1. Kujua Chanzo cha Upinzani wa Watu kwa Kazi Mpya ya Mungu katika Imani Yao kwa Mungu

Maneno Husika ya Mungu:

Sababu ya mwanadamu kumpinga Mungu inatoka, kwa upande mmoja, katika tabia potovu ya mwanadamu, na kwa upande mwingine, kutokana na kutomfahamu Mungu na kutoelewa kanuni za kazi ya Mungu na mapenzi Yake kwa mwanadamu. Vipengele hivi viwili vinaunganishwa katika historia ya upinzani wa mwanadamu kwa Mungu. Wachanga katika imani humpinga Mungu kwa sababu upinzani huo uko ndani ya asili yao, huku upinzani dhidi ya Mungu wa wale walio na miaka mingi katika imani unatokana na kutomjua Mungu, pamoja na tabia potovu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Watu Wote Wasiomjua Mungu Ni Watu Wanaompinga Mungu

Kazi ya Mungu inaendelea kusonga mbele, na ingawa madhumuni ya kazi Yake hubakia bila kubadilika, njia Anazotumia kufanya kazi zinabadilika kila mara, na hivyo ndivyo wale wanaomfuata Mungu. Kadiri kazi ya Mungu inavyoongezeka, ndivyo mwanadamu anavyomjua Mungu kwa undani zaidi, na tabia ya mwanadamu inabadilika ipasavyo pamoja na kazi Yake. Hata hivyo, ni kwa sababu kazi ya Mungu milele inabadilika ndio wale wasiojua kazi ya Roho Mtakatifu na wale wanadamu wajinga wasiojua ukweli wanakuwa wapinzani wa Mungu. Kazi ya Mungu kamwe haifuati dhana za mwanadamu, kwani kazi Yake daima ni mpya na siyo nzee. Kamwe Hairudii kazi ya zamani lakini badala Anasonga mbele na kazi ambayo haijafanywa hapo awali. Kwa sababu Mungu harudii kazi Yake na mwanadamu daima anahukumu kazi ya Mungu leo kulingana na kazi Yake ya zamani, ni vigumu sana kwa Mungu kutekeleza kila hatua ya kazi ya enzi mpya. Mwanadamu ana vizuizi vingi sana! Kufikiria kwa mwanadamu ni kwa akili finyu! Hakuna mwanadamu anayeijua kazi ya Mungu, lakini bado wote wanafafanua kazi hiyo. Mbali na Mungu, mwanadamu anapoteza uzima, ukweli na baraka za Mungu, lakini bado mwanadamu hajapokea uzima wala ukweli, sembuse baraka kuu zaidi ambazo Mungu huwapa wanadamu. Wanadamu wote wanataka kumpata Mungu lakini bado hawawezi kuvumilia mabadiliko yoyote kwa kazi ya Mungu. Wale wasiokubali kazi mpya ya Mungu wanaamini kwamba kazi ya Mungu haibadiliki, na kwamba kazi ya Mungu milele inabakia kusimama. Katika imani yao, kinachohitajika ili kupata wokovu wa milele kutoka kwa Mungu ni kushika sheria, na mradi tu watubu na kukiri dhambi zao, mapenzi ya Mungu yatatimizwa milele. Wana maoni kwamba Mungu anaweza tu kuwa Mungu chini ya sheria na Mungu aliyesulubiwa kwa sababu ya mwanadamu; pia ni maoni yao kwamba Mungu hastahili na Hawezi kuzidi kiwango cha Biblia. Ni hasa maoni haya yaliyowafunga imara kwa sheria ya zamani na kuendelea kuwafumba kwa kanuni ngumu. Hata zaidi wanaamini kwamba kazi yoyote ile mpya ya Mungu, ni lazima ithibitishwe na unabii, na kwamba katika kila hatua ya hiyo kazi, wote wanaomfuata na roho ya kweli lazima pia waonyeshwe ufunuo, vinginevyo kazi hiyo haiwezi kuwa ya Mungu. Tayari si kazi rahisi kwa mwanadamu kuja kumjua Mungu. Ikichukuliwa pamoja na moyo wa ujinga wa mwanadamu na asili yake ya kuasi ya kujiona muhimu na kujivunia, basi ni vigumu zaidi kwa mwanadamu kukubali kazi mpya ya Mungu. Mwanadamu haitafiti kazi mpya ya Mungu kwa utunzaji wala haikubali na unyenyekevu; badala yake, mwanadamu anachukua mtazamo wa dharau, kusubiri ufunuo na mwongozo wa Mungu. Je, hii si tabia ya mwanadamu anayemwasi na kumpinga Mungu? Watu kama hao wanawezaje kupata kibali cha Mungu?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Jinsi Gani Ambavyo Mwanadamu Ambaye Amemwekea Mungu Mipaka katika Fikira Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?

Kwa sababu kazi ya Mungu mara zote huwa na maendeleo mapya, kuna kazi ambayo inakuwa iliyopitwa na wakati na nzee kazi mpya inapoibuka. Hizi aina tofauti tofauti za kazi, nzee na mpya, hazikinzani, bali zinatoshelezana, kila hatua ikifuata iliyotangulia. Kwa kuwa kuna kazi mpya, mambo ya zamani, kwa hakika, ni sharti yaondolewe. Kwa mfano, baadhi ya vitendo vilivyokita mizizi na misemo ya mwanadamu iliyozoeleka, kuongeza juu miaka mingi ya mazoea na mafundisho ya mwanadamu, ilimuumbia mwanadamu kila aina ya dhana. Maelezo ya mwanadamu kuhusu dhana kama hizi ni kwamba bado Mungu hajafichua uso Wake halisi na tabia Yake ya asili kwa mwanadamu, pamoja na kuenea kwa nadharia za kale kwa miaka mingi zimekuwa za kupendelea uundaji wa mwanadamu wa fikira kama hizo. Inaweza kusewa kwamba, katika kipindi cha imani ya mwanadamu kwa Mungu, ushawishi wa fikira mbalimbali umesababisha kutengenezwa na kubadilika kwa ufahamu wote wa fikira kumhusu Mungu ndani ya watu, jambo ambalo limewafanya watu wengi wa kidini wanaomtumikia Mungu wageuke kuwa adui Zake. Hivyo, kadiri fikira za watu za kidini zinavyokuwa thabiti, ndivyo wanavyozidi kumpinga Mungu, na ndivyo wanavyozidi kuwa maadui wa Mungu. Kazi ya Mungu daima huwa mpya, si kongwe na huwa haitengenezi mafundisho ya kidini na badala yake inabadilika kila mara na kuwa mpya kwa kiwango fulani. Kazi hii ni onyesho la tabia ya asili ya Mungu Mwenyewe. Vilevile ni kanuni ya asili ya kazi ya Mungu na mojawapo ya njia ambazo Mungu hutimiza usimamizi Wake. Iwapo Mungu asingefanya kazi kwa njia hii, mwanadamu asingebadilika au kuweza kumfahamu Mungu, na Shetani asingeshindwa. Hivyo basi, kila mara katika kazi Yake, kunatokea mabadiliko ambayo yanaonekana hayatabiriki, ila ambayo, kwa hakika, yana kipindi chake. Njia mwanadamu anavyomwamini Mungu hata hivyo ni tofauti. Anashikilia mifumo ya zamani ya kidini na kadiri yalivyo ya zamani, ndivyo yanavyokuwa ya kupendeza kwake. Akili ya kipumbavu ya mwanadamu, akili isiyobadilika kama mawe inawezaje kukubali kazi nyingi isiyoeleweka mpya na maneno ya Mungu? Mwanadamu anamchukia Mungu ambaye ni mpya kila siku na si wa zamani; anampenda tu Mungu wa zamani, ambaye ni mzee kwa umri, aliyejaa mvi na Aliyekwama papo hapo. Hivyo, kwa sababu Mungu na mwanadamu kila mmoja analo alipendalo, mwanadamu amekuwa adui wa Mungu. Kwa kiwango kikubwa, huu utata upo hata leo, wakati ambao Mungu amekuwa akifanya kazi mpya kwa takribani miaka 6000. Hawawezi kusaidika. … Madhumuni ya Mungu mara zote ni kuona kazi Yake ikiwa mpya na hai, si kongwe na iliyokufa, na kile Anachotaka mwanadamu ashikilie kwa nguvu kinabadilika kulingana na enzi na kipindi, na si cha kudumu milele na kisichobadilika. Hii ni kwa sababu Yeye ni Mungu ambaye husababisha mwanadamu kuishi na kuwa mpya, tofauti na ibilisi anayemsababishia mwanadamu kufa na kuwa mzee. Je, bado hamlielewi hili? Una dhana kuhusu Mungu na umeshindwa kuziacha kwa kuwa hutafakari. Si kwa sababu kuna maana kidogo sana ndani ya kazi ya Mungu, wala kwa sababu kazi ya Mungu inatofautiana na matakwa ya binadamu, wala kwamba Mungu mara zote ni “mzembe katika wajibu Wake.” Huwezi kuacha dhana zako kwa kuwa umepungukiwa na utiifu, na huna sifa hata kidogo za kiumbe wa Mungu, na si kwamba Mungu anakufanyia mambo kuwa magumu. Yote haya umejisababishia na hayana uhusiano na Mungu; mateso na misukosuko yote husababishwa na mwanadamu. Dhamira za Mungu mara zote huwa nzuri: hakusudii kukufanya uzalishe dhana, ila angependa ubadilike na uwe mpya kadiri enzi zinavyopita. Ila bado huwezi kutofautisha chokaa na jibini na kila mara ama unachunguza au unachanganua. Si kwamba Mungu anakufanyia mambo kuwa magumu, ila ni kuwa humheshimu Mungu na uasi wako umezidi. Kiumbe mdogo anathubutu kuchukua sehemu ndogo ya kile alichopewa mwanzo na Mungu, na kisha kubadilika na kukitumia kumvamia Mungu—je, huu si uasi wa mwanadamu? Ni haki kusema kuwa binadamu hawana sifa kabisa za kutoa maoni yao mbele za Mungu, na sembuse hawana sifa za kuonyesha hadharani maneno yao yasiyo na thamani, yanukayo, yaliyooza wapendavyo—bila kutaja chochote kuhusu hizo fikira zilizooza. Je, si watu wasio na thamani zaidi?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Wale tu Wanaoijua Kazi ya Mungu Leo Ndio Wanaoweza Kumhudumia Mungu

Mjue kwamba mnapinga kazi ya Mungu, au mnatumia dhana zenu kupima kazi ya leo, kwa sababu hamjui kanuni za kazi ya Mungu, na kwa sababu hamchukulii kazi ya Roho Mtakatifu kwa umakini wa kutosha. Upinzani wenu kwa Mungu na kizuizi kwa kazi ya Roho Mtakatifu kumesababishwa na dhana zenu na kiburi cha asili. Si kwa sababu kazi ya Mungu si sahihi, lakini ni kwa sababu mna tabia ya kuasi kiasili. Baada ya kuja kumwamini Mungu, baadhi ya watu hawawezi hata kusema kwa uhakika mwanadamu alikotoka, lakini wanathubutu kutoa hotuba za hadharani wakitathmini usahihi na makosa ya kazi ya Roho Mtakatifu. Na wanawahutubia hata mitume ambao wana kazi mpya ya Roho Mtakatifu, wakitoa maoni huku wakizungumza kwa zamu; ubinadamu wao uko chini sana, na hawana hisia zozote ndani yao. Je, si kuna siku itafika ambapo watu kama hawa watakataliwa na kazi ya Roho Mtakatifu, na kuchomwa katika moto wa kuzimu? Hawafahamu kazi ya Mungu, lakini badala yake wanakosoa kazi Yake, na pia wanajaribu kumuelekeza Mungu jinsi ya kufanya kazi. Je, watu kama hao wasio na busara wanawezaje kumjua Mungu? Mwanadamu huja kumjua Mungu wakati wa mchakato wa kutafuta na kupitia; maarifa ya Mungu hayapatikani kupitia nuru ya Roho Mtakatifu kwa njia ya mwanadamu kutoa hukumu za kiholela. Kadiri maarifa ya watu kuhusu Mungu yanavyozidi kuwa sahihi, ndivyo upinzani wao Kwake unavyopungua. Kinyume na hayo, kadri watu wanavyomjua Mungu kwa kiasi kidogo, ndivyo wanavyokuwa na uwezekano wa kumpinga. Dhana zako, asili yako ya zamani, na ubinadamu wako, tabia na mtazamo wako wa kimaadili ndio “mtaji” ambao unatumia kumpinga Mungu, na kadri unavyokuwa mpotovu, ulivyoshushwa heshima na ulivyo duni, ndivyo unavyozidi kuwa adui wa Mungu. Wale walio na dhana imara na wenye tabia ya kujiinua wamo hata zaidi katika uadui na Mungu mwenye mwili, na watu kama hawa ni wapinga Kristo. Ikiwa dhana zako hazitarekebishwa, basi daima zitakuwa kinyume na Mungu; daima hutalingana na Mungu, na daima utakuwa mbali na Yeye.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu

Je, mngependa kujua kiini cha sababu ya Mafarisayo kumpinga Yesu? Je, mnataka kujua dutu ya Mafarisayo? Walikuwa wamejawa na mawazo makuu kuhusu Masiha. Kilicho zaidi, waliamini tu kuwa Masiha angekuja, ilhali hawakutafuta ukweli wa uzima. Na hivyo, hata leo bado wanamngoja Masiha, kwani hawana maarifa ya njia ya uzima, na hawajui ukweli ni nini. Ni vipi, hebu nielezeni, watu wapumbavu, wakaidi na washenzi kama hawa wangeweza kupata baraka za Mungu? Wangewezaje kumwona Masiha? Walimpinga Yesu kwa sababu hawakujua mwelekeo wa kazi ya Roho Mtakatifu, kwa sababu hawakuijua njia ya ukweli uliozungumziwa na Yesu, na zaidi, kwa sababu hawakumwelewa Masiha. Na kwa kuwa hawakuwa wamewahi kumwona Masiha na hawakuwa wamewahi kuwa pamoja na Masiha, walifanya kosa la kuning’inia bila mafanikio kwa jina la Masiha huku wakipinga dutu ya Masiha kwa kila njia iwezekanayo. Mafarisayo hawa kwa dutu walikuwa wakaidi, wenye kiburi na hawakutii ukweli. Kanuni ya imani yao kwa Mungu ni: Haijalishi mahubiri Yako ni makubwa vipi, haijalishi mamlaka Yako ni makubwa vipi, Wewe si Kristo iwapo Huitwi Masiha. Je, maoni haya si ya upuuzi na ya kudhihaki? Nawauliza tena: Je, si rahisi sana kwenu kufanya makosa ya Mafarisayo wa kwanza kabisa kwa kuwa hamna ufahamu hata kidogo kumhusu Yesu? Je, unaweza kuitambua njia ya ukweli? Je, unaweza kutoa uhakika kweli kuwa hutampinga Kristo? Je, una uwezo wa kuifuata kazi ya Roho Mtakatifu? Kama hujui iwapo utampinga Kristo, basi Nasema kuwa tayari unaishi kwenye ukingo wa kifo. Wale wote ambao hawakumfahamu Masiha walikuwa na uwezo wa kumpinga Yesu, wa kumkataa Yesu, wa kumpaka Yeye tope. Watu wote wasiomwelewa Yesu wako na uwezo wa kumkana, na kumtusi. Zaidi, wako na uwezo wa kuona kurejea kwa Yesu kama uwongo wa Shetani, na watu zaidi watamshutumu Yesu aliyerudi kwa mwili. Je, haya yote hayawafanyi muogope? Mtakachokumbana nacho kitakuwa kumkufuru Roho Mtakatifu, kuharibiwa kwa maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa, na kukataliwa kwa dharau ya yale yote ambayo yamedhihirishwa na Yesu. Mnaweza kupata nini kutoka kwa Yesu kama mmetatizwa kwa namna hii? Mtaielewaje kazi ya Yesu atakaporudi kwa mwili kwa wingu jeupe, kama mnakataa katakata kuona makosa yenu? Nawaambieni hili: Watu wasioukubali ukweli, ilhali wanangoja kufika kwa Yesu juu ya wingu jeupe kwa upofu, kwa hakika watamkufuru Roho Mtakatifu, na ni kundi ambalo litaangamizwa. Mnatamani tu neema ya Yesu, na kutaka tu kufurahia ulimwengu wa mbinguni wenye raha, ilhali hamjawahi kutii maneno yaliyonenwa na Yesu, na hamjawahi kupokea ukweli ulioonyeshwa na Yesu anaporudi katika mwili. Mtashikilia nini badala ya ukweli wa kurejea kwa Yesu juu ya wingu jeupe? Je, ni ukweli ambao ndani yake mnashinda mkitenda dhambi, na kisha kuzikiri, tena na tena? Mtatoa nini kama kafara kwa Yesu Anayerejea juu ya wingu jeupe? Je, ni miaka ya kazi ambayo mnajiinua nayo? Ni nini mtakachoinua kumfanya Yesu Anayerejea kuwaamini? Je, ni hiyo asili yenu ya kiburi, ambayo haitii ukweli wowote?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kufikia Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu, Mungu Atakuwa Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia

Chanzo cha upinzani wa mwanadamu na uasi dhidi ya Mungu ni kupotoshwa kwake na Shetani. Kwa sababu amepotoshwa na Shetani, dhamiri ya mwanadamu imekuwa bila hisia, yeye ni mwovu, mawazo yake yamepotoka, na ana mtazamo duni. Kabla ya kupotoshwa na Shetani, mwanadamu kawaida alimfuata Mungu na alitii maneno Yake baada ya kuyasikia. Alikuwa kawaida mwenye akili timamu na dhamiri, na wa ubinadamu wa kawaida. Baada ya kupotoshwa na Shetani, hali yake ya awali, dhamiri, na ubinadamu vilidhoofika sana na viliharibiwa na shetani. Hivyo, yeye amepoteza utii wake na upendo kwa Mungu. Akili ya mwanadamu imekuwa potovu, tabia yake imekuwa sawa na ile ya mnyama, na uasi wake kwa Mungu kabisa umekuwa wa mara kwa mara na wa kuhuzunisha zaidi. Hata hivyo mwanadamu bado hajui wala kutambua hili, na kwa upofu anapinga na kuasi. Ufunuo wa tabia ya mwanadamu ni udhihirisho wa hisia zake, utambuzi na dhamiri, na kwa sababu hisia yake na utambuzi si timamu, na dhamiri yake imezidi kuwa ndogo zaidi, hivyo tabia yake ni ya uasi dhidi ya Mungu. …

Chanzo cha ufunuo wa upotovu wa tabia ya mwanadamu ni dhamiri yake iliyofifia, asili yake mbovu na akili yake isiyo timamu; kama dhamiri ya mwanadamu na hisia vinaweza kurudi kawaida, basi atafaa kwa matumizi mbele za Mungu. Ni kwa sababu tu kuwa dhamiri ya mwanadamu daima imekuwa isiyosikia, akili ya mwanadamu haijawahi kuwa timamu, na inazidi kuwa hafifu ndio mwanadamu amezidisha uasi wake kwa Mungu, hata akamsulubisha Yesu msalabani na kumkataa Mungu mwenye mwili wa siku za mwisho kuingia katika nyumba yake, na analaani mwili wa Mungu, na anaona mwili wa Mungu kuwa wa hali ya chini. Ikiwa mwanadamu angekuwa na ubinadamu hata kidogo tu, hangekuwa mkatili sana katika kuutendea mwili wa Mungu mwenye mwili; kama angekuwa na akili hata kidogo tu, hangekuwa mkatili sana katika kuutendea mwili wa Mungu mwenye mwili; kama angekuwa na dhamiri hata kidogo tu, hangekuwa na “shukrani” sana kwa Mungu mwenye mwili kwa njia hii. Mwanadamu anaishi katika enzi ya Mungu kuwa mwili, ilhali hana uwezo wa kumshukuru Mungu kwa kumpa nafasi hiyo nzuri, na badala yake analaani ujio wa Mungu, au anapuuza kabisa ukweli wa kupata mwili kwa Mungu, na anaonekana kuupinga na anachoshwa nao. Haijalishi jinsi mwanadamu anachukulia kuja kwa Mungu, Mungu, kwa ufupi, daima ameendeleza kazi yake kwa uvumilivu—hata kama mwanadamu hajawahi kumkaribisha, na bila kujua yeye hufanya maombi kwa Mungu. Tabia ya mwanadamu imekuwa mbaya zaidi, akili yake imekuwa hafifu zaidi, na dhamiri yake imekanyagwa kabisa na yule muovu na kwa muda mrefu imekoma kuwa dhamiri ya awali ya mwanadamu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu

Iliyotangulia: 7. Tofauti Kati Ya Matendo Mazuri ya Nje na Mabadiliko Katika Tabia

Inayofuata: 2. Katika Kutafuta Njia ya Kweli, Lazima Uwe na Mantiki

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp