Sisitiza Uhalisi Zaidi

Kila mtu ana uwezekano wa kukamilishwa na Mungu, kwa hiyo kila mtu anapaswa kuelewa ni huduma gani kwa Mungu ndiyo inayolingana zaidi na makusudi Yake. Watu wengi hawajui kumwamini Mungu humaanisha nini na hawajui kwa nini wanapaswa kumwamini Yeye—yaani, wengi zaidi hawana ufahamu wa kazi ya Mungu au lengo la mpango Wake wa usimamizi. Leo, watu wengi zaidi bado wanadhani kumwamini Mungu kunahusu kwenda mbinguni na roho zao kuokolewa. Bado hawajui chochote kuhusu umuhimu mahususi wa kumwamini Mungu, na aidha hawana ufahamu wowote wa kazi muhimu kabisa ya Mungu katika mpango Wake wa usimamizi. Kwa sababu zao mbali mbali za kibinafsi, watu hawavutiwi kabisa na kazi ya Mungu wala hawatafakari juu ya makusudi ya Mungu au mpango wa Mungu wa usimamizi. Kama mtu binafsi katika mkondo huu, kila mtu anapaswa kujua lengo la mpango mzima wa usimamizi wa Mungu ni nini, ukweli ambao Mungu tayari ametimiza, kwa nini Amelichagua kundi hili la watu, malengo na umuhimu wa Yeye kuwachagua ni upi, na kile ambacho Anataka kufanikisha katika kundi hili. Mungu kuweza kuliinua kundi kama hilo la watu wasiofika katika nchi ya joka kubwa jekundu na kuweza kuendelea kufanya kazi hadi sasa, Akijaribu na kuwakamilisha kwa kila namna, Akizungumza maneno yasiyohesabika, Akitekeleza kazi kubwa na kutuma vitu vingi vya kuhudumu—kwa Mungu pekee kuweza kukamilisha kazi kubwa kama hiyo inaonyesha jinsi kazi Yake ilivyo muhimu. Kwa sasa, huna uwezo wa kuelewa hili kikamilifu. Hivyo, ni sharti msiichukulie kazi ambayo Mungu amefanya ndani yenu kama jambo dogo; hili si jambo dogo. Hata kile ambacho Mungu amewafichulia leo kinawatosha kujaribu kutafakari na kujua. Mkielewa tu kwa kweli na kwa kina ndipo matukio yenu yatakuwa ya kina na maisha yenu yatakua. Leo, watu wanaelewa na kufanya kidogo sana; hawana uwezo wa kutimiza makusudi ya Mungu kikamilifu. Huu ni upungufu wa wanadamu na kushindwa kwao kutimiza wajibu wao, hivyo, hawawezi kutimiza matokeo yanayotarajiwa. Roho Mtakatifu hana njia ya kufanya kazi ndani ya watu wengi kwa sababu wana ufahamu wa juu juu wa kazi ya Mungu na hawako tayari kuichukulia kazi ya nyumba ya Mungu kama kitu fulani cha thamani wanapoifanya. Siku zote wanafanya vitu kwa namna isiyo ya dhati ili wapate kuishi tu, au vinginevyo kuiga kile ambacho watu wengi zaidi wanafanya, au kufanya kazi tu kwa ajili ya maonyesho. Leo, kila mtu katika mkondo huu anapaswa kukumbuka iwapo katika matendo na vitendo vyake, kile ambacho amefanya kila ambacho angeweza kufanya, na iwapo ametia bidii zake zote. Watu wameshindwa kabisa kutimiza wajibu wao, si kwa sababu Roho Mtakatifu hafanyi kazi Yake bali kwa sababu watu hawafanyi kazi yao, wakifanya isiwezekane kwa Roho Mtakatifu kufanya kazi Yake. Mungu hana maneno zaidi ya kunena, lakini watu hawajaenda kwa kasi sawa kabisa, na wamebaki nyuma kabisa, hawawezi kukaa karibu na kila hatua, hawawezi kuzifuata nyayo za Mwanakondoo kwa karibu. Kile ambacho walipaswa kukitii hawajakitii; kile ambacho walipaswa kukitenda hawajakitenda; kile ambacho walipaswa kukiomba hawajakiomba; kile ambacho walipaswa kukiacha hawajakiacha. Bado hawajafanya kitu chochote kati ya hivi. Kwa hiyo, mazungumzo haya ya kuhudhuria karamu ni maneno matupu; hayana maana yoyote halisi na yote yamo katika fikira zao. Ikitazamwa kutoka leo, inaweza kusemwa kwamba hadi sasa watu hawajatimiza wajibu wao hata kidogo. Kila kitu kinategemea Mungu kufanya na kusema vitu Yeye Mwenyewe. Kazi ya mwanadamu kwa kweli imekuwa ndogo sana; watu ni taka isiyokuwa na maana ambao hawana uwezo wa kushirikiana na Mungu. Mungu amenena mamia ya maelfu ya maneno, lakini watu hawajayaweka katika vitendo kabisa—iwe ni kuukana mwili, kuacha dhana, kuwa watiifu kwa Mungu katika mambo yote huku ukikukuza ufahamu na kupata umaizi, kutowapa watu nafasi mioyoni mwao, kuondoa sanamu ambazo zinamiliki mioyo yao, kuasi dhidi ya makusudi yao binafsi ambayo si sahihi, kutotenda kwa msingi wa mihemko yao, kufanya mambo kwa haki na bila ubaguzi, kuyafikiria zaidi masilahi ya Mungu na ushawishi wao kwa wengine wanapozungumza, kufanya mambo zaidi yanayonufaisha kazi ya Mungu, kufikiri kuhusu kuinufaisha nyumba ya Mungu katika yote wanayofanya, kutoruhusu mihemko yao ziiamuru tabia yao, kuacha yale ambayo yanapendeza miili yao wenyewe, kuondoa maoni ya zamani ya ubinafsi, na kadhalika. Kwa kweli watu wanafahamu baadhi ya mahitaji haya ambayo Mungu anahitaji kutoka kwa mwanadamu, lakini hawako tayari kuyaweka katika vitendo. Ni kwa namna gani nyingine ambayo Mungu anaweza kufanya kazi na kuwashawishi? Waasi machoni pa Mungu wanawezaje bado kuwa na ujasiri wa kuchukua maneno Yake na kuyastahi? Wanawezaje kuwa na ujasiri wa kula chakula cha Mungu? Dhamiri ya watu ipo wapi? Hawajatimiza wajibu mdogo kabisa waliopaswa kutimiza, sembuse kufanya yote wawezayo. Je, wao si watu wa njozi tu? Hakuwezi kuwa na mazungumzo ya uhalisi bila matendo. Huo ni ukweli wa wazi!

Mnapaswa kuwa mkijifunza mafunzo yaliyo ya uhalisi zaidi. Hakuna haja ya hayo mazungumzo matupu, yenye kuvutia na ambayo watu wanayastahi. Linapokuja suala la kuzungumza kuhusu maarifa, ya kila mtu ni ya juu kuliko ya aliyetangulia, lakini bado hawana njia ya kutenda. Ni watu wangapi wameelewa kanuni za kutenda? Ni wangapi wamejifunza mafunzo halisi? Ni nani anayeweza kufanya ushirika kuhusu uhalisi? Kuweza kuzungumza juu ya maarifa ya maneno ya Mungu si sawa na kimo chako halisi. Hilo linaishia kuonyesha tu kuwa ulizaliwa ukiwa na akili, kwamba wewe una kipaji. Ikiwa huwezi kuionyesha njia, basi matokeo yatakuwa bure, na wewe utakuwa taka isiyo na maana! Je, hujifanyi tu ikiwa huwezi kusema chochote kuhusu njia halisi ya kufanya vitendo? Je, hujifanyi ikiwa huwezi kutoa uzoefu wako mwenyewe halisi kwa wengine, na hivyo kuwapa mafunzo ambayo wanaweza kujifunza kwayo au njia ya kufanya vitendo? Je, wewe si bandia tu? Una thamani gani? Mtu kama huyo angeweza tu kushikilia sehemu ya kuwa “mvumbuzi wa nadharia ya ujamaa,” na si “mchangiaji wa kuleta ujamaa.” Kutokuwa na uhalisi ni kutokuwa na ukweli. Kutokuwa na uhalisi ni kutokuwa na thamani. Kutokuwa na uhalisi ni kukosa uhai. Kutokuwa na uhalisi ni “kuwa na fikira za Umaksi na Ulenini,” bila thamani kama marejeo. Ninamsihi kila mtu kufunga mdomo kuhusu nadharia na kuzungumzia kitu ambacho ni halisi, kitu ambacho ni cha kweli na thabiti, kujifunza baadhi ya “sanaa za kisasa,” kusema kitu ambacho ni halisi, kuchangia uhalisi kiasi, na kuwa na roho ya kujitoa. Uukabili uhalisi unapozungumza; usijiingize katika mazungumzo yasiyokuwa na uhalisi na yaliyotiwa chumvi ili kuwafurahisha watu au wakae na kukustahi. Thamani yake ni nini? Kuna maana gani katika kuwafanya watu kukutendea kwa ukunjufu? Kuwa “stadi” kiasi katika usemi wako, tenda haki zaidi kiasi katika matendo yako, kuwa mwenye busara zaidi kiasi katika jinsi unavyoshughulikia vitu, kuwa mwenye vitendo zaidi kiasi katika kile unachosema, fikiri kuhusu kuleta manufaa kwa nyumba ya Mungu katika kila tendo, acha dhamiri yako unapokuwa na muhemuko, usilipize wema kwa chuki, au kutokuwa na shukrani kwa wema, na usiwe mnafiki, usije ukawa na “ushawishi mbaya.” Unapokula na kunywa maneno ya Mungu, yahusishe zaidi na uhalisi, na unapowasiliana, zungumza zaidi kuhusu mambo ya uhalisi. Usijikweze; Mungu hataridhishwa na hilo. Katika miingiliano yako na wengine, kuwa mstahimilivu zaidi, fanya mazoezi zaidi ya kukubali, kuwa mkarimu zaidi kiasi, na ujifunze kutoka kwa “roho ya waziri mkuu.”[a] Unapokuwa na mawazo ambayo si mazuri, fanya mazoezi zaidi ya kuukana mwili zaidi. Unapofanya kazi, zungumza zaidi kuhusu njia halisi na usiwe na majivuno sana, vinginevyo kile unachosema hakitaweza kufikiwa na watu. Starehe kidogo, mchango zaidi—onyesha roho yako ya kujitolea isiyo ya ubinafsi. Fikirieni zaidi makusudi ya Mungu, sikilizeni dhamiri zenu zaidi, kuweni wenye kuzingatia zaidi, na msisahau jinsi ambavyo Mungu huwanenea kila siku kwa uvumilivu na kwa dhati. Soma “shajara ya mwaka ya zamani” mara kwa mara. Omba zaidi na ufanye ushirika mara kwa mara. Usiendelee kuwa mtu aliyekanganyikiwa sana, bali onyesha busara zaidi na upate umaizi fulani. Mkono wa dhambi unaponyooka, urudishe nyuma na usiuache utandae zaidi. Haina maana! Mnachokipata kutoka kwa Mungu si chochote bali laana; kuweni waangalifu. Acheni mioyo yenu iwe na huruma kwa wengine na siku zote msiwapige kwa silaha mkononi. Shirikini zaidi kuhusu maarifa ya ukweli na mzungumze zaidi kuhusu maisha, mkiwa na roho ya kuwasaidia wengine. Tendeni zaidi na kusema kidogo. Tieni mengi zaidi katika vitendo na kidogo katika utafiti na uchambuzi. Acheni mguswe zaidi na Roho Mtakatifu, na mpeni Mungu fursa zaidi ya kuwakamilisha. Ondoeni sifa zaidi za kibinadamu; bado mna sifa nyingi za kibinadamu za kufanya mambo na matendo na namna yenu ya juujuu ya kufanya bado ni ya kuwachukiza wengine: Ziondoeni hizi zaidi. Hali zenu za akili bado zinachukiza sana; tumieni muda zaidi kuzirekebisha. Bado mnawapa watu hadhi kuu; mpeni Mungu hadhi zaidi, na usiwe mtu usiyekuwa na akili. “Hekalu” limekuwa la Mungu daima na halipaswi kutwaliwa na watu. Kwa ufupi, sisitiza zaidi juu ya haki na kidogo katika mihemuko. Ni bora zaidi kuuondoa mwili. Zungumza zaidi kuhusu uhalisi na kidogo kuhusu maarifa; kilicho bora zaidi kuwa kimya na kutosema lolote. Zungumza zaidi juu ya njia ya kutenda na ufanyemajivuno kidogo zaidi yasiyo na thamani. Itakuwa bora zaidi kuanza kutenda sasa.

Matakwa ya Mungu kwa watu si ya juu sana. Ikiwa watu wataweka hata jitihada kidogo wataweza kupata “alama ya kupita.” Kwa kweli, kufahamu, kujua, na kuelewa ukweli kunatatiza sana kuliko kuutenda ukweli; kuujua na kuutambua ukweli kunakuja baada ya kuutenda ukweli; hizi ndizo hatua na njia ambayo kwayo Roho Mtakatifu hufanya kazi. Unawezaje kutotii? Je, unaweza kupata kazi ya Roho Mtakatifu kwa kufanya mambo kwa namna yako? Je, Roho Mtakatifu hufanya kazi kwa kuzingatia ridhaa yako, au kwa msingi wa kasoro zako kulingana na maneno ya Mungu? Haina maana ikiwa huwezi kuliona hili kwa uwazi. Kwa nini watu wengi zaidi wametumia jitihada nyingi kusoma maneno ya Mungu lakini wana maarifa tu na hawawezi kusema kitu chochote kuhusu njia halisi baada ya hapo? Unadhani kwamba kuwa na maarifa ni sawa na kuwa na ukweli? Je, huo si mtazamo uliokanganywa? Unaweza kuzungumza maarifa mengi kama mchanga ulivyo ufuoni, lakini hakuna yaliyo na njia ya kweli. Je, wewe hujaribu kuwapumbaza watu kwa kufanya hivi? Je, unafanya maonyesho matupu, bila dutu ya kuyasitiri? Mienendo yote kama hii ni ya madhara kwa watu! Kadiri nadharia inavyokuwa ya juu, ndivyo inavyokosa uhalisi zaidi, na ndivyo inavyokosa zaidi uwezo wa kuwapeleka watu katika uhalisi; kadiri nadharia inavyokuwa ya juu, ndivyo inavyokufanya umuasi na kumpinga Mungu. Usizichukulie nadharia za kiwango cha juu kama hazina ya thamani; zina madhara, na hazina kazi yoyote! Pengine baadhi ya watu wanaweza kuzungumza juu ya nadharia za juu sana—lakini nadharia hizo hazina kitu chochote cha uhalisi, maana watu hawajazipitia wao binafsi, na kwa hiyo hawana njia ya kutenda. Watu kama hao hawawezi kuwaongoza wengine katika njia sahihi, na watawapotosha. Je, hili halileti madhara kwa watu? Angalau kabisa, unapaswa kuweza kutatua shida za sasa za watu na kuwaruhusu kupata kuingia; hii tu ndiyo inachukuliwa kama ibada, na baada ya hapo ndipo utakuwa na sifa za kufaa kumfanyia Mungu kazi. Siku zote usizungumze maneno ya kifahari, ya ajabu, na usiwalazimishe watu kukutii wewe pamoja na vitendo vyako visivyofaa. Kufanya hivyo hakutaleta matokeo, na kunaweza kuongeza tu mkanganyiko wa watu. Kuendelea kwa namna hii kutazalisha mafundisho mengi, ambazo zitawafanya watu wakuchukie. Hivyo ndivyo ulivyo udhaifu wa mwanadamu, na kwa kweli unadhalilisha. Kwa hivyo, zungumza zaidi juu ya matatizo ambayo yapo kwa kweli. Usiyachukulie matukio ya watu wengine kama mali yako binafsi na kuyaonyesha waziwazi ili wengine wastahi; unapaswa kutafuta suluhisho lako binafsi mwenyewe. Hiki ndicho ambacho kila mtu anapaswa kuweka katika vitendo.

Ikiwa kile unachoshiriki kinaweza kuwapa watu njia ya kufuata, basi hiyo ni sawa na wewe kuwa na uhalisi. Haijalishi kile unachosema, ni lazima uwalete watu katika vitendo na kuwapatia njia wanayoweza kuifuata. Usiwaruhu tu wapate maarifa; lililo muhimu zaidi ni kuwa na njia ya kufuata. Ili watu wamwamini Mungu, lazima waitembee njia inayoongozwa na Mungu katika kazi Yake. Yaani, mchakato wa kumwamini Mungu ni mchakato wa kuitembea njia inayoongozwa na Roho Mtakatifu. Vivyo hivyo, unapaswa kuwa na njia ambayo unaweza kuitembea kwa vyovyote vile, na unapaswa kuenenda kwenye njia ya kukamilishwa na Mungu. Usibaki nyuma sana, na usijishughulishe na mambo mengi sana. Ikiwa tu unaitembea njia inayoongozwa na Mungu bila kusababisha mwingiliano ndipo unaweza kupokea kazi ya Roho Mtakatifu na kuwa na njia ya kuingia. Hili tu ndilo linahesabika kama lenye kufaa makusudi ya Mungu na kutimiza wajibu wa binadamu. Kama mtu binafsi katika mkondo huu, kila mtu anapaswa kutimiza wajibu wake kikamilifu, fanya zaidi yale ambayo watu wanapaswa kuyafanya, na usitende kwa ukaidi. Watu wanaotekeleza kazi wanapaswa kuweka maneno yao wazi, watu wanaofuata wanapaswa kusisitiza zaidi kuhimili ugumu na kutii, na kila mtu anapaswa kutunza nafasi yake na kutotenda kwa namna isiyofaa. Linapaswa lieleweke wazi katika moyo wa kila mtu namna ambavyo wanapaswa kutenda na ni kazi gani wanapaswa kutimiza. Chukua njia inayoongozwa na Roho Mtakatifu; usipotoke au kukosea. Lazima muione kazi ya leo waziwazi. Kuingia katika njia ya leo ya kufanya kazi ndicho kitu mnachopaswa kutenda. Ni kitu cha kwanza mnachopaswa kuingia. Msipoteze maneno yoyote zaidi kwenye mambo mengine. Kufanya kazi ya nyumba ya Mungu leo ni jukumu lenu, kuingia katika mbinu ya kazi ya leo ni wajibu wenu, na kutenda ukweli wa leo ni mzigo wenu.

Tanbihi:

a. Roho ya waziri mkuu: Ni msemo wa jadi wa Kichina ambao hutumika kuelezea mtu ambaye ni mkarimu na anayekubali mawazo ya wengine.

Iliyotangulia: Uhusiano Wako na Mungu Ukoje?

Inayofuata: Kuzishika Amri na Kuutenda Ukweli

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp