Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Kondoo wa Mungu Huisikia Sauti ya Mungu

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Sura ya 6 Aina Mbalimbali za Utofautishaji Ambazo Unafaa Kumiliki katika Kusadiki Kwako kwa Mungu

7. Tofauti Kati Ya Matendo Mazuri ya Nje na Mabadiliko Katika Tabia.

Maneno Husika ya Mungu:

Je, "kubadailishwa kwa tabia" ni nini? Lazima uwe mpenzi wa ukweli, uikubali hukumu na kuadibiwa na neno la Mungu unapopitia kazi Yake, na kupitia aina zote za mateso na kusafishwa, ambayo kwayo unatakaswa kutokana na sumu ya kishetani iliyo ndani yako. Huku ndiko kubadilishwa kwa tabia. … Mabadiliko katika tabia yanamaanisha kuwa mtu, kwa sababu anapenda na anaweza kuukubali ukweli, hatimaye huja kujua asili yake ya uasi na ya kumpinga Mungu; anaelewa kuwa upotovu wa mwanadamu ni wenye kina zaidi na kuelewa upumbavu na udanganyifu wa mwanadamu. Anajua uduni wa mwanadamu na kusikitisha kwake, na hatimaye anaelewa kiini cha asili ya mwanadamu. Kwa kujua haya yote, anaweza kujikana na kujinyima kabisa, kuishi kwa neno la Mungu, na kutenda ukweli katika kila kitu. Mtu wa aina hii anamjua Mungu na tabia yake imebadilishwa.

kutoka kwa "Jinsi ya Kujua Asili ya Mwanadamu" katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Mgeuzo katika tabia hasa huhusu mgeuzo katika asili yako. Asili si kitu unachoweza kuona kutoka kwa mienendo ya nje; asili inahusisha moja kwa moja thamani na umuhimu wa kuishi kwa watu. Inahusisha moja kwa moja maadili ya maisha ya binadamu, mambo yaliyo ndani kabisa ya nafsi, na kiini cha watu. Kama watu hawangeweza kukubali ukweli, basi hawangekuwa na migeuzo katika hali hizi. Ni kama watu wamepitia kazi ya Mungu tu na wameingia kwa ukamilifu katika ukweli, wamebadilisha maadili na mitazamo yao kuhusu kuishi na maisha, wameyatazama mambo kwa njia sawa na Mungu, na wamekuwa na uwezo wa kutii na kujitoa kabisa kwa Mungu ndio tabia zao zinaweza kusemekana zimebadilika. Huenda ukaonekana kufanya juhudi fulani, huenda ukawa thabiti unapokabiliwa na shida, huenda ukaweza kutekeleza utaratibu wa kazi kutoka walio juu, au huenda ukaweza kwenda popote unapoambiwa kwenda, lakini haya ni mabadiliko madogo tu katika matendo yako, na hayatoshi kuwa mgeuzo katika tabia yako. Huenda ukaweza kukimbia katika njia nyingi, na huenda ukaweza kuvumilia shida nyingi na kustahamili fedheha kuu; huenda ukajihisi karibu sana na Mungu, na Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yako, lakini Mungu anapokuomba ufanye jambo fulani ambalo halipatani na fikira zako, bado hutii, unatafuta visababu, na unaasi na kumpinga Mungu, hata kufikia kiwango cha wewe kumlaumu Mungu na kumpinga Yeye. Hili ni tatizo kubwa! Hili linathibitisha kwamba bado una asili ya kumpinga Mungu na kwamba hujageuka hata kwa kiwango kidogo kabisa.

kutoka kwa "Unachopaswa Kujua Kuhusu Kuigeuza Tabia Yako" katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Imani kwa Mungu haimaanishi kwamba Anakuhitaji kuwa mtu mzuri, kuwa mtu ambaye ana tabia nzuri, au anayetii sheria, au mtu ambaye hawezi kufikiria mwenyewe au kutumia ubongo wake mwenyewe. Watu walikuwa wanafikiri kwamba mabadiliko katika tabia ambayo yalitoka kwa imani katika Mungu ilimaanisha kuwa mtu mwenye heshima, kwamba ilimaanisha kuwa na mfano fulani wa kibinadamu kwa nje, kulelewa vizuri, na mwenye subira, au kuonekana mcha Mungu, au mwenye upendo, na tayari kuwasaidia wengine, au mwenye msaada. Kwa ufupi, ilimaanisha kuwa aina ya mtu mzuri aliyekuwepo katika mawazo na dhana zao. Hii ni sawa na jinsi kuna watu duniani ambao wanasema: "Kama wewe ni tajiri, unapaswa kuwapa masikini au waombaji." ... Kwa hivyo, watu wengi waliamini kwamba imani katika Mungu haikuwa kingine ila mabadiliko machache katika tabia ya nje ya mtu, kufikiri, na matendo, na kulikuwa hata na watu wengine ambao waliamini kuwa imani katika Mungu ilimaanisha kupitia taabu nyingi sana, kutokula vyakula vizuri, na kutovaa nguo nzuri. Katika Magharibi, kwa mfano, kulikuwa na mtawa wa kike wa Kikatoliki (Ukatoliki pia ni dini; kwa watawa wa kike, pia ni aina ya imani) ambaye aliamini kwamba imani katika Mungu ilimaanisha kuishi akiteseka zaidi maisha yake yote, kula chakula kichache kizuri, kutojiruhusu kufurahia mambo mengi mazuri katika maisha, na kutoa fedha kwa masikini au wasiojiweza alipokuwa nazo—la sivyo kufanya matendo mema zaidi, kuwa wa usaidizi zaidi kwa watu, na kuwasaidia zaidi kwa wengine. Katika maisha yake yote hakufanya chochote ila kuteseka, wala hajikuruhusu kula chakula chochote kizuri au kuvaa nguo nzuri. Alipokufa, hakuwa amevaa kitu chochote kilichogharimu zaidi ya dola mbili; gharama zake za maisha ya kila siku, pia, zilifikia dola chache tu. Hadithi yake huenda ilionekana kama habari ya kawaida au kubwa duniani kote. Na hii inaonyesha nini? Kwa macho ya wanadamu, mtu kama huyu peke yake ndiye mtu mzuri na mwema, yeye pekee ndiye ambaye jamii ya kidini inamwamini kufanya mambo mema na matendo mema, ni yeye tu ndiye aliyebadilika, na kwa kweli ana imani kwa Mungu. Na hivyo inawezekana kwamba wewe si tofauti: Wewe bila shaka unaamini kwamba kumwamini Mungu na kuwa na imani kunahusu kuwa mtu mzuri. Na ni mtu wa aina gani? Mtu asiyepigana na wengine, au kuwalaani, au kuapa, mtu asiyefanya mambo mabaya, mtu anayeonekana kana kwamba anamwamini Mungu; kuna wengine, zaidi ya hayo, ambao wanasema kuwa mtu anayeleta utukufu kwa Mungu. ... Mungu anataka kumwokoa mwanadamu, Amenena maneno mengi, na kufanya kazi nyingi—na hivyo Anataka watu wawe namna gani? Anataka mawazo yao yaongozwe na ukweli, na kwa wao kuishi maisha yao kwa miito ya ukweli. Haombi kwamba uwe usiye na mawazo kama kikaragosi, sembuse Hataki uwe usiye na hisia kama mti, bila ya hisia yoyote ya kawaida. Badala yake, Anataka uwe mtu wa kawaida ambaye anapenda kile Anachopenda, na anachukia kile Anachochukia, ambaye anayeweza kufurahishwa na kile kinachomfurahisha, na kudharau na kukataa kile Anachokikana. ... Ni kwa sababu ya hili ndiyo Ninasema hujui nini maana ya mabadiliko katika tabia. Unajiwekea tu mipaka katika tabia yako, katika vitendo vyako vya nje, na katika hulka na mwenendo. Itakuwa vigumu kwako kufanikisha mabadiliko katika tabia yako kwa njia hii. Ni wapi katika maneno ya Mungu inasema, "Mnapaswa kujiwekea mipaka, mnapaswa kuchunga maneno yenu, kushikilia hisia zenu, na kuchunga hasira yenu, mnapaswa kuchunga msifichue asili zenu, na mnapaswa kuwa waangalifu katika nguo mnazonunua na kuvaa"? Je, Amewahi kusema maneno kama hayo? Hata pale ambapo kuna marejeleo ya mambo kama hayo, sio kiini cha maneno Yake, wala si ukweli mkuu ambao unaleta mabadiliko katika tabia za watu. Mengi ya maneno ya Mungu huzungumzia kiini potovu cha mtu, jinsi ya kujua kiini potovu cha mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyoweza kufanikisha mabadiliko katika tabia yake, jinsi anavyoweza kujua kweli tabia yake potovu, na jinsi anavyoweza kujiweka huru kutokana na tabia yake potovu ili kutenda kulingana na mahitaji ya Mungu na kuwa mtu ambaye anaupendeza moyo wa Mungu mwenyewe, na kutimiza matamanio ya Mungu. Kama unaelewa hili, je, bado utaendelea kuweka juhudi zako katika vitendo vya nje? Je, bado utakanganywa juu ya masuala kama hayo ya juu juu? Kwa hivyo, kama huelewi maana ya mabadiliko katika tabia, hutafahamu kamwe kiini cha mabadiliko katika tabia, na hutafanikisha mabadiliko katika tabia yako. Hasa, baadhi ya watu ambao wamekuja kutoka katika dini bado hawajafanya uhamisho kamili kutoka kwa sherehe za kidini na fikira na maoni ya kidini katika mtazamo wao na msimamo wa imani kwa Mungu; bado wanajaribu kuwa wa kiroho, na wacha Mungu, na wenye subira, kuwa mtu ambaye kiasili ni mzuri, ambaye anapenda kufanya mema na kuwapa wengine. Hii ni makosa kabisa! Ukifuatilia kuwa mtu kama huyo, hutasifiwa na Mungu kamwe.

kutoka kwa "Mabadiliko katika Tabia ni Nini na Njia inayoelekea kwa Mabadiliko katika Tabia" katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Watu wengi wanaweka mkazo maalum kwa tabia yao katika imani yao kwa Mungu, matokeo yakiwa mabadiliko yanayofanyika katika mienendo yao. Baada ya kuamini katika Mungu, wanakoma kubishana na wengine, wanakoma kupigana na watu na kuwatukana, wanakoma kuvuta sigara na kunywa, hawaibi mali ya uma—hata iwe msumari ama kipande cha mbao pekee—na hata wanaenda kiasi cha kutoipeleka kotini wanapopata hasara ama wamekosewa. Bila shaka, baadhi ya mabadiliko yanafanyika katika mienendo yao. Kwa sababu, baada ya kuamini katika Mungu, kukubali njia ya kweli inawafanya kuhisi vizuri kabisa, na kwa sababu wameonja neema pia ya kazi ya Roho Mtakatifu, wanakuwa na bidii hasa, na hata hakuna kitu chochote ambacho hawawezi kupuuza ama kufanya. Ilhali mwishowe—baada ya kuamini kwa miaka tatu, tano, kumi ama thelathini—kwa sababu hakujakuwa na mabadiliko katika tabia ya maisha yao, mwishowe wanateleza nyuma kwa njia zao za kitambo, kiburi chao na majivuno vinakua, na wanaanza kupigania nguvu na faida, wanatamani pesa ya kanisa, wanafanya chochote kinachofaidi maslahi yao, wanatamani cheo na raha, wanakuwa vimelea wa nyumba ya Mungu. Wengi wa viongozi, hasa, wameachwa. Na je ukweli huu unathibitisha nini? Mabadiliko katika kisicho zaidi ya mienendo ni kisicho endelevu. Kama hakuna mabadiliko katika tabia ya maisha ya watu,basi sasa ama baadaye upande wao wa uovu utajionyesha. Kwa sababu kiini cha mabadiliko katika mienendo yao ni juhudi, ikiongezwa na kazi ya Roho Mtakatifu katika wakati huo, ni rahisi sana kwao kuwa na juhudi, ama kuwa wazuri kwa muda. Kama wasioamini wanavyosema, "Kufanyia mtu tendo nzuri ni rahisi, kilicho kigumu ni kufanya matendo mazuri maisha yote." Watu hawana uwezo wa kufanya matendo mazuri maisha yao yote. Mienendo yao inaelekezwa na maisha; chochote ambacho maisha yao, pia mienendo yao ni hivo, na kile tu kinachofichuliwa kwa asili inawakilisha maisha, na asili ya mtu. Vitu vilivyo vya bandia havidumu. Mungu Anapofanya kazi kuokoa mwanadamu, sio kupamba mwanadamu na mienendo mizuri—kazi ya Mungu ni ili kubadilisha tabia za watu, kuwafanya wazaliwe kama watu wapya. Hivyo, hukumu ya Mungu, adibu, majaribu, na usafishaji wa mwanadamu ni yote ili kubadilisha tabia yake, ili aweze kupata kutii kabisa na uaminifu kwa Mungu, na kusifu Mungu kwa kawaida. Hili ndilo lengo la kazi ya Mungu. Kuwa na tabia nzuri siyo sawa na kumtii Mungu, pia kwa uchache zaidi si sawa na kulingana na Kristo. Mabadiliko katika tabia yanazingatia mafundisho, na kuzaliwa na juhudi—hayazingatii maarifa ya kweli ya Mungu, ama juu ya ukweli, kwa uchache zaidi, hayazingatii uongozi wa Roho Mtakatifu. Ingawa kuna nyakati ambazo baadhi ya yale watu wanafanya yanaongozwa na Roho Mtakatifu, haya siyo maonyesho ya maisha, ila sio sawa na kumjua Mungu; haijalishi mienendo ya mtu ni nzuri aje, haithibitishi kwamba wanamtii Mungu, ama kwamba wanaweka ukweli katika matendo. Mabadilikoya tabia ni udanganyifu wa muda, ni udhihirisho wa bidii, na siyo maonyesho ya maisha hayo. … Watu wanaweza kuwa na tabia nzuri, lakini hiyo haimanishi kuwa wako na ukweli. Juhudi ya watu inaweza tu kuwafanya kuzingatia mafundisho na kufuata kanuni; watu wasio na ukweli hawana namna ya kutatua shida muhimu, na mafundisho hayawezi kusimama kwa niaba ya ukweli. … Baadhi ya waumini wapya, baada ya kumwamini Mungu, wameacha dunia ya kilimwengu nyuma; wanapokutana na wasioamini hawana cha kusema, na ni vigumu sana kukutana kwao na jamaa na marafiki, na wasioamini wanasema, "Mtu huyu kweli amebadilika." Kwa hivyo wanafikiria, "Tabia yangu kweli imebadilika—wasioamini wanasema nimebadilika." Kwa weli, tabia yao kweli imebadilika? La hasha. Haya tu ni mabadiliko ya nje. Hakujakuwa na mabadiliko yoyote katika maisha yao, na asili yao ya kitambo imebaki kuwa na mizizi ndani yao, bila kuguzwa hata kidogo. Wakati mwingine, watu wanashikwa na juhudi kwa sababu ya kazi ya Roho Mtakatifu; baadhi ya mabadiliko ya nje yanatokea, na wanatenda vitendo chache nzuri. Lakini hii siyo sawa na mabadiliko kwa tabia. Uko bila ukweli, mtazamo wako kwa vitu haijabadilika, hata bila tofauti na ule wa wasioamini, na maadili yako na mtazamo wa maisha hayajabadilika. Hauna hata moyo unao heshimu Mungu, ambao angalau unafaa kuwa nayo. Hakuna kitu ambacho ni mbali na mabadiliko kwa tabia yako.

kutoka kwa "Tofauti Kati Ya Mabadiliko Ya Nje Na Mabadiliko Katika Tabia" katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Katika ulimwengu wa dini, watu wengi huteseka pakubwa maishani mwao mwote, kwa kuihini miili yao au kuubeba msalaba wao, au hata kuteseka na kustahimili hadi pumzi zao za mwisho! Wengine huwa wanafunga hadi siku ya kifo chao. Katika maisha yao yote wanajinyima chakula kizuri na mavazi mazuri, wakisisitiza mateso tu. Wanaweza kuihini miili yao na kuinyima miili yao. Uwezo wao wa kustahimili mateso unastahili sifa. Ila fikira zao, mawazo yao, mielekeo yao ya kiakili, na kwa hakika asili yao ya kale—hakuna kati yavyo kilichoshughulikiwa hata kidogo. Hawajifahamu. Picha ya Mungu akilini mwao ni ya kijadi na ya kidhahania, Mungu asiye yakini. Uamuzi wao wa kuteseka kwa ajili ya Mungu unaletwa na azma na asili yao chanya. Hata ikiwa wanamwamini Mungu, hawamfahamu Mungu wala kuyafahamu mapenzi Yake. Wanamfanyia Mungu kazi na kumtesekea Mungu kama vipofu. Hawawekei utambuzi thamani yoyote na hawajishughulishi na jinsi ambayo huduma yao inatimiza mapenzi ya Mungu kwa kweli. Aidha hawajui jinsi ya kutimiza ufahamu kuhusu Mungu. Mungu wanayemhudumia si Mungu katika sura Yake ya asili, ila ni Mungu waliyejifikiria, Mungu waliyemsikia, au Mungu wa kihadithi wanayemsoma katika maandiko. Kisha wanatumia mawazo yao dhahiri na mioyo yao ya kiungu kumtesekea Mungu na kuifanya kazi ambayo Mungu anapaswa kufanya. Huduma yao haiko sahihi, kiasi kwamba hakuna anayemhudumia Mungu kwa njia inayotimiza mapenzi Yake. Haijalishi wako radhi kiasi gani kuteseka, mitazamo yao asilia ya huduma na picha ya Mungu akilini mwao havibadiliki kwani hawajapitia hukumu ya Mungu na kuadibu na usafishaji Wake na ukamilifu, na kwa sababu hakuna yeyote aliyewaongoza na ukweli. Japo wanasadiki kwa Yesu Mwokozi, hamna kati yao aliyewahi kumwona Mwokozi. Wamemsikia tu kwa hadithi na uvumi. Hivyo huduma yao ni sawa na kuhudumu mara mojamoja macho yao yakiwa yamefungwa kama kipofu anayemhudumia baba yake. Ni nini kinaweza kupatikana kutokana na huduma kama hiyo? Na ni nani anaweza kuikubali? Huduma yao haibadiliki kamwe toka mwanzo hadi mwisho. Wanapokea mafunzo ya kibinadamu na kukita huduma yao katika uasili wao na kile wanachokipenda wao. Hili laweza kuzalisha faida gani? … Wale wote ambao hawajapokea hukumu, hawajapokea upogoaji na ushughulikiaji, na hawana mabadiliko—je, wao si waliokosa kushindwa kabisa? Wana manufaa gani watu kama hao? Ikiwa fikira zako, ufahamu wako wa maisha, na ufahamu wako wa Mungu hauonyeshi mabadiliko mapya na hautoi faida hata kidogo, hutatimiza chochote kizuri katika huduma yako. Bila maono na bila ufahamu mpya wa kazi ya Mungu, huwezi kuwa mtu aliyeshindwa. Njia yako ya kumfuata Mungu itakuwa kama ile ya wale wanaoteseka na kufunga—itakuwa ya thamani ndogo! Hii ni kwa sababu kuna ushuhuda kidogo katika yale wayafanyayo ndipo Nasema huduma yao ni bure! Kotekote katika maisha yao, hao watu huteseka, hukaa gerezani kwa muda, na kwa kila wakati, hustahimili, husisitiza mapenzi na ukarimu, na kubeba msalaba wao. Wanatukanwa na kukataliwa na ulimwengu na hupitia kila ugumu. Wanatii hadi mwisho ila bado hawapati ushindi na hawawezi kutoa ushuhuda wa kutwaliwa. Wameteseka si haba, ila kwa ndani hawamfahamu Mungu kabisa. Hakuna fikira zao za zamani, mawazo ya zamani, vitendo vyao, uelewa wa wanadamu, na mawazo ya wanadamu yaliyoshughulikiwa. Kamwe hakuna uelewa mpya ndani yao. Hakuna hata chembe ya ufahamu wao wa Mungu ambao ni wa kweli au ni sahihi. Wamekosa kuyaelewa mapenzi ya Mungu. Je, huku kwaweza kuwa kumhudumia Mungu? … Ikiwa katika kumwamini Mungu, yote ujuayo ni kuutiisha na kuuhini mwili wako na kustahimili na kuteseka, na hujui wazi ikiwa unachokifanya ni sawa au la, bila kujali unamfanyia nani kazi, basi vitendo kama hivi vitaletaje mabadiliko?

kutoka kwa "Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (3)" katika Neno Laonekana katika Mwili

Kila mara watu wa kidini kama hao wanapokusanyika, wanaulizana, "Dada, uko vipi siku hizi?" Anajibu, "Nahisi kuwa mimi ni mdeni wa Mungu na siwezi kutosheleza matakwa ya moyo Wake." Mwengine anasema, "Mimi, pia, ni mdeni wa Mungu na nimeshindwa kukidhi matakwa Yake." Sentensi na maneno haya machache pekee yanaonyesha maovu yaliyo ndani ya nyoyo zao. Maneno kama hayo ni ya kuchukiza zaidi na yenye makosa sana. Asili ya watu kama hao inaleta upinzani kwa Mungu. Wale ambao huzingatia ukweli halisi huwasilisha vilivyomo katika nyoyo zao na kufungua mioyo yao katika mawasiliano. Hakuna shughuli hata moja ya uongo, hakuna heshima ama salamu na mazungumzo matupu. Wao huwa na uwazi na hawafuati sheria za duniani. Kuna wale ambao wako na upendeleo wa kujionyesha kwa nje, hata bila maana yoyote. Wakati mwenziwe anaimba, yeye anaanza kucheza, bila hata kujua kuwa wali kwenye sufuria yake umeshaungua. Watu wa namna hii si wacha Mungu au waheshimiwa, bali ni watu wa kijinga kupindukia. Hizi zote ni dalili za ukosefu wa ukweli! Baadhi yao hukusanyika kuzungumza kuhusu mambo ya maisha katika roho, na ingawa hawasemi kuhusu kuwa kwao wadeni wa Mungu, wao hubaki na upendo wa kweli kwa Mungu ndani ya mioyo yao. Kuwa kwako mdeni kwa Mungu hakuhusiani na watu wengine; wewe ni mdeni kwa Mungu, si kwa mwanadamu. Kwa hiyo ina maana gani ya wewe daima kuzungumzia haya kwa watu wengine? Lazima uweke umuhimu kwa kuingia katika hali halisi, si kwa bidii ya nje au maonyesho.

Je, matendo ya kijuujuu ya mwanadamu yanawakilisha nini? Hayo huwakilisha mwili, na hata matendo yaliyo bora zaidi ya nje hayawakilishi maisha, ila tabia yako tu mwenyewe. Matendo ya nje ya mwanadamu hayawezi kutimiza tamaa za Mungu. Wewe daima huzungumza kuhusu udeni wako kwa Mungu, lakini huwezi kuyakidhi maisha ya wengine au kuwafanya wengine kumpenda Mungu. Je, unaamini kwamba matendo hayo yatamridhisha Mungu? Unaamini kwamba hii ndiyo hamu ya moyo wa Mungu, kwamba haya ni ya roho, lakini kwa kweli huu ni ujinga! Unaamini kwamba yale yanayokupendeza wewe na unayotaka ni yale yanayomfurahisha Mungu. Je, inawezekana kuwa unayoyataka wewe yanaweza kuwakilisha Anayotaka Mungu? Je, tabia ya mwanadamu inaweza kumwakilisha Mungu? Yale yanayokupendeza wewe ndiyo hasa yale humchukiza Mungu, na mienendo yako ni ile ambayo Mungu huchukia na kukataa. Kama wewe unahisi kuwa u mdeni, basi nenda na usali mbele za Mungu. Hakuna haja ya kuyazungumzia mambo haya kwa watu wengine. Usipoomba mbele za Mungu na badala yake mara kwa mara unavuta nadhari kwako wewe mwenyewe mbele ya wengine, jambo hili linaweza kutimiza hamu ya moyo wa Mungu? Kama matendo yako daima ni katika kuonekana tu, hii ina maana kuwa wewe ni mtu bure zaidi ya wote. Ni mtu wa aina gani yule aliye na matendo mema ya kijuujuu tu lakini hana uhalisi? Watu kama hao ni Wafarisayo wanafiki na watu wa dini! Usipoacha matendo yako ya nje na huwezi kufanya mabadiliko, basi mambo ya unafiki ndani yako yatazidi kuimarika. Namna mambo ya unafiki yanavyozidi kuwa, ndivyo upinzani kwa Mungu unavyozidi, na mwishowe, aina hii ya watu hakika watatupiliwa mbali!

kutoka kwa "Kumwamini Mungu Lazima Kulenge Uhalisi, Si Tamaduni za Kidini" katika Neno Laonekana katika Mwili

Inaweza kuwa kwamba katika miaka yako yote ya imani katika Mungu, kamwe hujamlaani mtu yeyote wala kumfanyia tendo mbaya, lakini katika uhusiano wako na Kristo, huwezi kusema ukweli, kutenda kweli, au kutii neno la Kristo; basi Ninasema kwamba wewe ni mdanganyifu mkubwa na mtenda dhambi katika dunia. Kama wewe ni hasa mtu mwema na mwaminifu kwa jamaa yako, marafiki, mke (au mume), wanao, na wazazi, na kamwe hujanyanyasa wengine, lakini huwezi kulingana na kuwa na amani na Kristo, basi hata iwapo utatuma vitu vyako vyote kama misaada kwa jirani zako au umemlinda vizuri baba yako, mama, na kaya, bado Nasema kwamba wewe ni mwovu, na mwenye hila pia. Usifikiri kwamba wewe unalingana na Kristo ikiwa unalingana na mwanadamu au unafanya baadhi ya matendo mema. Je, unaamini kwamba wema wako unaweza kujinyakulia baraka za Mbinguni? Je, unafikiri kwamba matendo mema yanaweza kubadilishwa na utii wako? Hakuna hata mmoja yenu anaweza kukubali ushughulikiaji na upogoaji na kupogoa, na wote huwa vigumu kukubali ubinadamu wa kawaida wa Kristo. Hata hivyo siku zote mnadai utiifu kwa Mungu. Imani kama yenu italeta adhabu ya kufaa.

kutoka kwa "Wale Wasiopatana Na Kristo Hakika Ni Wapinzani Wa Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili

Ushirika wa Mtu:

Watu ambao hawana ukweli huongea juu ya kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu mzuri kana kwamba ni sawa na ukweli. Je, wewe huthubutu kuthibitisha kwamba kuishi kwa kuthibitisha ubinadamu mzuri kunafanana na ukweli? Je, wewe huthubutu kuthibitisha kuwa ni kitu chanya? Haya, mnasema nini: Upendo wa mtu ni sawa na upendo wa Mungu? La. Wakati mwingine, upendo wa mtu ni upendo wa Shetani, ni upendo wenye jazba, upendo ambao ni matokeo ya tamaa na maslahi ya mtu mwenyewe. Kutoa mfano rahisi: Ikiwa mtu ni mwenye pepo mbaya kwa asili, kama anapenda pepo, ana upendo gani? Hampendi Mungu, lakini anapenda pepo. Si huu ni upendo wa Shetani? Upendo wa Shetani huenda dhidi ya ukweli, uko katika uadui na ukweli, na huenda kinyume na kile Mungu anacho na alicho na kwa upendo wa Mungu. Usifikiri kuwa kuwa na upendo huwafanya watu wawe wema. Upendo wao hauna ukweli, ni upendo wa mambo hasi, na hivyo ni upendo wa Shetani. Je, si baadhi ya wema wao uko katika upinzani kwa ukweli? Baadhi ya wema wa watu uko katika upinzani kwa ukweli, na hivyo, hata ingawa kwa wengine wao waelekea kuwa watu wema, na huonekana wazuri na wa kuheshimiwa, wao si lazima ni wale waupendezao moyo wa Mungu, na wanaweza kuwa watu hasi. Je, si hili ni sahihi? Kwa hiyo, bila kujali kama wapotovu huonekana kuwa watu wema au wabaya kwa watu, kwa Mungu wote ni wa Shetani, wote wana tabia ya kishetani, wote ni wapotovu, na wote  ni wa uadui na Mungu. Hebu tudondoe mifano kadhaa: Ni vipi, mnasema, watu katika dini wangeweza kumkongomeza Kristo msalabani? Na walipomkongomeza Kristo msalabani, walikuwa na motisha gani? Waliamini kuwa motisha yao ilikuwa mbaya? Walidhani walikuwa wakiwa waaminifu kwa Mungu, kwamba walikuwa wakiunga mkono kazi ya Mungu, na kusimama imara katika ushahidi wao–lakini mbele ya Mungu walikuwa wakimpinga Yeye, na walikuwa maadui Zake. Unafikiria nini juu ya hilo? Leo, jamii ya kidini inalaani kazi ya Mungu ya siku za mwisho, wao kwa mara nyingine tena wamemkongomeza Kristo msalabani, na katika vichwa vyao wanafikiri kuwa wanaiunga mkono kazi ya Mungu, na kuwa waaminifu kwa Mungu, na hawako katika uadui na Mungu. Wanafikiri kwamba ni wao tu wanaompenda Mungu, kwamba ni wao tu ambao ni waaminifu zaidi kwa Mungu. Je, si hivyo ndivyo wanavyofikiria? Kwa hiyo, kwa wapotovu, kwa kufikiri na kutenda jinsi hii, wanachokifanya ni sahihi, na sahihi kabisa–lakini, kwa Mungu, wao bila shaka wanampinga Yeye, ni adui Zake. Je, unatafsirije hili? Je, kuwa mzuri kunamaanisha kuwa watu wanaupendeza moyo wa Mungu? Je, kuna maana kwamba wao ni waadilifu? Je, kunamaanisha kuwa wao wanalingana na Mungu? Na hivyo, bila ukweli, watu wanaweza kuupendeza moyo wa Mungu? Bila ukweli, si wao wako katika upinzani kwa Mungu? Hivyo wema wa watu ni chanya au hasi? Sana sana, wema wa watu ni hasi, kwa sababu ni mchafu mno, umetiwa mawaa na sumu ya Shetani, na hauna chochote cha ukweli. Na hivyo, wakati "motisha" zao ni nzuri, katika vitendo vyao si lazima wawe wanaweka ukweli katika vitendo, na wanaweza kuwa wakimpinga Mungu, na kwa uadui dhahiri na Mungu; ushahidi kamili wa hili unapatikana katika upinzani na uasi wa jamii ya kidini dhidi ya Mungu, na katika kumsulubisha kwao Kristo kwa mara ya pili. ... Hivyo, wakati watu "wanaishi kwa kudhihirisha," wakati wanafanya "jambo sahihi" na kufanya "matendo mema," haya si lazima yawe yanafanana na ukweli; baadhi ya vitendo vyao humpinga Mungu, na pia vinaweza kuelezewa kama uovu, au kaidi, au katika kumsaliti Mungu. Sasa unaona mambo haya wazi, ndiyo? Bila kujali jinsi watu wanavyokifikiri kitu kuwa chema, hii haimaanishi kuwa wanamiliki ukweli, au uhalisi; ni kuweka  tu ukweli katika matendo ndiko kuwa na uhalisi.

kutoka "Ushirika na Mahubiri Kuhusu Maneno ya Mungu 'Ni Kuweka Ukweli Katika Vitendo Pekee Ndiko Kuwa na Uhalisi'" katika Mahubiri na Ushirika juu ya Kuingia Katika Maisha (VI)

Iliyotangulia:Unawezaje Kutofautisha Kati ya Viongozi wa Kweli na wa Uongo, na Wachungaji wa Kweli na wa Uongo?

Inayofuata:Lazima Ujue Chanzo cha Upinzani wa Watu kwa Kazi Mpya ya Mungu katika Imani Yao kwa Mungu.

Maudhui Yanayohusiana