Sura ya 43

Je, Sijawakumbusha? Msiwe wenye hofu; ninyi hamjanisikiliza tu, watu wasio na fikira ninyi! Je, mtaweza kuuelewa moyo Wangu lini? Kila siku kuna nuru mpya, kila siku kuna mwanga mpya. Ni mara ngapi mmeuelewa kwa ajili yenu wenyewe? Je, Sijawaambia Mwenyewe? Bado ninyi ni wa kukaa tu kama wadudu ambao watasonga tu wanaposukumwa, lakini hamwezi kuchukua hatua ya kushirikiana na Mimi, kuufikiria mzigo Wangu. Ningependa kuona tabasamu zenu changamfu na za kupendeza, kuona mwenendo wa Wanangu ulio wa vitendo na mchangamfu, lakini Siwezi. Badala yake, ninyi mmepungukiwa na akili, ni wajinga, na wapumbavu. Mnapaswa kuanza kutafuta. Fuatilia kwa ujasiri! Fungueni tu nyoyo zenu na mniruhusu Niishi ndani yenu. Tahadharini na muwe macho! Watu wengine katika kanisa ni wadanganyifu na mnapaswa kutilia mkazo sana maneno haya kila mara, maisha yenu yasije yakaathiriwa au kupata hasara fulani. Ondoa wasiwasi, mradi una ujasiri wa kusimama na kuzungumza kwa ajili Yangu, Nitachukua mzigo wa yote na kukupa uwezo! Mradi unauridhisha moyo Wangu, Nitakuonyesha tabasamu Yangu na mapenzi Yangu kila mara. Mradi una ujasiri na unaishi kwa kudhihirisha tabia ya mtoto wa kiume, Nitakuunga mkono na kukuweka katika nafasi muhimu. Unapokuja mbele Yangu, songa tu karibu na Mimi. Usiogope ikiwa huwezi kuzungumza. Mradi una moyo wa kutafuta, Nitakupa maneno. Sihitaji maneno matamu au kurai kwako; Ninachukia kitu cha aina hii zaidi ya vyote. Namchukia mtu wa aina hiyo zaidi ya wote. Yeye ni kama kipande cha kitu katika jicho Langu au mwiba katika mwili Wangu ambao lazima uondolewe. Vinginevyo wanangu hawawezi kutawala kwa ajili Yangu na watakuwa chini ya udhibiti wa kukaba. Kwa nini Nimekuja? Nimekuja kuwasaidia na kuwatia moyo wana Wangu, ili kwamba siku zao za kuvumilia ukandamizaji, unyanyasaji, ukatili, na dhuluma zitatoweka milele!

Kuwa jasiri. Nitatembea na wewe siku zote, Niishi na wewe, Nizungumze na wewe na Nitende nawe. Usiogope. Usisite kuzungumza. Daima ninyi ni wenye hisia, waoga, na wenye hofu. Wale ambao hawana faida yoyote kwa ujenzi wa kanisa lazima waondolewe. Hii ni pamoja na wale walio kanisani ambao hali zao si nzuri na wale ambao hawawezi kutenda kulingana na maneno Yangu, sembuse mama na baba yenu wasioamini. Sitaki mambo hayo. Lazima waondolewe, na asibaki hata mmoja. Fungua tu pingu zilizo kwenye mikono na miguu yako. Mradi unachunguza nia zako mwenyewe na hazihusiani na faida na hasara, wala kwa ajili ya umaarufu na utajiri, wala kwa ajili ya mahusiano ya kibinafsi, basi Nitaandamana na wewe, Nikuonyeshe mambo na kukupa mwongozo ulio wazi wakati wote.

Wanangu! Niseme nini? Ingawa Ninasema mambo haya, ninyi bado hamuufikirii moyo Wangu na bado ni waoga sana. Mnaogopa nini? Kwa nini bado mmefungwa kwa sheria na masharti? Nimewaachilia huru, lakini bado hamna uhuru. Kwa nini ni hivi? Wasiliana na Mimi zaidi na Nitakwambia. Usinijaribu. Mimi ni halisi. Sina udanganyifu, na vyote ni halisi! Kile Ninachosema ni kweli nami Sivunji ahadi Yangu kamwe.

Iliyotangulia: Sura ya 42

Inayofuata: Sura ya 44

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp