Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Kondoo wa Mungu Huisikia Sauti ya Mungu

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

Sura ya 6 Aina Mbalimbali za Utofautishaji Ambazo Unafaa Kumiliki katika Kusadiki Kwako kwa Mungu

5. Tofauti Kati Ya Kumfuata Mungu na Kuwafuata Watu.

Maneno Husika ya Mungu:

Kilicho na umuhimu mkuu katika kumfuata Mungu ni kwamba kila kitu kinapaswa kuwa kwa kadri ya maneno halisi ya Mungu: Kama unafuatilia kuingia katika uzima au kutimiza mapenzi ya Mungu, kila kitu kinapaswa kulenga maneno halisi ya Mungu. Kama kile ambacho unawasiliana kwa karibu na kufuatilia hakilengi maneno halisi ya Mungu, basi wewe ni mgeni kwa maneno ya Mungu, na umeondolewa kabisa katika kazi ya Roho Mtakatifu.

kutoka kwa "Jua Kazi Mpya Zaidi ya Mungu na Fuata Nyayo za Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili

Wengine kwa msukumo huamini kuwa palipo na kazi ya Roho Mtakatifu kuna kuonekana kwa Mungu. Ama sivyo watu huamini kuwa palipo na watu mashuhuri wa kiroho ndipo Mungu huonekana. Vinginevyo, wanaamini kuwa palipo na watu wanaojulikana vyema ndipo Mungu huonekana. Kwa sasa tusishauriane ikiwa imani hizi ni sahihi au la. Kujibu swali kama hilo, kwanza ni lazima tuwe wazi kuhusu lengo: tunazitafuta nyayo za Mungu. Hatutafuti viongozi wa kiroho, wala kutafuta watu mashuhuri; tunafuata nyayo za Mungu. Kwa hivyo, kwa kuwa tunatafuta nyayo za Mungu, ni sharti tufuate mapenzi ya Mungu, maneno ya Mungu, matamshi ya Mungu—kwani palipo na maneno mapya ya Mungu, kuna sauti ya Mungu, na palipo na nyayo za Mungu, pana matendo ya Mungu. Palipo na maonyesho ya Mungu pana kuonekana kwa Mungu, na palipo na kuonekana kwa Mungu, pana ukweli, njia na uzima. Ulipokuwa ukitafuta nyayo za Mungu, mliyapuuza maneno haya kuwa "Mungu ndiye ukweli, njia na uzima." Kwa hivyo, watu wengi wakipokea ukweli, hawaamini kuwa wamepata nyayo za Mungu na hata zaidi hawasadiki kuonekana kwa Mungu. Kosa hilo ni kuu kiasi gani?

kutoka kwa "Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya" katika Neno Laonekana katika Mwili

Watu wengi hawapati shangwe ndani ya ukweli, na vile vile katika hukumu. Badala yake, wao hupata furaha kwa nguvu na mali; watu kama hawa huchukuliwa kama wenye madharau. Wanatafuta tu madhehebu yaliyo na ushawishi duniani na wahubiri na waalimu wanaotoka katika seminari. Hata ingawa wameikubali njia ya ukweli, bado wako na shaka ndani yao na hawawezi kujitolea kikamilifu. Wanazungumzia kujinyima kwa sababu ya Mungu, lakini macho yao yamelenga tu wahubiri wakuu na waalimu, na Kristo anasukumwa pembeni. Mioyo yao imejaa umaarufu, mali na utukufu. Hawaamini kamwe kuwa mtu wa kawaida tu anaweza kuwashinda wengi vile, kwamba mtu asiye wa kutambulika kwa macho tu anaweza kukamilisha watu. Hawaamini kuwa hawa watu wasio na sifa, walio kwenye vumbi na vilima vya samadi ni watu waliochaguliwa na Mungu. Wanaamini kuwa kama watu wale wangekuwa vyombo vya wokovu Wake Mungu, basi mbingu na ardhi zitageuzwa juu na chini na watu wote watacheka kupindukia. Wanaamini kuwa iwapo Mungu atawachagua watu wasio na sifa yoyote wafanywe viumbe kamili, basi wao walio na sifa watakuwa Mungu Mwenyewe. Maoni yao yamechafuliwa na kutoamini; hakika, mbali na kutoamini, wao ni wanyama wasio na maana. Kwa maana wao wanathamini tu nyadhifa, hadhi kuu na mamlaka; wanachokithamini sana ni makundi makuu na madhehebu makuu. Hawana heshima hata kidogo kwa wale wanaoongozwa na Kristo; wao ni wasaliti tu waliomgeuka Kristo, kuugeuka ukweli na uhai.

Unachopendezwa nacho sio kujishusha kwa Kristo, ila ni wale wachungaji wa uongo wenye umaarufu. Haupendi wosia au kependeza kwa Kristo, bali unapenda wale wajeuri wanaojihusisha na ulimwengu mchafu. Unauchekelea uchungu wa Kristo asiyekuwa na pahali pa kulaza kichwa Chake, na badala yake unatamani maiti zinazokamata sadaka na kuishi katika uasherati. Hauko tayari kupokea mateso pamoja na Kristo, lakini unakimbilia mikononi mwa wapinzani wa Kristo hata ingawa wanakupa nyama za mwili pekee, barua na udhibiti pekee. Hata sasa, moyo wako bado unawaendea, sifa zao, misimamo yao katika mioyo ya mashetani wote, ushawishi wao, na mamlaka yao, ilhali unazidi kuipinga na kuikataa kazi ya Kristo. Hii ndiyo maana Ninasema hauna imani ya kumkubali Kristo. Sababu iliyokufanya Umfuate mpaka leo hii ni kuwa ulilazimishwa. Moyoni mwako milele mna picha nyingi refu; huwezi kusahau kila neno lao na matendo yao, au maneno yao ya ushawishi na mikono. Wao ni, katika moyo wako, wakuu milele na tena mashujaa milele. Lakini hivi sivyo ilivyo na Kristo wa leo hii. Yeye moyoni mwako kamwe Hana umuhimu na kamwe Hastahili heshima. Kwa maana Yeye ni wa kawaida sana, mwenye ushawishi mdogo zaidi na Yuko mbali na ukuu.

kutoka kwa "Je, Wewe ni Muumini wa Kweli wa Mungu?" katika Neno Laonekana katika Mwili

Tazama viongozi wa kila madhehebu na faraka. Wote ni wa kujigamba na kujisifu, na wanafafanua Biblia nje ya muktadha na kulingana na ubunifu wao wenyewe. Wote wanategemea zawadi na maarifa kufanya kazi yao. Kama hawangekuwa na uwezo wa kuhubiri chochote, wale watu wangewafuata? Wao, hata hivyo, wanamiliki ujuzi fulani, na wanaweza kuongea mafundisho kiasi, au wanajua jinsi ya kuwashawishi wengine na jinsi ya kutumia ustadi kadhaa, ambao kupitia kwake wamewaleta watu mbele yao wenyewe na kuwadanganya. Kwa jina, watu hao humwamini Mungu—lakini katika uhalisi wanafuata viongozi wao. Wakikutana na wale wanaohubiri njia ya kweli, baadhi yao wangesema, "Lazima tutafute ushauri kwake kuhusu imani yetu katika Mungu." Tazama jinsi wanavyohitaji ridhaa ya mtu ili kumwamini Mungu; hilo si tatizo?

kutoka kwa "Ukimbizaji Ukweli Tu Ndiyo Imani ya Kweli katika Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili

Watu wanaoamini katika Mungu wanapaswa kumtii na kumwabudu. Hupasi kusifu au kumwabudu mtu yeyote; hupaswi kumpa Mungu nafasi ya kwanza, binadamu unayemheshimu nafasi ya pili, kisha wewe mwenyewe nafasi ya tatu. Mtu yeyote asishikilie nafasi yoyote moyoni mwako, na hufai kuzingatia watu—hasa wale unaowaenzi—kuwa katika kiwango sawa na Mungu, kuwa sawa na Yeye. Mungu hawezi kustahimili hili.

kutoka kwa "Amri Kumi Za Utawala Ambazo Lazima Zitiiwe Na Watu Waliochaguliwa Na Mungu Katika Enzi Ya Ufalme" katika Neno Laonekana katika Mwili

Wale ambao hawauelewi ukweli siku zote wanawafuata wengine. Ikiwa watu wanasema kwamba hii ni kazi ya Roho Mtakatifu, basi, wewe pia utasema ni kazi ya Roho Mtakatifu; ikiwa watu watasema ni kazi ya roho mchafu, basi wewe pia utatilia mashaka, au utasema ni kazi ya roho mchafu. Siku zote unakuwa kama kasuku kwa maneno ya wengine, na huwezi kutofautisha kitu chochote wewe mwenyewe, wala huwezi kufikiri kwa ajili yako mwenyewe. Huyu ni mtu ambaye hana msimamo, ambaye hana uwezo wa kutofautisha—mtu wa aina hiyo ni masikini asiyejitambua. Watu kama hao siku zote wanarudia maneno ya wengine: Leo inasemwa kuwa hii ni kazi ya Roho Mtakatifu, lakini kuna uwezekano siku moja mtu atasema si kazi ya Roho Mtakatifu, na si chochote bali matendo ya mwanadamu—halafu huwezi kuelewa, na utakaposhuhudia watu wengine wanasema hivyo, nawe pia unasema kitu kile kile. Kwa kweli ni kazi ya Roho Mtakatifu, lakini unasema ni kazi ya mwanadamu; hujawa mmoja wa wale wanaoikufuru kazi ya Roho Mtakatifu? Katika hili, hujampinga Mungu kwa sababu huwezi kutofautisha? Nani ajuaye, siku moja mtu atatokea na kusema "hii ni kazi ya roho mchafu," na utakaposikia maneno haya utapotea, na kwa mara nyingine tena unafungwa na maneno ya wengine. Kila wakati mtu anachochea usumbufu huwezi kusimama katika msimamo wako, na hii ni kwa sababu huna ukweli ndani yako. Kuamini katika Mungu na kutafuta maarifa ya Mungu si jambo rahisi. Hayawezi kupatikana kwa kukusanyika pamoja na kusikiliza mahubiri, na huwezi kukamilishwa kwa kupenda tu. Lazima upitie uzoefu, na ujue, na kuongozwa na kanuni katika matendo yako, na kupata kazi za Roho Mtakatifu.

kutoka kwa "Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu" katika Neno Laonekana katika Mwili

Ushirika wa Mtu:

Kumfuata Mungu humaanisha kumsikiliza Mungu katika kila kitu, kuitii mipango yote ya Mungu, kutenda kulingana na maneno ya Mungu, na kuyakubali yote yatokayo kwa Mungu. Kama unamwamini Mungu, basi unapaswa kumfuata Mungu; lakini, bila kulitambua, wakati wanapomwamini Mungu watu wengi huwafuata watu, ambalo ni jambo la mzaha na la kuhuzunisha. Kusema kwa kweli, yeyote watu wanayemfuata ni yule wanayemwamini. Ingawa watu wengine humwamini Mungu kwa jina tu, mioyoni mwao hakuna Mungu; katika mioyo yao, wao huwaabudu viongozi wao. Kuwasikiliza viongozi wa fulani, na kwenda hata kiasi cha kuikataa mipango ya Mungu, ni onyesho la kumwamini Mungu lakini kuwafuata watu. Kabla ya hawajapata ukweli, imani ya kila mtu imevurugika na kuchanganyikiwa kama hili. Wao hata hawajui kabisa maana ya kumfuata Mungu, na wanashindwa kusema tofauti kati ya kumfuata Mungu na kuwafuata watu. Wao huamini tu kwamba yeyote anayesema mafundisho mema, na ya juu, ni baba au mama yao; kwao, yeyote aliye na maziwa ni mama yao, na yeyote aliye na nguvu ni baba yao. Hivyo ndivyo jinsi wanavyosikitisha. Inaweza kusemwa kuwa, kwa hatua tofauti tofauti, hii ndiyo hali ya kiroho ya watu wengi.

Inamaanisha nini kumfuata Mungu? Na unawezaje kutia hilo katika vitendo? Kumfuata Mungu hakuhusishi tu kumwomba Mungu na kumsifu Mungu; kilicho muhimu zaidi ni kula na kunywa maneno ya Mungu na kuishi kulingana na maneno ya Mungu, kutenda kulingana na ukweli, kutafuta njia ya kupata uzoefu wa maisha katikati ya maneno ya Mungu, kukubali agizo la Mungu, kutekeleza kila moja ya wajibu wako vizuri, na kuitembea njia iliyo mbele yako kama unavyoongozwa na Roho Mtakatifu. Hasa, katika nyakati muhimu, wakati matatizo makuu yanapokufika, kuna hata haja kubwa zaidi ya kutafuta maana ya Mungu, kuwa na hadhari ya kudanganywa na mafundisho ya mwanadamu, na kutokuwa chini ya udhibiti wa mtu yeyote. "Kile kitokacho kwa Mungu mimi hukitii na kukifuata, lakini ikiwa kinatoka kwa mapenzi ya mwanadamu mimi hukikataa kwa uthabiti; wakati kile kinachohubiriwa na viongozi au wafanyakazi kina mgongano na mipango ya Mungu, basi mimi bila shaka humfuata Mungu na kuwakataa watu. Kama kina makubaliano kamili na mipango na mapenzi ya Mungu, basi naweza kukisikiliza."

Watu ambao hutenda kwa njia hii ni wale ambao humfuata Mungu. Inamaanisha nini kuwafuata watu? Kuwafuata watu inamaanisha mtu huwafuata wafanyakazi au viongozi anaowaabudu. Mungu hana nafasi kubwa katika mioyo yaomoyo wake; yeye hutundika kidokezo akisema anamwamini Mungu, na katika kila kitu anachofanya yeye ni kujifananisha na watu au kuwaiga. Hasa wakati ni jambo kuu, anawaacha watu kuamua, anawaacha watu waongoze jaala yao, yeye mwenyewe hatafuti maana ya Mungu, na anashindwa kutambua maneno yanayosemwa na watu. Mradi anachokisikia kinaonekana kuwa cha maana, basi bila kujali kama kinapatana na ukweli bado yeye hukikubali na kukisikiliza. Haya ni maonyesho ya kuwafuata watu. Imani ya watu kama hao katika Mungu haina kanuni, hakuna ukweli katika matendo yao, wao husikiliza mtu yeyote anayesema jambo la maana, na hata vijimungu vyao vikichukua njia mbaya, wao huvifuata mpaka mwisho. Mungu Akivilaani vijimungu vyao, basi watakuwa na dhana juu ya Mungu, na kushikilia kikiki vijimungu vyao. Sababu zao ni kwamba "tunapaswa kumsikiliza yeyote aliye na madaraka juu yetu; nguvu ya karibu ni bora kuliko nguvu ya juu." Hii ni mantiki duni, upumbavu mtupu, lakini huo ndio upumbavu wa hao ambao huwafuata watu. Wale wanaowafuata watu hawana ukweli. Ni wale tu ambao humfuata Mungu wanaoamini kweli katika Mungu; Wale wanaowafuata watu huabudu sanamu, wamekuwa wakidanganywa na watu, na katika mioyo yao hakuna Mungu wala ukweli.

kutoka kwa "Kutofautisha kati ya Kumfuata Mungu na Kuwafuata Watu" katika Ushirikiano Kutoka kwa wa Juu

Watu wengi humwamini Mungu lakini hawajui ni nini maana ya kumtii Mungu, na hufikiri kwamba kuwasikiliza viongozi wao katika vitu vyote ni sawa na kumtii Mungu. Maoni kama haya ni ya upuuzi kabisa, kwa sababu chanzo cha utii wao si sahihi. Wao hudhukuru kuwasikiliza viongozi wao kuwa ni kumtii Mungu. Kumwamini Mungu kulingana na maoni haya ni kumwamini Mungu kwa jina tu; kwa uhakika, watu hawa huwaamini watu. …

Tunapomwamini Mungu, Mungu anapaswa kushikilia mahali pa kuongoza katika mioyo yetu, tunapaswa kusalimisha uongozi kwa Mungu katika mambo yote, tunapaswa kutafuta maana ya Mungu katika kila kitu, vitendo vyetu vinapaswa kulingana na maneno ya Mungu, na kwa mujibu wa mwongozo wa Roho Mtakatifu, na tunapaswa kutii yote yatokayo kwa Mungu. Ukiwasikiliza watu, basi hili linathibitisha kwamba Mungu hana mahali moyoni mwako, kwamba ni watu pekee walio na mahali katika moyo wako. Hakuna kilicho muhimu zaidi kwa watu kuliko kufuatilia ukweli na kuyaelewa mapenzi ya Mungu. Ikiwa huzingatii kuyatafuta malengo ya Mungu na kuyafahamu mapenzi ya Mungu, basi wako si utii wa kweli. Haijalishi ni sahihi jinsi gani wanavyosikika, ikiwa daima wewe huwasikiliza watu, basi kwa kiini wewe huwasikiliza watu–ambako si sawa na kumtii Mungu. Kwa kweli, kama wale wanaomwamini Mungu wanaweza kuelewa maana ya Mungu moja kwa moja kutoka kwa maneno Yake, ikiwa wanaweza kupata njia yao wenyewe ya kutenda katika maneno Yake, na huwasiliana ukweli kwa karibu, na kuuelewa ukweli, kwa maneno Yake, baada ya hayo wao waiweke katika vitendo, na ikiwa kwa wakati muhimu, wanaweza kuomba zaidi, na kutafuta uongozi wa Roho Mtakatifu, na kutii malengo ya Roho Mtakatifu, hivi kweli ni kumtii Mungu. Wale wanaomtii Mungu hutafuta njia katika maneno ya Mungu, matatizo yao hutatuliwa katika maneno ya Mungu, na wao hufanya kazi katikati ya uongozi wa Roho Mtakatifu; hivi kweli ni kumtii Mungu. Wale ambao husikiliza viongozi wao katika kila kitu wana hakika ya kupotea mbali na Mungu katika mioyo yao. Zaidi ya hayo, hawana amani mbele ya Mungu, sio wale wanaoishi mbele ya Mungu na kutafuta ukweli, hawana uhusiano na Mungu, na kanuni ya matendo yao ni kumsikiliza yeyote anayesema mambo halisi–mradi ni kiongozi, watatii. Vitendo kama hivyo ni vya dhihaka. Hawana ukweli wala uwezo wa kutofautisha, na wanaweza tu kudhibitisha kilicho sawa au kibaya kulingana na mawazo yao au akili, kwa hiyo jinsi gani wanaweza kujua kama kinafanana na ukweli? Kama wao huamini Mungu kulingana na maoni hayo, basi katika maisha yao yote hawatauelewa ukweli au kumjua Mungu. Aina hizo za imani zinaweza kusemwa kuwa kuamini katika ubongo wao wenyewe na kuitembea njia yao wenyewe, na hawana uhusiano na Mungu wa vitendo.

kutoka kwa "Kuwasikiza Viongozi Wako katika Kila Jambo si Sawa na Kumtii Mungu" katika Ushirikiano Kutoka kwa wa Juu

Maneno "amini tu katika Mungu" yanahusu nini? Yanamaanisha kuamini tu kwamba Mungu ni mwenyezi, kwamba Mungu ni kila kitu, kwamba Mungu anaweza kumwokoa mwanadamu, kwamba Mungu ni Mwenyezi na mwenye maarifa yote, kwamba katika Mungu hakuna chochote ambacho hakiwezi kufanikishika. Yanamaanisha kuamini kwa Mungu tu, na bila kuwa na shaka au kutoamini kwamba Mungu ni mwenyezi na mwenye maarifa yote, au kwamba Anaweza kufanikisha kila kitu. Watu kama hawa wanaweza kuomba mbele ya Mungu bila kujali kinachowafanyikia, na wanaweza kumtegemea Mungu bila kujali shida zinazowatokea. Kristo hushikilia mahali muhimu mioyoni mwao, hawastahi au kuwaabudu watu, wao huamini tu katika Mungu, wao humfuata tu Mungu wa vitendo, hawamtegemei na kumstahi mtu yeyote isipokuwa Mungu, hawampi imani pofu mtu yeyote, na ni Mungu pekee, na hakuna mwingine, aliye na mahali katika mioyo yao. Kama wamefikia hatua hiyo, basi wana uhalisi wa kumfuata na kumtegemea Mungu katika imani yao. Imani ya watu wengine katika Mungu ni kidogo mno: Hawamfikirii Mungu kama mwenyezi, na hivyo wakati kitu kinapowatokea, ni rahisi kwao kupoteza imani yao. Zaidi ya hapo, pia ni rahisi kwao kuwaabudu na kuwastahi watu, na ni kana kwamba wao hutumia hili kufidia sehemu za Mungu ambazo haziwatoshi. Kwa sababu wao daima huwastahi na kuwaabudu watu, bila wao kujua kuwa mahali pa Mungu katika mioyo yao huendelea kuwa padogo sana, na mahali pa watu wanaowaabudu panaendelea kuwa pakubwa zaidi. Hatimaye, wao bila kujua wanakuwa wale wanaomwamini Mungu kwa jina tu, ambao kwa kweli huwaamini watu, kuwafuata watu, kuwaabudu watu, na kuwastahi watu. Kama tu wale wa dini, imani yao kwa Mungu ni kwa jina tu; kwa kweli, yote wanayoamini na kufuata ni wachungaji, na ni wachungaji tu walio Bwana wao na Mungu. Kutoka kwa njia ya kumwamini Mungu, wananyiririka katika kuwafuata na kuwatii watu–si huku ni kupotoka? Je, watu kama hao wana imani ya kweli kwa Mungu? Hawana. Kwa hiyo, katika kila kitu hawamtegemei Mungu, lakini huwastahi na kuwaabudu watu. Wao daima hutafuta dokezo kutoka kwa wengine, huchukua ishara yao kutoka kwa wengine katika kutafuta njia, daima husikiliza kile watu husema na kutazama kile wanachokifanya, na kila neno na kitendo chao hakichangukani na watu hawa. Bila kulitambua, wamekuwa wale wanaowaamini na kuwafuata watu. Ni kweli kusema kwamba wale wote ambao ni wa kuwastahi na kuwaabudu mno watu kwa kweli huwaamini na kuwafuata watu.

kutoka kwa "Ukweli Kumi wa Maneno ya Mungu Ambao Lazima Uingiwe ili Kuokolewa na Kufanywa Mkamilifu" katika Mahubiri na Ushirika juu ya Kuingia Katika Maisha (IV)

Yeyote ambaye watu humwabudu mioyoni mwao ni sanamu yao; yeyote anayewaabudu viongozi wao ni mtu anayeziabudu sanamu. Yule ambaye watu humwabudu ni yule aliye na mahali ndani ya mioyo yao, na yule ambaye bila kuzuilika atawamiliki na kuwafanya watumwa wao. Wakati wa kazi ya kueneza injili, tunagundua kwamba watu kutoka kwa makundi mbalimbali ya kidini na madhehebu wote huabudu sanamu, wote hudhibitiwa na viongozi wao, kwamba hata hawathubutu kukubali ukweli. Wao ni kama watumwa wa kusikitisha. Watu wanaowaabudu viongozi wao ni wale wanaoabudu sanamu, nyoyo zao pasipo shaka hazina ukweli, na hawamjui Mungu kabisa; hivyo, Mungu hana mahali katika mioyo yao, na wao huchukiwa na kulaaniwa na Mungu. Mungu ni Mungu mwenye haki, Yeye ni Mungu mwenye wivu, na hakuna Anayemchukiza zaidi kuliko wakati watu wanapoabudu sanamu. Hakuna maneno ya kumtukana Mungu yaliyo makubwa zaidi kuliko kuwachukua viongozi kuwa sawa na Mungu. Kwa kweli, katika mioyo ya wale ambao wamerudi mbele ya Mungu, kunapaswa kuwa Mungu tu. Hakuna mwingine anayepaswa kuwa na mahali katika mioyo yao. Kwa vitu kama hivyo hata kuwa na sehemu muhimu katika fikira na mawazo yao ni najisi na potovu, na huchukiwa na kukirihiwa na Mungu. Katika hili, watu wengi ni najisi, na kwa kiwango kikubwa au kidogo, wale wanaowaabudu wana mahali katika mioyo yao. Inapoishia kwa tabia ya Mungu, haikubaliki kwamba watu wana mahali padogo pa wanadamu ndani ya mioyo yao, na kama hawawezi kufanikisha usafi tangu mwanzo hadi mwisho, basi watahukumiwa.

Kuna maonyesho maalum ndani ya wote wanaowaabudu viongozi wao katika mioyo yao. Wanaweza kutambuliwa kama ifuatavyo: Ikiwa utii wako kwa kiongozi wako ni mkubwa kuliko utii wako kwa Mungu, basi wewe huziabudu sanamu; ikiwa unawatamani sana na kuwataka sana watu unaowaabudu kuliko unavyomtamani sana na kumtaka sana Mungu, basi unaziabudu sanamu; Ikiwa wewe ni mwenye ari zaidi kwa kiongozi wako kuliko Mungu, basi unaziabudu sanamu; ikiwa, katika moyo wako, wewe u karibu na wale unaowaabudu na mbali na Mungu, basi unaziabudu sanamu; kama, katika moyo wako, wale unaowaabudu wana cheo sawa na Mungu, basi hili ni thibitisho hata kubwa mno kuwa unawachukulia watu unaowaabudu kuwa kama Mungu; na kama, bila kujali kinachokutokea, wewe hukubali kusikiliza kiongozi wako, na hukubali kuja mbele ya Mungu kutafuta ukweli, basi hili linatosha kuthibitisha kwamba humwamini Mungu, bali watu. Watu wengine, labda, watajaribu kujitetea, wakisema: "Kwa kweli namstahi fulani, kwa kweli ana mahali katika moyo wangu. Pasipo kulitambua, nimekuwa mbali kidogo na Mungu katika uhusiano wangu na Yeye." Maneno haya yanaonyesha ukweli wa jambo hilo; mara tu mtu fulani anapopata mahali katika moyo wa mtu, mtu huyo huwa mbali na Mungu. Hili ni hatari, lakini baadhi ya watu hulichukulia kwa wepesi, hawana shughuli hata kidogo, jambo ambalo linaonyesha kwamba hawajui tabia ya Mungu. ... kuwaabudu watu ni ujinga sana na upofu, ni upotovu sana na uovu. Kuwaabudu watu ni kumwabudu Shetani na pepo, ni kuwaabudu wapinga Kristo, na wale wanaowaabudu watu hawana ukweli hata kidogo. Watu kama hawa hakika hawana ujuzi wa Mungu hata kidogo; wao ni wapotovu ambao wamelaaniwa na Mungu. Wasemaje wewe, si ukweli uko hivyo?

kutoka kwa "Wale Wanaowaabudu Viongozi Wao Mioyoni Mwao Huabudu Sanamu" katika Ushirikiano Kutoka kwa wa Juu

Iliyotangulia:Unawezaje Kutambua Tofauti Kati ya Njia za Kweli na za Uongo, na Makanisa ya Kweli na ya Uongo?

Inayofuata:Unawezaje Kutofautisha Kati ya Viongozi wa Kweli na wa Uongo, na Wachungaji wa Kweli na wa Uongo?

Maudhui Yanayohusiana