Njia ya Huduma ya Kidini Lazima Ipigwe Marufuku

Tangu mwanzo wa kazi Yake katika ulimwengu mzima, Mungu amewaamulia kabla watu wengi kumhudumia, wakiwemo watu kutoka kila tabaka la maisha. Kusudio Lake ni kutimiza mapenzi Yake mwenyewe na kuhakikisha kwamba kazi Yake hapa ulimwenguni inatimia kwa urahisi. Hili ndilo kusudio la Mungu katika kuwachagua watu wa kumhudumia. Kila mtu anayemhudumia Mungu lazima aelewe mapenzi haya ya Mungu. Kupitia kazi hii Yake, watu wanaweza kuona vizuri zaidi hekima ya Mungu na kudura ya Mungu, na kuona kanuni za kazi Yake hapa ulimwenguni. Mungu kwa kweli anakuja ulimwenguni kufanya kazi Yake, kuwasiliana na watu, ili nao waweze kuona vizuri zaidi matendo Yake. Leo, kundi hili la watu lina bahati kubwa kwa kundi hili lenu kumhudumia Mungu wa utendaji. Hii ni baraka isiyopimika kwenu. Kwa kweli ni Mungu anayewainua. Katika kumteua mtu ili amhudumie, Mungu siku zote huwa na kanuni Zake binafsi. Kumhudumia Mungu hakika, kama vile watu wanavyofikiria, si suala tu la kuwa na shauku. Leo mnaona kwamba mtu yeyote anayeweza kumhudumia Mungu akiwa mbele Yake anafanya hivyo kwa sababu wana mwongozo wa Mungu na kazi ya Roho Mtakatifu, na kwa sababu wao ni watu wanaofuata ukweli. Haya ndiyo mahitaji ya kiwango cha chini zaidi ambayo wote wanaomhudumia Mungu wanapaswa kuwa nayo.

Kumtumikia Mungu si kazi rahisi. Wale ambao tabia yao potovu haibadiliki hawawezi kamwe kumhudumia Mungu. Kama tabia yako haijahukumiwa na kuadibiwa na neno la Mungu, basi tabia yako bado inamwakilisha Shetani. Hii inatosha kuthibitisha kwamba huduma yako kwa Mungu ni kutokana na nia yako nzuri wewe binafsi. Ni huduma inayotokana na asili yako ya kishetani. Unamhudumia Mungu na hulka yako ya kiasili, na kulingana na mapendeleo yako ya kibinafsi; na zaidi, unaendelea kufikiria kwamba Mungu anapenda chochote kile unachopenda kufanya, na kwamba Mungu anachukia chochote kile ambacho hupendi kufanya, na unaongozwa kabisa na mapendeleo yako binafsi katika kazi yako. Je, huku kunaweza kuitwa kumhudumia Mungu? Hatimaye tabia yako ya maisha haitabadilishwa hata chembe; badala yake, utakuwa msumbufu hata zaidi kwa sababu umekuwa ukimhudumia Mungu, na hii itafanya tabia yako potovu kukita mizizi zaidi. Kwa njia hii, utaendeleza kwa ndani sheria kuhusu huduma kwa Mungu zitokanazo kimsingi na hulka yako binafsi, na uzoefu unaotokana na kuhudumu kwako kulingana na tabia yako binafsi. Hili ni funzo kutokana na uzoefu wa kibinadamu. Ni falsafa ya binadamu ya kuishi katika dunia. Watu kama hawa ni wa Mafarisayo na wale wajumbe wa kidini. Kama hawatawahi kuzinduka na kutubu, basi hakika watageuka na kuwa wale Makristo wa uwongo na wapinga Kristo watakaowadanganya watu katika siku za mwisho. Makristo wa uwongo na wapinga Kristo waliozungumziwa watainuka kutoka miongoni mwa watu kama hawa. Kama wale wanaomhudumia Mungu watafuata hulka yao na kutenda kulingana na mapenzi yao binafsi, basi wamo katika hatari ya kutupwa nje wakati wowote. Wale wanaotumia miaka yao mingi ya uzoefu kwa kumhudumia Mungu ili kutega mioyo ya watu, kuwasomea na kuwadhibiti, kujiinua wao wenyewe—na wale katu hawatubu, katu hawakiri dhambi zao, katu hawakatai manufaa ya cheo—watu hawa wataanguka mbele ya Mungu. Hawa ni watu walio kama Paulo, waliojaa majivuno ya vyeo vyao na wanaoonyesha ukubwa wao. Mungu hatawakamilisha watu kama hawa. Aina hii ya huduma huzuia kazi ya Mungu. Watu wanapenda kushikilia vitu vya kale. Wanashikilia fikira za kale, wanashikilia vitu vya kale. Hiki ni kizuizi kikuu katika huduma yao. Kama huwezi kuvitupa vitu hivi, vitu hivyo vitayakaba maisha yako yote. Mungu hatakupongeza, hata kidogo, hata kama utaivunja miguu yako au mgongo wako ukitia bidii, au hata ukifa katika “huduma” ya Mungu. Kinyume cha mambo ni kwamba: Atasema kwamba wewe ni mtenda maovu.

Kufikia leo, Mungu atawakamilisha kirasmi wale wasiokuwa na fikira za kidini, ambao wako tayari kuweka pembeni nafsi zao za kale, na ambao wanamtii tu Mungu kwa moyo wa kawaida, na kuwafanya kuwa watimilifu wale wanaotamani neno la Mungu. Watu hawa wanafaa kusimama na kumhudumia Mungu. Kwake Mungu kunayo hekima nyingi na isiyoisha. Kazi Yake ya kustaajabisha na matamshi Yake yenye thamani vinasubiri hata idadi kubwa ya watu waweze kuvifurahia. Kama ilivyo sasa, wale walio na fikira za kidini, wanaochukua hali ya ukubwa, na wale ambao hawawezi kujiweka pembeni wanaona vigumu sana kukubali vitu hivi vipya. Hakuna fursa ya Roho Mtakatifu kuwakamilisha watu hawa. Kama mtu hajaamua kutii, na hana kiu ya neno la Mungu, basi mtu huyo hataweza kupokea mambo mapya. Wataendelea tu kuwa waasi zaidi na zaidi, kuwa wajanja zaidi na zaidi, na hatimaye kujipata kwenye njia mbaya. Katika kufanya kazi Yake sasa, Mungu atawainua watu zaidi wanaompenda kwa kweli na wanaoweza kukubali mwangaza mpya. Na Atakatiza kabisa maafisa wa kidini wanaoonyesha ukubwa wao. Wale wanaokataa mabadiliko kwa ukaidi: Hataki hata mmoja wao. Je, unataka kuwa mmoja wa watu hao? Je, unatekeleza huduma yako kulingana na mapendeleo yako, au unafanya kile Mungu anachotaka? Hili ni jambo ambalo lazima ujijulie mwenyewe. Je, wewe ni mmojawapo wa maafisa wa kidini, au wewe ni mtoto mchanga anayefanywa kuwa mtimilifu na Mungu? Je, ni kiwango kipi cha huduma yako ambacho kinapongezwa na Roho Mtakatifu? Ni kiwango kipi ambacho Mungu hatasumbuka kukumbuka? Baada ya miaka mingi ya huduma, maisha yako yamebadilika kiasi kipi? Je, uko wazi kuhusu mambo haya yote? Kama unayo imani ya kweli, basi utaweka pembeni fikira zako za kale za kidini na utamhudumia Mungu kwa njia bora zaidi na kwa njia mpya. Hujachelewa sana kusimama sasa. Fikira za kale za kidini zitayakaba maisha ya mtu. Uzoefu ambao mtu anapata utamwongoza mbali na Mungu, kufanya mambo kwa njia yake mwenyewe. Usipoviweka vitu hivi chini, vitakuwa kikwazo katika kukua kwa maisha yako. Mungu siku zote amewakamilisha wote wanaomhudumia. Hawatupilii mbali kwa urahisi tu. Kama tu utakubali kwa kweli hukumu na kuadibu kwa neno la Mungu, kama unaweza kuweka pembeni matendo yako na sheria za kidini za kale, na kukoma kutumia fikira za kale za kidini kama kipimo cha neno la Mungu hii leo, ni hapo tu ndipo kutakuwa na mustakabali kwako. Lakini kama utashikilia vitu vya kale, kama bado unavithamini, basi huwezi kupata wokovu. Mungu hawatambui watu kama hao. Kama kweli unataka kukamilishwa, basi lazima uamue kutupilia mbali kabisa kila kitu cha kale. Hata kama kile kilichokuwa kimefanywa awali kilikuwa sahihi, hata kama ilikuwa ni kazi ya Mungu, ni lazima bado uweze kuiweka pembeni na uache kuishikilia. Hata kama ilikuwa kazi ya Roho Mtakatifu iliyo wazi, iliyofanywa moja kwa moja na Roho Mtakatifu, leo lazima uiweke pembeni. Hufai kuishikilia. Hili ndilo Mungu anahitaji. Kila kitu lazima kifanywe upya. Katika kazi ya Mungu na neno la Mungu, Harejelei vitu vya kale ambavyo vilishapita, na vilevile Hafukui historia ya kale. Mungu siku zote ni mpya na kamwe si mzee. Hashikilii hata maneno Yake mwenyewe ya kitambo inayoonyesha kwamba Mungu hafuati mafundisho ya dini yoyote. Katika hali hii, kama mwanadamu, kama siku zote unashikilia kabisa vitu vya kale, ukikataa kuviachilia na kuvitumia kwa njia ya fomyula, huku naye Mungu hafanyi kazi tena katika njia Alizokuwa akifanya awali, basi maneno yako na matendo yako siyo ya kukatiza? Je, hujawa adui wa Mungu? Je, uko radhi kuyaacha maisha yako yote yaharibike kwa sababu ya mambo haya ya kale? Mambo haya ya kale yatakufanya kuwa mtu anayezuia kazi ya Mungu. Je, mtu kama huyo ndiye wewe unataka kuwa? Kama kweli hutaki kuwa hivyo, basi acha mara moja kile unachofanya na ubadilike; anza tena upya. Mungu hakumbuki huduma yako ya kale.

Iliyotangulia: Mwanadamu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu

Inayofuata: Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp