yote minne, na ni Yeye huita upepo, jalidi, theluji na mvua. Huwapa wanadamu mwangaza wa jua na huleta machweo ya jioni. Ni Yeye Aliyeumba mbingu na ardhi, Akampa mwanadamu milima, maziwa na mito na kila kitu kilicho na uhai ndani yake. Matendo Yake yamo kila mahali, nguvu Zake ziko kila mahali, busara Zake ziko kila mahali na mamlaka Yake yako kila mahali. Kila mojawapo ya hizi sheria na kanuni ni mfano mzuri wa matendo Yake, na kila mojawapo inafichua hekima na mamlaka Yake. Nani anayeweza kujiondoa kutoka kwa ukuu Wake? Na ni nani anayeweza kujitoa mwenyewe katika njia Zake? Kila kitu kinaishi chini ya uangalizi Wake, zaidi ya hayo, kila kitu huishi chini ya ukuu Wake. Matendo na nguvu Zake huwaacha wanadamu bila chaguo ila kutambua ukweli kwamba ni Yeye pekee Anayeishi na Ana ukuu juu ya kila kitu. Hakuna kitu chochote ila Yeye kinachoweza kuamuru dunia, wala kuwajibikia wanadamu bila kukoma. Bila kujali kama unaweza kutambua vitendo vya Mungu, bila kujali kama unaamini katika kuwepo kwa Mungu, hakuna shaka kuwa hatima yako inaegemea katika mipango ya Mungu, na hakuna shaka kuwa Mungu atakuwa na ukuu juu ya kila kitu. Uwepo na utawala Wake haviwezi kutabiriwa ikiwa vinatambulika na kufahamika na binadamu au la. Ni Yeye pekee Anayejua kuhusu yaliyopita ya mwanadamu, yaliyomo na yanayojiri, na Yeye pekee ndiye mwamuzi wa hatima ya wanadamu. Haijalishi kama unaukubali huu ukweli, haitachukua muda mrefu kabla mwanadamu kushuhudia haya yote kwa macho yake mwenyewe, na huu ni ukweli ambao hivi karibu Mungu Ataudhihirisha. Wanadamu huishi na hufa chini ya macho yake Mungu. Wanadamu huishi kwa usimamizi wa Mungu, na wakati macho Yake yatafumbika kwa mara ya mwisho, hio pia ni kwa usimamizi Wake. Tena na tena, mwanadamu huja na kwenda, nyuma na mbele. Bila mapendeleo, yote ni sehemu ya ukuu na michoro ya Mungu. Usimamizi wa Mungu ungali unaendelea mbele na haujawahi kusimama. Atawafanya wanadamu wafahamu uwepo Wake, waamini katika ukuu Wake, watazame matendo Yake, na warudi katika ufalme Wake. Huu ni mpango Wake, na kazi ambayo Amekuwa Akiitekeleza kwa maelfu ya miaka.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 3: Mwanadamu Anaweza tu Kuokolewa Katikati ya Usimamizi wa Mungu

Iliyotangulia: Kujua Kazi ya Mungu (II)

Inayofuata: Siri Kuhusu Biblia

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp