Sura ya 83

Hujui kwamba Mimi ni Mwenyezi Mungu; hujui kwamba mambo yote na vitu vyote viko chini ya udhibiti Wangu! Maana ya kila kitu huumbwa na kukamilishwa na Mimi ni nini? Baraka au misiba ya kila mtu hutegemea utimilifu Wangu, matendo Yangu. Mwanadamu anaweza kufanya nini? Mwanadamu anaweza kufanikisha nini kwa kufikiri? Katika enzi hii ya mwisho, katika enzi hii potovu, katika dunia hii ya giza ambayo Shetani amepotosha kwa kiwango fulani, ni wachache wagani wanaoweza kupatana na mapenzi Yangu? Ikiwa ni leo, jana, au katika siku zijazo zisizo mbali, maisha ya kila mtu huamuliwa na Mimi. Ikiwa wanapokea baraka au kupitia misiba, na kama wanapendwa au kuchukiwa na Mimi yote yaliamuliwa kabisa na Mimi kwa mkupuo mmoja. Nani kati yenu athubutuye kudai kuwa hatua zako ni za kujiamulia na kwamba majaliwa yako yako katika udhibiti wako? Ni nani athubutuye kusema hivyo? Ni nani athubutuye kuwa mwasi sana? Ni nani asiyeniogopa Mimi? Ni nani aliye mwasi Kwangu ndani yake? Ni nani anayethubutu kutenda kama anavyopenda? Nitamwadibu wakati uo huo, bila shaka sitakuwa tena na huruma kwa wanadamu au kuwaokoa. Wakati huu —yaani, wakati ambapo mmekubali jina Langu—ndiyo mara ya mwisho ambapo Nitaonyesha upole wowote kwa binadamu. Yaani, Nimechagua sehemu ya wanadamu, ambao, hata kama baraka zao sio za milele, wamefurahia neema Yangu kiasi fulani; Kwa hivyo, hata kama haijaamuliwa kabla kuwa utabarikiwa milele, Sikutendei vibaya, na wewe ni bora zaidi kuliko wale ambao watapata msiba moja kwa moja.

Kwa kweli, hukumu Yangu tayari imefika kiwango cha juu, ikiingia katika eneo lisilo na kifani. Hukumu Yangu ii juu ya kila mtu, sasa ni hukumu ya ghadhabu. Hapo zamani ilikuwa hukumu adhimu, tofauti sana na sasa. Watu wa zamani hawakuanza kuhisi hofu kidogo hadi walipokutana na hukumu inayotolewa, sasa wakisikia neno moja tu wanaogopa sana; mtu hata anaogopa Mimi kufungua kinywa Changu. Lakini sauti Yangu ikitoka, Ninapoanza kuzungumza, anaogopa sana hivi kwamba hajui afanye nini, akitamani sana wakati huo kujificha katika shimo ardhini, lililofichwa katika kona lenye giza kuu zaidi. Mtu wa aina hii hawezi kuokolewa kwa sababu ana roho wabaya. Ninapohukumu joka kuu jekundu, Ibilisi, atakuwa mwenye hofu, hata ataogopa kuonwa na watu; kweli yeye ni uzao wa Shetani aliyezaliwa katika giza.

Hapo zamani mara nyingi Nilitumia maneno “majaaliwa na uteuzi,” hii ina maana gani hasa? Je, Mimi hujaalia na kuchagua vipi? Kwa nini mtu asiwe mmoja wa waliojaaliwa na kuchaguliwa? Unawezaje kuelewa hili? Haya yote yanahitaji ufafanuzi wa wazi kutoka Kwangu na yote yanahitaji Mimi kunena moja kwa moja. Kama Ningefichua mambo haya ndani yenu, basi wapumbavu wangeamini kwamba ni wazo lililotolewa na Shetani! Ningekashifiwa bila haki! Sasa Nitazungumza kwa uwazi, bila kuzuia kitu chochote: Nilipoumba vitu vyote, kwanza Niliumba vifaa hivyo vya kutumiwa na wanadamu (maua, nyasi, miti, mbao, milima, mito, maziwa, nchi na bahari, kila aina ya wadudu, ndege, wanyama, wengine ni kwa ajili ya watu kula, na baadhi ni kwa ajili ya binadamu kuangalia). Aina mbalimbali za nafaka ziliumbwa kwa ajili ya wanadamu kulingana na tofauti kati ya mahali; ni baada tu ya kuumba haya yote ndipo Nilianza kuwaumba wanadamu. Kuna aina mbili za watu: Wa kwanza ni wateule Wangu na waliojaaliwa; wa pili wana tabia ya Shetani, na aina hii waliumbwa kabla ya Mimi kuiumba dunia, lakini kwa kuwa walipotoshwa kabisa na Shetani kwa hivyo Nimewatelekeza. Kisha Nikaumba aina iliyochaguliwa na kuamuliwa kabla na Mimi, kila mmoja akiwa na tabia Zangu kwa kiasi tofauti; kwa hivyo, wale waliochaguliwa na Mimi leo kila mmoja ana tabia Zangu kwa kiasi tofauti. Ingawa wamepotoshwa na Shetani, bado ni Wangu; kila hatua ni sehemu ya mpango Wangu wa usimamizi. Kwamba utawala wa uaminifu katika ufalme wote ulipangwa kabla ya wakati na Mimi; wale ambao ni wadanganyifu na wenye hila hawawezi kuwa waaminifu bila kujali lolote kwa sababu wao wamezaliwa kutoka kwa Shetani, wanamilikiwa na Shetani, daima ni watumishi wa Shetani walio chini ya amri yake, lakini yote ni kwa ajili ya kutimiza mapenzi Yangu. Nimefanya hilo liwe wazi ili kuondoa kukisia kwenu. Wale Ninaowakamilisha, Nitawatunza na kuwalinda; kwa wale Ninaowachukia, baada ya huduma yao kuisha wataondoka mahali Pangu. Watu hawa wanapotajwa Mimi hukasirika, watajwapo Ninataka sana kuwashughulikia wakati huo huo, lakini Ninajizuia katika vitendo Vyangu; Mimi ni mwenye kufikiria katika vitendo Vyangu na kauli Zangu. Naweza kuunyanyasa ulimwengu kwa hasira, lakini isipokuwa wale Niliowajaalia; baada ya kutulia Ninaweza kushikilia ulimwengu katika kiganja cha mkono Wangu, hiyo ni kusema Mimi hudhibiti kila kitu. Ninapoona kwamba ulimwengu umepotoshwa kwa kiasi ambacho watu hawawezi kuuvumilia, Nitauharibu mara moja. Je, si hilo litahitaji tu neno Langu moja?

Mimi ni Mungu wa vitendo Mwenyewe; Sifanyi ishara za ajabu na maajabu, lakini kila pahali hujaa kazi Zangu za ajabu. Njia iliyoko mbele itakuwa angavu mno. Ufunuo Wangu wa kila hatua ndio njia Ninayowaonyesha, mpango Wangu wa usimamizi. Hiyo ni kusema, baadaye ufunuo utakuwa mwingi zaidi na wazi zaidi. Hata katika Ufalme wa Milenia—katika siku za usoni za karibuni—ni lazima mwendelee kulingana na ufunuo Wangu na kwa kufuata hatua Zangu. Yote yamechukua umbo, yote yameandaliwa, waliobarikiwa wana baraka za milele zinazowasubiri; wale waliopigwa wana kuadibu kwa milele kunakowasubiri. Siri Zangu ni nyingi sana kwenu, yale ambayo Kwangu ni maneno rahisi zaidi yaweza yakawa magumu sana kwenu; kwa hiyo, Nasema zaidi na zaidi, kwa sababu ninyi huelewa kidogo sana, na mnahitaji Nieleze neno kwa neno, lakini msiwe na wasiwasi mwingi, Nitawanenea kulingana na kazi Yangu.

Iliyotangulia: Sura ya 82

Inayofuata: Sura ya 84

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp