Swali la 7: Miili miwili ya Mungu ilishuhudia kwamba Kristo ndiye ukweli, njia, na uzima. Tunapaswaje kuelewa Kristo kuwa ukweli, njia na uzima?
Jibu:
Kama waumini wanaweza kutambua kweli kwamba Kristo ni ukweli, njia, na uzima, hili ni lenye thamani kweli, na linaonyesha kwamba waumini kama hao wana ufahamu wa kweli kuhusu kiini cha Kristo. Mtu kama huyo pekee ndiye anaweza kusemekana kwamba anamjua Mungu kwa kweli. Kristo ni Mungu wa vitendo mwenye mwili. Wale tu wanaomtambua Kristo na wanaweza kumtii ndio wanamjua Mungu kwa kweli kwa sababu ukweli, njia, na uzima vyote vinatoka kwa Mungu, vyote vinatoka kwa maonyesha ya Kristo mwenye mwili. Isipokuwa Kristo, hakuna mtu anayeweza kusemekana kuwa ukweli, njia, na uzima, watu wachache sana ndio wanalielewa hili. Mungu anatumia uwezo wa mwanadamu kutambua kupata mwili kwa Mungu kama kiwango ambacho Anamjaribia mwanadamu. Wale tu wanaofikia kiwango hiki katika imani yao ndio wanaweza kupata sifa ya Mungu. Wale wote wanaokubali na kutii kupata mwili kwa Mungu ndio washindi ambao wananyakuliwa mbele za Mungu kukamilishwa kwanza. Wale ambao hawawezi kumkubali na kumtii Kristo watatumwa kustahimili mateso ya maafa kwa sababu hawatambui kupata mwili kwa Mungu na wanafikiriwa kuwa wanawali wapumbavu. Kama vile tu Bwana Yesu alipokuja, Aliwaleta juu ya mlima wale waliopenda ukweli na wale waliolikubali neno Lake na waliomfuata kweli, Akiwaongoza na kuwafundisha mwenyewe, huku Akikosa kuwazingatia hata kidogo wale wa ulimwengu wa dini na wale waliomwamini Mungu kwa ajili ya manufaa yao wenyewe kwa sababu walimwamini tu Mungu asiye yakini wa mbingu za juu na hawakukubali kupata mwili kwa Mungu. Walikuwa wasio fahamu katika kutoweza kwao kumtambua Mungu. Kwa hiyo wale tu wanaomkubali na kumtii Kristo mwenye mwili ndio watapokea sifa za Mungu na kukamilishwa na Yeye. Ni kwa nini Kristo pekee ndiye ukweli, njia, na uzima? Hebu tusome kifungu cha neno la Mwenyezi Mungu. “Njia ya maisha si kitu ambacho mtu yeyote anaweza kumiliki, wala si kitu ambacho mtu yeyote anaweza kufikia kwa urahisi. Hii ni kwa sababu maisha yanaweza kuja tu kutoka kwa Mungu, ambayo ni kusema, Mungu Mwenyewe tu ndiye Anamiliki mali ya maisha, hakuna njia ya maisha bila Mungu Mwenyewe, na hivyo Mungu tu ndiye chanzo cha uzima, na kijito cha maji ya uzima kinachotiririka nyakati zote. Kutoka Alipoumba dunia, Mungu amefanya kazi kubwa inayoshirikisha uhai wa maisha, Amefanya kazi kubwa ambayo huletea mwanadamu maisha, na Amelipa gharama kubwa ili mtu aweze kupata uzima, kwa kuwa Mungu Mwenyewe ni uzima wa milele, na Mungu Mwenyewe ni njia ambayo kwayo mtu hufufuliwa” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele). “Tayari nilishasema Mungu pekee ndiye maisha yasiyobadilika, na Mungu tu ndiye aliye na njia ya maisha. Kwa kuwa maisha Yake ni imara, hivyo ni ya milele; kwa kuwa Mungu tu ndiye njia ya maisha, basi Mungu Mwenyewe ni njia ya uzima wa milele” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele). Kutoka kwa neno la Mwenyezi Mungu tunaona kwamba ukweli, njia, na uzima vyote vinatoka kwa Mungu. Mungu Mwenyewe pekee Ndiye anamiliki njia ya uzima. Biblia inasema, “Mwanzoni kulikuwa na Neno, na Neno alikuwa na Mungu, na Neno alikuwa Mungu” (Yohana 1:1). Neno ni Mungu, Neno ni neno la Mungu. Neno ni ukweli, njia, na uzima. Neno kuwa mwili inahusu Roho wa Mungu aliyetokea katika mwili, yaani, ukweli, njia, na uzima vyote vimekuja katika mwili. Kama vile tu Mwenyezi Mungu anasema, “Neno limepata mwili na Roho wa ukweli amepatikana katika mwili—kwamba ukweli wote, njia, na uzima umekuja katika mwili, Roho wa Mungu hakika amewasili duniani na Roho amekuja katika mwili kwa kweli” (Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Utendaji (4)). Kupata mwili kwa Mungu kuwili kunashuhudia ukweli kwamba Yeye ni ukweli, njia, na uzima. Hili lilimpa mwanadamu ufunuo mkuu, lilimwonyesha kwamba Kristo pekee ndiye ukweli, njia, na uzima Maneno na kazi ya Mungu, chote ambacho Anacho na Alicho ni ukweli, njia, na uzima. Hiki ni kiini cha Kristo. Wakati Kristo anaonyesha neno la Mungu, Anafanya hivyo kama Mungu Mwenyewe Akiifanya kazi ya Mungu, Akihitimisha enzi ya awali na kuianzisha mpya, Akifanya kazi ya enzi nzima kwa ajili ya wanadamu wote. Neno la Mungu ambalo Kristo anaonyesha ni ukamilifu wa neno Lake katika hatua moja ya kazi hiyo. Kweli ni maonyesho ya tabia ya Mungu, chote ambacho Mungu anacho na Alicho, siri ya mpango wa usimamizi wa Mungu, na matakwa na kusudi la Mungu kwa wanadamu. Neno lote Lake ni ukweli. Haliwezi tu kufanyiza maisha ya mwanadamu, lakini pia linaweza kumpa mwanadamu uzima. Kama tu wakati Bwana Yesu alikuja, Alionyesha ukweli wote ambao mwanadamu alihitaji katika Enzi ya Neema, Akimruhusu mwanadamu kukiri dhambi zake, kutubu na kurudi mbele za Mungu, Akimfanya mwanadamu kustahili kuomba kwa Mungu na kuja mbele za Mungu kufurahia neema Yake, na kuona huruma na upendo Wake. Hili ni tokeo lililotimizwa na kazi ya ukombozi. Kazi ya Bwana Yesu iliruhusu dhambi za mwanadamu kusamehewa, ikiwakomboa wanadamu kutoka kwa dhambi. Bwana Yesu alitekeleza hatua ya kazi ya kuwakomboa wanadamu, Akiianzisha Enzi ya Neema na Akihitimisha Enzi ya Sheria. Mwenyezi Mungu wa siku za mwisho aliyepata mwili amekuja, Ameonyesha ukweli wote unaotakasa na kuwakomboa wanadamu, na Ametekeleza kazi ya hukumu akianza kwa nyumba ya Mungu, Akimruhusu mwanadamu aone tabia yenye haki na uweza na hekima ya Mungu, Akitakasa na kubadilisha tabia ya maisha ya mwanadamu, ili mwanadamu aweze kumcha Mungu na kuepuka maovu, na ajipokonye kabisa kutoka kwa ushawhisi wa Shetani, arudi mbele za Mungu na apatwe na Mungu. Kazi ya Mwenyezi Mungu inaanzisha Enzi ya Ufalme na inahitimisha Enzi ya Neema. Hili linatuonyesha kwamba yote ambayo Kristo anasema, Anafanya, Anaonyesha na kudhihirisha yote ni ukweli. Kristo pekee ndiye anaweza kumwelekeza mwanadamu kwa njia sahihi, na kumpa mwanadamu ruzuku ya maisha na wokovu, hakuna mwanadamu anayemiliki au anayeweza kuonyesha vitu hivi. Kristo ni kijito cha uzima wa mwanadamu, Yeye ni kuonekana kwa Mungu. Yeye ni ukweli, njia, na uzima, ukombozi na wokovu pekee wa Mungu. Isipokuwa Kristo, hakuna mwanadamu anayemiliki ukweli, na njia, na uzima, ukweli huu ni dhahiri kuona!
Kimetoholewa kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme