Kuingia Katika Uzima (I)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 374)

Mwenyezi Mungu, Mkuu wa vitu vyote, hushika madaraka Yake ya kifalme kutoka kwa kiti Chake cha enzi. Yeye hutawala ulimwengu na vitu vyote na Yeye yuko katika harakati ya kutuongoza katika dunia yote. Kila wakati tutakuwa karibu na Yeye, na kuja mbele Zake kwa utulivu; kamwe hatutakosa wakati mmoja, na kuna mambo ya kujifunza wakati wote. Mazingira yanayotuzunguka pamoja na watu, mambo na vitu, yote yameruhusiwa na kiti Chake cha enzi. Usiwe na moyo wa kunung’unika, au Mungu hatatupa neema Yake juu yako. Wakati ugonjwa hutokea ni kwa sababu ya upendo wa Mungu, na nia Yake nzuri kwa hakika inaiunga mkono. Hata wakati mwili wako unavumilia mateso, usichukue ushauri kutoka kwa Shetani. Sifu Mungu katikati ya ugonjwa na furahia Mungu katikati ya sifa yako. Usikate tamaa unapokabiliwa na ugonjwa, endelea kutafuta na kamwe usisalimu amri, na Mungu Ataangaza nuru Yake kwako. Ayubu alikuwa mwaminifu kiasi gani? Mwenyezi Mungu ni daktari mwenye nguvu zote! Kukaa katika ugonjwa ni kuwa mgonjwa, lakini kukaa katika roho ni kuwa mzima. Kama unayo pumzi moja tu, Mungu hatakuacha ufariki.

Ndani yetu tuna uzima wa Kristo Aliyefufuka. Bila shaka, hatuna imani mbele ya Mungu: Na iwe kwamba Mungu Atie imani ya kweli ndani yetu. Neno la Mungu ni tamu kweli! Neno la Mungu ni dawa yenye nguvu! Tilia aibu mapepo na Shetani! Kama sisi tutafahamu neno la Mungu tutakuwa na msaada na neno Lake litaokoa mioyo yetu kwa haraka! Linaondoa vitu vyote na kuweka yote kwa amani. Imani ni kama daraja moja la gogo la mti, wale ambao hushikilia maisha kwa unyonge watakuwa na ugumu katika kulivuka, lakini wale ambao wako tayari kujitolea wenyewe wanaweza kulivuka bila wasiwasi. Kama mtu ana mawazo ya uoga na ya kuogofya, wao wanadanganywa na Shetani. Ina hofu kwamba tutavuka daraja la imani ili kuingia katika Mungu. Shetani hubuni kila njia iwezekanayo kututumia mawazo yake, tunapaswa daima kuomba kwamba nuru ya Mungu itatuangazia sisi, na ni lazima daima tumtumainie Mungu kututakasa kutoka kwa sumu ya shetani. Daima tutakuwa tukitenda katika roho zetu kuja karibu na Mungu. Tutamruhusu Mungu kuwa na utawala juu ya asili yetu yote.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matamko ya Kristo Mwanzoni, Sura ya 6

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 376)

Bila kujali mtu anaelewa ukweli kiasi gani, ni kiasi kipi cha wajibu ambacho mtu ametimiza, ni kiasi gani cha uzoefu ambacho mtu amepata wakati wa kutekeleza wajibu huo, jinsi kimo cha mtu kilivyo kikubwa au kidogo, au aina ya mazingira ambayo mtu yuko ndani, jambo moja ambalo hawezi kulikosa ni kwamba katika kila kitu anachofanya, lazima amtegemee Mungu na kumtumainia Mungu. Hii ndiyo aina kubwa zaidi ya hekima. Kwa nini nasema kuwa hii ndiyo hekima kubwa zaidi? Hata kama mtu amekuja kuelewa ukweli mwingi, je, atafanikiwa iwapo hamtumainii Mungu? Watu wengine, baada ya kumwamini Mungu kwa muda mrefu kidogo, wamekuja kuelewa ukweli kiasi na wamepitia majaribu machache. Huenda wana uzoefu mdogo wa kiutendaji, lakini hawajui jinsi ya kumtegemea Mungu, na hawaelewi jinsi ya kumtumainia Mungu. Je, watu kama hawa wana hekima? Wao ndio watu wapumbavu zaidi, na ni aina ya watu ambao hujiona kuwa mahiri; hawamwogopi Mungu na kuepuka uovu. Watu wengine husema: “Ninaelewa ukweli mwingi na nina uhalisi wa ukweli. Ni sawa kufanya tu vitu kwa njia yenye maadili. Mimi ni mwaminifu kwa Mungu na ninajua jinsi ya kumkaribia Mungu. Je, si inatosha kwamba mimi natumainia ukweli?” “Kutumainia ukweli” ni sawa, kulingana na mafundisho. Lakini kuna nyakati nyingi na hali nyingi ambapo watu hawajui ukweli ni nini au kanuni za ukweli ni nini. Wote walio na uzoefu wa vitendo wanajua jambo hili. Kwa mfano, unapokumbana na masuala fulani, ikiwa hujui jinsi ambavyo ukweli unaohusika katika suala hili unapaswa kutendwa au jinsi unavyotakiwa kutumika, unapaswa kufanya nini nyakati kama hizi? Bila kujali una uzoefu wa vitendo kiasi gani, huwezi ukawa na ukweli katika hali zote. Bila kujali umemwamini Mungu kwa miaka mingapi, umepitia vitu vingapi, umepitia upogoaji, ushughulikiwaji, au kufundishwa nidhamu kiasi gani, je, wewe ndiye chanzo cha ukweli? Watu wengine husema: “Nimekariri maneno na vifungu vinavyojulikana sana katika kitabu cha Neno Laonekana katika Mwili. Sihitaji kumtegemea Mungu au kumtumainia Mungu. Wakati utakapofika, nitakuwa sawa tu nikitegemea maneno haya ya Mungu.” Maneno ambayo umeyakariri hayabadiliki, lakini mazingira unayokumbana nayo na hali zako hubadilika. Kuwa na ufahamu kuhusu maneno halisi na kuongea juu ya mafundisho mengi ya kiroho si sawa na ufahamu wa ukweli, sembuse kuwa sawa na wewe kuelewa kikamilifu mapenzi ya Mungu katika kila hali. Kwa hivyo kuna somo la muhimu sana la kujifunza hapa. Ni kwamba watu wanahitaji kumtegemea Mungu katika mambo yote, na kwamba kwa kumtegemea Mungu katika mambo yote, watu wanaweza kufanikisha imani katika Mungu. Ni kwa kumtegemea Mungu tu ndio watu wanakuwa na njia ya kufuata. Vinginevyo, unaweza kufanya kitu kwa usahihi na kwa kufuata kanuni za ukweli, lakini usipomtegemea Mungu, basi kile unachofanya ni tendo la mwanadamu tu, na si sharti kuwa linamridhishi Mungu. Kwa sababu watu wana ufahamu wa juu juu sana kuhusu ukweli, huenda wakafuata sheria na kushikilia kwa ukaidi maandiko na mafundisho kwa kutumia ukweli huo huo wanapokabiliwa na hali tofauti. Inawezekana kwamba mambo mengi yanaweza kukamilishwa kwa kawaida kwa kufuata kanuni za ukweli, lakini mwongozo wa Mungu haupo, wala kazi ya Roho Mtakatifu. Kuna tatizo kubwa hapa, ambalo ni kwamba watu hufanya mambo mengi kwa kutegemea uzoefu wao na sheria ambazo wameelewa, na mawazo fulani ya binadamu. Wanaweza kufikia matokeo bora kabisa kwa shida, ambayo hutokana na kuelewa mapenzi ya Mungu kwa wao kumtegemea Mungu na kumwomba Mungu, na kisha kwa kutumainia kazi na mwongozo wa Mungu. Kwa hivyo Nasema: Hekima kuu zaidi ni kumtegemea Mungu na kumtumainia Mungu katika mambo yote.

Kimetoholewa kutoka katika “Waumini Wanahitaji Kwanza Kubaini Mielekeo Mibaya ya Dunia” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 377)

Ukweli ni maisha ya Mungu Mwenyewe, ukiiwakilisha tabia Yake binafsi, ukiwakilisha dutu Yake binafsi, ukiwakilisha kila kitu ndani Yake. Ukisema kwamba kuwa na uzoefu fulani kunamaanisha kuwa una ukweli, basi unaweza kuwakilisha tabia ya Mungu? Huwezi. Mtu anaweza kuwa na uzoefu fulani ama mwanga kuhusu kipengele fulani ama upande wa ukweli, lakini hawezi kuwatolea wengine milele, kwa hivyo mwanga wake sio ukweli; ni kiwango tu ambacho kinaweza kufikiwa na mtu. Ni uzoefu unaofaa tu na ufahamu unaofaa ambao mtu anapaswa kuwa nao, ambao ni uzoefu na ufahamu wake halisi wa ukweli. Mwanga huu, nuru na uelewa kwa msingi wa uzoefu hayatawahi kuwa mbadala wa ukweli; hata kama watu wote wamepata uzoefu wa ukweli huu kabisa, na wakiweka pamoja uzoefu na ufahamu wao wote, hilo bado halilingani na ukweli huo mmoja. Kama ilivyosemwa zamani, “Nilifupisha hili kwa ajili ya dunia ya binadamu kwa kanuni: Miongoni mwa wanadamu hakuna yule anayenipenda Mimi.” Hii ni kauli ya ukweli, ni asili ya kweli ya maisha, ni kitu chenye cha maana sana, ni udhihirisho wa Mungu binafsi. Unaweza kuipitia. Ukiipitia kwa miaka mitatu utakuwa na uelewa usio na kina, ukiipitia kwa miaka minane utapata uelewa zaidi, lakini uelewa wako hautaweza kuwa mbadala wa kauli ya ukweli. Mtu mwingine akipata uzoefu wake kwa miaka miwili atakuwa na uelewa mdogo; akiupitia kwa miaka kumi atakuwa na uelewa wa juu, na akipata uzoefu kwa maisha yake yote atapata uelewa mkubwa zaidi, lakini mkiuweka uelewa wenu pamoja, haijalisha uelewa wa kiwango kipi, uzoefu wa kiwango kipi, ufahamu kiasi gani, mwanga wa kiasi kipi, ama mifano mingapi ambayo ninyi wawili mnayo, hayo yote hayawezi kuwa mbadala wa kauli hiyo. Ninamaanisha nini na hili? Namaanisha kwamba maisha ya mwanadamu daima yatakuwa maisha ya mwanadamu, na haijalishi uelewa wako unalingana vipi na ukweli, kulingana na maana ya Mungu, kulingana na nia za Mungu, hayataweza kamwe kuwa mbadala wa ukweli. Kusema kuwa watu wana ukweli kunamaanisha kuwa wana uhalisi fulani, kuwa wana uelewa fulani wa ukweli wa Mungu, kuwa wana kuingia wa kweli katika maneno ya Mungu, kuwa wana uzoefu fulani wa kweli na maneno ya Mungu, na kuwa wako katika njia sahihi katika imani yao kwa Mungu. Kauli moja tu ya Mungu inatosha mtu kupata uzoefu kwa maisha yake yote; hata kama watu wangekuwa na uzoefu wa maisha kadhaa ama wa milenia kadhaa, bado hawangeweza kuupitia ukweli kabisa. Kama umeelewa tu maneno ya juu juu kisha useme kuwa una ukweli, je si hilo halina msingi? …

Wakati watu wanaelewa ukweli, na kuishi na ukweli kama maisha, hili linaashiria maisha gani? Ni maisha ambayo watu wanaishi wakilitegemea neno la Mungu. Watu wanapokuwa na uzima huo ndani yao, basi maisha yao yanaishiwa kulingana na ukweli, maisha yao yanaishiwa katika eneo la ukweli, maisha yao yamejawa na uelewa wa ukweli, na uzoefu wa ukweli, kuwa kwa msingi huu na kutoenda nje ya mawanda hayo—hayo ndiyo maisha yanayorejelewa. Watu wanautegemea ukweli kama maisha yao, na kuishi maisha yao kulingana na ukweli. Si kwamba wakati watu wanautegemea ukweli kama maisha yao basi wana maisha ya ukweli; si kusema pia kuwa kama una ukweli kama maisha unakuwa ukweli, na maisha yako ndani yanakuwa maisha ya ukweli. Mwishowe maisha yako bado ni maisha ya mwanadamu. Unaweza kuishi ukiyategemea maneno ya Mungu, uwe na uelewa fulani wa ukweli, na kuelewa kwa kiwango cha juu, na uelewa huu hauwezi kuchukuliwa kutoka kwako; unapata uzoefu na kuelewa kikamilifu, unahisi kuwa vitu hivi ni vizuri, ni vya thamani sana, na unakuja kuvikubali kama msingi wa maisha yako, na unaishi ukitegemea vitu hivi, basi hakuna anayeweza kubadilisha hayo, haya ni maisha yako. Maisha yako yana vitu hivi tu, yana uelewa pekee, uzoefu, na ufahamu wa ukweli; haijalishi utakachofanya utakuwa unaishi kwa kutegemea vitu hivi, na haijalishi utakachofanya hutaenda zaidi ya mawanda haya, hutaenda zaidi ya mipaka hii; hayo yatakuwa maisha yako, na kusudi la mwisho la kazi ya Mungu ni kwamba watu watakuwa na maisha ya aina hii. Kama Mungu Mwenyewe binafsi Alikamilisha kikundi cha Miungu wakubwa na Miungu wadogo, je huo haungekuwa machafuko? Hata hivyo, hilo ni jambo lisilowezekana, ni jambo la upumbavu, ni dhana ya upumbavu kutoka kwa binadamu, na sio jambo linalowezekana. Mungu Anaweza tu kuwaumba watu, Mungu hawezi kumuumba Mungu; Mungu Anaweza tu kupata mwili kama mfano wa mwili, lakini haimaanishi kuwa Alimuumba Mungu. Mungu hakujiumba Mwenyewe, Yeye ana dutu Yake binafsi, ambayo haitabadilika kamwe. Hakujiumba Mwenyewe, Anaweza tu kuumba watu na kuumba vitu vingine. Kama una uzoefu fulani na maneno ya Mungu, na unaishi kwa kutegemea uelewa wako wa ukweli, basi neno la Mungu linakuwa maisha yako. Huwezi kusema kuwa ukweli ni maisha yako, kuwa unachoeleza ni ukweli; kama unafikiria hivyo, basi umekosea. Kama una uzoefu fulani na kipengele cha ukweli, je, hili linaweza kuuwakilisha ukweli? Haliwezi kuwakilisha ukweli kabisa. Kwa hivyo unaweza kunena ukweli kabisa? Je, unaweza kueleza ukweli kikamilifu? Huwezi kwa kweli. Unaweza kugundua tabia ya Mungu kutoka kwa ukweli? Unaweza kugundua kiini cha Mungu? Huwezi. Uzoefu wa kila mtu wa ukweli ni kipengele chake kimoja tu na mtazamo mmoja; kwa kupata uzoefu wake katika mawanda yako finyu, huwezi kugusia ukweli wote. Je, watu wanaweza kuishi kwa kudhihirisha maana asili ya ukweli? Uzoefu wako mdogo unajumuisha kiwango kipi? Chembe ya changarawe ufuoni, tone la maji baharini. Kwa hiyo, bila kujali jinsi ufahamu na hisi zako kutoka kwa uzoefu wako ni ya thamani, hata kama ni za thamani sana—haziwezi kuhesabika kama ukweli. Chanzo cha ukweli na maana ya ukweli ni pana sana. Hakuna kinachoweza kuupinga. Watu wengine husema pia, “Je uzoefu wangu hautapingwa kamwe?” Bila shaka, hali yako ya ukweli ambayo umeipata kutoka kwa uzoefu itawezaje kupingwa? Ukweli unaweza kuwa maisha yako katika mazingira yoyote, unaweza kukupa njia, na unaweza kukuruhusu kuishi. Hata hivyo, vitu ambavyo watu wanavyo, mwanga ambao watu wamepata, vinawafaa tu wao binafsi ama kwa wengine katika mawanda fulani, lakini havitafaa katika mawanda tofauti. Uzoefu wa mtu ni finyu sana haijalishi ni wa maana kiasi gani, na uzoefu wao hautawahi kufikia kamwe mawanda ya ukweli. Mwanga wa mtu, uelewa wa mtu, hauwezi kamwe kulinganishwa na ukweli.

Kimetoholewa kutoka katika “Je Unajua Ukweli Hakika Ni Nini?” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 380)

Wale ambao wanaweza kutia ukweli katika vitendo wanaweza kukubali uchunguzi makini wa Mungu katika matendo yao. Unapokubali uchunguzi makini wa Mungu, moyo wako unawekwa kuwa sawa. Ikiwa daima unafanya tu mambo kwa ajili ya wengine kuona na hukubali uchunguzi makini wa Mungu, je, una Mungu moyoni mwako? Watu kama hawa hawana moyo unaomcha Mungu. Usifanye mambo kwa ajili yako daima na usiyafikirie masilahi, hadhi na sifa yako mwenyewe kila wakati. Pia usiyafikirie masilahi ya mwanadamu. Lazima kwanza uyafikirie masilahi ya nyumba ya Mungu, na uyape kipaumbele. Unapaswa kuyafikiria mapenzi ya Mungu na uanze kwa kutafakari kama umekuwa mwenye najisi katika utimizaji wa wajibu wako au la, kama umefanya kila uwezalo kuwa mwaminifu, kama umefanya kila uwezalo kutimiza majukumu yako, na kufanya kadiri uwezavyo au la, na vile vile kama umefikiria wajibu wako na kazi ya nyumba ya Mungu kwa moyo wote au la. Lazima uyazingatie mambo haya. Yafikirie mara kwa mara, na itakuwa rahisi kwako kutekeleza wajibu wako. Iwapo wewe ni mwenye ubora duni wa tabia, uzoefu wako ni wa juu juu, au wewe hujabobeba katika kazi yako ya kitaalamu, basi kunaweza kuwa na makosa au upungufu katika kazi yako, na matokeo huenda yasiwe mazuri sana—lakini utakuwa umetiajuhudi zako zote. Wakati hufikirii tamaa zako za binafsi ama kufikiria maslahi yako mwenyewe katika mambo unayoyafanya, na badala yake unafikiria kila wakati kuhusu kazi ya nyumba ya Mungu, ukifikiria maslahi yake, na kutimiza wajibu wako vizuri, basi utakuwa ukikusanya matendo mema mbele za Mungu. Watu wanaotenda matendo haya mema ndio wale walio na uhalisi wa ukweli; hivyo, wamekuwa na ushuhuda. Ukiishi daima kulingana na mwili, daima kuridhisha tamaa zako mwenyewe za binafsi, basi mtu kama huyo hana uhalisi wa ukweli. Hii ni alama ya mtu ambaye anamwaibisha Mungu. Unasema, “Sijafanya chochote; nimemwaibisha Mungu vipi?” Katika mawazo na fikira zako, katika nia, malengo na sababu za matendo yako, na katika matokeo ya yale ambayo umeyafanya—katika kila njia unamridhisha Shetani, ukiwa kichekesho chake, na kumwacha ajue jambo litakalokuathiri. Huna ushuhuda unaopaswa kuwa nao kama Mkristo hata kidogo. Unafedhehesha jina la Mungu katika mambo yote na huna ushuhuda wa kweli. Je, Mungu atakumbuka mambo ambayo umeyafanya? Mwishowe, Mungu atakuwa na uamuzi upi kuhusu matendo yako na wajibu ambao umetimiza? Je, hakupaswi kuwa na matokeo ya hayo, aina fulani ya maelezo? Katika Biblia, Bwana Yesu anasema, “Wengi watasema kwangu siku hiyo, Bwana, Bwana, je, hatujatabiri kupitia jina Lako? na kutoa mapepo kupitia jina Lako? na kutenda miujiza mingi kupitia jina Lako? Na hapo ndipo Nitasema wazi kwao, Sikuwahi kuwajua: tokeni Kwangu, ninyi ambao hutenda udhalimu.” Kwa nini Bwana Yesu alisema hili? Kwa nini wale wanaowaponya wagonjwa na kuwatoa mapepo katika jina la Bwana, ambao wanasafiri kuhubiri katika jina la Bwana, wanageuka kuwa watenda maovu? Hawa watenda maovu ni nani? Je, ni wale wasiomwamini Mungu? Wote wanamwamini Mungu na kumfuata Mungu. Pia wanatelekeza vitu kwa ajili ya Mungu, kujitumia kwa ajili ya Mungu, na kutimiza wajibu wao. Hata hivyo, katika kutimiza wajibu wao wanakosa moyo na ushuhuda, kwa hiyo imekuwa kutenda maovu. Hii ndiyo maana Bwana Yesu anasema, “Tokeni Kwangu, ninyi ambao hutenda udhalimu.”

Ni kiwango kipi ambacho kulingana nacho matendo ya mtu yanaonwa kuwa mema au mabaya? Inategemea na iwapo katika fikira, maonyesho, na matendo yako, una ushuhuda wa kutia ukweli katika vitendo na wa kuishi kwa kudhihirisha uhalisi wa ukweli au la. Ikiwa huna uhalisi huu au huishi kwa kudhihirisha hili, basi bila shaka wewe ni mtenda maovu. Je, Mungu anawatazamaje watenda maovu? Fikira zako na matendo ya nje hayashuhudii kwa Mungu, wala hayamwaibishi Shetani au kumshinda; badala yake, yanamwaibisha Mungu, na katika kila kitu ni ishara za kumfanya Mungu aibike. Humshuhudii Mungu, hujitumii kwa ajili ya Mungu, na hutimizi jukumu na wajibu wako kwa Mungu lakini badala yake unatenda kwa ajili yako. Ni nini maana ya “kwa ajili yako”? Kwa ajili ya Shetani. Kwa hiyo, mwishowe Mungu atasema, “Tokeni Kwangu, ninyi ambao hutenda udhalimu.” Machoni pa Mungu, matendo yako hayajakuwa mema lakini badala yake yamekuwa matendo mabaya. Hakuna thawabu. Mungu hakukumbuki. Je, huu si utupu? Kwa kila mmoja wenu anayetimiza wajibu wake, haijalishi jinsi unavyoelewa ukweli kwa kina, iwapo ungependa kuingia katika uhalisi wa ukweli, basi njia rahisi zaidi ya kutenda ni kufikiria maslahi ya nyumba ya Mungu katika kila kitu unachofanya, na kuachana na tamaa zako za kibinafsi, nia zako binafsi, dhamira, heshima na hadhi. Yaweke maslahi ya nyumba ya Mungu kwanza—hili ndilo jambo la msingi kabisa unalopaswa kufanya. Ikiwa mtu anayetimiza wajibu wake hawezi hata kufanya kiwango hiki, basi anawezaje kusemwa kuwa anatimiza wajibu wake? Huku si kutimiza wajibu wa mtu. Unapaswa kwanza kufikiria maslahi ya nyumba ya Mungu, ufikirie maslahi ya Mungu mwenyewe, na ufikirie kazi Yake, na kuweka maslahi haya kwanza kabla kitu kingine; ni baada ya hapo tu ndipo unaweza kufikiria kuhusu uthabiti wa hadhi yako au jinsi wengine wanavyokuona. Je, huhisi kwamba inakuwa rahisi kidogo unapoyagawa katika hatua hizi na kufanya maafikiano fulani? Ukifanya hivi kwa muda, utakuja kuhisi kwamba kumridhisha Mungu si jambo gumu. Aidha, ikiwa unaweza kutimiza wajibu wako, kutenda faradhi na majukumu yako, kuweka kando tamaa zako binafsi, kuweka kando dhamira na nia zako mwenyewe, kufikiria nia ya Mungu na kuweka maslahi ya Mungu na nyumba Yake kwanza, basi baada ya kupitia hili kwa muda, utahisi kwamba hii ni njia nzuri ya kuishi: Ni kuishi kwa uhalisi na kwa uaminifu, bila kuwa mtu wa thamani ndogo au asiye na manufaa, na kuishi kwa haki na heshima badala ya kuwa na mawazo finyu au mchoyo. Utahisi kwamba hivi ndivyo mtu anapaswa kuishi na kutenda. Polepole, tamaa iliyo moyoni mwako ya kufurahisha maslahi yako mwenyewe itapungua.

Kimetoholewa kutoka katika “Mpe Mungu Moyo Wako wa Kweli, Na Unaweza Kupata Ukweli” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 381)

Watu wengi wanaweka mkazo maalum kwa tabia katika imani yao kwa Mungu, hivyo mabadiliko yanatokea katika mienendo yao. Baada ya kumwamini Mungu, wanakoma kubishana na wengine, wanakoma kupigana na watu na kuwatukana, wanakoma kuvuta sigara na kunywa pombe, hawaibi mali yoyote ya umma—hata iwe msumari ama kipande cha mbao—nao hawathubutu kuwashitaki watu wanapopata hasara ama wakikosewa. Bila shaka, baadhi ya mabadiliko yanatokea katika mienendo yao. Kwa sababu, baada ya kumwamini Mungu, kuikubali njia ya kweli kunawafanya kuhisi vizuri zaidi, na kwa sababu pia wameionja neema ya kazi ya Roho Mtakatifu, wanakuwa na bidii hasa, na hata hakuna kitu chochote ambacho hawawezi kutelekeza ama kufanya. Ilhali baada ya kuamini kwa miaka mitatu, mitano, kumi ama thelathini—kwa sababu hakujakuwa na mabadiliko katika tabia ya maisha yao, mwishowe wanarudia njia zao mbaya za awali, kiburi na majivuno yao vinakua, nao wanaanza kugombania mamlaka na faida, wanatamani pesa za kanisa, wanafanya chochote kwa maslahi yao, wanatamani vyeo na starehe, nao wanakuwa wanyonyaji wa nyumba ya Mungu. Viongozi wengi, hasa, wameachwa. Na ukweli huu unathibitisha nini? Mabadiliko katika tabia tu hayawezi kudumu. Kama hakuna mabadiliko katika tabia ya maisha ya watu, basi siku moja upande wao wa uovu utajionyesha. Kwa sababu kiini cha mabadiliko katika mienendo yao ni bidii, pamoja na kazi ya Roho Mtakatifu wakati huo, ni rahisi sana kwao kuwa na bidii, ama kuonyesha ukarimu kwa muda. Kama wasioamini wanavyosema, “kufanya tendo moja zuri ni rahisi, kilicho kigumu ni kufanya matendo mazuri maishani.” Watu hawana uwezo wa kufanya matendo mazuri katika maisha yao yote. Mienendo yao inaongozwa na maisha hayo; maisha yao yalivyo, ndivyo mwenendo wao ulivyo, na kile tu kinachofichuliwa kwa asili kinawakilisha maisha hayo, na asili ya mtu. Vitu vilivyo vya bandia haviwezi kudumu. Mungu anapofanya kazi ili kumwokoa mwanadamu, si kwa ajili ya kumpamba mwanadamu kwa mwenendo mzuri—kazi ya Mungu ni kwa ajili ya kubadilisha tabia za watu, kuwafanya wazaliwe na kuwa watu wapya. Hivyo, hukumu ya Mungu, kuadibu, majaribu, na usafishaji wa mwanadamu vyote ni kwa ajili ya kuibadilisha tabia yake, ili aweze kutimiza utii na uaminifu kamili kwa Mungu, na kumwabudu Mungu kwa kawaida. Hili ndilo lengo la kazi ya Mungu. Kuwa na tabia nzuri si sawa na kumtii Mungu, hasa si sawa na kulingana na Kristo. Mabadiliko katika tabia yanategemea mafundisho, na kuzaliwa na juhudi—hayategemei maarifa ya kweli kumhusu Mungu, ama juu ya ukweli, hasa hayategemei uongozi wa Roho Mtakatifu. Ingawa kuna nyakati ambapo baadhi ya yale watu wanayofanya yanaongozwa na Roho Mtakatifu, haya si maonyesho ya maisha, sembuse kuwa sawa na kumjua Mungu; haijalishi mienendo ya mtu ni mizuri kiasi gani, haithibitishi kwamba anamtii Mungu, ama kwamba anauweka ukweli katika matendo. Mabadiliko ya tabia ni udanganyifu wa muda, ni udhihirisho wa bidii, nayo si maonyesho ya maisha hayo.

Kimetoholewa kutoka katika “Tofauti Kati Ya Mabadiliko Ya Nje Na Mabadiliko Katika Tabia” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 382)

Watu wanaweza kuwa na tabia nzuri, lakini hiyo haimaanishi kuwa wako na ukweli. Bidii ya watu inaweza tu kuwafanya wazingatie mafundisho na kufuata kanuni; watu wasio na ukweli hawana namna ya kutatua shida halisi, na mafundisho hayawezi kushikilia nafasi ya ukweli. Wana ukweli ndani yao, wanatambua masuala yote, wanajua jinsi ya kutenda kulingana na mapenzi ya Mungu, jinsi ya kutenda kulingana na kanuni za ukweli, jinsi ya kutenda ili kumridhisha Mungu, nao wanaelewa asili ya upotovu wanaoufichua. Mawazo na dhana zao wenyewe vinapofichuliwa, wanaweza kutambua na kuunyima mwili. Hivi ndivyo mabadiliko katika tabia yanavyoonyeshwa. Kitu cha muhimu kuhusu mabadiliko katika tabia ni kwamba yana ukweli na uwazi, na unapotekeleza mambo, yanauweka ukweli katika matendo kwa usahihi wa karibu na upotovu wao hauonekani mara nyingi. Kwa jumla, mtu ambaye tabia yake imebadilika huonekana kuwa na busara na mwenye utambuzi, na kutokana na kuelewa kwake kwa ukweli, kujidai na kiburi havifichuliwi sana. Anaweza kuona kila kitu kwa uwazi, basi hawi mwenye kiburi baada ya kupata uwazi huu. Anaweza kuwa na ufahamu wa taratibu kuhusu ni ipi nafasi ya mwanadamu, jinsi ya kutenda kwa busara, jinsi ya kuwa mtiifu, nini anachofaa kusema na nini asichofaa kusema, na nini cha kusema na nini cha kutenda kwa watu gani. Hii ndiyo sababu inasemwa kuwa watu wa aina hii ni wenye busara kiasi. Wale ambao wana mabadiliko katika tabia zao wanaishi kwa kudhihirisha sura ya binadamu kwa kweli, nao wana0 ukweli; hawategemei ushawishi wa wengine. Wale ambao wamekuwa na mabadiliko katika tabia wako imara zaidi, hawasitasiti, na haijalishi wako katika hali gani, wanajua jinsi ya kutimiza wajibu wao sawasawa na jinsi ya kufanya mambo ili kumridhisha Mungu. Wale ambao tabia zao zimebadilika hawalengi nini cha kufanya ili kujifanya waonekane wazuri katika kiwango cha juujuu—wanao uwazi wa ndani kuhusu kile cha kufanya ili kumridhisha Mungu. Kwa hivyo, kutoka nje wanaweza kukosa kuonekana wenye shauku sana ama kama wamefanya jambo lolote kubwa, lakini kila kitu wanachofanya kina maana, kina thamani, na kina matokeo ya kiutendaji. Wale ambao tabia zao zimebadilika wana uhakika kuwa na ukweli mwingi—hii inaweza kuthibitishwa kwa mitazamo yao kuhusu mambo na kanuni zao katika vitendo vyao. Wale wasio na ukweli hawajakuwa na mabadiliko yoyote katika tabia hata kidogo. Mabadiliko katika tabia haimaanishi kuwa na ubinadamu uliokomaa au wenye uzoefu. Kwa kiasi kikubwa, inahusu matukio ambapo baadhi ya sumu za kishetani katika asili ya watu zinabadilika kama matokeo ya kufikia maarifa kuhusu Mungu na ufahamu wa ukweli. Hiyo ni kusema, sumu hizo zinatakaswa, na ukweli unaoonyeshwa na Mungu unaanza kustawi ndani ya watu hawa, unakuwa maisha yake, nao unakuwa msingi wa kuwepo kwake. Hapo tu ndipo wanakuwa watu wapya, na hivyo tabia yao inabadilika. Mabadiliko katika tabia hayamaanishi kwamba tabia za nje za watu ni za upole kuliko hapo awali, kuwa walikuwa na kiburi awali wanazungumza kwa busara, au kwamba hawakuwa wanamsikiza mtu yeyote lakini sasa wanaweza kuwasikiza wengine; mabadiliko haya ya nje hayawezi kusemwa kuwa ni mabadiliko katika tabia. Bila shaka, mabadiliko katika tabia yanajumuisha hali hizi, lakini jambo lililo muhimu zaidi ni kuwa maisha yao ya ndani yamebadilika. Ukweli unaoonyeshwa na Mungu unakuwa maisha yao hasa, baadhi ya sumu za kishetani zilizo ndani zimetolewa, mitazamo yao imebadilika kabisa, na hakuna kati ya hiyo inakubaliana na ile ya dunia. Anaona waziwazi njama na sumu za joka kubwa jekundu; amefahamu kiini cha kweli cha maisha. Kwa hivyo maadili ya maisha yake yamebadilika—hili ndilo badiliko la muhimu zaidi na kiini cha mabadiliko katika tabia.

Kimetoholewa kutoka katika “Tofauti Kati Ya Mabadiliko Ya Nje Na Mabadiliko Katika Tabia” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 383)

Mgeuzo wa tabia si badiliko katika matendo, si badiliko la nje lililobuniwa, si mgeuzo wa muda wa shauku, bali ni mgeuzo wa kweli wa tabia ambao huleta badiliko katika matendo. Mabadiliko kama hayo katika matendo ni tofauti kuliko mabadiliko katika mienendo ya nje. Mgeuzo wa tabia una maana kwamba umeelewa na umepitia ukweli, na kwamba ukweli umegeuka kuwa maisha yako. Zamani, ulifahamu ukweli kuhusu suala hili, lakini hukuweza kuchukua hatua kulihusu; kwako ukweli ulikuwa tu kama mafundisho ya dini yasiyodumu. Sasa, tabia yako imegeuka, na huelewi tu ukweli, lakini pia unatenda kulingana na ukweli. Unaweza sasa kuacha vitu ambavyo ulikuwa unavipenda mno zamani; unaweza kuacha vitu ulivyokuwa radhi kufanya, mawazo yako mwenyewe, na fikira zako. Unaweza sasa kuacha vitu ambavyo hukuweza kuviacha zamani. Huu ni mgeuzo wa tabia na ni mchakato wa kuigeuza tabia yako. Inasikika kuwa rahisi kabisa, lakini kwa kweli, mtu aliye katikati ya hilo lazima apitie shida nyingi, aushinde mwili wake na aache mambo ya mwili wake ambayo ni ya asili yake. Lazima pia apitie kushughulikiwa na kupogolewa, kuadibu na hukumu, na lazima apitie majaribio. Ni baada ya kupitia haya yote tu ndio mtu anaweza kuifahamu asili yake. Kuwa na ufahamu kiasi hakumaanishi kwamba anaweza kubadilika mara moja. Lazima apitie shida katika mchakato huo. Vivyo hivyo, je, unaweza tu kutia ukweli katika vitendo mara tu unapokuwa na ufahamu wa suala fulani? Huwezi kuutia katika vitendo mara moja. Katika kipindi cha kupata ufahamu, wengine wanakupogoa na kukushughulikia, na kisha mazingira yanakulazimu, yanakushurutisha kutenda kulingana na kanuni za ukweli. Wakati mwingine, huko radhi kulipitia hili, ukisema, “Kwa nini nisiweze kukifanya kwa njia hiyo? Ni lazima nikifanye kwa njia hii?” Wengine husema, “Kama unamwamini Mungu, basi unapaswa kukifanya kwa njia hii. Kukifanya kwa njia hii ni kunalingana na ukweli.” Unapofika mahali fulani ambapo umepitia majaribu fulani na kuishia kuelewa mapenzi ya Mungu na ukweli fulani, basi utakuwa na furaha kwa kiasi fulani na kuwa radhi kuyafanya mambo kulingana na kanuni za ukweli. Mwanadamu mwanzoni anasita kutenda ukweli. Chukua mfano wa kutimiza wajibu wa kwa bidii. Una ufahamu fulani kuhusu kutimiza wajibu wako na kujitolea kwa Mungu, na pia unaelewa ukweli unaohusika, lakini ni wakati gani ambapo utaweza kujitolea kabisa kwa Mungu? Utaweza kutatimiza wajibu wako kwa jina na matendo lini? Hili litahitaji mchakato. Wakati wa mchakato huu, huenda ukapitia shida nyingi. Watu watakushughulikia, kukupogoa, na kukudhibiti. Macho ya kila mtu yatakukazia, na hatimaye, utatambua: Ni tatizo langu. Kutimiza wajibu wangu huku nikikosa kujitolea hakukubaliki. Siwezi kuwa mvivu na mzembe. Roho Mtakatifu atakupa nuru kutoka ndani na kukushutumu unapofanya kosa. Wakati wa mchakato huu, utaelewa mambo mengine kukuhusu na utajua kwamba wewe ni mchafu sana, unaweka nia nyingi sana zako mwenyewe na tamaa nyingi sana za kupita kiasi katika kutimiza wajibu wako. Punde ambapo umeelewa asili ya mambo haya, wakati unaweza kuja mbele za Mungu katika sala na kutubu kwa kweli, mambo hayo machafu yanaweza kutakaswa. Ikiwa unatafuta ukweli mara kwa mara kwa njia hiyo kutatua shida zako za utendaji utaingia katika njia sahihi katika imani yako polepole. Kadri tabia potovu ya mwanadamu inazidi kutakaswa, ndivyo tabia yake ya maisha itabadilika zaidi.

Kuhusu kiini cha kutimiza wajibu wenu, ni jinsi gani mnatimiza wajibu wenu vizuri kwa kweli? Ni jinsi gani mnatimiza wajibu wenu kulingana na ukweli baada ya kugeuza tabia zenu? Kwa kuyatafakari haya, unaweza kujua tabia yako imegeuzwa kiasi gani kweli. Mgeuzo wa tabia si jambo rahisi hivyo. “Matendo yangu yamebadilika, na ninafahamu ukweli. Naweza pia kuzungumza kuhusu uzoefu fulani katika kila kipengele cha ukweli na naweza kuzungumza kuhusu umaizi fulani mdogo. Zaidi ya hayo, Roho Mtakatifu amenishutumu kuhusu jambo hili na sasa naweza kuliacha kidogo na naweza kutii kidogo.” Hili halihesabiki kama mgeuzo katika tabia ya maisha. Kwa nini? Unaweza kuacha kidogo, lakini unachotenda bado hakijafikia kiwango cha kutia ukweli katika vitendo kweli. Labda mazingira yako yanafaa kwa muda na hali zako zinafaa, au hali zako zinakushurutisha kutenda kwa njia hii, au hali yako ya akili ni imara na Roho Mtakatifu anafanya kazi, basi unaweza kulifanya. Kama ungekuwa katikati ya majaribio kama Ayubu ambaye alivumilia maumivu ya majaribio, au kama Petro ambaye Mungu alimwambia afe, je, ungeweza kusema, “Hata kama ningekufa baada ya kukujua, ingekuwa sawa”? Mgeuzo katika tabia haufanyiki ghafla sana, na haimaanishi kwamba unaweza kutia ukweli katika vitendo katika kila mazingira baada ya wewe kuelewa ukweli. Hii inahusisha asili ya mwanadamu. Upande wa nje, inaonekana kana kwamba unatia ukweli katika vitendo, lakini kwa kweli, hali ya matendo yako haionyeshi kwamba unatia ukweli katika vitendo. Kuna watu wengi ambao, punde tu wanayo mienendo fulani ya nje, huamini. “Je, kwani sitimizi wajibu wangu? Je, sikuacha familia na kazi yangu? Je, kwani sitii ukweli katika vitendo kwa kutimiza wajibu wangu?” Lakini Mungu hatambui kwamba unatia ukweli katika vitendo. Wale wote ambao matendo yao yamechafuliwa na nia na malengo ya kibinafsi hawatendi ukweli. Kusema kweli, aina hii ya mwenendo huenda itashutumiwa na Mungu; haitasifiwa au kukumbukwa na Yeye. Kulichangua hili zaidi, unafanya uovu na mwenendo wako unampinga Mungu. Kutoka nje, mambo haya unayoyafanya yanaonekana kuambatana na ukweli: Hukatizi wala kusumbua chochote na hujafanya maharibifu yoyote ya kweli au kukiuka ukweli wowote. Kinaonekana kuwa chenye mantiki na cha maana, ilhali asili ya matendo yako inahusika na kufanya uovu na kumpinga Mungu. Kwa hivyo unapaswa kupambanua kama kumekuwa na mabadiliko katika tabia yako na kama unatia ukweli katika vitendo kwa kutazama nia nyuma ya matendo yako kulingana na maneno ya Mungu. Haiamuliwi na maneno au maoni ya kibinadamu. Badala yake, inategemea Mungu kusema kama unakubali mapenzi Yake au la, kama matendo yako yana uhalisi wa ukweli au la, na kama yanafikia mahitaji Yake na viwango Vyake au la. Kujipima tu dhidi ya matakwa ya Mungu ndiyo sahihi. Mgeuzo katika tabia na kutia ukweli katika vitendo si sahili na rahisi kama wanavyodhani watu. Je, mnaelewa sasa? Mna uzoefu wowote katika jambo hili? Huenda msilielewe ikiwa linahusisha kiini cha masuala. Mmeingia juujuu sana. Mnakimbia huku na huko siku nzima, tangu macheo hadi magharibi, mnarauka mapema na kukawia kwenda kulala, lakini hamwelewi waziwazi mgeuzo wa tabia ni nini au hali yake ya kweli ni nini. Je, hii si ya juujuu? Haijalishi kama ninyi ni wa zamani au wapya, huenda msihisi kiini na kina cha mgeuzo katika tabia. Mnajuaje kama Mungu anawasifu au la? Angalau zaidi, utahisi imara kwa hali isiyo ya kawaida katika moyo wako kuhusu kila kitu ambacho unafanya, utahisi Roho Mtakatifu akikuongoza na kukupa nuru na Akifanya kazi ndani yako wakati unatimiza wajibu wako, unapofanya kazi yoyote katika familia ya Mungu, au katika nyakati za kawaida; mwenendo wako utapatana na maneno ya Mungu, na unapokuwa na kiwango fulani cha uzoefu, utahisi kwamba ulichofanya zamani kilikuwa cha kufaa kiasi. Ikiwa baada ya kupata uzoefu kwa kipindi cha muda, unahisi kwamba baadhi ya vitu ambavyo ulifanya zamani havikufaa na hujaridhika navyo, na kweli hakukuwa na ukweli ndani ya vitu ulivyofanya, basi inathibitisha kwamba kila kitu ulichofanya kilikuwa kinampinga Mungu. Inathibitisha kwamba huduma yako ilikuwa imejaa uasi, upinzani na mienendo ya binadamu.

Kimetoholewa kutoka katika “Unachopaswa Kujua Kuhusu Kuigeuza Tabia Yako” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 384)

Katika kupima ikiwa watu wanaweza kumtii Mungu au la, jambo muhimu la kuangalia ni ikiwa wanatamani kitu chochote cha kupita kiasi kutoka kwa Mungu, na ikiwa wana nia mbaya au la. Ikiwa watu humdai Mungu kila wakati, inathibitisha kuwa wao sio watiifu Kwake. Chochote kinachotokea kwako, ikiwa huwezi kukipokea kutoka kwa Mungu, huwezi kutafuta ukweli, kila wakati wewe unazungumza kutoka kwa hoja yako ya dhahania na kuhisi kila wakati kuwa wewe tu ndiye uliye sahihi, na hata bado una uwezo wa kumshuku Mungu, basi utakuwa taabani. Watu kama hao ndio wenye kiburi na waasi zaidi kwa Mungu. Watu ambao daima humdai Mungu hawawezi kamwe kumtii kweli. Ukimdai Mungu, hii inathibitisha kwamba unafanya maafikiano na Mungu, kwamba unachagua mawazo yako mwenyewe, na kutenda kulingana na mawazo yako mwenyewe. Kwa kufanya hivi, unamsaliti Mungu, na huna utiifu. Hakuna maana katika kumdai Mungu; ikiwa unaamini kweli kwamba Yeye ni Mungu, basi hutathubutu kumdai, wala hutastahiki kumdai, yawe madai ya maana au la. Ikiwa una imani ya kweli, na unaamini kuwa Yeye ni Mungu, basi hutakuwa na budi ila kumwabudu na kumtii. Siku hizi, sio tu kuwa watu wana chaguo, lakini hata wanadai kwamba Mungu atende kwa mujibu wa mawazo yao wenyewe, wanachagua mawazo yao wenyewe na wanataka Mungu atende kulingana nayo, na hawahitaji wao wenyewe kutenda kulingana na kusudi la Mungu. Kwa hivyo, hakuna imani ya kweli ndani yao, wala kiini ambacho kimo ndani ya imani hii.

Kimetoholewa kutoka katika “Watu Wanafanya Madai Mengi Sana kwa Mungu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 386)

Kutofaulu na kuanguka mara nyingi si jambo baya; na kufunuliwa pia si jambo baya. Iwe umeshughulikiwa, kupogolewa, au kufunuliwa, lazima ukumbuke hili wakati wote: Kufunuliwa hakumaanishi kuwa unashutumiwa. Kufunuliwa ni jambo zuri; ni fursa bora zaidi kwako kupata kujijua. Kunaweza kuuletea uzoefu wako wa maisha mabadiliko ya mwendo. Bila hilo, hutamiliki fursa, hali, wala muktadha wa kuweza kufikia ufahamu wa ukweli wa upotovu wako. Kama unaweza kujua vitu vilivyo ndani yako, vipengele hivyo vyote vilivyofichika ndani yako ambavyo ni vigumu kutambua na ni vigumu kufukua, basi hili ni jambo zuri. Kuweza kujijua mwenyewe kweli ndiyo fursa bora zaidi kwako kurekebisha njia zako na kuwa mtu mpya; ni fursa bora kwako kupata maisha mapya. Mara tu unapojijua mwenyewe kweli, utaweza kuona kwamba ukweli unapokuwa maisha ya mtu, ni jambo la thamani kweli, na utakuwa na kiu ya ukweli na kuingia katika uhalisi. Hili ni jambo zuri sana! Kama unaweza kunyakua fursa hii na ujitafakari mwenyewe kwa bidii na kupata ufahamu wa kweli kujihusu kila unaposhindwa au kuanguka, basi katikati ya uhasi na udhaifu, utaweza kusimama tena. Mara tu unapovuka kilele hiki, basi utaweza kuchukua hatua kubwa mbele na kuingia katika uhalisi wa ukweli.

Kama unaamini katika utawala wa Mungu, basi lazima uamini kuwa mambo ambayo hutokea kila siku, yawe mema au mabaya, si matukio ya kubahatisha. Sio kwamba mtu fulani ni mkali kwako au anakulenga kwa makusudi; yote kwa kweli husafidiwa na kupangwa na Mungu. Kwa nini Mungu hupanga mambo haya? Sio ili kuzifichua kasoro zako au kukukashifu; kukukashifu si lengo la mwisho. Lengo la mwisho ni kukukamilisha na kukuokoa. Mungu anafanyaje hilo? Kwanza, Anakufanya ufahamu tabia yako potovu, kufahamu asili na hali yako, kasoro zako, na kile unachokosa. Ni kwa kuelewa mambo haya yaliyomo katika moyo wako tu ndiyo utaweza kufuatilia ukweli na kuacha tabia yako potovu hatua kwa hatua. Huku ni Mungu kukupa fursa. Lazima ujue jinsi ya kuitumia fursa hii na usiwe mkaidi kwa Mungu. Hasa unapokabiliwa na watu, matukio, na mambo ambayo Mungu anapanga kando yako, usifikiri kila mara kwamba mambo hayako kama unavyotaka yawe, kila mara ukitaka kutoroka, kila mara ukimlaumu na kumwelewa Mungu visivyo. Huko si kuipitia kazi ya Mungu, na hiyo itafanya iwe vigumu sana kwako kuingia katika uhalisi wa ukweli. Lolote lile ambalo huwezi kulielewa kikamilifu, wakati ambapo una matatizo, lazima ujifunze kutii. Unapaswa kwanza kuja mbele ya Mungu na kuomba zaidi. Kwa njia hiyo, kabla ya wewe kujua kutakuwa na mabadiliko katika hali yako ya ndani na utaweza kutafuta ukweli ili kutatua tatizo lako utaweza kuipitia kazi ya Mungu. Katika kipindi hiki, uhalisi wa ukweli unahemshwa ndani yako, na hivi ndivyo jinsi utakavyoendelea mbele na jinsi mabadiliko katika hali ya maisha yako yatafanyika. Utakapokuwa umepitia mabadiliko haya na kuwa na aina hii ya uhalisi wa ukweli, basi utakuwa na kimo, na kimo huleta uzima. Ikiwa mtu huishi daima kulingana na tabia potovu ya Shetani, basi bila kujali ana shauku au bidii kiasi gani, bado hawezi kufikiriwa kuwa na kimo, au uzima. Mungu hufanya kazi ndani ya kila mtu, na bila kujali mbinu Yake ni ipi, ni watu, vitu au masuala ya aina gani ambayo Yeye hutumia kufanya huduma, au maneno Yake yana sauti ya aina gani, Ana lengo moja tu la mwisho: kukuokoa. Kabla ya kukuokoa, Anahitaji kukubadili, hivyo utakosaje kuteseka kidogo? Ni lazima upate kuteseka. Kuteseka huku kunaweza kuhusisha mambo mengi. Wakati mwingine Mungu huwainua watu, mambo, na vitu ambavyo viko karibu nawe ili kwamba uweze kujitambua, vinginevyo unaweza kushughulikiwa moja kwa moja, kukupogolewa, na kufunuliwa. Kama vile tu mtu aliye juu ya meza ya upasuaji–lazima upitie maumivu kiasi kwa ajili ya matokeo mazuri. Kama kila wakati Mungu anapokupogoa na kukushughulikia na kila wakati Anaibua watu, mambo, na vitu, hilo huchochea hisia zako na kukuongezea nguvu, basi kupitia hayo kwa njia hii ni sahihi, na utakuwa na kimo na utaingia katika uhalisi wa ukweli. Ikiwa, kila wakati unapopogolewa na kushughulikiwa, na kila wakati Mungu anapoinua mazingira yako, wewe huhisi maumivu au usumbufu wowote, na huhisi chochote kabisa, na kama huji mbele za Mungu kuelewa mapenzi Yake, wala huombi au kutafuta ukweli, basi wewe kweli ni mtu asiyejali kabisa! Watu ambao hawajali kabisa kamwe si hawatambui kiroho; kwa hiyo, Mungu hana njia ya kufanya kazi kwao. Mungu atasema: “Mtu huyu hajali kabisa na amepotoshwa sana. Nimemfanyia mambo mengi, nimetia bidii nyingi, lakini bado Siwezi kuuita moyo wake na Siwezi kuamsha roho yake. Jambo hili ni sumbufu na gumu sana.” Mungu akipanga mazingira, watu, vitu, na mambo fulani kwa ajili yako, Akikupogoa na kukushughulikia na ukijifunza kutokana na hili, ikiwa umejifunza kuja mbele za Mungu kutafuta ukweli, na, bila kujua, umetiwa nuru na kuangaziwa na kupata ukweli, ikiwa umepitia mabadiliko katika mazingira haya, umepata thawabu, na kupiga hatua, ukianza kuwa na ufahamu mdogo kuhusu mapenzi ya Mungu na kuacha kulalamika, basi yote haya yatamaanisha kuwa umesimama imara katikati ya majaribio ya mazingira haya, na umestahimili jaribio. Kwa hiyo, utakuwa umeshinda majaribu haya.

Kimetoholewa kutoka katika “Ili Kupata Ukweli, Lazima Ujifunze Kutoka kwa Watu, Mambo, na Vitu Vinavyokuzunguka” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 387)

Katika kazi yao, viongozi wa kanisa na wafanyakazi wanapaswa kuzingatia mambo mawili: Moja ni kufanya kazi yao kabisa kulingana na kanuni zilizowekwa masharti na mipangilio ya kazi, bila kamwe kukiuka kanuni hizi na kutotegemeza kazi yao juu ya chochote watakachofikiri au juu ya nia zao wenyewe. Katika kila kitu wafanyacho; wanapaswa kujali kazi ya familia ya Mungu, na siku zote kuweka maslahi yake kwanza. Kuna kitu kingine ambacho ni muhimu, nacho ni kwamba katika kila kitu wakifanyacho, lazima wazingatie kufuata mwongozo wa Roho Mtakatifu, na kufanya kila kitu kwa usahihi kulingana na neno la Mungu. Ikiwa bado una uwezo wa kuenda kinyume na mwongozo wa Roho Mtakatifu, au ikiwa kwa ukaidi unafuata mawazo yako mwenyewe na kufanya mambo kulingana na fikira zako mwenyewe, basi matendo yako yatakuwa na upinzani mkali sana dhidi ya Mungu. Mara kwa mara kuasi nuru na mwongozo wa Roho Mtakatifu kutakuongoza tu kwa mwisho kabisa. Ukipoteza kazi ya Roho Mtakatifu, basi hutaweza kufanya kazi, na hata ukiweza kufanya kazi, hutatimiza chochote. Hizi ndizo kanuni mbili kuu za kuzingatia wakati unafanya kazi: Moja ni kufanya kazi kulingana na mipangilio kutoka hapo juu kabisa na pia kutenda kulingana na kanuni zilizowekwa na hayo ya hapo juu. Jambo jingine ni kufuata mwongozo wa Roho Mtakatifu ndani. Mara tu mambo haya mawili yanapofahamika, hutafanya makosa kwa urahisi. Kwa nyinyi ambao uzoefu wenu katika eneo hili bado ni kidogo, ridhaa yenu wenyewe hughushi kazi yenu zaidi. Wakati mwingine, hamuwezi kuelewa kupata nuru au mwongozo kutoka kwa Roho Mtakatifu karibu; kwa wengine, mnaonekana kuielewa, lakini huenda mnaipuuza. Wewe daima hufikiria au kufikia hitimisho kwa njia ya kibinadamu, kufanya kama unavyofikiria kuwa sahihi, bila kujali kabisa juu ya nia ya Roho Mtakatifu. Wewe huendelea na kazi yako tu kulingana na mawazo yako mwenyewe, ukiweka kando upataji wa nuru kutoka kwa Roho Mtakatifu. Hali kama hizo hutokea mara kwa mara. Mwongozo wa ndani kutoka kwa Roho Mtakatifu si wa kupita uwezo wa binadamu kamwe. Kwa kweli ni wa kawaida sana: Mfiko wa ndani wa roho yako unajua hii ndiyo njia sahihi ya kufanya hivyo, na kwamba hii ndiyo njia bora zaidi. Wazo kama hilo ni wazi sana; si matokeo ya kutafakari, na wakati mwingine huwezi kuelewa kikamilifu ni kwa nini kuifanya kwa njia hii. Hii mara nyingi si kitu kingine bali kupata nuru kutoka kwa Roho Mtakatifu. Hali kama hiyo ndiyo hutokea kwa kawaida kwa watu wengi sana. Roho Mtakatifu hukuongoza utende kwa njia sahihi zaidi. Siyo matokeo ya fikira zako, badala yake una hisia moyoni mwako na unang'amua kwamba hii ndiyo njia bora zaidi ya kufanya hivyo. Pengine hili ni kutoka kwa Roho Mtakatifu. Mapenzi ya mtu mara nyingi ni matokeo ya mfanyiko tendani wa mawazo yake na yamepakwa rangi na mawazo yake: Mapato yangu ni nini, jinsi nitakavyofaidika—haya ni sehemu ya chochote ambacho watu huamua kukifanya wenyewe. Mwongozo kutoka kwa Roho Mtakatifu hauna ughushi kama huo hata kidogo. Ni muhimu kuzingatia kwa makini mwongozo au kupata nuru kutoka kwa Roho Mtakatifu; hasa katika masuala muhimu unapaswa kuwa makini ili ulielewe. Watu ambao hufikiria mengi sana, ambao hupenda kufuata mawazo yao huenda wakaukosa. Wafanyakazi wazuri, wafanyakazi waangavu, huzingatia kazi ya Roho Mtakatifu. Watu wanaomtii Roho Mtakatifu humwogopa Mungu na kutafuta ukweli bila kuchoka. Ili kumridhisha Mungu na kumshuhudia Yeye, mtu anapaswa kuchunguza kazi yake mwenyewe kwa dalili za ughushi na madhumuni, na kujaribu kuona ni kiasi gani kilichomotishwa na matakwa ya kibinafsi, ni kiasi gani kilichotokana na kupatiwa nuru na Roho Mtakatifu, na ni kiasi gani kilicho cha kuambatana na neno la Mungu. Ni lazima daima na katika hali zote uyakague maneno na matendo yako. Kutenda kwa njia hii daima kutakuweka kwenye njia sahihi ya kumtumikia Mungu. Ni muhimu kuwa na ukweli mwingi chini ya amri yako ili kutimiza huduma kwa Mungu ambayo ni ya kupendeza nafsi Yake. Watu wana uwezo wa kutofautisha baada tu ya kuelewa neno la Mungu, na wanaweza kutambua kinachotoka kwa mapenzi yao wenyewe na vitu vinavyoonyesha motisha yao. Wanaweza kutambua uchafu wa wanadamu, na maana ya kutenda kulingana na ukweli. Ni hapo tu utakapojua jinsi ya kutii zaidi kwa usafi. Bila ukweli haiwezekani kwa watu kutofautisha. Mtu mpumbavu anaweza kumwamini Mungu maisha yake yote bila kujua maana ya kufichua upotovu, wala hajui kumpinga Mungu ni nini, kwa sababu yeye hana ukweli, wazo hili halipo katika akili yake. Hili ni kama kukarabati kifaa cha umeme. Je, mtu anawezaje kukitengeneza ikiwa hajui ni mzunguko umeme upi una kosa? Ndani yenu pia kuna mizunguko mingi. Wakati mwingine hitilafu iko katika malengo yenu, au ambako mapenzi yenu wenyewe yanahusika. Wakati mwingine hitilafu ni upotovu wa ufahamu wenu au ujuzi. Ama inaweza kuwa kutokana na kufuata mapenzi yenu wenyewe au kwa kuamini na kupotoshwa na wengine. Wakati mwingine nyinyi hufuata mwili mnapojaribu kulinda sifa zenu au hadhi. Hitilafu kama hizi hutokea mara kwa mara, hivyo kupeleka kazi mrama na kuleta hasara kwa kazi ya familia ya Mungu na maisha ya ndugu. Thamani ya kazi ya aina hii ni nini? Ni katizo, usumbufu, na uharibifu tu. Ili kutimiza kazi ambayo Mungu huwapa ni muhimu kuelewa kanuni hizi mbili. Ni lazima mshike kabisa mipango ya kazi kama ilivyoelezwa hapo juu, na lazima mzingatie kuutii mwongozo kutoka kwa Roho Mtakatifu. Ni wakati tu kanuni hizi mbili zinapofahamika ndipo kazi inapoweza kuwa ya kufaa na mapenzi ya Mungu yaridhishwe.

Kimetoholewa kutoka katika “Kanuni Kuu za Kazi kwa Viongozi na Wafanyakazi” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 388)

Kile alichotafuta Petro ni kuja kujijua na kuona kilichofichuliwa ndani yake kupitia usafishaji wa maneno ya Mungu na ndani ya majaribio mbalimbali ambayo Mungu alimtolea. Mwishowe, alipokuja kujifahamu kweli, Petro aligundua jinsi mwanadamu ni mpotovu kwa kina, na jinsi hana thamani na hastahili kumtumikia Mungu, na kwamba mwanadamu hastahili kuishi mbele za Mungu. Kisha Petro alianguka chini mbele za Mungu. Mwishowe, Petro alihisi, “Kumjua Mungu ni jambo la thamani zaidi! Kama singeweza kumjua Mungu, basi kifo changu kingekuwa cha kusikitisha mno. Nahisi kwamba kumjua Mungu ndilo jambo muhimu sana, la maana sana. Ikiwa mwanadamu hamjui Mungu, basi hastahili kuishi, na hana uzima.” Kufikia wakati uzoefu wa Petro ulikuwa umefikia kiwango hiki, alikuwa na ufahamu kiasi wa asili yake mwenyewe na alikuwa na ufahamu mzuri kiasi kuihusu. Ingawa pengine hangeweza kuielezea vizuri kabisa kulingana na jinsi watu wanavyoweza kudhani, alikuwa amefikia hali hii. Kwa hivyo, njia ya kutafuta uzima na kufikia kukamilishwa na Mungu inahusu kupata uelewa zaidi wa asili ya mtu mwenyewe kutoka ndani ya maneno ya Mungu, pamoja na kuelewa vipengele vya asili ya mtu na kuieleza kwa usahihi katika maneno. Ili kuelewa kabisa maisha ya mtu ya kale—maisha ya asili ya kale ya shetani—kunamaanisha kuweza kutimiza matokeo yaliyohitajika na Mungu. Ikiwa ufahamu wako haujafikia kiwango hiki, ilhali unadai kujielewa na kwamba umepata uzima, je, si unajisifu tu? Hujijui, wala hujui ulicho mbele za Mungu, kama umefikia kweli kiwango cha mwanadamu, au ni vitu vingapi vya kishetani ambavyo bado unavyo. Bado huelewi vizuri wewe ni wa nani, na hata hujifahamu, hivyo unawezaje kuwa na mantiki mbele za Mungu? Wakati Petro alikuwa akiufuatilia uzima, alizingatia kujielewa na kubadilisha tabia yake katika kipindi cha majaribu yake. Alijitahidi kumjua Mungu, na mwishowe, alihisi, “Watu lazima watafute kumfahamu Mungu maishani; kumfahamu Yeye ndilo jambo muhimu zaidi. Ikiwa simjui Mungu, basi siwezi kupumzika kwa amani nitakapokufa. Punde ninapomjua, basi Mungu anaponifanya nife, bado nitahisi kupendezwa sana kufanya hivyo; sitalalamika hata kidogo, na maisha yangu yote yatakuwa yametimizwa.” Petro hakuweza kupata ufahamu huu au kufikia kiwango hiki punde baada ya kuanza kumwamini Mungu; ilimbidi kwanza kupitia majaribio mengi. Uzoefu wake ulipaswa kufikia kiwango fulani, na alipaswa kujifahamu kabisa, kabla ya kuweza kuhisi thamani ya kumjua Mungu. Kwa hivyo, njia aliyoichukua Petro ilikuwa njia ya kupata uzima na ya kukamilishwa; utendaji wake maalum ulizingatia hali hii hasa.

Je, nyote mnaishika njia gani sasa? Ikiwa hamjafikia ufuatiliaji wa maisha, wa kujifahamu, au kumfahamu Mungu kama Petro, basi hiyo bado si njia ya Petro. Hivi sasa watu wengi wako katika aina hii ya hali: “Ili kupata baraka ni lazima nijitumie kwa ajili ya Mungu na kulipa gharama kwa ajili Yake. Ili kupata baraka ni lazima niache kila kitu kwa ajili ya Mungu; lazima nikamilishe kile ambacho ameniaminia na kutekeleza wajibu wangu vizuri.” Hili linatawaliwa na nia ya kubarikiwa; ni kutumika kwa kusudi la kupata thawabu za Mungu, kwa ajili ya kupata taji. mtu wa aina hii hana ukweli ndani ya moyo wake, na hakika anaelewa tu maneno fulani ya mafundisho ya dini ambayo anaringia kila mahali. Njia yake ni njia ya Paulo. Kumwamini Mungu kwa mtu wa aina hii ni kitendo cha kazi ya siku zote, na katika akili yake anahisi kuwa kadri anavyofanya, ndivyo itakavyothibitisha zaidi kuwa ni mwaminifu kwa Mungu, kwamba kadri anavyofanya ndivyo Mungu ataridhika zaidi, na kwamba kadri anavyofanya ndivyo anavyopaswa zaidi kupata taji mbele za Mungu, na hakika atapata baraka kubwa zaidi katika nyumba ya Mungu. Anahisi kwamba kama anaweza kuvumilia mateso, kuhubiri, na kufa kwa ajili ya Kristo, kama anaweza kuyadharau maisha yake mwenyewe, na kama anaweza kukamilisha wajibu wote ambao Mungu alimwaminia nao, basi atakuwa mtu mwenye kubarikiwa zaidi na Mungu, yule anayepata baraka nyingi zaidi, na hakika atapokea taji. Hili ndilo hasa alilowaza Paulo alilofikiri na kile alichofuatilia; hii ndiyo hasa njia ambayo Paulo alitembea, na ilikuwa chini ya uongozi wa mawazo haya ndio Paulo alifanya kazi kumhudumia Mungu. Je, mawazo na madhumuni kama hayo hayatoki kwa asili ya Shetani? Kama tu watu wa dunia, hapa duniani lazima nifuatilie maarifa, na baada ya kupata maarifa tu ndio ninaweza kufanikiwa, kuwa afisa, na kuwa na cheo. Mara baada ya kupata cheo ninaweza kufikia lengo langu na kuifikisha nyumba yangu na biashara kwa viwango fulani. Je, wasioamini wote huwa hawaifuati njia hii? Wale ambao wanatawaliwa na asili hii ya shetani wanaweza tu kuwa kama Paulo baada ya kumwamini Mungu: “Ni lazima niache kila kitu ili nijitumie kwa ajili ya Mungu, lazima niwe mwaminifu mbele za Mungu, na mwishowe nitapokea taji kubwa zaidi na baraka kubwa zaidi.” Hii ni sawa na watu wa dunia wanaofuatilia vitu vya dunia, hakuna tofauti kabisa, na wanapaswa kutii asili hiyo. Watu wana asili ya shetani, kwa hiyo ulimwenguni watafuatilia maarifa, hadhi, kujifunza, na mafanikio ya dunia; nyumbani mwa Mungu, watatafuta kujitumia kwa ajili ya Mungu, kuwa waaminifu, na hatimaye watapokea taji na baraka nyingi. Kama watu hawana ukweli baada ya kumwamini Mungu na hawajakuwa na mabadiliko katika tabia yao, basi bila shaka watakuwa kwenye njia hii—huu ni ukweli ambao hakuna mtu anayeweza kuupinga, na ni wenye kupinga kabisa njia ya Petro. Nyote mnaishika njia gani sasa? Ingawa huwezi kupanga kuishika njia ya Paulo, asili yako inakutawala kwa njia hii, na unaelekea upande huo bila kupenda. Ingawa unataka kuishika njia ya Petro, ikiwa hufahamu vizuri jinsi ya kulifanya hilo, basi bado utaishika njia ya Paulo bila kupenda—huu ni ukweli wa hali hiyo.

Kwa hiyo mnawezaje hasa kuishika njia ya Petro? Kama huwezi kubainisha kati ya njia ya Petro na njia ya Paulo, au huzijui kabisa, basi hata ukisema unapaswa kuishika njia ya Petro hayo yatakuwa maneno matupu. Unahitaji kwanza kufahamu katika mawazo yako njia ya Petro ni gani na njia ya Paulo ni gani. Kama kweli unaelewa kwamba njia ya Petro ni njia ya uzima na njia pekee ya kukamilishwa, wakati huo tu ndipo utaweza kujua na kufahamu ukweli na njia maalum za kuishika njia yake. Ikiwa huifahamu njia ya Petro, basi njia unayoishika bila shaka itakuwa ya Paulo kwa sababu hakutakuwa na njia nyingine—hutakuwa na budi. Kama huna ukweli na huna hamu za kupata kitu basi ni vigumu kuishika njia ya Petro. Inaweza kusemekana kwamba Mungu amewafichulia sasa njia ya kuokolewa naye na ya kukamilishwa. Hii ni neema ya Mungu na kutia moyo na ni Yeye anayewaongoza kwenye njia ya Petro. Bila uongozi na kupata nuru kutoka kwa Mungu hakuna ambaye angeweza kuishika njia ya Petro; chaguo la pekee lingekuwa kuelekea kwa njia ya Paulo, kuzifuata nyayo za Paulo kuelekea kwa uharibifu. Wakati huo, Paulo hakuhisi kwamba haikuwa sahihi kutembea kwenye njia hiyo. Aliamini kwa ukamilifu kwamba ilikuwa sahihi, lakini hakuwa na ukweli na hasa hakuwa na mabadiliko katika tabia. Alijiamini kupita kiasi na akahisi kwamba hakukuwa na ubaya wowote kuishika njia hiyo. Aliendelea akiwa amejaa imani na kwa kujihakikishia kabisa. Kufikia mwisho, hakupata fahamu, bado alifikiria kwamba kwake kuishi ilikuwa ni Kristo. Aliendelea kuishika njia hiyo hadi mwisho, na alipoadhibiwa mwishowe, yote ilikuwa imekwisha. Njia ya Paulo haikuhusisha kujijua au ufuatiliaji wa mabadiliko katika tabia. Hakuchangua kamwe asili yake mwenyewe na hakuwa na ufahamu wa kile alichokuwa; alijua tu kwamba alikuwa mkosaji mkuu katika kumtesa Yesu. Hakuwa amepata ufahamu hata kidogo wa asili yake mwenyewe, na baada ya kumaliza kazi yake alihisi kwamba alikuwa Kristo na anapaswa kupewa thawabu. Kazi ambayo Paulo alifanya ilikuwa tu kutoa huduma kwa Mungu. Kwake mwenyewe, ingawa alipokea ufunuo kiasi kutoka kwa Roho Mtakatifu, hakuwa na ukweli au uzima hata hivyo. Hakuokolewa na Mungu—aliadhibiwa. Kwa nini inasemekana kwamba njia ya Petro ni njia ya kukamilishwa? Kwa sababu katika utendaji wake alizingatia hasa uzima, alifuatilia ufahamu wa Mungu, na akazingatia kujifahamu. Kupitia uzoefu wake wa kazi ya Mungu alikuja kujijua, alipata ufahamu wa hali potovu za mwanadamu, alijua kasoro zake, na ni jambo gani lilikuwa muhimu sana kwa mwanadamu kulifuatilia. Aliweza kumpenda Mungu kwa dhati, alijua jinsi ya kumlipa Mungu, alipata ukweli kiasi, na alikuwa na ukweli ambao Mungu huhitaji. Kutoka kwa vitu vyote alivyosema wakati wa majaribio yake, inaweza kuonekana kwamba Petro alikuwa kweli mwenye ufahamu zaidi wa Mungu. Kwa sababu alielewa ukweli mwingi sana kutoka kwa maneno ya Mungu, njia yake ikawa yenye kung’aa zaidi na zaidi na kuzidi kufungamana na mapenzi ya Mungu. Kama hangekuwa amepata ukweli huu, basi hangeweza kuendelea kuishika njia sahihi kama hiyo.

Kimetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kuitembea Njia ya Petro” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 389)

Petro alikuwa mwaminifu Kwangu kwa miaka mingi, lakini hakunung’unika wala kuwa na moyo wa kulalamika kamwe, na hata Ayubu hakuwa sawa na yeye. Katika enzi zote, watakatifu wote, pia, hawajamfikia hata kidogo. Yeye hakufuatilia kunijua Mimi tu, lakini pia alipata kunijua wakati ambapo Shetani alikuwa anatekeleza njama zake danganyifu. Hii ilisababisha miaka mingi ya huduma iliyoupendeza nafsi Yangu, na kwa sababu hii Shetani hakumnyonya kamwe. Petro alitumia imani ya Ayubu, ilhali yeye pia alifahamu wazi upungufu wake. Ingawa Ayubu alikuwa na imani kubwa, alikosa ufahamu wa masuala katika ulimwengu wa kiroho, na hivyo alisema maneno mengi ambayo hayakulingana na hali halisi; hii inaonyesha kwamba ufahamu wake bado haukuwa wa kina, na haukuwa na uwezo wa kufanywa kuwa kamilifu. Na hivyo, Petro siku zote alitazamia kufahamu roho, na daima alilenga kuchunguza mienendo ya ulimwengu wa kiroho. Kwa sababu hii, hakuwa tu na uwezo wa kutambua matakwa Yangu kiasi, lakini pia alielewa kidogo juu ya njama danganyifu za Shetani, na hivyo ufahamu wake kuhusu Mimi ulikuwa mkubwa zaidi kuliko mwingine wowote katika enzi zote.

Kutokana na matukio ya Petro si vigumu kuona kwamba mtu akitaka kunijua, lazima awe makini kwa kuzingatia kwa uangalifu katika roho. Sikuombi kwamba utoe kiasi kikubwa Kwangu kwa nje; hili ni la umuhimu wa ziada. Iwapo hunijui, basi imani, upendo na uaminifu wote unaozungumzia ni ndoto tu, ni upuuzi, na wewe hakika utakuwa mtu ambaye ana majivuno makubwa mbele Zangu lakini hajijui mwenyewe, na hivyo wewe utanaswa tena na Shetani na hutaweza kujinasua; utakuwa mwana wa kuteseka milele, na utakuwa mlengwa wa maangamizi. Lakini kama wewe huna hisia na hujali kuhusu maneno Yangu, basi bila shaka unanipinga Mimi. Huu ni ukweli, na ingekuwa vyema utazame kupitia lango la ulimwengu wa kiroho uone roho nyingi na tofautitofauti zilizoadibiwa na Mimi. Ni wapi kati yao hawakukaa tu na hawakujali, na hawakuyakubali maneno Yangu? Ni wapi kati yao hawakuwa na shaka kwa maneno Yangu? Ni yupi kati yao hakujaribu kutafuta makosa katika maneno Yangu? Ni wapi kati yao hawakuyatumia maneno Yangu kama silaha ya kujikinga itakayotumiwa kujilinda? Wao hawakutafuta kunijua kwa njia ya maneno Yangu, lakini waliyatumia kama vitu vya kuchezea tu. Katika hili, je, si wao walinipinga moja kwa moja? Nani ni maneno Yangu? Nani ni Roho Wangu? Mara nyingi Mimi nimeyanena maneno haya kwenu, lakini maono yenu yamewahi kuwa ya kiwango cha juu na yenye uwazi? Matukio yenu yamewahi kuwa ya kweli? Nawakumbusha mara nyingine: Iwapo hamyajui maneno Yangu, hamyakubali, na hamyaweki katika matendo, basi bila shaka mtaadibiwa na Mimi! Nyinyi kwa hakika mtakuwa waathirika wa Shetani!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 8

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 390)

Ingawa watu wengi wanaamini katika Mungu, ni wachache wanaoelewa ni nini maana ya imani katika Mungu, na ni nini wanachopaswa kufanya ili waupendeze moyo wa Mungu. Hii ni kwa sababu, hata ingawa watu wengi wanalifahamu neno “Mungu” na mafungu ya maneno kama “kazi ya Mungu”, hawamjui Mungu, sembuse kujua kazi ya Mungu. Si ajabu, basi, kwamba wale wote wasiomjua Mungu wamejawa na imani iliyovurugika. Watu hawachukulii imani kwa Mungu kwa uzito kwa kuwa kuamini Mungu ni jambo geni, jambo lisilo la kawaida sana kwao. Kwa njia hii, hawafikii mahitaji ya Mungu. Kwa maneno mengine, ikiwa watu hawamjui Mungu, hawajui kazi Yake, basi hawafai kwa matumizi na Mungu, sembuse kuweza kutimiza hamu ya Mungu. “Imani katika Mungu” inamaanisha kuamini kuwa kuna Mungu; hii ndiyo dhana rahisi zaidi ya imani katika Mungu. Zaidi ya hayo, kuamini kuwa kuna Mungu si sawa na kuamini katika Mungu kwa ukweli; bali, ni aina ya imani sahili ikiwa na vipengee vya uzito vya kidini. Imani ya kweli katika Mungu ina maana kupitia maneno na kazi ya Mungu kwa msingi wa imani kuwa Mungu ndiye mkuu juu ya vitu vyote. Kwa hivyo mtawekwa huru kutokana na tabia yenu ya upotovu, mtatimiza hamu ya Mungu, na mtapata kumjua Mungu. Ni kwa kupitia safari ya aina hii tu ndio mnaweza kusemekana kuwa mnaamini katika Mungu. Ilhali watu mara nyingi huona kuamini katika Mungu kama jambo rahisi sana na la kipuuzi tu. Watu wanaomwami Mungu kwa njia hii wamepoteza maana ya kumwamini Mungu, na ingawa wanaweza kuendelea kuamini mpaka mwisho, hawatawahi kupata idhini ya Mungu, kwa sababu wanatembea katika njia mbaya. Leo, kuna wale ambao bado wanaamini Mungu katika nyaraka, katika mafundisho ya dini yaliyo matupu. Hawana habari kuwa imani yao katika Mungu haina dutu, na hawawezi kupata idhini ya Mungu, na bado wanaomba kupata amani na neema ya kutosha kutoka kwa Mungu. Tunafaa kuweka kituo na kujiuliza wenyewe: Je, kuamini kwa Mungu linaweza kuwa jambo rahisi ya yote duniani? Je, kuamini kwa Mungu hakumaanishi chochote zaidi ya kupokea neema nyingi kutoka kwa Mungu? Je, watu wanaoamini kwa Mungu na hawamjui, na wanaamini kwa Mungu ila wanamuasi; je watu kama hawa wanaweza kutimiza hamu ya Mungu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 391)

Ni kitu gani ambacho mwanadamu amepokea tangu alipomwamini Mungu mara ya kwanza? Umejua kitu gani kumhusu Mungu? Umebadilika kiasi gani kwa sababu ya imani yako kwa Mungu? Leo, nyote mnajua ya kwamba imani ya mwanadamu katika Mungu si kwa ajili ya wokovu wa roho na hali njema ya mwili tu, wala si kuimarisha maisha yake kwa njia ya upendo kwa Mungu, na kadhalika. Kama ilivyo sasa, kama unampenda Mungu kwa ajili ya ustawi wa mwili au furaha ya muda, basi hata kama, mwishoni, upendo wako kwa Mungu utafikia kilele chake na wewe hutaulizia kitu chochote, upendo huu unaoutafuta ni upendo mchafu na haumpendezi Mungu. Wale wanaotumia upendo kwa Mungu kusitawisha maisha yao yasiyopendeza na kujaza utupu katika mioyo yao ni wale ambao wanataka kuishi katika raha, si wale ambao kweli wanatafuta kumpenda Mungu. Upendo wa aina hii ni kinyume na matakwa ya mtu, harakati ya ridhaa ya hisia, na Mungu hahitaji upendo wa aina hii. Upendo wako, basi, ni upendo wa aina gani? Ni kwa ajili gani unampenda Mungu? Je, ni kiasi gani cha upendo wa kweli, ulicho nacho kwa Mungu sasa? Upendo wa watu wengi kati yenu ni kama uliotajwa hapo awali. Upendo wa aina hii unaweza tu kudumisha hali kama ilivyo; hauwezi kufikia uthabiti wa milele, wala kuchukua mizizi katika mtu. Aina hii ya upendo ni ule wa ua ambalo halizai matunda baada ya kuchanuka na hatimaye kunyauka. Kwa maneno mengine, baada ya wewe kumpenda Mungu mara moja kwa jinsi hii na hakuna mtu wa kukuongoza kwa njia ya mbele, basi utaanguka. Kama unaweza tu kumpenda Mungu katika wakati wa kumpenda Mungu na kutofanya mabadiliko katika tabia ya maisha yako baadaye, basi utaendelea kufunikwa na ushawishi wa giza, bila uwezo wa kutoroka, na bila uwezo wa kujinasua kwa kufungwa na kupumbazwa na Shetani. Hakuna mtu kama huyu anayeweza kukubaliwa na Mungu; mwishowe, roho zao, nafsi na mwili bado ni mali ya Shetani. Hili ni bila ya shaka. Wale wote ambao hawawezi kukubaliwa kikamilifu na Mungu watarudi mahali pao pa awali, yaani, kwa Shetani, na watakwenda chini kwa ziwa liwakalo moto wa jahanamu kukubali hatua ya pili ya adhabu kutoka kwa Mungu. Wale wanaokubaliwa na Mungu ni wale ambao wanamkataa shetani na kutoroka kutoka kwa miliki ya Shetani. Watu kama wale watahesabiwa rasmi miongoni mwa watu wa ufalme. Hivi ndivyo watu wa ufalme huja kuwa. Je, uko tayari kuwa mtu wa aina hii? Je, uko tayari kukubaliwa na Mungu? Je, uko tayari kutoroka kutoka miliki ya Shetani na kurudi kwa Mungu? Je, sasa wewe ni mali ya Shetani au umehesabiwa miongoni mwa watu wa ufalme? Mambo hayo lazima yote yawe wazi na hayahitaji maelezo zaidi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maoni Wanayopaswa Kushikilia Waumini

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 392)

Katika nyakati zilizopita, watu wengi walifuatilia kwa jitihada na fikira za mwanadamu na kwa ajili ya matumaini ya mwanadamu. Mambo haya hayatajadiliwa sasa. La muhimu ni kupata njia ya kutenda ambayo itawezesha kila mmoja wenu kudumisha hali ya kawaida mbele ya Mungu na hatimaye kuvunja pingu za ushawishi wa Shetani, ili mpate kuwa wakubalika wa Mungu, na kuishi kwa kudhihirisha duniani matakwa ya Mungu kwenu. Ni haya tu yanayoweza kutimiza mapenzi ya Mungu. Wengi wanaamini katika Mungu, ila hawajui ni kitu gani Anachotamani Mungu wala ni nini anachotamani Shetani. Wao wanaamini kipumbavu na kuwafuata watu wengine kama vipofu, na kwa hivyo hawajakuwa kamwe na maisha ya kawaida ya Kikristo; hawana uhusiano wa kawaida wa binafsi na watu wengine, sembuse uhusiano wa kawaida ambao mwanadamu anao na Mungu. Kutoka kwa hili inaweza kuonekana kwamba matatizo na makosa ya mtu, na mambo mengine ambayo yanaweza kuzuia mapenzi ya Mungu ni mengi. Hili linatosha kuthibitisha kwamba mwanadamu bado hajaingia kwenye njia sahihi ya imani katika Mungu, wala hajaingia katika uzoefu halisi wa maisha ya binadamu. Hivyo, maana ya kuingia kwenye njia sahihi ya imani katika Mungu ni ipi? Kuingia kwenye njia iliyo sahihi ina maana kwamba unaweza kunyamazisha moyo wako mbele za Mungu wakati wote na kufurahia mawasiliano ya kawaida na Mungu, hatua kwa hatua ukipata kujua ni nini kinachokosa ndani ya mwanadamu na polepole kupata kumfahamu Mungu zaidi. Kwa njia hii, kila siku unapata maono mapya na kupata nuru kiroho; hamu yako inakua, na wewe kutafuta kuingia katika ukweli. Kila siku kuna mwanga mpya na ufahamu mpya. Kupitia njia hii, wewe hatua kwa hatua unavunja ushawishi wa Shetani na kuwa huru, na maisha yako yanakua kwa kiasi kikubwa. Mtu kama huyu ameweka mikakati ya kufuata mwenendo sawa. Tathmini uzoefu wako mwenyewe halisi na kuchunguza njia uliyoichukua katika imani yako kwa Mungu dhidi ya yaliyotajwa hapo juu. Wewe ni yule ambaye amepangwa kufuata mwenendo sawa? Ni katika masuala gani ambapo umejiweka huru kutokana na pingu za shetani na kutokana na ushawishi wa Shetani? Kama bado hujajiandaa kufuata njia iliyo sahihi, uhusiano wako na Shetani bado haujaisha. Kwa jinsi hiyo, ukimbiziaji huu wa upendo kwa Mungu inaweza kusababisha upendo ambao ni sahihi, wa kujitolea, na safi? Unasema kwamba upendo wako kwa Mungu ni wa dhati na imara, bali hujajinasua kutoka kwa pingu za Shetani. Je, wewe si unajaribu kumpumbaza Mungu? Ukitaka kuufikia upendo safi kwa Mungu, kuwa wa Mungu kikamilifu, na kuwa mhesabiwa miongoni mwa watu wa ufalme, basi lazima kwanza ujiandae kufuata njia iliyo sahihi ya imani katika Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maoni Wanayopaswa Kushikilia Waumini

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 393)

Tatizo la kawaida lililo miongoni mwa binadamu wote ni kwamba wao huuelewa ukweli lakini hawawezi kuuweka katika matendo. Sababu moja ni kwamba binadamu hana nia ya kulipa gharama, na sababu nyingine ni kwamba utambuzi wa mwanadamu ni duni mno; hawezi kuona zaidi ya ugumu mwingi ulio katika hali halisi ya maisha na hajui jinsi ya kutenda kwa njia inayofaa. Kwa vile mtu ana tajriba ndogo sana, mwenye uwezo wa chini, mwenye ufahamu mdogo wa ukweli, yeye hawezi kutatua matatizo yanayomkabili maishani. Anaweza tu kupiga domo kuhusu imani yake kwa Mungu, ilhali hawezi kumhusisha Mungu katika maisha yake ya kila siku. Hii ni kusema, Mungu ni Mungu, na maisha ni maisha, kama kwamba binadamu hana uhusiano na Mungu katika maisha yake. Hayo ndiyo binadamu wote wanayaamini. Aina hii ya imani kwa Mungu haitaruhusu binadamu kupatwa na kukamilishwa Naye kwa uhakika. Kwa kweli, si kwamba neno la Mungu ni pungufu, badala yake uwezo wa binadamu wa kupokea neno Lake ni duni mno. Inaweza kusemwa karibu binadamu wote hutenda kulingana na nia za Mungu. Badala yake, imani yao kwa Mungu ni kwa mujibu wa nia zao wenyewe, fikra za kidini zilizowekwa, na desturi. Ni wachache wanaopitia mabadiliko baada ya kulikubali neno la Mungu na kuanza kutenda kwa mujibu wa mapenzi Yake. Badala yake, wanaendelea katika imani yao potovu. Wakati mwanadamu anaanza kuamini katika Mungu, anafanya hivyo kwa kuzingatia sheria za kawaida za dini, na anaishi na kuhusiana na wengine kwa misingi ya falsafa yake ya kuishi. Hivyo ndivyo ilivyo kwa watu tisa kati ya kila watu kumi. Ni wachache sana wanaounda mpango mwingine na kuanza mwanzo mpya baada ya kuanza kumwamini Mungu. Hakuna anayeona au kuweka katika vitendo neno la Mungu kama ukweli.

Chukua imani katika Yesu, kwa mfano. Kama mtu alikuwa mwanafunzi katika imani au alikuwa wa imani hiyo kwa muda mrefu, wote walitumia vipaji vyovyote walivyokuwa navyo na kuonyesha ujuzi wowote waliokuwa nao. Mwanadamu aliongeza tu “imani katika Mungu,” maneno haya matatu, katika maisha yake ya kawaida, bado hayakufanya mabadiliko katika tabia yake, na imani yao kwa Mungu haikukua hata kidogo. Ukimbizaji wa mwanadamu wa swala hili haukuwa baridi wala moto. Hakusema kwamba hakuamini, lakini pia hakujitoa kikamilifu kwa Mungu. Hakuwahi kumpenda Mungu kwa kweli wala kumtii Mungu. Imani yake kwa Mungu ilikuwa halali na ya kujifanya, na aligeuka na akapuuza na wala hakuwa na bidii kwa kutenda imani yake. Aliendelea katika hali kama hiyo ya kuchanganyikiwa tangu mwanzo hadi wakati wake wa kufa. Ni nini maana ya hili? Leo, lazima uwe katika njia sahihi kwani unaamini katika Mungu wa vitendo. Kwa kuwa una imani katika Mungu, hupaswi tu kutafuta baraka, lakini pia kutafuta kumpenda Mungu na kumjua Mungu. Kupitia kwa kupata nuru kutoka Kwake na harakati yako mwenyewe, unaweza kula na kunywa neno Lake, kukuza ufahamu wa kweli kuhusu Mungu, na kuwa na upendo wa kweli kwa Mungu unaotoka moyoni mwako. Kwa maneno mengine, upendo wako kwa Mungu ni wa kweli zaidi, ambapo hakuna yeyote anayeweza kuharibu au kukuzuia kuonyesha upendo wako Kwake. Basi uko kwa njia ya kweli ya imani kwa Mungu. Inathibitisha kwamba wewe unamilikiwa na Mungu, kwani moyo wako umemilikiwa na Mungu na wala huwezi kumilikiwa na kitu kingine. Kutokana na tajriba yako, malipo uliyolipa, na kazi ya Mungu, wewe una uwezo wa kuendeleza upendo usioamriwa kwa Mungu. Kisha unawekwa huru kutoka kwa ushawishi wa Shetani na kuishi katika mwanga wa neno la Mungu. Ni wakati tu ambao umekuwa huru kutoka kwa ushawishi wa giza ndipo unaweza kuchukuliwa kuwa umempata Mungu. Katika imani yako kwa Mungu, lazima utafute lengo hili. Huu ni wajibu wa kila mmoja wenu. Hakuna anayelazimika kutosheka na mambo jinsi yalivyo. Hamuwezi kuwa na fikira aina mbili kwa kazi ya Mungu au uichukulie kwa wepesi. Mnapaswa kumfikiria Mungu katika mambo yako yote na wakati wote, na kufanya mambo yote kwa ajili yake. Na wakati mnasema au kufanya mambo, mnapaswa kutilia maanani maslahi ya nyumba ya Mungu kwanza. Ni hii tu ndio inayolingana na mapenzi ya Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kuishi kwa Ajili ya Ukweli kwa Maana Unamwamini Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 394)

Kosa kubwa sana la binadamu kuwa na imani katika Mungu ni kwamba imani yake ni ya maneno tu, na Mungu hayupo popote katika maisha yake ya utendaji. Watu wote, kwa kweli, wanaamini kuwepo kwa Mungu, lakini Mungu si sehemu ya maisha yao ya kila siku. Maombi mengi kwa Mungu hutoka katika kinywa cha mtu, lakini Mungu amepewa nafasi ndogo sana katika moyo wake, na hivyo Mungu humjaribu binadamu tena na tena. Kwa vile mtu ni mchafu, Mungu hana budi ila kumjaribu mtu, ili aweze kuona aibu na kisha aje kujitambua mwenyewe katika majaribu. La sivyo, mwanadamu atageuka mwana wa malaika mkuu, na kuzidi kuwa mpotovu. Wakati wa imani ya mtu katika Mungu, nia nyingi na malengo ya kibinafsi hutupwa mbali anavyotakaswa na Mungu bila kukoma. La sivyo, hakuna mwanadamu anayeweza kutumiwa na Mungu, na Mungu hana njia ya kufanya ndani ya mtu kazi anayopaswa kufanya. Mungu kwanza humtakasa mwanadamu. Katika mchakato huu, mtu anaweza kuja kujijua mwenyewe na Mungu huenda akambadilisha mwanadamu. Ni baada ya haya ndipo Mungu anaweza kuyashughulikia maisha ya mwanadamu, na kwa njia hii pekee ndio moyo wa binadamu unaweza kumgeukia Mungu kwa ukamilifu. Kwa hivyo, kumwamini Mungu si rahisi jinsi mwanadamu anaweza kuona. Mungu anavyoona, ukiwa tu na ufahamu lakini huna neno Lake kama uhai; ikiwa wewe unazingatia tu maarifa yako mwenyewe lakini huwezi kutenda ukweli au kuishi kwa kudhihirisha neno la Mungu, basi hii ni dhihirisho kwamba huna moyo wa upendo kwa Mungu, na inaonyesha kwamba moyo wako si mali ya Mungu. Kuja kumjua Mungu kwa kumwamini; hili ndilo lengo la mwisho na ambalo mwanadamu atatafuta. Lazima ufanye juhudi ya kuishi kwa kudhihirisha maneno ya Mungu ili yaweze kuonekana katika matendo yako. Kama unayo maarifa ya mafundisho ya dini pekee, basi imani yako kwa Mungu itakuwa kazi bure. Kama wewe utatenda pia na kuishi kwa kudhihirisha neno Lake basi imani yako inaweza kuchukuliwa kuwa kamili na kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu. Katika njia hii, wanadamu wengi wanaweza kusema wana maarifa mengi, lakini katika wakati wao wa kufa, macho yao hujawa machozi, nao hujichukia wenyewe kwa kuharibu maisha yao yote na kuishi maisha yasiyo na mazao hadi uzeeni. Wanaelewa tu mafundisho lakini hawawezi kutia ukweli katika vitendo na kushuhudia kwa Mungu, badala yake wakikimbia huku na kule, wakiwa na kazi kama nyuki; mara wanapochungulia kaburi wao hatimaye huona kwamba hawana ushuhuda wa kweli, kwamba hawamjui Mungu kamwe. Je, si huku ni kuchelewa mno? Kwa nini usichukue nafasi hii na kufuatilia ukweli unaoupenda? Kwa nini usubiri hadi kesho? Iwapo katika maisha huwezi kuteseka kwa ajili ya ukweli au kutafuta kuupata, inaweza kuwa kwamba unataka kujuta katika saa yako ya kufa? Ikiwa hivyo, basi kwa nini umwamini Mungu? Kwa kweli, kuna mambo mengi ambayo mtu, iwapo ataweka juhudi kidogo tu, anaweza kuweka ukweli katika vitendo na hivyo kumridhisha Mungu. Moyo wa binadamu daima umepagawa na mapepo na kwa hivyo hawezi kutenda mambo kwa ajili ya Mungu. Badala yake, yeye daima yumo katika safari ya huku na kule kwa sababu ya mwili, na hafaidiki na chochote mwishowe. Ni kwa sababu hizi ndio mtu hupata matatizo ya mara kwa mara na mateso. Je, haya sio mateso ya Shetani? Je, huu sio ufisadi wa mwili? Hufai kumdanganya Mungu kwa maneno ya mdomo. Badala yake, lazima uchukue hatua inayoonekana. Usijidanganye; ni nini maana katika hilo? Ni faida gani utakayopata kutokana na kuishi kwa ajili ya mwili wako na kufanya bidii kwa ajili ya umaarufu na mali ya dunia?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Unapaswa Kuishi kwa Ajili ya Ukweli kwa Maana Unamwamini Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 395)

Sasa, mnatakiwa kufuatilia kugeuka kuwa watu wa Mungu, na mtaanza kuingia kote katika njia sahihi. Kuwa watu wa Mungu kuna maana ya kuingia katika Enzi ya Ufalme. Leo, mnaanza rasmi kuingia katika mafunzo ya ufalme, na maisha yenu ya baadaye yatakoma kuwa goigoi na hobelahobela kama yalivyokuwa awali; maisha hayo ni yasiyoweza kufikia viwango vinavyotakiwa na Mungu. Kama huhisi umuhimu wowote, basi hili huonyesha kwamba huna hamu ya kujiendeleza mwenyewe, kwamba ukimbizaji wako umekanganywa na kuchanganywa, na wewe ni usiyeweza kutimiza mapenzi ya Mungu. Kuingia katika mafunzo ya ufalme kuna maana ya kuanza maisha ya watu wa Mungu—uko radhi kuyakubali mafunzo hayo? Uko radhi kuhisi kuthamini kwa umuhimu? Uko radhi kuishi chini ya nidhamu ya Mungu? Uko radhi kuishi chini ya kuadibu kwa Mungu? Wakati ambapo maneno ya Mungu yatakujia na kukujaribu, utafanyaje? Na utafanya nini wakati ambapo utakabiliwa na aina yote ya ukweli? Zamani, kulenga kwako hakukuwa juu ya maisha; leo, lazima uingie katika uhalisi wa maisha, na kufuatilia mabadiliko katika tabia ya maisha yako. Hili ndilo lazima litimizwe na watu wa ufalme. Wale wote ambao ni watu wa Mungu lazima wawe na uzima, lazima wakubali mafunzo ya ufalme, na kufuatilia mabadiliko katika tabia ya maisha yao. Hili ndilo Mungu huwashurutisha watu wa ufalme.

Masharti ya Mungu kwa watu wa ufalme ni kama yafuatayo:

1. Lazima wakubali maagizo ya Mungu, ambalo ni kusema, lazima wakubali maneno yote yaliyonenwa katika kazi ya Mungu ya siku za mwisho.

2. Lazima waingie katika mafunzo ya ufalme.

3. Lazima wafuatilie kufanya mioyo yao iguswe na Mungu. Wakati ambapo moyo wako umeelekea kwa Mungu kabisa, na una maisha ya kiroho ya kawaida, utaishi katika eneo la uhuru, ambalo lina maana kuwa utaishi chini ya utunzaji na ulinzi wa upendo wa Mungu. Ukiishi chini ya utunzaji na ulinzi wa Mungu tu ndipo utakuwa wa Mungu.

4. Lazima wapatwe na Mungu.

5. Lazima wawe dhihirisho la utukufu wa Mungu duniani.

Haya mawazo makuu matano ni maagizo Yangu kwenu. Maneno Yangu yananenwa kwa watu wa Mungu, na kama hutaki kuyakubali maagizo haya, Sitakulazimisha—lakini ukiyakubali kwa kweli, basi utaweza kuyafanya mapenzi ya Mungu. Leo, anzeni kuyakubali maagizo ya Mungu, na kufuatilia kuwa watu wa ufalme na kufikia viwango vinavyohitajika kuwa watu wa ufalme. Hii ndiyo hatua ya kwanza ya kuingia. Kama ungependa kufanya mapenzi ya Mungu kwa ukamilifu, basi lazima uyakubali maagizo haya matano, na kama unaweza kuyatimiza, utaupendeza moyo wa Mungu na kwa hakika utatumiwa sana na Mungu. Kilicho cha maana sana leo ni kuingia katika mafunzo ya ufalme. Kuingia katika mafunzo ya ufalme kunahusisha maisha ya kiroho. Awali, hakukuwa na mazungumzo ya maisha ya kiroho, lakini leo, unapoanza kuingia katika mafunzo ya ufalme, unaingia rasmi katika maisha ya kiroho.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Ufuate Nyayo Zake

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 396)

Maisha ya kiroho ni maisha ya aina gani? Maisha ya kiroho ni yale ambayo kwayo moyo wako umeelekea kwa Mungu kabisa, na unaweza kuwa mzingatifu wa upendo wa Mungu. Ni yale ambayo kwayo unaishi katika maneno ya Mungu, na hakuna kingine kinachoushughulisha moyo wako, na unaweza kuyafahamu mapenzi ya Mungu leo, na unaongozwa na nuru ya Roho Mtakatifu leo ili kutimiza wajibu wako. Maisha kama hayo kati ya mwanadamu na Mungu ndiyo maisha ya kiroho. Kama huwezi kuifuata nuru ya leo, basi umbali umefunguka katika uhusiano wako na Mungu—huenda hata ukawa umevunjwa—na huna maisha ya kiroho ya kawaida. Uhusiano wa kawaida na Mungu hujengwa juu ya msingi wa kukubali maneno ya Mungu leo. Je, una maisha ya kiroho ya kawaida? Je, una uhusiano wa kawaida na Mungu? Wewe ni mtu anayeifuata kazi ya Roho Mtakatifu? Kama unaweza kufuata nuru ya Roho Mtakatifu leo, na unaweza kufahamu mapenzi ya Mungu ndani ya maneno Yake, na kuingia katika maneno haya, basi wewe ni mtu ambaye hufuata mkondo wa Roho Mtakatifu. Kama hufuati mkondo wa Roho Mtakatifu, basi wewe bila shaka ni mtu asiyefuatilia ukweli. Roho Mtakatifu hana nafasi ya kufanya kazi ndani ya wale ambao hawana hamu ya kujiendeleza wenyewe, na kutokana na hayo, watu hao hawawezi kamwe kukusanya nguvu zao, na kila mara wao huwa baridi. Leo, wewe hufuata mkondo wa Roho Mtakatifu? Wewe uko ndani ya mkondo wa Roho Mtakatifu? Je, umeibuka kutoka kwa hali baridi? Wale wote ambao huamini katika maneno ya Mungu, ambao huchukulia kazi ya Mungu kama msingi, na hufuata nuru ya Roho Mtakatifu leo—wao wote wako ndani ya mkondo wa Roho Mtakatifu. Kama wewe huamini kwamba maneno ya Mungu ni kweli na sahihi kwa dhahiri, na kama wewe huamini maneno ya Mungu bila kujali kile Yeye husema, basi wewe ni mtu ambaye hufuatilia kuingia katika kazi ya Mungu, na kwa njia hii utatimiza mapenzi ya Mungu.

Ili kuingia katika mkondo wa Roho Mtakatifu lazima uwe na uhusiano wa kawaida na Mungu, na lazima kwanza ujiondoshe kwa hali yako baridi. Watu wengine kila mara hufuata walio wengi, na mioyo yao imetangatanga mbali sana na Mungu; watu hao hawana hamu ya kujiendeleza wenyewe, na viwango ambavyo wao hufuatilia ni vya chini sana. Ukimbizaji wa kumpenda Mungu tu na kupatwa na Mungu ndiyo mapenzi ya Mungu. Kuna watu ambao hutumia tu dhamiri yao kulipa mapenzi ya Mungu, lakini hili haliwezi kuridhisha mapenzi ya Mungu; kadri viwango unavyofuatilia vilivyo juu zaidi, ndivyo vitakavyokuwa vinawiana na mapenzi ya Mungu. Kama mtu aliye wa kawaida, na ambaye hufuatilia upendo wa Mungu, kuingia katika ufalme kuwa mmoja wa watu wa Mungu ni siku za usoni zenu za kweli, na maisha ambayo ni yenye thamani na maana sana; hakuna aliyebarikiwa kuliko ninyi. Mbona Nasema hili? Kwa sababu wale wasiomwamini Mungu huishi kwa ajili ya mwili, na wao huishi kwa ajili ya Shetani, lakini leo ninyi huishi kwa ajili ya Mungu, na huishi kufanya mapenzi ya Mungu. Ndiyo maana Nasema maisha yenu ni yenye maana sana. Ni kundi hili tu la watu, ambao wameteuliwa na Mungu, wanaweza kuishi kwa kudhihirisha maisha ya maana sana: Hakuna mwingine duniani anaweza kuishi kwa kudhihirisha maisha ya thamani na maana hivyo. Kwa sababu mmeteuliwa na Mungu, na mmekuzwa na Mungu, na, aidha, kwa sababu ya upendo wa Mungu kwenu, mmefahamu uzima wa kweli, na mnajua namna ya kuishi maisha yenye thamani sana. Hili si kwa sababu ukimbizaji wenu ni mzuri, lakini kwa sababu ya neema ya Mungu; ni Mungu aliyefungua macho ya roho zenu, na ni Roho wa Mungu aliyegusa mioyo yenu, kuwapa ninyi bahati nzuri ya kuja mbele Yake. Kama Roho wa Mungu hangekuwa amekupa nuru, basi hungekuwa na uwezo wa kuona kilicho cha kupendeza kuhusu Mungu, wala haingewezekana kwa wewe kumpenda Mungu. Ni kwa sababu kabisa Roho wa Mungu amegusa mioyo ya watu ndiyo mioyo yao imeelekea kwa Mungu. Mara nyingine, wakati ambapo unafurahia maneno ya Mungu, roho yako huguswa, na wewe huhisi kwamba huna budi kumpenda Mungu, kwamba kuna nguvu nyingi ndani yako, na kwamba hakuna chochote usichoweza kuweka kando. Kama wewe unahisi hivi, basi umeguswa na Roho wa Mungu, na moyo wako umeelekea kwa Mungu kabisa, na utamwomba Mungu na kusema: “Ee Mungu! Sisi kweli tumejaaliwa na kuteuliwa na Wewe. Utukufu Wako hunipa fahari, na inaonekana ya kuleta sifa kuu kwa mimi kuwa mmoja wa watu Wako. Nitatumia chochote na kutoa chochote ili kufanya mapenzi Yako, na nitayatoa maisha yangu yote, na juhudi za maisha yangu yote, Kwako.” Unapoomba hivi, kutakuwa na upendo usioisha na utiifu wa kweli kwa Mungu ndani ya moyo wako. Je, umewahi kuwa na tukio kama hili? Kama watu huguswa mara kwa mara na Roho wa Mungu, basi wako radhi hasa kujitolea wenyewe kwa Mungu katika maombi yao: “Ee Mungu! Ningependa kutazama siku Yako ya utukufu, na ningependa kuishi kwa ajili Yako—hakuna kilicho cha thamani au maana zaidi kuliko kuishi kwa ajili Yako, na sina hamu hata kidogo ya kuishi kwa ajili ya Shetani na mwili. Wewe huniinua kwa kuniwezesha mimi kuishi kwa ajili Yako leo.” Wakati ambapo umeomba kwa njia hii, utahisi kwamba huna budi ila kutoa moyo wako kwa Mungu, kwamba lazima umpate Mungu, na kwamba ungechukia kufa bila kumpata Mungu wakati ambapo uko hai. Baada ya kunena ombi hilo, kutakuwa na nguvu isiyoisha ndani yako, na hutajua hiyo hutoka wapi; ndani ya moyo wako kutakuwa na nguvu bila kikomo, na utakuwa na hisi kwamba Mungu ni wa kupendeza sana, na kwamba Anastahili kupendwa. Huu ndio wakati ambapo utakuwa umeguswa na Mungu. Wale wote ambao wamekuwa na tukio hilo wameguswa na Mungu. Kwa wale ambao mara kwa mara huguswa na Mungu, mabadiliko hutokea ndani ya maisha yao, wao huweza kufanya azimio lao na wako radhi kumpata Mungu kabisa, upendo kwa Mungu ndani yao ni thabiti zaidi, mioyo yao imeelekea kwa Mungu kabisa, wao huwa hawastahi familia, ulimwengu, matatizo, au siku zao za baadaye, na wao huwa radhi kutoa juhudi za maisha yote kwa Mungu. Wale wote ambao wameguswa na Roho wa Mungu ni watu wanaofuatilia ukweli, na ambao huwa na tumaini la kufanywa wakamilifu na Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Ufuate Nyayo Zake

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 397)

Kilicho na umuhimu mkuu katika kumfuata Mungu ni kwamba kila kitu kinapaswa kuwa kwa kadri ya maneno ya Mungu leo: Kama unafuatilia kuingia katika uzima au kutimiza mapenzi ya Mungu, kila kitu kinapaswa kulenga maneno ya Mungu leo. Kama kile ambacho unawasiliana kwa karibu na kufuatilia hakilengi maneno ya Mungu leo, basi wewe ni mgeni kwa maneno ya Mungu, na umeondolewa kabisa katika kazi ya Roho Mtakatifu. Kile ambacho Mungu hutaka ni watu ambao huzifuata nyayo Zake. Haijalishi vile ulichoelewa awali ni cha ajabu na safi, Mungu hakitaki, na kama huwezi kuweka kando vitu hivyo, basi vitakuwa kizuizi kikubwa mno kwa kuingia kwako katika siku za baadaye. Wale wote ambao wanaweza kufuata nuru ya sasa ya Roho Mtakatifu wamebarikiwa. Watu wa enzi zilizopita pia walifuata nyayo za Mungu, ilhali hawangeweza kufuata mpaka leo; hii ndiyo baraka ya watu wa siku za mwisho. Wale ambao wanaweza kufuata kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu, na ambao wanaweza kuzifuata nyayo za Mungu, kiasi kwamba wamfuate Mungu popote Awaongozapo—hawa ni watu ambao wamebarikiwa na Mungu. Wale wasiofuata kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu hawajaingia katika kazi ya maneno ya Mungu, na haijalishi wanafanya kazi kiasi gani, au mateso yao ni makubwa vipi, au wanakimbia hapa na pale kiasi gani, hakuna linalomaanisha chochote kwa Mungu kati ya hayo, na Yeye hatawasifu. Leo, wale wote ambao hufuata maneno ya sasa ya Mungu wako ndani ya mkondo wa Roho Mtakatifu; wale ambao ni wageni kwa maneno ya leo ya Mungu wako nje ya mkondo wa Roho Mtakatifu, na watu hao hawasifiwi na Mungu. Huduma ambayo imetenganishwa na matamshi ya sasa ya Roho Mtakatifu ni huduma ambayo ni ya mwili, na ya dhana, na haiwezi kuwa kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu. Kama watu huishi miongoni mwa dhana za kidini, basi hawawezi kufanya lolote lenye kustahili kwa mapenzi ya Mungu, na hata ingawa wao humhudumia Mungu, wao huhudumu katikati ya mawazo na dhana zao, na hawawezi kabisa kuhudumu kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu. Wale ambao hawawezi kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu hawaelewi mapenzi ya Mungu, na wale ambao hawaelewi mapenzi ya Mungu hawawezi kumhudumia Mungu. Mungu hutaka huduma inayoupendeza moyo Wake mwenyewe; Hataki huduma ambayo ni ya dhana na mwili. Kama watu hawawezi kuzifuata hatua za kazi ya Roho Mtakatifu, basi wao huishi katikati ya dhana. Huduma ya watu hao hukatiza na huvuruga, na huduma ya aina hii huenda kinyume na Mungu. Hivyo wale ambao hawawezi kuzifuata nyayo za Mungu hawawezi kumhudumia Mungu; wale ambao hawawezi kuzifuata nyayo za Mungu humpinga Mungu bila shaka, na ni wasioweza kulingana na Mungu. “Kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu” kuna maana ya kufahamu mapenzi ya Mungu leo, kuweza kutenda kwa mujibu wa masharti ya sasa ya Mungu, kuweza kutii na kumfuata Mungu wa leo, na kuingia kwa mujibu wa matamshi mapya zaidi ya Mungu. Huyu pekee ndiye mtu ambaye hufuata kazi ya Roho Mtakatifu na yuko ndani ya mkondo wa Roho Mtakatifu. Watu hao hawawezi tu kupokea sifa za Mungu na kumwona Mungu, lakini wanaweza pia kujua tabia ya Mungu kutoka kwa kazi ya karibuni zaidi ya Mungu, na wanaweza kujua dhana na ukaidi wa mwanadamu, na asili na kiini cha mwanadamu, kutoka kwa kazi Yake ya karibuni zaidi; pia, wanaweza kutimiza polepole mabadiliko katika tabia yao wakati wa huduma yao. Ni watu kama hawa pekee ndio wanaoweza kumpata Mungu, na ambao wamepata kwa halisi njia ya kweli. Wale ambao huondoshwa na kazi ya Roho Mtakatifu ni watu wasioweza kufuata kazi ya karibuni zaidi ya Mungu, na ambao huasi dhidi ya kazi ya karibuni zaidi ya Mungu. Kwamba watu hao humpinga Mungu waziwazi ni kwa sababu Mungu amefanya kazi mpya, na kwa sababu picha ya Mungu si sawa na ile iliyo ndani ya dhana zao—kutokana na hilo wao humpinga Mungu waziwazi na kumhukumu Mungu, kusababisha wao kuchukiwa na kukataliwa na Mungu. Kuwa na ufahamu wa kazi ya karibuni zaidi ya Mungu si jambo rahisi, lakini kama watu wana nia ya kutii kazi ya Mungu kwa kudhamiria na kuitafuta kazi ya Mungu, basi watakuwa na nafasi ya kumwona Mungu, na watakuwa na nafasi ya kupata uongozi mpya zaidi wa Roho Mtakatifu. Wale ambao hupinga kazi ya Mungu kwa kudhamiria hawawezi kupata nuru ya Roho mtakatifu au uongozi wa Mungu. Hivyo, kama watu wanaweza kupokea kazi ya karibuni zaidi ya Mungu au la hutegemea neema ya Mungu, hutegemea ukimbizaji wao, na hutegemea makusudi yao.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Ufuate Nyayo Zake

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 398)

Wale wote ambao huweza kutii matamshi ya sasa ya Roho Mtakatifu wamebarikiwa. Haijalishi vile walikuwa, au vile Roho Mtakatifu alikuwa akifanya kazi ndani yao—wale ambao wamepata kazi ya karibuni zaidi ni waliobarikiwa zaidi, na wale ambao hawawezi kufuata kazi ya karibuni zaidi huondoshwa. Mungu anataka wale wanaoweza kukubali nuru mpya, na Anataka wale ambao hukubali na kujua kazi Yake ya karibuni zaidi. Kwa nini husemwa kwamba lazima uwe mwanamwali safi? Mwanamwali safi anaweza kutafuta kazi ya Roho Mtakatifu na kuelewa mambo mapya, na zaidi ya hayo, kuweza kuweka kando dhana za zamani, na kutii kazi ya Mungu leo. Kundi hili la watu, ambao hukubali kazi mpya zaidi ya leo, walijaaliwa na Mungu kabla ya enzi, na ni ambao wamebarikiwa zaidi ya watu wote. Ninyi huisikia sauti ya Mungu moja kwa moja, na kutazama kuonekana kwa Mungu, na hivyo, kotekote mbinguni na duniani, na kotekote katika enzi, hakuna waliobarikiwa kuliko ninyi, hili kundi la watu. Haya yote ni kwa sababu ya kazi ya Mungu, kwa sababu ya majaaliwa na uteuzi wa Mungu, na kwa sababu ya neema ya Mungu; kama Mungu hangeongea na kutamka maneno Yake, hali zenu zingekuwa kama zilivyo leo? Vivi hivi, utukufu wote na sifa ziwe kwa Mungu, kwani haya yote ni kwa sababu Mungu huwainua ninyi. Na mambo haya yakiwa akilini, bado ungeweza kuwa baridi? Nguvu zako bado hazingeweza kuongezeka?

Kwamba wewe huweza kukubali hukumu, kuadibu, kuangamiza, na usafishaji wa maneno ya Mungu, na, aidha, unaweza kukubali maagizo ya Mungu, lilijaaliwa na Mungu mwanzoni mwa wakati, na hivyo lazima usihuzunishwe sana wakati ambapo wewe huadibiwa. Hakuna anayeweza kuondoa kazi ambayo imefanywa ndani yenu, na baraka ambazo zimetolewa ndani yenu, na hakuna anayeweza kuondoa yote ambayo mmepewa ninyi. Watu wa dini hawastahimili mlingano na ninyi. Ninyi hamna ubingwa mkuu katika Biblia, na hamjajizatiti na nadharia za kidini, lakini kwa sababu Mungu amefanya kazi ndani yenu, mmepata zaidi ya yeyote kotekote katika enzi—na kwa hiyo hii ni baraka yenu kuu zaidi. Kwa sababu ya hili, lazima mjitolee hata zaidi kwa Mungu, na hata waaminifu zaidi kwa Mungu. Kwa sababu Mungu hukuinua, lazima utegemeze juhudi zako, na lazima utayarishe kimo chako kukubali maagizo ya Mungu. Lazima usimame imara mahali ambapo Mungu amekupa, ufuatilie kuwa mmoja wa watu wa Mungu, ukubali mafunzo ya ufalme, upatwe na Mungu na hatimaye kuwa ushuhuda wa kuleta sifa kuu kwa Mungu. Je, wewe una maazimio haya? Kama una maazimio hayo, basi hatimaye una hakika ya kupatwa na Mungu, na utakuwa ushuhuda wa kuleta sifa kuu kwa Mungu. Unapaswa kuelewa kwamba agizo kuu ni kupatwa na Mungu na kugeuka kuwa ushuhuda wa kuleta sifa kuu kwa Mungu. Haya ni mapenzi ya Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Ufuate Nyayo Zake

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 399)

Maneno ya Roho Mtakatifu leo ni nguvu za kazi ya Roho Mtakatifu, na kuendelea kwa Roho Mtakatifu kumpa nuru mwanadamu wakati wa kipindi hiki ni mwelekeo wa kazi ya Roho Mtakatifu. Na mwelekeo ni upi katika kazi ya Roho Mtakatifu leo? Ni uongozi wa watu ndani ya kazi ya Mungu leo, na ndani ya maisha ya kiroho ya kawaida. Kuna hatua kadhaa za kuingia katika maisha ya kiroho ya kawaida:

1. Kwanza, lazima uumimine moyo wako ndani ya maneno ya Mungu. Lazima usiyafuatilie maneno ya Mungu katika siku za zamani, na lazima usiyasome wala kuyafananisha na maneno ya sasa. Badala yake, lazima uumimine moyo wako kabisa katika maneno ya sasa ya Mungu. Kama kuna watu ambao bado wangependa kuyasoma maneno ya Mungu, vitabu vya kiroho, au maelezo mengine ya mahubiri kutoka kwa siku za zamani, ambao hawafuati maneno ya Roho Mtakatifu leo, basi wao ni wapumbavu zaidi ya watu wote; Mungu huchukia sana watu kama hao. Kama uko radhi kukubali nuru ya Roho Mtakatifu leo, basi mimina moyo wako kabisa katika matamshi ya Mungu leo. Hili ni jambo la kwanza ambalo lazima utimize.

2. Lazima uombe juu ya msingi wa maneno yaliyonenwa na Mungu leo, uingie ndani ya maneno ya Mungu na uwasiliane kwa karibu na Mungu, na ufanye maazimio yako mbele ya Mungu, ni viwango vipi ambavyo ungependa kufuatilia ufanikishaji wake.

3. Lazima ufuatilie kuingia kwa maana sana ndani ya ukweli juu ya msingi wa kazi ya Roho Mtakatifu leo. Usishikilie matamshi na nadharia zilizopitwa na wakati kutoka zamani.

4. Lazima utafute kuguswa na Roho Mtakatifu, na kuingia katika maneno ya Mungu.

5. Lazima ufuatilie kuingia katika njia ambayo Roho Mtakatifu anatembea leo.

Na ni vipi ambavyo wewe hutafuta kuguswa na Roho Mtakatifu? Kilicho muhimu ni kuishi ndani ya maneno ya sasa ya Mungu, na kuomba juu ya msingi wa masharti ya Mungu. Baada ya kuomba kwa njia hii, Roho Mtakatifu kwa kweli atakugusa. Kama hutafuti kwa kutegemea msingi wa maneno yaliyonenwa na Mungu leo, basi hili ni bure. Unapaswa kuomba, na kusema: “Ee Mungu! Mimi hukupinga Wewe, na unanidai Mimi mengi sana; mimi ni mkaidi sana, na siwezi kamwe kukuridhisha Wewe. Ee Mungu, natamani Wewe uniokoe, natamani kukupa Wewe huduma hadi mwisho kabisa, natamani kufa kwa ajili Yako. Wewe hunihukumu na kuniadibu, na sina malalamiko; mimi hukupinga Wewe na nastahili kufa, ili watu wote waweze kutazama tabia Yako yenye haki katika kifo changu.” Wakati ambapo wewe huomba kutoka moyoni mwako kwa njia hii, Mungu atakusikia, na atakuongoza; kama huombi juu ya msingi wa maneno ya Roho Mtakatifu leo, basi hakuna uwezekano wa Roho Mtakatifu kukugusa wewe. Kama wewe huomba kwa kadri ya mapenzi ya Mungu, na kwa kadri ya kile ambacho Mungu hutaka kufanya leo, utasema: “Ee Mungu! Nataka kukubali maagizo Yako na kuwa mwaminifu kwa maagizo Yako, na niko radhi kuyatoa maisha yangu yote kwa utukufu Wako, ili yote nifanyayo yaweze kufikia kiwango cha watu wa Mungu. Moyo wangu na uweze kuguswa na Wewe. Nataka Roho Wako anipe nuru wakati wowote, kusababisha yote nifanyayo yalete aibu kwa Shetani, ili hatimaye nipatwe na Wewe.” Kama wewe huomba kwa njia hii, ukilenga mapenzi ya Mungu, basi Roho Mtakatifu atafanya kazi ndani yako bila kuzuilika. Haijalishi maneno ya maombi yako ni mangapi—kilicho muhimu ni kama unaelewa mapenzi ya Mungu au la. Huenda ninyi nyote mmekuwa na tukio lifuatalo: Wakati mwingine, ukiwa unaomba katika kusanyiko, nguvu za kazi ya Roho Mtakatifu hufikia kilele chake, kusababisha nguvu za kila mtu kuongezeka. Watu wengine hulia kwa uchungu na kutoa machozi huku wakiomba, kwa kulemewa na majuto mbele ya Mungu, na watu wengine huonyesha azimio lao, na kuweka nadhiri. Hiyo ndiyo athari ya kutimizwa na kazi ya Roho Mtakatifu. Leo, ni ya muhimu sana kwamba watu wote wamimine mioyo yao kabisa ndani ya maneno ya Mungu. Usisisitize kwa maneno yaliyonenwa awali; kama bado unashikilia kilichokuja awali, basi Roho Mtakatifu hatafanya kazi ndani yako. Je, waona vile hili ni muhimu?

Je, mnajua njia ambayo Roho Mtakatifu hutembea leo? Mawazo makuu kadhaa hapo juu ni kile kitakachotimizwa na Roho Mtakatifu leo na katika siku za baadaye; ni njia inayofuatwa na Roho Mtakatifu, na kuingia ambako kunapaswa kufuatiliwa na mwanadamu. Katika kuingia kwako maishani, kwa kiasi kidogo sana lazima umimine moyo wako ndani ya maneno ya Mungu, na uweze kukubali hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu; moyo wako lazima uwe na shauku kwa Mungu, lazima ufuatilie kuingia kwa maana sana katika ukweli, na malengo ambayo Mungu hutaka. Wakati ambapo unakuwa na nguvu hizi, basi hilo huonyesha kuwa umeguswa na Mungu, na moyo wako umeanza kuelekea kwa Mungu.

Hatua ya kwanza ya kuingia katika uzima ni kuumimina moyo wako kabisa ndani ya maneno ya Mungu, na hatua ya pili ni kukubali kuguswa na Roho Mtakatifu. Ni nini athari ya kutimizwa kwa kukubali kuguswa na Roho Mtakatifu? Kuweza kuwa na shauku ya, kutafuta, na kuchunguza ukweli wa maana sana, na kuwa na uwezo wa kushirikiana na Mungu katika njia nzuri. Leo, wewe hushirikiana na Mungu, ambalo ni kusema kuna lengo kwa ukimbizaji wako, kwa maombi yako, na kwa mawasiliano yako ya maneno ya Mungu, na wewe hutekeleza wajibu wako kwa mujibu wa masharti ya Mungu—huku pekee ndiko kushirikiana na Mungu. Ukizungumza tu kuhusu kumwacha Mungu atende, lakini usichukue hatua yoyote, wala kuomba au kutafuta, basi hili lingeweza kuitwa ushirikiano? Kama huna chochote kuhusu ushirikiano ndani yako, na umeondolewa mafunzo ya kuingia ambayo yana lengo, basi wewe hushirikiani? Watu wengine husema: “Kila kitu hutegemea majaaliwa ya Mungu, yote hufanywa na Mungu mwenyewe: kama Mungu hangelifanya, basi mwanadamu angewezaje?” Kazi ya Mungu ni ya kawaida, na siyo ya rohoni hata kidogo, na ni kupitia tu kwa utafutaji wako wa utendaji ndiyo Roho Mtakatifu hufanya kazi, kwani Mungu hamlazimishi mwanadamu—lazima umpe Mungu nafasi ya kufanya kazi, na kama hufuatilii au kuingia, na kama hakuna shauku hata kidogo ndani ya moyo wako, basi Mungu hana nafasi ya kufanya kazi. Ni kwa njia ipi ndio unaweza kutafuta kuguswa na Mungu? Kupitia maombi, na kuja karibu na Mungu. Lakini la muhimu zaidi, kumbuka, lazima iwe juu ya msingi wa maneno yanayonenwa na Mungu. Wakati ambapo unaguswa mara kwa mara na Mungu, hutawaliwi kabisa na mwili: Mume, mke, watoto, na pesa—yote ni yasiyoweza kukufunga wewe, na wewe hutamani kufuatilia tu ukweli na kuishi mbele ya Mungu. Wakati huu, utakuwa mtu anayeishi katika eneo la uhuru.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Ufuate Nyayo Zake

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 400)

Mungu ameamua kumfanya mwanadamu mkamilifu, na bila kujali mtazamo ambao Ananena kutoka, yote ni kwa sababu ya kuwafanya watu wawe wakamilifu. Maneno yanenwayo kutoka katika mtazamo wa Roho ni magumu kwa watu kuelewa; hawana namna ya kupata njia ya kutenda, kwa kuwa uwezo wao wa kuelewa ni finyu. Kazi ya Mungu inafikia matokeo tofauti, na katika kuchukua kila hatua ya kazi Ana kusudi Lake. Aidha, ni muhimu kwamba Azungumze kutoka katika mitazamo tofauti, kwa kuwa ni kwa kufanya hivyo tu ndipo Anaweza kumkamilisha mwanadamu. Kama Angetamka sauti Yake kutoka katika mtazamo wa Roho tu, hakungekuwa na njia yoyote ya kukamilisha hatua hii ya kazi ya Mungu. Kutoka katika sauti Anayozungumza nayo, unaweza kuona kwamba Amedhamiria kulifanya kundi hili la watu kamilifu. Kwa hivyo, hatua ya kwanza kwa kila anayetamani kukamilishwa inapasa kuwa ipi? Zaidi ya yote, lazima uijue kazi ya Mungu. Leo, njia mpya imeanza katika kazi ya Mungu; enzi imebadilika, namna ambavyo Mungu hufanya kazi pia imebadilika, na njia ambayo Mungu huzungumza ni tofauti. Leo, sio tu kwamba njia ya kazi Yake imebadilika, lakini pia enzi imebadilika. Sasa ni Enzi ya Ufalme. Pia ni Enzi ya kumpenda Mungu. Ni kionjo cha Enzi ya Ufalme wa Milenia—ambayo pia ni Enzi ya Neno, na ambayo Mungu hutumia njia nyingi za kunena ili kumkamilisha mwanadamu, na Ananena kutoka katika mitazamo tofauti ili kumruzuku mwanadamu. Baada ya kuingia katika Enzi ya Ufalme wa Milenia, Mungu ataanza kutumia maneno kumfanya mwanadamu awe mkamilifu, Akimruhusu mwanadamu aingie katika uhalisi wa maisha na kumwongoza kwenye njia sahihi. Mwanadamu amepitia hatua nyingi sana za kazi Yake na ameona kuwa kazi ya Mungu haibaki vile vile, lakini inageuka na kuongezeka kwa kina bila kukoma. Baada ya watu kuipitia kwa muda mrefu sana, kazi imebadilika kwa kurudia rudia, ikibadilika tena na tena. Hata hivyo, bila kujali kiasi inachobadilika, kamwe haikengeuki kutoka kwa kusudi la Mungu la kuwaletea binadamu wokovu. Hata kupitia katika mabadiliko elfu kumi, kamwe haipotei kutoka kwa kusudi lake la asili. Bila kujali jinsi mbinu ya kazi ya Mungu inavyoweza kubadilika, kazi hii kamwe haiuachi ukweli au uzima. Mabadiliko katika njia ambayo kazi hufanywa inahusisha mabadiliko katika muundo wa kazi tu, na mtazamo ambao kwao Mungu ananena; hakuna mabadiliko katika kusudi kuu la kazi ya Mungu. Mabadiliko katika toni ya sauti ya Mungu na njia ya kazi Yake hufanywa ili kufikia matokeo. Mabadiliko katika toni ya sauti hayamaanishi mabadiliko katika madhumuni au kanuni ya kazi hiyo. Watu wanamwamini Mungu hasa ili kutafuta uzima; ikiwa unaamini katika Mungu lakini hutafuti uzima au hufuatilii ukweli au maarifa ya Mungu, basi hii siyo imani katika Mungu! Na, je, bado ni jambo lenye uhalisi kutafuta kuingia katika ufalme kuwa mfalme? Kufanikisha upendo wa kweli kwa Mungu kupitia kutafuta uzima—huu pekee ndio uhalisi; ufuatiliaji na utendaji wa ukweli—hivi vyote ni uhalisi. Kusoma maneno ya Mungu, na kuyapitia maneno haya, utakuja kufahamu maarifa ya Mungu katika uzoefu halisi, na hii ndiyo maana ya kufuatilia kweli.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Enzi ya Ufalme Ni Enzi ya Neno

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 401)

Sasa ni Enzi ya Ufalme. Ikiwa umeingia katika enzi hii mpya inategemea ikiwa umeingia katika uhalisi wa maneno ya Mungu, ikiwa maneno Yake yamekuwa uhalisi wa maisha yako. Maneno ya Mungu yanafahamishwa kwa kila mtu ili, mwishowe, watu wote wataishi katika ulimwengu wa maneno ya Mungu, na maneno Yake yatampa nuru na kumwangazia kila mtu kutoka ndani. Ikiwa, wakati huu, wewe ni mzembe katika kusoma maneno ya Mungu, na huna shauku ya maneno Yake, basi hili linaonyesha kuwa hali yako ni mbaya. Ikiwa huwezi kuingia katika Enzi ya Neno, basi Roho Mtakatifu hafanyi kazi ndani yako; ikiwa umeingia katika enzi hii, Atafanya kazi Yake. Je, unaweza kufanya nini mwanzoni mwa Enzi ya Neno ili upate kazi ya Roho Mtakatifu? Katika enzi hii, na miongoni mwenu, Mungu atatimiza ukweli ufuatao: kwamba kila mtu ataishi kwa kuyadhihirisha maneno ya Mungu, ataweza kuuweka ukweli katika vitendo, na atampenda Mungu kwa dhati; kwamba watu wote watatumia maneno ya Mungu kama msingi na kama uhalisi wao, na watakuwa na mioyo inayomcha Mungu; na kwamba, kupitia kutenda maneno ya Mungu, mwanadamu kisha atashikilia mamlaka ya kifalme pamoja na Mungu. Hii ndiyo kazi inayopaswa kufanikishwa na Mungu. Je, unaweza kuishi bila kusoma maneno ya Mungu? Leo, kuna wengi ambao wanahisi kuwa hawawezi kuishi hata siku moja au mbili bila kusoma maneno Yake. Lazima wayasome maneno Yake kila siku, na ikiwa muda hauruhusu, kuyasikiza kutatosha. Hii ndiyo hisia ambayo Roho Mtakatifu huwapa watu, na ndiyo njia ambayo Anaanza kuwagusa. Yaani, Yeye huwatawala watu kupitia maneno, ili kwamba waweze kuingia katika uhalisi wa maneno ya Mungu. Ikiwa, baada ya siku moja tu bila kula na kunywa maneno ya Mungu, unahisi giza na kiu, na huwezi kustahimili hali hiyo, hili linaonyesha kwamba umeguswa na Roho Mtakatifu, na kwamba Hajakukuacha. Wewe basi, ni mtu aliye kwenye mkondo huu. Hata hivyo, ikiwa baada ya siku moja au mbili bila kula na kunywa maneno ya Mungu, huhisi kitu, ikiwa huna kiu, na hujaguswa hata kidogo, hili linaonyesha kwamba Roho Mtakatifu amekuacha. Hili linamaanisha, basi, kwamba kuna kitu kibaya na hali yako; hujaingia katika Enzi ya Neno, na wewe ni mmoja wa wale ambao wamebaki nyuma. Mungu hutumia maneno kuwatawala watu; unahisi vizuri ukila na kunywa maneno ya Mungu, na usipokula na kunywa maneno ya Mungu, huna njia ya kufuata. Maneno ya Mungu huwa chakula cha watu, na nguvu inayowaendesha. Biblia inasema “Mwanadamu hataishi kwa mkate pekee, lakini kwa kila neno linalotoka kinywani mwa Mungu”. Leo, Mungu ataikamilisha kazi hii, naye Ataukamilisha ukweli huu ndani yenu. Ni vipi kwamba hapo zamani, watu wangeweza kwenda siku nyingi bila kusoma maneno ya Mungu na bado waweze kula na kufanya kazi kama kawaida, lakini hivi sivyo ilivyo leo? Katika enzi hii, Mungu haswa hutumia maneno kutawala vyote. Kupitia katika maneno ya Mungu, mwanadamu anahukumiwa na kukamilishwa, kisha hatimaye kupelekwa katika ufalme. Maneno ya Mungu tu ndiyo yanayoweza kuyaruzuku maisha ya mwanadamu, na ni maneno ya Mungu tu yanayoweza kumpa mwanadamu mwangaza na njia ya kutenda, hasa katika Enzi ya Ufalme. Alimradi hupotei kutoka katika ukweli wa maneno ya Mungu, kula na kunywa maneno Yake kila siku, Mungu ataweza kukufanya mkamilifu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Enzi ya Ufalme Ni Enzi ya Neno

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 402)

Ufuatiliaji wa maisha si jambo ambalo linaweza kuharakishwa; ukuaji wa maisha haufanyiki kwa siku moja au mbili. Kazi ya Mungu ni ya kawaida na ya vitendo, na kuna mchakato ambao lazima ipitie. Ilimchukua Yesu mwenye mwili miaka thelathini na mitatu na nusu kukamilisha kazi Yake ya kusulubiwa—sembuse kazi ya kumtakasa mwanadamu na kuyabadilisha maisha yake, kazi ngumu zaidi? Sio kazi rahisi kumfanya mwanadamu wa kawaida ambaye anamdhihirisha Mungu. Hili ni hivyo hasa kwa watu ambao wamezaliwa katika taifa la joka kubwa jekundu, ambao ni wenye ubora duni wa tabia na wanahitaji muda mrefu wa maneno na kazi ya Mungu. Kwa hivyo usiwe bila subira kutaka kuona matokeo. Lazima uwe mwenye kujitolea katika kula na kunywa maneno ya Mungu, na uweke bidii zaidi katika maneno ya Mungu. Unapomaliza kusoma maneno Yake, lazima uweze kuyaweka katika vitendo halisi, ukikua katika maarifa, ufahamu, utambuzi, na hekima katika maneno ya Mungu. Kupitia katika hili, utabadilika bila kufahamu. Ikiwa unaweza kuchukua kula na kunywa maneno ya Mungu kama kanuni yako, ukiyasoma, ukija kuyajua, kuyapitia, na kuyatenda, utakuwa mkomavu bila kufahamu. Kuna wale ambao wanasema kuwa hawawezi kuyaweka maneno ya Mungu katika vitendo hata baada ya kuyasoma. Haraka yako ni nini? Utakapofikia kimo fulani, utaweza kuyaweka maneno Yake katika vitendo. Je, mtoto wa umri wa miaka minne au mitano anaweza kusema kuwa hawezi kuwasaidia au kuwaheshimu wazazi wake? Unapaswa kujua jinsi kimo chako cha sasa kilivyo kikubwa. Weka katika vitendo kile unachoweza kuweka katika vitendo, na uepukane na kuwa mtu ambaye anasumbua usimamizi wa Mungu. Kula na kunywa maneno ya Mungu tu, na ulichukue hilo kama kanuni yako kuanzia sasa kuendelea. Usijali, kwa wakati huu, kuhusu ikiwa Mungu anaweza kukufanya mkamilifu. Usilichunguze hilo kwa sasa. Kula na kunywa maneno ya Mungu tu yanavyokujia, na Mungu hakika Atakufanya mkamilifu. Hata hivyo, kuna kanuni ambayo kwayo lazima ule na kunywa maneno Yake. Usifanye hivyo tu bila kufikiria. Katika kula na kunywa maneno ya Mungu, kwa upande mmoja, yatafute maneno ambayo unapaswa kuyajua—yaani, yale yanayohusiana na maono—na kwa upande mwingine, tafuta kile unachopaswa kuweka katika vitendo halisi—yaani, kile unachopaswa kuingia ndani. Kipengele kimoja kinahusiana na maarifa, na kingine kinahusiana na kuingia. Mara unapovifahamu vyote viwili—wakati umeshaelewa kile unachopaswa kujua na kile unachopaswa kutenda utajua jinsi ya kula na kunywa maneno ya Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Enzi ya Ufalme Ni Enzi ya Neno

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 403)

Kuanzia sasa kuendela, mazungumzo ya maneno ya Mungu yanapaswa kuwa kanuni ambayo kwayo unazungumza. Kwa kawaida, mnapojumuika pamoja, mnapaswa kushiriki katika ushirika kuhusu maneno ya Mungu, mkiyachukua maneno ya Mungu kama maudhui ya mwingiliano wenu, mkiongea juu ya yale mnayojua kuhusu maneno haya, jinsi mnavyoyaweka katika vitendo, na jinsi Roho Mtakatifu afanyavyo kazi. Alimradi unashiriki maneno ya Mungu, Roho Mtakatifu atakupa nuru. Kufanikisha ulimwengu wa maneno ya Mungu kunahitaji ushirikiano wa mwanadamu. Usipoingia katika hili, Mungu hatakuwa na njia ya kufanya kazi; ukiufunga mdomo wako na usizungumze kuhusu maneno Yake, Hatakuwa na njia ya kukuangazia. Wakati wowote ambapo huna shughuli nyingine, zungumza juu ya maneno ya Mungu, na usijishughulishe na mazungumzo yasiyo na maana! Acha maisha yako yajazwe na maneno ya Mungu—ni hapo tu ndipo utakapokuwa mwumini mwenye kumcha Mungu. Haijalishi ikiwa ushirika wako ni wa juu juu. Bila ujuu juu hakuwezi kuwepo kina kirefu. Lazima kuwe na mchakato. Kupitia mafunzo yako, utafahamu kuangaziwa kwako na Roho Mtakatifu, na jinsi ya kula na kunywa maneno ya Mungu kwa matokeo yanayotarajiwa. Baada ya muda wa uchunguzi, utaingia katika ukweli wa maneno ya Mungu. Ni ukiamua kushirikiana tu ndipo utaweza kupokea kazi ya Roho Mtakatifu.

Kati ya kanuni za kula na kunywa maneno ya Mungu, moja inahusiana na maarifa, na nyingine inahusiana na kuingia. Ni maneno yapi unayopaswa kujua? Unapaswa kujua maneno yanayohusiana na maono (kama vile, yale yanayohusiana na ni enzi ipi ambayo kazi ya Mungu imeingia sasa, kile ambacho Mungu anataka kufanikisha sasa, kupata mwili ni nini, na kadhalika; haya yote yanahusiana na maono). Je, njia ambayo mwanadamu anapaswa kuingia katika inamaanisha nini? Hii inahusu maneno ya Mungu ambayo mwanadamu anapaswa kutenda na kuingia ndani. Yaliyo hapo juu ni vipengele viwili vya kula na kunywa maneno ya Mungu. Kuanzia sasa, kula na kunywa maneno ya Mungu kwa njia hii. Ukiwa na ufahamu wazi wa maneno Yake kuhusu maono, basi hakuna haja ya kuendelea kusoma kila wakati. Jambo la umuhimu wa msingi ni kula na kunywa maneno zaidi ya kuingia, kama vile kuugeuza moyo wako kwa Mungu, jinsi ya kuutuliza moyo wako mbele za Mungu, na jinsi ya kuunyima mwili. Hivi ni vitu ambavyo unapaswa kuweka katika vitendo. Bila kujua jinsi ya kula na kunywa maneno ya Mungu, ushirika wa kweli hauwezekani. Mara tu unapojua jinsi ya kula na kunywa maneno Yake, wakati ambapo umeelewa kile kilicho muhimu, ushirika utakuwa wazi, na suala lolote liibuliwalo, utaweza kushirikiana na kufahamu uhalisi. Ikiwa, wakati unashiriki kuhusu maneno ya Mungu, huna uhalisi wowote, basi hujaelewa kile kilicho cha muhimu, ambalo linaonyesha kuwa hujui jinsi ya kula na kunywa maneno ya Mungu. Watu wengine wanaweza kupata kusoma maneno ya Mungu kuwa jambo la kuchosha, ambayo sio hali ya kawaida. Kilicho cha kawaida ni kamwe kutochoka kuyasoma maneno ya Mungu, kuwa na kiu ya maneno hayo kila wakati, na daima kuyaona maneno ya Mungu kuwa mazuri. Hivi ndivyo mtu ambaye ameingia kwa kweli hula na kunywa maneno ya Mungu. Unapohisi kuwa maneno ya Mungu ni ya vitendo sana na ndiyo mwanadamu anapaswa kuingia katika hasa; unapohisi kuwa maneno Yake ni ya msaada mkubwa na yenye faida kwa mwanadamu, na kwamba ni riziki ya maisha ya mwanadamu—ni Roho Mtakatifu anayekupa hisia hii, na Roho Mtakatifu anayekugusa. Hii inathibitisha kuwa Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yako na kwamba Mungu hajakuacha. Watu wengine, wakiona kuwa Mungu huzungumza kila wakati, huchoka na maneno Yake, na hufikiria kwamba haina athari wakiyasoma au la—ambayo si hali ya kawaida. Wanakosa moyo ambao unatamani kuingia katika uhalisi, na watu kama hao hawana kiu wala hawaoni umuhimu wa kukamilishwa. Kila unapopata kuwa huna kiu ya maneno ya Mungu, hii inaonyesha kuwa hauko katika hali ya kawaida. Hapo zamani, ikiwa Mungu angekuwa Amekuacha kungeweza kuamuliwa na ikiwa ulikuwa na amani ndani yako, na ikiwa uliona furaha. Sasa cha muhimu ni ikiwa una kiu ya maneno ya Mungu, ikiwa maneno Yake ni uhalisi wako, ikiwa wewe ni mwaminifu, na ikiwa unaweza kumfanyia Mungu yote uwezayo. Kwa maneno mengine, mwanadamu anahukumiwa na uhalisi wa maneno ya Mungu. Mungu huelekeza maneno Yake kwa binadamu wote. Ikiwa uko tayari kuyasoma, Atakupa nuru, lakini ikiwa hauko tayari, Hatafanya hivyo. Mungu huwapa nuru wale ambao wana njaa na kiu ya haki, na Huwapa nuru wale wanaomtafuta. Wengine husema kwamba Mungu hakuwapa nuru hata baada ya kusoma maneno Yake. Lakini uliyasoma maneno haya kwa njia gani? Ukiyasoma maneno Yake kama ambavyo mtu asiye ba shauku, na usiweke umuhimu katika uhalisi, Mungu angewezaje kukupa nuru? Mtu ambaye hayathamini maneno ya Mungu anawezaje kufanywa mkamilifu na Yeye? Ikiwa huyathamini maneno ya Mungu, basi hutakuwa na uhalisi wala ukweli. Ikiwa unayathamini maneno Yake, basi utaweza kuuweka ukweli katika vitendo, na ni hapo tu ndipo utakapomiliki uhalisi. Hii ndiyo maana lazima ule na kunywa maneno ya Mungu wakati wote, iwe una shughuli nyingi au la, hali iwe mbaya au la, na iwe unajaribiwa au la. Kwa jumla, maneno ya Mungu ndiyo msingi wa kuwepo kwa mwanadamu. Hakuna anayeweza kuyaepuka maneno Yake, lakini lazima ale maneno Yake kama anavyokula milo mitatu ya siku. Je, kufanywa mkamilifu na kupatwa na Mungu kunaweza kuwa rahisi vile? Ikiwa wewe unaelewa kwa sasa au la, na ikiwa una utambuzi juu ya kazi ya Mungu au la, lazima ule na kunywa maneno mengi ya Mungu iwezekanavyo. Huku ni kuingia kwa njia ya vitendo. Baada ya kusoma maneno ya Mungu, harakisha kutia katika vitendo kile unachoweza kuingia katika, na uweke kando kwa sasa kile ambacho huwezi. Kunaweza kuwa na maneno mengi ya Mungu ambayo huwezi kuelewa mwanzoni, lakini baada ya miezi miwili au mitatu, pengine hata mwaka, utayaelewa. Je, hili linawezekanaje? Ni kwa sababu Mungu hawezi kuwafanya watu wawe wakamilifu kwa siku moja au mbili. Wakati mwingi, unaposoma maneno Yake, huenda usielewe papo hapo. Wakati huo, yanaweza kuonekana kama maandishi tu; lazima uyapitie kwa muda kabla ya kuyaelewa. Mungu akiwa Amezungumza mengi sana, unapaswa kufanya kila uwezalo kula na kunywa maneno Yake, kisha, bila ya wewe kutambua, utakuja kuelewa, na bila wewe kutambua, Roho Mtakatifu atakupa nuru. Roho Mtakatifu anapompa mwanadamu nuru, mara nyingi huwa bila ufahamu wa mwanadamu. Yeye hukupa nuru na kukuongoza unapoona kiu na kutafuta. Kanuni ambayo kwayo Roho Mtakatifu hufanya kazi ina msingi katika maneno ya Mungu ambayo wewe hula na kunywa. Wale wote ambao hawaweki umuhimu katika maneno ya Mungu na daima huwa wenye mtazamo tofauti kwa maneno Yake—wakiamini, katika fikira zao zilizochanganyikiwa, kuwa ni jambo lisilo na athari yoyote wakisoma maneno Yake au la—ni wale ambao hawana uhalisi. Kazi ya Roho Mtakatifu wala utoaji nuru Wake haviwezi kuonekana ndani ya mtu kama huyo. Watu kama hawa wanasairi tu, wanaojifanya na wasio na sifa za kweli, kama Bwana Nanguo wa mfano.[a]

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Enzi ya Ufalme Ni Enzi ya Neno

Tanbihi:

a. Maandishi ya asili hayana maneno “wa mfano.”

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 404)

Maneno ya Mungu yanapotokea, unapaswa kuyapokea mara moja, na kuyala na kuyanywa. Haijalishi wewe unaelewa kiasi gani, mtazamo mmoja ambao lazima ushikilie imara ni kula na kunywa, kujua, na kutebda maneno Yake. Hiki ni kitu ambacho unapaswa kuweza kufanya. Kamwe usijali kuhusu jinsi kimo chako kinavyoweza kuwa kikubwa; lenga tu kula na kunywa maneno Yake. Hiki ndicho mwanadamu anapaswa kushiriki katika. Maisha yako ya kiroho hasa ni kujaribu kuingia katika ukweli wa kula na kunywa maneno ya Mungu na kuyaweka katika vitendo. Sio shughuli yako kulenga juu ya kitu kingine chochote. Viongozi wa kanisa wanapaswa kuwaongoza ndugu zao wote ili wajue jinsi ya kula na kunywa maneno ya Mungu. Hili ndilo jukumu la kila kiongozi wa kanisa. Wawe wachanga au wazee, wote wanapaswa kuzingatia kula na kunywa maneno ya Mungu kama jambo lenye umuhimu mkubwa na wanapaswa kuwa na maneno Yake mioyoni mwao. Kuingia katika ukweli huu kunamaanisha kuingia katika Enzi ya Ufalme. Leo, watu wengi wanahisi kuwa hawawezi kuishi bila kula na kunywa maneno ya Mungu, na wanahisi kuwa maneno Yake ni mapya bila kujali wakati. Hii inamaanisha kuwa wanaanza kwenda katika njia sahihi. Mungu hutumia maneno kufanya kazi Yake na kumruzuku mwanadamu. Wakati kila mtu anatamani na kuwa na kiu ya maneno ya Mungu, binadamu wataingia katika ulimwengu wa maneno Yake.

Mungu amezungumza mengi sana. Je, ni kiasi gani ambacho wewe umepata kujua? Umeingia kwa kiasi gani? Kama kiongozi wa kanisa hajawaongoza ndugu zake kuingia katika ukweli wa maneno ya Mungu, basi atakuwa hajatimiza wajibu wake, na atakuwa ameshindwa kutekeleza majukumu yake! Ufahamu wako uwe wa kina au wa juu juu, bila kujali kiwango cha ufahamu wako, lazima ujue jinsi ya kula na kunywa maneno Yake, lazima uyazingatie kwa makini sana maneno Yake, na uelewe umuhimu na haja ya kuyala na kuyanywa. Kwa kuwa Mungu amezungumza sana, usipokula na kunywa maneno Yake, au kujaribu kutafuta, au kuyaweka maneno Yake katika vitendo, huku hakuwezi kuitwa kumwamini Mungu. Kwa kuwa unamwamini Mungu, basi lazima uyale na kuyanywa maneno Yake, uyapitie maneno Yake, na uishi kwa kuyadhihirisha maneno Yake. Hii tu ndiyo inayoweza kuitwa imani katika Mungu! Ukisema kwa mdomo wako kwamba unamwamini Mungu lakini huwezi kuyaweka maneno Yake yoyote katika vitendo au kutoa ukweli wowote, huku hakuitwi kumwamini Mungu. Badala yake, ni "kutafuta mkate ili kumaliza njaa." Kuzungumza tu kuhusu ushuhuda mdogo, vitu visivyo na maana, na mambo ya juujuu, bila kuwa hata na ukweli mdogo kabisa: hivi havijumuishi imani katika Mungu, na hujafahamu tu njia sahihi ya kuamini katika Mungu. Kwa nini lazima ule na kunywa maneno mengi ya Mungu iwezekanavyo? Usipokula na kunywa maneno Yake lakini utafute tu kupaa mbinguni, je, huko ni kumwamini Mungu? Je, hatua ya kwanza ambayo mtu amwaminiye Mungu anapaswa kuchukua ni ipi? Ni kwa njia gani ndiyo Mungu humkamilisha mwanadamu? Je, unaweza kukamilishwa bila kula na kunywa maneno ya Mungu? Je, unaweza kuchukuliwa kama mtu wa ufalme bila ya maneno ya Mungu kutumika kama ukweli wako? Je, ni nini hasa maana ya imani katika Mungu? Waumini katika Mungu wanapaswa, angalau, kuwa na tabia njema kwa nje; la muhimu zaidi ni kuwa na maneno ya Mungu. Bila kujali chochote, kamwe huwezi kuyaacha maneno Yake. Kumjua Mungu na kutimiza nia Zake vinafanikishwa kupitia katika maneno Yake. Katika siku zijazo, kila taifa, dhehebu, dini, na sehemu zitashindwa kwa njia ya maneno ya Mungu. Mungu atazungumza moja kwa moja, na watu wote watashikilia maneno ya Mungu mikononi mwao, na kwa njia hii, binadamu watakamilishwa. Ndani na nje, maneno ya Mungu yanapenyeza kotekote: Binadamu watazungumza maneno ya Mungu kwa vinywa vyao, watende kulingana na maneno ya Mungu, na kuweka maneno ya Mungu ndani, wakisalia wamelowa na maneno ya Mungu ndani na nje. Hivi ndivyo binadamu watakamilishwa. Wale wanaotimiza nia za Mungu na wanaweza kumshuhudia, hawa ni watu wanaomiliki maneno ya Mungu kama ukweli wao.

Kuingia katika enzi ya Neno—Enzi ya Ufalme wa Milenia—ni kazi ambayo inatimizwa leo. Kuanzia sasa kuendelea, fanya mazoezi ya ushirika kuhusu maneno ya Mungu. Ni kwa njia ya kula na kunywa na pia kupitia maneno ya Mungu ndiyo utaweza kuishi kwa kuyadhihirisha maneno ya Mungu. Lazima uwe na uzoefu wa vitendo ili uwashawishi wengine. Ikiwa huwezi kuishi kwa kuudhihirisha ukweli wa maneno ya Mungu, hakuna atakayeshawishika! Wale wote wanaotumiwa na Mungu wanaweza kuishi kwa kuudhihirisha ukweli wa maneno ya Mungu. Ikiwa huwezi kutoa ukweli huu na kumshuhudia Mungu, hii inaonyesha kwamba Roho Mtakatifu hajafanya kazi ndani yako, na kwamba wewe hujakamilishwa. Huu ndio umuhimu wa maneno ya Mungu. Je, wewe una moyo wenye kiu ya maneno ya Mungu? Wale ambao wana kiu ya maneno ya Mungu wana kiu ya ukweli, na watu tu kama hawa tu ndio ambao hubarikiwa na Mungu. Katika siku zijazo, kuna maneno mengi zaidi ambayo Mungu atanena kwa dini zote na madhehebu yote. Kwanza Ananena na kutamka sauti Yake kati yenu ili Awakamilishe kabla ya kusonga mbele kunena na kutamka sauti Yake kati ya watu wa Mataifa ili Awashinde. Kupitia katika maneno Yake, wote watashawishika kwa dhati na kikamilifu. Kupitia katika maneno ya Mungu na ufunuo Wake, tabia potovu ya mwanadamu inapungua, anapata kuonekana kwa mwanadamu, na tabia yake ya uasi inapungua. Maneno hayo hufanya kazi kwa mwanadamu kwa mamlaka na humshinda mwanadamu katika nuru ya Mungu. Kazi ambayo Mungu hufanya katika enzi ya sasa, na vile vile mabadiliko ya kazi Yake, yote yanaweza kupatikana ndani ya maneno Yake. Usiposoma maneno Yake, hutaelewa chochote. Kupitia kula kwako na kunywa maneno Yake, na kupitia kushiriki katika ushirika na ndugu na uzoefu wako halisi, utapata ufahamu kamili wa maneno ya Mungu. Ni hapo tu ndipo utaweza kweli kuishi kwa kudhihirisha ukweli wake.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Enzi ya Ufalme Ni Enzi ya Neno

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 405)

Nimesema hapo awali kuwa “Wale wote wanaoangazia kuona ishara na maajabu watatelekezwa; wao sio wale watakaofanywa wakamilifu.” Nimenena maneno mengi sana, ilhali mwanadamu hana maarifa hata kidogo ya kazi hii, na, baada ya kufika katika hatua hii, bado mwanadamu anaulizia ishara na maajabu. Je, kuamini kwako kwa Mungu ni harakati ya kuona ishara na maajabu, au ni kwa sababu ya kupata uzima? Yesu pia Alinena maneno mengi, na mengine bado hayajatimika leo. Je unaweza kusema kuwa Yesu sio Mungu? Mungu alishuhudia kuwa Yeye ni Kristo na ni Mwana mpendwa wa Mungu. Je unaweza kukataa haya? Leo, Mungu anazungumza tu maneno, na iwapo huna uwezo wa kufahamu kabisa, basi huwezi kusimama kidete. Je unamwamini kwa sababu Yeye ni Mungu, au unamwamini kwa msingi kwamba maneno Yake yatatimika au la? Je unaamini katika ishara na maajabu, au unaamini katika Mungu? Leo, Haonyeshi ishara na maajabu—je Yeye kweli ni Mungu? Iwapo maneno Anayonena hayatimiki, je Yeye kweli ni Mungu? Je dutu ya Mungu inaamuliwa na iwapo maneno Anenayo yatatimika au hapana? Ni kwa nini watu wengine daima hungoja kutimika kwa maneno ya Mungu kabla ya kumwamini? Je hii si maana kwamba hawamjui? Wote walio na dhana za aina hii ni watu wanaomkana Mungu. Wanatumia dhana kumpima Mungu; maneno ya Mungu yakitimika wanamwamini Mungu, na yasipotimika hawamwamini Mungu; na kila wakati wanatafuta kuona ishara na maajabu. Je wao si Mafarisayo wa wakati wa sasa? Kama unaweza ama huwezi kusimama imara kunategemea iwapo unamjua ama humjui Mungu wa kweli—hili ni muhimu! Jinsi ulivyo ukuu wa uhalisi wa neno la Mungu ndani Yako, ndivyo ulivyo ukubwa wa maarifa yako kuhusu uhakika wa Mungu, na ndivyo utaweza kusimama kidete katika majaribu. Kadri unavyotazamia kuona ishara na maajabu, ndivyo utakavyokosa zaidi kusimama imara, na utaanguka katika majaribu. Ishara na maajabu sio msingi; uhakika wa Mungu tu ndio uzima. Watu wengine hawajui matokeo yanayotokana na kazi ya Mungu. Wanaishi katika mshangao kila siku, wakikosa kutafuta ufahamu wakazi ya Mungu. Harakati zao ni kumfanya Mungu atimize mapenzi yao, na ni baada tu ya haya ndio wawe makini katika imani yao. Wanasema kuwa watautafuta uzima iwapo maneno ya Mungu yatatimika, lakini iwapo maneno ya Mungu hayatatimika, basi hakuna uwezekano wa wao kuutafuta uzima. Mwanadamu anafikiri kuwa imani kwa Mungu ni kutafuta kuona ishara na maajabu na harakati ya kupanda mbinguni na mbingu ya tatu. Hakuna asemaye kuwa imani yake kwa Mungu ni harakati ya kuingia katika ukweli, kutafuta uzima, na kutafuta kupatwa na Mungu. Harakati ya aina hii ina thamani gani? Wale wasiofuata ufahamu wa Mungu na kuridhika kwa Mungu ni watu ambao hawamwamini Mungu, ni watu ambao hukufuru Mungu!

Je sasa mnaelewa imani kwa Mungu ni nini? Je kuamini Mungu ni kuona ishara na maajabu? Je ni kupanda mbinguni? Kuamini Mungu sio rahisi hata kidogo. Zile desturi za kidini lazima zitakaswe; kufuata uponyaji wa wagonjwa na kukemea mapepo, kusisitiza ishara na maajabu, kutamani zaidi neema, amani na furaha ya Mungu, kufuata mandhari na raha za mwili—haya ni matendo ya kidini, na matendo haya ya aina hii ya kidini ni aina ya imani isiyo dhahiri. Leo, imani ya kweli kwa Mungu ni nini? Ni kukubali neno la Mungu kama ukweli wa maisha yako na kumjua Mungu kutoka kwa neno Lake ili uufikie upendo wa kweli Kwake. Kuondoa tashwishi: Imani katika Mungu ni ili uweze kumtii Mungu, kumpenda Mungu, na kufanya majukumu ambayo kiumbe wa Mungu anapaswa kufanya. Hili ndilo lengo la kuamini katika Mungu. Lazima upate ufahamu wa upendo wa Mungu, jinsi Mungu anavyostahili heshima, jinsi, katika viumbe Vyake, Mungu anafanya kazi ya wokovu na kuwafanya wakamilifu—haya ndiyo mahitaji ya chini kabisa ya imani yako katika Mungu. Imani katika Mungu hasa ni mabadiliko kutoka kwa maisha ya mwili kwenda kwa maisha ya kumpenda Mungu; kutoka katika kuishi ndani ya upotovu hadi katika kuishi ndani ya maisha ya maneno ya Mungu; ni kutoka kumilikiwa na Shetani na kuishi chini ya utunzaji na ulinzi wa Mungu, ni kuweza kupata kumtii Mungu na sio kuutii mwili, ni kukubali Mungu kuupata moyo wako wote, kukubali Mungu akufanye mkamilifu, na kujitoa kutoka kwa tabia potovu ya kishetani. Imani kwa Mungu kimsingi ni kwa kuwezesha nguvu na sifa za Mungu kudhihirishwa kwako, ili uweze kufanya mapenzi ya Mungu, na kutimiza mpango wa Mungu, na uweze kutoa ushuhuda kwa Mungu mbele ya Shetani. Imani kwa Mungu haipaswi kuwa kwa ajili ya kuona ishara na maajabu, wala haipaswi kuwa kwa ajili ya mwili wako mwenyewe. Inapaswa kuwa kwa ajili ya kutafuta kumjua Mungu, na kuweza kumtii Mungu, na kama Petro, kumtii mpaka kifo. Hili ndilo imani hiyo inapaswa kupata. Kula na kunywa neno la Mungu ni kwa ajili ya kumjua Mungu na kumtosheleza Mungu. Kula na kunywa neno la Mungu kunakupa maarifa kubwa ya Mungu, na ndipo tu utakapoweza kumtii. Ukiwa na maarifa ya Mungu tu ndipo unapoweza kumpenda, na hili ndilo lengo ambalo mwanadamu anapaswa kuwa nalo katika imani yake kwa Mungu. Iwapo katika imani yako kwa Mungu, unajaribu kila wakati kuona ishara na maajabu, basi mtazamo wa imani hii kwa Mungu si sahihi. Imani kwa Mungu ni hasa kukubali neno la Mungu kama ukweli wa maisha. Ni kuweka tu katika matendo maneno ya Mungu kutoka kwa kinywa Chake na kuyatekeleza mwenyewe ndiko kupatikana kwa lengo la Mungu. Katika kuamini Mungu, mwanadamu anapaswa kutafuta kufanywa mkamilifu na Mungu, kuweza kujiwasilisha kwa Mungu, na kumtii Mungu kikamilifu. Iwapo unaweza kumtii Mungu bila kulalamika, kuyajali mapenzi ya Mungu, kupata kimo cha Petro, na kuwa na mtindo wa Petro ilivyozungumziwa na Mungu, basi hapo ndipo utakuwa umefanikiwa katika imani kwa Mungu, na itadhihirisha kuwa umepatwa na Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu

Iliyotangulia: Kuingia Katika Uzima

Inayofuata: Kuingia Katika Uzima (II)

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp