Uhusiano Wako na Mungu Ukoje?
Katika kumwamini Mungu, angalau kabisa lazima utatue suala la kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu. Ikiwa huna uhusiano wa kawaida na Mungu, basi maana ya imani yako katika Mungu inapotea. Kuanzisha uhusiano wa kawaida na Mungu kunafikiwa kabisa kupitia kuutuliza moyo wako mbele za Mungu. Kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu kunamaanisha kuwa na uwezo wa kutokuwa na shaka wala kuikana kazi Yake yoyote na kuweza kutii kazi Yake. Kunamaanisha kuwa na nia sahihi mbele za Mungu na kutofanya mipango kwa ajili yako mwenyewe, na pia kunamaanisha kutanguliza masilahi ya nyumba ya Mungu, kukubali uchunguzi wa Mungu, na kutii mipango Yake, bila kujali kile unachofanya. Lazima uweze kuutuliza moyo wako mbele za Mungu katika yote unayofanya. Hata kama huelewi nia za Mungu, bado lazima utimize wajibu na majukumu yako kwa uwezo wako wote. Mara tu nia za Mungu zinapodhihirishwa kwako, tenda kulingana nazo, na haitakuwa imechelewa mno. Uhusiano wako na Mungu unapokuwa wa kawaida, basi pia utakuwa na mahusiano ya kawaida na watu. Ili kujenga uhusiano wa kawaida na Mungu, yote lazima yajengwe juu ya msingi wa maneno ya Mungu, lazima uweze kufanya wajibu wako kulingana na maneno ya Mungu na kile Mungu anachotaka, lazima uweke mitazamo yako sawa, lazima utafute ukweli katika mambo yote, na lazima utende ukweli unapouelewa. Bila kujali kile kinachokutendekea, lazima umwombe Mungu na utafute kwa moyo wa utii kwa Mungu. Ukitenda hivi, utaweza kudumisha uhusiano wa kawaida na Mungu. Wakati huohuo unapotimiza wajibu wako ipasavyo, lazima pia uhakikishe kwamba hufanyi chochote ambacho hakina manufaa kwa ajili ya kuingia katika uzima kwa watu wateule wa Mungu, na husemi chochote ambacho hakiwajengi ndugu na dada. Kama kiwango cha chini kabisa, lazima usifanye chochote kinachokwenda kinyume na dhamiri yako, na lazima usifanye kabisa jambo lolote la aibu. Hasa, lazima usifanye kabisa jambo linalomwasi wala kumpinga Mungu, wala jambo lolote linalosumbua kazi au maisha ya kanisa. Uwe wazi na mnyoofu katika kila kitu unachofanya na uhakikishe kwamba kila kitendo chako kinaweza kuwekwa mbele za Mungu. Ingawa mwili unaweza kuwa dhaifu wakati mwingine, lazima uweze kutanguliza masilahi ya nyumba ya Mungu, bila tamaa ya faida ya kibinafsi, bila kufanya chochote cha binafsi na chenye kudharauliwa, ukijitafakari mara kwa mara. Kwa namna hii, utaweza kuishi mbele za Mungu mara kwa mara, na uhusiano wako na Mungu utakuwa wa kawaida kabisa.
Katika kila kitu unachofanya, lazima uchunguze iwapo nia zako ni sahihi. Ikiwa unaweza kutenda kulingana na matakwa ya Mungu, basi uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida. Hiki ndicho kiwango cha chini kabisa. Ikiwa, kupitia kuchunguza nia zako, unagundua kwamba umekuza nia zisizo sahihi, na unaweza kuasi dhidi ya nia hizo na kutenda kulingana na maneno ya Mungu, basi utakuwa mtu sahihi mbele za Mungu. Hili linaonyesha kwamba uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida, na kwamba yote unayofanya ni kwa ajili ya Mungu, si kwa ajili yako mwenyewe. Katika yote unayofanya na yote unayosema, uweze kuuweka moyo wako sawa na uwe mwenye haki katika matendo yako, na usiongozwe na hisia zako wala mapenzi yako mwenyewe unapotenda. Hizi ni kanuni ambazo waumini wa Mungu lazima wafuate katika matendo yao. Hata jambo dogo linaweza kufunua nia na kimo cha mtu, na hivyo, ili mtu aingie katika njia ya kufanywa kuwa mtimilifu na Mungu, lazima kwanza ashughulikie nia zake na uhusiano wake na Mungu. Ni wakati tu uhusiano wako na Mungu unapokuwa wa kawaida ndipo unaweza kufanywa kuwa mtimilifu na Yeye; ni hapo tu ndipo upogoaji, adabu, na usafishaji wa Mungu unaweza kufikia matokeo yaliyokusudiwa ndani yako. Yaani, ikiwa binadamu wanaweza kumweka Mungu mioyoni mwao na hawafuatilii faida ya kibinafsi wala hawafikirii matarajio yao wenyewe (yaani, kwa mwili wao), lakini badala yake wanaubeba mzigo kwa ajili ya kuingia katika uzima, wanafanya wawezavyo kufuatilia ukweli, na wanatii kazi ya Mungu—ikiwa unaweza kufanya hivi, basi malengo unayofuatilia yatakuwa sahihi, na uhusiano wako na Mungu utakuwa wa kawaida. Inaweza kusemwa kwamba kuuweka uhusiano wa mtu na Mungu sahihi ni hatua ya kwanza ya kuingia katika safari yake ya kiroho. Ingawa majaliwa ya mwanadamu yako mikononi mwa Mungu na yameamuliwa kabla na Mungu, na hayawezi kubadilishwa na mwanadamu, iwapo unaweza kufanywa kuwa mtimilifu na Mungu au kupatwa na Yeye kunategemea iwapo uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida. Huenda kuna sehemu fulani ndani yako zilizo dhaifu au zenye uasi—lakini mradi tu mitazamo yako na nia zako ni sahihi, na mradi tu uhusiano wako na Mungu ni sahihi na ni wa kawaida, basi una sifa za kufanywa kuwa mtimilifu na Mungu. Ikiwa huna uhusiano sahihi na Mungu, na unatenda kwa ajili ya mwili au familia yako, basi haijalishi unafanya kazi kwa bidii kiasi gani, yote yatakuwa bure. Ikiwa uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida, basi kila kitu kingine kitakuwa sawa. Mungu haangalii kitu kingine chochote, bali huangalia tu iwapo mitazamo yako katika imani yako katika Mungu ni sahihi: hatimaye, unamwamini nani, unaamini kwa ajili ya nani, na kwa nini unaamini. Ikiwa unaweza kuona mambo haya waziwazi na kutenda ukiwa na mitazamo yako iliyonyooka, basi utafanya maendeleo katika maisha yako, na pia utahakikishiwa kuingia katika njia sahihi. Ikiwa uhusiano wako na Mungu si wa kawaida, na mitazamo ya imani yako kwa Mungu imekengeuka, basi mambo mengine yote ni ya bure, na haijalishi unatendaje imani yako, hutapata chochote. Ni baada tu ya uhusiano wako na Mungu kuwa wa kawaida ndipo utakapopata kibali Chake unapoasi dhidi ya mwili, unapoomba, unapoteseka, unapovumilia, unapotii, unapowasaidia ndugu na dada zako, unapojitumia zaidi kwa ajili ya Mungu, na kadhalika. Kama kile unachofanya kina thamani na maana kunategemea ikiwa nia zako ni sahihi na mitazamo yako ni sahihi. Siku hizi, watu wengi wanamwamini Mungu kana kwamba walikuwa wanainamisha shingo zao ili watazame saa—mitazamo yao imepotoka, na kile wanachohitaji kufanya ni kulishinda jambo hili. Ikiwa tatizo hili litatatuliwa, kila kitu kitakuwa sawa; la sivyo, kila kitu kitakuwa bure. Watu wengine hujiendesha vyema mbele Yangu, lakini nyuma Yangu, kile wanachofanya ni kunipinga Mimi. Hili ni dhihirisho la upotovu na udanganyifu, na mtu wa aina hii ni mtumishi wa Shetani; yeye ni mfano halisi wa Shetani, aliyekuja kumshawishi Mungu. Wewe ni mtu sahihi tu ikiwa unaweza kutii kazi Yangu na maneno Yangu. Mradi tu unaweza kula na kunywa maneno ya Mungu; mradi tu kila kitu unachofanya kinaweza kuwekwa mbele za Mungu na unajiendesha kwa namna ya wazi na unyoofu katika kila jambo unalofanya; mradi tu hufanyi mambo ya aibu, wala mambo ambayo yangedhuru uzima wa wengine; na mradi tu unaishi katika nuru na hujiruhusu kutumiwa na Shetani, basi uhusiano wako na Mungu umewekwa katika utaratibu upasao.
Kumwamini Mungu kunakuhitaji uweke nia na mitazamo yako sahihi; Lazima uwe na ufahamu sahihi na namna sahihi ya kushughulikia maneno ya Mungu, kazi ya Mungu, mazingira yote ambayo Mungu huandaa, mwanadamu ambaye Mungu anamshuhudia, na Mungu wa vitendo. Hupaswi kutenda kulingana na mawazo yako mwenyewe wala kupanga hila zako ndogo ndogo. Chochote unachofanya, lazima uweze kuutafuta ukweli na, katika nafasi yako kama kiumbe aliyeumbwa, kutii kazi yote ya Mungu. Ukitamani kufuatilia kufanywa kuwa mtimilifu na Mungu na kuingia katika njia sahihi ya uzima, basi moyo wako lazima daima uishi mbele za Mungu. Usiwe mtu asiye na nidhamu, usimfuate Shetani, usimpe Shetani fursa zozote za kutekeleza kazi yake, na usimruhusu Shetani akutumie. Lazima ujitoe kwa Mungu kikamilifu na umwache Mungu akutawale.
Je, uko tayari kuwa mtumishi wa Shetani? Je, uko tayari kutumiwa na Shetani? Je, unamwamini Mungu na unamfuatilia Yeye ili kwamba uweze kufanywa kuwa mtimilifu na Yeye, au ili kwamba uweze kuwa foili kwa ajili ya kazi ya Mungu? Katika maisha haya, je, uko tayari kupatwa na Mungu na uishi maisha yenye maana, au afadhali uishi maisha yasiyo na thamani na yaliyo matupu? Je, ungependelea kutumiwa na Mungu, au kutumiwa na Shetani? Je, ungependelea kuruhusu maneno ya Mungu na ukweli vikujaze, au kuruhusu dhambi ikujaze na Shetani akujaze? Yafikirie mambo haya kwa uangalifu. Katika maisha yako ya kila siku, lazima uelewe ni maneno yapi unayosema na ni mambo yapi unayofanya ambayo yanaweza kusababisha hali isiyo ya kawaida katika uhusiano wako na Mungu, na kisha ujirekebishe ili uingie katika namna sahihi. Wakati wote, chunguza maneno yako, matendo yako, kila hatua yako, na fikira na mawazo yako yote. Pata ufahamu upasao wa hali yako halisi na uingie katika namna ya kazi ya Roho Mtakatifu. Hii ndiyo njia pekee ya kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu. Kwa kutathmini iwapo uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida, utaweza kusahihisha nia zako, kuelewa kiini cha asili cha mwanadamu, na kujielewa kweli, na, kwa kufanya hivyo, utaweza kuingia katika uzoefu halisi, kujiasi kwa namna halisi, na kutii kwa nia. Unapopitia mambo haya yanayohusu iwapo uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida au la, utapata fursa za kufanywa kuwa mtimilifu na Mungu na utaweza kuelewa hali nyingi za kazi ya Roho Mtakatifu. Pia utaweza kung’amua hila nyingi za Shetani na kufichua njama zake. Njia hii pekee ndiyo inayoongoza katika kufanywa kuwa mtimilifu na Mungu. Uweke uhusiano wako na Mungu sahihi, ili uweze kutii mipango Yake yote, na ili uweze kuingia kwa kina zaidi katika uzoefu halisi na upokee kazi zaidi ya Roho Mtakatifu. Unapotenda kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu, katika hali nyingi, mafanikio yatafikiwa kwa kuasi dhidi ya mwili na kupitia ushirikiano wa kweli na Mungu. Unapaswa kuelewa kwamba “bila moyo wa ushirikiano, ni vigumu kupokea kazi ya Mungu; ikiwa mwili hauteseki, hakutakuwa na baraka kutoka kwa Mungu; ikiwa roho haipambani, Shetani hataaibishwa.” Ukitenda kanuni hizi na kuzielewa kabisa, mitazamo ya imani yako katika Mungu itawekwa sahihi. Katika utendaji wenu wa sasa, lazima mtupilie mbali fikira ya “kutafuta kula mikate mpaka mshibe”; lazima mtupilie mbali maoni kwamba “kila kitu kinafanywa na Roho Mtakatifu, na watu hawawezi kuingilia kati.” Kila mtu anayesema hivyo hufikiri, “Watu wanaweza kufanya chochote wanachotaka, na wakati utakapofika, Roho Mtakatifu atafanya kazi Yake. Watu hawana haja ya kuuzuia mwili wala kushirikiana; jambo muhimu ni kwamba waguswe na Roho Mtakatifu.” Maoni haya yote ni ya upuuzi. Katika hali kama hizo, Roho Mtakatifu hawezi kufanya kazi. Ni mtazamo wa aina hii ndio ambao unazuia sana kazi ya Roho Mtakatifu. Mara nyingi, kazi ya Roho Mtakatifu hufikiwa kupitia ushirikiano wa mwanadamu. Watu hawashirikiani na hawana azimio, lakini wanatamani kufikia mabadiliko katika tabia yao na wapokee kazi ya Roho Mtakatifu na nuru na mwangaza kutoka kwa Mungu; hizi ni fikira za kupita kiasi. Huku kunaitwa “kujilegeza mwenyewe na kumsamehe Shetani.” Watu kama hao hawana uhusiano wa kawaida na Mungu. Unapaswa kugundua ufunuo na udhihirisho mwingi wa tabia ya kishetani ndani yako mwenyewe na kugundua matendo yoyote uliyo nayo ambayo yanakwenda kinyume na matakwa ya Mungu ya sasa. Je, sasa utaweza kuasi dhidi ya Shetani? Unapaswa kufikia uhusiano wa kawaida na Mungu, kutenda kulingana na nia za Mungu, na kuwa mtu mpya mwenye maisha mapya. Usikae sana kwenye makosa ya zamani; usijute kupita kiasi; uweze kusimama na ushirikiane na Mungu, na utimize wajibu ambao ni wako kutimiza. Kwa namna hii, uhusiano wako na Mungu utakuwa wa kawaida.
Ikiwa baada ya kusoma haya, unadai tu kuyakubali maneno haya, lakini moyo wako unabaki bila kuguswa, na hutafuti kufanya uhusiano wako na Mungu uwe wa kawaida, jambo hili linathibitisha kwamba huweki umuhimu kwenye uhusiano wako na Mungu. Linathibitisha kwamba mitazamo yako bado haijawekwa sahihi, kwamba nia zako bado hazijawekwa katika kupatwa na Mungu na kumletea Yeye utukufu, bali badala yake zimewekwa katika kuruhusu njama za Shetani zishinde na kufikia malengo yako mwenyewe. Watu kama hao wana nia zisizo sahihi na mitazamo isiyo sahihi. Haijalishi Mungu anasema nini au jinsi Anavyosema jambo hilo, watu kama hao hubaki bila kujali kabisa, na hakuna mabadiliko hata kidogo yanayoweza kuonekana ndani yao. Hawaogopi wala hawana aibu. Mtu kama huyo hana roho na amekanganyika kichwa. Kwa kila tamko ambalo Mungu anatoa, mara tu unapokuwa umelisoma na umelielewa, litie katika vitendo. Bila kujali jinsi ulivyojiendesha wakati uliopita, huenda kulikuwa na nyakati ambapo mwili wako ulikuwa dhaifu, au ulikuwa mwasi, au ulipinga; si jambo muhimu sana, na haliwezi kuzuia uzima wako kukomaa leo. Mradi tu unaweza kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu leo, kuna matumaini. Ikiwa kuna mabadiliko ndani yako kila wakati unaposoma maneno ya Mungu, na wengine wanaweza kuona kwamba maisha yako yamebadilika kuwa bora, hili linaonyesha kwamba uhusiano wako na Mungu sasa ni wa kawaida, kwamba umewekwa sahihi. Mungu hawatendei watu kulingana na makosa yao. Mara tu unapoelewa na kufahamu, mradi tu unaweza kuacha kuasi au kupinga, basi Mungu bado atakuwa na rehema juu yako. Unapokuwa na ufahamu huu na azimio la kufuatilia kufanywa kuwa mtimilifu na Mungu, basi hali yako mbele za Mungu itakuwa ya kawaida. Haijalishi unafanya nini, fikiria: Mungu atafikiri nini nikifanya hivi? Je, jambo hili litawanufaisha ndugu zangu? Je, litakuwa na manufaa kwa kazi katika nyumba ya Mungu? Iwe katika maombi, ushirika, usemi, kushughulikia mambo, au katika kuwasiliana na wengine, chunguza nia zako, na uangalie iwapo uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida. Ikiwa huwezi kutambua nia na fikira zako mwenyewe, hili linamaanisha unakosa utambuzi, jambo ambalo linathibitisha kwamba unaelewa ukweli kwa kiwango kidogo sana. Ikiwa unaweza kuelewa waziwazi kila kitu ambacho Mungu hufanya, na unaweza kuona mambo kupitia mtazamo wa maneno Yake, ukisimama upande Wake, basi mitazamo yako itakuwa sahihi. Kwa hivyo, kuanzisha uhusiano mzuri na Mungu ni jambo la muhimu sana kwa mtu yeyote anayemwamini Mungu; kila mtu anapaswa kulichukulia kuwa jukumu la kipaumbele cha juu kabisa na tukio kubwa kabisa katika maisha yake. Pima kila kitu unachofanya kulingana na kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu—ikiwa jambo hilo litakuongoza kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu na nia zako ni sahihi, basi lifanye. Ili kudumisha uhusiano wa kawaida na Mungu, lazima usiogope kupata hasara kwa masilahi yako ya kibinafsi; huwezi kumruhusu Shetani ashinde, huwezi kumruhusu Shetani apate mwanya wa kukudhibiti, na huwezi kumruhusu Shetani akufanye kichekesho. Kuwa na nia kama hizo ni ishara kwamba uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida—si kwa ajili ya mwili, bali kwa ajili ya amani ya roho, kwa ajili ya kuipata kazi ya Roho Mtakatifu, na kwa ajili ya kuridhisha nia za Mungu. Ili kuingia katika hali sahihi, lazima uanzishe uhusiano mzuri na Mungu na uweke sahihi mitazamo ya imani yako katika Mungu. Hii ni ili kwamba Mungu aweze kukupata, na ili kwamba Aweze kudhihirisha matunda ya maneno Yake ndani yako na Akutie nuru na Akuangazie hata zaidi. Kwa namna hii, utakuwa umeingia katika namna sahihi. Endelea kula na kunywa maneno ya Mungu ya leo, ingia katika namna ya wakati wa sasa ya kazi ya Roho Mtakatifu, tenda kulingana na matakwa ya Mungu ya leo, usizingatie mbinu za zamani za kutenda, usishikilie njia za zamani za kufanya mambo, na uingie katika namna ya kufanya kazi ya leo haraka iwezekanavyo. Hivyo, uhusiano wako na Mungu utakuwa wa kawaida kabisa na utakuwa umeanza njia sahihi ya imani katika Mungu.