Kuingia Katika Uzima (V)

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 520)

Katika kipindi hiki akimfuata Yesu, Petro alikuwa na maoni mengi kuhusu Yeye na siku zote Alimhukumu kutokana na mtazamo wake. Ingawa alikuwa na kiwango fulani cha ufahamu wa Roho Mtakatifu, ufahamu huu haukuwa wazi kabisa, na haya yanaonekana katika maneno yake aliposema: “Lazima nimfuate yeye aliyetumwa na Baba wa mbinguni. Lazima nimtambue yule aliyechaguliwa na Roho Mtakatifu.” Hakuelewa mambo yale ambayo Yesu alifanya na hakuwa dhahiri kuyahusu. Baada ya kumfuata kwa muda fulani alivutiwa kwa kile alichofanya Yeye na kusema, na kwa Yesu Mwenyewe. Alikuja kuhisi kwamba Yesu alivutia upendo na heshima; alipenda kujihusisha na Yeye na kuwa kando Yake, na kusikiliza maneno Yake Yesu kulimpa ruzuku na msaada. Katika kipindi kile alichomfuata Yesu, Petro alitazama na kutia moyoni kila kitu kuhusu maisha Yake: Matendo Yake, maneno Yake, mwendo Wake na maonyesho Yake. Alipata ufahamu wa kina kwamba Yesu hakuwa kama binadamu wa kawaida. Ingawa mwonekano Wake wa binadamu ulikuwa wa kawaida kabisa, Alijaa upendo, huruma, na ustahimilivu kwa binadamu. Kila kitu alichokifanya au kusema kilikuwa chenye msaada mkubwa kwa wengine, na akiwa kando Yake, Petro aliona na kujifunza mambo ambayo hakuwahi kuyaona wala kuyasikia awali. Aliona kwamba ingawa Yesu hakuwa na kimo kikubwa wala ubinadamu usio wa kawaida, Alikuwa na umbo la ajabu na lisilo la kawaida kwa kweli. Ingawa Petro hakuweza kuyafafanua kabisa, aliweza kuona kwamba Yesu alikuwa na mwenendo tofauti na kila mtu mwingine, kwani Aliyafanya mambo yaliyokuwa tofauti kabisa na yale yaliyofanywa na binadamu wa kawaida. Tangu wakati huo akiwa na Yesu, Petro alitambua pia kwamba hulka Yake ilikuwa tofauti na ile ya binadamu wa kawaida. Siku zote alikuwa na mwenendo dhabiti na hakuwahi kuwa na haraka, hakupigia chuku wala kupuuza chochote, na aliyaishi maisha Yake kwa njia iliyofichua hulka iliyokuwa ya kawaida na ya kuvutia. Katika mazungumzo, Yesu alikuwa mwenye madaha na uzuri, mwenye uwazi na mchangamfu ilhali pia mtulivu, na Hakuwahi kupoteza heshima Yake katika utekelezaji wa kazi Yake. Petro aliona kwamba Yesu wakati mwingine alikuwa mnyamavu, ilhali nyakati nyingine alizungumza kwa mfululizo. Wakati mwingine Alikuwa na furaha sana kiasi kwamba alionekana kuwa njiwa anayerukaruka na kuchezacheza, na ilhali nyakati nyingine Alihuzunika sana kiasi cha kwamba hakuzungumza kamwe, ni kana kwamba alikuwa mama aliyechoka sana. Nyakati nyingine Alijawa na hasira, kama askari jasiri anayefyatuka kuwaua adui, na wakati mwingine hata kama simba anayenguruma. Nyakati nyingine Alicheka; nyakati nyingine aliomba na kulia. Haijalishi ni vipi Yesu alivyotenda, Petro alizidi kuwa na upendo na heshima isiyokuwa na mipaka Kwake. Kicheko cha Yesu kilimjaza kwa furaha, huzuni Yake ikamtia simanzi, hasira Yake ikamtetemesha, huku huruma Zake, msamaha na madai makali Aliyotoa kwa watu yalimfanya aje kumpenda Yesu kwa kweli, na akaweza kumcha na kumtamani kwa kweli. Bila shaka, Petro alikuja kutambua haya yote kwa utaratibu baada ya kuishi kando yake Yesu kwa miaka michache.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 521)

Kulikuwepo na kilele katika yale Petro alipitia, wakati mwili wake ulikuwa karibu kunyenyekea kabisa, lakini Yesu akamtia moyo ndani. Na akajitokeza kwake mara moja. Wakati Petro alikuwa katika mateso makuu na kuhisi kwamba moyo wake ulisikitika, Yesu alimwelekeza: “Ulikuwa na Mimi ulimwenguni, na Nilikuwa na wewe hapa. Na Ingawa awali tulikuwa pamoja mbinguni, hata hivyo, ni ya ulimwengu wa kiroho. Sasa Nimerudi katika ulimwengu wa kiroho, na wewe umo ulimwenguni. Kwani Mimi si wa ulimwengu, na Ingawa wewe pia si wa ulimwengu, lazima utimize kazi yako hapa ulimwenguni. Kwani wewe ni mtumishi, lazima uwajibike kwa njia bora zaidi uwezayo.” Petro alipata tulizo, kwa kusikia kwamba angeweza kurudi kwa upande wa Mungu. Wakati Petro alipokuwa katika masumbuko hayo kiasi kwamba karibu awe mahututi kitandani, alisikitika kiasi cha kusema hivi: “Nimepotoka kwelikweli, siwezi kumtosheleza Mungu.” Yesu alijitokeza kwake na kusema: “Petro, huenda ikawa umesahau azimio ulilowahi kutoa mbele Yangu? Je, kwa kweli umesahau kila kitu Nilichosema? Umesahau azimio ulilonitolea?” Petro aliona kwamba alikuwa Yesu na akainuka kutoka kitandani, naye Yesu akamfariji: “Mimi si wa ulimwengu, tayari Nimekuambia wewe—hili lazima uelewe, lakini umesahau kitu kingine Nilichokuambia? ‘Wewe pia si wa ulimwengu, si wa dunia.’ Sasa hivi kunayo kazi unayohitaji kufanya, huwezi kuhuzunika namna hivi, huwezi kuteseka hivi. Ingawa binadamu na Mungu hawawezi kuishi pamoja katika ulimwengu mmoja, Ninayo kazi Yangu na wewe unayo yako, na siku moja wakati kazi yako imekamilika, tutakuwa pamoja katika himaya moja, nami Nitakuongoza wewe kuwa pamoja Nami milele na milele.” Petro alipata tulizo na hakikisho baada ya kuyasikia maneno hayo. Alijua kwamba kuteseka huku kulikuwa ni jambo ambalo lazima angevumilia na kupitia, na akatiwa msukumo kuanzia hapo kuendelea. Yesu alijitokeza haswa kwake katika kila muda muhimu, akimpa nuru na mwongozo maalum, na akifanya kazi nyingi ndani yake. Na ni nini ambacho Petro alijutia zaidi? Yesu alimwuliza Petro swali jingine (ingawa haijarekodiwa katika Biblia kwa njia hii) si kipindi kirefu baadaye Petro alikuwa amesema “Wewe ndiwe Mwana wa Mungu aliye hai,” nalo swali lenyewe lilikuwa: “Petro! Umewahi kunipenda?” Petro alielewa kile alichomaanisha, na kusema: “Bwana! Niliwahi kumpenda Baba wa mbinguni, lakini nakubali sijawahi kukupenda Wewe.” Yesu naye akasema: “Kama watu hawampendi Baba wa mbinguni, watawezaje kumpenda Mwana hapa ulimwenguni? Na kama watu hawampendi Mwana aliyetumwa na Mungu, Baba, wanawezaje kumpenda Baba aliye mbinguni? Kama kweli watu wanampenda Mwana aliye ulimwenguni, basi kwa kweli wanampenda Baba aliye mbinguni.” Wakati Petro alipoyasikia maneno haya aligundua upungufu wake. Siku zote alihisi huzuni hadi kiwango cha kulia kutokana na maneno yake “niliwahi kumpenda Baba wa mbinguni, lakini sikuwahi kukupenda Wewe.” Baada ya ufufuo na kupaa angani kwa Yesu alihuzunika na kuwa na simanzi zaidi kwa yale yote yaliyokuwa yamefanyika. Huku akikumbuka kazi yake iliyopita na kimo chake cha sasa, mara nyingi angekuja mbele ya Yesu kwa maombi, siku zote akiwa na hisia za majuto na masikitiko kwa kutoweza kwake kutosheleza tamanio la Mungu, na kutoweza kufikia viwango vya Mungu. Masuala haya yakawa ndiyo mzigo wake mkubwa. Alisema: “Siku moja nitatoa kila kitu nilicho nacho na kila nilicho, nitakupa kile chenye thamani zaidi.” Alisema: “Mungu! Ninayo imani moja tu na upendo mmoja tu. Maisha yangu hayana thamani, na mwili wangu hauna thamani. Ninayo imani moja tu na upendo mmoja tu. Ninayo imani kwako Wewe katika akili yangu na upendo Kwako wewe katika moyo wangu; mambo haya mawili tu ndiyo niliyonayo kukupatia Wewe, na wala sina kingine chochote.” Petro alihimizwa pakubwa na maneno yake Yesu, kwa sababu kabla ya Yesu kusulubishwa alikuwa amemwambia: “Mimi si wa ulimwengu huu, na wewe pia si wa ulimwengu huu.” Baadaye, wakati Petro alipofikia hali ya maumivu makali, Yesu alimkumbusha: “Petro, je, umesahau? Mimi si wa ulimwengu huu, na ni kwa ajili tu ya kazi Yangu ndipo Niliondoka mapema. Wewe pia si wa ulimwengu huu, umesahau? Nimekuambia mara mbili, kwani hukumbuki?” Petro alimsikia na kumwambia: “Sijasahau!” Yesu naye akasema: “Uliwahi kuwa na wakati mzuri ukiwa umekusanyika pamoja na Mimi kule mbinguni na kwa kipindi fulani kando Yangu mimi. Unanidata Mimi, na Mimi ninakudata. Ingawa viumbe hawa hawastahili kutajwa machoni Pangu, ninawezaje kukosa kupenda yule ambaye hana hatia na anapendeka? Je, umesahau ahadi Yangu? Lazima ulikubali agizo Langu hapa ulimwenguni, lazima utimize kazi Niliyokuaminia. Bila shaka siku moja Nitakuongoza kuwa kando Yangu.” Baada ya kuyasikia haya, Petro akahimizwa zaidi, na kupata msukumo mkubwa zaidi, kiasi cha kwamba alipokuwa msalabani, aliweza kusema hivi: “Mungu! Siwezi kukupenda vya kutosha! Hata ukiniomba nife, siwezi bado kukupenda vya kutosha! Popote Utakapotuma nafsi yangu, utimize au ukose kutimiza ahadi Zako za awali, chochote ufanyacho baadaye, ninakupenda na ninakuamini.” Kile alichoshikilia kilikuwa imani yake, na upendo wa kweli.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 522)

Sasa unafaa uweze kuona waziwazi njia iliyochukuliwa na Petro. Kama umeona hili waziwazi, basi utakuwa na hakika kuhusu kazi inayofanywa leo, kwa hiyo usingelalamika au kuwa kukaa tu, au kutamani chochote. Unafaa kupitia hali halisi aliyopitia Petro wakati huo: Alikumbwa na huzuni; hakuomba tena kuwa na mustakabali au baraka yoyote. Hakutafuta faida, furaha, umaarufu, au utajiri wa ulimwengu na alitafuta tu kuishi maisha yenye maana zaidi, ambayo yalikuwa ya kulipiza upendo wa Mungu na kujitolea kile alichokuwa nacho cha thamani kabisa kwa Mungu. Kisha angetosheka katika moyo wake. Mara nyingi aliomba kwa Yesu akitumia maneno haya: “Bwana Yesu Kristo, niliwahi kukupenda Wewe, lakini sikukupenda Wewe kwa kweli. Ingawa nilisema nina imani kwako Wewe, sikuwahi kukupenda kwa moyo wa kweli. Nilikuwa nakutazamia Wewe tu, nikikuabudu Wewe, na kukudata Wewe, lakini sikuwahi kukupenda Wewe au kuwa na imani ya kweli kwako Wewe.” Siku zote aliomba ili kutoa azimio lake, alihimizwa kila wakati na maneno Yake Yesu na kuyageuza kuwa motisha. Baadaye, baada ya kipindi cha kile alichopitia, Yesu alimjaribu yeye, akimchochea kumtaka Yeye zaidi. Alisema: “Bwana Yesu Kristo! Ninakudata kweli, na kutamani kukutazamia. Ninakosa mengi mno, na siwezi kufidia upendo Wako. Ninakusihi kunichukua hivi karibuni. Utanihitaji mimi lini? Utanichukua lini? Ni lini nitakapoutazama uso Wako tena? Sitamani kuishi tena katika mwili huu, kuendelea kupotoka, na vilevile sitamani kuasi zaidi ya nilivyoasi. Niko tayari kujitolea vyote nilivyonavyo Kwako punde iwezekanavyo, na sitamani kukuhuzunisha Wewe zaidi ya hivi nilivyofanya.” Hivi ndivyo alivyoomba, lakini hakujua wakati huo kwamba Yesu angemfanya kuwa mkamilifu. Katika makali ya majaribio yake, Yesu alijitokeza kwake tena na kusema: “Petro, Ningependa kukufanya kuwa mkamilifu, ili uwe kipande cha tunda ambacho ni dhihirisho la Mimi kukukamilisha, ambacho Nitafurahia. Unaweza kweli kunishuhudia Mimi? Umefanya kile Nilichokuomba kufanya? Umeishi kwa kudhihirisha yale maneno Niliyoyaongea? Uliwahi kunipenda Mimi, lakini Ingawa ulinipenda Mimi, umeishi kwa kunidhihirisha? Ni nini ulichonifanyia Mimi? Unatambua kwamba wewe hufai upendo Wangu, lakini wewe umenifanyia nini?” Petro aliona kwamba alikuwa hajamfanyia Yesu chochote na akakumbuka kiapo cha awali cha kumpa Mungu maisha yake. Na kwa hiyo, hakulalamika tena, na maombi yake baadaye yakazidi kuwa bora zaidi. Akaomba, akisema: “Bwana Yesu Kristo! Niliwahi kukuacha Wewe, na Wewe pia uliwahi kuniacha mimi. Tumekuwa mbalimbali kwa kipindi cha muda, na muda kiasi tukiwa pia pamoja. Ilhali unanipenda mimi zaidi ya kila kitu kingine. Nimekuasi Wewe mara nyingi na nikakuhuzunisha mara nyingi. Ninawezaje kusahau mambo kama haya? Kazi uliyofanya ndani yangu mimi na kile ambacho umeniaminia nazingatia daima, sikisahau kamwe. Pamoja na kazi uliyonifanyia mimi nimejaribu kadri ya uwezo wangu. Unajua kile ninachoweza kufanya, na unajua zaidi wajibu ninaoweza kutekeleza. Ningependa kujitiisha kwa mipango Yako, na nitajitolea kila kitu nilicho nacho Kwako. Wewe tu ndiwe unayejua kile ninachoweza kukufanyia Wewe. Ingawa Shetani alinidanganya sana na nikakuasi Wewe, ninaamini kwamba Hunikumbuki mimi kwa ajili ya dhambi hizo, kwamba hunichukulii mimi kutokana na hizo dhambi. Ningependa kuyatoa maisha yangu yote kwa ajili Yako wewe. Siombi chochote, na wala sina matumaini au mipango mingine; ningependa tu kuchukua hatua kulingana na nia Zako na kutimiza mapenzi Yako. Nitakunywa kutoka kwenye kikombe Chako kichungu, na mimi ni Wako wa kuamuru.”

Lazima muwe wazi kuhusu njia mnayotembelea; lazima muwe wazi kuhusu njia mtakayotumia katika siku za usoni, ni nini haswa ambacho Mungu atafanya kuwa mkamilifu na ni nini ambacho mmeaminiwa nacho. Siku moja, pengine, mtajaribiwa, na kama wakati huo mtaweza kutiwa msukumo kutoka kwa yale aliyopitia Petro, yatawaonyesha kwamba kwa kweli mnatembea njia ya Petro. Petro alipongezwa na Mungu kwa ajili ya imani na upendo wake wa kweli, na kwa ajili ya utiifu wake kwa Mungu. Na ilikuwa kutokana na uaminifu wake na kutamani kwake Mungu katika moyo wake ndiposa Mungu akamkamilisha kuwa timilifu. Kama kweli unao upendo na imani kama hiyo ya Petro, basi Yesu kwa kweli atakufanya kuwa timilifu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 523)

Alipokuwa akiadibiwa na Mungu, Petro aliomba, “Ee Mungu! Mwili wangu ni mkaidi, na unaniadibu na kunihukumu mimi. Nafurahi katika adabu Yako na hukumu, na hata kama Hunitaki mimi, katika hukumu Yako mimi ninaona tabia Yako takatifu na tabia Yako ya haki. Unaponihukumu, ili wengine wapate kuiona hali Yako ya haki katika hukumu Yako, ninaridhika. Ikiwa inaweza kuionyesha tabia Yako na kuiruhusu tabia Yako ya haki iweze kuonekana na viumbe wote, na kama inaweza kuufanya upendo wangu Kwako uwe safi zaidi, kwamba naweza kufikia mfano wa yule ambaye ni mwenye haki, basi hukumu Yako ni nzuri, kwa maana hivyo ndivyo mapenzi Yako ya neema yalivyo. Najua kwamba bado kuna mengi ndani yangu yaliyo ya uasi, na kwamba mimi bado sifai kuja mbele Yako. Ningependa unihukumu hata zaidi, iwe ni kupitia mazingira ya uhasama au mateso makubwa; haijalishi ni nini Utakayofanya, kwangu ni ya thamani. Upendo Wako ni mkuu, na mimi niko tayari kujiweka katika huruma Yako bila malalamiko hata kidogo.” Huu ni ufahamu wa Petro baada ya yeye kuiona kazi ya Mungu, na pia ni ushahidi wa upendo wake kwa Mungu. Leo hii, nyinyi tayari mmeshashindwa—lakini ni jinsi gani ushindi huu unaonekana ndani yenu? Baadhi ya watu wanasema, “Ushindi Wangu ni neema kuu na kuinuliwa kwa Mungu. Ni sasa tu ndipo ninapotambua kwamba maisha ya mwanadamu ni bure na yasiyo na maana. Mwanadamu hutumia maisha yake kukimbia huku na kule, kuzalisha na kuongeza kizazi baada ya kizazi cha watoto, na hatimaye huwachwa bila chochote. Leo, baada tu ya kushindwa na Mungu ndio nimeona kwamba hakuna thamani ya kuishi kwa njia hii; kwa kweli ni maisha yasiyo na maana. Afadhali nife na kuyasahau haya!” Je, watu kama hao ambao wameshindwa wanaweza kukombolewa na Mungu? Je, wanaweza kuwa vielelezo na mifano? Watu kama hao ni somo katika kutoshughulika, hawana matarajio, na wala kujitahidi kujiboresha wenyewe! Ingawa wao huhesabiwa kama walioshindwa na Mungu, watu kama hao wasioshughulika hawawezi kufanywa wakamilifu. Karibu mwishoni mwa maisha yake, baada ya yeye kufanywa kuwa mkamilifu, Petro akasema, “Ee Mungu! Kama ningeweza kuishi miaka michache zaidi ya hapa, ningependa kufikia usafi zaidi na upendo wa ndani Kwako.” Alipokuwa karibu kusulubiwa, katika moyo wake akaomba, “Ee Mungu! Wakati Wako umewadia, wakati ulionitayarishia umefika. Mimi lazima nisulubiwe kwa ajili Yako, lazima niwe na ushuhuda huu Kwako, na ninatumai kwamba upendo wangu utaweza kukidhi mahitaji Yako, na kwamba unaweza kuwa safi zaidi. Leo, kuwa na uwezo wa kufa kwa ajili Yako, na kusulubiwa kwa ajili Yako, ni faraja na ya kutia moyo kwangu, kwa maana hakuna kinachonifurahisha kuliko kuweza kusulubiwa kwa ajili Yako na kukidhi matakwa Yako, na kuweza kujitoa Kwako, kutoa maisha yangu Kwako. Ee Mungu! Wewe ni wa kupendeza kweli! Kama Ungeniruhusu niishi, ningenuia kukupenda zaidi. Mradi tu ninaishi, mimi nitakupenda. Natamani kukupenda kwa undani zaidi. Unanihukumu, Unaniadibu, na kunijaribu kwa sababu mimi si mwenye haki, kwa sababu nimetenda dhambi. Na tabia Yako ya haki inakuwa dhahiri zaidi kwangu. Hii ni baraka kwangu, kwa maana ninapata uwezo wa kukupenda kwa undani zaidi, na mimi niko tayari kukupenda kwa njia hii hata kama Hunipendi. Mimi niko tayari kutazama tabia Yako ya haki, kwa maana inafanya niweze kuishi maisha ya maana zaidi. Mimi ninahisi kwamba maisha yangu sasa ni ya maana zaidi, kwa maana nimesulubiwa kwa ajili Yako, na ni jambo la maana kufa kwa ajili Yako. Hata hivyo bado mimi sijaridhika, kwa maana najua kidogo sana kukuhusu, najua kwamba siwezi kutimiza matakwa Yako kikamilifu, na kuwa nimekulipa kidogo mno. Katika maisha yangu, sijaweza kurudisha nafsi yangu Kwako kikamilifu; Niko mbali sana na hili. Nikitazama nyuma kwa wakati huu, mimi huhisi kuwa nina mzigo mkubwa wa madeni kwako, na sina muda mwingine ila huu kwa ajili ya kurekebisha makosa yangu na upendo wote ambao sijakulipa Wewe.”

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 524)

Mwanadamu lazima azingatie kuishi kwa kudhihirisha maisha ya maana, na hapaswi kuridhika na hali yake ya sasa. Kuishi kama mfano wa Petro, lazima awe na maarifa na uzoefu wa Petro. Mtu lazima ashikilie mambo ambayo ni ya juu na zaidi ya yaliyo makuu. Ni lazima yeye afuatilie kwa ndani zaidi, usafi zaidi wa upendo wa Mungu, na maisha ambayo yana thamani na umuhimu. Haya tu ndiyo maisha; hivi tu ndivyo mwanadamu atakuwa sawa na Petro. Lazima kuzingatia kuwa makini kwa kuingia kwako kwa upande mwema, na lazima uhakikishe kwamba haurudi nyuma kwa ajili ya urahisi wa kitambo na kupuuza mambo mengine makubwa, zaidi maalum, na zaidi kwa ukweli wa vitendo. Upendo wako lazima uwe wa vitendo, na lazima utafute njia ya kujitoa katika upotovu huu, maisha yasiyo na kujali ambayo hayana tofauti na ya mnyama. Lazima uishi maisha ya maana, maisha ya thamani, na usijipumbaze, au kufanya maisha yako kama kitu cha kuchezea. Kwa kila mtu ambaye anatumai kumpenda Mungu, hakuna ukweli usioweza kupatikana, na hakuna haki wasioweza kusimama imara nayo. Unafaa kuishije maisha Yako? Unapaswa kumpenda Mungu vipi na kutumia upendo huu ili kukidhi hamu Yake? Hakuna kubwa zaidi katika maisha Yako. Zaidi ya yote, lazima uwe na matarajio hayo na uvumilivu, na hupaswi kuwa kama wanyonge wasio na nia. Lazima ujifunze jinsi ya kupitia maisha ya maana, na kuuona ukweli wa maana, na hupaswi kujichukua kipurukushani katika njia hiyo. Bila wewe kujua, maisha Yako yatakupita tu; na baada ya hapo, je utakuwa una fursa nyingine ya kumpenda Mungu? Je, mwanadamu anaweza kumpenda Mungu baada ya kufa? Lazima uwe na matarajio na dhamiri sawa na ya Petro; maisha Yako ni lazima yawe na maana, na usifanye mchezo na nafsi yako. Kama mwanadamu, na kama mtu ambaye anamfuata Mungu, ni lazima uweze kufikiria kwa makini jinsi unavyoendesha maisha yako, jinsi unapaswa kujitoa mwenyewe kwa Mungu, jinsi unapaswa kuwa na imani yenye maana zaidi katika Mungu, na jinsi, kwa kuwa wewe unampenda Mungu, unapaswa kumpenda Yeye kwa njia ambayo ni safi zaidi, nzuri zaidi, na bora zaidi. Leo hii, huwezi tu kuridhika na jinsi wewe umeshindwa, lakini lazima pia uzingatie njia ambayo utatembelea siku zijazo. Lazima uwe na matarajio na ujasiri wa kufanywa mkamilifu, na hupaswi daima kufikiria kwamba huwezi. Je, ukweli una maonevu? Je, ukweli huwapinga watu kwa makusudi? Kama wewe utaufuata ukweli, je unaweza kukushinda? Kama wewe utasimama imara kwa ajili ya haki, je utakuangusha chini? Kama ni hamu yako kwa kweli kufuata maisha, je, maisha yanaweza kukuhepa? Kama wewe huna ukweli, si kwamba ukweli unakupuuza, lakini ni kwa sababu wewe unakaa mbali na ukweli; kama huwezi kusimama imara kwa ajili ya haki, hiyo si kwa sababu kuna kitu kibaya na haki, lakini ni kwa sababu unaamini kuwa ni kinyume na ukweli; kama hujapata maisha baada ya kuyatafuta kwa miaka mingi, si kwa sababu maisha hayana dhamira kwako, bali ni kwa sababu wewe huna dhamira kwa maisha, na kuwa umeyafukuzilia mbali maisha; Iwapo unaishi katika mwanga, na hujaweza kuupata mwanga, hiyo siyo kwa sababu mwanga hauwezi kukuangazia, lakini kwa sababu wewe hujaweka makini kwa kuwepo kwa mwanga, na hivyo mwanga umeondoka kwa kimya. Kama huwezi kufuata, basi inaweza kusemwa kwamba wewe ni taka usiye na maana, na huna ujasiri katika maisha yako, na huna roho ya kupinga nguvu za giza. Wewe ni mdhaifu mno! Huwezi kutoroka nguvu za Shetani ambazo zimekuzingira, na kuwa uko tayari tu kuishi haya maisha ya usalama na kufa katika ujinga. Kile unachopaswa kufanya ni kutekeleza azma yako ya kuwa mshinde; huu ni wajibu wako uliokushikilia. Kama wewe umeridhika na kushindwa, basi unafukuza kuwepo kwa mwanga. Lazima uvumilie mateso kwa ajili ya ukweli, lazima ujitoe kwa ajili ya ukweli, lazima uvumilie udhalilishaji kwa ajili ya ukweli, na kupata ukweli zaidi lazima upate mateso zaidi. Hili ndilo unalopaswa kufanya. Msitupilie mbali ukweli kwa ajili ya maisha ya amani ya familia, na lazima msiipoteze heshima na uadilifu wa maisha kwa ajili ya starehe ya muda mfupi. Unapaswa kufuata yote ambayo ni ya kupendeza na mema, na unapaswa kufuatilia njia katika maisha ambayo ni ya maana zaidi. Kama wewe unaishi maisha ya kishenzi, na wala hufuati malengo yoyote, je, si huko ni kupoteza maisha Yako? Ni nini unachoweza kupata kutoka kwa maisha ya aina hii? Unapaswa kuziacha starehe zote za mwili kwa ajili ya ukweli mmoja, na hupaswi kutupilia mbali ukweli wote kwa ajili ya starehe ya muda mfupi. Watu kama hawa hawana uadilifu au heshima; hakuna maana ya kuwepo kwao!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 525)

Mungu humuadibu na kumhukumu mwanadamu kwa sababu inatakiwa vile na kazi Yake, na zaidi ya hayo, kwa sababu yanahitajika na mwanadamu. Mwanadamu anahitaji kuadibiwa na kuhukumiwa, na ni vile tu ndivyo anaweza kufikia upendo wa Mungu. Leo, mmeshawishiwa kikamilifu, lakini wakati mnapokutana na kizingiti kidogo mtakuwa mashakani; kimo chenu bado ni kidogo mno, na nyinyi bado mnahitaji kupata adabu na hukumu hiyo zaidi ili mfikie ufahamu zaidi. Leo, mna heshima kidogo kwa Mungu, na mnamcha Mungu, na mnajua Yeye ni Mungu wa kweli, lakini hamna upendo mkubwa wa Kwake, na bado hamjafikia upendo safi; maarifa yenu ni ya juujuu, na kimo chenu bado hakitoshi. Wakati nyinyi mnapatana na mazingira, bado hamjashuhudia, sehemu ndogo ya kuingia kwenu ndiyo makini, na nyinyi hamjui jinsi ya kufanya mazoezi. Watu wengi ni watazamaji tu na si watendaji; wao humpenda Mungu tu kwa siri katika nyoyo zao, lakini hawana njia ya mazoezi, wala hawafahamu vizuri malengo yao ni nini. Wale ambao wamefanywa wakamilifu hawana tu ubinadamu wa kawaida, lakini wanao ukweli unaozidi vipimo vya dhamiri, na kwamba ni kuu zaidi kuliko viwango ya dhamiri; wao hawatumii tu dhamiri yao kulipia upendo wa Mungu, lakini, zaidi ya hayo, wanajua Mungu, na wameona kwamba Mungu ni mzuri, na Anastahili upendo wa mtu, na kwamba kuna mambo mengi ya upendo katika Mungu ambayo mtu hana budi ila kumpenda Mungu. Upendo kwa Mungu wa wale ambao wamekuwa wakamilifu ni kwa ajili ya kutimiza matarajio yao binafsi. Upendo wao ni wa papo hapo, upendo usiouliza chochote, na usio wa kubadilisha na kitu. Wanampenda Mungu kwa sababu ya ufahamu wao Kwake, na sio kwa sababu nyingine. Watu kama hawa hawajali kama Mungu anawapa neema au la, wanaridhishwa na kumridhisha Mungu. Hawabishani na Mungu wapate kitu kwa badala yake, wala kupima upendo wao kwa Mungu na dhamiri: Umenipa, kwa hivyo nitakupenda kwa badala yake; kama Wewe Hunipi, basi sina chochote cha kukupa kwa badala yake. Wale ambao wamekuwa wakamilifu daima huamini kwamba: Mungu ni Muumba, na Yeye hufanya kazi Yake juu yetu. Kwa vile nina fursa hii, hali, na uwezo wa kufanywa kamili, azma yangu inafaa kuwa kuishi kwa kudhihirisha maisha yaliyo na maana, na ninapaswa kumridhisha Yeye. Ni kama yale aliyopitia Petro: Alipokuwa katika hatua ya udhaifu, alisali kwa Mungu na kusema, “Ee Mungu! Bila kujali wakati au mahali, Unajua kuwa mimi daima hukukumbuka. Haijalishi wakati au mahali, Unajua kuwa mimi nataka kukupenda, lakini kimo changu ni kidogo mno, mimi ni mdhaifu mno na sina nguvu, upendo wangu ni mdogo sana, na uaminifu wangu kwako pia mdogo. Ikilinganishwa na upendo Wako, mimi sifai kuishi. Natamani tu kwamba maisha yangu yasiwe bure, na kwamba nisiweze tu kulipa upendo wako, lakini, kwamba niweze kukukabidhi vyote nilivyo navyo. Kama naweza kukuridhisha, basi kama kiumbe, mimi nitakuwa na amani moyoni, na sitauliza chochote zaidi. Ingawa mimi ni mdhaifu na asiye na nguvu sasa, siwezi kusahau ushauri Wako, na siwezi kusahau upendo Wako. Sasa sifanyi kitu chochote zaidi ya kulipa upendo wako. Ee Mungu, ninahisi kuwa mbaya! Ninawezaje kukupa upendo ulio moyoni mwangu, nitafanyaje yote ninayoweza, na niwe na uwezo wa kutimiza matakwa Yako, na kuwa na uwezo wa kukupa kila nilicho nacho? Unajua udhaifu wa mwanadamu; ninawezaje kuustahili upendo wako? Ee Mungu! Unajua mimi ni wa kimo kidogo, kwamba upendo wangu pia ni mdogo. Jinsi gani niweze kufanya jinsi niwezavyo katika aina hii ya mazingira? Ninajua napaswa kuulipa upendo Wako, najua kwamba napaswa kutoa yote niliyo nayo Kwako, lakini leo kimo changu ni kidogo mno. Naomba kwamba Wewe Unipe nguvu, na kunipa ujasiri, ili niweze kuwa na upendo safi zaidi na kujitoa kwa ajili Yako, na niweze kutoa yote niliyo nayo Kwako; sitaweza kuulipa upendo Wako tu, lakini zaidi nitaweza kupitia adabu Yako, hukumu na majaribu, na hata laana kali zaidi. Umeniruhusu kutazama upendo wako, na sina uwezo wa kutokukupenda Wewe, na ingawa mimi ni mdhaifu na asiye na nguvu leo, inawezekanaje nikusahau Wewe? Upendo wako, adabu na hukumu imenisababisha mimi kujua Wewe, lakini nahisi sina uwezo wa kutimiza upendo Wako kwa hakika, kwa maana Wewe ni Mkuu zaidi. Nitawezaje kutoa yote niliyo nayo kwa Muumba?” Hilo ndilo lilikuwa ombi la Petro, ilhali kimo chake kilikuwa duni. Wakati huu, alijisikia kama kisu kilikuwa kinasukumwa katika moyo wake na alikuwa katika maumivu makali; hakujua cha kufanya katika hali hiyo. Hata hivyo bado aliendelea kuomba: “Ee Mungu! Mwanadamu ni wa kimo cha kitoto, dhamiri yake ni dhaifu, na kitu tu naweza kufikia ni kurejesha upendo Wako. Leo, mimi sijui jinsi ya kukidhi matamanio Yako, na ningependa tu kufanya yote ninayoweza, kutoa yote niliyo nayo, na kukukabidhi Wewe yote niliyo nayo. Licha ya Hukumu Yako, licha ya adabu Yako, licha ya yote uliyonipa, licha ya yale Unachukua kutoka kwangu, Niokoe kutokana na aina yoyote ya lalamiko Kwako kutoka kwangu. Mara nyingi, wakati uliniadibu na kunihukumu, nilijinung’unikia, na sikuwa na uwezo wa kufikia usafi, au wa kutimiza matakwa Yako. Ulipaji wangu wa upendo Wako ulizaliwa kutokana na lazima, na katika wakati huu najichukia hata zaidi.” Ilikuwa ni kwa sababu yeye alitaka upendo safi zaidi wa Mungu kwamba Petro aliomba kwa njia hii. Alikuwa akitafuta, na kumwomba, na, zaidi ya hayo, alikuwa akiishtaki nafsi yake, na kukiri dhambi zake kwa Mungu. Alijisikia mdeni kwa Mungu, na aliichukia nafsi yake, ilhali alikuwa pia kwa kiasi fulani mwenye huzuni na asiyeshughulika. Yeye daima aliona hivyo, kama kwamba hakuwa mzuri wa kutosha kwa ajili ya matakwa ya Mungu, na kuwa hakuweza kufanya bora zaidi. Katika hali kama hiyo, Petro bado alifuata imani ya Ayubu. Aliona jinsi imani ya Ayubu ilivyokuwa kubwa, kwa maana Ayubu aliona kwamba yote yalifanywa na Mungu, na ilikuwa ni ya asili ya Mungu kuchukua kila kitu kutoka kwake, na kwamba Mungu angempa yeyote ambaye Angependa kumpa—hivyo ndivyo ilivyokuwa tabia ya haki ya Mungu. Ayubu hakuwa na malalamiko, na bado aliweza kumtukuza Mungu. Petro pia alijua mwenyewe, na katika moyo wake akaomba, “Leo mimi siwezi kuridhika na kulipa upendo Wako kwa kutumia dhamiri yangu na kwa upendo wowote ninaokupa, kwa sababu mawazo yangu yamepotoshwa sana, na kwa sababu mimi sina uwezo wa kukuona Wewe kama Muumba. Kwa sababu mimi bado sifai kukupenda, lazima kukamilisha uwezo wa kutoa yote niliyonayo Kwako, na hivyo nitafanya kwa hiari. Ni lazima nijue yote Uliyofanya, na sina budi, na mimi lazima nitazame upendo Wako, na kuwa na uwezo wa kusema sifa Zako, na kutaja jina lako takatifu, ili Uweze kupata utukufu mwingi kupitia kwangu. Mimi niko tayari kusimama imara katika ushuhuda huu Kwako. Ee Mungu! Upendo wako ni wenye thamani na wa kupendeza; jinsi gani mimi ningetaka kuishi katika mikono ya yule mwovu? Je, mimi sikuumbwa na Wewe? Ningewezaje kuishi chini ya miliki ya Shetani? Ningependa nafsi yangu nzima iishi chini ya adabu Yako. Sitaki kuishi chini ya miliki ya yule mwovu. Kama mimi ninaweza kutakaswa, na ninaweza kutoa yote niliyonayo Kwako, mimi niko tayari kutoa mwili wangu na akili kwa hukumu na adabu Yako, kwa maana mimi nachukizwa na Shetani, na sina nia ya kuishi chini ya uwanja wake. Kupitia hukumu Yako kwangu, umenionyesha tabia Yako ya haki; Nina furaha, na sina malalamiko hata kidogo. Kama mimi nina uwezo wa kutekeleza jukumu la kiumbe, mimi niko tayari kuwa maisha yangu yote yaambatane na hukumu Yako, kwa njia ambayo mimi nitapata kujua tabia Yako ya haki, na kujiondolea ushawishi wa yule mwovu.” Petro aliomba hivyo kila mara, na daima alitafuta hivyo, na aliufikia ulimwengu wa juu, kwa ulinganisho. Hakuweza tu kuulipa upendo wa Mungu, lakini, la muhimu zaidi, yeye alitimiza wajibu wake kama kiumbe. Hakutuhumiwa tu na dhamiri yake, lakini alikuwa pia na uwezo wa kuvuka viwango vya dhamiri. Maombi yake yaliendelea kwenda mbele za Mungu, hivyo kwamba matarajio yake yalikuwa milele juu, na upendo wake kwa Mungu ulikuwa milele mkuu. Ingawa yeye alipitia maumivu makali, bado hakusahau kumpenda Mungu, na bado alitaka kufikia uwezo wa kuelewa mapenzi ya Mungu. Kwa maombi yake yalitamkwa maneno yafuatayo: Sijatimiza chochote zaidi ya ulipaji wa upendo wako. Sijatoa ushuhuda Kwako mbele ya Shetani, sijajiweka huru mwenyewe kutokana na ushawishi wa Shetani, na bado naishi miongoni mwa umbo la mwili. Ningependa kutumia upendo wangu kumshinda shetani, na kumwaibisha, na hivyo kuridhisha hamu Yako. Ningependa kujitoa mzima Kwako, nisijitoe hata kidogo kwa Shetani, kwani Shetani ni adui Wako. Zaidi ya alivyoendelea kwa njia hii, ndivyo alivyozidi kusongeshwa, na ndivyo ujuzi wake wa mambo haya ulivyozidi kukua. Bila kujua, alitambua kwamba anapaswa kujikwamua kutokana na ushawishi wa Shetani, na kujirudisha mwenyewe kabisa kwa Mungu. Huo ndio ulimwengu alioufikia. Alikuwa anauzidi kwa mbali ushawishi wa Shetani, na kujitoa mwenyewe kwenye raha na starehe za mwili, na alikuwa tayari kupitia kwa kina zaidi adabu zote na hukumu ya Mungu. Alisema, “Hata ingawa ninaishi katika adabu Yako, na huku kukiwa na hukumu Yako, bila kujali ugumu unaohusiana na maisha, bado mimi sina nia ya kuishi chini ya miliki ya Shetani, sina nia ya kuteseka na hila za Shetani. Mimi nina furaha kuishi kwenye laana Yako, na ninapata uchungu kwa kuishi katika baraka za shetani. Nakupenda kwa kuishi katika hukumu Yako, na hii huniletea furaha kuu. Adabu Yako na hukumu ni yenye uadilifu na takatifu; ni vyema ukinitakasa, na hata zaidi kuniokoa. Ninapenda niishi maisha yangu yote katika hukumu Yako na kuwa chini ya uchungaji Wako. Sina nia ya kuishi chini ya mamlaka ya Shetani hata kwa dakika moja; Napenda kutakaswa na Wewe; hata kama ninapitia taabu, sina nia ya kutumiwa na kuhadaiwa na shetani. Mimi, kiumbe hiki, nafaa nitumike na Wewe, nijazwe na Wewe, nihukumiwe na Wewe, na kuadibiwa na Wewe. Nafaa hata nipokee laana kutoka Kwako. Moyo wangu hufurahi wakati Uko tayari kunibariki, kwa maana nimeona upendo Wako. Wewe ni Muumba, na mimi ni kiumbe: Sifai kukusaliti Wewe na kuishi chini ya himaya ya Shetani, wala sifai kutumiwa na Shetani. Mimi nafaa kuwa farasi wako, au ng’ombe, badala ya kuishi kwa ajili ya Shetani. Afadhali niishi katika adabu Yako, bila neema ya kimwili, na hii itanipa raha na starehe hata kama ningepoteza neema Yako. Ingawa neema Yako haiko nami, mimi nafurahia kuadibiwa na kuhukumiwa na Wewe; Hii ndiyo baraka Yako nzuri zaidi, neema Yako kuu. Ingawa Wewe daima ni Mkuu na mwenye ghadhabu kwangu, bado mimi siwezi kukuacha, bado sina uwezo wa kukupenda vya kutosha. Ningependelea kuishi katika nyumba Yako, Ningependa kulaaniwa, kuadibiwa, na kuchapwa na Wewe, na sina nia ya kuishi chini ya himaya ya Shetani, wala mimi sina nia ya kukimbilia na kushughulika kwa ajili ya mwili tu, zaidi ya hayo siko tayari kuishi kwa ajili ya mwili.” Upendo wa Petro ulikuwa upendo safi. Huu ni ujuzi wa kufanywa mkamilifu, na ni ulimwengu wa juu wa kufanywa mkamilifu, na hakuna maisha yaliyo na maana zaidi ya haya. Alikubali adabu ya Mungu na hukumu, aliipenda tabia ya Mungu ya haki, na hakuna jambo kuhusu Petro lililokuwa la thamani zaidi ya hili. Alisema, “Shetani ananipa starehe za mwili, lakini mimi sithamini hayo. Adabu ya Mungu na hukumu inakuja juu yangu—na katika hili mimi nimeneemeka, katika hili mimi ninapata starehe, na katika hili mimi nimebarikiwa. Kama si kwa hukumu Yake, mimi singeweza kumpenda Mungu, bado ningeishi chini ya himaya ya Shetani, bado ningedhibitiwa nayo, na ningekuwa naamuriwa nayo. Kama ingekuwa vile, singewahi kuwa binadamu wa kweli, kwa maana singeweza kumtosheleza Mungu, na singejitoa kikamilifu kwa Mungu. Japokuwa Mungu Hanibariki, na kuniacha bila faraja ndani yangu, kana kwamba moto mkuu unachoma ndani yangu, na hakuna amani au furaha, na hata ingawa adabu na nidhamu ya Mungu kamwe iko na mimi, katika adabu ya Mungu na hukumu ninao uwezo wa kuona tabia Yake ya haki. Mimi hupata furaha katika hili; hakuna kitu cha thamani zaidi au cha maana zaidi ya hili katika maisha. Ingawa ulinzi Wake na huduma vimekuwa adabu kali, hukumu, laana na mipigo, bado mimi hupata starehe katika mambo haya, kwani yanaweza kunitakasa bora zaidi na kunibadilisha, yanaweza kunileta karibu na Mungu zaidi, yanaweza kufanya niweze kumpenda Mungu zaidi, na yanaweza kufanya upendo wangu kwa Mungu uwe safi zaidi. Hii inanifanya niwe na uwezo wa kutimiza wajibu wangu kama kiumbe, na inanichukua mbele za Mungu na kuniweka mbali na ushawishi wa Shetani, ili nisije tena nikamtumikia Shetani. Wakati siishi chini ya himaya ya Shetani, na ninaweza kutoa kila kitu nilicho nacho na kile ninachoweza kwa ajili ya Mungu, bila kubakisha chochote—hapo ndipo nitakuwa nimeridhika kikamilifu. Ni adabu ya Mungu na hukumu Yake ndiyo iliyoniokoa, na maisha yangu hayawezi kutengwa kutoka kwenye adabu na hukumu ya Mungu. Maisha yangu hapa duniani yamo chini ya himaya ya Shetani, na isingekuwa huduma na ulinzi na adabu ya Mungu na hukumu Yake, ningeliishi daima chini ya himaya ya Shetani, na, zaidi ya hayo, singekuwa na nafasi au njia ya kuishi kwa kudhihirisha maisha yenye maana. Ni wakati tu ambapo adabu ya Mungu na hukumu kamwe hainiachi, ndio nitakapokuwa na uwezo wa kutakaswa na Mungu. Ni kwa maneno makali na tabia ya haki ya Mungu, na hukumu kuu ya Mungu, ndipo nimepata ulinzi mkuu, na kuishi katika mwanga, na kupokea baraka za Mungu. Kuwa na uwezo wa kutakaswa, na kujiweka huru kutokana na Shetani, na kuishi chini ya utawala wa Mungu—hii ndiyo baraka kubwa zaidi katika maisha yangu leo.” Huu ndio ulimwengu wa juu zaidi aliopitia Petro.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 526)

Mwanadamu anaishi katika mwili, ambayo ina maana anaishi katika kuzimu ya binadamu, na bila hukumu na adabu ya Mungu, mwanadamu ni mchafu kama Shetani. Mwanadamu atawezaje kuwa mtakatifu? Petro aliamini kwamba adabu na hukumu ya Mungu ndio uliokuwa ulinzi bora zaidi wa mwanadamu na neema kubwa. Ni kwa njia ya adabu na hukumu ya Mungu ndipo mwanadamu angeweza kugutuka, na kuchukia mwili, na kumchukia Shetani. Nidhamu kali ya Mungu inamweka huru kutokana na ushawishi wa Shetani, inamweka huru kutokana na dunia yake ndogo, na inamruhusu kuishi katika mwanga wa uwepo wa Mungu. Hakuna wokovu bora zaidi kuliko adabu na hukumu! Petro aliomba, “Ee Mungu! Mradi tu Wewe unaniadibu na kunihukumu, nitajua kwamba Wewe hujaniacha. Hata kama Huwezi kunipa furaha au amani, na kufanya niishi katika mateso, na kunirudi mara nyingi, bora tu Hutaniacha moyo wangu utakuwa na amani. Leo hii, adabu Yako na hukumu umekuwa ulinzi wangu bora na baraka yangu kubwa. Neema unayonipa inanilinda. Neema unayoweka juu yangu leo ni kielelezo cha tabia Yako ya haki, na ni adabu na hukumu; zaidi ya hayo, ni majaribu, na, zaidi ya hapo, ni maisha ya mateso.” Petro alikuwa na uwezo wa kuweka kando raha ya mwili na kutafuta mapenzi zaidi na ulinzi zaidi, kwa sababu alikuwa amepata neema nyingi kutoka kwa adabu na hukumu ya Mungu. Katika maisha yake, kama mwanadamu anatamani kutakaswa na kufikia mabadiliko katika tabia yake, kama anatamani kuishi kwa kudhihirisha maisha yenye maana, na kutimiza wajibu wake kama kiumbe, basi lazima akubali adabu na hukumu ya Mungu, na lazima asiruhusu nidhamu ya Mungu na kipigo cha Mungu kiondoke kwake, ili aweze kujiweka huru kutokana na kutawalwa na ushawishi wa Shetani na kuishi katika mwanga wa Mungu. Ujue kwamba adabu ya Mungu na hukumu ni mwanga, na mwanga wa wokovu wa mwanadamu, na kwamba hakuna baraka bora zaidi, neema au ulinzi bora kwa ajili ya mwanadamu. Mwanadamu anaishi chini ya ushawishi wa Shetani, na yupo katika mwili; kama yeye hatatakaswa na kupokea ulinzi wa Mungu, basi mwanadamu atakuwa milele mpotovu zaidi. Kama yeye anataka kumpenda Mungu, basi lazima atakaswe na kuokolewa. Petro aliomba, “Mungu, wakati Unanitendea wema ninapata furaha, na kuhisi faraja; wakati unaniadibu, najisikia faraja kubwa zaidi na furaha. Ingawa mimi ni mdhaifu, na kuvumilia mateso yasiyotajika, ingawa kuna machozi na huzuni, Unajua kwamba huzuni huu ni kwa sababu ya kutotii kwangu, na kwa sababu ya udhaifu wangu. Mimi ninalia kwa sababu siwezi kukidhi hamu Yako, nahisi huzuni na majuto kwa sababu mimi sitoshi kwa mahitaji Yako, lakini niko tayari kufikia ulimwengu huu, niko tayari kufanya yote niwezayo ili nikuridhishe. Adabu Yako imeniletea ulinzi, na kunipa wokovu bora; hukumu Yako inazidi ustahimili Wako na uvumilivu Wako. Bila adabu Yako na hukumu, singefurahia huruma Yako na rehema. Leo, naona zaidi kwamba upendo wako umepita mipaka ya mbinguni na kuwa bora ya yote. Upendo wako sio tu huruma na fadhili; hata zaidi ya hayo, ni adabu na hukumu. Adabu Yako na hukumu imenipa mengi. Bila adabu Yako na hukumu, hakuna hata mmoja angetakaswa, na hakuna hata mmoja angeweza kupata upendo wa Muumba. Ingawa nimevumilia mamia ya majaribio na mateso, na hata nimekuwa karibu na kifo, haya yameniruhusu kukujua Wewe kwa kweli na kupata wokovu mkuu. Kama adabu Yako, hukumu na nidhamu vingeondoka kutoka kwangu, basi ningeishi gizani, chini ya himaya ya Shetani. Mwili wa binadamu una faida gani? Kama adabu Yako na hukumu ingeniwacha, ingekuwa kana kwamba Roho Wako alikuwa ameniacha, ni kama Wewe Haukuwa tena pamoja nami. Kama ingekuwa vile, ni jinsi gani ningeendelea kuishi? Kama Wewe utanipa ugonjwa, na kuchukua uhuru wangu, naweza kuendelea kuishi, lakini adabu Yako na hukumu vikiondoka kutoka kwangu, sitakuwa na njia ya kuendelea kuishi. Kama ningekuwa bila adabu Yako na hukumu, ningepoteza upendo Wako, upendo ambao ni mkuu sana mpaka sina maneno ya kuueleza. Bila Upendo wako, ningeishi chini ya miliki ya Shetani, na singeweza kuuona uso wako mtukufu. Ningewezaje kuendelea kuishi? Giza kama hili, maisha kama haya, singeweza kuvumilia. Mimi kuwa na wewe ni kama kukuona Wewe, hivyo ni jinsi gani ningeweza kukuacha? Ninakusihi, nakuomba usichukue faraja yangu kubwa kutoka kwangu, hata kama ni maneno machache tu ya uhakikisho. Nimefurahia upendo wako, na leo hii siwezi kuwa mbali na Wewe; ningewezaje kutokupenda Wewe? Nimemwaga machozi mengi ya huzuni kwa sababu ya upendo Wako, ilhali daima nimehisi kuwa maisha kama haya ni ya maana zaidi, yenye uwezo mwingi wa kuniimarisha, yenye uwezo zaidi wa kunibadilisha, na yenye uwezo zaidi wa kunifanya nifikie ukweli ambao lazima viumbe wawe nao.”

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 527)

Maisha yote ya mwanadamu yamekuwa chini ya himaya ya Shetani, na hakuna mtu yeyote anayeweza kujitoa kutoka katika ushawishi wa Shetani yeye mwenyewe. Wote wanaishi katika dunia chafu, kwa upotovu na utupu, bila maana yoyote au thamani; wanaishi maisha ya kutojali kwa ajili ya mwili, tamaa, na kwa ajili ya Shetani. Hakuna maana yoyote kwa kuwepo kwao. Mwanadamu hana uwezo wa kupata ukweli utakaomweka huru kutoka kwa ushawishi wa Shetani. Ingawa mwanadamu anaamini katika Mungu na anasoma Biblia haelewi jinsi ya kujitoa kutoka kwa ushawishi wa Shetani. Kutoka kitambo, watu wachache sana wametambua siri hii, wachache sana wameielewa. Hivyo, hata kama mwanadamu anamchukia Shetani, na anachukia mwili, hajui jinsi ya kujitoa kutoka kwa ushawishi mkuu wa Shetani. Je, leo bado hamjamilikiwa na Shetani? Hamjuti juu ya matendo yenu ya uasi, zaidi ya hayo, hamhisi kama wachafu na waasi. Baada ya kumpinga Mungu, bado mna amani ya moyo na mnahisi utulivu mwingi. Je, utulivu wako si kwa sababu wewe ni mpotovu? Je, hii amani ya mawazo haitokani na kuasi kwako? Mwanadamu anaishi katika jehanamu ya binadamu, anaishi katika ushawishi wa giza la Shetani; mkabala katika ardhi, mapepo yanaishi na mwanadamu, yakienea katika mwili wa mwanadamu. Duniani, hauishi katika Paradiso ya kupendeza. Mahali ambapo ulipo ni ulimwengu wa Shetani, jehanamu ya binadamu, dunia ya chini. Mwanadamu asipotakaswa, basi yeye ni wa uchafu; asipolindwa na kutunzwa na Mungu, basi yeye bado ni mfungwa wa Shetani; asipohukumiwa na kuadibiwa, basi hatakuwa na njia ya kuepuka ukandamizaji na ushawishi mbaya wa Shetani. Tabia potovu unayoonyesha, na tabia ya uasi unayoishi kwa kudhihirisha inatosha kuonyesha kwamba bado unaishi katika himaya ya Shetani. Kama akili na mawazo yako hayajatakaswa, na tabia yako haijahukumiwa na kuadibiwa, basi nafsi yako yote bado inadhibitiwa na himaya ya Shetani, akili yako bado inadhibitiwa na Shetani, mawazo yako yanatawaliwa na Shetani, na nafsi yako yote inadhibitiwa na mikono ya Shetani. Je, unajua uko umbali gani, sasa, na viwango alivyokuwa navyo Petro? Je, wewe unamiliki kiwango hicho? Ni kiasi gani unajua kuhusu adabu na hukumu ya wakati wa leo? Unacho kiasi gani cha yale Petro alipata kujua? Iwapo, leo, huna uwezo wa kutambua, je utaweza kupata maarifa haya baadaye? Mtu mzembe na mwoga kama wewe hawezi kujua kuhusu adhabu na hukumu. Ukifuata amani ya kimwili, na raha za kimwili, basi hutakuwa na njia yoyote ya kutakaswa, na mwishowe utarudishwa kwa Shetani, kwa sababu hali unayoishi kwa kudhihirisha ni ya Shetani, na ya mwili. Vitu vilivyo sasa, watu wengi hawayafuati maisha, kwa hivyo inamaanisha kuwa hawajali kuhusu kutakaswa, ama kuingia katika uzoefu wa ndani ya maisha. Je, watawezaje kufanywa kuwa wakamilifu? Wale wasiofuata maisha hawana fursa ya kufanywa wakamilifu, na wale wasiofuata maarifa ya Mungu, na hawafuati mabadiliko katika tabia zao, hawataweza kuepuka ushawishi wa giza wa Shetani. Kwa kuashiria maarifa yao kuhusu Mungu na kuingia kwao katika mabadiliko ya tabia zao, hawana umakini kuzihusu, kama wale wanaoamini katika dini pekee, na wale wanaofuata tu sherehe na kuhudhuria huduma za kawaida. Je, hiyo si kupoteza wakati? Kama, kwa imani yake kwa Mungu, mwanadamu hayuko makini katika mambo ya maisha, hafuati kuingia katika ukweli, hazingatii mabadiliko katika tabia yake, ama kufuata maarifa ya kazi ya Mungu, basi hawezi kufanywa mkamilifu. Kama unatamani kufanywa mkamilifu, lazima uelewe kazi ya Mungu. Hasa, lazima uelewe umuhimu wa adabu na hukumu Yake, na kwa nini kazi hii inafanywa juu ya mwanadamu. Je, unaweza kukubali? Wakati wa adabu ya aina hii, unaweza kupata uzoefu na maarifa kama Petro? Ukifuata maarifa ya Mungu na ya kazi ya Roho Mtakatifu, na kuzingatia mabadiliko katika tabia yako, basi una fursa ya kufanywa mkamilifu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 528)

Kwa wale ambao wanatakiwa kufanywa wakamilifu, hatua hii ya kazi ya kushinda ni ya lazima; Ni baada ya kushindwa tu ndipo mwanadamu anaweza kuiona kazi ya kufanywa mkamilifu. Hakuna maana kubwa ya kufanya kazi ya kushindwa, ambayo itakufanya usiwe mwenye kufaa kufanya kazi yoyote ya Mungu. Hutakuwa na uwezo wowote wa kufanya kazi yako ya kueneza injili, kwa sababu hufuati maisha, na hujibadilishi na kujifanya mpya, na hivyo basi huna uzoefu kamili wa maisha. Katika kazi hii ya hatua kwa hatua, uliwahi kuwa na nafasi ya mtendaji-huduma, na foili[a], lakini kwa hakika usipofuata kuwa kama Petro, na ufuasi wako sio kama wenye njia ambayo Petro alifanywa mkamilifu, basi, kiasili hutapata mabadiliko katika tabia yako. Kama wewe ni mtu anayefuata kuwa mkamilifu, basi utakuwa na ushuhuda, na utasema: “Katika hii kazi ya hatua kwa hatua ya Mungu, nimekubali kazi ya Mungu ya adabu na hukumu, na hata kama nimepitia mateso mengi, nimepata kujua jinsi Mungu hufanya mwanadamu kuwa mkamilifu, nimepata kazi iliyofanywa na Mungu, nimekuwa na maarifa ya haki ya Mungu, na adabu Yake imeniokoa. Tabia Yake ya haki imekuja juu yangu, na ikaniletea baraka na neema; ni hukumu Yake na adabu ambazo zimenilinda na kunitakasa. Kama singeadibiwa na kuhukumiwa na Mungu, na kama maneno makali ya Mungu hayangekuja juu yangu, singalimjua Mungu, ama kuokolewa. Leo, naona, kama kiumbe, kwamba mtu hafurahii tu vitu vilivyoumbwa na Muumba, lakini pia, la maana sana ni kwamba viumbe vyote watafurahia haki ya tabia ya Mungu, na kufurahia hukumu Yake ya haki, kwa sababu tabia ya Mungu ina umuhimu katika furaha ya Mwanadamu. Kama kiumbe ambaye amepotoshwa na Shetani, kila mmoja anafaa kufurahia tabia ya haki ya Mungu. Katika tabia Yake ya haki, kuna adabu na hukumu, na pia, kuna upendo mkuu. Ingawa sina uwezo wa kupata kwa kikamilifu upendo wote wa Mungu leo, nimekuwa na bahati nzuri ya kuuona, na katika haya, nimebarikiwa.” Hii ndio njia ambayo wale waliofanywa wakamilifu hutembea na maarifa wanayoongelea. Watu hao wanafanana na Petro; wanao uzoefu sawa na wa Petro. Watu kama hao pia ndio wale ambao wamepokea maisha, na walio na ukweli. Wanapokuwa na uzoefu mpaka mwisho kabisa, wakati wa hukumu ya Mungu kwa hakika wataweza kikamilifu kujitoa katika ushawishi wa Shetani, na atakuwa wa Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu

Tanbihi:

a. “Foili” inahusu mtu au kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 529)

Adamu na Hawa waliumbwa na Mungu hapo mwanzo wakiwa watu watakatifu, ni kama kusema, katika bustani ya Edeni, walikuwa watakatifu, wasiokuwa na uchafu. Walikuwa watiifu kwa Yehova, na hawakujua chochote kuhusu kuasi Yehova. Hii ni kwa sababu hawakuwa na kusumbuliwa na ushawishi wa Shetani, hawakuwa na sumu ya Shetani, na walikuwa watu wasafi kati ya binadamu wote. Waliishi katika bustani ya Edeni, bila kutiwa najisi na uchafu wowote, bila kuingiliwa na mwili, na heshima kwa Yehova. Baadaye, walipojaribiwa na Shetani, wakawa na sumu ya nyoka, na tamaa ya kuasi Yehova, na wakaishi chini ya ushawishi wa Shetani. Hapo mwanzo, walikuwa watakatifu na wenye kuheshimu sana Yehova; hivyo tu ndivyo walikuwa binadamu. Baadaye, baada ya kujaribiwa na Shetani, wakala tunda la maarifa ya kujua mazuri na mabaya, na wakaishi chini ya ushawishi wa Shetani. Waliendelea kupotoshwa na Shetani, na wakapoteza sura asili ya mwanadamu. Hapo mwanzo, mwanadamu alikuwa na pumzi ya Yehova, na hakuwa muasi hata kidogo, na hakuwa na uovu wowote katika moyo wake. Wakati huo, mwanadamu alikuwa binadamu wa kweli. Baada ya kupotoshwa na Shetani, mwanadamu akawa mnyama. Fikra zake zikajawa na uovu na uchafu, bila mazuri ama utakatifu. Je, huyu si Shetani? Umepata kujua mengi kuhusu kazi ya Mungu, ilhali haujabadilika wala kutakaswa. Bado unaishi katika himaya ya Shetani, na bado hujajitoa na kunyenyekea kwa Mungu. Huyu ni mtu ambaye ameshindwa lakini hajafanywa mkamilifu. Na mbona inasemekana kuwa mtu kama huyu hajafanywa mkamilifu? Kwa sababu mtu huyu hafuati maisha ama maarifa ya kazi ya Mungu, na hutamani tu raha za kimwili na starehe ya muda mfupi. Na kwa hivyo hakuna mabadiliko katika tabia zao, na hawajapata sura asili ya mwanadamu ilivyoumbwa na Mungu. Watu hao ni maiti zinazotembea, ni waliokufa na hawana roho! Wale wasiofuata maarifa ya mambo katika Roho, wasiofuata utakatifu, na wasiofuata kuishi kulingana na maisha ya ukweli, wanaotosheka na kushindwa kwa upande wa kanusho, na wasioweza kuishi kwa kufuata maneno ya Mungu na kuwa binadamu watakatifu—hawa ni watu ambao hawajaokolewa. Kwani, kama hana ukweli, mwanadamu hataweza kusimama imara katika majaribu ya Mungu; wale watakaoweza kusimama imara katika majaribu ya Mungu pekee ndio wale ambao wameokolewa. Ninalotaka Mimi ni watu kama Petro, watu wanaofuata kufanywa wakamilifu. Ukweli wa leo unatolewa kwa wale ambao wanautamani na kuutafuta. Wokovu huu unapewa wale ambao wanatamani kuokolewa na Mungu, na haujakusudiwa kuwafaidi tu, lakini ili pia ili mpatwe na Mungu. Mnampata Mungu ili Mungu pia awapate. Leo nimenena hayo maneno kwenu, na mmeyasikia, na mnafaa kutenda kulingana na maneno haya. Mwishowe, mkiweka maneno haya katika matendo ndipo nitakapowapata nyinyi kupitia katika maneno haya; na pia, mtakuwa mmepata maneno haya, kumaanisha, mtakuwa mmepata wokovu mkuu. Punde mtakapofanywa wasafi, mtakuwa wanadamu halisi. Kama huwezi kuishi kulingana na ukweli, ama kuishi kulingana na aliyefanywa mkamilifu, basi inaweza kusemwa kuwa wewe si binadamu, ila wewe ni mfu anayetembea, mnyama, kwa sababu huna ukweli, ni kusema huna pumzi ya Yehova, na basi wewe ni mtu aliyekufa ambaye hana roho! Ingawa unaweza kuwa na ushuhuda baada ya kushindwa, unachopata ni wokovu kidogo, na hujakuwa kiumbe chenye roho. Ingawa umepata adabu na hukumu, tabia yako haijafanywa upya ama kubadilishwa kama matokeo; umebaki tu ulivyokuwa, bado wewe ni wa Shetani, na wewe si mtu aliyetakaswa. Wale tu waliofanywa wakamilifu ndio wenye thamani, na watu tu kama hao ndio wamepata maisha ya kweli.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 530)

Leo, watu wengine wanatafuta kutumiwa na Mungu, lakini baada ya kushindwa hawawezi kutumika moja kwa moja. Kwa maneno yaliyonenwa leo, kama, wakati Mungu anapotumia watu, bado huwezi kuyakamilisha, basi hujafanywa mkamilifu. Kwa maneno mengine, kufika kwa mwisho wa wakati ambao mwanadamu anafanywa mkamilifu kutabaini iwapo mwanadamu atatupwa ama atatumiwa na Mungu. Wale walioshindwa ni mifano wa kutojihusisha na uhasi tu; ni sampuli na mifano, lakini si chochote ila ni ujazio wa wimbo. Ni wakati tabia ya maisha ya mwanadamu imebadilika, na amepata mabadiliko ndani na nje, ndipo atakapokuwa amefanywa mkamilifu. Leo, ni nini utakacho, kushindwa ama kufanywa mkamilifu? Ni nini unachotamani kupata? Umetimiza masharti ya kufanywa mkamilifu? Ni yapi ambayo bado unakosa? Unapaswa kujihami vipi, na utaweka mikakati ipi ili kuondoa upungufu wako? Utaingia vipi katika njia ya kufanywa mkamilifu? Utajiwasilisha vipi kikamilifu? Unataka kufanywa mkamilifu, je, unafuata utakatifu? Je, wewe ni mtu anayetaka kupitia hukumu na kuadibu ili uweze kutakaswa? Unatafuta kutakaswa, kwa hivyo una nia ya kukubali adabu na hukumu? Unataka kujua Mungu, lakini je, una maarifa ya adabu na hukumu Yake? Leo, kazi nyingi Anayofanya kwenu ni adabu na hukumu; ufahamu wako wa kazi hii ni upi, ambayo imetekelezwa juu yako? Je, adabu na hukumu ambayo umepitia imekutakasa? Imekubadilisha? Imekuwa na mabadiliko yoyote kwako? Umechoka sana na kazi hii nyingi ya leo—laana, hukumu na ufichuzi—ama unaona mambo haya yakiwa ya manufaa kwako? Unapenda Mungu, lakini kwa nini unampenda Yeye? Je, unampenda Mungu kwa sababu umepokea neema kidogo? Ama unapenda Mungu baada ya kupata amani na furaha? Ama unampenda Mungu baada ya kutakaswa na adabu na hukumu yake? Ni nini hasa kinachokufanya umpende Mungu? Ni masharti yapi ndiyo Petro alikamilisha ili afanywe mkamilifu? Baada ya kufanywa mkamilifu, ni njia gani muhimu ndiyo ilitumiwa kudhihirisha? Je, alimpenda Bwana Yesu kwa sababu alitamani kuwa na Yeye, ama kwa sababu hangeweza kumuona, ama ni kwa sababu alikuwa ameshutumiwa? Ama alimpenda Bwana Yesu zaidi kwa sababu alikubali mateso ya shida, na alikuwa amejua uchafu wake na kuasi, alikuwa amepata kujua utakatifu wa Bwana? Je, mapenzi yake kwa Mungu yalikuwa safi kwa sababu ya adabu na hukumu ya Mungu, ama kwa sababu ya kitu kingine? Ni nini hasa? Unampenda Mungu kwa sababu ya neema ya Mungu, na kwa sababu leo amekupa baraka kidogo. Je, huu ni upendo wa ukweli? Unapaswa kumpenda Mungu vipi? Je, unapaswa kukubali kuadibu na hukumu Yake, na, baada ya kuona tabia Yake yenye haki, uweze kumpenda kwa kweli, hivi kwamba umeshawishika kabisa, na kuwa na maarifa Yake? Kama Petro, unaweza kusema kwamba huwezi kumpenda Mungu vya kutosha? Je, unachofuata kishindwe baada ya adabu na hukumu, ama kutakaswa, kimelindwa na kushughulikiwa baada ya adabu na hukumu? Ni gani kati ya haya unayofuata? Je, maisha yako yana maana ama hayana maana wala dhamani? Unataka mwili ama ukweli? Unataka hukumu, ama faraja? Baada ya kupitia na kuiona kazi nyingi ya Mungu, na baada ya kuuona utakatifu na haki ya Mungu, unafaa kumfuata vipi? Unapaswa kutembea vipi katika njia hii? Utahitajika kuweka mapenzi ya Mungu katika matendo kivipi? Je, adabu na hukumu ya Mungu zimekuwa na athari yoyote kwako? Kama una maarifa ya adabu na hukumu ya Mungu itategemea jinsi unavyoishi kwa kudhihirisha, na kiwango gani unapenda Mungu! Kinywa chako kinasema unampenda Mungu, ilhali unachoishi kwa kudhihirisha ni tabia nzee, zilizo potovu; humchi Mungu, na sembuse kuwa na dhamiri. Je, watu wa aina hii wanampenda Mungu? Je, watu wa aina hii ni waaminifu kwa Mungu? Je, wao ni wale wanaokubali adabu na hukumu ya Mungu? Unasema unampenda na kumwamini Mungu, ilhali huachi hisia zako. Katika kazi yako, kuingia kwako, maneno uzungumzayo, na katika maisha yako, hakuna udhihirisho wa mapenzi yako kwa Mungu, na hakuna heshima kwa Mungu. Je, huyu ni mtu ambaye amepata adabu na hukumu? Mtu kama huyu anaweza kuwa Petro? Wale walio kama Petro wana maarifa, lakini je, wanaishi kulingana nayo? Leo, ni hali gani inahitaji mwanadamu aishi kwa kudhihirisha maisha ya ukweli? Maombi ya Petro hayakuwa maneno matupu yaliyotoka mdomoni mwake? Hayakuwa maneno kutoka moyoni mwake? Petro aliomba tu, na hakuweka ukweli katika matendo? Kufuata kwako ni kwa niaba ya nani? Utajiwezeshaje kupokea ulinzi na utakaso wakati wa hukumu na kuadibu kwa Mungu? Je, adabu na hukumu ya Mungu haina faida yoyote kwa mwanadamu? Je, hukumu yote ni adhabu? Je, amani na furaha, baraka ya vitu vya dunia na faraja, ni muhimu kwa maisha ya mwanadamu? Mwanadamu akiishi katika mazingira mazuri ya raha, bila maisha ya hukumu, anaweza kutakaswa? Iwapo mwanadamu anataka kubadilika na kutakaswa, anafaa kukubali vipi kufanywa mkamilifu? Ni njia gani unayopaswa kuchagua leo?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 531)

Punde tu anapotajwa Petro, kila mtu anajawa na sifa, akikumbushwa mara moja hizi hadithi zote kumhusu Petro—jinsi alikana kumjua Mungu mara tatu na zaidi ya hayo kumhudumia Shetani, na hivyo kumjaribu Mungu, lakini mwishowe alisulubiwa juu chini kwa ajili Yake, na kadhalika. Sasa Naweka umuhimu mkubwa juu ya kukusimulia jinsi Petro alikuja kunijua na pia matokeo yake ya mwisho. Huyu mwanadamu Petro alikuwa wa kimo bora sana, lakini hali yake ilikuwa tofauti na ile ya Paulo. Wazazi wake walinitesa, walikuwa wa mapepo yaliyomilikiwa na Shetani, na kwa sababu hii mtu hawezi kusema kwamba walipitisha njia kwa Petro. Petro alikuwa na busara nyepesi, alipewa akili asili, kupendwa sana kutoka utotoni na wazazi wake; baada ya kukua, hata hivyo, akawa adui zao, kwani daima alitaka kunijua, na hii ilimfanya kuwapuuza wazazi wake. Hii ilikuwa kwa sababu, kwanza kabisa, aliamini kwamba mbingu na dunia na mambo yote yako mikononi mwa Mwenyezi, na kwamba mambo yote mazuri yanatoka kwa Mungu na yanakuja moja kwa moja kutoka Kwake, bila kupitia usindikaji wowote na Shetani. Na mfano usiofaa wa wazazi wake kuwa kama kikwazo, hii ilimwezesha kwa urahisi kutambua upendo na huruma Yangu, na hivyo kuchochea ndani yake hamu kubwa zaidi ya kunitafuta. Alikuwa makini sana sio tu kula na kunywa maneno Yangu, lakini hata zaidi kufahamu nia Zangu, na daima alikuwa na busara na tahadhari katika mawazo yake, kwa hivyo daima alikuwa mwerevu kwa makini ndani ya roho yake, na hivyo aliweza kuniridhisha kwa vyote alivyofanya. Kwa maisha ya kawaida, alikuwa makini kuunganisha katika maisha[a] masomo ya wale walioshindwa katika siku za nyuma ili kujichochea mwenyewe kufanya juhudi kubwa zaidi, akihofia sana kwamba anaweza kuanguka ndani ya nyavu za ushinde. Alikuwa pia makini kupata imani na upendo wa wote ambao kupitia enzi nyingi walikuwa wamempenda Mungu. Kwa njia hii, aliharakisha maendeleo ya ukuaji wake sio tu kwa masuala hasi, lakini hasa kwa masuala chanya, hadi akawa katika uwepo Wangu mwanadamu pekee aliyenijua bora kabisa. Kwa sababu hii, si vigumu kuwazia jinsi alivyoweza kuweka yote aliyokuwa nayo mikononi Mwangu, kukosa kuwa tena bwana wake mwenyewe hata kwa kula, kuvaa, ama mahali aliishi, lakini alifanya kuniridhisha kwa mambo yote msingi ambao alifurahia fadhila Yangu. Mara nyingi Nilimweka chini ya jaribio, ambalo hakika lilimwacha nusu mfu, lakini hata katikati ya haya mamia ya majaribio, hakupoteza imani Kwangu hata mara moja ama kusikitishwa nami. Hata Niliposema nimemtupa kando, hakufa moyo wala kukata tamaa, lakini aliendelea kama mbeleni akitekeleza kanuni zake ili kunipenda kwa njia ya vitendo. Nilimwambia kwamba, ingawa alinipenda, Sikumsifu ila Ningemtupa katika mikono ya Shetani mwishowe. Katikati ya majaribio haya, ambayo hayakufikia mwili wake lakini yalikuwa majaribio ya njia ya maneno, bado alisali Kwangu: “Ee, Mungu! Miongoni mwa mbingu na dunia na mambo lukuki, kuna mwanadamu yeyote, kiumbe chochote, ama kitu chochote kisicho mikononi Mwako, Mwenyezi? Unapotaka kunionyesha huruma, moyo wangu unafurahishwa sana na huruma Yako; unapotaka kunihukumu, ingawa sifai, nahisi hata zaidi siri ya kushangaza ya matendo Yako, kwa sababu Umejawa na mamlaka na hekima. Ingawa mwili wangu unapitia mateso, roho yangu ina faraja. Ningewezaje kutosifu hekima Yako na matendo Yako? Hata kama nitafa baada ya kuja kukujua, kamwe nitakuwa tayari. Ee, Mwenyezi! Hakika si kwamba Wewe kweli hutaki kuniruhusu nikuone? Hakika si kwamba sistahili kweli kupokea hukumu Yako? Inaweza labda kuwa kwamba kuna kitu ndani yangu usichotaka kuona?” Katikati ya majaribu ya aina hizi, hata kama Petro hakuweza kufahamu nia Zangu kwa usahihi, ni wazi kwamba aliliona kuwa suala la fahari na utukufu binafsi kutumiwa na Mimi (iwe tu kupokea hukumu Yangu ili binadamu waweze kuuona ukuu na ghadhabu Yangu), na hakuwa mwenye huzuni kwa ajili ya kuwekwa chini ya jaribio. Kwa sababu ya uaminifu wake mbele Yangu, na kwa sababu ya baraka Zangu juu yake, amekuwa mfano mwema na mfano wa kuigwa kwa mwanadamu kwa maelfu ya miaka. Je, huui si hasa mfano unaopaswa kufuata? Wakati huu, unapaswa kufikiria sana na kujaribu kutatua mbona Nimepeana ripoti ndefu ya Petro. Hii inapaswa kukutumikia kama kanuni ya maadili.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 6

Tanbihi:

a. Nakala ya awali imeacha “katika maisha yake mwenyewe.”

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 532)

Petro alimfuata Yesu kwa miaka kadhaa na aliona mambo mengi ndani ya Yesu ambayo watu hawana. Baada ya kumfuata Yeye kwa mwaka mmoja, aliteuliwa na Yesu kama mkuu wa wanafunzi kumi na wawili. (Bila shaka hili lilikuwa jambo la moyo wa Yesu, na watu hawakuweza kabisa kuliona.) Kila kitendo cha Yesu kilikuwa mfano kwake katika maisha yake, na mahubiri ya Yesu yaliwekwa hasa katika kumbukumbu ndani ya moyo wake. Alikuwa mwenye busara sana na wa kujitolea kwa Yesu, na kamwe hakuwa na malalamiko kumhusu Yesu. Hii ndiyo maana alikuwa mwandani mwaminifu wa Yesu popote Alipoenda. Petro alichunguza mafunzo ya Yesu, maneno Yake yasiyo makali, na kile Alichokula, Alichovaa, maisha Yake ya kila siku, na safari Zake. Alifuata mfano wa Yesu katika kila njia. Hakuwa wa kujidai, lakini alitupa vitu vyake yote vya awali vilivyopitwa na wakati akafuata mfano wa Yesu katika maneno na matendo. Ni wakati huo ndipo alihisi kwamba mbingu na dunia na vitu vyote vilikuwa ndani ya mikono ya Mwenyezi, na kwa sababu hii hakuwa na chaguo lake mwenyewe, lakini alichukua kila kitu ambacho Yesu alikuwa ili kiwe mfano wake. Angeweza kuona kutoka kwa maisha yake kwamba Yesu hakuwa wa kujivuna katika kile Alichofanya, wala Hakujigamba kuhusu Mwenyewe, lakini badala yake, Aliwavuta watu na upendo. Katika hali mbalimbali Petro angeweza kuona kile ambacho Yesu alikuwa. Hiyo ndiyo maana kila kitu ndani ya Yesu kilikuwa chombo ambacho Petro alikifuata kama mfano. Katika uzoefu wake, alihisi kupendeza kwa Yesu zaidi na zaidi. Alisema kitu kama hiki: “Nilimtafuta Mwenyezi katika ulimwengu na nikaona maajabu ya mbingu na dunia na vitu vyote, na hivyo nilikuwa na hisi kuu ya kupendeza kwa Mwenyezi. Lakini sikuwa kamwe na upendo halisi ndani ya moyo wangu, na sikuona kamwe kupendeza kwa Mwenyezi kwa macho yangu mwenyewe. Leo, katika macho ya Mwenyezi, nimetazamwa na fadhila na Yeye na hatimaye nimehisi kupendeza kwa Mungu, na hatimaye nimegundua kwamba kwa Mungu, siyo tu kuumba vitu vyote ambavyo vingewafanya wanadamu wampende Yeye. Katika maisha yangu ya kila siku nimepata kupendeza Kwake kusiko na kikomo; ni vipi ambavyo ingewezekana kuwekewa mipaka tu katika hali hii leo?” Muda ulipopita, vitu vingi vya kupendeza vilipatikana pia ndani ya Petro. Alikuwa mtiifu sana kwa Yesu, na bila shaka alipitia hasa vipingamizi vingi kwa kiasi fulani. Wakati ambapo Yesu alimpeleka katika sehemu mbalimbali kuhubiri, yeye alijinyenyekeza kila mara na kuyasikiliza mahubiri ya Yesu. Hakuwa kamwe mwenye kiburi kwa sababu ya miaka yake ya kufuata. Baada ya Yesu kumwambia kwamba sababu ya Yeye kuja ilikuwa kusulubiwa ili kuimaliza kazi Yake, alikuwa na huzuni sana mara kwa mara na angetokwa na machozi akiwa pekee yake kisiri. Hata hivyo, siku ile “ya kusikitisha” ilifika. Baada ya Yesu kushikwa, Petro alitokwa na machozi pekee yake juu ya mashua yake ya kuvua na akaomba kiasi kikubwa kuhusu jambo hili, lakini ndani ya moyo wake alijua kwamba yalikuwa mapenzi ya Mungu Baba na hakuna ambaye angeyabadilisha. Yeye alikuwa akihuzunika na kutokwa na machozi siku zote kwa sababu ya athari ya upendo—bila shaka, huu ni udhaifu wa binadamu, kwa hiyo wakati ambapo alijua kwamba Yesu angepigiliwa misumari msalabani, alimuuliza Yesu: “Baada ya Wewe kuondoka Utarudi kuwa miongoni mwetu na kutuchunguza? Je, bado tutaweza kukuona Wewe?” Ingawa maneno haya yalikuwa manyofu kabisa, na pia yalikuwa yamejawa na fikira za binadamu, Yesu alijua ladha ya mateso ya Petro, kwa hiyo kupitia upendo Wake alikuwa mwenye huruma kuhusu udhaifu wake: “Petro, Nimekupenda wewe. Je, wajua hilo? Ingawa hakuna maana katika kile usemacho, Baba ameahidi kwamba baada ya kufufuka Kwangu, Nitaonekana kwa wanadamu kwa siku 40. Je, huamini kwamba Roho Wangu atawapa ninyi nyote neema mara kwa mara?” Baada ya hilo Petro alikuwa na faraja kiasi kidogo, lakini alihisi kila mara kulikuwa na kipingamizi katika kile ambacho kilikuwa kamili kwa upande mwingine. Kwa hiyo, baada ya Yesu kufufuliwa, Alionekana kwake wazi kwa mara ya kwanza, lakini ili kumzuia Petro kuendelea kushikilia fikira zake, Yesu alikataa chakula kingi mno ambacho Petro alikuwa amemwandalia Yeye na akatoweka kufumba na kufumbua macho. Wakati huo Petro hatimaye alikuwa na ufahamu wa kina kuhusu Yesu, na akampenda Bwana Yesu hata zaidi. Baada ya kufufuka Kwake, Yesu alimwonekania Petro mara kwa mara. Baada ya siku 40 wakati ambapo Alipaa mbinguni, Alimwonekania Petro mara tatu. Kila wakati ambapo Yeye alionekana ulikuwa wakati ambao kazi ya Roho Mtakatifu ilikuwa karibu kukamilishwa na kazi mpya ilikuwa karibu kuanzwa.

Petro alipata riziki kwa kuvua kotekote katika maisha yake yote, lakini hata zaidi, aliishi kwa ajili ya kuhubiri. Katika miaka yake ya baadaye, aliandika waraka wa kwanza na wa pili wa Petro, na aliandika barua kadhaa kwa kanisa la Filadelfia la wakati huo. Watu wakati huo walivutwa sana na yeye. Hakuwahubiria watu kamwe kwa kutegemea sifa zake mwenyewe, bali aliwapa ruzuku ya kufaa ya uzima. Katika maisha yake, hakusahau kamwe mafunzo ya Yesu wakati wa maisha Yake—alisalia kutiwa moyo. Wakati ambapo alikuwa akimfuata Yesu aliamua kuulipiza upendo wa Bwana kwa kifo chake na kwamba angefuata mfano wa Yesu katika vitu vyote. Yesu alimuahidi hili, kwa hiyo wakati ambapo alikuwa na umri wa miaka 53 (zaidi ya miaka 20 baada ya kuachana na Yesu), Yesu alionekana kwake kutambua azimio lake. Katika miaka saba ya kufuata jambo hilo, Petro alitumia maisha yake katika kujijua. Siku moja, mwisho wa miaka hii saba, alisulubiwa juu chini, kukakomesha maisha yake yasiyo ya kawaida.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufafanuzi wa Mafumbo ya “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima”, Kuhusu Maisha ya Petro

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 533)

Je, ushawishi wa giza ni nini? “Ushawishi wa giza” ni ushawishi wa Shetani kuwadanganya, kuwapotosha kuwafunga na kuwatawala watu; ushawishi wa shetani ni ushawishi ambao una hali ya kifo. Wale wote ambao wanaishi chini ya miliki ya shetani wamehukumiwa kuangamia.

Unawezaje kuepuka ushawishi wa giza baada ya kupata imani katika Mungu? Baada ya kumwomba Mungu kwa dhati, unaelekeza moyo wako Kwake kikamilifu. Katika hatua hii, moyo wako unasongezwa na Roho wa Mungu, uko tayari kujitoa mwenyewe kikamilifu, na katika wakati huu, umeepuka ushawishi wa giza. Kama yote ambayo mtu anafanya yanampendeza Mungu na anapatana na matakwa Yake, basi yeye ni mtu ambaye anaishi ndani ya maneno ya Mungu, yeye ni mtu anayeishi chini ya utunzaji na ulinzi wa Mungu. Kama watu hawawezi kutenda maneno ya Mungu, daima wakimpumbaza na kutenda katika namna ya uzembe na Yeye, na hawaamini katika uwepo Wake, watu kama hao wote wanaishi chini ya ushawishi wa giza. Watu ambao hawajapokea wokovu wa Mungu wote wamemilikiwa na Shetani, yaani, hao wote wanaishi chini ya ushawishi wa giza. Wale ambao hawamwamini Mungu wamemilikiwa na Shetani. Hata wale ambao wanaamini katika kuwepo kwa Mungu huenda si lazima wawe wanaishi katika nuru ya Mungu, kwa sababu wale ambao wanamwamini huenda si lazima wawe wanaishi ndani ya maneno ya Mungu, na huenda si lazima wawe watu ambao wanaweza kumtii Mungu. Mtu anamwamini tu Mungu, na kwa sababu ya kushindwa kwake kumjua Mungu, bado anaishi ndani ya sheria za zamani, anaishi ndani ya maneno yaliyokufa, anaishi katika maisha ambayo ni giza na si ya hakika, hajatakaswa kikamilifu na Mungu au kupatwa kikamilifu na Mungu. Kwa hivyo, ni dhahiri ya kwamba wale wasiomwamini Mungu wanaishi chini ya ushawishi wa giza, hata wale ambao wanamwamini Mungu huenda wakawa bado wanaishi chini ya ushawishi wake, kwa ajili Roho Mtakatifu hajatekeleza kazi juu yao. Wale ambao hawajapokea neema ya Mungu au rehema ya Mungu, na wale ambao hawawezi kuona kazi ya Roho Mtakatifu, wote wanaishi chini ya ushawishi wa giza; wale ambao wanafurahia tu neema ya Mungu na bado hawamjui pia wanaishi chini ya ushawishi wa giza wakati mwingi. Kama mtu anamwamini Mungu na bado anatumia wakati mwingi wa maisha yake akiishi chini ya ushawishi wa giza, basi kuwepo kwa mtu huyu kumepoteza maana yake, bila kutaja wale ambao hawaamini katika uwepo wa Mungu.

Wale wote ambao hawawezi kukubali kazi ya Mungu au wanaokubali kazi ya Mungu lakini hawawezi kukidhi matakwa Yake wanaishi chini ya ushawishi wa giza; wale tu wanaofuatilia ukweli na wana uwezo wa kukidhi matakwa ya Mungu watapokea baraka kutoka Kwake, na ni wao tu wataepuka ushawishi wa giza. Watu ambao hawajafunguliwa, ambao siku zote wamedhibitiwa na mambo fulani na ambao hawawezi kutoa mioyo yao kwa Mungu, ni watu ambao wako chini ya utumwa wa Shetani, na wanaoishi chini ya hali ya kifo. Wale wasio waaminifu kwa wajibu wao wenyewe, wasio waaminifu kwa agizo la Mungu na wale ambao hawatekelezi jukumu lao kanisani wanaishi chini ya ushawishi wa giza. Wale ambao husumbua maisha ya kanisa kimakusudi, wale ambao huharibu mahusiano kati ya akina ndugu na kimakusudi, au kuweka pamoja magenge yao wenyewe, wanaishi hata zaidi chini ya ushawishi wa giza; wao wanaishi ndani ya utumwa wa Shetani. Wale walio na uhusiano usio sahihi na Mungu, walio na tamaa za kifahari daima, ambao daima wanataka kupata faida, na ambao kamwe hawatafuti mabadiliko katika tabia yao ni watu ambao wanaishi chini ya ushawishi wa giza. Wale ambao hawako imara daima, ambao hawajatilia maanani utendaji wao wa ukweli, na ambao hawatafuti kukidhi matakwa ya Mungu ila kuridhisha tu miili yao wenyewe ni watu ambao pia wanaishi chini ya ushawishi wa giza na kufunikwa katika kifo. Wale ambao hujihusisha na hila na udanganyifu wakati wa kutekeleza kazi ya Mungu, ambao wanashughulikia Mungu katika njia ya kizembe, wanamdanganya Mungu, na ambao daima hujifikiria, ni watu wanaoishi chini ya ushawishi wa giza. Wale wote ambao hawawezi kumpenda Mungu kwa dhati, ambao hawafuatilii ukweli, na wasiozingatia kubadilisha tabia yao, wanaishi chini ya ushawishi wa giza.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Epuka Ushawishi wa Giza na Utapatwa na Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 534)

Kama unataka kusifiwa na Mungu, lazima kwanza uepuke ushawishi wa giza wa Shetani, ufungue moyo wako kwa Mungu, na uuelekeze kwa Mungu kikamilifu. Je, mambo ambayo unafanya kwa sasa yanasifiwa na Mungu? Umeelekeza moyo wako kwa Mungu? Je, mambo ambayo umeyafanya ni yale ambayo Mungu ametaka kutoka kwako? Je, yanaingiana na ukweli? Lazima ujichunguze kila wakati, uzingatie kula na kunywa maneno ya Mungu, uweke moyo wako wazi mbele Yake, umpende kwa uwazi, na ujitumie kwa bidii kwa ajili ya Mungu. Watu kama hao hakika watapokea sifa ya Mungu.

Wote ambao humwamini Mungu ilhali hawafuatilii ukweli hawana namna ya kuepuka ushawishi wa shetani. Wale wote ambao hawaishi maisha yao kwa uaminifu, wanaotenda kwa njia moja mbele ya wengine na njia nyingine kwa siri, wanaotoa mwonekano wa unyenyekevu, uvumilivu, na upendo ilhali katika kiini ni wenye kudhuru kwa siri, wana hila, na hawana uaminifu kwa Mungu—watu hawa ni mfano halisi wa wale wanaoishi chini ya ushawishi wa giza. Wao ni wa kizazi cha nyoka. Wale ambao imani yao katika Mungu daima ni kwa ajili ya faida zao wenyewe, ambao ni wa kujidai na wenye maringo, ambao hujigamba, na hulinda hadhi zao wenyewe ni wale wanaompenda Shetani na kuupinga ukweli. Wao wanapinga Mungu na ni wa Shetani kikamilifu. Wale ambao hawako makini kwa mizigo ya Mungu, ambao hawamtumikii Mungu kwa moyo wote, ambao daima wanajali maslahi yao wenyewe na maslahi ya familia zao, ambao hawawezi kuacha kila kitu ili wajitumie kwa ajili ya Mungu, na ambao kamwe hawaishi kulingana na maneno Yake wanaishi nje ya maneno ya Mungu. Watu kama hawa hawawezi kupokea sifa ya Mungu.

Wakati Mungu aliumba watu, ilikuwa ili kuwafanya wafurahie utajiri Wake na wampende kwa kweli; katika njia hii, watu wangeishi katika nuru Yake. Leo, wote ambao hawawezi kumpenda Mungu, ambao hawako makini kwa mizigo Yake, ambao hawawezi kutoa mioyo yao kikamilifu kwa Mungu, ambao hawawezi kuchukua moyo wa Mungu kama wao wenyewe, ambao hawawezi kubeba mizigo ya Mungu kama yao wenyewe—nuru ya Mungu haiangazi juu ya watu wowote kama hawa, kwa hivyo, wote wanaishi chini ya ushawishi wa giza. Wako kwenye njia ambayo huenda kinyume kabisa na mapenzi ya Mungu, na yote wanayoyafanya hayana hata chembe ya ukweli. Wanazamia katika matatizo na Shetani na ni wale ambao wanaishi chini ya ushawishi wa giza. Kama unaweza daima kula na kunywa maneno ya Mungu na pia kuwa makini na mapenzi Yake na kutenda maneno Yake, basi wewe ni wa Mungu, na wewe ni mtu anayeishi ndani ya maneno ya Mungu. Je, uko tayari kuepuka kumilikiwa na Shetani na kuishi katika nuru ya Mungu? Kama unaishi ndani ya maneno ya Mungu, basi Roho Mtakatifu atakuwa na nafasi ya kutenda kazi Yake; kama unaishi chini ya ushawishi wa Shetani, basi Roho Mtakatifu hatakuwa na nafasi ya kutenda kazi yoyote. Kazi ambayo Roho Mtakatifu hutenda kwa watu, nuru ambayo Yeye huangaza kwa watu, na imani ambayo Yeye hutoa kwa watu hukaa kwa muda tu; kama hawako makini na hawampi kipaumbele, kazi iliyotendwa na Roho Mtakatifu itawapita. Kama watu wanaishi ndani ya maneno ya Mungu, basi Roho Mtakatifu atakuwa pamoja nao na kutenda kazi juu yao; kama watu hawaishi ndani ya maneno ya Mungu, basi wanaishi ndani ya utumwa wa Shetani. Watu wanaoishi katika tabia ya kiufisadi hawana uwepo wala kazi ya Roho Mtakatifu. Kama unaishi ndani ya nyanja ya maneno ya Mungu, kama unaishi katika hali inayohitajika na Mungu, basi wewe ni Wake na kazi Yake itatendwa juu yako; kama huishi ndani ya nyanja ya matakwa ya Mungu lakini badala yake unamilikiwa na Shetani, basi hakika wewe unaishi chini ya upotovu wa Shetani. Ni kwa kuishi ndani ya maneno ya Mungu tu na kutoa moyo wako Kwake, ndipo unaweza kukidhi matakwa Yake; lazima ufanye asemavyo Mungu, lazima ufanye maneno ya Mungu msingi wa kuwepo kwako na hali halisi ya maisha yako, na ni hapo tu ndipo utakuwa wa Mungu. Kama kwa dhati unatenda kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu, Atatenda kazi juu yako na kisha utaishi chini ya baraka za Mungu, uishi katika nuru ya uso wa Mungu, kufahamu kazi ambayo Roho Mtakatifu hutenda, na pia kuhisi furaha ya uwepo wa Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Epuka Ushawishi wa Giza na Utapatwa na Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 535)

Kuepuka ushawishi wa giza, lazima kwanza uwe mwaminifu kwa Mungu na kuwa na hamu ya kufuatilia ukweli—ni hapo tu ndipo utakuwa na hali sahihi. Kuishi katika hali sahihi ndilo sharti la mwanzo la kuepuka ushawishi wa giza. Kukosa hali sahihi ina maana kwamba wewe si mwaminifu kwa Mungu na ya kwamba huna hamu ya kutafuta ukweli. Basi, kuepuka ushawishi wa giza hakutawezekana. Mtu kuepuka ushawishi wa giza ni kwa msingi wa maneno Yangu, na kama mtu hawezi kutenda kwa mujibu wa maneno Yangu, hataepuka utumwa wa ushawishi wa giza. Kuishi katika hali sahihi ni kuishi chini ya uongozi wa maneno ya Mungu, kuishi katika hali ya kuwa mwaminifu kwa Mungu, kuishi katika hali ya kutafuta ukweli, kuishi katika uhalisi wa kugharamia rasilmali kwa ajili ya Mungu kwa dhati, kuishi katika hali ya kumpenda Mungu kwa kweli. Wale ambao wanaishi katika hali hizi na ndani ya hali halisi hii watabadilika hatua kwa hatua wanapoingia ndani zaidi katika ukweli, nao watabadilika kwa kuongezeka kwa kazi, mpaka hatimaye hakika watapatwa na Mungu, na watakuja kwa kweli kumpenda Mungu. Wale ambao wameepuka ushawishi wa giza wataweza kufahamu mapenzi ya Mungu hatua kwa hatua, wataelewa mapenzi ya Mungu hatua kwa hatua, na hatimaye kuwa wasiri wa Mungu. Hawatakosa dhana kumhusu Mungu tu, na kukosa uasi dhidi Yake, lakini watakuja kuchukia hata zaidi dhana na uasi ambao walikuwa nao kabla, kusababisha upendo wa kweli kwa Mungu mioyoni mwao. Wale ambao hawawezi kuepuka ushawishi wa giza wanashughulika na miili yao, na wamejaa uasi; mioyo yao imejazwa dhana za kibinadamu na falsafa za kuishi, pamoja na nia zao na majadiliano. Mungu anataka upendo mmoja wa mtu, naye humhitaji mtu amilikiwe na maneno Yake na upendo wa mtu Kwake. Kuishi ndani ya maneno ya Mungu, kugundua kile ambacho mtu anapaswa kutafuta kutoka ndani ya maneno Yake, kumpenda Mungu kama matokeo ya maneno Yake, kukimbiakimbia kwa ajili ya maneno ya Mungu, kuishi kwa ajili ya maneno ya Mungu—haya yote ni mambo ambayo mtu anapaswa kufikia. Kila kitu lazima kijengwe kulingana na maneno ya Mungu, na hapo tu ndipo mtu ataweza kukidhi matakwa ya Mungu. Kama mwanadamu hajatayarishwa na maneno ya Mungu, basi yeye ni funza tu ambaye amemilikiwa na Shetani. Yapime moyoni mwako mwenyewe—ni maneno mangapi ya Mungu ambayo umekita mizizi yake ndani yako? Ni katika mambo gani unaishi kulingana na maneno Yake? Ni katika mambo gani ndiyo hujakuwa ukiishi kulingana nayo? Kama maneno ya Mungu hayajakumiliki kikamilifu, basi ni nini hasa kilicho moyoni mwako? Katika maisha yako ya kila siku, je, unadhibitiwa na Shetani, au unamilikiwa na maneno ya Mungu? Je, maombi yako yameanzishwa kutoka kwa maneno Yake? Je, umeondoka katika hali yako mbaya kupitia nuru ya maneno ya Mungu? Kuchukua maneno ya Mungu kama msingi wa kuwepo kwako, hili ndio jambo kila mtu anapaswa kuingia ndani. Kama maneno ya Mungu hayapo katika maisha yako, basi unaishi chini ya ushawishi wa giza, wewe ni muasi dhidi ya Mungu, unampinga Mungu, na huheshimu jina Lake—imani ya watu kama hao katika Mungu ni uharibifu na usumbufu kabisa. Je, ni kiasi gani cha maisha yako kimeishiwa kwa mujibu wa maneno Yake? Ni kiasi gani cha maisha yako hakijaishiwa kwa mujibu wa maneno Yake? Je, ni kiasi gani cha kile ambacho maneno ya Mungu yamehitaji kwako kimetimizwa ndani yako? Ni mangapi yamepotea ndani yako? Je, umechunguza mambo kama hayo kwa karibu?

Kuepuka ushawishi wa giza, kipengele kimoja ni kwamba kunahitaji kazi ya Roho Mtakatifu, na kipengele kingine ni kwamba kunahitaji ushirikiano wa kujitolea kutoka kwa mtu. Mbona Nasema ya kwamba mtu hayuko kwenye njia sahihi? Kwanza, kama mtu yuko kwenye njia sahihi, ataweza kutoa moyo wake kwa Mungu, ambayo ni jukumu linalohitaji muda mrefu kuingia ndani kwa sababu mwanadamu daima amekuwa akiishi chini ya ushawishi wa giza na amekuwa chini ya utumwa wa Shetani kwa maelfu ya miaka. Kwa hivyo, kuingia huku hakuwezi kupatikana katika siku moja au mbili. Nilileta suala hili leo ili watu waweze kuwa na ufahamu wa hali yao wenyewe; kuhusu ushawishi wa giza ni nini na kuishi ndani ya nuru ni nini, kuingia kunawezekana wakati mtu ana uwezo wa kutambua mambo haya. Hii ni kwa sababu ni lazima ujue ushawishi wa Shetani ni nini kabla uuepuke, na hapo tu ndipo utakuwa na njia ya kuuepuka hatua kwa hatua mwenyewe. Kuhusu ni nini cha kufanya baada ya hapo, hilo ni suala la wanadamu wenyewe. Lazima daima uingie kutoka mtazamo mwema na hupaswi kusubiri kamwe kwa utulivu. Ni kwa njia hii tu ndiyo unaweza kupatwa na Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Epuka Ushawishi wa Giza na Utapatwa na Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 536)

Kila neno la Mungu hugonga eneo letu moja la kufisha, likituwacha na uchungu na kujawa na hofu Yeye hufichua dhana zetu, mawazo yetu, na tabia zetu potovu. Kutoka kwa yale yote sisi husema na kutenda, hadi kwa kila wazo na fikra zetu, asili na kiini chetu kinafichuliwa katika maneno Yake, yakituweka katika hali ya hofu na kutetemeka na bila mahali pa kuficha aibu yetu. Mmoja baada ya mwingine, Anatueleza kuhusu matendo yetu yote, malengo yetu na nia, hata tabia potovu ambazo hatujawahi kugundua sisi wenyewe, na kutufanya tuhisi kwamba tumewekwa wazi katika dosari zetu mbaya na hata zaidi kushindwa kikamilifu. Yeye hutuhukumu kwa ajili ya upinzani wetu Kwake, hutuadibu kwa ajili ya kufuru kwetu na kumshutumu kwetu, na kutufanya tuhisi kwamba, machoni Pake, hatuna sifa hata moja inayoweza kutuokoa, kwamba sisi ndio Shetani anayeishi. Matumaini yetu yanavunjika, na hatuthubutu tena kumpa madai yoyote yasiyo na busara au kuendeleza matumaini yoyote ya Yeye, na hata ndoto zetu hupotelea mara moja. Huu ni ukweli ambao hakuna kati yetu anaweza kufikiria, na ambao hakuna yeyote kati yetu anayeweza kukubali. Katika muda mfupi, tunapoteza usawa wetu wa ndani, na hatujui jinsi ya kuendelea kwa njia iliyo mbele wala jinsi ya kuendelea katika imani zetu. Inaonekana kana kwamba imani yetu imerudi kama ilivyokuwa mwanzoni, na tena ya kana kwamba hatujawahi kukutana na Bwana Yesu au kupata kumjua. Kila kitu machoni petu hutujaza na mkanganyo, na kutufanya kuyumba kwa shaka. Tunasikitishwa, tunahuzunika, na ndani ya mioyo yetu kuna ghadhabu isiyozuilika na aibu. Tunajaribu kujieleza, kupata suluhisho, na, aidha, sisi huendelea kumsubiri Mwokozi Yesu, ili tuweze kujieleza kwa dhati Kwake. Ingawa kuna nyakati zingine ambazo sisi huonekana hatuyumbiyumbi kwa kutazamwa nje, tusio wenye kiburi wala wanyenyekevu, mioyoni mwetu tunateseka na hisia ya hasara kuliko ile tumewahi kuwa nayo. Ingawa wakati mwingine tunaweza kuonekana ni kama tuna utulivu kwa kutazamwa nje, akili zetu zinasokoteka kwa mateso kama bahari yenye dhoruba. Hukumu Yake na kuadibu Kwake zimechukua matumaini na ndoto zetu zote, kukomesha tamaa zetu kuu na kutuacha tusitake kuamini kuwa Yeye ndiye Mwokozi wetu na anayeweza kutuokoa. Hukumu Yake na kuadibu zimefungua ghuba kati yetu na Yeye, ghuba kubwa kiasi kwamba hakuna aliye tayari hata kujaribu kuivuka. Hukumu na kuadibu Kwake ni mara ya kwanza ambapo sisi tumepitia pingamizi kubwa hivi, udhalilishaji kiasi kikubwa hivyo maishani mwetu. Hukumu na kuadibu Kwake kwa kweli zimetusababisha kuthamini heshima ya Mungu na kutovumilia Kwake kosa la binadamu, ambazo tukilinganishwa nazo, sisi ni waovu sana, wachafu sana. Hukumu Yake na kuadibu zimetufanya sisi kutambua kwa mara ya kwanza jinsi ambavyo tuna kiburi na wenye majivuno, na jinsi ambavyo mwanadamu kamwe hataweza kulingana na Mungu, ama kuwa sawa na Mungu. Hukumu Yake na kuadibu Kwake zimetufanya tutumaini kutoishi tena katika tabia potovu hivi, kujiondoa asili na kiini hiki haraka iwezekanavyo, na kuwacha kuwa waovu na wa kuchukiwa na Yeye. Hukumu na kuadibu Kwake zimetufanya tufurahie kutii maneno Yake, na tusiasi matayarisho na mipangilio Yake tena. Hukumu na kuadibu Kwake kwa mara nyingine zimetuwezesha sisi tuwe na tamaa ya kuendelea kuwepo na zilituwezesha kufurahia kumkubali kama Mwokozi wetu…. Sisi tumetoka nje ya kazi ya ushindi, nje yaa kuzimu, tumetoka nje ya bonde la uvuli wa mauti…. Mwenyezi Mungu ametupata, kundi hili la watu! Ameshinda dhidi ya Shetani, na kuwashinda adui Zake wengi!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 4: Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 537)

Ni wakati tu ambapo umetupa tabia zako potovu na kutimiza kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida ndiyo utafanywa kuwa mkamilifu. Ingawa utakuwa huwezi kunena unabii, wala siri zozote, utakuwa unaishi kulingana na kufichua taswira ya mwanadamu. Mungu alimuumba mwanadamu, baada ya hapo mwanadamu akaharibiwa na Shetani, na uharibifu huu umewafanya watu wawe “maiti”—na hivyo, baada ya kuwa umebadilika, utakuwa tofauti na maiti hizi. Ni maneno ya Mungu ndiyo yanatoa uzima kwa roho za watu na kuwasababisha kuzaliwa upya, na roho za watu zinapozaliwa upya, watakuwa hai tena. Neno “wafu” linarejelea maiti ambazo hazina roho, kwa watu ambao roho zao zimekufa. Roho za watu zinapowekewa uhai, wanakuwa hai tena. Watakatifu waliozungumziwa awali huashiria watu ambao wamekuwa hai, wale ambao walikuwa chini ya ushawishi wa Shetani lakini wakamshinda Shetani. Wateule wa China wamestahimili ukatili na mateso na ulaghai wa joka kuu jekundu, ambalo limewaacha wakiwa wameharibika kiakili na kuwachwa wakiwa hawana hata ujasiri wa kuishi. Hivyo, kuamsha roho zao kunapaswa kuanza na hulka zao. Kidogo kidogo, katika hulka yao roho yao itaamshwa. Siku moja, watakapokuwa hai tena, hakutakuwa na vizuizi zaidi, na vyote vitasonga mbele bila tatizo. Kwa sasa, hii inabakia kuwa bado haijafanikiwa. Kuishi kwa kudhihirisha kwa watu wengi kunajumuisha mazingira ya kifo, wamezungukwa na hali ya kifo, na wamepungukiwa sana. Maneno ya baadhi ya watu yanabeba kifo, matendo yao yanabeba kifo, na takribani kila kitu wanachoishi kwa kudhihirisha ni kifo. Ikiwa leo, watu wanamshuhudia Mungu waziwazi, basi kazi hii itashindwa, maana bado hawajakuwa hai tena kikamilifu, na kuna wafu wengi sana miongoni mwenu. Leo, baadhi ya watu wanauliza kwa nini Mungu haonyeshi ishara na maajabu ili kwamba aweze kusambaza kazi Yake miongoni mwa nchi za Wamataifa. Wafu hawawezi kuwa na ushuhuda wa Mungu; walio hai pekee ndio wanaweza, lakini watu wengi leo ni wafu, wengi wao wanaishi katika kifungo cha kifo, wanaishi chini ya ushawishi wa Shetani, na hawawezi kupata ushindi—na hivyo wanawezaje kuchukua ushuhuda wa Mungu? Wanawezaje kueneza kazi ya injili?

Wale wanaoishi chini ya ushawishi wa giza, ni wale ambao wanaishi katikati ya kifo, ni wale ambao wametawaliwa na Shetani. Bila kuokolewa na Mungu, na kuhukumiwa na kuadibiwa na Mungu, watu wanakuwa hawana uwezo kukwepa athari ya kifo, hawawezi kuwa hai. Wafu hawa hawawezi kuwa ushuhuda kwa Mungu, wala hawawezi kutumiwa na Mungu, wala kuingia katika ufalme. Mungu anataka ushuhuda wa walio hai, na sio wafu, na Anaomba kwamba walio hai, wala sio wafu, wamfanyie Yeye kazi. “Wafu” ni wale ambao wanampinga na kumwasi Mungu, ni wale ambao ni mbumbumbu katika roho na hawaelewi maneno ya Mungu, ni wale ambao hawaweki ukweli katika matendo na hawana utii hata kidogo kwa Mungu, na ni wale ambao wamemilikiwa na Shetani na kunyanyaswa na Shetani. Wafu wanajionyesha wenyewe kwa kuupinga ukweli, kwa kumwasi Mungu, na kwa kuwa duni, wa kudharaulika, kuwa waovu, katili, wadanganyifu, na kudhuru kwa siri. Ingawa watu wa namna hiyo wanakula na kunywa maneno ya Mungu, hawana uwezo wa kuishi kwa kudhihirisha maneno ya Mungu; wanaishi, lakini ni wafu wanaotembea, ni maiti zinazopumua. Wafu hawawezi kabisa kumridhisha Mungu, wala kumtii kikamilifu. Wanaweza tu kumdanganya, kusema maneno ya makufuru juu Yake, na kumsaliti, na yote wanayoyaishi kwa kudhihirisha hufichua asili ya Shetani. Ikiwa watu wanatamani kuwa viumbe hai, na kuwa na ushuhuda wa Mungu, na kuthibitishwa na Mungu, wanapaswa kukubali wokovu wa Mungu, wanapaswa kuwa watiifu katika hukumu na kuadibu Kwake, na wanapaswa kukubali kwa furaha kushughulikiwa na kupogolewa na Mungu. Ni hapo tu ndipo wataweza kuweka katika matendo ukweli wote unaohitajika na Mungu, na baada ya hapo ndipo wataweza kupata wokovu wa Mungu, na kuwa viumbe hai kabisa. Walio hai wanaokolewa na Mungu, wamehukumiwa na kuadibiwa na Mungu, wapo tayari kujitoa wenyewe na wana furaha kutoa maisha yao kwa Mungu, na wapo tayari kujitoa maisha yao yote kwa Mungu. Pale ambapo walio hai watachukua ushuhuda wa Mungu ndipo Shetani ataweza kuaibishwa, ni walio hai tu ndio wanaweza kueneza kazi ya injili ya Mungu, ni walio hai tu ndio wanaoupendeza moyo wa Mungu, ni walio hai tu ndio watu halisi. Mwanadamu wa asili aliyeumbwa na Mungu alikuwa hai, lakini kwa sababu ya uharibifu wa Shetani mwanadamu anaishi katikati ya kifo, na anaishi chini ya ushawishi wa Shetani, na hivyo watu hawa wamekuwa wafu ambao hawana roho, wamekuwa ni maadui ambao wanampinga Mungu, wamekuwa nyenzo ya Shetani, na wamekuwa mateka wa Shetani. Watu wote walio hai ambao wameumbwa na Mungu wamekuwa wafu, na hivyo Mungu amepoteza ushuhuda wake, na Amempoteza mwanadamu, ambaye Alimuumba na ndiye kiumbe pekee aliye na pumzi Yake. Ikiwa Mungu ataamua kurejesha ushuhuda Wake, na kuwarejesha wale ambao waliumbwa kwa mkono wake lakini ambao wamechukuliwa mateka na Shetani, basi ni lazima awafufue ili waweze kuwa viumbe hai, na ni lazima awaongoe ili kwamba waweze kuishi katika nuru Yake. Wafu ni wale ambao hawana roho, wale ambao ni mbumbumbu kupita kiasi, na wale ambao wanampinga Mungu. Aidha, ni wale ambao hawamjui Mungu. Watu hawa hawana nia hata ndogo ya kumtii Mungu, kazi yao ni kumpinga na kuasi dhidi Yake, na hawana hata chembe ya utii. Walio hai ni wale ambao roho zao zimezaliwa upya, wale wanaojua kumtii Mungu, na ambao ni watii kwa Mungu. Wanao ukweli, na ushuhuda, na ni watu wa aina hii tu ndio wanaompendeza Mungu katika nyumba Yake. Mungu anawaokoa wale ambao wanaweza kuwa hai tena, ambao wanaweza kuuona wokovu wa Mungu, ambao wanaweza kuwa watii kwa Mungu, na wapo tayari kumtafuta Mungu. Anawaokoa wanaomwamini Mungu aliyepata mwili, na wanaamini katika kuonekana Kwake. Baadhi ya watu wanaweza kuwa hai tena, na baadhi hawawezi; inategemea na asili yao kama inaweza kuokolewa au la. Watu wengi wamesikia sana kuhusu maneno ya Mungu lakini bado hawaelewi mapenzi ya Mungu, wameyasikia maneno mengi sana ya Mungu lakini bado hawawezi kuyaweka katika vitendo, hawawezi kuishi kwa kudhihirisha ukweli wowote na pia kwa kukusudia kabisa wanaingilia kazi ya Mungu. Hawawezi kufanya kazi yoyote kwa ajili ya Mungu, hawawezi kujitolea chochote Kwake, na pia wanatumia kwa siri pesa za kanisa, na kula katika nyumba ya Mungu bure. Watu hawa ni wafu, na hawataokolewa. Mungu anawaokoa wale ambao wapo katika kazi Yake. Lakini kuna sehemu ya watu hao ambao hawawezi kupokea wokovu Wake; ni idadi ndogo tu ndiyo inaweza kupokea wokovu Wake. Hii ni kwa sababu watu wengi wamepotoshwa kwa kina sana na wakuwa wafu, na wamepita kiwango cha kuokolewa; wametumiwa vibaya kabisa na Shetani, na ni wenye hila sana katika asili yao. Watu hao wachache pia hawawezi kumtii Mungu kikamilifu. Hawakuwa wale ambao walikuwa waaminifu kabisa kwa Mungu tangu mwanzo, au wale ambao walikuwa na upendo wa hali ya juu kabisa kwa Mungu toka mwanzo; badala yake, wamekuwa watiifu kwa Mungu kwa sababu ya kazi Yake ya ushindi, wanamwona Mungu kwa sababu ya upendo wake mkuu, kuna mabadiliko katika tabia zao kwa sababu ya tabia ya Mungu ya haki, na wanamjua Mungu kwa sababu ya kazi Yake, ambayo ni halisi na ya kawaida. Bila kazi hii ya Mungu, haijalishi watu hawa ni wazuri kiasi gani bado wangebaki kuwa wa Shetani, bado wangekuwa ni wa kifo, bado wangekuwa wafu. Kwamba, leo, watu hawa wanaweza kupokea wokovu wa Mungu ni kwa sababu kabisa wanaweza kushirikiana na Mungu.

Kwa sababu ya utiifu wao kwa Mungu, walio hai wanaweza kuchukuliwa na Mungu na kuishi katika ahadi Zake, na kwa sababu ya upinzani wao kwa Mungu, wafu watachukiwa zaidi na kukataliwa na Mungu na kuishi katikati ya adhabu na laana Zake. Hiyo ndiyo tabia ya haki ya Mungu, na haiwezi kubadilishwa na mwanadamu yeyote. Kwa sababu ya utafutaji wao wenyewe, watu wanapokea kibali cha Mungu na kuishi katika nuru; kwa sababu ya hila zao za kutisha, watu wanalaaniwa na Mungu, na kushuka chini katika adhabu; kwa sababu ya matendo yao maovu, watu wanaadhibiwa na Mungu; na kwa sababu ya kutamani kwao sana na utii wao, watu wanapokea baraka za Mungu. Mungu ni mwenye haki: Anawabariki walio hai, na kuwalaani wafu, ili kwamba siku zote wanakuwa katikati ya kifo, na kamwe hawataishi katika nuru ya Mungu. Mungu atawachukua walio hai kwenda katika ufalme Wake, Atawachukua walio hai kwenda katika baraka Zake milele. Wafu Atawaangusha katika kifo cha milele; wao ni wahusika wa uharibifu Wake, na siku zote watakuwa kwa Shetani. Mungu hamtendei mtu yeyote bila haki. Wale wote ambao kweli wanamtafuta Mungu hakika watabaki katika nyumba ya Mungu, na wale wote ambao hawamtii Mungu, na wale ambao hawana ulinganifu naye hakika wataishi katika adhabu Yake. Pengine huna uhakika kuhusu kazi ya Mungu katika mwili—lakini siku moja mwili wa Mungu hautapangilia hatima ya mwanadamu moja kwa moja; badala yake, Roho Wake, atapanga mwisho wa mwanadamu, na wakati huo watu watajua kwamba mwili wa Mungu na Roho Wake ni kitu kimoja, kwamba mwili Wake hauwezi kufanya kosa, na hata Roho Wake hawezi kabisa kufanya kosa. Na hatimaye, hakika atawachukua wale ambao watakuwa hai tena na kuwapeleka katika ufalme Wake, hakuna zaidi, wala pungufu, na wale wafu ambao hawakutoka wakiwa hai watatupwa katika shimo la Shetani.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Wewe ni Mtu Ambaye Amepata Uzima?

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 538)

Njia ambayo Roho Mtakatifu huchukua ndani ya watu ni kuvuta kwanza mioyo yao kutoka kwa watu, matukio, na vitu vyote, na kuingiza ndani ya maneno ya Mungu ili ndani ya mioyo yao wote waamini kwamba maneno ya Mungu hayana shaka kabisa na ni kweli kabisa. Kwa vile unaamini katika Mungu lazima uamini katika maneno Yake; ikiwa umeamini katika Mungu kwa miaka mingi lakini hujui njia ambayo Roho Mtakatifu hufuata, wewe kweli ni muumini? Ili kutimiza maisha ya mtu wa kawaida na maisha yanayofaa ya mtu na Mungu, lazima kwanza uamini maneno Yake. Ikiwa hujakamilisha hatua ya kwanza ya kazi ambayo Roho Mtakatifu hufanya ndani ya watu, huna msingi. Unakosa kanuni ya msingi kabisa, kwa hiyo unawezaje kutembea njia iliyo mbele? Kufuata njia sahihi ya Mungu kumkamilisha mwanadamu ni kuingia katika njia sahihi ya kazi halisi ya Roho Mtakatifu; pia ni kufuata njia ambayo Roho Mtakatifu hutembea. Hivi sasa, njia ambayo Roho Mtakatifu hutembea ni maneno halisi ya Mungu. Kwa hiyo, kwa mtu kuitembea, ni lazima atii, na kula na kunywa maneno halisi ya Mungu mwenye mwili. Anafanya kazi ya neno, na kila kitu kinaanza kutoka kwa neno Lake, na kila kitu kinaanzishwa juu ya neno Lake, neno Lake la sasa. Kama ni kuwa bila shaka yoyote kabisa kuhusu Mungu kuwa mwili au kumjua Yeye, mtu anapaswa kuweka bidii zaidi katika maneno Yake. Vinginevyo, hawezi kutimiza chochote kamwe, na ataachwa bila chochote. Ni kwa kuja kumjua Mungu tu na kumridhisha kwa msingi wa kula na kunywa maneno Yake ndipo mtu anaweza kuanzisha polepole uhusiano unaofaa na Yeye. Kula na kunywa maneno Yake na kuyaweka katika matendo ni ushirikiano bora zaidi na Mungu, na ni kitendo kinachotoa ushuhuda vizuri zaidi kama mmoja wa watu Wake. Mtu akielewa na aweze kutii kiini cha maneno halisi ya Mungu, anaishi katika njia inayoongozwa na Roho Mtakatifu na ameingia katika njia sahihi ya Mungu kumkamilisha mwanadamu. Zamani ilikuwa kwamba watu walitafuta neema na walitafuta amani na furaha, na kisha waliweza kupata kazi ya Mungu. Ni tofauti sasa. Ikiwa hawana maneno ya Mungu aliyepata mwili, ikiwa hawana uhalisi wa maneno hayo, hawawezi kupata kibali kutoka kwa Mungu na wataondoshwa na Mungu. Ili kutimiza maisha ya kiroho ya kufaa, kwanza kula na kunywa maneno ya Mungu na kuyaweka katika vitendo; na juu ya msingi huu anzisha uhusiano wa kufaa kati ya mwanadamu na Mungu. Ni vipi ambavyo unashirikiana? Ni vipi ambavyo unakuwa shahidi kama mmoja wa watu Wake? Ni vipi ambavyo unaanzisha uhusiano wa kufaa na Mungu?

Hivi ndivyo namna ya kuona ikiwa una uhusiano wa kufaa na Mungu katika maisha yako ya kila siku:

1. Unaamini ushuhuda wa Mungu mwenyewe?

2. Unaamini katika moyo wako kwamba maneno ya Mungu ni kweli na yasiyoweza kukosea?

3. Wewe ni mtu unayeweka maneno Yake katika vitendo?

4. Umejitolea kwa kile Alichokuaminia? Unawezaje kujitolea kwa hicho?

5. Je, kila kitu unachofanya ni kwa ajili ya kumridhisha na kuwa mwaminifu kwa Mungu?

Kupitia mambo haya, unaweza kutathmini ikiwa una uhusiano wa kufaa na Mungu katika hatua hii ya sasa.

Ikiwa unaweza kukubali kile Mungu anakuaminia wewe, kukubali ahadi Yake, na kufuata njia ya Roho Mtakatifu, hii ni kufanya mapenzi ya Mungu. Una uwazi wa ndani kuhusu njia ya Roho Mtakatifu? Je, matendo yako ya sasa ni ya kufuatana na njia Yake? Moyo wako unasonga karibu na Mungu? Uko radhi kuifuata nuru mpya kabisa kutoka kwa Roho Mtakatifu? Uko radhi kupatwa na Mungu? Uko radhi kuwa dhihirisho la utukufu wa Mungu duniani? Una nia ya kutimiza anachohitaji Mungu? Ikiwa, mara tu Mungu anapozungumza, na una azimio la kushirikiana na Yeye na kumridhisha Yeye, ikiwa hii ndiyo hali ya saikolojia yako ya ndani, inamaanisha kwamba maneno ya Mungu yamezaa matunda ndani ya moyo wako. Ikiwa huna aina hiyo ya hiari na huna lengo katika kazi yako, inamaanisha kwamba moyo wako bado haujasisimuliwa na Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Ambao Tabia Zao Imebadilika ni Wale Ambao Wameingia Katika Uhalisi wa Neno la Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 539)

Ili mtu kufuatilia mabadiliko katika tabia ya maisha yake, njia ya kutenda ni rahisi. Ikiwa unaweza kufuata maneno halisi ya Roho Mtakatifu katika uzoefu wako wa utendaji, utaweza kutimiza mabadiliko katika tabia yako. Ikiwa utafuata na kutafuta chochote ambacho Roho Mtakatifu husema, wewe ni mtu anayemtii Yeye, na kwa njia hii utaweza kuwa na mabadiliko katika tabia. Tabia ya mwanadamu hubadilika na maneno halisi ya Roho Mtakatifu; ikiwa kila mara wewe hutetea uzoefu wako wa zamani na sheria, tabia yako haitabadilika. Ikiwa Roho Mtakatifu angezungumza leo kuwaambia watu wote waingie katika uzima wa ubinadamu wa kawaida lakini ukaendelea kulenga sehemu ya juu na kuchanganyikiwa kuhusu uhalisi na usiuchukulie kwa makini, utakuwa mtu ambaye haendelei na kazi Yake na hutakuwa mtu aliyeingia katika njia inayoongozwa na Roho Mtakatifu. Ikiwa tabia yako inaweza kubadilika au la inategemea na ikiwa unaweza kuendelea na maneno halisi ya Roho Mtakatifu au la na una ufahamu wa kweli. Hili ni tofauti na kile mlichoelewa awali. Kile ulichoelewa kuhusu mabadiliko katika tabia awali kilikuwa kwamba wewe, ambaye ni rahisi kuhukumu, kupitia kwa kufundishwa nidhamu na Mungu huzungumzi ovyo ovyo tena. Lakini hii ni hali moja tu ya mabadiliko, na hivi sasa suala muhimu zaidi ni kufuata uongozi wa Roho Mtakatifu. Unafuata chochote asemacho Mungu; unatii chochote asemacho Yeye. Watu hawawezi kubadilisha tabia yao wenyewe; lazima wapitie hukumu na kuadibu, mateso na usafishaji wa maneno ya Mungu, au kushughulikiwa, kufunzwa nidhamu, na kupogolewa na maneno Yake. Ni baada ya hapo tu ndipo wanaweza kutimiza utiifu na ibada kwa Mungu, na wasijaribu tena kumdanganya Yeye na kumshughulikia kwa uzembe. Ni kupitia kwa usafishaji wa maneno ya Mungu ndio watu hupata mabadiliko katika tabia. Ni wale tu wanaopitia mfichuo, hukumu, kufundishwa nidhamu, na kushughulikiwa kwa maneno Yake ambao hawatathubutu tena kufanya mambo kwa kutojali, na watakuwa watulivu na makini. Jambo muhimu sana ni kwamba wanaweza kutii neno la sasa la Mungu na kutii kazi ya Mungu, na hata kama hayalingani na fikira za binadamu, wanaweza kuweka kando fikira hizi na kutii kwa hiari. Mabadiliko katika tabia yalipozungumziwa hapo awali, imekuwa hasa kuhusu kujinyima mwenyewe, kuruhusu mwili kuteseka, kufunza nidhamu mwili wa mtu, na kujiondolea mapendeleo ya mwili—hii ni aina moja ya mabadiliko katika tabia. Watu sasa wanajua kwamba maonyesho halisi ya mabadiliko katika tabia ni kutii maneno halisi ya Mungu na vilevile kuweza kuwa na ufahamu halisi wa kazi Yake mpya. Kwa njia hii, ufahamu wa awali wa watu kumhusu Mungu, ambao ulipotoshwa na fikira zao wenyewe, na kutimiza ufahamu wa kweli wa na utiifu Kwake. Hii tu ndio maonyesho halisi ya mabadiliko katika tabia.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Ambao Tabia Zao Imebadilika ni Wale Ambao Wameingia Katika Uhalisi wa Neno la Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 540)

Kufuatilia kwa watu kuingia katika uzima kunalingana na maneno ya Mungu; imesemwa hapo awali kwamba kila kitu hutimizwa kwa sababu ya maneno Yake, lakini hakuna aliyeona ukweli. Ikiwa katika hatua hii utaingia katika uzoefu utakuwa wazi kabisa—huku ni kujenga msingi mzuri kwa majaribio ya siku za baadaye, na haijalishi anachosema Mungu, unatakiwa tu kuingia katika maneno Yake. Mungu anaposema Anaanza kuadibu watu, unakubali kuadibu Kwake. Mungu anapowauliza watu wafe, unakubali jaribio hilo. Ikiwa kila mara unaishi ndani ya matamshi Yake mapya zaidi, mwishowe maneno ya Mungu yatakukamilisha wewe. Kadri unavyoingia katika maneno ya Mungu, ndivyo utakavyokamilisha haraka zaidi. Kwa nini Ninawasiliana tena na tena na kuwaambia muelewe na kuingia katika maneno ya Mungu? Ni kwa kulenga tu kazi yako kwa maneno ya Mungu na kuyapitia na kuingia katika uhalisi wake ndipo Roho Mtakatifu atakuwa na nafasi ya kufanya kazi ndani yako. Kwa hiyo nyote ni washindani katika kila mbinu ya kazi ya Mungu, na haijalishi ikiwa mateso yenu yamekuwa makubwa au madogo mwishowe, nyote mtapata “hidaya”. Ili kutimiza ukamilifu wenu wa mwisho, lazima muingie katika maneno yote ya Mungu. Kwa Roho Mtakatifu kuwakamilisha watu, Hafanyi kazi kwa upande mmoja tu. Anahitaji ushirikiano wa watu; Anahitaji kila mtu ashirikiane Naye kwa makusudi. Haijalishi anachosema Mungu, unaingia tu katika maneno Yake—hii ni ya manufaa zaidi kwa maisha yenu. Kila kitu ni kwa ajili ya mabadiliko yenu katika tabia. Unapoingia katika maneno ya Mungu, moyo wako utasisimuliwa na Mungu, na utaweza kuelewa kila kitu ambacho Mungu anataka kutimiza katika hatua hii ya kazi, na utakuwa na nia ya kukitimiza. Katika wakati wa kuadibu, baadhi ya watu waliamini kwamba hiyo ilikuwa mbinu ya kazi na hawakuamini katika maneno ya Mungu. Kutokana na hilo, hawakupitia usafishaji na wakatoka katika wakati wa kuadibu bila kupata chochote na hawakuelewa chochote. Kuna baadhi ambao huingia kwa hakika katika maneno haya bila chembe ya shaka yoyote; wanasema kuwa maneno ya Mungu ni kweli na yasioweza kukosea na kwamba watu wanapaswa kuadibiwa. Wanang’ang’ana katika hili kwa kipindi fulani cha wakati na kuachilia siku zao za baadaye na majaliwa yao, na wanapotoka tu hapo tabia yao huwa imebadilika vilivyo na wao huwa na hata ufahamu wa kina zaidi kuhusu Mungu. Wale ambao wametoka katikati ya kuadibu wote huhisi kupendeza kwa Mungu, na wanajua kwamba hatua hiyo ya kazi ya Mungu ni upendo Wake mkuu ukija juu ya wanadamu, kwamba ni ushindi na wokovu wa upendo wa Mungu. Nao pia husema kwamba mawazo ya Mungu ni mazuri kila mara, na kila jambo ambalo Mungu hufanya ndani ya mwanadamu ni upendo, sio chuki. Wale wasioamini maneno ya Mungu au kuyachukulia kuwa muhimu hawakupitia usafishaji katika wakati wa kuadibu, na matokeo yake ni kwamba Roho Mtakatifu haandamani nao, na hawajapata chochote. Kwa wale walioingia katika wakati wa kuadibu, ingawa walipitia usafishaji, Roho Mtakatifu alikuwa anafanya kazi ndani yao kwa njia iliyofichika, na matokeo ni kwamba walipitia mabadiliko katika tabia yao ya maisha. Watu wengine huonekana kuwa wazuri sana kwa nje. Kila mara wao huwa na furaha, lakini hawajaingia katika hali hiyo ya usafishaji wa maneno ya Mungu na hawajabadilika kamwe, ambayo ni matokeo ya kutoamini maneno ya Mungu. Ikiwa huamini maneno Yake Roho Mtakatifu hatafanya kazi ndani yako. Mungu huonekana kwa wote wanaoamini maneno Yake; wale wanaoamini na kufahamu maneno Yake watapata upendo Wake!

Ili kuingia katika uhalisi wa maneno ya Mungu, unapaswa kupata njia ya kutenda na ujue jinsi ya kuweka maneno ya Mungu katika vitendo. Ni hivi tu ndivyo kutakuwa na mabadiliko katika tabia ya maisha yako, ni kwa njia hii tu ndiyo utaweza kukamilishwa na Mungu, na watu tu ambao wamekamilishwa na Mungu kwa njia hiyo ambao wanaweza kuwa sambamba na mapenzi Yake. Kupokea nuru mpya, lazima uishi ndani ya maneno Yake. Ikiwa umesisimuliwa na Roho Mtakatifu mara moja pekee, hiyo haitoshi kamwe—lazima uzame ndani zaidi. Wale ambao wamesisimuliwa mara moja pekee ari iliyo ndani yao imeamshwa hivi karibuni na wanakuwa radhi kutafuta, lakini hawawezi kudumisha hilo kwa kipindi kirefu, na lazima wapokee kila mara kusisimuliwa na Roho Mtakatifu. Kuna nyakati nyingi Nimetaja kuwa Natarajia kwamba Roho wa Mungu aweze kusisimua roho za watu, kwamba wafuatilie mabadiliko katika tabia ya maisha yao, na wanapotafuta kusisimuliwa na Mungu wafahamu udhaifu wao, na kwamba wakati wa kupitia maneno Yake, waondoe mambo machafu ndani yao (kujidai, kiburi, na fikira zao wenyewe, na kadhalika.) Usiamini kwamba kupokea tu kwa utendaji nuru mpya kunafaa—lazima pia uachane na vitu kutoka kwa hali mbaya. Hamhitaji tu kuingia kutoka kwa hali nzuri, lakini pia mnahitaji kujisafisha wenyewe kutoka kwa mambo yote machafu katika hali mbaya. Lazima ujichunguze siku zote na uone ni mambo yapi machafu bado yako ndani yako. Fikira za watu za kidini, makusudi, matarajio, kujidai, na kiburi yote ni mambo machafu. Jilinganishe na maneno yote ya Mungu ya ufunuo, na ujiangalie ndani yako kuona fikira zozote za kidini unazoshikilia, Ukizitambua kwa kweli tu ndipo unaweza kuziacha. Baadhi ya watu husema: “Inatosha sasa kufuata tu nuru ya kazi ya wakati huu ya Roho Mtakatifu bila kushughulika kuhusu kitu kingine chochote.” Basi ni vipi ambavyo utaondoa fikira zako za kidini zinapojitokeza? Unadhani ni rahisi hivyo kufuata maneno ya Mungu? Ndani ya maisha yako halisi, bado kuna mambo ya kidini yanayoweza kuwa ya kuvuruga, na mambo haya yanapojitokeza, yanaweza kuvuruga uwezo wako wa kukubali mambo mapya. Haya yote ni matatizo ambayo huwepo kwa kweli. Ikiwa utafuatilia tu maneno halisi ya Roho Mtakatifu huwezi kuridhisha mapenzi ya Mungu. Unapofuatilia nuru ya sasa ya Roho Mtakatifu, unapaswa kutambua ni fikira na makusudi gani ambayo bado unashikilia, ni kujidai gani kwa binadamu kupo hasa, na ni mienendo gani inakosa kumtii Mungu. Na baada ya kutambua mambo haya yote, lazima uachane nayo. Kukufanya wewe utupe matendo na mienendo yako ya awali yote ni kwa ajili ya kuyafuata maneno ya sasa ya Roho Mtakatifu. Kwa mabadiliko katika tabia, kwa upande mmoja, yanatimizwa kupitia kwa maneno ya Mungu, na kwa upande mwingine, yanahitaji watu washirikiane. Yaani, kazi ya Mungu na kutenda kwa watu vyote ni vya lazima.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Ambao Tabia Zao Imebadilika ni Wale Ambao Wameingia Katika Uhalisi wa Neno la Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 541)

Katika njia yako ya baadaye ya huduma, unawezaje kutimiza mapenzi ya Mungu? Jambo moja muhimu ni kufuatilia kuingia katika uzima, kufuatilia mabadiliko katika tabia, na kufuatilia kuingia kwa kina zaidi ndani ya ukweli—hii ndiyo njia ya kutimiza kufanywa mkamilifu na kupatwa na Mungu. Nyote mnapaswa kupokea agizo la Mungu, kwa hiyo ni nini hicho? Hii inahusiana na hatua inayofuata ya kazi, ambayo itakuwa kazi kuu zaidi itakayotekelezwa kotekote katika ulimwengu mzima. Kwa hiyo sasa mnapaswa kufuatilia mabadiliko katika tabia yenu ya maisha ili muwe kweli thibitisho la Mungu kupata utukufu kupitia kwa kazi Yake katika siku za baadaye, na kufanywa kuwa vielelezo vya kazi Yake ya siku za baadaye. Kazi yote ya leo inaweka msingi kwa ajili ya kazi ya siku za baadaye; ni kwa wewe kutumiwa na Mungu na ili uweze kuwa na ushuhuda Wake. Ikiwa hii ni chombo cha kazi yako, utaweza kupata uwepo wa Roho Mtakatifu. Kadri chombo cha kazi yako kilivyo juu, ndivyo itawezekana kwako wewe kukamilishwa zaidi. Kadri unavyofuatilia ukweli, ndivyo Roho Mtakatifu atafanya kazi zaidi. Kadri unavyokuwa na nguvu zaidi kwa kazi, ndivyo utakavyopata zaidi. Roho Mtakatifu huwakamilisha watu kulingana na hali yao ya ndani. Baadhi ya watu husema kwamba hawako radhi kutumiwa na Mungu au kukamilishwa na Yeye, kwamba itakuwa sawa alimuradi mwili wao unabaki salama na kamili na hawapitii msiba wowote. Watu wengine hawako radhi kuingia katika ufalme, lakini wako radhi kushuka katika shimo lisilo na mwisho. Katika hali hiyo, Mungu atakupa matamanio hayo. Chochote unachofuatilia, Mungu atakutimizia. Kwa hiyo unafuatilia nini sasa? Je, unafuatilia kukamilishwa? Matendo na mienendo yako ya sasa ni kwa ajili ya kufanywa mkamilifu na Mungu, kwa ajili ya kupatwa na Yeye? Ni lazima siku zote ujipime kwa njia hii katika maisha yako ya kila siku. Ukilenga moyo wako katika kufuatilia lengo moja, Mungu bila shaka atakukamilisha. Hii ni njia ya Roho Mtakatifu. Njia inayoongozwa na Roho Mtakatifu inapatikana kupitia kwa kutafuta kwa watu. Kadri unavyotamani kukamilishwa na kupatwa na Mungu, ndivyo Roho Mtakatifu atafanya kazi zaidi ndani yako. Kadri usivyotafuta, na kadri unavyokuwa mbaya na kukimbia, ndivyo zaidi Roho Mtakatifu anakosa nafasi za kufanya kazi. Roho Mtakatifu atakuacha polepole. Uko radhi kukamilishwa na Mungu? Uko radhi kupatwa na Mungu? Uko radhi kutumiwa na Mungu? Mnapaswa kufuatilia kufanya kila kitu kwa ajili ya kukamilishwa, kupatwa, na kutumiwa na Mungu, kuruhusu kila kitu katika ulimwengu kuona matendo ya Mungu yakifichuliwa ndani yenu. Miongoni mwa mambo yote, nyinyi ni watawala wa hayo, na miongoni mwa yote yaliyopo, mtamruhusu Mungu kupata ushuhuda Wake na utukufu Wake kwa sababu yenu—hii inaonyesha kwamba nyinyi ni kizazi kilichobarikiwa zaidi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Ambao Tabia Zao Imebadilika ni Wale Ambao Wameingia Katika Uhalisi wa Neno la Mungu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 542)

Kadiri unavyozingatia mapenzi ya Mungu, ndivyo unavyokuwa na mzigo zaidi; kadiri unavyokuwa na mzigo, ndivyo uzoefu wako utakuwa mwingi zaidi. Unapokuwa mzingatifu wa mapenzi ya Mungu, Mungu atakupa mzigo huu, na Mungu atakupa nuru ya mambo ambayo amekuaminia. Baada ya Mungu kukupa mzigo huu, utaangalia ukweli wa kipengele hiki unapokula na kunywa maneno ya Mungu. Kama una mzigo unaohusiana na hali ya maisha ya ndugu, huu ni mzigo ulioaminiwa kwako na Mungu, na sala zako za kila siku daima zitaubeba mzigo huu. Kile ambacho Mungu hufanya kimeaminiwa kwako, uko radhi kutekeleza kile ambacho Mungu anataka kufanya, na hivi ndivyo inavyomaanisha kuuchukua mzigo wa Mungu kama wako. Wakati huu, kula na kunywa kwako maneno ya Mungu kutalenga masuala katika vipengele hivi, na utafikiri: Nitayatatuaje masuala haya? Nitawaruhusu vipi ndugu kufunguliwa, wawe na furaha katika nafsi zao? Utalenga kusuluhisha masuala haya unapokuwa katika ushirika, utalenga kula na kunywa maneno yanayohusiana na masuala haya wakati ambapo unakula na kunywa maneno ya Mungu, utakuwa ukila na kunywa maneno ya Mungu na wakati huo ukiubeba mzigo huu, na utaelewa matakwa ya Mungu. Wakati huu, utakuwa wazi zaidi kuhusu njia ya kutembelea. Huku ni kupata nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu kunakosababishwa na mzigo wako, na huku ni Mungu kukupa mwongozo Wake. Kwa nini Nasema hili? Ikiwa huna mzigo, basi huzingatii unapokula na kunywa maneno ya Mungu; unapokuwa ukila na kunywa maneno ya Mungu na wakati huo kuubeba mzigo, unakuwa na uwezo wa kuelewa kiini cha maneno ya Mungu, kutafuta njia yako, na kuzingatia mapenzi ya Mungu. Kwa hivyo, unapaswa kumsihi Mungu akuongezee mizigo zaidi katika sala zako ili aweze kukuaminia mambo makuu zaidi, unaweza vyema zaidi kupata njia ya utendaji mbele, unakuwa wa kufaa zaidi katika kula na kunywa maneno ya Mungu, unakuwa na uwezo wa kuelewa kiini cha maneno Yake, na unaweza zaidi kukubali kuguswa hisi na Roho Mtakatifu.

Kula na kunywa maneno ya Mungu, kufanya maombi, kukubali mzigo wa Mungu, kukubali Anachokuaminia—haya yote ni kwa ajili ya kuwa na njia mbele yako. Kadiri unavyozidi kuwa na mzigo mwingi wa agizo la Mungu, ndivyo itakavyokuwa rahisi zaidi kwako kufanywa mtimilifu na Mungu. Wengine hawako tayari kushirikiana katika kumtumikia Mungu hata wakati ambapo wameshurutishwa; hao ni watu wavivu ambao hutamani kufurahia faraja. Kadiri unavyotakiwa kushirikiana katika kumhudumia Mungu, ndivyo utakavyopata uzoefu zaidi. Kwa sababu una mizigo zaidi na una uzoefu zaidi, utakuwa na nafasi zaidi ya kufanywa mtimilifu. Kwa hivyo, ikiwa unaweza kumhudumia Mungu kwa uaminifu utazingatia mzigo wa Mungu, na kwa njia hii utakuwa na nafasi nyingi zaidi za kufanywa mtimilifu na Mungu. Kundi kama hili la watu linafanywa kamilifu na Mungu wakati huu. Kadiri Roho Mtakatifu anavyokugusa hisia, ndivyo utakavyotenga muda zaidi wa kuzingatia mzigo wa Mungu, ndivyo utakavyofanywa mtimilifu na Mungu zaidi, ndivyo Mungu atakavyokupata zaidi, na mwishowe, utakuwa mtu anayetumiwa na Mungu. Sasa, kuna baadhi ambao hawalibebei kanisa mzigo. Watu hawa ni wazembe na wenye ubwege, na wanajali tu miili yao. Wao ni wenye ubinafsi sana na ni vipofu pia. Hutakuwa na mzigo wowote ikiwa huna uwezo wa kuona suala hili kwa dhahiri. Kadiri unavyozidi kuwa mzingatifu wa mapenzi ya Mungu, ndivyo mzigo ambao Mungu atakuaminia utakavyozidi kuwa mzito. Watu wenye ubinafsi hawako tayari kuyapitia mambo kama haya, na hawako radhi kulipa gharama, na kwa sababu hiyo watakosa nafasi ya kufanywa wakamilifu na Mungu. Je, si huku ni kujiumiza? Ikiwa wewe ni mtu ambaye ni mzingatifu wa mapenzi ya Mungu, utakuza mzigo wa kweli kwa ajili ya kanisa. Kwa kweli, badala ya kuuita huu mzigo wa kanisa, badala yake ni mzigo wa maisha yako, kwa sababu mzigo unaoukuza kwa ajili ya kanisa ni kwa ajili yako kufanywa mtimilifu na Mungu kwa kupitia uzoefu kama huu. Kwa hivyo, yeyote anayelibebea kanisa mzigo mzito zaidi na yeyote abebaye mzigo wa kuingia katika maisha watakuwa wale ambao wanafanywa watimilifu na Mungu. Je, umeona hili kwa dhahiri? Ikiwa kanisa unaloshiriki limetawanyika kama mchanga, lakini bado huna wahaka wala wasiwasi, na hata unajitia hamnazo wakati kina ndugu zako hawali au kunywa maneno ya Mungu kwa kawaida, basi huibebi mizigo yoyote. Watu kama hawa hawapendwi na Mungu. Wale wanaopendwa na Mungu huwa na shauku na kiu ya haki na ni wazingatifu wa mapenzi Yake. Kwa hivyo mnapaswa kuwa wazingatifu wa mzigo wa Mungu sasa. Hupaswi kusubiri tabia ya Mungu yenye haki ifunuliwe kwa watu wote kabla ya wewe kuwa mzingatifu wa mzigo wa Mungu. Je, si muda utakuwa umeshapita wakati huo? Sasa ni nafasi nzuri ya kufanywa mtimilifu na Mungu. Ukiruhusu nafasi hii ipotee, utajuta katika maisha yako yote, kama vile Musa alivyoshindwa kuingia katika nchi nzuri ya Kanani na alijuta katika maisha yake yote, akifa kwa majuto. Mara tu Mungu ameifichua tabia Yake yenye hakikwa watu wote, utajawa na majuto. Hata kama Mungu hakuadibu, utajiadibu kutokana na majuto yako mwenyewe. Wengine hawaridhishwi na hili. Ikiwa huamini, basi subiri uone. Watu wengine watatumika kama utimizaji wa maneno haya. Je, uko tayari kuwa sadaka ya dhabihu kwa maneno haya?

Usipotafuta fursa za kufanywa mtimilifu na Mungu, na usipojitahidi kuwa mbele katika kutafuta kwako kukamilishwa, basi hatimaye utajawa na majuto. Sasa ni fursa nzuri ya kufanywa mtimilifu—huu ni wakati mzuri. Usipotafuta kwa bidii kufanywa mtimilifu na Mungu, mara tu kazi Yake itakapokuwa imekamilika utakuwa umechelewa—utakuwa umekosa fursa hii. Bila kujali jinsi matarajio yako yalivyo makuu, ikiwa Mungu hatendi kazi tena, bila kujali jitihada unazotia, hutaweza kamwe kufanywa mtimilifu. Lazima uchukue fursa hii na ushirikiane kupitia huku Roho Mtakatifu akiwa anafanya kazi Yake kuu. Ukipoteza fursa hii, hutapewa nyingine bila kujali juhudi unazotia. Watu wengine hulia: “Mungu, niko radhi kuzingatia mzigo Wako, na niko radhi kuyaridhisha mapenzi Yako.” Ilhali hawana njia ya utendaji, kwa hivyo mizigo yao haitadumu. Ikiwa kuna njia, utapata uzoefu hatua kwa hatua, na itakuwa na muundo na ratiba. Baada ya mzigo mmoja kukamilika, mwingine unakabidhiwa kwako. Kupitia kuongezeka kwa uzoefu wako wa maisha, mizigo yako inakua pia. Watu wengine hubeba mzigo tu wanapoguswa hisia na Roho Mtakatifu, na baada ya kipindi cha muda, hawaubebi tena mizigo yoyote wakati ambapo hakuna njia ya utendaji. Huwezi kupata mizigo kwa kula na kunywa tu maneno ya Mungu. Kwa kuelewa ukweli mwingi, utapata umaizi, utakuwa na uwezo wa kutatua matatizo kwa kutumia ukweli, na ufahamu mzuri zaidi wa maneno ya Mungu na mapenzi ya Mungu. Kwa mambo haya, utakuza mizigo, na utaweza kufanya kazi nzuri mara tu unapokuwa na mzigo. Ikiwa una mzigo tu lakini huna ufahamu wa ukweli ulio wazi, hiyo pia haitasaidia. Lazima wewe mwenyewe uwe na uzoefu wa maneno ya Mungu, na ujue jinsi ya kuyatenda, na lazima kwanza uingie katika hali halisi kabla ya kuwakimu wengine, kuwaongoza wengine, na kufanywa mtimilifu na Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuwa Mzingatifu wa Mapenzi ya Mungu ili Upate Utimilifu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 543)

Kwa sasa, kazi ya Mungu ni kuwa kila mtu aingie kwenye njia sahihi, awe na maisha ya kawaida ya kiroho na uzoefu wa kweli, aongozwe na Roho Mtakatifu, na kwa msingi wa msingi huu, kukubali kile kilichowekwa na Mungu. Kusudi la kuingilia katika mafunzo ya ufalme ni kuruhusu kila neno lenu, kila tendo, kila mwendo na kila mawazo na wazo la kuingilia katika maneno ya Mungu, kuwawezesha kuguswa na Mungu mara nyingi zaidi na kukuza upendo kwa Mungu na kukuza mzigo mzito zaidi kwa ajili ya mapenzi ya Mungu, ili kila mtu awe kwenye njia ya kufanywa mtimilifu na Mungu, na kila mtu awe kwenye njia sahihi. Mara unapokuwa kwenye njia ya kufanywa mtimilifu na Mungu, basi uko kwenye njia sahihi. Wakati ambapo mawazo yako na dhana zako pamoja na malengo yako mabaya yanaweza kurekebishwa na unaweza kugeuka kutoka katika kuzingatia mwili wako hadi kuzingatia mapenzi ya Mungu, na wakati ambapo malengo mabaya yanajitokeza na unaweza kutosumbuliwa nayo na kutenda kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu—ikiwa unaweza kufikia mageuzo hayo, basi uko kwenye njia sahihi ya uzoefu wa maisha. Utendaji wako wa sala unapokuwa kwenye njia sahihi, hapo ndipo utakapoongozwa na Roho Mtakatifu katika sala zako. Kila wakati unapoomba, utaguswa hisia na Roho Mtakatifu; kila wakati utakapoomba, utakuwa na uwezo wa kutuliza moyo wako mbele ya Mungu. Kila wakati ambapo unakula na kunywa kifungu cha neno la Mungu, ikiwa unaweza kuelewa kazi ambayo anafanya sasa, na unaweza kujua jinsi ya kuomba, jinsi ya kushirikiana, na jinsi ya kuingia ndani, huku tu ndiko kufikia matokeo kutokana na kula na kunywa maneno ya Mungu. Unapoweza kupata njia ya kuingia kutoka kwa maneno ya Mungu, na unaweza kuelewa mienendo ya sasa ya kazi ya Mungu na mwenendo wa kazi ya Roho Mtakatifu kwa maneno Yake, hii inaonyesha kwamba wewe u kwenye njia sahihi. Ikiwa hujafahamu hoja muhimu unapokula na kunywa maneno ya Mungu, ikiwa huwezi kupata njia ya kutenda baada ya kula na kunywa maneno ya Mungu, inaonyesha kuwa bado hujui jinsi ya kula na kunywa maneno Yake na kwamba wewe hujapata njia au kanuni ya kula na kunywa maneno Yake. Ikiwa hamjaelewa kazi iliyofanywa na Mungu kwa sasa, hutaweza kukubali Agizo la Mungu. Kazi ambayo sasa inafanywa na Mungu ni ile wanapaswa kuingia ndani na kuwa na ujuzi kuhusu kwa sasa. Je, mnaelewa mambo haya?

Ukila na kunywa maneno ya Mungu kwa njia inayofaa, maisha yako ya kiroho yanakuwa ya kawaida, na bila kujali ni majaribu gani unayoweza kukabili, ni hali gani unazoweza kukumbana nazo, ni magonjwa gani ya kimwili unayoweza kuvumilia, ni mafarakano gani kutoka kwa ndugu au ni shida zipi za kifamilia unazoweza kupitia, unaweza kula na kunywa maneno ya Mungu kwa kawaida, kuomba kawaida, na kuendelea na maisha yako ya kanisa kawaida; ikiwa unaweza kutimiza haya yote, itaonyesha kuwa uko kwenye njia sahihi. Watu wengine ni dhaifu sana na hawana uvumilivu. Wanapokutana na kizuizi kidogo, wao hunung’unika na kuwa hasi. Ufuatiliaji wa ukweli unahitaji uvumilivu na uamuzi. Ikiwa huwezi kuyakidhi mapenzi ya Mungu wakati huu, lazima uweze kujidharau, kwa kimya kuwa na uamuzi ndani ya moyo wako kwamba utayaridhisha mapenzi ya Mungu wakati mwingine ujao. Ikiwa wakati huu hukuwa mzingatifu wa mzigo wa Mungu, unapaswa kuwa na azimio la kuasi dhidi ya mwili wakati ambapo unakabiliwa na kile kikwazo sawa katika siku zijazo, na kukusudia kuyaridhisha mapenzi ya Mungu. Hivi ndivyo unavyokuwa wa kustahili sifa. Watu wengine hata hawajui kama mawazo yao na dhana zao ni sawa—watu kama hao ni wapumbavu! Ikiwa ungependa kuuhini moyo wako na kuasi dhidi ya mwili, lazima kwanza ujue kama malengo yako ni sahihi, na hapo tu ndipo utaweza kuuhini moyo wako. Ikiwa hujui ikiwa nia yako ni sawa, unaweza kuuhini moyo wako na kuasi dhidi ya mwili? Hata ukiasi, unafanya hivyo kwa njia ya kuchanganyikiwa. Unapaswa kujua jinsi ya kuasi dhidi ya malengo yako potovu; hii ndiyo maana ya kuasi dhidi ya mwili. Unapojua kwamba malengo yako, mawazo yako na dhana zako si sahihi, unapaswa kukimbilia kurudi nyuma na kutembea kwenye njia sahihi. Tatua tatizo hili kwanza na ujifunze kufikia uingiaji kwa namna hii, kwa sababu unajua bora zaidi kama nia yako ni sawa au la. Wakati malengo mabaya yanarekebishwa na ni kwa ajili ya Mungu, basi umefikia lengo la kuuhini moyo wako.

Cha muhimu kwenu sasa ni kuwa na maarifa ya Mungu, kuwa na maarifa ya kazi ya Mungu, na lazima ujue jinsi Roho Mtakatifu anavyofanya kazi Yake kwa mwanadamu; huu ndio ufunguo wa kuingia kwenye njia sahihi. Itakuwa rahisi kwako kuingia kwenye njia sahihi baada ya kufahamu ufunguo huu. Unamwamini Mungu na kumjua Mungu, ambayo inaonyesha kwamba imani yako kwake ni ya kweli. Ikiwa utaendelea kupata uzoefu mpaka mwisho lakini bado huna uwezo wa kumjua Mungu, basi wewe hakika ni mtu anayempinga Mungu. Wale ambao huamini tu katika Yesu Kristo lakini hawaamini katika Mungu mwenye mwili wa leo wote wamehukumiwa. Wote ni Mafarisayo wa wakati wa sasa, kwa kuwa hawamtambui Mungu wa leo; wote wanampinga Mungu. Bila kujali imani yao katika Yesu ni ya kujitolea kiasi gani, itakuwa bure; hawatapata sifa ya Mungu. Wote wanaosema kuwa wanaamini katika Mungu ilhali hawana maarifa ya kweli ya Mungu katika mioyo yao ni wanafiki!

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuwa Mzingatifu wa Mapenzi ya Mungu ili Upate Utimilifu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 544)

Ili kutafuta kufanywa mtimilifu na Mungu, mtu lazima kwanza aelewe maana ya kufanywa mtimilifu na Yeye, ni hali gani ambazo mtu anapaswa kumiliki ili kufanywa mtimilifu, na kisha kutafuta njia ya kutenda mara mtu ameelewa mambo kama hayo. Mtu lazima awe na ubora fulani wa tabia ili afanywe mtimilifu na Mungu. Wengi wenu hawana ubora muhimu wa tabia, ambao unahitaji wewe kulipa gharama fulani na jitihada zako za nafsi. Kadiri ubora wako wa tabia unavyozidi kuwa wa chini, ndivyo lazima utie juhudi zaidi za binafsi. Kadiri ufahamu wako wa maneno ya Mungu ulivyo mkuu na kadiri unavyoyatia kwenye matendo, ndivyo unavyoweza kuingia kwenye njia ya kufanywa mtimilifu na Mungu haraka. Kupitia katika maombi, unaweza pia kufanywa mtimilifu katika maombi; pia unaweza kufanywa mtimilifu kwa kula na kunywa maneno ya Mungu, kuelewa kiini cha maneno hayo, na kuishi kwa kudhihirisha ukweli wa maneno ya Mungu, unaweza kufanywa kuwa mtimilifu. Kupitia uzoefu wa maneno ya Mungu kila siku, unapaswa kujua kile unachokosa ndani yako, na, zaidi ya hayo, unapaswa kujua dosari yako kubwa na upungufu wako, na umwombe na kumsihi Mungu. Kwa kufanya hivyo, utafanywa mtimilifu polepole. Njia za kufanywa mtimilifu: kuomba, kula na kunywa maneno ya Mungu, kuelewa kiini cha maneno ya Mungu, kuingia katika uzoefu wa maneno ya Mungu, kuja kujua kinachokosa ndani yako, kuitii kazi ya Mungu, kuzingatia mzigo wa Mungu na kuunyima mwili kwa kupitia upendo wako kwa Mungu, na kuwa na ushirika wa mara kwa mara na ndugu, ambayo yanaboresha uzoefu wako. Iwe ni maisha ya jumuiya au maisha yako binafsi, na iwe ni makusanyiko makubwa au madogo, yote yanaweza kukuwezesha kupata uzoefu na kupata mafunzo ili moyo wako uwe na utulivu mbele ya Mungu na kurudi kwa Mungu. Haya yote ni mchakato wa kufanywa mtimilifu. Kuyapitia maneno ya Mungu ambayo yamesemwa kunamaanisha kuwa na uwezo wa kwa kweli kuyaonja maneno ya Mungu na kuyaruhusu yaweze kuishi kwa kudhihirishwa ndani yako ili uwe na imani kubwa na upendo kwa Mungu. Kupitia njia hii, utaondoa tabia potovu ya kishetani polepole, utaachana na motisha isiyofaa polepole, na kuishi kwa kudhihirisha mfano wa mtu wa kawaida. Kadiri upendo kwa Mungu ndani yako unavyozidi kuwa mkuu—yaani, kadiri unavyozidi kufanywa mtimilifu na Mungu mara nyingi—ndivyo unayopotoshwa na Shetani kwa kiasi kidogo. Kupitia uzoefu wako wa vitendo, utaingia kwenye njia ya kufanywa mtimilifu polepole. Hivyo, ikiwa unataka kufanywa mtimilifu, kuzingatia mapenzi ya Mungu na kuyapitia maneno ya Mungu hasa ni muhimu sana.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuwa Mzingatifu wa Mapenzi ya Mungu ili Upate Utimilifu

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 545)

Kundi la watu ambao Mungu anataka kupata sasa ni wale ambao wanajitahidi kushirikiana na Mungu, wanaoweza kuiheshimu kazi Yake, na wanaoamini kuwa maneno Anayonena Mungu ni ya kweli, wale wanaoweza kuweka mahitaji ya Mungu katika vitendo. Ni wale walio na uelewa wa kweli katika mioyo yao. Ni hao ndio wanaoweza kukamilishwa, na wale ambao bila shaka watatembea katika njia ya ukamilisho. Wale wasio na uelewa wa wazi wa kazi ya Mungu, wale wasiokula na kunywa neno la Mungu, wale wasiotilia maanani neno la Mungu, na wale wasio na upendo wowote kwa Mungu katika mioyo yao. Wale walio na shaka na Mungu mwenye mwili, wasio na uhakika juu Yake, wasioyachukulia maneno ya Mungu kwa uzito na ambao daima humdanganya Mungu ni watu wanaompinga Mungu na ni wa Shetani; hakuna njia ya kukamilisha watu kama hao.

Kama unataka kufanywa mkamilifu, lazima kwanza uwe na neema ya Mungu, kwa sababu Mungu anawakamilisha wale ambao Amewapa neema, wale wanaoupendeza moyo Wake. Kama unataka kuupendeza moyo wa Mungu, lazima uwe na moyo unaotii kazi Yake yote, lazima ujitahidi kuufuata ukweli, na lazima uukubali uchunguzi wa Mungu katika kila kitu. Je, kila kitu unachofanya kimepitia uchunguzi wa Mungu? Je, nia yako iko sawa? Kama nia yako iko sawa, Mungu Atakubaliana nawe; kama nia yako sio sawa, hii inathibitisha kwamba kile moyo wako unapenda sio Mungu, ni mwili na Shetani. Kwa hiyo, lazima utumie maombi kama njia ya kukubali uchunguzi wa Mungu katika kila. Unapoomba, ingawa Mimi mwenyewe sisimami mbele yako, Roho Mtakatifu yuko pamoja nawe, na unaomba kwa Mimi mwenyewe na Roho wa Mungu. Kwa nini unaamini katika mwili huu? Unaamini kwa sababu Yuko na Roho wa Mungu. Je, ungemwamini mtu huyu ikiwa hangekuwa na Roho wa Mungu. Unapoamini katika mtu huyu, unaamini katika Roho wa Mungu. Unapomwogopa mtu huyu, unamwogopa Roho wa Mungu. Imani katika Roho wa Mungu ni imani katika mtu huyu, imani katika mtu huyu pia ni imani katika Roho wa Mungu. Unapoomba, unahisi Roho wa Mungu akiwa pamoja nawe, Mungu yuko mbele yako, kwa hivyo unamwomba Roho wa Mungu. Leo, watu wengi wanaogopa sana kuyaleta matendo yao mbele za Mungu, na ingawa unaweza kuudanganya mwili wa Mungu, huwezi kumdanganya Roho wa Mungu. Yale yote ambayo hayawezi kustahimili uchunguzi wa Mungu hayakubaliani na ukweli nayo lazima yawekwe kando, ama unatenda dhambi dhidi ya Mungu. Kwa hivyo, haijalishi kama ni wakati unaomba, unaponena na kushiriki na ndugu na dada zako, ama unapofanya wajibu wako na kufanya biashara yako, lazima uuweke moyo wako mbele za Mungu. Unapoitimiza kazi yako, Mungu yuko nawe, na bora nia yako iwe sawa, nayo iwe kwa ajili ya kazi ya nyumba ya Mungu, Atakubali kila kitu ufanyacho, kwa hivyo ni lazima uweke bidii kwa dhati kujishughulisha na kuitimiza kazi yako. Unapoomba, kama una upendo kwa Mungu katika moyo wako, na kama unatafuta utunzaji wa Mungu, ulinzi, na uchunguzi, kama haya ndio nia yako, maombi yako yatafaulu. Unapoomba katika mikutano, ndivyo unafaa kufungua moyo wako na kuomba Mungu, ambia Mungu kile kilicho moyoni mwako, na bila kuongea uongo, basi maombi yako yatafaulu. Kama unampenda Mungu moyoni mwako kwa dhati, basi fanya kiapo kwa Mungu: “Mungu, uliye mbinguni na nchini na vitu vyote, naapa Kwako: Hebu Roho Wako achunguze kila kitu ninachofanya na unilinde na kunijali kila wakati. Kinafanya kila kitu nifanyacho kiweze kusimama katika uwepo Wako. Ikiwa moyo wangu utawahi kukoma kukupenda ama kukusaliti Wewe, nipe adhabu Yako na laana kali zaidi. Usinisamehe katika dunia hii ama inayofuata!” Unaweza kuthubutu kula kiapo kama hiki? Kama huwezi, hii inadhibitisha kuwa wewe ni mwoga, na kwamba bado unajipenda. Je, mnao uamuzi huu? Kama kweli huu ndio uamuzi wako, lazima ufanye kiapo hiki. Kama una azimio la kula kiapo kama hiki, Mungu ataridhisha uamuzi wako. Unapoapa kwa Mungu, Mungu anasikiza. Mungu Anaamua kama wewe ni mwenye dhambi ama mwenye haki kupitia maombi yako na matendo yako. Huu sasa ndio mchakato wa kukukamilisha, na kama kweli unayo imani katika kukamilishwa kwako na Mungu, basi utaleta kila kitu ufanyacho mbele za Mungu na kuukubali uchunguzi Wake; ukifanya kitu kinachoasi sana ama ukimsaliti Mungu, basi atatimiza kiapo chako, na kisha haijalishi kitakachokufanyikia, iwe kuangamia ama kuadibu, ni shida yako mwenyewe. Ulikula kiapo, basi lazima ukitekeleze. Ukila kiapo, lakini ukose kukitekeleza, utaangamia. Kwa kuwa unakula kiapo, Mungu atatimiza kiapo chako. Wengine wanaogopa baada ya kuomba, na kusema, “Ee, jamani, nafasi yangu katika ufisadi imepotea, nafasi yangu kufanya mambo maovu imepotea, nafasi yangu ya kujiingiza katika ulafi wangu wa kidunia imepotea!” Watu hawa bado wanaipenda dunia na dhambi, nao ni hakika wataangamia.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu Anawakamilisha Wale Wanaoupendeza Moyo Wake

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 546)

Kuwa muumini katika Mungu kunamaanisha kuwa kila kitu ufanyacho lazima kiletwe mbele za Mungu na kupitia uchunguzi wa Mungu. Kama kile ufanyacho kinaweza kuletwa mbele za Roho wa Mungu lakini sio mbele ya mwili wa Mungu, hii inadhibitisha kuwa hujajitiisha katika uchunguzi wa Roho wa Mungu. Roho wa Mungu ni nani? Mtu huyu aliyeshuhudiwa na Mungu ni nani? Je, Wote si sawa? Wengi Huwaona kama nafsi mbili tofauti, wakiamini kwamba Roho wa Mungu ni Roho wa Mungu, naye mtu anayeshuhudiwa na Mungu ni binadamu tu. Lakini, je, hujakosea? Je, mtu huyu anafanya kazi kwa niaba ya nani? Wale ambao hawaujui mwili wa Mungu hawana uelewa ya kiroho. Roho wa Mungu na mwili Wake ni mmoja, kwa sababu Roho wa Mungu anatokea kwa mwili. Kama mtu huyu si mwema kwako, Roho wa Mungu Atakuwa mwema? Ni nini kimekuchanganya? Leo, hakuna asiyekubali uchunguzi wa Mungu anaweza kupokea idhini ya Mungu, na yeyote asiyemjua Mungu mwenye mwili hawezi kukamilishwa. Jiangalie nawe ujiulize kama kila kitu unachofanya kinaweza kuletwa mbele ya Mungu. Iwapo huwezi kuleta kila kitu unachofanya mbele za Mungu, hii inaonyesha kuwa wewe ni mtenda maovu. Je, watenda maovu wanaweza kufanywa wakamilifu? Kila kitu unachofanya, kila tendo, kila nia, na kila jibu lazima kiletwe mbele za Mungu. Hata maisha yako ya kawaida ya kiroho—maombi yako, ukaribu wako kwa Mungu, jinsi unavyokula na kunywa maneno ya Mungu, ushirika wako na kina ndugu zako na maisha yako ndani ya kanisa—na huduma yako katika ushirikiano wako vinaweza kuletwa mbele za Mungu ili Yeye avichunguze. Ni matendo kama hayo ndiyo yatakayokusaidia kustawi katika maisha. Mchakato wa kukubali uchunguzi wa Mungu ni mchakato wa kutakaswa. Kadri unavyoukubali uchunguzi wa Mungu, ndivyo unavyotakaswa zaidi na kadri unavyokubaliana na matakwa ya Mungu, ili kwamba hutajipata katika uasherati, na moyo wako utaishi katika uwepo wa Mungu; kadri unavyokubali uchunguzi wa Mungu, ndivyo unavyomuaibisha Shetani na kuutelekeza mwili. Kwa hivyo, kukubali uchunguzi wa Mungu ni njia ambayo watu wanafaa kutenda. Haijalishi kile unachokifanya, hata katika ushirika na ndugu na dada zako, ukiyaleta matendo yako mbele za Mungu na kutafuta uchunguzi wa Mungu, na kama nia yako ni kumtii Mungu Mwenyewe, unachotenda ni sahihi zaidi. Kama tu wewe ni mtu anayeleta kila kitu anachofanya mbele za Mungu na kukubali uchunguzi wa Mungu ndipo utakapokuwa mtu anayeishi kwa hakika katika uwepo wa Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu Anawakamilisha Wale Wanaoupendeza Moyo Wake

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 547)

Wale wasio na uelewa wa Mungu hawawezi kumtii Mungu kikamilifu. Watu kama hao ni wana wa uasi. Ni wenye kutaka makuu sana, na kunao uasi mwingi sana ndani mwao, kwa hivyo wanajitenga na Mungu na hawana nia ya kukubali uchunguzi wa Mungu. Watu kama hao hawawezi kufanywa wakamilifu na Mungu kwa urahisi. Watu wengine wana uchaguzi katika vile wanavyokula na kunywa neno la Mungu na katika hali yao ya kulikubali. Wanakubali sehemu za neno la Mungu zinazolingana na dhana zao wakikataa zile zisizokubaliana nazo. Je, hawamwasi na kumkataa Mungu kwa uwazi? Kama mtu anaamini katika Mungu kwa miaka mingi bila kupata uelewa hata kidogo wa Mungu, yeye ni mtu asiyeamini. Wale walio tayari kukubali uchunguzi wa Mungu ni wale wanao tafuta uelewano wa Mungu, walio tayari kukubali neno la Mungu. Ni wale ambao watapokea uridhi wa Mungu na mibaraka, nao ni wale waliobarikiwa zaidi. Mungu analaani wale wasio na nafasi Yake katika mioyo yao. Anawaadibu na kuwaacha watu kama hao. Kama humpendi Mungu, Mungu atakuacha, na kama hutasikia Ninachosema, Naahidi kwamba Roho wa Mungu atakuacha. Jaribu hili iwapo hauniamini! Leo Nawaambia njia ya kufuata, lakini kama utafanya hivyo ni juu yako. Kama huamini hilo, kama hulitii katika vitendo, utaona kama Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yako au la! Kama hautatafuta uelewano wa Mungu, Roho Mtakatifu hatafanya kazi ndani mwako. Mungu anafanya kazi ndani ya wale wanaotafuta na kulithamini neno la Mungu. Kadri unavyolithamini neno la Mungu, ndivyo Roho wa Mungu atakavyofanya kazi zaidi ndani mwako. Kadri mtu anavyolithamini neno la Mungu, ndivyo nafasi yake ya kukamilishwa na Mungu inavyokuwa kubwa. Mungu anawakamilisha wale ambao wanampenda Yeye kwa kweli. Anawakamilisha wale ambao mioyo yao iko katika amani mbele Yake. Ukiithamini kazi yote ya Mungu, yaani, ukiuthamini mwanga wa Mungu, ukiuthamini uwepo wa Mungu, ukithamini kujali na kuwekwa kwa Mungu, ukithamini jinsi neno la Mungu linakuwa ukweli wako na utoaji wa maisha, unafuata zaidi moyo wa Mungu. Ukiithamini kazi ya Mungu, ukiithamini kazi yote ambayo Mungu Amefanya juu yako, Mungu Atakubariki na kufanya kila kitu kilicho chako kuongezeka. Usipoithamini kazi ya Mungu, Mungu Hatafanya kazi kwako, Atakuruhusu tu nyakati za neema kwa imani yako, ama kukubariki na utajiri kidogo ama usalama kwa familia yako. Lazima utie bidii kuyafanya maneno ya Mungu kuwa ukweli wako ili umridhishe Yeye na kuupendeza moyo Wake, sio tu kutia bidii kufurahia neema ya Mungu. Hakuna kitu muhimu zaidi kwa waumini kama kupokea kazi ya Mungu, kupata ukamilifu, na kuwa wanaofanya mapenzi ya Mungu. Hili ndilo lengo unalofaa kufuata.

Kila ambacho mwanadamu alitafuta katika Enzi ya Neema sasa hakiko tena, kwa sababu kiwango cha juu cha ufuatiliaji; kinachofuatiliwa ni cha juu zaidi na cha vitendo zaidi, linalofuatiliwa linaweza kukidhi zaidi kile ambacho mwanadamu anahitaji ndani. Katika enzi zilizopita, Mungu hakuwafanyia watu kazi kama Afanyavyo leo; Hakunena nao sana jinsi Amenena leo, wala mahitaji Yake kwao hayakuwa ya juu kama ya leo. Kwamba Mungu anainua vitu hivi kwenu kunathibitisha kuwa nia ya mwisho ya Mungu, kumelengwa kwenu, kundi hili. Iwapo kweli unataka kufanywa mkamilifu na Mungu, basi lifuate kama lengo lako kuu. Haijalishi kama unakwenda huku na kule, unajitumia, unatenda wajibu, ama kama umepokea agizo la Mungu, nia daima ni kukamilishwa na kuridhisha mapenzi ya Mungu, kutimiza malengo haya. Mtu akisema kuwa hafuati kukamilishwa na Mungu ama kuingia katika maisha, lakini anafuata tu amani na furaha ya kimwili, basi yeye ni kipofu kabisa. Wale wasiofuata ukweli wa maisha, lakini wanafuata maisha ya milele pekee katika maisha ya baadaye na usalama katika maisha haya ni vipofu kabisa. Kwa hivyo, kila kitu ufanyacho lazima kifanywe kwa madhumuni ya kufanywa mkamilifu na kupatwa na Mungu.

Kazi ambayo Mungu anafanya kwa watu ni kuwakimu kulingana na mahitaji yao tofauti. Kadri maisha ya mwanadamu yalivyo makubwa, ndivyo anavyohitaji mengi zaidi, na ndivyo anavyotafuta zaidi. Kama katika awamu hii huna harakati, inathibitisha kuwa Roho Mtakatifu amekuacha. Wale wote wanaofuata maisha hawatawahi kuachwa na Roho Mtakatifu, wao hufuata kila wakati, wanatamani kila wakati. Watu kama hao hawatosheki kamwe kupumzika mahali walipo. Kila awamu ya kazi ya Roho Mtakatifu inalenga kufikia athari ndani mwako, lakini ukikua wa kutojali, kama hauhitaji tena, kama huikubali kazi ya Roho Mtakatifu, Yeye atakuacha. Watu wanahitaji uchunguzi wa Mungu kila siku, wanahitaji kupewa kwa wingi kutoka kwa Mungu kila siku. Je, watu wanaweza kuishi bila kula na kunywa neno la Mungu kila siku? Kama mtu anahisi kuwa hawezi kula ama kunywa neno la Mungu vya kutosha, kama analitafuta kila siku na kuwa na njaa na kiu kwake, Roho Mtakatifu atafanya kazi juu yao. Kadri mtu anavyotamani, ndivyo atakavyokuwa na ushirika kuhusu vitu vya hakika. Kadri mtu anavyoutafuta ukweli sana, ndivyo maisha yake yanavyokua kwa haraka, yakimpa uzoefu wa hali ya juu na kumfanya tajiri katika nyumba ya Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu Anawakamilisha Wale Wanaoupendeza Moyo Wake

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 548)

Roho Mtakatifu ana njia ya kutembea katika kila mtu, na humpa kila mtu fursa za kukamilishwa. Kupitia uhasi wako unajulishwa upotovu wako mwenyewe, na kisha kwa njia ya kuacha uhasi utapata njia ya kutenda, na huku ndiko kukamilishwa kwako. Aidha, kwa njia ya mwongozo na mwangaza wa siku zote wa mambo fulani chanya ndani yako, utatimiza shughuli yako kwa kuamili na kukua katika umaizi na kupata utambuzi. Wakati hali zako ni nzuri, uko tayari hasa kusoma neno la Mungu, na hasa tayari kumwomba Mungu, na unaweza kuyahusisha mahubiri unayoyasikia na hali zako mwenyewe. Kwa nyakati kama hizo Mungu hukupatia nuru na kukuangaza ndani, na kukufanya utambue mambo fulani ya kipengele chanya. Huku ni kukamilishwa kwako katika kipengele chanya. Katika hali hasi, wewe ni dhaifu na hasi, na huhisi kuwa huna Mungu moyoni mwako, lakini Mungu hukuangaza, akikusaidia kupata njia ya kutenda. Kutoka nje ya hili ni kupata ukamilisho katika hali chanya. Mungu anaweza kumkamilisha mwanadamu katika vipengele hasi na chanya. Inategemea kama unaweza kupata uzoefu, na kama wewe hufuatilia kukamilishwa na Mungu. Kama kwa hakika unatafuta kukamilishwa na Mungu, basi kilicho hasi hakiwezi kukufanya upoteze, lakini kinaweza kukuletea mambo ambayo ni halisi zaidi, na kinaweza kukufanya uweze zaidi kujua kile kilichopunguka ndani yako, uweze zaidi kufahamu sana hali zako halisi, na kuona kwamba mtu hana kitu, wala si kitu; kama hupitii majaribio, hujui, na daima utahisi kuwa wewe ni wa hadhi ya juu kuliko wengine na bora kuliko kila mtu mwingine. Kwa njia hii yote utaona kwamba yote yaliyotangulia yalifanywa na Mungu na kulindwa na Mungu. Kuingia katika majaribio hukuacha bila upendo au imani, huna sala, na huwezi kuimba nyimbo—na, bila kulitambua, katikati ya hili unakuja kujijua. Mungu ana njia nyingi za kumkamilisha mwanadamu. Yeye hutumia mazingira ya kila aina ili shughulikia tabia potovu ya mwanadamu, na hutumia vitu mbalimbali ili kumuweka mwanadamu wazi; katika suala moja Yeye humshughulikia mwanadamu, katika jingine Yeye humuweka mwanadamu wazi, na katika jingine Yeye humfichua mwanadamu, kuzichimbua na kuzifichua “siri” katika vina vya moyo wa mwanadamu, na kumwonyesha mwanadamu asili yake kwa kuzifichua hali zake nyingi. Mungu humkamilisha mwanadamu kupitia mbinu nyingi—kupitia ufunuo, ushughulikiaji, usafishwaji, na kuadibu—ili mwanadamu aweze kujua kwamba Mungu ni wa vitendo.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Wale Wanaolenga Kutenda tu Ndio Wanaoweza Kukamilishwa

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 549)

Ni nini mnachokitaka sasa? Kukamilishwa na Mungu, kumjua Mungu, kumpata Mungu—ama labda mnataka kujiendeza kama Petro wa miaka ya 90, ama kuwa na imani kubwa zaidi kuliko ile ya Ayubu, ama labda mnataka kuitwa wenye haki na Mungu na kufika mbele ya kiti cha Mungu cha enzi, ama kuweza kumridhisha Mungu duniani na kumtolea ushuhuda wa nguvu na mkubwa. Bila kujali kile mnachotaka, kwa jumla mnattaka kwa ajili ya kuokolewa na Mungu. Bila kujali iwapo unataka kuwa mtu mwenye haki ama unataka namna ya Petro, ama imani ya Ayubu, ama kukamilishwa na Mungu, yote ni kazi ambayo Mungu anamfanyia mwanadamu. Hivyo ni kusema, bila kujali unachokitafuta, yote ni kwa ajili ya kukamilishwa na Mungu, yote ni kwa ajili ya kupitia neno la Mungu, ili kuuridhisha moyo wa Mungu; yote ni kwa ajili ya kugundua uzuri wa Mungu, yote ni kwa ajili ya kutafuta njia ya kutenda katika uzoefu halisi kwa lengo la kuweza kuiacha tabia yako ya uasi, kufanikisha hali ya kawaida ndani yako mwenyewe, kuweza kufuata kabisa mapenzi ya Mungu, kuwa mtu sahihi, na kuwa na nia sahihi katika kila kitu unachokifanya. Sababu ya wewe kupitia vitu hivi vyote ni kufikia kumjua Mungu na kufanikisha ukuaji wa maisha. Ingawa kile unachokipitia ni neno la Mungu, na kile unachokipitia ni matukio halisi, watu, mambo, na vitu katika mazingira yako, hatimaye unaweza kumjua Mungu na kukamilishwa na Mungu. Kutafuta kuitembea njia ya mtu mwenye haki au kutafuta kutia neno la Mungu katika vitendo, hizi ndizo njia. Kumjua Mungu na kukamilishwa na Mungu ndiyo hatima. Kama unatafuta sasa kukamilishwa na Mungu, au kumshuhudia Mungu, kwa ujumla, hatimaye ni ili kumjua Mungu; ni ili kwamba kazi Anayoifanya ndani yako sio ya bure, ili hatimaye uje kuujua uhalisi wa Mungu, kujua ukuu Wake, vivyo hivyo hata zaidi kuujua unyenyekevu wa Mungu na hali Yake ya kutoonekana, na kujua kazi nyingi ambazo Mungu hufanya ndani yako. Mungu amejinyenyekeza Mwenyewe kwa kiwango fulani, kufanya kazi Yake katika watu hawa wachafu na wapotovu, na kukikamilisha kikundi hiki cha watu. Mungu hakupata mwili tu ili kuishi na kula kati ya watu, kuwalisha watu, kutoa wanachohitaji watu. Jambo muhimu zaidi ni kwamba Yeye hufanya kazi Yake kubwa ya wokovu na ushindi kwa watu hawa walio na upotovu usiovumilika. Alikuja katika kiini cha joka kubwa jekundu ili kuwaokoa watu hawa wapotovu mno, ili watu wote waweze kubadilishwa na kufanywa wapya. Tatizo kubwa ambalo Mungu huvumilia siyo tu shida ambayo Mungu mwenye mwili huvumilia, lakini hasa ni kwamba Roho wa Mungu hupitia udhalilishaji uliokithiri—Yeye hujinyenyekeza na kujificha Mwenyewe sana kiasi kwamba Yeye huwa mtu wa kawaida. Mungu alipata mwili na kuchukua mfano wa mwili ili watu waone kwamba Ana maisha ya kawaida ya binadamu, na kwamba ana mahitaji ya kawaida ya binadamu. Hili linatosha kuthibitisha kwamba Mungu amejinyenyekeza Mwenyewe kwa kiwango fulani. Roho wa Mungu hufanyika katika mwili. Roho Wake ni wa juu sana na mkuu, lakini Yeye huchukua mfano wa mwanadamu wa kawaida, wa mwanadamu asiye muhimu ili kufanya kazi ya Roho Wake. Ubora wa tabia, umaizi, hisi, ubinadamu, na maisha ya kila mmoja wenu vinaonyesha kwamba hamfai kweli kupokea kazi ya Mungu ya aina hii. Hakika hamfai kumruhusu Mungu kuvumilia shida kama hiyo kwa ajili yenu. Mungu ni mkubwa sana. Yeye ni mkuu sana, na watu ni duni sana na wa hali ya chini, lakini Yeye bado huwafanyia kazi. Yeye hakupata mwili tu ili kuwaruzuku watu, kuzungumza na watu, Yeye hata huishi pamoja na watu. Mungu ni mnyenyekevu sana, wa hupendeka sana. Ikiwa punde upendo wa Mungu unapotajwa, mara tu neema ya Mungu inapotajwa, unatoa machozi unapotamka sifa kubwa, ukifika katika hali hii, basi una maarifa ya kweli ya Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Wale Wanaolenga Kutenda tu Ndio Wanaoweza Kukamilishwa

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 550)

Kuna mchepuko katika kutafuta kwa watu siku hizi; wao hutafuta tu kumpenda Mungu na kumridhisha Mungu, lakini hawana maarifa yoyote juu ya Mungu, na wametelekeza nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu ndani yao. Hawana maarifa ya kweli ya Mungu kama msingi. Kwa njia hii wanapoteza nguvu wakati uzoefu wao unapoendelea. Wale wote wanaotafuta kuwa na maarifa ya kweli ya Mungu, ingawa hapo zamani hawakuwa katika hali nzuri, na walielekea kwa uhasi na udhaifu, na mara nyingi walitoa machozi, wakakata tamaa, na kupoteza tumaini—sasa, wakati wanapopata uzoefu zaidi, hali zao zinaimarika. Baada ya kushughulikiwa na kuvunjwa, na baada ya kupitia mfululizo mmoja wa majaribu na usafishaji, walikuwa na maendeleo makubwa. Hizo hali hasi zinapunguka, na kumekuwa na mabadiliko kiasi katika tabia zao za maisha. Huku wakipitia majaribu zaidi, mioyo yao inaanza kumpenda Mungu. Kuna kanuni kwa kukamilishwa kwa watu na Mungu, ambayo ni kwamba Yeye hukupa nuru kwa kutumia sehemu yako inayofaa ili uwe na njia ya kutenda na unaweza kujitenga na hali zote hasi, ikisaidia roho yako kupata uhuru, na ikikufanya uweze kumpenda zaidi. Kwa njia hii, unaweza kuiacha tabia potovu ya Shetani. Wewe huna hila na uko wazi, ukiwa tayari kujijua nakutia ukweli katika vitendo. Mungu hakika atakubariki, kwa hiyo unapokuwa dhaifu na hasi, Yeye hukupa nuru maradufu, Akikusaidia kujijua zaidi, kuwa tayari kujitubia, na kuweza zaidi kutenda mambo ambayo unapaswa kuyatenda. Ni kwa njia hii tu ambapo moyo wako unahisi amani na utulivu. Mtu ambaye kwa kawaida huzingatia kumjua Mungu, ambaye huzingatia kujijua, ambaye huzingatia vitendo vyake mwenyewe ataweza kupokea kazi ya Mungu mara kwa mara, mara kwa mara kupokea mwongozo na nuru kutoka kwa Mungu. Hata ingawa yuko katika hali hasi, anaweza kugeuka mara moja, iwe ni kwa sababu ya matendo ya dhamiri au kwa sababu ya nuru kutoka kwa neno la Mungu. Mabadiliko ya tabia ya mtu hufanikishwa daima anapojua hali yake mwenyewe halisi na kujua tabia na kazi ya Mungu. Mtu ambaye yuko tayari kujijua na yuko tayari kuwasiliana ataweza kutekeleza ukweli. Aina hii ya mtu ni mtu ambaye ni mwaminifu kwa Mungu, na mtu ambaye ni mwaminifu kwa Mungu ana ufahamu wa Mungu, uwe ni wa kina au wa juu juu, haba au maridhawa. Hii ni haki ya Mungu, na ni kitu ambacho watu hupata, ni faida yao wenyewe. Mtu ambaye ana maarifa ya Mungu ni yule ambaye ana msingi, ambaye ana maono. Mtu wa aina hii ana hakika kuhusu mwili wa Mungu, na ana hakika kuhusu neno la Mungu na kazi ya Mungu. Bila kujali jinsi Mungu hufanya kazi au kuzungumza, au jinsi watu wengine husababisha vurugu, anaweza kushikilia msimamo wake, na kuwa shahidi kwa Mungu. Kadiri mtu alivyo katika njia hii ndivyo anavyoweza kutekeleza zaidi ukweli anaouelewa. Kwa sababu daima anatenda neno la Mungu, yeye hupata ufahamu zaidi wa Mungu, na analo azimio la kuwa shahidi kwa Mungu milele.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Wale Wanaolenga Kutenda tu Ndio Wanaoweza Kukamilishwa

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 551)

Kuwa na utambuzi, kuwa na utii, na kuwa na uwezo wa kubaini mambo ili uwe hodari katika roho ina maana kuwa maneno ya Mungu yanakuangaza na kukupa nuru ndani mara tu unapokabiliwa na kitu fulani. Huku ni kuwa hodari katika roho. Kila kitu ambacho Mungu hufanya ni kwa ajili ya kusaidia kufufua roho za watu. Kwa nini Mungu daima husema kuwa watu ni wa kujijali na wajinga? Ni kwa sababu roho za watu zimekufa, na wamekuwa wa kutojali kiasi kwamba hawajui kabisa mambo ya roho. Kazi ya Mungu ni kuyafanya maisha ya watu yaendelee na ni kusaidia roho za watu zichangamke, ili waweze kubaini mambo ya roho, na wao daima waweze kumpenda Mungu mioyoni mwao na kumridhisha Mungu. Ufikaji mahali hapa huonyesha kwamba roho ya mtu imefufuliwa, na wakati mwingine atakapokabiliwa na kitu fulani, anaweza kuonyesha hisia mara moja. Yeye huitikia mahubiri, na kuonyesha hisia haraka kwa hali mbalimbali. Huku ndiko kufanikisha uhodari wa roho. Kuna watu wengi ambao wana majibu ya haraka kwa tukio la nje, lakini mara tu kuingia katika uhalisi au mambo kinaganaga ya roho yanapotajwa, wao huwa wa kutojali na wajinga. Wao huelewa kitu tu kikiwa ni dhahiri. Hizi zote ni ishara za kuwa wa kutojali kiroho na mjinga, za kuwa na uzoefu kidogo wa mambo ya roho. Watu wengine ni hodari wa roho na wana utambuzi. Mara tu wanaposikia maneno yanayoonyesha hali zao, wanaharakisha kuyaandika. Mara wanaposikia maneno kuhusu kanuni za kutenda, wanaweza kuyakubali na kuyatumia katika uzoefu wao unaofuata. Huyu ni mtu ambaye ni hodari katika roho. Kwa nini anaweza kuonyesha hisia haraka hivyo? Ni kwa sababu yeye hulenga mambo haya katika maisha ya kila siku. Anaposoma maneno ya Munu, anaweza kuzipima hali zake kwa kuyatumia na kujitafakari. Anaposikia ushirika na mahubiri na kusikia maneno yanayoleta nuru na mwanga, anaweza kuyapokea mara moja. Ni sawa na kumpa mtu mwenye njaa chakula; anaweza kula mara moja. Ukimpa chakula mtu asiye na njaa, hana haraka kuonyesha hisia. Daima wewe humwomba Mungu, na kisha unaweza kuonyesha hisia mara moja unapokabiliwa na kitu fulani: kile Mungu huhitaji katika jambo hili, na jinsi unavyopaswa kutenda. Mungu alikuongoza juu ya suala hili mara ya mwisho; unapokabiliwa na kitu cha aina hii leo, kwa kawaida utajua jinsi ya kutenda kwa namna inayoridhisha moyo wa Mungu. Ikiwa unatenda daima kwa njia hii na daima upate uzoefu kwa njia hii, wakati fulani utakuwa stadi kwayo. Wakati unasoma neno la Mungu unajua ni mtu wa aina gani Mungu anamzungumzia, unajua ni aina gani ya hali za roho Anayozungumzia, na unaweza kuelewa jambo muhimu na kulitia katika vitendo; hii inaonyesha kuwa unaweza kupata uzoefu. Kwa nini watu wengine hawana jambo hili? Ni kwa sababu hawaweki jitihada nyingi katika kipengele cha kutenda. Ingawa wako tayari kutia ukweli katika vitendo, hawana umaizi wa kweli katika utondoti wa huduma, katika utondoti wa ukweli katika maisha yao. Wanachanganyikiwa jambo linapotokea. Kwa njia hii, unaweza kupotoshwa nabii wa uongo au mtume wa uongo anapokuja. Lazima ushiriki mara nyingi kuhusu maneno na kazi ya Mungu—ni kwa njia hii tu ndiyo utaweza kuuelewa ukweli na kukuz utambuzi. Ikiwa huelewi ukweli, basi hutakuwa na utambuzi. Kwa mfano, kile Mungu husema, jinsi Mungu hufanya kazi, yale yaliyo matakwa Yake kwa watu, ni watu wa namna gani unapaswa kuwasiliana nao, na ni watu wa aina gani unaopaswa kuwakataa—ni lazima ushiriki mara nyingi kuhusu mambo haya. Ukipitia neno la Mungu kwa njia hii daima, utaelewa ukweli na uelewe vizuri vitu vingi, na utakuwa na utambuzi pia. Ni nini kufundishwa nidhamu na Roho Mtakatifu, ni nini lawama inayotokana na nia ya mwanadamu, ni nini mwongozo kutoka kwa Roho Mtakatifu, ni nini mpango wa mazingira, ni nini maneno ya Mungu yanatolea nuru ndani, kama huna uhakika juu ya mambo haya, hutakuwa na utambuzi. Unapaswa kujua kile ambacho huja kutoka kwa Roho Mtakatifu, ni nini tabia ya uasi, jinsi ya kulitii neno la Mungu, na jinsi ya kuacha uasi wako mwenyewe; ikiwa una ufahamu wa vitendo wa mambo haya, utakuwa na msingi; kitu kinapotendeka, utakuwa na ukweli unaofaa wa kutumia kukipima na maono yanayofaa kama msingi. Utakuwa na kanuni katika kila kitu unachofanya, na utaweza kutenda kulingana na ukweli. Halafu maisha yako yatajazwa na nuru ya Mungu, yatajazwa na baraka za Mungu. Mungu hatamtendea vibaya mtu yeyote ambaye humtafuta kwa kweli. Hatamtendea vibaya mtu yeyote ambaye huishi kwa kumdhihirisha na ambaye hushuhudia kwa ajili Yake, na hatamlaani mtu yeyote ambaye kwa kweli anaweza kuona kiu ya ukweli. Ikiwa, unapokula na kunywa maneno ya Mungu, unaweza kuzingatia hali yako mwenyewe ya kweli, kuzingatia vitendo vyako mwenyewe, na kuzingatia ufahamu wako mwenyewe, basi, unapokabiliwa na tatizo, utapokea nuru na utapata ufahamu wa utendaji. Kisha utakuwa na njia ya kutenda na utakuwa na utambuzi kwa kila kitu. Mtu aliye na ukweli si rahisi kudanganywa, na rahisi kutenda kwa vurugu au kutenda kwa kupita kiasi. Kwa sababu ya ukweli amelindwa, na pia kwa sababu ya ukweli yeye hupata ufahamu zaidi. Kwa sababu ya ukweli ana njia zaidi za kutenda, hupata fursa zaidi za Roho Mtakatifu kufanya kazi ndani yake, na hupata fursa zaidi za kukamilishwa.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Wale Wanaolenga Kutenda tu Ndio Wanaoweza Kukamilishwa

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 552)

Kunacho kigezo cha kufikiwa iwapo utakamilishwa. Kupitia kwa uamuzi wako, ustahimilivu wako, na dhamiri yako, na kupitia ufuatiliaji wako, utaweza kupitia maisha na kutimiza mapenzi ya Mungu. Haya ndiyo kuingia kwako na kile kinachohitajika kwenye njia ya kuwa mkamilifu. Kazi ya kuwa mkamilifu inaweza kufanywa kwa watu wote. Yeyote anayemfuatilia Mungu anaweza kufanywa kuwa mkamilifu na anayo fursa na sifa za kufanywa kuwa mkamilifu. Hakuna sheria ngumu na ya haraka hapa. Ikiwa mtu anaweza kukamilishwa hasa kunategemea kile anachofuatilia. Watu wanaopenda ukweli na walio na uwezo wa kuishi kwa kudhihirisha ukweli bila shaka wanaweza kufanywa kuwa wakamilifu. Watu wasioupenda ukweli hawasifiwi na Mungu; hawamiliki maisha ambayo Mungu anadai, na hawawezi kufanywa kuwa kamilifu. Kazi ya kufanywa kuwa mkamilifu ni kwa minajili tu ya kuwamiliki watu, na wala si hatua katika kupigana na Shetani; kazi ya ushindi ipo tu kwa minajili ya kupigana na Shetani, kumaanisha kwamba kutumia ushindi wa mwanadamu ili kumzidi Shetani nguvu. Sehemu hii ya nyuma ndiyo kazi kuu, kazi mpya zaidi ambayo haijawahi kufanywa katika enzi zote. Mtu anaweza kusema kwamba shabaha ya hatua hii ya kazi kimsingi ni kuwashinda watu wote ili kuweza kumshinda Shetani. Kazi ya kufanya watu kuwa wakamilifu—hiyo si kazi mpya. Kazi yote katika kipindi ambapo Mungu anafanya kazi katika mwili inayo shabaha yake kuu kama ushindi wa watu. Hii ni sawa na ile Enzi ya Neema. Ukombozi wa wanadamu wote kupitia kwa kusulubishwa ndiyo iliyokuwa kazi kuu. “Kuwapata watu” kulikuwa nyongeza katika kazi ya mwili na kulifanywa tu baada ya kusulubishwa. Wakati Yesu alipokuja na kufanya kazi Yake, shabaha Yake ilikuwa hasa kutumia kusulubishwa Kwake kushinda utumwa wa kifo na Kuzimu, kuweza kushinda ushawishi wa Shetani, kumaanisha kumshinda Shetani. Ilikuwa tu baada ya kusulubishwa kwa Yesu ndipo Petro alipoanza hatua kwa hatua kushika njia ya kuwa ukamilifu. Bila shaka alikuwa miongoni mwa wale waliomfuata Yesu wakati Yesu alipokuwa akifanya kazi, lakini hakufanywa kuwa mkamilifu wakati huo. Badala yake, ilikuwa ni baada ya Yesu kumaliza kazi Yake ndipo Petro alipoanza kuelewa taratibu ukweli na kisha akafanywa kuwa mkamilifu. Mungu mwenye mwili huja ulimwenguni tu kukamilisha hatua muhimu na ya maana sana ya kazi katika kipindi kifupi cha muda, si kuishi kwa kipindi kirefu miongoni mwa watu ulimwenguni na kuwafanya kuwa kamili kwa makusudi. Huwa hafanyi kazi hiyo. Hasubirii mpaka wakati ule ambao binadamu amefanywa kuwa mkamilifu kabisa ili kuhitimisha kazi Yake. Hiyo siyo shabaha na umuhimu wa kupata mwili Kwake. Yeye huja tu ili kufanya kazi ya kipindi kifupi ya kuwaokoa binadamu, na wala si kufanya ile kazi ya kipindi kirefu sana ya kuwafanya binadamu kuwa wakamilifu. Kazi ya kuwaokoa binadamu ni ya uwakilishi, inayoweza kuzindua enzi mpya na inaweza kukamilishwa katika kipindi kifupi cha muda. Lakini kuwafanya binadamu kuwa wakamilifu kunahitaji kuwaleta binadamu hadi kiwango fulani na ni kazi inayoweza kuchukua muda mrefu. Kazi hii lazima ifanywe na Roho wa Mungu, lakini inafanywa kwa msingi wa ukweli unaozungumzwa wakati wa kazi Yake akiwa mwili. Au aidha Yeye huwainua mitume kufanya kazi ya uchungaji ya kipindi kirefu, ili kufikia shabaha Yake ya kuwafanya binadamu kuwa wakamilifu. Mungu mwenye mwili hafanyi kazi hii. Huongea tu kuhusu njia ya maisha ili watu waweze kuelewa na kuwapatia tu binadamu ukweli, badala ya kuandamana na mwanadamu bila kusita katika kutenda ukweli kwani kufanya hivyo hakumo ndani ya huduma Yake. Kwa hivyo Hatakuwa akiandamana na mwanadamu mpaka siku ile ambayo mwanadamu ataelewa kabisa ukweli na kupata kabisa ukweli. Kazi Yake akiwa mwili inahitimishwa wakati mwanadamu anapoingia rasmi kwenye njia sahihi ya kumwamini Mungu, wakati mwanadamu anapoingia kwenye njia sahihi ya kufanywa kuwa mkamilifu. Hapa, bila shaka ndipo pia wakati ambapo atakuwa Ameshinda Shetani kabisa na kuutawala ulimwengu. Hajali kama mwanadamu hatimaye ameingia ukweli wakati huo, wala kujali kuhusu kama maisha ya binadamu ni makubwa au madogo. Hakuna kati ya hayo ambayo Yeye akiwa katika mwili anafaa kusimamia; hakuna kati ya hayo iko ndani ya huduma ya Mungu mwenye mwili. Punde Anapomaliza kazi aliyonuia, Yeye huhitimisha kazi Yake katika mwili. Kwa hiyo, kazi ambayo Mungu mwenye mwili anafanya ni kazi ile tu ambayo Roho wa Bwana hawezi kufanya moja kwa moja. Aidha, ni ile kazi ya wokovu ya kipindi kifupi, na wala si kazi ya kipindi kirefu hapa ulimwenguni.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Waliokamilishwa Pekee Ndio Wanaoweza Kuishi Maisha Yenye Maana

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 553)

Kazi hii miongoni mwenu inatekelezwa kwenu kulingana na ile kazi inayohitajika kufanywa. Baada ya ushindi wa watu hawa, kundi la watu litafanywa kuwa kamilifu. Kwa hivyo, kazi nyingi ya sasa pia inatayarisha shabaha ya kuwafanya kuwa wakamilifu, kwa sababu wapo wengi sana walio na hamu ya ukweli ambao wanaweza kufanywa kuwa wakamilifu. Kama kazi ya kushinda ilifaa kutekelezwa kwenu na baadaye kusiwe kazi ya ziada kufanywa, basi ni kwamba baadhi ya wale wanaotamani ukweli hawangepata? Kazi ya sasa inalenga kufungua njia ya kuwafanya watu kuwa wakamilifu baadaye. Ingawa kazi Yangu ni ya ushindi tu, njia ya maisha iliyotamkwa na Mimi hata hivyo ni inatayarisha kuwafanya watu kuwa wakamilifu baadaye. Kazi inayokuja baada ya ushindi inaweka msingi wa kukamilisha hukukamili, na hivyo basi ushindi unafanywa ili kuweka msingi wa kule kufanywa kuwa wakamilifu. Mwanadamu anaweza kufanywa kuwa mkamilifu baada ya kushindwa tu. Sasa hivi kazi kuu ni kushinda; baadaye wale wanaotafuta na kutamani ukweli watafanywa kuwa wakamilifu. Kufanywa kuwa mkamilifu kunahusisha dhana nzuri za watu kuhusu maisha: Je, unao moyo unaompenda Mungu? Kina cha yale umeyapitia ulipotembea kwenye njia hii ni kipi? Upendo wako wa Mungu ni safi vipi? Kutenda kwako ukweli ni sahihi vipi? Ili kufanywa kuwa mkamilifu, lazima mtu awe na maarifa ya kimsingi ya vipengele vyote vya ubinadamu. Hili ni hitaji la kimsingi. Wale wote wasioweza kufanywa kuwa wakamilifu baada ya kushindwa hugeuka na kuwa vyombo vya huduma na hatimaye bado watatupwa kwenye ziwa la moto na kibiriti na bado wataanguka ndani ya shimo lisilokuwa na mwisho kwa sababu ya tabia yao ambayo haijabadilika na wangali ni wa Shetani. Mtu akikosa sifa za kukamilishwa, basi yeye ni bure—hana manufaa, ni chombo, kitu ambacho hakiwezi kustahimili majaribio ya moto! Upendo wako wa Mungu sasa hivi ni mkubwa kiasi gani? Chuki yako kwako ni kubwa kiasi gani? Je, kweli unamjua Shetani kwa kina kiasi gani? Umekaza uamuzi wenu? Maisha yako katika ubinadamu yamethibitiwa vyema? Maisha yako yamebadilika? Unayaishi maisha mapya? Mtazamo wenu wa maisha umebadilika? Kama mambo haya hayajabadilika, huwezi kufanywa kuwa mkamilifu hata kama hurudi nyuma; badala yake, wewe umeshindwa tu. Wakati ukifika wa kukujaribu, unakosa ukweli, ubinadamu wako si wa kawaida, na wewe ni wa kiwango cha chini kama mnyama. Umeshindwa tu, umekuwa tu mtu aliyeshindwa tu na Mimi. Kama vile tu, punde punda anapopitia mjeledi wa bwana wake, yeye huwa na woga na hofu ya kufanya chochote kila wakati anapomwona bwana wake, ndivyo pia wewe ulivyo kama punda huyo aliyedhibitiwa. Kama mtu anakosa vipengele hivyo vizuri na badala yake yeye ni wa kutoonyesha hisia na mwenye woga, mwepesi kutishwa na wa kusitasita katika mambo yote, asiyeweza kutambua chochote kwa njia iliyo wazi, asiyeweza kukubali ukweli, ambaye bado hana njia ya kutendea, na hata zaidi asiye na moyo wa upendo wa Mungu—kama mtu hana uelewa wa namna ya kumpenda Mungu, namna ya kuishi maisha yenye maana, au namna ya kuwa mtu halisi—mtu kama huyu anawezaje kumshuhudia Mungu? Hii inaonyesha kwamba maisha yako yanayo thamani ndogo na wewe si kingine ila punda aliyedhibitiwa. Wewe umeshindwa, lakini hilo linamaanisha tu kwamba umelikataa lile joka kubwa jekundu na umekataa kumilikiwa nalo; hiyo inamaanisha kwamba wewe unaamini kuwa kunaye Mungu, unataka kutii mipango yote ya Mungu na huna malalamiko yoyote. Lakini je, katika vipengele vyema, unaweza kuishi kwa kudhihirisha neno la Mungu na kumbainisha Mungu? Ikiwa huna lolote kati ya haya, inamaanisha kwamba hujamilikiwa na Mungu, na kwamba wewe ni punda aliyedhibitiwa tu. Hakuna chochote cha kutamanika ndani yako, na Roho Mtakatifu hayumo kazini ndani yako. Ubinadamu wako unakosa mengi na haiwezekani Mungu kukutumia. Lazima uidhinishwe na Mungu na kuwa bora zaidi mara mia moja kuliko wanyama wasioamini na kuliko wanaotembea wakiwa wafu—wale tu wanaofikia kiwango hiki ndio wanaostahili kufanywa kuwa wakamilifu. Ni iwapo tu mtu anao ubinadamu na dhamiri ndio anafaa kutumiwa na Mungu. Ni wakati tu ambapo mnakamilishwa ndio mnaweza kufikiriwa kuwa binadamu. Wale waliofanywa kuwa wakamilifu tu ndio wale wanaoishi maisha yenye maana. Watu kama hawa tu ndio wanaoweza kumshuhudia Mungu hata pakubwa.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Waliokamilishwa Pekee Ndio Wanaoweza Kuishi Maisha Yenye Maana

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 554)

Ni njia gani ambayo Mungu hutumia kumkamilisha mwanadamu? Ni vipengele vipi vinavyojumuishwa? Je, uko tayari kukamilishwa na Mungu? Je, uko tayari kukubali hukumu na kuadibu kwa Mungu? Unajua nini kuhusu maswali haya? Kama huwezi kuzungumzia maarifa kama haya, basi hii inaonyesha kwamba bado huijui kazi ya Mungu na hujapatiwa nuru katu na Roho Mtakatifu. Binadamu wa aina hii hawezi kukamilishwa. Wanaweza tu kupokea kiasi kidogo cha neema ili kufurahia kwa muda mfupi na haiwezi kuendelezwa kwa kipindi kirefu. Kama mtu hufurahia tu neema ya Mungu, hawezi kukamilishwa na Mungu. Baadhi wanaweza kutoshelezwa na amani na furaha ya mwili, maisha yenye furaha bila ya dhiki au msiba, huku wakiishi kwa amani na familia zao bila ya mapigano au ugomvi. Wanaweza hata kuamini kwamba hii ni baraka ya Mungu, lakini kwa kweli, ni neema ya Mungu tu. Hamwezi kutosheka tu kwa kufurahia neema ya Mungu. Kufikiria kwa aina hii ni kuchafu mno. Hata ukisoma neno la Mungu kila siku, uombe kila siku, na roho yako ihisi furaha na amani halisi, ilhali mwishowe huwezi kuzungumzia maarifa yoyote ya Mungu na kazi Yake au hujapata uzoefu wa mambo kama hayo, na haijalishi ni kiasi gani cha neno la Mungu ambacho umekula na kunywa, ukihisi tu amani na furaha katika roho yako na kwamba neno la Mungu ni tamu mno kiasi kwamba haliwezi kulinganishwa na kingine chochote, kana kwamba huwezi kulifurahia ukatosheka, lakini huna uzoefu halisi na huna hakika yoyote na neno la Mungu, basi ni nini unachoweza kupokea kutoka kwa aina hii ya imani katika Mungu? Kama huwezi kuishi kwa kudhihirisha kiini cha neno la Mungu, kula na kunywa kwako kwa maneno ya Mungu na maombi vyote vinahusu dini. Basi binadamu wa aina hii hawezi kukamilishwa na hawezi kupatwa na Mungu. Wale wote waliopatwa na Mungu ni wale wanaofuatilia ukweli. Kile ambacho Mungu hufaidi si mwili wa binadamu wala miliki zake, lakini sehemu iliyo ndani yake inayomilikiwa na Mungu. Kwa hivyo, Mungu huukamilisha moyo wa binadamu wala si mwili wake, ili moyo wa binadamu uweze kupatwa na Mungu. Kwa maneno mengine, kiini cha kusema kwamba Mungu humkamilisha mwanadamu ni kwamba Mungu huukamilisha moyo wa mwanadamu ili uweze kumgeukia Mungu na kumpenda Yeye.

Mwili wa binadamu hufa. Haifaidi chochote kwa Mungu kuupata mwili wa binadamu, kwani ndio ule ule ambao bila shaka huoza. Hauwezi kupokea urithi wa Mungu au baraka Zake. Kama Mungu anaupata tu mwili wa binadamu na kuuhifadhi mwili wa binadamu katika mfululizo huu, binadamu atakuwa katika mfululizo huu kwa jina tu, lakini moyo wa binadamu ungemilikiwa na Shetani. Basi binadamu hangeweza tu kuwa maonyesho ya Mungu, bali badala yake angekuwa mzigo Wake. Kwa hivyo Mungu kuchagua binadamu hakungekuwa na maana. Wale watakaokamilishwa na Mungu ni wale watakaopokea baraka za Mungu na urithi Wake. Yaani, wanasikia na kuelewa kile Mungu Alicho nacho na Alicho, ili kiwe kile ambacho walicho nacho ndani yao; wanayo maneno yote ya Mungu ndani yao; haijalishi ni vipi nafsi ya Mungu ilivyo, mnaweza kusikia na kuelewa kila kitu Anachokuambia vile kilivyo, na hivyo kuishi kwa kudhihirisha ukweli. Huyu ndiye aina ya binadamu aliyekamilishwa na Mungu na aliyepatwa na Mungu. Binadamu wa aina hii tu ndiye anayestahili kurithi baraka hizi alizofadhiliwa na Mungu:

1. Kupokea upendo mzima wa Mungu.

2. Kutenda kulingana na mapenzi ya Mungu katika kila kitu.

3. Kupokea mwongozo wa Mungu, kuishi chini ya mwangaza wa Mungu, na kupatiwa nuru na Mungu.

4. Kuishi kwa kudhihirisha taswira inayopendwa na Mungu hapa ulimwenguni; kumpenda Mungu kwa kweli kama vile Petro alivyofanya, kusulubishwa kwa sababu ya Mungu na kustahili kufa kwa kuufidia upendo wa Mungu; kuwa na utukufu sawa na Petro.

5. Kupendwa, kuheshimiwa, na kuvutiwa na wote ulimwenguni.

6. Kushinda utumwa wote wa kifo na Kuzimu, kutoipatia fursa yoyote kazi ya Shetani, kumilikiwa na Mungu, kuishi ndani ya roho safi na changamfu, na kutokuwa na hisia zozote za uchovu.

7. Kuwa na hisia isiyoelezeka ya msisimko na furaha siku zote katika maisha yako yote, ni kana kwamba ameona kuja kwa siku ya utukufu wa Mungu.

8. Kupokea utukufu pamoja na Mungu, na kuwa na sura inayofanana na watakatifu wapendwa wa Mungu.

9. Kuwa kile ambacho Mungu anapenda zaidi ulimwenguni, yaani, mwana mpendwa wa Mungu.

10. Kubadilisha maumbile na kupaa juu pamoja na Baba kwenye mbingu ya tatu, na kuuzidi mwili.

Wale tu wanaoweza kurithi baraka za Mungu ni wale waliokamilishwa na Mungu na kupatwa na Mungu. Je, umefaidi chochote? Mungu amekukamilisha hadi kiwango gani? Mungu hamkamilishi binadamu bila mpango. Kunayo masharti na matokeo dhahiri yanayoweza kuonekana na binadamu. Si jinsi mwanadamu anavyoamini, kwamba mradi tu awe na imani katika Mungu, anaweza kukamilishwa na kupatwa na Mungu, na anaweza kupokea hapa ulimwenguni baraka na urithi wa Mungu. Mambo kama haya ni magumu mno, na hata zaidi inapohusu kubadilika kwa taratibu. Kwa sasa, kile ambacho mnafaa kutafuta kimsingi ni kukamilishwa na Mungu katika mambo yote, na kukamilishwa na Mungu kupitia kwa watu wote, mambo yote na vitu vyote ambavyo mnakumbwa navyo, ili mambo zaidi ya kile Mungu Alicho yatashirikishwa ndani yenu. Lazima kwanza mpokee urithi wa Mungu ulimwenguni kabla ya kustahili kurithi baraka nyingi na kubwa zaidi kutoka kwa Mungu. Mambo yote haya ndiyo ambayo mnafaa kutafuta na ambayo kwanza mnafaa kuelewa. Zaidi unavyotafuta kukamilishwa na Mungu katika mambo yote, ndivyo utakavyoweza kuona mkono wa Mungu zaidi katika mambo yote, na hivyo kutafuta kwa bidii kuingia katika hali ya neno la Mungu na uhalisia wa neno Lake kupitia mitazamo tofauti na katika mambo tofauti. Huwezi kutosheka na hali hasi kama kutotenda dhambi tu, au kutokuwa na dhana, kutokuwa na filosofia ya kuishi, na kutokuwa na hiari ya binadamu. Mungu humkamilisha mwanadamu kwa njia tofauti, na inawezekana katika mambo yote kwako kukamilishwa hatimaye. Huwezi tu kukamilishwa kwa kuzingatia mambo halisi, lakini pia mambo hasi, na hivyo kuboresha kile unachopata. Kila siku kunazo fursa za kukamilishwa na muda wa kupatwa na Mungu. Baada ya kipindi cha kupitia mambo kama haya, utabadilika pakubwa. Utaweza sasa kimaumbile kufaidi utambuzi katika mambo mengi ambayo hukuyaelewa awali; bila ya kuhitaji wengine kukufunza, bila kujua, utaweza kufahamishwa na Mungu, ili uweze kuwa na fahamisho katika mambo yote na mambo yote utakayopitia yatakuwa mengi. Mungu atakuongoza wewe ili usije ukapotoka kwa vyovyote vile. Kisha utawekwa wazi kwenye njia ya kufanywa kuwa mtimilifu na Yeye.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ahadi kwa Wale Ambao Wamekamilishwa

Maneno ya Mungu ya Kila Siku (Dondoo 555)

Kukamilishwa na Mungu hakuwezi kuwa kukamilishwa kupitia kwa kula na kunywa neno la Mungu tu. Aina hii ya uzoefu inaegemea upande mmoja sana na haijumuishi pande zote; inamzuia binadamu katika uwezo mdogo sana. Kwa hiyo, binadamu hukosa chakula cha kiroho kinachohitajiwa zaidi. Kama mtapenda kukamilishwa na Mungu, lazima mjifunze kupitia mambo yote na kupatiwa nuru katika yote mnayoyapitia. Kila unapokumbwa na kitu, kiwe kizuri au kibaya, unafaa kufaidi kutoka katika kitu hicho na hakifai kukufanya ukae tu. Haijalishi ni nini, unafaa kuweza kukitilia maanani kwa kusimama upande wa Mungu, na wala si kuchambua au kukisoma kutoka kwa mtazamo wa binadamu (huku ni kupotoka katika hali unayopitia). Kama hivi ndivyo utakavyopitia mambo katika maisha yako, basi moyo wako utazidiwa na mizigo ya maisha yako; utaishi siku zote katika mwanga wa uso wa Mungu na hutaweza kupotoka kwa urahisi katika matendo yako. Binadamu wa aina hii ana matarajio makubwa. Kunazo fursa nyingi za kukamilishwa na Mungu. Yote haya yanategemea kama ni nyinyi ndinyi mnaompenda Mungu kwa kweli na kama mnalo azimio la kukamilishwa na Mungu, kupatwa na Mungu, na kupokea baraka na urithi Wake. Haitakubalika kwenu kuwa na azimio tu. Lazima muwe na maarifa mengi, vinginevyo siku zote mtapotoka katika matendo yenu. Mungu yuko radhi kumkamilisha kila mmoja wenu. Kama ilivyo sasa, ingawa wengi tayari wamekubali kazi ya Mungu kwa muda mwingi, wamejiwekea mipaka ya kufurahia tu neema ya Mungu na wako radhi tu kupokea tulizo fulani la mwili kutoka Kwake. Hawako radhi kupokea ufunuo zaidi na wa kiwango cha juu zaidi, hali ambayo inaonyesha kwamba moyo wa binadamu ungali nje siku zote. Ingawa kazi ya binadamu, huduma yake, na moyo wake wa upendo kwa Mungu vyote vina kasoro chache zaidi, kuhusiana na kiini cha binadamu na kufikiria kwake kusiko na nuru, binadamu bado daima hutafuta amani na furaha ya mwili, na huwa hajali masharti na makusudio Mungu ya katika kumkamilisha binadamu ni yapi. Kwa hivyo maisha ya wengi yangali machafu na yaliyooza, bila dalili zozote za mabadiliko. Yeye hasa haichukilii imani katika Mungu kama suala lenye umuhimu. Badala yake, ni kana kwamba anayo imani tu kwa ajili ya binadamu mwengine, akitenda bila ukweli au kujitolea, na akiishi tu kwa vile viwango vya chini zaidi vya maisha, akiendelea kuwepo tu bila kusudi lolote. Wachache ndio wanaotafuta kuingia ndani ya neno la Mungu katika mambo yote, huku wakifaidi mambo mengi ya kusitawisha, wakiwa wenye utajiri mkubwa zaidi katika nyumba ya Mungu siku hii, na wakipokea baraka zaidi za Mungu. Kama unatafuta kukamilishwa na Mungu katika mambo yote na unaweza kurithi ahadi za Mungu hapa ulimwenguni; kama unatafuta kupatiwa nuru na Mungu katika mambo yote na huiruhusu miaka kuyoyoma tu huku ukiwa umezubaa, hii ndiyo njia inayostahili kuingia kwa bidii. Ni kupitia kwa njia hii tu ndipo unastahili na unafaa kukamilishwa na Mungu. Wewe ndiwe kweli unayetafuta kukamilishwa na Mungu? Wewe ndiwe kweli uliye mwenye bidii katika mambo yote? Unayo roho sawa ya upendo kwa Mungu kama Petro? Unayo hiari ya kumpenda Mungu kama Yesu alivyofanya? Umekuwa na imani katika Yesu kwa miaka mingi; umeona namna Yesu alivyompenda Mungu? Yesu ndiye kweli unayemwamini? Unamwamini Mungu wa matendo wa siku hii; umeona namna ambavyo Mungu wa matendo katika mwili anavyompenda Mungu kule mbinguni? Unayo imani katika Bwana Yesu Kristo; hiyo ni kwa sababu kusulubishwa kwa Yesu ili kuwakomboa wanadamu na miujiza Aliyoifanya vyote kwa ujumla ni ukweli unaokubaliwa. Hata hivyo, imani ya mwanadamu haitokani na maarifa na ufahamu wa kweli wa Yesu Kristo. Unaamini tu katika jina la Yesu lakini huna imani katika Roho Wake, kwani hujali kuhusu namna Yesu alivyompenda Mungu. Imani yako katika Mungu ni changa sana. Ingawa umekuwa na imani katika Yesu kwa miaka mingi, hujui namna ya kumpenda Mungu. Je, jambo hili halikufanyi kuwa mjinga mkubwa zaidi kote ulimwenguni? Hii inaonyesha kwamba kwa miaka mingi umekila chakula cha Bwana Yesu Kristo bure. Simpendi tu binadamu wa aina hii, Naamini kwamba pia Bwana Yesu Kristo, ambaye unamwabudu, hampendi. Mtu wa aina hii anawezaje kukamilishwa? Huaibiki? Huhisi aibu? Bado unao ujasiri wa kumkabili Bwana Yesu Kristo? Je, nyinyi nyote mnaelewa maana ya maneno Yangu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ahadi kwa Wale Ambao Wamekamilishwa

Iliyotangulia: Kuingia Katika Uzima (IV)

Inayofuata: Kuingia Katika Uzima (VI)

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp