Sura ya 80

Kila kitu kinahitaji mawasiliano halisi na Mimi ili kupata nuru na kuangazwa; aidha, ni kwa njia hii tu ndio roho inaweza kuwa na amani. La sivyo, haitakuwa na amani. Sasa ugonjwa mbaya zaidi kati yenu ni kutenganisha ubinadamu Wangu wa kawaida kutoka kwa uungu Wangu kamili; aidha, wengi wenu husisitiza juu ya ubinadamu Wangu wa kawaida, kama kwamba kamwe hawajui kuwa Mimi nina uungu kamili pia. Hii inanikufuru Mimi! Je, mnajua? Ugonjwa wenu ni mbaya sana kiasi kwamba msipoharakisha kuurekebisha mtauawa kwa mikono Yangu. Mbele Zangu mnatenda kwa njia moja (mkionekana kama wenye heshima; wanyenyekevu na wastahimilivu), ilhali bila Mimi kufahamu nyinyi hutenda kwa njia tofauti kabisa (wanafiki kabisa, wapotovu na msio wa kujizuia, mkifanya chochote mnachotaka kufanya, mkiunda mifarakano, mkianzisha falme za kujitegemea, mkitaka kunisaliti), ninyi ni vipofu! Fungua macho yako ambayo yametiwa mchanga na Shetani! Tazama Mimi ni nani hasa! Huna aibu! Hujui kwamba matendo Yangu ni ya ajabu! Hujui kuhusu uweza Wangu! Je, ni nani ambaye ingesemekana kwamba anamfanyia Kristo huduma lakini hajaokolewa? Hujui ni wajibu gani unaotekeleza! Kwa kweli wewe huja mbele Zangu kwa kujifanya ukionyesha uzuri wako, fidhuli sana! Mimi nitakutimua kutoka kwa nyumba Yangu, Situmii mtu wa aina hii kwa sababu sikumwamua kabla au kumchagua.

Ninafanya kile Ninachosema, wale wanaotenda uovu hawapaswi kuogopa. Simkosei mtu yeyote. Daima Mimi hutenda kulingana na mpango Wangu, Nikitenda kulingana na haki Yangu. Kwa sababu wale wanaotenda uovu wamekuwa dhuria ya Shetani tangu uumbaji, Sikuwachagua, hii ndiyo maana ya “chui hawabadili madoa yao.” Katika mambo ambayo wanadamu hawawezi kuelewa, kila kitu kimeelezwa wazi na hakuna kitu kilichofichwa Kwangu. Labda wewe unaweza kuficha kitu kutoka kwa macho ya idadi ndogo ya watu, ukiwafanya watu wachache sana wakwamini, lakini na Mimi si rahisi sana. Mwishowe huwezi kutoroka hukumu Yangu. Mtazamo wa wanadamu ni finyu, na hata wale ambao wanaweza kuelewa sehemu ndogo ya hali ya sasa wanahesabiwa kama wana ujuzi fulani. Kwangu kila kitu kinaendelea vizuri, hakuna kitu kinachonizuia hata kidogo, kwa sababu yote yako chini ya udhibiti na utaratibu Wangu. Ni nani angeweza kuthubutu kutojisalimisha chini ya udhibiti Wangu! Nani angeweza kuthubutu kuvuruga usimamizi Wangu! Nani angeweza kuthubutu kuniasi au na asiye na upendo Kwangu! Ni nani angeweza kuthubutu kuniambia jambo ambalo si kweli, badala yake aniambie uongo mtupu! Hakuna hata mmoja wao atakayetoroka mikono Yangu yenye ghadhabu. Hata kama wewe sasa umejisalimisha, na uko tayari kuadibiwa, na kuingia shimo lisilo na mwisho, Sitakuhurumia kwa urahisi. Lazima Nikutoe kutoka katika shimo lisilo na mwisho ili uwe chini ya adhabu Yangu yenye hasira (kuchukia kwa kiwango cha juu sana), Nikiona mahali unapotorokea. Kitu ambacho Ninachukia zaidi ni kutenganisha ubinadamu Wangu wa kawaida kutoka kwa uungu Wangu kamili.

Heri wale walio waaminifu Kwangu; yaani, heri wao ambao kweli wananitambua kama Mungu Mwenyewe ambaye huchunguza kwa karibu moyo wa mwanadamu. Hakika Nitazidisha baraka zenu, Nikiwawezesha kufurahia baraka nzuri katika ufalme Wangu milele. Hii pia ni njia yenye ufanisi zaidi ya kumwaibisha Shetani. Hata hivyo, usiwe na pupa au wasiwasi sana, kuna muda uliotengwa Nami kwa ajili ya kila jambo. Ikiwa muda Wangu Nilioamua kabla bado haujafika, hata kama ni sekunde kabla, Sitatenda. Mimi hutenda kwa usahihi na kulingana na mpangilio, si kutenda bila mantiki. Kwa wanadamu Mimi sina wasiwasi, Niko thabiti kama Mlima Tai—lakini hujui kwamba Mimi ni Mwenyezi Mungu Mwenyewe? Usiwe na pupa sana, yote yako mikononi Mwangu. Yote yameandaliwa kitambo, yote yanangoja kwa hamu kunitumikia. Ulimwengu dunia wote unaonekana kuwa na vurugu kutoka nje, lakini kulingana na mtazamo Wangu ni wenye utaratibu. Kile Nilichokuandalia wewe ni kwa ajili yako tu kufurahia, unatambua hili? Msijihanikize katika usimamizi Wangu, Nitawaacha watu wote na mataifa yote yaone uweza Wangu kutoka kwa vitendo Vyangu, walibariki na kulisifu jina Langu takatifu kwa ajili ya matendo Yangu ya ajabu. Kwa sababu Nilisema kuwa hakuna chochote Ninachofanya kisicho bila msingi, lakini kila kitu kimejazwa na hekima Yangu na nguvu Zangu, kimejazwa na haki na uadhama Wangu, na hata zaidi ghadhabu Yangu.

Wale ambao mara moja wanazinduka wanaposikia maneno Yangu hakika watapata baraka Zangu na bila shaka watapata ulinzi na utunzaji Wangu. Hawatapitia mateso ya kuadibiwa; badala yake watafurahia furaha ya familia. Je, unajua hili? Mateso ni ya milele, na furaha ni ya milele hata zaidi; yote yanapitiwa kuanzia sasa hivi. Iwapo unateseka au kuona furaha, inategemea ni mtazamo upi ulio nao unapokubali dhambi yako. Kuhusu ikiwa wewe ni mmojawapo wa waliowajaalia na wateule Wangu au la, wewe unapaswa kuwa na uhakika kuhusu hilo kulingana na kile ambacho Nimesema. Unaweza kuwapumbaza watu, lakini huwezi kunipumbaza. Wale ambao Nimewajaaliana kuwateua watabarikiwa sana kuanzia sasa; wale ambao Sijawajaalia na kuwateua Nitawaadibu vikali kuanzia sasa. Hili litakuwa thibitisho Langu kwenu. Wale ambao wamebarikiwa sasa bila shaka ni wapendwa Wangu; wale ambao wanaadibiwa, haina haja ya kusema kuwa hawajaamuliwa kabla na kuchaguliwa na Mimi. Unapaswa kuelewa hili! Yaani, kama unayopata sasa ni Mimi kukushughulikia, ikiwa ni maneno Yangu ya hukumu kali, basi wewe unachukiwa na unasinywa moyoni Mwangu na wewe utakuwa yule Nitakayemtelekeza. Ikiwa unapokea faraja Yangu na unapokea utoaji Wangu wa maisha, Ninakumiliki, wewe ni mmoja wa wapendwa Wangu. Wewe huwezi kuamua jambo hili kulingana na sura Yangu ya nje. Usiwaze zaidi kuhusu jambo hili!

Maneno Yangu yanathibitisha hali halisi ya kila mtu. Je, ninyi mnaamini kwamba Ninaendeleza tu mada zisizo na mpangilio? Kwamba Ninasema chochote Ninachotaka kusema? La hasha! Katika kila neno Langu pamefichwa hekima Yangu. Yachukueni tu maneno Yangu kuwa ukweli. Baada ya muda mfupi sana, wageni ambao wanatafuta njia ya kweli wataingia. Wakati huo ninyi mtapigwa na butwaa na kila kitu kitafanyika bila ugumu wowote. Je, hamjui kuwa Mimi ndiye Mwenyezi Mungu? Kwa kusikia maneno Yangu mnayaamini kabisa, sivyo? Mimi sikosei, sembuse kukosea kusema, mnajua hili? Kwa hiyo, Nimesisitiza mara kwa mara kwamba mnapaswa kukubali mafundisho Yangu kwa haraka, ili muwaongoze na kuwachunga. Je, mnajua hili? Kupitia kwenu Nitawafanya wawe wakamilifu. Hata muhimu zaidi, kupitia kwenu Nitaonyesha ishara na maajabu Yangu tele, yaani, miongoni mwa wale wanaodharauliwa na wanadamu Nimechagua kikundi cha watu kunidhihirisha, kulitukuza jina Langu, kusimamia kila kitu kwa niaba Yangu, kutawala kama wafalme pamoja nami. Kwa hiyo, kwamba Ninawafunza sasa ni usimamizi mkubwa zaidi wa ulimwengu; hili ni jambo la kushangaza ambalo wanadamu hawawezi kutekeleza. Kwa kuwakamilisha Nitamtupa Shetani ndani ya ziwa la moto na kiberiti na ndani ya shimo lisilokuwa na mwisho, Nitalitupa kabisa joka kubwa jekundu hadi life, lisiinuke tena kamwe. Kwa hiyo, wote ambao wanatupwa katika shimo lisilokuwa na mwisho ni dhuria ya joka kubwa jekundu. Ninawachukia kwa kiwango kikubwa sana. Nimeyasababisha haya, kwani hamwezi kuona? Wote wasio waaminifu, wote wanaotumia uhalifu na udanganyifu wamefichuliwa. Wenye kiburi, wenye majivuno, wanaojidai, wajeuri ni dhuria ya malaika mkuu na wao wafanana zaidi na Shetani—wote ni maadui Zangu wa jadi, wapinzani Wangu. Lazima Niwaadhibu mmoja mmoja ili kutuliza chuki ndani ya moyo Wangu. Nitafanya hili moja moja, Nikilitatua moja moja.

Sasa, hata hivyo, ziwa la moto na kiberiti na shimo lisilo na mwisho ni nini? Katika mawazo ya wanadamu ziwa la moto na kiberiti ni jambo yakinifu, lakini wanadamu hawajui kuwa haya ni maelezo yenye makosa sana, lakini bado yana nafasi fulani katika akili za wanadamu. Ziwa la moto na kiberiti ni mkono Wangu ukigawa kuadibu kwa wanadamu. Yeyote anayetupwa katika ziwa la moto na kiberiti ameuawa kwa mkono Wangu. Nafsi, roho, na miili ya watu hawa vinateseka milele. Hii ndiyo maana ya kweli ya kile Nilichosema wakati Niliposema kuwa yote yamo mikononi Mwangu. Na shimo lisilo na mwisho linamaanisha nini? Katika dhana za mwanadamu linafikiriwa kuwa lindi kuu ambalo halina mwisho na lenye kina kirefu sana. Shimo lisilo na mwisho la kweli ni ushawishi wa Shetani. Mtu akianguka mikononi mwa Shetani, mtu huyu yuko katika shimo lisilo na mwisho; hata akipata mabawa hawezi kuruka nje. Kwa hiyo, linaitwa shimo lisilo na mwisho. Watu hawa wote watapitia kuadibu kwa milele, Nimepanga iwe hivi.

Iliyotangulia: Sura ya 79

Inayofuata: Sura ya 81

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp