Swali 8: Unashuhudia kwamba Mungu kujipatia mwili Mwenyewe katika siku za mwisho kumeanza Enzi ya Ufalme, kuimaliza enzi nzee ya utawala wa Shetani. Tunachotaka kuuliza ni, kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho imemaliza vipi enzi ya giza ya imani ya wanadamu katika Mungu asiye yakini, na ya utawala wa Shetani? Tafadhali shiriki ushirika wenye maelezo.
Jibu:
Katika kazi ya Mwenyezi Mungu ya hukumu katika siku za mwisho, Ameonyesha ukweli wote wa kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu. Pia Amewafungulia watu mafumbo yote ya mpango wa usimamizi wa Mungu, mapenzi Yake, mipango Yake kwa hatima ya mwisho ya wanadamu, na kadhalika. Hili limefunga kabisa pengo kati ya Mungu na mwanadamu, likiruhusu wanadamu kuwa kana kwamba walikuwa uso kwa uso na Mungu. Kazi kama hiyo ya Mwenyezi Mungu kwa hakika imehitimisha enzi ya watu kumwamini Mungu asiye yakini, na pia imehitimisha enzi ya giza na uovu ya Shetani kuwatawala na kuwapotosha wanadamu. Kazi ya Mwenyezi Mungu kwa hakika ni kazi ya kuhitimisha enzi na kuanza enzi mpya. Hebu tusome vifungu vichache kutoka kwa maneno Yake.
“Ni leo tu, Nikujapo binafsi miongoni mwa wanadamu na kuongea maneno Yangu, ndipo mwanadamu anapata maarifa kidogo kunihusu, kutoa nafasi ‘Yangu’ ndani ya mawazo yao, badala yake kutengeneza mahali pa Mungu wa vitendo ndani ya fahamu zake. Mwanadamu ana dhana na amejawa na udadisi; ni nani ambaye hangetaka kumwona Mungu? Ni nani ambaye hangetamani kukutana na Mungu? Lakini bado kitu pekee kilicho na nafasi ya uhakika ndani ya moyo wa mwanadamu ni Mungu ambaye mwanadamu anahisi kuwa dhahania na asiye dhahiri. Nani angetambua haya kama Singewaeleza wazi? Nani angeamini kwa kweli Mimi nipo? Kwa hakika bila shaka yoyote? Kuna tofauti kubwa kati ya ‘Mimi’ aliye ndani ya mwanadamu na ‘Mimi’ wa ukweli, na hakuna anayeweza kuwalinganisha. Nisingekuwa mwili, mwanadamu hangewahi Nijua, na hata angekuja kunijua, je, maarifa kama hayo bado hayangekuwa dhana?” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 11).
“Kwa sababu mwanadamu amejaribiwa na kupotoshwa na Shetani, kwa sababu amechukuliwa na fikira na kuwaza, Nimekuwa mwili ili kuwashinda binafsi wanadamu wote, kufichua dhana zote za mwanadamu, na kupasua mawazo ya mwanadamu. Matokeo yake ni kuwa mwanadamu hajionyeshi mbele Yangu tena, na hanitumikii tena akitumia dhana zake mwenyewe, na hivyo, ‘Mimi’ katika dhana za mwanadamu huondolewa kabisa” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 11).
“Katika ujenzi wa ufalme, Natenda moja kwa moja katika hali ya uungu Wangu, na kuruhusu watu wote kujua kile Nilicho nacho na Nilicho kwa msingi wa maarifa ya maneno Yangu, hatimaye kuwaruhusu kutimiza ufahamu kunihusu Mimi kama mwili halisi. Hivyo hukamilisha ufuatiliaji wote wa binadamu wa Mungu asiye dhahiri, na hivyo basi huacha kushikilia nafasi ndani ya nyoyo zao ya Mungu aliye mbinguni; yaani, Ninamruhusu mwanadamu ajue matendo Ninayotenda Nikiwa mwenye mwili, na hivyo nitahitimisha wakati Wangu duniani” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 8).
“Kwa wale wote ambao wanaishi katika mwili, kubadilisha tabia zao kunahitaji kuwe na malengo ya kufuata, na kumjua Mungu kunahitaji kushuhudia matendo halisi na sura halisi ya Mungu. Yote haya yanaweza kufikiwa tu na Mungu mwenye mwili, na yote yanaweza kukamilishwa na mwili wa kawaida na halisi. Hii ndiyo maana kufanyika mwili ni muhimu, na kwa nini kunahitajika na wanadamu wote wapotovu. Kwa kuwa watu wanahitajika kumjua Mungu, taswira za Mungu wa kufikirika na wa kimiujiza zinapaswa ziondolewe kutoka katika mioyo yao, na kwa kuwa wanatakiwa kutupilia mbali tabia zao potovu, lazima kwanza wajue tabia yao potovu. Ikiwa mwanadamu anafanya tu kazi ya kuondoa taswira za Miungu isiyo dhahiri kutoka katika mioyo ya watu, basi atashindwa kupata matokeo sahihi. Taswira za Miungu isiyo dhahiri katika mioyo ya watu haziwezi kufichuliwa, kuachwa, au kuondolewa kikamilifu kwa maneno pekee. Kwa kufanya hivyo, mwisho wake haitawezekana kuondoa vitu hivi vilivyokita mizizi kwa watu. Ni kwa kubadilisha vitu hivi visivyo dhahiri na vya kimiujiza na Mungu anayeonekana tu na mwenye taswira halisi ya Mungu, na kuwafanya watu wayajue hatua kwa hatua ndipo matokeo mazuri yanaweza kupatikana. Mwanadamu anatambua kwamba Mungu aliyekuwa anamtafuta huko nyuma ni asiye dhahiri na wa kimiujiza. Kile ambacho kinaweza kufanikisha matokeo haya sio uongozi wa moja kwa moja wa Roho, sembuse mafundisho ya mtu fulani, bali ni Mungu mwenye mwili. Dhana za mwanadamu huwekwa wazi Mungu mwenye mwili anapofanya kazi Yake rasmi, kwa sababu hali ya kawaida na uhalisi wa Mungu mwenye mwili ni kinyume cha Mungu asiye yakini na asiye wa kawaida katika fikira za mwanadamu. Dhana asili za mwanadamu zinaweza tu kufunuliwa kupitia tofauti zao na Mungu mwenye mwili. Bila ulinganisho na Mungu mwenye mwili, dhana za mwanadamu zisingefichuliwa; kwa maneno mengine, bila tofauti ya uhalisi vitu visivyo dhahiri visingefichuliwa. Hakuna anayeweza kutumia maneno ili kufanya kazi hii, na hakuna anayeweza kuizungumzia kazi hii kwa kutumia maneno. Ni Mungu Mwenyewe pekee ndiye Anayeweza kufanya kazi Yake, na hakuna mtu mwingine anayeweza kufanya kazi hii kwa niaba Yake. Haijalishi lugha ya mwanadamu ni tajiri kiasi gani, haiwezi kuzungumzia uhalisi na ukawaida wa Mungu. Mwanadamu anaweza tu kumjua Mungu kivitendo zaidi, na anaweza tu kumwona kwa uwazi zaidi, ikiwa Mungu binafsi anafanya kazi miongoni mwa wanadamu na kuonyesha kabisa sura Yake na uungu Wake. Athari hii haiwezi kutimizwa na mwanadamu yeyote yule mwenye mwili. Bila shaka, Roho wa Mungu pia hawezi kupata matokeo haya” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili).
“Wakati watu wote wana ujuzi mkubwa kunihusu baada ya kukubali matamshi Yangu ndio wakati ambapo watu Wangu wananiishi kwa kudhihirisha, ni wakati ambapo kazi Yangu katika mwili imekamilika, na wakati ambapo uungu Wangu unaishi kwa kudhihirishwa kikamilifu katika mwili. Wakati huu, watu wote watanitambua Mimi katika mwili, na kweli wataweza kusema kwamba Mungu huonekana katika mwili, na hili litakuwa ndilo tunda. … Hatimaye, watu wa Mungu wataweza kumpatia Mungu sifa ambayo ni ya kweli, si ya kulazimishwa, na ambayo inatoka mioyoni mwao. Hiki ndicho kipo katika kiini cha mpango wa Mungu wa usimamizi wa miaka 6,000. Yaani, ni udhihirisho wa mpango huu wa usimamizi wa miaka 6,000: kuwafanya watu wote kujua umuhimu wa kupata mwili kwa Mungu—kuwafanya kumjua Mungu kupata mwili kwa vitendo, ambayo ni kusema, matendo ya Mungu katika mwili—ili kwamba wamkane Mungu asiye yakini, na kumjua Mungu ambaye ni wa leo na pia wa jana, na zaidi ya hilo, Mungu wa kesho, ambaye kwa kweli Ameishi toka milele hadi milele. Ni baada ya hapo tu, ndipo Mungu ataingia pumzikoni!” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ufafanuzi wa Mafumbo ya “Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima”, Sura ya 3).
Kabla ya Mungu kuwa mwili—yaani, miaka elfu mbili iliyopita—wanadamu wote (isipokuwa Wana wa Israeli) walikuwa gizani kabisa kuhusu kuwepo kwa Mungu, na kwamba Aliumba na kutawala vitu vyote. Kulikuwa na watu wengi ambao waliamini kuwa ni asili ambayo iliwaumba wanadamu. Wengi wa watu waliabudu pepo kadhaa wabaya na sanamu, walichoma uvumba na kusujudu kichina, na kulikuwa na mahekalu yaliyoitukuza miungu ya uongo kila mahali. Watu walichukulia kila aina ya pepo wabaya na Shetani kama Mungu wa kweli, kiasi kwamba wanadamu wote walimwabudu na kumtumikia Shetani. Wanadamu walikuwa chini ya udhibiti wa Shetani kabisa na waliishi kabisa chini ya uwanja wake. Walianguka katika giza na dhambi—huu ni ukweli unaojulikana sana. Baada ya Mungu kuhitimisha kazi Yake ya Enzi ya Sheria nchini Israeli, Waisraeli walianza kumwabudu na kumtumikia Mungu wa kweli. Lakini Mungu alifanya kazi tu kupitia wanadamu, na hakuwa amekuwa mwili ili kufanya kazi hiyo. Kwa hiyo, matokeo ya kazi ya Mungu katika Enzi ya Sheria yalifanikishwa tu miongoni mwa Waisraeli, lakini ulimwengu wote wa Mataifa bado ulimwabudu na kumtumikia Shetani na kuendelea kuishi katika giza na dhambi—hawakuweza kujinasua. Ilikuwa chini ya usuli huu ambapo Mungu alikuwa mwili ndani ya ulimwengu kama Bwana Yesu kwa mara ya kwanza ili kufanya kazi ya kuwakomboa wanadamu. Alihubiri njia ya toba, “Tubuni: kwa kuwa ufalme wa mbinguni uko karibu.” Alionyesha ukweli kiasi ili watu waweze kuona kuonekana kwa Mwokozi, na ni hapo tu ambapo watu walianza kutambua kwamba Mungu ndiye aliyeziumba mbingu na ardhi, na vitu vyote, na kwamba Yeye ndiye Mtawala wao. Ni hapo tu ambapo watu wengi walianza kumwamini na kumwabudu Mungu, lakini bado kulikuwa na watu wengi sana kati ya binadamu wapotovu ambao walimkana Mungu, waliamini pepo wabaya, na kumfuata Shetani. Shetani bado alikuwa anaendelea kuwadanganya wanadamu wapotovu. Aidha, watu wengi wa kidini walimwamini Mungu lakini kwa hakika hawakumjua Yeye, na walikuwa mbali sana na utii wa kweli na ibada ya Mungu. Hata hivyo, kuonekana na kazi ya Bwana Yesu iliwawezesha watu kuona kuonekana kwa Mwokozi kwa mara ya kwanza, kama tu kuona kuonekana kwa Mungu. Huu ni ukweli ambao hakuna mtu anayeweza kukataa. Katika siku za mwisho, Mungu akawa mwili tena—Yeye ni Mwenyezi Mungu—na alifanya kazi ya hukumu ya siku za mwisho, na kwa kufanya hivyo hatimaye Mungu alipata kundi la watu kati ya wanadamu wenye moyo na wazo moja na Yeye. Kundi hili la watu limepata ufahamu halisi wa tabia ya haki ya Mungu kwa sababu ya hukumu na kuadibu Kwake ambavyo wamevipitia, na wamekuza moyo wa uchaji Kwake, kuwa watu ambao ni watii kabisa kwa Mungu na wamepatwa na Yeye. Hili ndilo kundi la kwanza la watu ambalo Mungu amelipata kati ya binadamu wapotovu, na wao ni washindi wa kwanza waliofanywa na kazi ya hukumu ya Mungu ya siku za mwisho. Kwa kuwa maonyesho ya Mwenyezi Mungu—Neno Laonekana katika Mwili—yameenezwa na kusambazwa ulimwenguni kote, binadamu wameanza kuamka, na wamekuza shauku katika maneno ya Mungu. Kuna watu wengi ambao wanachunguza njia ya kweli na kutafuta ukweli, na binadamu wote wapotovu kwa shida wanaanza hatua kwa hatua, kurudi rasmi ili kuwa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Haya yote ni matokeo yanayofanikishwa na Mungu kupata mwili na kusema maneno kati ya wanadamu. Maneno ya Mungu yatafanya vitu vyote vifanyike, ambayo ndiyo maana Alisema: “Maneno Yangu yanavyokamilika, ufalme utaumbwa duniani hatua kwa hatua na mwanadamu atarudishwa kwa ukawaida hatua kwa hatua, na hivyo basi kutaanzishwa duniani ufalme ndani ya moyo Wangu. Katika ufalme, watu wote wa Mungu hupata maisha ya mwanadamu wa kawaida. Msimu wa barafu yenye baridi kali umeenda, umebadilishwa na dunia ya miji ya majira ya chipuko, ambapo majira ya chipuko yanadumu mwaka mzima. Kamwe, watu hawako wazi tena kwa ulimwengu wa mwanadamu usio na matumaini, na hawavumilii kuishi kwenye baridi kali ya dunia ya mwanadamu. Watu hawapigani na wenzao, mataifa hayaendi vitani dhidi ya wenzao, hakuna tena uharibifu na damu imwagikayo kutokana na uharibifu huo; ardhi nzima imejawa na furaha, na kila mahali pote panafurikwa na joto baina ya wanadamu” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 20).
“Nichukuapo kirasmi mamlaka Yangu na kutawala kama Mfalme katika ufalme, watu Wangu wote watakamilishwa na Mimi baada ya muda. Wakati mataifa yote ya dunia yatavurugwa, hapo ndipo hasa ufalme Wangu utaanzishwa na kupata umbo na pia Nitabadilika na kurejea kwa ulimwengu mzima. Wakati huo, watu wote watauona uso Wangu tukufu, watauona uso Wangu wa kweli” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 14).
“Mwishowe, Atachoma yote ambayo si safi na ambayo ni dhalimu ndani ya wanadamu katika ulimwengu mzima, ili kuwaonyesha kwamba Yeye si Mungu wa Rehema, na upendo tu, si Mungu wa hekima, na maajabu tu, si Mungu mtakatifu tu, bali, hata zaidi ni Mungu anayemhukumu mwanadamu. Kwa waovu miongoni mwa wanadamu, Yeye ni mwenye kuchoma, kuhukumu na kuadhibu; kwa wale ambao wanapaswa kukamilishwa, Yeye ni mateso, usafishaji, na majaribu, na vilevile faraja, ruzuku, utoaji wa maneno, kushughulika na kupogoa. Na kwa wale ambao wanaondolewa, Yeye ni adhabu na vilevile malipo” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili).
“Wakati mataifa na watu wa dunia watakaporudi mbele ya kiti Changu cha enzi, basi Nitachukua fadhila ya mbinguni na kuiweka kwa sababu ya ulimwengu wa binadamu, ili, kwa mujibu Wangu, itajazwa na fadhila isiyo ya kufananisha. Lakini ulimwengu wa kitambo ukiendelea kuwepo, Nitavurumisha hasira Yangu kwa mataifa yake, Nikieneza amri Zangu za utawala katika ulimwengu mzima, na kuleta kuadibu kwa yeyote anayezikiuka:
“Ninapozungumza na ulimwengu mzima, watu wote huisikia sauti Yangu, yaani, watu wote huona matendo yote ambayo Nimetekeleza katika ulimwengu mzima. Wale wanaokwenda kinyume na nia Zangu, yaani, wanaonipinga kwa matendo ya mwanadamu, wataanguka chini katikati ya kuadibu Kwangu. Nitazifanya upya halaiki ya nyota mbinguni; kwa nguvu Yangu, jua na mwezi vitafanywa upya, mbingu hazitakuwa kama zilivyokuwa; na vitu vyote duniani vitafanywa upya—haya yote yatatimia kwa sababu ya maneno Yangu. Nchi zote ulimwenguni zitagawanywa upya na nafasi yake kuchukuliwa na ufalme Wangu, ili kwamba nchi zilizo duniani zitatoweka milele, na kutakuwepo na ufalme unaoniabudu Mimi tu; nchi zote za dunia zitaangamizwa na zitatoweka. Kati ya wanadamu walio ulimwenguni, wale wote ambao ni wa mashetani wataangamizwa. Wote wanaomwabudu Shetani wataanguka chini katikati ya moto Wangu unaochoma—yaani, kando na wale walio ndani ya mkondo, wote watageuka kuwa majivu. Ninapowaadibu kila watu, jamii za kidini, kwa viwango tofauti, zitarudi katika ufalme Wangu, na kushindwa kupitia kwa matendo Yangu, kwa sababu watakuwa wameona kwamba ‘Mtakatifu aliye juu ya wingu jeupe’ tayari Amewasili. Watu wote wataainishwa kulingana na aina zao, na watapata kuadibu mbalimbali kulingana na matendo yao; wale wote walionipinga Mimi wataangamia, na kwa wale ambao matendo yao duniani hayajanihusisha Mimi, kwa sababu ya jinsi walivyotenda, wataendelea kuwepo duniani chini ya utawala wa wana Wangu na watu Wangu. Nitazionekania nchi zisizohesabika na watu wasiohesabika, na Nitaionyesha sauti Yangu mwenyewe duniani, Nikitangaza kukamilika kwa kazi Yangu kuu, nikiwaruhusu watu wote waone hili kwa macho yao wenyewe” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Sura ya 26).
Kutoka kwa neno la Mwenyezi Mungu tunaweza sote kuona kwamba kuonekana na kazi ya Mungu hasa vimekamilisha enzi ya imani ya wanadamu katika Mungu asiye yakini, na vilevile enzi ya giza na uovu wa Shetani kuwatawala na kuwapotosha wanadamu. Limefungua Enzi ya Ufalme ya kuonekana binafsi kwa Mungu na kazi, na utawala wa neno la Mungu. Kwa nini dunia ya kidini pia imefichuliwa na kuondolewa kabisa na kazi ya Mungu katika siku za mwisho, na hata imekuwa na uelekeo wa laana Yake ya milele? Ni kwa sababu watu wengi katika ulimwengu wa kidini bado wanamwamini Mungu asiye yakini, Mungu wa mawazo yao, lakini mioyoni mwao picha ya kweli ya Mungu na tabia Yake ya kweli havipo. Kwa hiyo, wana uwezo wa kumpinga na kumshutumu Mungu katika mwili, na kumtundika Yeye msalabani mara nyingine tena, ndiyo maana Mungu amewalaani, akisema: “Ole wao wamsulubishao Mungu” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Waovu Hakika Wataadhibiwa). Kuonekana kwa Mwenyezi Mungu na kazi katika siku za mwisho vimetimiza ukweli wa Neno kuonekana katika mwili. Tabia ya Mungu imeonyeshwa waziwazi kwa wanadamu wote, ikiwaruhusu watu wote kuona na kusikia maneno ya Mungu, na kuishi ndani ya utakaso wa hukumu Yake na kuadibu Kwake. Miongoni mwa wanadamu, kama mtu fulani humwamini au hamwamini Mungu, na kama ni wa na Mungu au Shetani, watu wote huainishwa kulingana na aina yao kwa njia ya mfichuo wa maneno ya Mungu. Wote ambao ni wa Mungu wameanza kuamka kwa maneno Yake na kumwelewa Yeye hatua kwa hatua kutoka kwa riziki ya maneno Yake, kuja uso kwa uso na Yeye, kuona kwamba Mungu hutawala kila kitu, na kwamba Yeye ndiye huongoza majaaliwa ya watu. Wote pia wameona haki na utakatifu wa Mungu ambavyo havivumilii makosa ya watu. Watu wote watarudi kwa Mungu, na maneno Yake yatatimiza vitu vyote. Kile ambacho ni cha Mungu kutarudi kwa Mungu, na kile ambacho ni cha Shetani kitarudi kwa Shetani. Punde baada ya hilo, Mungu atayatuza mema na kuadhibu mabaya, na atatumia maafa kuwaangamiza wote walio wa Shetani. Nguvu zote za uovu zitapinduliwa na kuadibu Kwake bila kuepuka, na Mungu atawaletea wale wote wanaoweza kuitii kazi Yake na kwa hakika kumgeukia Yeye hadi ndani ya Ufalme Wake. Huu ni ukweli wa kile ambacho Mungu atakamilisha hivi karibuni. Enzi ya Ufalme ni enzi ya tabia ya Mungu kufichuliwa waziwazi kwa wanadamu, na pia ni enzi ya wanadamu wakianza kumjua Mungu. Aidha, Enzi ya Ufalme ni enzi ya Mungu kusema maneno na kuonekana wazi kwa watu. Hakuna nguvu inayoweza kuzuia utekelezaji wa mapenzi ya Mungu duniani. Ufalme wa Kristo tayari umeonekana duniani, na unabii kutoka Kitabu cha Ufunuo umetimizwa kabisa: “Tazama, hema takatifu la Mungu liko pamoja nao watu, na yeye atakaa pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Na yeye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao, na kuwa Mungu wao. Na Mungu atayafuta machozi yote kutoka kwa macho yao, na hakutakuwa na kifo tena, wala huzuni, wala kilio, wala hakutakuwa na uchungu tena; maana yale mambo ya kale yamepita” (Ufunuo 21:3-4). Mwenyezi Mungu anasema, “Katika ufalme, maisha ambayo watu wa Mungu wanaishi pamoja na Mungu ni yenye furaha kupita kiasi. Maji yanacheza kwa furaha katika maisha ya watu yenye baraka, milima inafurahia pamoja na watu katika wingi Wangu. Wanadamu wote wanajitahidi, wakifanya bidii, wakionyesha uaminifu wao katika ufalme Wangu. Katika ufalme, uasi haupo tena, upinzani haupo tena; mbingu na dunia zinategemeana, Mimi na mwanadamu tunakaribiana katika hisia ya kina, katika furaha kuu tamu ya maisha, tukiegemeana….” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima, Furahini, Enyi Watu Wote!).
Kimetoholewa Kutoka Katika Majibu ya Mswada wa Filamu