Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Neno Laonekana katika Mwili

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Epuka Ushawishi wa Giza na Upatwe na Mungu

Je, ushawishi wa giza ni nini?

Ushawishi wa giza ni utumwa wa Shetani, ni ushawishi wa Shetani, na ni ushawishi ambao una hali ya kifo.

Baada ya kumwomba Mungu kwa dhati, unaelekeza moyo wako kwa Mungu kikamilifu, katika hatua hii, moyo wako unasongezwa na Roho wa Mungu, uko tayari kujitoa mwenyewe kikamilifu, na katika wakati huu, umeepuka ushawishi wa giza. Kama yote ambayo mtu anafanya yanampendeza Mungu na anapatana na matakwa ya Mungu, basi yeye ni mtu ambaye anaishi ndani ya maneno ya Mungu, yeye ni mtu anayeishi chini ya uangalizi na ulinzi wa Mungu. Kama watu hawawezi kutenda maneno ya Mungu, daima wakimpumbaza Mungu na kutenda katika namna ya uzembe na Mungu, bila kuamini katika uwepo wa Mungu, watu kama hao wote wanaishi chini ya ushawishi wa giza. Watu ambao hawajapokea wokovu wa Mungu wote wamemilikiwa na Shetani, ambayo ni, hao wote wanaishi chini ya ushawishi wa giza. Wale ambao hawaamini katika Mungu wamemilikiwa na Shetani. Hata wale ambao wanaamini katika kuwepo kwa Mungu huenda si lazima wawe wanaishi katika nuru ya Mungu, kwa sababu wale ambao wanaamini katika Mungu huenda si lazima wawe wanaishi ndani ya maneno ya Mungu, na huenda si lazima wawe watu ambao wanaweza kutii Mungu. Mtu anaamini tu katika Mungu, na kwa sababu ya kushindwa kwa mtu kumjua Mungu, bado anaishi ndani ya kanuni za zamani, anaishi ndani ya maneno yaliyokufa, anaishi katika maisha ambayo ni giza na si ya hakika, hajatakaswa kikamilifu na Mungu, hajapatwa kikamilifu na Mungu. Kwa hivyo, ni dhahiri ya kwamba wale wasioamini katika Mungu wanaishi chini ya ushawishi wa giza, hata wale ambao wanaamini katika Mungu huenda wakawa bado wanaishi chini ya ushawishi wa giza, kwa ajili Roho Mtakatifu hajatekeleza kazi juu yao. Wale ambao hawajapokea neema ya Mungu au rehema ya Mungu, ambao hawawezi kuona kazi iliyotekelezwa na Roho Mtakatifu, wote wanaishi chini ya ushawishi wa giza; wale ambao wanafurahia tu neema ya Mungu na bado hawajui Mungu, hao pia wanaishi chini ya ushawishi wa giza, wakati mwingi. Kama mtu anaamini katika Mungu na bado anatumia wakati mwingi wa maisha yake akiishi chini ya ushawishi wa giza, basi kuwepo kwa mtu huyu kumepoteza maana yake, bila kutaja wale ambao hawaamini katika uwepo wa Mungu.

Wale wote ambao hawawezi kukubali kazi ya Mungu na kwa hivyo hawawezi kukidhi matakwa ya Mungu, wao wanaishi chini ya ushawishi wa giza; wale wanaotafuta ukweli na wana uwezo wa kukidhi matakwa ya Mungu watapokea baraka kutoka kwa Mungu, na wataepuka ushawishi wa giza.

Watu ambao hawajafunguliwa, ambao siku zote wamedhibitiwa na mambo fulani, ambao hawawezi kutoa moyo wao kwa Mungu, hawa ndio watu ambao wako chini ya utumwa wa Shetani, na wanaishi chini ya anga ya kifo.

Wale wasio waaminifu kwa wajibu wao wenyewe, wale wasio waaminifu kwa agizo la Mungu, wale ambao hawatekelezi jukumu lao kanisani, wao wanaishi chini ya ushawishi wa giza.

Wale ambao wanasumbua uwepo wa kanisa kimakusudi, wale ambao wanaharibu mahusiano kati ya akina ndugu na dada kimakusudi, wale ambao wanakutanisha magenge yao wenyewe, wao wanaishi hata zaidi chini ya ushawishi wa giza, wao wanaishi ndani ya utumwa wa Shetani.

Wale walio na uhusiano usio wa kawaida na Mungu, wale walio na tamaa za kifahari daima, wale ambao daima wanataka kufaidika kutoka kwa kila hali, wale ambao kamwe hawatafuti mabadiliko katika tabia yao, watu kama hao ni wale ambao wanaishi chini ya ushawishi wa giza.

Wale ambao hawako imara daima, ambao hawajatilia maanani katika utendaji wao wa ukweli, ambao hawatafuti kukidhi matakwa ya Mungu, wale ambao wanaridhisha tu miili yao wenyewe, hawa ni watu ambao pia wanaishi chini ya ushawishi wa giza, na wamefunikwa katika kifo.

Wale ambao hutumia hila na udanganyifu wakati wa kutekeleza kazi ya Mungu, ambao wanashughulika na Mungu katika njia ya kizembe, ambao wanadanganya Mungu, ambao daima wanafikiria kwa ajili yao wenyewe, watu kama hao wanaishi chini ya ushawishi wa giza.

Wale wote ambao hawawezi kumpenda Mungu kwa dhati, wale ambao hawatafuti ukweli, wale ambao hawazingatii kubadilisha tabia yao, wao wanaishi chini ya ushawishi wa giza.

Kama unataka kusifiwa na Mungu, lazima kwanza uepuke ushawishi wa giza wa Shetani, ufungue moyo wako kwa Mungu, na uuelekeze kwa Mungu kikamilifu. Je, mambo ambayo unafanya kwa sasa yanasifiwa na Mungu? Umeelekeza moyo wako kwa Mungu? Mambo ambayo umefanya, je, ni yale ambayo Mungu ametaka kwako? Je, yanaingiana na ukweli? Lazima daima ujichunguze, uzingatie kula na kunywa maneno ya Mungu, uweke moyo wako wazi mbele ya Mungu, umpende Mungu kwa uwazi, na ugharamie rasilmali kwa ajili ya Mungu kwa uaminifu. Watu kama hao hakika watapokea sifa ya Mungu.

Wale ambao hawaishi maisha yao kwa uaminifu, wakijifanya kuwa watu wasio wakati wako mbele ya wengine, wakitoa muonekano wa unyenyekevu, uvumilivu na upendo, lakini katika kiini ni wenye kudhuru kwa siri, wana hila na hawana uaminifu kwa Mungu, watu kama hao ni mfano wa kuigwa wa kawaida wa wale wanaoishi chini ya ushawishi wa giza, wao ni kizazi cha nyoka.

Wale ambao imani yao katika Mungu ni daima kwa ajili ya faida zao wenyewe, wale ambao wamejaa majivuno na jeuri, wale ambao hujigamba wenyewe, ambao daima wanalinda hadhi zao wenyewe, hawa ndio watu wanaopenda Shetani na kupinga ukweli, wao wanapinga Mungu na wao ni wa Shetani kikamilifu.

Wale ambao hawako makini na mizigo ya Mungu, ambao hawamtumikii Mungu kwa moyo mmoja, ambao daima wanajali maslahi yao wenyewe na maslahi ya familia zao, ambao hawawezi kuacha kila kitu ili wagharamie rasilmali kwa ajili ya Mungu, ambao kamwe hawaishi maisha yao kwa mujibu wa maneno ya Mungu, wao wanaishi nje ya maneno ya Mungu. Watu kama hawa hawatapokea sifa ya Mungu.

Wakati Mungu aliumba watu, ilikuwa watu wafurahie utajiri Wake, ili watu wampende kwa ukweli, na katika njia hii, watu wanaishi katika nuru Yake. Leo, wote ambao hawawezi kumpenda Mungu, ambao hawako makini na mizigo ya Mungu, ambao hawawezi kutoa moyo wao kikamilifu kwa Mungu, ambao hawawezi kuchukua moyo wa Mungu kama wao wenyewe, ambao hawawezi kubeba mizigo ya Mungu kama yao wenyewe, nuru ya Mungu haiangazi juu ya mtu yeyote kama hawa, kwa hivyo, wote wanaishi chini ya ushawishi wa giza. Watu kama hao wako kwenye njia ambayo huenda kinyume na mapenzi ya Mungu, yote wanayoyafanya hayana hata chembe ya ukweli, wako katika ushirikiano na Shetani, na watu kama hao wanaishi chini ya ushawishi wa giza. Kama unaweza daima kula na kunywa maneno ya Mungu na pia kuwa makini na mapenzi ya Mungu na kutenda maneno ya Mungu, basi wewe ni wa Mungu, basi wewe ni mtu anayeishi ndani ya maneno ya Mungu. Je, uko tayari kuepuka kumilikiwa na Shetani na kuishi katika nuru ya Mungu? Kama unaishi ndani ya maneno ya Mungu, basi Roho Mtakatifu atakuwa na nafasi ya kutenda kazi Yake; kama unaishi chini ya ushawishi wa Shetani, basi Roho Mtakatifu hatakuwa na nafasi ya kutenda kazi yoyote. Kazi ambayo Roho Mtakatifu hutenda kwa watu, nuru ambayo Yeye huangaza kwa watu, imani ambayo Yeye hutoa kwa watu hukaa kwa muda tu; kama watu hawako makini na hawampi kipaumbele, kazi iliyotendwa na Roho Mtakatifu itawapita. Kama watu wanaishi ndani ya maneno ya Mungu, basi Roho Mtakatifu atakuwa pamoja nao na kutenda kazi juu yao; kama watu hawaishi ndani ya maneno ya Mungu, basi wanaishi ndani ya utumwa wa Shetani. Watu wanaoishi katika tabia ya kiufisadi hawana uwepo wa Roho Mtakatifu na wala kuwa na Roho Mtakatifu kutenda kazi juu yao. Kama unaishi ndani ya nyanja ya maneno ya Mungu, kama unaishi katika hali kama inavyotakiwa na Mungu, basi wewe ni wa Mungu, na kazi ya Mungu itatendwa juu yako; kama huishi ndani ya nyanja ya matakwa ya Mungu, lakini badala yake unamilikiwa na Shetani, basi hakika wewe unaishi chini ya ufisadi wa Shetani. Kwa kuishi tu ndani ya maneno ya Mungu, kwa kutoa moyo wako kwa Mungu, unaweza kukidhi matakwa ya Mungu; lazima ufanye asemavyo Mungu, lazima ufanye maneno ya Mungu msingi wa kuwepo kwako na hali halisi ya maisha yako, ni basi tu ndipo utakuwa wa Mungu. Kama kwa dhati unatenda kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu, basi Mungu atatenda kazi juu yako, na kisha utaishi chini ya baraka za Mungu, utaishi katika nuru ya uso wa Mungu, ndipo pia utakuwa na uwezo wa kufahamu kazi ambayo Roho Mtakatifu hutenda, nawe utajihisi furaha ya uwepo wa Mungu.

Kuepuka ushawishi wa giza, lazima kwanza uwe mwaminifu kwa Mungu na kuwa na hamu ya kutafuta ukweli, basi ni hapo tu utakuwa na hali ya sahihi. Kuishi katika hali ya haki ni muhimu kwa ajili ya kuepuka ushawishi wa giza. Kukosa hali ya haki ina maana kwamba wewe si mwaminifu kwa Mungu na ya kwamba huna hamu ya kutafuta ukweli, basi uwezekano wa kuepuka ushawishi wa giza haupo. Mtu kuepuka ushawishi wa giza ni kwa msingi wa maneno Yangu, na kama mtu hawezi kutenda kwa mujibu wa maneno Yangu, mtu hataepuka utumwa wa ushawishi wa giza. Kuishi katika hali ya haki ni kuishi chini ya uongozi wa maneno ya Mungu, kuishi katika hali ya kuwa mwaminifu kwa Mungu, kuishi katika hali ya kutafuta ukweli, kuishi katika ukweli wa kugharamia rasilmali kwa ajili ya Mungu kwa dhati, kuishi katika hali ya kumpenda Mungu kwa kweli. Wale ambao wanaishi katika hali hizi na ndani ya hali halisi hii watabadilika hatua kwa hatua, wanapoingia ndani zaidi katika ukweli, nao watabadilika kwa kuongezeka kwa kazi ya Mungu, mpaka hatimaye hakika watapatwa na Mungu, na watakuja kwa kweli kumpenda Mungu. Wale ambao wameepuka ushawishi wa giza wataweza kufahamu mapenzi ya Mungu hatua kwa hatua, wataelewa moyo wa Mungu hatua kwa hatua, na hatimaye kuwa karibu na Mungu; hawatakuwa tu na dhana za Mungu, wala uasi kinyume na Mungu, watakuja kuchukia hata zaidi dhana na uasi ambao walikuwa nao kabla, kusababisha upendo wa kweli kwa Mungu mioyoni mwao. Wale ambao hawawezi kuepuka ushawishi wa giza wanashughulika na miili yao, na wamejaa uasi; moyo wao umejazwa na dhana za kibinadamu na falsafa ya maisha, pamoja na nia zao na majadiliano. Mungu anataka upendo mmoja wa mtu, Mungu anataka mtu amilikiwe kikamilifu na maneno Yake na upendo wa mtu kwa ajili Yake. Kuishi ndani ya maneno ya Mungu, kugundua kile ambacho mtu anatafuta kutoka ndani ya maneno ya Mungu, kumpenda Mungu kama matokeo ya maneno ya Mungu, kukimbiakimbia kutokana na maneno ya Mungu, kuishi kutokana na maneno ya Mungu, haya ndio mambo ambayo mtu anapaswa kufikia. Kila kitu lazima kijengwe kulingana na maneno ya Mungu, na hapo tu ndipo mtu ataweza kukidhi matakwa ya Mungu. Kama mtu hajiandai na maneno ya Mungu, basi mtu ni funza tu anayepagawa na Shetani. Yapime moyoni mwako mwenyewe, ni maneno mangapi ya Mungu ambayo umekita mizizi yake ndani yako? Ni katika mambo gani unaishi kwa mujibu wa maneno ya Mungu? Ni katika mambo gani hujakuwa ukiishi kwa mujibu wa maneno ya Mungu? Kama hujakuwa umemilikiwa kikamilifu na maneno ya Mungu, basi ni kwa kiasi gani umekuwa umemilikiwa? Katika maisha yako ya kila siku, je, unadhibitiwa na Shetani, au unaongozwa na maneno ya Mungu? Je, maombi yako yameanzishwa kutoka kwa maneno ya Mungu? Je, uliondoka katika hali zako mbaya kutokana na nuru ya maneno ya Mungu? Kuchukua maneno ya Mungu kama msingi wa kuwepo kwako, hili ndio jambo kila mtu anapaswa kuingia ndani. Kama maneno ya Mungu hayapo katika maisha yako, basi unaishi chini ya ushawishi wa giza, wewe ni muasi kwa Mungu, unampinga Mungu, hauheshimu jina la Mungu, na imani ya watu kama hao katika Mungu ni kabisa na usumbufu. Je, ni kiasi gani cha maisha yako umeishi kwa mujibu wa maneno ya Mungu? Ni kiasi gani cha maisha yako hujaishi kwa mujibu wa maneno ya Mungu? Kile ambacho maneno ya Mungu yamehitaji kwako, je, ni kiasi gani cha hicho kimetimia juu yako? Ni mangapi yamepotea kwako? Je, umechunguza mambo kama hayo kwa karibu?

Kuepuka ushawishi wa giza, kwa upande mmoja, inahitaji kazi iliyotendwa na Roho Mtakatifu, wakati kwa upande mwingine inahitaji ushirikiano wa kujitolea kutoka kwa mtu. Mbona Nasema ya kwamba mtu hayuko kwenye njia sahihi? Kama mtu yuko kwenye njia sahihi, kwanza, ataweza kutoa moyo wake kwa Mungu, na hili ni jukumu ambalo linahitaji muda mrefu kuingia ndani, kwa ajili mtu daima amekuwa akiishi chini ya ushawishi wa giza, akiwa chini ya utumwa wa Shetani kwa maelfu ya miaka, kwa hivyo kuingia huku hakuwezi kupatikana katika siku moja au mbili. Nilileta suala hili leo ili watu waweze kuwa na ufahamu wa hali yao wenyewe; kuhusu ushawishi wa giza ni nini na kuishi ndani ya nuru ni nini, kuingia kunawezekana wakati mtu ana uwezo wa kutambua mambo haya. Kwa sababu ni lazima ujue ushawishi wa Shetani ni nini kabla uepuke ushawishi wa Shetani, na hapo tu ndipo utakuwa na upatikanaji wa njia ya kuuepuka hatua kwa hatua mwenyewe. Kuhusu nini cha kufanya baada ya hapo, hilo ni suala la mtu mwenyewe. Lazima daima uingie kutoka chema, lazima usisubiri kiutulivu, na hii ndio jinsi utapatwa na Mungu.

Iliyotangulia:Tofauti Muhimu Kati ya Mungu Mwenye Mwili na Watu Wanaotumiwa na Mungu

Inayofuata:Kumwamini Mungu Kunapaswa Kulenge Uhalisi, Si Kaida za Kidini

Maudhui Yanayohusiana