Sura ya 84

Kwa sababu ya ukosefu wake wa ujuzi kunihusu Mimi, mwanadamu amekatiza usimamizi Wangu na kudhoofisha mipango Yangu mara zisizohesabika, lakini hawajawahi kuweza kuzuia hatua Zangu zinazoendelea mbele. Hii ni kwa sababu Mimi ni Mungu wa hekima. Pamoja na Mimi kuna hekima isiyo na mipaka; pamoja na Mimi kuna siri isiyo na mipaka na isiyoweza kueleweka. Mwanadamu hajawahi kuweza kuielewa na kuifahamu kabisa tangu zamani za kale hadi milele. Je, hilo haliko hivyo? Sio hekima tu iliyo katika kila neno Ninalolisema, kunayo pia siri Yangu iliyofichwa. Pamoja na Mimi, yote ni siri, na kila sehemu Yangu ni siri. Nyinyi mmeona tu siri leo, ambayo ni kwamba mmeona nafsi Yangu, lakini bado hamjapata kufumbua siri hii iliyofichwa. Mwanadamu anaweza tu kuingia katika ufalme Wangu kwa kufuata uongozi Wangu. Vinginevyo, wataangamia pamoja na ulimwengu na kuwa majivu. Mimi ndiye Mungu Mwenyewe aliye kamili, na si mwingine ila Mungu mwenyewe. Misemo ya zamani kama “udhihirisho wa Mungu” tayari imepitwa na wakati; hivyo ni vitu chakavu na vikongwe ambavyo havitumiki kwa sasa. Ni wangapi kati yenu ambao wameliona hili wazi? Je, ni wangapi kati yenu wamekuwa na uhakika na Mimi kwa kiasi hiki? Yote lazima ielezwe wazi na kuagizwa na Mimi.

Ufalme wa Shetani umeharibiwa na watu wake hivi karibuni watakuwa wamemaliza huduma yao kwa ajili Yangu. Wao watafukuzwa nje ya nyumba Yangu mmoja baada ya mwingine, ambayo ni kusema kwamba hali za kweli za wale ambao wamekuwa wakijifanya huku wakijificha katika nafasi mbalimbali hapo mbeleni zote zitaonyeshwa leo, na wote wataondolewa kutoka kwa ufalme Wangu. Nyinyi lazima mkumbuke! Kutoka leo na kuendelea, wale ambao Nawaacha, ikiwa ni pamoja na wale wa zamani, ni wale ambao wanaigiza tu, wale ambao ni bandia. Walikuwa tu wakijifanya kwa ajili Yangu, na lazima waondoke jukwaani onyesho linapoisha. Wale ambao kwa kweli ni wana Wangu watakuwa katika ufalme Wangu kirasmi kupokea upendo Wangu na kufurahia baraka ambazo tayari Nimeziandaa kwa ajili yenu. Heri wazaliwa wa kwanza! Nyinyi mnafaa kwa matumizi Yangu leo ​​kwa kuwa mlipokea mafunzo Yangu hapo awali. Amini ya kwamba Mimi ndiye mwenyezi Mungu. Mambo ambayo watu hawawezi kuyatimiza, Naweza kuyafanya bila kikwazo, na hakuna nafasi yoyote kabisa ya kubishana. Msifikiri kwamba nyinyi hamuwezi kufanya kitu chochote na ya kwamba hamfai kuwa Wangu wazaliwa wa kwanza. Nyinyi mnastahili kikamilifu! Hii ni kwa sababu Mimi ndimi Ninayefanya na huvitimiza vitu vyote. Ni kwa nini mnajihisi sasa kuwa nyinyi ni wa kimo kama hicho? Ni kwa sababu tu wakati Wangu wa kuwatumia kweli haujafika. Vipaji vikuu haviwezi kutumika kwa makusudi yasiyo ya maana; nyinyi mnaelewa? Je, nyinyi mmefungwa tu katika China ndogo kutoka kwa ulimwengu dunia wote? Hiyo ni kusema, ninyi mtapewa watu wote katika ulimwengu dunia wote mpate kuwachunga na kuwaongoza, kwa maana nyinyi ni wazaliwa wa kwanza, na kuwaongoza ndugu ndio wajibu mnaopaswa kuutimiza. Jueni hili! Mimi ni mwenyezi Mungu! Nasisitiza mara nyingine tena kuwa Nawaruhusu kufurahia. Mimi ndiye Ninayefanya kazi—Roho Mtakatifu anafanya kazi kila mahali na binafsi anachukua uongozi.

Watu hawakuelewa wokovu Wangu hapo zamani—je, mnalielewa wazi jambo hili sasa? Wokovu Wangu unajumuisha vipengele kadhaa: Mojawapo ni kuwa hakuna majaaliwa kwa watu wengine hata kidogo, ambayo inamaanisha kuwa hawawezi kufurahia neema Yangu hata kidogo; kipengele kingine ni kwamba kuna wale ambao wamejaaliwa mwanzoni, ambao wanafurahia neema Yangu kwa kipindi cha wakati lakini ambao wataondolewa na Mimi baada ya wakati fulani, wakati ambao Nitaamua kabla, na kisha maisha yao yataisha kabisa; kipengele kingine bado ni kwamba kuna wale ambao Nimewajaalia na kuwachagua, ambao wanafurahia baraka za milele; wanafurahia neema Yangu tangu mwanzo mpaka mwisho, ikiwa ni pamoja na taabu walizoteswa nazo kabla na baada ya Kunikubali pamoja na kupata nuru na kuangaziwa wanakopokea baada ya kunikubali Mimi. Kutoka wakati huo na kuendelea, wataanza kufurahia baraka, yaani, hao ndio Nawaokoa kikamilifu. Haya ndiyo maonyesho ya dhahiri zaidi ya kukamilika kwa kazi Yangu kuu. Ni nini, basi, ambacho baraka inarejelea? Ningependa kuuliza, Ni nini mnachotaka zaidi kukifanya? Ni nini mnachochukia zaidi? Je, ni nini mnachotumaini zaidi kukipata? Nyinyi mmepitia maumivu na taabu katika siku zilizopita yote kwa ajili ya kunipata Mimi na kwa ajili ya kukua kwa maisha yenu; hayo ni sehemu ya neema. Baraka ina maana kuwa mambo ambayo mnayachukia hayatafanyika tena kwenu wakati ujao, ambayo ni kusema, mambo haya hayatakuwako tena katika maisha yenu halisi, na yataondolewa kabisa mbele za macho yenu. Familia, kazi, mke, mume, watoto, marafiki na jamaa na hata ile milo mitatu kwa siku ambayo mnaichukia kila siku, itaondoka. (Hii inamaanisha kutozuiliwa na wakati na kutembea nje ya mwili kabisa. Mwili wako unaweza kudumishwa tu na kuridhika kwako katika roho. Ni mwili wako, sio nyama, ambao unarejelewa. Utakuwa huru kabisa na kupita kiwango cha kibinadamu. Huu ndio muujiza mkubwa zaidi na dhahiri sana ambao Mungu ameudhihirisha tangu uumbaji wa dunia). Chembe zote za mchanga zitaondolewa kutoka katika miili yenu, nanyi mtakuwa miili ya kiroho kabisa ambayo ni mitakatifu na haijatiwa doa, mkiweza kusafiri katika ulimwengu mzima na hadi miisho ya dunia. Kuanzia wakati huo kuendelea, pia mtakuwa mmeondokana na huko kuosha na kusugua, nanyi mtafurahia tu kwa ukamilifu. Kutoka wakati huo na kuendelea, nyinyi hamtashikilia tena dhana ya ndoa (kwa sababu Naifikisha mwisho enzi, sio kuumba ulimwengu), na hakutakuwa tena uchungu wa uzazi ambao ni wa mateso zaidi kwa wanawake. Wala hamtafanya kazi au kujitahidi kazini tena katika siku zijazo. Mtajizamisha kabisa katika kumbatio Langu la upendo na kufurahia baraka ambazo Nimewapa. Hili ni bila shaka. Mnapofurahia baraka hizi, neema itaendelea kuwafuata. Kile ambacho Nimewaandalia nyinyi, yaani, hazina nadra za thamani kutoka duniani kote, zote mtapewa nyinyi. Nyinyi hamuwezi kufahamu kuhusu wala hamuwezi kufikiri yote haya kwa sasa, na hakuna mwanadamu aliyefurahia hili hapo kabla. Wakati baraka hizi zitawajia, nyinyi mtajawa na furaha bila kikomo, lakini msisahau kwamba hizi zote ni nguvu Zangu, matendo Yangu, haki Yangu na hata zaidi, uadhama Wangu. (Nitawapa neema wale ambao Nitaamua kuwapa neema, na Nitawahurumia wale ambao Nitaamua kuwahurumia). Wakati huo, ninyi hamtakuwa na wazazi, wala hakutakuwa na mahusiano ya damu. Nyinyi nyote ni watu ambao Nawapenda, wana Wangu wapendwa. Hakuna mtu atakayethubutu kuwakandamiza nyinyi kutoka wakati huo na kuendelea. Utakuwa wakati wenu wa kukua na kuwa watu wazima, na wakati wenu wa kutawala mataifa kwa fimbo ya chuma! Ni nani anayethubutu kuwazuia Wana wangu wapendwa? Ni nani anayethubutu kuwashambulia wana Wangu wapendwa? Wote watawaheshimu wana Wangu wapendwa kwa sababu Baba ametukuzwa. Vitu vyote ambavyo hakuna mtu angeweza kufikiria daima vitaonekana mbele ya macho yenu. Vitakuwa havina kikomo, wasivyoisha, visivyo na mwisho. Kabla ya muda mrefu, nyinyi hakika hamtahitaji tena kuunguzwa na jua na kuvumilia joto linalotesa. Wala hamtalazimika kuteseka na baridi, wala mvua, theluji au upepo havitawafikia. Hii ni kwa sababu Nawapenda, na yote itakuwa ni dunia ya upendo Wangu. Nitawapa kila kitu mnachotaka, nami Nitawaandaa kwa ajili ya kila kitu ambacho mnahitaji. Nani anathubutu kusema kuwa Mimi si mwenye haki? Nitakuua mara moja, kwa sababu Nimewaambia kabla ya kuwa ghadhabu Yangu (dhidi ya waovu) itaendelea milele, nami Sitaachilia hata kidogo. Hata hivyo, upendo Wangu (kwa wana Wangu wapendwa) pia utaendelea milele; Sitauzuia hata kidogo.

Leo, wale wanaosikia maneno Yangu kama hukumu ni wale ambao hawako katika hali nzuri, lakini wakati wanapogundua hilo, Roho Mtakatifu huwa tayari amewaacha. Wazaliwa wa kwanza wanachaguliwa kutoka kati yenu kutoka ulimwengu dunia wote, lakini wana na watu hufanya tu sehemu ndogo miongoni mwenu. Mkazo Wangu uko katika ulimwengu dunia wote, ambao una maana kuwa wana na watu huchaguliwa kutoka mataifa yote ya dunia. Je, mnaelewa? Ni kwa nini Naendelea kusisitiza wazaliwa wa kwanza wanapaswa kukua haraka na kuwaongoza hao wageni? Je, mnaelewa maana halisi iliyo katika maneno Yangu? Hii ni kwa sababu China ni taifa ambalo Nimelilaani, limenitesa Mimi zaidi, na Nalichukia zaidi. Lazima mjue kwamba Mimi na wazaliwa Wangu wa kwanza tulikuja kutoka mbinguni na sisi ni watu wa ulimwengu. Sisi sio wa taifa lolote. Msishikilie mawazo ya kibinadamu! Hii ni kwa sababu Nimeonyesha nafsi Yangu kwenu. Kila kitu kiko juu Yangu. Je, mnaweza kukumbuka maneno Yangu? Kwa nini Nasema kuwa kuna watu wachache zaidi na zaidi miongoni mwenu na idadi ya watu imekuwa iliyosafishwa zaidi na zaidi? Hii ni kwa sababu wokovu Wangu unageuka hatua kwa hatua kuelekea katika ulimwengu dunia. Wale wanaoondolewa, ambao wamekubali jina Langu, wote ni wale ambao walihudumu kuwakamilisha wazaliwa wa kwanza. Je, mnaelewa? Kwa nini Nasema wote ni wale ambao huwahudumia wana Wangu? Sasa mmeelewa kweli, sivyo? Kwa kweli idadi ni ndogo, hakika kunao wachache, lakini watu hao wamefaidika kwa kiasi kikubwa kwa sababu ya wana Wangu na wamefurahia sana neema Yangu nyingi, na hiyo ndiyo sababu Nilisema kuwa Naiokoa jamii ya wanadamu kwa mara ya mwisho. Sasa mnajua maana halisi katika maneno Yangu! Nitamwadibu sana mtu yeyote anayenipinga Mimi, nami Nitageuza uso Wangu kuelekea mtu yeyote anayenilinda Mimi, kwa sababu Nimekuwa daima, tangu mwanzo hadi mwisho, Mungu aliye adhimu na mwenye haki, na kila kitu kitafichuliwa kwenu. Nafanya kazi kwa haraka na kwa njia za ajabu, na hivi karibuni, mambo ya ajabu ambayo hayawezi kufikirika kwa wanadamu yatatokea. Nina maana kuwa mara moja na hivi karibuni, je, mnaelewa? Tafuteni kuingia katika maisha bila kuchelewa! Wana Wangu wapendwa, vitu vyote vipo hapa kwa ajili yenu, na vitu vyote vipo kwa ajili yenu.

Iliyotangulia: Sura ya 83

Inayofuata: Sura ya 85

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp