Kufunua Upotovu wa Wanadamu (II)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 336)

Unasema kwamba unatambua Mungu mwenye mwili na unatambua kuwa Neno laonekana katika mwili, na bado unafanya mambo fulani bila Yeye kujua, mambo ambayo yanaenda kinyume na kile Anachotaka, na moyoni mwako humwogopi. Je, huku ni kumtambua Mungu? Unatambua Anachokisema ila unakataa kuyaweka katika vitendo hata yale mambo unayoweza kufanya na huzifuati njia zake. Je, huku ni kumtambua? Unamtambua ila mawazo yako ni kujikinga dhidi Yake, kutomcha kamwe. Ikiwa umeona na kuitambua kazi Yake na unafahamu kuwa Yeye ni Mungu, na bado unaendelea kuwa vuvuwaa na bado hujabadilika hata kidogo, basi wewe ni aina ya mtu ambaye bado hajashindwa kabisa. Wale ambao wameshindwa lazima wafanye yote wawezayo, na ingawa hawawezi kuingia katika ukweli wa juu zaidi, na ukweli huu huenda ukawashinda, watu kama hawa wako tayari moyoni mwao kufikia hili. Ni kwa sababu kuna mipaka kwa kile wanachoweza kukubali, kuna mipaka na vikomo kwa kile wanachoweza kutenda. Hata hivyo angalau, ni lazima wafanye yote wawezayo, na ikiwa unaweza kufikia hilo, haya ni matokeo ambayo yametimizwa kwa sababu ya kazi ya ushindi. Huenda ukasema, “Kwa sababu Anaweza kunena maneno mengi ambayo mwanadamu hawezi, ikiwa si Mungu, ni nani?” Kuwa na mawazo kama haya hakumaanishi unamtambua Mungu. Ikiwa unamtambua Mungu, unapaswa kuonyesha hilo kupitia kwa matendo yako halisi. Ukiongoza kanisa lakini usiweze kutenda haki, na kutamani pesa na kufuja pesa za kanisa kisiri kwa faida yako—je, huku ni kutambua kuwa kuna Mungu? Mungu ni mwenye Uweza na wa kumcha. Unawezaje kukosa kuogopa kama kweli unatambua kuwa kuna Mungu? Unawezaje kuwa ulifanya kitu cha kuchukiza namna hiyo? Je, huko kunaweza kuitwa kuamini? Je, kweli wamtambua Mungu? Ikiwa unaweza kufanya jambo la kudharauliwa kama hilo, je, huko kweli ni kumtambua Yeye? Je, unamwamini Mungu? Unayemwamini ni Mungu asiye yakini; ndiyo maana huogopi! Wale wote wanaomtambua Mungu kweli na kumfahamu wanamcha na wanaogopa kufanya chochote kinachompinga na chochote kinachoenda kinyume na dhamiri yao; hususan wanaogopa kufanya chochote kinachoenda kinyume na mapenzi ya Mungu. Hili tu ndilo laweza kuwa ni kumtambua Mungu. Utafanya nini wazazi wako wakikuzuia kumwamini Mungu? Utampenda vipi Mungu ikiwa mume wako asiye muumini anakutendea mema? Aidha utampendaje Mungu ikiwa ndugu na dada zako wanakuchukia? Ikiwa unamtambua, basi utatenda ipasavyo na kuishi kwa kudhihirisha uhalisi katika hali hizi zote. Ukikosa kutenda wazi na kusema tu kwamba unatambua uwepo wa Mungu, basi wewe ni msemaji tu! Unasema unamwamini na kumtambua. Je, unamtambua kwa njia gani? Unamwamini kwa njia gani? Je, unamwogopa? Unamcha? Unampenda moyoni mwako? Unapokuwa na huzuni bila yeyote wa kuegemea, unahisi Mungu ni wa kupendwa, halafu baadaye unasahau. Huku si kumpenda au kumwamini Mungu! Je, Mungu anataka mwanadamu apate nini mwishoni? Hali zote Nilizozitaja, kama vile: kufikiri kuwa wewe ni mtu mkubwa, kwamba unaelewa mambo upesi, kuwadhibiti wengine, kuwadharau wengine, kuwahukumu watu kwa misingi ya sura zao, kuwadhulumu watu waaminifu, kutamani pesa za kanisa, na kadhalika—ni wakati tu ambapo tabia hizi zote potovu zimeondolewa kwa kiwango fulani kutoka kwako, ndipo ushindi wako utafanywa dhahiri.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (4)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 337)

Nimefanya kazi na kusema kwa njia hii miongoni mwenu, Nimetumia nguvu na juhudi, ila ni wakati upi kamwe mmewahi kusikiliza kile Ninachowaambia wazi wazi? Ni wapi mmeniinamia Mimi, Mwenyezi? Kwa nini mnanitendea namna hii? Kwa nini kila kitu mnachokisema na kufanya huchochea hasira Yangu? Kwa nini, mioyo yenu imeshupaa? Je, Nimewahi kuwapiga kumbo kamwe? Kwa nini hamfanyi kitu chochote kingine ila kunifanya mwenye huzuni na wasiwasi? Mnasubiri siku ya ghadhabu Yangu, Yehova, kuja juu yenu? Je, mnanisubiri Mimi kutuma hasira kwenu iliyochochewa na makosa yenu? Si kila kitu Ninachokifanya ni kwa ajili yenu? Ilhali kila wakati mmenitendea Mimi, Yehova, kwa njia hii: kuiba sadaka Yangu, kuchukua sadaka ya madhabahu Yangu nyumbani kwa jamii ya mbwa mwitu kuwalisha wana wa mbwa mwitu na vitukuu vyake; watu wanapigana wenyewe kwa wenyewe, wakikabiliana na mtazamo wa hasira kwa panga na mikuki, kurusha maneno ya Mimi, Mwenyezi, kwenye choo kuwa machafu kama kinyesi. Uadilifu wenu uko wapi? Ubinadamu wenu umekuwa unyama! Mioyo yenu kwa muda mrefu imegeuka kuwa jiwe. Je, hamjui kwamba siku Yangu ya ghadhabu itakapofika itakuwa ndio wakati Nitakapokuhukumu mabaya mliyotenda dhidi Yangu leo, Mwenyezi? Je, mnafikiri kwamba kwa kunidanganya Mimi kwa njia hii, kwa kutupa maneno Yangu katika matope na kutoyasikiza—unafikiri kwamba kwa kutenda namna hii nyuma Yangu mnaweza kutoroka macho Yangu ya ghadhabu? Je, hamjui kwamba mlishaonekana na macho Yangu, Mimi Yehova, wakati mliiba sadaka Yangu na kutamani mali Yangu? Je, hamjui kwamba wakati mliiba sadaka Yangu, ilikuwa mbele ya madhabahu ambapo dhabihu hutolewa? Mnawezaje kujiamini wenyewe mlivyo wajanja kutosha kunidanganya Mimi kwa njia hii? Ghadhabu Yangu kali ingewezaje kuondoka kutoka katika dhambi zenu za kuchukiza? Ghadhabu Yangu yenye hasira ingepitaje juu ya matendo yenu maovu? Maovu mnayotenda leo hayawafungulii njia yenu kutokea, bali huhifadhi kuadibu kwa ajili ya kesho yenu; yanachochea kuadibu Kwangu, Mwenyezi, kwenu. Matendo yenu maovu na maneno yenu mabaya yangewezaje kuepuka kuadibu Kwangu? Maombi yenu yangeyafikiaje masikio Yangu? Ningefunguaje njia kwa ajili ya udhalimu wenu? Ningewezaje kuyatupilia mbali matendo yenu maovu ya kunikaidi? Ingewezekanaje Nisizikate ndimi zenu ambazo ni za sumu kama ya nyoka? Hamniombi msaada kwa ajili ya haki yenu, lakini badala yake mnahifadhi ghadhabu Yangu kama matokeo ya udhalimu wenu. Ningewezaje kuwasamehe? Katika macho Yangu, Mwenyezi, maneno na matendo yenu ni machafu. Macho Yangu, Mwenyezi, huona udhalimu wenu kama kuadibu kusikolegea. Kuadibu Kwangu kwa haki na hukumu vingeondokaje kwenu? Kwa sababu mmenitendea hivi, na kunifanya mwenye huzuni na ghadhabu, Ningewaachaje nyinyi muepe kutoka mikono Yangu na muondoke katika siku ambayo Mimi, Yehova, Nawaadibu na kuwalaani wewe? Je, hamjui kwamba maneno yenu yote mabaya na matamko tayari yamefikia masikio Yangu? Je, hamjui kwamba udhalimu wenu tayari umelilaghai vazi Langu takatifu la haki? Je, hamjui kwamba makosa yenu tayari yameichochea hasira Yangu kali? Je, hamjui kwamba kwa muda mrefu mmeniacha Nikitokota, na kwa muda mrefu mmeujaribu uvumilivu Wangu? Je, hamjui kwamba tayari mmeshauharibu mwili Wangu kuwa matambara? Nimevumilia mpaka sasa, kiasi kwamba Natoa hasira Zangu, kutokuwa mvumilivu kwenu tena. Je, hamjui kwamba matendo yenu maovu tayari yamefikia Macho Yangu, na kwamba kilio changu tayari kimefikia masikio ya Baba Yangu? Angewaruhusu vipi mnitendee Mimi jinsi hii? Kuna kazi yoyote Ninayofanya ndani yenu isiyo kwa ajili yenu? Ilhali nani kati yenu amekuwa na upendo zaidi kwa kazi Yangu, Yehova? Ningeweza kutokuwa mwaminifu kwa mapenzi ya Baba Yangu kwa sababu Mimi ni mnyonge, na kwa sababu ya uchungu Nilioupitia? Je, hamwelewi Moyo Wangu? Nasema na ninyi kama Yehova alivyofanya; je, Sijajinyima mengi kwa ajili yenu? Hata ingawa Niko tayari kuvumilia mateso haya yote kwa ajili ya kazi ya Baba Yangu, ni jinsi gani nyinyi mnaweza kuachwa huru kutokana na kuadibu ambako Nawaleteeni kama matokeo ya mateso Yangu? Je, hamjanifurahia kwa wingi sana? Leo, Nimetolewa kwenu na Baba Yangu; hamfahamu kwamba mnafurahia zaidi ya maneno Yangu mengi? Je, hamjui kwamba maisha Yangu yalibadilishwa na maisha yenu na mambo yote mnayofurahia? Je, hamjui kwamba Baba Yangu alitumia maisha Yangu kupigana na Shetani, na kwamba Yeye pia ametoa maisha Yangu kwenu, na kusababisha nyinyi kupokea mara mia zaidi, na kuwaruhusu kuepuka majaribu mengi? Je, hamjui kwamba ni kwa njia ya Kazi Yangu kwamba mmepewa msamaha kutokana na vishawishi vingi, na kuadibu kwingi kukali? Je, hamjui kwamba ni kwa sababu Yangu tu ndio Baba Yangu anawaruhusu kufurahia mpaka sasa? Jinsi gani mmebaki wagumu na wasiyoyumba leo, kiasi kwamba ni kana kwamba ugume umemea rohoni mwenu? Maovu mnayoyatenda leo yangeepukaje siku ya ghadhabu itakayofuata kuondoka Kwangu duniani? Ningewezaje kuwaruhusu wale ambao ni wagumu na wasiokubali kuepuka hasira ya Yehova?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Hakuna Aliye wa Mwili Anayeweza Kuepuka Siku ya Ghadhabu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 338)

Tafakarini kuhusu siku za nyuma: Ni lini macho Yangu yamekuwa na hasira, na sauti Yangu kuwa kali, kwenu? Ni wakati upi Nimegombana nanyi? Ni wakati upi Nimewakaripia bila mantiki? Ni wakati upi Nimewakemea usoni mwenu? Je, si ni kwa ajili ya kazi Yangu ndio kwamba Mimi namwomba Baba Yangu kuwaweka mbali na majaribu? Kwa nini mnanitendea Mimi hivi? Je, Nimewahi kutumia mamlaka Yangu kuipiga miili yenu? Kwa nini mnanilipa Mimi kwa njia hii? Baada ya ninyi kuwa moto na baridi Kwangu, nyinyi si moto wala baridi, na kisha mnajaribu kunirairai Mimi na kuficha mambo kutoka Kwangu, na vinywa vyenu vimejaa mate ya wasio haki. Je, mnafikiri kuwa ndimi zenu zinaweza kumdanganya Roho Wangu? Je, mnafikiri kwamba ndimi zenu zinaweza kuepuka ghadhabu Yangu? Je, mnafikiri kuwa ndimi zenu zinaweza kupitisha hukumu kwa matendo Yangu, Yehova, jinsi zinavyopenda? Je, Mimi ni Mungu ambaye mwanadamu hupishia hukumu? Ningewezaje kuruhusu buu dogo linikufuru hivyo? Ningewezaje kudai wana wa uasi kuwa miongoni mwa baraka Zangu za milele? Maneno na matendo yenu kwa muda mrefu yamewafichua na kuwahukumu. Wakati Nilieneza mbingu na kuumba vitu vyote, Sikuruhusu kiumbe yeyote kushiriki atakavyo, sembuse kuruhusu jambo lolote kuvuruga kazi Yangu na usimamizi Wangu, vile linavyopenda. Sikuvumilia mtu au kitu chochote; Ningewezaje kuwaacha walio wakatili na wa kinyama Kwangu? Ningewezaje kuwasamehe wale ambao wanaasi dhidi ya maneno Yangu? Ningewezaje kuwaacha wanaoniasi? Je, majaliwa ya mwanadamu hayako katika mikono Yangu, Mwenyezi? Ningeuchukua vipi udhalimu wako na uasi kama vitu vitakatifu? Jinsi gani dhambi zako zingenajisi utakatifu Wangu? Mimi sijanajisika na uchafu wa wasio haki, wala kufurahia sadaka ya wasio haki. Kama ungekuwa mwaminifu Kwangu, Yehova, je, ungeweza kujichukulia sadaka kutoka katika madhabahu Yangu? Je, ungeweza kutumia ulimi wako wa sumu kukufuru jina Langu takatifu? Ungeweza kuliasi neno Langu kwa njia hii? Je, ungeweza kuuchukua utukufu Wangu na jina langu takatifu kama chombo ambacho kwalo unamtumikia Shetani, yule mwovu? Maisha Yangu yametolewa kwa ajili ya furaha ya watakatifu. Ningewezaje kukuruhusu ucheze na maisha Yangu jinsi utakavyo, na kuyatumia kama chombo kwa ajili ya migogoro kati yenu? Mngewezaje kuwa wakatili sana, na watovu sana katika njia ya wenye wema, katika jinsi mlivyo Kwangu? Je, hamjui kwamba tayari Nimeandika matendo yenu maovu katika neno hili la maisha? Jinsi gani mngeweza kuepuka siku ya ghadhabu Ninapoadibu Misri? Ningewezaje kuwaruhusu kunipinga na kuniasi kwa njia hii, mara kwa mara? Nawaambia wazi, siku itakapokuja, basi kuadibu kwenu kutakuwa kusikovumilika zaidi kuliko ile ya Misri! Mnawezaje kuitoroka siku ya ghadhabu Yangu? Nawaambia kwa kweli: Uvumilivu Wangu ulitayarishwa kwa ajili ya matendo yenu maovu, na upo kwa ajili ya kuadibu kwenu siku hiyo. Je, ninyi si wale mtakaopata hukumu ya ghadhabu Yangu punde Nifikapo mwisho wa uvumilivu Wangu? Si mambo yote yapo mikononi Mwangu, Mwenyezi? Ningewezaje kuwaruhusu mniasi hivyo, chini ya mbingu? Maisha yenu yatakuwa magumu sana kwa kuwa mmekutana na Masiha, ambaye ilisemekana Angekuja, lakini ambaye kamwe Hakuja. Je, si nyinyi ni maadui Wake? Yesu amekuwa rafiki wenu, lakini bado mu maadui wa Masiha. Je, hamjui kwamba ingawa nyinyi ni marafiki wa Yesu, matendo yenu maovu yamejaza vyombo vya wale ambao ni wa karaha? Ingawa nyinyi mu karibu sana na Yehova, je, hamjui kwamba maneno yenu mabaya yamefikia masikio ya Yehova na kuchochea ghadhabu Yake? Ingekuwaje awe karibu nawe, na jinsi gani Yeye asingevichoma hivyo vyombo vyako, ambavyo vimejaa matendo mabaya? Ingekuwaje Asiwe adui wako?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Hakuna Aliye wa Mwili Anayeweza Kuepuka Siku ya Ghadhabu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 339)

Naona sasa mwili wako usiozuiwa ambao umenibembeleza Mimi, na Nina onyo kidogo tu kwako. Mimi bila shaka sichukui hatua kupitia kuadibu “kukutumikia” wewe. Unapaswa kujua ni wajibu gani ambao wewe huchukua katika kazi Yangu, na kisha Nitaridhika. Kuongezea kwa hili, ukinipinga Mimi au kutumia pesa Zangu, au kula sadaka za Mimi, Yehova, au ninyi mabuu mnaumana, au kuna ugomvi au kuingiliana kati ya ninyi viumbe mfano wa mbwa—Sihusiki na yoyote kati ya hayo. Mnahitaji tu kujua ninyi ni vitu vya aina gani, na Nitaridhika. Mbali na vitu hivi, ni sawa kama mko radhi kuvutiana panga au mikuki au kupigana kwa maneno yenu. Sina tamaa ya kuingilia mambo hayo, na Mimi sihusiki hata kidogo katika mambo ya binadamu. Sio kwamba Sijali kuhusu ugomvi kati yenu, lakini ni kwa sababu Mimi si mmoja wenu, hivyo, Sishiriki katika mambo yaliyo kati yenu. Mimi Mwenyewe si mmoja wa uumbaji na si wa dunia hii, kwa hiyo, Nachukia kabisa maisha ya kuharakisha miongoni mwa watu na hayo mahusiano yasiyofaa, yasiyofaa kati ya watu. Mimi hasa Nachukia kabisa hayo makundi ya makelele ya watu. Hata hivyo, Najua kwa kina uchafu ndani ya mioyo ya kila kiumbe, na kabla ya Mimi kuwaumba ninyi, Nilijua tayari udhalimu uliokuwepo ndani ya kina cha mioyo ya binadamu, na Niliujua udanganyifu na uhalifu wote katika mioyo ya binadamu. Kwa hiyo, hata ingawa hakuna kabisa dalili zozote wakati ambapo watu hufanya mambo ya udhalimu, bado Najua kwamba udhalimu uliowekwa ndani ya mioyo yenu hushinda utajiri wa vitu vyote Nilivyoumba. Kila mmoja wenu amepanda vilele vya juu zaidi vya umati; ninyi mmepanda kuwa mababu wa umati. Ninyi ni wadhalimu mno, na mnacharuka miongoni mwa mabuu wote, mkitafuta mahali pa amani na mkijaribu kuwameza mabuu walio wadogo kuwaliko ninyi. Ninyi ni wenye kijicho na wa husuda katika mioyo yenu, kuwashinda wale pepo ambao wamezama chini ya bahari. Mnaishi chini ya samadi, mkiwasumbua mabuu kutoka juu hadi chini ili wasiwe na amani, mkipigana wenyewe kwa wenyewe kwa muda mfupi na kisha kutulia. Ninyi hamjui hali yenu wenyewe, ilhali bado ninyi hupigana wenyewe kwa wenyewe ndani ya samadi. Ni nini ambacho mnaweza kupata kutokana na mapambano hayo? Kama ninyi kweli mngekuwa na moyo wa kunicha Mimi, mngewezaje kupigana wenyewe kwa wenyewe bila Mimi kujua? Haijalishi vile hali yako ilivyo juu, je, bado wewe si mnyoo mdogo mwenye uvundo ndani ya samadi? Utaweza kuota mbawa na kuwa njiwa angani? Ninyi, minyoo wadogo wenye uvundo mnaiba sadaka kutoka kwa madhabahu ya Mimi, Yehova; kwa kufanya hivyo, mnaweza kuokoa majina yenu yaliyoharibika, yenye kasoro kuwa wateule wa Israeli? Ninyi ni mafukara wasio na haya! Hizo sadaka juu ya madhabahu zilizotolewa Kwangu na watu, kuonyesha hisia karimu kutoka kwa wale ambao hunicha Mimi. Ni za udhibiti Wangu na za matumizi Yangu, kwa hiyo inawezekanaje wewe kuniibia Mimi hua wadogo waliotolewa na watu? Je, huogopi kuwa Yuda? Je, huogopi nchi yako kuwa “konde la damu”? Wewe kitu kisicho na haya! Unadhani kwamba hua waliotolewa na watu wote ni wa kustawisha tumbo la wewe buu? Kile ambacho Nimekupa ni kile ambacho Nimefurahia na kuwa radhi kukupa wewe; kile ambacho Sijakupa kiko chini ya Mamlaka Yangu, na huwezi tu kuiba sadaka Yangu. Yule Anayefanya kazi ni Mimi, Yehova—Bwana wa uumbaji, na sababu ya watu kutoa sadaka ni Mimi. Unadhani kwamba ni fidia ya kukimbia kila mahali ambako wewe hufanya? Wewe kwa kweli ni usiye haya! Ni nani ambaye unamkimbilia kila mahali? Je, si kwa ajili yako mwenyewe? Kwa nini wewe huiba sadaka Zangu? Kwa nini wewe huiba pesa kutoka kwa mfuko Wangu wa pesa? Je, wewe si mwana wa Yuda Iskariote? Sadaka Zangu, za Yehova, ni za kufurahiwa na makuhani. Je, wewe ni kuhani? Wewe huthubutu kula kwa kujisikia sadaka Zangu na hata unazitandaza juu ya meza; huna thamani yoyote! Wewe fukara asiye na thamani! Moto Wangu, wa Yehova, utakuteketeza wewe!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Majani Yaangukayo Yatakaporudi kwa Mizizi Yake, Utajuta Maovu Yote Ambayo Umefanya

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 340)

Imani yenu ni ya kupendeza sana; mnasema kwamba mko tayari kutumia maisha yenu yote kwa ajili ya kazi Yangu, na kwamba mko tayari kutoa maisha yenu kwa ajili ya kazi hiyo, lakini tabia zenu hazijabadilika sana. Mnazungumza tu kwa kiburi, licha ya ukweli kwamba tabia yenu halisi ni mbovu sana. Ni kana kwamba ndimi na midomo ya watu iko mbinguni lakini miguu yao iko chini duniani, na kwa sababu hiyo, maneno na matendo yao na sifa zao bado ni mbovu na zisizoheshimika. Sifa zenu zimeharibiwa, tabia yenu imepotoka, njia yenu ya kuzungumza ni duni, na maisha yenu ni yenye kustahili dharau; hata ubinadamu wenu wote umezama katika hali duni ya chini kabisa. Ninyi ni wenye mawazo finyu kuhusu wengine, na ninyi hubishana kuhusu kila jambo dogo. Ninyi hugombana kuhusu heshima na hadhi zenu wenyewe, hadi kufikia kiwango ambapo mko tayari kushuka kuzimuni na kuingia kwenye ziwa la moto. Maneno na matendo yenu ya sasa yanatosha Mimi kubaini kwamba ninyi ni wenye dhambi. Mitazamo yenu kwa kazi Yangu inatosha Mimi kubaini kuwa ninyi ni wadhalimu, na tabia zenu zote zinatosha kuonyesha kwamba ninyi ni watu wachafu mliojaa machukizo. Maonyesho yenu na kile mnachofichua vinatosha kusema kwamba ninyi ni watu ambao mmekunywa damu ya roho wachafu hadi mkatosheka. Kuingia katika ufalme kunapotajwa, hamfichui hisia zenu. Je, mnaamini ya kwamba jinsi mlivyo sasa inatosha kwa ninyi kupita katika lango la kuingia katika ufalme Wangu wa mbinguni? Je, mnaamini ya kwamba mnaweza kuingia katika nchi takatifu ya kazi na maneno Yangu, bila maneno na matendo yenu wenyewe kujaribiwa na Mimi kwanza? Ni nani anayeweza kunihadaa? Tabia na mazungumzo yenu yenye kustahili dharau na yaliyo duni yanaweza kuepukaje macho Yangu? Maisha yenu yamebainiwa na Mimi kuwa maisha ya kunywa damu na kula nyama ya roho hao wachafu kwa sababu ninyi huwaiga mbele Yangu kila siku. Mbele Yangu, tabia yenu imekuwa mbaya hasa, kwa hiyo Ninawezaje kukosa kuwaona kuwa wenye kuchukiza? Maneno yenu yana uchafu wa roho wachafu: Mnabembeleza, kuficha na kujipendekeza kama tu wale wanaoshiriki katika uchawi na kama wale walio wadanganyifu na wanaokunywa damu ya wadhalimu. Maonyesho yote ya mwanadamu ni dhalimu mno, kwa hivyo watu wote wanaweza kuwekwaje katika nchi takatifu ambako wenye haki wako? Je, unafikiri kwamba hiyo tabia yako yenye kustahili dharau inaweza kukubainisha kama mtakatifu ikilinganishwa na wale wadhalimu? Ulimi wako ulio kama wa nyoka hatimaye utauangamiza huu mwili wako ambao huleta uharibifu na kutekeleza machukizo, na hiyo mikono yako iliyojaa damu ya roho wachafu pia hatimaye itaipeleka roho yako jahannamu. Basi, kwa nini huipokei kwa furaha nyingi fursa hii ili uitakase mikono yako iliyojaa uchafu? Na kwa nini huchukui fursa hii kwa manufaa yako uukate huo ulimi wako unaozungumza maneno ya kudhulumu? Je, inawezekana kwamba uko tayari kuteseka katika moto wa jahannamu kwa ajili ya mikono, ulimi na midomo yako? Mimi huuchunga moyo wa kila mtu kwa macho yote mawili, kwa sababu muda mrefu kabla Niwaumbe wanadamu, Nilikuwa nimeifumbata mioyo yao mikononi Mwangu. Nilikuwa nimeibaini mioyo ya watu kitambo, kwa hiyo mawazo yao yangeyaepukaje macho Yangu? Muda utakosaje kuwa umewaishia wa kuepuka kuchomwa na Roho Wangu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ninyi Nyote Ni Waovu Sana Katika Tabia!

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 341)

Midomo yako ni mikarimu zaidi kuliko njiwa, lakini moyo wako ni mwovu zaidi kuliko yule nyoka wa zamani. Midomo yako ni ya kupendeza hata kama wanawake wa Lebanoni, lakini moyo wako si mwema zaidi kuliko yao, na hakika hauwezi kulinganishwa na uzuri wa Wakanaani. Moyo wako ni mdanganyifu mno! Vitu Ninavyochukia ni midomo na mioyo ya wadhalimu tu, na matakwa Yangu kwa watu si ya juu zaidi ya yale Ninayotarajia kutoka kwa watakatifu hata kidogo; ni kwamba tu Natiwa kinyaa kwa ajili ya matendo maovu ya wadhalimu, nami Natumai kwamba waweze kutupilia mbali uchafu wao na kutoroka kutoka katika hatari waliyomo sasa ili waweze kusimama kutoka kwa hao wadhalimu na wawe watakatifu na kuishi na wale ambao ni wenye haki. Ninyi mko katika hali sawa na Yangu, lakini mmejaa uchafu; hamna hata mfano kidogo zaidi wa asili wa wanadamu walioumbwa hapo mwanzo. Aidha, kwa sababu kila siku mnaiiga mifano ya hao roho wachafu, mkifanya kile wanachofanya na kusema kile wanachosema, kila sehemu yenu—hata ndimi na midomo yenu—imelowezwa katika maji yao machafu, kiasi kwamba mmejaa madoa kama hayo kabisa, na hakuna sehemu yenu hata moja inayoweza kutumika kwa ajili ya kazi Yangu. Ni jambo la kusikitisha sana! Mnaishi katika dunia ya farasi na ng’ombe kabisa, lakini kwa kweli hamhisi kufadhaishwa; mmejaa furaha na mnaishi kwa uhuru na bila matatizo. Mnaogelea huku na kule katika maji hayo machafu, lakini kwa kweli hamtambui ya kwamba mmeingia katika hatari kama hiyo. Kila siku, mnaandamana na roho wachafu na kuingiliana na “kinyesi.” Maisha yenu ni ya kishenzi sana, ilhali hujui kweli kwamba haupo katika ulimwengu wa wanadamu kabisa na kwamba hujidhibiti. Je, hujui kwamba maisha yako yalikandamizwa na roho hao wachafu zamani, au kwamba tabia yako ilishachafuliwa na maji machafu zamani? Je, unafikiri kwamba unaishi katika paradiso ya duniani, na kwamba uko katikati ya furaha? Je, hujui kwamba umeishi maisha pamoja na roho wachafu, na kwamba umeishi pamoja kwa amani na kila kitu ambacho wamekuandalia? Jinsi unavyoishi inawezaje kuwa na maana yoyote? Maisha yako yanawezaje kuwa na thamani yoyote? Umekuwa ukikimbia huku na kule kwa ajili ya wazazi wako, wazazi wa roho wachafu, lakini hujui kweli kuwa wale wanaokutega ni hao wazazi wa roho wachafu waliokuzaa na kukukela. Aidha, huna habari kwamba kweli ni wao ndio waliokupa uchafu wako wote; kile unachojua tu ni kwamba wanaweza kukuletea “furaha”, hawakuadibu, wala hawakuhukumu, na hususani hawakulaani. Hawajawahi kukulipukia kwa hasira, lakini wanakutendea kwa upendo na fadhila. Maneno yao huusitawisha moyo wako na kukuvutia sana kiasi kwamba unakanganyikiwa, na bila kutambua, unafyonzwa na unakuwa tayari kuwahudumia, ukigeuka kuwa njia yao ya kutoka na kuwa mtumishi wao. Huna malalamiko hata kidogo, bali uko tayari kuwafanyia kazi kama mbwa, kama farasi; unadanganywa na wao. Kwa sababu hii, huna majibu yoyote kabisa kwa kazi Ninayoifanya. Si ajabu kwamba kila wakati wewe hutaka kuponyoka kutoka Kwangu kwa siri, na si ajabu kwamba kila wakati wewe hutaka kutumia maneno matamu kupata kibali kutoka Kwangu kwa njia danganyifu. Kama inavyotokea, tayari ulikuwa na mpango mwingine, na mpangilio mwingine. Unaweza kuona matendo Yangu kidogo kama mwenye Uweza, lakini huna ufahamu hata kidogo kuhusu hukumu na kuadibu Kwangu. Hujui kuadibu Kwangu kulianza lini; unajua tu jinsi ya kunidanganya—lakini hujui kwamba Sitastahimili ukiukaji wowote kutoka kwa mwanadamu. Kwa kuwa tayari umeweka uamuzi wako kunitumikia Mimi, sitakuacha uende. Mimi ni Mungu anayechukia uovu, na Mimi ni Mungu ambaye ana wivu kwa mwanadamu. Kwa kuwa tayari umewekelea maneno yako juu ya madhabahu, Sitakuvumilia wewe kuhudumia mabwana wawili. Je, ulifikiri ungepata upendo mwingine baada ya kuweka maneno yako juu ya madhabahu Yangu, baada ya kuyaweka mbele ya macho Yangu? Ningewezaje kuwaruhusu watu kunidanganya Mimi kwa njia hiyo? Je, ulidhani kwamba ungeweza kuweka nadhiri kikawaida, kula kiapo Kwangu Mimi na ulimi wako? Je, ungewezaje kula kiapo kwa kiti Changu cha enzi, Aliye Juu Zaidi? Je, ulifikiri kwamba viapo vyako vilikuwa tayari vimekufa? Nawaambia, hata kama miili yenu ikifa, viapo vyenu haviwezi kufa. Hatimaye, Nitawahukumu kwa msingi wa viapo vyenu. Lakini mnadhani kwamba mnaweza kuweka maneno yenu mbele Yangu ili kunivumilia Mimi na kwamba mioyo yenu inaweza kuwatumikia pepo wachafu na pepo wabaya. Je, hasira Yangu ingewezaje kuwavumilia hao watu mithili ya mbwa na nguruwe wanaonidanganya? Lazima Nitekeleze amri Zangu za kiutawala, na kuwapokonya kutoka kwa mikono ya pepo wachafu wale wote wenye fukuto, “wacha Mungu” ambao wanaamini katika Mimi “kunitumikia” Mimi kwa njia ya mpango, kuwa ng’ombe Wangu, kuwa farasi Wangu na kudhibitiwa na Mimi. Nitakufanya ushike uamuzi wako wa awali na kunitumikia Mimi tena. Siwezi kuvumilia kiumbe yeyote kunidanganya Mimi. Je, ulifikiria kwamba ungeweza kufanya maombi tu kiutukutu na kudanganya kiutukutu mbele Yangu? Je, ulifikiri kwamba Mimi sikuwa nimesikia au kuona maneno na matendo yako? Je, maneno yako na matendo yako yangekosaje kuwa katika mtazamo Wangu? Ningewezaje kuwaruhusu watu kunidanganya Mimi kwa njia hiyo?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ninyi Nyote Ni Waovu Sana Katika Tabia!

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 342)

Nimekuwa miongoni mwenu, Nimeshirikiana nanyi kwa majira kadhaa ya kuchipua na kwa majira kadhaa ya kupukutika, Nimeishi kati yenu kwa muda mrefu—ni kiasi gani cha tabia yenu ya kudharaulika kimeponyoka mbele ya macho Yangu? Maneno yenu hayo ya dhati daima yarudisha mwangwi ndani ya masikio Yangu; mamilioni na mamilioni ya matarajio yenu yamewekwa juu ya madhabahu Yangu—hayawezi hata kuhesabiwa. Lakini kwa kujitolea kwako na kile mnachokitumia, hakuna hata kidogo. Hakuna hata tone dogo la uaminifu wenu kwenye madhabahu Yangu. Yako wapi matunda ya imani yenu Kwangu? Mmepokea neema isiyo na mwisho kutoka Kwangu na mmeona mafumbo yasiyo na mwisho kutoka mbinguni, na Nimewaonyesha hata miale ya mbinguni lakini Sijawahi kuwa na moyo wa kuwachoma, na ni kiasi gani mmenipa Mimi kama malipo? Je, mko radhi kunipa Mimi kiasi gani? Kama umeshikilia chakula Nilichokupa, unageuka na kunitolea Mimi, hata ukisema kuwa ni kitu ambacho umepata kama malipo kwa jasho la kazi yako ngumu, kwamba unatoa yote uliyo nayo Kwangu. Je, unawezaje kukosa kujua kwamba “michango” yako Kwangu ni vitu vyote vilivyoibwa kutoka kwa madhabahu Yangu? Na sasa unavitoa Kwangu—si wewe unanidanganya Mimi? Unawezaje kukosa kujua kuwa vitu Ninavyovifurahia leo ni matoleo yote juu ya madhabahu Yangu, na sicho kile ulichokichuma kama malipo ya kazi yako ngumu halafu ukanitolea Mimi? Kwa kweli mnathubutu kunidanganya Mimi kwa njia hii, kwa hiyo ni kwa jinsi gani Ninaweza kuwasamehe? Ninawezaje kuvumilia hili zaidi? Nimewapa kila kitu. Nimewafungulia kila kitu, Nikakimu mahitaji yenu, na kuyafungua macho yenu, lakini bado mnanidanganya Mimi kwa njia hii, mkipuuza dhamiri yenu. Bila ubinafsi Nimewapa kila kitu, ili kwamba hata kama mnateseka, mmepata kutoka Kwangu kila kitu Nilichokileta kutoka mbinguni. Lakini hamna kujitolea kamwe, na hata kama mna mchango mdogo, mnalipa deni baada ya hapo. Je, si mchango wako utakuwa bure? Kile ambacho umenipa si chochote isipokuwa chembe moja ya mchanga, lakini kile ulichouliza kutoka Kwangu ni tani moja ya dhahabu. Je, si wewe unakuwa muhali? Ninafanya kazi miongoni mwenu. Hakuna kabisa dalili ya asilimia kumi ambayo Ninapaswa kupata, sembuse dhabihu za ziada. Zaidi ya hayo, asilimia kumi inayochangwa na wale ambao ni wacha Mungu inachukuliwa na wale waovu. Je, si nyinyi wote mmetawanyika kutoka Kwangu? Je, si nyinyi nyote mna uhasama na Mimi? Je, si nyinyi nyote mnaharibu madhabahu Yangu? Je, mtu wa aina hii anawezaje kuonekana kama hazina machoni Pangu? Je, si yeye ni nguruwe, mbwa ambao Ninawachukia? Ningewezaje kurejelea uovu wenu kama hazina? Kazi Yangu kwa kweli ni ya nani? Inawezekana kuwa tu ni ya kuwapiga nyinyi nyote ili kufichua mamlaka Yangu? Je, si maisha yenu yameshikiliwa na neno moja kutoka Kwangu? Ni kwa nini Ninatumia maneno tu kuwaagiza na Sijayageuza maneno kuwa ukweli ili kuwapiga haraka iwezekanavyo? Je, maneno Yangu na kazi Yangu ni ya kuwapiga wanadamu tu? Je, Mimi ni Mungu ambaye huwaua wasio na hatia bila ubaguzi? Hivi sasa, ni wangapi wenu ambao wako hapo mbele Yangu ambao wanatafuta njia sahihi ya maisha ya mwanadamu na nafsi zao nzima? Ni miili yenu tu iliyo mbele Yangu, lakini mioyo yenu iko huru, na iko mbali, mbali na Mimi. Kwa sababu hamjui kwa kweli kazi Yangu ni nini, kuna baadhi yenu ambao mnataka kuondoka Kwangu, mnaojitenga na Mimi, na mnataka kuishi katika mahali hapo pa raha ambapo hakuna kuadibu, hakuna hukumu. Je, hili ndilo watu wanatamani katika mioyo yao? Mimi hakika sikulazimishi. Njia yoyote utakayoichukua ni uchaguzi wako mwenyewe, na njia ya leo huenda sambamba na hukumu na laana, lakini nyote mnapaswa kujua kwamba kile Niliyowapa, iwe ni hukumu au kuadibu, zote ni zawadi bora kabisa Ninazoweza kuwapa, na vyote ni vitu ambavyo mnahitaji kwa dharura.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ninyi Nyote Ni Waovu Sana Katika Tabia!

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 343)

Nimetekeleza kazi nyingi sana duniani na Nimetembea kati ya wanadamu kwa miaka mingi sana. Ilhali watu kwa nadra sana huwa na ufahamu wa sura Yangu na tabia Yangu, na watu wachache wanaweza kuelezea kikamilifu kazi Ninayofanya. Watu wanakosa mengi sana, daima wanakosa ufahamu wa kile Ninachokifanya, na mioyo yao daima iko tayari kana kwamba wanaogopa sana Nitawaleta katika hali nyingine na kisha kuwapuuza. Kwa hivyo, mtazamo wa watu Kwangu daima ni vuvuwaa pamoja na tahadhari kubwa sana. Hili ni kwa sababu watu wamekuja kwa wakati wa sasa bila kuelewa kazi Ninayofanya, na wao hasa hukanganywa na maneno ambayo Ninawaambia. Wao huyabeba maneno Yangu mikononi mwao, wasijue kama wanapaswa kujitahidi kuamini au kama wanapaswa kuyasahau kwa shaka. Hawajui kama wanapaswa kuyatia katika vitendo, au kama wanapaswa kungoja kuona. Hawajui kama wanapaswa kuachana na kila kitu na kisha kufuata kwa ujasiri, au kama wanapaswa kuendelea kuwa wa kirafiki na ulimwengu kama hapo awali. Ulimwengu wa ndani wa watu ni wenye utata sana, na wao ni wajanja sana. Kwa sababu watu hawawezi kuyaona kwa dhahiri maneno Yangu na hawawezi kuyaona kikamilifu, wengi wao wana wakati mgumu kuyatenda, na wana shida kuweka moyo wao mbele Yangu. Ninayaelewa kwa kina matatizo yenu. Udhaifu mwingi hauepukiki wakati mtu anapoishi ndani ya mwili, na vipengele vingi ya kuhusu mambo huwaletea shida. Mnalisha familia zenu, mnatumia siku zenu mkifanya kazi kwa bidii, na wakati hupita vigumu. Kuna shida nyingi za kuishi katika mwili—Sikatai hili, na bila shaka mahitaji Yangu kwenu yanalingana na shida zenu. Mahitaji katika kazi Ninayofanya yote yana msingi katika kimo chenu halisi. Labda wakati watu walipokuwa wakifanya kazi zamani mahitaji yao kwenu yalichanganywa na dalili za uziada, lakini mnapaswa kujua kwamba Sijawahi kuwa na mahitaji ya ziada kwenu katika yale Ninayosema na kutenda. Yote yanahitajika kulingana na asili ya watu, mwili, na kile wanachohitaji. Mnapaswa kujua, na Naweza kuwaambia kwa dhahiri sana, kwamba Sikupingi kufikiria fulani kwa maana kwa watu na Sipingi asili ya kimaumbile ya binadamu. Ni tu kwa sababu watu hawaelewi kwa kweli kile kilicho kiwango cha mahitaji Yangu kwao, wala hawaelewi maana ya asili ya maneno Yangu ambayo hadi sasa, watu bado wana wasiwasi na maneno Yangu, na hata chini ya nusu ya watu huyaamini maneno Yangu. Waliosalia ni wasioamini, na hata zaidi ni wale wanaopenda kunisikia “Nikisimulia hadithi.” Aidha, kuna wengi ambao hufurahia tukio hilo. Ninawapa onyo: Maneno Yangu mengi tayari yamefunguliwa kwa wale wanaoniamini Mimi, na wale ambao wanafurahia mandhari mazuri ya ufalme lakini wamefungiwa nje ya lango lake tayari wameondolewa na Mimi. Je, nyinyi si magugu tu ambavyo yamechukiwa na kukataliwa na Mimi? Je, Mngeniaga vipi na kisha kukaribisha kurudi Kwangu kwa furaha? Nawaambieni, baada ya watu wa Ninawi kusikia maneno ya hasira ya Yehova, mara moja walitubu kwa magunia na majivu. Ilikuwa kwa sababu waliyaamini maneno Yake kwamba walijawa na woga na hofu na wakatubu kwa magunia na majivu. Na ingawa watu wa leo pia wanaamini maneno Yangu na hata zaidi kuamini kuwa Yehova amekuja tena kati yenu leo, mtazamo wenu sio chochote ila usioheshimu vitu vitakatifu, kana kwamba mnamwangalia tu Yesu aliyezaliwa Yudea maelfu kadhaa ya miaka iliyopita na sasa Ameshuka katikati yenu. Ninaelewa kabisa udanganyifu ulio ndani ya mioyo yenu; wengi wenu hunifuata kutokana na udadisi na mmekuja kunitafuta kutokana na utupu. Wakati matakwa yenu ya tatu yanavunjwavunjwa—kwa ajili ya maisha ya amani na yenye furaha—udadisi wenu pia unatapanywa. Udanganyifu ulio ndani ya mioyo ya kila mmoja wenu wote hufunuliwa kupitia maneno na matendo yenu. Kusema kweli, nyinyi mnataka tu kujua kunihusu, hamwogopi; hamjali matamshi yenu, na mnazuia tabia zenu hata mara chache zaidi. Basi imani yenu iko vipi kwa kweli? Je, ni ya kweli? Mnatumia tu maneno Yangu kuondoa wasiwasi wenu na kupunguza uchoshi wenu, ili kujaza nafasi zilizobaki tupu katika maisha yako. Ni nani miongoni mwenu ambaye ameyatia katika vitendo? Nani ana imani ya kweli? Mnaendelea kupiga kelele kwamba Mungu ni Mungu ambaye huona ndani kabisa ya mioyo ya watu, lakini ni vipi Mungu mnayepiga kelele kuhusu mioyoni mwenu analingana na Mimi? Kwa kuwa mnapiga kelele kwa njia hii, basi kwa nini mnatenda kwa njia ile? Inawezea kuwa kwamba huu ndio upendo mnaotaka kunilipizia nao? Hakuna kiasi kidogo cha upendo kwenye midomo yenu, lakini ziko wapi dhabihu zenu, na matendo yenu mema? Isingalikua maneno yenu kuyafikia masikio Yangu, Ningaliwezaje kuwachukia sana? Ikiwa kweli mliniaminia, mngewezaje kuangukia hali kama hii ya dhiki? Mnazo sura za huzuni kwenye nyuso zenu kana kwamba mko kuzimu mkishtakiwa. Hamna uhai wowote, na mnanena kuhusu sauti yenu ya ndani kwa udhaifu; mmejawa hata na malalamiko na laana. Mlipoteza imani katika yale Nifanyayo zamani na hata imani yenu ya asili imepotea, basi mnawezaje kufuata mpaka mwisho? Mnawezaje kuokolewa kwa njia hii?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno kwa Vijana na kwa Wazee

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 344)

Ingawa kazi Yangu ni yenye msaada mkubwa kwenu sana, maneno Yangu daima hushindwa kuwashawishi na kutofanikiwa ndani yenu. Ni vigumu kupata chombo cha kukamilishwa na Mimi na leo karibu Nimepoteza tumaini kwenu. Nimetafuta kati yenu kwa miaka kadhaa lakini ni vigumu kupata msiri. Ninahisi kama Sina imani ya kuendelea kufanya kazi ndani yenu, na Sina upendo kuendelea kuwapenda. Hili ni kwa sababu Nilikuwa Nimechukizwa kitambo na yale mafanikio yenu madogo ya kusikitisha; ni kana kwamba Sikuwahi kuzungumza kati yenu na Sikuwahi kufanya kazi ndani yenu. Mafanikio yenu yanachafua moyo sana—daima mmetiwa fedheha na karibu hamna thamani yoyote. Kwa nadra Ninapata mfano wa mwanadamu ndani yenu au kusikia harufu ya mwanadamu. Iko wapi harufu yenu mpya? Iko wapi gharama ambayo mmelipa kwa miaka mingi, na matokeo yako wapi? Hamjawahi kuyapata? Kazi Yangu sasa ina asili mpya, mwanzo mpya. Ninaenda kutekeleza mipango mikubwa na Ninataka kutekeleza kazi kubwa, ilhali bado mnavingirika katika matope kama hapo awali, kuishi katika maji machafu ya zamani, na kwa utendaji hamjatupa mashaka yenu ya awali. Kwa hivyo, bado hamjapata chochote kutoka kwa maneno Yangu. Bado hamjatupa pahali penu pa awali pa matope na maji machafu, na mnayajua maneno Yangu tu, lakini kwa kweli hamjaingia katika eneo la uhuru wa maneno Yangu, hivyo maneno Yangu hayajawahi kufunguliwa kwenu, na yako kama kitabu cha unabii ambacho kimefungwa kwa maelfu ya miaka. Ninaonekana kwenu katika maisha yenu lakini daima hamjui, na hamnitambui hata. Takriban nusu ya maneno Ninayoyasema ni hukumu ya nyinyi, na hayo hufanikisha tu nusu ya athari ambayo yanapaswa kufanikisha, ambayo ni kutia hofu kuu ndano yenu. Nusu iliyobaki ni maneno ya kuwafundisha kuhusu maisha na jinsi ya kutenda, lakini ni kana kwamba hayapo kwenu, na kana kwamba nyinyi mnasikiliza maneno ya watoto wanaocheza, ambayo daima nyinyi huyatolea tabasamu iliyofichwa, na kisha hakuna kitu kinachofanywa. Hamjawahi kujishughulisha na mambo haya; daima mmefuata matendo Yangu kutokana na udadisi wenu ili kwamba sasa mmeanguka gizani na hamwezi kuuona mwanga—mnalia kwa huruma gizani. Kile Ninachotaka ni utiifu wenu, utiifu wenu usio na masharti na hata zaidi, Nahitaji kwamba muwe na hakika kabisa juu ya kila kitu Ninachosema. Hampaswi kukubali mtazamo wa kutokujali na hasa hampaswi kuuvumilia kwa kuchagua, ni wazi kwamba nyinyi daima hamjali maneno Yangu na kazi Yangu. Kazi Yangu inafanywa katikati yenu na Nimewapa maneno Yangu mengi, lakini mkinilaghai kwa njia hii, Ninaweza tu kutoa bure kile ambacho hamjapata na hamjatia katika vitendo kwa familia za Mataifa. Ni nini kati ya uumbaji hakipo mikononi Mwangu? Wengi wa wale kati yenu ni wa “wa miaka mingi sana” na hamna nguvu ya kukubali aina hii ya kazi Yangu. Nyinyi ni kama ndege wa Hanhao[a], mnaishi kwa shida, na hamjawahi kuyachukulia maneno Yangu kwa uzito. Vijana ni bure sana na wanajifurahisha sana na hata zaidi wanaipuuza kazi Yangu. Hawahisi kufurahia vyakula vitamu vya karamu Yangu; Wao ni kama ndege mdogo ambaye ameruka nje ya tundu lake kwenda mbali kabisa. Je, wazee na vijana wa aina hii wanawezaje kuwa na manufaa Kwangu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno kwa Vijana na kwa Wazee

Tanbihi:

a. Hadithi ya ndege wa Hanhao inafanana sana na hekaya ya Aesop ya mchwa na panzi. Ndege wa Hanhao hupenda zaidi kulala kuliko kujenga kiota wakati hali ya hewa ni ya vuguvugu, licha ya onyo la marudio kutoka kwa jirani wake, ndege wa jamii ya kunguru. Wakati majira ya baridi hufika, ndege huyo huganda hadi kifo.

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 345)

Ingawa nyinyi vijana wote ni kama simba wachanga, kwa nadra mnakuwa na njia ya kweli mioyoni mwenu. Ujana wenu hauwezi kuwapa nafasi ya kupata kazi Yangu zaidi; kinyume na hilo, daima nyinyi husababisha chuki Yangu kwenu. Ingawa nyinyi ni wachanga, ama mnakosa uhai au hamna tamaa ya makuu, daima nyinyi hamjihusishi na siku zenu zijazo; ni kana kwamba hamjali, na pia mnawaza sana. Ingeweza kusemwa kuwa uchangamfu, maadili, na msimamo yanayochukuliwa ambayo yanapaswa kupatikana kwa vijana hayawezi kabisa kupatikana kwenu; nyinyi, vijana wa aina hii, mnakosa msimamo na hamna uwezo wa kutofautisha kati ya sahihi na isiyo sahihi, mema na maovu, mazuri na mabaya. Haiwezekani kupata dalili zozote zenu ambazo ni mpya. Nyinyi karibu mmepitwa na wakati kabisa, na nyinyi, vijana wa aina hii, pia mmejifunza kukubali tu, kuwa bila mantiki. Hamwezi kamwe kutofautisha kwa dhahiri mazuri kutoka kwa mabaya, hamwezi kutofautisha kati ya ukweli na uongo katika masuala, kamwe hamjitahidi kupata ubora, wala hamwezi kusema nini ni sahihi na nini si sahihi, nini ni ukweli, na nini ni unafiki. Ndani yenu kunabakia mipulizo ya ghafla ya dini hata zaidi na hata mikubwa zaidi kuliko kwa watu wazee. Nyinyi hata ni wenye kiburi na msio na busara, nyinyi ni wa ushindani, na kupenda kwenu uchokozi ni mzito sana—kijana wa aina hii anawezaje kumiliki ukweli? Mtu asiyeweza kuchukua msimamo anawezaje kushuhudia? Mtu asiye na uwezo wa kutofautisha kati ya yaliyo sahihi na yasiyo sahihi anawezaje kuitwa kijana? Mtu asiye na uhai, nguvu, utulivu, ubichi, utulivu na udhabiti wa kijana anawezaje kuitwa mfuasi Wangu? Mtu asiye na ukweli wowote wala hisia ya haki, lakini hupenda kucheza na kupigana anawezaje kufaa kuwa shahidi Wangu? Macho ambayo yamejaa uongo na chuki bila sababu kwa watu siyo wanayopaswa kuwa nayo vijana, na wale wanaotekeleza vitendo vya uharibifu, vinavyochukiza mno hawapaswi kuwa vijana. Hawapaswi kuwa bila maadili, matarajio, au tabia ya maendeleo ya shauku; hawapaswi kuvunjika moyo juu ya matarajio yao wala hawapaswi kupoteza matumaini maishani au kupoteza imani katika siku zijazo; wanapaswa kuwa na uvumilivu kuendelea na njia ya ukweli ambayo sasa wamechagua kufanikisha matamanio yao ya kutumia maisha yao yote kwa ajili Yangu; hawapaswi kuwa bila ukweli, wala kuficha unafiki na udhalimu, bali wanapaswa kusimama imara katika msimamo unaofaa. Hawapaswi tu kuzurura, bali wanapaswa kuwa na roho ya kuthubutu kujitolea mhanga na kujitahidi kwa ajili ya haki na ukweli. Vijana wanapaswa kuwa na ujasiri wa kutoshindwa na ukandamizaji wa nguvu za giza na kubadili umuhimu wa uwepo wao. Vijana hawapaswi kukubali shida bila kulalamika, bali wanapaswa wawe wazi na wa kusema bila kuficha, na roho ya msamaha kwa ndugu wao. Bila shaka haya ni mahitaji Yangu ya kila mtu pamoja na ushauri Wangu kwa kila mtu. Hata zaidi, ni maneno Yangu ya kutuliza kwa vijana wote. Mnapaswa kutenda kulingana na maneno Yangu. Hasa vijana hawapaswi kuwa bila azimio la utambuzi katika masuala, na la kutafuta haki na ukweli. Yale mnayopaswa kufuata ni mambo yote mazuri na mema, na mnapaswa kupata uhalisi wa mambo yote mazuri, na pia kuwajibika juu yaa maisha yenu—hampaswi kuyachukulia kwa wepesi. Watu huja duniani na ni nadra kupatana na Mimi, na pia ni nadra kuwa na fursa ya kutafuta na kupata ukweli. Kwa nini msithamini wakati huu mzuri kama njia sahihi ya kutafuta katika maisha haya? Na ni kwa nini daima nyinyi hupuuza sana ukweli na haki? Kwa nini daima nyinyi hujikanyaga na kujiangamiza kwa ajili ya ule udhalimu na uchafu ambao huchezea watu? Na kwa nini mnajishughulisha na kile ambacho wadhalimu hufanya kama watu wazee? Kwa nini mnaiga njia za zamani za mambo ya kale? Maisha yenu yanapaswa kujaa haki, ukweli, na utakatifu; maisha yenu hayapaswi kupotoshwa katika umri mdogo hivyo, yakiwasababisha kuanguka kuzimuni. Je, hamhisi kwamba hili ni la kusikitisha sana? Je, hamhisi kwamba hili silo haki kwenu sana?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno kwa Vijana na kwa Wazee

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 346)

Ikiwa kazi nyingi, na maneno mengi, hayajakuwa na mabadiliko kwako, basi wakati utakapofika wa kueneza kazi ya Mungu hutaweza kufanya kazi yako, na utaaibika na kufedheheshwa. Wakati huo utajisikia kuwa una deni kubwa kwa Mungu, kwamba maarifa yako juu ya Mungu ni juujuu. Usipofuata maarifa ya Mungu leo, Akiwa bado Anafanya kazi, basi baadaye itakuwa umechelewa. Mwishowe hutakuwa na maarifa yoyote ya kuongelea—utawachwa tupu, bila chochote. Ni nini utakachotumia kupeana uwajibikaji wako kwa Mungu? Je, una uchungu kuangalia Mungu? Unafaa kujitahidi katika shughuli yako sasa, ili mwishowe uweze, kama, Petro, kujua jinsi adabu na hukumu ya Mungu ina manufaa kwa binadamu, na bila adabu na hukumu Yake mwanadamu hawezi kuokolewa, na atazidi kuzama kwenye ardhi chafu, ndani zaidi kwenye tope. Wanadamu wamepotoshwa na Shetani, wamefitini wenyewe kwa wenyewe, wamekuliana njama wenyewe kwa wenyewe, wamepoteza heshima yao kwa Mungu, na uasi wao ni mkubwa sana, fikira zao ni nyingi, na wote ni wa Shetani. Bila adabu na hukumu ya Mungu, tabia potovu ya mwanadamu haiwezi kutakaswa na hangeweza kuokolewa. Kinachoelezwa na Mungu anayefanya kazi katika mwili hasa ndicho kile kinachoelezwa na Roho, na kazi afanyayo inafanyika kulingana na ile ifanywayo na Roho. Leo, kama huna maarifa yoyote juu ya hii kazi, basi wewe ni mpumbavu sana, na umepoteza mengi! Kama hujapata wokovu wa Mungu, basi imani yako ni ya kidini, na wewe ni Mkristo wa dini. Kwa sababu umeshikilia mafundisho yaliyokufa, umepoteza kazi mpya ya Roho Mtakatifu; wengine, wanaofuata upendo wa Mungu, wanaweza kupata ukweli na uhai, ambapo imani yako haiwezi kupata idhini ya Mungu. Badala yake, umekuwa mtenda maovu, mtu afanyaye vitendo vyenye kuharibu na vya chuki, umekuwa kilele cha utani wa Shetani, na mfungwa wa Shetani. Mungu si wa kuaminiwa na mwanadamu, lakini wa kupendwa na yeye, na kufuatwa na kuabudiwa na yeye. Usipomfuata leo, basi siku itakuja ambapo utasema, “Hapo zamani mbona sikumfuata Mungu vizuri sikumridhisha vizuri, sikufuatilia mabadiliko katika tabia yangu ya maisha? Najuta kutojiwasilisha kwa Mungu kwa wakati ufaao, na kutotafuta maarifa ya neno la Mungu. Mungu alisema mengi wakati ule; nilikosa vipi kufuata? Nilikuwa mjinga!” Utajichukia mpaka kiwango fulani. Leo, huamini maneno ninayosema, na huyatilii maanani; wakati utakapofika kwa hii kazi kuenezwa, na unaona ukamilifu wake, utajuta, na wakati huo utakuwa bubu. Kuna baraka, ilhali hujui kuzifurahia, na kuna ukweli, ilhali hujui kuufuata. Je, hujiletei dharau? Leo ingawa hatua inayofuata kwa kazi ya Mungu haijaanza, hakuna kitu cha kipekee juu ya mahitaji yanayohitajika kwako na unachoulizwa kuishi kwa kudhihirisha. Kuna kazi nyingi, na ukweli mwingi; Je, hazina maana kujulikana na wewe? Je, adabu na hukumu ya Mungu haitoshi kuamsha roho yako? Je, adabu na hukumu ya Mungu haitoshi kukufanya ujichukie? Umetosheka kuishi katika ushawishi wa Shetani, kwa amani na furaha, na raha kidogo ya kimwili? Je, wewe si mtu wa chini zaidi kati ya watu wote? Hakuna aliye mpumbavu kuliko wale ambao wameona wokovu lakini hawaufuati ili kuupata; hawa ni watu ambao wanalafua mwili na kufurahia Shetani. Unatumai kwamba imani yako kwa Mungu haitakuwa na changamoto ama dhiki, ama mateso yoyote. Unafuata vile vitu ambavyo havina maana, na huambatanishi faida yoyote kwa maisha, badala yake kuweka mawazo ya fujo kabla ya ukweli. Huna maana! Unaishi kama nguruwe—kuna tofauti gani kati yako, nguruwe na mbwa? Je, hao wasiofuata ukweli na badala yake wanafuata mapenzi ya kimwili, si wote ni wanyama? Hao waliokufa na bila roho si wafu wanaotembea? Maneno mangapi yamenenwa kati yenu? Je, kazi kidogo imefanywa kati yenu? Ni kiasi gani nimetoa kati yenu? Na mbona hujapata chochote? Una nini cha kulalamikia? Je, si ni kweli kuwa hujapata chochote kwa sababu unapenda mwili sana? Na ni kwa sababu mawazo yako ni ya fujo sana? Je, si kwa sababu wewe ni mpumbavu sana? Kama huna uwezo wa kupata baraka hizi, unaweza kumlaumu Mungu kwa kutokukuokoa? Unachofuata ni cha kukuwezesha kupata amani baada ya kumwamini Mungu—watoto wako wawe huru kutokana na magonjwa, ili mme wako apate kazi nzuri, ili mwana wako apate mke mwema, binti wako apate mme anayeheshimika, ili ndume na farasi wako walime shamba vizuri, kwa mwaka wa hali ya anga nzuri kwa mimea yako. Hili ndilo unalolitafuta. Harakati yako ni kuishi kwa starehe, ili ajali isipate familia yako, ili upepo ukupite, ili uso wako usiguswe na changarawe, ili mazao ya familia yako yasipate mafuriko, ili usiguswe na majanga yoyote, kuishi katika mikono ya Mungu, kuishi kwenye kiota chenye joto. Mwoga kama wewe, anafuata mwili kila wakati—je, una moyo, una roho? Si wewe ni mnyama? Nakupa njia ya ukweli bila kukuuliza chochote, ilhali hauifuati. Je, wewe ni wale wamwaminio Mungu? Nahifadhi uhai wa ukweli wa binadamu juu yako, ila hauufuati. Je, una tofauti kati ya nguruwe na mbwa? Nguruwe hawafuati maisha ya binadamu, hawafuati kutakaswa, na hawaelewi maana ya maisha. Kila siku wanapokula na kushiba, wanalala. Nimekupa njia ya ukweli, ila hujaipata: Wewe u mkono mtupu. Je, unakubali kuendelea na maisha haya, maisha ya nguruwe? Umuhimu wa watu hao kuwa hai ni nini? Maisha yako ni ya kudharauliwa na kutoheshimika, unaishi huku ukiwa na uchafu na uzinzi, na hufuati lengo lolote; je, si maisha yako ni ya kutoheshimika kwa yote? Je, una ujasiri wa kumtazamia Mungu? Ukiendelea kuwa na uzoefu wa haya, je, si utakosa kupata chochote? Umepewa njia ya ukweli, lakini kama utaipata ama hapana inategemea na kutafuta kwako.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 347)

Miili yenu, matamanio yenu ya kupita kiasi, ulafi wenu, na ashiki yenu vyote vimekita mizizi ndani yenu. Mambo haya yanaidhibiti sana mioyo yenu kiasi kwamba hamna nguvu za kutupa huo utumwa wa mawazo hayo ya kikabaila na yaliyooza. Hamtamani kubadilisha hali yenu ya sasa, wala kuukimbia ushawishi wa giza. Mmefanywa kuwa watumwa tu wa mambo hayo. Hata kama mnajua kwamba maisha kama hayo ni yenye maumivu sana na kwamba ulimwengu kama huo ni wenye giza la kupindukia, bado, hakuna hata mmoja wenu anao ujasiri wa kubadilisha maisha ya aina hii. Mnatamani tu kutoroka aina hii ya maisha halisi, kuondoa nafsi zenu kutoka kwenye mahali pa mateso ya muda na kuishi katika mazingira yenye amani, furaha na yafananayo na mbinguni. Hamko radhi kuvumilia magumu ili kuweza kubadilisha maisha yenu ya sasa; vilevile hamko radhi kutafuta ndani ya hukumu hii na kuadibu huku maisha ambayo mnafaa kuyaishi. Badala yake, mnaziota ndoto zisizo na uhalisi kabisa kuhusu ulimwengu mzuri wa nje ya miili yenu. Maisha mnayotamani ni yale mnayoweza kupata kwa urahisi bila kupitia maumivu yoyote. Hayo si ya kihalisi kamwe! Kwa sababu kile mnachotumainia si kuishi kwa kudhihirisha maisha ya maana katika mwili na kupata ukweli kwenye harakati ya maisha yenu, yaani, kuishi kwa ajili ya ukweli na kutetea haki. Haya siyo yale maisha ambayo mngedhani ni ya kupendeza, ya kusisimua. Mnahisi kwamba haya hayatakuwa maisha yanayovutia au ya maana. Machoni mwenu, kuishi maisha kama hayo kutatoa hisia za kudhalilishwa! Hata Ingawa mnakubali kuadibu huku leo, hata hivyo kile mnachofuatilia si kupata ule ukweli au kuishi kwa njia ya ukweli katika wakati wa sasa, bali kuweza kuingia katika maisha yenye furaha nje ya miili yenu baadaye. Hamtafuti ukweli wala hamtetei ukweli, wala hamtetei ukweli na bila shaka hampo kwa ajili ya kweli. Hamtafuti kuingia leo, lakini badala yake kila wakati mnafikiria “siku moja,” huku mkitazama mbingu ya samawati na kudondokwa na machozi machungu, na mkitarajia kuchukuliwa kuenda mbinguni siku moja. Je, hamjui kwamba kufikiria huku kama kwenu tayari kumeondokwa na uhalisi? Unaendelea kufikiria kwamba Mwokozi mwenye upole na huruma isiyoisha bila shaka atakuja siku moja kukuchukua pamoja na Yeye, wewe ambaye umevumilia ugumu na mateso ulimwenguni humu, na kwamba Yeye bila shaka atalipiza kisasi kwa ajili yako wewe ambaye umedhalilishwa na kunyanyaswa. Je, si kweli kwamba umejaa dhambi? Wewe pekee ndiwe ambaye umeteseka ulimwenguni humu? Umemilikiwa na Shetani wewe mwenyewe na kuteseka—je, bado Mungu anahitaji kukulipizia kisasi? Wale wasioweza kutosheleza mahitaji ya Mungu—kwani wao wote si adui wa Mungu? Wale wasioamini katika Mungu mwenye mwili—kwani wao si wapinga Kristo? Matendo yako mazuri yana maana gani? Yanaweza kuchukua nafasi ya moyo unaomwabudu Mungu? Huwezi kupokea baraka za Mungu kwa kufanya baadhi ya matendo mazuri tu, naye Mungu hatakulipizia kisasi yale mabaya uliyofanyiwa kwa sababu tu umeonewa na kukandamizwa. Wale wanaomwamini Mungu ilhali hawamjui Mungu, lakini wanaofanya matendo mazuri—kwani wao nao hawaadibiwi pia? Unamwamini Mungu tu, unataka Mungu akushughulikie na Akulipizie kisasi tu kwa mabaya uliofanyiwa wewe, na unataka Mungu kukupa njia ya kimbilio kutoka kwa umaskini wako. Lakini unakataa kutilia maanani ukweli; wala hutamani kuishi kwa kudhihirisha ukweli. Hata zaidi, huwezi kuyakimbia maisha haya magumu na yasiyo na maana. Badala yake, huku ukiishi maisha yako katika mwili na maisha yako ya dhambi, unamwangalia Mungu kwa matarajio ya kusahihisha manung’uniko yako na kuondoa ukungu wa kuwepo kwako. Haya yanawezekanaje? Ukimiliki ukweli, unaweza kumfuata Mungu. Kama unaishi kwa kudhihirisha, unaweza kuwa onyesho la neno la Mungu. Kama unao uzima, unaweza kufurahia baraka ya Mungu. Ni wale tu walio na ukweli wanaweza kufurahia baraka ya Mungu. Mungu huhakikisha kwamba anawafidia wale wote wanaompenda kwa moyo wao wote pamoja na pia wanaovumilia magumu na mateso, na wala si kwa wale wanaojipenda tu na wamejipata kwenye mtego wa uwongo wa Shetani. Kunawezaje kuwa na wema miongoni mwa wale wasiopenda ukweli? Kunawezaje kuwa na haki miongoni mwa wale wanaopenda mwili tu? Si kweli kwamba haki na wema vyote vinarejelea ukweli? Si kweli kwamba vyote hivi vimehifadhiwa wale wanaompenda Mungu kwa moyo wao wote? Wale wasiopenda ukweli na ambao ni maiti zinazooza—je, watu hawa wote huwa hawajaficha maovu? Wale wasioweza kuishi ukweli—hawa wote si adui wa ukweli? Na je ninyi?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Waliokamilishwa Pekee Ndio Wanaoweza Kuishi Maisha Yenye Maana

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 348)

Kumsimamia mwanadamu ndio Kazi Yangu, na ushindi Wangu dhidi yake ni kitu ambacho kilikuwa hata zaidi kimeshaamuliwa kabla Nilipoiumba dunia. Watu huenda hawajui kwamba Nitashinda kabisa katika siku za mwisho na pia huenda hawajui kwamba ushahidi Wangu kumshinda Shetani ni kuwashinda wale walio waasi miongoni mwa binadamu. Lakini, adui Yangu alipoungana katika vita na Mimi, Nilikuwa Nimeshamwambia kwamba Nitakuwa mshindi wa wale waliokuwa wamechukuliwa na Shetani na kufanywa watoto wake na watumishi wake waaminifu wanaoangalia nyumba yake. Maana ya asili ya kushinda ni kuangamiza, kufedhehesha. Katika lugha Waisraeli walivyoeleza, ni kushinda kabisa, kuharibu, na kumfanya mwanadamu kutoweza kunipinga zaidi. Lakini leo kama linavyotumika kati yenu binadamu, maana yake ni kushinda. Mnapaswa kujua kwamba dhamira Yangu ni kuzima kabisa na kuangamiza yule mwovu kati ya binadamu, ili asiweze tena kuasi dhidi Yangu, sembuse kuwa na pumzi ya kupinga au kuleta fujo kwa Kazi Yangu. Hivyo, kulingana na wanadamu, imekuja kumaanisha kushinda. Haijalishi kidokezo cha neno hili, kazi Yangu ni kumshinda mwanadamu. Kwani, wakati ni ukweli kwamba mwanadamu ni kijalizo cha usimamizi Wangu, kwa usahihi zaidi, mwanadamu si kitu kingine ila ni adui Yangu. Mwanadamu ni yule mwovu anayenipinga na kuniasi. Mwanadamu si mwingine ila kizazi cha yule mwovu aliyelaaniwa na Mimi. Mwanadamu si mwingine ila ukoo wa malaika mkuu ambaye alinisaliti Mimi. Mwanadamu si mwingine ila mrithi wa shetani ambaye, akiwa amekataliwa kwa dharau na Mimi kitambo, amekuwa adui Wangu asiyeweza kupatanishwa tangu wakati huo. Anga iliyo juu ya jamii ya binadamu ni nzito sana, ni yenye giza na huzuni, bila hata dalili ya uwazi, na ulimwengu wa mwanadamu uko katika giza totoro, kiasi kwamba anayeishi ndani yake hawezi hata kuona mkono wake mwenyewe wakati anapounyosha mbele yake au jua anapoinua kichwa chake. Barabara chini ya miguu yake, ni matope na imejaa mashimo makubwa, ni mipindopindo na ya minyongo; nchi yote imejaa maiti. Pembe za giza zimejaa mabaki ya wafu. Na katika pembe zenye baridi na giza magenge ya mapepo yameshika makazi. Na kila mahali katika dunia ya binadamu, mapepo yanakuja na kwenda katika magenge. Kizazi cha wanyama wa aina yote, waliojawa na uchafu, wanapigana mkono kwa mkono katika mapambano ya kikatili, sauti ambayo huleta hofu moyoni. Nyakati kama hizo, katika dunia kama hiyo, “paradiso ya kidunia” ya aina hii, ni wapi ambako mwanadamu huenda kutafuta bahati ya maisha? Ni wapi ambako mtu ataenda kupata hatima ya maisha yake? Mwanadamu, akiwa amekanyagwa chini ya miguu ya Shetani kwa muda mrefu, amekuwa tangu mwazo mwigizaji akitenda kwa mfano wa Shetani—hata zaidi, kuwa na mwili wake, wakitumika kama shahidi wa kushuhudia kwa Shetani, kwa uwazi. Aina hii ya jamii ya binadamu, aina hii ya watu wachafu walioharibika tabia, na watoto wa aina hii wa familia hii ya binadamu potovu, inawezaje kuwa na ushuhuda kwa Mungu? Utukufu Wangu unatoka wapi? Mtu anaweza kuanza wapi kuongea juu ya shahidi Wangu? Kwa adui ambaye, baada ya kupotosha mwanadamu, anasimama dhidi Yangu, tayari amemchukua mwanadamu—mwanadamu ambaye niliumba kitambo sana na ambaye alikuwa amejawa na utukufu Wangu kuishi kulingana na Mimi—na kumchafua. Amepokonya utukufu Wangu, na yote ambayo imetia moyoni mwa mwanadamu ni sumu iliyojawa na ubaya wa Shetani, na maji ya matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Hapo mwanzo, Nilimuumba mwanadamu, yaani, Nilimuumba babu wa binadamu, Adamu. Alijaliwa na umbo na sura, mwenye kujawa na uhai, kujawa na nguvu ya maisha, na isitoshe, pamoja na utukufu Wangu. Hiyo ilikuwa ni siku tukufu Nilipomuumba mwanadamu. Baada ya hapo, Hawa alitengenezwa kutoka katika mwili wa Adamu, naye alikuwa pia babu wa binadamu, na hivyo watu niliowaumba walikuwa wamejazwa na pumzi Yangu na kujazwa na utukufu Wangu. Adamu kiasili aliumbwa kutoka kwa mkono Wangu na alikuwa akiwasilisha mfano Wangu. Hivyo maana ya asili ya “Adamu” ilikuwa kiumbe kilichoumbwa na Mimi, kilichojawa na nishati Yangu ya uhai, kilichojawa utukufu Wangu, kinacho sura na umbo, kinacho roho na pumzi. Alikuwa kiumbe wa pekee, aliyemilikiwa na roho, ambaye aliweza kuniwakilisha Mimi, kuwa na picha Yangu, na kupokea pumzi Yangu. Hapo mwanzo Hawa alikuwa mtu wa pili kujazwa na pumzi ambaye uumbaji wake nilikuwa nimeamuru, hivyo maana asili ya “Hawa” ilikuwa kiumbe ambaye angeendeleza utukufu Wangu, aliyejazwa na nguvu Zangu na zaidi ya hayo aliyejawa na utukufu Wangu. Hawa aliumbwa kutoka kwa Adamu, kwa hivyo alikuwa pia mfano Wangu, kwa maana yeye alikuwa mtu wa pili kuumbwa kwa mfano Wangu. Maana ya asili ya “Hawa” ilikuwa kiumbe hai, mwenye roho, mwili na mifupa, ushuhuda Wangu wa pili na pia mfano Wangu wa pili miongoni mwa mwanadamu. Walikuwa mababu wa wanadamu, hazina safi na ya thamani ya binadamu, na, kutoka awali, viumbe hai waliojaliwa na roho. Hata hivyo yule mwovu alikichukua kizazi cha mababu wa wanadamu na kukikanyaga na kukiteka nyara, kutosa ulimwengu wa binadamu katika giza totoro, na kuifanya kwamba kizazi chenyewe hakiamini tena katika uwepo Wangu. Kilicho cha chukizo zaidi ni kwamba, hata yule mwovu anapowapotosha watu na kuwakanyagia chini, anapokonya kwa ukatili utukufu Wangu, ushuhuda Wangu, nguvu Yangu Niliyowatolea watu, pumzi na maisha Niliyopuliza ndani yao, utukufu Wangu wote katika dunia ya binadamu, na damu yote ya roho ambayo nimetumia kwa mwanadamu. Mwanadamu hayupo tena katika mwanga, na amepoteza kila kitu Nilichompa, akiutupilia mbali utukufu ambao nimeutoa. Wanawezaje kukiri kwamba Mimi ndiye Bwana wa viumbe vyote? Wanawezaje kuendelea kuamini kuwepo Kwangu mbinguni? Wanawezaje kugundua udhihirisho wa utukufu Wangu duniani? Hawa wajukuu wa kiume na kike wanaweza kumchukua vipi Mungu ambaye mababu zao walimcha kama Bwana Aliyewaumba? Hawa wajukuu wenye kuhurumiwa “wamewasilisha” kwa ukarimu kwa yule mwovu utukufu, mfano, na vile vile ushahidi ambao Nilikuwa nimewatolea Adamu na Hawa, na pia maisha Niliyompa binadamu na ambayo ategemea ili kuwepo, na, bila kujali hata kidogo uwepo wa yule mwovu, amempa utukufu Wangu wote. Je, si hiki ni chanzo cha jina la “uchafu”? Jinsi gani aina hii ya mwanadamu, mapepo mabaya, aina hii ya maiti inayotembea, aina hii ya umbo la Shetani, na aina hii ya maadui Wangu zinaweza kumilikiwa na utukufu Wangu? Nitaumiliki tena utukufu Wangu, niumiliki ushuhuda Wangu ambao huwa miongoni mwa wanadamu na vyote vilivyowahi kuwa mali Yangu na Nilivyokuwa Nimewapa wanadamu hapo zamani—nitamshinda mwanadamu kikamilifu. Hata hivyo, unapaswa kujua, wanadamu Nilioumba walikuwa watu watakatifu na wenye mfano Wangu na utukufu Wangu. Hawakuwa wa Shetani, wala hawakukabiliwa na kukanyagwa kwake, bali walikuwa tu udhihirisho Wangu, walikuwa huru kutokana na dalili hata kidogo ya sumu yake. Na hivyo, Niliwajulisha wanadamu wote kwamba Ninataka tu kile kilichoumbwa na mkono Wangu, wale watakatifu ambao nawapenda na wasio wa mwingine yeyote. Aidha, Mimi nitakuwa na furaha nao, na kuwaona kama utukufu Wangu. Hata hivyo, Ninachotaka sio mwanadamu aliyepotoshwa na Shetani, ambaye ni wa Shetani leo, ambaye si kiumbe Changu cha asili tena. Kwa sababu Ninanuia kuchukua tena utukufu Wangu katika dunia ya wanadamu, Nitashinda kikamilifu manusura waliobaki kwa wanadamu, kama ushahidi wa utukufu Wangu katika kumshinda Shetani. Mimi huchukua tu ushahidi Wangu kama udhihirisho wa nafsi Yangu, kama kusudi la starehe Yangu. Haya ndiyo mapenzi Yangu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maana ya Kuwa Mtu Halisi

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 349)

Mwanadamu ameendelea kwa makumi ya maelfu ya miaka ya historia mpaka kufikia alipo leo. Hata hivyo, mwanadamu wa uumbaji Wangu wa asili kwa muda mrefu uliopita amezama katika upotovu. Tayari amecha kuwa kile Ninachotaka, kwa hivyo wanadamu, Ninavyowaona, hawastahili tena jina la uanadamu. Badala yake wao ni uchafu wa wanadamu, ambao Shetani amewateka nyara, maiti zilizooza zinazotembea ambamo Shetani huishi na huvalia. Watu hawaamini hata kidogo kuwepo Kwangu, wala hawakaribishi kuja Kwangu. Mwanadamu kwa shingo upande tu huyajibu maombi Yangu, na kwa muda anakubaliana nayo, na hashiriki kwa kweli katika furaha na huzuni za maisha pamoja na Mimi. Kwa vile wanadamu huniona Mimi kama Asiyeeleweka, bila ya kutaka wao hujifanya wanatabasamu Kwangu, kuleta namna ya kujidekeza kwa yule aliye na madaraka. Hii ni kwa sababu watu hawana ufahamu wa kazi Yangu, sembuse mapenzi Yangu kwa wakati wa sasa. Nitakuwa wazi na nyinyi nyote: Siku itakapofika, mateso ya mwanadamu yeyote ambaye huniabudu yatakuwa rahisi kubeba kuliko yenu. Kiwango cha imani yenu Kwangu hakiwezi, kwa hakika, kuzidi kile cha Ayubu—hata imani ya Mafarisayo Wayahudi inaishinda yenu—na hivyo, siku ya moto ikifika, kuteseka kwenu kutakuwa kali zaidi kuliko kule kwa Mafarisayo walipokemewa na Yesu, kuliko kule kwa wale viongozi 250 waliompinga Musa, na kuliko kule kwa Sodoma chini ya moto mkali wa uharibifu wake. Musa alipougonga mwamba, na maji yaliyokuwa yametolewa na Yehova yakaruka, ilikuwa ni kwa sababu ya imani yake. Daudi alipocheza kinubi kwa kunisifu Mimi, Yehova—moyo wake ukiwa umejaa furaha—ilikuwa ni kwa sababu ya imani yake. Ayubu alipowapoteza wanyama wake waliojaa kote milimani na mali nyingi sana, na mwili wake kujawa na majipu mabaya, ilikuwa ni kwa sababu ya imani yake. Alipoweza kusikia sauti Yangu, Yehova, na kuuona utukufu Wangu, Yehova, ilikuwa ni kwa sababu ya imani yake. Kwamba Petro aliweza kumfuata Yesu Kristo, ilikuwa ni kwa imani yake. Kwamba Alitundikwa misumari msalabani kwa ajili Yangu na kutoa ushahidi mtukufu, pia ilikuwa kwa imani yake. Yohana alipoona mfano wa utukufu wa Mwana wa Adamu, ilikuwa kwa imani yake. Alipoona maono ya siku za mwisho, yote yalikuwa zaidi kwa sababu ya imani yake. Sababu ya yanayodaiwa kuwa mataifa mengi yasiyo ya Kiyahudi kupata ufunuo Wangu, na yakajua kwamba Nimerudi katika mwili kufanya kazi Yangu miongoni mwa wanadamu, pia ni kwa sababu ya imani yao. Je si wote ambao wamepigwa na maneno Yangu makali na bado wanafarijiwa nayo na wameokoka—wamefanya hivyo kwa sababu ya imani yao? Wale wanaoamini Kwangu lakini bado hupitia mateso, je si pia wamekataliwa na dunia? Wale wanaoishi nje ya neno Langu, wakikimbia mateso ya majaribu, si wao wote wanazurura tu ulimwengu? Wao ni sawa na majani ya msimu wa kupukutika kwa majani yanayopeperuka hapa na pale, bila pahali pa kupumzika, sembuse neno Langu la kufutia machozi. Ingawa adabu na usafishaji wangu hauwafuati wao, je, wao si waombaji, wanaoelea kila mahali, ambao wakitangatanga katika mitaa iliyo nje ya Ufalme wa mbinguni? Je, dunia ni mahali pako pa mapumziko kweli? Je, unaweza kweli kupata tabasamu hata dhaifu ya kutosheleza kutoka kwa dunia kwa kuepuka adabu yangu? Je, unaweza kweli kutumia starehe zako za kidunia kuficha utupu ulio katika moyo wako usioweza kufichika? Unaweza kumdanganya mtu yeyote katika familia yako, ilhali huwezi kunidanganya Mimi kamwe. Kwa kuwa imani yako ni ndogo sana, mpaka wa leo huna uwezo wa kupata raha inayoletwa na maisha. Nakushauri: heri kutumia nusu ya maisha yako kwa ajili Yangu kwa dhati kuliko kuishi maisha yako yote katika hali hafifu na kujishughulisha kwa ajili ya mwili, kuvumilia mateso yote ambayo ni vigumu binadamu kuvumilia. Kuna faida gani ya wewe kujipenda sana na kuikimbia adabu Yangu? Kuna faida gani wewe kujificha kutoka kwa adabu Yangu ya muda mfupi tu, na mwishowe kupate aibu ya milele, na adabu ya milele? Mimi, kwa hakika, Simlazimishi yeyote kufanya mapenzi Yangu. Iwapo mtu kweli anayo nia ya kujiwasilisha kwa mipango Yangu yote, Sitamtendea vibaya. Lakini Nahitaji kwamba watu wote waamini ndani Yangu, kama vile Ayubu alivyoamini ndani Yangu, Yehova. Iwapo imani yenu inazidi ile ya Tomaso, basi imani yenu itapata pongezi Zangu, katika uaminifu wenu mtapata furaha Yangu, na hakika mtapata utukufu Wangu katika siku zenu. Hata hivyo, watu, wanaoamini katika dunia na wanaomwamini ibilisi, wamefanya mioyo yao kuwa migumu, kama vile halaiki za mji wa Sodoma, na chembe za mchanga zilizovumwa na upepo katika macho yao na sadaka kutoka kwa ibilisi zikiwa zimeshikiliwa vinywani mwao, akili zao zilizodanganywa tangu kitambo zimemilikiwa na yule mwovu ambaye ameipora dunia. Mawazo yao nusura yameporwa na ibilisi wa nyakati za kale. Na hivyo, imani ya mwanadamu imekwenda na upepo, na hawezi hata kuitambua Kazi Yangu. Anachoweza tu kufanya ni kujaribu nkwa unyonge kuvumilia au kuchambua kwa kukisia sana, kwa sababu kwa muda mrefu tayari amejawa na sumu ya Shetani.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maana ya Kuwa Mtu Halisi

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 350)

Mimi Nitawashinda wanadamu kwa sababu wanadanu waliumbwa na Mimi wakati mmoja na pia, kilicho cha ziada, wamefurahia vitu vyote karimu vya uumbaji Wangu. Lakini wanadamu pia wamenikataa Mimi, na nyoyo zao haziko na Mimi ndani yao, na wao huniona kama mzigo kwa uwepo wao, hadi kwa kiwango ambacho, wakiwa kwa kweli wameniona, watu bado wananikataa, na kukuna vichwa wakiwaza kila njia inayoweza kuwawezesha kunishinda Mimi. Watu huwa hawaniruhusu Mimi kuwachukulia kwa umakini au kuweka madai kali juu yao, wala hawanikubali huhukumu au kuadibu udhalimu wao. mbali na kuona hili kuwa jambo la kuvutia, wanakasirika. Na hivyo Kazi Yangu ni kuchukua mwanadamu ambaye hula, hunywa na kusherehekea Kwangu lakini hanijui na kumshinda. Nitawapokonya zana wanadamu, na kisha, Nikiwachukua malaika Wangu, Nikiuchukua utukufu Wangu Nitarejea kwenye makao Yangu. Kwa kuwa kile ambacho watu wamefanya kimenivunja moyo kabisa na kuitawanya kazi Yangu kwa vipande muda mrefu uliopita. Nanuia kuumiliki tena utukufu ambao yule mwovu ameiba kabla ya kuondoka kwa furaha, na kuwaacha wanadamu waendelee kuishi maisha yao, waendelee na “kuishi na kufanya kazi kwa amani na furaha,” na Mimi sitaingilia kati tena katika maisha yao. Lakini Mimi sasa Nanuia kikamilifu kuumiliki tena utukufu Wangu kutoka kwa mkono wa yule mwovu, kuurejesha ukamilifu wa utukufu Niliouumba ndani ya mwanadamu wakati wa kuumbwa kwa dunia, na kamwe tena kutotolea mwanadamu wa dunia. Kwa kuwa wanadamu hawajashindwa tu kuuhifadhi utukufu Wangu, bali pia wao wameugeuza kuwa mfano wa Shetani. Watu hawathamini kuja Kwangu, wala hawaiwekei thamani siku ya utukufu Wangu. Wao hawasherehekei kupokea adabu Yangu, sembuse kuwa tayari kuurejesha utukufu Wangu Kwangu. Wala hawako tayari kutupa mbali sumu ya yule mwovu. Wanadamu bado siku zote wananidanganya kwa njia ile ile ya zamani, bado wakivaa tabasamu za kung’aa na nyuso zenye furaha kwa njia ile ile ya zamani. Wao hawajui kina cha huzuni ambayo wanadamu watakabiliwa nao baada ya utukufu Wangu kuwaondoka, na hasa hawajui kwamba siku Yangu itakapokuja kwa wanadamu wote, watakuwa na wakati hata mgumu zaidi kuliko watu katika nyakati za Nuhu. Kwa maana wao hawajui giza iliyokuwepo Israeli wakati utukufu Wangu ulitoweka kwa kuwa mwanadamu husahau kunapokucha jinsi ilivyokuwa vigumu kupita katika giza la usiku wa manane. Jua linaporejea mafichoni tena na giza kumshukia mwanadamu, ataanza tena kuomboleza na kusaga meno yake gizani. Je, mmesahau, wakati utukufu Wangu ulipotoweka kutoka Israeli, ilivyokuwa vigumu kwa watu wake kuishi siku zao za mateso? Huu ndio wakati ambapo mnaona utukufu Wangu, na pia ndio wakati ambapo mnashiriki siku ya utukufu Wangu. Mwanadamu ataomboleza katikati ya giza wakati utukufu Wangu unapoondoka kutoka katika nchi chafu. Sasa ndio siku ya utukufu Ninapofanya kazi Yangu, na pia ndio siku ambapo Namwondoa mwanadamu kutoka kwa mateso, kwa kuwa sitapitia nyakati za uchungu na ugumu nao. Mimi Nataka tu ushindi kamili juu ya wanadamu na kumshinda kikamilifu yule mwovu wa wanadamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maana ya Kuwa Mtu Halisi

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 351)

Nimewatafuta wengi duniani wawe wafuasi Wangu. Kati ya hawa wafuasi wote, kuna wale wanaohudumu kama makuhani, wale wanaoongoza, wanaojumuisha wana, wanaojumuisha watu, na wale wanaotoa huduma. Nawagawa katika makundi haya tofauti kwa msingi wa uaminifu wanaonionyesha. Wakati wanadamu wote wameainishwa kulingana na aina zao, yaani, asili ya kila aina ya mwanadamu inapowekwa wazi, basi Nitamhesabu kila mwanadamu miongoni mwa aina yake kamili na kuweka kila aina katika nafasi yake kamili ili Nikamilishe lengo Langu la ukombozi wa mwanadamu. Moja baada ya mwingine, Nayaita makundi ya wale Ningependa kuwaokoa kurejea katika nyumba Yangu, kisha Nawaruhusu watu hawa wote wakubali kazi Yangu katika siku za mwisho. Wakati uo huo, Nawaainisha wanadamu kulingana na aina, kisha Namtunuku au kumwadhibu kila mmoja kulingana na matendo yake. Hizi ndizo hatua zinazojumuisha kazi Yangu.

Sasa Naishi duniani na Naishi miongoni mwa wanadamu. Wanadamu wote wanashuhudia kazi Yangu na kutazama matamko Yangu, na pamoja na hili Natoa ukweli kwa kila mfuasi Wangu ili waweze kupokea uzima kutoka Kwangu na hivyo apate njia anayoweza kufuata. Kwa maana Mimi ni Mungu, mpaji wa uhai. Katika miaka mingi ya kazi Yangu, mwanadamu amepokea vitu vingi na kujinyima vitu vingi, lakini bado Nasema kuwa mwanadamu haniamini kikamilifu. Kwa maana mwanadamu anakubali kijuujuu tu kuwa Mimi ni Mungu lakini hakubaliani na ukweli Ninaounena, sembuse kuuweka ukweli katika matendo Ninavyohitaji kwake. Hiyo ni kusema, mwanadamu anakubali tu uwepo wa Mungu, lakini sio ule wa ukweli; mwanadamu hukubali tu uwepo wa Mungu, lakini sio wa uzima; mwanadamu anakubali tu jina la Mungu, lakini sio kiini Chake. Kutokana na ari yake, mwanadamu amekuwa chukizo mbele Zangu. Kwa kuwa mwanadamu anatumia tu maneno yanayofurahisha masikio kunihadaa, na hakuna anayeniabudu kwa moyo wa kweli. Maneno yenu yanabeba majaribu ya ibilisi. Na maneno yenu ni yenye kiburi kupindukia, ni vile tu kama yamesemwa na malaika mkuu. Zaidi ya hayo, matendo yenu yamechakaa; tamaa zenu zisizo na kiasi na nia zenu zenye tamaa ni za kukera zikisikizwa. Nyote mmegeuka nondo katika nyumba Yangu, vyombo vya kukataliwa na chukizo. Kwa maana hapana kati yenu ambao ni wapenda ukweli, bali ni wanadamu wanaopenda baraka tu, walio na matamanio ya kupaa mbinguni, na ya kumwona Kristo anapoonyesha nguvu Zake duniani. Lakini mmewahi kuwaza jinsi mwanadamu kama ninyi, aliyepotoka sana, na asiyejua kabisa Mungu ni nini, angestahili kumfuata Mungu? Mnawezaje kupaa mbinguni? Mnawezaje kustahili kuuona uzuri wa ukuu usio na kifani? Vinywa vyenu vimejaa maneno ya uongo na uchafu, usaliti na kiburi. Kamwe hamjawahi kunena maneno ya ukweli Kwangu, wala maneno matakatifu, wala maneno ya kunitii baada ya kulipitia neno Langu. Hatimaye, hii imani yenu ni ya aina gani? Nyoyo zenu zimejaa tamaa na mali, mawazo yenu yamejaa mali ya kilimwengu. Kila siku, mnafanya hesabu jinsi mtakavyofaidika kutoka Kwangu, mkihesabu kiasi cha mali na vitu vya kidunia mlivyopata kutoka Kwangu. Kila siku, mnangoja baraka zaidi ziwashukie ili muweze kufurahia, hata zaidi na vyema zaidi, vitu zaidi vya raha. Vile vilivyo katika mawazo yenu kila wakati si Mimi, wala ukweli utokao Kwangu, bali ni mume (mke), mwanao, bintiyo au mlacho na kuvaa, na vile mtakavyoburudika na starehe nzuri zaidi. Hata mlishindilie tumbo lenu kwa vyakula hadi pomoni, je, si nyinyi bado ni zaidi ya maiti tu? Hata wakati ambapo, kwa nje, mnavalia mavazi ya kupendeza sana, si nyinyi bado ni maiti inayotembea isiyo na uhai? Mnafanya kazi kwa bidii kwa ajili ya tumbo lenu mpaka mnapotokwa na mvi, ilhali hakuna aliye tayari kuutoa unywele mmoja kwa ajili ya kazi Yangu. Mnasafiri kila mara, mnafanya kazi na kupiga bongo kwa ajili ya miili yenu, na kwa sababu ya watoto wenu, ilhali hakuna yeyote anayeshughulika wala kufikiria kuhusu mapenzi Yangu. Ni nini ambacho bado mnatarajia kufaidi kutoka Kwangu?

Katika kufanya kazi Yangu, kamwe Siharakishwi. Hata mwanadamu anifuate vipi, Mimi hufanya kazi Yangu kulingana na kila hatua, kulingana na mpango Wangu. Kwa hivyo, hata ingawa mnaweza kuasi dhidi Yangu sana, bado Sisimamishi kazi Yangu na Ninaendelea kunena maneno Ninayotaka kunena. Nawaita katika nyumba Yangu wale Niliowajaalia kulisikiliza neno Langu, kisha Nawaweka wote wanaotii na kulitarajia neno Langu mbele ya kiti Changu cha enzi. Wale wanaolisaliti neno Langu, wale wasiotii na kujisalimisha Kwangu, na wale wanaonipinga kwa wazi, watatupwa kando wakingoja adhabu ya mwisho. Wanadamu wote wanaishi katika upotovu na chini ya mkono wa yule mwovu, kwa hivyo sio wengi wanaonifuata wako na hamu ya ukweli kwa hakika. Hiyo ni kusema, wengi wao hawaniabudu kwa moyo wa kweli au kwa ukweli, lakini wanajaribu kupata uaminifu Wangu kupitia ufisadi, uasi na njia nyinginezo danganyifu. Ni kwa sababu hii ndiyo Nasema: Wengi wameitwa, lakini ni wachache wamechaguliwa. Wote walioitwa wametoka kupindukia na wanaishi katika enzi sawa, lakini wale waliochaguliwa ni lile kundi tu la wanaoamini na kuukubali ukweli na kuutia ukweli katika matendo. Wanadamu hawa ni sehemu ndogo tu ya wanadamu wote, na kutoka miongoni mwa wanadamu hawa Nitapata utukufu zaidi. Ukijipima kulingana na maneno haya, je, mnajua kama nyinyi mumo kati ya waliochaguliwa? Je, hatima yenu itakuwa namna gani?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wengi Wanaitwa, Lakini Wachache Wanachaguliwa

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 352)

Tayari Nimeshasema kuwa wale wanaonifuata ni wengi lakini wanaonipenda kwa moyo wa kweli ni wachache. Huenda ikawa wengine wanasema, “Ningeweza kulipa gharama kubwa kiasi hicho kama ningekuwa sikupendi Wewe? Ningefuata mpaka hatua hii kama singekuwa nakupenda?” Kwa hakika, unazo sababu nyingi, kwa hakika, upendo wako ni mkubwa sana, lakini umuhimu wa mapenzi yako Kwangu ni nini? “Upendo,” kama unavyoitwa, unaashiria hisia safi isiyo na dosari, ambapo unatumia moyo wako kupenda, kuhisi, na kuwa na mawazo. Katika upendo hakuna masharti, hakuna vizuizi na hakuna kutenga. Katika upendo hakuna shaka, hakuna uongo na hakuna ujanja. Katika upendo hakuna mabadilishano na hakuna kitu kisicho safi. Ukipenda, basi hutadanganya, hutalalamika, hutalalamika, hutaasi kulazimisha au kutafuta kupata kitu au kupata kiwango fulani. Ukipenda, basi utajinyima bila kusononeka na kuvumilia hali ngumu, na utaambatana na Mimi. Utaacha kila kitu chako kwa sababu Yangu, utaacha familia yako, siku zako za baadaye, ujana wako, na ndoa yako. La sivyo, basi upendo wako haungekuwa upendo hata kidogo, bali ungekuwa uongo na usaliti! Upendo wako ni upendo wa aina gani? Je, ni upendo wa kweli? Je, ni wa uongo? Umejinyima kiasi gani? Umejitolea kiasi gani? Je, Nimepata upendo kiasi gani kutoka kwako? Je, unajua? Mioyo yenu imejaa maovu, usaliti na uongo na hivyo kuna kiwango kipi cha uchafu katika upendo wenu? Mnafikiri kuwa mmeacha ya kutosha kwa ajili Yangu; mnafikiri kuwa upendo wenu Kwangu tayari umetosha. Ila ni kwa nini basi maneno yenu na matendo yenu huambatana na uasi na uongo daima? Mnanifuata, ilhali hamkubali neno Langu. Je, hili linachukuliwa kama upendo? Mnanifuata, kisha mnanitenga na kunitupa kando. Je, huu unachukuliwa kama upendo? Mnanifuata, na bado mko na shaka na Mimi. Je, huu unachukuliwa kama upendo? Mnanifuata, ilhali hamkubali kuwepo Kwangu. Je, huu ni upendo? Mnanifuata, ilhali hamnitendei vile Ninavyopaswa kutendewa na mnafanya mambo yawe magumu Kwangu katika kila hatua. Je, hili linachukuliwa kama upendo? Mnanifuata, na bado mnanichukua kama mjinga na kunidanganya Mimi katika kila jambo. Je, hili linachukuliwa kama upendo? Mnanihudumia, na bado hamnichi. Je, hili linachukuliwa kama upendo? Mnanipinga katika kila hali na kila jambo. Je, yote haya yanachukuliwa kama upendo? Mmejinyima mengi, huu ni ukweli, lakini bado hamjawahi kutenda Ninayowaagiza mfanye. Je, huu unaweza kuchukuliwa kama upendo? Uchunguzi wa makini unaashiria kuwa hamna upendo Kwangu ndani yenu. Baada ya miaka mingi sana ya kazi na maneno yote mengi Niliyosambaza, ni kiasi kipi mlichopokea kwa hakika? Je, hili halistahili kuangaliwa tena kwa makini? Nawaonya: Wale Niwaitao Kwangu sio wale ambao hawajawahi kupotoshwa, bali wale Ninaowachagua ni wale wanaonipenda kwa ukweli. Kwa hivyo, mnapaswa kuwa makini na maneno na matendo yenu, na mchunguze maazimio na mawazo yenu ili vitu hivi visije vikavuka mipaka. Wakati huu wa siku za mwisho, fanyeni jitihada ili muonyeshe mapenzi yenu Kwangu, isije ghadhabu yangu ikabaki kwenu milele!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wengi Wanaitwa, Lakini Wachache Wanachaguliwa

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 353)

Kila siku, fikira na matendo ya kila mmoja yanachunguzwa na Yeye na, katika wakati uo huo, wamo katika matayarisho ya siku zao zinazofuata. Hii ni njia ambayo lazima kila mtu aliye hai aipitie na ambayo Nimeamulia kabla kila mmoja. Hakuna anayeweza kuepuka hili na hakuna atakayepata upendeleo. Nimezungumza maneno yasiyohesabika na zaidi ya yote Nimefanya kazi kubwa mno. Kila siku, Ninatazama vile kila mwanadamu kiasili anafanya yote ambayo anafaa kufanya kulingana na asili yake na vile inavyoendelea. Bila kujua, wengi tayari wamo katika “njia sahihi”, ambayo Niliiweka kwa ufunuo wa mwanadamu wa kila aina. Tayari Nimemweka kila aina ya mwanadamu katika mazingira tofauti tofauti, na katika sehemu zao, kila mmoja amekuwa akionyesha tabia zake za asili. Hakuna mtu wa kuwafunga, hakuna mtu wa kuwatongoza. Wako huru katika nafsi yao yote na lile wanalolieleza linakuja kwa wepesi. Kuna kitu kimoja tu ambacho huwaweka katika nidhamu, na hayo ni maneno Yangu. Kwa hivyo watu wengine huyasoma maneno Yangu shingo upande, bila kuyatenda kamwe, wakifanya hivyo ili kuepuka kifo tu. Kwa upande mwingine, wanadamu wengine huona ugumu kuvumilia siku bila maneno Yangu kuwaelekeza na kuwapa, kwa hivyo wao hushikilia maneno Yangu kiasili wakati wote. Muda unavyopita, wao basi hugundua siri ya maisha ya mwanadamu, hatima ya mwanadamu na thamani ya kuwa na utu. Mwanadamu si zaidi ya haya katika uwepo wa maneno Yangu, na Mimi huruhusu tu mambo yachukue mkondo wake. Sifanyi chochote kinachomlazimisha mwanadamu kuishi kulingana na maneno Yangu kama msingi wa kuwepo kwake. Na kwa hivyo wale wasiokuwa na dhamiri au thamani katika kuwepo kwao hutazama kwa kimya mambo yanavyoenda kisha wanayatupa maneno Yangu kando kwa ujasiri na kufanya vile wanavyopenda. Wanaanza kuchoshwa na ukweli na mambo yote yatokayo Kwangu. Isitoshe, wao huchoka kukaa katika nyumba Yangu. Wanadamu hawa hukaa katika nyumba Yangu kwa ufupi tu kwa ajili ya hatima zao na kuepuka adhabu, hata kama wanafanya huduma. Lakini nia zao huwa hazibadiliki, wala matendo yao. Hii huendeleza zaidi hamu zao za Baraka, hamu za njia moja kwenda katika ufalme ambako wanaweza kubakia milele, na pia njia ya kuingia mbingu ya milele. Jinsi wanavyotamani zaidi siku Yangu ije hivi karibuni, ndivyo wanavyohisi zaidi kuwa ukweli umekuwa kizingiti, kizuizi njiani mwao. Wanangoja kwa hamu kuingia katika ufalme ili wafurahie daima baraka za ufalme wa mbinguni, bila kutaka kuufuata ukweli ama kukubali hukumu na kuadibu, na zaidi ya yote, bila kuhitaji kuishi kwa utumishi katika nyumba Yangu na kufanya vile Ninavyoamuru. Wanadamu hawa hawaingii katika nyumba Yangu kuukamilisha moyo unaotaka kujua ukweli wala kufanya kazi pamoja na uongozi Wangu. Lengo lao tu ni wawe miongoni mwa wale ambao hawataangamizwa katika enzi inayofuata. Kwa hivyo nyoyo zao hazijawahi kuujua ukweli wala kujua jinsi ya kuukubali ukweli. Hii ndiyo sababu wanadamu wa aina hii hawajawahi kutia vitendoni ukweli au kujua undani wa ufisadi wao, ilhali wameishi katika nyumba yangu kama “wajakazi” mpaka mwisho. Wanangoja “kwa uvumilivu” kuja kwa siku Yangu, na hawachoki wanaporushwa huku na kule na hali ya kazi Yangu. Haijalishi bidii zao ni kubwa namna gani au ni gharama gani wamelipa, hakuna atakayeona kuwa wameteseka kwa ajili ya ukweli ama kujitoa kwa ajili Yangu. Katika mioyo yao, wanangoja kwa hamu siku ambayo Nitakomesha enzi nzee, na zaidi ya hayo, wanangoja kwa hamu kujua jinsi nguvu na mamlaka Yangu ni kuu. Kile hawajawahi kimbilia kufanya ni kujibadilisha na kufuata ukweli. Wanapenda kile kinachonichosha na kuchoshwa na kile ninachopenda. Wanangoja kwa hamu kile Ninachokuwa na kinyongo nacho lakini wakati uo huo wanaogopa kupoteza kile Ninachochukia. Wanaishi katika dunia hii yenye maovu ila hawajawahi kuwa na chuki nayo na wana hofu sana kuwa Nitaiangamiza dunia hii. Nia walizo nazo zinakanganya: Wanapendezwa na dunia hii Ninayochukia, na kwa wakati uo huo wanangoja kwa hamu Niiharibu dunia hii hivi karibuni. Kwa njia hii, wataepuka mateso ya uharibifu na wabadilishwe kuwa watawala wa enzi mpya kabla hawajapotoshwa kutoka katika njia ya kweli. Hii ni kwa sababu hawapendi ukweli na wanahofia kila kitu kitokacho Kwangu. Huenda ikawa watakuwa “watu watiifu” kwa muda mfupi kwa minajili ya kutopoteza baraka, lakini fikira zao za kungoja baraka kwa hamu na woga wao wa kuangamia na kuingia katika ziwa la moto haziwezi kukingwa kuonekana. Siku Yangu inapokaribia, hamu zao zinazidi kuimarika. Na vile janga lilivyo kubwa, ndivyo wanavyopoteza tumaini wasijue watakapoanzia ili kunifanya Nifurahi na kuzuia wasipoteze baraka ambazo wamezingoja kwa muda mrefu. Pindi mkono Wangu unapoanza kazi yake, wanadamu hawa wana hamu kuchukua hatua kuhudumu kama watangulizi. Wanafikiri tu kusonga kwa nguvu mpaka mstari wa mbele wa majeshi, wakiwa na woga mwingi kuwa Sitawaona. Wanafanya na kusema kile wanachodhani ni ukweli, bila kujua kuwa vitendo na matendo yao hayajawahi na umuhimu kwa ukweli, na kuwa hutatiza na kuingilia tu mipango Yangu. Hata ingawa wanaweza kuwa wameweka juhudi nyingi na wanaweza kuwa wa kweli katika ridhaa na nia zao kustahimili ugumu, kila wanachokifanya hakihusiani na Mimi, kwa maana Sijaona hata mara moja kwamba matendo yao yametoka kwa nia njema, na zaidi ya hayo, Sijawaona kama wameweka kitu chochote kwenye madhabahu Yangu. Hayo ndiyo matendo yao mbele Yangu kwa miaka hii mingi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mnapaswa Kuzingatia Matendo Yenu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 354)

Mwanzoni, Nilitaka kuwapa ukweli zaidi, lakini kwa sababu mtazamo wenu kwa ukweli ni baridi sana na usiojali, Nimesalimu amri. Sipendi kuona jitihada Zangu zikipotea bure, na pia Sipendi kuwaona watu wakishika maneno Yangu na ilhali katika kila kipengele wakifanya yale ya Kunipinga Mimi, kunidhuru Mimi, na kunikufuru. Kwa sababu ya mtazamo wenu na utu wenu, Ninawapa sehemu kidogo tu ya maneno yaliyo muhimu zaidi kwenu kama jaribio Langu kwa wanadamu. Ni mpaka sasa ndiyo Naweza thibitisha kwa hakika kwamba uamuzi na mipango Niliyoweka ni kulingana na yale mnayohitaji na kuwa mtazamo Wangu kwa wanadamu uko sawa. Miaka yenu mingi ya matendo mbele Yangu imenipa jibu ambalo Sijawahi kupata hapo awali. Na swali la jibu hili ni: “Mtazamo wa mwanadamu mbele ya ukweli na Mungu wa ukweli ni upi?” Juhudi ambazo Nimemwagia mwanadamu ni dhihirisho la kiini Changu cha kumpenda mwandamu, na vitendo na matendo ya mwanadamu mbele Yangu pia yamedhihirisha kiini cha mwanadamu cha kuchukia ukweli na kunipinga Mimi. Katika wakati wote Mimi hujali wale wote ambao wamenifuata, lakini hakuna wakati ambao wale wanaonifuata wameweza kupokea neno Langu; hawana uwezo kabisa wa kukubali hata maoni yanayotoka Kwangu. Hili ndilo hunihuzunisha zaidi ya yote. Hakuna anayeweza kunielewa na, zaidi ya hayo, hakuna anayeweza kunikubali, hata ingawa mtazamo Wangu ni wa kweli na maneno Yangu ni ya upole. Wote wanafanya kazi Niliyowaaminia kuifanya kulingana na fikira zao; hawatafuti nia Zangu, wala kuuliza maombi Yangu. Bado wanadai kuwa Wananihudumia kwa uaminifu, wakati huu wote wakiwa wananiasi. Wengi wanaamini kuwa ukweli usiokubalika nao au ukweli ambao hawawezi kutia vitendoni sio ukweli. Kwa watu kama hawa, ukweli Wangu unakuwa kitu cha kukataliwa na kutupiliwa kando. Kwa wakati uo huo Ninakuwa mmoja anayetambuliwa na mwanadamu kwa neno tu kama Mungu, lakini pia kuchukuliwa kama mtu wa nje ambaye sio ukweli, njia na uhai. Hakuna anyejua ukweli huu: Maneno yangu ndio ukweli usiobadilika milele. Mimi Ndiye msambazaji wa binadamu na kiongozi wa pekee wa mwanadamu. Thamani na maana ya maneno Yangu haibainishwi na kama yanakubaliwa au kutambuliwa na mwanadamu, ila ni kwa kiini cha maneno yenyewe. Hata kama hakuna mtu hata mmoja duniani anaweza kupokea maneno Yangu, thamani ya maneno Yangu na usaidizi wake kwa mwanadamu hayapimiki na mwanadamu yeyote. Kwa hivyo, Ninapokumbwa na wanadamu wengi wanaoasi, kukataa au kudharau kabisa maneno Yangu, msimamo Wangu ni huu tu: Wacha wakati na ukweli uwe shahidi Wangu na uonyeshe kuwa maneno Yangu ndiyo ukweli, njia na uhai. Wacha vionyeshe kuwa yote Niliyosema ni ya ukweli, na kuwa ni yale ambayo mwanadamu lazima apewe, na, zaidi ya yote, yale ambayo mwanadamu anafaa akubali. Nitawaruhusu wote wanaonifuata wajue ukweli huu: Wote wasioyakubali maneno Yangu kikamilifu, wale wasioyaweka maneno Yangu katika vitendo, wale wasiopata sababu ndani ya maneno Yangu, na wale wasiopata wokovu kwa sababu ya maneno Yangu, ni wale ambao wamehukumiwa na maneno Yangu na, zaidi ya hayo, wamepoteza wokovu Wangu, na fimbo Yangu haitaondoka kamwe miongoni mwao.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mnapaswa Kuzingatia Matendo Yenu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 355)

Kutoka wakati mwanadamu kwanza alikuwa na sayansi ya jamii, akili yake ilishughulishwa na sayansi na maarifa. Kisha sayansi na maarifa vikawa vyombo vya kutawala mwanadamu, na hapakuwa tena na nafasi ya kutosha kumwabudu Mungu, na hapakuwa tena na mazingira mazuri ya kumwabudu Mungu. Nafasi ya Mungu ikashuka hata chini zaidi moyoni mwa mwanadamu. Dunia moyoni mwa mwanadamu bila nafasi ya Mungu ni giza, tupu bila matumaini. Na hivyo kukatokea wanasayansi wa jamii, wataalamu wa historia na wanasiasa wengi kueleza nadharia ya sayansi ya jamii, nadharia ya mageuko ya binadamu, na nadharia nyingine zinazopinga ukweli kwamba Mungu alimuumba mwanadamu, kujaza moyo na akili ya mwanadamu. Na kwa njia hii, wanaoamini kwamba Mungu aliumba kila kitu wanakuwa wachache zaidi, na wale wanaoamini nadharia ya mageuko wanakuwa hata wengi kwa nambari. Watu zaidi wanachukulia rekodi za kazi ya Mungu na maneno Yake wakati wa enzi ya Agano la Kale kuwa hadithi na hekaya. Kwa mioyo yao, watu wanakuwa wasiojali heshima na ukubwa wa Mungu, kwa imani kwamba Mungu yupo na anatawala kila kitu. Kusalia kwa mwanadamu na majaliwa ya nchi na mataifa si muhimu kwao tena. Mwanadamu anaishi katika dunia tupu akijishughulisha tu na kula, kunywa, na ufuatiliaji wa furaha. … Watu wachache wanashughulika kutafuta Afanyapo Mungu kazi Yake leo, ama kutafuta jinsi Anavyoongoza na kupanga majaliwa ya mwanadamu. Na kwa njia hii, ustaarabu wa ubinadamu bila fahamu ukawa huwezi kukutana na matakwa ya mwanadamu hata zaidi, na hata kuna watu zaidi wanaohisi kwamba, kuishi kwa dunia kama hii, wanayo furaha ya chini kuliko watu walioenda. Hata watu wa nchi zilizokuwa na ustaarabu wa juu wanaeleza malalamiko haya. Kwani bila mwongozo wa Mungu, bila kujali jinsi viongozi na wanasosiolojia wanatafakari kuhifadhi ustaarabu wa binadamu, haina mafanikio. Hakuna anayeweza kujaza utupu kwa moyo wa mwanadamu, kwani hakuna anayeweza kuwa uhai wa mwanadamu, na hakuna nadharia ya kijamii inayoweza kumwokoa kutokana na utupu unaomtesa. Sayansi, maarifa, uhuru, demokrasia, wasaa wa mapumziko, faraja, haya yote ni mapumziko ya muda, Hata na mambo haya, mwanadamu hataepuka kufanya dhambi na kuomboleza udhalimu wa jamii. Mambo haya hayawezi kupunguza tamaa ya mwanadamu na hamu ya kuchunguza. Kwa sababu mwanadamu aliumbwa na Mungu na kafara na uchunguzi usio na sababu wa mwanadamu vitamwongoza tu kwa dhiki zaidi. Mwanadamu daima atakuwa katika hali ya hofu isiyoisha, hatajua jinsi ya kuukabili mustakabali wa wanadamu, ama jinsi ya kuikabili njia iliyo mbele. Mwanadamu atakuja hata kuogopa sayansi na elimu, na kuhofia hata zaidi utupu ulio ndani yake sana. Duniani humu, bila kujali kama unaishi katika nchi huru ama isiyo na haki za binadamu, huwezi kabisa kuponyoka majaliwa ya mwanadamu. Kama wewe ni kiongozi ama anayeongozwa, huwezi kabisa kuponyoka hamu ya kuchunguza majaliwa, siri na majaliwa ya mwanadamu. Chini ya hayo, huna uwezo wa kutoroka hisia ya utupu inayotatiza. Matukio kama haya, yaliyo kawaida kwa wanadamu wote, yanaitwa matukio ya kijamii na wanasosiolojia, lakini hakuna mtu mkubwa anayeweza kuja mbele kutatua shida kama hizi. Mwanadamu, hata hivyo, ni mwanadamu. Nafasi na maisha ya Mungu hayawezi kubadilishwa na mwanadamu yeyote. Mwanadamu hahitaji tu jamii iliyo na haki, ambapo kila mtu analishwa vyema na ana uhuru na usawa, lakini wokovu wa Mungu na Yeye kuwapa uhai. Wakati tu mwanadamu atapokea wokovu wa Mungu na kupatiwa uhai na Yeye ndipo mahitaji, hamu ya kuchunguza, na utupu wa kiroho wa mwanadamu utaweza kutatuliwa. Iwapo watu wa nchi ama taifa hawawezi kupokea wokovu na utunzaji wa Mungu, basi nchi ama taifa kama hilo litatembelea njia inayoelekea uharibifuni, inayoelekea gizani, na litaangamizwa na Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 2: Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 356)

Kunayo siri kubwa moyoni mwako, ambayo hujawahi kuifahamu kamwe, kwa sababu umekuwa ukiishi katika ulimwengu bila mwanga. Moyo wako na roho yako vimepokonywa na yule mwovu. Macho yako yamezuiwa kwa giza yasione, na huwezi kuliona jua angani wala nyota ikimetameta wakati wa usiku. Masikio yako yamezibwa na maneno ya udanganyifu, na husikii sauti ya Yehova ingurumayo kama radi, wala sauti ya maji yakitiririka kutoka katika kiti cha enzi. Umepoteza kila kitu ambacho kilipaswa kuwa chako kwa haki, kila kitu ambacho Mwenye uweza alikupa. Umeingia katika bahari ya mateso isiyokuwa na mwisho, bila nguvu ya kukuokoa, bila matumaini ya kurudi ukiwa hai, na yote unayofanya ni kupambana na kusonga kila siku.… Tokea wakati huo, hungeweza kuepuka kuteswa na yule mwovu, uliwekwa mbali na baraka za mwenye Uweza, mbali na kukimu kwa mwenye Uweza, unatembea katika njia ambayo huwezi kurejea nyuma tena. Kuitwa mara milioni hakuwezi kusisimua moyo wako na roho yako. Unalala fofofo mikononi mwa yule mwovu, ambaye amekushawishi katika ulimwengu usio na mipaka, bila mwelekeo na bila alama za barabarani. Tokea hapo, umepoteza hali yako ya asili ya kutokuwa na hatia na utakatifu wako, na kuanza kujificha kutokana na utunzaji wa mwenye Uweza. Ndani ya moyo wako, yule mwovu anakuelekeza katika kila jambo na anakuwa uhai wako. Humwogopi tena, kumwepuka, au kumshuku; badala yake, unamchukulia kama Mungu aliye moyoni mwako. Unaanza kumtukuza na kumwabudu, na nyinyi wawili mnakuwa msiotengana kama mwili na kivuli chake, kila akitoa nafsi yake kwa mwingine katika uzima na mauti. Hujui lolote kabisa kuhusu mahali ulikotoka, kwa nini ulizaliwa, au kwa nini utakufa. Unamtazama Mwenye uweza kama mgeni; hujui mwanzo Wake, sembuse yale yote ambayo Amekutendea. Kila kitu kitokacho Kwake kimekuwa cha kuchukiza kwako. Huvitunzi wala kujua thamani yavyo. Unatembea kando na yule mwovu, kuanzia siku ile ulipoanza Mwenye uweza alianza kukukimu. Wewe na yule mwovu mmepitia maelfu ya miaka ya dhoruba na tufani pamoja, na pamoja naye, mnampinga Mungu ambaye alikuwa chanzo cha uhai wako. Hujui lolote kuhusu kutubu, sembuse kwamba umefikia ukingo wa kuangamia. Unasahau kwamba yule mwovu amekujaribu na kukutesa; umesahau asili yako. Kwa njia hii, yule mwovu amekuwa akikuharibu, hatua baada ya hatua, hata mpaka leo. Moyo wako na roho yako vimekufa ganzi na vimeoza. Umeacha kulalamika juu ya maudhi ya dunia ya wanadamu, na huamini tena kwamba dunia si ya haki. Bado hujali sana kama Mwenye uweza yupo. Hii ni kwa sababu ulimchukulia yule mwovu kuwa baba yako wa kweli kitambo, na huwezi tena kutengana naye. Hii ndiyo siri iliyo moyoni mwako.

Alfajiri inapofika, nyota ya asubuhi inaanza kuangaza mashariki. Hii ni nyota ambayo haijawahi kuwepo hapo awali. Inaliangaza anga lililo bado na nyota, ikikuwasha nuru iliyozimwa katika mioyo ya wanadamu. Binadamu si wapweke tena, kwa sababu ya mwanga huu, ambao hukuangazia wewe sawia na wengine. Lakini ni wewe tu unayebaki ukiwa umelala fofofo katika usiku wa giza. Huwezi kuisikia sauti, wala kuiona nuru, hujui kuhusu ujio wa mbingu mpya na nchi mpya, enzi mpya, kwa sababu baba yako hukwambia, “Mwanangu, usiamke, bado ni mapema. Hali ya anga ni baridi, kwa hivyo usiende nje, usije ukachomwa machoni kwa mkuki na upanga.” Unaamini maonyo ya baba yako pekee, maana unaamini kwamba baba yako tu ndiye yuko sahihi, kwa sababu baba yako ana umri mkubwa kuliko wewe na kwamba baba yako anakupenda sana. Maonyo kama hayo na upendo kama huo unakufanya uwache kuamini hekaya kwamba kuna nuru ulimwenguni, na uwache kujali kama ukweli bado upo ulimwenguni humu. Huthubutu tena kutumainia ukombozi kutoka kwa mwenye Uweza. Umeridhika kuwa katika hali hiyo, hutumainii tena ujio wa nuru, na hutazamii tena kuja kwa Mwenye uweza kama ilivyo katika hekaya. Inavyokuhusu wewe, yote yaliyo mazuri hayawezi kufufuliwa tena, wala hayawezi kuendelea kuwepo. Kesho ya wanadamu, siku za baadaye za wanadamu zinapotea, zinaharibika kabisa machoni pako. Unayashika sana mavazi ya baba yako kwa nguvu zako zote, ukifurahia kushiriki taabu zake, ukihofu sana kumpoteza mwenzako wa kusafiri na mwelekeo wa safari yako ya mbali. Ulimwengu huu mkubwa na wenye giza wa binadamu umewaunda wengi wenu, kuwa majasiri na watu wa kujitahidi sana katika kutekeleza majukumu mbalimbali ya ulimwengu huu. Umewaunda “mashujaa” wengi ambao hawaogopi kifo kabisa. Zaidi ya hayo, umetengeneza kundi baada ya kundi la watu waliokufa ganzi na wanadamu waliopooza ambao hawajui makusudi ya kuumbwa kwao. Macho ya Mwenye uweza hukagua kila mmoja wa jamii ya wanadamu walio katika mateso makali. Anachosikia ni vilio vya wale wanaoteseka, Anachoona ni kutokua kwa aibu kwa wale wanaoteseka, na Anachohisi ni kutojiweza na hofu ya jamii ya wanadamu ambayo imepoteza neema ya wokovu. Wanadamu wanakataa utunzaji Wake, wakichagua kutembea katika njia yao wenyewe, na wakijaribu kukwepa macho Yake yanayochunguza kwa karibu, wakiona ni afadhali waonje uchungu wa kilindi cha bahari hadi mwisho, pamoja na adui. Kutanafusi kwa Mwenye uweza hakusikiki tena na binadamu. Mikono ya Mwenye uweza haiko tayari kuwapapasa tena wanadamu hawa wenye huzuni. Anarudia kazi Yake, mara kwa mara akikamata tena, na mara kwa mara akipoteza tena, na kutoka wakati huo, Yeye anaanza kuchoka, kujihisi mchovu, na hivyo Anasitisha kazi inayofanyika, na kuwacha kutembea kati ya wanadamu…. Wanadamu hawana ufahamu kabisa kuhusu mabadiliko haya, hawajui kuhusu kuja na kuondoka, huzuni na ghamu ya Mwenye uweza.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kutanafusi kwa Mwenye Uweza

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 357)

Japo usimamizi wa Mungu waweza kuonekana mkubwa kwa mwanadamu, si jambo la kutofahamika kwa mwanadamu, kwa kuwa kazi yote ya Mungu imefungamanishwa na usimamizi wake, inahusiana na Kazi ya kuokoa mwanadamu, na inajishughulisha na maisha, kuishi, na hatima ya wanadamu. Kazi ambayo Mungu Anaifanya kati ya na kwa mwanadamu, yaweza kusemwa kuwa, ni ya utendaji na yenye maana kubwa. Inaweza kuonekana na mwanadamu, kuhusishwa na mwanadamu, na iko mbali na dhahania. Kama mwanadamu hana uwezo wa kukubali kazi zote Anazozifanya Mungu, basi ni upi umuhimu wa kazi hii? Na ni vipi usimamizi huu unaweza kusababisha kuokolewa kwa mwanadamu? Wengi wa watu wanaomfuata Mungu wanashughulika tu na jinsi watakavyopata baraka nyingi na kuepuka majanga. Panapotajwa kazi na usimamizi wa Mungu, wanakaa kimya na kupoteza matamanio yao yote. Wanaamini kuwa kujua maswali ya kuchosha kama hayo hakutakuza maisha yao au kuwa na faida yoyote, na kwa hivyo hata kama wamezisikia habari kuhusu usimamizi wa Mungu, wanazichukulia kikawaida. Na hawazichukulii kama kitu cha thamani kukipokea, na hata kukikubali kama sehemu ya maisha yao. Watu kama hao wana nia sahili sana katika kumfuata Mungu, na nia hiyo ni kupokea Baraka. Watu kama hao hawawezi kujishughulisha kuzingatia kitu chochote kingine ambacho hakihusiani na nia hii moja kwa moja. Kwao, kuamini kwa Mungu ili kupata baraka ndilo lengo halali na la thamani kwa imani yao. Hawaathiriwi na kitu chochote ambacho hakiwezi kutekeleza lengo hili. Hivyo ndivyo ilivyo na watu wengi wanaomfuata Mungu leo. Nia yao na motisha huonekana kuwa halali, kwa sababu wakati huo huo wa kumwamini Mungu, wanatumia rasilmali kwa ajili ya Mungu, wanajitolea kwa Mungu, na kutekeleza wajibu wao. Wanauacha ujana wao, wanajinyima kwa familia na kazi zao, na hata hukaa miaka mingi wakijishughulisha mbali na nyumbani kwao. Kwa ajili ya lengo lao kuu, wanabadili matamanio yao, wanabadili mtazamo wao wa nje wa maisha, hata kubadili njia wanayoitafuta, ila bado hawawezi kubadili nia ya imani yao kwa Mungu. Wanajishughulisha na usimamizi wa matamanio yao wenyewe; haijalishi njia iko mbali vipi, na ugumu na vikwazo vilivyo njiani, wanashikilia msimamo wao bila uoga hadi kifo. Ni nguvu zipi zinazowafanya wawe wa kujitolea kwa njia hii? Ni dhamiri yao? Ni sifa zao kubwa na nzuri? Ni kujitolea kwao kupigana na nguvu za maovu hadi mwisho? Ni imani yao wanayomshuhudia Mungu kwayo bila kutaka malipo? Ni utiifu wao ambao kwao wanajitolea kuacha kila kitu ili kutimiza mapenzi ya Mungu? Au ni roho yao ya kujitolea ambayo kwayo wanajinyima kila mara mahitaji badhirifu ya kibinafsi? Kwa watu ambao hawajawahi kujua kazi ya usimamizi wa Mungu kutoa zaidi, kwa hakika, ni muujiza wa ajabu! Hivi sasa, acha tusijadiliane kuhusu kiasi ambacho hawa watu wametoa. Tabia yao, hata hivyo, inastahili sana sisi kuichambua. Mbali na manufaa ambayo yanahusiana nao, je, kuna uwezekano wa kuweko kwa sababu nyingine ya wale hawajawahi kumfahamu Mungu kujitolea zaidi Kwake? Kwa hili, tunagundua tatizo ambalo halikutambuliwa hapo awali: Uhusiano wa mwanadamu na Mungu ni ule wa mahitaji ya kibinafsi yaliyo wazi. Ni uhusiano baina ya mpokeaji na mpaji wa baraka. Kwa kuiweka wazi, ni kama ule uhusiano baina ya mwajiriwa na mwajiri. Mwajiriwa hufanya kazi ili tu kupokea malipo yanayotolewa na mwajiri. Katika uhusiano kama huu, hakuna upendo, ila maafikiano tu, hakuna kupenda au kupendwa, ni fadhila na huruma tu; hakuna maelewano, ila hasira iliyofichwa na udanganyifu; hakuna mapenzi, ila ufa usioweza kuzibika. Mambo yanapofikia hapa, nani anaweza kubadilisha mwelekeo kama huu? Na ni watu wangapi ambao wanaweza kufahamu kwa kweli jinsi uhusiano huu ulivyokosa matumaini? Naamini kuwa watu wanapojitosa wenyewe kwenye raha ya kubarikiwa, hakuna anayeweza kukisia jinsi uhusiano na Mungu ulivyo wa aibu na usiopendeza.

Jambo la kusikitisha mno kuhusu imani ya wanadamu kwa Mungu ni kuwa wanadamu wanatekeleza usimamizi wao wenyewe katikati ya kazi ya Mungu na hawasikilizi usimamizi wa Mungu. Udhaifu mkubwa wa mwanadamu unaegemea katika jinsi, wakati huo huo anatafuta kujitoa kwa Mungu na kumwabudu, mwanadamu anaunda hatima yake kamilifu na kuhesabu jinsi ya kupokea baraka kubwa zaidi na hatima iliyo bora zaidi. Hata kama watu watafahamu jinsi walivyo wa kuhurumiwa, wenye chuki na walivyo ovyo, ni wangapi hapo ambao wanaweza kuachana na ukamilifu na matumaini yao? Na ni nani anayeweza kusimamisha hatua zake na kuacha kujifikiria yeye mwenyewe? Mungu Anawahitaji wale watakaojihusisha kwa karibu Naye kukamilisha usimamizi Wake. Anawahitaji wale ambao watatoa mawazo yao na mwili kwa ajili ya kazi Yake ya usimamizi ili kujitoa Kwake; Hawahitaji wale watakaoinua mikono yao na kuomba kutoka Kwake kila siku, na hata wale wanaotoa kidogo na kusubiri kulipwa kwa hilo tendo la kutoa. Mungu Anawadharau wale wanaotoa michango kidogo na kuridhika. Anawachukia wenye roho katili ambao hukataa kazi ya usimamizi Wake na hutaka tu kuongea kuhusu kwenda mbinguni na kupata baraka. Anachukia hata zaidi na wale ambao hufaidika na fursa inayowezeshwa na kazi Anayoifanya katika kuokoa wanadamu. Hii ni kwa sababu hawa watu hawajawahi kushughulishwa na Anachotarajia kupata Mungu kutokana na kazi Yake ya usimamizi. Wanashughulishwa tu na jinsi wanavyoweza kutumia hiyo fursa iliyowezeshwa na kazi ya Mungu ili kupata baraka. Hawajali roho Yake Mungu, kwa kuwa wanajishughulisha na mustakabali na hatima yao. Wale ambao wanakataa kazi ya usimamizi wa Mungu na hawana hata tamanio dogo katika jinsi Mungu Anavyowaokoa wanadamu na mapenzi Yake, wote wanafanya wapendavyo kando na kazi ya usimamizi wa Mungu. Tabia yao haikumbukwi na Mungu, na haikubaliwi na Mungu, na hata haiangaliwi kwa fadhila ya Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 3: Mwanadamu Anaweza tu Kuokolewa Katikati ya Usimamizi wa Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 358)

Kazi Yangu iko karibu kukamilika. Miaka mingi ambayo tumeshinda pamoja imekuwa kumbukumbu zisizovumilika za siku za nyuma. Nimeendelea kurudia maneno Yangu na Sijakoma kuendelea katika kazi Yangu mpya. Bila shaka, ushauri Wangu ni sehemu muhimu katika kila sehemu ya kazi Ninayoifanya. Bila ushauri Wangu, ninyi nyote mtapotea, na kuchanganyikiwa hata zaidi. Kazi Yangu sasa karibu inakamilika na kuisha; bado Nataka kufanya kazi fulani katika kutoa ushauri, hiyo ni, kutoa baadhi ya maneno ya ushauri ili muyasikilize. Natumai tu kwamba hamtapoteza juhudi Zangu zenye kujitahidi na zaidi ya hayo, kwamba mnaweza kuelewa utunzaji wote na fikira ambazo Nimetumia, mkiyachukulia maneno Yangu kama msingi wa jinsi mnavyotenda kama binadamu. Iwe ni maneno ambayo mko tayari kuyasikiliza au la, iwe ni maneno ambayo mnafurahia kuyakubali au mnayakubali bila raha, lazima muyachukulie kwa uzito. Vinginevyo, tabia na mielekeo yenu isiyokuwa ya kujali itanifadhaisha Mimi kweli na hata zaidi, kuniudhi. Natumai sana kwamba nyote mnaweza kuyasoma maneno Yangu tena na tena—mara elfu kadhaa—na hata kuyakariri. Ni kwa namna hiyo tu ndiyo hamtayaacha matarajio Yangu kwa ajili yenu. Hata hivyo, hakuna hata mmoja wenu anayeishi hivi sasa. Hata, nyote mmezama katika maisha fisadi ya kula na kunywa hadi kushiba, na hakuna yeyote kati yenu anayeyatumia maneno Yangu kuusitawisha moyo na nafsi yake. Kwa sababu hii ndiyo Nimehitimisha kuhusu uso wa kweli wa mwanadamu: Mwandamu anayeweza kunisaliti wakati wowote, na hakuna yeyote anayeweza kuwa mwaminifu kabisa kwa maneno Yangu.

“Mwanadamu amepotoshwa sana na Shetani kiasi kwamba hana sura ya mwanadamu tena.” Usemi huu sasa umepata utambuzi kidogo kutoka kwa idadi kubwa ya watu. Inasemwa hivyo kwa sababu “utambuzi” hapa ni kukiri juu juu tu kinyume na maarifa ya kweli. Kwa kuwa hakuna yeyote kati yenu anayeweza kujitathmini kwa usahihi wala kujichanganua kabisa, daima mnaamini nunu nusu, mnayashuku maneno Yangu nusu nusu. Lakini wakati huu Nautumia ukweli kuelezea tatizo kubwa zaidi mlio nalo, na hilo ni usaliti. Nyote mnao uzoefu wa neno “usaliti” kwa sababu watu wengi wamefanya kitu kuwasaliti wengine awali, kama vile mume kumsaliti mke wake, mke kumsaliti mume wake, mwana kumsaliti baba yake, binti kumsaliti mama yake, mtumwa kumsaliti bwana wake, marafiki kusalitiana, jamaa kusalitiana, wauzaji kuwasaliti wanunuzi, na mengineyo. Mifano hii yote ina asili ya usaliti. Kwa kifupi, usaliti ni aina ya tabia ambayo mtu huvunja ahadi, hukiuka kanuni za maadili, au huenda dhidi ya maadili ya kibinadamu, na ambayo huonyesha kupoteza ubinadamu. Kama mwanadamu, bila kujali kama unakumbuka iwapo umewahi kufanya kitu cha kumsaliti mwingine au ikiwa tayari umewasaliti wengine mara nyingi, kuzungumza kwa ujumla, kama ninyi mmezaliwa katika dunia hii basi mmefanya kitu kuusaliti ukweli. Kama una uwezo wa kuwasaliti wazazi au marafiki basi una uwezo wa kuwasaliti wengine, na zaidi ya hayo una uwezo wa kunisaliti Mimi na kufanya mambo ambayo Ninayadharau. Kwa maneno mengine, usaliti si aina ya utovu wa maadili tu kwa nje, lakini ni kitu ambacho hakikubaliani na ukweli. Aina hii ya kitu hasa ni chanzo cha upinzani wa mwanadamu na uasi kuhusiana na Mimi. Hii ndio sababu Nimeufupisha katika maelezo yafuatayo: Usaliti ni asili ya mwanadamu. Asili hii ni adui wa kimaumbile wa kila mtu kuwa sambamba na Mimi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tatizo Zito Sana: Usaliti (1)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 359)

Tabia ambayo haiwezi kunitii kabisa ni usaliti. Mwenendo ambao hauwezi kuwa mwaminifu Kwangu ni usaliti. Kunidanganya na kutumia uongo kunilaghai ni usaliti. Kujawa na dhana na kuzieneza kila mahali ni usaliti. Kutozilinda shuhuda na maslahi Yangu ni usaliti. Kubuni tabasamu wakati mtu ameniacha moyoni mwake ni usaliti. Tabia hizi ni mambo yote ambayo daima mna uwezo wa kuyafanya, na pia ni za kawaida kati yenu. Hakuna mmoja wenu anayeweza kufikiri kwamba hilo ni tatizo, lakini Mimi sifikirii hivyo. Siwezi kuchukulia kunisaliti kama jambo dogo, na zaidi ya hayo siwezi kulipuuza. Sasa, Nafanyapo kazi miongoni mwenu, mnakuwa wenye tabia ya aina hii—ijapo siku ile ambapo hakutakuwa na mtu wa kuwalinda, hamtakuwa kama wezi waliojitangaza kuwa wafalme? Wakati hili linafanyika na mnasababisha janga kubwa, nani atakuwa hapa kuvisafisha vitu tena na kuondoa uchafu? Mnaweza kufikiri kwamba baadhi ya vitendo vya usaliti ni kitu cha mara moja tu badala ya tabia ya kuendelea, na hakipaswi kutajwa kwa uzito hivi, kikiwasababisha kuadhirika. Kama kweli mnaamini hivyo, basi mnakosa wepesi wa kuhisi. Kadiri mtu anavyofikiri hivi, ndivyo anavyokuwa kielelezo na umboasili wa uasi. Asili ya mtu ni maisha yake, ni kanuni ambayo anaitegemea ili kuendelea kuishi, na anashindwa kuibadilisha. Jinsi ilivyo hali ya usaliti—kama unaweza kufanya kitu ili kumsaliti ndugu au rafiki, hii inathibitisha kwamba ni sehemu ya maisha yako na hali ambayo ulizaliwa nayo. Hiki ni kitu ambacho hakuna mtu anaweza kukikana. Kwa mfano, kama mtu anapenda kuiba vitu vya watu wengine, basi hii “kupenda kuiba” ni sehemu ya maisha yake. Ni kwamba tu wakati mwingine anaiba, na wakati mwingine haibi. Bila kujali kama anaiba au la, haiwezi kuthibitisha kwamba kuiba kwake ni aina ya tabia. Badala yake, inathibitisha kwamba kuiba kwake ni sehemu ya maisha yake, yaani, asili yake. Baadhi ya watu watauliza: Kwa kuwa ni asili yake, basi kwa nini wakati mwingine anaona vitu vizuri lakini haviibi? Jibu ni rahisi sana. Kuna sababu nyingi kwa nini haibi, kama vile kama bidhaa ni kubwa mno kwake kuinyakua akitazamwa na watu, au hakuna wakati mzuri wa kutenda, au bidhaa ni ghali sana, imelindwa vikali, au hana nia hasa ya kitu kizuri kama hicho, au bado hajafikiria matumizi ya kitu hicho, na mengineyo. Sababu hizi zote zinawezekana. Lakini haidhuru, akikiiba au la, hii haiwezi kuthibitisha kuwa hiyo dhana humjia akilini kwa muda tu. Kinyume chake, hii ni sehemu ya asili yake ambayo ni ngumu kuirudia tena. Mtu kama huyo haridhiki na kuiba mara moja tu, lakini mawazo ya kudai vitu vya wengine kama vyake huamshwa wakati wowote anapokutana na kitu kizuri au hali inayofaa. Hii ndiyo sababu Nasema kwamba wazo hili haliinuki kila mara, lakini linatokana na asili ya mtu huyu mwenyewe.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tatizo Zito Sana: Usaliti (1)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 360)

Mtu yeyote anaweza kutumia maneno na vitendo vyake wenyewe kuwakilisha tabia yake halisi. Sura hii ya kweli bila shaka ni asili yake. Kama wewe ni mtu anayeongea bila kuwa dhahiri, basi una asili mbovu. Kama asili yako ni yenye hila sana, basi namna ambayo unafanya mambo ni janja na laghai sana, nawe unafanya iwe rahisi sana kwa watu kulaghaiwa nawe. Kama asili yako ni mbovu sana, huenda maneno yako ni mazuri kusikiliza, lakini vitendo vyako haviwezi kuficha njia zako mbovu. Kama asili yako ni vivu sana, basi kila kitu unachosema vyote vinalenga kukwepa lawama na wajibu wa uzembe na uvivu wako, na vitendo vyako vitakuwa vya polepole sana na vizembe, na vizuri sana katika kuuficha ukweli. Kama asili yako ni yenye uwezo wa kuhisi maono ya wengine sana, basi maneno yako yatakuwa yenye busara na hatua zako pia zitalingana sana na ukweli. Kama asili yako ni aminifu sana, basi maneno yako lazima yawe ya dhati na namna ambayo unafanya mambo lazima iwe yenye kuhusika na mambo halisi, bila mengi ya kufanya bwana wako asikuamini. Kama asili yako ni yenye tamaa sana au ni yenye tamaa ya fedha, basi moyo wako mara nyingi utajazwa na mambo haya na utafanya baadhi ya mambo yaliyopotoka bila kukusudia, mambo maovu ambayo hufanya iwe vigumu kwa watu kusahau na zaidi ya hayo yatawaudhi. Kama Nilivyosema, kama una asili ya usaliti basi ni kujinasua kutoka kwake kwa nadra sana. Msiamini kuwa hivyo ndivyo ilivyo kwamba hamna asili ya usaliti kwa sababu hamjamkosea mtu yeyote. Kama hivyo ndivyo unavyofikiri basi unachukiza sana. Maneno ambayo Nimenena kila wakati yamewalenga watu wote, sio tu mtu mmoja au aina ya mtu. Kwa sababu tu hujanisaliti Mimi kwa jambo moja haithibitishi kwamba huwezi kunisaliti katika jambo moja haiashirii kwamba huwezi kunisaliti Mimi katika jambo jingine. Kwa kutafuta ukweli, baadhi ya watu hupoteza imani yao katika kuutafuta ukweli wakati wa kipingamizi katika ndoa zao. Baadhi ya watu huwacha wajibu wao wa kuwa waaminifu Kwangu wakati wa kuvunjika kwa familia. Baadhi ya watu huniacha kwa ajili ya kutafuta wakati wa furaha na msisimko. Baadhi ya watu afadhali waanguke katika korongo lenye giza kuliko kuishi katika mwanga na kupata furaha ya kazi ya Roho Mtakatifu. Baadhi ya watu hupuuza ushauri wa marafiki kwa ajili ya kuridhisha tamaa zao kwa ajili ya mali, na hata sasa hawawezi kuyakubali uovu wao na kugeuza mkondo. Baadhi ya watu wanaishi tu kwa muda chini ya jina Langu ili wapate ulinzi Wangu, wakati wengine hujitolea tu kidogo tu Kwangu kwa kulazimishwa kwa sababu wameyashikilia maisha na wanahofu kifo. Si vitendo hivi na vingine viovu na zaidi ya hayo visivyofaa tabia tu ambazo watu wamenisaliti kwa muda mrefu ndani ya mioyo yao? Bila shaka, Najua usaliti wa watu haukuwa umepangwa mapema, lakini ni ufunuo wa kimaumbile wa asili zao. Hakuna mtu anayetaka kunisaliti, na zaidi ya hayo hakuna mtu aliye na furaha kwa sababu amefanya kitu kunisaliti. Kinyume chake, wanatetemeka kwa hofu, sivyo? Hivyo mnafikiri kuhusu jinsi mnavyoweza kuzikomboa saliti hizi, na jinsi mnavyoweza kubadili hali ya sasa?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tatizo Zito Sana: Usaliti (1)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 361)

Asili ya mwanadamu ni tofauti kabisa na kiini Changu, kwa sababu asili potovu ya mwanadamu hutoka kwa Shetani kabisa; asili ya mwanadamu imetengenezwa na kupotoshwa na Shetani. Yaani, mwanadamu anaishi chini ya ushawishi wa uovu na ubaya wake. Mwanadamu hakui katika ulimwengu wa ukweli au mazingira matakatifu, sembuse mwanadamu kuishi katika nuru. Kwa hiyo, haiwezekani kwa mtu yeyote kuwa na ukweli ndani ya asili yake tangu wakati wa kuzaliwa, sembuse mtu kuweza kuzaliwa na kiini kinachomwogopa na kumtii Mungu. Badala yake, watu wana asili ambayo humpinga na kumwasi Mungu, na haipendi ukweli. Asili hii ndilo tatizo Ninalotaka kujadili—usaliti. Usaliti ndicho chanzo cha kila mtu kumpinga Mungu. Hili ni tatizo ambalo linapatikana ndani ya mwanadamu tu, na sio ndani Yangu. Wengine watauliza: Kwa kuwa watu wote wanaishi ulimwenguni jinsi tu Kristo aishivyo, mbona watu wote wana asili ambazo zinamsaliti Mungu, ilhali Kristo hana asili hiyo? Hili ni tatizo ambalo lazima muelezwe wazi.

Msingi wa uwepo wa wanadamu ni kuzaliwa upya kwa nafsi tena na tena. Kwa maneno mengine, kila mtu hupata maisha ya kibinadamu katika mwili nafsi yake inapozaliwa upya. Baada ya mwili wa mtu kuzaliwa, maisha yake huendelea hadi mwili unapofikia vikomo vyake hatimaye, ambao ndio wakati wa mwisho, wakati nafsi inapoliacha ganda lake. Utaratibu huu hujirudia tena na tena, nafsi ya mtu ikija na kwenda mara kwa mara, na kwa hiyo uwepo wa wanadamu unadumishwa. Maisha ya mwili pia ni maisha ya nafsi ya mwanadamu, na nafsi ya mwanadamu hukimu uwepo wa mwili wa mwanadamu. Hiyo ni kusema, maisha ya kila mtu hutoka kwenye nafsi yake, na maisha hayana asili katika mwili. Kwa hiyo, asili ya mwanadamu hutoka kwenye nafsi, si kutoka kwa mwili. Nafsi ya kila mtu tu ndiyo inayojua jinsi alivyopitia majaribu, mateso na upotovu wa Shetani. Mwili wa mwanadamu hauyajui mambo haya. Kwa hiyo, bila kujua, wanadamu huwa waovu zaidi, wachafu zaidi, na wabaya zaidi, wakati umbali kati ya mwanadamu na Mimi unazidi kuwa mkubwa, na maisha yanakuwa yenye giza zaidi kwa wanadamu. Shetani huzishika nafsi za wanadamu kwa nguvu, kwa hiyo, bila shaka, mwili wa mwanadamu pia umemilikiwa na Shetani. Mwili kama huo na wanadamu kama hao wangewezaje kutompinga Mungu? Wangewezaje kulingana naye kiasili? Sababu iliyofanya Nimtupe Shetani chini angani ni kwa sababu alinisaliti. Je, basi wanadamu wanawezaje kutohusishwa? Hii ndiyo sababu usaliti ni asili ya kibinadamu. Ninaamini kwamba mara mnapoielewa fikira hii, pia mnapaswa kukiamini kiini cha Kristo. Mwili uliovaliwa na Roho wa Mungu ni mwili wa Mungu mwenyewe. Roho wa Mungu ni mwenye mamlaka; Yeye ni mwenye uweza, mtakatifu, na mwenye haki. Vivyo hivyo, mwili Wake pia ni wenye mamlaka, wenye uweza, mtakatifu, na wenye haki. Mwili kama huo unaweza kufanya tu kile ambacho ni cha haki na chenye faida kwa wanadamu, kile ambacho ni kitakatifu, kitukufu na chenye nguvu; Yeye hawezi kutenda jambo lolote ambalo linakiuka ukweli, ambalo linakiuka maadili na haki, sembuse kufanya jambo lolote linaloweza kumsaliti Roho wa Mungu. Roho wa Mungu ni mtakatifu, na kwa hiyo mwili Wake hauwezi kupotoshwa na Shetani; mwili Wake ni wenye kiini tofauti na mwili wa mwanadamu. Kwa maana ni mwanadamu na si Mungu, ambaye anapotoshwa na Shetani; Shetani hawezi kamwe kuupotosha mwili wa Mungu. Kwa hiyo, licha ya ukweli kwamba mwanadamu na Kristo wanaishi katika sehemu sawa, ni mwanadamu tu ndiye anayemilikiwa, anayetumiwa, na anayenaswa na Shetani. Kinyume na hilo, Kristo hapenyeki kabisa na upotovu wa Shetani, kwa sababu Shetani hatawahi kuweza kupanda hadi mahali pa juu zaidi, na hatawahi kuweza kumkaribia Mungu. Leo, nyote mnapaswa kuelewa kuwa ni wanadamu tu, jinsi walivyopotoshwa na Shetani, ndio hunisaliti. Usaliti hautawahi kuwa suala linalomhusisha Kristo hata kidogo.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tatizo Zito Sana: Usaliti (2)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 362)

Nafsi zote zilizopotoshwa na Shetani zimeshikwa mateka katika miliki ya Shetani. Ni wale tu wanaomwamini Kristo ndio waliotengwa, waliookolewa kutoka katika kambi ya Shetani, na kuletwa ndani ya ufalme wa leo. Watu hawa hawaishi tena chini ya ushawishi wa Shetani. Hata hivyo, asili ya mwanadamu bado imekita mizizi katika mwili wa mwanadamu, yaani, ingawa nafsi zenu zimeokolewa, asili yenu bado ni kama ilivyokuwa awali, na uwezekano kwamba mtanisaliti unabaki kuwa asilimia mia moja. Hii ndiyo sababu kazi Yangu hudumu kwa muda mrefu sana, kwa kuwa asili yenu haiwezi kudhibitiwa kwa urahisi. Sasa, ninyi nyote mnapitia shida kadri ya uwezo wenu mnapotimiza wajibu wenu, ilhali kila mmoja wenu anaweza kunisaliti na kurudi katika miliki ya Shetani, kambini mwake, na kurudia maisha yenu ya zamani—huu ni ukweli usiopingika. Wakati huo, haitawezekana kwenu kudhihirisha chembe ya ubinadamu au mfano wa binadamu, kama mnavyofanya sasa. Katika hali mbaya zaidi, mtaangamizwa, na zaidi ya hayo, mtahukumiwa milele, mwadhibiwe vikali, msizaliwe upya kamwe. Hii ndiyo shida iliyowekwa mbele yenu. Ninawakumbusha kwa njia hii, kwanza, ili kazi Yangu isiwe imekuwa bure, na pili, ili ninyi nyote mweze kuishi katika siku za nuru. Kwa kweli, kama kazi Yangu ni bure si tatizo la muhimu sana. Kilicho cha muhimu sana ni kwamba mnaweza kuwa na maisha yenye furaha na mustakabali mzuri sana. Kazi Yangu ni kazi ya kuziokoa nafsi za watu. Nafsi yako ikianguka mikononi mwa Shetani, mwili wako hautaishi kwa amani. Ikiwa Ninaulinda mwili wako, hakika nafsi yako pia itakuwa chini ya uangalizi Wangu. Nikikuchukia sana, mwili na nafsi yako vitaanguka mikononi mwa Shetani mara moja. Je, unaweza kukisia hali yako wakati huo? Ikiwa, siku moja mtayapuuza maneno Yangu, basi Nitawakabidhi nyote kwa Shetani, ambaye atawatesa sana hadi hasira Yangu itakapoisha kabisa, au Mimi binafsi Nitawaadhibu ninyi wanadamu wasioweza kuokoleka, kwa kuwa mioyo yenu inayonisaliti haitakuwa imewahi kubadilika.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tatizo Zito Sana: Usaliti (2)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 363)

Nyote mnapaswa sasa kujichunguza haraka iwezekanavyo, ili muone ni kiasi gani cha kunisaliti kimebaki ndani yenu. Ninangojea jibu lenu kwa pupa. Msiwe wazembe katika kunishughulikia. Kamwe Mimi huwa sichezi michezo na watu. Nikisema Nitatenda jambo basi hakika Nitalitenda. Natumai kila mmoja wenu atakuwa mtu anayeyachukulia maneno Yangu kwa uzito, na asifikirie kana kwamba maneno hayo ni ubuni wa sayansi. Ninachotaka ni kitendo thabiti kutoka kwenu, siyo mawazo yenu. Baadaye, lazima mjibu maswali Yangu, ambayo ni kama ifuatavyo: 1. Ikiwa kwa kweli wewe ni mtendaji huduma, je, unaweza kutoa huduma Kwangu kwa uaminifu, bila dalili yoyote ya uzembe au mtazamo hasi? 2. Je, ukigundua kuwa Sijawahi kukuthamini, bado utaweza kusalia na kunitolea huduma ya maisha yote? 3. Ikiwa bado Ninakudharau sana licha ya wewe kutumia bidii nyingi, je, utaweza kuendelea kunifanyia kazi katika mashaka? 4. Ikiwa, baada ya wewe kufanya matumizi kwa ajili Yangu, Siyaridhishi mahitaji yako madogo, je, utavunjika moyo na kusikitishwa na Mimi, au hata ukasirike na kunitukana kwa sauti kubwa? 5. Ikiwa daima umekuwa mwaminifu sana, ukinipenda sana, ilhali unateseka na ugonjwa, umaskini, na kutengwa na marafiki na jamaa zako, au ikiwa unavumilia taabu nyingine zozote maishani, bado uaminifu na upendo wako Kwangu utaendelea? 6. Ikiwa hakuna lolote kati ya yale ambayo umefikiria moyoni mwako linalingana na kile ambacho Nimefanya, je, utaitembea njia yako ya baadaye kwa namna gani? 7. Ikiwa hupokei lolote kati ya mambo ambayo ulitarajia kupokea, je, unaweza kuendelea kuwa mfuasi Wangu? 8. Ikiwa hujawahi kuelewa kusudi na umuhimu wa kazi Yangu, je, unaweza kuwa mtu mtiifu ambaye hatoi hukumu kiholela na kufanya maamuzi? 9. Je, unaweza kuthamini maneno yote ambayo Nimeyanena na kazi yote ambayo Nimeifanya wakati Nimekuwa pamoja na wanadamu? 10. Je, unaweza kuwa mfuasi Wangu mwaminifu, aliye tayari kuvumilia mateso ya maisha kwa ajili Yangu, ingawa hupokei chochote? 11. Je, unaweza kuachilia kuzingatia, kupanga, au kuandaa njia yako ya kuendelea kuishi ya siku za baadaye kwa ajili Yangu? Maswali haya yanawakilisha mahitaji Yangu ya mwisho ninayotaka kutoka kwenu, nami Natumai kuwa ninyi nyote mnaweza kunipa majibu. Ikiwa umetimiza jambo moja au mawili ambayo maswali haya yanataka ufanye, basi lazima uendelee kujitahidi. Ikiwa huwezi kutimiza hata moja kati ya mahitaji haya, hakika wewe ni aina ya mtu ambaye atatupwa kuzimu. Sihitaji kusema chochote zaidi kwa watu kama hawa, kwa sababu hakika wao sio watu ambao wanaweza kukubaliana nami. Je, Ninawezaje kumweka nyumbani Kwangu mtu ambaye anaweza kunisaliti katika hali yoyote ile? Kwa wale ambao bado wanaweza kunisaliti katika hali nyingi, Nitazingatia utendaji wao kabla ya kufanya mipango mingine. Hata hivyo, wote wanaoweza kunisaliti, bila kujali ni chini ya hali gani, Sitawahi kusahau; Nitawakumbuka moyoni Mwangu, na kungojea fursa ya kulipiza matendo yao maovu. Mahitaji yote ambayo Nimeibua ni shida ambazo lazima nyote mzichunguze ndani yenu wenyewe. Natumai ninyi nyote mnaweza kuyazingatia kwa makini na kutonishughulika kwa uzembe. Hivi karibuni, Nitaangalia majibu ambayo mmenipa dhidi ya mahitaji Yangu. Kufikia wakati huo, Sitahitaji chochote zaidi kutoka kwenu na Sitawapa onyo lenye ari zaidi. Badala yake, Nitatumia mamlaka Yangu. Wale wanaopaswa kuhifadhiwa watahifadhiwa, wale wanaopaswa kupewa thawabu watapewa thawabu, wale wanaopaswa kukabidhiwa kwa Shetani watakabidhiwa kwa Shetani, wale wanaopaswa kuadhibiwa vikali wataadhibiwa vikali, na wale wanaopaswa kuangamia wataangamizwa. Kwa hiyo, hakutakuwa tena na mtu wa kunisumbua katika siku Zangu. Je, unaamini maneno Yangu? Je, unaamini kulipiza kisasi? Je, unaamini kuwa Nitawaadhibu wale waovu wote wanaonidanganya na kunisaliti? Je, unatarajia siku hiyo ije haraka au ije baadaye? Je, wewe ni mtu ambaye anaogopa adhabu, ama mtu ambaye angenipinga ingawa lazima avumilie adhabu? Siku hiyo itakapowadia, unaweza kukisia ikiwa utaishi katikati ya shangwe na kicheko, au ikiwa utalia na kusaga meno yako? Je, unatarajia kukumbana na mwisho wa aina gani? Je, umewahi kufikiria kwa uzito ikiwa unaniamini asilimia mia moja au una tashwishi nami asilimia mia moja? Je, umewahi kufikiria kwa uangalifu matendo na mwenendo wako vitakuletea matokeo ya aina gani? Je, unatumaini kwa kweli kuwa maneno Yangu yote yatatimizwa, ama unaogopa kuwa maneno Yangu yatatimizwa kama matokeo? Ikiwa unatumaini kuwa Nitaondoka hivi karibuni ili Niyatimize maneno Yangu, je, unapaswa kuyachukuliaje maneno na matendo yako mwenyewe? Ikiwa hutumainii kuondoka Kwangu na hutumaini maneno Yangu yote yatimizwe mara moja, kwa nini uniamini hata kidogo? Kwa kweli unajua mbona unanifuata? Ikiwa sababu yako ni kupanua upeo wako tu, hakuna haja ya kujisumbua kufanya hivyo. Ikiwa ni ili ubarikiwe na kuepukana na msiba unaokuja, mbona hujali kuhusu tabia yako mwenyewe? Mbona hujiulizi ikiwa unaweza kuyakidhi mahitaji Yangu? Mbona pia hujiulizi ikiwa unastahili kupokea baraka zitakazokuja?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Tatizo Zito Sana: Usaliti (2)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 364)

Watu Wangu wote wanaohudumu mbele Zangu wanapaswa kutafakari kuhusu siku zilizopita: Je, upendo wenu Kwangu ulikuwa umetiwa doa na uchafu? Je, uaminifu wenu Kwangu ulikuwa safi na wa moyo wako wote? Je, ufahamu wenu kunihusu ulikuwa wa kweli? Je, Nilikuwa na nafasi kiasi gani katika nyoyo zenu? Je, Nilikuwa Nimejaza nyoyo zenu zote? Je, maneno Yangu yalitimiza kiasi gani ndani yenu? Msinichukue kama mpumbavu! Hivi vitu viko wazi kabisa Kwangu! Leo, sauti ya wokovu Wangu inapopazwa nje, je, kumekuwa na ongezeko la upendo wenu Kwangu? Je, sehemu ya uaminifu wenu Kwangu imekuwa safi? Je, ufahamu wenu kunihusu umezidishwa? Je, sifa ya zamani iliweka msingi dhabiti kwa maarifa yenu leo hii? Je, ni kiasi gani cha undani wenu kinamilikiwa na Roho Wangu? Mfano Wangu unamiliki sehemu kiasi gani ndani yenu? Je, matamshi Yangu yamewagonga katika sehemu yenu ya udhaifu? Je, mnahisi kwa kweli kuwa hamna mahali pa kuficha aibu yenu? Je, mnaamini kwa kweli kuwa hamjafuzu kuwa watu Wangu? Iwapo hutambui kabisa maswali haya, basi hii inaashiria kuwa unafanya kazi gizani, kwamba uko tu pale kuongeza idadi, na kwamba katika muda ulioamuliwa na Mimi kabla ya siku hii, kwa hakika utaangamizwa na kutupwa katika shimo lisilo na mwisho kwa mara ya pili. Haya ni maneno Yangu ya onyo, na yeyote anayeyachukulia kwa wepesi atapigwa na hukumu Yangu, na, kwa wakati ulioteuliwa atapatwa na janga. Sivyo? Je, bado Ninahitaji kutoa mifano ili kueleza hili? Je, inanilazimu kuzungumza kwa uwazi zaidi ili Niweke kigezo kwa ajili yenu? Tangu wakati wa uumbaji mpaka sasa, watu wengi wamekosa kutii maneno Yangu na hivyo wametupwa nje na kutolewa katika mtiririko wa urejesho Wangu; hatimaye, miili yao inaangamia na roho zao zinatupwa kuzimu, na mpaka wa leo bado wanapitia adhabu kali. Watu wengi wameyafuata maneno Yangu, lakini wameenda kinyume na nuru na mwanga Wangu, na hivyo wametupwa kando na Mimi, wakaanguka katika miliki ya Shetani na kuwa wale wanaonipinga. (Leo hii wote wanaonipinga moja kwa moja wanatii ujuu juu wa maneno Yangu peke yake, na kuasi kiini cha maneno Yangu.) Kumekuwa na wengi, pia, ambao wameyasikiza tu maneno Niliyonena jana, ambao wameshikilia vikorokoro vya kale na hawajathamini mazao ya siku hii. Watu hawa hawajafanywa tu wafungwa na Shetani, bali wamekuwa watenda dhambi wa milele na kuwa adui Zangu, na wananipinga moja kwa moja. Watu wa aina hii ndio viumbe Nitakaohukumu wakati wa ghadhabu Yangu kali, na leo hii wao bado ni vipofu, wakiwa bado ndani ya jela zenye giza (ambayo ni kusema, watu kama hawa wameoza, maiti zisizo na hisia ambazo zinadhibitiwa na Shetani; kwa sababu macho yao yamefunikwa na Mimi, Ninasema kuwa wao ni vipofu). Ingekuwa vema kutoa mfano kwa ajili ya kurejelea kwenu, ili mpate funzo kutoka kwa mfano huu:

Kwa kumtaja Paulo, mtafikiria historia yake, na baadhi ya hadithi kumhusu zisizo sahihi na zisizo sawa na hali halisi. Yeye alifunzwa na wazazi wake kutoka umri mdogo, na akapata uhai Wangu, na kwa sababu ya majaliwa Yangu alipata kuwa na ubora wa tabia Ninaohitaji. Akiwa na umri wa miaka 19, alisoma vitabu kadhaa kuhusu maisha; hivyo Sihitaji kueleza kwa kina kuhusu vile, kwa sababu ya ubora wake wa tabia, na kwa sababu ya nuru na mwanga Wangu, hakuweza tu kuzungumza na baadhi ya utambuzi kuhusu mambo ya kiroho, bali pia aliweza kufahamu nia Yangu. Bila shaka, hili haliachi nje muungano wa mambo ya ndani na ya nje. Hata hivyo, udhaifu wake mmoja ulikuwa kwamba, kwa sababu ya talanta zake, mara nyingi angekuwa mwepesi wa kusema maneno yasiyo ya kweli na mwenye kujigamba. Kwa sababu ya hili, kwa ajili ya kutotii kwake, ambako kwa kiasi kuliwakilisha malaika mkuu, Nilipokuwa mwili mara ya kwanza, alijaribu kabisa kuniasi Mimi. Alikuwa mmojawapo wa wale wasiojua maneno Yangu, na nafasi Yangu katika moyo wake ilikuwa tayari imeshapotea. Watu wa aina hii moja kwa moja wanaasi uungu Wangu, na wanaangamizwa na Mimi, na wanainama na kutubu dhambi zao mwishowe tu. Hivyo, baada ya Mimi kumaliza kutumia uwezo wake—ambayo ni kusema, baada ya yeye kunifanyia kazi kwa muda fulani—alirudi tena katika njia zake za zamani, na hata ingawa hakuasi maneno Yangu moja kwa moja, alipuuza mwongozo Wangu na nuru Yangu ya ndani, na hivyo yote aliyokuwa amefanya mbeleni yalikuwa bure; kwa maneno mengine, taji la utukufu alilozungumzia lilikuwa limekuwa maneno tupu, matokeo ya mawazo yake, kwa kuwa hata leo, yeye bado yuko katika hukumu yangu katika minyororo Yangu.

Kutokana na mfano huo hapo juu inaweza kuonekana kuwa yeyote anayeniasi (na sio kuuasi tu mwili Wangu lakini la muhimu zaidi, maneno Yangu na Roho Wangu—ambayo ni kusema, uungu Wangu), anapata hukumu Yangu katika mwili wake. Wakati Roho Wangu Anakuwacha, unaporomoka kwenda chini, unateremka moja kwa moja mpaka kuzimu. Na hata ingawa mwili wako wa nyama uko duniani, wewe ni kama mtu aliye na ugonjwa wa akili: Umepoteza akili yako, na ghafla unahisi ni kama wewe ni maiti, mpaka unanisihi Niutoe mwili wako bila kungoja. Wengi wenu ambao mmejawa na Roho mnao uwezo wa kuelewa hali hii kwa undani, na Mimi sihitaji kuenda katika maelezo mengi zaidi. Katika siku zilizopita, Nilipofanya kazi katika ubinadamu wa kawaida, watu wengi walikuwa tayari wamejipima dhidi ya ghadhabu Yangu na uadhama Wangu, na tayari walijua kiasi kidogo kuhusu hekima na tabia Yangu. Leo hii, Ninazungumza na kutenda moja kwa moja katika uungu, na bado kuna baadhi ya watu ambao wanaona ghadhabu na hukumu Yangu kwa macho yao wenyewe; zaidi ya hayo, kazi muhimu ya sehemu ya pili ya enzi ya hukumu ni kuwafanya watu Wangu wote wajue matendo Yangu katika mwili moja kwa moja, na kuwafanya ninyi nyote muone tabia Yangu moja kwa moja. Ilhali kwa sababu Niko katika mwili, Mimi bado ni mwenye huruma kwa udhaifu wenu. Matumaini Yangu ni kuwa hamtachukua roho, nafsi na mwili wenu kama vitu vya kuchezea, na bila kujali mvikabidhi kwa Shetani. Ni vema mthamini vyote mlivyo navyo, na kutovichukulia kama mchezo, kwa maana vitu hivyo vinahusiana na majaliwa yenu. Je, kweli mnao uwezo wa kuyaelewa maneno Yangu? Je, kweli mnao uwezo wa kujali hisia Zangu za kweli?

Je, mnayo nia ya kustarehe katika baraka Zangu duniani, baraka zilizo sawa na zile za mbinguni? Je, mko tayari kuchukua kuelewa kwao kunihusu, na kufurahia kwa maneno Yangu na ufahamu wako kunihusu, kama vitu vya thamani zaidi na vya muhimu zaidi katika maisha yenu? Je, kweli mnaweza kuwa watiifu Kwangu kikamilifu, bila fikira kwa matarajio yenu wenyewe? Je, kweli mna uwezo wa kujiruhusu kuuwawa na Mimi, na kuongozwa na Mimi, kama kondoo? Je, kunao kati yenu walio na uwezo wa kutimiza vitu kama hivi? Inawezekana kuwa wote wanaokubaliwa na Mimi na kupokea ahadi Zangu ndio wanaopokea baraka Zangu? Je, mmeelewa chochote kutoka katika maneno haya? Nikiwajaribu, je, mnaweza kweli kujiweka wenyewe katika huruma Yangu, na, katikati ya majaribu haya, mtafute nia Yangu na muelewe moyo Wangu? Mimi sitamani wewe uweze kuongea maneno mengi matamu, au utoe hadithi nyingi za kufurahisha; badala yake Ninauliza kuwa uweze kuwa na ushuhuda mzuri Kwangu, na kwamba unaweza kuingia kikamilifu na kwa kina katika hali halisi. Kama Singezungumza moja kwa moja, je, ungewacha kila kitu kilicho karibu na wewe na ukubali kutumiwa na Mimi? Je, hii siyo hali halisi Ninayohitaji? Je, ni nani aliye na uwezo wa kuelewa maana iliyo katika maneno Yangu? Ilhali Ninauliza kuwa msishushwe na wasiwasi tena, kwamba mwe msitari ya mbele katika kuingia kwenu na muelewe kiini cha maneno Yangu. Hii itazuia hali ya nyinyi kutoelewa maneno Yangu, na hali ya kutokuwa na uwazi kuhusu maana Yangu, na hivyo kukiuka amri Zangu za utawala. Natumaini kuwa mtaelewa Nia Yangu kwenu katika maneno Yangu. Msifikiri juu ya matarajio yenu tena, na mtende vile ambavyo mmeamua mbele Yangu kutii mipango ya Mungu katika kila kitu. Wale wote wanaosimama miongoni mwa kaya Yangu wanapaswa kufanya mengi kiasi wanachoweza; unafaa utoe hali yako bora zaidi kwa sehemu ya mwisho ya kazi Yangu duniani. Je, unayo nia ya kuviweka vitu vya aina hii katika matendo?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 4

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 365)

Duniani, kila aina ya pepo wanazungukazunguka bila mwisho wakitafuta mahali pa kupumzika, na bila kukoma wanatafuta maiti za wanadamu zinazoweza kuliwa. Watu Wangu! Lazima mbaki ndani ya utunzaji Wangu na ulinzi. Kamwe msiwahi kuishi katika hali ya upotovu! Msiwahi tenda mambo kiholela! Badala yake, salimisha uaminifu wako katika nyumba Yangu, na ni kwa uaminifu tu ndio unaweza kupinga hila ya Shetani. Katika hali yoyote usiishi kama ilivyokuwa katika siku za awali, kufanya jambo moja mbele Yangu na jingine nyuma Yangu—ukifanya hivyo umeshapita kiwango cha kukombolewa. Hakika Nimetamka zaidi ya kiasi cha kutosha maneno ya aina hii, sivyo? Ni kwa sababu asili ya mwanadamu ya zamani hairekebiki ndiyo maana Nimemkumbusha tena na tena. Usichoke! Haya yote Niyasemayo ni kwa mujibu wa kuhakikisha hatima yako! Kile Shetani anahitaji kwa hakika ni uchafu na pahali pabaya; na kadri unavyokosa kuokoleka kabisa, na kadri unavyokuwa mpotovu, ukikataa kujiwasilisha kwa hali ya kujizuia, ndivyo roho wachafu watakavyotumia nafasi yoyote ya kupenyeza. Mara unapowasili katika hii nafasi, uaminifu wako utakuwa kelele tupu, bila uhalisi wowote, na azimio lako litaliwa na pepo wachafu, kugeuzwa kuwa uasi au hila za Shetani, na kutumiwa kuzuia kazi Yangu. Kuanzia hapo, unaweza kupigwa na Mimi wakati wowote. Hakuna anayeelewa uzito wa hali hii; watu wote hupuuza tu yale wanayosikia na hawachukui tahadhari kwa vyovyote. Sikumbuki kile kilichofanywa katika siku za nyuma. Je, bado unasubiri Niwe mpole kwako Nisahau kwa mara nyingine tena? Ingawa binadamu umenipinga Mimi, Sitashikilia lolote dhidi yake, kwa maana kimo cha mwanadamu ni kidogo mno, na kwa hiyo Sihitaji makubwa kwake. Yote Ninayotaka ni kwamba yeye asijitumie mwenyewe kwa ubadhirifu, na ajiwasilishe kwa kujizuia. Hakika si zaidi ya uwezo wako kufikia sharti hili moja? Wengi wa watu wanasubiri Nifichue mafumbo zaidi ili walishe macho yao. Ilhali, iwapo utakuja kuelewa siri zote za mbinguni, je, ni nini utakalofanya na hayo maarifa? Je, yataweza kuongeza upendo wako Kwangu? Je, yatachochea upendo wako Kwangu? Mimi Simdharau mwanadamu, wala kukata kauli kwa wepesi juu yake. Kama hizi hazingekuwa hali halisi za mwanadamu, Mimi kamwe Singewahi kamwe kuwavisha watu taji na vitambulisho hivi kwa kawaida. Fikiria kuhusu siku za nyuma: Kumekuwepo na nyakati zozote ambazo Nimewahi kuwakashifu nyinyi? Nyakati zozote ambazo Niliwadharau nyinyi? Nyakati zozote ambazo Nimekutazama bila kuzingatia hali zako halisi? Nyakati zozote ambazo Nilichosema kilishindwa kujaza moyo wako na kinywa chako na kusadiki? Nyakati zozote ambazo Nimenena bila ya kuwa na sauti ya undani ndani yenu? Ni nani kati yenu ambaye amesoma maneno Yangu bila hofu na kutetemeka, akiwa na hofu sana kwamba Nitampiga na kumwingiza kuzimu? Ni nani asiyeweza kuvumilia majaribio ndani ya maneno Yangu? Ndani ya maneno Yangu kuna mamlaka, lakini haya si ya kupitisha hukumu ya kawaida juu ya mtu; Badala yake, kwa kujali hali halisi za mwanadamu, daima Namwonyesha mwanadamu maana iliyopo katika maneno Yangu. Kwa kweli, yupo aliye na uwezo wa kutambua nguvu za kudura katika maneno Yangu? Yupo ambaye anaweza kupokea ndani ya nafsi yake dhahabu safi zaidi ambayo maneno Yangu yanaundwa nayo? Nimezungumza maneno mangapi, lakini kuna yeyote ambaye amewahi kuyathamini?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 10

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 366)

Siku baada ya nyingine, Nasimama kwa uchunguzi juu ya ulimwengu, na hujificha Mimi Mwenyewe kwa unyenyekevu katika makazi Yangu nikipitia maisha ya binadamu, na kuchunguza kwa karibu matendo yote ya binadamu. Hakuna aliyewahi kujitolea Kwangu kwa kweli. Hakuna aliyewahi kufuata ukweli. Hakuna aliyewahi kuwa mwangalifu Kwangu. Hakuna aliyewahi kufanya maazimio mbele Yangu na kufanya wajibu wake. Hakuna aliyewahi kuniruhusu kuishi ndani yake. Hakuna aliyewahi kunithamini kama afanyavyo maisha yake. Hakuna aliyewahi kuona, kwa vitendo, kile ambacho uungu Wangu ni; hakuna aliyewahi kutamani kuwasiliana na Mungu wa vitendo Mwenyewe. Wakati maji yanameza wanadamu, Nawaokoa kutokana na maji yaliyotuama na kuwapa nafasi ya kuishi upya. Wanadamu wanapopoteza imani yao ya kuishi, Nawavuta juu kutoka ukingo wa kifo, na kuwapa ujasiri wa kuishi, ili kwamba wananichukua kama msingi wa kuwepo kwao. Wanadamu wanaponiasi, Nawafanya Kunijua kwa kuasi kwao. Kutokana na asili ya zamani ya binadamu na kutokana na huruma Yangu, badala ya kuwaua binadamu, Nawaruhusu kutubu na kuanza upya. Wakati wanadamu wanateseka na kiangazi, Nawatoa kifoni kama bado wamesalia na pumzi moja, kuwazuia kudanganywa na Shetani. Watu wameona mikono Yangu mara ngapi; watu wameona uso Wangu karimu mara ngapi, kuuona uso Wangu wa tabasamu; na wameona adhama Yangu mara ngapi, kuona ghadhabu Yangu. Ingawa binadamu haujawahi kunijua, Siwakamati juu ya udhaifu wao kufanya matata yasiyohitajika. Kupitia ugumu wa binadamu, Nina huruma na udhaifu wake. Ni kwa sababu ya kuasi kwa wanadamu, kutokuwa na shukrani kwao, ndiko Nawaadibu kwa viwango tofauti.

Najificha wakati wanadamu wana kazi nyingi na kujifichua wakati wao wa burudani. Binadamu unanidhania kuwa Anayejua yote na kuwa Mungu Mwenyewe anayekubali maombi yote. Wote basi wanakuja mbele Yangu kutafuta tu msaada wa Mungu, bila kuwa na tamaa ya kunijua. Wakiwa katika maumivu ya magonjwa, wanadamu wananiomba msaada. Wakiwa na shida, wananiambia matatizo yao kwa nguvu zao zote ili kumwaga mateso yao. Na bado hakuna mwanadamu hata mmoja ameweza kunipenda pia akiwa na faraja. Hakuna mtu hata mmoja amenitafuta wakati wa amani na furaha ili Nishiriki furaha yake. Wakati jamii zao ndogo zina furaha na ziko sawa, watu wameniweka kando ama kunifungia mlango, kunikataza kuingia, ili waweze kufurahia baraka za furaha za familia zao jamii. Akili ya binadamu ni nyembamba sana, nyembamba sana hata kumshikilia Mungu, apendaye, mwenye huruma, na mkunjufu kama Mimi. Nimekataliwa mara ngapi na wanadamu wakati wao wa kicheko na furaha, Nimetegemewa kama gongo mara ngapi na wanadamu wakati wanaanguka; Ni mara ngapi Nimelazimishwa kuwa daktari wa wanadamu wanaougua magonjwa. Mwanadamu ni katili jinsi gani! Hawana akili na ni wabaya kabisa. Hawana hata hisia zinazopatikana kwa binadamu. Nusura hawana ubinadamu hata kidogo. Fikiria siku za nyuma na linganisha na sasa. Kuna mabadiliko yanayofanyika ndani zenu? Kuna siku kidogo za zamani sasa? Ama zamani bado haijabadilishwa?

Juu ya mlima na chini ya bonde Nimepitia, na kuwa na uzoefu wa panda shuka za dunia. Nimetembea na kuishi miongoni mwa wanadamu kwa miaka mingi, lakini bado inaonekana tabia ya binadamu imebadilika kidogo. Na ni kama asili ya zamani ya mwanadamu imeeneza mizizi na kuota ndani yao. Hawawezi kamwe kubadili hiyo asili ya zamani, kuiboresha tu kwa msingi wa kwanza. Wasemavyo wanadamu, kiini hakijabadilika, lakini umbo limebadilika sana. Watu wote wanaonekana wakijaribu kunidanganya na kunihadaa, ili waweze kujionyesha ili wapate kuthami na kukubaliwa na Mimi. Sipendi wala kutia maanani ujanja wa wanadamu. Badala ya kukasirika, Nachukua mtazamo wa kuangalia lakini si kuona. Napanga kuwapa binadamu kiwango fulani cha uhuru, na hivyo, kushughulikia wanadamu wote kwa pamoja. Kwa sababu wanadamu wote hawajiheshimu na ni maskini wasio na faida, wasiojithamini, watawezaje kunihitaji kuonyesha huruma na mapenzi mapya? Wanadamu wote hawajijui, na hawajui uzito wao. Wanapaswa kujipima uzito. Binadamu haunitambui, hivyo Nami pia siutilii maanani. Wanadamu hawanitambui, kwa hivyo Mimi pia Siweki juhudi kwao. Je, hii ni bora? Je, hii haiwazungumzii, watu Wangu? Nani amefanya maazimio mbele Yangu na kukosa kuyatupilia mbali baadaye? Nani amefanya maazimio ya muda mrefu mbele Yangu badala ya kutatua mara nyingi juu ya hii na hiyo? Daima, wanadamu hufanya maazimio mbele Yangu wakati wa raha na kuyafuta kabisa wakati wa shida. Baadaye, wanachukua uamuzi wao na kuuweka mbele Yangu. Je, Mimi si wa kuheshimika hadi Naweza kubali kwa kawaida taka iliyookotwa na mwanadamu kutoka pipani? Wanadamu wachache hushikilia maazimio yao, wachache ni safi, na wachache wanatoa yenye thamani kubwa zaidi kama sadaka Kwangu. Je, nyinyi wote si sawa kwa njia hii? Iwapo, kama mmoja wa watu Wangu kwenye ufalme, huwezi kufanya wajibu wenu, mtachukiwa na kukataliwa na Mimi!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 14

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 367)

Wanadamu wote ni viumbe wasio na ufahamu kujihusu, na hawezi kujijua mwenyewe, yeye hata hivyo anajua kila mwanadamu mwingine kama kiganja cha mkono wake, kana kwamba watu wengine wote wamepitia ukaguzi wake na kupokea kibali chake kabla waseme au kufanya chochote, na hivyo ionekane kama yeye amewapima kikamilifu wengine wote mpaka katika hali yao ya kisaikolojia. Binadamu wote wako namna hii. Mwanadamu ameingia katika Enzi ya Ufalme leo hii, lakini asili yake bado haijabadilika. Yeye bado anafanya kama Ninavyofanya akiwa mbele Yangu, lakini nyuma Yangu anaanza kufanya “shughuli” zake mwenyewe za kipekee. Hata hivyo, mara hiyo inapokamilika na anarudi mbele Yangu tena, yeye huwa kama mwanadamu tofauti, akiwa na hali ya utulivu safihi, hali yake ni shwari, na mpigo wa moyo wake ni mtulivu. Je, si hili ndilo hasa hufanya mwanadamu kudharauliwa? Ni watu wangapi huvaa sura mbili tofauti kabisa, moja mbele Yangu na nyingine nyuma Yangu? Wangapi kati yao ni kama wanakondoo wachanga mbele Yangu lakini nyuma Yangu hugeuka na kuwa chui wabaya wenye milia wakali kinyama, na kisha kugeuka ndege wadogo wakirukaruka huku na kule kwa furaha milimani? Ni wangapi huonyesha lengo na uamuzi mbele Yangu? Ni wangapi huja mbele Zangu, kutafuta maneno Yangu kwa kiu na hamu lakini, nyuma Yangu, kukerwa nayo na kuyaacha, kana kwamba maneno Yangu ni mzigo unaosumbua? Mara nyingi, Nikiona jamii ya binadamu ikipotoshwa na adui Yangu, Mimi Nimeacha kuweka matumaini Yangu katika mwanadamu. Mara nyingi, Nikiona mwanadamu akija mbele Zangu kwa machozi akiomba msamaha, lakini kwa sababu ya kutojiheshimu kwake, utundu wake usiorekebika, Nimefunga macho Yangu kwa vitendo vyake kwa hasira, hata wakati moyo wake ni wa kweli na nia yake ni ya dhati. Mara nyingi, Naona mwanadamu akiwa na uwezo wa kuwa na imani ya kushirikiana na Mimi, ambaye, wakati ako mbele Yangu, anaonekana kuwa katika kumbatio Langu, akionja joto lake. Mara nyingi, kwa kuona upole, uchangamfu, na uzuri wa watu Wangu Niliowachagua, katika Moyo wangu Mimi daima Nimekuwa na furaha kwa sababu ya mambo haya. Binadamu hawajui jinsi ya kufurahia baraka Nilizowaamulia kabla katika mikono Yangu, kwa sababu wao hawajui ni nini hasa maana ya baraka au mateso. Kwa sababu hii, wanadamu wako mbali na kweli katika jitihada zao za kunitafuta. Kama hakungekuwa na kesho, ni yupi kati yenu mliosimama mbele Yangu atakuwa safi kama theluji na asiye na lawama kama jiwe la thamani? Hakika upendo wako Kwangu si kitu ambacho kinaweza kubadilishwa kwa mlo wenye ladha, au suti yenye ufahari, au ofisi ya juu na mishahara mikubwa? Au inaweza kubadilishwa na upendo ambao wengine wako nao kwako? Hakika, kupitia majaribu hakutawafukuza wanadamu waache upendo wao Kwangu? Hakika, mateso na dhiki hayatasababisha mwanadamu alalamike dhidi ya kile Nimepanga? Hakuna mwanadamu aliyewahi kweli kufahamu upanga ulio katika kinywa Changu: Yeye anajua maana yake ya juu bila kufahamu undani wake. Kama wanadamu wangeweza kweli kuona ukali wa upanga Wangu, wangekimbia kwa hofu hadi ndani ya mashimo kama panya. Kwa sababu ya kutokuwa kwao na hisia, wanadamu hawaelewi kitu chochote cha maana halisi ya maneno Yangu, na hivyo wao hawana kidokezo kuhusu jinsi maneno Yangu ni yenye kuogofya, au kiasi gani asili yao imefichuliwa, na ni kiasi gani cha upotovu wao umepokea hukumu, ndani ya maneno hayo. Kwa sababu hii, kulingana na mawazo yao yasiyo kamili kuhusu maneno Yangu, watu wengi wamechukua msimamo vuguvugu na usio wa kuwajibika.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 15

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 368)

Katika enzi zote, wengi wametoweka duniani kwa taabu, na kusita, na wengi wamekuja duniani kwa matumaini na imani. Nimeandaa kuja kwa wengi, na pia Nimewaondoa wengi. Watu wengi wamepitia mikono Yangu. Roho nyingi zimetupwa Kuzimu, wengi wameishi katika mwili, na wengi wamekufa na wamezaliwa upya duniani. Hata hivyo kamwe hakuna yeyote kati yao aliyepata nafasi ya kufurahia baraka za ufalme leo. Mimi nimewapa wanadamu mengi sana, lakini wamepata kidogo, lakini kwa sababu mashambulizi ya jeshi la Shetani imewafanya wasiweze kufurahia utajiri Wangu wote. Amekuwa tu na bahati nzuri ya kuangalia juu, lakini hajawahi kuwa na uwezo wa kujifurahisha kikamilifu. Mwanadamu hajawahi gundua nyumba ya hazina mwilini mwake ili kupokea utajiri wa mbinguni, kwa hivyo amepoteza baraka ambazo Nimempa. Je, si roho ya mwanadamu ndio haswa uwezo wa kumuunganisha na Roho Wangu? Mbona mwanadamu hajawahi Kunihusisha na roho yake? Mbona ananikaribia kimwili na asiweze kunikaribia kiroho? Je, sura Yangu ya kweli ni ya kimwili? Mbona mwanadamu hatambui kiini Changu? Kuna uwezekano kuwa hakujawahi kuonekana ishara yoyote Yangu ndani ya roho ya mwanadamu? Je, Nimetoweka kabisa katika roho ya mwanadamu? Ikiwa mwanadamu hataingia katika ulimwengu wa kiroho, atawezaje kufahamu nia Zangu? Je, kuna chochote machoni mwa mwanadamu ambacho kinaweza penyeza moja kwa moja mpaka ulimwengu wa kiroho? Ni mara nyingi Nimemwita mwanadamu kwa Roho Wangu, lakini matendo yake huwa ni kama amechomwa kisu na Mimi, anahusiana nami kwa umbali, katika hofu kubwa kuwa Nitamwongoza kwenda ulimwengu mwingine. Kwa mara nyingi Nimepeleleza ndani ya moyo wa mwanadamu, lakini anabaki bila ufahamu kabisa, akiwa na hofu kubwa kabisa kuwa Nitaingia nyumbani mwake na kuchukua fursa hiyo kumnyang’anya mali yake yote. Kwa hivyo, ananifungia nje, kuniacha bila chochote ila mlango uliofungwa na kukazwa na kuniacha nje kwenye baridi. Ni mara nyingi mwanadamu ameanguka na Nimemwokoa, lakini baada ya kuamka ananiacha mara moja, bila kuguswa na upendo Wangu, mwanadamu kunipiga macho ya hadhari; Sijawahi pasha joto moyo wa mwanadamu. Mwanadamu ni kiumbe kikatili kisichokuwa na hisia. Hata kama amepashwa joto na kumbatio Langu, kamwe hajawahi guswa na jambo hili. Mwanadamu ni kama kiumbe katili cha mlimani. Hajawahi thamini upendo Wangu wa binadamu. Hana nia ya kunikaribia, akipendelea kukaa katika milima, ambapo anavumilia tishio la wanyama pori—lakini bado hana nia ya kuchukua makao ndani Yangu. Simshawishi mwanadamu yeyote: Ninafanya tu kazi Yangu. Siku itawadia ambapo mwanadamu ataogelea kuja upande Wangu kutoka katikati ya bahari kuu, ili aweze kufurahia mali yote ya dunia na kuacha hatari ya kumezwa na bahari.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 20

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 369)

Watu wengi wangependa kunipenda kwa kweli, lakini kwa sababu mioyo yao si yao wenyewe, hawawezi kujidhibiti wenyewe; watu wengi hunipenda kwa kweli katika majaribio Ninayotoa, lakini hawana uwezo wa kuelewa kwamba Mimi kwa kweli Nipo, na wananipenda tu katikati ya utupu; na si kwa sababu ya kuwepo Kwangu halisi; watu wengi, baada ya kuweka nyoyo zao mbele Zangu, hawazijali, na hivyo nyoyo zao zinanyakuliwa na Shetani wakati wowote anapopata nafasi, na baada yake huniacha; watu wengi hunipenda kwa dhati Ninapotoa maneno Yangu, lakini hawathamini maneno Yangu katika roho zao, badala yake wakiyatumia kwa kawaida kama mali ya umma na kuyatupa yalipotoka wakati wowote wanapotaka. Mwanadamu hunitafuta akiwa na maumivu, na hunitazamia akiwa na majaribu. Wakati kuna amani yeye hunifurahia, wakati wa hatari yeye hunikana, wakati ana kazi nyingi yeye hunisahau, na asipokuwa na kitu cha kufanya yeye hufanya vitu kwa namna isiyo ya dhati—lakini kamwe hakuna yeyote ambaye amenipenda katika maisha yake yote. Ningependa mwanadamu awe mwenye bidii mbele Zangu: Mimi Simuombi chochote, ila tu watu wote wanichukulie kwa umakini, kwamba, badala ya kunirairai, waniruhusu kurudisha uaminifu wa mwanadamu. Nuru Yangu, mwangaza na gharama ya juhudi Zangu huenea kwa watu wote, ilhali hivyo pia ukweli halisi wa kila tendo la mwanadamu huenea kwa watu wote, kama ufanyavyo wao kunidanganya. Ni kama kwamba viungo vya udanganyifu wa mwanadamu vimekuwa naye tangu tumboni mwa mamake, kama kwamba amekuwa na mbinu hizi maalum za kuhadaa tangu kuzaliwa kwake. Kuzidisha, hajawahi kufichua siri yake; hakuna mwanadamu aliyewahi kutambua chanzo cha ujuzi huu wa udanganyifu. Matokeo yake ni kuwa mwanadamu anaishi katika udanganyifu bila kujua, na ni kana kwamba yeye hujisamehe mwenyewe, kana kwamba ni mipango ya Mungu na sio yeye kunidanganya. Je, hiki sicho chanzo halisi cha mwanadamu kunidanganya? Je, huu sio mpango wake wa ujanja? Sijawahi kuchanganywa na ushawishi na hila za mwanadamu, kwa maana Mimi Nilishatambua kiini chake muda mrefu uliopita. Nani anayejua kiasi cha uchafu ulio katika damu yake, na kiasi gani cha sumu ya Shetani kimo ndani ya mafupa yake? Mwanadamu anapata uzoefu wa sumu hii kila uchao, hata anakosa busara ya kufahamu maafa ya Shetani na hivyo hana nia ya kutambua “sanaa ya uwepo wa afya.”

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 21

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 370)

Mwanadamu anaishi katikati ya mwanga, ilhali hana habari kuhusu thamani ya mwanga huo. Hana ufahamu kuhusu kiini cha mwanga huo, na chanzo cha mwanga huo, na, zaidi ya hayo, hajui mmiliki wake ni nani. Ninapotuza mwanga huo miongoni mwa binadamu, papo hapo Ninachunguza hali ilivyo miongoni mwa wanadamu: Kwa sababu ya mwanga huo, watu wote wanabadilika, na wanakua, na wametoka gizani. Ninaangalia kila pembe ya ulimwengu, na Ninaona kuwa milima yote imefunikwa na ukungu, kwamba maji yameganda kwa ajili ya baridi, na kwamba, kwa sababu ya kuja kwa mwanga, watu wanatazama Mashariki ili wapate kuona kitu kilicho na thamani zaidi—ilhali mwanadamu bado hana uwezo wa kutambua njia ya wazi kwenye ukungu huo. Kwa sababu dunia nzima imefunikwa kwa ukungu, Ninapotazama kutoka mawinguni, kuwepo Kwangu hakujawahi kutambuliwa na mwanadamu; mwanadamu anatafuta kitu fulani duniani, anaonekana akichakura, anayo nia, inaonekana, ya kusubiri kurudi Kwangu—ilhali yeye hajui siku Yangu, na anaweza tu kutegemea mara kwa mara mwanga unaong’aa mashariki. Miongoni mwa watu wote, Ninatafuta wale wanaoupendeza moyo Wangu kwa kweli. Natembea miongoni mwa watu wote, na kuishi miongoni mwa watu wote, lakini mwanadamu yuko salama salimini duniani, na kwa hivyo hakuna wanaopendeza nafsi Yangu kwa kweli. Watu hawajui jinsi ya kuyajali mapenzi Yangu, hawawezi kuona matendo Yangu, na hawawezi kutembea katika mwanga na kumulikwa na mwanga huo. Hata ingawa mwanadamu daima anayathamini maneno Yangu, yeye hana uwezo wa kuona katika mikakati ya udanganyifu ya Shetani; kwa kuwa kimo cha mwanadamu ni kidogo sana, hana uwezo wa kufanya vile ambavyo moyo wake unatamani. Mwanadamu hajawahi kunipenda kwa dhati. Ninapompandisha, yeye hujiona asiyefaa, lakini hili halimfanyi awe na ari ya kuniridhisha. Yeye hushikilia tu nafasi Niliyompa mikononi mwake na kukichunguza; bila hisia yoyote kwa uzuri Wangu, yeye anasisitiza badala yake kujijaza na baraka za kituo chake. Je, huu sio upungufu wa mwanadamu? Milima inaposonga, je, inaweza kubadili mkondo kwa ajili ya kituo chako? Maji yanaposonga, je, yanaweza kukoma kabla ya kufikia kituo cha mwanadamu? Je, mbingu na dunia zinaweza kubadilishwa na kituo cha mwanadamu? Wakati mmoja Nilikuwa mwenye huruma kwa mwanadamu, mara kwa mara—ilhali hakuna anayependa kwa dhati wala kuthamini haya, waliyasikiliza tu kama hadithi, au waliisoma tu kama tamthilia. Je, maneno Yangu hayauguzi moyo wa mwanadamu? Je, matamshi Yangu kwa kweli hayaleti mabadiliko yoyote? Inawezekana kuwa hakuna anayeamini katika kuwepo Kwangu? Mwanadamu hajipendi mwenyewe; badala yake, anaungana na Shetani ili kunivamia Mimi, na kumtumia Shetani kama “chombo” cha kunitumikia Mimi. Nitapenyeza katika mipango yote ya Shetani, na kuwazuia watu wote wa duniani dhidi ya kukubali uongo wa Shetani, ili wasije wakaniasi Mimi kwa ajili ya kuwepo kwa Shetani.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 22

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 371)

Machoni Pangu, mwanadamu ndiye mtawala wa vitu vyote. Nimempa mamlaka si haba, Nikimwezesha kusimamia vitu vyote duniani—nyasi iliyo juu ya milima, wanyama katika misitu, na samaki majini. Badala ya kuwa na furaha kwa sababu ya haya, mwanadamu anasumbuliwa na wasiwasi. Maisha yake yote ni yale ya maumivu makali, na kukimbia hapa na pale, na raha kuongezwa kwa utupu, na katika maisha yake yote hakuna uvumbuzi na uundaji mpya. Hakuna anayeweza kujinasua kutoka katika utupu huu wa maisha, hakuna ambaye amegundua maisha ya maana, na hakuna ambaye amepitia maisha ya kweli. Ingawa watu wa leo wote wanaishi chini ya mwanga Wangu unaong’aa, hawajui lolote kuhusu maisha ya mbinguni. Nisipokuwa na huruma kwa mwanadamu na Nisipomwokoa binadamu, basi watu wote wamekuja bure, maisha yao duniani hayana maana, na wataondoka bure, bila chochote cha kujigamba nacho. Watu wa kila dini, nyanja ya jamii, taifa, na dhehebu wote wanajua utupu ulio duniani, na wote wananitafuta na kungoja kurejea Kwangu—ilhali nani ana uwezo wa kunifahamu nitakapofika? Nilitengeneza vitu vyote, niliumba binadamu, na leo nimeshuka kati ya mwanadamu. Mwanadamu, lakini, anagonga nyuma Yangu, na kulipisha kisasi Kwangu. Je, kazi Ninayofanya kwa mwanadamu haina faida yoyote kwake? Je, Mimi hakika sina uwezo wa kumtosheleza mwanadamu? Mbona mwanadamu ananikataa? Mbona mwanadamu ni baridi na hana hisia Kwangu? Mbona ardhi imejawa na maiti? Je, hii ndiyo hali ya dunia Niliyomtengenezea mwanadamu? Mbona Nimempa mwanadamu mali isiyo ya kufananishwa, ilhali ananipa Mimi mikono miwili mitupu? Mbona mwanadamu hanipendi kwa kweli? Mbona haji kamwe mbele Zangu? Maneno Yangu yote yamekuwa ya bure? Je, maneno yamepotea jinsi joto lipoteavyo kwa maji? Mbona mwanadamu hataki kushirikiana na Mimi? Je, wakati wa kufika kwa siku Yangu ni wakati wa kufa kwa mwanadamu kweli? Je, hakika Ningeweza kumwangamiza mwanadamu wakati ufalme Wangu utatengenezwa? Mbona, wakati wa mpango Wangu wa usimamizi wote, hakuna ambaye ameweza kuelewa nia Zangu? Mbona, badala ya kuyatunza matamshi ya kutoka kwa mdomo Wangu, mwanadamu anayachukia na kuyakataa? Simkashifu yeyote, ila tu Nawafanya watu wote watulie na kutekeleza kazi ya kujiangalia kwa undani.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 25

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 372)

Mwanadamu ameshuhudia upendo Wangu, mwanadamu amenitumikia kwa dhati, na mwanadamu amenitii kwa kweli, akinifanyia kila kitu katika uwepo Wangu. Ilhali jambo hili haliwezi kutimizwa na watu ; wanalia tu katika roho zao kana kwamba wamenyakuliwa na mbweha mwenye njaa, na wanaweza tu kunitazama na macho yenye hamu, wakinililia bila kukoma. Lakini mwishowe, hawawezi kujiondoa katika matatizo yanayowakumba. Ninakumbuka jinsi ambavyo watu wa kale waliweka ahadi mbele Zangu, wakiapa kwa mbingu na dunia mbele Zangu kulipiza ukarimu Wangu kwa upendo. Walilia kwa uchungu mbele Yangu, na kilio chao kilikuwa cha kuvunja moyo, kigumu kuvumilia. Kwa sababu ya azimio lao, mara nyingi niliwapa watu msaada. Mara nyingi, wanadamu wamekuja mbele Zangu kunitii, mienendo yao ya kupendeza isiyoweza kusahaulika. Mara nyingi, wamenipenda bila kutikisika katika uaminifu wao, bidii yao ikiwa ya kupendeza. Mara nyingi, wamenipenda hadi kiwango cha kuhatarisha maisha yao, wakanipenda Mimi hata zaidi ya wanavyojipenda wenyewe—na kwa vile Nimeona upendo huu ni wa kweli, Nimeukubali. Mara nyingi, wamejitoa kama sadaka mbele Yangu, bila kujali mauti kwa sababu Yangu, na Nimepangusa wasiwasi huo nyusoni mwao, na kwa uangalifu nimekadiria maumbile yao. Kumekuwa na nyakati zisizohesabika ambapo Nimewapenda kama kitu kinachothaminiwa, na kuna wakati mwingine mwingi ambao Nimewachukia kama adui Zangu. Hata hivyo, kile kilicho fikirani Mwangu hakiwezi kueleweka na mwanadamu. Wanadamu wakiwa na huzuni, Mimi huja kuwafariji, na wakiwa wanyonge Mimi huja kuwasaidia katika mwendo. Wanapopotea njia, Mimi huwapa mwelekeo. Wanapolia, Mimi hufuta machozi yao. Lakini, Nionapo huzuni, nani anaweza kunifariji kwa moyo wake? Ninapopatwa na hofu, ni nani hujali hisia Zangu? Ninapoona huzuni, ni nani anayeweza kutibu kidonda kilicho moyoni Mwangu? Ninapohitaji mtu karibu Nami, ni nani anayejitolea kushirikiana na Mimi? Inawezekana kuwa malengo yao ya kale Kwangu yamebadilika yasiweze kurudi tena? Ni kwa nini kwamba hakuna lolote kati ya haya wanalokumbuka? Inawezekanaje kuwa wanadamu wameyasahau yote haya? Je, haya yote si kwa sababu ya mwanadamu kupotoshwa na adui yake?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 27

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 373)

Mungu aliwaumba wanadamu, lakini Anapokuja kwa ulimwengu wa wanadamu, watu hutaka kumpinga na humfukuza kutoka kwa eneo lao, kana kwamba Yeye ni yatima fulani tu, akielea duniani, au kama mtu wa dunia asiye na nchi. Hakuna mtu anayehisi kumpenda Mungu sana, hakuna mtu anayempenda kweli, hakuna mtu ambaye amekaribisha kuja kwake. Badala Yake, wanapoona kuja kwa Mungu, kufumba na kufumbua nyuso zao za furaha huwa na huzuni, kana kwamba dhoruba ya ghafula inakaribia, kana kwamba Mungu angeondoa raha ya familia zao, kana kwamba Mungu hakuwahi kamwe kuwabariki wanadamu, lakini badala yake Alikuwa Amewapa wanadamu taabu. Kwa hivyo, katika akili za wanadamu, Mungu si mwandani kwao, lakini Yule ambaye daima huwalaani; kwa hivyo, wanadamu hawamtilii maanani, hawamkaribishi, kila mara wao huwa hasimu Kwake, na hili halijawahi kubadilika kamwe. Kwa sababu wanadamu wana mambo haya katika mioyo yao, Mungu asema wanadamu hawana akili na ni waovu, na kwamba hata hisia ambazo wanadamu kwa kuwazia wamejizatiti nazo haziwezi kuonekana ndani yao. Wanadamu hawadhihirishi fikira yoyote kwa hisia za Mungu, lakini hutumia kinachoitwa “haki” kumshughulikia Mungu. Wanadamu wamekuwa hivi kwa miaka mingi na kwa sababu hii Mungu amesema tabia yao haijabadilika. Hili linaonyesha wazi kwamba hawana dutu linalozidi manyoya machache. Inaweza kusemwa kwamba wanadamu ni wanyonge wasio na thamani kwa sababu hawajithamini. Kama hata hawajipendi, bali hujikandamiza, hili halionyeshi kwamba hawana thamani? Wanadamu ni kama mwanamke mwovu ambaye hujihadaa na ambaye hujitoa kwa wengine kwa hiari kuingiliwa bila heshima. Lakini hata hivyo, bado hawajui vile walivyo duni. Wao hufurahia kuwatumikia wengine, au kuzungumza na wengine, kujiweka chini ya utawala wa wengine; huu kweli si uchafu wa wanadamu? Ingawa Sijapitia maisha miongoni mwa wanadamu, kwa vile Sijapitia kweli maisha ya binadamu, Nina ufahamu kamili wa kila mwendo, kila hatua, kila neno, na kila kitendo cha mwanadamu. Naweza hata kuwaweka wanadamu wazi mpaka waaibike kabisa, kiasi cha kutoweza tena kuthubutu kuonyesha hila zao na kutoweza tena kuthubutu kujiachilia kwa tamaa zao. Kama konokono ambaye hurudi ndani ya kombe lake, hawathubutu tena kuonyesha hali zao mbaya. Kwa sababu wanadamu hawajijui, dosari yao kubwa sana ni kuonyesha kwa hiari haiba yao mbele ya wengine, wakionyesha sura yao mbaya; Hiki ni kitu ambacho Mungu hukichukia zaidi. Kwa sababu mahusiano kati ya watu si ya kawaida, na hakuna mahusiano ya kawaida ya mtu mmoja na mwingine kati ya watu, sembuse uhusiano wa kawaida kati yao na Mungu. Mungu amesema mengi sana, na kwa kufanya hivyo lengo Lake kuu ni kumiliki nafasi ndani ya mioyo ya wanadamu, kuwafanya watu waondoe sanamu zote ndani ya mioyo yao, ili Mungu aweze kuwatawala wanadamu wote na Atimize lengo Lake la kuwa duniani.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufafanuzi wa Mafumbo ya “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima”, Sura ya 14

Iliyotangulia: Kufunua Upotovu wa Wanadamu (I)

Inayofuata: Kuingia Katika Uzima

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp