M. Kuhusu Jinsi ya Kutupilia Mbali Ushawishi wa Shetani na Kupata Wokovu

488. Mwanadamu alipoteza moyo wake wa kumcha Mungu baada ya kupotoshwa na Shetani na kupoteza kazi ambayo kiumbe mmoja wa Mungu anapaswa kuwa nayo, kuwa adui asiyemtii Mungu. Mwanadamu alimilikiwa na Shetani na kufuata amri za Shetani; hivyo Mungu hakuwa na njia ya kufanya kazi miongoni mwa viumbe Wake, na hakuweza zaidi kuwafanya viumbe Wake kumcha. Mwanadamu aliumbwa na Mungu, na anapaswa kumwabudu Mungu, lakini mwanadamu kwa kweli alimpuuza Mungu na kumwabudu Shetani. Shetani alikuwa sanamu katika moyo wa mwanadamu. Hivyo Mungu alipoteza nafasi yake katika moyo wa mwanadamu, kusema kwamba Alipoteza maana ya uumbaji Wake wa mwanadamu, na ili kurejesha maana ya uumbaji Wake wa mwanadamu lazima arejeshe mfano wa awali wa mwanadamu na kumtoa mwanadamu tabia yake potovu. Ili kumrejesha mwanadamu kutoka kwa Shetani, lazima Amwokoe mwanadamu kutoka kwa dhambi. Kwa njia hii tu ndiyo Anaweza kurejesha mfano wa awali wa mwanadamu polepole na kurejesha kazi halisi ya mwanadamu, na mwishowe kurejesha ufalme Wake. Maangamizo ya mwisho ya wale wana wa uasi pia yatafanywa ili kumruhusu mwanadamu kumwabudu Mungu vizuri zaidi na kuishi duniani vizuri zaidi. Kwa sababu Mungu alimuumba mwanadamu, Atamfanya mwanadamu amwabudu; kwa sababu Anataka kurejesha kazi halisi ya mwanadamu, Atairejesha kabisa, na bila ughushi wowote. Kurudisha mamlaka Yake kunamaanisha kumfanya mwanadamu amwabudu na kumfanya mwanadamu amtii; kunamaanisha kwamba Atamfanya mwanadamu aishi kwa sababu Yake na kufanya adui zake waangamie kwa sababu ya mamlaka Yake; kunamaanisha kwamba Atafanya kila sehemu Yake kuendelea miongoni mwa binadamu na bila upinzani wowote wa mwanadamu. Ufalme Anaotaka kuanzisha ni ufalme Wake Mwenyewe. Binadamu Anaotaka ni wale wanaomwabudu, wale wanaomtii kabisa na wana utukufu Wake. Asipookoa binadamu wapotovu, maana ya uumbaji Wake wa mwanadamu hautakuwa chochote; Hatakuwa na mamlaka yoyote miongoni mwa mwanadamu, na ufalme Wake hautaweza kuweko tena duniani. Asipoangamiza wale adui wasiomtii, Hataweza kupata utukufu Wake wote, wala Hataweza kuanzisha ufalme Wake duniani. Hizi ndizo ishara za ukamilishaji wa kazi Yake na ishara za ukamilishaji wa utimilifu Wake mkubwa; kuangamiza kabisa wale miongoni mwa binadamu wasiomtii, na kuwaleta wale waliokamilika rahani.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja

489. Mwanadamu wa kwanza kabisa alikuwa kwa mikono ya Mungu, lakini kwa sababu ya majaribu ya Shetani na upotovu wake, mwanadamu alifungwa na Shetani na kuanguka katika mikono ya yule mwovu. Kwa hivyo, Shetani akakuwa mlengwa wa kushindwa katika kazi ya Mungu ya usimamizi. Kwa sababu Shetani alichukua umiliki wa mwanadamu, na kwa sababu mwanadamu ndiye kiini cha usimamizi wote wa Mungu, kama mwanadamu ni wa kuokolewa, basi ni lazima anyakuliwe kutoka mikononi mwa Shetani, yaani mwanadamu ni lazima achukuliwe baada ya kutekwa nyara na Shetani. Hivyo, Shetani lazima ashindwe kupitia mabadiliko ya tabia ya mwanadamu ya zamani, mabadiliko ambayo hurejesha hisia zake za awali, na kwa njia hii, mwanadamu, ambaye ametekwa nyara, anaweza kunyakuliwa kutoka mikononi mwa Shetani. Kama mwanadamu anawekwa huru kutokana na ushawishi wa Shetani na utumwa wake, Shetani ataaibika, mwanadamu hatimaye atarejeshwa, na Shetani atakuwa ameshindwa. Na kwa sababu mwanadamu amewekwa huru kutoka kwa ushawishi wa giza wa Shetani, mwanadamu atakuwa mabaki ya vita hivi vyote, na Shetani atakuwa ndiye mlengwa ambaye ataadhibiwa punde tu vita hivi vitakapokamilika, na baada ya hapo kazi nzima ya wokovu wa mwanadamu itakuwa imekamilika.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu

490. Wale wanaoishi chini ya ushawishi wa giza, ni wale ambao wanaishi katikati ya kifo, ni wale ambao wametawaliwa na Shetani. Bila kuokolewa na Mungu, na kuhukumiwa na kuadibiwa na Mungu, watu wanakuwa hawana uwezo kukwepa athari ya kifo, hawawezi kuwa hai. Wafu hawa hawawezi kuwa ushuhuda kwa Mungu, wala hawawezi kutumiwa na Mungu, wala kuingia katika ufalme. Mungu anataka ushuhuda wa walio hai, na sio wafu, na Anaomba kwamba walio hai, wala sio wafu, wamfanyie Yeye kazi. “Wafu” ni wale ambao wanampinga na kumwasi Mungu, ni wale ambao ni mbumbumbu katika roho na hawaelewi maneno ya Mungu, ni wale ambao hawaweki ukweli katika matendo na hawana utii hata kidogo kwa Mungu, na ni wale ambao wamemilikiwa na Shetani na kunyanyaswa na Shetani. Wafu wanajionyesha wenyewe kwa kuupinga ukweli, kwa kumwasi Mungu, na kwa kuwa duni, wa kudharaulika, kuwa waovu, katili, wadanganyifu, na kudhuru kwa siri. Ingawa watu wa namna hiyo wanakula na kunywa maneno ya Mungu, hawana uwezo wa kuishi kwa kudhihirisha maneno ya Mungu; wanaishi, lakini ni wafu wanaotembea, ni maiti zinazopumua. Wafu hawawezi kabisa kumridhisha Mungu, wala kumtii kikamilifu. Wanaweza tu kumdanganya, kusema maneno ya makufuru juu Yake, na kumsaliti, na yote wanayoyaishi kwa kudhihirisha hufichua asili ya Shetani. Ikiwa watu wanatamani kuwa viumbe hai, na kuwa na ushuhuda wa Mungu, na kuthibitishwa na Mungu, wanapaswa kukubali wokovu wa Mungu, wanapaswa kuwa watiifu katika hukumu na kuadibu Kwake, na wanapaswa kukubali kwa furaha kushughulikiwa na kupogolewa na Mungu. Ni hapo tu ndipo wataweza kuweka katika matendo ukweli wote unaohitajika na Mungu, na baada ya hapo ndipo wataweza kupata wokovu wa Mungu, na kuwa viumbe hai kabisa. Walio hai wanaokolewa na Mungu, wamehukumiwa na kuadibiwa na Mungu, wapo tayari kujitoa wenyewe na wana furaha kutoa maisha yao kwa Mungu, na wapo tayari kujitoa maisha yao yote kwa Mungu. Pale ambapo walio hai watachukua ushuhuda wa Mungu ndipo Shetani ataweza kuaibishwa, ni walio hai tu ndio wanaweza kueneza kazi ya injili ya Mungu, ni walio hai tu ndio wanaoupendeza moyo wa Mungu, ni walio hai tu ndio watu halisi. Mwanadamu wa asili aliyeumbwa na Mungu alikuwa hai, lakini kwa sababu ya uharibifu wa Shetani mwanadamu anaishi katikati ya kifo, na anaishi chini ya ushawishi wa Shetani, na hivyo watu hawa wamekuwa wafu ambao hawana roho, wamekuwa ni maadui ambao wanampinga Mungu, wamekuwa nyenzo ya Shetani, na wamekuwa mateka wa Shetani. Watu wote walio hai ambao wameumbwa na Mungu wamekuwa wafu, na hivyo Mungu amepoteza ushuhuda wake, na Amempoteza mwanadamu, ambaye Alimuumba na ndiye kiumbe pekee aliye na pumzi Yake. Ikiwa Mungu ataamua kurejesha ushuhuda Wake, na kuwarejesha wale ambao waliumbwa kwa mkono wake lakini ambao wamechukuliwa mateka na Shetani, basi ni lazima awafufue ili waweze kuwa viumbe hai, na ni lazima awaongoe ili kwamba waweze kuishi katika nuru Yake. Wafu ni wale ambao hawana roho, wale ambao ni mbumbumbu kupita kiasi, na wale ambao wanampinga Mungu. Aidha, ni wale ambao hawamjui Mungu. Watu hawa hawana nia hata ndogo ya kumtii Mungu, kazi yao ni kumpinga na kuasi dhidi Yake, na hawana hata chembe ya utii. Walio hai ni wale ambao roho zao zimezaliwa upya, wale wanaojua kumtii Mungu, na ambao ni watii kwa Mungu. Wanao ukweli, na ushuhuda, na ni watu wa aina hii tu ndio wanaompendeza Mungu katika nyumba Yake.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Je, Wewe ni Mtu Ambaye Amepata Uzima?

491. Je, ushawishi wa giza ni nini? “Ushawishi wa giza” ni ushawishi wa Shetani kuwadanganya, kuwapotosha kuwafunga na kuwatawala watu; ushawishi wa shetani ni ushawishi ambao una hali ya kifo. Wale wote ambao wanaishi chini ya miliki ya shetani wamehukumiwa kuangamia.

Unawezaje kuepuka ushawishi wa giza baada ya kupata imani katika Mungu? Baada ya kumwomba Mungu kwa dhati, unaelekeza moyo wako Kwake kikamilifu. Katika hatua hii, moyo wako unasongezwa na Roho wa Mungu, uko tayari kujitoa mwenyewe kikamilifu, na katika wakati huu, umeepuka ushawishi wa giza. Kama yote ambayo mtu anafanya yanampendeza Mungu na anapatana na matakwa Yake, basi yeye ni mtu ambaye anaishi ndani ya maneno ya Mungu, yeye ni mtu anayeishi chini ya utunzaji na ulinzi wa Mungu. Kama watu hawawezi kutenda maneno ya Mungu, daima wakimpumbaza na kutenda katika namna ya uzembe na Yeye, na hawaamini katika uwepo Wake, watu kama hao wote wanaishi chini ya ushawishi wa giza. Watu ambao hawajapokea wokovu wa Mungu wote wamemilikiwa na Shetani, yaani, hao wote wanaishi chini ya ushawishi wa giza. Wale ambao hawamwamini Mungu wamemilikiwa na Shetani. Hata wale ambao wanaamini katika kuwepo kwa Mungu huenda si lazima wawe wanaishi katika nuru ya Mungu, kwa sababu wale ambao wanamwamini huenda si lazima wawe wanaishi ndani ya maneno ya Mungu, na huenda si lazima wawe watu ambao wanaweza kumtii Mungu. Mtu anamwamini tu Mungu, na kwa sababu ya kushindwa kwake kumjua Mungu, bado anaishi ndani ya sheria za zamani, anaishi ndani ya maneno yaliyokufa, anaishi katika maisha ambayo ni giza na si ya hakika, hajatakaswa kikamilifu na Mungu au kupatwa kikamilifu na Mungu. Kwa hivyo, ni dhahiri ya kwamba wale wasiomwamini Mungu wanaishi chini ya ushawishi wa giza, hata wale ambao wanamwamini Mungu huenda wakawa bado wanaishi chini ya ushawishi wake, kwa ajili Roho Mtakatifu hajatekeleza kazi juu yao. Wale ambao hawajapokea neema ya Mungu au rehema ya Mungu, na wale ambao hawawezi kuona kazi ya Roho Mtakatifu, wote wanaishi chini ya ushawishi wa giza; wale ambao wanafurahia tu neema ya Mungu na bado hawamjui pia wanaishi chini ya ushawishi wa giza wakati mwingi. Kama mtu anamwamini Mungu na bado anatumia wakati mwingi wa maisha yake akiishi chini ya ushawishi wa giza, basi kuwepo kwa mtu huyu kumepoteza maana yake, bila kutaja wale ambao hawaamini katika uwepo wa Mungu.

Wale wote ambao hawawezi kukubali kazi ya Mungu au wanaokubali kazi ya Mungu lakini hawawezi kukidhi matakwa Yake wanaishi chini ya ushawishi wa giza; wale tu wanaofuatilia ukweli na wana uwezo wa kukidhi matakwa ya Mungu watapokea baraka kutoka Kwake, na ni wao tu wataepuka ushawishi wa giza. Watu ambao hawajafunguliwa, ambao siku zote wamedhibitiwa na mambo fulani na ambao hawawezi kutoa mioyo yao kwa Mungu, ni watu ambao wako chini ya utumwa wa Shetani, na wanaoishi chini ya hali ya kifo. Wale wasio waaminifu kwa wajibu wao wenyewe, wasio waaminifu kwa agizo la Mungu na wale ambao hawatekelezi jukumu lao kanisani wanaishi chini ya ushawishi wa giza. Wale ambao husumbua maisha ya kanisa kimakusudi, wale ambao huharibu mahusiano kati ya akina ndugu na kimakusudi, au kuweka pamoja magenge yao wenyewe, wanaishi hata zaidi chini ya ushawishi wa giza; wao wanaishi ndani ya utumwa wa Shetani. Wale walio na uhusiano usio sahihi na Mungu, walio na tamaa za kifahari daima, ambao daima wanataka kupata faida, na ambao kamwe hawatafuti mabadiliko katika tabia yao ni watu ambao wanaishi chini ya ushawishi wa giza. Wale ambao hawako imara daima, ambao hawajatilia maanani utendaji wao wa ukweli, na ambao hawatafuti kukidhi matakwa ya Mungu ila kuridhisha tu miili yao wenyewe ni watu ambao pia wanaishi chini ya ushawishi wa giza na kufunikwa katika kifo. Wale ambao hujihusisha na hila na udanganyifu wakati wa kutekeleza kazi ya Mungu, ambao wanashughulikia Mungu katika njia ya kizembe, wanamdanganya Mungu, na ambao daima hujifikiria, ni watu wanaoishi chini ya ushawishi wa giza. Wale wote ambao hawawezi kumpenda Mungu kwa dhati, ambao hawafuatilii ukweli, na wasiozingatia kubadilisha tabia yao, wanaishi chini ya ushawishi wa giza.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Epuka Ushawishi wa Giza na Utapatwa na Mungu

492. Mwanadamu anaishi katika mwili, ambayo ina maana anaishi katika kuzimu ya binadamu, na bila hukumu na adabu ya Mungu, mwanadamu ni mchafu kama Shetani. Mwanadamu atawezaje kuwa mtakatifu? Petro aliamini kwamba adabu na hukumu ya Mungu ndio uliokuwa ulinzi bora zaidi wa mwanadamu na neema kubwa. Ni kwa njia ya adabu na hukumu ya Mungu ndipo mwanadamu angeweza kugutuka, na kuchukia mwili, na kumchukia Shetani. Nidhamu kali ya Mungu inamweka huru kutokana na ushawishi wa Shetani, inamweka huru kutokana na dunia yake ndogo, na inamruhusu kuishi katika mwanga wa uwepo wa Mungu. Hakuna wokovu bora zaidi kuliko adabu na hukumu! Petro aliomba, “Ee Mungu! Mradi tu Wewe unaniadibu na kunihukumu, nitajua kwamba Wewe hujaniacha. Hata kama Huwezi kunipa furaha au amani, na kufanya niishi katika mateso, na kunirudi mara nyingi, bora tu Hutaniacha moyo wangu utakuwa na amani. Leo hii, adabu Yako na hukumu umekuwa ulinzi wangu bora na baraka yangu kubwa. Neema unayonipa inanilinda. Neema unayoweka juu yangu leo ni kielelezo cha tabia Yako ya haki, na ni adabu na hukumu; zaidi ya hayo, ni majaribu, na, zaidi ya hapo, ni maisha ya mateso.” Petro alikuwa na uwezo wa kuweka kando raha ya mwili na kutafuta mapenzi zaidi na ulinzi zaidi, kwa sababu alikuwa amepata neema nyingi kutoka kwa adabu na hukumu ya Mungu. Katika maisha yake, kama mwanadamu anatamani kutakaswa na kufikia mabadiliko katika tabia yake, kama anatamani kuishi kwa kudhihirisha maisha yenye maana, na kutimiza wajibu wake kama kiumbe, basi lazima akubali adabu na hukumu ya Mungu, na lazima asiruhusu nidhamu ya Mungu na kipigo cha Mungu kiondoke kwake, ili aweze kujiweka huru kutokana na kutawalwa na ushawishi wa Shetani na kuishi katika mwanga wa Mungu. Ujue kwamba adabu ya Mungu na hukumu ni mwanga, na mwanga wa wokovu wa mwanadamu, na kwamba hakuna baraka bora zaidi, neema au ulinzi bora kwa ajili ya mwanadamu. Mwanadamu anaishi chini ya ushawishi wa Shetani, na yupo katika mwili; kama yeye hatatakaswa na kupokea ulinzi wa Mungu, basi mwanadamu atakuwa milele mpotovu zaidi. Kama yeye anataka kumpenda Mungu, basi lazima atakaswe na kuokolewa. Petro aliomba, “Mungu, wakati Unanitendea wema ninapata furaha, na kuhisi faraja; wakati unaniadibu, najisikia faraja kubwa zaidi na furaha. Ingawa mimi ni mdhaifu, na kuvumilia mateso yasiyotajika, ingawa kuna machozi na huzuni, Unajua kwamba huzuni huu ni kwa sababu ya kutotii kwangu, na kwa sababu ya udhaifu wangu. Mimi ninalia kwa sababu siwezi kukidhi hamu Yako, nahisi huzuni na majuto kwa sababu mimi sitoshi kwa mahitaji Yako, lakini niko tayari kufikia ulimwengu huu, niko tayari kufanya yote niwezayo ili nikuridhishe. Adabu Yako imeniletea ulinzi, na kunipa wokovu bora; hukumu Yako inazidi ustahimili Wako na uvumilivu Wako. Bila adabu Yako na hukumu, singefurahia huruma Yako na rehema. Leo, naona zaidi kwamba upendo wako umepita mipaka ya mbinguni na kuwa bora ya yote. Upendo wako sio tu huruma na fadhili; hata zaidi ya hayo, ni adabu na hukumu. Adabu Yako na hukumu imenipa mengi. Bila adabu Yako na hukumu, hakuna hata mmoja angetakaswa, na hakuna hata mmoja angeweza kupata upendo wa Muumba. Ingawa nimevumilia mamia ya majaribio na mateso, na hata nimekuwa karibu na kifo, haya yameniruhusu kukujua Wewe kwa kweli na kupata wokovu mkuu. Kama adabu Yako, hukumu na nidhamu vingeondoka kutoka kwangu, basi ningeishi gizani, chini ya himaya ya Shetani. Mwili wa binadamu una faida gani? Kama adabu Yako na hukumu ingeniwacha, ingekuwa kana kwamba Roho Wako alikuwa ameniacha, ni kama Wewe Haukuwa tena pamoja nami. Kama ingekuwa vile, ni jinsi gani ningeendelea kuishi? Kama Wewe utanipa ugonjwa, na kuchukua uhuru wangu, naweza kuendelea kuishi, lakini adabu Yako na hukumu vikiondoka kutoka kwangu, sitakuwa na njia ya kuendelea kuishi. Kama ningekuwa bila adabu Yako na hukumu, ningepoteza upendo Wako, upendo ambao ni mkuu sana mpaka sina maneno ya kuueleza. Bila Upendo wako, ningeishi chini ya miliki ya Shetani, na singeweza kuuona uso wako mtukufu. Ningewezaje kuendelea kuishi? Giza kama hili, maisha kama haya, singeweza kuvumilia. Mimi kuwa na wewe ni kama kukuona Wewe, hivyo ni jinsi gani ningeweza kukuacha? Ninakusihi, nakuomba usichukue faraja yangu kubwa kutoka kwangu, hata kama ni maneno machache tu ya uhakikisho. Nimefurahia upendo wako, na leo hii siwezi kuwa mbali na Wewe; ningewezaje kutokupenda Wewe? Nimemwaga machozi mengi ya huzuni kwa sababu ya upendo Wako, ilhali daima nimehisi kuwa maisha kama haya ni ya maana zaidi, yenye uwezo mwingi wa kuniimarisha, yenye uwezo zaidi wa kunibadilisha, na yenye uwezo zaidi wa kunifanya nifikie ukweli ambao lazima viumbe wawe nao.”

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu

493. Mwili wa mwanadamu ni wa Shetani, umejaa tabia za uasi, ni mchafu kiasi cha kusikitisha, na ni kitu chenye najisi. Watu hutamani raha ya mwili kupita kiasi na kuna maonyesho mengi sana ya mwili; hii ndiyo maana Mungu hudharau mwili wa mwanadamu kwa kiwango fulani. Watu wanapotupa mambo machafu, potovu ya Shetani, wao hupata wokovu wa Mungu. Lakini bado wasipoachana na uchafu na upotovu, basi bado wanamilikiwa na Shetani. Ujanja, udanganyifu, na ukora wa watu yote ni mambo ya Shetani. Wokovu wa Mungu kwako ni ili kukuokoa kutoka katika mambo haya ya Shetani. Kazi ya Mungu haiwezi kuwa na kosa; yote inafanywa ili kuwaokoa watu kutoka gizani. Wakati ambapo umeamini hadi kwa kiwango fulani na unaweza kuachana na upotovu wa mwili, na hufungwi tena pingu na upotovu huu, je, hutakuwa umeokolewa? Wakati ambapo unamilikiwa na Shetani huwezi kumdhihirisha Mungu, wewe ni kitu kichafu, na huwezi kupokea urithi wa Mungu. Mara tu unapotakaswa na kufanywa mkamilifu, utakuwa mtakatifu, utakuwa mtu wa kawaida, na utabarikiwa na Mungu na kuwa mtu anayemfurahisha Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Utendaji (2)

494. Maisha yote ya mwanadamu yamekuwa chini ya himaya ya Shetani, na hakuna mtu yeyote anayeweza kujitoa kutoka katika ushawishi wa Shetani yeye mwenyewe. Wote wanaishi katika dunia chafu, kwa upotovu na utupu, bila maana yoyote au thamani; wanaishi maisha ya kutojali kwa ajili ya mwili, tamaa, na kwa ajili ya Shetani. Hakuna maana yoyote kwa kuwepo kwao. Mwanadamu hana uwezo wa kupata ukweli utakaomweka huru kutoka kwa ushawishi wa Shetani. Ingawa mwanadamu anaamini katika Mungu na anasoma Biblia haelewi jinsi ya kujitoa kutoka kwa ushawishi wa Shetani. Kutoka kitambo, watu wachache sana wametambua siri hii, wachache sana wameielewa. Hivyo, hata kama mwanadamu anamchukia Shetani, na anachukia mwili, hajui jinsi ya kujitoa kutoka kwa ushawishi mkuu wa Shetani. Je, leo bado hamjamilikiwa na Shetani? Hamjuti juu ya matendo yenu ya uasi, zaidi ya hayo, hamhisi kama wachafu na waasi. Baada ya kumpinga Mungu, bado mna amani ya moyo na mnahisi utulivu mwingi. Je, utulivu wako si kwa sababu wewe ni mpotovu? Je, hii amani ya mawazo haitokani na kuasi kwako? Mwanadamu anaishi katika jehanamu ya binadamu, anaishi katika ushawishi wa giza la Shetani; mkabala katika ardhi, mapepo yanaishi na mwanadamu, yakienea katika mwili wa mwanadamu. Duniani, hauishi katika Paradiso ya kupendeza. Mahali ambapo ulipo ni ulimwengu wa Shetani, jehanamu ya binadamu, dunia ya chini. Mwanadamu asipotakaswa, basi yeye ni wa uchafu; asipolindwa na kutunzwa na Mungu, basi yeye bado ni mfungwa wa Shetani; asipohukumiwa na kuadibiwa, basi hatakuwa na njia ya kuepuka ukandamizaji na ushawishi mbaya wa Shetani. Tabia potovu unayoonyesha, na tabia ya uasi unayoishi kwa kudhihirisha inatosha kuonyesha kwamba bado unaishi katika himaya ya Shetani. Kama akili na mawazo yako hayajatakaswa, na tabia yako haijahukumiwa na kuadibiwa, basi nafsi yako yote bado inadhibitiwa na himaya ya Shetani, akili yako bado inadhibitiwa na Shetani, mawazo yako yanatawaliwa na Shetani, na nafsi yako yote inadhibitiwa na mikono ya Shetani. Je, unajua uko umbali gani, sasa, na viwango alivyokuwa navyo Petro? Je, wewe unamiliki kiwango hicho? Ni kiasi gani unajua kuhusu adabu na hukumu ya wakati wa leo? Unacho kiasi gani cha yale Petro alipata kujua? Iwapo, leo, huna uwezo wa kutambua, je utaweza kupata maarifa haya baadaye? Mtu mzembe na mwoga kama wewe hawezi kujua kuhusu adhabu na hukumu. Ukifuata amani ya kimwili, na raha za kimwili, basi hutakuwa na njia yoyote ya kutakaswa, na mwishowe utarudishwa kwa Shetani, kwa sababu hali unayoishi kwa kudhihirisha ni ya Shetani, na ya mwili. Vitu vilivyo sasa, watu wengi hawayafuati maisha, kwa hivyo inamaanisha kuwa hawajali kuhusu kutakaswa, ama kuingia katika uzoefu wa ndani ya maisha. Je, watawezaje kufanywa kuwa wakamilifu? Wale wasiofuata maisha hawana fursa ya kufanywa wakamilifu, na wale wasiofuata maarifa ya Mungu, na hawafuati mabadiliko katika tabia zao, hawataweza kuepuka ushawishi wa giza wa Shetani.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu

495. Wote ambao humwamini Mungu ilhali hawafuatilii ukweli hawana namna ya kuepuka ushawishi wa shetani. Wale wote ambao hawaishi maisha yao kwa uaminifu, wanaotenda kwa njia moja mbele ya wengine na njia nyingine kwa siri, wanaotoa mwonekano wa unyenyekevu, uvumilivu, na upendo ilhali katika kiini ni wenye kudhuru kwa siri, wana hila, na hawana uaminifu kwa Mungu—watu hawa ni mfano halisi wa wale wanaoishi chini ya ushawishi wa giza. Wao ni wa kizazi cha nyoka. Wale ambao imani yao katika Mungu daima ni kwa ajili ya faida zao wenyewe, ambao ni wa kujidai na wenye maringo, ambao hujigamba, na hulinda hadhi zao wenyewe ni wale wanaompenda Shetani na kuupinga ukweli. Wao wanapinga Mungu na ni wa Shetani kikamilifu. Wale ambao hawako makini kwa mizigo ya Mungu, ambao hawamtumikii Mungu kwa moyo wote, ambao daima wanajali maslahi yao wenyewe na maslahi ya familia zao, ambao hawawezi kuacha kila kitu ili wajitumie kwa ajili ya Mungu, na ambao kamwe hawaishi kulingana na maneno Yake wanaishi nje ya maneno ya Mungu. Watu kama hawa hawawezi kupokea sifa ya Mungu.

Wakati Mungu aliumba watu, ilikuwa ili kuwafanya wafurahie utajiri Wake na wampende kwa kweli; katika njia hii, watu wangeishi katika nuru Yake. Leo, wote ambao hawawezi kumpenda Mungu, ambao hawako makini kwa mizigo Yake, ambao hawawezi kutoa mioyo yao kikamilifu kwa Mungu, ambao hawawezi kuchukua moyo wa Mungu kama wao wenyewe, ambao hawawezi kubeba mizigo ya Mungu kama yao wenyewe—nuru ya Mungu haiangazi juu ya watu wowote kama hawa, kwa hivyo, wote wanaishi chini ya ushawishi wa giza. Wako kwenye njia ambayo huenda kinyume kabisa na mapenzi ya Mungu, na yote wanayoyafanya hayana hata chembe ya ukweli. Wanazamia katika matatizo na Shetani na ni wale ambao wanaishi chini ya ushawishi wa giza. Kama unaweza daima kula na kunywa maneno ya Mungu na pia kuwa makini na mapenzi Yake na kutenda maneno Yake, basi wewe ni wa Mungu, na wewe ni mtu anayeishi ndani ya maneno ya Mungu. Je, uko tayari kuepuka kumilikiwa na Shetani na kuishi katika nuru ya Mungu? Kama unaishi ndani ya maneno ya Mungu, basi Roho Mtakatifu atakuwa na nafasi ya kutenda kazi Yake; kama unaishi chini ya ushawishi wa Shetani, basi Roho Mtakatifu hatakuwa na nafasi ya kutenda kazi yoyote. Kazi ambayo Roho Mtakatifu hutenda kwa watu, nuru ambayo Yeye huangaza kwa watu, na imani ambayo Yeye hutoa kwa watu hukaa kwa muda tu; kama hawako makini na hawampi kipaumbele, kazi iliyotendwa na Roho Mtakatifu itawapita. Kama watu wanaishi ndani ya maneno ya Mungu, basi Roho Mtakatifu atakuwa pamoja nao na kutenda kazi juu yao; kama watu hawaishi ndani ya maneno ya Mungu, basi wanaishi ndani ya utumwa wa Shetani. Watu wanaoishi katika tabia ya kiufisadi hawana uwepo wala kazi ya Roho Mtakatifu. Kama unaishi ndani ya nyanja ya maneno ya Mungu, kama unaishi katika hali inayohitajika na Mungu, basi wewe ni Wake na kazi Yake itatendwa juu yako; kama huishi ndani ya nyanja ya matakwa ya Mungu lakini badala yake unamilikiwa na Shetani, basi hakika wewe unaishi chini ya upotovu wa Shetani. Ni kwa kuishi ndani ya maneno ya Mungu tu na kutoa moyo wako Kwake, ndipo unaweza kukidhi matakwa Yake; lazima ufanye asemavyo Mungu, lazima ufanye maneno ya Mungu msingi wa kuwepo kwako na hali halisi ya maisha yako, na ni hapo tu ndipo utakuwa wa Mungu. Kama kwa dhati unatenda kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu, Atatenda kazi juu yako na kisha utaishi chini ya baraka za Mungu, uishi katika nuru ya uso wa Mungu, kufahamu kazi ambayo Roho Mtakatifu hutenda, na pia kuhisi furaha ya uwepo wa Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Epuka Ushawishi wa Giza na Utapatwa na Mungu

496. Kuepuka ushawishi wa giza, lazima kwanza uwe mwaminifu kwa Mungu na kuwa na hamu ya kufuatilia ukweli—ni hapo tu ndipo utakuwa na hali sahihi. Kuishi katika hali sahihi ndilo sharti la mwanzo la kuepuka ushawishi wa giza. Kukosa hali sahihi ina maana kwamba wewe si mwaminifu kwa Mungu na ya kwamba huna hamu ya kutafuta ukweli. Basi, kuepuka ushawishi wa giza hakutawezekana. Mtu kuepuka ushawishi wa giza ni kwa msingi wa maneno Yangu, na kama mtu hawezi kutenda kwa mujibu wa maneno Yangu, hataepuka utumwa wa ushawishi wa giza. Kuishi katika hali sahihi ni kuishi chini ya uongozi wa maneno ya Mungu, kuishi katika hali ya kuwa mwaminifu kwa Mungu, kuishi katika hali ya kutafuta ukweli, kuishi katika uhalisi wa kugharamia rasilmali kwa ajili ya Mungu kwa dhati, kuishi katika hali ya kumpenda Mungu kwa kweli. Wale ambao wanaishi katika hali hizi na ndani ya hali halisi hii watabadilika hatua kwa hatua wanapoingia ndani zaidi katika ukweli, nao watabadilika kwa kuongezeka kwa kazi, mpaka hatimaye hakika watapatwa na Mungu, na watakuja kwa kweli kumpenda Mungu. Wale ambao wameepuka ushawishi wa giza wataweza kufahamu mapenzi ya Mungu hatua kwa hatua, wataelewa mapenzi ya Mungu hatua kwa hatua, na hatimaye kuwa wasiri wa Mungu. Hawatakosa dhana kumhusu Mungu tu, na kukosa uasi dhidi Yake, lakini watakuja kuchukia hata zaidi dhana na uasi ambao walikuwa nao kabla, kusababisha upendo wa kweli kwa Mungu mioyoni mwao. Wale ambao hawawezi kuepuka ushawishi wa giza wanashughulika na miili yao, na wamejaa uasi; mioyo yao imejazwa dhana za kibinadamu na falsafa za kuishi, pamoja na nia zao na majadiliano. Mungu anataka upendo mmoja wa mtu, naye humhitaji mtu amilikiwe na maneno Yake na upendo wa mtu Kwake. Kuishi ndani ya maneno ya Mungu, kugundua kile ambacho mtu anapaswa kutafuta kutoka ndani ya maneno Yake, kumpenda Mungu kama matokeo ya maneno Yake, kukimbiakimbia kwa ajili ya maneno ya Mungu, kuishi kwa ajili ya maneno ya Mungu—haya yote ni mambo ambayo mtu anapaswa kufikia. Kila kitu lazima kijengwe kulingana na maneno ya Mungu, na hapo tu ndipo mtu ataweza kukidhi matakwa ya Mungu. Kama mwanadamu hajatayarishwa na maneno ya Mungu, basi yeye ni funza tu ambaye amemilikiwa na Shetani. Yapime moyoni mwako mwenyewe—ni maneno mangapi ya Mungu ambayo umekita mizizi yake ndani yako? Ni katika mambo gani unaishi kulingana na maneno Yake? Ni katika mambo gani ndiyo hujakuwa ukiishi kulingana nayo? Kama maneno ya Mungu hayajakumiliki kikamilifu, basi ni nini hasa kilicho moyoni mwako? Katika maisha yako ya kila siku, je, unadhibitiwa na Shetani, au unamilikiwa na maneno ya Mungu? Je, maombi yako yameanzishwa kutoka kwa maneno Yake? Je, umeondoka katika hali yako mbaya kupitia nuru ya maneno ya Mungu? Kuchukua maneno ya Mungu kama msingi wa kuwepo kwako, hili ndio jambo kila mtu anapaswa kuingia ndani. Kama maneno ya Mungu hayapo katika maisha yako, basi unaishi chini ya ushawishi wa giza, wewe ni muasi dhidi ya Mungu, unampinga Mungu, na huheshimu jina Lake—imani ya watu kama hao katika Mungu ni uharibifu na usumbufu kabisa. Je, ni kiasi gani cha maisha yako kimeishiwa kwa mujibu wa maneno Yake? Ni kiasi gani cha maisha yako hakijaishiwa kwa mujibu wa maneno Yake? Je, ni kiasi gani cha kile ambacho maneno ya Mungu yamehitaji kwako kimetimizwa ndani yako? Ni mangapi yamepotea ndani yako? Je, umechunguza mambo kama hayo kwa karibu?

Kuepuka ushawishi wa giza, kipengele kimoja ni kwamba kunahitaji kazi ya Roho Mtakatifu, na kipengele kingine ni kwamba kunahitaji ushirikiano wa kujitolea kutoka kwa mtu. Mbona Nasema ya kwamba mtu hayuko kwenye njia sahihi? Kwanza, kama mtu yuko kwenye njia sahihi, ataweza kutoa moyo wake kwa Mungu, ambayo ni jukumu linalohitaji muda mrefu kuingia ndani kwa sababu mwanadamu daima amekuwa akiishi chini ya ushawishi wa giza na amekuwa chini ya utumwa wa Shetani kwa maelfu ya miaka. Kwa hivyo, kuingia huku hakuwezi kupatikana katika siku moja au mbili. Nilileta suala hili leo ili watu waweze kuwa na ufahamu wa hali yao wenyewe; kuhusu ushawishi wa giza ni nini na kuishi ndani ya nuru ni nini, kuingia kunawezekana wakati mtu ana uwezo wa kutambua mambo haya. Hii ni kwa sababu ni lazima ujue ushawishi wa Shetani ni nini kabla uuepuke, na hapo tu ndipo utakuwa na njia ya kuuepuka hatua kwa hatua mwenyewe. Kuhusu ni nini cha kufanya baada ya hapo, hilo ni suala la wanadamu wenyewe. Lazima daima uingie kutoka mtazamo mwema na hupaswi kusubiri kamwe kwa utulivu. Ni kwa njia hii tu ndiyo unaweza kupatwa na Mungu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Epuka Ushawishi wa Giza na Utapatwa na Mungu

497. Kila kitu ambacho Mungu anafanya kinahitajika, na kina umuhimu usio wa kawaida, kwani kila kitu anachofanya ndani ya binadamu kinahusu usimamizi wake na wokovu wa wanadamu. Kiasili kazi ambayo Mungu alimfanyia Ayubu si tofauti, ingawaje Ayubu alikuwa mtimilifu na mnyofu mbele ya macho ya Mungu. Kwa maneno mengine, licha ya kile ambacho Mungu anafanya au mbinu ambazo Anatumia kufanya, licha ya gharama, au lengo Lake, kusudio la hatua Zake halibadiliki. Kusudio Lake ni kuweza kumshughulikia binadamu ili maneno ya Mungu yaingie ndani yake, mahitaji ya Mungu, na mapenzi ya Mungu kwa binadamu; kwa maneno mengine, ni kufanyia kazi huyu binadamu ili vyote ambavyo Mungu Anasadiki kuwa vizuri kulingana na hatua Zake, kumwezesha binadamu kuuelewa moyo wa Mungu na kufahamu kiini cha Mungu, na kumruhusu yeye kutii ukuu na mipangilio ya Mungu, na hivyo basi kumruhusu binadamu kuweza kufikia kiwango cha kumcha Mungu na kujiepusha na maovu—yote ambayo ni kipengele kimoja ya kusudio la Mungu katika kila kitu Anachofanya. Kipengele kingine ni kwamba, kwa sababu Shetani ndiye foili na chombo cha huduma katika kazi ya Mungu, mara nyingi binadamu hukabidhiwa Shetani; hizi ndizo mbinu ambazo Mungu hutumia ili kuwaruhusu watu kuweza kuona maovu, ubaya, kudharaulika kwa Shetani katikati ya majaribio na mashambulizi ya Shetani na hivyo basi kuwasababisha watu kumchukia Shetani na kuweza kutambua kile ambacho ni kibaya. Mchakato huu unawaruhusu kwa utaratibu kuanza kuwa huru dhidi ya udhibiti wa Shetani, na dhidi ya mashtaka, uingiliaji kati, na mashambulizi ya Shetani—mpaka, kwa sababu ya maneno ya Mungu, maarifa yao na utiifu wao kwa Mungu, na imani yao kwa Mungu na kuweza kwao kumcha Mungu, wanashinda dhidi ya mashambulizi ya Shetani na kushinda dhidi ya mashtaka ya Shetani; hapo tu ndipo watakapokuwa wamekombolewa kabisa dhidi ya utawala wa Shetani. Ukombozi wa watu unamaanisha kwamba Shetani ameshindwa, unamaanisha kwamba wao si tena chakula kwenye kinywa cha Shetani—kwamba badala ya kuwameza wao, Shetani amewaachilia. Hii ni kwa sababu watu kama hao ni wanyofu, kwa sababu wanayo imani, utiifu na wanamcha Mungu, na kwa sababu wako huru kabisa dhidi ya Shetani. Wamemletea Shetani aibu, wamemfanya kuonekana mjinga, na wamemshinda kabisa Shetani. Imani yao katika kumfuata Mungu, na utiifu na kumcha Mungu kunamshinda Shetani, na kumfanya Shetani kukata tamaa kabisa na wao. Watu kama hawa ndio ambao Mungu amewapata kwa kweli, na hili ndilo lengo kuu la Mungu katika kumwokoa binadamu. Kama wangependa kuokolewa, na wangependa Mungu awapate kabisa, basi wote wanaomfuata Mungu lazima wakabiliane na majaribio na mashambulizi yakiwa makubwa na hata madogo kutoka kwa Shetani. Wale wanaoibuka katika majaribio na mashambulizi haya na wanaweza kumshinda Shetani ni wale waliookolewa na Mungu. Hivi ni kusema kwamba wale waliookolewa na Mungu ni wale ambao wamepitia majaribio ya Mungu, na ambao wamejaribiwa na kushambuliwa na Shetani mara nyingi. Wale waliookolewa na Mungu wanayaelewa mapenzi na mahitaji ya Mungu, na wanaweza kuukubali ukuu na mipangilio ya Mungu na hawaachi njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu katikati ya majaribio ya Shetani. Wale waliookolewa na Mungu wanamiliki uaminifu, wao ni wakarimu, na wanaweza kutofautisha upendo na chuki, wanayo hisia ya haki na urazini, na wanaweza kumtunza Mungu na kuthamini sana kila kitu ambacho ni cha Mungu. Watu kama hao hawatekwi bakunja, kufanyiwa upelelezi, kushtakiwa au kudhulumiwa na Shetani; wako huru kabisa, wamekombolewa na kuachiliwa kabisa. Ayubu alikuwa mtu kama huyo mwenye uhuru na huu ndio umuhimu hasa wa kwa nini Mungu alikuwa amemkabidhi kwa Shetani.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II

498. Imani, utiifu, na ushuhuda wake Ayubu wa kushinda Shetani, vyote hivi vimekuwa ni chanzo cha msaada mkubwa na himizo kwa watu. Kwa Ayubu, wanaona tumaini la wokovu wao binafsi, na wanaona kwamba kupitia kwa imani na utiifu kwa na kumcha Mungu, inawezekana kabisa kushinda Shetani, na kumshinda Shetani. Wanaona kwamba mradi tu waukubali ukuu na mipangilio ya Mungu, na kumiliki uamuzi na imani ya kutomwacha Mungu baada ya kupoteza kila kitu, basi wanaweza kumletea Shetani aibu na hali ya kushindwa, na kwamba wanahitaji tu kumiliki uamuzi na ustahimilivu wa kusimama imara katika ushuhuda wao—hata kama itamaanisha kupoteza maisha yao—ili Shetani aweze kuaibika na kurejea nyuma haraka. Ushuhuda wa Ayubu ni onyo kwa vizazi vya baadaye, na onyo hili linawaambia kwamba kama hawatamshinda Shetani, basi hawatawahi kuweza kujiondolea mashtaka na uingiliaji kati wa Shetani, na wala hawatawahi kuweza kutoroka dhulma na mashambulizi ya Shetani. Ushuhuda wa Ayubu ulipatia nuru vizazi vya baadaye. Upatiaji Nuru huu unafunza watu kwamba ni pale tu wanapokuwa watimilifu na wanyofu ndipo watakapoweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu; unawafunza kwamba ni pale tu wanapomcha Mungu na kujiepusha na maovu ndipo watakapoweza kuwa na ushuhuda wenye udhabiti na wa kipekee kwa Mungu; pale tu watakapokuwa na ushuhuda dhabiti na wakipekee wa Mungu ndipo hawatawahi kudhibitiwa na Shetani, na kuishi katika mwongozo na ulinzi wa Mungu—na hapo tu ndipo watakapokuwa wameokolewa kwa kweli. Hulka ya Ayubu na ufuatiliaji wake wa maisha unafaa kuigwa na kila mmoja anayefuata wokovu. Kile alichoishi kwa kudhihirisha katika maisha yake yote na mwenendo wake wakati wa majaribio yake ni hazina yenye thamani kwa watu wote wanaotaka kufuata njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II

499. Wakati watu bado hawajaokolewa, maisha yao mara nyingi yanaingiliwa kati na hata kudhibitiwa na, Shetani. Kwa maneno mengine, watu ambao hawajaokolewa ni wafungwa wa Shetani, hawana uhuru, hawajaachiliwa na Shetani, hawajafuzu wala kustahili kumwabudu Mungu, na wanafuatiliwa kwa karibu na kushambuliwa kwa ukali na Shetani. Watu kama hawa hawana furaha ya kuzungumzia, hawana haki ya uwepo wa kawaida wa kuzungumzia, na zaidi hawana heshima ya kuzungumzia. Ni pale tu unaposimama imara na kupigana na Shetani, kwa kutumia imani yako katika Mungu na utiifu kwake, pamoja na kumcha Mungu kama silaha ambazo utatumia kupigana vita vya maisha na mauti dhidi ya Shetani, kiasi cha kwamba utamshinda kabisa Shetani na kumsababisha kukata tamaa na kuwa mwoga kila anapokuona wewe, ili aache kabisa mashambulizi na mashtaka yake dhidi yako—hapo tu ndipo utakapookolewa na kuwa huru. Kama umeamua kutengana kabisa na Shetani lakini huna silaha zitakazokusaidia kupigana na Shetani, basi bado utakuwa katika hatari; kwa kadri muda unaposonga, baada ya wewe kuteswa na Shetani kiasi cha kwamba huna hata usuli wa nguvu uliobakia ndani mwako, lakini bado hujaweza kuwa na ushuhuda, bado hujajifungua kabisa kuwa huru dhidi ya mashtaka na mashambulizi ya Shetani dhidi yako, basi utakuwa na tumaini dogo la wokovu. Mwishowe, wakati hitimisho la kazi ya Mungu itakapotangazwa, bado utakuwa katika mashiko ya Shetani, usiweze kujiachilia kuwa huru, na hivyo hutawahi kuwa na fursa au tumaini. Matokeo yake, hivyo basi, ni kwamba watu kama hao watakuwa mateka kabisa wa Shetani.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II

500. Wakati wa kazi wa utoaji Wake wa kudumu na msaada kwa binadamu, Mungu anaambia binadamu kuhusu mapenzi Yake na mahitaji Yake yote, na anaonyesha vitendo Vyake, tabia, na kile Anacho na alicho kwa binadamu. Lengo ni kuweza kumtayarisha binadamu ili awe na kimo, na kumruhusu binadamu kupata ukweli mbalimbali kutoka kwa Mungu wakati anaendelea kumfuata Yeye—ukweli ambao ni silaha alizopewa binadamu na Mungu ambazo atatumia kupigana na Shetani. Hivyo akiwa na silaha hizo, binadamu lazima akabiliane na mitihani ya Mungu. Mungu anazo mbinu na njia nyingi za kumjaribu binadamu, lakini kila mojawapo inahitaji “ushirikiano” wa adui wa Mungu: Shetani. Hivi ni kusema, baada ya kumpa binadamu silaha ambazo atatumia kupigana na Shetani, Mungu anamkabidhi binadamu kwa Shetani na kuruhusu Shetani “kujaribu” kimo cha binadamu. Kama binadamu anaweza kufanikiwa dhidi ya uundaji wa vita vya Shetani, kama anaweza kutoroka mizunguko ya Shetani na bado akaishi, basi mwanadamu atakuwa ameupita mtihani. Lakini kama binadamu atashindwa kuondoka kwenye uundaji wa vita vya Shetani, na kujinyenyekeza kwa Shetani, basi hatakuwa ameupita mtihani. Haijalishi ni kipengele kipi cha binadamu ambacho mungu anachunguza, kigezo cha uchunguzi Wake ni kama binadamu atasimama imara katika ushuhuda wake atakaposhambuliwa na Shetani au la, kujua kama amemuacha Mungu au la na akajisalimisha na akajinyenyekeza kwa Shetani baada ya kunaswa na Shetani. Inaweza kusemekana kwamba, iwapo binadamu anaweza kuokolewa au la yote haya yanategemea kama anaweza kumzidi na kumshinda Shetani, na kama ataweza kupata uhuru au la yanategemea kama anaweza kuinua, yeye binafsi, silaha alizopewa na Mungu ili kushinda utumwa wa Shetani, na kumfanya Shetani kuwacha kabisa tumaini na kumwacha pekee. Kama Shetani ataliacha tumaini na kumwachilia mtu, hii inamaanisha kwamba Shetani hatawahi tena kujaribu kuchukua mtu huyu kutoka kwa Mungu hatawahi tena kumshtaki na kuingilia kati mtu huyu, hatawahi tena kutaka kumtesa au kumshambulia; mtu kama huyu tu ndiye atakuwa kwa kweli amepatwa na Mungu. Huu ndio mchakato mzima ambao Mungu anapata watu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II

501. Leo, unaweza kutafuta kufanywa kuwa mkamilifu au kutafuta mabadiliko katika ubinadamu wako wa nje na maendeleo katika ubora wa tabia yako, lakini muhimu kabisa ni kwamba unaweza kuelewa kwamba kila kitu ambacho Mungu anafanya leo kina maana na ni cha manufaa: Kinakuwezesha wewe ambaye unazaliwa katika nchi ya uchafu kuepuka uchafu na kuuondoa wote, kinakuwezesha kushinda ushawishi wa Shetani na kuacha nyuma ushawishi wa giza wa Shetani—na kwa kulenga vitu hivi, unakuwa umelindwa katika nchi hii ya uchafu. Mwishowe, utaambiwa utoe ushuhuda gani? Unazaliwa katika nchi ya uchafu lakini unaweza kuwa mtakatifu, usichafuliwe na najisi tena, unamilikiwa na Shetani, lakini unaachana na ushawishi wa Shetani, na humilikiwi au kunyanyaswa na Shetani, na unaishi mikononi mwa Mwenyezi. Huu ndio ushuhuda, na thibitisho la ushindi katika vita na Shetani. Unaweza kumwacha Shetani, hufichui tabia za kishetani tena katika kile unachoishi kwa kudhihirisha, lakini badala yake unaishi kwa kudhihirisha kile ambacho Mungu alitaka mwanadamu afikie Alipomuumba mwanadamu: ubinadamu wa kawaida, urazini wa kawaida, umaizi wa kawaida, azimio la kawaida la kumpenda Mungu, na utii kwa Mungu. Huo ndio ushuhuda ambao kiumbe wa Mungu huwa nao. Unasema, “Tunazaliwa katika nchi ya uchafu, lakini kwa sababu ya ulinzi wa Mungu, kwa sababu ya uongozi Wake, na kwa sababu Ametushinda, tumejiondoa katika ushawishi wa Shetani. Kwamba tunaweza kutii leo pia ni matokeo ya kushindwa na Mungu, na sio kwa sababu sisi ni wema, au kwa sababu tunampenda Mungu kwa asili. Ni kwa sababu Mungu alituchagua, na kutujaalia, ndio tumeshindwa leo, tunaweza kuwa na ushuhuda Kwake, na tunaweza kumhudumia, kwa hiyo, pia, ni kwa sababu Alituchagua, na kutulinda, ndio tumechaguliwa na kutolewa katika miliki ya Shetani, na tunaweza kuachana na uchafu na kutakaswa katika nchi ya joka kuu jekundu.”

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (2)

502. Leo, huamini maneno ninayosema, na huyatilii maanani; wakati utakapofika kwa hii kazi kuenezwa, na unaona ukamilifu wake, utajuta, na wakati huo utakuwa bubu. Kuna baraka, ilhali hujui kuzifurahia, na kuna ukweli, ilhali hujui kuufuata. Je, hujiletei dharau? Leo ingawa hatua inayofuata kwa kazi ya Mungu haijaanza, hakuna kitu cha kipekee juu ya mahitaji yanayohitajika kwako na unachoulizwa kuishi kwa kudhihirisha. Kuna kazi nyingi, na ukweli mwingi; Je, hazina maana kujulikana na wewe? Je, adabu na hukumu ya Mungu haitoshi kuamsha roho yako? Je, adabu na hukumu ya Mungu haitoshi kukufanya ujichukie? Umetosheka kuishi katika ushawishi wa Shetani, kwa amani na furaha, na raha kidogo ya kimwili? Je, wewe si mtu wa chini zaidi kati ya watu wote? Hakuna aliye mpumbavu kuliko wale ambao wameona wokovu lakini hawaufuati ili kuupata; hawa ni watu ambao wanalafua mwili na kufurahia Shetani. Unatumai kwamba imani yako kwa Mungu haitakuwa na changamoto ama dhiki, ama mateso yoyote. Unafuata vile vitu ambavyo havina maana, na huambatanishi faida yoyote kwa maisha, badala yake kuweka mawazo ya fujo kabla ya ukweli. Huna maana! Unaishi kama nguruwe—kuna tofauti gani kati yako, nguruwe na mbwa? Je, hao wasiofuata ukweli na badala yake wanafuata mapenzi ya kimwili, si wote ni wanyama? Hao waliokufa na bila roho si wafu wanaotembea? Maneno mangapi yamenenwa kati yenu? Je, kazi kidogo imefanywa kati yenu? Ni kiasi gani nimetoa kati yenu? Na mbona hujapata chochote? Una nini cha kulalamikia? Je, si ni kweli kuwa hujapata chochote kwa sababu unapenda mwili sana? Na ni kwa sababu mawazo yako ni ya fujo sana? Je, si kwa sababu wewe ni mpumbavu sana? Kama huna uwezo wa kupata baraka hizi, unaweza kumlaumu Mungu kwa kutokukuokoa?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu

503. Mungu anafanya kazi kwa kiwango kikubwa sana na kukiokoa kabisa kikundi hiki cha watu ili uweze kuponyoka kutoka kwa ushawishi wa Shetani, uishi katika nchi takatifu, uishi katika nuru ya Mungu, na uwe na uongozi na mwongozo wa nuru. Kisha kuna maana katika maisha yako. Mnachokula na kuvaa ni tofauti na wasioamini; mnafurahia maneno ya Mungu na kuishi maisha yenye maana—na wao hufurahia nini? Wao hufurahia tu “urithi wa babu” zao na “fahari yao ya kitaifa.” Hawana hata chembe ndogo kabisa ya ubinadamu! Mavazi, maneno, na matendo yenu yote ni tofauti na yao. Hatimaye, mtatoroka kabisa kutoka katika uchafu, msitegwe tena katika majaribu ya Shetani, na mpate riziki ya Mungu ya kila siku. Mnapaswa kila mara kuwa waangalifu. Ingawa mnaishi mahali pachafu hamjawekwa mawaa na uchafu na mnaweza kuishi ubavuni mwa Mungu, mkipokea ulinzi Wake mkuu. Mungu amewachagua kutoka miongoni mwa wote walio katika nchi hii ya manjano. Je, ninyi sio watu waliobarikiwa zaidi? Wewe ni kiumbe aliyeumbwa—unapaswa bila shaka kumwabudu Mungu na kufuatilia maisha yenye maana. Usipomwabudu Mungu lakini unaishi ndani ya mwili wako mchafu, basi wewe si mnyama tu aliye ndani ya vazi la mwanadamu? Kwa kuwa wewe ni binadamu, unapaswa kujitumia kwa ajili ya Mungu na kuvumilia kila mateso! Unapaswa kukubali kwa furaha na kwa hakika mateso kidogo unayopitia leo na kuishi maisha yenye maana, kama Ayubu na Petro. Katika ulimwengu huu, mwanadamu huvaa mavazi ya ibilisi, hula chakula kutoka kwa ibilisi, na hufanya kazi na kutumika chini ya uelekezi wa Shetani, na kukanyagiwa kabisa ndani ya uchafu wake. Usipoelewa maana ya maisha au kupata njia ya kweli, basi kuna umuhimu gani katika kuishi kwa namna hii? Ninyi ni watu mnaofuatilia njia sahihi, wale mnaotafuta maendeleo. Ninyi ni watu ambao huinuka katika nchi ya joka kuu jekundu, wale ambao Mungu huwaita wenye haki. Je, hayo si maisha yenye maana zaidi?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Utendaji (2)

Iliyotangulia: L. Kuhusu Jinsi ya Kumtumikia Mungu na Kumshuhudia

Inayofuata: N. Kuhusu Jinsi ya Kufuatilia Mabadiliko ya Tabia na Kukamilishwa na Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp