Kuingia Katika Uzima (VI)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 556)

Kwa kufuatilia ukweli tu ndipo mtu anaweza kutimiza mabadiliko katika tabia: Hili ni jambo ambalo watu wanafaa kufahamu na kulielewa vizuri kabisa. Usipokuwa na ufahamu wa kutosha wa ukweli, utateleza kwa urahisi na kupotoka. Ukitaka kukua katika maisha, lazima utafute ukweli katika kila kitu. Haijalishi kile unachokifanya, unapaswa utafute njia ya kutenda iliulingane na ukweli na utambue dosari zilizo ndani yako zinazoukiuka; ni lazima uwe na ufahamu wa wazi wa haya masuala. Haijalishi kile unachokifanya, unapaswa kuzingatia iwapo kina thamani au la. Unaweza kufanya mambo yaliyo na maana, lakini lazima usifanye mambo yasiyo na maana. Kuhusu mambo ambayo ungeweza kuyafanya ama kutoyafanya, iwapo yanaweza kuachiliwa, basi yafaa uyaachilie. Vinginevyo, ukifanya mambo haya kwa muda fulani na baadaye utambue kwamba unapaswa uyaachilie, basi fanya uamuzi upesi na uyaachilie haraka. Hii ndiyo kanuni unayofaa kuifuata katika kila kitu unachofanya. Watu wengine wanauliza swali hili: Mbona ni vigumu sana kutafuta ukweli na kuuweka katika matendo jambo gumu sana—kana kwamba unaelekeza mashua dhidi ya mkondo, na lingeweza kurudi nyuma iwapo utaiacha kuielekeza mbele? Mbona ni jambo rahisi zaidi kufanya mambo maovu ama vitu visivyo na maana—sawa na kuilekeza mashua kuufuata mkondo? Mbona iko hivi? Ni kwa sababu asili ya binadamu ni kumsaliti Mungu. Asili ya Shetani imechukua usukani wa kutawala ndani ya mwanadamu na hii ni nguvu ya kupinga. Wanadamu wenye asili ambayo inamsaliti Mungu bila shaka wana wepesi wa kufanya vitu vinavyomsaliti Yeye, na matendo mazuri kwa kawaida ni magumu kwao kutenda. Hii inaamuliwa kabisa na asili ya ubinadamu na kiini. Mara tu unapoelewa ukweli na unaanza kuupenda ukweli kutoka ndani yako mwenyewe, utakuwa na nguvu ya kufanya vitu vinavyopatana na ukweli. Hii kisha inakuwa kawaida, na hata bila juhudi na yenye kufurahisha, na unahisi kuwa kufanya chochote hasi kitahitaji juhudi za kiwango kikubwa. Hii ni kwa sababu ukweli umechukua utawala wa uongozi katika moyo wako. Kama kweli unauelewa ukweli kuhusianana maisha ya mwanadamu, na kuhusu aina gani ya mtu wa kuwa—jinsi ya kuwa mtu wa tabia ya hali ya juu na wazi, mtu mwaminifu, mtu anayetoa ushuhuda kwa Mungu na kumtumikia Yeye—basi kamwe hutaweza kufanya tena mambo maovu ambayo Yanamkataa na kamwe hutachukua jukumu la kuwa kuongozi wa uongo, mfanyakazi wa uongo au mpinga Kristo. Hata kama Shetani akikudanganya, au mtu mwovu akikulazimisha, bado hutatenda kwa njia hiyo. Watu wanapopata ukweli na kuhisi chuki ndani kwa vitu hasi. Itakuwa vigumu kwao kutenda uovu, kwa sababu tabia yao ya maisha imebadilika na wamekamilishwa na Mungu.

Kama kwa kweli una ukweli ndani yako, njia unayotembea kiasili itakuwa njia sahihi. Bila ukweli, ni rahisi kufanya uovu na hutakuwa na budi kuufanya. Kwa mfano, kama kiburi na majivuno, vingekuwa ndani yako, ungeona kwamba haiwezekani kuepuka kumwasi Mungu; ungehisi kulazimishwa kumwasi. Hutafanya hivyo kimakusudi; utafanya hivyo chini ya utawala wa asili yako ya kiburi na majivuno. Kiburi na majivuno yako vitakufanya umdharau Mungu na kumwona kuwa asiye na maana; vitakufanya ujiinue, vitakufanya kujiweka kila wakati kwenye maonyesho, na mwishowe vitakufanya ukae katika nafasi ya Mungu na kujitolea ushuhuda mwenyewe. Mwishowe utayabadilisha mawazo yako mwenyewe, fikira zako mwenyewe na dhana zako yawe ukweli wa kuabudiwa. Tazama ni kiasi gani cha uovu kinafanywa na watu chini ya utawala wa asili yao ya kiburi na majivuno! Kutatua matendo yao maovu, lazima kwanza watatue matatizo ya asili yao. Bila mabadiliko katika tabia, haitawezekana kuleta suluhu ya kimsingi kwa shida hii. Unapokuwa na uelewa fulani wa Mungu, unapoweza kuona upotovu wako mwenyewe na kutambua uhafifu na ubaya wa kiburi na majivuno, basi utahisi chuki, kughadhabishwa na kutatizwa. Utaweza kufanya mambo kwa ufahamu kumridhisha Mungu na kwa kufanya hivi, utahisi utulivu. Utaweza kwa ufahamu kutoa ushuhuda kwa Mungu na kwa kufanya hivi, utahisi raha. Kwa ufahamu utajifichua mwenyewe, huku ukifunua ubaya wako, na kwa kufanya hivi, utahisi vizuri ndani yako na kujihisi kuwa katika hali iliyoboreka ya akili. Hivyo basi, hatua ya kwanza ya kutafuta mabadiliko katika tabia yako ni kutafuta kuyaelewa maneno ya Mungu na kuingia katika ukweli. Ni kwa kuuelewa tu ukweli ndio unaweza kufikia utambuzi; ni kwa kuwa na utambuzi tu ndio unaweza kuelewa mambo kabisa; ni kwa kuelewa mambo tu kwa wazi ndio unaweza kuutelekeza mwili na, hatua kwa hatua, kuwa kwa njia sahihi ukiwa na imani kwa Mungu. Hii imeungana na jinsi wanadamu walivyo na uamuzi wanapotafuta ukweli. Kama mtu amefanya uamuzi wa kweli, basi baada ya miezi sita ama mwaka mmoja wataanza kuingia katika njia sahihi. Katika miaka mitatu au mitano, wataona matokeo, na watahisi kuwa wamefanya maendeleo katika maisha. Kama unamwamini Mungu lakini hautafuti ukweli, basi utaweza kuamini kwa miaka 10 bila kupata mabadiliko yoyote. Mwishowe, utafikiri kwamba hii hasa ndiyo maana ya kumwamini Mungu, utafikiri ni sawa tu na jinsi ilivyoishi duniani awali na kuwa hasi hakuna maana. Hii kwa kweli inaonyesha kuwa bila ukweli, maisha ni matupu. Unaweza kunena baadhi ya maneno ya kanuni, lakini bado utahisi usiyefarijika na kutokuwa na utulivu. Kama watu wanaujuzi fulani kumhusu Mungu, kama wanajua jinsi ya kuishi maisha yenye maana, na wanaweza kufanya mambo yanayomridhisha Mungu, basi watahisi kuwa haya ni maisha ya kweli, kuwa kwa kuishi tu kwa njia hii ndiposa maisha yao yatakuwa na maana, na kuwa mtu inawalazimu kuishi kwa njia hii ili kuweza kumridhisha Mungu kidogo na kuhisi wenye kuridhika. Kama wanaweza kumridhisha Mungu kwa ufahamu, kuweka ukweli katika matendo, wajitelekeze mwenyewe, waache mawazo yao wenyewe, na wawe watiifu na kuyafikiria mapenzi ya Mungu—kama wanaweza kufanya mambo haya yote kwa ufahamu—basi hii ndio maana ya kuuweka ukweli katika matendo kisahihi, na kuuweka ukweli kwa kweli katika matendo na ni kinyume kwani walitegemea mawazo yao awali na kufuata kwako kwa kanuni na sheria. Kwa ukweli halisi, inachosha kufanya chochote wakati hawaelewi ukweli, inachosha kufuata mafundisho na sheria, na inachosha kutokuwa na malengo na kuwa unafanya mambo kwa upofu. Ni kwa ukweli tu ndiyo wanaweza kuwa huru—huu sio uongo—na kwa ukweli wanaweza kufanya mambo kwa urahisi na kwa njia ya furaha. Wale walio na hali ya aina hii ni watu walio na ukweli; wao ndio wale ambao tabia zao zimebadilishwa.

Kimetoholewa kutoka katika “Ni Kwa Kufuatilia Ukweli Tu Ndiyo Unaweza Kupata Mabadiliko Katika Tabia Yako” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 557)

Wakati wa kutafuta kuingia, kila jambo lazima lichunguzwe. Mambo yote lazima yatafakiriwe kulingana na neno la Mungu na ukweli ili ujue jinsi ya kuyashughulikia kwa njia ambayo inalingana kikamilifu na mapenzi ya Mungu. Mambo yanayotokea kutoka kwa mapenzi yako kisha yanaweza kuachwa. Utajua jinsi ya kufanya mambo kulingana na mapenzi ya Mungu na basi utaenda uyafanye; itahisi kana kwamba kila kitu kinafuata mkondo wake, na itaonekana ikiwa rahisi kabisa. Hivi ndivyo watu walio na ukweli hufanya mambo. Kisha unaweza kuonyesha wengine kuwa tabia yako imebadilika, na wataona kuwa kwa hakika umetenda matendo mazuri, kwamba unafanya mambo kulingana na kanuni, na kwmba unafanya kila kitu sawa. Huyu ni mtu anayeelewa ukweli, na ambaye kwa kweli ana mfano fulani wa ubinadamu. Kwa hakika kabisa, neno la Mungu limevuna matokeo kwa watu. Mara tu watu kwa kweli wanaelewa ukweli, wanaweza kutambua hali zao wenyewe za kuwa, kuona hadi kina cha masuala magumu na kujua njia inayofaa kutenda. Iwapo huelewi ukweli, hutaweza kutambua hali zako za kuwepo. Utataka kuasi dhidi yako mwenyewe lakini hutakuwa na wazo la kukifanya ama unachoasi dhidi yake. Utataka kujiacha mapenzi yako lakini ukifikiria kuwa mapenzi yako yanapatana na ukweli, basi utaweza vipi kuiacha? Unaweza hata kufikiri kuwa imepewa nuru na Roho Mtakatifu, na kwa hivyo kukataa kuiacha hata iweje.Hivyo, wakati watu hawana ukweli, wana uwezekano wa kufikiri kwamba chochote kinachotokana na mapenzi yao ya kibinafsi, uchafu wao wa kibinadamu na nia njema, upendo wa uliokanganyika wa binadamu na mazoea ya kibinadamu ni sahihi, na kwamba yanalingana na ukweli. Unawezaje, basi, kuasi dhidi ya vitu hivi? Kama huelewi ukweli, au kujua ni maana ya kuuweka ukweli katika matendo, na kama macho yako yamefungwa na hujui pa kugeukia njia gani na hivyo basi unaweza tu kufanya mambo tu kulingana na kile unachofikiri ni sawa, basi utatenda mambo mengine ambayo yatapotoka na yenye makossa. Baadhi ya haya matendo yatakuwa ni kwa kutelekeza kulingana na, masharti, mengine yatatokea kwa shauku na mengine yatakuwa yametokea kutoka kwa Shetani na kuwa yatasababisha usumbufu. Watu wasio na umiliki wa ukweli wanatenda mambo kwa njia hii: kidogo kushoto, kisha kidogo kwa kulia, sahihi dakika moja na kisha kupotoka inayofuata, bila usahihi wowote. Wale wasiomiliki n ukweli wanachukua mtazamo mbaya wa vitu, hivyo basi watawezaje kushughulikia masuala vizuri? Wataweza kutatua vipi shida zozote? Kuuelewa ukweli sio kitu rahisi kufanya. Kuweza kuelewa maneno ya Mungu inategemea, kuelewa ukweli na ukweli ambao watu wanaweza kuelewa pia una viwango vyake. Kuelewa kwao kwa maneno ya Mungu kutazuiliwa hata iwapo wamwamini Yeye kwa maisha yao yote. Hata wale ambao wamepata uzoefu kiasi wanaweza kufikia wakati ambapo wanakoma kuepuka kufanya yale mambo ambayo yanamkataa Mungu, kukoma kufanya yale mambo ambayo kwa dhahiri ni maovu, na kukoma kufanya yale mambo ambayo hayamsaidii yeyote. Haiwezekani kwao kutimia hali ambayo haina mchanganyiko wa mapenzi yao wenyewe ndani yake. Hii ni kwa sababu watu huwaza mawazo ya kawaida, na baadhi ya mawazo yao yanazingatia maneno ya Mungu na ni ya kipengele cha ufahamu ambacho hakiwezi kuainishwa kama mapenzi ya kibinafsi. Hata hivyo cha msingi ni kutambua sehemu ya mapenzi ya kibinafsi ambayo yanaenda kinyume na maneno ya Mungu, kinyume na ukweli na kinyume na mwangaza kutoka kwa Roho Mtakatifu. Kwa hivyo lazima utie juhudi kujua manenoya Mungu na ni kwa kuuelewa ukweli tu ndio unaweza kuwa na utambuzi.

Kimetoholewa kutoka katika “Ni Kwa Kufuatilia Ukweli Tu Ndiyo Unaweza Kupata Mabadiliko Katika Tabia Yako” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 558)

Ili ujijue, ni lazima ujue maonyesho ya upotovu, udhaifu wako mkuu, tabia yako, na asili yako na kiini chako. Lazima pia ujue, maelezo yote kabisa, mambo hayo ambayo hufichuliwa katika maisha yako ya kila siku—nia zako, mitazamo yako, na msimamo wako kuhusu kila kitu—iwe uko nyumbani au nje, unapokuwa kwenye mikusanyiko, unapokuwa ukila na kunywa maneno ya Mungu, au katika kila suala unalokumbana nalo. Kupitia vitu hivi lazima uje kujijua. Ili kujijua kwa kina, lazima ujumuishe maneno ya Mungu; unaweza tu kupata matokeo kwa kujijua kulingana na maneno Yake. Wakati ambapo tunapokea hukumu ya maneno ya Mungu, hatupaswi kuogopa mateso, wala hatupaswi kuogopa maumivu; na sembuse kuogopa kwamba maneno ya Mungu yataumiza mioyo yetu. Tunapaswa kusoma matamshi Yake zaidi kuhusu jinsi Anavyotuhukumu na kutuadibu na kufichua asili zetu potovu. Lazima tuyasome na kuyafuata na kujilinganisha kwayo mara kwa mara. Kamwe usiwalinganishe wengine nayo—tunafaa tujilinganishe wenyewe dhidi. Hatuna upungufu wowote katika vitu hivi vyote; sote tunaweza kulingana nao. Kama huamini hili, nenda ujionee mwenyewe. Baada ya kusoma maneno ya Mungu, watu wengine hawawezi kuyatumia wao wenyewe; wanadhani kwamba sehemu fulani za maneno haya haziwahusu lakini badala yake, zinawahusu watu wengine. Kwa mfano, Mungu anapowafunua watu kama wazinzi na makahaba, kina dada wengine huhisi kwamba kwa sababu hakika wamekuwa waaminifu kwa waume zao, maneno kama hayo hakika hayawahusu; kina dada wengine huhisi kwamba kwa kuwa hawajaolewa na hawajawahi kufanya mapenzi, maneno kama hayo hakika hayawahusu pia. Ndugu wengine huhisi kuwa maneno haya yanalenga wanawake tu na hayahusiani nao; watu wengine huamini kuwa maneno kama haya ya Mungu hayapendezi sana wanapoyasikia na wao hukataa kuyakubali. Hata kuna watu wanaosema kuwa katika mifano mingine, maneno ya Mungu si sawa. Je, huu ni mtazamo unaofaa kuwa nao kwa maneno ya Mungu? Watu hawana uwezo wa kutafakari juu yao wenyewe kulingana na maneno ya Mungu. Hapa, maneno “wazinzi” na “makahaba” yanahusu upotovu wa watu wa uzinzi. Iwe mtu ni mwanamume au mwanamke, iwe amefunga ndoa au la, kila mtu ana upotovu wa uzinzi—kwa hivyo jambo hilo linawezaje kutokuhusu? Maneno ya Mungu hufunua tabia potovu za watu; wawe wa kiume au wa kike, kiwango cha mtu cha upotovu ni sawa. Je, huu si ukweli? Kabla ya kufanya chochote kingine, tunafaa kutambua kwamba tunafaa kukubali kila mojawapo ya neno lililonenwa na Mungu, iwe matamshi haya yanavutia kusikia au hayavutii na ikiwa yanatupatia hisia chungu au tamu. Huu ndio mtazamo tunaopaswa kuwa nao juu ya maneno ya Mungu. Je, hii ni aina gani ya mtazamo? Je, ni mtazamo wa mcha Mungu, Mtazamo wa uvumilivuau, ni mtazamo wa kukumbatia mateso? Ninawaambia, hayo si kati ya yeyote ya haya. Katika imani yetu, lazima tusisitize kwa uthabiti kwamba maneno ya Mungu ndiyo ukweli. Kwa kuwa kweli ndiyo ukweli, tunapaswa kuyakubali kwa busara. Bila kujali ikiwa tunaweza kutambua au kukubali au la, mtazamo wetu wa kwanza kuelekea maneno ya Mungu unapaswa kuwa ule wa kukubali kabisa. Kila mstari wa maneno ya Mungu unafungamana na hali fulani. Yaani, hakuna kati ya mistari yote ya matamshi Yake yanahusu kuonekana nje, sembuse sheria za nje au tabia ya aina rahisi ndani ya watu. Hayako hivyo. Ikiwa wewe huona kila mstari unaotamkwa na Mungu kama linahusu aina rahisi ya tabia ya mwanadamu au kama jambo linaloonekana nje, basi huna ufahamu wa kiroho na huelewi ukweli ni nini. Maneno ya Mungu ni ya maana sana. Je, ni ya maana vipi? Kila kitu ambacho Mungu husema, kila kitu ambacho hufichua kinahusu tabia potovu za watu, na vitu muhimu na vilivyokita mizizi ndani ya maisha yao. Hayo ni mambo muhimu, si mambo yanayoonekana nje, na haswa si tabia za nje. Kwa kuwatazama watu kutoka kwa jinsi wanaonekana nje, wote wanaweza kuonekana kuwa sawa. Kwa nini, basi, Mungu anasema kuwa watu wengine ni roho waovu na wengine ni roho wachafu? Hili ni jambo ambalo halionekani kwako. Kwa hvyo, huwezi kutegemea sura au kile unachoona kwa nje kulinganisha na maneno ya Mungu. Baada ya kufanyiwa ushirika kwa namna hiyo, je, mmepitia mabadiliko katika mtazamo wenu kwa maneno ya Mungu? Bila kujali mabadiliko ni makubwa au madogo jinsi gani, wakati ujao mtakaposoma maneno kama haya, angalau hamtajaribu kujadiliana na Mungu. Hutasema, “Ni vigumu kuyasikiliza maneno ya Mungu; sitasoma ukurasa huu. Nitauruka tu! Hebu nitafute mambo ya kusoma yanayohusu baraka na ahadi ili nipate faraja kiasi.” Sharti msichague yale mnayosoma kwa namna hiyo.

Kimetoholewa kutoka katika “Umuhimu wa Kufuatilia Ukweli na Njia ya Kuufuatilia” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 559)

Mnaelewa vipi asili ya mwanadamu? Kuifahamu asili yako kunamaanisha kugawanya vina vya nafsi yako kwa kweli; kunahusu kile kilicho katika maisha yako. Ni mantiki ya Shetani na mitazamo ya Shetani ambayo umekuwa ukiishi kulingana nayo; yaani, ni maisha ya Shetani ambayo umekuwa ukiishi kulingana nayo. Ni kwa kufukua tu sehemu za kina kabisa za nafsi yako ndio unaweza kuifahamu asili yako. Vitu hivi vinaweza kufukuliwa namna gani? Hayawezi kufukuliwa au kugawanywa kupitia tu tukio moja au matukio mawili; wakati mwingi, baadaa ya kukamilisha kufanya jambo, bado hutakuwa umepata kuelewa. Inaweza kuchukua miaka mitatu au mitano kabla Kuweza kupata hata chembe kidogo cha ugunduzi na ufahamu. Katika hali nyingi, lazima ujitafakari na ujijue, na ni wakati tu unapofanya mazoezi ya kuchimba kwa kina ndipo utaona matokeo. Kadiri ufahamu wako wa ukweli unavyozidi kuwa wa kina, pole pole utapata kujua asili na kiini chako mwenyewe kupitia kujitafakari na kujitambua. Ili kujua asili yako, lazima utimize vitu vichache. Kwanza, lazima uwe na uelewa dhahiri wa kile upendacho. Hili halihusu vitu unavyopenda kula au kuvaa; bali, linamaanisha aina ya vitu unavyofurahia, vitu unavyohusudu, vitu unavyoabudu, vitu unavyotafuta, na vitu unavyozingatia moyoni mwako. Aina ya watu unaofurahia kuwasiliana nao, aina ya vitu unavyopenda kufanya, na aina ya watu unaopenda mno ndani ya moyo wako. Kwa mfano, watu wengi huwapenda watu mashuhuri, watu ambao ni wa madaha katika usemi wao na tabia zao, au kama wale ambao huzungumza kwa lugha ya ushawishi yenye sifa mno au wale ambao hujifanya. Lililotajwa hapa mbeleni linahusu watu ambao wanapenda kushirikiana nao. Kuhusu vitu ambavyo watu hufurahia, hivi vinajumlisha kuwa radhi kufanya vitu fulani ambavyo ni rahisi kufanya, kufurahia kufanya vitu ambavyo watu wengine hufikiri ni vizuri na ambavyo vitasababisha watu kuimba sifa na kupeana taadhima. Katika asili za watu, kuna sifa zenye usawa kuhusu vitu ambavyo wao hupenda. Yaani, wanapenda watu, matukio na vitu ambavyo watu wengine wanahusudu kwa sababu ya mwonekano wa nje, wanapenda watu, matukio na vitu vinavyoonekana vizuri na vya anasa, na wanapenda watu, matukio na vitu ambavyo huwafanya watu wengine kuwaabudu kwa sababu ya sura zao za nje. Hivi vitu ambavyo watu hupenda ni vizuri, vya kung'aa, vya kupendeza, na vya fahari. Watu wote huabudu vitu hivi. Inaweza kuonekana kwamba watu hawana ukweli wowote, wala hawana mfano wa wanadamu wa kweli. Hakuna kiwango hata kidogo cha umuhimu katika kuabudu vitu hivi, ilhali watu bado huvipenda. …Unaweza kuwa mzuri kwa mtu fulani kwa muda, lakini hili halithibitishi kwamba unampenda. Kile unachopenda sana kweli ndicho hasa kilicho katika asili yako; hata kama mifupa yako ingekuwa imevunjwa, bado ungekifurahia na hungeweza kukiacha. Hili si rahisi kubadilisha. Chukua mfano wa kutafuta mwenzi. Kama mwanamke amezama katika mapenzi na mtu fulani kwa kweli, basi hakuna yeyote anayeweza kumzuia. Hata kama miguu yake ingevunjika, bado angetaka kuwa na mwanamume huyo; angetaka aolewe na mume huyo hata iwapo angekufa. Hili linawezekanaje? Ni kwa sababu hakuna anayeweza kubadilisha yale ambayo watu wanayo ndaniyao kabisa. Hata kama mtu angekufa, nafsi yake bado ingekipenda vitu vile vile; hivi ndivyo vitu vya asili ya binadamu, na vinawakilisha kiini cha mtu. Vitu ambavyo watu huvipenda huwa na udhalimu fulani, vingine ni dhahiri na vingine sio; vingine ni kali na vingine sivyo; watu wengine wana kiasi, ilihali wengine hawawezi kujidhibiti. Baadhi yawatu ni wepesi wa kuzama ndani ya vitu visivyo na uwazi, ambavyo vinathibitisha kwamba hawana hata chembe kidogo cha uhai. Kama watu wanaweza kutomilikiwa na kubanwa na vitu hivyo, inathibitisha kwamba tabia zao zimegeuzwa kidogo na kwamba walikuwa na kimo kidogo. Watu wengine huelewa ukweli fulani na huhisi kwamba wana uzima na kwamba wanampenda Mungu. Kwa kweli, bado ni mapema sana, na wanapitia mageuzi ya tabia ya mtu si jambo rahisi. Je, asili ya mtu ni rahisi kuifahamu? Hata kama ungeielewa kidogo, haingekuwa rahisi kubadilisha. Hii ni sehemu ngumu kwa watu. Haijalishi jinsi watu, masuala, au vitu karibu nawe vinaweza kubadilika, na haijalishi jinsi ulimwengu unaweza kugeuzwa juu chini, ikiwa ukweli ndani yako unakuongoza kutoka ndani, ikiwa imekita mizizi ndani yako, na maneno ya Mungu yanaongoza maisha yako, unayopenda, uzoefu na maisha yako, wakati huo basi utakuwa umegeuka kweli. Sasa hiki kinachodaiwa kuwa mgeuzo ni watu kushirikiana na kuwa na kiasi kidogo cha shauku na imani tu, lakini hili kamwe haliwezi kufikiriwa kuwa geuzo na halithibitishi kamwe kwamba watu wana uzima; ni hiari tu za watu hakuna la ziada.

Kuongezea kwa kufukua vitu ambavyo watu huvipenda sana ndani ya asili zao, vipengele vingine vinavyohusiana na asili zao vinahitaji kufukuliwa pia, Kwa mfano, mitazamo ya watu kuhusu vitu, mbinu na malengo ya watu katika maisha, maadili ya maisha na mitazamo kuhusu maisha ya watu, pamoja na mitazamo kuhusu vitu vyote vinavyohusiana na ukweli. Hivi ni vitu vyote vilivyo ndani kabisa ya nafsi za watu na vina uhusiano wa moja kwa moja na mgeuzo wa tabia. Je, basi mtamzamo wa Maisha kuhusu mtu aliye na nafsi potovu ni upi? Inaweza kusemw kuwa hili: “Kila mwamba ngoma huvutia upande wake.” Watu wote wanaishi kwa ajili yao wenyewe; kuiweka wazi zaidi, wanaishi kwa ajili ya mwili. Wanaishi tu ili wapatae chakula. Je, kuishi huku kunatofautianaje na kule kwa wanyama? Hakuna thamani yoyote katika kuishi namna hii, sembuse kuwepo maana yoyote. Mtazamo wa maisha ya mtu unahusu kile unachotegemea kuishi duniani, kile unachokiishia, na jinsi unavyoishi—na haya yote ni mambo yanayohusiana na kiini cha asili ya wanadamu. Kwa kugawanya asili za watu, utaona kwamba watu wote wanampinga Mungu. Wote ni mashetani na hakuna mtu mzuri kwa kweli. Ni kwa kuchangua tu asili za watu tu ndio unaweza kujua kweli dutu na upotovu wa mwanadamu na kufahamu watu wanamilikiwa na nini hasa, kile watu wanakosa kweli, kile wanapaswa kujizatiti nacho, na jinsi wanapaswa kuishi kwa kudhihirisha mfano wa binadamu. Kuchangua kweli asili ya mtu si rahisi, na haiwezi kufanywa bila kupitia maneno ya Mungu au kuwa na uzoefu wa kweli.

Kimetoholewa kutoka katika “Unachopaswa Kujua Kuhusu Kuigeuza Tabia Yako” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 560)

Je, ni vitu vipi vya asili ya mwanadamu? Unajua tu kuhusu upotovu wa mwanadamu, uasi, upungufu, dosari, fikra, na dhamira, lakini huwezi kugundua sehemu za ndani za asili ya mwanadamu—unafahamu tu safu ya nje, lakini huwezi kugundua chanzo chake. Baadhi hata hufikiri haya mambo ya juu kuwa ni asili ya mwanadamu, wakisema, “Ona, ninaelewa asili ya mwanadamu; ninatambua ufidhuli wangu. Je, hiyo si asili ya mwanadamu?” Je, haitoshi kuikubali kikanuni pekee? Ufidhuli ni kitu cha asili ya mwanadamu; huu ni ukweli kabisa. Je, kujua asili ya mtu binafsi ni nini? Inawezaje kujulikana? Je, inajulikana kutoka kwa vipengele vipi? Aidha, asili ya mtu inapaswa kutazamwa vipi kupitia vitu ambavyo mtu amefichua? Kwanza kabisa, unaweza kuona asili ya mtu kupitia mapendeleo yake. Jinsi gani? Mathalani, baadhi ya watu hususan hupenda kudansi, wengine hususan huwapenda waimbaji ama magwiji wa kuigiza filamu, na watu wengine hususan hupenda sana watu fulani mashuhuri. Kwa kutazama mapendeleo haya, ni nini asili ya watu hawa? Nitatoa mfano mwingine ambao ni rahisi: Wengine huenda wanampenda mwimbaji fulani mno, hata kwa kiasi kwamba wameshika kila mwondoko wa mwimbaji huyu, kila tabasamu, na kila neno lake. Wanatawaliwa na tama ya mwimbaji, na wanapiga picha kila kitu anachovaa mwimbaji huyu na kuiiga. Je, kiwango hiki cha kupenda mno kinaonyesha nini kuhusu asili ya mtu? Kinaonyesha kuwa moyo wa mtu kama huyu una vitu hivyo tu, wala hauna Mungu. Vitu vyote ambavyo mtu huyu huwaza, hupenda, na kutafuta vinafichuliwa kabisa na Shetani; vinamiliki moyo wa mtu huyu, ambao unajishughulisha sana na vitu hivyo. Je, unaona tatizo ni lipi? Ikiwa kitu kinapendwa kupita kiasi, basi kitu hicho kinaweza kuwa maisha ya mtu na kumiliki moyo wake, kudhihirisha wazi kuwa mtu huyo ni mwabudu sanamu asiyemtaka Mungu na badala yake anampenda ibilisi. Kwa hivyo tunaweza kufikia uamuzi kuwa asili ya mtu kama huyu ni ile inayopenda na kuabudu ibilisi, haipendi ukweli, na haimtaki Mungu. Je, hii ni njia sahihi kabisa ya kutazama asili ya mtu? Ni sahihi kabisa. Hivi ndivyo asili ya mtu inavyochanguliwa. Kwa mfano, watu wengine hususan humpenda Paulo sana. Wanapenda kwenda na kuhutubu na kufanya kazi, wanapenda kukutana pamoja na kuzungumza; wanapenda watu kuwasikiza, kuwaabudu, na kuwazingira. Wanapenda kuwa na hadhi katika mawazo ya wengine, na wanafurahia wakati wengine wanathamini mifano yao. Hebu tuchanganue asili yao kutoka kwa tabia hizi: Je, asili yao ni ipi? Kama kweli wanatenda kwa njia hii, basi hilo linatosha kuonyesha kuwa wao ni fidhuli na wenye majivuno. Hawamwabudu Mungu hata kidogo; wanatafuta hadhi ya juu zaidi, na wangependa kuwa na mamlaka juu ya wengine, kuwamiliki, na kuwa na hadhi akilini mwao. Huu ni mfano bora wa Shetani. Vipengele vya asili yao vinavyojitokeza ni ufidhuli na majivuno, kutokuwa radhi kumwabudu Mungu, na tamaa ya kuabudiwa na wengine. Tabia kama hizi zinaweza kupa mtazamo dhahiri sana juu ya asili yao.

Kimetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 561)

Wanadamu wote wamepotoshwa na Shetani, na asili ya mwanadamu ni kumsaliti Mungu. Hata hivyo, miongoni mwa wanadamu wote ambao wamepotoshwa na Shetani, kuna baadhi yao wanaoweza kulitii neno la Mungu na kukubali ukweli; hawa ndio wale wanaoweza kupata ukweli na kutimiza mbadiliko wa tabia. Pia kuna wale ambao hawazingatii kutafuta ukweli. Wanaridhika na kuelewa tu mafundisho; wao husikia mafundisho mazuri na kuyashika, na baada ya kuyaelewa, wanaweza kutekeleza wajibu wao—kwa ukamilifu. Watu hawa hufanya kile wanachoambiwa na wana ubinadamu duni. Wako radhi, kwa kiasi fulani, kujitumia, kuacha ya malimwengu, na kuvumilia mateso. Hata hivyo, kamwe hawana bidii kuhusu ukweli; wanaamini inatosheleza kwamba hawatendi dhambi na wana uwezo wa kuelewa kiini cha ukweli. Ikiwa watu kama hao wanaweza kusimama imara mwishowe wanaweza kusamehewa, lakini haiwezekani tabia yao kubadilishwa. Iwapo ungependa kusafishwa kutokana na upotovu na kupitia mabadiliko ya tabia maishani mwako basi unahitaji kuupenda ukweli na uwezo wa kuukubali ukweli. Inaamanisha nini kuukubali ukweli? Kukubali ukweli kunaashiria kwamba bila kujali aina ya tabia potovu unayo au ni sumu gani ya joka kuu jekundu imeingia ndani ya asili yako, unakiri unapofichuliwa na manenoya Mungu na kulitii maneno haya; unayakubali bila kupinga, bila kutoa sababu za kutotii au kufanya chaguo, na unakuja kujijua mwenyewe kwa mujibu wa yale Amesema. Hivi ndivyo inavyomaanisha kukubali neno la Mungu. Bila kujali kile ambacho Amesema, bila kujali kiasi ambacho matamshi Yake yanaweza kuuchoma moyo wako, na bila kujali maneno Anayotumia, unaweza kulikubali mradi uwe ukweli, unaweza kuyakubali mradi yanapatana na uhalisi. Unaweza kuyatii maneno ya Mungu bila kujali unayaelewa kwa kina kiasi gani, na ukubali na kutii mwanga ambao unafichuliwa na Roho Mtakatifu ambao unashirikiwa ba ndugu na dada. Wakati mtu wa aina hii amefuata ukweli hadi kiwango fulanianaweza kupata ukweli na kufikia kubadilishwa kwa tabia yake. Hata iwapo wale wasiopenda ukweli wanaweza kuwa wenye ubinadamu mwema, inapokuja kwa ukweli, wao hawachukui msimamo na hawalichukulii kwa makini. Ingawa wanaweza kuwa wenye matendo mema, na wanaweza kujitoa kwa kutumiwa na Mungu, na wanaweza kumkana Shetani, hawawezi kutimiza kubadilika kwa tabia zao. Kwa kulinganisha, ubinadamu wa Petro ulikuwa kama ule wa mitume wengine na ndugu na dada zake lakini alijitokea vizuri katika kutafuta. Alitafakari kwa dhati kila kitu ambacho Yesu alikisema kwa bidii. Yesu aliuliza, “Simoni, wanipenda?” Akajibu moja kwa kweli, “Ee, nampenda tu Baba ambaye yuko mbinguni, ilihali sijampenda Bwana aliye duniani!” Baadaye alielewa, akifikiria “Hili si sawa!” Mungu aliye duniani ndiye Mungu aliye mbinguni. Je, si Mungu yule yule mbinguni na duniani? Iwapo ninampenda tu Mungu aliye mbinguni pekee, basi upendo wangu sio halisi; sharti nimpende Mungu duniani, kwani hapo tu ndipo upendo wangu utakuwa halisi.” Hivyo, Petro alikuja kuelewa maana ya kweli ya kile ambacho Yesu alisema kwa kutafakari maneno Yake. Ili kumpenda Mungu, na ili upendo huu uwe halisi, mtu lazima apende Mungu mwenye mwili dunian. Kumpenda Mungu asiye dhahiri na asiyeonekana hakuna tu uhalisi ila pia hakuna vitendo Ilihali kumpenda Mungu halisi na Anayeonekana ni ukweli. Kutokana na maneno ya Yesu, Petro alipata ukweli na ufahamu wa mapenzi ya Mungu. Bila shaka, imani ya Petro kwa Mungu ilikuwa imezingatia ufuatiliaji wa ukweli, na hatimaye akatimiza upendo wa Mungu wa vitendo—Mungu aliye duniani. Petro hususan alikuwa na ari katika ufuatiliaji wake wa ukweli. Kila wakati Yesu alipomshauri, alitafakari maneno ya Yesu kwa ari. Labda alitafakari kwa miezi, mwaka, ama hata miaka kabla ya Roho Mtakatifu kumpatia nuru na akaelewa maana ya maneno ya Mungu. Kwa kupitia njia hii, Petro aliingia katika ukweli, na baadaye maisha yake ikabadilishwa na kufanywa upya. Mtu asipoutafuta ukweli, kamwe hatauelewa. Unaweza kusema maandiko na mafundisho mara elfu kumi, lakini bado yatakuwa tu maandiko na mafundisho. Baadhi ya watu husema tu, “Kristo ndiye ukweli, njia na uzima.” Hata ukirudia maneno haya mara elfu kumi, bado itakuwa ni bure; huna ufahamu wa maana yake. Kwa nini inasemwa kuwa Kristo ndiye ukweli, njia na uzima? Je, unaweza kuelezea kwa ufasaha ufahamu uliopata kuhusu haya kwa uzoefu? Je, umeingia katika uhalisi wa ukweli, njia na uzima? Mungu ametamka maneno yake ili wewe uweze kuyapata na kupata maarifa; kuongea tu maandiko na mafundisho haina maana. Unaweza tu kujijua mara unapoelewa na kuingia katika maneno ya Mungu. Ikiwa huelewi maneno ya Mungu, basi huwezi kujijua. Unaweza tu kumaizi unapokuwa na ukweli; bila ukweli huwezi kumaizi. Unaweza tu kuelewa kikamilifu jambo unapokuwa na ukweli; bila kuwa na ukweli huwezi kuelewa jambo. Unaweza tu kujijua unapokuwa na ukweli; bila kuwa naukweli huwezi kujijua. Asili yako inaweza tu kubadilika unapokuwa na ukweli; bila ukweli asili yako haiwezi kubadilika. Ni baada tu ya wewe kuwa na ukweli ndipo unaweza kuhudumu kulingana na mapenzi ya Mungu; bila ukweli huwezi kutumiki kulingana na mapenzi ya Mungu. Ni baada tu ya kuwa na ukweli ndipo unaweza kumwabudu Mungu; bila ukweli, ibada yako itakuwa tu utendaji wa kaida za kidini. Haya yote yanategemea kupata ukweli kutoka kwa maneno ya Mungu.

Kimetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 562)

Kupata ufahamu wa kweli kuhusu maana halisi katika neno la Mungu sio jambo rahisi. Usifikiri kwa na namna hii: Naweza kutafsiri maana halisi ya maneno ya Mungu, na kila mtu anasema ni vizuri na kunipa hongera, hivyo inahesabika kama kuelewa neno la Mungu. Hilo si sawa na kuelewa neno la Mungu. Ikiwa umepata nuru kiasi kutoka ndani ya neno la Mungu na umefahamu umuhimu wa kweli wa neno la Mungu, ikiwa unaweza kueleza nia ya neno la Mungu na kile ambacho yatafanikisha hatimaye, punde haya yote yanaeleweka hilo linahesabika kama kuwa na kiwango fulani cha ufahamu wa neno la Mungu. Hivyo, kuelewa neno la Mungu si jambo rahisi kabisa. Kwa sababu tu unaweza kutoa maelezo ya madoido ya maandishi ya neno la Mungu haimaanishi kuwa unalielewa. Bila kujali vile unavyoweza kueleza maandishi ya neno la Mungu bado ni mawazo na jinsi ya kufikiria kwa mwanadamu—ni bure! Je, neno la Mungu linapasa kutafsiriwa vipi? Je, neno la Mungu linapasa kueleweka vipi? Msingi ni kuelewa neno Lake kutoka ndani ya neno Lake. Kila mara Mungu anenapo hakika Haneni kwa ujumla tu. Ndani ya kila sentensi kuna maudhui yenye maelezo ambayo yana uhakika wa kufichuliwa zaidi katika neno la Mungu, na yanaweza kuonyeshwa kwa njia tofauti. Mwanadamu hawezi kuelewa njia ambazo Mungu huonyesha ukweli. Neno la Mungu lina undani na haliwezi kuingiliwa na njia ya mwanadamu ya kufikiria. Watu wanaweza kugundua maana kamili ya kila kipengele cha ukweli mradi watie bidii, na maelezo yanayosalia yanajazwa kabisa Roho Mtakatifu anapotia ufahamu wako nuru wa hali dhabiti kwa kupitia. Sehemu moja ni kuelewa neno la Mungu kwa kupitia neno Lake, kutafuta maudhui mahsusi ya neno Lake. Sehemu nyingine ni kuelewa athari za neno la Mungu kwa kulipitia na kupokea nuru kutoka kwa Roho Mtakatifu. Kimsingi ni kwa njia hizi mbili ndipo ufahamu wa kweli wa Mungu unatimizwa. Ukieleza hili kwa uhalisi au kutoka kwa fikira au mawazo yako mwenyewe, basi ufahamu wako si wa kweli bila kujali jinsi unavyoweza kueleza kwa umbuji. Inawezekana kwamba wewe hata unaweza hata kutoka maana nje ya muktadha na kueleza neno la Mungu vibaya, na hilo ni la taabu hata zaidi. Hivyo, ukweli kimsingi unapatikana kwa kupokea nuru kutoka kwa Roho Mtakatifu kupitia kujua neno la Mungu. Kuelewa maana halisi ya neno Lake au kuweza kulieleza hakuhesabiki kama kupata ukweli. Kama ungehitaji tu kueleza maandishi ya neno Lake, basi kungekuwa na haja gani ya kupata nuru kutoka kwa Roho Mtakatifu? Katika hali hiyo ungehitaji kuwa na kiwango fulani cha masomo, na wale ambao hawajasoma wangekuwa kwenye hatari kabisa. Kazi ya Mungu si kitu ambacho kinaweza kufahamika na akili ya mwanadamu. Ufahamu wa kweli wa neno la Mungu unategemea hasa kupata nuru kutoka kwa Roho Mtakatifu; hii ni namna ya kuupata ukweli.

Kimetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 563)

Inapofikia kujua asili ya wanadamu, kitu cha muhimu zaidi ni kuijua kutoka kwa mtazamo wa maoni yao ya dunia, maoni ya maisha, na maadili. Wale wote walio wa ibilisi wote huishi kwa ajili yao wenyewe. Mitazamo yao ya maisha na kanunizinatoka kwa misemo ya Shetani, kama vile, “Kila mtu kivyake, na ibilisi achukue ya nyuma kabisa.” Maneno yaliyonenwa na hao ibilisi wafalme, wakuu, na wanafalsafa wa dunia yamekuwa maisha yao. Hasa, maneno mengi ya Konfyushasi, ambaye anatangazwa na watu wa Kichina kuwa “mtu mwenye hekima” yamekuwa maisha ya watuyamekuwa maisha ya watu. Pia kuna methali maarufu ya Ubudha na Utao, na misemo maarufu zaidi ya inayosemwa mara kwa mara ya watu mbalimbali mashuhuri; haya yote ni muhtasari wa falsafa ya Shetani na asili ya Shetani. Pia ni vielezo vizuri sana na maelezo ya asili ya Shetani. Sumu hizi ambazo zimetiliwa mioyoni mwa wanadamu zote hutoka kwa Shetani; hakuna hata chembe yao inayotoka kwa Mungu. Uongo na upuuzi kama huu pia ni upinzani wa moja kwa moja kwa neno la Mungu hasa. Ni wazi kabisa kuwa uhalisi wa vitu vyote vyema hutoka kwa Mungu, na vitu vyote hivyo hasi ambavyo huwatia sumu wanadamu hutoka kwa Shetani. Kwa hivyo, unaweza kumaizi asili ya mtu na yeye yu wa nani kutoka kwa maoni yake ya maisha na maadili. Shetani huwapotosha watu kwa kupitia masomo na ushawishi wa serikali za kitaifa na walio mashuhuri na wakuu. Upuuzi wao umekuwa uzima wa mwanadamu na asili. “Kila mtu kivyake na ibilisi achukue ya nyuma kabisa” ni msemo wa kishetani unaojulikana sana ambao umeingizwa ndani ya kila mtu na umekuwa maisha ya watu. Kuna maneno mengine ya falsafa ya kuishi ambayo pia ni kama haya. Shetani hutumia utamaduni mzuri wa kila taifa kuwaelimisha watu, akisababisha wanadamu kuanguka ndani na kumezwa na lindi kuu lisilo na mipaka la uharibifu, na mwishowe watu wanaangamizwa na Mungu kwa sababu wanamtumikia Shetani na kumpinga Mungu. Hebu fikiri kumwuliza mtu ambaye amekuwa mtendaji katika jamii kwa miongo swali lifuatalo: ‘Kuona kwamba umeishi duniani kwa muda mrefu sana na umetimiza mengi sana, je, ni misemo ipi mikuu maarufu unayofuata katika maisha yako?’ ‘Ule ulio muhimu zaidi ni “Wenye madaraka hawawapigi wanaowapa zawadi, na wale wasiojipendekeza hamna wanachofanikisha.’” Je, maneno haya hayaiwakilishi asili ya mtu huyo? Kutumia kila mbinu ili kupata cheo imekuwa asili yake na, kuwa na madaraka rasmi ndiko kunakompa uzima. Bado kuna sumu nyingi za kishetani maishani mwa watu, katika mienendo yao na shughuli zao na wengine; hawana ukweli wowote hata kidogo. Kwa mfano, falsafa zao za kuishi, njia zao za kufanya vitu, na kanuni zao zote zimejazwa sumu za joka kuu jekundu, na zote zinatoka kwa Shetani. Hivyo, vitu vyote vinavyopita katika mifupa na damu ya watu ni vitu vyote vya Shetani. Wale maafisa wote, wale wanaoshikilia mamlaka, na wale waliofaulu wana njia zao na siri za kufaulu. Je, si siri kama hizo ni uwakilishi mzuri zaidi wa asili yao? Wameyafanya mambo makubwa sana duniani, na hakuna anayeweza kung’amua njama ambazo ziko katika mambo haya. Hili linaonyesha jinsi asili yao ilivyo yenye kudhuru kwa siri na yenye uovu. Wanadamu wamepotoshwa kwa kina zaidi na Shetani. Sumu ya Shetani inabubujika kwa damu ya kila mtu, na inaweza kuonekana kwamba asili ya mwanadamu imepotoka, ni yenye uovu, na ya kupinga maendeleo, ikijawa na kuzamishwa katika falsafa za Shetani—kwa jumla ni asili inayomsaliti Mungu. Hii ndiyo maana watu humkataa Mungu na humpinga Mungu. Asili ya mwanadamu inaweza kujulikana na kila mtu ikichanguliwa hivi.

Kimetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 564)

Umuhimu wa kujitafakari na kujijua ni huu: Kadiri unavyozidi kuhisi kuwa katika sehemu fulani umefanya vizuri au umefanya jambo linalofaa, na kadiri unavyofikiri kuwa unaweza kuyaridhisha mapenzi ya Mungu au kuweza kujivunia katika sehemu fulani, basi ndivyo inavyofaa zaidi kwako kujijua katika sehemu hizo na inavyofaa zaidi kwako kuzichunguza zaidi ili kuona ni uchafu gani uko ndani yako, pamoja na mambo gani ndani yako hayawezi kuyaridhisha mapenzi ya Mungu. Hebu tumchukue Paulo kama mfano. Paulo alikuwa mwenye maarifa mno, na alivumilia mengi katika kazi yake ya kuhubiri. Alipendwa hasa sana na Wengu. Kama matokeo, baada ya kumaliza wingi wa kazi, alidhani kungekuwa na taji lililowekwa kando kwa ajili yake. Hili lilimfanya atembee zaidi na zaidi kwenye njia isiyo sahihi, hadi mwishowe akaadhibiwa na Mungu. Ikiwa, wakati huo, angetafakari juu yake mwenyewe na kujichambua, basi asingefikiria hivyo. Kwa maneno mengine, Paulo hakuwa amelenga kutafuta ukweli katika maneno ya Bwana Yesu; alikuwa tu ameamini mawazo na fikira zake mwenyewe. Alikuwa amedhani kwamba almradi afanye mambo machache mazuri na kuonyesha tabia nzuri, angesifiwa na kutuzwa kupewa tuzo na Mungu. Mwishowe, mawazo na fikira zake zilipofusha roho yake na kufunika hali yake ya kweli. Hata hivyo, watu hawakujua hili, na bila Mungu kuliweka wazi, waliendelea kumweka Paulo kama kiwango cha kufikia, mfano wa kuishi kulingana naye, na wakamwona kama ambaye walitamani kuwa kama na kama kitu cha kufuatilia kwao na kama mtu wa kuigwa nao. Hadithi hii kumhusu Paulo inatumika kama onyo kwa kila mtu amwaminiye Mungu, ambalo ni kwamba wakati wowote tunapohisi kuwa tumefanya vizuri zaidi, au kuamini kwamba tuna vipawa zaidi katika mambo fulani, au kufikiria kwamba hatuhitaji kubadilika au kushughulikiwa katika jambo fulani, tunapaswa kujitahidi kutafakari na kujijua wenyewe zaidi katika suala hilo; jambo hili ni muhimu. Hii ni kwa sababu bila shaka hujafichua, kutilia maanani au kuchanganua vipengele kujihusu ambavyo unaamini kuwa mzuri, ili kuona kama kweli vina chochote kinachompinga Mungu au la. Kwa mfano, kuna watu wanaojiamini kuwa wema mno. Wao hawawachukii au kuwadhuru wengine kamwe na wao humsaidia ndugu yeyote ambaye familia yake inahitaji msaada ili tatizo lake lisije likakosa kutatuliwa; wana ukarimu mkubwa na wao hufanya kila wawezalo ili kumsaidia kila mtu ambaye wanaweza kumsaidia. Je, matokeo ya msaada kama huu ni yapi? Wao hutelekeza mambo muhimu katika maisha yao wenyewe lakini wao huridhika sana na wao huridhishwa mno na yote ambayo wameyafanya. Zaidi ya hayo, wao hujivunia sana jambo hilo, wakiamini yote ambayo wamefanya hakika yanatosha kuridhisha mapenzi ya Mungu na kwamba wao ni waumini wa kweli wa Mungu. Wanaona wema wao wa asili kama kitu cha kutumia kwa faida yao, na mara wanapouchukulia kwa njia hiyo, wanakuja kuona kama huo bila shaka ni ukweli. Ukweli ni kwamba, yote wanayoyafanya ni wema wa wanadamu. Hawajatafuta ukweli hata kidogo na matendo yao yote ni bure, kwa maana wao huyafanya mbele ya wanadamu wala si mbele ya Mungu na hawatendi kulingana na matakwa ya Mungu na ukweli. Hakuna wanachofanya ambacho ni utendaji wa ukweli na hakuna wanachofanya ambacho ni utendaji wa maneno ya Mungu, wala hawafuati mapenzi Yake; badala yake, wao hutumia wema wa kibinadamu na tabia nzuri kuwasaidia wengine. Kwa ufupi, hawatafuti mapenzi ya Mungu katika kile wanachofanya na hawatendi kulingana na matakwa Yake. Kwa hivyo, kutoka kwa mtazamo wa Mungu, tabia nzuri ya mwanadamu hushutumiwa na haistahili kukumbukwa na Yeye.

Kimetoholewa kutoka katika “Ni kwa Kutambua Maoni Yako Yaliyopotoka Tu Ndipo Unapoweza Kujijua Mwenyewe” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 565)

La muhimu katika kufikia badiliko katika tabia ni kujua asili ya mtu mwenyewe, na hili ni lazima lifanyike kulingana na ufunuo kutoka kwa Mungu. Ni katika neno la Mungu tu ambapo mtu anaweza kujua asili yake mbaya, afahamu katika asili yake mwenyewe sumu mbalimbali za Shetani, atambue kuwa yeye ni mjinga na mpumbavu, na atambue dalili dhaifu na hasi katika asili yake. Baada ya haya kujulikana kikamilifu, na unaweza kwa hakika kujichukia na kunyima mwili, daima kutekeleza neno la Mungu, na kuwa na mapenzi ya kujiwasilisha kikamilifu kwa Roho Mtakatifu na kwa neno la Mungu, basi utakuwa umeianza njia ya Petro. Bila neema ya Mungu, na bila nuru na mwongozo kutoka kwa Roho Mtakatifu, ingekuwa vigumu kuitembea njia hii, kwa sababu watu hawamiliki ukweli na hawawezi kujisaliti wenyewe. Kuitembea njia ya Petro ya ukamilisho inaegemea kuwa na azimio, kuwa na imani, na kumtegemea Mungu. Mbali na haya, mtu lazima ajiweke chini ya kazi ya Roho Mtakatifu; katika mambo yote, mtu hawezi kutenda bila maneno ya Mungu. Hivi ndivyo vipengele muhimu, Kupata kujitambua mwenyewe kupitia uzoefu ni vigumu sana bila kazi ya Roho mtakatifu, ni vigumu sana kuingia ndani. Kuitembea njia ya Petro mtu lazima azingatie juu ya kujijua mwenyewe na kubadili tabia yake. Njia ya Paulo haikuwa ya kutafuta maisha au kusisitiza ufahamu wa kibinafsi; yeye hasa alizingatia kufanya kazi na ushawishi wake na ukasi wake. Motisha yake ilikuwa kupata baraka za Mungu kwa ubadilishano na kazi na mateso yake, na kupokea tuzo kutoka kwa Mungu. Hii motisha yake ilikuwa mbovu. Paulo hakuzingatia uzima, wala hakuweka umuhimu kutimiza badiliko la kitabia; alilenga tu juu ya tuzo. Kwa sababu alikuwa na malengo yasiyofaa, njia aliyoitembelea bila shaka ilikuwambaya. Hili ililetwa na kiburi na hali yake ya majivuno. Kwa dhahiri, Paulo hakumiliki ukweli wowote, wala hakuwa na dhamiri au sababu yeyote. Katika kuwaokoa na kuwabadilisha watu, Mungu kimsingi hubadilisha watu kwa kubadilisha tabia zao. Kusudi la maneno Yake ni kufikia katika watu matokeo ya mabadiliko katika tabia uwezo wa kumjua Mungu, kujiweka chini Yake, na kumwabudu Yeye kwa njia ya kawaida. Hili ndilo kusudi la maneno ya Mungu na la kazi Yake. Njia aliyoitumia Paulo kutafuta ilikuwa ya ukiukaji wa moja kwa moja na katika mgongano namapenzi ya Mungu; ilienda kinyume kabisa. Hata hivyonjia ya Petro ya kutafuta, ilifanana kabisa na mapenzi ya Mungu, ambayo hasa ni matokeo ambayo Mungu hutamani kutimiza kwa wanadamu. Kwa hiyo, njia ya Petro imebarikiwa na hupata sifa ya Mungu. Kwa sababu njia ya Paulo ni ukiukaji wa mapenzi ya Mungu, Mungu kwa hiyo anaichukia na huilaani. Kuitembelea njia ya Petro mtu lazima aijue mapenzi ya Mungu. Kama mtu kwa kweli anaweza kuielewa kikamilifu mapenzi Yake kupitia maneno Yake—ambayo inamaanisha kukielewa kile Mungu anachotaka kukifanya kwa mwanadamu na hatimaye yale matokeo Yeye hutamani kutimizahapo tu ambapo mtu anaweza kuwa na ufahamu barabara wa ni njia ipi ya kufuata. Kama huielewi kikamilifu njia ya Petro, na una tu tamaa ya kuifuata, basi hutaweza kuianza. Kwa maneno mengine, unaweza kuwa unayajua mafundisho mengi, lakini hatimaye hutaweza kuingia katika ukweli. Ingawa unaweza kufanya kuingia kwa juujuu, hutaweza kutimiza matokeo yoyote ya kweli.

Kimetoholewa kutoka katika “Kujijua Mwenyewe Hasa Ni Kujua Asili ya Binadamu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 566)

Siku hizi, watu wengi wana ufahamu wa juu juu sana kujihusu. Hawajapata kujua waziwazi vitu ambavyo ni sehemu ya maumbile yao hata kidogo. Wana ufahamu mdogo tu kuhusu hali zao potovu, kuhusu vitu ambavyo wana uwezekano wa kufanya, au dosari zao chache, na hili huwafanya waamini kuwa wanajijua. Aidha, ikiwa wanafuata sheria chache, wanahakikisha kwamba hawafanyi makosa katika maeneo fulani, na wanajiepusha na kutenda dhambi fulani, basi wanajiona kwamba wana uhalisi katika imani yao katika Mungu na wanadhani kwamba wataokolewa. Haya ni mawazo ya kibinadamu kabisa. Ukifuata mambo hayo, je, utaweza kuwa mwenye uwezo wa kujizuia kutenda dhambi zozote kweli? Je, utakuwa umefikia mabadiliko ya kweli katika tabia? Je, utakuwa kweli unaishi kwa kudhihirisha mfano wa binadamu? Je, unaweza kumridhisha Mungu kwa kweli kwa njia hiyo? Huwezi kabisa, hili ni bila shaka. Imani katika Mungu hufanikiwa tu wakati mtu ana viwango vya juu na amefikia ukweli na mabadiliko kiasi katika tabia yake ya maisha. Kwa hivyo kama ujuzi wa watu juu yao wenyewe ni wa juujuu sana, watapata kuwa haiwezekani kutatua matatizo, na tabia zao za maisha hazitabadilika kabisa. Ni muhimu kujijua mwenyewe kwa kiwango cha kina kabisa, ambayo inamaanisha kuijua asili yako mwenyewe: ni vipengele vipi ambavyo vimejumuishwa katika asili hiyo, jinsi vitu hivi vilivyoanza, na kule vilipotoka. Aidha, unaweza kuchukia mambo haya kweli? Je, umeona nafsi yako mwenyewe mbaya na asili yako mbovu? Ikiwa kwa hakika unaweza kuuona ukweli kujihusu mwenyewe, basi utaanza kujichukia mwenyewe kabisa. Wakati unapojichukia mwenyewe kabisa na kisha unatenda neno la Mungu, utakuwa na uwezo wa kunyima mwili na kuwa na nguvu ya kutekeleza ukweli bila shida. Kwa nini watu wengi hufuata tamaa zao za kimwili? Kwa sababu wanajiona kuwa wazuri kabisa, wakihisi kuwa vitendo vyao ni viadilifu na vya haki, kwamba hawana makosa, na hata kwamba wako sahihi kabisa, kwa hiyo wao wana uwezo wa kutenda kwa dhana kuwa haki iko upande wao. Wakati mtu anapotambua asili yake ya kweli ilivyo—jinsi ilivyo mbaya, jinsi inavyostahili kudharauliwa, na jinsi ilivyo ya kusikitisha—basi yeye si mwenye majivuno sana, hajigambi ovyo ovyo sana, hajifurahii kama hapo awali. Mtu kama huyo huhisi, “Lazima niwe mwenye ari na mpole, na nitende baadhi ya maneno ya Mungu. Kama sivyo, basi siwezi kufikia kiwango cha kuwa mwanadamu, na nitaona aibu kuishi mbele ya Mungu.” Kwa hakika mtu hujiona kuwa hafifu, kama kweli asiye na maana. Wakati huu, inakuwa rahisi kwake kutekeleza ukweli, naye ataonekana kwa kiwango fulani kuwa kama mwanadamu anavyopaswa kuwa. Ni pale tu ambapo watu kwa hakika hujichukia kabisa ndipo wanaweza kunyima mwili. Kama hawajichukii, hawataweza kunyima mwili. Mtu kujichukia kweli kunajumuisha mambo machache: Kwanza, kujua asili yake mwenyewe; na pili, kujiona kama yeye ni mwenye shida na wa kudharaulika, kujiona kuwa mdogo kupindukia na asiye na maana, na kuona nafsi yake kuwa yenye kudharaulika na chafu. Mtu anapoona kikamilifu kile alicho kwa hakika, na matokeo haya yakafikiwa, basi yeye kweli hupata ufahamu juu yake mwenyewe, na inaweza kusemwa kwamba amekuja kujijua mwenyewe kikamilifu. Ni hapo tu ndipo anaweza kwa hakika kujichukia mwenyewe, kufikia hata kujilaani mwenyewe, na ahisi kwa kweli kwamba amepotoshwa sana na Shetani kiasi kwamba hafanani tena na mwanadamu. Kisha, siku moja, wakati tishio la kifo linapoonekana, mtu kama huyu atafikiri, “Hii ni adhabu ya haki ya Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye haki; Kwa hakika mimi lazima nife!” Wakati huu, yeye hatalalamika, wala kumlaumu Mungu, akihisi tu kwamba yeye ni wa kudharaulika, mchafu sana na mpotovu, kwamba anapaswa kuangamizwa na Mungu na roho kama yake haifai kuishi duniani. Wakati huu, mtu huyu hatampinga Mungu, sembuse kumsaliti Mungu. Iwapo mtu hajijui mwenyewe, na bado hujiona kuwa mzuri sana, basi wakati kifo kinapokuja kubisha, mtu huyu atafikiria, “Nimetenda vyema sana katika imani yangu. Jinsi nimetafuta kwa nguvu! Nimejitolea mengi sana, nimeumia sana, ilhali hatimaye, Mungu sasa ananiuliza nife. Sijui haki ya Mungu iko wapi. Kwa nini Ananitaka nife? Ikiwa hata mtu kama mimi anafaa kufa, basi ni nani atakayeokolewa? Je! Si jamii ya wanadamu itafikia mwisho?” Kwanza kabisa, mtu huyu ana dhana juu ya Mungu. Pili, mtu huyu analalamika, na hatii hata kidogo. Hii ni kama tu Paulo: Wakati alipokaribia kufa, hakujijua mwenyewe, Na kufikia wakati adhabu ya Mungu ilipokaribia, hakukuwa na muda wa kutubu.

Kimetoholewa kutoka katika “Kujijua Mwenyewe Hasa Ni Kujua Asili ya Binadamu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 567)

Kwa ufupi, kuichukua njia ya Petro katika imani ya mtu kunamaanisha kuitembea njia ya kufuatilia ukweli, ambayo pia ni njia ya kupata kujijua na kubadilisha tabia yako kwa kweli. Ni kwa kuitembea njia ya Petro tu ndipo mtu atakuwa katika njia ya kukamilishwa na Mungu. Mtu lazima aelewe jinsi hasa ya kuitembea njia ya Petro, na vilevile jinsi ya kuiweka katika vitendo. Kwanza, mtu lazima aweke kando madhumuni yake mwenyewe, shughuli zisizofaa, na hata familia na vitu vyote vya mwili wake mwenyewe. Yeye lazima ajitolee kwa moyo wote; yaani, lazima ajitolee kabisa kwa neno la Mungu, alenge kula na kunywa maneno ya Mungu, azingatie kutafuta ukweli na kutafuta madhumuni ya Mungu katika maneno Yake, na ajaribu kufahamu mapenzi ya Mungu katika kila kitu. Hii ndiyo mbinu ya msingi na muhimu zaidi ya utendaji. Hilo ndilo alilofanya Petro baada ya kumwona Yesu, na ni kwa kutenda kwa njia hii tu ndio mtu anaweza kufanikisha matokeo bora zaidi. Kujitolea kwa moyo wote kwa maneno ya Mungu kimsingi kunajumuisha kutafuta ukweli, kutafuta nia za Mungu ndani ya maneno Yake, kuzingatia kuyaelewa mapenzi ya Mungu, na kuelewa na kupata ukweli zaidi kutoka katika maneno ya Mungu. Wakati wa kusoma maneno Yake, Petro hakuwa anazingatia kuelewa mafundisho ya dini, sembuse kuzingatia kwa kiasi kidogo kupata maarifa ya teolojia; badala yake, alitilia maanani kuelewa ukweli na kufahamu mapenzi ya Mungu, na vile vile kutimiza ufahamu wa tabia yake na uzuri wake. Petro pia alijaribu kuelewa hali potovu mbalimbali za mwanadamu kutoka katika maneno ya Mungu, na vile vile asili potovu ya mwanadamu na dosari yake halisi hivyo kufikia vipengele vyote vya matakwa ya Mungu kwa mwanadamu ili kumridhisha Yeye. petro alikuwa na vitendo vingi sahihi vilivyofuata maneno ya Mungu; hili lililingana zaidi na mapenzi ya Mungu, na ni njia bora zaidi ambayo mtu angeshirikiana huku akipitia kazi ya Mungu. Wakati ambapo alipitia mamia ya majaribio kutoka kwa Mungu, Petro alijichunguza kabisa dhidi ya kila neno la hukumu ya Mungu kwa mwanadamu, kila neno la ufunuo wa Mungu kwa mwanadamu, na kila neno la madai Yake kwa mwanadamu, na akajitahidi kuelewa maana ya maneno hayo. Alijaribu kwa bidii kutafakari na kukariri kila neno ambalo Yesu alimwambia, na alitimiza matokeo mazuri sana. Kupitia namna hii ya utendaji, aliweza kutimiza kujifahamu kutoka kwa maneno ya Mungu, na hakuja tu kuelewa hali potovu mbalimbali za mwanadamu, lakini pia alikuja kuelewa kiini, asili, na dosari mbalimbali za mwanadamu. Hii ndiyo maana ya kujifahamu kwa kweli. Kutoka kwa maneno ya Mungu, Petro hakutimiza tu kujifahamu kwa kweli, lakini kutokana na mambo yaliyoonyeshwa katika maneno ya Mungu—tabia ya Mungu yenye haki, kile Anacho na alicho, mapenzi ya Mungu kwa kazi Yake, mahitaji Yake kwa wanadamu—kutoka kwa maneno haya alikuja kumjua Mungu kabisa. Alikuja kujua tabia ya Mungu, na asili yake; alikuja kujua na kuelewa kile Mungu anacho na Alicho, na vilevile uzuri wa Mungu na mahitaji ya Mungu kwa mwanadamu. Ingawa Mungu hakuzungumza wakati huo sana kama Anavyofanya leo, matokeo katika vipengele hivi, hata havyo yalipatikanana Petro. Hili lilikuwa jambo adimu na la thamani. Petro alipitia mamia ya majaribio, lakini hakuteseka bure. Hakuja kujielewa tu kutokana na maneno na kazi ya Mungu, lakini pia alikuja kumjua Mungu. Aidha, alizingatia hasa matakwa ya Mungu kwa wanadamu ndani ya maneno Yake. Bila kujali ni katika hali gani mwanadamu anapaswa kumridhisha Mungu ili kukubaliana na mapenzi ya Mungu, Petro aliweza kufanya juhudi kubwa katika vipengele hivi na kupata uwazi kamili; hili lilikuwa la manufaa kubwa sana kwa kuingia kwake mwenyewe. Haijalishi kile ambacho Mungu alizungumzia, maadamu maneno hayo yangeweza kuwa maisha yake na yalikuwa ya ukweli, Petro aliweza kuyaweka ndani ya moyo wake kuyatafakari na kuyathamini mara kwa mara. Baada ya kuyasikia maneno ya Yesu, aliweza kuathiriwa nayo, ambalo linaonyesha kuwa alikuwa akizingatia hasa maneno ya Mungu, na alitimiza matokeo mwishowe kwa kweli. Yaani, aliweza kuyatia maneno ya Mungu katika vitendo kwa uhuru, kutenda kwa usahihi ukweli na kukubaliana na mapenzi ya Mungu, kutenda kikamilifu kwa mujibu wa nia ya Mungu, na kuacha maoni na mawazo yake mwenyewe. Kwa njia hii, Petro aliingia katika ukweli wa maneno ya Mungu. Huduma ya Petro ililingana na mapenzi ya Mungu hasa kwa sababu alikuwa amefanya hili.

Ikiwa mtu anaweza kumridhisha Mungu huku akitimiza wajibu wake, ni mwenye maadili katika maneno ya matendo yake, na anaweza kuingia katika uhalisi a vipengele vya ukweli, basi huyu ni mtu ambaye anakamilishwa na Mungu. Inaweza kusemekana kuwa kazi na maneno ya Mungu yamekuwa ya kufaa kabisa kwa watu kama hao, kwamba maneno ya Mungu yamekuwa maisha yao, wamepata ukweli, na wanaweza kuishi kulingana na maneno ya Mungu. Baada ya hili, asili ya mwili wao—yaani, msingi maalum wa uwepo wao wa kwanza—itatikisika na kuanguka. Baada ya watu kuwa na maneno ya Mungu kama maisha yao, watakuwa watu wapya. Maneno ya Mungu yakiwa maisha yao, maono ya kazi ya Mungu, matakwa Yake kwa wanadamu, ufunuo Wake kwa wanadamu, na viwango vya maisha ya kweli ambayo Mungu anawahitaji watimize vikiwa maisha yao, wakiishi kulingana na maneno haya na ukweli huu, basi wanakamilishwa na Mungu. Watu kama hawa wanazaliwa tena, na wamekuwa watu wapya kupitia maneno ya Mungu. Hii ni njia ambayo Petro aliitumia kuufuatilia ukweli; Ilikuwa njia ya kukamilishwa, kukamilishwa na maneno ya Mungu, na kupata uzima kutoka kwa maneno ya Mungu. Ukweli ulioonyeshwa na Mungu ulikuwa maisha yake, na wakati huo tu ndipo alikuwa mtu aliyepata ukweli.

Kimetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kuitembea Njia ya Petro” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 568)

Mpaka watu wawe wamepitia kazi ya Mungu na kupata ukweli, ni asili ya Shetani inayotwaa madaraka na kuwatawala kwa ndani. Ni nini, hasa, kilicho ndani ya asili hiyo? Kwa mfano, kwa nini wewe ni mchoyo? Kwa nini wewe hulinda nafasi yako mwenyewe? Kwa nini una hisia kali sana namna hiyo? Kwa nini unafurahia hivyo vitu visivyo vya haki? Kwa nini unapenda maovu hayo? Msingi wa kupenda kwako vitu hivi ni upi? Mambo haya hutoka wapi? Kwa nini unafurahia sana kuyakubali? Kufikia sasa, nyote mmekuja kuelewa kwamba sababu kuu ya mambo haya yote ni kwamba sumu ya Shetani iko ndani yenu. Kuhusu sumu ya Shetani ni nini, inaweza kuelezwa kwa ukamilifu kwa maneno. Kwa mfano, ukiwauliza baadhi ya watenda maovu kwa nini walitenda jinsi walivyotenda, watajibu, “Kwa sababu kila mwamba ngoma huvutia upande wake.” Msemo huu mmoja unaonyesha asili ya shida. Mantiki ya Shetani imekuwa maisha ya watu. Wanaweza kutenda mambo kwa ajili ya madhumuni fulani au mengine, lakini wanajifanyia tu. Kila mtu hudhani kwamba kwa kuwa ni kila mwamba ngoma huvutia upande wake, watu wanafaa kuishi kwa sababu yake mwenyewe tu, na kufanya kila awezalo kupata wadhifa mzuri kwa ajili ya chakula na mavayi mazuri. “Kila mwamba ngoma huvutia upande wake”—haya ndiyo maisha na falsafa ya mwanadamu, na pia inawakilisha asili ya binadamu. Maneno haya ya Shetani ni sumu ya Shetani hasa, na watu wanapopoiweka moyoni, inakuwa asili yao. Asili ya Shetani hufunuliwa kupitia maneno haya; yanamwakilisha yeye kabisa. Sumu hii inakuwa maisha ya watu pamoja na msingi wa kuwepo kwao; na wanadamu waliopotoshwa wametawaliwa kwa uthabiti na sumu hii kwa maelfu ya miaka. Kwa kweli, wito wa watu wengi unaweza kuwakilisha na kuakisi asili yao. Haijalishi jinsi watu hujaribu kuificha, katika kila kitu wafanyacho na kila kitu wasemacho, hawawezi kuificha asili yao. Kuna wengine ambao huwa hawasemi ukweli kamwe na wanajua sana kujifanya, lakini punde tu wengine wanapoingiliana nao kwa muda, asili yao ya udanganyifu na wao kutokuwa waaminifu kabisa kutagunduliwa. Muda utafichua yote. Baada ya kuwajua kwa muda, asili yao itagunduliwa. Mwishowe, wengine hufikia hitimisho hili: Mtu huyo kamwe hasemi neno lolote la ukweli na ni mdanganyifu. Kauli hii ni ukweli wa asili ya mtu wa aina hiyo; ni ushahidi na kielezo cha asili yake; falsafa yake ya maisha ni kutomwambia yeyote ukweli, na pia kutomwamini mtu yeyote. Asili ya kishetani ya mwanadamu ina kiwango kikubwa cha falsafa. Wakati mwingine wewe mwenyewe huna hata habari ya hilo na hulielewi, ilhali kila muda wa maisha yako unategemea hilo. Isitoshe, unafikiri kuwa falsafa hii ni sahihi sana, yenye mantiki na isiyo na kosa. Falsafa ya Shetani imekuwa ukweli wa watu, na wanaishi kulingana na falsafa ya Shetani kabisa, bila kumpinga hata kidogo. Kwa hivyo, kila mara wanaonyesha asili yao ya kishetani. mwanadamu daima hufichua asili ya Shetani, na katika vipengele vyote, wanaishi daima kulingana na falsafa ya ya kishetani. Asili ya Shetani ni maisha ya mwanadamu.

Kimetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kuitembea Njia ya Petro” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 569)

Watu wana ufahamu wa juujuu sana kuhusu asili yao wenyewe, na kuna tofauti kubwa kati ya hili na maneno ya Mungu ya hukumu na ufunuo. Hili si kosa katika lile ambalo Mungu hulifunua, bali badala yake ni ukosefu wa wanadamu wa ufahamu wa kina wa asili yao. Watu hawana ufahamu wa kimsingi au wa halisi wa wao wenyewe; badala yake, wao wanalenga na kutenga nguvu zao kwa matendo na maonyesho ya nje. Hata kama mtu fulani angelisema jambo mara chache kuhusu kujifahamu, halingekuwa la kina sana. Hakuna mtu aliyewahi kufikiria kwamba yeye ni aina hii ya mtu au ana asili ya aina hii kutokana na kulitenda jambo kama hili au kulifunua jambo. Mungu ameifunua asili na kiini cha mwanadamu, lakini wanadamu wanafahamu kwamba njia yao ya kuyatenda mambo na njia yao ya kusema ni yenye mawaa na yenye kasoro; kwa hiyo, ni kazi yenye kutumia juhudi nyingi kwa watu kutia ukweli katika vitendo. Watu wanafikiria kwamba makosa yao ni udhihirisho wa muda tu ambao unafunuliwa bila kujali, badala ya kuwa ufunuo wa asili yao. Watu ambao hujiona kwa namna hii hawauweki ukweli katika vitendo, kwa sababu hawawezi kukubali ukweli kama ukweli na hawatamani ukweli; kwa hiyo, wakati wanatia ukweli wao katika vitendo wanaifuata tu sheria kwa uzembe. Watu hawaoni asili yao wenyewe kama iliyo potovu sana, na wanaamini kwamba wao si wabaya sana kiasi kwamba wanapaswa kuangamizwa au kuadhibiwa. Wao hufikiri kuwa si jambo kubwa kudanganya mara kwa mara, na hujiona kuwa bora zaidi kuliko jinsi walivyokuwa zamani; hata hivyo, kwa kweli wako mbali sana na kiwango kinachohitajika, kwa sababu watu wana matendo fulani tu ambayo kwa nje hayakiuki ukweli, wakati kwa kweli hawatii ukweli katika vitendo.

Mabadiliko katika tabia au mwenendo wa mtu hayamaanishi mabadiliko katika asili yake. Hii ni kwa sababu mwenendo wa mtu kimsingi hauwezi kubadilisha sura yake ya asili wala hauwezi kubadilisha asili yake. Utendaji wa mtu unaweza kuwa wa kina na uwe zaidi ya kufuata sheria baada tu ya mtu kujua asili yake mwenyewe. Utendaji wa ukweli wa sasa wa mwanadamu bado haujafikia kiwango kinachotakiwa na hauwezi kufikia kikamilifu yote ambayo ukweli unahitaji. Watu hutenda sehemu fulani tu ya ukweli na wanapokuwa katika hali na mazingira fulani pekee; hawawezi kutia ukweli katika vitendo katika mazingira na hali zote. Wakati maalum ambapo mtu ana furaha na hali yake ni nzuri, au anapofanya ushirika pamoja na kikundi na ahisi kwamba amekombolewa zaidi kuliko ilivyo kawaida, anaweza kufanya kwa muda, mambo kiasi yanayokubaliana na ukweli; lakini anapokuwa katika kikundi cha watu hasi na wale ambao hawafuatilii ukweli, utendaji wake unakuwa duni zaidi na matendo yake hayafai kwa kiasi fulani. Hii ni kwa sababu watu hutenda ukweli bila mtazamo wa uvumilivu, lakini badala yake wao huutia katika vitendo wakiongozwa na mvuto wa mhemko au hali ya muda mfupi. Pia, ni kwa sababu hujaelewa hali yako wala hujaelewa asili yako, kwa hivyo, wakati mwingine, bado unaweza kufanya mambo ambayo huwezi kufikiria kwamba unaweza kuyafanya. Unajua tu baadhi ya hali zako, lakini kwa kuwa hujaelewa asili yako, huwezi kudhibiti yale unayoweza kufanya katika siku zijazo—yaani, huna hakika kabisa kwamba utasimama imara. Kuna wakati mwingine ambapo upo katika hali fulani na unaweza kutia ukweli katika vitendo, na unaonekana kudhihirisha mabadiliko fulani, lakini katika mazingira tofauti, huwezi kuutia katika vitendo. Huwezi kudhibiti jambo hili. Wakati mwingine unaweza kutenda ukweli na wakati mwingine huwezi. Wakati mmoja unaelewa, na wakati mwingine unachanganyikiwa. Hivi sasa, hufanyi jambo lolote baya, lakini labda utalifanya baada ya muda kidogo. Hii inathibitisha kuwa mambo yaliyopotoka bado yamo ndani yako, na usipoweza kujifahamu kwa kweli, hayatatatulika kwa urahisi. Usipofikia ufahamu kamili kuhusu tabia yako mwenyewe potovu na mwishowe uwe na uwezo wa kufanya mambo yanayompinga Mungu, basi umo hatarini. Iwapo unaweza kupata utambuzi wa kina kuhusu asili yako na uichukie, basi utakuwa na uwezo wa kujidhibiti, kujikana na kutia ukweli katika vitendo.

Kimetoholewa kutoka katika “Kuifahamu Asili ya Mtu na Kuutia Ukweli Katika Vitendo” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 570)

Kusudi la ushurika wazi kuhusu ukweli ni ili kuwawezesha watu kutenda ukweli na kubadilisha tabia zao; sio tu kwa ajili ya kuwafanya wauelewe. Kama unaelewa ukweli lakini hauuweki katika vitendo, basi kufanya ushirika kuuhusu na ufahamu wa ukweli hautakuwa na maana yoyote. Iwapo unaelewa ukweli lakini kamwe hauuweki katika matendo, utapoteza nafasi ya kuupata ukweli, na pia nafasi yoyote ya kuokolewa. Iwapo umeuweka ukweli unaoelewa katika vitendo, basi utapata ukweli wa mwingi wa kina zaidi; utafikia wokovu wa Mungu, vile vile nuru, mwangaza na uongozi wa Roho Mtakatifu. Wengi tu huweza kulalamika tu kuwa Roho Mtakatifu kamwe hawapi nuru, bila kutambua kuwa kimsingi hawauweki ukweli katika matendo. Kwa hivyo, hali zao hazitawahi kupata ukawaida, wala hawatawahi kuelewa mapenzi ya Mungu daima.

Baadhi ya watu husema kuwa kutenda ukweli hakuwezi kutatua tabia zao potovu. Wengine huamini kuwa ukweli hauwezi kutatua kikamilifu tabia potovu za mtu. Ukweli ni kwamba shida zote za watu zaweza kutatuliwa; cha muhimu ni kama wao wanaweza kutenda kulingana na ukweli au hapana. Matatizo yanayowakumba sasa sio saratani ama magonjwa yasiotibika. Iwapo mnaweza kuweka ukweli katika matendo, basi matatizo hayo yote yanaweza kubadilishwa, ikitegemea kama unaweza kutenda kwa mujibu wa ukweli. Kama unatembea katika njia ya kufuatilia ukweli, basi bila shaka utafanikiwa; hata hivyo, kama unatembea katika njia mbaya, basi wewe umemalizwa. Kwa mfano, watu wengine hufanya kazi zao bila kufikiria kuhusu jinsi ya kufanya vitu kwa njia ya kuifaidi kazi ya nyumba ya Mungu ama njia zao za kufanya mambo zinapatana na mapenzi ya Mungu; kama tokeo, wanafanya mambo mengi ambayo Anachukia. Kama wangetenda sambamba na ukweli katika kila jambo wanalolitenda, je, hawangekuwa basi watu ambao wanaupendeza moyo wa Mungu? Watu wengine wanajua ukweli lakini hawauweki katika matendo, wakiamini kuwa ukweli ni hiki kitu kimoja tu na sio zaidi. Wanaamini kuwa hakiwezi kusafisha mapenzi yao wenyewe na kutatua upotovu wao. Je, si mtu wa aina hii ni mpumbavu? Je, si watu kama hawa wapumbavu? Je hawajioni wenyewe kuwa werevu? Watu wakitenda kulingana na ukweli, tabia zao potovu zitabadilishwa; hata hivyo, ikiwa wanategemeza imani na huduma yao kwa Mungu kulingana na hulka zao asili, basi hakuna kati yao atakayefaulu kubadilisha tabia zake. Watu wengine wanajipata wamebanwa katika shughuli zao wenyewe siku nzima huku wakikosa kuchunguza ama kutenda ukweli unaopatikana tayari. Njia hii ya kutenda ni ya kipumbavu sana; watu wa aina hii ni watesekaji kiasili, kwa kuwa wanazo baraka lakini hawazifurahii! Njia ya kwenda mbele ipo; kinachofaa kufanywa tu ni wewe uitende. Kama umeamua kuuweka ukweli katika matendo, basi udhaifu wako na dosari mbaya vinaweza kubadilishwa. Hata hivyo, lazima kila wakati uchukue tahadhari na mwenye busara na kupitia ugumu zaidi. Kuwa na imani kunahitaji kuwa mwenye busara. Je, unaweza kumwamini Mungu vizuri ukichukua namna hii ya kawaida?

Kimetoholewa kutoka katika “Wale Wanaopenda Ukweli Wana Njia ya Kufuata” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 571)

Ikiwa huelewi mapenzi ya Mungu, ikiwa huelewi madhumuni ya maneno Yake, ikiwa huelewi lengo au matokeo ambayo Anatafuta kutimiza, ikiwa huelewi kile ambacho maneno Yake yanatafuta kutimiza na kukamilisha katika mwanadamu, basi bado huulewi ukweli. Kwa nini Mungu asema kile Anasemacho? Kwa nini Anasema kwa toni hiyo? Kwa nini Yeye ni mwenye bidii sana na mwaminifu katika kila neno Analosema? Kwa nini huchagua kutumia maneno fulani, na sio mengine? Unajua? Ikiwa sio, inamaanisha kuwa huelewi mapenzi ya Mungu au madhumuni Yake, huelewi muktadha nyuma ya maneno Yake. Ikiwa hulifahamu jambo hili, basi unawezaje kuupata ukweli? Kuufikia ukweli kunamaanisha kuwa unaelewa mapenzi Yake kupitia katika kila neno ambalo Anasema. Mara unapoelewa, unaliweka katika vitendo. Unaishi kwa kudhihirisha neno la Mungu, na kulifanya kuwa uhalisia wako. Ni hapo tu, ndipo unaweza kusema kwamba unaufahamu ukweli kwa kweli. Ni wakati tu unapokuwa na ufahamu wa kina wa neno la Mungu ndipo unaweza kuushika ukweli kwa kweli. Unalielewa tu neno la Mungu kwa kiwango cha juu juu. Kwa mfano, unasema, “Mungu Anataka tuwe waaminifu na sio wadanganyifu; kwa hiyo, lazima tuwe waaminifu.” Lakini kwa nini Mungu anataka watu wawe waaminifu na sio wadanganyifu? Kwa nini Mungu anataka watu wampende? Kwa nini Anahitaji hilo kutoka kwa watu? Kwa nini Yeye hufanya ufafanuzi kama huo? Kila kitu husemwa kutimiza matokeo fulani.

Ukweli ambao Mungu anaonyesha unaelekezwa kwa wale ambao wana kiu ya ukweli, wale wanaotafuta ukweli na wale wanaopenda ukweli. Na kwa wale ambao wanajihusisha na barua na mafundisho na wanapenda kutoa hotuba ndefu na za utukufu, hawatapata ukweli kamwe. Wanajidanganya wenyewe. Watu kama hao wana maoni yasiyo sahihi ya kusoma maneno ya Mungu; kama vile msimamo wao haujafungama, vivyo hivyo ndivyo mtazamo wao ulivyo. Watu wengine wanajua tu kuchunguza maneno ya Mungu, kujifunza kile ambacho Mungu anasema kuhusu kubarikiwa na juu ya hatima ya mwisho ya mwanadamu. Ikiwa maneno ya Mungu hayafanani na mawazo yao, wanakuwa hasi na kuacha kutafuta. Hili lina maana kwamba hawana shauku katika ukweli. Yote wanayotaka ni kuchukua njia ya mkato, kutafuta njia za kufanya mema ili waweze kujionyesha vizuri na mwishowe kupata hatima nzuri. Mtu wa aina hii anaweza kula na kunywa maneno ya Mungu, lakini hajapata ukweli. Bado kuna watu wengine ambao hula na kunywa maneno ya Mungu, lakini wanapita tu katika mizunguko; wanafikiri wameupata ukweli kwa kuelewa maana halisi ya maneno ya Mungu. Wao hawana hekima kama nini! Kula na kunywa maneno ya Mungu si sawa na kuufahamu ukweli; kuusoma ukweli si kuwa sawa hasa na kuuelewa ukweli. Neno la Mungu ni ukweli. Hata hivyo, kusoma maneno ya Mungu haimaanishi kwamba utaelewa maana yake hasa na kuupata ukweli. Kula na kunywa maneno ya Mungu ama kutakuletea ukweli au kukuletea barua na mafundisho. Hujui ni nini maana ya kuupata ukweli. Unaweza kuyashikilia maneno ya Mungu katika kiganja cha mkono wako; lakini baada ya kuyasoma, bado unashindwa kuyaelewa mapenzi ya Mungu, unapata tu barua na mafundisho kiasi. Kwanza kabisa, unapaswa kutambua kwamba neno la Mungu sio halisi vile; Neno la Mungu ni lenye kina kabisa. Bila uzoefu wa miaka mingi, unawezaje kulielewa neno la Mungu? Hata sentensi moja itahitaji maisha yako yote kuielewa kikamilifu. Unasoma maneno ya Mungu, lakini huelewi mapenzi ya Mungu; huelewi madhumuni ya maneno Yake, asili yake, matokeo yanayotafuta kutimiza, au kile yatakachotimiza. Wewe huelewi chochote kuhusu mambo haya, kwa hivyo unawezaje kuuelewa ukweli? Unaweza kuwa umepindua kurasa za kitabu mara nyingi; unaweza kuwa umekisoma mara nyingi. Labda unaweza kukariri vifungu vyake vingi kwa moyo, lakini bado hujabadilika; bado hujafanya maendeleo yoyote. Uhusiano wako na Mungu uko mbali na na wenye kufarakana kama ulivyokuwa. Bado kuna vizuizi kati yako na Mungu, kama hapo awali. Bado unaendelea kuwa na shaka Kwake. Sio tu kwamba humfahamu Mungu, lakini unampinga na hata kumkufuru. Unatoa visingizio kwa Mungu na una dhana juu Yake. Katika hali hii, unawezaje kusema kwamba umepata ukweli?

Kimetoholewa kutoka katika “Ni Wale wenye Uhalisi wa Ukweli Pekee Ndio Wanaoweza Kuongoza” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 572)

Mambo yote yanayoinuka kila siku, makubwa ama madogo, ambayo yanaweza kutikisa uamuzi wako, kuumiliki moyo wako aukuzuilia uwezo wako wa kufanya wajibu wako, na kuendelea kwako mbele vinahitaji kushughulikiwa kwa bidii; lazima vichunguzwe kwa makini na ukweli wa vitu hivi utafutwe. Hivi ni vitu vyote ambavyo vinafanyika katika ulimwengu wa uzoefu. Watu wengine huacha kazi zao wakati kitu kibaya kinawafikia, na wanashindwa kusimama kwa miguu yao baada ya kila pingamizi. Watu hawa wote ni wapumbavu ambao hawapendi ukweli, na hawatapata faida i hata wakiishi maisha yao yote kwa imani. Watu wapumbavu kama hao watawezaje kufuata hadi mwisho? Iwapo jambo kama hili litatokea mara kumi lakini usipate chochote kutoka kwalo, basi wewe ni mtu duni na asiye na maana. Watu werevu na wale ambao wana ubora wa ndani wa kweli amabao wanaelewa masuala ya kiroho ni watafutaji wa ukweli; jambo likiwafanyikia mara kumi, basi mara nane kwa kumi pengine wataweza kupata ufunuo kiasi, kupata funzo fulani, kfikia nuru na kufanya maendeleo. Mambo yanapomfanyikia mpumbavu mara kumi—yule asiyeelewa masuala ya kiroho—haitamfaidi maishani hata mara moja, haitawabadilisha hata mara moja, na haitawasababisha waelewe asili yao hata mara moja, na huu ndio mwisho wao. Kila wakati kitu kinapowafanyikia, wanaanguka chini, na kila wakati wanapoanguka chini, wanahitaji mtu mwingine kuwasaidia kusimama tena, kuwabembeleza; bila kusaidiwa na kubembelezwa, hawataweza kuinuka. Iwapo, kila wakati ambapo kitu kinafanyika, wamo kwenye hatari ya kuanguka, na kila wakati wamokwenye hatari ya yeye kudhalilika, je, huu sio mwisho kwao? Je, bado kuna sababu zinginezo kwa watu kama hawa wasio na maana kuokolewa? Wokovu wa Mungu wa binadamu ni wokovu wa wale wanaopenda ukweli, wokovu wa sehemu ndani yao ambayo ina ari ya mapenzi na maazimio na sehemu yao inayotamani ukweli na haki mioyoni mwao. Azimio la mtu ni sehemu yao ndani ya mioyo yao inayotamani haki, wema na ukweli, na iliyo na dhamiri. Mungu hukoa sehemu hii ya watu, na kupitia hiyo Anabadili tabia yao potovu, ili waweze kuelewa na kupata ukweli, ili upotovu wao uweze kutakaswa na tabia ya maisha yao ikaweze kubadilishwa. Ikiwa kamwe huna vitu hivi ndani yako, basi huwezi kuokolewa. Ikiwa ndani yako hakuna upendo wa ukweli ama hamu ya haki na mwanga wakati wowote unapokumbana na uovu, hutakuwa na hiari ya kutupa mbali vitu viovu ama azimio la kupitia shida, au azimio la kuvumilia mateso, iwapo dhamiri yako ni yenye ganzi, iwapo welekevu wako wa kupokea ukweli pia ni wenye kuwa ba ganzi na, huna umakini kwa ukweli na masuala amabayo hutokea, na iwapo una dhamira katika mambo yote, na, huwezi kushughulika au kutatua mambo wewe mwenyewe, basi hakuna njia ya kuokolewa. Mtu wakama huyu hana chochote cha kumpendekeza, hana chochote cha thamani cha kufanya kazi Dhamiri yao imekufa ganzi, akili yake imevurugwa, na hawapendi ukweli wala kutamani haki katika kina cha mioyo yao, na haijalishi jinsi Mungu Anavyonena kwa wazi ama kwa dhahiri kuhusiana n ukweli, wao hawajibu, kana kwamba walikufa tayari. Je, mambo kwao hayajafika mwisho? Mtu aliye na pumzi bakshishi ndani mwao anaweza kuokolewa kwa upumuaji bandia,lakini iwapoi kama wamekufa tayari na roho yao imeondoka, basi upumuaji bandia hautafanya lolote. Iwapo, kila mara unapokabiliwa na jambo unajikunja kutokana na hilo na kujaribu kuliepuka, hii inamaanisha bado hujashuhudia; hivyo basi huwezi kuokolewa na hakika umefika mwisho. Wakati jambo linakukumba, ni lazima kuwa mtulivu, na mtazamo unaofaa, na ni lazima kufanya chaguo. Unapaswa kujifunza kuutumia ukweli kutatua jambo lile.Katika wati wa kawaida, kuna maana gani ya wewe kuelewa ukweli fulani? Haiko hapo tu ili kujaza tumbo lako, na sio tu hapo kukupa kitu cha kusema, wala hauko hapo kwa ajili ya kutatua shida za wengine. Lililo muhimu zaidi, matumizi yake ni kutatua matatizo yako mwenyewe, shida zako mwenyewe—ni baada tu ya kutatua shida zako binafsi ndipo utaweza kutatua shida za wengine. Mbona inasemwa kuwa Petro ni tunda? Kwa sababu kuna vitu vya thamani ndani yake, vitu vilivyo na thamani ya kukamilisha, alikuwa na azimio la kuutafuta ukweli na alikuwa imara kwa makusudi; alikuwa na sababu, alikuwa tayari kupitia shida, na alipenda ukweli katika moyo wake, na hakukiachilia. Hizi zote ni hoja zenye nguvu. Kama huna yoyote kati ya hoja hizi nzito, inamaanisha kuna tatizo. Huwezi kuwa na uzoefu, na huna wowote,huna uwezo wa kutatua ugumu wa wengine. Hii ni kwa sababu hujui jinsi ya kuingia. Unachanganyikiwa unapofikwa na mambo, unahisi kuhuzunishwa, unalia, unakuwa hasi, unatoroka, na haijalishi ya kile unafanya, huna uwezo wa kushughulikia kwa usahihi.

Kimetoholewa kutoka katika “Watu Waliochanganyikiwa Hawawezi Kuokolewa” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 573)

Haidhuru nini ufanyalo, unapaswa kwanza kuelewa kwa nini unalifanya, nia inayokupeleka kulifanya jambo hili ni gani, umuhumu ni gani katika wewe kulifanya, asili ya jambo hilo ni ipi, na iwapo ufanyalo ni jambo chanya au jambo hasi. Lazima uwe na ufahamu dhahiri kuhusu masuala haya yote; hii inahitajika sana kuweza kutenda kulingana na kanuni. Ikiwa unafanya kitu kutimiza wajibu wako, basi unapaswa kutafakari: Nitalifanyaje hili? Nitatimizaje wajibu wangu vyema ili nisiwe nafanya kwa uzembe tu? Unapaswa kusogea karibu na Mungu katika jambo hili. Kusogea karibu na Mungu kunamaanisha kutafuta ukweli katika jambo hili, kutafuta njia ya kutenda, kutafuta mapenzi ya Mungu, kutafuta jinsi ya kumridhisha Mungu. Hivi ndivyo jinsi ya kusonga karibu na Mungu katika kila jambo ufanyalo. Haihusu kufanya taratibu za kidini au tendo lionekanalo kwa nje. Inafanywa kwa kusudi la kutenda kulingana na kweli baada ya kutafuta mapenzi ya Mungu. Ikiwa daima unasema “Asante Mungu” wakati hujafanya chochote, lakini unapofanya kitu, unaendelea kukifanya jinsi upendavyo, basi aina hii ya asante ni tendo la kuonekana kwa nje tu. Unapotimiza wajibu wako au kushughulikia kitu, unapaswa daima kufikiri: Ninapaswaje kutimiza wajibu huu? Mapenzi ya Mungu ni yapi? Ni ili wewe usogee karibu na Mungu kupitia unachofanya, na, kwa hufanya hivyo, unazitafuta kanuni na ukweli wa matendo yako pamoja na mapenzi ya Mungu, na usipotee kutoka kwa Mungu katika chochote utendacho. Mtu wa aina hii tu ndiye anayemwamini Mungu kwa kweli. Siku hizi, kila wakati ambapo watu wanakumbana na mambo, bila kujali hali yao halisi ilivyo, wanafikiri wanaweza kufanya hili na ile, kwa hivyo hawana Mungu mioyoni mwao, na wanafanya haya kulingana na mapenzi yao. Bila kujali iwapo matendo yao yanafaa au la, au kwamba yanalingana na ukweli au la, wanaendelea tu kwa ukaidi, na kutenda kulingana na nia zao binafsi. Kwa kawaida inaweza kuonekana kwamba Mungu yupo mioyoni mwao, lakini wafanyapo vitu, Mungu hayupo mioyoni mwao. Watu wengine husema, “Siwezi kumkaribia Mungu katika vitu nivitendavyo. Zamani, nilizoea kufanya sherehe za kidini, na nilijaribu kumkaribia Mungu, lakini ilikuwa bure. Sikuweza kusogea karibu na Yeye.” Watu wa aina hii hawana Mungu ndani yao, ni wabinafsi tu moyoni mwao na hawawezi tu kuuweka ukweli katika matendo katika kitu chochote afanyacho. Kutotenda kulingana na ukweli kunamaanisha kufanya vitu kulingana na mapenzi yao wenyewe, na kufanya vitu kulingana na mapenzi yao wenyewe kunamaanisha kumwacha Mungu; yaani, Mungu hayupo ndani ya ndani ya mioyo yao. Mawazo ya binadamu kwa kawaida yanaonekana mazuri na sahihi kwa watu, na yanaonekana kana kwamba hayawezi kukiukaukweli kwa kiasi kikubwa sana. Watu huhisi kwamba kufanya mambo kwa jinsi hii kutakuwa kuweka ukweli katika matendo; wanahisi kwamba kufanya mambo kwa jinsi hiyo kutakuwa kumtii Mungu. Hakika, hawamtafuti Mungu kwa kweli au kumwomba Mungu kulihusu, na hawajitahidi kulifanya vizuri kulingana na mahitaji ya Mungu, ili kuridhisha mapenzi Yake. Hawamiliki hali hii ya kweli, wala hawana hamu kama hiyo. Hili ndilo kosa kubwa zaidi ambalo watu hufanya katika kutenda kwao. Unamwamini Mungu, lakini humweki Mungu moyoni mwako. Hii sio dhambi vipi? Je, hujidanganyi mwenyewe? Ni aina gani za athari ambazo unaweza kuvuna ukiendelea kuamini jinsi hiyo? Isitoshe, umuhimu wa imani unaweza kuonyeshwa vipi?

Kimetoholewa kutoka katika “Kutafuta Mapenzi ya Mungu ni Kwa Ajili ya Kutenda Ukweli” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 574)

Ulipofanya jambo fulani, Mungu hakuridhika kabisa. Ulipokuwa unakaribia kufanya jambo hilo, je, ulimwomba Yeye? Je, uliwahi kutafakari, “Je, jambo hili lingetazamwaje na Mungu ikiwa lingeletwa mbele Yake? Je, Angefurahi au angekerwa ikiwa Angejua kulihusu? Je, Angelichukia?” Wewe hukulitafuta, sivyo? Hata wengine walipokukumbusha, bado ulifikiria kuwa jambo hilo halikuwa jambo kubwa, na kwamba halikwenda kinyume na kanuni zozote na halikuwa dhambi. Hivyo, kitu hiki ulichofanya kiliikosea tabia ya Mungu na kuchochea hasira kubwa sana kutoka Kwake, hata kufikia hatua ya Yeye kukudharau. Ikiwa ungetafuta na kuchunguza, na kuona jambo hilo wazi wazi kabla ya kuchukua hatua, je, usingewza basi kulidhibiti? Ingawa wakati mwingine watu hawako katika hali nzuri, wakichukua kila kitu wanachopanga kufanya kwa dhati mbele za Mungu kwa uchunguzi na utafutaji, hawatafanya makosa yoyote makubwa. Wapokuwa wakitenda ukweli, ni vigumu kwa watu kuepuka kufanya makosa, lakini ikiwa unajua jinsi ya kufanya mambo kulingana na ukweli unakuwa ukiyafanya, lakini usiyafanye kulingana na ukweli, basi tatizo ni kwamba wewe huupendi ukweli. Tabia ya mtu asiyependa ukweli haitabadilishwa. Ikiwa huwezi kuyafahamu kwa usahihi mapenzi ya Mungu, na hujui jinsi ya kutenda, basi unapaswa kufanya ushirika na wengine. Ikiwa hakuna mtu yeyote anayehisi kwamba anaweza kuliona jambo hilo wazi, basi unapaswa kutekeleza suluhisho lililo la busara zaidi. Hata hivyo, ikiwa hatimaye utagundua kwamba katika kulitekeleza kwa njia hii umefanya kosa dogo, basi unapaswa kulirekebisha haraka, na kisha Mungu hatalihesabu kosa hili kama dhambi. Kwa sababu ulikuwa na nia nzuri ulipokuwa ukilitia jambo hili katika vitendo, na ulikuwa ulikuwa ukitenda kulingana na ukweli na kwamba hukuliona tu vizuri, na matendo yako yalisababisha makosa fulani, basi hii ilikuwa hali ya kupunguzia hatia. Hata hivyo, siku hizi watu wengi hutegemea tu mikono yao miwili kufanya kazi na kwa akili zao wenyewe kufanya hili na lile, na wao huzingatia maswali haya kwa nadra sana: Je, kutenda kwa njia hii kunalingana na mapenzi ya Mungu? Je, Mungu atafurahi nikifanya jambo hili hivi? Je, Mungu ataniamini nikilifanya hivi? Je, nitakuwa nikiuweka ukweli katika vitendo nikilifanya hivi? Mungu akisikia kuhusu jambo hili, je, Ataweza kusema, “Umefanya jambo hili vizuri na inavyofaa. Endelea vivyo hivyo”? Je, unaweza kuchunguza kwa uangalifu kila jambo unalokumbana nalo? Je, unaweza kuwa mwangalifu na mwenye umakini katika kila mojawapo ya mambo haya? Au, je, unaweza kutafakari ikiwa Mungu anadharau njia unayofanya, jinsi kila mtu anavyohisi kuhusu njia zako, na ikiwa unazifanya kulingana na mapenzi yako mwenyewe au kuridhisha tama zako mwenyewe…? Lazima ufikirie zaidi na utafute zaidi, na makosa yako yatazidi kuwa madogo zaidi. Kufanya vitu kwa njia hii kutathibitisha kwamba wewe ni mtu ambaye anatafuta ukweli kwa dhati na kwamba wewe ni mtu anayemcha Mungu, kwa sababu unafanya mambo kulingana na mwelekeo ambao ukweli unahitaji.

Ikiwa vitendo vya muumini havilingani na ukweli, basi yeye ni sawa na asiyeamini. Huyu ni aina ya mtu asiye na Mungu ndani ya moyo wake, na ambaye anamwacha Mungu, na mtu kama huyu ni kama mfanyikazi aliyeajiriwa katika familia ya Mungu anayemfanyia bwana wake kazi duni duni, hupokea fidia kidogo, na kisha anaondoka. Huyu si mtu anayemwamini Mungu. Hapo awali, kulitajwa kile unachoweza kufanya ili kupata idhini kutoka kwa Mungu. Idhini kutoka kwa Mungu ni jambo la kwanza unalopaswa kufikiria kuhusu na kulifanyia kazi; inapaswa kuwa kanuni na wigo la matendo yako. Sababu ikupasayo kuamua iwapo kile unachokitenda kinapatana na ukweli ni kwamba kikipatana na ukweli, basi hakika kinalingana na mapenzi ya Mungu. Si kwamba unapaswa kupima iwapo jambo ni sahihi au kosa, au kama linalingana na kile watu wote wanachopenda, au ikiwa kinapatana na tamaa zako mwenyewe; badala yake, unapaswa kuamua iwapo inalingana na ukweli, na iwapo inafaidi kazi na masalahi ya kanisa au la. Ukizingatia vitu hivi, basi utakuwa zaidi na zaidi sawa na mapenzi ya Mungu unapofanya vitu. Kama huzingatii vipengele hivi, na utegemee tu mapenzi yako unapofanya vitu, basi una uhakikisho kuvifanya kimakosa, kwa sababu mapenzi ya mwanadamu sio ukweli na, bila shaka, hayalingani na Mungu. Ukitaka kupewa idhini na Mungu, basi ni lazima utende kulingana na ukweli badala ya kulingana na mapenzi yako mwenyewe. Watu wengine hujihusisha na mambo fulani ya faragha wakidai kwamba ni kutimiza wajibu wao. Kina ndugu zao basi wanaona hili kuwa lisilofaa, na wanawasuta kwa ajili ya hilo, lakini watu hawa hawakubali lawama. Wanafikiri kwamba kwa sababu lilikuwa jambo la kibinafsi ambalo halikuhusisha kazi, fedha, au watu wa kanisa, kwa hivyo halihesabiwi kama kukiuka mawanda ya ukweli, na Mungu hapaswi kuingilia kati katika jambo hili. Vitu vingine vinaweza kukuonekania kuwa ni mambo ya kibinafsi ambayo hayahusishi kanuni au ukweli wowote. Hata hivyo, ukiangalia kitu ulichofanya, wewe ulikuwa mbinafsi sana kwa kuwa hukuzingatia kazi ya familia ya Mungu au jinsi ambavyo kile ulichofanya kingeiathiri; ulikuwa ukizingatia tu faida yako mwenyewe. Hii tayari inahusisha usahihi wa watakatifu, na vilevile masuala yanayohusiana na ubinadamu wa mtu. Ingawa kile ulichokuwa ukifanya hakikuhusisha masilahi ya kanisa, wala hakikujumuisha ukweli, kujihusisha na jambo la faragha huku ukidai kuwa unatekeleza wajibu wako hakulingani na ukweli. Bila kujali unachokifanya, jambo ni kubwa au dogo kiasi gani, na kama unalifanya ili kutimiza wajibu wako katika familia ya Mungu au kwa ajili ya sababu zako za faragha, lazima ufikirie kama kile unachofanya kinalingana na mapenzi ya Mungu, na vile vile kama ni kitu ambacho mtu ambaye ana ubinadamu anapaswa kufanya. Ukitafuta ukweli kwa namna hiyo katika kila kitu unachofanya, basi wewe ni mtu anayemwamini Mungu kwa kweli. Ukishughulikia kwa moyo wote kila jambo na kila ukweli kwa njia hii, basi utaweza kufanikisha mabadiliko katika tabia yako. Watu wengine hufikiri kwamba wanapokuwa wakifanya kitu cha kibinafsi, wanaweza tu kupuuza ukweli, wakifanye watakavyo, na wakifanye kwa njia yoyote inayowafurahisha na kwa namna yoyote ile iliyo na faida kwao. Hawafikirii hata kidogo jinsi inavyoweza kuathiri familia ya Mungu, wala hawafikirii kama kile wanachofanya kinastahili umakini wa kitakatifu. Hatimaye, punde wanapomalizana na jambo hili, wanakuwa waovu ndani yao na kuhisi wasiwasi, ingawa hawajui ni kwa nini. Je, si hii ni adhabu inayowafaa? Ukifanya vitu ambavyo havijaidhinishwa na Mungu basi umemkosea Mungu. Ikiwa mtu hapendi ukweli, na mara nyingi nafanya vitu kulingana na mapenzi yake, basi atamkosea Mungu mara kwa mara. Watu kama hao kwa kawaida hawakubaliwi na Mungu katika yale wayatendayo, na wasipotubu, basi adhabu haitakuwa mbali sana nao.

Kimetoholewa kutoka katika “Kutafuta Mapenzi ya Mungu ni Kwa Ajili ya Kutenda Ukweli” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 575)

Unapokuwa ukitimiza wajibu wako, unapaswa kujichunguza kila wakati ili uone iwapo unafanya mambo kulingana na kanuni, iwapo utendaji wa wajibu wako unafikia kiwango kinachotakiwa, iwapo unaufanya tu kwa uzembe au la, iwapo umejaribu kukwepa majukumu yako na iwapo kuna matatizo yoyote katika mtazamo wako na jinsi unavyofikiri. Mara baada ya kutafakari juu yako mwenyewe na kuelewa kabisa mambo haya, utatimiza wajibu wako kwa urahisi zaidi. Bila kujali unakabiliwa na nini unapokuwa ukifanya wajibu wako—uhasi na udhaifu, au kuwa katika hali mbaya baada ya kushughuliwa—unapaswa kuuchukulia vizuri, na lazima pia utafute ukweli na uelewe mapenzi ya Mungu. Kwa kufanya mambo haya, utakuwa na njia ya kutenda. Iwapo ungependa kutimiza wajibu wako vizuri, basi sharti usiathiriwe na hali yako ya moyo. Bila kujali unahisi kwamba wewe ni hasi au dhaifu jinsi gani, unapaswa kutenda ukweli katika kila kitu unachofanya, kwa ukamilifu kabisa na kwa kufuata kanuni. Ukifanya hivi, mbali na watu wengine kukupenda, Mungu pia atakupenda. Hasa, utakuwa mtu mwaminifu na anayewajibika; utakuwa mtu mzuri kwa kweli ambaye hutimiza wajibu wake kufikia kiwango kinachotakiwa na anayeishi kwa kudhihirisha kikamilifu mfano wa mtu halisi. Watu kama hao hutakaswa na hufanikisha mabadiliko ya kweli wanapotimiza wajibu wao, na wanaweza kusemekana kuwa waaminifu machoni pa Mungu. Watu waaminifu pekee ndio wanaoweza kuvumilia kutenda ukweli na kufanikiwa katika kutenda kwa maadili, na wanaweza kutekeleza wajibu wao kufikia kiwango kinachotakiwa.

Kimetoholewa kutoka katika “Uingiaji Katika Uzima Lazima Uanze na Uzoefu wa Kutenda Wajibu wa Mtu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 576)

Kwa watu wengine, bila kujali suala wanalokumbana nalo wanapokuwa wakitimiza wajibu wao, hawatafuti ukweli na daima wanatenda kulingana na dhana, mawazo, fikira na tamaa zao wenyewe. Wao daima huridhisha tamaa zao za binafsi na tabia zao potovu huwa zinaongoza vitendo vyao kila mara. Ingawa wanaweza kukamilisha wajibu waliopewa, hawapati ukweli wowote. Kwa hiyo mtu huyu anategemea nini katika utimizaji wa wajibu wake? Hategemei ukweli na hamtegemei Mungu. Kiasi cha ukweli anachoelewa hakijachukua nafasi kuu moyoni mwake. Anategemea vipaji na uwezo wake, ujuzi ambao amepata na talanta zake, na pia utashi wao wenyewe au nia nzuri ya kuwezesha kazi hiyo kufanyika. Asili ni tofauti, siyo? Ingawa wakati mwingine unaweza kutegemea asili, mawazo, fikira, ujuzi na kujifunza kwako katika kutimiza wajibu wako, hakuna masuala ya kanuni hujitokeza katika mambo unayofanya. Kwa juu inaonekana kana kwamba hujachukua njia mbaya, lakini kuna jambo moja ambalo haliwezi kupuuzwa: Wakati wa mchakato wa kufanya wajibu wako, ikiwa mawazo, fikira na tamaa zako za kibinafsi hazibadiliki kamwe na hazibadilishwi kamwe na ukweli, ikiwa vitendo na matendo yako hayalingani kamwe na kanuni za kweli, basi matokeo ya mwisho yatakuwa nini? Utakuwa mtendaji huduma, na hili ndilo tu lililoandikwa katika Biblia: “Wengi watasema Kwangu siku hiyo, Bwana, Bwana, hatujatabiri kupitia jina Lako? Na kutoa mapepo kupitia jina Lako? Na kutenda miujiza mingi kupitia jina Lako? Na hapo ndipo Nitasema wazi kwao, Sikuwahi kuwajua: tokeni Kwangu, ninyi ambao hutenda udhalimu.” Je, kwa nini Mungu huwaita watu hawa ambao huchangia juhudi zao na ambao hutoa huduma “ninyi ambao hutenda udhalimu”? Kuna hoja moja ambayo tunaweza kuwa na uhakika nayo, na hiyo ni kwamba, haijalishi watu hawa wanafanya wajibu upi au ni kazi ipi wanayoifanya, motisha, chanzo, nia na mawazo ya watu hawa yanatokana kabisa na tamaa zao za ubinafsi, yametegemezwa kabisa kwa mawazo yao wenyewe na juu ya masilahi yao ya kibinafsi, na yamelenga kabisa maanani na mipango kama vile kujiheshimu, hadhi na majivuno, na matarajio ya siku za usoni. Hawana ukweli mioyoni mwao, na hawatendi kulingana na kanuni za ukweli. Kwa hivyo, cha muhimu wewe kufuatilia sasa ni nini? (Kutafuta ukweli, na kutenda wajibu wetu kulingana na mapenzi ya Mungu na mahitaji ya Mungu.) Unapaswa kufanya nini hasa, wakati ambapo unatekeleza wajibu wako kulingana na mahitaji ya Mungu? Kuhusiana na nia na mawazo uliyo nayo unapokuwa ukifanya kitu, lazima ujue jinsi ya kutambua kama yanakubaliana na ukweli au la, na kama hayo ni kwa ajili ya matamanio yako ya kibinafsi au kwa ajili ya masilahi ya familia ya Mungu. Ikiwa yanakubaliana na ukweli, basi unaweza kufuata mwelekeo wa mawazo yako kufanya wajibu wako. Ikiwa hayakubaliani na ukweli, basi lazima ugeuke upesi na uachane na njia hiyo. Njia hiyo si sahihi, na huwezi kutenda kwa namna hiyo; ukitenda kwa namna hiyo, basi utakuwa mtu anayeshiriki katika udhalimu.

Kimetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kupitia Maneno ya Mungu katika Wajibu wa Mtu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 577)

Kuna kanuni ya msingi zaidi ya Bwana wa uumbaji anavyovishughulikia viumbe, ambayo pia ndiyo kanuni ya juu zaidi. Jinsi anavyoshughulikia viumbe walioumbwa hutegemea kabisa mpango Wake wa usimamizi na matakwa Yake; Hahitaji kushauriana na mtu yeyote yule, wala Hahitaji kukubaliana na mtu yeyoye yule. Chochote Alichotafuta kufanya, na jinsi Alivyokusudia kuwatendea watu, Anafanya hivyo, na haijalishi Afanyacho na jinsi anayowatendea watu, yote yanapatana na kanuni, kanuni ambazo kwazo Bwana wa uumbaji hufanya kazi. Kama kiumbe aliyeumbwa, kitu cha pekee cha kufanya ni kutii; hakupaswi kuwa na chaguo lingine. Hii inaonyesha nini? Inaonyesha kwamba Bwana wa uumbaji atakuwa Bwana wa uumbaji kila wakati; Ana nguvu na sifa zinazostahili kupanga na kutawala kiumbe yeyote aliyeumbwa kama Anavyopenda, na Hahitaji sababu ya kufanya hivyo. Haya ni mamlaka Yake. Hakuna yeyote kati ya viumbe walioumbwa ambaye, kulingana na alivyo kiumbe aliyeumbwa, ana nguvu au anayestahili kutoa uamuzi juu ya jinsi Muumba anavyopaswa kutenda au juu ya ikiwa kile anachofanya ni chema au kibaya, wala hakuna kiumbe yeyote aliyeumbwa anayestahili kuchagua ikiwa anapaswa kutawaliwa, kupangiwa, au kutupwa na Bwana wa uumbaji. Vivyo hivyo, hakuna kiumbe yeyote aliyeumbwa anayestahili kuchagua jinsi anavyotawaliwa na kutupwa na Bwana wa uumbaji. Huo ndio ukweli wa juu zaidi. Bila kujali Bwana wa uumbaji Amewafanyia nini viumbe Wake walioumbwa, na bila kujali ameifanyaje, wanadamu Aliowaumba wanapaswa kutenda tu jambo moja: Kutafuta, kutii, kujua na kukubali ukweli huu uliowekwa na Bwana wa uumbaji. Matokeo ya mwisho yatakuwa kwamba Bwana wa uumbaji atakuwa amekamilisha mpango Wake wa usimamizi na kumaliza kazi Yake, baada ya kusababisha mpango Wake wa usimamizi kusonga bila vizuizi vyovyote; wakati huo huo, kwa sababu viumbe walioumbwa wamekubali utawala na mipango ya Muumba, na kutii utawala na mipango Yake, watakuwa wamepata ukweli, wameelewa mapenzi ya Muumbaji, na kuja kujua tabia Yake. Bado kuna kanuni nyingine ambayo lazima Niwaambie: Bila kujali anachofanya Muumba, bila kujali Anavyojidhihirisha, na bila kujali iwapo Anachofanya ni tendo kubwa au dogo, Yeye bado ni Muumba; ilhali wanadamu wote Aliowaumba watasalia kuwa viumbe, bila kujali wamefanya nini na bila kujali walivyo na vipaji au jinsi ambavyo wamepata fadhila. Kuhusiana na binadamu walioumbwa, bila kujali wamepokea neema na baraka kiasi gani kutoka kwa Muumba, au rehema, wema au ukarimu kiasi gani, hawapaswi kujiona kama wao ni tofauti na watu wengine au kufikiri kwamba wanaweza kuwa sawa na Mungu na kwamba wamewekwa katika tabaka la juu kuliko viumbe wengine. Bila kujali Mungu amekupa vipaji vingapi au Amekupa neema kiasi gani, au Amekutendea kwa wema jinsi gani, au iwapo Amekupa vipawa vichache vya pekee, hakuna vyovyote kati ya vitu hivi ambavyo ni mali yako. Wewe ni kiumbe na kwa hivyo utakuwa kiumbe milele. Hupaswi kufikiri kamwe kwamba, “Mimi ni kipenzi mikononi mwa Mungu. Yeye hawezi kunipiga. Mtazamo wa Mungu kwangu daima utakuwa wa upendo, utunzaji na mpapaso wa upole wenye mnong'ono wa faraja na wa kutia moyo.” Kinyume na hayo, machoni pa Muumba wewe ni sawa na viumbe wengine wote; Mungu anaweza kukutumia jinsi Atakavyo, na pia Anaweza kukupangia jinsi Atakavyo, na Anaweza kukupangia jinsi Atakavyo ufanye kila wajibu miongoni mwa watu, matukio na vitu vya kila aina. Haya ndiyo maarifa ambayo watu wanapaswa kuwa nayo na utambuzi mzuri ambao wanapaswa kuwa nao. Iwapo mtu anaweza kuelewa na kuyakubali maneno haya, uhusiano wake na Mungu utazidi kuwa wa kawaida na ataunda uhusiano halali zaidi na Yeye; iwapo mtu anaweza kuelewa na kukubali maneno haya, ataweza kuelewa nafasi yake vizuri, kuchukua nafasi hiyo na kuendelea kufanya wajibu wake.

Kimetoholewa kutoka katika “Unaweza Kujua Matendo Ya Mungu kwa Kutafuta tu Ukweli” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 578)

Kumjua Mungu kunapaswa kutimizwa kupitia kwa kusoma na kuyaelewa maneno ya Mungu. Wengine husema: “Sijamwona Mungu mwenye mwili, hivyo ningewezaje kumjua Mungu?” Kwa kweli, maneno ya Mungu ni maonyesho ya tabia Yake. Kutoka kwa maneno ya Mungu unaweza kuuona upendo Wake na wokovu kwa wanadamu, na vile vile mbinu Yake ya kuwaokoa … Hii ni kwa sababu maneno ya Mungu yanaonyeshwa na Mungu Mwenyewe bali hayajaandikwa na mwanadamu. Yameonyeshwa na Mungu binafsi- Yeye; Mungu mwenyeweAnaeleza maneno Yake mwenyewe na sauti Yake ya ndani. Kwa nini yanaitwa maneno kutoka moyoni? Ni kwa sababu hayo hutolewa kutoka ndani kabisa, na yanaonyesha tabia Yake, mapenzi Yake, mawazo Yake, upendo Wake kwa wanadamu, wokovu Wake wa wanadamu, na matarajio Yake ya wanadamu…. Matamshi ya Mungu yanajumuisha maneno makali, na maneno ya upole na yenye kuzingatia, na vile vile maneno mengine ya ufunuo ambayo hayalingani na matakwa ya binadamu. Ikiwa unayaangalia tu maneno ya ufunuo, unaweza kuhisi kwamba Mungu ni mkali. Ikiwa unaangalia maneno ya upole tu, utaweza kuhisi kuwa Mungu sio mweneye mamlaka sana. Hivyo basi hupaswi kuyachukua nje ya muktadha; badala yake yaangalie kutoka kila pembe. Wakati mwingine Mungu huzungumza kwa mtazamo mpole na wenye huruma, na hivyo basi watu wanauona upendo Wake kwa wanadamu; wakati mwingine Yeye huzungumza kwa mtazamo mkali sana, na hivyo basi watu wanaona tabia Yake ambayo haitavumilia kosa lolote. Mwanadamu ni mchafu kwa njia ya kusikitisha, na hastahili kuuona uso wa Mungu au kuja mbele Zake. Kuwa watu sasa wanaweza kukubaliwa kuja mbele Zake ni kwa neema Yake tu. Hekima ya Mungu inaweza kuonekana kutokana na jinsi Yeye anavyofanya kazi na kwa umuhimu wa kazi Yake. Watu bado wanaweza kuona mambo haya katika maneno ya Mungu hata bila mwingiliano wa moja kwa moja kutoka Kwake. Wakati mtu ambaye kwa kweli ana ufahamu wa wa Mungu anapowasiliana na Kristo, kuwasiliana kwake na Kristo kunaweza kulingana na ufahamu wake wa Mungu; hata hivyo, wakati mtu ambaye ana ufahamu tu wa kinadharia anakutana na Mungu, hawezi kuona uhusiano. Kipengele hiki cha ukweli ni siri kubwa zaidi; ni ngumu kuelewa. Jumlisha maneno ya Mungu ya siri ya kupata mwili, yaangalie kutoka pande zote, na kisha Sali pamoja, tafakari, na shiriki zaidi kuhusu kipengele hiki cha ukweli. Kwa kufanya hili utaweza kupata nuru ya Roho mtakatifu na uje kuelewa. Kwa sababu wanadamu hawana nafasi ya kuwasiliana na Mungu moja kwa moja, lazima wategemee uzoefu wa aina hii kupata njia zao na kuingia kidogo kwa wakati ili kupata maarifa ya kweli ya Mungu.

Kimetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kumjua Mungu Mwenye Mwili” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 579)

Kumjua Mungu kunamaanisha nini? Kunamaanisha kuwa na uwezo wa kujua shangwe, hasira, huzuni na furaha Yake; huku ndiko kumjua Mungu. Unadai kwamba umemwona Yeye, ilhali huelewi shangwe, hasira, huzuni, na furaha Yake, na huelewi tabia Yake. Vile vile huelewi haki Yake wala rehema Zake, wala hujui Anachokipenda ama Anachokichukia. Huu si ufahamu wa Mungu. Kwa hivyo, watu wengine wanaweza kumfuata Mungu lakini hawawezi kwa kweli kumwamini: hii ndiyo tofauti. Ikiwa unamjua Mungu, unamwelewa, na unaweza kuelewa mapenzi Yake kiasi, basi unaweza kumwamini kwa kweli, kumtii kwa kweli, kumpenda kwa kweli, na kumwabudu Yeye kwa kweli. Ikiwa huelewi mambo haya, basi wewe ni mfuasi tu ambaye hufuata tukuenda na umati. Hiyo haiwezi kuitwa kutii kwa kweli au ibada ya kweli. Je, ibada ya kweli inafanyika vipi? Bila ubaguzi wale wote ambao kwa kweli wanamjua Mungu humwabudu na kumcha kila wanapomwona; wote hulazimika kusujudu na kumwabudu Yeye. Kwa sasa, wakati Mungu mwenye mwili yuko kazini, ndivyo kadri ufahamu watu walionao wa tabia Yake na kile Alicho nacho na kile Alicho, ndivyo zaidi watakavyovithamini vitu hivi na ndivyo zaidi watamchaa Yeye. Kwa kawaida, kadiri watu walivyo na ufahamu mdogo, ndivyo wanavyokosa kuwa makini zaidi, na hivyo wanamtendea Mungu kama mwanadamu. Ikiwa watu kwa kweli wanngemjua na kumwona Mungu wangetetemeka kwa hofu. “Lakini yule ajaye baada ya mimi ni mwenye nguvu zaidi kuliko mimi, ambaye sistahili kuvichukua viatu vyake.”—kwa nini Yohana alisema haya? Ijapokuwa kwa kina hakuwa na ufahamu mkubwa, alijua kwamba Mungu ni wa kustaajabisha. Ni watu wangapi siku hizi wanaweza kumcha Mungu? Iwapo hawajui tabia Yake, basi wanawezaje kumcha Mungu? Watu hawajui kiini cha Kristo wala kuelewa tabia ya Mungu, sembuse kuwezakumwabudu Mungu. Ikiwa wanaona tu kuonekana kwa nje kwa kawaida kwa Kristo ilihali hawajui asili Yake, basi ni rahisi kwa wao kumchukulia Kristo kama tu mtu wa kawaida. Huenda wakachukua mtazamo usio wa heshima Kwake, na wanaweza kumdanganya, kumkataa, kutomtii, na kutoa hukumu Kwake. Wanaweza kujiona wenye haki na kutochukulia neno Lake kwa makini; wanaweza hata kuibua fikira, shutuma na kumkufuru Mungu. Ili kutatua masuala haya mtu lazima ajue kiini na uungu wa Kristo. Hiki ndicho kipengele kikuu cha kumjua Mungu; ni kile amabacho yeyote anayeamini katika Mungu wa utendaji wanapaswa kuingia na kufanikisha.

Kimetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kumjua Mungu Mwenye Mwili” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: Kuingia Katika Uzima (V)

Inayofuata: Hatima na Matokeo

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp