Kuingia Katika Uzima (II)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 406)

Watu wanaamini katika Mungu, wanampenda Mungu, na kumkidhi Mungu kwa kugusa Roho wa Mungu kwa moyo wao, hivyo kupata ridhaa ya Mungu; na wakati wanajihusisha na maneno ya Mungu kwa moyo wao, kwa hivyo wanasisimuliwa na Roho wa Mungu. Ikiwa unataka kufikia maisha ya kawaida ya kiroho na kuanzisha uhusiano wa kawaida na Mungu, basi lazima kwanza umpe Yeye moyo wako, na kuutuliza moyo wako mbele za Mungu. Ni baada tu ya kuumimina moyo wako mzima kwa Mungu ndipo unaweza kuingia hatua kwa hatua katika maisha ya kiroho yanayostahili. Kama, kwa imani yao katika Mungu, watu hawautoi moyo wao kwa Mungu, ikiwa moyo wao hauko katika Mungu, na wala hawauchukulii mzigo wa Mungu kama wao wenyewe, basi kila kitu wanachofanya ni kumdanganya Mungu, nayo ni matendo ya watu wa kidini, wasioweza kuipokea sifa ya Mungu. Mungu hawezi kupata kitu chochote kutoka kwa aina hii ya mtu; aina hii ya mtu anaweza tu kutumika kama foili[a] kwa kazi ya Mungu, kama pambo katika nyumba ya Mungu, kuchukua nafasi, naye hana manufaa—Mungu hamtumii aina hii ya mtu. Katika mtu kama huyo, sio tu kwamba hakuna nafasi kwa ajili ya kazi ya Roho Mtakatifu, hata zaidi hakuna thamani ya ukamilifu; aina hii ya mtu ni “mfu atembeaye” halisi—hana sehemu ambazo zinaweza kutumika na Roho Mtakatifu—wao wote wametwaliwa na Shetani, kupotoshwa kwa kiwango kilichokithiri na Shetani, ambao ni chombo cha kuondolewa na Mungu. Kwa sasa, katika kuwatumia watu, Roho Mtakatifu hatumii tu hizo sehemu zao zinazopendeza ili kufanikisha mambo, pia Anazikamilisha na kuzibadilish sehemu zao zisizopendeza. Kama moyo wako unaweza kumiminwa ndani ya Mungu, na kukaa kimya mbele za Mungu, basi utakuwa na nafasi na sifa za kuhitimu ili kutumiwa na Roho Mtakatifu, kupokea nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu, na hata zaidi, utakuwa na nafasi kwa Roho Mtakatifu kufidia dosari zako. Unapompa Mungu moyo wako, katika upande chanya, unaweza kupata uingiaji wa kina zaidi na ufikie kiwango cha juu zaidi cha uelewaji; katika upande hasi, utakuwa na uelewa zaidi wa makosa na dosari zako mwenyewe, utakuwa na hamu zaidi ya kutafuta kuyakidhi mapenzi ya Mungu, na hutakuwa katika hali ya kukaa tu, utaingia ndani kwa utendaji. Hii itamaanisha kuwa wewe ni mtu sahihi. Katika kigezo cha kwamba moyo wako uko shwari mbele za Mungu, jambo muhimu kama unapokea sifa kutoka kwa Roho Mtakatifu au la na kama unampendeza Mungu au la ni kama unaweza kuingia ndani kwa utendaji. Wakati Roho Mtakatifu anampa mtu nuru na anamtumia mtu, Hamfanyi hasi kamwe, lakini mara zote Humfanya aendelee kwa utendaji. Hata kama ana udhaifu, anaweza kutoishi kulingana nao, anaweza kuepukana na kuchelewesha kukuza maisha yake, naye kutafuta kuyakidhi mapenzi ya Mungu. Hiki ni kiwango. Ukiweza kufikia hili, ni thibitisho la kutosha kwamba mtu ameupata uwepo wa Roho Mtakatifu. Ikiwa mtu yuko hasi daima, na hata baada ya kupata nuru ili kujijua bado yuko hasi na wa kukaa tu, bila uwezo wa kusimama na kutenda pamoja na Mungu, basi aina hii ya mtu anaipokea tu neema ya Mungu, bali Roho Mtakatifu hayuko naye. Mtu akiwa hasi, hii inamaanisha kuwa moyo wake haujamgeukia Mungu na roho yake haijaguswa na Roho wa Mungu. Hii inapaswa kutambuliwa na wote.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Muhimu Sana Kuanzisha Uhusiano wa Kawaida na Mungu

Tanbihi:

a. “Foili” inahusu mtu au kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 407)

Katika uzoefu wako unaona kuwa moja ya masuala muhimu zaidi ni kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu. Ni suala ambalo linahusu maisha ya kiroho ya watu, na kuendelea kwa maisha yao. Ni kama tu moyo wako uko na amani mbele za Mungu ndio kutafuta kwako ukweli na mabadiliko katika tabia yako kutazaa matunda. Kwa sababu unakuja ukiwa na mizigo mbele za Mungu na huwa unahisi kila mara kuwa unapungukiwa kiasi kikubwa, kwamba kuna ukweli mwingi ambao unahitaji kujua, uhalisi mwingi unaohitaji kupitia, na kwamba unapaswa kujali kikamilifu kuhusu mapenzi ya Mungu—mambo haya kila mara huwa mawazoni mwako, ni kana kwamba yamekufinyia chini sana kiasi kwamba huwezi kupumua, na hivyo unahisi mzito wa moyo (lakini sio kwa hali hasi). Ni watu wa aina hii pekee ndio wanastahili kukubali kupata nuru ya maneno ya Mungu na kuguswa na Roho wa Mungu. Ni kwa sababu ya mzigo wao, kwa sababu ni wenye moyo mzito, na, inaweza kusemwa, kwa sababu ya gharama ambayo wamelipa na mateso ambayo wamepitia mbele ya Mungu ndio wanapata nuru na mwangaza wa Mungu, kwa kuwa Mungu hamtendei yeyote kwa upendeleo. Yeye huwa mwenye haki kila mara katika kuwatendea watu, lakini Yeye sio holela katika kuwakimu watu, na hawapi bila masharti. Huu ni upande mmoja wa tabia Yake yenye haki. Katika maisha halisi, watu wengi bado hawajaufikia ulimwengu wa aina hii. Kwa kiwango cha chini zaidi, mioyo yao bado haijamgeukia Mungu kikamilifu, na hivyo bado hakujakuwa na mabadiliko yoyote makubwa katika tabia ya maisha yao. Hii ni kwa sababu wanaishi tu kati ya neema ya Mungu, na bado hawajapata kazi ya Roho Mtakatifu. Vigezo vya Mungu kuwatumia watu ni kama ifuatavyo: Mioyo yao inamgeukia Mungu, wanasumbuliwa na maneno ya Mungu, wanakuwa na mioyo ya kutamani, na wako na azimio la kutafuta ukweli. Ni watu wa aina hii tu ndio wanaoweza kupata kazi ya Roho Mtakatifu na mara kwa mara wapate nuru na mwangaza. Watu ambao Mungu huwatumia huonekana kwa nje kama watu wasio na akili na kama wasio na uhusiano wa kawaida na wengine, ingawa wao huzungumza na adabu, hawazungumzi kiholela, na wanaweza daima kuwa na moyo uliotulia mbele ya Mungu. Lakini ni mtu wa aina hiyo tu ndiye anatosha kutumiwa na Roho Mtakatifu. Mtu huyu asiye na akili anayezungumziwa na Mungu huonekana kama asiye na uhusiano wa kawaida na wengine, na hana upendo wa kuelekea nje au matendo ya juu juu, lakini anapokuwa akieleza mambo ya kiroho anaweza kufungua roho yake na kwa kujinyima awatolee wengine mwangaza na nuru ambayo amepata kutoka kwa uzoefu wake wa hakika mbele za Mungu. Hivi ndivyo anavyodhihirisha upendo wake kwa Mungu na kuridhisha mapenzi ya Mungu. Wengine wote wanapokuwa wanamkashifu na kumdhihaki, ana uwezo wa kutoelekezwa na watu wa nje, matukio, au vitu, na bado anaweza kutulia mbele za Mungu. Mtu wa aina hii inavyooneka yuko na utambuzi wake mwenyewe wa pekee. Bila kujali wengine, moyo wake kamwe haumwachi Mungu. Wengine wanapokuwa wakizungumza kwa furaha na kwa vichekesho, moyo wake bado unasalia mbele za Mungu, kutafakari neno la Mungu au kusali kwa kimya kwa Mungu aliye moyoni mwake, akitafuta makusudi ya Mungu. Kamwe hawatilii maanani udumishaji wa uhusiano wa kawaida na wengine. Mtu wa aina hii inavyoonekana hana falsafa ya maisha. Kwa nje, mtu huyu ni mchangamfu, anayependwa, asiye na hatia, lakini pia anamiliki hisia ya utulivu. Huu ni mfano wa mtu ambaye Mungu anamtumia. Mambo kama falsafa ya kuishi au “mantiki ya kawaida” hayawezi kufanya kazi kwa mtu wa aina hii; mtu wa aina hii ameutoa moyo wake wote kwa neno la Mungu, ambaye anaonekana kuwa na Mungu tu katika moyo wake. Hii ni aina ya mtu ambaye Mungu anamrejelea kama mtu “bila mantiki,” naye tu ni mtu ambaye anatumiwa na Mungu. Alama ya mtu ambaye anatumiwa na Mungu ni: Haijalishi ni lini au wapi, moyo wake daima uko mbele za Mungu, na haijalishi jinsi gani wengine ni wenye anasa, jinsi gani wanavyoshiriki katika tamaa, wanajiingiza katika anasa za kimwili—moyo wake kamwe haumwachi Mungu, naye hafuatani na umati. Aina hii ya mtu pekee ndiye anafaa kwa ajili ya matumizi ya Mungu, naye hasa ni yule ambaye amekamilika na Roho Mtakatifu. Ikiwa huwezi kufikia hatua hii, basi hustahili kupatwa na Mungu, ili kukamilishwa na Roho Mtakatifu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Muhimu Sana Kuanzisha Uhusiano wa Kawaida na Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 408)

Ikiwa unataka kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu, basi lazima moyo wako umgeukie Mungu. Hili likiwa msingi, pia utakuwa na uhusiano wa kawaida na watu wengine. Iwapo huna uhusiano wa kawaida na Mungu, basi haijalishi unachofanya kudumisha uhusiano wako na watu wengine, haijalishi jinsi gani unafanya kazi kwa bidii au ni nguvu kiasi gani unaweka ndani yake, bado ni ya falsafa ya mwanadamu ya maisha. Unadumisha nafasi yako miongoni mwa watu kupitia mtazamo wa mwanadamu na falsafa ya mwanadamu ili kwamba watu wakupe wewe sifa, lakini hufuati neno la Mungu ili kuanzisha uhusiano wa kawaida na watu. Iwapo huzingatii uhusiano wako na watu lakini unadumisha uhusiano wa kawaida na Mungu, ikiwa uko tayari kumpa Mungu moyo wako na ujifunze kumtii, basi kwa kawaida sana, uhusiano wako na watu wote utakuwa wa kawaida. Kwa njia hii, uhusiano huu haujengwi kwa mwili, bali juu ya msingi wa upendo wa Mungu. Kwa kiasi kikubwa hakuna ushirikiano uliojengwa juu ya mwili, lakini katika roho kuna ushirikiano na vilevile upendo, starehe, na kutoleana kwa wenza. Haya yote yanafanywa kwa msingi wa moyo unaomridhisha Mungu. Uhusiano huu haudumishwi kwa kutegemea falsafa ya mwanadamu ya maisha, bali unaundwa kwa kawaida kupitia mzigo wa Mungu. Hauhitaji jitihada zilizofanywa na binadamu. Unahitaji tu kutenda kulingana na maadili ya neno la Mungu. Je, unayo hiari ya kuwa mwenye kufikiria mapenzi ya Mungu? Je, uko tayari kuwa mtu “bila mantiki” mbele za Mungu? Je, uko tayari kuutoa moyo wako kwa Mungu kabisa, na kutofikiri kuhusu msimamo wako kati ya watu? Kati ya watu wote ambao una mawasiliano nao, ni gani ambao kati yao unayo mahusiano bora zaidi? Wepi kati yao ambao unayo mahusiano mabaya zaidi nao? Je, mahusiano yako na watu ni ya kawaida? Je, unawachukulia watu wote kwa usawa? Je, uhusiano wako na wengine umeimarishwa kwa mujibu wa falsafa yako ya maisha, ama umejengwa kwenye msingi wa upendo wa Mungu? Wakati mtu hautoi moyo wake kwa Mungu, basi roho yake inakuwa butu, inakufa ganzi na kutofahamu. Mtu wa aina hii kamwe hataelewa maneno ya Mungu na kamwe hatakuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu; tabia ya mtu wa aina hiikamwe haitabadilika. Kubadilisha tabia ya mtu ni mchakato wa mtu kuutoa kabisa moyo wake kwa Mungu, na wa kupokea nuru na mwangaza kutoka kwa maneno ya Mungu. Kazi ya Mungu inaweza, kumruhusu mtu kuingia kwa utendaji, na pia kumwezesha kuepuka masuala yake hasi baada ya kupata maarifa. Unapoweza kuutoa moyo wako kwa Mungu, utaweza kuhisi kila harakati yenye hila ndani ya roho yako, nawe utajua kila nuru na mwangaza upokelewao kutoka kwa Mungu. Shikilia hili, nawe utaingia katika njia ya kukamilishwa na Roho Mtakatifu hatua kwa hatua. Kadri moyo wako unavyoweza kuwa mtulivu mbele za Mungu, ndivyo roho yako itakavyokuwa makini zaidi na wa kutaka uangalifu mkubwa, na kadri roho yako itakavyoweza kutambua kuchochewa na Roho Mtakatifu, kisha uhusiano wako na Mungu utakuwa wa kawaida zaidi na zaidi. Uhusiano wa kawaida kati ya watu huundwa juu ya msingi wa kumpa Mungu mioyo yao haufanikishwi kupitia jitihada za binadamu. Bila Mungu mioyoni mwao, uhusiano kati ya watu ni uhusiano wa mwili tu. Sio uhusiano wa kawaida, lakini badala yake, ni utelekezaji kwa ajili ya tamaa za mwili. Ni uhusiano ambao Mungu anachukia, Asioupenda. Ukisema kuwa roho yako imeguzwa, lakini daima unataka kuwa na ushirika na watu wanaokupendeza, na wale unaowachukulia kwa hali ya juu, na iwapo kuna mtafutaji mwingine ambaye hakupendezi, ambaye huna upendeleo kwake na huwezi kujihusisha naye, huu ni ushahidi zaidi kuwa wewe uko chini ya hisia zako na kuwa huna uhusiano wa kawaida na Mungu kamwe. Unajaribu kumdanganya Mungu na kuficha ubaya wako mwenyewe. Hata ingawa unaweza kushirikisha uelewano kiasi lakini unabeba ubaya moyoni mwako, kila kitu unachofanya ni kizuri tu kwa kiwango cha mwanadamu. Mungu hatakusifu—unatenda kulingana na mwili, sio kulingana na mzigo wa Mungu. Iwapo unaweza kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu na kuwa na ushirikiano wa kawaida na wale wote wanaompenda Mungu, ni hapo tu ndipo utakuwa uko tayari kwa matumizi ya Mungu. Kwa njia hii, haijalishi jinsi unavyopatana na wengine, haitakuwa kulingana na falsafa ya maisha, lakini itakuwa kuishi mbele ya Mungu, kuufikiria mzigo Wake. Je, ni watu wangapi wa aina hii wapo miongoni mwenu? Je, mahusiano yako na watu wengine ni ya kawaida kweli? Yamejengwa katika msingi upi? Je, ni falsafa ngapi za maisha zimo ndani mwako? Je, zimetupiliwa mbali? Ikiwa moyo wako hauwezi kumgeukia Mungu kabisa, basi wewe si wa Mungu—unatoka kwa Shetani, na mwishowe utarudishwa kwa Shetani. Wewe hustahili kuwa mmoja wa watu wa Mungu. Yote haya yanahitaji kufikiria kwako kwa makini.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Muhimu Sana Kuanzisha Uhusiano wa Kawaida na Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 409)

Katika kumwamini Mungu, angalau lazima utatue suala la kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu. Ikiwa huna uhusiano wa kawaida na Mungu, basi maana ya imani yako katika Mungu imepotea. Kuanzishwa kwa uhusiano wa kawaida na Mungu kunaweza kufikiwa kabisa kwa moyo ulio kimya katika uwepo wa Mungu. Kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu kunamaanisha kuweza kutokuwa na shaka na kutoikana kazi yoyote Yake na kuweza kuitii kazi Yake. Kunamaanisha kuwa na nia zisizo na makosa katika uwepo wa Mungu, kutofanya mipango kwa ajili yako mwenyewe, na kuzingatia masilahi ya familia ya Mungu kwanza katika mambo yote; kunamaanisha kukubali uchunguzi wa Mungu na kuitii mipango ya Mungu. Lazima uweze kuutuliza moyo wako katika uwepo wa Mungu katika yote ufanyayo. Hata kama huyaelewi mapenzi ya Mungu, bado unapaswa kutekeleza wajibu na majukumu yako kadiri uwezavyo. Mara tu mapenzi ya Mungu yanapofichuliwa kwako, lichukulie hatua, na hutakuwa umechelewa mno. Wakati ambapo uhusiano wako na Mungu umekuwa wa kawaida, basi pia utakuwa na uhusiano wa kawaida na watu. Kila kitu kimejengwa kwa msingi wa maneno ya Mungu. Kula na unywe maneno ya Mungu, kisha uyatie matakwa ya Mungu katika vitendo, rekebisha maoni yako, na uepuke kufanya chochote ili kumpinga Mungu au kulivuruga kanisa. Usifanye chochote ambacho hakifaidi maisha ya ndugu zako, usiseme chochote kisichowasidia wengine, na usifanye jambo lolote la aibu. Kuwa mwenye haki na mwenye heshima katika jambo unalotenda na uhakikishe kuwa kila kitendo chako kinapendeza mbele za Mungu. Ingawa wakati mwingine mwili unaweza kuwa dhaifu, lazima uweze kuweka masilahi ya familia ya Mungu kwanza, bila tamaa ya kupata faida ya kibinafsi, na lazima uweze kutenda kwa haki. Ikiwa unaweza kutenda kwa namna hii, basi uhusiano wako na Mungu utakuwa wa kawaida.

Katika kila jambo unalofanya, sharti uchunguze ikiwa nia zako hazina makosa. Ikiwa unaweza kutenda kulingana na matakwa ya Mungu, basi uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida. Hiki ndicho kiwango cha chini kabisa. Chunguza nia zako, na ukiona kwamba nia mbaya zimejitokeza, uweze kuziacha na kutenda kulingana na maneno ya Mungu; hivyo utakuwa mtu aliye sawa mbele za Mungu, ambayo inaonyesha kwamba uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida, na kwamba yote unayoyafanya ni kwa ajili ya Mungu, si kwa ajili yako. Katika yote unayofanya na yote unayosema, uweze kuuweka moyo wako uwe sawa na uwe mwenye haki katika matendo yako, na usiongozwe na hisia zako, wala kutenda kulingana na mapenzi yako mwenyewe. Hizi ni kanuni ambazowaumini katika Mungu wanapaswa kutenda. Mambo madogo yanaweza kufichua nia na kimo cha mtu, na kwa hivyo, ili mtu aweze kuingia kwenye njia ya kukamilishwa na Mungu, lazima kwanza arekebishe nia zake na uhusiano wake na Mungu. Ni wakati tu uhusiano wako na Mungu unapokuwa wa kawaida ndipo unaweza kukamilishwa na Yeye; ni wakati huo tu ndipo ushughulikiaji, upogoaji, ufundishaji nidhamu, na usafishaji wa Mungu vifanikisha athari zake zilizokusudiwa ndani yako. Hiyo ni kusema, ikiwa wanadamu wanaweza kumweka Mungu mioyoni mwao na wasifuatilie faida ya kibinafsi au kufikiria matarajio yao wenyewe (kwa njia ya mwili), lakini badala yake wabebe mzigo wa kuingia katika uzima, wajitahidi kabisa kuufuatilia ukweli, na kuitii kazi ya Mungu—ikiwa unaweza kufanya hivi, basi malengo unayoyafuatilia yatakuwa sawa, na uhusiano wako na Mungu utakuwa wa kawaida. Kuufanya uhusiano wa mtu na Mungu uwe muwafaka kunaweza kuitwa hatua ya kwanza ya kuingia katika safari ya kiroho ya mtu. Ingawa hatima ya mwanadamu iko mikononi mwa Mungu na imeamuliwa kabla na Mungu, na haiwezi kubadilishwa na mwanadamu, kama unaweza kukamilishwa na Mungu au kupatwa na Yeye kunategemea ikiwa uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida. Kunaweza kuwa na sehemu fulani ndani yako ambazo ni dhaifu au zisizotii—lakini mradi maoni yako na nia zako ni sawa, na mradi uhusiano wako na Mungu uko sawa na wa kawaida, basi unastahili kukamilishwa na Mungu. Ikiwa huna uhusiano muwafaka na Mungu, na unatenda kwa ajili ya mwili au familia yako, basi bila kujali jinsi unavyotia bidii, itakuwa bure. Ikiwa uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida, basi kila kitu kingine kitakuwa sawa. Mungu haangalii kitu kingine chochote, lakini tu ikiwa maoni yako katika imani yako katika Mungu yako sawa: unamwamini nani, unaamini kwa ajili ya nani, na kwa nini unaamini. Ikiwa unaweza kuona mambo haya waziwazi na kutenda wakati maoni yako yakiwa na mwelekeo mzuri, basi utaendelea katika maisha yako, na pia utahakikishiwa kuingia kwenye njia muwafaka. Ikiwa uhusiano wako na Mungu si wa kawaida, na maoni ya imani yako katika Mungu yamepotoka, basi mengine yote ni bure, na haijalishi kadiri unavyoamini, hutapokea chochote. Ni baada tu ya uhusiano wako na Mungu kuwa wa kawaida ndipo utakapopata sifa kutoka Kwake unapoukana mwili, uombe, uteseke, uvumilie, utii, uwasaidie ndugu zako, ujitumie zaidi kwa ajili ya Mungu, na kadhalika. Kama kile unachofanya kina thamani na umuhimu inategemea ikiwa nia zako ni sawa na maoni yako hazina makosa. Siku hizi, watu wengi wanamwamini Mungu kana kwamba wanageuza vichwa vyao ili kutazama saa—mitazamo yao imepotoka, na lazima irekebishwe kwa mafanikio mapya. Ikiwa shida hii itatatuliwa, kila kitu kitakuwa sawa; la sivyo, kila kitu kitakuwa bure. Watu wengine ni wenye tabia nzuri mbele Zangu, lakini bila Mimi kujua, wananipinga tu. Hili ni onyesho la upotovu na udanganyifu, na mtu wa aina hii ni mtumishi wa Shetani; yeye ni mfano halisi wa Shetani, aliyekuja kumjaribu Mungu. Wewe ni mtu sahihi tu ikiwa unaweza kuitii kazi Yangu na maneno Yangu. Mradi unaweza kula na kunywa maneno ya Mungu; mradi kila kitu unachofanya kinapendeza mbele za Mungu na unaenenda kwa njia ya haki na kwa heshima katika yote unayofanya; mradi hufanyi mambo ya aibu, au mambo ambayo yanaweza kuyadhuru maisha ya wengine; na mradi unaishi katika nuru na hujiruhusu kudhulumiwa na Shetani, basi uhusiano wako na Mungu uko katika mpangilio unaofaa.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Uhusiano Wako Na Mungu Ukoje?

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 410)

Kumwamini Mungu kunakuhitaji uweke nia na maoni yako katika mpangilio unaofaa; unapaswa kuwa na ufahamu muwafaka wa, na njia muwafaka ya kuyachukulia maneno ya Mungu na kazi ya Mungu, mazingira yote ambayo Mungu hupanga, mtu ambaye Mungu humshuhudia, na Mungu wa vitendo. Hupaswi kutenda kulingana na dhana zako mwenyewe au kubuni miradi yako mwenyewe iliyo midogomidogo. Chochote unachofanya, sharti uweze kuutafuta ukweli na, katika nafasi yako kama kiumbe aliyeumbwa, uitii kazi yote ya Mungu. Ikiwa unataka kufuatilia kukamilishwa na Mungu na kuingia kwenye njia muwafaka ya maisha, basi lazima moyo wako uishi katika uwepo wa Mungu daima. Usiwe mwovu, usimfuate Shetani, usimpe Shetani fursa zozote za kutekeleza kazi yake, na usimruhusu Shetani akutumie. Lazima ujitolee kwa Mungu kabisa na umruhusu Mungu akutawale.

Je, uko tayari kuwa mtumishi wa Shetani? Uko tayari kutumiwa vibaya na Shetani? Unamwamini Mungu na kumfuatilia ili uweze kukamilishwa na Yeye, au ili uweze kuwa foili[a] kwa ajili ya kazi Mungu? Ungependa maisha yenye kusudi ambayo unapatwa na Mungu, au maisha yasiyofaa na matupu? Ungependa kutumiwa na Mungu, au kudhulumiwa na Shetani? Ungependa kuruhusu maneno na ukweli wa Mungu vikujaze, au uruhusu kujazwa na dhambi na Shetani? Zingatia mambo haya kwa uangalifu. Katika maisha yako ya kila siku, lazima uelewe ni maneno gani unayoyasema na ni mambo gani unayoyafanya ndiyo yanaweza kusababisha hitilafu katika uhusiano wako na Mungu, na kisha ujibadilishe ili uingie katika njia muwafaka. Wakati wote, yachunguze maneno yako, matendo yako, kila harakati yako, na mawazo na maoni yako yote. Pata ufahamu muwafaka kuhusu hali yako halisi na uingie katika njia ya kazi ya Roho Mtakatifu. Hii ndiyo njia ya pekee ya kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu. Kwa kutathmini kama uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida, utaweza kurekebisha nia zako, kuelewa asili na kiini cha mwanadamu, na kujielewa kwa kweli, na kwa kufanya hivyo, utaweza kuingia katika matukio halisi, ujikane kwa njia halisi, na kutii kwa kusudi. Unapopitia mambo haya kuhusu ikiwa uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida au la, utapata fursa za kukamilishwa na Mungu na kuweza kufahamu hali nyingi za kazi ya Roho Mtakatifu. Pia utaweza kubaini hila nyingi za Shetani na kufahamu njama zake. Njia hii tu ndiyo inayosababisha kukamilishwa na Mungu. Rekebisha uhusiano wako na Mungu, ili uweze kutii mpangilio Wake kwa ukamilifu, na ili uweze kuingia kwa undani hata zaidi katika matukio halisi na kupokea kazi zaidi ya Roho Mtakatifu. Ukijizoeza kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu, mara nyingi, mafanikio yatapatikana kwa kuukana mwili na kupitia kwa ushirikiano wa kweli na Mungu. Unapaswa kuelewa kwamba “bila moyo wa kushirikiana, ni vigumu kuipokea kazi ya Mungu; ikiwa mwili hautateseka, hakutakuwa na baraka kutoka kwa Mungu; ikiwa roho haijitahidi sana, Shetani hataaibishwa.” Ukifuata kanuni hizi na uzielewe kabisa, maoni ya imani yako katika Mungu yatarekebishwa. Katika kutenda kwako kwa sasa, lazima uache fikira ya “kutafuta mkate ili kukidhi njaa”; lazima uache fikira ya “kila kitu kinafanywa na Roho Mtakatifu, na watu hawawezi kuingilia kati.” Kila mtu asemaye hivyo hufikiria, “Watu wanaweza kufanya chochote watakacho, na wakati ufikapo, Roho Mtakatifu atafanya kazi Yake. Watu hawana haja ya kuuzuia mwili au kushirikiana; jambo la maana ni kwamba waguswe na Roho Mtakatifu.” Maoni haya yote ni ya kipumbavu. Katika hali kama hizo, Roho Mtakatifu hawezi kufanya kazi. Ni mtazamo wa aina hii ndio unaoizuia sana kazi ya Roho Mtakatifu. Mara nyingi, kazi ya Roho Mtakatifu hufikiwa kupitia ushirikiano wa binadamu. Wale ambao hawashirikiani na hawajaamua, ilhali wanataka kupata mabadiliko katika tabia yao na kuipokea kazi ya Roho Mtakatifu na nuru na mwangaza kutoka kwa Mungu, wana mawazo ya kupita kiasi kweli. Hii inaitwa “kujifurahisha na kumsamehe Shetani.” Watu kama hao hawana uhusiano wa kawaida na Mungu. Unapaswa kuona ufunuo na udhihirisho mwingi wa tabia ya kishetani ndani yako mwenyewe na uone mazoea yoyote ambayo unayo yaliyo kinyume na kile ambacho Mungu anahitaji sasa. Je, sasa utaweza kumkana Shetani? Unapaswa kufikia uhusiano wa kawaida na Mungu, kutenda kulingana na nia ya Mungu, na kuwa mtu mpya aliye na maisha mpya. Usifikiri sana kuhusu makosa ya zamani; usiwe mwenye kujuta mno; uweze kusimama na kushirikiana na Mungu, na utimize wajibu unaopaswa kutimiza. Kwa njia hii, uhusiano wako na Mungu utakuwa wa kawaida.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Uhusiano Wako Na Mungu Ukoje?

Tanbihi:

a. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 411)

Ikiwa baada ya kusoma makala haya, unadai tu kukubali maneno haya, ilhali moyo wako hauguswi, na hutafuti kufanya uhusiano wako na Mungu uwe wa kawaida, inathibitisha kwamba hutilii maanani uhusiano wako na Mungu. Inathibitisha kwamba maoni yako bado hayajarekebishwa, kwamba nia zako bado hazijadhamiria kupatwa na Mungu na kumletea Yeye utukufu, lakini badala yake zimedhamiria kuruhusu njama za Shetani zitawale na kufanikisha malengo yako mwenyewe. Watu kama hao wanahodhi nia mbaya na maoni yaliyo na makosa. Haijalishi lile analosema Mungu au jinsi Anavyolisema, watu kama hao hubaki wasiojali kabisa na hawabadiliki hata kidogo. Mioyo yao haihisi woga na wao hawaoni haya. Mtu kama huyo ni mjinga aliyekata tamaa. Soma matamko yote ya Mungu na uyatie katika vitendo mara tu utakapoyaelewa. Labda kulikuwa na nyakati ambapo mwili wako ulikuwa dhaifu, au ulikuwa mwasi, au ulipinga; bila kujali jinsi ulivyotenda zamani, si muhimu, na haiwezi kuyazuia maisha yako kukomaa leo. Mradi unao uhusiano wa kawaida na Mungu leo, kuna matumaini. Ikiwa kuna mabadiliko ndani yako kila wakati unapoyasoma maneno ya Mungu, na wengine wanaweza kukuambia kuwa maisha yako yamebadilika na kuwa bora, inaonyesha kuwa uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida sasa, kwamba umerekebishwa. Mungu hawatendei watu kulingana na makosa yao. Mara tu unapoelewa na kufahamu, mradi unaweza kuacha kuasi au kupinga, basi bado Mungu atakuonea huruma. Unapokuwa na ufahamu na azimio la kufuatilia kukamilishwa na Mungu, basi hali yako katika uwepo wa Mungu itakuwa ya kawaida. Haijalishi unachofanya, fikiria yafuatayo wakati unapofanya jambo hilo: Je, Mungu atafikiria nini nikifanya hili? Litawafaidi ndugu zangu? Litaifaidi kazi katika nyumba ya Mungu? Iwe ni katika sala, ushirika, hotuba, kazi, au kuwasiliana na wengine, zichunguze nia zako, na uchunguze ikiwa uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida. Ikiwa huwezi kutambua nia na mawazo yako mwenyewe, hii inamaanisha kuwa huna upambanuzi, ambayo inathibitisha kwamba unaelewa ukweli kidogo sana. Ikiwa unaweza kuelewa vizuri kila kitu ambacho Mungu hufanya, na unaweza kuyatazama mambo kupitia katika maneno Yake, ukisimama upande Wake, basi maoni yako yatakuwa yamekuwa yasiyo na makosa. Kwa hivyo, kuanzisha uhusiano mzuri na Mungu ni muhimu sana kwa mtu yeyote anayemwamini Mungu; kila mtu anapaswa kuliona kama kazi muhimu sana na tukio kubwa kabisa katika maisha yake. Kila kitu unachofanya kinapimwa na kama una uhusiano wa kawaida na Mungu. Ikiwa uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida na nia zako ni zisizo na makosa, basi chukua hatua. Ili kudumisha uhusiano wa kawaida na Mungu, hupaswi kuogopa kupata hasara kwa masilahi yako ya kibinafsi; huwezi kumruhusu Shetani atawale, huwezi kumruhusu Shetani akununue, na huwezi kumruhusu Shetani akufanye uwe kichekesho. Kuwa na nia kama hiyo ni ishara kwamba uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida—si kwa ajili ya mwili, bali ni kwa ajili ya amani ya roho, kwa ajili ya kuipata kazi ya Roho Mtakatifu, na kwa ajili ya kuyaridhisha mapenzi ya Mungu. Ili kuingia katika hali inayofaa, lazima uimarishe uhusiano mzuri na Mungu na urekebishe maoni ya imani yako katika Mungu. Hii ni ili Mungu aweze kukupata, na ili Aweze kudhihirisha matunda ya maneno Yake ndani yako na kukupa nuru na kukuangazia hata zaidi. Kwa njia hii, utakuwa umeingia katika njia inayofaa. Endelea kula na kunywa maneno ya Mungu ya leo, ingia katika njia ya sasa ya Roho Mtakatifu ya kufanya kazi, tenda kulingana na matakwa ya Mungu ya leo, usifuate mbinu za zamani za kutenda, usishikilie njia za zamani za kufanya mambo, na uingie katika njia ya leo ya kufanya kazi haraka iwezekanavyo. Hivyo, uhusiano wako na Mungu utakuwa wa kawaida kabisa na utakuwa umeanza kutembea katika njia muwafaka ya imani katika Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Uhusiano Wako Na Mungu Ukoje?

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 412)

Kadiri watu wanavyokubali maneno ya Mungu zaidi, ndivyo wanavyopata nuru zaidi, na ndivyo wanavyokuwa na njaa na kiu zaidi katika kufuatilia kwao kumjua Mungu. Ni wale tu wanaoyakubali maneno ya Mungu ndio wanaoweza kuwa na uzoefu mkuu na wa kina zaidi, na wao pekee ndio ambao maisha yao yanaweza kuendelea kukua kama maua ya ufuta. Wote wanaofuatilia maisha wanapaswa kuchukulia hili kama kazi yao ya wakati wote; wanapaswa kuhisi kwamba “bila Mungu, siwezi kuishi; bila Mungu, siwezi kutimiza chochote; bila Mungu, kila kitu ni tupu.” Vile vile pia, wanapaswa kuwa na azimio kwamba “bila uwepo wa Roho Mtakatifu, sitafanya chochote, na ikiwa kuyasoma maneno ya Mungu hakuna matokeo basi sijali kufanya chochote.” Msijifurahishe. Uzoefu wa maisha hutoka kwa nuru na mwongozo wa Mungu, na ndilo dhihirisho la juhudi zenu za nafsi. Mnachopaswa kuhitaji kutoka wenyewe kufanya ni: “Inapokuja kwa suala la uzoefu wa maisha, siwezi kujipa uhuru wa kufanya nipendavyo.”

Wakati mwingine, unapokuwa katika hali zisizo zakawaida, unapoteza uwepo wa Mungu, na unashindwa kumhisi Mungu unapoomba. Ni kawaida kuhisi hofu nyakati kama hizo. Unapaswa kuanza kutafuta mara moja. Usipofanya hivyo, Mungu atakuwa mbali zaidi na wewe, na utakuwa bila uwepo wa Roho Mtakatifu—na zaidi ya hayo, utakuwa bila kazi ya Roho Mtakatifu kwa siku moja, siku mbili, hata mwezi mmoja au miezi miwili. Katika hali hizi, unakuwa mtu asiye na hisia hata kidogo na kwa mara nyingine unachukuliwa mateka na Shetani, hadi kwa kiwango ambapo unaweza kufanya vitendo vya kila aina. Unatamani utajiri, unawadanganya ndugu zako, unatazama filamu na video, unacheza mahjong, na hata kuvuta sigara na kunywa pombe bila nidhamu. Moyo wako umepotoka mbali kutoka kwa Mungu, umeenda katika njia yako mwenyewe kwa siri, na umeihukumu kazi ya Mungu kiholela. Katika visa vingine, watu hupotoka sana kiasi kwamba hawahisi haya au aibu katika kufanya dhambi za kingono. Mtu wa aina hii ametelekezwa na Roho Mtakatifu; kwa kweli, kazi ya Roho Mtakatifu haijakuwa kwa mtu kama huyo kwa muda mrefu. Mtu anaweza tu kumwona akizama zaidi katika upotovu huku mikono ya uovu ikizidi kunyooka. Mwishowe, anakana uwepo wa njia hii, na anachukuliwa mateka na Shetani anapotenda dhambi. Ukigundua kuwa una uwepo wa Roho Mtakatifu tu, lakini huna kazi ya Roho Mtakatifu, tayari hiyo ni hali hatari kuwa ndani. Wakati huwezi hata kuhisi uwepo wa Roho Mtakatifu, basi uko karibu kufa. Usipotubu, basi utakuwa umemrudia Shetani kabisa, na utakuwa miongoni mwa wale wanaoondolewa. Kwa hivyo, unapogundua kuwa uko katika hali ambayo kuna uwepo wa Roho Mtakatifu tu (hutendi dhambi, unajizuia, na hufanyi chochote kinachompinga Mungu waziwazi) lakini unakosa kazi ya Roho Mtakatifu (huhisi kuguswa unapoomba, hupati nuru au mwangaza wa wazi unapokula na kunywa maneno ya Mungu, hujali kuhusu kula na kunywa maneno ya Mungu, hakuna ukuaji wowote katika maisha yako kamwe, na umeondolewa mwanga mkuu kwa muda mrefu sasa)—katika nyakati kama hizi, lazima uwe mwangalifu zaidi. Lazima usijifurahishe, lazima usiipe tabia yako uhuru zaidi. Uwepo wa Roho Mtakatifu unaweza kutoweka wakati wowote. Hii ndiyo maana hali kama hii ni hatari sana. Ukijipata katika hali ya aina hii, jaribu kuyabadilisha mambo haraka iwezekanavyo. Kwanza, unapaswa kusema sala ya toba na uombe kwamba Mungu akupe huruma Yake kwa mara nyingine tena. Omba kwa bidii zaidi na uutulize moyo wako ili ule na kunywa maneno zaidi ya Mungu. Ukiwa na msingi huu, lazima utumie wakati zaidi katika maombi; uongeze bidii yako mara dufu katika kuimba, kusali, kula na kunywa maneno ya Mungu, na kutekeleza wajibu wako. Unapokuwa dhaifu kabisa, moyo wako unamilikiwa na Shetani kwa urahisi kabisa. Hilo linapofanyika, moyo wako unachukuliwa kutoka kwa Mungu na kurudishwa kwa Shetani, na punde baada ya hapo unakuwa bila uwepo wa Roho Mtakatifu. Katika nyakati kama hizi, inakuwa vigumu mara dufu kupata tena kazi ya Roho Mtakatifu. Ni bora kutafuta kazi ya Roho Mtakatifu wakati bado Yeye yuko pamoja nawe, jambo ambalo litamruhusu Mungu kukupa nuru Yake zaidi na kutomfanya Akuache. Kuomba, kuimba nyimbo, kufanya shughuli yako, na kula na kunywa maneno ya Mungu—yote haya yanafanywa ili Shetani asiwe na fursa ya kufanya kazi yake, na ili kwamba Roho Mtakatifu aweze kufanya kazi ndani yako. Usipoipata tena kazi ya Roho Mtakatifu kwa njia hii, ukingojea tu, basi kuipata tena kazi ya Roho Mtakatifu haitakuwa rahisi wakati ambapo umepoteza uwepo wa Roho Mtakatifu, isipokuwa kama Roho Mtakatifu amekugusa wewe hasa, au Amekupa nuru na kukuangazia hasa. Hata hivyo, haichukui siku moja au mbili tu kwa hali yako kurejea; wakati mwingine hata miezi sita inaweza kupita bila urejesho wowote. Hii yote ni kwa sababu watu huwa wazembe sana, hawawezi kupitia vitu kwa njia ya kawaida na hivyo wanaachwa na Roho Mtakatifu. Hata ukipata tena kazi ya Roho Mtakatifu, kazi ya sasa ya Mungu bado inaweza kukosa kuwa wazi kabisa kwako, kwa kuwa umesalia nyuma sana katika uzoefu wako wa maisha, kana kwamba umeachwa maili elfu kumi nyuma. Je, hili si jambo baya sana? Hata hivyo, nawaambia watu kama hao kwamba hawajachelewa sana kutubu sasa, lakini kwamba kuna sharti moja: Lazima ufanye kazi kwa bidii zaidi, na usijiingize katika uvivu. Ikiwa watu wengine wanaomba mara tano kwa siku moja, wewe lazima uombe mara kumi; ikiwa watu wengine wanakula na kunywa maneno ya Mungu kwa saa mbili kwa siku, wewe lazima ufanye hivyo kwa saa nne au sita; na ikiwa watu wengine wanasikiliza nyimbo kwa saa mbili, lazima wewe usikilize kwa angalau siku nusu. Kuwa na amani mara kwa mara mbele za Mungu na ufikirie kuhusu upendo wa Mungu hadi uguswe, moyo wako umrudie Mungu, na usithubutu kupotoka kutoka kwa Mungu—ni hapo tu ndipo matendo yako yatazaa matunda; ni hapo tu ndipo utaweza kurejesha hali yako ya kawaida ya zamani.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jinsi ya Kuingia Katika Hali ya Kawaida

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 413)

Mmetembea tu sehemu ndogo sana ya njia ya muumini katika Mungu, na bado hamjaingia kwenye njia sahihi, kwa hiyo bado mko mbali na kutimiza kiwango cha Mungu. Hivi sasa, kimo chenu hakitoshi kuyakidhi mahitaji Yake. Kwa sababu ya ubora wenu wa tabia na vilevile asili yenu ya maumbile ya upotovu, nyinyi daima huichukulia kazi ya Mungu kwa uzembe na hamuichukulii kwa uzito. Hii ni dosari yenu kubwa zaidi. Zaidi ya hayo, hamwezi kuipata njia ya Roho Mtakatifu. Wengi wenu hamuifahamu na hamwezi kuiona kwa dhahiri. Zaidi ya hayo, wengi wenu hamtilii maanani suala hili, na hata hamlichukulii kwa uzito. Mkiendelea kufanya hivi na msipoijua kazi ya Roho Mtakatifu, basi njia ambayo mnaichukua kama muumini katika Mungu itakuwa bure. Hii ni kwa sababu hamfanyi kila liwezekanalo ili kutafuta kutimiza mapenzi ya Mungu, na pia kwa sababu hamshirikiani vizuri na Mungu. Sio kwamba Mungu hajawafanyia kazi, au kwamba Roho Mtakatifu hajawasisimua. Ni kuwa nyinyi ni wazembe sana kiasi kwamba hamuichukulii kazi ya Roho Mtakatifu kwa uzito. Lazima mbadilike mara moja na kutembea njia inayoongozwa na Roho Mtakatifu. Hii ndiyo mada kuu ya leo. “Njia hii inayoongozwa na Roho Mtakatifu” ni ili watu wapate nuru katika roho zao, wawe na ufahamu wa neno la Mungu, wapate ufahamu kuhusu njia iliyo mbele yao, na waweze kuingia katika ukweli hatua kwa hatua, na kuja kumwelewa Mungu zaidi na zaidi. Njia inayoongozwa na Roho Mtakatifu hasa ni kwamba watu wawe na ufahamu zaidi wa neno la Mungu, bila mikengeuko na kuelewa kubaya, ili waweze kutembea ndani yake. Ili kutimiza athari hii, mtahitaji kufanya kazi kwa upatanifu na Mungu, kutafuta njia sahihi ya kutia katika vitendo, na kutembea katika njia inayoongozwa na Roho Mtakatifu. Hii inahusu ushirikiano kwa upande wa mwanadamu, yaani, mnachofanya kutimiza mahitaji ya Mungu kwenu, na jinsi mnavyotenda ili kuingia katika njia sahihi ya imani katika Mungu.

Inaonekana kuwa changamano sana kutembea kwenye njia inayoongozwa na Roho Mtakatifu, lakini utatambua kuwa mchakato huu ni rahisi zaidi ikiwa njia ya kutenda ni dhahiri kabisa kwako. Ukweli ni kwamba watu wana uwezo wa yote ambayo Mungu anahitaji kutoka kwao—Yeye hajaribu kumfunza nguruwe kuimba. Katika hali zote, Mungu hutafuta kutatua matatizo ya watu na kusuluhisha mahangaiko yao. Nyinyi nyote lazima muelewe hili; msimuelewe Mungu vibaya. Njia ya Roho Mtakatifu ni kulitumia neno la Mungu kuwaongoza watu. Kama ilivyotajwa hapo awali, lazima mpeane mioyo yenu kwa Mungu. Hili ni sharti la kutembea kwenye njia inayoongozwa na Roho Mtakatifu. Lazima mfanye hili ili muingie kwenye njia sahihi. Mtu anawezaje kumpa Mungu moyo wake kwa kusudi? Mnapopitia kazi ya Mungu na kumwomba katika maisha yenu ya kila siku, ninyi hufanya hivyo kwa uzembe—ninyi humwomba Mungu huku mkifanya kazi. Je, huku kunaweza kuitwa kumpa Mungu mioyo yenu? Mnafikiria kuhusu mambo ya nyumbani au shughuli za mwili; ninyi daima mna nia mbili. Je, hili linaweza kufikiriwa ni kuituliza mioyo yenu mbele za Mungu? Hii ni kwa sababu moyo wako daima umetawaliwa na tamaa ya mambo ya nje, na hauwezi kumgeukia Mungu. Ikiwa mnataka kweli kuifanya mioyo yenu kuwa na amani mbele za Mungu, lazima mfanye kazi ya ushirikiano kwa makusudi. Hiyo ni kusema, kila mmoja wenu lazima achukue muda kuwa mbali na kila mtu, jambo, na chombo kwa ajili ya ibada zenu binafsi za kiroho, ambapo mtaweza kuleta amani kwa mioyo yenu na kujituliza mbele za Mungu. Mnapaswa kuwa na muhtasari wenu binafsi wa ibada ambapo mnaweza kurekodi ufahamu wenu wa neno la Mungu na jinsi roho zenu zimesisimuliwa, haijalishi kama mnachoandika ni cha kina au ni cha juujuu. Tulizeni mioyo yenu mbele za Mungu kwa kusudi. Ikiwa unaweza kutoa saa moja au mbili kwa maisha ya kiroho ya kweli wakati wa mchana, basi maisha yako siku hiyo yatahisi kusitawishwa na moyo wako utakuwa mchangamfu na bila hatia. Ikiwa unaishi maisha haya ya kiroho kila siku, basi utaweza kumpa Mungu moyo wako zaidi na zaidi, roho yako itakuwa imara zaidi na zaidi, hali yako itakuwa bora zaidi na zaidi, utakuwa na uwezo zaidi wa kutembea katika njia inayoongozwa na Roho Mtakatifu, na Mungu atakupa baraka zaidi na zaidi. Lengo la maisha yenu ya kiroho ni kutafuta kwa makusudi na kupata kuwepo kwa Roho Mtakatifu. Sio kuzingatia sheria au kufanya taratibu za dini, bali kutenda kweli pamoja na Mungu na kudhibiti miili yenu. Hiki ndicho mwanadamu anapaswa kufanya, kwa hiyo lazima mtumie juhudi zenu zote ili kufanya hivi. Kadri unavyoshirikiana bora zaidi na kadri unavyojitahidi zaidi, ndivyo utakavyoweza zaidi kugeuza moyo wako kwa Mungu, na ndivyo utakavyozidi kutuliza moyo wako mbele Yake. Mara tu utakapofikia hali fulani, Mungu ataupata moyo wako kabisa. Hakuna atakayeweza kuyumbisha au kuuteka moyo wako, na utakuwa wa Mungu kabisa. Ikiwa unatembea katika njia hii, neno la Mungu litajifichua kwako wakati wote na kukupa nuru kwa kila kitu ambacho huelewei—hii yote inaweza kutimizwa kwa sababu ya ushirikiano wako. Hii ndiyo maana Mungu daima husema, “Wote wanaofanya kazi pamoja na Mimi, Nitawatuza mara mbili.” Lazima muione njia hii kwa dhahiri. Ikiwa mnataka kutembea katika njia sahihi, basi lazima mfanye yote muwezayo kumridhisha Mungu. Lazima mfanye yote muwezayo kufikia maisha ya kiroho. Mwanzoni, huenda usiweze kutimiza mengi katika suala hili, lakini usijiruhusu kurudi nyuma au kugaagaa katika ukanaji—lazima uendelee kufanya kazi kwa bidii! Kadri unavyoishi maisha ya kiroho, ndivyo moyo wako utakavyomilikiwa zaidi na maneno ya Mungu, ukishughulika na mambo haya daima na kuubeba mzigo huu daima. Baada ya hiyo, unaweza kufichua ukweli wako wa ndani kabisa kwa Mungu kupitia maisha yako ya kiroho, mwambie unachotaka kufanya, kile ambacho umekuwa ukifikiri, ufahamu wako na maoni yako mwenyewe ya neno la Mungu. Usizuie chochote, hata kidogo! Jizoeze kuzungumza maneno yaliyo ndani ya moyo wako kwa Mungu, mwambie ukweli, na usisite kuzungumza yaliyo moyoni mwako. Kadri unavyofanya hivi, ndivyo utakavyohisi zaidi upendo wa Mungu, na moyo wako utavutiwa zaidi na zaidi kumwelekea Mungu. Wakati ambapo hili litafanyika, utahisi kwamba Mungu ni mpenzi zaidi kwako kuliko mtu mwingine yeyote. Hutawahi kumwacha Mungu kamwe, lolote liwalo. Ikiwa utafanya aina hii ya ibada ya kiroho kila siku na usiiondoe akilini mwako, bali uichukulie kama wito wako katika maisha, basi neno la Mungu litaumiliki moyo wako. Hii ndiyo maana ya kuguswa na Roho Mtakatifu. Itakuwa kana kwamba moyo wako daima umetawaliwa na Mungu, kana kwamba kumekuwa na upendo ndani ya moyo wako daima. Hakuna anayeweza kuliondoa hilo kutoka kwako. Wakati hili litatokea, Mungu ataishi ndani yako kweli na kuwa na nafasi ndani ya moyo wako.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maisha ya Kawaida ya Kiroho Huwaongoza Watu Kwenye Njia Sahihi

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 414)

Imani katika Mungu husababisha maisha ya kawaida ya kiroho, ambayo ndiyo msingi wa kupitia maneno ya Mungu na kuingia katika uhalisi. Je, matendo yenu yote ya sasa ya maombi, ya kumkaribia Mungu, ya kuimba nyimbo za dini, sifa, taamali na kutafakari maneno ya Mungu yanajumuisha “maisha ya kawaida ya kiroho”? Hakuna mmoja kati yenu anayeonekana kujua. Maisha ya kawaida ya kiroho hayazuiliwi katika matendo kama kuomba, kuimba nyimbo za kidini, kushiriki katika maisha ya kanisa, na kula na kunywa maneno ya Mungu. Badala yake, yanahusisha kuishi maisha mapya na machangamfu ya kiroho. Kilicho muhimu si jinsi unavyotenda, lakini matunda yanayozalishwa na kutenda kwako. Watu wengi sana huamini kwamba maisha ya kawaida ya kiroho ni lazima yahusishe kuomba, kuimba nyimbo za kidini, kula na kunywa maneno ya Mungu ama kutafakari maneno Yake, bila kujali iwapo matendo kama haya kweli yana athari yoyote ama yanasababisha ufahamu wa kweli. Watu hawa hulenga kufuata taratibu za kijuujuu bila kufikiria matokeo yake, wao ni watu wanaoishi katika kaida za kidini, sio watu wanaoishi ndani ya kanisa, sembuse watu wa ufalme. Maombi yao, kuimba nyimbo za kidini, na kula na kunywa maneno ya Mungu ni kufuata kanuni tu, vitu vinavyofanywa kwa sababu ya kulazimishwa na kuwa sambamba na mitindo, sio kwa sababu ya kutaka wala kutoka moyoni. Bila kujali jinsi watu hawa wanavyoomba ama kuimba, juhudi zao hazitazaa matunda, kwa kuwa kile wanachotenda ni kanuni na kaida za kidini tu; kwa kweli hawatendi maneno ya Mungu. Wanalenga tu kulalamika kuhusu jinsi ya kutenda, na wanayachukulia maneno ya Mungu kama kanuni za kufuatwa. Watu kama hawa hawatii maneno ya Mungu katika vitendo; wanaridhisha tu mwili, na kutenda ili watu wengine wawaone. Kanuni na kaida hizi za kidini zote zina asili yake kwa binadamu; hazitoki kwa Mungu. Mungu hafuati sheria, wala Haathiriwi na sheria yoyote. Badala yake, Yeye hufanya mambo mapya kila siku, Akitimiza kazi ya vitendo. Kama watu katika Kanisa la Kanuni Tatu za Binafsi, wanaojiwekea mipaka kwa matendo kama vile kuhudhuria ibada za asubuhi kila siku, kutoa sala za jioni na sala za shukrani kabla ya milo, na kutoa shukrani katika vitu vyote—bila kujali kiasi wanachofanya ama wanakifanya kwa muda gani, hawatakuwa na kazi ya Roho Mtakatifu. Watu wanapoishi kati ya kanuni na kuzingatia mbinu za utendaji, Roho Mtakatifu hawezi kufanya kazi, kwa sababu mioyo yao imejazwa na kanuni na fikira za kibinadamu. Kwa hivyo, Mungu hawezi kuingilia kati na kuwafanyia kazi, na wanaweza tu kuendelea kuishi wakidhibitiwa na sheria. Watu kama hawa daima hawawezi kupokea sifa ya Mungu.

Maisha ya kawaida ya kiroho ni maisha ambayo mtu anaishi mbele za Mungu. Mtu anapoomba, anaweza kuutuliza moyo wake mbele za Mungu, na kupitia maombi, mtu anaweza kutafuta nuru ya Roho Mtakatifu, ayajue maneno ya Mungu na aelewe mapenzi ya Mungu. Kwa kula na kunywa maneno Yake, watu wanaweza kupata ufahamu dhahiri na kamili zaidi wa kazi ya sasa ya Mungu. Pia wanaweza kupata njia mpya ya kutenda, na hawatashikilia ile ya kale; yote wanayotenda yatakuwa ili kufanikisha ukuaji katika maisha. Kuhusiana na maombi, hayahusu kunena maneno machache yanayosikika kuwa mazuri ama kulia kwa ghafla mbele za Mungu ili kuonyesha jinsi unavyowiwa naye; badala yake, lengo lake ni kujifunza kutumia roho, ikimwezesha kuutuliza moyo wake mbele za Mungu, kujifunza kutafuta mwongozo kutoka kwa maneno ya Mungu katika masuala yote, ili moyo wake uweze kukaribia mwanga mpya na safi kila siku, na ili mtu asiwe mwenye kukaa tu ama mzembe na aweze kuingia kwenye njia sahihi ya kuyaweka maneno ya Mungu katika vitendo. Watu wengi siku hizi wanalenga mbinu za utendaji, lakini hawafanyi hivyo ili kuufuatilia ukweli na kufanikisha ukuaji wa maisha. Hapa ndipo walipopotoka. Pia kuna wengine wanaoweza kupokea mwanga mpya, lakini mbinu zao za utendaji hazibadiliki. Wao hutumia fikira zao za kale wanapotazamia kupokea maneno ya Mungu ya leo, kwa hivyo kile wanachopokea bado ni mafundisho yaliyoathiriwa na fikira za kidini; hawapokei mwanga wa leo hata kidogo. Kwa hiyo, matendo yao yametiwa doa; ni matendo yale yale ya kale katika kifurushi kipya. Bila kujali wanaweza kutenda vyema jinsi gani, wao ni wanafiki. Mungu huwaongoza watu katika kufanya mambo mapya kila siku, Akitaka kwamba kila siku wapate umaizi na ufahamu mpya, na kuwahitaji wasiwe waliopitwa na wakati na wenye kurudiarudia. Ikiwa umemwamini Mungu kwa miaka mingi, lakini mbinu zako za utendaji hazijabadilika hata kidogo, na ikiwa wewe bado ni mwenye raghba na mwenye shughuli nyingi kuhusu masuala ya nje, lakini huna moyo mtulivu wa kuleta mbele za Mungu ili uyafurahie maneno Yake, basi hutapata chochote. Inapofikia kuikubali kazi mpya ya Mungu, usipopanga kwa njia tofauti, usipotenda kwa njia mpya, na usifuatilie ufahamu wowote mpya, lakini badala yake ushikilie ya kale na kupokea tu mwanga finyu mpya, bila kubadili jinsi unavyotenda, basi watu kama wewe wako katika mkondo huu kwa jina tu; kwa kweli, wao ni Mafarisayo wa kidini walio nje ya mkondo wa Roho Mtakatifu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Maisha ya Kawaida ya Kiroho

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 415)

Ili kuishi maisha ya kawaida ya kiroho, lazima mtu aweze kupokea mwanga mpya kila siku na afuatilie ufahamu wa kweli wa maneno ya Mungu. Ni lazima mtu aone ukweli vyema, apate njia ya utendaji katika masuala yote, agundue maswali mapya kupitia kusoma maneno ya Mungu kila siku, na atambue upungufu wake mwenyewe ili aweze kuwa na moyo unaotamani na kutafuta ambao unaigusa nafsi yake nzima, na ili aweze kutulia mbele za Mungu nyakati zote, akiogopa sana kubaki nyuma. Mtu aliye na moyo kama huu unaotamani na kutafuta, aliye tayari kupata kuingia bila kusita, yuko kwenye njia sahihi ya maisha ya kiroho. Wale wanaoguswa na Roho Mtakatifu, wanaotaka kufanya vizuri zaidi, walio tayari kufuatilia kukamilishwa na Mungu, wanaotamani ufahamu wa kina wa maneno ya Mungu, wasiofuatilia jambo la mwujiza lakini badala yake wanalipa gharama ya kweli, wanaoyajali mapenzi ya Mungu kwa kweli, ambao kwa kweli wanapata kuingia ili uzoefu wao uwe wa kweli na halisi zaidi, wasiofuatilia maneno na mafundisho matupu ama kufuatilia kuhisi jambo la mwujiza, wasiomwabudu mtu yeyote mashuhuri—hawa ndio wale ambao wameingia katika maisha ya kawaida ya kiroho. Kila kitu wanachofanya kinanuiwa kufanikisha ukuaji zaidi katika maisha na kuwafanya wawe wapya na wachangamfu katika roho, na daima wanaweza kupata kuingia kwa shauku. Bila wao kujua, wanakuja kuuelewa ukweli na kuingia katika uhalisi. Wale walio na maisha ya kawaida ya kiroho hupata ukombozi na uhuru wa roho kila siku, na wanaweza kutenda maneno ya Mungu kwa njia huru mpaka Aridhike. Kwa watu hawa, kuomba si jambo la kidesturi ama utaratibu; kila siku, wanaweza kuwa sambamba na mwanga mpya. Kwa mfano, watu hujifunza kuituliza mioyo yao mbele za Mungu, na mioyo yao inaweza kutulia mbele za Mungu kwa kweli, na hawawezi kusumbuliwa na yeyote. Hakuna mtu, tukio ama jambo linaloweza kuzuia maisha yao ya kawaida ya kiroho. Mafunzo kama hayo yananuiwa kuleta matokeo; hayanuiwi kuwafanya watu wafuate kanuni. Utendaji huu hauhusu kufuata kanuni, lakini badala yake unahusu kukuza ukuaji katika maisha ya watu. Ikiwa unaona utendaji huu kuwa kanuni za kufuatwa tu, maisha yako hayatawahi kubadilika. Unaweza kuwa umeshiriki katika matendo sawa kama wengine, lakini wakati wao wanaweza hatimaye kuwa sambamba na kazi ya Roho Mtakatifu, unaondolewa kutoka katika mkondo wa Roho Mtakatifu. Je, hujidanganyi? Lengo la maneno haya ni kuwawezesha watu waitulize mioyo yao mbele za Mungu, waigeuze mioyo yao kumwelekea Mungu, ili kazi ya Mungu ndani yao iweze kutozuiwa na iweze kuzaa matunda. Ni baada ya hayo tu ndiyo watu wataweza kukubaliana na mapenzi ya Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Maisha ya Kawaida ya Kiroho

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 416)

Nyinyi hamtilii maanani sala katika maisha yenu ya kila siku. Watu daima wamepuuza sala. Hapo awali sala zilikuwa za uzembe, huku mwanadamu akifanya tu mambo kwa namna isiyo ya dhati mbele za Mungu. Hakuna mwanadamu aliyeutoa moyo wake kwa ukamilifu mbele ya Mungu na alifanya sala ya kweli kwa Mungu. Mwanadamu alimwomba tu Mungu wakati ambapo tatizo lilitokea. Katika wakati huu wote, umewahi kweli kumwomba Mungu? Je, umewahi kutoa machozi ya uchungu mbele ya Mungu? Je, umewahi kujijua mwenyewe mbele ya Mungu? Je, umewahi kumwomba Mungu maombi ya kutoka? Sala huja kupitia kufanya mazoezi: Ikiwa kwa kawaida huombi nyumbani, basi hutakuwa na njia yoyote ya kuomba kanisani, na kama kwa kawaida huombi wakati wa mikusanyiko midogo, basi hutaweza kusali wakati wa mikusanyiko mikubwa. Ikiwa kwa kawaida humkaribii Mungu au kutafakari juu ya maneno ya Mungu, basi hutakuwa na chochote cha kusema wakati wa kuomba—na hata kama utaomba, utakuwa tu unaunga mkono kwa maneno matupu; hutakuwa unaomba kwa kweli.

Ni nini maana ya kuomba kwa kweli? Ina maana ya kuzungumza maneno yaliyo ndani ya moyo wako kwa Mungu, na kuwasiliana na Mungu baada ya kufahamu mapenzi Yake na kutegemea maneno Yake; ina maana ya kuhisi kuwa karibu na Mungu hasa, kuhisi kwamba Yeye yuko mbele yako, na kwamba una kitu cha kumwambia; na inamaanisha kuwa mwangavu hasa ndani ya moyo wako, na kuhisi kwamba Mungu ni wa kupendeza hasa. Utajisikia kutiwa moyo sana, na baada ya kusikia maneno yako ndugu zako watajisikia kufurahishwa, watahisi kwamba maneno unayosema ni maneno yaliyo ndani ya mioyo yao, maneno ambayo wangependa kusema, na kwamba kile unachosema kinawakilisha kile wanachotaka kusema. Hii ndiyo maana ya kuomba kwa kweli. Baada ya kuomba kwa kweli, moyoni mwako utahisi kuwa na amani, na kufurahishwa; nguvu ya kumpenda Mungu itaongezeka, na utahisi kwamba hakuna kitu chochote katika maisha yako yote kinachostahili au ni muhimu zaidi kuliko kumpenda Mungu—na yote haya yatathibitisha kuwa maombi yako yamekuwa yenye ufanisi. Je, umewahi kuomba kwa njia hiyo?

Na je, kuhusu maudhui ya sala? Unapaswa kuomba, hatua kwa hatua, kwa mujibu wa hali yako ya kweli na kile kinachotakiwa kufanywa na Roho Mtakatifu, na unapaswa kuwasiliana kwa karibu na Mungu kulingana na mapenzi ya Mungu na mahitaji Yake kwa mwanadamu. Unapoanza kufanya mazoezi ya maombi yako, kwanza peana moyo wako kwa Mungu. Usijaribu kufahamu mapenzi ya Mungu; jaribu tu kuzungumza maneno yaliyo ndani ya moyo wako kwa Mungu. Unapokuja mbele za Mungu, sema hivi: “Ee Mungu! Leo tu ndio natambua kuwa nilikuwa nikikuasi. Mimi kweli ni mpotovu na mwenye kustahili dharau. Awali, nilikuwa nikipoteza muda wangu; kuanzia leo nitaishi kwa ajili Yako, nitaishi kwa kudhihirisha maisha ya maana, na kuridhisha mapenzi Yako. Ningependa Roho Wako afanye kazi ndani yangu daima, na daima aniangaze na kunipa nuru, ili nipate kuwa na ushuhuda wenye nguvu na unaosikika mbele Zako, unaomruhusu Shetani kuuona utukufu Wako, ushuhuda Wako, na thibitisho la ushindi Wako ndani yetu.” Wakati unapoomba kwa njia hii, moyo wako utawekwa huru kabisa, baada ya kuomba kwa njia hii, moyo wako utakuwa karibu na Mungu, na kwa kuomba hivi mara kwa mara, Roho Mtakatifu atafanya kazi ndani yako bila shaka. Ikiwa daima wewe humwita Mungu kwa njia hii na kufanya azimio lako mbele ya Mungu, siku itawadia ambapo azimio lako litaweza kukubalika mbele ya Mungu, wakati moyo wako na nafsi yako vyote vitapokelewa na Mungu, na hatimaye utakamilishwa na Mungu. Sala ni ya muhimu sana kwenu. Unapoomba, unapokea kazi ya Roho Mtakatifu, hivyo moyo wako unaguswa na Mungu, na nguvu za upendo kwa Mungu ndani yako huchipuka. Ikiwa hutaomba kwa moyo wako, ikiwa hutafungua moyo wako kuwasiliana kwa karibu na Mungu, basi Mungu hatakuwa na njia ya kufanya kazi ndani yako. Ikiwa, baada ya kusali, umesema maneno yote yaliyo ndani ya moyo wako na Roho wa Mungu hajafanya kazi, ikiwa huhisi kutiwa moyo ndani, basi hili linaonyesha kwamba moyo wako hauna ari, kwamba maneno yako si ya kweli, na bado wewe ni mchafu. Ikiwa, baada ya kusali, unafurahishwa, basi sala zako zimekubaliwa na Mungu na Roho wa Mungu amefanya kazi ndani yako. Kama mtu ambaye huhudumu mbele ya Mungu, huwezi kuwa bila sala. Ikiwa unaona ushirika na Mungu kama kitu ambacho kina maana na cha thamani, ungeweza kuacha sala? Hakuna mtu anayeweza kuwa bila mawasiliano ya karibu na Mungu. Bila sala, unaishi katika mwili, unaishi katika utumwa wa Shetani; bila sala ya kweli, unaishi chini ya ushawishi wa giza. Natumaini kwamba ndugu wanaweza kuomba kila siku. Huku si kuzingatia mafundisho ya dini, hata hivyo, bali matokeo ambayo yanapaswa kutimizwa. Je, uko tayari kuacha usingizi kidogo na anasa, kusema sala za asubuhi wakati wa alfajiri na kisha kufurahia maneno ya Mungu? Ukiomba kwa moyo safi na kula na kunywa maneno ya Mungu hivi, utakubalika zaidi Kwake. Ukifanya hivi kila asubuhi, ukifanya mazoezi ya kumpa Mungu moyo wako kila siku na kuwasiliana kwa karibu na Mungu, basi ufahamu wako wa Mungu utaongezeka bila shaka, na utaweza kufahamu vizuri zaidi mapenzi ya Mungu. Unapaswa kusema: “Ee Mungu! Ningependa kutimiza wajibu wangu. Ili Uweze kutukuzwa ndani yetu, na Uweze kufurahia ushuhuda ulio ndani yetu, kikundi hiki cha watu, naweza tu kutoa nafsi yangu yote kwako. Nakuomba Ufanye kazi ndani yetu, ili niweze kukupenda na kukuridhisha kwa kweli, na kukufanya Uwe lengo ambalo ninafuatilia.” Wakati ambapo unakuwa na mzigo huu, Mungu atakufanya uwe mkamilifu bila shaka; hupaswi tu kuomba kwa ajili yako mwenyewe, bali pia kwa ajili ya kufanya mapenzi ya Mungu, na kwa ajili ya kumpenda Yeye. Hiyo ndiyo aina ya sala ya kweli kabisa. Je, wewe huomba ili kutenda mapenzi ya Mungu?

Hapo awali, nyinyi hamkujua jinsi ya kuomba, na mlipuuza maombi; leo, lazima mjitahidi kabisa kujifundisha kuomba. Ikiwa huwezi kuwa na ujasiri wa kumpenda Mungu, basi unawezaje kuomba? Unapaswa kusema: “Ee Mungu! Moyo wangu hauwezi kukupenda kweli, nataka kukupenda lakini sina nguvu. Napaswa kufanya nini? Napenda Ufungue macho ya roho yangu, napenda Roho Wako auguse moyo wangu, ili mbele Yako nivuliwe hali zote za kutoonyesha hisia, na nisishurutishwe na mtu yeyote, jambo, au kitu; nauweka moyo wangu wazi kabisa mbele Yako, ili nafsi Yangu yote ijitoe mbele Yako, na Uweze kunijaribu vile Utakavyo. Sasa, siwazii matarajio yangu, wala sifungwi na kifo. Kwa kuutumia moyo wangu ambao unakupenda, napenda kutafuta njia ya uzima. Vitu vyote na matukio viko mikononi Mwako, majaliwa yangu yako mikononi Mwako, na, zaidi ya hayo, maisha yangu yanadhibitiwa na mikono Yako. Sasa, nafuatilia kukupenda Wewe, na bila kujali kama Wewe unaniruhusu kukupenda, haijalishi jinsi Shetani anavyoingilia, nimeamua kukupenda Wewe.” Unapokabiliwa na mambo kama hayo, unasali kwa njia hii. Ikiwa utafanya hivyo kila siku, nguvu ya kumpenda Mungu itaongezeka polepole.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Desturi ya Sala

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 417)

Mtu huingiaje katika sala ya kweli?

Unapoomba, lazima uwe na moyo ambao ni mtulivu mbele ya Mungu, na lazima uwe na moyo mwaminifu. Wewe kweli unawasiliana kwa karibu na kuomba na Mungu—usimdanganye Mungu kwa kutumia maneno ya kupendeza. Sala lazima ilenge kile ambacho Mungu anataka kukamilisha leo. Mwombe Mungu akupe nuru na mwangaza mwingi zaidi, na ulete hali halisi na matatizo yako mbele za Mungu kuomba, na ufanye azimio mbele za Mungu. Sala sio kufuata utaratibu, bali ni kumtafuta Mungu kwa kutumia moyo wako wa kweli. Omba kwamba Mungu aulinde moyo wako, na Aufanye uwe na amani mara nyingi mbele za Mungu, Akuwezeshe kujijua, na kujidharau, na kujitupa katika mazingira ambayo Mungu amekuwekea, hivyo kukuruhusu uwe na uhusiano wa kawaida na Mungu na kukufanya mtu anayempenda Mungu kweli.

Ni nini umuhimu wa sala?

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato ambao mtu huguswa na Roho wa Mungu. Inaweza kusemwa kwamba wale ambao hawana sala ni wafu wasio na roho, ushahidi kwamba hawana uwezo wa kuguswa na Mungu. Bila sala, watu hawawezi kupata maisha ya kawaida ya kiroho, sembuse kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu; bila sala, wao huvunja uhusiano wao na Mungu, na hawawezi kupokea kibali cha Mungu. Ukiwa mtu anayemwamini Mungu, kadri unavyoomba, ndivyo unavyozidi kuguswa na Mungu. Watu kama hao wana azimio kubwa zaidi na wanaweza kupokea zaidi nuru ya hivi karibuni kutoka kwa Mungu; kwa hivyo, watu kama hawa pekee ndio wanaweza kukamilishwa mapema iwezekanavyo na Roho Mtakatifu.

Je, ni matokeo gani yanayofaa kutimizwa kwa sala?

Watu wanaweza kutekeleza mazoea ya sala na kuelewa umuhimu wa sala, lakini matokeo yanayofaa kutimizwa kwa sala sio jambo rahisi. Sala sio jambo la kupitia urasmi wa kisheria, au kufuata utaratibu, au kukariri maneno ya Mungu, ambalo ni kusema, sala haimaanishi kuiga maneno kama kasuku na kuwaiga wengine. Katika sala, lazima umpe Mungu moyo wako, ukishiriki maneno yaliyo ndani ya moyo wako na Mungu ili uweze kuguswa na Mungu. Ikiwa maombi yako yatakuwa na matokeo, basi lazima yategemee usomaji wako wa maneno ya Mungu. Ni kwa kuomba tu katikati ya maneno ya Mungu ndipo utaweza kupokea nuru na mwangaza zaidi. Sala ya kweli huonyeshwa kwa kuwa na moyo ambao unatamani sana matakwa yaliyowekwa na Mungu, na kuwa tayari kutimiza matakwa haya; utaweza kuchukia yote ambayo Mungu huchukia, kwa msingi huo utakuwa na maarifa, na utajua na kuelewa wazi kuhusu ukweli ulioelezwa na Mungu. Kuwa na azimio, na imani, na maarifa, na njia ya kufanya mazoezi baada ya kuomba—huku tu ndiko kuomba kwa kweli, na sala kama hii tu ndiyo inaweza kuwa na ufanisi. Lakini sala lazima ijengwe juu ya msingi wa kufurahia maneno ya Mungu na kuwasiliana kwa karibu na Mungu katika maneno Yake, moyo wako ukiweza kumtafuta Mungu na kuwa na amani mbele ya Mungu. Sala kama hiyo tayari imefikia kiwango cha kuwasiliana kwa kweli na Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Desturi ya Sala

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 418)

Maarifa ya msingi kuhusu kuomba:

1. Usiseme kijinga chochote kinachokuja kwenye akili. Lazima kuwe na mzigo ndani ya moyo wako, ambalo ni kusema, lazima uwe na lengo wakati unapoomba.

2. Sala lazima iwe na maneno ya Mungu; lazima itegemezwe kwa maneno ya Mungu.

3. Wakati unapoomba, ni sharti usitumie tena masuala yaliyopitwa na wakati. Maombi Yako yanapaswa kuhusiana na maneno ya sasa ya Mungu, na unapoomba, umwambie Mungu mawazo yako ya ndani kabisa.

4. Sala ya kikundi inapaswa kulenga kiini, ambacho lazima kiwe kazi ya Roho Mtakatifu leo.

5. Watu wote lazima wajifunze sala ya kuombea. Hii pia ni njia ya kuyadhukuru mapenzi ya Mungu.

Maisha ya maombi ya kibinafsi yanategemea kuelewa umuhimu wa sala na maarifa ya msingi ya sala. Katika maisha ya kila siku, omba mara kwa mara kwa ajili ya dosari zako, omba upate mabadiliko katika tabia yako maishani, na omba kwa msingi wa maarifa yako ya maneno ya Mungu. Kila mtu anapaswa kuanzisha maisha yake ya maombi, anapaswa kuombea maarifa kutegemea maneno ya Mungu, anapaswa kuomba ili kutafuta maarifa ya kazi ya Mungu. Weka hali zako za kweli mbele ya Mungu, na uwe wa vitendo, na usitilie maanani mbinu; la muhimu ni kupata maarifa ya kweli, na kupata maneno ya Mungu kwa kweli. Yeyote anayefuatilia kuingia katika maisha ya kiroho lazima aweze kuomba kwa njia nyingi. Sala ya kimya, kutafakari maneno ya Mungu, kuja kuijua kazi ya Mungu, na kadhalika—kazi hii inayolengwa ya kuwasiliana kwa karibu, ni ili kutimiza kuingia katika maisha ya kawaida ya kiroho, kuifanya hali yako mwenyewe mbele za Mungu iwe bora zaidi, na kusababisha maendeleo makubwa zaidi katika maisha yako. Kwa kifupi, yote unayoyafanya—kama ni kula na kunywa maneno ya Mungu, au kuomba kimya au kutangaza kwa sauti—ni ili kuona wazi maneno ya Mungu, na kazi Yake, na kile Anachotaka kutimiza ndani yako. La muhimu zaidi, ni ili kufikia viwango ambavyo Mungu anahitaji na kuyapeleka maisha yako kwa kiwango kinachofuata. Kiwango cha chini zaidi ambacho Mungu anahitaji kwa watu ni kwamba waweze kufungua mioyo yao Kwake. Ikiwa mwanadamu atautoa moyo wake wa kweli kwa Mungu na kusema kile kilicho ndani ya moyo wake kwa Mungu, basi Mungu yuko tayari kufanya kazi ndani ya mwanadamu; Mungu hataki moyo wa mwanadamu uliopotoka, lakini moyo wake ulio safi na mwaminifu. Ikiwa mwanadamu hasemi yaliyo moyoni mwake kwa Mungu kwa kweli, basi Mungu haugusi moyo wa mwanadamu, au kufanya kazi ndani yake. Hivyo, jambo muhimu sana kuhusu kuomba ni kusema maneno ya moyo wako wa kweli kwa Mungu, kumwambia Mungu kuhusu dosari zako au tabia ya kuasi na kujifungua kabisa kwa Mungu. Wakati huo tu ndipo Mungu atakuwa na hamu ya sala zako; la sivyo, basi Mungu atauficha uso Wake kutoka kwako. Kigezo cha chini kabisa cha sala ni kwamba lazima uweze kuuweka moyo wako kwa amani mbele za Mungu, na hupaswi kuondoka kwa Mungu. Pengine, wakati huu, hujapata mtazamo mpya au wa juu, lakini lazima utumie sala ili mambo yaendelee kama yalivyo—huwezi kurudi nyuma. Hili ndilo jambo dogo zaidi ambalo unapaswa kutimiza. Ikiwa huwezi kufanikisha hata hili, basi inathibitisha kwamba maisha yako ya kiroho hayajaingia katika njia sahihi; kwa hiyo, huwezi kushikilia maono yako ya mwanzo, na kuondolea imani kwa Mungu, na uamuzi wako hatimaye hutoweka. Kuingia kwako katika maisha ya kiroho kunadhihirishwa na iwapo sala zako zimeingia katika njia sahihi au la. Watu wote lazima waingie katika uhalisi huu, lazima wafanye kazi ya kujifunza wenyewe kwa kufahamu katika sala, sio kusubiri kwa kukaa tu, lakini kwa ufahamu watafute kuguswa na Roho Mtakatifu. Wakati huo tu ndipo watakuwa watu wanaomtafuta Mungu kwa kweli.

Unapoanza kuomba, lazima uwe mwenye uhalisi, na usitake kufanya kupita kiasi; huwezi kufanya madai ya ubadhirifu, ukitumaini kwamba mara tu utakapofungua kinywa chako utaguswa na Roho Mtakatifu, utapata nuru na mwangaza, na kupewa neema nyingi. Hilo haliwezekani—Mungu hafanyi mambo yaliyo ya rohoni. Mungu hutimiza sala za watu kwa wakati Wake mwenyewe na wakati mwingine Yeye hujaribu imani yako kuona kama wewe ni mwaminifu mbele Zake. Unapoomba lazima uwe na imani, uvumilivu, na azimio. Watu wengi wanapoanza kujifunza kuomba, hawahisi kuwa wameguswa na Roho Mtakatifu na hivyo huvunjika moyo. Hili halikubaliki! Lazima uwe na nia ya kutobadili msimamo, lazima ulenge kuhisi mguso wa Roho Mtakatifu, na kutafuta na kuchunguza. Wakati mwingine, njia unayofuata ni ile isiyo sahihi; wakati mwingine, misukumo na dhana zako haviwezi kusimama imara mbele za Mungu, na hivyo Roho wa Mungu hakusisimui; vivyo pia kuna nyakati ambapo Mungu huangalia kama wewe ni mwaminifu au la. Kwa kifupi, lazima ujitahidi zaidi katika kujifunza. Ikiwa utatambua kuwa njia unayoifuata ni ya kuacha maadili, unaweza kubadilisha jinsi unavyoomba. Maadamu unatafuta kwa kweli, na unatamani kupokea, basi Roho Mtakatifu atakuingiza kwenye ukweli huu. Wakati mwingine unasali kwa moyo wa ukweli lakini huhisi kama umeguswa hasa. Katika nyakati kama hizi lazima utegemee imani yako, na uamini kwamba Mungu anayaangalia maombi yako; lazima uwe na uvumilivu katika sala zako.

Lazima uwe mwaminifu, na lazima uombe ili uondoe ujanja ndani ya moyo wako. Unapotumia maombi ili kujitakasa wakati wowote inapohitajika, na kuyatumia ili uguswe na Roho wa Mungu, tabia yako itabadilika polepole. Maisha ya kweli ya kiroho ni maisha ya sala, na ni maisha ambayo yanaguswa na Roho Mtakatifu. Mchakato wa kuguswa na Roho Mtakatifu ni mchakato wa kubadilisha tabia ya mwanadamu. Maisha ambayo hayajaguswa na Roho Mtakatifu si maisha ya kiroho, bado ni ibada ya kidini; wale tu ambao huguswa na Roho Mtakatifu mara kwa mara, na wamepewa nuru na kuangazwa na Roho Mtakatifu, ndio watu ambao wameingia katika maisha ya kiroho. Tabia ya mwanadamu hubadilika kwa uthabiti wakati anapoomba, na kadri anavyosisimuliwa na Roho wa Mungu, ndivyo anavyozidi kuwa hai na mtiifu. Kwa hiyo, pia, moyo wake utatakaswa polepole, baada ya hapo tabia yake itabadilika polepole. Hayo ndiyo matokeo ya sala ya kweli.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Desturi ya Sala

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 419)

Kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu ni mojawapo ya hatua muhimu sana za kuingia katika maneno ya Mungu, na ni funzo ambalo watu wote sasa wana haja ya haraka kuingia ndani. Njia za kuingia za kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu ni:

1. Ondoa moyo wako kwa mambo ya nje, tulia mbele ya Mungu, na uombe Mungu kwa moyo uliolenga.

2. Moyo wako ukiwa umetulia mbele ya Mungu, kula, kunywa, na kufurahia maneno ya Mungu.

3. Tafakari na uzingatie maneno ya Mungu na kufikiria kazi ya Mungu kwa moyo wako.

Kwanza anza na jambo la sala. Kuwa na nia moja, na uombe wakati usiobadilika. Haijalishi umepungukiwa na muda namna gani, au uwe na shughuli vipi, au chochote kitakachokufanyikia, omba kila siku kama kawaida, na ule na kunywa maneno ya Mungu kama kawaida. Mradi unakula na kunywa maneno ya Mungu, haijalishi mazingira yako ni yapi, utakuwa na raha nyingi katika roho yako, na hutasumbuliwa na watu, matukio, au mambo yanayokuzunguka. Unapotafakari juu ya Mungu kwa kawaida ndani ya moyo wako, kinachoendelea nje hakiwezi kukusumbua wewe. Hii ndiyo maana ya kuwa na kimo. Anzia kwa maombi: Kuomba kwa amani mbele ya Mungu huzaa matunda zaidi. Baada ya hapo, kuna kula na kunywa maneno ya Mungu, kuweza kuelewa mwangaza ulio kwenye maneno ya Mungu, kuweza kupata njia ya kutenda, kujua maazimio ya matamshi ya Mungu ni yapi, na kuelewa bila mkengeuko. Kwa kawaida, lazima moyo wako uweze kusongea karibu na Mungu kwa kawaida, lazima uweze kuzingatia upendo wa Mungu, kutafakari juu ya maneno ya Mungu, na usiweze kuathiriwa na kuingiliwa kwa dunia ya nje. Moyo wako unapokuwa na amani mbele ya Mungu kiasi kwamba unaweza kutafakari, ukiwa, ndani yako mwenyewe, unazingatia upendo wa Mungu, na kusonga karibu na Mungu kwa kweli, bila kujali mazingira uliyomo, na, kwa hakika ukiwa umefika kiwango ambacho unapeana sifa moyoni mwako, na ni bora zaidi hata kuliko kuomba, basi katika hili utakuwa wa kimo fulani. Ikiwa una uwezo wa kutimiza hali iliyoelezewa hapa juu, basi hii itathibitisha kuwa moyo wako kwa kweli uko na amani mbele ya Mungu. Hii ni hatua ya kwanza; ni ujuzi wa kimsingi. Ni baada tu ya kuwa na uwezo wa kuwa na amani mbele ya Mungu ndipo watu wanaweza kuguswa na Roho Mtakatifu, na kupata nuru na kuangaziwa na Roho Mtakatifu, ni hapo tu ndipo wanaweza kuwasiliana kwa karibu kwa kweli na Mungu, na kuweza kushika mapenzi ya Mungu na mwongozo wa Roho Mtakatifu—na katika hii, watakuwa wameingia katika njia sahihi katika maisha yao ya kiroho. Kujizoeza mwenyewe kuishi mbele ya Mungu kufikia kina fulani ili uweze kujiasi mwenyewe, kujidharau mwenyewe, na kuishi katika maneno ya Mungu, hii kweli ni kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu. Kuweza kujidharau, kujilaani, na kujiasi ni matokeo ambayo kazi ya Mungu hutimiza, na watu hawawezi kufanya hili. Kwa hivyo mazoezi ya kuutuliza moyo wa mtu mbele ya Mungu ni funzo ambalo watu wanapaswa kuingia ndani mara moja. Watu wengine hawawezi tu kwa kawaida kuituliza mioyo yao mbele ya Mungu, lakini mioyo yao hata haitulii mbele ya Mungu wanapoomba. Hii kwa jumla ni mbali sana na viwango vya Mungu! Ikiwa moyo wako hauwezi kutulia mbele ya Mungu unaweza kusisimuliwa na Roho Mtakatifu? Ikiwa huwezi kutulia mbele ya Mungu, unaweza kuvurugwa mawazo mtu akija, unaweza kuvurugwa mawazo watu wanapoongea, na moyo wako unaweza kuvutwa mbali watu wengine wanapofanya mambo, kwa hiyo wewe si mtu anayeishi mbele ya Mungu. Ikiwa moyo wako kweli umetulia mbele ya Mungu hutasumbuliwa na chochote kinachoendelea huko nje duniani, na hakuna mtu, tukio au jambo litakalokumiliki. Ikiwa mmeingia katika hili, basi zile hali hasi na mambo yote hasi—fikira za binadamu, falsafa za kuishi, mahusiano yasiyo ya kawaida na watu, na mawazo ndani ya moyo wako yatatoweka kwa kawaida. Kwa sababu kila mara unatafakari maneno ya Mungu, na moyo wako kila mara unasonga karibu na Mungu na kumilikiwa na maneno ya sasa ya Mungu, mambo hayo mabaya huvuliwa bila kufahamu. Mambo mapya mazuri yanapokumiliki, mambo ya zamani mabaya hayatakuwa na nafasi, kwa hiyo usitilie maanani mambo hayo mabaya. Huhitaji kufanya jitihada za kujaribu kuyadhibiti. Tilia maanani kutulia mbele ya Mungu, kula na kunywa maneno zaidi ya Mungu na kuyafurahia, imba nyimbo nyingi zaidi za dini ukimsifu Mungu, na wacha Mungu awe na nafasi ya kukushughulikia, kwa sababu Mungu wakati huu anataka binafsi kuwakamilisha watu, Anataka kuupata moyo wako, Roho Wake husisimua moyo wako, na ukiishi mbele ya Mungu ukifuata uongozi wa Roho Mtakatifu utamridhisha Mungu. Ukitilia maanani kuishi katika maneno ya Mungu na kushiriki zaidi kuhusu ukweli ili kupata nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu, basi fikira hizo za kidini, kujidai na kujikweza vitatoweka vyote, na kisha utajua namna ya kugharimia rasilmali kwa ajili ya Mungu, kujua namna ya kumpenda Mungu, na namna ya kumridhisha Mungu. Mambo hayo nje ya Mungu kisha husahaulika bila kufahamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Kuutuliza Moyo Wako Mbele ya Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 420)

Kutafakari juu ya maneno ya Mungu na kusali juu ya maneno ya Mungu kwa wakati sawa na kula na kunywa maneno ya sasa ya Mungu—hii ndiyo hatua ya kwanza ya kuwa na amani mbele ya Mungu. Iwapo unaweza kuwa na amani kwa uhakika mbele ya Mungu, basi utafuatwa na nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu. Maisha yote ya kiroho hutimizwa kwa kutegemea kutulia mbele ya Mungu. Katika kuomba lazima utulie mbele ya Mungu kabla ya kuweza kusisimuliwa na Roho Mtakatifu. Kwa kutulia mbele ya Mungu unapokula na kunywa maneno ya Mungu unaweza kupata nuru na kuangaziwa na kuweza kutimiza kwa kweli ufahamu wa maneno ya Mungu. Katika tafakuri na ushirika wako wa kawaida, na wakati unasonga karibu na Mungu na moyo wako, ni wakati unapotulia tu mbele ya Mungu ndipo unaweza kuwa na ukaribiano halisi na Mungu, ufahamu halisi wa upendo wa Mungu na kazi ya Mungu, na uangalifu wa kweli kwa makusudi ya Mungu. Kadri unavyoweza kwa kawaida kutulia mbele ya Mungu ndivyo unavyoweza kuangaziwa zaidi, na ndivyo unavyoweza kufahamu tabia yako mwenyewe ya upotovu zaidi, unachokosa, unachopaswa kuingia, shughuli unayopaswa kuhudumu, na pale ulipo na dosari. Haya yote hutimizwa kwa kutegemea kuwa mtulivu mbele ya Mungu. Ikiwa utafikia kweli kina fulani cha kuwa mtulivu mbele ya Mungu, unaweza kugusa miujiza fulani katika roho, kugusa kile ambacho Mungu wakati huu anataka kufanya juu yako, kugusa ufahamu wa kina wa maneno ya Mungu, na kugusa asili ya maneno ya Mungu, kiini cha maneno ya Mungu, nafsi ya maneno ya Mungu, na unaweza kuona njia ya kutenda kwa kweli zaidi na sawasawa zaidi. Ikiwa huwezi kutulia katika roho yako kwa kina fulani, utaweza kusisimuliwa tu kiasi na Roho Mtakatifu, ndani utahisi nguvu, na furaha na amani kiasi, lakini hutagusa chochote kwa kina zaidi. Nimesema hapo awali, ikiwa mtu hatumii nguvu zake zote, itakuwa vigumu kwake kusikia sauti Yangu au kuona uso Wangu. Hii inanena juu ya kutimiza kina katika kutulia mbele ya Mungu, sio kwa juhudi za nje. Mtu anayeweza kuwa mtulivu kwa kweli mbele ya Mungu anaweza kujiachilia huru kutoka kwa vifungo vyote vya kidunia na anaweza kutimiza kumilikiwa na Mungu. Watu wote wasioweza kutulia mbele ya Mungu ni wafisadi na wasiozuiwa kwa yakini. Wale wote wanaoweza kutulia mbele ya Mungu ni watu ambao ni wacha Mungu mbele ya Mungu, watu wanaomtamani Mungu. Ni watu walio watulivu tu mbele ya Mungu ndio wanaotilia maanani maisha, wanaotilia maanani ushirika katika roho, walio na kiu ya maneno ya Mungu, na wanaofuatilia ukweli. Wale wote wasiotilia maanani kutulia mbele ya Mungu, wasiofanya mazoezi ya kuwa watulivu mbele ya Mungu ni watu ovyo ambao wamejifunga kabisa kwa dunia, wasio na uzima; hata wakisema wanaamini katika Mungu wanaunga mkono kwa maneno matupu tu. Wale ambao Mungu hukamilisha na kufanya kamili hatimaye ni watu wanaoweza kuwa watulivu mbele ya Mungu. Kwa hivyo, watu walio watulivu mbele ya Mungu ni watu walioneemeshwa na baraka nyingi. Watu ambao mchana hutumia muda mchache kula na kunywa maneno ya Mungu, ambao wameshughulika kabisa na mambo ya nje, na hawatilii maanani kuingia katika uzima wote ni wanafiki wasiokuwa na matarajio ya kuendelea katika siku za usoni. Ni wale wanaoweza kutulia mbele ya Mungu na kushiriki kwa uhalisi na Mungu ndio watu wa Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Kuutuliza Moyo Wako Mbele ya Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 421)

Kuja mbele ya Mungu kukubali maneno Yake kama uzima wako, lazima kwanza uwe mtulivu mbele ya Mungu. Ni wakati unapokuwa tu mtulivu mbele ya Mungu ndio Mungu atakupa nuru na kukufanya uelewe. Kadri watu wanavyokuwa watulivu zaidi mbele ya Mungu, ndivyo wanavyoweza kupata nuru na mwangaza wa Mungu zaidi. Haya yanawahitaji watu kuwa na uchaji Mungu na imani. Ni hivyo tu ndivyo wanaweza kutimiza ukamilifu. Zoezi la msingi la kuingia katika maisha ya kiroho ni kuwa mtulivu mbele ya Mungu. Mazoezi yako yote ya kiroho yatafaa tu ikiwa unatulia mbele ya Mungu. Ikiwa huwezi kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu huwezi kupokea kazi ya Roho Mtakatifu. Ikiwa moyo wako umetulia mbele ya Mungu haijalishi unachofanya basi wewe ni mtu unayeishi mbele ya Mungu. Ikiwa moyo wako umetulia mbele ya Mungu na unasonga karibu na Mungu haijalishi unachofanya, hii inathibitisha kuwa wewe ni mtu uliye mtulivu mbele ya Mungu. Unapozungumza na wengine, unapotembea, unaweza kusema, “Moyo wangu unasonga karibu na Mungu, na haulengi mambo ya nje, na naweza kutulia mbele ya Mungu.” Huyu ni mtu aliyetulia mbele ya Mungu. Usiingiliane na vitu vinavyoweza kuelekeza moyo wako kwa mambo ya nje, na usiingiliane na watu wanaoweza kuondoa moyo wako kwa Mungu. Achana na chochote kile kinachoweza kuvuta moyo wako usiwe karibu na Mungu, au kukaa mbali nacho. Njia hiyo ni ya manufaa zaidi kwa maisha yako. Huu ndio wakati wa kazi kuu ya Roho Mtakatifu. Ni wakati ambao Mungu Mwenyewe anawakamilisha watu. Ikiwa kwa wakati huu huwezi kutulia mbele ya Mungu basi wewe si mtu unayerudi mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Ikiwa unafuatilia vitu badala ya Mungu hakuna uwezekano wa kukamilishwa na Mungu. Wale ambao leo wanaweza kusikia matamshi kama haya kutoka kwa Mungu na bado hawawezi kutulia mbele ya Mungu ni watu wasiopenda ukweli, watu wasiompenda Mungu. Ikiwa hutajitoa sasa utafanya hivyo lini? Kujitoa mwenyewe ni kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu. Huku ni kujitoa kwa halisi. Yeyote anayetoa moyo wake kwa Mungu sasa kwa kweli bila shaka anaweza kukamlishwa na Mungu. Hakuna chochote, haijalishi ni nini, kinaweza kukusumbua, ikiwa ni cha kukupogoa, au kukushughulikia, au ikiwa wewe hukutana na kuvunjwa moyo au kutofaulu, moyo wako unapaswa kila mara kutulia mbele ya Mungu. Haijalishi watu wanakutendea vipi, moyo wako unapaswa kutulia mbele ya Mungu. Haijalishi unakabiliwa na mazingira gani, iwe ni dhiki, taabu, au mateso, au ikiwa aina nyingi ya majaribio yanakukumba, moyo wako unapaswa kila mara kutulia mbele ya Mungu. Hii ni njia ya kukamilishwa. Ikiwa tu mmetulia kwa kweli mbele ya Mungu ndipo mtaelewa kuhusu maneno ya sasa ya Mungu, kutenda kwa usahihi zaidi mwanga na kupata nuru kwa Roho Mtakatifu na kutopotoka, kuweza kuelewa dhahiri zaidi makusudi ya Mungu na kuwa na mwelekeo wazi zaidi katika huduma yako, kuweza kuelewa kwa usahihi zaidi mguso na uongozi wa Roho Mtakatifu na kuwa na uhakika wa kuishi chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu. Haya ndiyo matokeo ambayo kuwa mtulivu kwa kweli mbele ya Mungu hutimiza. Wakati watu hawaelewi kuhusu maneno ya Mungu, hawana njia ya kutenda, hawawezi kuyaelewa makusudi ya Mungu, au hawana kanuni za kutenda, hii ni kwa sababu mioyo yao haijatulia mbele ya Mungu. Kusudi la kuwa mtulivu mbele ya Mungu ni kuwa mwenye ari na wa vitendo na kutafuta usahihi na uangavu katika maneno ya Mungu, hatimaye kutimiza kufahamu ukweli na kumjua Mungu.

Ikiwa moyo wako hauwezi siku zote kutulia mbele ya Mungu, Mungu hawezi kukukamilisha. Ikiwa mtu hana nia iliyo sawa na kukosa moyo, na watu wasio na mioyo hawawezi kutulia mbele ya Mungu. Hawajui ni kazi kiasi gani ambayo Mungu hufanya au kiasi gani Yeye husema, wala hawajui namna ya kuyaweka katika vitendo. Je, hawa si watu wasio na mioyo? Watu wasio na mioyo wanaweza kutulia mbele ya Mungu? Mungu hawezi kuwakamilisha watu wasio na mioyo, nao wako miongoni mwa wanyama. Mungu amenena wazi sana na kikamilifu, ilhali moyo wako bado hauwezi kusisimuliwa na bado huwezi kutulia mbele ya Mungu; je, huku sio kuwa mnyama? Watu wengine hupotoka katika kufanya mazoezi ya kutulia mbele ya Mungu. Ikiwa ni wakati wa kupika hawapiki, na ikiwa ni wakati wa kufanya kazi hawafanyi kazi, lakini wanaendelea tu kuomba na kutafakari. Kutulia mbele ya Mungu hakumaanishi kutopika au kutofanya kazi, wala kuyapuuza maisha, lakini kuweza kuutuliza moyo wa mtu mbele ya Mungu, kuweza kuweka nafasi ya Mungu ndani ya moyo wa mtu katika hali zote za kawaida. Unapoomba, piga magoti chini vizuri mbele ya Mungu kuomba; unapofanya kazi au kutayarisha chakula, tuliza moyo wako mbele ya Mungu, tafakari maneno ya Mungu au imba nyimbo za dini. Haijalishi ni mazingira gani uko ndani, una njia ya kufanya mazoezi, fanya kila uwezalo kuwa karibu na Mungu, fanya kila uwezalo kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu. Hali zinaporuhusu, omba kwa nia moja; hali zisiporuhusu, mkaribie Mungu ndani ya moyo wako unapofanya kazi hiyo kwa mikono yako. Unapoweza kula na kunywa maneno ya Mungu basi kula na kunywa maneno ya Mungu; unapoweza kuomba basi omba; unapoweza kumtafakari Mungu basi mtafakari Yeye; fanya kila uwezalo kujizoeza kwa ajili ya kuingia kwa kutegemea mazingira yako. Watu wengine wanaweza kutulia mbele ya Mungu wakati hakuna kinachotokea, lakini punde tu jambo hufanyika mioyo yao hulifuatilia. Huko si kutulia mbele ya Mungu. Njia sahihi ya kupata uzoefu ni kwamba moyo wa mtu usimwache Mungu kwa hali yoyote ile, au kuhisi kusumbuliwa na watu, matukio, au mambo ya nje: Huyu ni mtu ambaye ametulia kweli mbele ya Mungu. Watu wengine husema kwamba wanapoomba katika mikutano mioyo yao huweza kutulia mbele ya Mungu, lakini wakiwa katika ushirika hawawezi kutulia mbele ya Mungu na mawazo yao hayadhibitiki. Huku si kutulia mbele ya Mungu. Watu wengi sana wakati huu wako katika hali hii, na mioyo yao haiwezi kila mara kutulia mbele ya Mungu. Kwa hiyo mnahitaji kuongeza juhudi zaidi katika kujizoeza katika eneo hili, kuingia hatua kwa hatua katika njia sahihi ya uzoefu wa maisha na kutembea juu ya njia ya kukamilishwa na Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Kuutuliza Moyo Wako Mbele ya Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 422)

Kazi na neno la Mungu vinanuiwa kusababisha badiliko katika tabia yenu; lengo Lake si tu kuwafanya muelewe ama mjue kazi na neno Lake. Hilo halitoshi. Wewe ni mtu aliye na uwezo wa kufahamu, kwa hivyo hupaswi kuona ugumu kuelewa neno la Mungu, kwa sababu maneno mengi ya Mungu yameandikwa katika lugha ya mwanadamu, na Anazungumza kwa uwazi sana. Kwa mfano, unaweza kabisa kujifunza ni nini ambacho Mungu angetaka uelewe na utende; hili ni jambo ambalo mtu wa kawaida aliye na uwezo wa kufahamu anapaswa kuweza kufanya. Hasa, maneno ambayo Mungu anasema katika hatua ya sasa ni ya wazi na dhahiri zaidi, na Mungu anaonyesha mambo mengi ambayo watu hawajayazingatia, na vilvile kila aina ya hali za binadamu. Maneno Yake yanajumuisha yote na ni dhahiri kama mwanga wa mwezi kamili. Kwa hivyo sasa, watu wanaelewa masuala mengi, lakini bado kuna kitu kinachokosa—watu kuweka neno Lake katika vitendo. Ni lazima watu wapitie vipengele vyote vya ukweli kwa utondoti, na wauchunguze na kuutafuta kwa kina zaidi, badala ya kusubiri tu kufyonza chochote wanachopewa; vinginevyo wanakuwa kupe tu. Wanajua neno la Mungu, lakini hawaliweki katika vitendo. Mtu wa aina hii hapendi ukweli na mwishowe ataondolewa. Ili kuwa kama Petro wa miaka ya tisini, hili linamaanisha kwamba kila mmoja wenu anapaswa kutenda neno la Mungu, aingie kwa kweli katika yale unayoyapitia na apate nuru hata zaidi na kubwa zaidi katika ushirikiano wake na Mungu, ambao utakuwa wa msaada unaozidi daima kwa maisha yenu mwenyewe. Ikiwa mmesoma maneno mengi ya Mungu lakini mnaelewa tu maana ya maandiko na hamna maarifa ya moja kwa moja ya neno la Mungu kupitia uzoefu wenu halisi, basi hutajua neno la Mungu. Kwa kadiri inavyokuhusu, neno la Mungu si uzima, bali tu nyaraka zisizovutia. Na ikiwa unaishi tu kwa kufuata nyaraka zisizovutia, basi huwezi kuelewa asili ya neno la Mungu wala hutaelewa mapenzi Yake. Ni wakati tu ambapo unapitia neno Lake katika matukio yako halisi ndipo maana ya kiroho ya neno la Mungu itafichuka kwako, na ni kupitia uzoefu tu ndiyo unaweza kuelewa maana ya kiroho ya ukweli mwingi na ufungue siri za neno la Mungu. Usipouweka katika vitendo, basi bila kujali jinsi neno Lake lilivyo dhahiri, yote uliyoelewa ni nyaraka na mafundisho matupu tu, ambayo yamekuwa kanuni za kidini kwako. Je, Mafarisayo hawakufanya hivi? Mkitenda na kupitia neno la Mungu, linakuwa la utendaji kwenu; usipotafuta kulitenda, basi neno la Mungu kwako ni hekaya ya mbinguni ya tatu tu. Kwa kweli, mchakato wa kumwamini Mungu ni mchakato wa ninyi kupitia neno Lake na vilevile kupatwa na Yeye, ama kuzungumza dhahiri zaidi, kumwamini Mungu ni kuwa na maarifa na ufahamu wa neno Lake na kupitia na kuishi kwa kudhihirisha neno Lake; huu ndio uhalisi wa ninyi kumwamini Mungu. Ikiwa mnamwamini Mungu na mnatumai kupata uzima wa milele bila kutafuta kutenda neno la Mungu kama kitu kilicho ndani yenu, basi ninyi ni wapumbavu. Hii itakuwa sawa na kwenda katika karamu na kuangalia tu chakula na kujua na kuweza kuvikariri vitu vitamu bila kuvionja kwa kweli. Je, mtu kama huyu si mpumbavu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Punde Unapoelewa Ukweli, Unapaswa Kuuweka Katika Vitendo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 423)

Ukweli ambao mwanadamu anahitaji kuwa nao unapatikana katika neno la Mungu, na ni ukweli wenye manufaa na usaidizi zaidi kwa wanadamu. Ni dawa na ruzuku ambayo miili yenu inahitaji, kitu kinachomsaidia mwanadamu kurejesha tena ubinadamu wake wa kawaida. Ni ukweli ambao mwanadamu anapaswa kujitayarisha nao. Kadiri mnavyotenda neno la Mungu, ndivyo maisha yenu yatakavyositawi haraka zaidi, na ndivyo ukweli utakavyokuwa dhahiri zaidi. Mnapozidi kukua katika kimo, mtaona vitu vya dunia ya kiroho kwa dhahiri zaidi, na ndivyo mtakavyokuwa na nguvu zaidi kumshinda Shetani. Ukweli mwingi ambao hamwelewi utafanywa kuwa dhahiri mtakapotenda neno la Mungu. Watu wengi wanaridhishwa kuelewa tu maandiko ya neno la Mungu na hawalengi kujitayarisha kwa mafundisho badala ya kuzidisha uzoefu wao kwa vitendo, lakini, je, hiyo si njia ya Mafarisayo? Kwa hivyo msemo “Neno la Mungu ni uzima” unawezaje kuwa wa kweli kwao? Maisha ya mtu hayawezi kukua kwa kusoma neno la Mungu tu, bali ni wakati tu neno la Mungu linawekwa katika vitendo. Ikiwa unaamini kwamba kuelewa neno la Mungu ndicho kitu pekee kinachohitajika kuwa na uzima na kimo, basi ufahamu wako umepotoka. Kuelewa neno la Mungu kwa kweli hutokea unapoweka ukweli katika vitendo, na ni lazima uelewe kwamba “ni kwa kutenda ukweli tu ndipo unaweza kueleweka.” Leo, baada ya kusoma neno la Mungu, unaweza tu kusema kwamba unajua neno la Mungu, lakini huwezi kusema kwamba unalielewa. Wengine husema kwamba njia ya pekee ya kutenda ukweli ni kuuelewa kwanza, lakini hii ni sahihi kwa kiwango fulani tu, na hakika si sahihi kikamilifu. Kabla uwe na maarifa ya ukweli fulani, hujapitia ukweli huo. Kuhisi kwamba unaelewa kitu unachosikia katika mahubiri si kuelewa kwa kweli—huku ni kuwa na maneno halisi ya ukweli tu, na si sawa na kuelewa maana ya kweli ndani yake. Kuwa tu na maarifa ya juujuu ya ukweli hakumaanishi kwamba kweli unauelewa ama una maarifa yoyote kuuhusu; maana ya kweli ya ukweli hutokana na kuupitia. Kwa hiyo, ni wakati tu unapopitia ukweli ndiyo unaweza kuuelewa, na ni hapo tu ndiyo unaweza kufahamu sehemu zake zilizofichika. Kukuza uzoefu wako ndiyo njia ya pekee ya kuelewa vidokezo, na kuelewa asili ya ukweli. Kwa hiyo, unaweza kuenda popote ukiwa na ukweli, lakini iwapo hakuna ukweli ndani yako, basi usifikirie kujaribu kuwashawishi hata wanafamilia wako sembuse watu wa kidini. Bila ukweli wewe ni kama vipande vidogo sana vya theluji vinavyopepea. lakini ukiwa na ukweli unaweza kuwa na furaha na uhuru, na hakuna anayeweza kukushambulia. Bila kujali jinsi nadharia fulani ilivyo thabiti, haiwezi kuushinda ukweli. Kukiwa na ukweli, dunia yenyewe haiwezi kuyumba na milima na bahari kusogezwa, wakati ukosefu wa ukweli unaweza kusababisha nyuta zenye nguvu za mji kuangushwa na mabuu. Huu ni ukweli dhahiri.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Punde Unapoelewa Ukweli, Unapaswa Kuuweka Katika Vitendo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 424)

Katika hatua ya sasa, ni muhimu sana kujua ukweli kwanza, na kisha kuuweka katika vitendo na kujitayarisha zaidi na maana ya kweli ya ukweli. Mnapaswa kutafuta kupata hili. Badala ya kutafuta tu kuwafanya wengine wafuate maneno yako, unapaswa kuwasababisha wafuate vitendo vyako. Ni kwa njia hii pekee ndiyo unaweza kupata kitu cha maana. Bila kujali kitakachokukumba, bila kujali utakutana na nani, alimradi una ukweli, utaweza kusimama imara. Neno la Mungu ndicho kitu kimleteacho mwanadamu uzima, si kifo. Ikiwa baada ya kusoma neno la Mungu huchangamki, bali bado wewe ni mfu, basi una kasoro. Ikiwa baada ya muda fulani umesoma maneno mengi ya Mungu, na umesikiza mahubiri mengi ya vitendo, lakini bado uko katika hali ya kifo, basi hili ni thibitisho kwamba wewe si mtu anayethamini ukweli, wala wewe si mtu anayefuatilia ukweli. Ikiwa kweli mngetafuta kumpata Mungu, hamngelenga kujitayarisha na mafundisho na kutumia mafundisho ya juu sana kuwafunza wengine, lakini badala yake mngelenga kupitia neno la Mungu na kuweka ukweli katika vitendo. Je, hampaswi kutafuta kuingia katika hili sasa?

Mungu ana muda mdogo wa kufanya kazi Yake ndani ya mwanadamu, kwa hivyo kunaweza kuwa na matokeo yapi ikiwa hushirikiani na Yeye? Mbona Mungu daima anawataka mtende neno Lake punde mnapolielewa? Ni kwa sababu Mungu amewafichulia maneno Yake, na hatua yenu ifuatayo ni kuyatenda kwa kweli. Mnapotenda maneno haya, Mungu atatekeleza kazi ya nuru na mwongozo. Hivi ndivyo inavyopaswa kufanywa. Neno la Mungu linamwezesha mwanadamu asitawi maishani na asiwe na dalili zozote zinavyoweza kumsababisha mwanadamu apotoke ama asionyeshe hisia. Unasema umesoma neno la Mungu na umelitenda, lakini bado hujapokea kazi yoyote kutoka kwa Roho Mtakatifu. Maneno yako yanaweza tu kumpumbaza mtoto. Huenda watu wengine wasijue ikiwa dhamira zako ni njema, lakini, je, unafikiri kwamba inawezekana Mungu asijue? Ni kwa nini wengine wanatenda neno la Mungu na kupokea nuru ya Roho Mtakatifu, lakini unatenda neno Lake na hupokei nuru ya Roho Mtakatifu? Je, Mungu ana mhemuko? Ikiwa dhamira zako kweli ni njema na wewe ni wa kushirikiana, basi Roho wa Mungu atakuwa nawe. Watu wengine daima hutaka kuonyesha utawala wao wenyewe, lakini kwa nini Mungu hawaruhusu wainuke na kuliongoza kanisa? Watu wengine wanatimiza kazi zao na kutenda wajibu wao tu, lakini kufumba na kufumbua, wamepata idhini ya Mungu. Hilo linawezekanaje? Mungu huchunguza moyo wa ndani sana wa mwanadamu, na watu wanaofuatilia ukweli lazima wafanye hivyo kwa dhamira njema. Watu wasio na dhamira njema hawawezi kusimama imara. Kimsingi kabisa, lengo lenu ni kuacha neno la Mungu lifanye kazi ndani yenu. Yaani, ni kuwa na ufahamu wa kweli wa neno la Mungu mnapolitenda. Pengine uwezo wenu wa kufahamu neno la Mungu ni duni, lakini unapotenda neno la Mungu, Anaweza kurekebisha dosari hii, kwa hivyo hampaswi tu kujua ukweli mwingi, lakini pia lazima muutende. Hili ni lengo kubwa zaidi ambalo haliwezi kupuuzwa. Yesu alivumilia fedheha nyingi na mateso mengi katika maisha Yake ya miaka thelathini na tatu na nusu. Aliteseka sana kwa sababu tu Alitenda ukweli, alifanya mapenzi ya Mungu katika vitu vyote, na alijali tu mapenzi ya Mungu. Haya yalikuwa mateso ambayo Hangepitia iwapo Angejua ukweli bila kuutenda. Ikiwa Yesu angefuata mafundisho ya Wayahudi na awafuate Mafarisayo, basi Hangeteseka. Unaweza kujifunza kutoka kwa matendo ya Yesu kwamba ufanisi wa kazi ya Mungu kwa mwanadamu hutokana na ushirikiano wa mwanadamu, na hili ni jambo ambalo lazima mtambue. Je, Yesu angeteseka jinsi Alivyoteseka msalabani ikiwa Hangetenda ukweli? Je, Angesali sala ya huzuni sana kama Hangetenda kulingana na mapenzi ya Mungu? Kwa hiyo, mnapaswa kuteseka kwa ajili ya kutenda ukweli; mtu anapaswa kupitia mateso ya aina hii.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Punde Unapoelewa Ukweli, Unapaswa Kuuweka Katika Vitendo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 425)

Katika matendo, kushika amri zapaswa kuunganishwa na matendo ya ukweli. Wakati unapozishika amri, mtu anapaswa kutenda ukweli. Wakati anapotenda ukweli, mtu hapaswi kukiuka kanuni za amri au kwenda kinyume na amri. Fanya yale ambayo Mungu anahitaji uyafanye. Kuzishika amri na kuutenda ukweli vinahusiana, bali havikinzani. Zaidi unavyotenda ukweli, ndivyo unavyoweza kutilia maanani zaidi kiini cha amri. Zaidi unavyotenda ukweli, ndivyo utakavyoweza kulielewa zaidi neno la Mungu kama ilivyoonyeshwa katika amri. Kutenda ukweli na kuzishika amri sio vitendo vinavyopingana, lakini badala yake vinahusiana. Mwanzoni, ni kwa kuzishika tu amri ndipo mwanadamu anaweza kuutenda ukweli na kufikia kuipata nuru kutoka kwa Roho Mtakatifu. Lakini hii sio nia ya awali ya Mungu. Mungu inakuhitaji umwabudu Mungu kwa moyo, sio tu kutenda tabia nzuri. Lakini lazima uzishike amri angalau hivi hivi. Hatua kwa hatua, kupitia uzoefu, mwanadamu hupata ufahamu wa wazi zaidi wa Mungu. Yeye huacha kumwasi na kumpinga Mungu, naye anaacha kuitilia shaka kazi ya Mungu. Kwa njia hii mtu anaweza kuzingatia kiini cha amri. Kwa hiyo, kuzishika tu amri bila kutenda ukweli ni hafifu nako hakufanyizi ibada ya kweli ya Mungu kwa sababu bado hujafikia kimo cha kweli. Ukizishika amri bila ukweli, hii ni sawa na kuzingatia tu sheria bila kushawishika. Katika kufanya hivyo, amri zinakuwa sheria yako, ambayo haitakusaidia kukua katika maisha. Badala yake, zitakuwa mzigo wako, nazo zitakufunga imara kama sheria ya Agano la Kale, zikusababishe kuupoteza uwepo wa Roho Mtakatifu. Kwa hiyo, ni kwa kuutenda ukweli tu ndipo utakapoweza kuzishika amri kwa ufanisi. Mtu huzishika amri ili autende ukweli. Unautenda hata ukweli zaidi kwa kuzishika amri. Unapata hata uelewa zaidi wa maana halisi ya amri kwa kuutenda ukweli. Kusudi na maana ya sharti la Mungu ni kwamba lazima mwanadamu azishike amri sio kuzifuata sheria kama mwanadamu anavyoweza kufikiria, lakini inahusiana na mwanadamu kuingia katika maisha. Zaidi unavyokua katika maisha, ndivyo unapata kiwango kibukwa zaidi ambacho utaweza kutii amri. Ingawa amri ni za mwanadamu kuzishika, asili ya amri inakuwa tu dhahiri kupitia kwa uzoefu wa maisha ya mwanadamu. Watu wengi wanadhani kwamba kuzishika amri vizuri inamaanisha “kila kitu kiko tayari, kile kimebaki ni kuchukuliwa juu.” Huku ni kufikiria badhirifu nako sio mapenzi ya Mungu. Wale wanaosema mambo kama haya hawataki kufanya maendeleo nao wanayo tamaa ya mwili. Hili halina maana! Hili haliambatani na uhalisi! Siyo mapenzi ya Mungu kutenda ukweli tu bila kushika amri kwa kweli. Wale wanaofanya hivi ni vilema; wao ni kama watu wasio na mguu mmoja. Wakifuata tu amri kana kwamba wanafuata masharti, lakini hawana ukweli—huku si kuridhisha mapenzi ya Mungu, pia; kama kama wale wasio na jicho moja, watu wanaofanya hivi pia, wanateseka kwa ajili ya aina fulani ya ulemavu. Inaweza kusemwa kwamba ukizishika amri vizuri na kupata uelewa wa wazi wa Mungu wa vitendo, basi utakuwa na ukweli. Kutokana na mtazamo wa uhusiano, utakuwa umepata kimo cha kweli. Unatenda ukweli unaopaswa kutenda na kuzishika amri kwa wakati mmoja bila migogoro ya pande zote. Kuutenda ukweli na kuzishika amri ni mifumo miwili, yote ambayo ni sehemu muhimu ya uzoefu wa maisha ya mtu. Uzoefu wa mtu lazima uafikiane na muungano wa kuzishika amri kwa kuutenda ukweli, sio kugawanya. Hata hivyo, kunazo tofauti na uhusiano kati ya mambo haya mawili.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuzishika Amri na Kuutenda Ukweli

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 426)

Kutangazwa rasmi kwa amri katika enzi mpya ni ushahidi wa ukweli kwamba wanadamu wote katika mkondo huu na wale ambao husikia sauti ya Mungu leo wameingia katika enzi mpya. Huu ni mwanzo mpya kwa ajili ya kazi ya Mungu nao ni mwanzo wa sehemu ya mwisho ya kazi katika mpango wa usimamizi wa Mungu katika kipindi cha miaka elfu sita. Amri za enzi mpya zinaashiria kuwa Mungu na binadamu wameingia katika eneo la mbingu mpya na nchi mpya, na kwamba Mungu, kama vile Yehova alifanya kazi miongoni mwa Waisraeli naye Yesu alifanya kazi miongoni mwa Wayahudi, Ataifanya kazi zaidi ya vitendo na kuifanya kazi zaidi na kubwa zaidi duniani. Pia zinaashiria kwamba kundi hili la watu watapokea agizo zaidi na kubwa zaidi kutoka kwa Mungu, nao watapokea ugavi wa vitendo, malisho, msaada, huduma na ulinzi kutoka kwa Mungu. Zaidi ya hayo watafanywa kupitia katika mazoezi zaidi ya vitendo, na pia kushughulikiwa, kuvunjwa na kusafishwa kwa neno la Mungu. Maana ya amri za enzi mpya ni kubwa sana. Zinaonyesha kwamba Mungu kweli ataonekana kwenye ardhi naye Mungu ataushinda ulimwengu mzima juu ya nchi, akiuonyesha utukufu Wake wote katika mwili. Pia zinaonyesha kwamba Mungu wa vitendo anaenda kuifanya kazi zaidi ya vitendo duniani ili akamilishe yote ambayo Amechagua. Zaidi ya hayo, Mungu atatimiza kila kitu kwa maneno duniani na kufanya wazi amri kwamba “Mungu mwenye mwili huinuka juu zaidi naye ametukuzwa, nao watu wote na mataifa yote hupiga magoti kumwabudu Mungu—ambaye ni mkuu.” Ingawa amri za enzi mpya ni za mwanadamu kuzishika, na ingawa kufanya hivyo ni wajibu wa mwanadamu na jukumu lake, maana ambazo zinawakilisha ni ya kina sana kuweza kuonyeshwa kikamilifu katika neno moja au mawili. Amri za enzi mpya zinachukua nafasi ya sheria za Agano la Kale na maagizo ya Agano Jipya kama zilivyotangazwa rasmi na Yehova na Yesu. Hili ni somo la ndani zaidi, sio jambo rahisi kama mtu anavyoweza kufikiria. Amri za enzi mpya zinazo kipengele cha maana ya vitendo: Zinatumika kama kipengee kinachojitokeza kati ya Enzi ya Neema na Enzi ya Ufalme. Amri za enzi mpya zinahitimisha mazoea yote na maagizo yote ya enzi ya zamani na pia zinahitimisha mazoea yote ya enzi ya Yesu na zile kabla yake. Zinamleta mwanadamu katika uwepo wa Mungu wa vitendo zaidi na kumruhusu mtu kuanza kuupokea ukamilifu wa binafsi wa Mungu, ambazo ni mwanzo wa njia ya kukamilika. Kwa hiyo, ninyi mtamiliki mtazamo sahihi kuelekea amri za enzi mpya na wala hamtazifuata ovyo wala kuzidharau. Amri za enzi mpya zinasisitiza hoja moja: kwamba mwanadamu atamwabudu Mungu wa vitendo Mwenyewe wa leo, ambayo ni kutii kiini cha Roho katika matendo zaidi. Pia zinasisitiza kanuni ambayo Mungu atamhukumu mwanadamu kuwa na hatia au haki Atakapoonekana kama Jua la haki. Amri zinaeleweka kwa urahisi kuliko kutendwa. Hivyo, kama Mungu anataka kumkamilisha mwanadamu, lazima Atafanya hivyo kupitia kwa maneno Yake mwenyewe na mwongozo, mwanadamu hawezi kufikia ukamilifu kupitia asili ya akili yake peke yake. Ikiwa mwanadamu anaweza kuzishika amri za enzi mpya au la inahusiana na maarifa ya mwanadamu ya Mungu wa vitendo. Kwa hiyo, kama unaweza kuzishika amri au la sio swali litakalotatuliwa katika siku chache. Hili ni somo la kina.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuzishika Amri na Kuutenda Ukweli

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 427)

Kuutenda ukweli ni njia ambayo kwayo maisha ya mwanadamu yanaweza kukua. Msipotenda ukweli, mtaachwa na nadharia tu nanyi hamtakuwa na maisha ya kweli. Ukweli ni ishara ya kimo cha mwanadamu. Ikiwa hauutendi ukweli au la inahusiana na kufikia kimo cha kweli. Kama hauutendi ukweli, hutendi kwa haki, au unashawishiwa na hisia na kuujali mwili, basi uko mbali na kuzishika amri. Hili ni somo la kina zaidi. Kunazo kweli nyingi kwa mwanadamu kuingia na mwanadamu kuelewa katika kila enzi. Lakini kunazo amri mbalimbali zinazoambatana na ukweli katika kila enzi. Ukweli ambao mwanadamu huutenda unahusiana na enzi na amri zinazowekwa na mwanadamu pia huhusiana na enzi. Kila enzi inazo kweli zake ambazo lazima zitendwe na amri za kuhifadhiwa. Hata hivyo, kulingana na amri mbalimbali ambazo zimetangazwa rasmi na Mungu, ambayo ni, kulingana na enzi tofauti, lengo na athari ya kuutenda ukweli kwa mwanadamu vinatofautiana kwa kadri iliyo sawa. Inaweza kusemwa kwamba amri huutumikisha ukweli nao ukweli huwepo kuzidumisha amri. Kama kunao ukweli tu, hakutakuwa na mabadiliko katika kazi ya Mungu kuyataja. Hata hivyo, kwa kuzirejelea amri, mwanadamu anaweza kutambua ukubwa wenye nguvu wa kazi iliyofanywa na Roho Mtakatifu naye mwanadamu anaweza kujua enzi ambayo Mungu hufanya kazi. Katika dini, kunao watu wengi ambao wanaweza kutenda ukweli unaotendwa na mwanadamu wa Enzi ya Sheria. Hata hivyo, hawana amri za enzi mpya nao hawawezi kuzishika amri za enzi mpya. Wao huifuata njia ya zamani nao hubaki kama binadamu wa asili. Hawaambatani na namna mpya ya kazi nao hawawezi kuziona amri ya enzi mpya. Kimsingi, kazi ya Mungu haipo. Wao ni kama mtu aliyeshika ganda tupu la yai: Hakuna roho kama hakuna kifaranga ndani mwake. Tukizungumza kwa udhahiri, hakuna maisha. Watu kama hawa hawajaingia katika enzi mpya nao wamekawia nyuma kwa hatua nyingi. Kwa hiyo, ni bure kama watu wanao ukweli wa enzi ya miaka ya zamani lakini hawana amri za enzi mpya. Wengi wenu mnautenda ukweli wa wakati huu lakini hamzishiki amri za wakati huu. Hamtapata chochote, ukweli mnaoutenda utakuwa bure na bila maana naye Mungu hatausifu. Kuutenda ukweli lazima ufanyike kwa njia ambayo Roho Mtakatifu hufanya kazi leo; ni lazima ufanyike kwa kufuata sauti ya Mungu wa vitendo leo. Bila hii, kila kitu ni bure—kama vile kuchota maji na kikapu cha mianzi. Hii ndiyo maana halisi ya kutangazwa rasmi kwa amri za enzi mpya. Ikiwa watu wanapaswa kutii amri hizo, angalau kabisa wanafaa kumjua Mungu mwenye vitendo anayeonekana katika mwili bila kukanganyikiwa. Yaani, watu wanapaswa kuelewa kanuni za kutii sheria. Kutii sheria hakumaanishi kuzifuata kiholela ama bila mpangilio, bali kuzitii ukiwa na msingi, na lengo, na kanuni. Kitu cha kwanza cha kufanikishwa ni maono yako kuwa dhahiri. Ikiwa unao uelewa wa kina wa kazi ya Roho Mtakatifu katika wakati wa sasa nawe uingie namna ya kazi ya leo, kwa kawaida utaona kiini cha kuziweka amri. Kama siku itakuja utakapoona kiini cha amri za enzi mpya nawe utaweza kuzishika amri, basi wakati huo utakuwa umekamilika. Hii ndiyo maana ya kweli ya kuutenda ukweli na kuzishika amri. Ikiwa unaweza kuutenda ukweli au la inategemea jinsi unavyotambua kiini cha amri ya enzi mpya. Kazi ya Roho Mtakatifu itaonekana daima kwa mwanadamu naye Mungu itahitaji zaidi na zaidi kutoka kwa mwanadamu. Kwa hiyo, kweli ambazo mwanadamu huzitenda kwa kweli zitakuwa zaidi na kubwa zaidi nayo madhara ya kuzishika amri yatakuwa ya kushangaza zaidi. Kwa hiyo, ninyi mtautenda ukweli na kuzishika amri kwa wakati mmoja. Hakuna mtu atakayepuuza jambo hili. Hebu ukweli mpya na amri mpya zianze kwa wakati mmoja katika enzi hii mpya.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuzishika Amri na Kuutenda Ukweli

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 428)

Watu wengi wanaweza kuzungumza kidogo juu ya matendo na wanaweza kuzungumza kuhusu fikira zao za kibinafsi, lakini mengi ya hayo ni mwanga kutoka kwa maneno ya wengine. Hayajumuishi chochote kutoka kwa matendo yao binafsi hata kidogo, wala kujumuisha kile wanachokiona kutokana na uzoefu wao. Nimechambua suala hili mapema; usifikiri kwamba Sijui chochote. Wewe ni tishio la bure tu, lakini unazungumza juu ya kumshinda Shetani, juu ya kutoa ushuhuda wa ushindi, na kuishi kwa kudhihirisha mfano wa Mungu? Huu wote ni upuuzi! Je, unadhani kwamba maneno yote ambayo Mungu amenena leo ni ya wewe kupendezwa nayo? Kinywa chako hunena juu ya kutelekeza nafsi yako ya zamani na kuweka ukweli katika matendo, lakini mikono yako inafanya vitendo vingine na moyo wako unapanga hila zingine—wewe ni mtu wa aina gani? Kwa nini moyo wako na mikono yako si kitu kimoja? Kuhubiri kwingi sana kumekuwa maneno matupu; si hili ni jambo la kuvunja moyo? Ikiwa huwezi kuweka neno la Mungu katika matendo, inathibitisha kuwa bado hujaingia katika njia ambayo Roho Mtakatifu hufanya kazi, bado hujapata kuwa na kazi ya Roho Mtakatifu ndani yako, na bado hujapata mwongozo Wake. Ukisema kuwa unaweza tu kuelewa neno la Mungu lakini huwezi kuliweka katika matendo, basi wewe ni mtu asiyependa ukweli. Mungu haji kumwokoa mtu wa aina hii. Yesu alipatwa na maumivu makubwa wakati Aliposulubiwa ili kuwaokoa wenye dhambi, kuwaokoa maskini, na kuwaokoa wale watu wote wanyenyekevu. Kusulubiwa Kwake kulitumika kama sadaka ya dhambi. Ikiwa huwezi kutenda neno la Mungu, basi ni heri uondoke haraka iwezekanavyo; usikawie katika nyumba ya Mungu kama mdoezi. Watu wengi hata huona vigumu kujizuia kufanya mambo ambayo humpinga Mungu kwa dhahiri. Je, si wanaalika kifo? Wanawezaje kuzungumza juu ya kuingia katika ufalme wa Mungu? Je, wataweza kuwa na ujasiri wa kuuona uso wa Mungu? Kula chakula ambacho Mungu hukupa, kufanya mambo ya uhalifu ambayo humpinga Mungu, kuwa mwenye nia mbaya, mwenye kudhuru kwa siri, na mwenye kufanya hila, hata wakati ambapo Mungu anakuruhusu ufurahie baraka ambazo Yeye amekupa—je, huzihisi zikiichoma mikono yako unapozipokea? Je, huhisi aibu? Baada ya kufanya kitu kinachompinga Mungu, baada ya kufanya hila ili “kuwa laghai,” je, huhisi hofu? Kama huhisi chochote, unawezaje kuzungumza juu ya wakati wowote ujao? Tayari kulikuwa hakuna wakati ujao kwako zamani za kale, kwa hiyo ni matarajio yapi makubwa zaidi unayoweza kuwa nayo bado? Ukisema kitu bila haya lakini huhisi lawama, na moyo wako hauna ufahamu, basi haimaanishi kwamba tayari umeachwa na Mungu? Kuzungumza na kutenda kwa kujiachilia na bila kuzuiwa kumekuwa asili yako; je, unawezaje kukamilishwa na Mungu hivi? Je, unaweza kutembea ulimwenguni kote? Ni nani anayeweza kushawishiwa na wewe? Wale ambao wanaijua asili yako ya kweli watakaa mbali nawe. Je, si hii ni adhabu ya Mungu? Kwa jumla, ikiwa kuna mazungumzo tu bila matendo, hakuna ukuaji. Ingawa Roho Mtakatifu anaweza kuwa akifanya kazi ndani yako unapozungumza, kama hutendi, Roho Mtakatifu ataacha kufanya kazi. Ukizidi kuendelea kwa njia hii, kunawezaje kuwa na majadiliano yoyote ya wakati ujao au kutoa nafsi yako yote kwa kazi ya Mungu? Unaweza tu kuzungumza juu ya kutoa nafsi yako yote, lakini hujampa Mungu upendo wako wa kweli. Yote Anayopata kutoka kwako ni upendo wa maneno tu; Yeye hapewi kusudi lako la kutenda ukweli. Je, hiki kinaweza kuwa ndicho kimo chako halisi? Ikiwa utaendelea kwa jinsi hii, utakamilishwa na Mungu lini? Je, huhisi wasiwasi juu ya kesho yako ya giza na majonzi? Je, huhisi kwamba Mungu amepoteza tumaini kwako? Je, hujui kwamba Mungu anatamani kuwakamilisha watu wengi zaidi na wapya zaidi? Je, vitu vya zamani vinaweza kudumu? Wewe huyazingatii maneno ya Mungu leo: Je, unasubiri kesho?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mtu Anayepata Wokovu ni Yule Ambaye Yuko Tayari Kutenda Ukweli

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 429)

Kuwa na uwezo wa kuyaeleza maneno ya Mungu kwa uwazi haimaanishi kwamba wewe unaumiliki uhalisi—mambo si rahisi kama ulivyoweza kufikiria. Ikiwa unaumiliki uhalisi au la haina msingi kwa kile unachokisema, badala yake, inatokana na kile unachoishi kwa kudhihirisha. Wakati maneno ya Mungu yanakuwa maisha yako na kujionyesha kwako kwa asili, hili tu ndilo linalochukuliwa kama uhalisi, na hili tu ndilo linachukuliwa kama wewe kumiliki uelewa na kimo cha kweli. Lazima uwe na uwezo wa kuhimili uchunguzi kwa muda mrefu, na lazima uwe na uwezo wa kuishi kwa kuidhihirisha sura ambayo inahitajika kwako na Mungu; isiwe mkao tu, lakini ni lazima ibubujike kwa kawaida kutoka ndani mwako. Hapo tu ndipo basi utakapokuwa na uhalisi kikweli, na ndipo tu basi utakapopata maisha. Wacha Nitumie mfano wa jaribio la watendaji huduma ambao kila mtu ana uzoefu nao. Mtu yeyote anaweza kuzungumzia nadharia zenye fahari sana kuhusu watendaji huduma, na kila mtu ana ufahamu unaofaa wa mada hii; wanazungumza juu yake na kila usemi unazidi ule wa awali, kana kwamba kuna mashindano. Hata hivyo, kama mwanadamu hajapitia jaribio kubwa, ni vigumu kusema ana ushahidi mzuri. Kwa ufupi, kuishi kwa kudhihirisha kwa mwanadamu bado kuna upungufu mwingi, na hii inatofautiana na uelewa wake. Kwa hiyo, bado hakijakuwa kimo halisi cha mwanadamu, na bado hayajakuwa maisha ya mwanadamu. Kwa sababu uelewa wa mwanadamu haujaletwa katika uhalisi, kimo chake bado ni kama ngome iliyojengwa kwenye mchanga, ikiyumbayumba na ikiwa karibu kuanguka. Mwanadamu anao uhalisi kidogo mno—ni vigumu kuupata uhalisi wowote katika mwanadamu. Kunao uhalisi kidogo mno unaobubujika kwa asili kutoka kwa mwanadamu na uhalisi wote katika maisha yake umelazimishwa, ndiyo maana nasema kwamba mwanadamu hamiliki uhalisi wowote. Usiweke hisa nyingi sana katika wanadamu wakisema kwamba upendo wao wa Mungu haubadiliki kamwe—hiki tu ndicho kile wao husema kabla ya kukabiliwa na majaribu. Mara tu wanapokabiliwa na majaribu kwa ghafla, mambo ambayo wao hunena kwa mara nyingine tena hayalingani na uhalisi, na kwa mara nyingine yatathibitisha kwamba wanadamu hawana uhalisi. Inaweza kusemwa kwamba wakati wowote unapokumbana na mambo ambayo hayalingani na dhana zako nayo yanakuhitaji kujiweka kando, haya ni majaribu yako. Kabla mapenzi ya Mungu kufichuliwa, kuna mtihani mkali kwa kila mwanadamu, jaribio kubwa kwa kila mtu—je, waweza kuliona wazi jambo hili? Wakati Mungu anapotaka kuwajaribu wanadamu, Yeye daima huwaacha kufanya maamuzi yao kabla ya ukweli wa uhalisi kufichuliwa. Yaani wakati Mungu anamweka mwanadamu katika majaribu, kamwe Yeye hatakwambia ukweli, na hivyo ndivyo wanadamu wanaweza kufichuliwa. Hii ni njia mojawapo ambayo Mungu huifanya kazi yake, ili kuona kama unamwelewa Mungu wa leo, na ili kuona kama unaumiliki uhalisi wowote. Je, kweli wewe huna shaka yoyote kuhusu kazi ya Mungu? Je, utaweza kusimama imara wakati jaribio kuu linakujia? Ni nani anayethubutu kusema maneno kama vile “Nahakikisha hakutakuwa na matatizo”? Nani anayethubutu kusema maneno kama vile “Wengine wanaweza kuwa na mashaka, lakini Mimi sitakuwa na shaka kamwe”? Kama vile nyakati Petro alipitia majaribu—alikuwa siku zote akizungumza maneno makubwa kabla ukweli haujafichuliwa. Huu sio udhaifu wa kibinafsi wa kipekee kwa Petro; hii ni shida kubwa zaidi inayomkabili kila mwanadamu sasa. Kama ningetembelea maeneo kadhaa, au kama ningewatembelea ndugu na dada kadhaa, kuuangalia uelewa wenu wa kazi ya Mungu ya leo, hakika mngeweza kweli kuzungumza kuhusu mengi ya uelewa wenu, nayo ingeonekana kwamba ninyi hamna mashaka yoyote. Kama ningewauliza: “Je, kweli waweza kutabainisha kwamba kazi ya leo inatekelezwa na Mungu Mwenyewe? Bila shaka yoyote”? ungejibu bila shaka: “Bila shaka yoyote, ni kazi inayotekelezwa na Roho wa Mungu.” Mara tu unapojibu kwa namna hiyo, kwa hakika usingekuwa hata na chembe cha shaka na unaweza hata kuhisi starehe kubwa—unaweza kuhisi kuwa umepata uhalisi kiasi kidogo. Wale ambao mara nyingi huelewa mambo kwa njia hii ni wale ambao wanamiliki uhalisi kidogo zaidi; kadri mtu anavyodhani kwamba amelipata, ndivyo atakavyokosa uwezo wa kusimama imara katika majaribio. Ole wao walio na kiburi na wenye maringo, na ole wao wasio na maarifa ya wao wenyewe. Watu kama hawa ni hodari katika kuzungumza ilhali huendelea vibaya zaidi katika matendo yao. Wakati kuna dalili ndogo zaidi ya matatizo, watu hawa wataanza kuwa na mashaka na mawazo ya kukata tamaa huingia akilini mwao. Hawana umiliki wa uhalisi wowote; yote waliyo nayo ni nadharia zenye fahari zaidi kuliko zile za dini, bila ya hali halisi ambazo Mungu anadai sasa. Nachukizwa zaidi na wale wanaosema kuhusu nadharia tu nao hawana uhalisi. Wao kufanya kilio kikubwa zaidi wanapoitenda kazi yao, lakini wao husambaratika punde tu wanapokabiliwa na uhalisi. Je, si inaonyesha kwamba watu hawa hawana uhalisi? Haijalishi jinsi upepo na mawimbi yalivyo kali, kama unaweza kubaki umesimama bila hata dalili ya shaka kuingia mawazoni mwako, na unaweza kusimama imara na usiwe kati hali ya kukana hata kama hakuna mtu mwingine aliyebaki, basi hili linachukuliwa kama wewe kuwa na uelewa wa kweli na wewe kuwa na umiliki wa uhalisi. Ukifuata njia yoyote ambayo upepo unavuma, ukiwafuata walio wengi na kujifunza kusema yale ambayo wengine wanasema, haijalishi jinsi gani unavyosema mambo hayo vizuri, sio thibitisho kwamba unao umiliki wa uhalisi. Kwa hiyo, napendekeza kwamba usiwe na haraka ya kupiga kelele kwa maneno matupu. Je, unaijua kazi ambayo Mungu ataitekeleza? Usitende kama Petro mwingine usije ukajiletea aibu na usiweze tena kutembea bila haya—hii haimfaidi mtu yeyote. Wanadamu wengi hawana kimo cha kweli. Mungu ametekeleza kazi kubwa sana lakini hajafanya uhalisi kuwajia watu; kwa kuwa sahihi zaidi, Mungu hajawahi kumwadibu yeyote binafsi. Baadhi ya watu wamefichuliwa na majaribio kama haya, na minyiri yao ya dhambi ikitambaa nje zaidi na zaidi, wakifikiri kwamba ni rahisi kumhadaa Mungu, wanaweza kumchukulia Mungu kwa kutojali, na kufanya chochote wanachotaka. Kwa kuwa hawawezi hata kustahimili majaribu ya aina hii, kadri majaribio yenye changamoto yasivyowezekana, na uhalisi pia hauwezekani. Je, si hii ni kujaribu kumpumbaza Mungu? Kuwa na uhalisi si kitu ambacho kinaweza kubuniwa, na wala si kitu ambacho unaweza kukipata kutokana na maarifa yako kukihusu. Unalingana na kimo chako cha ukweli, na unalingana na kama unao uwezo wa kuhimili majaribu yote. Je, unaelewa sasa?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuuweka tu Ukweli Katika Matendo Ndiko Kuwa na Uhalisi

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 430)

Masharti ya Mungu kwa wanadamu siyo tu kuweza kuzungumza kuhusu uhalisi. Je, si hiyo itakuwa rahisi sana? Kwa nini basi Mungu anazungumza kuhusu kuingia katika maisha? Kwa nini Anaongea kuhusu mabadiliko? Kama mtu ana uwezo wa mazungumzo matupu tu kuhusu uhalisi, mabadiliko katika tabia yangeweza kupatikana? Kulifunza kundi la wanajeshi wazuri wa ufalme sio sawa na kuwafunza wanadamu ambao wanaweza tu kuongea kuhusu uhalisi au watu ambao hujigamba tu, bali ni kuwafunza wanadamu ambao wanajivunia tu, lakini wanadamu ambao wanaweza kuishi kwa kudhihirisha maneno ya Mungu wakati wote, ambao ni wagumu bila kujali vikwazo wanavyokumbana navyo, na wanaoishi kwa mujibu wa maneno ya Mungu wakati wote, na hawarudi kwa ulimwengu. Huu ndio uhalisi ambao Mungu anauzungumzia, nayo ni matakwa ya Mungu kwa binadamu. Kwa hiyo, usiuone uhalisi ulionenwa na Mungu kama rahisi sana. Kupata nuru tu kwa Roho Mtakatifu sio sawa na kuumiliki uhalisi: Hiki sicho kimo cha wanadamu, lakini neema ya Mungu, nayo haihusishi mafanikio yoyote ya wanadamu. Kila mwanadamu ni lazima ayavumilie mateso ya Petro, na hata zaidi aumiliki utukufu wa Petro, ambao ndio watu huishi kwa kudhihirisha baada ya kupata kazi ya Mungu. Hii tu ndiyo inaweza kuitwa uhalisi. Usidhani kwamba utamiliki uhalisi kwa sababu unaweza kuzungumza kuhusu uhalisi. Huu ni uongo, huu haulingani na mapenzi ya Mungu, na hauna maana halisi. Usiseme mambo kama haya katika siku zijazo—komesha misemo kama hii! Wale wote walio na uelewa wa uongo wa maneno ya Mungu ni makafiri. Hawana maarifa yoyote halisi, sembuse kimo chochote halisi; wao ni watu wenye kujigamba bila ya uhalisi. Hiyo ni, wale wote wanaoishi nje ya dutu ya maneno ya Mungu ni makafiri. Wale wanaoonekana kuwa makafiri na wanadamu ni wanyama mbele za Mungu, na wale wanaoonekana kuwa makafiri na Mungu ni wale ambao hawana maneno ya Mungu kama maisha yao. Kwa hiyo, wale ambao hawana uhalisi wa maneno ya Mungu nao wanashindwa kuishi kwa kudhihirisha maneno ya Mungu ni makafiri. Nia ya Mungu ni kufanya iwe kwamba kila mmoja anaishi kwa kudhihirisha uhalisi wa maneno ya Mungu. Sio tu kwamba kila mtu anaweza kuzungumza kuhusu uhalisi, lakini muhimu zaidi, kwamba kila mmoja anaweza kuishi kwa kudhihirisha uhalisi wa maneno ya Mungu. Uhalisi ambao mwanadamu anautambua ni wa juu juu sana, hauna thamani, hauwezi kutimiza mapenzi ya Mungu, ni duni sana, hata haustahili kutajwa, una upungufu sana, na uko mbali sana na kiwango cha mahitaji ya Mungu. Kila mmoja wenu atapitia ukaguzi mkuu ili kuona ni nani kati yenu anayejua tu kuzungumza kuhusu uelewa wake lakini hawezi kuonyesha njia, na kuona ni nani kati yenu ni taka bure. Kumbuka hili katika siku zijazo! Usizungumze kuhusu uelewa mtupu—zungumza tu kuhusu njia ya utendaji, na kuhusu uhalisi. Geuka kutoka maarifa halisi hadi kwenye vitendo halisi, na kisha geuka kutoka kutenda hadi kuishi kwa kudhihirisha uhalisi. Usiwahutubie wengine, na usizungumze kuhusu maarifa ya ukweli. Kama uelewa wako ni njia, basi unaweza kuuachilia; kama si njia, basi tafadhali nyamaza, na uache kuongea. Kile unachosema ni bure. Ni baadhi tu ya maneno ya uelewa ya kumpumbaza Mungu na kuwafanya wengine wakuonee wivu. Si hilo ni lengo lako? Je, hii si kuwachezea wengine kimakusudi? Je, kunayo thamani yoyote katika hili? Zungumza tu kuhusu uelewa baada ya kuwa na uzoefu kuuhusu, na kisha hutakuwa unajisifu tena. La sivyo wewe ni mtu tu ambaye anasema maneno yenye kiburi. Huwezi hata kuyashinda mambo mengi au kuasi dhidi ya mwili wako wenyewe katika uzoefu wako halisi, siku zote ukifanya chochote unachoelekezwa kukifanya kwa tamaa zako, sio kwa kuyaridhisha mapenzi ya Mungu, lakini bado unayo nyongo ya kuzungumzia uelewa wa kinadharia—huna haya! Bado unayo nyongo ya kuzungumza kuhusu uelewa wako wa maneno ya Mungu—wewe ni fidhuli jinsi gani! Kuhutubu na kujisifu kumekuwa asili yako, na umekuwa na desturi ya kufanya hili. Unalijua sana kila wakati unapotaka kuzungumza, unalifanya kwa ustadi na bila kufikiria, nawe unajiingiza katika mapambo inapokuja wakati wa kutenda. Je, si hii ni kuwapumbaza wengine? Unaweza kuwapumbaza wanadamu, lakini Mungu hawezi kupumbazwa. Wanadamu hawajui na hawana utambuzi, lakini Mungu anatilia maanani masuala hayo, naye hatakusaza. Ndugu na dada zako wanaweza kukutetea, wakiusifu uelewa wako, wakipendezwa nawe, lakini ikiwa huna uhalisi, Roho Mtakatifu hatakusaza. Pengine Mungu wa matendo hatazikaripia dosari zako, lakini Roho wa Mungu hataweka makini yoyote kwako, na hiyo itatosha wewe kuvumilia. Je, unaamini hili? Zungumza zaidi kuhusu uhalisi wa utendaji; Je, umeshasahau tayari? Zungumza zaidi kuhusu njia za kiutendaji; Je, ushasahau tayari? “Zungumza kwa uchache kuhusu nadharia za fahari au mazungumzo mazuri yasiyo na maana, na ni bora kuanza mazoezi kuanzia sasa.” Je, umesahau maneno haya? Je, huelewi yoyote haya? Je, hauna uelewa wa mapenzi ya Mungu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuuweka tu Ukweli Katika Matendo Ndiko Kuwa na Uhalisi

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 431)

Mnapaswa kuwa mkijifunza mafunzo yaliyo ya uhalisi zaidi. Hakuna haja ya hayo mazungumzo matupu, yenye kuvutia na ambayo watu wanayastahi. Linapokuja suala la kuzungumza kuhusu maarifa, ya kila mtu ni ya juu kuliko ya aliyetangulia, lakini bado hawana njia ya kutenda. Ni watu wangapi wameelewa kanuni za kutenda? Ni wangapi wamejifunza mafunzo halisi? Ni nani anayeweza kufanya ushirika kuhusu uhalisi? Kuweza kuzungumza juu ya maarifa ya maneno ya Mungu si sawa na kimo chako halisi. Hilo linaishia kuonyesha tu kuwa ulizaliwa ukiwa na akili, kwamba wewe una kipaji. Ikiwa huwezi kuionyesha njia, basi matokeo yatakuwa bure, na wewe utakuwa taka isiyo na maana! Je, hujifanyi tu ikiwa huwezi kusema chochote kuhusu njia halisi ya kufanya vitendo? Je, hujifanyi ikiwa huwezi kutoa uzoefu wako mwenyewe halisi kwa wengine, na hivyo kuwapa mafunzo ambayo wanaweza kujifunza kwayo au njia ya kufanya vitendo? Je, wewe si bandia tu? Una thamani gani? Mtu kama huyo angeweza tu kushikilia sehemu ya kuwa “mvumbuzi wa nadharia ya ujamaa,” na si “mchangiaji wa kuleta ujamaa.” Kutokuwa na uhalisi ni kutokuwa na ukweli. Kutokuwa na uhalisi ni kutokuwa na thamani. Kutokuwa na uhalisi ni kukosa uhai. Kutokuwa na uhalisi ni “kuwa na fikira za Umaksi na Ulenini,” bila thamani kama marejeo. Ninamsihi kila mtu kufunga mdomo kuhusu nadharia na kuzungumzia kitu ambacho ni halisi, kitu ambacho ni cha kweli na thabiti, kujifunza baadhi ya “sanaa za kisasa,” kusema kitu ambacho ni halisi, kuchangia uhalisi kiasi, na kuwa na roho ya kujitoa. Uukabili uhalisi unapozungumza; usijiingize katika mazungumzo yasiyokuwa na uhalisi na yaliyotiwa chumvi ili kuwafurahisha watu au wakae na kukustahi. Thamani yake ni nini? Kuna maana gani katika kuwafanya watu kukutendea kwa ukunjufu? Kuwa “stadi” kiasi katika usemi wako, tenda haki zaidi kiasi katika matendo yako, kuwa mwenye busara zaidi kiasi katika jinsi unavyoshughulikia vitu, kuwa mwenye vitendo zaidi kiasi katika kile unachosema, fikiri kuhusu kuleta manufaa kwa nyumba ya Mungu katika kila tendo, acha dhamiri yako unapokuwa na muhemuko, usilipize wema kwa chuki, au kutokuwa na shukrani kwa wema, na usiwe mnafiki, usije ukawa na “ushawishi mbaya.” Unapokula na kunywa maneno ya Mungu, yahusishe zaidi na uhalisi, na unapowasiliana, zungumza zaidi kuhusu mambo ya uhalisi. Usijikweze; Mungu hataridhishwa na hilo. Katika miingiliano yako na wengine, kuwa mstahimilivu zaidi, fanya mazoezi zaidi ya kukubali, kuwa mkarimu zaidi kiasi, na ujifunze kutoka kwa “roho ya waziri mkuu.”[a] Unapokuwa na mawazo ambayo si mazuri, fanya mazoezi zaidi ya kuukana mwili zaidi. Unapofanya kazi, zungumza zaidi kuhusu njia halisi na usiwe na majivuno sana, vinginevyo kile unachosema hakitaweza kufikiwa na watu. Starehe kidogo, mchango zaidi—onyesha roho yako ya kujitolea isiyo ya ubinafsi. Fikirieni zaidi makusudi ya Mungu, sikilizeni dhamiri zenu zaidi, kuweni wenye kuzingatia zaidi, na msisahau jinsi ambavyo Mungu huwanenea kila siku kwa uvumilivu na kwa dhati. Soma “shajara ya mwaka ya zamani” mara kwa mara. Omba zaidi na ufanye ushirika mara kwa mara. Usiendelee kuwa mtu aliyekanganyikiwa sana, bali onyesha busara zaidi na upate umaizi fulani. Mkono wa dhambi unaponyooka, urudishe nyuma na usiuache utandae zaidi. Haina maana! Mnachokipata kutoka kwa Mungu si chochote bali laana; kuweni waangalifu. Acheni mioyo yenu iwe na huruma kwa wengine na siku zote msiwapige kwa silaha mkononi. Shirikini zaidi kuhusu maarifa ya ukweli na mzungumze zaidi kuhusu maisha, mkiwa na roho ya kuwasaidia wengine. Tendeni zaidi na kusema kidogo. Tieni mengi zaidi katika vitendo na kidogo katika utafiti na uchambuzi. Acheni mguswe zaidi na Roho Mtakatifu, na mpeni Mungu fursa zaidi ya kuwakamilisha. Ondoeni sifa zaidi za kibinadamu; bado mna sifa nyingi za kibinadamu za kufanya mambo na matendo na namna yenu ya juujuu ya kufanya bado ni ya kuwachukiza wengine: Ziondoeni hizi zaidi. Hali zenu za akili bado zinachukiza sana; tumieni muda zaidi kuzirekebisha. Bado mnawapa watu hadhi kuu; mpeni Mungu hadhi zaidi, na usiwe mtu usiyekuwa na akili. “Hekalu” limekuwa la Mungu daima na halipaswi kutwaliwa na watu. Kwa ufupi, sisitiza zaidi juu ya haki na kidogo katika mihemuko. Ni bora zaidi kuuondoa mwili. Zungumza zaidi kuhusu uhalisi na kidogo kuhusu maarifa; kilicho bora zaidi kuwa kimya na kutosema lolote. Zungumza zaidi juu ya njia ya kutenda na ufanyemajivuno kidogo zaidi yasiyo na thamani. Itakuwa bora zaidi kuanza kutenda sasa.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Sisitiza Uhalisi Zaidi

Tanbihi:

a. Roho ya waziri mkuu: Ni msemo wa jadi wa Kichina ambao hutumika kuelezea mtu ambaye ni mkarimu na anayekubali mawazo ya wengine.

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 432)

Matakwa ya Mungu kwa watu si ya juu sana. Ikiwa watu wataweka hata jitihada kidogo wataweza kupata “alama ya kupita.” Kwa kweli, kufahamu, kujua, na kuelewa ukweli kunatatiza sana kuliko kuutenda ukweli; kuujua na kuutambua ukweli kunakuja baada ya kuutenda ukweli; hizi ndizo hatua na njia ambayo kwayo Roho Mtakatifu hufanya kazi. Unawezaje kutotii? Je, unaweza kupata kazi ya Roho Mtakatifu kwa kufanya mambo kwa namna yako? Je, Roho Mtakatifu hufanya kazi kwa kuzingatia ridhaa yako, au kwa msingi wa kasoro zako kulingana na maneno ya Mungu? Haina maana ikiwa huwezi kuliona hili kwa uwazi. Kwa nini watu wengi zaidi wametumia jitihada nyingi kusoma maneno ya Mungu lakini wana maarifa tu na hawawezi kusema kitu chochote kuhusu njia halisi baada ya hapo? Unadhani kwamba kuwa na maarifa ni sawa na kuwa na ukweli? Je, huo si mtazamo uliokanganywa? Unaweza kuzungumza maarifa mengi kama mchanga ulivyo ufuoni, lakini hakuna yaliyo na njia ya kweli. Je, wewe hujaribu kuwapumbaza watu kwa kufanya hivi? Je, unafanya maonyesho matupu, bila dutu ya kuyasitiri? Mienendo yote kama hii ni ya madhara kwa watu! Kadiri nadharia inavyokuwa ya juu, ndivyo inavyokosa uhalisi zaidi, na ndivyo inavyokosa zaidi uwezo wa kuwapeleka watu katika uhalisi; kadiri nadharia inavyokuwa ya juu, ndivyo inavyokufanya umuasi na kumpinga Mungu. Usizichukulie nadharia za kiwango cha juu kama hazina ya thamani; zina madhara, na hazina kazi yoyote! Pengine baadhi ya watu wanaweza kuzungumza juu ya nadharia za juu sana—lakini nadharia hizo hazina kitu chochote cha uhalisi, maana watu hawajazipitia wao binafsi, na kwa hiyo hawana njia ya kutenda. Watu kama hao hawawezi kuwaongoza wengine katika njia sahihi, na watawapotosha. Je, hili halileti madhara kwa watu? Angalau kabisa, unapaswa kuweza kutatua shida za sasa za watu na kuwaruhusu kupata kuingia; hii tu ndiyo inachukuliwa kama ibada, na baada ya hapo ndipo utakuwa na sifa za kufaa kumfanyia Mungu kazi. Siku zote usizungumze maneno ya kifahari, ya ajabu, na usiwalazimishe watu kukutii wewe pamoja na vitendo vyako visivyofaa. Kufanya hivyo hakutaleta matokeo, na kunaweza kuongeza tu mkanganyiko wa watu. Kuendelea kwa namna hii kutazalisha mafundisho mengi, ambazo zitawafanya watu wakuchukie. Hivyo ndivyo ulivyo udhaifu wa mwanadamu, na kwa kweli unadhalilisha. Kwa hivyo, zungumza zaidi juu ya matatizo ambayo yapo kwa kweli. Usiyachukulie matukio ya watu wengine kama mali yako binafsi na kuyaonyesha waziwazi ili wengine wastahi; unapaswa kutafuta suluhisho lako binafsi mwenyewe. Hiki ndicho ambacho kila mtu anapaswa kuweka katika vitendo.

Ikiwa kile unachoshiriki kinaweza kuwapa watu njia ya kufuata, basi hiyo ni sawa na wewe kuwa na uhalisi. Haijalishi kile unachosema, ni lazima uwalete watu katika vitendo na kuwapatia njia wanayoweza kuifuata. Usiwaruhu tu wapate maarifa; lililo muhimu zaidi ni kuwa na njia ya kufuata. Ili watu wamwamini Mungu, lazima waitembee njia inayoongozwa na Mungu katika kazi Yake. Yaani, mchakato wa kumwamini Mungu ni mchakato wa kuitembea njia inayoongozwa na Roho Mtakatifu. Vivyo hivyo, unapaswa kuwa na njia ambayo unaweza kuitembea kwa vyovyote vile, na unapaswa kuenenda kwenye njia ya kukamilishwa na Mungu. Usibaki nyuma sana, na usijishughulishe na mambo mengi sana. Ikiwa tu unaitembea njia inayoongozwa na Mungu bila kusababisha mwingiliano ndipo unaweza kupokea kazi ya Roho Mtakatifu na kuwa na njia ya kuingia. Hili tu ndilo linahesabika kama lenye kufaa makusudi ya Mungu na kutimiza wajibu wa binadamu. Kama mtu binafsi katika mkondo huu, kila mtu anapaswa kutimiza wajibu wake kikamilifu, fanya zaidi yale ambayo watu wanapaswa kuyafanya, na usitende kwa ukaidi. Watu wanaotekeleza kazi wanapaswa kuweka maneno yao wazi, watu wanaofuata wanapaswa kusisitiza zaidi kuhimili ugumu na kutii, na kila mtu anapaswa kutunza nafasi yake na kutotenda kwa namna isiyofaa. Linapaswa lieleweke wazi katika moyo wa kila mtu namna ambavyo wanapaswa kutenda na ni kazi gani wanapaswa kutimiza. Chukua njia inayoongozwa na Roho Mtakatifu; usipotoke au kukosea. Lazima muione kazi ya leo waziwazi. Kuingia katika njia ya leo ya kufanya kazi ndicho kitu mnachopaswa kutenda. Ni kitu cha kwanza mnachopaswa kuingia. Msipoteze maneno yoyote zaidi kwenye mambo mengine. Kufanya kazi ya nyumba ya Mungu leo ni jukumu lenu, kuingia katika mbinu ya kazi ya leo ni wajibu wenu, na kutenda ukweli wa leo ni mzigo wenu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Sisitiza Uhalisi Zaidi

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 433)

Mungu ni Mungu wa uhalisi: kazi Zake zote ni halisi, maneno yote Anayoyanena ni halisi, na ukweli wote Anaouonyesha ni halisi. Kila kisicho maneno Yake ni kitupu, kisichokuwepo, na kisicho timamu. Leo, Roho Mtakatifu yupo kwa ajili ya kuwaongoza watu katika maneno ya Mungu. Ikiwa watu wanatafuta kuingia katika uhalisi, basi ni lazima wauandame uhalisi, na waujue uhalisi, baadaye ni lazima wapitie uhalisi, na kuishi kwa kudhihirisha uhalisi. Kadiri watu wanavyoujua uhalisi zaidi, kadiri wanavyoweza kugundua ikiwa maneno ya wengine ni halisi; kadiri watu wanavyojua uhalisi zaidi, ndivyo wanavyokuwa na dhana chache zaidi; kadiri watu wanavyopitia uhalisi zaidi, kadiri wanavyojua zaidi matendo ya Mungu wa uhalisi, na ndivyo inavyokuwa rahisi kwao kujiweka huru kutokana na tabia zao potovu na za kishetani; kadiri watu walivyo na uhalisi mkubwa, ndivyo wanavyomjua Mungu zaidi na kuuchukia mwili zaidi na kupenda ukweli; na kadiri watu walivyo na uhalisi mkubwa, ndivyo wanavyofika karibu na ubora wa mahitaji ya Mungu. Watu waliopatikana na Mungu ni wale walio na uhalisi, na wanaojua uhalisi; wale ambao wamepatikana na Mungu wamepata kuyajua matendo halisi ya Mungu kutokana na kupitia katika uhalisi. Kadiri hasa unavyoshirikiana zaidi na Mungu na kuudhibiti mwili wako, ndivyo utakavyopokea zaidi kazi ya Roho Mtakatifu, ndivyo utakavyopata uhalisi zaidi, na ndivyo utapatiwa nuru zaidi na Mungu—na hivyo ukubwa wa ufahamu wako wa matendo halisi ya Mungu. Ikiwa unaweza kuishi katika mwangaza wa sasa wa Roho Mtakatifu, njia ya sasa ya kutenda itakuwa wazi kwako, na utaweza kujitenga zaidi na dhana za kidini na vitendo vilivyopita zamani. Leo tunalenga uhalisi: Kadiri watu walivyo na uhalisi zaidi, ndivyo ufahamu wao wa ukweli unavyokuwa wazi, na ufahamu wao wa mapenzi ya Mungu unaongezeka. Uhalisi unaweza kuzishinda nyaraka zote na mafundisho yote ya kidini, unaweza kushinda nadharia na utaalamu wote, na kadiri watu wanavyoangazia uhalisi zaidi, ndivyo wanavyompenda Mungu kwa dhati zaidi na kuyatamani maneno Yake. Ikiwa daima unalenga uhalisi, falsafa yako ya maisha, dhana za kidini, na tabia asilia zitafutwa kutokana na kazi ya Mungu. Wale wasiouandama uhalisi, na hawafahamu uhalisi, wanaelekea kutafuta kile kilicho na nguvu za juu, na watalaghaiwa kwa urahisi. Roho Mtakatifu hana namna ya kufanya kazi ndani ya watu kama hao, na kwa hivyo wanajisikia watupu, na kwamba maisha yao hayana maana.

Roho Mtakatifu anaweza tu kufanya kazi ndani yako ukijifunza kweli, ukitafuta kweli, ukiomba kweli, na ukiwa radhi kuteseka kwa ajili ya kuutafuta ukweli. Wale ambao hawautafuti ukweli hawana chochote ila tu nyaraka na mafundisho ya kidini, na nadharia tupu, na wale wasio na ukweli kiasili wana dhana nyingi kuhusu Mungu. Watu kama hawa hutamani tu Mungu aibadilishe miili yao ya nyama kuwa miili ya kiroho ili kwamba waweze kupaa katika mbingu ya tatu. Hawa watu ni wapumbavu kiasi gani? Wote wasemao mambo sampuli hii hawana ufahamu wa Mungu, au uhalisi; watu kama hawa hawawezi kushirikiana na Mungu, na wanaweza tu kusubiri bila kufanya chochote. Ikiwa watu wanataka kuelewa ukweli, na kuuona ukweli wazi wazi, na ikiwa, aidha, wanataka kuingia ndani ya ukweli, na kuuweka katika vitendo, ni sharti wajifunze kweli, watafute kweli, na wawe na hitaji la kweli. Unapotamani, na unaposhirikiana na Mungu kweli, Roho wa Mungu kwa hakika atakugusa na kufanya kazi ndani yako, jambo ambalo litakuletea nuru zaidi na kukupa ufahamu zaidi kuhusu uhalisi na kuwa wa msaada mkubwa kwa maisha yako.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jinsi ya Kujua Uhalisi

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 434)

Ikiwa watu wanataka kumjua Mungu, ni sharti kwanza wajue kuwa Mungu ni Mungu halisi, na ni sharti wajue maneno ya Mungu, kuonekena halisi kwa Mungu katika mwili, kazi halisi ya Mungu. Ni baada tu ya kujua kwamba kazi ya Mungu ni halisi ndiyo utaweza kweli kushirikiana na Mungu, na ni kupitia kwa njia hii tu ndipo utaweza kutimiza ukuaji wa maisha yako. Wale wote wasiokuwa na ufahamu wa uhalisi hawana namna ya kuyapitia maneno ya Mungu, wametekwa katika dhana zao, wanaishi katika mawazo yao, na hivyo hawana ufahamu wa maneno ya Mungu. Kadiri ufahamu wako kuhusu uhalisi ulivyo mkubwa, ndivyo unakuwa karibu zaidi na Mungu, na ndivyo unakuwa rafiki Yake wa karibu zaidi; jinsi unavyotafuta zaidi kutokuwa yakini na udhahania, na mafundisho ya kidini, ndivyo unavyojitenga zaidi na Mungu, na ndivyo utakavyohisi zaidi kuwa kuyapitia maneno ya Mungu ni kazi na ni kugumu, na kwamba huna uwezo wa kuingia. Ikiwa unataka kuingia katika uhalisi wa maneno ya Mungu, na katika njia sahihi ya maisha yako ya kiroho, ni sharti kwanza ujue uhalisi na ujitenge na vitu visivyo yakini na vya miujiza—ambako ni kumaanisha kuwa, kwanza ni sharti uelewe jinsi Roho Mtakatifu anapeana nuru na kukuongoza kutoka ndani. Kwa njia hii, ikiwa kwa kweli unaweza kuielewa kazi ya Roho Mtakatifu ndani yako, utakuwa umeingia katika njia sahihi ya kufanywa mkamilifu na Mungu.

Leo, kila kitu kinaanza kwa uhalisi. Kazi ya Mungu ndiyo halisi zaidi, na inaweza kuguswa na watu; ndicho kitu kinachoweza kupitiwa na wanadamu, na kufanikisha. Ndani ya watu mna mengi ambayo si yakini na ya miujiza, ambayo yanawazuia kuijua kazi ya sasa ya Mungu. Hivyo katika mazoea yao mara zote hupotoka na kuhisi vigumu, ambayo yote yanasababishwa na dhana zao. Watu wanashindwa kuelewa kanuni za kazi ya Roho Mtakatifu, hawajui uhalisi, na kwa hivyo daima njia zao za kuingia ni hasi. Wanatazama mahitaji ya Mungu kwa mbali, bila kuweza kuyatimiza; wanaona tu kwamba maneno ya Mungu kwa hakika ni mazuri, ila hawawezi kupata njia ya kuingilia. Roho Mtakatifu anafanya kazi kwa kanuni hii: kupitia ushirikiano na watu, kupitia kwa wao kuomba kimatendo, kumtafuta na kusonga karibu na Mungu, matokeo yanaweza kupatikana na wanaweza kupata nuru na kuangaziwa na Roho Mtakatifu. Si kwamba Roho Mtakatifu anafanya kazi kivyake, au mwanadamu anafanya kazi kivyake. Wote ni wa muhimu, na jinsi wanadamu wanavyoshiriki zaidi na jinsi wanavyotaka zaidi kufikia viwango vya mahitaji ya Mungu, ndivyo kazi ya Roho Mtakatifu inaimarika. Ni ushirikiano halisi tu wa wanadamu, kupitia kazi ya Roho Mtakatifu, ndivyo vinaweza kutoa matukio halisi na ufahamu wa kweli wa kazi ya Mungu. Hatua kwa hatua, kupitia kwa mazoea kwa njia hii, mwanadamu mkamilifu hatimaye huzalishwa. Mungu hafanyi vitu vya miujiza; katika dhana za mwanadamu, Mungu ni mwenye uweza, na kila kitu kinafanywa na Mungu—na hutokea kwamba watu wanasubiri tu bila kufanya chochote, hawasomi maneno ya Mungu au kuomba, na wanasubiri tu kuguswa na Roho Mtakatifu. Walio na ufahamu sahihi, hata hivyo, wanaamini hili: matendo ya Mungu yanaweza kufikia pale ambapo ushirikiano wangu umefikia, na athari ya kazi ya Mungu kwangu inategemea namna ninavyoshirikiana. Mungu anenapo, ninapaswa kufanya lolote niwezalo na kuyaelekea maneno ya Mungu; hili ndilo ninapaswa kufanikisha.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Jinsi ya Kujua Uhalisi

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 435)

Je, ni desturi ngapi za kidini unazozizingatia? Ni mara ngapi umeasi dhidi ya neno la Mungu na kwenda kwa njia yako? Ni mara ngapi umetia katika vitendo neno la Mungu kwa sababu kwa kweli unajali mizigo Aliyobeba na unatafuta kutimiza mapenzi Yake? Lielewe neno la Mungu na uliweke katika vitendo. Kuwa mwenye maadili katika vitendo na matendo yako; huku si kutii sheria au kufanya hivyo shingo upande kwa ajili ya kujionyesha. Badala yake, huku ni kutenda ukweli na kuishi kulingana na neno la Mungu. Vitendo kama hivi pekee ndivyo humridhisha Mungu. Desturi yoyote inayompendeza Mungu si kanuni bali ni kutenda ukweli. Wanadamu wengine wana upendeleo wa kujivutia nadhari. Mbele ya ndugu zao, wanasema kweli ni wadeni wa Mungu, lakini akiwapa kisogo, hawatendi ukweli ila wanafanya tofauti kabisa. Je, hawa si ni Mafarisayo wa dini? Mtu ambaye anampenda Mungu kwa kweli na ana ukweli ni yule ambaye ni mwaminifu kwa Mungu, lakini bila ya hafichui kwa nje. Yeye yuko tayari kutenda ukweli wakati mambo yanapotokea wala hasemi au kutenda kinyume cha dhamiri yake. Anaonyesha hekima wakati mambo yanapotokea na ni mwenye maadili katika matendo yake, bila kujali hali. Mtu kama huyu ni mtu ambaye anahudumu kwa kweli. Kuna watu wengine ambao mara nyingi shukrani zao kwa kuwa wadeni wa Mungu ni kwa mdomo tu. Siku zao huisha wakiwa na nyuso za wasiwasi, kuonekana wameathiriwa, na kuvalia nyuso za huzuni. Hali ya kuchukiza kweli! Na kama ungewauliza, “Ni kwa njia zipi wewe ni mdeni wa Mungu? Tafadhali niambie!” Hawangeweza kutamka lolote. Kama wewe ni mwaminifu kwa Mungu, basi usizungumze kwa nje kuhusu hilo; badala yake, onyesha upendo wako kwa Mungu kwa njia ya matendo halisi, na kumwomba kwa moyo wa kweli. Wale wanaotumia maneno pekee kushughulika na Mungu ni wanafiki wote! Baadhi yao husema kuwa wao ni wadeni kwa Mungu katika kila sala, na kuanza kulia wakati wowote wanaposali, hata bila kuguswa na Roho Mtakatifu. Watu kama hawa wamepagawa na kaidi na fikira za kidini; wanaishi kulingana na hizo kaidi na fikra, daima wakiamini kwamba matendo kama hayo humpendeza Mungu, na kwamba kumcha Mungu kijuujuu au machozi ya huzuni ndivyo Mungu hupendelea. Ni kitu kipi kizuri kinachoweza kutoka kwa watu kama hao wa kushangaza? Ili kuonyesha unyenyekevu wao, baadhi yao huonyesha neema bandia wakati wanapozungumza mbele ya watu wengine. Baadhi yao kwa makusudi ni wanyonge mbele ya watu wengine, kama mwanakondoo asiye na nguvu yoyote. Je, hii ni tabia ya watu wa ufalme? Mtu wa ufalme sharti awe wa kusisimua na aliye huru, asiye na hatia na aliye na uwazi, mwaminifu na wa kupendeza; mtu aishiye katika hali ya uhuru. Ana uadilifu na heshima, na anaweza kushuhudia kokote aendako; yeye ni yule anayependwa na Mungu na wanadamu. Wale ambao ni wanafunzi katika imani huwa na matendo mengi ya nje; lazima kwanza wapitie kipindi cha ushughulikiaji na kuvunjwa. Wale ambao wana imani kwa Mungu katika nyoyo zao hawawezi kutofautishwa na wengine kwa nje, lakini vitendo na matendo yao ni ya kupongezwa kwa wengine. Watu wa aina hii pekee ndio wanaoweza chukuliwa kuwa wanaishi kwa kudhihirisha neno la Mungu. Ukihubiri injili kila siku kwa mtu huyu na yule, ukiwaleta kwa wokovu, ilhali mwishowe, wewe bado unaishi katika sheria na mafundisho, basi wewe huwezi kuleta utukufu kwa Mungu. Watu wa aina hii ni watu wa dini, na wanafiki pia.

Je, matendo mazuri ya kijuujuu ya mwanadamu yanawakilisha nini? Hayo huwakilisha mwili, na hata matendo yaliyo bora zaidi ya nje hayawakilishi maisha, ila tabia yako tu mwenyewe. Matendo ya nje ya mwanadamu hayawezi kutimiza matakwa ya Mungu. Wewe daima huzungumza kuhusu udeni wako kwa Mungu, lakini huwezi kuyaruzuku maisha ya wengine au kuwafanya wengine kumpenda Mungu. Je, unaamini kwamba matendo kama hayo yatamridhisha Mungu? Unaamini kwamba hii ndiyo matakwa ya moyo wa Mungu, kwamba haya ni ya roho, lakini kwa kweli huu ni ujinga! Unaamini kwamba yale yanayokupendeza wewe na unayotaka ni yale yanayomfurahisha Mungu. Je, yanayokupendeza yanaweza kuwakilisha yanayompendeza Mungu? Je, tabia ya mwanadamu inaweza kumwakilisha Mungu? Yale yanayokupendeza wewe ndiyo hasa yale humchukiza Mungu, na mienendo yako ni ile ambayo Mungu huchukia na kukataa. Kama unahisi kuwa wewe ni mdeni, basi nenda na usali mbele za Mungu. Hakuna haja ya kuzungumzia jambo hilo kwa watu wengine. Usipoomba mbele za Mungu na badala yake mara kwa mara unajivuta nadhari kwako mbele ya wengine, jambo hili linaweza kutimiza matakwa ya moyo wa Mungu? Kama matendo yako daima yanaonekana tu, hii ina maana kuwa wewe ni mtu bure zaidi ya wote. Ni mtu wa aina gani yule aliye na matendo mazuri ya kijuujuu tu lakini hana uhalisi? Watu kama hao ni Mafarisayo wanafiki na watu wa dini! Msipoacha matendo yenu ya nje na hamuwezi kufanya mabadiliko, basi dalili za unafiki ndani yenu zitazidi kuimarika. Kadiri dalili za unafiki zinavyozidi, ndivyo upinzani kwa Mungu unavyozidi, na mwishowe, watu wa aina hii hakika watatupiliwa mbali!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Katika Imani, Mtu Lazima Alenge Ukweli—Kujihusisha na Kaida za Dini Sio Imani

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 436)

Ili kurudisha mfanano wa mtu wa kawaida, yaani, kutimiza ubinadamu wa kawaida, watu hawawezi tu kumpendeza Mungu kwa maneno yao. Wanajiumiza wenyewe kwa kufanya hivyo, na haileti faida yoyote kwa kuingia na kubadili kwao. Kwa hivyo, ili kufikia mbadiliko, watu lazima watende kidogo kidogo, waingie taratibu, watafute na kuchunguza kidogo kidogo, waingie ndani kutoka kwa halisi, na kuishi maisha ya utendaji wa ukweli, maisha ya watakatifu. Tangu sasa kuendelea, inahusisha mambo halisi, vitu halisi, na mazingira halisi, kuwaruhusu watu kuwa na mafunzo ya utendaji. Haiwahitaji hao kutoa maneno matupu; badala yake, inahitaji mafunzo katika mazingira halisi. Watu huja kutambua kuwa wao ni wenye ubora duni wa tabia, na kisha wana kula na kunywa halisii kwa maneno ya Mungu halisi, kuingia halisi, na utandaji halisi, hivi ndivyo wanavyopokea uhalisi na hivi ndivyo kuingia kunaweza kufanyika hata haraka zaidi. Ili kuwabadili watu, lazima kuwe na utendaji, lazima wafanye mazoezi na mambo halisi, vitu halisi, na mazingira halisi. Kwa kutegemea tu maisha ya kanisa, inawezekana kutimiza mafunzo ya kweli? Je, mwanadamu angeingia katika uhalisi? La. Iwapo mwanadamu hawezi kuingia katika maisha halisi, basi yeye hawezi kubadili njia zake za zamani za kufanya mambo na kuishi maisha. Sio tu kwa sababu ya uvivu wa mwanadamu au utegemezi wake wa nguvu, bali ni kwa sababu mwanadamu hana uwezo wa kuishi, na zaidi, hana ufahamu wa kiwango cha mfanano wa mtu wa kawaida. Hapo kale, watu walikuwa daima wakiongea, wakinena, wakiwa na ushirika, hata wakawa “wanenaji hodari”; lakini hakuna yeyote kati yao alitafuta mabadiliko katika tabia ya maisha; walishikilia tu kutafuta nadharia za kina. Kwa hivyo, leo inapasa mbadili maisha haya ya kidini ya kumwamini Mungu. Lazima muingie ndani na kutenda kwa kulenga kitu kimoja, jambo moja, mtu mmoja. Lazima mfanye mambo na malengo—hapo tu ndio mtafikia matokeo. Ili kuwabadili watu, lazima kuanze na kiini chao. Kazi lazima ilenge kiini cha watu, maisha yao, uvivu, utegemezi, na utumwa wa watu, na kwa njia hii tu ndio wanaweza kubadilishwa.

Ijapokuwa maisha ya kanisa yanaweza kuleta matokeo katika sehemu nyingine, msingi bado ni kuwa maisha halisi yanaweza kuwabadilisha watu, na hali yao ya kale haiwezi kubadilika bila maisha halisi. Hebu tuchukue kazi ya Yesu katika Enzi ya Neema. Yesu alipoharamisha sheria za awali na kuanzisha amri za enzi mpya, Alinena kupitia mifano ya maisha halisi. Wakati Yesu Alipowaongoza wanafunzi wake kupita katika shamba la ngano siku ya Sabato, wanafunzi Wake walihisi njaa na wakatunda na kula masuke ya nafaka, Mafarisayo walipoona hivi walisema kuwa hawakuitii Sabato. Pia walisema kuwa watu hawakuruhusiwa kuwaokoa ndama walioanguka shimoni katika siku ya Sabato, wakisema kuwa hakuna kazi ingepaswa kufanywa wakati wa Sabato. Yesu alitumia matukio haya ili kutangaza rasmi amri za enzi mpya hatua kwa hatua. Wakati huo, Alitumia mambo mengi ya kiutendaji ili watu waelewe na kubadilika. Hii ndiyo kanuni ambayo kwayo Roho Mtakatifu hutekeleza kazi Yake, na ni njia hii pekee inayoweza kubadili watu. Wanapokosa mambo ya kiutendaji, watu wanaweza tu kupata ufahamu katika nadharia na wanaweza kuelewa tu mambo kiakili—hii si njia ya kufaa kubadili watu. Tukiongea juu ya kupata busara na ufahamu kupitia mafundisho, hili lingetimizwaje? Je, mwanadamu angeweza kupata busara na ufahamu kwa kusikiza, kusoma na kukuza ujuzi wake tu? Je, hili linasababishaje kupata busara na ufahamu? Mtu lazima afanye bidii kuelewa na kuwa na uzoefu kupitia maisha halisi. Kwa hivyo, mafunzo hayawezi kukosa na mtu hawezi kuacha maisha halisi. Mtu lazima azingatie hali tofauti na aingie kwa hali mbalimbali: kiwango cha elimu, ufafanuzi, uwezo wa kuona mambo, utambuzi, uwezo wa kuelewa maneno ya Mungu, maarifa ya kawaida na kanuni za ubinadamu, na vitu vingine vinavyohusiana na ubinadamu ambavyo mtu lazima awe navyo. Baada ya ufahamu kufikiwa, mtu lazima alenge kuingia, na hapo tu ndio mabadiliko yanaweza kufikiwa. Iwapo mwanadamu amefikia ufahamu lakini anakaidi utendaji, mabadiliko yanawezaje kutokea? Sasa, mwanadamu amefahamu mengi, lakini haishi kwa kudhihirisha uhalisi, hivyo basi anaweza kuwa tu na ufahamu halisi kidogo wa maneno ya Mungu. Umepata nuru kwa kiasi kidogo, umepokea mwangaza kidogo kutoka kwa Roho Mtakatifu, lakini huna kuingia katika maisha halisi, au hata huenda hujali juu ya kuingia, hivyo basi utakuwa na mabadiliko kidogo tu. Baada ya muda mrefu hivyo, watu wameelewa mengi na wanaweza kusema mengi juu ya ujuzi wao wa nadharia, lakini tabia yao ya nje husalia ile ile, na ubora wa tabia yao wa asili hudumu bila upandaji hadhi hata kidogo. Iwapo mambo yako hivi, mtaingia lini humo hatimaye?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kujadili Maisha ya Kanisa na Maisha Halisi

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 437)

Maisha ya kanisa ni aina ya maisha tu ambapo watu hukutana kufurahia maneno ya Mungu, na huchukua tu kipande kidogo cha maisha ya mtu. Iwapo maisha halisi ya watu yangekuwa kama maisha yao ya kanisani—ikiwemo maisha ya kawaida ya kiroho, kufurahia maneno ya Mungu kwa kawaida, kuomba na kuwa karibu na Mungu kwa kawaida, kuishi maisha halisi ambapo kila kitu kinatekelezwa kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu, kuishi maisha halisi ambapo kila kitu kinatekelezwa kwa mujibu wa ukweli, kuishi maisha halisi ya kutekeleza maombi na kuwa kimya mbele ya Mungu, ya kufanya mazoezi ya kuimba nyimbo za kidini na kucheza, maisha kama haya tu yangemleta mtu katika maisha ya maneno ya Mungu. Watu wengi sana hulenga tu masaa kadhaa ya maisha yao ya kanisa bila “kutunza” maisha yao nje ya masaa hayo, kana kwamba hayahusiki nao. Pia kunao watu wengi ambao huingia tu katika maisha ya watakatifu wanapokula na kunywa maneno ya Mungu, wakiimba nyimbo za kidini au wakiomba, kisha hurejelea nafsi zao za kale nje ya nyakati hizo. Maisha kama hayo hayawezi kubadili watu, na hayatawaruhusu kumjua Mungu. Katika kumwamini Mungu, iwapo mwanadamu anataka mabadiliko kwa tabia yake mwenyewe, basi lazima asijitenge na maisha halisi. Katika maisha halisi, lazima ujijue mwenyewe, ujitelekeze mwenyewe, utende ukweli, na vilevile kujifunza kanuni, maarifa ya kawaida na masharti ya kujiendesha katika mambo yote kabla ya wewe kuweza kutimiza mabadiliko ya polepole. Iwapo utalenga tu ujuzi katika nadharia na kuishi tu katika sherehe za dini bila ya kuingia ndani ya uhalisi, bila kuingia kwenye maisha halisi, basi hutaweza kamwe kuingia katika uhalisi, hutaweza kujijua mwenyewe, kuujua ukweli, au kumjua Mungu, na utakuwa kipofu na mjinga milele. Kazi ya Mungu ya kuwaokoa watu sio kuwaruhusu waishi maisha ya kawaida ya binadamu baada ya kipindi cha muda mfupi, na wala sio ili kubadili mawazo na mafundisho yao yasiyo sahihi. Badala yake, kusudi Lake ni kubadili tabia za zamani za watu, kubadilisha kikamilifu njia yao ya zamani ya maisha, na kubadilisha njia zao zote za mawazo na mtazamo wa akili zilizopitwa na wakati. Kulenga tu maisha ya kanisa pekee hakuwezi kubadili mazoea ya kale ya watu au kubadili njia za kale walizoishi kwa muda mrefu. Lolote litokealo, watu hawapaswi kujitenga na maisha halisi. Mungu anauliza kwamba watu waishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida katika maisha halisi, sio tu katika maisha ya kanisani; kwamba waishi kwa kudhihirisha ukweli katika maisha halisi, sio tu katika maisha ya kanisani; kwamba watimize majukumu yao katika maisha halisi, sio tu katika maisha ya kanisani. Ili kuingia katika uhalisi, mtu lazima apindue vitu vyote kuelekea maisha halisi. Iwapo waumini katika Mungu, watu hawawezi kuja kujijua kupitia kuingia katika maisha halisi, na ikiwa hawawezi kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida katika maisha halisi, watashindwa. Wale wanaomkaidi Mungu wote ni watu ambao hawawezi kuingia katika maisha halisi. Wote ni watu wanaozungumza kuhusu ubinadamu lakini wanaishi kwa kudhihirisha asili ya pepo mbaya. Wote ni watu wanaozungumza kuhusu ukweli lakini wanaishi kwa kudhihirisha kanuni badala yake. Wale wasioweza kuishi kwa kudhihirisha ukweli katika maisha halisi ni wale wanaoamini katika Mungu lakini wanachukiwa na kukataliwa na Yeye. Lazima ufanye mazoezi ya kuingia kwako katika maisha halisi, ujue upungufu wako mwenyewe, ukaidi na upumbavu, na ujue ubinadamu wako usio wa kawaida na udhaifu. Kwa njia hiyo, ufahamu wako wote utaambatanishwa ndani ya hali yako halisi na ugumu. Ni aina hii ya ufahamu pekee ndiyo ya kweli na inaweza kukufanya ushike kwa hakika hali yako mwenyewe na ufanikishe mabadiliko ya tabia yako.

Sasa kwa vile kukamilishwa kwa mwanadamu kumeanza rasmi, mtu lazima aingie katika maisha halisi. Kwa hivyo, ili kutimiza mabadiliko, lazima mtu aanzie kwa kuingia katika maisha halisi, na kubadilika kidogo kidogo. Ukihepa maisha ya kawaida ya binadamu na kuongea tu kuhusu mambo ya kiroho, basi mambo hugeuka makavu na bapa, hugeuka yasiyo ya uhalisi, na mtu angebadilika vipi? Sasa unaambiwa uingie katika maisha halisi kufanya mazoezi, ili uweze kuweka msingi wa kuingia katika uzoefu wa kweli. Hii ni mojawapo ya mambo ambayo mtu anapaswa kufanya. Kazi ya Roho Mtakatifu hasa ni kuongoza, ilhali iliyosalia hutegemea utendaji wa watu na kuingia. Kila mmoja anaweza kufikia kuingia katika maisha halisi kwa njia mbalimbali, kiasi kwamba wanaweza kumleta Mungu katika maisha halisi, na kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida halisi. Haya tu ndiyo maisha yenye maana!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kujadili Maisha ya Kanisa na Maisha Halisi

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 438)

Hapo awali, ilisemwa kwamba kuwa na uwepo wa Roho Mtakatifu na kuwa na kazi ya Roho Mtakatifu ni tofauti. Hali ya kawaida ya kuwa na uwepo wa Roho Mtakatifu inadhihirishwa katika kuwa na mawazo ya kawaida, mantiki ya kawaida, na ubinadamu wa kawaida. Tabia ya mtu itabaki kama ilivyokuwa, lakini ndani yake kutakuwa na amani, na nje atamstahi mtakatifu. Hivi ndivyo atakavyokuwa wakati ambapo Roho Mtakatifu yuko naye. Wakati ambapo mtu yuko na uwepo wa Roho Mtakatifu, kufukiria kwake ni kwa kawaida. Anapokuwa na njaa yeye hutaka chakula, anapoona kiu yeye hutaka kunywa maji. … Udhihirisho kama huu wa ubinadamu wa kawaida si nuru kutoka kwa Roho Mtakatifu; ni kufikiria kwa kawaida kwa watu na hali ya kawaida ya kuwa na uwepo wa Roho Mtakatifu. Watu wengine huamini kimakosa kwamba wale walio na uwepo wa Roho Mtakatifu huwa hawaoni njaa, kwamba huwa hawahisi uchovu, na huwa hawaifikirii familia, wakiwa takribani wamejitenga kabisa kutoka kwa mwili. Kwa kweli, kadiri Roho Mtakatifu alivyo na watu, ndivyo wanavyokuwa wa kawaida zaidi. Wanajua kuteseka na kujitolea kwa ajili ya Mungu, kujitumia kwa ajili ya Mungu, na kuwa waaminifu kwa Mungu; zaidi ya hayo, wao hufikiria kuhusu chakula na mavazi. Kwa maneno mengine, hawajapoteza chochote cha ubinadamu wa kawaida wanachopaswa kuwa nacho na, badala yake, wanakuwa hasa na mantiki. Wakati mwingine, wao husoma maneno ya Mungu na kuitafakari kazi ya Mungu; kuna imani ndani ya mioyo yao na wako radhi kufuatilia ukweli. Kwa kawaida, kazi ya Roho Mtakatifu inategemezwa juu ya msingi huu. Kama watu hawana fikira za kawaida, basi hawana mantiki—hii si hali ya kawaida. Watu wanapokuwa na fikira za kawaida na Roho Mtakatifu yuko nao, hakika wao huwa na mantiki ya mtu wa kawaida na hivyo, wao huwa na hali ya kawaida. Katika kupitia kazi ya Mungu, kuwa na kazi ya Roho Mtakatifu hutokea mara chache, ilhali uwepo wa Roho Mtakatifu uko takribani nyakati zote. Maadamu mantiki na fikira za watu ni za kawaida, na maadamu hali zao ni za kawaida, basi Roho Mtakatifu yuko nao kwa hakika. Wakati ambapo mantiki na fikira za watu si za kawaida, basi ubinadamu wao sio wa kawaida. Ikiwa, wakati huu, kazi ya Roho Mtakatifu iko ndani yako, basi Roho Mtakatifu atakuwa nawe pia kwa hakika. Lakini ikiwa Roho Mtakatifu yuko nawe, si lazima kwamba Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yako, kwani Roho Mtakatifu hufanya kazi katika nyakati maalumu. Kuwa na uwepo wa Roho Mtakatifu kunaweza tu kudumisha kuishi kwa kawaida kwa watu, lakini Roho Mtakatifu hufanya kazi tu katika nyakati fulani. Kwa mfano, kama wewe ni kiongozi au mfanyakazi, unapofanya kazi ya unyunyizaji au kuruzuku kwa ajili ya kanisa, Roho Mtakatifu atakupa nuru kufikia maneno fulani ambayo ni ya kuwaadilisha wengine na yanayoweza kutatua baadhi ya matatizo ya utendaji ya kina ndugu—katika wakati kama huo, Roho Mtakatifu anafanya kazi. Wakati mwingine, unapokuwa ukila na kunywa maneno ya Mungu, Roho Mtakatifu hukupa nuru kwa maneno fulani ambayo yanahusiana na matukio uliyopitia hasa, yakikuruhusu upate ufahamu mkubwa zaidi wa hali zako; hii pia ni kazi ya Roho Mtakatifu. Wakati mwingine, Ninapozungumza, ninyi husikiliza na huweza kupima hali zenu wenyewe dhidi ya maneno Yangu, na wakati mwingine ninyi huguswa au kutiwa moyo; hii yote ni kazi ya Roho Mtakatifu. Watu wengine husema kwamba Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yao nyakati zote. Hili haliwezekani. Ikiwa wangesema kwamba Roho Mtakatifu yuko nao kila mara, hilo lingekuwa la kweli. Ikiwa wangesema kwamba fikira na hisia zao ni za kawaida nyakati zote, hilo pia lingekuwa la kweli, na lingeonyesha kwamba Roho Mtakatifu yuko nao. Ikiwa wanasema kwamba Roho Mtakatifu hufanya kazi ndani yao kila mara, kwamba wamepata nuru kutoka kwa Mungu na kuguswa na Roho Mtakatifu kila wakati, na wanapata ufahamu mpya kila wakati, basi hili si la kawaida hata kidogo! Ni la kupita uwezo wa binadamu kabisa! Bila tashwishi yoyote, watu kama hao ni pepo wabaya! Hata wakati ambapo Roho wa Mungu huja ndani ya mwili, kuna nyakati ambapo lazima Ale, na lazima apumzike—sembuse mwanadamu. Wale ambao wamemilikiwa na pepo wabaya huonekana kutokuwa na hisia na udhaifu wa mwili. Wanaweza kutelekeza na kuacha kila kitu, ni wasio na hisia, ni wenye uwezo wa kustahimili mateso na hawahisi uchovu hata kidogo sana, kana kwamba wamevuka mipaka ya mwili. Je, hili silo la kupita uwezo wa binadamu kabisa? Kazi ya pepo waovu ni ya kupita uwezo wa binadamu—hakuna mwanadamu anayeweza kutimiza mambo kama haya. Wale wasio na utambuzi huwa na wivu wanapowaona watu kama hao; Wao husema kwamba wana nguvu mno katika imani yao katika Mungu, wana imani kubwa na kamwe hawaonyeshi ishara yoyote ya udhaifu!. Kwa kweli, hili lote ni dhihirisho la kazi ya pepo mwovu. Kwa sababu watu wa kawaida bila kuzuilika huwa na udhaifu wa binadamu; hii ni hali ya kawaida ya wale walio na uwepo wa Roho Mtakatifu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Utendaji (4)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 439)

Maana ya kusimama imara katika ushuhuda wa mtu ni ipi? Watu wengine husema kwamba wao hufuata tu jinsi wanavyofanya sasa na hawajishughulishi na kama wana uwezo wa kupata uzima; wao hawafuatilii uzima, lakini hawajiuzulu pia. Wanakubali tu kwamba hii hatua ya kazi hutekelezwa na Mungu. Je, huku si kushindwa katika ushuhuda wao? Watu kama hao hata hawashuhudii kuhusu kushindwa. Wale ambao wameshindwa hufuata haijalishi mengine yote na wanaweza kuufuatilia uzima. Wao hawaamini tu katika Mungu wa vitendo, lakini pia hujua kuifuata mipango yote ya Mungu. Hao ndio huwa na ushuhuda. Wale wasiokuwa na ushuhuda hawajawahi kuufuatilia uzima na bado wanafuata kwa kumaliza jambo kwa kubahatisha. Unaweza kufuata, lakini hili halimaanishi kwamba umeshindwa, kwani huna ufahamu wowote kuhusu kazi ya Mungu leo. Masharti fulani lazima yatimizwe ili kushindwa. Sio wote wanaofuata wameshindwa, kwani ndani ya moyo wako hufahamu chochote kuhusu kwa nini ni lazima umfuate Mungu wa leo, wala hujui vile ambavyo umefaulu hadi leo, nani amekusaidia mpaka leo. Utendaji wa imani katika Mungu wa watu wengine huwa wenye kuchanganyikiwa na kukanganyikiwa; hivyo, kufuata si lazima kumaanishe kwamba unakuwa na ushuhuda. Ushuhuda wa kweli ni nini hasa? Ushuhuda uliozungumziwa hapa una sehemu mbili: Mojawapo ni ushuhuda wa kushindwa, na nyingine ni ushuhuda kwa kuweza kufanywa mkamilifu (ambako, kwa kawaida, utakuwa ushuhuda unaofuata majaribio makuu zaidi na majonzi ya siku za usoni). Kwa maneno mengine, ikiwa unaweza kusimama imara wakati wa majonzi na majaribio, basi utakuwa umekuwa na hatua ya pili ya ushuhuda. Kilicho cha maana sana leo ni hatua ya kwanza ya ushuhuda: kuweza kusimama imara wakati wa kila namna ya majaribu ya kuadibu na hukumu. Huu ni ushuhuda wa kushindwa. Hilo ni kwa sababu sasa ni wakati wa ushindi. (Unapaswa kujua kwamba sasa ni wakati wa kazi ya Mungu duniani; kazi kuu ya Mungu mwenye mwili duniani ni kushinda hili kundi la watu duniani wanaomfuata Yeye kupitia hukumu na kuadibu.) Kama una uwezo wa kushuhudia kuhusu kushindwa au la hakutegemei tu kama unaweza kufuata hadi mwisho, lakini, la muhimu zaidi, kama, unapopitia kila hatua ya kazi ya Mungu, unakuwa ba uwezo wa kuelewa kweli kuadibu na hukumu ya Mungu, na kama wewe kweli wewe unaitazama kazi hii yote. Hutaweza kupenyeza kwa kufuata tu hadi mwisho kabisa. Lazima uweze kusalimu amri kwa hiari wakati wa kila nafasi ya kuadibu na hukumu, lazima uwe na uwezo kuelewa kweli kila hatua ya kazi upitiayo, na lazima uweze kupata ufahamu wa, na utiifu kwa tabia ya Mungu. Huu ndio ushuhuda wa mwisho wa kushindwa ambao wewe unatakiwa kuwa nao. Ushuhuda wa kushindwa kimsingi unahusu ufahamu wako wa kupata mwili kwa Mungu. Cha msingi, hatua hii ya ushuhuda ni kwa kupata mwili kwa Mungu. Haijalishi kile ambacho unafanya au kusema mbele ya watu wa ulimwengu au wale wanaotawala; kilicho na maana kuliko vyote ni kama unaweza kuyatii maneno yote kutoka kinywani mwa Mungu na kazi Yake yote. Kwa hivyo, hatua hii ya ushuhuda inaelekezwa kwa Shetani na maadui wote wa Mungu—pepo na wenye uadui ambao hawaamini kwamba Mungu atakuwa mwili mara ya pili na kuja kufanya kazi hata kubwa zaidi, na zaidi ya hayo, hawaamini katika ukweli wa kurudi kwa Mungu kwa mwili. Kwa maneno mengine, inaelekezwa kwa wapinga Kristo wote—maadui wote wasioamini katika kupata mwili kwa Mungu.

Kumfikiria Mungu na kumtamani sana Mungu hakuthibitishi kwamba umeshindwa na Mungu; hili linategemea kama unaamini kwamba Yeye ni Neno lililopata mwili, kama unaamini kwamba Neno limepata mwili, na kama unaamini kwamba Roho amekuwa Neno, na Neno limeonekana katika mwili. Huu ndio ushuhuda muhimu. Haijalishi jinsi wewe unafuata, wala vile unavyojitumia mwenyewe; kilicho muhimu ni kama wewe unaweza kugundua kutoka kwa ubinadamu huu wa kawaida kwamba Neno limepata mwili na Roho wa kweli amepatikana katika mwili—kwamba ukweli wote, njia, na uzima umekuja katika mwili, na Roho wa Mungu hakika amewasili duniani na Roho amekuja katika mwili kwa kweli. Ingawa, kijuujuu, hili linaonekana kuwa tofauti na utungaji mimba kwa Roho Mtakatifu, katika kazi hii mnaweza kuona dhahiri zaidi kwamba Roho tayari amedhihirika katika mwili, na, zaidi ya hayo, kwamba Neno limepata mwili, na Neno limeonekana katika mwili. Unaweza kufahamu maana ya kweli ya maneno haya: “Mwanzoni kulikuwa na Neno, na Neno alikuwa na Mungu, na Neno alikuwa Mungu.” Zaidi ya hayo, lazima ufahamu kwamba Neno la leo ni Mungu, na utazame Neno likiwa mwili. Huu ni ushuhuda bora zaidi unaoweza kuwa nao. Hili linathibitisha kwamba una ufahamu wa kweli wa Mungu kupata mwili—mbali na kumjua Yeye, lakini pia unajua kwamba njia unayoifuata leo ni njia ya uzima, na njia ya ukweli. Hatua ya kazi ambayo Yesu alitekeleza ilitimiza tu kiini cha “Neno alikuwako kwa Mungu”: Ukweli wa Mungu ulikuwako kwa Mungu, na Roho wa Mungu alikuwa na mwili na alikuwa asiyetenganishwa kutoka katika mwili huo. Yaani, mwili wa Mungu mwenye mwili ulikuwa na Roho wa Mungu, ambalo ni thibitisho kuu zaidi kwamba Yesu mwenye mwili alikuwa kupata mwili wa kwanza wa Mungu. Hatua hii ya kazi hasa inatimiza maana ya ndani ya “Neno lakuwa mwili,” ilichangia kwenye maana ya kina zaidi ya “naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu,” na inakuruhusu wewe uamini kwa uthabiti maneno “Hapo mwanzo kulikuwako na Neno.” Ambalo ni kusema, wakati wa uumbaji Mungu alikuwa na maneno, Maneno Yake yalikuwa na Yeye na yasiyotenganishwa kutoka Kwake, na katika enzi ya mwisho, Yeye anafanya nguvu na mamlaka ya maneno Yake yawe hata wazi zaidi, na kumruhusu mwanadamu kuziona njia Zake zote—kuyasikia maneno Yake yote. Hiyo ndiyo kazi ya enzi ya mwisho. Lazima uelewe mambo haya yote kabisa. Si suala la kuujua mwili, bali la jinsi unavyouelewa mwili na Neno. Huu ndio ushuhuda unaopaswa kuwa nao, kile ambacho kila mtu lazima akijue. Kwa sababu hii ni kazi ya kupata mwili kwa pili—na mara ya mwisho ambapo Mungu anapata mwili—inakamilisha kwa ukamilifu umuhimu wa kupata mwili, inatekeleza kabisa na kutoa kazi yote ya Mungu katika mwili, na kuitamatisha enzi ya Mungu kuwa katika mwili. Hivyo, lazima ujue maana ya kupata mwili. Haijalishi unavyokimbia huku na huko, au vile unavyotekeleza vizuri masuala mengine ya nje; kilicho muhimu ni kama unaweza kutii kwa kweli mbele ya Mungu mwenye mwili na kuitoa nafsi yako yote kwa Mungu, na kutii maneno yote yatokayo kinywani Mwake. Hili ndilo unalopaswa kufanya, na unalopaswa kutii.

Hatua ya mwisho ya ushuhuda ni ushuhuda wa kama unaweza kufanywa mkamilifu au la—ambako ni kusema, kwa kuwa umeelewa maneno yote yaliyonenwa na kinywa cha Mungu mwenye mwili, umekuja kupata ufahamu wa Mungu na kuwa na hakika kumhusu Yeye, unaishi kwa kudhihirisha maneno yote kutoka kinywani mwa Mungu, na kutimiza masharti ambayo Mungu anakwambia—mtindo wa Petro na imani ya Ayubu—kiasi kwamba unaweza kutii hadi kufa, kujitoa mwenyewe kabisa Kwake, na hatimaye kutimiza mfano wa mtu ambaye anafikia kiwango kilichowekwa, kinachomaanisha mfano wa mtu ambaye ameshindwa na kufanywa mkamilifu Baada ya kupitia hukumu na kuadibu kwa Mungu. Huu ndio ushuhuda wa mwisho—ni ushuhuda ambao mtu ambaye hatimaye amefanywa mkamilifu anapaswa kuwa nao. Hizi ni hatua mbili za ushuhuda mnaopaswa kuwa nao, na zinahusiana, kila moja ni ya msingi. Lakini kuna jambo moja unalotakiwa kujua: Ushuhuda Ninaotaka kutoka kwako leo hauelekezwi kwa watu wa ulimwengu, wala kwa mtu yeyote mmoja, lakini kwa kile ambacho Nitakacho kutoka kwako. Kinatathminiwa na kama unaweza kuniridhisha Mimi, na kama unaweza kutimiza kabisa viwango vya masharti Yangu kwa kila mmoja wenu. Hili ndilo mnalopaswa kufahamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Utendaji (4)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 440)

Mnapopitia shida au kikwazo kidogo, ni yenye manufaa kwenu; kama lingekuwa jambo rahisi kwenu basi mngeangamia, na kisha mngelindwaje? Leo, ni kwa sababu mnaadibiwa, kuhukumiwa, na kulaaniwa ndiyo mnapewa ulinzi. Ni kwa sababu mmeteseka sana ndiyo mnalindwa. Kama sivyo, mngekuwa tayari mmepotoka. Huku si kufanya mambo yawe magumu kwenu kwa makusudi—asili ya mwanadamu ni ngumu kubadili, na lazima iwe hivyo ili tabia zao zibadilishwe. Leo, hamna hata dhamiri au akili ambazo Paulo alikuwa nazo, wala hamwezi hata kujitambua kama yeye. Lazima mushurutishwe kila wakati, na kila wakati lazima muadibiwe na kuhukumiwa ili roho zenu zichangamshwe. Kuadibu na hukumu ndivyo bora kabisa kwa maisha yenu. Na inapolazimu, lazima pia ukweli unaowafikia uadibiwe; ni hapo tu ndipo mtakapotii kikamilifu. Asili zenu ni kana kwamba bila kuadibu na kulaani, hamngetaka kuinamisha vichwa vyenu, hamngetaka kutii. Bila ukweli ulio mbele yenu, hakungekuwa na matokeo. Ninyi ni duni sana na msio na thamani katika tabia! Bila kuadibu na hukumu, itakuwa vigumu kwenu kushindwa, na itakuwa vigumu kwa udhalimu na kutotii kwenu kushindwa. Asili yenu ya zamani imekita mizizi sana. Kama mngewekwa juu ya kiti cha enzi, hamngefahamu urefu wa mbingu na kina cha dunia, sembuse kujua mnakoelekea. Hamjui hata mlikotoka, hivyo mngewezaje kumjua Bwana wa uumbaji? Bila kuadibiwa na kulaaniwa kwa wakati unaofaa leo, siku yenu ya mwisho ingekuwa imeshawadia kitambo. Hiyo ni kando na majaaliwa yenu—je, hayo hayatakuwa katika hatari ya karibu zaidi? Bila kuadibu na hukumu hii ya wakati unaofaa, ni nani anayejua jinsi ambavyo mngekuwa wenye kiburi, au jinsi ambavyo mngekuwa wapotovu. Kuadibu huku na hukumu hii vimewafikisha leo, na vimehifadhi kuwepo kwenu. Kama bado “mngeelimishwa” kwa kutumia njia zile zile kama za “baba” yenu, ni nani ajuaye mngeingia katika ulimwengu upi! Hamna uwezo wa kujidhibiti na kutafakari kujihusu wenyewe hata kidogo. Kwa watu kama ninyi, mkifuata na kutii tu bila kusababisha ukatizaji au usumbufu wowote, malengo Yangu yatatimia. Je, hamfai kufanya vema zaidi katika kukubali kuadibu na hukumu ya leo? Je, mna chaguo gani jingine?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Utendaji (6)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 441)

Unapojitayarisha kwa ajili ya maisha, lazima ulenge kula na kunywa maneno ya Mungu, lazima uweze kuzungumzia maarifa ya Mungu, maoni yako ya maisha ya binadamu, na hasa, maarifa yako ya kazi iliyofanywa na Mungu wakati wa siku za mwisho. Kwa kuwa unafuatilia uzima, ni lazima ujitayarishe na vitu hivi. Unapokula na kunywa maneno ya Mungu, lazima utathmini uhalisi wa hali yako mwenyewe kulingana na vitu hivi. Yaani, unapogundua dosari zako wakati wa uzoefu wako wa kweli, lazima uweze kupata njia ya kutenda, uweze kupuuza nia na fikira zako zisizo sahihi. Ukijitahidi daima kupata vitu hivi na utake kuvitimiza kwa dhati, basi utakuwa na njia ya kufuata, hutahisi mwenye utupu, na hivyo utaweza kudumisha hali ya kawaida. Ni hapo tu ndipo utakuwa mtu anayebeba mzigo katika maisha yako mwenyewe, aliye na imani. Mbona watu wengine hawawezi kuyaweka maneno ya Mungu katika vitendo baada ya kuyasoma? Je, si kwa sababu hawawezi kuelewa vitu muhimu kabisa? Je, si kwa sababu hawayachukulii maisha kwa uzito? Sasabu ya wao kutoelewa vitu muhimu na kukosa njia ya kutenda ni kuwa wanaposoma maneno ya Mungu, hawawezi kuyahusisha na hali zao wenyewe, wala hawawezi kuwa na ujuzi wa hali zao wenyewe. Watu wengine husema: “Mimi huyasoma maneno ya Mungu na kuyahusisha na hali yangu mwenyewe, na najua kwamba mimi ni mpotovu na mwenye ubora duni wa tabia, lakini siwezi kuyaridhisha mapenzi ya Mungu.” Umeona tu mambo ya nje kabisa; kuna vitu vingi halisi ambavyo huvijui: jinsi ya kuweka kando raha za mwili, jinsi ya kuweka kando kujidai, jinsi ya kujibadili, jinsi ya kuviingia vitu hivi, jinsi ya kuboresha ubora wako wa tabia, na kuanzia kutoka kipengele kipi. Unaelewa tu mambo machache ya nje, na yote unayoyajua ni kwamba kweli umepotoka sana. Unapokutana na ndugu zako, unazungumzia jinsi ulivyopotoka, na inaonekana kwamba unajijua na unabeba mzigo mkubwa kwa ajili ya maisha yako. Kwa kweli, tabia yako potovu haijabadilika, jambo linalothibitisha kwamba hujapata njia ya kutenda. Ikiwa unaongoza kanisa, lazima uweze kuelewa hali za kina ndugu na kuzionyesha. Je, itatosha kusema tu: “Ninyi watu ni wasiotii na wenye maendeleo kidogo mno!” La, lazima uzungumze hasa kuhusu jinsi kutotii kwao na wao kuwa wenye maendeleo kidogo mno kunavyodhihirishwa. Lazima uzungumzie hali zao za kutotii, mienendo yao ya kutotii, na tabia zao za kishetani, na lazima uyazungumzie mambo haya kwa namna ambayo wanashawishika kabisa kuhusu ukweli katika maneno yako. Tumia mambo ya hakika na mifano kutoa hoja zako, na useme hasa jinsi wanavyoweza kujiondoa kwa tabia ya uasi, na uonyeshe njia ya kutenda—hivi ndivyo jinsi ya kuwashawishi watu. Ni wale tu wanaofanya hivi ndio wanaoweza kuwaongoza wengine; ni wao tu walio na uhalisi wa ukweli.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Utendaji (7)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 442)

Kumshuhudia Mungu hasa ni suala la kuzungumza kuhusu maarifa yako ya kazi ya Mungu, kuhusu jinsi Mungu huwashinda watu, kuhusu jinsi Yeye huwaokoa watu, kuhusu jinsi Yeye huwabadili watu; ni suala la kuzungumza kuhusu jinsi Yeye huwaongoza watu kuingia katika uhalisi wa ukweli, Akiwawezesha washindwe, wakamilishwe na kuokolewa na Yeye. Kushuhudia kunamaanisha kuzungumza kuhusu kazi Yake na yote ambayo umepitia. Ni kazi Yake pekee inayoweza kumwakilisha, na ni kazi Yake pekee inayoweza kumfichua kwa umma, kwa ukamilifu Wake; kazi Yake inamshuhudia. Kazi na matamshi Yake vinamwakilisha Roho moja kwa moja; kazi Anayofanya inatekelezwa na Roho, na maneno Anayonena yanazungumzwa na Roho. Vitu hivi vinaonyeshwa tu kupitia mwili wa Mungu, lakini kwa kweli, ni maonyesho ya Roho. Kazi yote Anayofanya na maneno yote Anayozungumza yanawakilisha kiini Chake. Ikiwa Mungu hangezungumza ama kufanya kazi baada ya kujivika mwili na kuja miongoni mwa wanadamu, na kisha Awatake mjue uhalisi Wake, ukawaida Wake na kudura Yake, je, ungeweza? Je, ungeweza kujua kiini cha Roho? Je, ungeweza kujua sifa za kiasili za mwili Wake ni zipi? Ni kwa sababu tu mmepitia kila hatua ya kazi Yake ndiyo Anawataka mumshuhudie. Ikiwa hamngekuwa na uzoefu kama huu, basi Hangesisitiza kwamba mumshuhudie. Kwa hivyo, unapomshuhudia Mungu, hushuhudii tu kuhusu sura Yake ya nje ya ubinadamu wa kawaida, lakini pia kazi Anayofanya na njia Anayoongoza; unapaswa kushuhudia kuhusu jinsi ulivyoshindwa na Yeye na umekamilishwa katika vipengele vipi. Unapaswa kuwa na ushuhuda wa aina hii. Ikiwa kila uendapo unasema kwa sauti kubwa: “Mungu wetu amekuja kufanya kazi, na kazi Yake kweli ni ya vitendo! Ametupata bila matendo yasiyo ya kawaida, bila miujiza na maajabu yoyote hata kidogo!” Wengine watauliza: “Unamaanisha nini unaposema kwamba Hafanyi miujiza na maajabu? Anawezaje kuwa Amekushinda bila kufanya miujiza na maajabu?” Na unasema: “Anazungumza na bila kuonyesha miujiza ama maajabu yoyote, Ametushinda. Kazi Yake imetushinda.” Hatimaye, ikiwa huwezi kusema chochote cha maana, ikiwa huwezi kuzungumzia mambo maalum, je, huu ni ushuhuda wa kweli? Mungu mwenye mwili anapowashinda watu, ni maneno Yake ya uungu yanayofanya hivyo. Ubinadamu hauwezi kutimiza hili; silo jambo ambalo mtu yeyote anaweza kutimiza, na hata wale wenye ubora wa juu zaidi wa tabia miongoni mwa watu wa kawaida hawawezi kutimiza hili, kwani uungu Wake ni wa juu zaidi kuliko kiumbe yeyote. Hili ni jambo la ajabu kwa watu; hata hivyo Muumba ni wa juu zaidi kuliko kiumbe yeyote. Viumbe hawawezi kuwa wa juu zaidi kuliko Muumba; ungekuwa wa juu zaidi kumliko, Hangeweza kukushinda, na Anaweza tu kukushinda kwa sababu Yeye ni wa juu zaidi kukuliko. Yeye anayeweza kuwashinda wanadamu wote ndiye Muumba, na hakuna mwingine ila Yeye anayeweza kufanya kazi hii. Maneno haya ni “ushuhuda”—aina ya ushuhuda ambayo unapaswa kuwa nayo. Umepitia kuadibiwa, hukumu, usafishaji, majaribu, vipingamizi na majaribio hatua kwa hatua, na umeshindwa; umeweka kando matarajio ya mwili, nia zako binafsi, na maslahi ya ndani ya mwili. Yaani, maneno ya Mungu yameushinda moyo wako kabisa. Ingawa hujakua katika maisha yako kwa kiwango Anachotaka, unayajua mambo haya yote na unashawishika kabisa na kile Anachofanya. Kwa hivyo, hili linaweza kuitwa ushuhuda, ushuhuda ambao ni halisi na wa kweli. Kazi ambayo Mungu amekuja kufanya, kazi ya hukumu na kuadibu, inakusudiwa kumshinda mwanadamu, lakini pia Anahitimisha kazi Yake, akimaliza enzi na kutekeleza kazi ya hitimisho. Anakamilisha enzi nzima, Akiwaokoa wanadamu wote, Akiwakomboa wanadamu kutoka katika dhambi kabisa; Anawapata wanadamu Aliowaomba kikamilifu. Unapaswa kushuhudia haya yote. Umepitia kazi nyingi sana ya Mungu, umeiona kwa macho yako mwenyewe na kuipitia wewe binafsi; wakati umefika mwisho kabisa, ni lazima uweze kutenda kazi inayokupasa uifanye. Litakuwa jambo la kusikitisha kweli usipoweza! Katika siku zijazo, wakati injili inaenezwa, unapaswa kuweza kuzungumzia maarifa yako mwenyewe, ushuhudie yote uliyoyapata moyoni mwako na utumie jitihada yote. Kiumbe aliyeumbwa anapaswa kufanikisha hili. Umuhimu wa kweli wa hatua hii ya kazi ya Mungu ni upi? Athari yake ni ipi? Na ni kiwango chake kipi kinatekelezwa ndani ya mwanadamu? Watu wanapaswa kufanya nini? Unapoweza kuzungumza kwa uwazi kuhusu kazi yote ambayo Mungu mwenye mwili amefanya tangu aje duniani, basi ushuhuda wako utakuwa kamili. Unapoweza kuzungumza kwa uwazi kuhusu vitu hivi vitano: umuhimu wa kazi Yake; maudhui yake; kiini chake; tabia inayowakilisha; na kanuni zake, basi hili litathibitisha kwamba unaweza kumshuhudia Mungu, kwamba kweli una maarifa. Mahitaji yangu kwenu si ya juu sana, na yanaweza kutimizwa na wale wote wanaofuatilia kwa kweli. Ikiwa umeazimia kuwa mmoja wa mashahidi wa Mungu, ni lazima uelewe kile Mungu anachochukia sana na kile Mungu Anachopenda. Umepitia kazi Yake nyingi; kupitia kazi hii, ni lazima upate kujua tabia Yake, uelewe mapenzi Yake na mahitaji Yake kwa wanadamu, na utumie maarifa haya kumshuhudia na kutenda wajibu wako. Unaweza tu kusema: “Tunamjua Mungu. Hukumu na kuadibu Kwake havina huruma hata kidogo. Maneno Yake ni makali sana; ni ya haki na uadhama, na hayawezi kukosewa na mtu yeyote,” lakini maneno haya humkimu mwanadamu hatimaye? Yana athari gani kwa watu? Kweli unajua kwamba kazi hii ya hukumu na kuadibu ni ya manufaa zaidi kwako? Hukumu na kuadibu kwa Mungu vinafichua uasi na upotovu wako, sivyo? Vinaweza kutakasa na kuondoa vile vitu vichafu na vipotovu vilimo ndani yako, sivyo? Kusingekuwa na hukumu na kuadibu, hatima yako ingekuwa ipi? Kweli unafahamu kwamba Shetani amekupotosha kwa kiwango cha juu zaidi? Leo, mnapaswa kujitayarisha kwa vitu hivi na mvijue vyema.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Utendaji (7)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 443)

Je, mnajua ni nini mnachopaswa kujiandaa nacho? Jambo moja ni maono juu ya kazi, na jambo jingine ni matendo yako. Lazima ufahamu mambo yote mawili. Kama huna maono katika jitihada zako za kufanya maendeleo katika maisha, basi huna msingi. Kama una njia za matendo tu na huna maono hata kidogo, na huna ufahamu wowote wa kazi ya mpango mzima wa usimamizi, basi wewe ni bure. Lazima uelewe ukweli wa kipengele cha njozi, na kwa ukweli kuhusu matendo, unahitaji kupata njia mwafaka za kutenda mara unapozielewa; unahitaji kutenda kulingana na maneno, na uingie kulingana na hali zako. Maono ndiyo msingi, na usipozingatia hili, hutaweza kufuata hadi mwisho. Unapopitia njia hii, ama utapotea au kuanguka chini na kushindwa. Hakutakuwa na njia ya kufanikiwa! Watu ambao hawana maono makubwa kama msingi wao wanaweza tu kushindwa na si kufanikiwa. Huwezi kusimama imara! Je, unajua kuamini katika Mungu ni nini? Je, unajua kumfuata Mungu ni nini? Bila maono, ni njia gani ungeitembea? Katika kazi ya leo, kama huna maono hutaweza kufanywa mkamilifu kamwe. Unaamini katika nani? Kwa nini unamwamini Yeye? Mbona unamfuata Yeye? Je, unaamini kama aina ya mchezo? Je, unashughulikia maisha yako kama aina ya mtu anayechezewa? Mungu wa leo ndiye maono makubwa zaidi. Je, ni kiasi gani Chake unachokijua? Je, ni kiasi gani Chake ambacho umekiona? Je, baada ya kumwona Mungu wa leo, msingi wa imani yako katika Mungu u salama? Je, unafikiri kwamba mradi unafuata katika njia hii iliyovurugika, utapata wokovu? Unafikiri unaweza kuvua samaki katika maji yenye tope? Je, ni rahisi hivyo? Je, ni maoni mangapi yako kuhusu kile ambacho Mungu wa leo anasema umeweka chini? Je, una maono ya Mungu wa leo? Ufahamu wako wa Mungu wa leo umesimamia wapi? Daima wewe huamini kuwa unaweza kumpata Yeye[a] kwa kumfuata tu, kwamba kwa kumuona Yeye, na kwamba hakuna yeyote anayeweza kukukwepa. Usifikiri kwamba kumfuata Mungu ni rahisi sana. Cha muhimu ni kwamba ni lazima umjue Yeye, lazima uijue kazi Yake, na lazima uwe na nia ya kuvumilia shida kwa ajili Yake, uwe na nia ya kutoa maisha yako kwa ajili Yake, na uwe na nia ya kukamilishwa na Yeye. Haya ndiyo maono ambayo unapaswa kuwa nayo. Haitafaidi kama wewe daima unafikiria kufurahia neema. Usifikiri kwamba Mungu yupo tu kwa ajili ya starehe za watu, na kukirimu neema kwa watu. Wewe ulifikiri vibaya! Kama mtu hawezi kuhatarisha maisha yake ili kufuata, ama mtu hawezi kuacha kila mali ya dunia ili kufuata, basi kwa uhalisi hataweza kufuata hadi mwisho. Lazima uwe na maono kama msingi wako. Kama siku ya kupatwa kwako na maafa itakapokuja, unapaswa kufanya nini? Bado ungeweza kufuata? Usiseme kwa wepesi kama utaweza kufuata hadi mwisho. Ni bora kwanza ufungue macho yako wazi kabisa ili uone wakati wa sasa ni upi. Ingawa sasa mnaweza kuwa kama nguzo za hekalu, wakati utakuja ambapo nguzo hizi zote zitatafunwa na funza, na kusababisha hekalu kuanguka, kwa sababu kwa sasa kuna maono mengi sana ambayo mmekosa. Mnachozingatia tu ni dunia zenu wenyewe ndogo, na hamjui njia iliyo ya kutegemewa kabisa, njia iliyo mwafaka zaidi ya kutafuta ni ipi. Hamtilii maanani maono ya kazi ya leo, na hamyashikilii mambo haya mioyoni mwenu. Je, mmefikiria kwamba siku moja Mungu atawaweka katika mahali pasipojulikana? Je, mnaweza kuwazia siku ambayo huenda Nikawapokonya kila kitu, ni kipi kingewakumba? Nguvu yenu siku hiyo ingekuwa vile ilivyo sasa? Je, imani yenu ingejitokeza tena? Katika kumfuata Mungu, lazima myajue maono haya makubwa ambayo ni “Mungu.” Hili ndilo suala muhimu zaidi. Pia, msidhani kwamba katika kuachana na watu wa kidunia ili kuwa watakatifu kwamba nyinyi ni familia ya Mungu. Leo ni Mungu Mwenyewe ambaye anafanya kazi miongoni mwa uumbaji. Ni Mungu aliyekuja miongoni mwa watu kufanya kazi Yake mwenyewe, si kutekeleza kampeni. Miongoni mwenu, hakuna hata wachache ambao wanaweza kujua kwamba kazi ya leo ni kazi ya Mungu aliye mbinguni ambaye amekuwa mwili. Siyo juu ya nyinyi kufanywa watu waliojipambanua wenye vipaji. Badala yake, ni kuwasaidia kujua umuhimu wa maisha ya binadamu, kujua hatima ya binadamu, na kuwasaidia kumjua Mungu na uzima Wake. Unapaswa kujua kwamba wewe ni uumbaji mikononi mwa Muumba. Unachopaswa kufahamu, unachopaswa kufanya, na unavyopaswa kumfuata Mungu—je, huu si ni ukweli unaopaswa kuuelewa? Je, haya si ni maono ambayo unapaswa kuyaona?

Wakati ambapo mtu ana maono ana msingi. Unapotenda kwa msingi wa kanuni hii, itakuwa rahisi zaidi kuingia ndani. Kwa njia hii hutakuwa na wasiwasi punde unapopata msingi wa kuingia ndani, na itakuwa rahisi sana kwako kuingia ndani. Kipengele hiki cha kuyaelewa maono, cha kuielewa kazi ya Mungu ni muhimu. Lazima muwe mmejiandaa na kipengele hiki. Kama hujajiandaa na kipengele hiki cha ukweli, na wewe huongea tu juu ya njia za matendo, hii ni kasoro kubwa. Nimegundua kwamba wengi wenu hamsisitizi kipengele hiki, na wakati unaposikiliza kipengele hiki cha ukweli ni kama tu kusikiliza maneno ya mafundisho. Siku moja huenda ukapoteza. Kuna baadhi ya maneno sasa ambayo huyafahamu na huyakubali; kwa hiyo unapaswa kutafuta kwa uvumilivu, na siku itakuja utakapoelewa. Jiandae kidogo kidogo. Hata kama unaelewa mafundisho machache tu ya kiroho, ni bora kuliko kutoyazingatia. Ni bora kuliko kutoelewa mafundisho yoyote kamwe. Haya yote ni ya kusaidia kwa kuingia kwako, na yataondoa mashaka hayo yako. Ni bora kuliko kujazwa kwako na dhana. Ni bora zaidi kuwa na maono haya kama msingi. Bila kuwa na wasiwasi kamwe, inawezekana kuingia ndani kwa mikogo na majivuno. Kwa nini kujisumbua daima ukifuata kwa kukanganyikiwa kwa njia ya shaka? Je, hiyo si ni kama kuziba masikio yako wakati unaiba kengele? Ni jambo zuri kama nini kuingia katika ufalme kwa mikogo na majivuno! Kwa nini ujawe wasiwasi? Je, si huku hasa kungekuwa ni kupitia mateso? Unapokuwa na ufahamu wa kazi ya Yehova, wa kazi ya Yesu, na wa hatua hii ya kazi, basi utakuwa na msingi. Sasa unaweza kufikiri kwamba ni rahisi sana. Baadhi ya watu husema, “Wakati unapofika na Roho Mtakatifu anaanza kazi hii kubwa, nitaweza kuzungumza kuhusu mambo haya yote. Ukweli kwamba kwa kweli sielewi sasa ni kwa sababu Roho Mtakatifu hajanipatia nuru sana.” Si rahisi sana; sio kwamba huko tayari kuikubali ukweli[b] sasa, na kisha wakati utakapowadia utaitumia kwa ustadi. Si lazima iwe hivyo! Unaamini kuwa sasa umejiandaa vizuri sana, na kwamba haingekuwa shida kuwajibu wale watu wa kidini na wanadhaharia wakuu zaidi, na hata kuwakanusha. Je, ungeweza kweli kufanya hivyo? Je, ni ufahamu upi unaoweza kuuzungumzia na huo uzoefu wako duni tu? Kuwa umejiandaa na ukweli, kupigana vita ya ukweli, na kutoa ushuhuda kwa jina la Mungu si kile unachofikiri ndicho—kwamba mradi Mungu yuko kazini yote yatakamilishwa. Wakati huo labda utatatizwa na swali fulani, na utafadhaishwa. Cha muhimu ni kama uko dhahiri kuhusu hatua hii ya kazi au la, na ni kiasi gani unaielewa. Ikiwa huwezi kuyashinda majeshi ya adui, na wala kuyashinda majeshi ya kidini, basi si wewe ungekuwa bure? Kama umepata uzoefu wa kazi ya leo, ukaiona kwa macho yako mwenyewe na kuisikia kwa masikio yako mwenyewe, lakini mwishowe unashindwa kushuhudia, bado unathubutu kuendelea kuishi? Ungeweza kukabiliana na nani? Usifikiri kwa kawaida sana sasa. Kazi baadaye haitakuwa rahisi kama unavyofikiri itakuwa. Kupigana vita vya ukweli si rahisi au kawaida sana. Sasa unahitaji kujiandaa. Usipokuwa umejiandaa kwa ukweli sasa, wakati utakapowadia na Roho Mtakatifu hafanyi kazi kwa njia ya mwujiza, basi utakuwa umechanganyikiwa.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Lazima Muielewe Kazi—Msifuate kwa Rabsha!

Tanbihi:

a. Maandishi ya awali hayana neno “Yeye.”

b. Maandishi ya wali hayana neno “ukweli.”

Iliyotangulia: Kuingia Katika Uzima (I)

Inayofuata: Kuingia Katika Uzima (III)

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp