Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho Chaguzi

Yaliyomo

Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu Kwa Ukweli

Kazi ya siku za mwisho ni kutenganisha vitu vyote kulingana na jinsi yalivyo, kukamilisha mpango wa usimamizi wa Mungu, kwa maana muda u karibu na siku ya Mungu imewadia. Mungu huwaleta wote walioingia katika ufalme Wake, yaani, wale wote waliokuwa waaminifu Kwake mpaka mwisho, katika enzi ya Mungu Mwenyewe. Hata hivyo, kabla ya kuja kwa enzi ya Mungu Mwenyewe, kazi Anayotamani kufanya Mungu si kutazama matendo ya mwanadamu wala kuuliza kuhusu maisha ya wanadamu, ila ni kuhukumu uasi wake, kwa maana Mungu Atawatakasa wale wote wanaokuja mbele ya kiti Chake cha enzi. Wale wote ambao wamefuata nyayo za Mungu mpaka siku hii ni wale ambao wamekuja mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, kwa hivyo wote wanaokubali kazi ya mwisho ya Mungu ni wale watakaotakaswa na Mungu. Kwa hali nyingine, wale wote wanaoikubali kazi ya mwisho ya Mungu ni wale watakaohukumiwa na Mungu.

Kama ilivyozungumziwa awali, hukumu ingeanza na nyumba ya Mungu. “Hukumu” hii inarejelea hukumu ambayo Mungu hutoa leo hii kwa wale wanaokuja mbele ya kiti Chake cha enzi siku za mwisho. Pengine kuna wale wanaoamini katika mawazo ya kimiujiza kama yale ya kuwa siku za mwisho zitakapowadia, Mungu Ataandaa meza kubwa mbinguni, ambako kitambaa cheupe kitatandikwa, kisha Mungu Ataketi kwenye kiti kikuu cha enzi na wanadamu wote watapiga magoti ardhini. Kisha Mungu Atafunua dhambi zote zilizowekwa dhidi ya kila mwanadamu kubainisha iwapo atapaa juu mbinguni ama atatupwa chini kwenye ziwa la moto wa jehanamu. Haijalishi mawazo ya mwanadamu yalivyo, kiini cha kazi ya Mungu hakiwezi kubadilishwa. Mawazo ya mwanadamu ni miundo ya fikra za mwanadamu tu na zinatoka kwenye ubongo wa mwanadamu, na zimetungwa na kuunganishwa kutokana na mambo aliyoyaona na kuyasikia. Kwa hivyo Ninasema, kwa vyovyote vile picha zilizowazwa ziwe za hali ya juu kiasi gani, hizo ni kama mchoro tu na haziwezi kubadilishwa na mpango wa kazi ya Mungu. Isitoshe, mwanadamu mzima amepotoshwa na Shetani, sasa atawezaje kuyaelewa mawazo ya Mungu? Mwanadamu huiona kazi ya hukumu ya Mungu kuwa ya ajabu mno. Mwanadamu anaamini kwamba kwa sababu ni Mungu Mwenyewe Anayefanya kazi ya kuhukumu, basi lazima ni ya kiwango cha juu zaidi na isiyoeleweka kwa wanadamu wenye mwili wa kufa; lazima inasikika katika mbingu yote na kutetemesha dunia, vinginevyo, itakuwaje kazi ya hukumu ya Mungu? Mwanadamu anaamini kuwa kwa maana hii ni kazi ya hukumu, basi lazima Mungu ni wa kuvutia na wa adhimu Anapofanya kazi, na wale wanaohukumiwa wanalia kwa sauti wakitoa machozi wakiwa kwenye magoti wakiomba msamaha. Onyesho hili lazima ni la kuvutia na la kusisimua mno…Kila mwanadamu huona kazi ya hukumu ya Mungu kuwa ya ajabu. Je, unajua kwamba muda mrefu baada ya Mungu kuanza kazi ya kuhukumu miongoni mwa wanadamu, wewe bado umestarehe usingizini? Je, unajua kwamba, wakati ambao unadhani kuwa kazi ya hukumu ya Mungu imeanza rasmi, utakuwa tayari umewadia wakati ambapo Mungu Anazibadili mbingu na nchi? Wakati huo, pengine utakuwa tu umeelewa maana ya maisha, lakini kazi ya adhabu ya Mungu isiyo na huruma itakuleta kuzimu, ukiwa bado usingizini. Hapo ndipo kwa ghafla utafahamu kuwa kazi ya hukumu ya Mungu itakuwa imeshakamilika.

Tusipoteze muda wa thamani tukizungumzia mada hizi za kuchukiza. Badala yake, tuzungumzie kinachofanyiza hukumu. Ikifika kwa neno “hukumu,” utawaza juu ya maneno yote ambayo Yehova Alizungumza juu ya kila mahali na pia maneno ya kukaripia ambayo Yesu Aliwaambia Mafarisayo. Ingawa maneno haya ni yenye ukali, sio hukumu ya Mungu kwa mwanadamu; maneno haya ni yale ambayo yamezungumzwa na Mungu katika mazingira tofauti, kumaanisha, mandhari tofauti, na ni tofauti kabisa na yale maneno Anayonena Kristo wakati Anamhukumu mwanadamu siku za mwisho. Katika siku za mwisho, Kristo Anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufunua kiini cha mwanadamu, na kuchunguza maneno na matendo ya mwanadamu. Maneno haya yanajumuisha kweli mbali mbali, kama vile jukumu la mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida kikamilifu, na pia hekima na asili ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yanalenga nafsi na asili potovu ya mwanadamu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu anavyomkataa Mungu kwa dharau, yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu za adui dhidi ya Mungu. Mungu Anapofanya kazi ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu, bali Anatoa ufunuo, na kushughulika naye na kumpogoa kwa muda mrefu. Namna hii ya ufunuo, kushughulika na kupogoa haiwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Kazi kama hii pekee ndiyo huchukuliwa kama hukumu; na kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kushawishiwa, na kugeuzwa mawazo na kujisalimisha kwa Mungu, na kufaidi ufahamu kamili wa Mungu. Kazi ya hukumu humletea mwanadamu kuelewa kwa uso wa kweli wa Mungu na pia ukweli kuhusu uasi wa mwanadamu. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, ufahamu wa makusudi ya kazi ya Mungu, na pia ufahamu wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na mizizi ya upotovu huo, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake. Kazi hii ni kazi ya hukumu inayofanywa na Mungu. Usipouchukulia ukweli huu kama muhimu na kila mara kufikiri kuuepuka au kutafuta njia nyingine isipokuwa ukweli, basi Ninasema kuwa wewe ni mtenda dhambi mkubwa. Iwapo una imani kwa Mungu, lakini hutafuti ukweli au mapenzi ya Mungu, wala hupendi njia inayokuleta karibu na Mungu, basi Nakwambia kuwa wewe ni mmoja anayejaribu kuepuka hukumu. Wewe ni kibaraka na msaliti anayekikimbia kiti kikuu cheupe cha enzi, na Mungu Hatawasamehe waasi wowote wanaotoroka kutoka machoni Pake. Wanadamu wa aina hii watapokea adhabu kali zaidi. Wale wanaokuja mbele za Mungu ili wahukumiwe, na wametakaswa wataishi milele katika ufalme wa Mungu. Bila shaka, hii ni katika siku za usoni.

Kazi ya hukumu ni kazi Yake Mungu Mwenyewe, kwa hivyo lazima ifanywe na Mungu Mwenyewe kwa kawaida; haiwezi kufanywa na mwanadamu kwa niaba Yake. Kwa sababu hukumu ni kumshinda mwanadamu kupitia ukweli, hakuna shaka kuwa Mungu bado Anaonekana kama kiumbe cha nyama Anayepaswa kufanya kazi hii miongoni mwa wanadamu. Hiyo ni kumaanisha, wakati wa siku za mwisho, Kristo atautumia ukweli kuwafunza wanadamu duniani kote na kufanya ukweli wote ujulikane kwao. Hii ni kazi ya hukumu ya Mungu. Wengi wana ladha ya shubiri mdomoni kuhusu nafsi ya pili ya Mungu, kwa maana mwanadamu huona vigumu kuamini ya kwamba Mungu atafanya kazi ya hukumu akiwa na mwili. Lakini lazima Nikueleze kwamba mara nyingi kazi ya Mungu huzidi matarajio ya mwanadamu na ni vigumu kwa mawazo yao kukubali. Kwa maana wanadamu ni mabuu kwenye ardhi, ilhali Mungu ni mkuu Anayejaza ulimwengu mzima; mawazo ya mwanadamu ni kama shimo la maji machafu ambayo yanazalisha mabuu peke yake, ilhali kila hatua ya kazi inayoelekezwa na mawazo ya Mungu ni matunda ya hekima ya Mungu. Mwanadamu hutaka kila wakati kushindana na Mungu; kwa hivyo Nasema ni wazi kuwa ni nani yuko katika nafasi ya kupoteza mwishowe. Kwa hivyo Nawasihi nyote msijichukue kuwa wa maana zaidi kushinda dhahabu. Ikiwa wengine wanaweza kukubali hukumu ya Mungu, ni kwa nini wewe usiikubali? Unasimama kiwango kipi juu ya wengine? Iwapo wengine wanaweza kuinamisha vichwa vyao mbele ya ukweli, ni kwa nini usifanye vile pia? Mwelekeo mkuu wa kazi ya Mungu hauwezi kukomeshwa. Hatarudia kazi ya hukumu tena kwa sababu ya “kustahili” kwako, na utajuta kwa uchungu kupoteza nafasi nzuri kama hiyo. Usipoyaamini maneno Yangu, basi kingoje kiti cheupe kikuu cha enzi kilicho angani “kipitishe hukumu” juu yako! Lazima ujue kwamba Waisraeli wote walimkataa kwa dharau na kumkana Yesu, ilhali uhakika wa ukombozi wa Yesu kwa wanadamu ulizidi kusambaa mpaka mwisho wa ulimwengu. Je, hili silo jambo ambalo Mungu tayari Amelitimiza? Iwapo bado unangoja Yesu Aje Akupeleke mbinguni, basi Nasema kuwa wewe ni mti mkavu.[a] Yesu Hatamkubali mfuasi bandia kama wewe asiye mwaminifu kwa ukweli na anayetafuta baraka pekee. Badala yake, Hataonyesha huruma Anapokutupa kwenye ziwa la moto uungue kwa makumi ya maelfu ya miaka.

Je, sasa unaelewa hukumu ni nini na ukweli ni nini? Ikiwa umeelewa, basi Nakusihi ujisalimishe kwa hukumu, la sivyo hutapata kamwe fursa ya kupendwa na Mungu au kupelekwa na Mungu katika ufalme Wake. Wale wanaokubali hukumu pekee yake na hawawezi kamwe kutakaswa, yaani, wale wanaotoroka wakati kazi ya hukumu inapoendelea, watachukiwa na kukataliwa na Mungu milele. Dhambi zao ni nyingi zaidi, na za kusikitisha zaidi, kuliko zile za Mafarisayo, kwa maana wamemsaliti Mungu na ni waasi dhidi ya Mungu. Wanadamu wa aina hii wasiostahili hata kufanya huduma watapokea adhabu kali zaidi inayodumu milele. Mungu Hatamsamehe msaliti yeyote ambaye kwa wakati mmoja alidai uaminifu kwa Mungu kwa maneno tu ilhali alimsaliti Mungu. Wanadamu kama hao wataona adhabu ya malipo kupitia adhabu ya roho, nafsi na mwili. Je, hii haiweki wazi haki ya hali halisi ya Mungu? Je, hii siyo sababu kamili ya hukumu ya Mungu na ufunuo wa mwanadamu? Wakati wa hukumu, Mungu Atawaweka wote wanaofanya aina zote za uovu mahali roho wa uovu huishi ili miili yao ya nyama iharibiwe vile wapendavyo roho hao waovu. Miili yao itatoa harufu ya maiti, na adhabu kama hiyo ndiyo inayowafaa. Mungu huandika kwenye vitabu vya kumbukumbu kila mojawapo ya dhambi za waumini hawa wanafiki wasio waaminifu, wafuasi wanafiki, na wafanyakazi bandia, kisha wakati unapowadia, Anawatupa katikati ya roho wachafu ili miili yao inajisiwe na roho hao wachafu wanavyopenda, na matokeo yake ni kwamba hawatawahi kamwe kuzaliwa upya katika miili mipya na hawatauona mwanga kamwe. Wale wanafiki waliotoa huduma wakati mmoja lakini hawakuwa waaminifu mpaka mwisho watahesabiwa na Mungu miongoni mwa waovu ili watembee katika baraza la waovu, na kuungana na halaiki ya wasio na mpangilio. Mwishowe, Mungu Atawaangamiza. Mungu Huwatenga na Hawatambui wote ambao hawajawahi kuwa waaminifu kwa Kristo au kuweka juhudi yoyote, na Atawaangamiza wote wakati wa mabadiliko ya enzi. Hawatakuwepo tena duniani, na zaidi ya hayo hawatapata njia ya kuingia katika ufalme wa Mungu. Wale ambao hawajawahi kuwa wa kweli kwa Mungu lakini wamelazimika kuhusiana na Mungu watahesabiwa miongoni mwa wale wanaotoa huduma kwa watu wa Mungu. Ni idadi ndogo tu ya wanadamu wa aina hii ndio watapona, na wengi wao wataangamia pamoja na wasiohitimu hata kufanya huduma. Hatimaye, Mungu Ataleta kwenye ufalme Wake wale wote walio na mawazo kama Yake, watu na wana wa Mungu na vile vile waliopangiwa na Mungu kuwa makuhani. Haya ndiyo matunda Anayopata Mungu kutokana na kazi Yake. Na kwa wale wasio katika sehemu zozote zilizotengwa na Mungu, watahesabiwa miongoni mwa makafiri. Na kwa hakika mnaweza kuwaza jinsi hatima yenu itakavyokuwa. Tayari Nimewaambia yote Ninayopaswa kusema; njia mnayochagua itakuwa uamuzi wenu kufanya. Mnachopaswa kuelewa ni hiki: Kazi ya Mungu haimsubiri yeyote asiyeweza kuwa katika hatua moja na Mungu, na asili ya Mungu ya haki haimwonyeshi mwanadamu yeyote huruma.

Tanbihi:

a. Mti mkavu: nahau ya Kichina inayomaanisha “hali isiyo na matumaini.”