N. Kuhusu Jinsi ya Kufuatilia Mabadiliko ya Tabia na Kukamilishwa na Mungu

504. Mabadiliko yanafanikishwa kwa tabia ya mwanadamu kupitia njia tofauti ya kazi ya Mungu; bila mabadiliko ya aina hii katika tabia ya mwanadamu, mwanadamu hangeweza kuwa na ushuhuda kwa Mungu, na hangekuwa wa kuupendeza moyo wa Mungu. Mabadiliko katika tabia ya mwanadamu yanaashiria kwamba mwanadamu amejiweka huru kutokana na minyororo ya Shetani, amejiweka huru kutokana na ushawishi wa giza, na kwa kweli amekuwa mfano na kifaa cha kujaribiwa cha kazi ya Mungu, amekuwa shahidi wa kweli wa Mungu na mtu aliye wa kuupendeza moyo wa Mungu. Leo hii, Mungu mwenye mwili Amekuja kufanya kazi Yake duniani, na Anahitaji kwamba mwanadamu apate ufahamu kumhusu, aweze kumtii, awe na ushuhuda Kwake—aweze kujua kazi Yake ya matendo na ya kawaida, atii maneno Yake yote na kazi ambayo haiambatani na mawazo ya mwanadamu, na kuwa na ushuhuda kwa kazi Yake yote ya kumwokoa mwanadamu, na matendo yote Anayofanya ya kumshinda mwanadamu. Wale walio na ushuhuda kwa Mungu lazima wawe na ufahamu wa Mungu; ni aina hii tu ya ushuhuda ndio ulio sahihi, na wa kweli, na ni aina hii tu ya ushuhuda ndio unaoweza kumpa Shetani aibu. Mungu Anawatumia wale waliomjua baada ya kupitia hukumu Yake na kuadibu, ushughulikiaji na upogoaji, kuwa na ushuhuda Kwake. Anawatumia wale waliopotoshwa na Shetani kumtolea Yeye ushuhuda, na vilevile Anawatumia wale ambao tabia yao imebadilika, na wale basi ambao wamepokea baraka Zake, kumtolea ushuhuda. Yeye hana haja na mwanadamu kumsifu kwa maneno tu, wala hana hitaji lolote la sifa na ushuhuda kutoka kwa namna ya Shetani, ambao hawajaokolewa na Yeye. Ni wale tu wanaomjua Mungu ndio wanaohitimu kumtolea Mungu ushuhuda, na ni wale tu ambao tabia zao zimebadilika ndio wanaofaa kumshuhudia Mungu, na Mungu hatamruhusu mwanadamu kwa makusudi aliletee jina Lake aibu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu

505. Watu hawawezi kubadilisha tabia yao wenyewe; lazima wapitie hukumu na kuadibu, mateso na usafishaji wa maneno ya Mungu, au kushughulikiwa, kufunzwa nidhamu, na kupogolewa na maneno Yake. Ni baada ya hapo tu ndipo wanaweza kutimiza utiifu na ibada kwa Mungu, na wasijaribu tena kumdanganya Yeye na kumshughulikia kwa uzembe. Ni kupitia kwa usafishaji wa maneno ya Mungu ndio watu hupata mabadiliko katika tabia. Ni wale tu wanaopitia mfichuo, hukumu, kufundishwa nidhamu, na kushughulikiwa kwa maneno Yake ambao hawatathubutu tena kufanya mambo kwa kutojali, na watakuwa watulivu na makini. Jambo muhimu sana ni kwamba wanaweza kutii neno la sasa la Mungu na kutii kazi ya Mungu, na hata kama hayalingani na fikira za binadamu, wanaweza kuweka kando fikira hizi na kutii kwa hiari. Mabadiliko katika tabia yalipozungumziwa hapo awali, imekuwa hasa kuhusu kujinyima mwenyewe, kuruhusu mwili kuteseka, kufunza nidhamu mwili wa mtu, na kujiondolea mapendeleo ya mwili—hii ni aina moja ya mabadiliko katika tabia. Watu sasa wanajua kwamba maonyesho halisi ya mabadiliko katika tabia ni kutii maneno halisi ya Mungu na vilevile kuweza kuwa na ufahamu halisi wa kazi Yake mpya. Kwa njia hii, ufahamu wa awali wa watu kumhusu Mungu, ambao ulipotoshwa na fikira zao wenyewe, na kutimiza ufahamu wa kweli wa na utiifu Kwake. Hii tu ndio maonyesho halisi ya mabadiliko katika tabia.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Ambao Tabia Zao Imebadilika ni Wale Ambao Wameingia Katika Uhalisi wa Neno la Mungu

506. Kubadilisha tabia ya mwanadamu huanza na maarifa ya kiini chake na kupitia mabadiliko katika mawazo yake, asili, na mtazamo wa akili—kwa njia ya mabadiliko ya msingi. Ni kwa njia hii tu ndio mabadiliko ya kweli yatapatikana katika tabia ya mwanadamu. Tabia ya upotovu ya mwanadamu inatokana na hali yake ya kupewa sumu na kukanyagwa na Shetani, kutokana na madhara mabaya sana ambayo Shetani ameweka katika mawazo yake, maadili, ufahamu, na hisia. Ni hasa kwa sababu mambo ya msingi ya mwanadamu yamepotoshwa na Shetani, na ni tofauti kabisa na jinsi Mungu aliwaumba kwa asili, kwamba mwanadamu humpinga Mungu na haelewi ukweli. Hivyo, mabadiliko katika tabia za mwanadamu lazima yaanze na mabadiliko katika mawazo yake, ufahamu na hisia ambayo yatabadilisha maarifa yake ya Mungu na maarifa yake ya ukweli.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu

507. Katika maisha yake, kama mwanadamu anatamani kutakaswa na kufikia mabadiliko katika tabia yake, kama anatamani kuishi kwa kudhihirisha maisha yenye maana, na kutimiza wajibu wake kama kiumbe, basi lazima akubali adabu na hukumu ya Mungu, na lazima asiruhusu nidhamu ya Mungu na kipigo cha Mungu kiondoke kwake, ili aweze kujiweka huru kutokana na kutawalwa na ushawishi wa Shetani na kuishi katika mwanga wa Mungu. Ujue kwamba adabu ya Mungu na hukumu ni mwanga, na mwanga wa wokovu wa mwanadamu, na kwamba hakuna baraka bora zaidi, neema au ulinzi bora kwa ajili ya mwanadamu. Mwanadamu anaishi chini ya ushawishi wa Shetani, na yupo katika mwili; kama yeye hatatakaswa na kupokea ulinzi wa Mungu, basi mwanadamu atakuwa milele mpotovu zaidi. Kama yeye anataka kumpenda Mungu, basi lazima atakaswe na kuokolewa. Petro aliomba, “Mungu, wakati Unanitendea wema ninapata furaha, na kuhisi faraja; wakati unaniadibu, najisikia faraja kubwa zaidi na furaha. Ingawa mimi ni mdhaifu, na kuvumilia mateso yasiyotajika, ingawa kuna machozi na huzuni, Unajua kwamba huzuni huu ni kwa sababu ya kutotii kwangu, na kwa sababu ya udhaifu wangu. Mimi ninalia kwa sababu siwezi kukidhi hamu Yako, nahisi huzuni na majuto kwa sababu mimi sitoshi kwa mahitaji Yako, lakini niko tayari kufikia ulimwengu huu, niko tayari kufanya yote niwezayo ili nikuridhishe. Adabu Yako imeniletea ulinzi, na kunipa wokovu bora; hukumu Yako inazidi ustahimili Wako na uvumilivu Wako. Bila adabu Yako na hukumu, singefurahia huruma Yako na rehema. Leo, naona zaidi kwamba upendo wako umepita mipaka ya mbinguni na kuwa bora ya yote. Upendo wako sio tu huruma na fadhili; hata zaidi ya hayo, ni adabu na hukumu. Adabu Yako na hukumu imenipa mengi. Bila adabu Yako na hukumu, hakuna hata mmoja angetakaswa, na hakuna hata mmoja angeweza kupata upendo wa Muumba.”

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu

508. Kama unataka kufanywa mkamilifu, lazima kwanza uwe na neema ya Mungu, kwa sababu Mungu anawakamilisha wale ambao Amewapa neema, wale wanaoupendeza moyo Wake. Kama unataka kuupendeza moyo wa Mungu, lazima uwe na moyo unaotii kazi Yake yote, lazima ujitahidi kuufuata ukweli, na lazima uukubali uchunguzi wa Mungu katika kila kitu. Je, kila kitu unachofanya kimepitia uchunguzi wa Mungu? Je, nia yako iko sawa? Kama nia yako iko sawa, Mungu Atakubaliana nawe; kama nia yako sio sawa, hii inathibitisha kwamba kile moyo wako unapenda sio Mungu, ni mwili na Shetani. Kwa hiyo, lazima utumie maombi kama njia ya kukubali uchunguzi wa Mungu katika kila. Unapoomba, ingawa Mimi mwenyewe sisimami mbele yako, Roho Mtakatifu yuko pamoja nawe, na unaomba kwa Mimi mwenyewe na Roho wa Mungu. Kwa nini unaamini katika mwili huu? Unaamini kwa sababu Yuko na Roho wa Mungu. Je, ungemwamini mtu huyu ikiwa hangekuwa na Roho wa Mungu. Unapoamini katika mtu huyu, unaamini katika Roho wa Mungu. Unapomwogopa mtu huyu, unamwogopa Roho wa Mungu. Imani katika Roho wa Mungu ni imani katika mtu huyu, imani katika mtu huyu pia ni imani katika Roho wa Mungu. Unapoomba, unahisi Roho wa Mungu akiwa pamoja nawe, Mungu yuko mbele yako, kwa hivyo unamwomba Roho wa Mungu. Leo, watu wengi wanaogopa sana kuyaleta matendo yao mbele za Mungu, na ingawa unaweza kuudanganya mwili wa Mungu, huwezi kumdanganya Roho wa Mungu. Yale yote ambayo hayawezi kustahimili uchunguzi wa Mungu hayakubaliani na ukweli nayo lazima yawekwe kando, ama unatenda dhambi dhidi ya Mungu. Kwa hivyo, haijalishi kama ni wakati unaomba, unaponena na kushiriki na ndugu na dada zako, ama unapofanya wajibu wako na kufanya biashara yako, lazima uuweke moyo wako mbele za Mungu. Unapoitimiza kazi yako, Mungu yuko nawe, na bora nia yako iwe sawa, nayo iwe kwa ajili ya kazi ya nyumba ya Mungu, Atakubali kila kitu ufanyacho, kwa hivyo ni lazima uweke bidii kwa dhati kujishughulisha na kuitimiza kazi yako. Unapoomba, kama una upendo kwa Mungu katika moyo wako, na kama unatafuta utunzaji wa Mungu, ulinzi, na uchunguzi, kama haya ndio nia yako, maombi yako yatafaulu. Unapoomba katika mikutano, ndivyo unafaa kufungua moyo wako na kuomba Mungu, ambia Mungu kile kilicho moyoni mwako, na bila kuongea uongo, basi maombi yako yatafaulu. Kama unampenda Mungu moyoni mwako kwa dhati, basi fanya kiapo kwa Mungu: “Mungu, uliye mbinguni na nchini na vitu vyote, naapa Kwako: Hebu Roho Wako achunguze kila kitu ninachofanya na unilinde na kunijali kila wakati. Kinafanya kila kitu nifanyacho kiweze kusimama katika uwepo Wako. Ikiwa moyo wangu utawahi kukoma kukupenda ama kukusaliti Wewe, nipe adhabu Yako na laana kali zaidi. Usinisamehe katika dunia hii ama inayofuata!” Unaweza kuthubutu kula kiapo kama hiki? Kama huwezi, hii inadhibitisha kuwa wewe ni mwoga, na kwamba bado unajipenda. Je, mnao uamuzi huu? Kama kweli huu ndio uamuzi wako, lazima ufanye kiapo hiki. Kama una azimio la kula kiapo kama hiki, Mungu ataridhisha uamuzi wako. Unapoapa kwa Mungu, Mungu anasikiza. Mungu Anaamua kama wewe ni mwenye dhambi ama mwenye haki kupitia maombi yako na matendo yako. Huu sasa ndio mchakato wa kukukamilisha, na kama kweli unayo imani katika kukamilishwa kwako na Mungu, basi utaleta kila kitu ufanyacho mbele za Mungu na kuukubali uchunguzi Wake; ukifanya kitu kinachoasi sana ama ukimsaliti Mungu, basi atatimiza kiapo chako, na kisha haijalishi kitakachokufanyikia, iwe kuangamia ama kuadibu, ni shida yako mwenyewe. Ulikula kiapo, basi lazima ukitekeleze. Ukila kiapo, lakini ukose kukitekeleza, utaangamia. Kwa kuwa unakula kiapo, Mungu atatimiza kiapo chako. Wengine wanaogopa baada ya kuomba, na kusema, “Ee, jamani, nafasi yangu katika ufisadi imepotea, nafasi yangu kufanya mambo maovu imepotea, nafasi yangu ya kujiingiza katika ulafi wangu wa kidunia imepotea!” Watu hawa bado wanaipenda dunia na dhambi, nao ni hakika wataangamia.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu Anawakamilisha Wale Wanaoupendeza Moyo Wake

509. Kuna kanuni kwa kukamilishwa kwa watu na Mungu, ambayo ni kwamba Yeye hukupa nuru kwa kutumia sehemu yako inayofaa ili uwe na njia ya kutenda na unaweza kujitenga na hali zote hasi, ikisaidia roho yako kupata uhuru, na ikikufanya uweze kumpenda zaidi. Kwa njia hii, unaweza kuiacha tabia potovu ya Shetani. Wewe huna hila na uko wazi, ukiwa tayari kujijua nakutia ukweli katika vitendo. Mungu hakika atakubariki, kwa hiyo unapokuwa dhaifu na hasi, Yeye hukupa nuru maradufu, Akikusaidia kujijua zaidi, kuwa tayari kujitubia, na kuweza zaidi kutenda mambo ambayo unapaswa kuyatenda. Ni kwa njia hii tu ambapo moyo wako unahisi amani na utulivu. Mtu ambaye kwa kawaida huzingatia kumjua Mungu, ambaye huzingatia kujijua, ambaye huzingatia vitendo vyake mwenyewe ataweza kupokea kazi ya Mungu mara kwa mara, mara kwa mara kupokea mwongozo na nuru kutoka kwa Mungu. Hata ingawa yuko katika hali hasi, anaweza kugeuka mara moja, iwe ni kwa sababu ya matendo ya dhamiri au kwa sababu ya nuru kutoka kwa neno la Mungu. Mabadiliko ya tabia ya mtu hufanikishwa daima anapojua hali yake mwenyewe halisi na kujua tabia na kazi ya Mungu. Mtu ambaye yuko tayari kujijua na yuko tayari kuwasiliana ataweza kutekeleza ukweli. Aina hii ya mtu ni mtu ambaye ni mwaminifu kwa Mungu, na mtu ambaye ni mwaminifu kwa Mungu ana ufahamu wa Mungu, uwe ni wa kina au wa juu juu, haba au maridhawa. Hii ni haki ya Mungu, na ni kitu ambacho watu hupata, ni faida yao wenyewe. Mtu ambaye ana maarifa ya Mungu ni yule ambaye ana msingi, ambaye ana maono. Mtu wa aina hii ana hakika kuhusu mwili wa Mungu, na ana hakika kuhusu neno la Mungu na kazi ya Mungu. Bila kujali jinsi Mungu hufanya kazi au kuzungumza, au jinsi watu wengine husababisha vurugu, anaweza kushikilia msimamo wake, na kuwa shahidi kwa Mungu. Kadiri mtu alivyo katika njia hii ndivyo anavyoweza kutekeleza zaidi ukweli anaouelewa. Kwa sababu daima anatenda neno la Mungu, yeye hupata ufahamu zaidi wa Mungu, na analo azimio la kuwa shahidi kwa Mungu milele.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Wale Wanaolenga Kutenda tu Ndio Wanaoweza Kukamilishwa

510. Katika kumwamini Mungu, iwapo mwanadamu anataka mabadiliko kwa tabia yake mwenyewe, basi lazima asijitenge na maisha halisi. Katika maisha halisi, lazima ujijue mwenyewe, ujitelekeze mwenyewe, utende ukweli, na vilevile kujifunza kanuni, maarifa ya kawaida na masharti ya kujiendesha katika mambo yote kabla ya wewe kuweza kutimiza mabadiliko ya polepole. Iwapo utalenga tu ujuzi katika nadharia na kuishi tu katika sherehe za dini bila ya kuingia ndani ya uhalisi, bila kuingia kwenye maisha halisi, basi hutaweza kamwe kuingia katika uhalisi, hutaweza kujijua mwenyewe, kuujua ukweli, au kumjua Mungu, na utakuwa kipofu na mjinga milele. Kazi ya Mungu ya kuwaokoa watu sio kuwaruhusu waishi maisha ya kawaida ya binadamu baada ya kipindi cha muda mfupi, na wala sio ili kubadili mawazo na mafundisho yao yasiyo sahihi. Badala yake, kusudi Lake ni kubadili tabia za zamani za watu, kubadilisha kikamilifu njia yao ya zamani ya maisha, na kubadilisha njia zao zote za mawazo na mtazamo wa akili zilizopitwa na wakati. Kulenga tu maisha ya kanisa pekee hakuwezi kubadili mazoea ya kale ya watu au kubadili njia za kale walizoishi kwa muda mrefu. Lolote litokealo, watu hawapaswi kujitenga na maisha halisi. Mungu anauliza kwamba watu waishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida katika maisha halisi, sio tu katika maisha ya kanisani; kwamba waishi kwa kudhihirisha ukweli katika maisha halisi, sio tu katika maisha ya kanisani; kwamba watimize majukumu yao katika maisha halisi, sio tu katika maisha ya kanisani. Ili kuingia katika uhalisi, mtu lazima apindue vitu vyote kuelekea maisha halisi. Iwapo waumini katika Mungu, watu hawawezi kuja kujijua kupitia kuingia katika maisha halisi, na ikiwa hawawezi kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida katika maisha halisi, watashindwa. Wale wanaomkaidi Mungu wote ni watu ambao hawawezi kuingia katika maisha halisi. Wote ni watu wanaozungumza kuhusu ubinadamu lakini wanaishi kwa kudhihirisha asili ya pepo mbaya. Wote ni watu wanaozungumza kuhusu ukweli lakini wanaishi kwa kudhihirisha kanuni badala yake. Wale wasioweza kuishi kwa kudhihirisha ukweli katika maisha halisi ni wale wanaoamini katika Mungu lakini wanachukiwa na kukataliwa na Yeye. Lazima ufanye mazoezi ya kuingia kwako katika maisha halisi, ujue upungufu wako mwenyewe, ukaidi na upumbavu, na ujue ubinadamu wako usio wa kawaida na udhaifu. Kwa njia hiyo, ufahamu wako wote utaambatanishwa ndani ya hali yako halisi na ugumu. Ni aina hii ya ufahamu pekee ndiyo ya kweli na inaweza kukufanya ushike kwa hakika hali yako mwenyewe na ufanikishe mabadiliko ya tabia yako.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kujadili Maisha ya Kanisa na Maisha Halisi

511. Kula na kunywa maneno ya Mungu, kufanya maombi, kukubali mzigo wa Mungu, kukubali Anachokuaminia—haya yote ni kwa ajili ya kuwa na njia mbele yako. Kadiri unavyozidi kuwa na mzigo mwingi wa agizo la Mungu, ndivyo itakavyokuwa rahisi zaidi kwako kufanywa mtimilifu na Mungu. Wengine hawako tayari kushirikiana katika kumtumikia Mungu hata wakati ambapo wameshurutishwa; hao ni watu wavivu ambao hutamani kufurahia faraja. Kadiri unavyotakiwa kushirikiana katika kumhudumia Mungu, ndivyo utakavyopata uzoefu zaidi. Kwa sababu una mizigo zaidi na una uzoefu zaidi, utakuwa na nafasi zaidi ya kufanywa mtimilifu. Kwa hivyo, ikiwa unaweza kumhudumia Mungu kwa uaminifu utazingatia mzigo wa Mungu, na kwa njia hii utakuwa na nafasi nyingi zaidi za kufanywa mtimilifu na Mungu. Kundi kama hili la watu linafanywa kamilifu na Mungu wakati huu. Kadiri Roho Mtakatifu anavyokugusa hisia, ndivyo utakavyotenga muda zaidi wa kuzingatia mzigo wa Mungu, ndivyo utakavyofanywa mtimilifu na Mungu zaidi, ndivyo Mungu atakavyokupata zaidi, na mwishowe, utakuwa mtu anayetumiwa na Mungu. Sasa, kuna baadhi ambao hawalibebei kanisa mzigo. Watu hawa ni wazembe na wenye ubwege, na wanajali tu miili yao. Wao ni wenye ubinafsi sana na ni vipofu pia. Hutakuwa na mzigo wowote ikiwa huna uwezo wa kuona suala hili kwa dhahiri. Kadiri unavyozidi kuwa mzingatifu wa mapenzi ya Mungu, ndivyo mzigo ambao Mungu atakuaminia utakavyozidi kuwa mzito. Watu wenye ubinafsi hawako tayari kuyapitia mambo kama haya, na hawako radhi kulipa gharama, na kwa sababu hiyo watakosa nafasi ya kufanywa wakamilifu na Mungu. Je, si huku ni kujiumiza? Ikiwa wewe ni mtu ambaye ni mzingatifu wa mapenzi ya Mungu, utakuza mzigo wa kweli kwa ajili ya kanisa. Kwa kweli, badala ya kuuita huu mzigo wa kanisa, badala yake ni mzigo wa maisha yako, kwa sababu mzigo unaoukuza kwa ajili ya kanisa ni kwa ajili yako kufanywa mtimilifu na Mungu kwa kupitia uzoefu kama huu. Kwa hivyo, yeyote anayelibebea kanisa mzigo mzito zaidi na yeyote abebaye mzigo wa kuingia katika maisha watakuwa wale ambao wanafanywa watimilifu na Mungu. Je, umeona hili kwa dhahiri? Ikiwa kanisa unaloshiriki limetawanyika kama mchanga, lakini bado huna wahaka wala wasiwasi, na hata unajitia hamnazo wakati kina ndugu zako hawali au kunywa maneno ya Mungu kwa kawaida, basi huibebi mizigo yoyote. Watu kama hawa hawapendwi na Mungu. Wale wanaopendwa na Mungu huwa na shauku na kiu ya haki na ni wazingatifu wa mapenzi Yake. Kwa hivyo mnapaswa kuwa wazingatifu wa mzigo wa Mungu sasa. Hupaswi kusubiri tabia ya Mungu yenye haki ifunuliwe kwa watu wote kabla ya wewe kuwa mzingatifu wa mzigo wa Mungu. Je, si muda utakuwa umeshapita wakati huo? Sasa ni nafasi nzuri ya kufanywa mtimilifu na Mungu. Ukiruhusu nafasi hii ipotee, utajuta katika maisha yako yote, kama vile Musa alivyoshindwa kuingia katika nchi nzuri ya Kanani na alijuta katika maisha yake yote, akifa kwa majuto. Mara tu Mungu ameifichua tabia Yake yenye hakikwa watu wote, utajawa na majuto. Hata kama Mungu hakuadibu, utajiadibu kutokana na majuto yako mwenyewe. Wengine hawaridhishwi na hili. Ikiwa huamini, basi subiri uone. Watu wengine watatumika kama utimizaji wa maneno haya. Je, uko tayari kuwa sadaka ya dhabihu kwa maneno haya?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuwa Mzingatifu wa Mapenzi ya Mungu ili Upate Utimilifu

512. Roho Mtakatifu ana njia ya kutembea katika kila mtu, na humpa kila mtu fursa za kukamilishwa. Kupitia uhasi wako unajulishwa upotovu wako mwenyewe, na kisha kwa njia ya kuacha uhasi utapata njia ya kutenda, na huku ndiko kukamilishwa kwako. Aidha, kwa njia ya mwongozo na mwangaza wa siku zote wa mambo fulani chanya ndani yako, utatimiza shughuli yako kwa kuamili na kukua katika umaizi na kupata utambuzi. Wakati hali zako ni nzuri, uko tayari hasa kusoma neno la Mungu, na hasa tayari kumwomba Mungu, na unaweza kuyahusisha mahubiri unayoyasikia na hali zako mwenyewe. Kwa nyakati kama hizo Mungu hukupatia nuru na kukuangaza ndani, na kukufanya utambue mambo fulani ya kipengele chanya. Huku ni kukamilishwa kwako katika kipengele chanya. Katika hali hasi, wewe ni dhaifu na hasi, na huhisi kuwa huna Mungu moyoni mwako, lakini Mungu hukuangaza, akikusaidia kupata njia ya kutenda. Kutoka nje ya hili ni kupata ukamilisho katika hali chanya. Mungu anaweza kumkamilisha mwanadamu katika vipengele hasi na chanya. Inategemea kama unaweza kupata uzoefu, na kama wewe hufuatilia kukamilishwa na Mungu. Kama kwa hakika unatafuta kukamilishwa na Mungu, basi kilicho hasi hakiwezi kukufanya upoteze, lakini kinaweza kukuletea mambo ambayo ni halisi zaidi, na kinaweza kukufanya uweze zaidi kujua kile kilichopunguka ndani yako, uweze zaidi kufahamu sana hali zako halisi, na kuona kwamba mtu hana kitu, wala si kitu; kama hupitii majaribio, hujui, na daima utahisi kuwa wewe ni wa hadhi ya juu kuliko wengine na bora kuliko kila mtu mwingine. Kwa njia hii yote utaona kwamba yote yaliyotangulia yalifanywa na Mungu na kulindwa na Mungu. Kuingia katika majaribio hukuacha bila upendo au imani, huna sala, na huwezi kuimba nyimbo—na, bila kulitambua, katikati ya hili unakuja kujijua. Mungu ana njia nyingi za kumkamilisha mwanadamu. Yeye hutumia mazingira ya kila aina ili shughulikia tabia potovu ya mwanadamu, na hutumia vitu mbalimbali ili kumuweka mwanadamu wazi; katika suala moja Yeye humshughulikia mwanadamu, katika jingine Yeye humuweka mwanadamu wazi, na katika jingine Yeye humfichua mwanadamu, kuzichimbua na kuzifichua “siri” katika vina vya moyo wa mwanadamu, na kumwonyesha mwanadamu asili yake kwa kuzifichua hali zake nyingi. Mungu humkamilisha mwanadamu kupitia mbinu nyingi—kupitia ufunuo, ushughulikiaji, usafishwaji, na kuadibu—ili mwanadamu aweze kujua kwamba Mungu ni wa vitendo.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Wale Wanaolenga Kutenda tu Ndio Wanaoweza Kukamilishwa

513. Kwa sasa, kile ambacho mnafaa kutafuta kimsingi ni kukamilishwa na Mungu katika mambo yote, na kukamilishwa na Mungu kupitia kwa watu wote, mambo yote na vitu vyote ambavyo mnakumbwa navyo, ili mambo zaidi ya kile Mungu Alicho yatashirikishwa ndani yenu. Lazima kwanza mpokee urithi wa Mungu ulimwenguni kabla ya kustahili kurithi baraka nyingi na kubwa zaidi kutoka kwa Mungu. Mambo yote haya ndiyo ambayo mnafaa kutafuta na ambayo kwanza mnafaa kuelewa. Zaidi unavyotafuta kukamilishwa na Mungu katika mambo yote, ndivyo utakavyoweza kuona mkono wa Mungu zaidi katika mambo yote, na hivyo kutafuta kwa bidii kuingia katika hali ya neno la Mungu na uhalisia wa neno Lake kupitia mitazamo tofauti na katika mambo tofauti. Huwezi kutosheka na hali hasi kama kutotenda dhambi tu, au kutokuwa na dhana, kutokuwa na filosofia ya kuishi, na kutokuwa na hiari ya binadamu. Mungu humkamilisha mwanadamu kwa njia tofauti, na inawezekana katika mambo yote kwako kukamilishwa hatimaye. Huwezi tu kukamilishwa kwa kuzingatia mambo halisi, lakini pia mambo hasi, na hivyo kuboresha kile unachopata. Kila siku kunazo fursa za kukamilishwa na muda wa kupatwa na Mungu. Baada ya kipindi cha kupitia mambo kama haya, utabadilika pakubwa. Utaweza sasa kimaumbile kufaidi utambuzi katika mambo mengi ambayo hukuyaelewa awali; bila ya kuhitaji wengine kukufunza, bila kujua, utaweza kufahamishwa na Mungu, ili uweze kuwa na fahamisho katika mambo yote na mambo yote utakayopitia yatakuwa mengi. Mungu atakuongoza wewe ili usije ukapotoka kwa vyovyote vile. Kisha utawekwa wazi kwenye njia ya kufanywa kuwa mtimilifu na Yeye.

… Kama mtapenda kukamilishwa na Mungu, lazima mjifunze kupitia mambo yote na kupatiwa nuru katika yote mnayoyapitia. Kila unapokumbwa na kitu, kiwe kizuri au kibaya, unafaa kufaidi kutoka katika kitu hicho na hakifai kukufanya ukae tu. Haijalishi ni nini, unafaa kuweza kukitilia maanani kwa kusimama upande wa Mungu, na wala si kuchambua au kukisoma kutoka kwa mtazamo wa binadamu (huku ni kupotoka katika hali unayopitia). Kama hivi ndivyo utakavyopitia mambo katika maisha yako, basi moyo wako utazidiwa na mizigo ya maisha yako; utaishi siku zote katika mwanga wa uso wa Mungu na hutaweza kupotoka kwa urahisi katika matendo yako. Binadamu wa aina hii ana matarajio makubwa. Kunazo fursa nyingi za kukamilishwa na Mungu. Yote haya yanategemea kama ni nyinyi ndinyi mnaompenda Mungu kwa kweli na kama mnalo azimio la kukamilishwa na Mungu, kupatwa na Mungu, na kupokea baraka na urithi Wake. Haitakubalika kwenu kuwa na azimio tu. Lazima muwe na maarifa mengi, vinginevyo siku zote mtapotoka katika matendo yenu. Mungu yuko radhi kumkamilisha kila mmoja wenu. Kama ilivyo sasa, ingawa wengi tayari wamekubali kazi ya Mungu kwa muda mwingi, wamejiwekea mipaka ya kufurahia tu neema ya Mungu na wako radhi tu kupokea tulizo fulani la mwili kutoka Kwake. Hawako radhi kupokea ufunuo zaidi na wa kiwango cha juu zaidi, hali ambayo inaonyesha kwamba moyo wa binadamu ungali nje siku zote. Ingawa kazi ya binadamu, huduma yake, na moyo wake wa upendo kwa Mungu vyote vina kasoro chache zaidi, kuhusiana na kiini cha binadamu na kufikiria kwake kusiko na nuru, binadamu bado daima hutafuta amani na furaha ya mwili, na huwa hajali masharti na makusudio Mungu ya katika kumkamilisha binadamu ni yapi. Kwa hivyo maisha ya wengi yangali machafu na yaliyooza, bila dalili zozote za mabadiliko. Yeye hasa haichukilii imani katika Mungu kama suala lenye umuhimu. Badala yake, ni kana kwamba anayo imani tu kwa ajili ya binadamu mwengine, akitenda bila ukweli au kujitolea, na akiishi tu kwa vile viwango vya chini zaidi vya maisha, akiendelea kuwepo tu bila kusudi lolote. Wachache ndio wanaotafuta kuingia ndani ya neno la Mungu katika mambo yote, huku wakifaidi mambo mengi ya kusitawisha, wakiwa wenye utajiri mkubwa zaidi katika nyumba ya Mungu siku hii, na wakipokea baraka zaidi za Mungu. Kama unatafuta kukamilishwa na Mungu katika mambo yote na unaweza kurithi ahadi za Mungu hapa ulimwenguni; kama unatafuta kupatiwa nuru na Mungu katika mambo yote na huiruhusu miaka kuyoyoma tu huku ukiwa umezubaa, hii ndiyo njia inayostahili kuingia kwa bidii. Ni kupitia kwa njia hii tu ndipo unastahili na unafaa kukamilishwa na Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ahadi kwa Wale Ambao Wamekamilishwa

514. Roho Mtakatifu hafanyi kazi tu kwa baadhi ya wanadamu wanaotumiwa na Mungu, lakini hata zaidi kanisani. Anaweza kuwa akifanya kazi kwa yeyote. Anaweza kufanya kazi ndani yako sasa, na baada ya wewe kuwa na uzoefu nayo, Anaweza kufanya kazi ndani ya mtu mwingine ajaye. Fanya hima ufuate; unapozidi kufuata mwangaza wa sasa, ndivyo maisha yako yanaweza ku kua. Haijalishi yeye ni mwanadamu wa aina gani, alimradi Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yake, kuwa na hakika kufuata. Chukua uzoefu wake kupitia wako mwenyewe, na utapokea mambo ya juu hata zaidi. Kwa kufanya hivyo utaona ukuaji haraka zaidi. Hii ni njia ya ukamilifu kwa mwanadamu na njia ambayo maisha hukua. Njia ya ukamilifu inafikiwa kupitia utii wako wa kazi ya Roho Mtakatifu. Hujui ni kupitia kwa mtu wa aina gani ndiyo Mungu Atafanya kazi kukukamilisha, wala kupitia mtu yupi, tukio, ama jambo ndiyo Atakuwezesha kuingia katika umiliki na kupata ufahamu fulani. Ukiweza kutembea kwenye njia hii sawa, hii inaonyesha kwamba kuna matumaini makubwa kwako kukamilishwa na Mungu. Kama huwezi kufanya hivyo, inaonyesha kwamba maisha yako ya baadaye ni ya dhalili na giza. Mara unapoenda kwenye njia iliyo sahihi, utapata ufunuo katika mambo yote. Bila kujali yale ambayo Roho Mtakatifu atafichua kwa wengine, ukiendelea kupitia mambo wewe mwenyewe kwa msingi wa maarifa yao, basi uzoefu huu utakuwa sehemu ya maisha yako, na utaweza kuwakimu wengine kwa sababu ya huu uzoefu. Wale wanaowakimu wengine kwa kuyarudia maneno ni wale wasio na uzoefu wowote; lazima ujifunze kupata, kupitia mwangaza na nuru ya wengine, njia ya kutenda kabla ya kuzungumza kuhusu uzoefu na maarifa yako halisi. Hii itakuwa ya manufaa zaidi kwa maisha yako binafsi. Unapaswa kuwa na uzoefu kwa njia hii, kutii yote yatokayo kwa Mungu. Unapaswa kutafuta mapenzi ya Mungu katika vitu vyote na kujifunza masomo katika vitu vyote, ili maisha yako yaweze kukua. Vitendo vya aina hii huleta ukuaji wa haraka zaidi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watapatwa na Mungu

515. Uko tayari kweli kukamilishwa? Kama kweli uko tayari kukamilishwa na Mungu, basi utakuwa na ujasiri kuweka kando mwili wako, na utaweza kutekeleza maneno ya Mungu na kutokuwa mtu anayekaa tu ama mnyonge. Utaweza kutii yote yatokayo kwa Mungu, na vitendo vyako vyote, viwe vimefanywa hadharani au faraghani, vitastahiki kwa Mungu. Kama wewe ni mtu mwaminifu, na unatenda ukweli katika mambo yote, basi utakamilishwa. Wale wanadamu wadanganyifu wanaotenda njia moja mbele ya wengine na nyingine nyuma yao hawako tayari kukamilishwa. Wote ni wana wa maangamizo na uharibifu; wao si wa Mungu lakini ni wa Shetani. Hao si aina ya wanadamu waliochaguliwa na Mungu! Kama vitendo na tabia yako haviwezi kustahiki mbele ya Mungu ama kufikiriwa na Roho wa Mungu, hii ni thibitisho kwamba wewe una shida. Ukikubali tu hukumu na kuadibu kwa Mungu, na kuweka umuhimu katika mabadiliko ya tabia yako ndipo utafika kwenye njia ya kukamilishwa. Ikiwa kweli uko tayari kukamilishwa na Mungu na kufanya mapenzi ya Mungu, basi unapaswa kutii kazi yote ya Mungu na kutotoa neno lolote la kulalamika, wala hupaswi kutathmini ama kuhukumu kazi ya Mungu utakavyo. Haya ni masharti ya msingi kabisa ya kukamilishwa na Mungu. Mahitaji ya lazima kwa wale wanaotaka kukamilishwa na Mungu ni haya: fanya mambo yote kwa moyo unaompenda Mungu. Inamaanisha nini “kufanya mambo kwa moyo unaompenda Mungu”? Inamaanisha kwamba vitendo na tabia yako yote inaweza kuletwa mbele ya Mungu. Kwa sababu una nia sawa, iwapo vitendo vyako ni sawa ama vibaya, huogopi vikionyeshwa kwa Mungu ama kwa ndugu zako; unathubutu kuapa mbele ya Mungu. Lazime uonyeshe kila nia, fikra, na wazo lako mbele ya Mungu ili ayachunguze; ukitenda na kuingia kwa njia hii, basi maendeleo katika maisha yako yatakuwa mepesi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watapatwa na Mungu

516. Iwapo unataka kutumika na kukamilishwa na Mungu, ni lazima umiliki kila kitu: uwe tayari kuteseka, imani, uvumilivu, utiifu na uwezo wa kupitia kazi ya Mungu, kufahamu mapenzi Yake kujali huzuni Yake, na kadhalika. Kumkamilisha mtu si rahisi, na kila kisa cha usafishaji unachopitia kinahitaji imani na upendo wako. Kama unataka kukamilishwa na Mungu, haitoshi kukimbia tu mbele kwenye njia, wala haitoshi kujitumia tu kwa ajili ya Mungu. Ni lazima umiliki mambo mengi ili uweze kuwa mtu ambaye anakamilishwa na Mungu. Unapokabiliwa na mateso ni lazima uweze kuweka kando masilahi ya mwili na usifanye malalamiko dhidi ya Mungu. Wakati Mungu anajificha kutoka kwako, ni lazima uweze kuwa na imani ya kumfuata Yeye, kudumisha upendo wako wa awali bila kuuruhusu ufifie au kutoweka. Haijalishi anachofanya Mungu, ni lazima utii mpango Wake na uwe tayari kuulaani mwili wako mwenyewe badala ya kulalamika dhidi Yake. Wakati unakabiliwa na majaribu, lazima umridhishe Mungu, ingawa unaweza kulia kwa uchungu au uhisi kusita kuhusu kuacha kitu unachopenda. Huu tu ndio upendo wa kweli na imani. Haijalishi kimo chako halisi ni kipi, ni lazima kwanza umiliki nia ya kupitia ugumu na imani ya kweli, na ni pia lazima uwe na nia ya kuutelekeza mwili. Unapaswa kuwa tayari kuvumilia ugumu wa kibinafasi na kupata hasara kwa maslahi yako binafsi ili kuridhisha mapenzi ya Mungu. Lazima pia uwe na uwezo wa kuhusi majuto kujihusu moyoni mwako: Hapo zamani, hukuweza kumridhisha Mungu, na sasa unaweza kujuta mwenyewe. Ni lazima usipungukiwe katika yoyote ya hali hizi—Ni kupitia katika vitu hivi ndiyo Mungu atakukamilisha. Usipoweza kufikia viwango hivi, basi huwezi kukamilishwa.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Wanaopaswa Kukamilishwa Lazima Wapitie Usafishaji

517. Mabadiliko katika tabia hasa huhusu mabadiliko katika asili ya watu. Mambo ya asili ya mtu hayawezi kuonekana kutoka kwa mienendo ya nje; yanahusisha moja kwa moja thamani na umuhimu wa kuwepo kwake. Yaani, yanahusisha moja kwa moja mitazamo ya mtu kuhusu maisha na maadili yake, mambo yaliyo ndani kabisa ya nafsi yake, na kiini chake. Mtu ambaye hawezi kukubali ukweli hatakuwa na mabadiliko katika hali hizi. Ni kwa kupitia kazi ya Mungu pekee, kuingia kikamilifu katika ukweli, kubadili maadili na mitazamo yake kuhusu kuwepo na maisha, kulinganisha msoni yake na ya Mungu, na kuwa na uwezo wa kutii na kujitoa kabisa kwa Mungu ndio tabia zake zinaweza kusemekana zimebadilika. Huenda ukaonekana kufanya juhudi fulani, unaweza ukawa thabiti unapokabiliwa na shida, huenda ukaweza kutekeleza utaratibu wa kazi kutoka walio juu, au huenda ukaweza kwenda popote unapoambiwa kwenda, lakini haya ni mabadiliko madogo tu katika mienendo yako, na hayatoshi kujumuisha mabadiliko katika tabia yako. Huenda ukaweza kukimbia katika njia nyingi, kuvumilia shida nyingi na kustahamili fedheha kuu; huenda ukajihisi karibu sana na Mungu, na Roho Mtakatifu anaweza kukufanyia kazi fulani. Hata hivyo, Mungu anapokuomba ufanye jambo fulani ambalo halipatani na fikira zako, huenda bado usitii, lakini utafute visababu, na kuasi na kumpinga Mungu, hata kufikia kiwango cha wewe kumhakiki Mungu na kumpinga Yeye. Hili ni tatizo kubwa! Hili linaonyesha kwamba bado una asili inayompinga Mungu na kwamba hujapitia mabadiliko yoyote kabisa.

Kimetoholewa kutoka katika “Unachopaswa Kujua Kuhusu Kuigeuza Tabia Yako” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

518. Mgeuzo wa tabia si jambo rahisi hivyo. “Matendo yangu yamebadilika, na ninafahamu ukweli. Naweza pia kuzungumza kuhusu uzoefu fulani katika kila kipengele cha ukweli na naweza kuzungumza kuhusu umaizi fulani mdogo. Zaidi ya hayo, Roho Mtakatifu amenishutumu kuhusu jambo hili na sasa naweza kuliacha kidogo na naweza kutii kidogo.” Hili halihesabiki kama mgeuzo katika tabia ya maisha. Kwa nini? Unaweza kuacha kidogo, lakini unachotenda bado hakijafikia kiwango cha kutia ukweli katika vitendo kweli. Labda mazingira yako yanafaa kwa muda na hali zako zinafaa, au hali zako zinakushurutisha kutenda kwa njia hii, au hali yako ya akili ni imara na Roho Mtakatifu anafanya kazi, basi unaweza kulifanya. Kama ungekuwa katikati ya majaribio kama Ayubu ambaye alivumilia maumivu ya majaribio, au kama Petro ambaye Mungu alimwambia afe, je, ungeweza kusema, “Hata kama ningekufa baada ya kukujua, ingekuwa sawa”? Mgeuzo katika tabia haufanyiki ghafla sana, na haimaanishi kwamba unaweza kutia ukweli katika vitendo katika kila mazingira baada ya wewe kuelewa ukweli. Hii inahusisha asili ya mwanadamu. Upande wa nje, inaonekana kana kwamba unatia ukweli katika vitendo, lakini kwa kweli, hali ya matendo yako haionyeshi kwamba unatia ukweli katika vitendo. Kuna watu wengi ambao, punde tu wanayo mienendo fulani ya nje, huamini. “Je, kwani sitimizi wajibu wangu? Je, sikuacha familia na kazi yangu? Je, kwani sitii ukweli katika vitendo kwa kutimiza wajibu wangu?” Lakini Mungu hatambui kwamba unatia ukweli katika vitendo. Wale wote ambao matendo yao yamechafuliwa na nia na malengo ya kibinafsi hawatendi ukweli. Kusema kweli, aina hii ya mwenendo huenda itashutumiwa na Mungu; haitasifiwa au kukumbukwa na Yeye. Kulichangua hili zaidi, unafanya uovu na mwenendo wako unampinga Mungu. Kutoka nje, mambo haya unayoyafanya yanaonekana kuambatana na ukweli: Hukatizi wala kusumbua chochote na hujafanya maharibifu yoyote ya kweli au kukiuka ukweli wowote. Kinaonekana kuwa chenye mantiki na cha maana, ilhali asili ya matendo yako inahusika na kufanya uovu na kumpinga Mungu. Kwa hivyo unapaswa kupambanua kama kumekuwa na mabadiliko katika tabia yako na kama unatia ukweli katika vitendo kwa kutazama nia nyuma ya matendo yako kulingana na maneno ya Mungu. Haiamuliwi na maneno au maoni ya kibinadamu. Badala yake, inategemea Mungu kusema kama unakubali mapenzi Yake au la, kama matendo yako yana uhalisi wa ukweli au la, na kama yanafikia mahitaji Yake na viwango Vyake au la. Kujipima tu dhidi ya matakwa ya Mungu ndiyo sahihi. Mgeuzo katika tabia na kutia ukweli katika vitendo si sahili na rahisi kama wanavyodhani watu. Je, mnaelewa sasa? Mna uzoefu wowote katika jambo hili? Huenda msilielewe ikiwa linahusisha kiini cha masuala. Mmeingia juujuu sana. Mnakimbia huku na huko siku nzima, tangu macheo hadi magharibi, mnarauka mapema na kukawia kwenda kulala, lakini hamwelewi waziwazi mgeuzo wa tabia ni nini au hali yake ya kweli ni nini. Je, hii si ya juujuu? Haijalishi kama ninyi ni wa zamani au wapya, huenda msihisi kiini na kina cha mgeuzo katika tabia. Mnajuaje kama Mungu anawasifu au la?

Kimetoholewa kutoka katika “Unachopaswa Kujua Kuhusu Kuigeuza Tabia Yako” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

519. Watu wanaweza kuwa na tabia nzuri, lakini hiyo haimaanishi kuwa wako na ukweli. Bidii ya watu inaweza tu kuwafanya wazingatie mafundisho na kufuata kanuni; watu wasio na ukweli hawana namna ya kutatua shida halisi, na mafundisho hayawezi kushikilia nafasi ya ukweli. Wana ukweli ndani yao, wanatambua masuala yote, wanajua jinsi ya kutenda kulingana na mapenzi ya Mungu, jinsi ya kutenda kulingana na kanuni za ukweli, jinsi ya kutenda ili kumridhisha Mungu, nao wanaelewa asili ya upotovu wanaoufichua. Mawazo na dhana zao wenyewe vinapofichuliwa, wanaweza kutambua na kuunyima mwili. Hivi ndivyo mabadiliko katika tabia yanavyoonyeshwa. Kitu cha muhimu kuhusu mabadiliko katika tabia ni kwamba yana ukweli na uwazi, na unapotekeleza mambo, yanauweka ukweli katika matendo kwa usahihi wa karibu na upotovu wao hauonekani mara nyingi. Kwa jumla, mtu ambaye tabia yake imebadilika huonekana kuwa na busara na mwenye utambuzi, na kutokana na kuelewa kwake kwa ukweli, kujidai na kiburi havifichuliwi sana. Anaweza kuona kila kitu kwa uwazi, basi hawi mwenye kiburi baada ya kupata uwazi huu. Anaweza kuwa na ufahamu wa taratibu kuhusu ni ipi nafasi ya mwanadamu, jinsi ya kutenda kwa busara, jinsi ya kuwa mtiifu, nini anachofaa kusema na nini asichofaa kusema, na nini cha kusema na nini cha kutenda kwa watu gani. Hii ndiyo sababu inasemwa kuwa watu wa aina hii ni wenye busara kiasi. Wale ambao wana mabadiliko katika tabia zao wanaishi kwa kudhihirisha sura ya binadamu kwa kweli, nao wana0 ukweli; hawategemei ushawishi wa wengine. Wale ambao wamekuwa na mabadiliko katika tabia wako imara zaidi, hawasitasiti, na haijalishi wako katika hali gani, wanajua jinsi ya kutimiza wajibu wao sawasawa na jinsi ya kufanya mambo ili kumridhisha Mungu. Wale ambao tabia zao zimebadilika hawalengi nini cha kufanya ili kujifanya waonekane wazuri katika kiwango cha juujuu—wanao uwazi wa ndani kuhusu kile cha kufanya ili kumridhisha Mungu. Kwa hivyo, kutoka nje wanaweza kukosa kuonekana wenye shauku sana ama kama wamefanya jambo lolote kubwa, lakini kila kitu wanachofanya kina maana, kina thamani, na kina matokeo ya kiutendaji. Wale ambao tabia zao zimebadilika wana uhakika kuwa na ukweli mwingi—hii inaweza kuthibitishwa kwa mitazamo yao kuhusu mambo na kanuni zao katika vitendo vyao. Wale wasio na ukweli hawajakuwa na mabadiliko yoyote katika tabia hata kidogo. Mabadiliko katika tabia haimaanishi kuwa na ubinadamu uliokomaa au wenye uzoefu. Kwa kiasi kikubwa, inahusu matukio ambapo baadhi ya sumu za kishetani katika asili ya watu zinabadilika kama matokeo ya kufikia maarifa kuhusu Mungu na ufahamu wa ukweli. Hiyo ni kusema, sumu hizo zinatakaswa, na ukweli unaoonyeshwa na Mungu unaanza kustawi ndani ya watu hawa, unakuwa maisha yake, nao unakuwa msingi wa kuwepo kwake. Hapo tu ndipo wanakuwa watu wapya, na hivyo tabia yao inabadilika. Mabadiliko katika tabia hayamaanishi kwamba tabia za nje za watu ni za upole kuliko hapo awali, kuwa walikuwa na kiburi awali wanazungumza kwa busara, au kwamba hawakuwa wanamsikiza mtu yeyote lakini sasa wanaweza kuwasikiza wengine; mabadiliko haya ya nje hayawezi kusemwa kuwa ni mabadiliko katika tabia. Bila shaka, mabadiliko katika tabia yanajumuisha hali hizi, lakini jambo lililo muhimu zaidi ni kuwa maisha yao ya ndani yamebadilika. Ukweli unaoonyeshwa na Mungu unakuwa maisha yao hasa, baadhi ya sumu za kishetani zilizo ndani zimetolewa, mitazamo yao imebadilika kabisa, na hakuna kati ya hiyo inakubaliana na ile ya dunia. Anaona waziwazi njama na sumu za joka kubwa jekundu; amefahamu kiini cha kweli cha maisha. Kwa hivyo maadili ya maisha yake yamebadilika—hili ndilo badiliko la muhimu zaidi na kiini cha mabadiliko katika tabia.

Kimetoholewa kutoka katika “Tofauti Kati Ya Mabadiliko Ya Nje Na Mabadiliko Katika Tabia” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

520. Iwapo ungependa kusafishwa kutokana na upotovu na kupitia mabadiliko ya tabia maishani mwako basi unahitaji kuupenda ukweli na uwezo wa kuukubali ukweli. Inaamanisha nini kuukubali ukweli? Kukubali ukweli kunaashiria kwamba bila kujali aina ya tabia potovu unayo au ni sumu gani ya joka kuu jekundu imeingia ndani ya asili yako, unakiri unapofichuliwa na manenoya Mungu na kulitii maneno haya; unayakubali bila kupinga, bila kutoa sababu za kutotii au kufanya chaguo, na unakuja kujijua mwenyewe kwa mujibu wa yale Amesema. Hivi ndivyo inavyomaanisha kukubali neno la Mungu. Bila kujali kile ambacho Amesema, bila kujali kiasi ambacho matamshi Yake yanaweza kuuchoma moyo wako, na bila kujali maneno Anayotumia, unaweza kulikubali mradi uwe ukweli, unaweza kuyakubali mradi yanapatana na uhalisi. Unaweza kuyatii maneno ya Mungu bila kujali unayaelewa kwa kina kiasi gani, na ukubali na kutii mwanga ambao unafichuliwa na Roho Mtakatifu ambao unashirikiwa ba ndugu na dada. Wakati mtu wa aina hii amefuata ukweli hadi kiwango fulanianaweza kupata ukweli na kufikia kubadilishwa kwa tabia yake. Hata iwapo wale wasiopenda ukweli wanaweza kuwa wenye ubinadamu mwema, inapokuja kwa ukweli, wao hawachukui msimamo na hawalichukulii kwa makini. Ingawa wanaweza kuwa wenye matendo mema, na wanaweza kujitoa kwa kutumiwa na Mungu, na wanaweza kumkana Shetani, hawawezi kutimiza kubadilika kwa tabia zao.

Kimetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

521. La muhimu katika kufikia badiliko katika tabia ni kujua asili ya mtu mwenyewe, na hili ni lazima lifanyike kulingana na ufunuo kutoka kwa Mungu. Ni katika neno la Mungu tu ambapo mtu anaweza kujua asili yake mbaya, afahamu katika asili yake mwenyewe sumu mbalimbali za Shetani, atambue kuwa yeye ni mjinga na mpumbavu, na atambue dalili dhaifu na hasi katika asili yake. Baada ya haya kujulikana kikamilifu, na unaweza kwa hakika kujichukia na kunyima mwili, daima kutekeleza neno la Mungu, na kuwa na mapenzi ya kujiwasilisha kikamilifu kwa Roho Mtakatifu na kwa neno la Mungu, basi utakuwa umeianza njia ya Petro. Bila neema ya Mungu, na bila nuru na mwongozo kutoka kwa Roho Mtakatifu, ingekuwa vigumu kuitembea njia hii, kwa sababu watu hawamiliki ukweli na hawawezi kujisaliti wenyewe. Kuitembea njia ya Petro ya ukamilisho inaegemea kuwa na azimio, kuwa na imani, na kumtegemea Mungu. Mbali na haya, mtu lazima ajiweke chini ya kazi ya Roho Mtakatifu; katika mambo yote, mtu hawezi kutenda bila maneno ya Mungu. Hivi ndivyo vipengele muhimu, Kupata kujitambua mwenyewe kupitia uzoefu ni vigumu sana bila kazi ya Roho mtakatifu, ni vigumu sana kuingia ndani. Kuitembea njia ya Petro mtu lazima azingatie juu ya kujijua mwenyewe na kubadili tabia yake. Njia ya Paulo haikuwa ya kutafuta maisha au kusisitiza ufahamu wa kibinafsi; yeye hasa alizingatia kufanya kazi na ushawishi wake na ukasi wake. Motisha yake ilikuwa kupata baraka za Mungu kwa ubadilishano na kazi na mateso yake, na kupokea tuzo kutoka kwa Mungu. Hii motisha yake ilikuwa mbovu. Paulo hakuzingatia uzima, wala hakuweka umuhimu kutimiza badiliko la kitabia; alilenga tu juu ya tuzo. Kwa sababu alikuwa na malengo yasiyofaa, njia aliyoitembelea bila shaka ilikuwambaya. Hili ililetwa na kiburi na hali yake ya majivuno. Kwa dhahiri, Paulo hakumiliki ukweli wowote, wala hakuwa na dhamiri au sababu yeyote. Katika kuwaokoa na kuwabadilisha watu, Mungu kimsingi hubadilisha watu kwa kubadilisha tabia zao. Kusudi la maneno Yake ni kufikia katika watu matokeo ya mabadiliko katika tabia uwezo wa kumjua Mungu, kujiweka chini Yake, na kumwabudu Yeye kwa njia ya kawaida. Hili ndilo kusudi la maneno ya Mungu na la kazi Yake. Njia aliyoitumia Paulo kutafuta ilikuwa ya ukiukaji wa moja kwa moja na katika mgongano namapenzi ya Mungu; ilienda kinyume kabisa. Hata hivyonjia ya Petro ya kutafuta, ilifanana kabisa na mapenzi ya Mungu, ambayo hasa ni matokeo ambayo Mungu hutamani kutimiza kwa wanadamu. Kwa hiyo, njia ya Petro imebarikiwa na hupata sifa ya Mungu. Kwa sababu njia ya Paulo ni ukiukaji wa mapenzi ya Mungu, Mungu kwa hiyo anaichukia na huilaani.

Kimetoholewa kutoka katika “Kujijua Mwenyewe Hasa Ni Kujua Asili ya Binadamu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

522. Kwa hivyo kama ujuzi wa watu juu yao wenyewe ni wa juujuu sana, watapata kuwa haiwezekani kutatua matatizo, na tabia zao za maisha hazitabadilika kabisa. Ni muhimu kujijua mwenyewe kwa kiwango cha kina kabisa, ambayo inamaanisha kuijua asili yako mwenyewe: ni vipengele vipi ambavyo vimejumuishwa katika asili hiyo, jinsi vitu hivi vilivyoanza, na kule vilipotoka. Aidha, unaweza kuchukia mambo haya kweli? Je, umeona nafsi yako mwenyewe mbaya na asili yako mbovu? Ikiwa kwa hakika unaweza kuuona ukweli kujihusu mwenyewe, basi utaanza kujichukia mwenyewe kabisa. Wakati unapojichukia mwenyewe kabisa na kisha unatenda neno la Mungu, utakuwa na uwezo wa kunyima mwili na kuwa na nguvu ya kutekeleza ukweli bila shida. Kwa nini watu wengi hufuata tamaa zao za kimwili? Kwa sababu wanajiona kuwa wazuri kabisa, wakihisi kuwa vitendo vyao ni viadilifu na vya haki, kwamba hawana makosa, na hata kwamba wako sahihi kabisa, kwa hiyo wao wana uwezo wa kutenda kwa dhana kuwa haki iko upande wao. Wakati mtu anapotambua asili yake ya kweli ilivyo—jinsi ilivyo mbaya, jinsi inavyostahili kudharauliwa, na jinsi ilivyo ya kusikitisha—basi yeye si mwenye majivuno sana, hajigambi ovyo ovyo sana, hajifurahii kama hapo awali. Mtu kama huyo huhisi, “Lazima niwe mwenye ari na mpole, na nitende baadhi ya maneno ya Mungu. Kama sivyo, basi siwezi kufikia kiwango cha kuwa mwanadamu, na nitaona aibu kuishi mbele ya Mungu.” Kwa hakika mtu hujiona kuwa hafifu, kama kweli asiye na maana. Wakati huu, inakuwa rahisi kwake kutekeleza ukweli, naye ataonekana kwa kiwango fulani kuwa kama mwanadamu anavyopaswa kuwa. Ni pale tu ambapo watu kwa hakika hujichukia kabisa ndipo wanaweza kunyima mwili. Kama hawajichukii, hawataweza kunyima mwili. Mtu kujichukia kweli kunajumuisha mambo machache: Kwanza, kujua asili yake mwenyewe; na pili, kujiona kama yeye ni mwenye shida na wa kudharaulika, kujiona kuwa mdogo kupindukia na asiye na maana, na kuona nafsi yake kuwa yenye kudharaulika na chafu. Mtu anapoona kikamilifu kile alicho kwa hakika, na matokeo haya yakafikiwa, basi yeye kweli hupata ufahamu juu yake mwenyewe, na inaweza kusemwa kwamba amekuja kujijua mwenyewe kikamilifu. Ni hapo tu ndipo anaweza kwa hakika kujichukia mwenyewe, kufikia hata kujilaani mwenyewe, na ahisi kwa kweli kwamba amepotoshwa sana na Shetani kiasi kwamba hafanani tena na mwanadamu. Kisha, siku moja, wakati tishio la kifo linapoonekana, mtu kama huyu atafikiri, “Hii ni adhabu ya haki ya Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye haki; Kwa hakika mimi lazima nife!” Wakati huu, yeye hatalalamika, wala kumlaumu Mungu, akihisi tu kwamba yeye ni wa kudharaulika, mchafu sana na mpotovu, kwamba anapaswa kuangamizwa na Mungu na roho kama yake haifai kuishi duniani. Wakati huu, mtu huyu hatampinga Mungu, sembuse kumsaliti Mungu. Iwapo mtu hajijui mwenyewe, na bado hujiona kuwa mzuri sana, basi wakati kifo kinapokuja kubisha, mtu huyu atafikiria, “Nimetenda vyema sana katika imani yangu. Jinsi nimetafuta kwa nguvu! Nimejitolea mengi sana, nimeumia sana, ilhali hatimaye, Mungu sasa ananiuliza nife. Sijui haki ya Mungu iko wapi. Kwa nini Ananitaka nife? Ikiwa hata mtu kama mimi anafaa kufa, basi ni nani atakayeokolewa? Je! Si jamii ya wanadamu itafikia mwisho?” Kwanza kabisa, mtu huyu ana dhana juu ya Mungu. Pili, mtu huyu analalamika, na hatii hata kidogo. Hii ni kama tu Paulo: Wakati alipokaribia kufa, hakujijua mwenyewe, Na kufikia wakati adhabu ya Mungu ilipokaribia, hakukuwa na muda wa kutubu.

Kimetoholewa kutoka katika “Kujijua Mwenyewe Hasa Ni Kujua Asili ya Binadamu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

523. Watu waingiapo katika njia ya ukamilifu, tabia zao za zamani zaweza kubadilishwa. Aidha, maisha yao huendelea kukua na taratibu hujitosa zaidi katika ukweli. Wanaweza kuchukia dunia na kuwachukia wale wote ambao hawafuati ukweli. Hususan hujichukia wao wenyewe, na hata zaidi ya hayo, wanajitambua vyema. Wana hiari kuishi kulingana na ukweli na hulenga kufuata ukweli. Hawako radhi kuishi katika mawazo ya bongo zao, na huchukia kujitukuza, kujisifu, na kujiinua kwa mwanadamu. Wananena kwa adabu ya hali ya juu, wanafanya mambo kwa utambuzi na hekima, ni waaminifu na watiifu kwa Mungu. Wakipitia kuadibu na hukumu, wao hawakuwi wanyonge au wasioonyesha hisia tu, bali hutoa shukrani kwa ajili ya kuadibu na hukumu zitokazo kwa Mungu. Wanaamini hawawezi kuishi bila kuadibu na hukumu ya Mungu; wanaweza kupata ulinzi Wake kupitia haya. Hawafuati imani ya amani na furaha na ya kutafuta mkate wa kuwashibisha. Wala hawafuati raha za muda za kimwili. Hili ndilo wakamilifu huwa nalo.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (4)

524. Ikiwa mtu anaweza kumridhisha Mungu huku akitimiza wajibu wake, ni mwenye maadili katika maneno ya matendo yake, na anaweza kuingia katika uhalisi a vipengele vya ukweli, basi huyu ni mtu ambaye anakamilishwa na Mungu. Inaweza kusemekana kuwa kazi na maneno ya Mungu yamekuwa ya kufaa kabisa kwa watu kama hao, kwamba maneno ya Mungu yamekuwa maisha yao, wamepata ukweli, na wanaweza kuishi kulingana na maneno ya Mungu. Baada ya hili, asili ya mwili wao—yaani, msingi maalum wa uwepo wao wa kwanza—itatikisika na kuanguka. Baada ya watu kuwa na maneno ya Mungu kama maisha yao, watakuwa watu wapya. Maneno ya Mungu yakiwa maisha yao, maono ya kazi ya Mungu, matakwa Yake kwa wanadamu, ufunuo Wake kwa wanadamu, na viwango vya maisha ya kweli ambayo Mungu anawahitaji watimize vikiwa maisha yao, wakiishi kulingana na maneno haya na ukweli huu, basi wanakamilishwa na Mungu. Watu kama hawa wanazaliwa tena, na wamekuwa watu wapya kupitia maneno ya Mungu. Hii ni njia ambayo Petro aliitumia kuufuatilia ukweli; Ilikuwa njia ya kukamilishwa, kukamilishwa na maneno ya Mungu, na kupata uzima kutoka kwa maneno ya Mungu. Ukweli ulioonyeshwa na Mungu ulikuwa maisha yake, na wakati huo tu ndipo alikuwa mtu aliyepata ukweli.

Kimetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kuitembea Njia ya Petro” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

525. Ikiwa watu wana ufahamu wa kweli wa tabia ya Mungu, na wanaweza kutoa sifa ya kweli kwa utakatifu Wake na haki Yake, basi wanajua Mungu kwa kweli na kumiliki ukweli; ni hapo tu ndipo wanaishi nuruni. Ni wakati tu ambapo maoni ya watu kuhusu dunia na maisha yanabadilika ndipo wanabadilika kimsingi. Mtu anapokuwa na lengo la maisha na kujiheshimu kulingana na ukweli, mtu anapomtii Mungu kabisa na kuishi kulingana na neno la Mungu, mtu anapohisi kuwa na amani na kuchangamshwa ndani ya roho yake, moyo wa mtu unapokuwa huru bila giza, na mtu anapoishi kwa huru kabisa na bila kuzuiwa kwa uwepo wa Mungu—hapo tu ndipo atakapoishi maisha ya mwanadamu ya kweli na kuwa mtu anayemiliki ukweli. Aidha, ukweli wote unaomiliki unatoka kwa neno la Mungu na kwa Mungu Mwenyewe. Mtawala wa ulimwengu mzima na kila kitu—Mungu Mkuu Zaidi—Anakupenda wewe, kama mtu halisi anayeishi maisha ya kweli ya mwanadamu. Je, nini linaweza kuwa la maana zaidi kuliko kibali cha Mungu? Mtu wa aina hii ni yule aliye na ukweli.

Kimetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

526. Kama, kwa imani yake kwa Mungu, mwanadamu hayuko makini katika mambo ya maisha, hafuati kuingia katika ukweli, hazingatii mabadiliko katika tabia yake, ama kufuata maarifa ya kazi ya Mungu, basi hawezi kufanywa mkamilifu. Kama unatamani kufanywa mkamilifu, lazima uelewe kazi ya Mungu. Hasa, lazima uelewe umuhimu wa adabu na hukumu Yake, na kwa nini kazi hii inafanywa juu ya mwanadamu. Je, unaweza kukubali? Wakati wa adabu ya aina hii, unaweza kupata uzoefu na maarifa kama Petro? Ukifuata maarifa ya Mungu na ya kazi ya Roho Mtakatifu, na kuzingatia mabadiliko katika tabia yako, basi una fursa ya kufanywa mkamilifu.

Kwa wale ambao wanatakiwa kufanywa wakamilifu, hatua hii ya kazi ya kushinda ni ya lazima; Ni baada ya kushindwa tu ndipo mwanadamu anaweza kuiona kazi ya kufanywa mkamilifu. Hakuna maana kubwa ya kufanya kazi ya kushindwa, ambayo itakufanya usiwe mwenye kufaa kufanya kazi yoyote ya Mungu. Hutakuwa na uwezo wowote wa kufanya kazi yako ya kueneza injili, kwa sababu hufuati maisha, na hujibadilishi na kujifanya mpya, na hivyo basi huna uzoefu kamili wa maisha. Katika kazi hii ya hatua kwa hatua, uliwahi kuwa na nafasi ya mtendaji-huduma, na foili[a], lakini kwa hakika usipofuata kuwa kama Petro, na ufuasi wako sio kama wenye njia ambayo Petro alifanywa mkamilifu, basi, kiasili hutapata mabadiliko katika tabia yako. Kama wewe ni mtu anayefuata kuwa mkamilifu, basi utakuwa na ushuhuda, na utasema: “Katika hii kazi ya hatua kwa hatua ya Mungu, nimekubali kazi ya Mungu ya adabu na hukumu, na hata kama nimepitia mateso mengi, nimepata kujua jinsi Mungu hufanya mwanadamu kuwa mkamilifu, nimepata kazi iliyofanywa na Mungu, nimekuwa na maarifa ya haki ya Mungu, na adabu Yake imeniokoa. Tabia Yake ya haki imekuja juu yangu, na ikaniletea baraka na neema; ni hukumu Yake na adabu ambazo zimenilinda na kunitakasa. Kama singeadibiwa na kuhukumiwa na Mungu, na kama maneno makali ya Mungu hayangekuja juu yangu, singalimjua Mungu, ama kuokolewa. Leo, naona, kama kiumbe, kwamba mtu hafurahii tu vitu vilivyoumbwa na Muumba, lakini pia, la maana sana ni kwamba viumbe vyote watafurahia haki ya tabia ya Mungu, na kufurahia hukumu Yake ya haki, kwa sababu tabia ya Mungu ina umuhimu katika furaha ya Mwanadamu. Kama kiumbe ambaye amepotoshwa na Shetani, kila mmoja anafaa kufurahia tabia ya haki ya Mungu. Katika tabia Yake ya haki, kuna adabu na hukumu, na pia, kuna upendo mkuu. Ingawa sina uwezo wa kupata kwa kikamilifu upendo wote wa Mungu leo, nimekuwa na bahati nzuri ya kuuona, na katika haya, nimebarikiwa.” Hii ndio njia ambayo wale waliofanywa wakamilifu hutembea na maarifa wanayoongelea. Watu hao wanafanana na Petro; wanao uzoefu sawa na wa Petro. Watu kama hao pia ndio wale ambao wamepokea maisha, na walio na ukweli. Wanapokuwa na uzoefu mpaka mwisho kabisa, wakati wa hukumu ya Mungu kwa hakika wataweza kikamilifu kujitoa katika ushawishi wa Shetani, na atakuwa wa Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu

527. Ninalotaka Mimi ni watu kama Petro, watu wanaofuata kufanywa wakamilifu. Ukweli wa leo unatolewa kwa wale ambao wanautamani na kuutafuta. Wokovu huu unapewa wale ambao wanatamani kuokolewa na Mungu, na haujakusudiwa kuwafaidi tu, lakini ili pia ili mpatwe na Mungu. Mnampata Mungu ili Mungu pia awapate. Leo nimenena hayo maneno kwenu, na mmeyasikia, na mnafaa kutenda kulingana na maneno haya. Mwishowe, mkiweka maneno haya katika matendo ndipo nitakapowapata nyinyi kupitia katika maneno haya; na pia, mtakuwa mmepata maneno haya, kumaanisha, mtakuwa mmepata wokovu mkuu. Punde mtakapofanywa wasafi, mtakuwa wanadamu halisi. Kama huwezi kuishi kulingana na ukweli, ama kuishi kulingana na aliyefanywa mkamilifu, basi inaweza kusemwa kuwa wewe si binadamu, ila wewe ni mfu anayetembea, mnyama, kwa sababu huna ukweli, ni kusema huna pumzi ya Yehova, na basi wewe ni mtu aliyekufa ambaye hana roho! Ingawa unaweza kuwa na ushuhuda baada ya kushindwa, unachopata ni wokovu kidogo, na hujakuwa kiumbe chenye roho. Ingawa umepata adabu na hukumu, tabia yako haijafanywa upya ama kubadilishwa kama matokeo; umebaki tu ulivyokuwa, bado wewe ni wa Shetani, na wewe si mtu aliyetakaswa. Wale tu waliofanywa wakamilifu ndio wenye thamani, na watu tu kama hao ndio wamepata maisha ya kweli.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu

528. Katika njia yako ya baadaye ya huduma, unawezaje kutimiza mapenzi ya Mungu? Jambo moja muhimu ni kufuatilia kuingia katika uzima, kufuatilia mabadiliko katika tabia, na kufuatilia kuingia kwa kina zaidi ndani ya ukweli—hii ndiyo njia ya kutimiza kufanywa mkamilifu na kupatwa na Mungu. Nyote mnapaswa kupokea agizo la Mungu, kwa hiyo ni nini hicho? Hii inahusiana na hatua inayofuata ya kazi, ambayo itakuwa kazi kuu zaidi itakayotekelezwa kotekote katika ulimwengu mzima. Kwa hiyo sasa mnapaswa kufuatilia mabadiliko katika tabia yenu ya maisha ili muwe kweli thibitisho la Mungu kupata utukufu kupitia kwa kazi Yake katika siku za baadaye, na kufanywa kuwa vielelezo vya kazi Yake ya siku za baadaye. Kazi yote ya leo inaweka msingi kwa ajili ya kazi ya siku za baadaye; ni kwa wewe kutumiwa na Mungu na ili uweze kuwa na ushuhuda Wake. Ikiwa hii ni chombo cha kazi yako, utaweza kupata uwepo wa Roho Mtakatifu. Kadri chombo cha kazi yako kilivyo juu, ndivyo itawezekana kwako wewe kukamilishwa zaidi. Kadri unavyofuatilia ukweli, ndivyo Roho Mtakatifu atafanya kazi zaidi. Kadri unavyokuwa na nguvu zaidi kwa kazi, ndivyo utakavyopata zaidi. Roho Mtakatifu huwakamilisha watu kulingana na hali yao ya ndani. Baadhi ya watu husema kwamba hawako radhi kutumiwa na Mungu au kukamilishwa na Yeye, kwamba itakuwa sawa alimuradi mwili wao unabaki salama na kamili na hawapitii msiba wowote. Watu wengine hawako radhi kuingia katika ufalme, lakini wako radhi kushuka katika shimo lisilo na mwisho. Katika hali hiyo, Mungu atakupa matamanio hayo. Chochote unachofuatilia, Mungu atakutimizia. Kwa hiyo unafuatilia nini sasa? Je, unafuatilia kukamilishwa? Matendo na mienendo yako ya sasa ni kwa ajili ya kufanywa mkamilifu na Mungu, kwa ajili ya kupatwa na Yeye? Ni lazima siku zote ujipime kwa njia hii katika maisha yako ya kila siku. Ukilenga moyo wako katika kufuatilia lengo moja, Mungu bila shaka atakukamilisha. Hii ni njia ya Roho Mtakatifu. Njia inayoongozwa na Roho Mtakatifu inapatikana kupitia kwa kutafuta kwa watu. Kadri unavyotamani kukamilishwa na kupatwa na Mungu, ndivyo Roho Mtakatifu atafanya kazi zaidi ndani yako. Kadri usivyotafuta, na kadri unavyokuwa mbaya na kukimbia, ndivyo zaidi Roho Mtakatifu anakosa nafasi za kufanya kazi. Roho Mtakatifu atakuacha polepole. Uko radhi kukamilishwa na Mungu? Uko radhi kupatwa na Mungu? Uko radhi kutumiwa na Mungu? Mnapaswa kufuatilia kufanya kila kitu kwa ajili ya kukamilishwa, kupatwa, na kutumiwa na Mungu, kuruhusu kila kitu katika ulimwengu kuona matendo ya Mungu yakifichuliwa ndani yenu. Miongoni mwa mambo yote, nyinyi ni watawala wa hayo, na miongoni mwa yote yaliyopo, mtamruhusu Mungu kupata ushuhuda Wake na utukufu Wake kwa sababu yenu—hii inaonyesha kwamba nyinyi ni kizazi kilichobarikiwa zaidi.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Wale Ambao Tabia Zao Imebadilika ni Wale Ambao Wameingia Katika Uhalisi wa Neno la Mungu

Tanbihi:

a. “Foili” inahusu mtu au kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.

Iliyotangulia: M. Kuhusu Jinsi ya Kutupilia Mbali Ushawishi wa Shetani na Kupata Wokovu

Inayofuata: XI. Maneno Juu ya Kumjua Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp