4. Utofautishaji Kati ya Njia za Kweli na za Uongo, na Kati ya Makanisa ya Kweli na ya Uongo

Maneno Husika ya Mungu:

Kanuni ya msingi kabisa katika kuutafuta ukweli ni nini? Unapaswa kuangalia kama kuna kazi ya Roho Mtakatifu au la kwa njia hii, iwapo maneno haya ni maonyesho ya ukweli, yanamshuhudia nani, na ni kitu gani yanaweza kukupatia. Kutofautisha kati ya njia ya kweli na hizi njia za uongo kunahitaji njia kadhaa za maarifa ya msingi, ya msingi kabisa kati ya zote ni kusema iwapo kuna Kazi ya Roho Mtakatifu au la. Maana kiini cha imani ya mwanadamu katika Mungu ni imani katika Roho Mtakatifu. Hata imani yake katika Mungu mwenye mwili ni kwa sababu mwili huu ni mfano halisi wa Roho wa Mungu, ikiwa na maana kwamba imani hiyo bado ni imani katika Roho. Kuna tofauti kati ya Roho na mwili, lakini kwa kuwa mwili unatokana na Roho, na ndio Neno linakuwa mwili, hivyo kile ambacho mwanadamu anaamini katika ni uungu halisi wa Mungu. Na hivyo, katika kutofautisha kama ni njia sahihi au la, zaidi ya yote unapaswa kuangalia kama kuna kazi ya Roho Mtakatifu, na baada ya hapo unapaswa kuangalia kama kuna ukweli katika njia hii. Ukweli huu ni tabia ya maisha ya ubinadamu wa kawaida, ni sawa na kusema, kile ambacho Mungu alitaka kwa mwanadamu alipomuumba hapo mwanzo, yaani, ubinadamu wote wa kawaida (ikiwa ni pamoja na hisia za kibinadamu, umaizi, hekima, na maarifa ya msingi ya kuwa mwanadamu). Yaani, unapaswa kuangalia iwapo njia hii inaweza kumpeleka mwanadamu katika maisha ya ubinadamu wa kawaida au la, iwapo ukweli uliozungumzwa unahitajika kulingana na uhalisi wa ubinadamu wa kawaida au la, iwapo ukweli huu ni wa kiutendaji au hali, na iwapo ni wa wakati muafaka au la. Ikiwa kuna ukweli, basi unaweza kumpeleka mwanadamu katika uzoefu wa kawaida na halisi; aidha, mwanadamu anakuwa wa kawaida zaidi, hisia za kawaida za kibinadamu zinakuwa kamili zaidi, maisha ya mwanadamu katika mwili na maisha ya kiroho yanakuwa katika mpangilio mzuri zaidi, na mihemko ya mwanadamu inakuwa ya kawaida kabisa. Hii ni kanuni ya pili. Kuna kanuni nyingine moja zaidi, ambayo ni kama mwanadamu ana maarifa mengi juu ya Mungu au la, kama unapitia uzoefu wa kazi hiyo na ukweli unaweza kuchochea upendo wa Mungu ndani yake au la, na kumsogeza karibu zaidi na Mungu. Katika hili inaweza kupimwa kama ni njia sahihi au la. Kanuni ya msingi ni iwapo njia hii ni ya uhalisi badala ya kuwa ya kimiujiza, na iwapo inaweza kutoa maisha ya mwanadamu. Kama inakubaliana na kanuni hizi, hitimisho linaweza kuwekwa kwamba njia hii ni njia ya kweli. Ninasema maneno haya si kuwafanya mkubali njia nyingine katika uzoefu mtakaoupitia baadaye, wala si utabiri kwamba kutakuwa na kazi ya enzi nyingine mpya hapo baadaye. Ninayasema ili mweze kuwa na uhakika kwamba kazi ya leo ni kazi ya kweli, ili kwamba msiwe na uhakika nusu katika imani yenu katika kazi ya leo na kushindwa kuielewa kwa ndani. Kuna hata watu wengi ambao, licha ya kuwa na uhakika, bado wanafuata kwa mkanganyiko; uhakika kama huo hauna kanuni, na wanapaswa kuondolewa siku moja. Hata wale ambao wapo motomoto katika imani yao wanakuwa na uhakika katika mambo matatu na mambo matano wanakuwa hawana uhakika, kitu kinachoonyesha kuwa hawana msingi. Kwa sababu tabia yenu ni dhaifu sana na msingi wenu hauna kina, hivyo hamna uelewa wa kutofautisha. Mungu harudii kazi Yake, Hafanyi kazi ambayo si halisi, Hamtaki mwanadamu afanye mambo zaidi ya uwezo wake, na Hafanyi kazi ambayo inazidi akili ya mwanadamu. Kazi yote Anayofanya ipo ndani ya mawanda ya akili ya kawaida ya mwanadamu, na haizidi ufahamu wa ubinadamu wa kawaida, na kazi Yake ni kulingana na mahitaji ya kawaida ya mwanadamu. Ikiwa ni kazi ya Roho Mtakatifu, mwanadamu anakuwa wa kawaida zaidi, na ubinadamu wake unakuwa wa kawaida kabisa. Mwanadamu ana maarifa mengi ya tabia yake ya kishetani na iliyopotoka, na asili ya mwanadamu, na ana shauku kubwa ya kuuelewa ukweli. Hiyo ni kusema, maisha ya mwanadamu yanakua zaidi na zaidi, na tabia upotovu ya mwanadamu inakuwa na uwezo wa mabadiliko zaidi na zaidi—yote hiyo ni maana ya Mungu kuwa maisha ya mwanadamu. Kama njia haiwezi kufunua vitu hivyo ambavyo ni asili ya mwanadamu, haiwezi kubadilisha tabia ya mwanadamu, na, zaidi ya hayo, hauwezi kumleta mbele ya Mungu au kumpa ufahamu wa kweli juu ya Mungu, na hata kufanya ubinadamu wake kuwa duni zaidi na hisia zake kuwa si za kawaida zaidi, basi njia hii itakuwa si njia ya kweli, na inaweza kuwa ni kazi ya roho mchafu, au njia ya zamani. Kwa ufupi, haiwezi kuwa kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu.

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake Ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu

Katika kila hatua ya kazi ya Mungu yapo pia matakwa sawia kwa mwanadamu. Wale wote walio katika mkondo wa Roho Mtakatifu wanamilikiwa na uwepo na nidhamu ya Roho Mtakatifu na wasiokuwemo katika mkondo wa Roho Mtakatifu wako chini ya utawala wa Shetani na hawana kazi yoyote ya Roho Mtakatifu. Walio katika mkondo wa Roho Mtakatifu ni wale wanaoikubali kazi mpya ya Mungu, wanaoshiriki katika kazi mpya ya Mungu. Iwapo walio ndani ya mkondo huu hawana uwezo wa kushirikiana, na hawawezi kuweka ukweli unaotakiwa na Mungu katika vitendo wakati huu, basi watafundishwa nidhamu, na hali ikiwa mbaya zaidi kuachwa na Roho Mtakatifu. Wale ambao wanakubali kazi mpya ya Roho Mtakatifu, wataishi katika mkondo wa Roho Mtakatifu, wapokee utunzaji na ulinzi wa Roho Mtakatifu. Wale ambao wako tayari kuweka ukweli katika vitendo wanapewa nuru na Roho Mtakatifu na wale wasiotaka kuweka ukweli katika vitendo wanafundishwa nidhamu na Roho Mtakatifu na huenda hata wakaadhibiwa. Bila kujali wao ni aina gani ya watu, ilimradi tu wamo katika mkondo wa Roho Mtakatifu, Mungu atawawajibikia wote wanaoikubali kazi Yake mpya kwa minajili ya jina Lake. Wale wanaolitukuza jina Lake na wako radhi kuweka maneno Yake katika vitendo watapokea baraka Zake; wale wasiomtii na wasioyaweka maneno Yake katika vitendo watapokea adhabu Yake. Watu walio katika mkondo wa Roho Mtakatifu ni wale wanaoikubali kazi mpya, na kwa sababu wameikubali kazi mpya, wanafaa kuwa na ushirika wa kufaa na Mungu na hawafai kuwa kama waasi wasiofanya wajibu wao. Hili ndilo sharti la pekee la Mungu kwa mwanadamu. Sio hivyo kwa watu wasioikubali kazi mpya: Wako nje ya mkondo wa Roho Mtakatifu, na nidhamu na lawama ya Roho Mtakatifu hayatumiki kwao. Kila siku hawa watu wanaishi ndani ya mwili, wanaishi ndani ya akili zao, na yote wayafanyayo ni kulingana na mafundisho ya kidini yaliyozalishwa na uchanganuzi pamoja na utafiti wa bongo zao. Si matakwa ya kazi mpya ya Roho Mtakatifu sembuse ushirika na Mungu. Wale wasioikubali kazi mpya ya Mungu hawana uwepo wa Mungu na, zaidi, wanakosa baraka na ulinzi wa Mungu. Maneno na matendo yao mengi yanashikilia matakwa ya zamani ya kazi ya Roho Mtakatifu; ni mafundisho ya kidini, si ukweli. Mafundisho na taratibu kama hizo ni thibitisho la kutosha kuwa kukutana pamoja kwa watu hawa si linguine ila dini; si watu walioteuliwa au vyombo vya kazi ya Mungu. Mkutano wa wale wote walio miongoni mwao unaweza tu kuitwa mkutano mkubwa wa watu wa dini, na bali hauwezi kuitwa kanisa. Huu ni ukweli usioweza kubadilishwa. Hawana kazi mpya ya Roho Mtakatifu; wakifanyacho kinaonekana chenye kunuka dini, wanachoishi kwa kudhihirisha katika maisha yao kinaonekana kimejaa dini; hawana uwepo na kazi ya Roho Mtakatifu, sembuse kustahiki kupokea nidhamu au nuru ya Roho Mtakatifu. Watu hawa wote ni miili isiyo na uhai, na funza wasio na mambo ya kiroho. Hawana ufahamu wa uasi na pingamizi wa mwanadamu, hawana ufahamu wa uovu wote wa mwanadamu, sembuse kujua kazi yote ya Mungu na mapenzi ya sasa ya Mungu. Wote ni watu wapumbavu, waovu, ni watu duni wasiostahili kuitwa waumini! Hakuna wafanyacho kinachohusiana na usimamizi wa Mungu, sembuse kuweza kuidhoofisha mipango ya Mungu. Maneno na matendo yao yanaudhi sana, yanasikitisha mno, na hayafai kutajwa kabisa. Hakuna chochote wakifanyacho walio nje ya mkondo wa Roho Mtakatifu kinahusiana na kazi mpya ya Roho Mtakatifu hata kidogo. Kwa sababu hii, haijalishi wanafanya nini, hawana nidhamu ya Roho Mtakatifu na zaidi, hawana nuru ya Roho Mtakatifu. Kwani wao ni watu wasiopenda ukweli, na wamechukiwa na kukataliwa na Roho Mtakatifu. Wanaitwa watenda maovu kwani wanatembea katika mwili, na kufanya chochote kiwafurahishacho kwa kisingizio cha bango la Mungu. Mungu anapofanya kazi, wao wanakuwa maadui Kwake kwa makusudi, na kumkimbia Yeye. Kutoweza kushirikiana kwa mwanadamu na Mungu ni uasi wa hali ya juu, kwa hivyo wale watu wanaokimbia kinyume na Mungu makusudi si watapokea hakika malipo yao ya haki?

Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu

Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:

Iwapo jamii ya kidini nzima haingekuwa na uhasama na kuipinga, basi hii haingekuwa njia ya kweli. Kumbuka: Njia ya kweli lazima ipingwe na watu wengi, hata na duniani. Wakati Bwana Yesu Alikuja mara ya kwanza kufanya kazi na kuhubiri, je, Uyahudi mzima haukumpinga Yeye? Kila wakati Mungu anapoanza kazi mpya, ubinadamu mpotovu unapata ugumu mkubwa katika kuikubali, kwa kuwa kazi ya Mungu inakinzana na na inakanusha dhana za watu; watu hawana uwezo wa kuelewa, na hawana uwezo wa kuupenya ulimwengu wa kiroho, na kama sio kazi ya Roho Mtakatifu, hawangeweza kukubali njia ya kweli. Ikiaminiwa kuwa ni kazi ya Mungu, lakini haipingwi na jamii za kidini, na inakosa upinzani na uhasama wa dunia, basi hii inathibitisha kwamba kazi hii ya Mungu ni ya uongo. Kwa nini wanadamu hawawezi kuukubali ukweli? Kwanza, mwanadamu ni wa mwili, yeye ni wa dutu ya kimwili. Mambo ya kimwili hayawezi kupenya ulimwengu wa kiroho. Inamaanisha nini kwamba “hayawezi kupenya ulimwengu wa kiroho”? Hii ina maana ya kushindwa kuona roho, shughuli za roho na ulimwengu wa kiroho, kuwa asiyeona Anayofanya na kusema Mungu. Watu wangekuwa vipofu kuhusu kinachofanyika katika ulimwengu wa kiroho. Ukifunga macho yako katika ulimwengu wa kimwili, huoni chochote. Ukiyafungua, unaweza kuona nini? Dunia ya asili. Je, unaweza kuona ni roho yupi anafanya kazi gani ndani ya watu? Je, unaweza kuona kile ambacho Roho wa Mungu amekuja kufanya na kusema? Huwezi. Wakati mwingine unaweza kusikia sauti Yake, na kusoma maneno ya Mungu yaliyoandikwa kwenye kitabu, lakini bado hujui ni vipi au lini Mungu Alinena maneno haya. Unaweza kusikia sauti Yake, lakini hujui inakotoka; unayaona maneno ya Mungu yamechapishwa kwenye ukurasa, lakini hujui ni nini maana yake. Watu hawawezi kupenya ulimwengu wa kiroho, au kushika chanzo cha maneno ya Mungu, na hivyo wanahitaji kupata nuru na kuangaziwa kwa Roho Mtakatifu, na kazi ya Roho Mtakatifu, ili kupata matokeo. Pili, ubinadamu umekuwa mpotovu kwa undani sana, na ndani yake imejazwa na sumu nyingi ya Shetani na ufahamu mwingi; akitathmini kila kitu kwa kutumia falsafa mbalimbali za kishetani na maarifa, basi kamwe hataweza kusadikisha ukweli ni upi. Bila kupata nuru na kuangaziwa kwa Roho Mtakatifu, mwanadamu hangekuwa na uwezo wa kuelewa ukweli. Binadamu mpotovu kwa silika hawezi kupenya ulimwengu wa kiroho. Amejazwa na falsafa za kishetani na maarifa, na hawezi kuutambua ukweli. Na hivyo njia ya kweli bila kuepukika inakabiliwa na mateso na kukataliwa kwa mwanadamu. Kwa nini ni rahisi kwa watu kukubali maarifa na falsafa za Shetani? Kwanza, iko sambamba na dhana zao na maslahi ya miili yao, na ni ya manufaa kwa miili yao. Wanajiambia wenyewe, “Kukubali maarifa kama haya yananisaidia: Yatanipa kuongezwa cheo, yatanifanya niwe mwenye mafanikio, na kuniruhusu kufanikisha mambo. Na maarifa kama haya watu wataniheshimu.” Tazama jinsi vinavyowafaa watu viko sambamba na dhana zao. ... Kuwa wapotovu kwa kiasi hiki, na kushindwa kupenya ulimwengu wa kiroho, watu wanaweza tu kumpinga Mungu, na hivyo kuwasili kwa kazi ya Mungu kumekutana na kukataliwa na mwanadamu, upinzani, na hukumu. Je, si hili linatarajiwa? Kama kuwasili kwa kazi ya Mungu hakungekutana na hukumu na upinzani wa dunia na wanadamu, basi hili lingethibitisha kuwa sio ukweli. Iwapo yote yaliyosemwa na Mungu yangekuwa sambamba na dhana ya watu, je, wangeyashutumu? Je, wangeyapinga? Bila shaka hawangefanya hivyo.

Kimetoholewa kutoka katika Ushirika kutoka kwa Aliye Juu

Kanisa linajumuisha wale ambao hakika wameamuliwa kabla na kuchaguliwa na Mungu—linajumuisha wale wanaopenda ukweli, wanaotafuta ukweli, na wanamiliki kazi ya Roho Mtakatifu. Ni wakati tu watu hawa wanakusanyika ili kula na kunywa neno la Mungu, kuishi maisha ya kanisa, kupitia kazi ya Mungu, na kufanya wajibu wao kama viumbe wa Mungu ndio linaweza kuwa kanisa. Umati wenye zogo ukisema kwa kweli unaamini katika Mungu, lakini haupendi au kuutafuta ukweli, na hauna kazi ya Roho Mtakatifu, na unafanya sherehe za kidini, na kuomba, na kusoma maneno ya Mungu, basi hili sio kanisa. Kwa usahihi, makanisa yasiyo na kazi ya Roho Mtakatifu si makanisa; hayo ni kumbi za kidini na watu ambao hufanya sherehe za kidini tu. Wao si watu ambao kwa kweli wanamtii Mungu na kupitia kazi ya Mungu. …

…………

… Kanisa ni mkusanyiko wa watu ambao wanaamini katika Mungu kwa kweli na kufuatilia ukweli, na halishirikishi waovu kabisa—wao si wa kanisa. Iwapo kundi la watu ambao hawakutafuta ukweli na wala kufanya kitu chochote kuuweka ukweli katika vitendo wangekusanyika pamoja, je, hili lingekuwa kanisa? Je, mkusanyiko huu ungekuwa nini? Ungekuwa ukumbi wa kidini, au umati wenye zogo. Kanisa lazima liundwe na watu ambao kwa kweli wanaamini katika Mungu na kuufuatilia ukweli, wanaokula na kunywa maneno ya Mungu, na kumwabudu Mungu, kufanya wajibu wao, na kupitia kazi ya Mungu na wamepata kazi ya Roho Mtakatifu. Hili tu ndilo kanisa. Hivyo, unapotathmini kanisa, lazima kwanza uangalie ni aina gani ya watu linao. Pili, lazima uangalie iwapo wana kazi ya Roho Mtakatifu au la; kama mkutano wao hauna kazi ya Roho Mtakatifu, hilo si kanisa, na kama si mkusanyiko wa wale wanaofuatilia ukweli, basi sio kanisa. Iwapo kanisa halina mtu yeyote anayefuatilia ukweli, na liko bila kazi ya Roho Mtakatifu kabisa, basi kama kuna mtu ndani lake aliye na nia ya kuufuatilia ukweli, na wanabakia katika kanisa kama lile, je, mtu huyo anaweza kuokolewa? Hawezi, na anapaswa kuuacha umati huo wenye zogo na kutafuta kanisa haraka awezavyo. Iwapo, ndani ya kanisa, kuna watu watatu au watano ambao huufuatilia ukweli, na watu 30 au 50 ambao ni umati wenye zogo, basi wale watu watatu au watano ambao wanaamini katika Mungu kwa kweli na kuufuatilia ukweli lazima waje pamoja; wakija pamoja mkutano wao bado ni kanisa, kanisa la wanachama wachache zaidi, lakini lililo safi.

Kimetoholewa kutoka katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha

Viongozi na wachungaji wa ulimwengu wa kidini hawajapitia kazi ya Mungu au kukamilishwa na kujengwa na Roho Mtakatifu, lakini badala yake wamekuwa viongozi na wachungaji katika jamii ya kidini baada ya kuhitimu kutoka seminari na kupewa diploma. Hawana kazi na uthibitisho wa Roho Mtakatifu, hawana ufahamu wa kweli wa Mungu hata kidogo, na midomo yao haiwezi kuzungumza kuhusu kitu kingine ila maarifa ya kitheolojia na nadharia. Wao kwa kweli hawana uzoefu wa kitu chochote. Watu kama hao hawajafuzu kabisa kutumiwa na Mungu; watawezaje kumwongoza mwanadamu kwenda mbele za Mungu? Kwa kiburi hushikilia kuhitimu kutoka chuo seminari kama ushahidi wa haki yao wenyewe, wanafanya kila wawezalo ili kuonyesha kwa majivuno maarifa yao ya Biblia, ni wenye kiburi kisichostahimilika—na kwa sababu hii, wanahukumiwa na Mungu, na kuchukiwa na Mungu, na wamepoteza kazi ya Roho Mtakatifu. Kuhusu hili hakuna shaka. Kwa nini jamii ya kidini imekuwa adui mkubwa wa Kristo ni swali la kuchochea fikira nyingi sana. Inaonyesha nini kuwa, katika Enzi ya Neema, Uyahudi ulimpiga Yesu Kristo msalabani? Katika Enzi ya Ufalme wa siku za mwisho, jamii za kidini zimeungana na kuweka juhudi zake zote katika kupinga na kuhukumu kazi ya Mungu ya siku za mwisho, zinamkana na kumkataa Kristo mwenye mwili wa siku za mwisho, zimeunda uvumi mbalimbali kuhusu, na kushambulia, kusingizia na kukufuru dhidi ya Mungu mwenye mwili na kanisa la Mungu, na kwa muda mrefu sasa zimempiga misumari Yesu Aliyerudi, Kristo wa siku za mwisho, msalabani. Hii inathibitisha kuwa jamii za kidini kwa muda mrefu sasa zimepotoka na kuwa majeshi ya Shetani yanayopinga na kuasi dhidi ya Mungu. Jamii ya kidini haitawaliwi na Mungu, wala kutawaliwa na ukweli kweli; inatawaliwa kikamilifu na binadamu wapotovu, na zaidi ya hayo, na wapinga Kristo.

Watu wanapoamini katika Mungu kwenye ukumbi wa dini kama huu—ambao ni mali ya Shetani na unatawaliwa na kudhibitiwa na mapepo na wapinga Kristo—wanaweza tu kuelewa mafundisho ya dini, wanaweza tu kufuata sherehe za kidini na kanuni, na kamwe hawatawahi kuuelewa ukweli, kamwe hawatawahi kuipitia kazi ya Mungu, na kwa kikamilifu hawawezi kuokolewa. Hii ni bila shaka. Kwa kuwa hakuna jambo lolote la kazi ya Roho Mtakatifu katika kumbi za kidini, na ni maeneo ambayo yanamkera Mungu, ambayo yanachukiwa na Mungu, na yanashutumiwa na kulaaniwa na Yeye. Mungu hajawahi kuitambua dini, wala hajawahi kuisifu, na kutoka wakati wa Yesu jamii ya kidini imekuwa ikishutumiwa na Mungu. Hivyo, unapoamini katika Mungu lazima upate mahali palipo na kazi ya Roho Mtakatifu; haya tu ndiyo makanisa ya kweli, na ni katika makanisa ya kweli pekee ndiyo utaweza kusikia sauti ya Mungu, na kugundua nyayo za kazi ya Mungu. Hivyo ndivyo ilivyo njia ambayo Mungu Anatafutwa.

Kimetoholewa kutoka katika Ushirika kutoka kwa Aliye Juu

Iliyotangulia: 3. Utofautishaji Kati ya Kristo wa Kweli na Makristo wa Uongo

Inayofuata: 5. Tofauti Kati Ya Kumfuata Mungu na Kuwafuata Watu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp