Je, Wewe Kweli Unamwamini Mungu?
Unaweza kuwa umeitembea njia ya imani katika Mungu kwa zaidi ya mwaka mmoja au miwili, na labda umevumilia ugumu mwingi maishani mwako katika miaka hii; au labda hujavumilia ugumu wowote, na badala yake umepokea neema nyingi. Inaweza pia kuwa kwamba hujapitia ugumu wala neema, lakini umeishi maisha ya kawaida kabisa. Bila kujali, wewe bado ni mfuasi wa Mungu, kwa hivyo hebu tufanye ushirika kuhusu mada ya kumfuata Mungu. Hata hivyo, lazima Niwakumbushe wote wanaosoma maneno haya kwamba neno la Mungu linaelekezwa kwa kila mtu anayemkiri na kumfuata Yeye, sio kwa watu wote, bila kujali kama wanamkiri Yeye au la. Ukiamini kwamba Mungu anazungumza na umma, kwa watu wote duniani, basi neno la Mungu halitakuwa na athari yoyote kwako. Hivyo, unapaswa kuyakumbuka maneno haya yote moyoni mwako, na usijitenge nayo kila mara. Bila kujali hayo, hebu tuzungumze kuhusu kile kinachofanyika katika nyumba yetu.
Ninyi nyote sasa mnapaswa kuelewa maana ya kweli ya imani katika Mungu. Maana ya imani katika Mungu ambayo Niliizungumzia hapo awali ilihusiana na kuingia kwenu katika mambo chanya. Leo ni tofauti: Leo, Nitachanganua kiini cha imani yenu katika Mungu. Bila shaka, huku ni kuwaongoza kutokea katika kipengele hasi; Nisingefanya hivyo, basi msingejua kamwe sura yenu ya kweli, na mngejisifu milele kuhusu uchaji na uaminifu wenu. Ni haki kusema kwamba kama Nisingechimbua ubaya katika vilindi vya mioyo yenu, basi kila mmoja wenu angejiwekea taji kichwani pake na kujipa utukufu wote. Asili zenu za kiburi na zenye majivuno zinawasukuma kusaliti dhamiri zenu wenyewe, kumwasi na kumpinga Kristo, na kufichua sura zenu mbaya, na hivyo kuweka wazi nia zenu, fikira zenu, matamanio yenu ya kupita kiasi, na macho yaliyojaa tamaa. Na bado mnaendelea kutangaza shauku yenu ya maisha yote kwa kazi ya Kristo, na mnaendelea kusema na kurudia ukweli uliosemwa zamani na Kristo. Hii ndiyo "imani" yenu—“imani isiyo na uchafu” yenu. Nimemwekea mwanadamu kiwango kikali wakati wote. Ikiwa uaminifu wako unakuja na nia na masharti, basi Mimi afadhali nisiwe na kile kinachoitwa uaminifu wako, kwa maana Ninawachukia watu wanaonidanganya Mimi kwa nia zao na kunishinikiza kwa masharti. Natamani tu mwanadamu awe mwaminifu kabisa Kwangu, na afanye mambo yote kwa ajili ya neno moja, na ili kuthibitisha neno hili: imani. Ninachukia sana matumizi yenu ya maneno ya kujipendekeza ili kujaribu kunifanya Nifurahi, kwa maana Nimewatendea ninyi kwa uaminifu sikuzote, na hivyo Natamani ninyi pia mtende kwa imani ya kweli Kwangu. Linapokuja suala la imani, wengi wanaweza kufikiri kwamba wanamfuata Mungu kwa sababu wana imani, na hawangevumilia mateso kama hayo vinginevyo. Kwa hivyo Nakuuliza hili: Ikiwa unaamini katika uwepo wa Mungu, kwa nini humwogopi Yeye kamwe? Ikiwa unaamini katika uwepo wa Mungu, kwa nini hakuna hofu hata kidogo juu Yake moyoni mwako? Ikiwa unakiri kwamba Kristo ni kupata mwili kwa Mungu, kwa nini unamdharau? Kwa nini unatenda bila heshima Kwake? Kwa nini unamhukumu Yeye waziwazi? Kwa nini kila mara unafuatilia vitendo Vyake kwa siri? Kwa nini hutii mipango Yake? Kwa nini hulichukulii neno Lake kama kigezo chako katika matendo yako? Kwa nini unanyang'anya na kuiba matoleo Yake? Kwa nini unajaribu kuzungumza kutoka katika nafasi ya Kristo? Kwa nini unatathmini iwapo kazi Yake na neno Lake ni sahihi? Kwa nini unathubutu kumkufuru Yeye nyuma Yake? Je, haya na mengine ndiyo yanayounda imani yenu?
Katika maneno na tabia yenu kunafichuliwa vipengele vya kutokuamini kwenu katika Kristo. Kutoamini kunajaza nia na malengo ya yote mnayofanya. Hata silika ya mtazamo wenu ina kutomwamini Kristo. Inaweza kusemwa kwamba kila dakika, kila mmoja wenu ana vipengele vya kutoamini. Hii inamaanisha kwamba, kila wakati, ninyi mko katika hatari ya kumsaliti Kristo, kwa maana damu inayotiririka katika miili yenu imejazwa na kutomwamini Mungu mwenye mwili. Kwa hivyo, Ninasema kwamba nyayo mnazoacha katika njia ya imani katika Mungu sio za kweli; mnapotembea katika njia ya imani katika Mungu, hamweki miguu yenu kwa uthabiti ardhini—mnafanya mambo kwa kijuujuu tu. Hamjawahi kuamini kikamilifu neno la Kristo na hamwezi kulitia katika vitendo mara moja. Hii ndiyo sababu hamna imani katika Kristo. Kuwa na fikira juu Yake kila mara ni sababu nyingine inayofanya msiwe na imani Kwake. Kuwa na shaka daima kuhusu kazi ya Kristo, kuliacha neno la Kristo lipuuzwe, kuwa na maoni juu ya kila kitu anachofanya Kristo na kutoweza kukielewa kwa usahihi, kutatizika kuachana na fikira zenu haijalishi mnapokea maelezo gani, na kadhalika—hivi vyote ni vipengele vya kutoamini vilivyochanganyika ndani ya mioyo yenu. Ingawa mnafuata kazi ya Kristo na hamjawahi kubaki nyuma, kuna uasi mwingi sana uliochanganyika katika mioyo yenu. Uasi huu ni uchafu katika imani yenu katika Mungu. Labda ninyi hamfikiri hivi ndivyo ilivyo, lakini ikiwa wewe huwezi kutambua nia zako kutoka ndani ya hili, basi wewe hakika utakuwa miongoni mwa wale wanaoangamia, kwa maana Mungu huwafanya kuwa watimilifu wale tu wanaomwamini kweli, sio wale wanaomwamini nusu nusu, na sembuse wale wanaomfuata shingo upande licha ya kutowahi kuamini kwamba Yeye ni Mungu.
Watu wengine hawapendi ukweli, sembuse hukumu. Badala yake, wanapenda mamlaka na utajiri; watu kama hao wanaitwa watafuta mamlaka. Wanatafuta tu yale madhehebu duniani yaliyo na mamlaka, na wanatafuta tu wachungaji na walimu wanaotoka katika seminari. Ingawa wameikubali njia ya ukweli, wanaamini nusu nusu tu, na hawawezi kutoa miili na akili zao zote; vinywa vyao vinanena maneno ya kujitumia kwa ajili ya Mungu, lakini macho yao yanalenga wachungaji na walimu wakuu, na hawamtazami Kristo hata mara moja. Akili zao zimejaa mawazo ya umaarufu na faida, na utukufu. Wanafikiri haiwezekani kabisa kwamba mtu mdogo kama huyo angeweza kuwashinda watu wengi sana, kwamba mtu wa kawaida kabisa angeweza kumfanya mwanadamu kuwa mtimilifu. Wanafikiri haiwezekani kabisa kwamba watu hawa wasio na maana walio kati ya mavumbi na malundo ya samadi ndio watu wateule wa Mungu. Wanaamini kwamba kama watu kama hao wangekuwa walengwa wa wokovu wa Mungu, basi mbingu na ardhi zingepinduliwa, na watu wote wangecheka sana. Wanaamini kwamba kama Mungu angewachagua watu kama hao kufanywa kuwa watimilifu, basi watu hao wakuu wangekuwa Mungu Mwenyewe. Mitazamo yao imechafuliwa na kutoamini; zaidi ya kutoamini, wao ni wanyama tu wasio na urazini. Kwa maana wanathamini tu hadhi, sifa, na mamlaka, na wanastahi makundi makubwa na madhehebu, na hawawajali hata kidogo wale wanaoongozwa na Kristo. Wao ni wasaliti tu ambao wamempa kisogo Kristo, ukweli, na uzima.
Huvutiwi na unyenyekevu wa Kristo, lakini unawaheshimu sana wale wachungaji wa uwongo wenye hadhi mashuhuri. Huabudu uzuri au hekima ya Kristo, lakini unawapenda wale waasherati wanaoenda sambamba na uchafu wa dunia. Unadhihaki tu maumivu ya Kristo ya kutokuwa na mahali pa kulaza kichwa Chake, lakini unavutiwa na wale maiti wanaoiba matoleo na kuishi katika uasherati. Huko tayari kuteseka pamoja na Kristo, lakini kwa hiari unajitupa mikononi mwa wale wapinga Kristo wasiojali na wakaidi, ingawa wanakupa tu mwili, maneno, na udhibiti. Hata sasa, moyo wako bado unawaelekea wao, kuelekea sifa yao, kuelekea hadhi yao, nguvu zao. Na bado unaendelea kuwa na mtazamo wa kuona kazi ya Kristo kuwa ngumu kuikubali na kutokuwa tayari kuikubali. Ni kwa sababu ya hili tu ndiyo maana Ninasema kwamba huna imani ya kumkiri Kristo. Sababu iliyokufanya umfuate hadi leo ni kwa sababu tu hukuwa na chaguo lingine. Msururu wa taswira kuu unainuka milele moyoni mwako; huwezi kusahau kila neno na tendo lao, wala maneno na mikono yao yenye ushawishi. Wao ni wakuu milele na mashujaa milele, moyoni mwenu. Lakini sivyo ilivyo kwa Kristo wa leo. Moyoni mwako, Yeye si wa maana daima, Yeye ni mwanadamu asiyestahili hofu milele. Kwa maana Yeye ni wa kawaida mno, ana ushawishi mdogo mno, na Yeye si mkuu hata kidogo.
Bila kujali hayo, Ninasema kwamba wale wote wasiothamini ukweli ni wasioamini na wasaliti wa ukweli. Watu kama hao hawatapokea kamwe kibali cha Kristo. Je, sasa umetambua ni kiasi gani cha kutoamini kiko ndani yako, na una kiasi gani cha usaliti kwa Kristo? Nakuhimiza hivi: Kwa kuwa umechagua njia ya ukweli, basi unapaswa kujitoa kwa moyo wako wote; usiwe na kusitasita au kuwa shingo upande. Unapaswa kuelewa kwamba Mungu si Mungu wa dunia wala wa mtu yeyote mmoja, bali ni Mungu wa wale wote wanaomwamini kweli, wale wote wanaomwabudu, na wale wote waliojitoa na ambao ni waaminifu Kwake.
Leo, kutoamini kwingi bado kumo ndani yenu. Tazameni kwa makini ndani yenu wenyewe, na hakika mtapata jibu lenu. Utakapopata jibu la kweli, basi utakubali kwamba wewe si muumini wa Mungu, bali ni mtu anayemdanganya, kumkufuru, na kumsaliti Yeye, na mtu ambaye si mwaminifu Kwake. Kisha utatambua kwamba Kristo si mwanadamu, bali ni Mungu. Siku hiyo itakapofika, utamwogopa, kumhofu, na kumpenda Kristo kweli. Kwa sasa, asilimia thelathini tu ya moyo wenu imejawa na imani, huku asilimia sabini nyingine ikijawa na shaka. Kila kitu anachofanya na kusema Kristo kinaweza kuwapa fikira na maoni juu Yake, fikira na maoni yanayotokana na kutoamini kwenu kikamilifu ndani Yake. Mnamstahi na kumhofu tu Mungu asiyeonekana aliye mbinguni, na hamumjali Kristo aliye hai duniani. Je, huku pia si kutoamini kwenu? Mnamtamani tu Mungu aliyefanya kazi zamani, lakini hamkabiliani na Kristo wa leo. Hii yote ni "imani," iliyochanganyika daima mioyoni mwenu, imani ambayo haiamini katika Kristo wa leo. Mimi siwadharau kwa njia yoyote ile, kwa maana kuna kutoamini kwingi sana ndani yenu, kuna mengi sana ndani yenu yaliyo na uchafu na ambayo lazima yachanganuliwe. Uchafu huu ni ishara kwamba hamna imani hata kidogo; ni alama ya kumkataa kwenu Kristo, na unawatambulisha kama wasaliti wa Kristo. Ni shela kwa maarifa yenu juu ya Kristo, kizuizi cha kupatwa kwenu na Kristo, kikwazo kwa ulinganifu wenu na Kristo, na uthibitisho kwamba Kristo hawakubali. Sasa ndio wakati wa kuchunguza sehemu zote za maisha yenu! Kufanya hivyo kutawanufaisha kwa kila njia inayofikirika!