420 Athari ya Maombi ya Kweli
Lazima uwe mwaminifu, na lazima uombe ili uondoe ujanja ndani ya moyo wako. Unapotumia maombi ili kujitakasa wakati wowote inapohitajika, na kuyatumia ili uguswe na Roho wa Mungu, tabia yako itabadilika polepole. Maisha ya kweli ya kiroho ni maisha ya sala, na ni maisha ambayo yanaguswa na Roho Mtakatifu. Mchakato wa kuguswa na Roho Mtakatifu ni mchakato wa kubadilisha tabia ya mwanadamu. Maisha ambayo hayajaguswa na Roho Mtakatifu si maisha ya kiroho, bado ni ibada ya kidini; wale tu ambao huguswa na Roho Mtakatifu mara kwa mara, na wamepewa nuru na kuangazwa na Roho Mtakatifu, ndio watu ambao wameingia katika maisha ya kiroho. Tabia ya mwanadamu hubadilika kwa uthabiti wakati anapoomba, na kadri anavyosisimuliwa na Roho wa Mungu, ndivyo anavyozidi kuwa hai na mtiifu. Kwa hiyo, pia, moyo wake utatakaswa polepole, baada ya hapo tabia yake itabadilika polepole. Hayo ndiyo matokeo ya sala ya kweli.
Umetoholewa kutoka katika “Kuhusu Desturi ya Sala” katika Neno Laonekana katika Mwili